Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

BREAKING NEWZZZZ: Waziri Dkt. Kigwangala atengua uongozi wa bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala ametengua uongozi bodi ya utalii Tanzania TTB 

Waziri Kigwangala ametoa maamuzi hayo leo Januari 18. 2019 jijini Dar es Salaam Katika ofisi ya bodi hiyo na kusema kuwa maamuzi hayo yanatokana na watendaji wa bodi hiyo kutoendana na kasi yake katika utekelezaji wa majukumu katika wizara hiyo.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDA MAKABIDHIANO YA MFUMO WA KUTHIBITI MAWASILIANO YA NDANI NA NJE YA NCHI (TTMS)

$
0
0
 : Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akiwasili katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakimsikiliza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiongea machache wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.

 Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. James Kilaba akiwa kapigwa na butwaa na baadaye kushukuru wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipomhakikishia kumwongeza mkataba wa miaka mitano kuongoza taasisi hiyo katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na viongozi wa dini katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. James Kilaba   katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zacharia Kakobe  katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  viongozi wengine meza kuu  wakishuhudia makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) baina ya wakandarasi Bw. James Gabriel Claude CEO wa kampuni ya GVG na Samuel Kiki Gyan Mkurugenzi wa kampuni ya SGS na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA  Dkt. James Kilaba katika hafla iliyofanyika makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.

PICHA NA IKULU

Bundesliga inarejea tena Ijumaa hii, Dortmund wataendeleza moto wa raundi ya kwanza?

$
0
0
Baadaa ya mapumziko ya Siku kuu ni muda wa mzunguko wa pili wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, mzunguko wa pili ama hatua ya lala salama ni nafasi kwa timu zilizofanya vibaya mzunguko wa kwanza kupindua matokeo, na kwa zile zilizofanya vizuri kuendelea kujiimarisha zaidi.

Ijumaa hii, Bayern Munich ambao hawakufanya vizuri sana mzunguko wa kwanza wana nafasi ya kusahihisha makosa na kuanza kuwafukuzia Borussia Dortmund wanaoongoza ligi kwa sasa. Bayern Munich watakuwa ugenini kwa Hoffeiheim kwenye mchezo utakaopigwa saa 4:30 Usiku majira ya Afrika Mashariki na kuonyeshwa Mubashara kupitia ST World Football.

Mchezo mkubwa wikendi hii unatarajiwa kuwa ule wa RB Leipzig dhidi ya vinara Borussia Dortmund. Leipzig watakuwa nyumbani katika dimba la Red Bull Arena kukabiliana Dortmund wamepoteza mchezo mmoja tu hadi sasa. Mechi hiyo itachezwa siku ya Jumamosi saa 2:30 Usiku na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee. 

Kocha wa Dortmund Lucian Fevre huenda anasema nyota wake Marco Reus na kinara wa magoli Bundesliga Paco Alcacer wako fiti kucheza mchezo wa jumamosi. Reus alikuwa anasumbuliwa na tumbo, huku Alcacer akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. 

Kwa upande wa RB Leipzig wao wako vizuri na watawategemea zaidi Timo Werner mwenye kasi zaidi na Mshambuliaji wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen ambaye ana nguvu za kutosha kuwasumbua mabeki wa kati wa Dortmund Dani Axel Zagadou na Manuel Akanji.

Bayer Leverkusen watawakaribisha Borussia Mochengladbach jumamosi saa 11:30 jioni na mchezo utakuwa LIVE kupitia ST World Football. Wapenzi wa Soka nchini wataweza kutazama mechi hizi kupitia StarTimes pekee kwa kulipia kifurushi cha MAMBO Tsh 14,000 (watumiaji wa Antenna) na SMART Tsh 21,000 (watumiaji wa Dish) 

MIRADI MIKUBWA MITATU YENYE THAMANI YA BIL. 1.2..PWANI MATATANI -TAKUKURU

$
0
0
Naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani, Sadiki Nombo akitoa taarifa ya utendaji kazi katika kipindi cha oktoba hadi desemba 2018 kwa baadhi ya waandishi wa habari mkoani humo. (picha na Mwamvua Mwinyi).

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Pwani, inaitilia shaka ujenzi wa miradi mikubwa mitatu ya afya na maji, yenye thamani ya zaidi ya sh. Bilioni 1.259 ambayo imeanza kuchunguzwa ili kubainika kama kuna ubadhilifu hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

Aidha, imechukua hatua ya kuwahamisha vituo vya kazi askari wa usalama wapatao wanne baada ya kudaiwa kujihusisha na kuomba rushwa ,kwa kushirikiana na jeshi la polisi .

Akitoa taarifa ya utendaji kazi katika kipindi cha oktoba hadi desemba 2018 ,naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani, Sadiki Nombo alisema, jumla ya miradi Tisa iliyogharimu Bilioni 3.373 .670 ilifuatiliwa katika kipindi hicho.

Hata hivyo alieleza, miradi hiyo ni pamoja na sekta ya maji, afya, uvuvi na elimu, kati ya miradi hiyo mitatu inadaiwa kuwa na ubabaishaji.

Alitaja mikakati waliojiwekea kwa mwaka 2019 ikiwemo kufuatilia miradi ya maendeleo inayoendelea katika halmashauri mbalimbali ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa kiwango kinachotakiwa.

Nombo alisema, watakaa na wadau kwa yale maeneo waliyoyabaini yana mianya ya rushwa na kuweka mikakati ya kuziba mianya hiyo.

Pia wataendelea kufanya uchunguzi kwa zile taarifa ambazo tayari wamezipokea na hasa za rushwa ndogo ambazo ni kero kubwa ndani ya jamii.

"Uchunguzi utakapobainika pasipo shaka kuwa kuna yeyote aliyejihusisha rushwa atafikishwa mahakamani "alisema Nombo.

Akizungumzia rushwa ya barabarani Nombo aliwaasa, wamiliki wa magari mbalimbali kutengeneza magari yao na kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani ili kujiepusha na mkono wa askari wa usalama barabarani.

Alitoa rai kwa madereva endapo wakiombwa rushwa na askari wa usalama barabarani wanapaswa kupiga simu namba 113 ili mhusika achukuliwe hatua stahiki.

MTU AKIITWA NA SPIKA NDUGAI LAZIMA AENDE-SHEIKH ALHAD

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema Spika wa Bunge akimuita mtu lazima aende.

Ametoa kauli hiyo leo Januari 18,2019 mbele ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kuratibu na kudhibiti Mawasiliano(TTMS) yaliyofanyika Mamlaka yaMamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA).

Sheikh Alhad wakati anaomba dua kwa ajili ya viongozi wa ngazi mbalimbali nchini alianza kwa kumuombea Rais Magufuli, Makamu wa Rais Samoa Suluhu Hassan ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge.

"Mwenyezi Mungu tunakuomba uumpe afya njema Spika wetu wa Bunge mzee Ndugai.Huyu Spika akimuita mtu lazima aende," amesema Sheikh Alhad huku baadhi ya watu waliokuwa wanasikiliza dua yake kuanza kucheka.

Haikufahamika mara moja walikuwa wanacheka nini lakini ukweli kauli ya Sheikh Alhad inakuja kipindi ambacho kunamjadala baada Spika Ndugai kumuita Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG)Profess Mussa Assad katika Kamati ya Bunge ya Kinga,Haki na Maadili ili ahojiwe baada ya kuelezea Bunge ni dhaifu.

Hata hivyo wakati Sheikh Alhad akisema kwamba mtu akiitwa na Spika Ndugai lazima aende inakuja kipindi ambavyo tayari CAG Profesa Assad amethibitisha ataitikia mwito wa Spika Januari 21 mwaka huu.

Kwa upande wa Spika jana wakati anazungumza na waandishi wa habari amesema ana uhakika Profesa Assad atakwenda kwenye kamati kuhojiwa ili apate fursa ya kuwasilisha utetezi wake na kwamba iwapo hatafika atajua nani muajiri wake.

RAIS DK.JOHN MAGUFULI AWAKUNA VIONGOZI WA DINI,WAMSHUKURU KWA KUWAJALI,KUWAPA NAFASI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

VIONGOZI wa dini mbalimbali nchini wamesema wanaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli kwa kudhihirisha namna ambavyo inatambua na kuthamini uwepo wa viongozi wa dini na kuwapa nafasi.

Wakizungumza leo Januari 18,2019 wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano TTMS yaliyofanyika eneo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ambapo mgeni rasmi ni Rais Dk.John Magufuli.

Viongozi hao wamemwambia Rais Dk.Magufuli kuwa tangu ameingia madarakani viongozi wa dini wamekuwa wakipewa nafasi kubwa na ya kuheshimiwa na hivyo wanamshukuru kwa namna ambavyo amewapa nafasi hiyo.Wamesema kwa nyakati tofauti viongozi wa dini wamekuwa wakijadiliana namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano ambavyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na viongozi hao wa dini.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhad Mussa Salum amesema Rais Magufuli amewapa nafasi kubwa viongozi wa dini kuliko kipindi chochote kile."Hakika viongozi wa dini tunayo sababu ya kukiri utawala huu wa Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa karibu nasi,tunashirikishwa kwenye mambo mbalimbali.

"Hivyo wamekubaliana kutambua kuwa Serikali ya inayoongozwa na Rais Magufuli imeamua kuwaweka karibu viongozi wa dini," amesema Sheikh Alhad na kuongeza viongozi wa dini wataendelea kumuombea yeye na viongozi wengine wa Serikali na wananchi wote kwa ujumla.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Full Gospell Bible Zacharia Kakobe amesema anaungana na Sheikh Alhad kwa kuelezea kuhusu namna ambavyo viongozi wa dini wanapewa kipaumbele kwenye Serikali.Amefafanua Rais Magufuli ameonesha unyenyekevu mbele ya viongozi wa dini na kwake madhehebu yote ya dini kwake yako sawa,hakuna dhehebu kubwa wala dogo.

"Rais kabla kuja hapa mbele wakati tumekaa pale tulikuwa tunajadiliana namna ambavyo umetoa kipaumbele kwa viongozi wa dini.Tunakushukuru kwa uamuzi wako wa kuwa karibu na viongozi wa dini," amesema Askofu Kakobe.

Kila viongozi wa dini ambaye alipata nafasi ya kukaribishwa kuomba dua alitumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Rais Magufuli amekuwa na hofu ya Mungu na amekuwa akimtanguliza Mungu kwa kila jambo na ndio maana amekuwa akifanikiwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. James Kilaba   katika  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA  Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019

WAZIRI MKUU AITAKA BODI YA PAMBA IFANYE KAZI KARIBU NA WAKUU WA MIKOA

$
0
0
*Ataka viongozi wote wasimamie kilimo hicho
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Bodi ya Pamba ifanye kazi kwa karibu na Wakuu wa Mikoa ili kuhakikisha msimu huu zao hilo linafikia malengo ya uzalishaji.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019) wakati akizungumza na Wakuu wa mikoa nane ya Mara, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga, Singida na Tabora inayolima pamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga.

Waziri Mkuu ameendesha kikao hicho kwa njia ya video (video conference) kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ili aweze kupata picha halisi ya kilimo cha pamba na hatua zilizofikiwa hadi sasa katika msimu huu wa kilimo.

“Lego letu mwaka huu 2019 ni kuzalisha tani zisizopungua 600,000. Wote mmeeleza kuwa wakulima wako kazini, pamba inalimwa, mnachosubiria ni dawa za kuuza wadudu waharibifu, na Bodi imeeleza kuhusu upatikanaji wa dawa hizo.”

Waziri Mkuu pia amesema viongozi wote wanapaswa kuwa karibu na wakulima ili waweze kubaini shida zao na kuzitatua kwa haraka. “Viongozi wote huko tuliko, zaidi ya asilimia 75 ya wa wananchi wetu ni wakulima. Kwa hiyo basi, tunapaswa tutenge asilimia zaidi ya 50 ya muda wa wetu kwenye mpango kazi ili tuweze kusimamia kilimo,” amesema.

“Wakuu wa mikoa peke yenu hamuwezi kufika kila mahali. Ni lazima maafisa ugani, maafisa kilimo na maafisa ushirika kwenye Halmashauri zetu waende kwa wakulima. Nikisema viongozi siyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya peke yao, Wizara nayo ina jukumu la kusimamia, viongozi wa AMCOS, vyama vikuu vya ushirika wote wawajibike kushirikiana na Serikali, waangilie ni nini tufanye ili kumkomboa mkulima.”

“Warajis wasaidizi, Ma-Ras wasaidizi wanaohusika na kilimo ni lazima washirikane kuhakikisha wakulima wetu wanajikwamua kutoka hapo walipo,” amesisitiza.

Mapema, akitoa taarifa ya maandilizi ya kilimo cha pamba kwa msimu huu, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba alisema hadi sasa wamekwishasambaza tani 27,000 za mbegu ambao ni zaidi ya asilimia 37 ikilinganishwa na usambazaji wa mbegu wa msimu uliopita.

“Hadi sasa mikoa yote imepata mbegu na zimeshapandwa na hali ya uotaji ni asilimia 100 kwani hatujapata malalamiko yoyote,” alisema. Kuhusu dawa za viuadudu, Mkurugenzi huyo alisema wameshanunua chupa milioni sasa na vinyunyizi 23,000.

Wakichangia mjadala kwenye kikao hicho, kwa nyakati tofauti, Wakuu hao wa mikoa waliunga mkono dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kufufua ushirika kama njia pekee ya kumkomboa mkulima.

Walisema kuna haja ya kutafuta njia mbadala ya kuwatoa wakulima wa pamba kwenye utegemezi wa mikopo ili waweze kupata mbegu na pembejeo na badala yake wapewe elimu ya kujiwekea akiba tangu wanapovuna na lkuuza mazao yao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la pamba ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Geita, Kagera, Singida na Tabora katika kikao alichokiongoza kwa njia ya video akiwa Ofisini kwake jijini Dodoma, Januari 18, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

REST IN PEACE HASSAN "WA MOROCCO" GOBBOS, BEKI NO.4 MAHIRI WA YANGA NA TAIFA STARS!!!

$
0
0
Beki hodari wa zamani wa YANGA na TAIFA STARS, HASSAN "WA MORROCO" GOBBOS amefariki dunia. Moja ya mechi yake aliyong'ara vilivyo ni ile ya mwaka 1972. Katika picha hii, Rais wa Sudan, JAFFAR MOHAMED AL- NIMEIRY anaonekana akisalimiana na wachezaji wa Taifa stars mwaka huo 1972.

Mh. NIMEIRY anaonekana akiongozwa na ABRAHAMAN JUMA, Kapteni wa Dar Es Salaam YOUNG AFRICANS na Timu ya Taifa huku pembeni akiwa ni Mwanamume wa shoka KITWANA MANARA "POPAT" aliyeweka rekodi kwa kuchezea Timu ya Taifa toka 1960 hadi 1976 na wa kwanza ni Chinga-Boy, MOHAMED CHUMA, beki Tatu Bora kuwahi kutokea Bongo! Anaeonekana kwa mbali ni ABDALLAH KIBADEN "KING" wa Simba.

Kipute hicho kilipigwa tarehe 4.7.1972 Shamba la bibi shamrashamra za sikukuu ya Sabasaba.

Jenerali NIMEIRY alimtania Mwalimu- "Ndugu yangu, umefilisika kiasi kwamba hata jezi hamna?. Mwalimu aliumia ila "aliua soo" kwa kusema We subiri, tutawafungeni tu"! Mwalimu baadae alitaka maelezo ya kina ni kwanini fedheha hiyo ilitupata.

Mtanange huo ulichezeshwa na mwamuzi GRATIAN MATOVU na Tanzania ikashinda 3-1. Magoli yakiwa yamefungwa na ABDALLAH KIBADEN "KING" (79) mchezaji aliyekuwa na chenga za maudhi na mfungaji hodari wa magoli. 


Magoli mengine mawili yalifungwa na GIBSON SEMBULI, Mshambuliaji nambari 9 wa kipekee  wa YANGA NA TAIFA STARS. Tanzania haijawahi kuwa na mchezaji mwenye kupiga mashuti makali kama SEMBULI! Makipa walikuwa wakikwepa mashuti yake hasa baada ya kumvunja mikono kipa "MACHAPATI"!! Katika mechi hiyo, SEMBULI alitupia kambani dk ya 65 na 68 ambapo bao lake la pili alifumua GRUNETI toka katikati ya uwanja na mpira kujaa wavuni na kushangiliwa mno!!!



GOBBOS aliyekuwa ndiye mchezaji kipenzi wa kocha wa Timu ya Taifa, Mkorea PAK YUNG TANG kutokana na kuwa msomi na mwepesi kuelewa mafunzo na mbinu, ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo kwa kuwadhibiti vilivyo washambuliaji wepesi wa Sudan wakiongozwa na DAHIESH.

Fedheha ya aina hiyo ilijirudia tena tarehe 9.10.2010 katika mechi ya Tanzania Vs Morocco "Kwa Mchina"(Sio Shamba la bibi) huku mgeni rasmi akiwa Mh. Rais KIKWETE ambapo CD ya nyimbo za taifa iligoma ikabidi ziimbwe kavukavu na wapenzi wa YANGA kubadili na kuimba MUNGU IBARIKI YANGA-FRIKA badala ya Mungu Ibariki Afrika!!!

Watanzania wengi hawajui ni kwanini Timu ya Taifa ilicheza vifua wazi mwaka 1972 na wengine wametumia fursa hiyo kutunga uongo. Sababu hasa ni hii:

"Jezi za Taifa Stars zilikuwa zimepelekwa kwa Mganga ili ishinde. Siku ya mechi tarehe 4.7.1972, Meneja wa Taifa Stars alimfuata Mganga nyumbani kwake lakini bahati mbaya hakumkuta. Kwakuwa Meneja alikwenda na basi la timu, ilibidi wachezaji watembee kwa miguu toka kambini Hostel ya Jeshi la Wokovu Kurasini. Ndio maana Timu yetu ilicheza vifua wazi siku hiyo na ikawa ni aibu kubwa kwa Taifa"
HASSAN CHABANGA DYAMWALE(Aliyekuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa mwaka 1972) kama alivyoeleza tarehe 10.10.2016.

REST IN PEACE HASSAN "WAMOROCCO" GOBBOS !

RUVUMA YA SHIKA NASAFI YA TATU KITAIFA KWA MIMBA ZA UTOTONI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme akiwa anaendelea na kampeni yake ya KATA FUNUA inayohusu wazazi wasiopeleka watoto shule kuchukuliwa hatua, Akiwa katika kikao cha kuratibu mpango wa kunusuru mkoa wa Ruvuma na tatizo la mimba za utotoni unaojulikana kwa jina la Adolesence Three Sixty uliofanyika January 17 mwaka huu mjini Songea mkoani Ruvuma , amesema tatizo la mimba mkoani humo ni kubwa ambapo kitaifa Ruvuma inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na mimba za utotoni kwa asilimia 32.

MOROGORO WATAKIWA WASIFICHE WAGONJWA WA UKOMA MAJUMBANI

$
0
0
Na WAMJW,Morogoro

Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na halmashauri zake wametakiwa kutowaficha wagonjwa wenye ukoma majumbani ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa hadi ifikapo mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari wakati wa ufunguzi wa semina ya uhamasishaji wa uongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya mvomero kuhusu maadhimisho ya miaka sitini (60) ya Ushirikiano kati ya serikali na Shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania(GLRA) pamoja na siku ya ukoma Duniani itakayofanyika Kitaifa wilayani Mvomero mwishoni mwa mwezi huu.

“Serikali inawajali sana wananchi wake hivyo wananchi hampaswi kuwaficha wagonjwa majumbani kwani dawa na vipimo zinatolewa bila malipo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini” Alisema Tandari
Aidha, alisema kuwa mkoa wake utaendelea kufanya kila liwezekanalo ili kutokomeza ugonjwa wa ukoma mkoani hapa kwani wajibu wao ni kuwasaidia watu hao kupona na kurudi kwenye kazi zao za kila siku watu wagonjwa hao wakishapatiwa dawa wanapona kabisa.

Kwa upande wa ongezeko la wagonjwa wilayani Mvomero Katibu Tawala huyo alisema sababu kubwa ya kuongezeka kwa wagonjwa hao wilayani hapo ni muingiliano hususan kwenye mashamba hivyo inakua rahisi maambukizi kuwa juu”tutafanya jitihada ili kuweza kufikia viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kutokomeza ugonjwa huu ambapo malengo ni mgonjwa mmoja kati ya watu elfu kumi.

Naye Mratibu wa Taifa wa ugonjwa wa Ukoma kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Deus Kamara alisema kuwa zipo halmashauri 20 ambazo hazijafikia kiwango cha kutokomeza ukoma nchini hivyo wizara kupitia mpango wa Taifa wa kutokomeza Kifua kikuu na Ukoma, Mikoa inatakiwa kutengeneza mkakati wa kuwasaka,kuwafikia, kuwaibua na kuwaweka katika matibabu stahili pamoja na kuzifikia kaya zote zenye wagonjwa wa ukoma kwa kufanyiwa uchunguzi ili wale ambao hawajaugua kuwapatia tiba kinga ili kutokomeza ukoma katika halmashauri zote ifikapo mwaka 2020.

Wakati huo huo Mwakilishii Mkazi wa Shirika la GLRA Buchard Rwamtoga alisema kuwa shirika hilo mwaka huu linatimiza miaka sitini(60) hapa nchini katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutokomeza ugonjwa wa ukoma Tanzania ikiwemo ya kuwajengea makazi bora familia 120 kutoka familia 739 ya watu waliougua ukoma hapa nchini.

“Dhamira yetu ni kuhakikisha kwamba kupitia michango ya wadau mbalimbali,shirika linaweza kusaidia mashirika na taasisi nyingine hasa mpango wa taifa wa kudhitibi ugonjwa wa kifua kikuu na Ukoma kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa haya”alisisitiza Rwamtoga.

Alitaja mafanikio waliyoyapata kwa miaka 60 Mwakilishi Mkazi huyo alisema shirika lake wameweza kutoa viatu maalum kwa walioathirika na ukoma pea 94,500 kwa watu 47, 250, miguu bandia magongo na baiskeli kwa watu 2, 655, magari 270 kwa Tanzania bara na Zanzibar,kusaidia masuala ya elimu kwa wanafunzi 3,765 pamoja na kuwezesha vikundi vya kusaidiana vipatavyo 50 vyenye wanachama 677 kwa familia za watu wenye kuishi na ugonjwa wa Ukoma nchini.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya ukoma mwaka huu ni “Tutokomeze ubaguzi ,Unyanyapaa na chuki dhidi ya waathirika wa Ukoma” na kitaifa yatafanyika kwenye kitongoji cha Chazi kijiji cha kigugu Wilayani Mvomero tarhe 27 mwezi huu.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali  na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
 Baadhi ya wakuu wa idara kutoka mkoa na wilaya wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa(hayupo pichani)ambapo wametakiwa kuhamasisha utekelezaji wa kuwaibua wagonjwa wa ukoma kutoka kila kaya ili kufanikisha malengo ya kutokomeza ugonjwa wa Ukoma ifikapo mwaka 2020
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Clifford Tandari akifungua semina ya Uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Mvomero katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya serikali  na shirika la German Leprosy and Tb Relief nchini Tanzania (GLRA).Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mohamed Utay na kushoto ni Mganga Wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Frank Jacob
Picha ya pamoja ya viongozi wa mkoa,wilaya,Wizara ya afya na GLRA mara baada ya ufunguzi

Shirika la posta lahamasisha ufundishwaji uandishi wa barua kwa wanafunzi ngazi zote

$
0
0
 Meneja Masoko Msaidizi wa Shirika la Posta mkoa wa Dar es Salaam, Evord Mwauzi amesema tatizo la uandishi wa barua kwa wanafunzi ikiwamo wa elimu ya juu bado ni tatizo kubwa. Meneja huyo,ameyasema hayo leo Januari 18.2019 wakati wa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Posta Afrika yaliyofanyika katika ofisi za Posta zilizopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala.
Amesema, katika utekelezaji wao wa majukumu, wamebaini kuwa uandishi wa barua hasa kwa wanafunzi wakiwamo wa vyuo vikuu bado ni tatizo kubwa hapa nchini. Akiwaelezea wanafunzi hao jinsi shirika hilo la posta linavyotoa huduma,Mwauzi ametoa wito kuwa  siku  zijazo baadhi ya huduma za Shirika la Posta ziingizwe katika mitaala ya elimu.

Amebainisha kuwa, Shirika la Posta limetenga siku ya Jumatano kwa ajili ya kutoa elimu hasa ya uandishi wa barua kwa wanafunzi na  huduma wanazozitoa na kuzitaka shule kuwatumia maombi  iwapo wanahitaji elimu hiyo. Ameongeza,  hali hiyo inatokana na kuwa namabadiliko ya teknolojia, kitu ambacho kimepelekea pia hata hali ya watu kumiliki masanduku ya posta kupungua, lakini utaratibu uliopo  mtu yoyote anayekuja nchini kuwekeza  lazima awe na sanduku la Posta.

Hata hivyo alibainisha kwa kwa sasa Shirika la Posta linatoa kila huduma kwa kutumia njia ya mtandao  ikiwamo huduma ya Post Code ambayo humfanya mtu, kufahamu nyumba ya mtu  anayoitafuta iko mahali gani ikiwa tu atakuwa akifahamu jina la mtaa na barabara husika.

Kwa upande wake, Afisa Masoko Mwandamizi wa shirika hilo, James Musyangi amesema maadhimisho hayo ya Siku ya Umoja wa Posta Afrika yalianzishwa Januari 17, mwaka 1980 yakiwa na lengo la kuhakikisha uelewa wa wafanyakazi wa Posta Afrika kuwa mmoja katika mambo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao na kutetea maslahi na hata katika nyanja ya elimu pia.

Aidha,Afisa Masoko huyo Mwandamizi aliwatembeza wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala katika vitengo mbalimbali vya shirika hilo ikiwamo maeneo ya kutuma barua za ndani na nje ya nchi na  ukaguzi wa mizigo inayotumwa kutoka ndani kwenda nje ya nchi na inayotoka nje ya nchi kuingia nchini kama ni halali na inastahili kulipiwa kodi ama la.

WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA UJENZI WA HOSPITALI YA UHURU CHAMWINO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019), Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya maeneo mengine.

“Uamuzi wenu wa kutenga maeneo ya miradi ya maendeleo umekuwa na tija, ndiyo maana Mheshimiwa Rais Magufuli aliposema ijengwe hospitali, hamkupata shida sababu eneo tayari lilikuwepo. Ninawapongeza wazee waliojitolea maeneo yao ili kuongeza kwenye eneo la hospitali,” amesema.

Wazee waliotoa maeneo yao ni Mzee Meshack Njamasi (ekari 5.50), Mzee Jobu Malogo (ekari 3.50) na Bw. Nehemia Mwikwi (ekari 4.50). Ekari 95.5 zilizobakia, zimetolewa na Seriakli ya kijiji hicho.

Waziri Mkuu aliwataka wakazi wa wilaya ya Chamwino wasibweteke bali wajipange na kila mmoja ajipange kufanya kazi kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akihimiza. “Ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea hivi sasa ni fursa kwenu. Na ujio wa hospitali hii ni fursa nyingine kwa wana-Chamwino hasa kwa vile ujenzi wake utatumia mfumo wa force account ambao unatoa fursa kwa wanajamii kushiriki kazi za miradi ya eneo husika,” amesema.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa hospitali hiyo yenye hadhi ya wilaya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoelekeza wananchi wapatiwe huduma za matibabu huko huko waliko. “Hadi sasa tumeshajenga vituo vya afya 350 ili kusogeza huduma kwa wananchi na jumla ya hospitali za wilaya 67, zinajengwa nchi nzima kwa mwaka huu,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa vijiji jirani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. Selemani Jafo alisema eneo la ujenzi wa hospitali hiyo liko umbali wa kilometa mbili kutoka barabara kuu ya Dar es Salaaam-Dodoma na kilometa tatu kutoka Ikulu ya Chamwino.

Naye, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine aliwataka wakazi hao wachangamkie fursa hiyo kwa kusomba mawe, mchango, maji na kwamba Kamati za usimamizi wa ujenzi zitapaswa kusimamiwa na wanakijiji.

Aliwataka wakazi hao wasiishie kwenye lengo la kuwa na hospitali ya wilaya, bali walenge kujenga hospitali yenye hadhi ya mkoa kwa kadri bajeti itakavyoruhusu.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Bilinith Mahenge alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni wa hadhi ya wilaya ikiwa na nyongeza ya huduma za wagonjwa wa dharura na wagonjwa mahututi (Emergency Department and Critical Care Unit).

Alimshukru Rais Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa hospitali hiyo sh. milioni 995.18 ambazo zilipaswa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru, Desemba 9, mwaka jana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutuongezea kiasi kingine cha fedha cha sh. bilioni 2.35 na kutufanya sasa tuwe na sh. bilioni 3.22 za ujenzi huo,” alisema.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge  (kulia) wakati alipokagua eneo itakapojengwa Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha michoro ya majengo ya Hospitali ya Uhuru inayotarajiwa kujengwa katika  kijiji cha Maduma wilayani Chamwino wakati alipokagua eneo hilo, Januari 18, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (katikati) na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile wakati alipokagua eneo itakapojengwa  Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee, Meshack Njamasi, mmoja wa wananchi waliotoa maeneo yao bure kwa serikali ili yatumike kwa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru  Mzee,  Job Mahogo, mmoja wa wananchi waliotoa maeneo yao bure kwa serikali ili yatumike kwa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino, Januari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAMKO LA HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA - WAZIRI UMMY MWALIMU

UMOJA WA AFRIKA SASA WATOA NENO KUHUSU MATOKEO UCHAGUZI WA RAIS JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

$
0
0

Na Ripota Wetu

UMOJA wa Afrika umetoa mwito wa kuaihirisha kwa muda wa kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa Rais unaozusha mabishano katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa sababu ya "shaka shaka kubwa ."

Imeelezwa kuwa Wawakilishi wa Umoja wa Afrika wamekutana leo Januari 18,2019 Mjini Addis Ababa na kisha wakakubaliana kutuma ujumbe wa ngazi ya juu mjini Kinshasa kwa lengo la kusaka njia za kuupatia ufumbuzi mzozo 
wa kisiasa.

Viongozi wa Taifa na Serikali wanaohudhuria mkutano huo wamekiri kuwa kuna mashaka makubwa hasa kuhusu ulinganifu wa matokeo ya awali kama yalivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) na yale ya kura zilizopigwa.

Umoja wa Afrika umesema katika taarifa yake. "Ingawa hali ni tulivu hadi sasa, lakini wasi wasi umetanda pia, amesema mwenyejkiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat mbele ya viongozi wakiwemo pia wale wa Afrika 

Kusini, Zambia, na Jamhuri ya Congo waliokutana kuzungumzia matokeo yanayobishwa ya uchaguzi katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo. Serikali mjini Kinshasa imeukosoa wito wa Umoja wa Afrika na kusema korti ya nchi hiyo ni huru. Korti ya Katiba inasikiliza malalamiko ya Martin Fayulu dhidi ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais.

CHANZO -DW 

WAZIRI MAMBO YA NCHI ZA NJE UJERUMAN HEIKO MAAS AFANYA ZIARA MJINI MOSCOW

$
0
0

WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Heiko Maas yuko ziarani mjini Moscow kwa mazungumzo pamoja na 

Waziri mwenzake Sergei Lawrov kuhusu mzozo wa Ukraine na vita nchini Syria. 

Kwa mujibu wa DW ni kwamba mvutano kati ya Urusi na Ukraine umezidi makali mnamo siku za hivi karibuni baada 

ya korti moja ya mjini Moscow kurefusha hadi kati kati ya mwezi wa April unaokuja, muda wa kushikiliwa kizuwizini 

wanamaji 24 wa Ukraine waliokamatwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana . 

Baada ya mazungumzo yake mjini Moscow, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani Heiko Maas amepangiwa 

kwenda Kiew baadae leo kwa mazungumzo pamoja na waziri mwenzake Pawel Klimkin.

CHANZO-DW

SEKTA YA AFYA YAENDELEA KUPAA - SERIKALI

$
0
0
Na WAMJW - DOM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Sekta ya Afya nchini yaendelea kukua kwa kasi, kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Huduma kwa Wananchi zikiwemo upatikanaji wa Dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, huduma za chanjo, huduma za afya ya uzazi na mtoto na Huduma za Dharura.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari na baadhi ya viongozi wa Wizara, kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa Katika mwaka 2018, jumla ya wajawazito 2,086, 930 walihudhuria na kuandikishwa Kliniki, ikilinganishwa na wajawazito 2,009,879 Mwaka 2017, huku mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto unaelekeza wajawazito kuanza huduma mapema kabla ya majuma 12 ya ujauzito na kuhudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa, Katika kipindi cha mwaka 2018 jumla ya watoto 1,568,832 walizaliwa ikilinganishwa na Watoto 1,498,488 mwaka 2017, huku wakipatiwa huduma mbalimbali za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayowaathiri Watoto ikiwemo ugonjwa Kupooza, Kuharisha, Pepopunda, Pneumonia, homa ya ini na Surua.

"Katika kipindi cha mwaka 2018 hali ya chanjo kwa Watoto nchini imeendelea kuwa katika kiwango cha juu zaidi ya asilimia 85 ya kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kama inavyoonyeshaa katik hapa chini" Alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo nWaziri Ummy amesema mwaka 2018 kumetokea jumla ya vifo 20,087 ikilinganishwa na vifo 19,693 mwaka 2017, huku Katika kipindi cha miaka yote miwili 2017 na 2018, homa ya mapafu imeongoza kwa kusababisha vifo, ambapo kwa mwaka 2017, imechangia asilimia 18.2 ya vifo vyote na mwaka 2018 imechangia kwa asilimia 12.9 ya vifo vyote. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Mwaka 2018, ugonjwa usio wa kuambukiza (shinikizo la damu) umejitokeza katika magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo ambapo umechangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa Hali ya upatikanaji wa Dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini imeendelea kuimarika, hii ni kutokana na Serikali kuongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Milioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Shilingi milioni 251 mwaka 2016/17 na Shilingi 270 mwaka 2018/19.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa hali ya upatikanaji wa Damu Salama ambapo katika kipindi cha mwaka 2018, huku jumla ya chupa za damu salama 307,835 sawa na asilimia 85.5 ya lengo zilikusanywa ikilinganishwa na chupa 233,933 mwaka 2017, huku akiwahasa Wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuendelea kuokoa maisha ya wahitaji.

"Chupa zote 307,835 zilizokusanywa zilipimwa makundi ya damu pamoja na magonjwa makuu manne ambayo ni Ukimwi (HIV,) Homa ya Ini B na C (HBV, HCV) na Kaswende (Syphilis). Jumla ya chupa 262,283 sawa na asilimia 85.3 zilikuwa salama na kusambazwa katika hospitali kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu." Alisema Waziri Ummy. 

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa, katika mwaka 2018 jumla watu 47,967 waligundulika kuwa na vijidudu vya Kifua kikuu ikilinganishwa na wagonjwa 44,714 waliogunduliwa mwaka 2017., huku akisisitiza kuwa tatizo la ugonjwa wa Kifua Kikuu limeendelea kuwepo takribani mikoa yote nchini.

kwa upande mwingine, Waziri Ummya amesema kuwa, hadi kufikia Desemba 2018, jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya vilifikia 7,768 kutoka vituo 7,435 mwaka 2017 sawa na ongezeko la vituo 333 kwa mwaka, amedai kuwa Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 71 ya vituo vya kutolea huduma; Mashirika ya dini asilimia 12, Taasisi za Serikali asilimia 3 na vituo binafisi asilimia 15.

Sambamba na hilo, waziri Ummy amesema kuwa, hadi kufikia Desemba mwaka 2018, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na jumla ya wanachama 899,654 na ikihudumia jumla ya wanufaika 4,219,192 sawa na asilimia 8 ya Watanzania wote.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakar Kambi.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakifuatilia tamko kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018 kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MADINI KUFANYA MAZUNGUMZO BARABARA MGODI WA MAKAA, NGAKA

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Mbinga 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema Wizara yake itafanya mazungumzo na Mamlaka zinazohusika na masuala ya barabara ili kuweka mazingira bora ya miundombinu hiyo kwa lengo la kuwezesha biashara ya makaa ya mawe na shughuli za uzalishaji makaa hayo kufanyika kwa ufanisi zaidi katika mgodi wa makaa ya mawe Ngaka, uliopo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma. 

Alisema mgodi huo wa Ngaka chini ya kampuni ya TANCOAL ndiyo taswira ya uzalishaji makaa ya mawe nchini hivyo, serikali haina budi kuweka mazingira bora yatakayowezesha kupunguza gharama za uendeshaji jambo ambalo litapunguza gharama kwa walaji wa nje na ndani ikizingatiwa kuwa, ni kampuni ya Kimataifa kutokana na kuhudumia wateja kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Rwanda, Burundi, Uganda nchi na nyingine. 

Kauli ya Naibu Waziri Nyongo inafuatia changamoto ya barabara iliyowasilishwa kwake na Meneja Mgodi wa TANCOAL Mhandisi David Kamenya, ambaye alimweleza Naibu Waziri kuwa, ukosefu wa miundombinu imara ikiwemo madaraja imechangia shughuli za upakiaji makaa hayo kutokuzidi tani 20 kwa kila gari jambo ambalo linapelekea kuwepo na foleni kubwa kutokana na uhitaji wa makaa hayo. 

Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara mgodini hapo Januari 17 ikilenga kukagua shughuli za madini mkoani Ruvuma pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali ambazo mgodi huo unakabiliana nazo katika utekelezaji wa shughuli zake. 

Pamoja na kuridhia ombi hilo, Naibu Waziri aliitaka kampuni hiyo kuongeza kasi ya uzalishaji kutokana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika soko la nje na ndani na kuitaka kutobweteka huku ikitakiwa kuboresha huduma inazotoa ikiwemo kuongeza vifaa vya kazi. 

“Nimeona changamoto ya barabara. Kama serikali ni lazima tuifanyie kazi changamoto hii ili kuwezesha uzalishaji zaidi wa makaa. Sisi tutaendelea kutoa leseni kwa wazalishaji wengine ili kuweka ushindani, hivyo msibeweteke, tunahitaji sana makaa haya kwa uchumi wa taifa letu kwa kuwa tunayo hazina ya kutosha ya rasilimali hii,” alisema Nyongo. 

Aliongeza kuwa, kufuatia serikali kuweka zuio la uingizaji makaa kutoka nje, ni lazima kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa madini hayo ikiwemo kuwezesha biashara hiyo na kuutaja mgodi wa makaa ya mawe wa Kabulo unaomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwa ni eneo jingine ambalo miundombinu ya barabara ni lazima iboreshwe kuwezesha ufanisi zaidi wa shughuli za uzalishaji madini hayo. 

Alisema kuwa, ili serikali iendelee kupata mrabaha zaidi kutokana na rasilimali hiyo suala hilo lazima lichukuliwe kwa uzito ili kuongeza mapato zaidi. 

Aidha, akijibu ombi la kampuni hiyo kutaka kurudishiwa eneo ambalo lilitolewa kwa ajili ya Kiwanda cha Dangote na Rais John Magufuli, kwa kuwa bado haijanza kuchimba mpaka sasa, Naibu Waziri Nyongo alizitaka pande zote ikiwemo wizara na kampuni hizo kukutana Januari 22 mara baada ya kikao cha wadau wa sekta ya madini ili kujadili suala hilo ili hatimaye shughuli za uzalishaji zianze katika eneo hilo. 

Mbali na hilo, kampuni hiyo ilimwomba Naibu Waziri kuwezesha upatikanaji wa leseni mbili zilizoombwa na kampuni hiyo ikilenga kutumia makaa hayo kuzalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya mgodi. Naibu Waziri aliahidi kuwa, kupitia Tume ya Madini, suala hilo litakuwa limekamilika ndani ya kipindi cha wiki mbili. 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliitaka Halmashauri ya Mbinga kubuni miradi kwa ajili ya vijana na wanawake yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya makaa ya mawe kwa ajili ya matumizi ya majumbani na kuachana na matumizi ya mkaa kwa kuwa umekuwa ukisababisha uharibifu wa mazingira. 

Wakati huo huo, akizungumzia suala la Mrabaha wa serikali wa asilimia 3, alisema usilipwe kwa bei ya maeneo ya uchimbaji bali ulipwe kwa bei ya sokoni. Hivyo, aliwataka wazalishaji wote na Maafisa wa Tume ya Madini kuhakikisha wanatoza bei ya sokoni na siyo ya uzalishaji. 

Kwa upande wake, Meneja wa mgodi Mhandisi David Kamenya akizungumzia ubora wa makaa hayo, alisema kuwa, Makaa ya Ngaka yana ubora wa kimataifa na ndiyo sababu imepelekea kupata wateja wengi kutoka nchi mbalimbali na kuongeza kwamba makaa hayo yana uwezo wa kufanya matumizi mbalimbali na kuongeza kuwa, kwa siku kampuni hiyo inapakia idadi ya magari yapatayo 100. 

AKizungumzia malengo ya baaaye, alisema kuwa, idadi ya mashine ndani ya siku chache zinatarajiwa kuongezwa na kwamba kampuni imelenga kuzalisha hadi tani 5,000 kwa siku kutoka 3,000 za sasa. 

Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana na akina mama, alisema kuwa, tayari kipo kikundi cha wakina Mama cha Mbarawala ambacho kimewezeshwa na mgodi huo kwa kupatiwa mafunzo ya namna ya kuandaa makaa hayo maalum kwa matumizi ya majumbani na kuongeza kuwa, hivi karibuni kikundi hicho kimepata Cheti cha ubora kutoka shirika la Viwango nchini (TBS) jambo ambalo litawezesha kikundi hicho kuuza makaa yake kwa ajili ya matumizi ya majumbani na hivyo kupunguza matumizi ya mkaa unaotokana na kukatwa miti. 

Pia, Mhandisi Kamenya alimweleza Naibu Waziri Nyongo kuwa, mbali na kupatiwa mafunzo kikundi hicho pia kimepatiwa mashine ambayo inauwezo wa kuzalisha tani mbili za makaa hayo kwa saa. 

Akishukuru kwa niaba ya kikundi, Meneja Usimamizi wa Mbarawala, Joyce Haule alisema kuwa, wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha na kwamba kikundi kinalenga kuzalisha tani 10 kwa siku na kuongeza kuwa, hadi sasa tayari kimepata wateja kutoka maeneo mbalimbali zikiwemo nchi za Rwanda ambao awali walitaka kwanza kikundi hicho kuwa na cheti cha ubora wa makaa hayo. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Cosmas Ishenyi alimweleza Naibu Waziri kuwa, kama Wilaya itahakikisha kuwa, inashirikiana na mamlaka zinazohusika kuweka mazingira bora ya kuwezesha mundombinu bora ya barabaraba ili TANCOAL iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi. 

Katika hatua nyingine, akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Prof. Riziki Shemdoe, ofisini kwake Januari 18, Naibu Waziri alimweleza Prof. Shemdoe umuhimu wa kuwezesha miundombinu ya barabra kuelekea katika mgodi huo wa Ngaka. 

Pia, Naibu Waziri alimweleza Prof. Riziki kuhusu mipango ya Serikali ya kuwa na vituo kwa ajili ya biashara ya madini na umuhimu wa mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli hizo. “ Tunataka kuwa na utaratibu wa kuwa na maeneo ya kuuza na kununua madini ili kuwa na utaratibu maalumu,” aliongeza 

Kwa upande wake, Prof. Shemdoe alimwomba Naibu Waziri kusaidia upatikanaji wa wawekezaji kwa ajili ya viwanda vya kuchenjua dhahabu mkoani humo na kukumbushia suala la uchimbaji madini katika Mto Muhuwesi. 

TANCOAL ni kampuni yenye ubia na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambapo serikali inamiliki hisa kwa asilimia 30. 
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akiongozwa na Meneja wa mgodi wa Makaa ya Mawe TANCOAL, David Kamenya (aliyenyoosha mikono) kutembelea maeneo ambapo uchimbaji wa makaa hayo unafanywa katika machibo yaliyopo Wilayni Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akiongozwa na Meneja wa mgodi wa Makaa ya Mawe TANCOAL, David Kamenya (aliyenyoosha mikono) kutembelea maeneo ambapo uchimbaji wa makaa hayo unafanywa katika machibo yaliyopo Wilayni Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akieleza jambo baada ya kutembelea eneo ambalo shughuli za upakiaji makaa ya mawe zinafanywa na mgodi wa TANCOAL kwa ajili ya makaa hayo kusafirishwa maenezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Makaa ya Mawe wa TANCOAL 
Baadhi ya magari yakisubiri kupakia makaa ya mawe tayari kwa usafirishwa maeneo mbalimbali ndani nan je ya nchi,

Sughuli za upakiaji Mkaa ya Mawe zikiendelea katika Mgodi wa TANCOALtayari kwa ajili ya kusafirishwa maeneo mbalimbali.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Makaa ya Mawe wa TANCOAL. Wengine ni baadhi ya Wataala kutoka ofisi ya Madini Songea na baadhi viongozi wa wachimbaji wadogo Mkoa wa Ruvuma. 

MNYAMA SIMBA LEO KWA WACONGOMANI- WANYAMBILIS AS VITA CLUB!!!

$
0
0
1. Usuli:
Mnyama SIMBA leo majira ya saa 11 jioni kwa saa za DRC au saa 1 ya usiku kwa Bongo, atashuka dimba la Stade de Martyr, jijini Kinshasa, kupambana na ASSOCIATION SPORTIVE VITA CLUB@ AS VITA CLUB "The Black Dolphins" , mabingwa wa DRC, katika mtanange ambao kocha mwenye uzoefu wa AS VITA, mzee mzima FLORENT IBENGE amesema "lije jua, ije mvua, SIMBA lazma ichezee kichapo"!.

AL AHLY ya Masri ndiyo timu inayoongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi 4 baada ya usiku wa jana kwenda sare ya 1-1 ugenini Algeria dhidi ya JS SAOURA. Katika mechi hiyo, Al Ahly, kama kawaida yake ugenini, ilikuwa ikitafuta sare tu na ikawaikipoteza muda mara kwa mara. Js Saoura ilipata bao dk ya 59 na Al Ahly ikasawazisha dk ya 85.

2. AS VITA kama YANGA!!!:

Timu ya AS VITA inatumia rangi 3 zitumiwazo na YANGA yaani njano, kijani na nyeusi na manazi wa timu hiyo huwa na kawaida ya kula mihogo na nyama ya nyani kabla ya mechi ambayo wanaamini inawapa nguvu na huishangilia timu yao mwanzo mwenga hivyo SIMBA ijitayarishe kisaikolojia kukumbana na kelele nyingi sana uwanjani!.

3.  SIMBA Yafikia Hoteli ya DC MOTEMA PEMBE!

SIMBA imefanya figisu baada ya kuwasili Kinshasa alhamis kwa kuamua kufikia hoteli ya Venus, iliyopo nje kidogo ya Kinshasa, ambayo ndiyo hutumiwa na DC MOTEMA PEMBE, wapinzani wakubwa wa AS VITA.


Kitendo hicho kimewakasirisha wapenzi wa AS VITA ambao sasa wameipa chagizo kubwa timu yao kuiangushia kipondo SIMBA kama inavyoifanyaga DC MOTEMA PEMBE!. Jiji la Kinshasa siku ya Ijumaa maongezi yalikuwa ni mechi hii ambapo suala la  matokeo ya uchaguzi liliwekwa kando na kwa hakika leo mtoto hatumwi dukani.!.


4. SIMBA Vs AS VITA 1978:

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa SIMBA kupambana na AS VITA katika michuano hiyo.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1978 timu hizo zilipopambana katika raundi ya pili ya michuano hii. Katika mechi ya kwanza iliyopigwa 'Shamba la bibi', Dsm, AS VITA ikicheza pungufu kwa takriban muda wote wa mchezo, baada ya mchezaji wao, BAKU MONDELA KAZADI, kulimwa kadi nyekundu dk 10, iliitandika SIMBA kwa bao 1-0.

Kwenye mechi ya marudiano ya kihistoria iliyopigwa jijini Kinshasa, kwenye uwanja unaopigwa mechi ya leo wa Stade de Martyr, unaoingiza mtu 70.000 wenye nyasi bandia,  Mnyama SIMBA alionesha uoga ambao hata "Mwoga-mkongwe" JOSE MOURINHO anasubiri kwani MOURINHO hupaki basi lakini SIMBA siku hiyo jijini Kinshasa ilipaki Basi, Meli na Treni kwa wakati mmoja!.

Hii ni kutokana na timu ya AS VITA kuogopewa sana barani Afrika enzi hizo kwa kuwa na sifa ya kutopoteza mchezo kwenye uwanja huo ambao huitwa Machinjioni . Katika mtanange huo, SIMBA ilielemewa mno kwani ilichezewa robo uwanja( na sio nusu uwanja) na haikuwezi kupiga hata shuti moja kwenye lango la AS VITA kwa dakika zote 90. Ni mchezaji mmoja tu aliyekuwa akijitahidi walau kufika katikati ya uwanja, GEORGE "BEST" KULAGWA. Huyu alikuwa winga hodari wa SIMBA aliyepewa jina la "BEST" kwa kufananishwa na GEORGE BEST, mmoja wa wachezaji hodari kabisa kuwahi kuichezea MAN U.

AS VITA ilikuwa na safu ya ushambuliaji matata sana ya akina LOFOMBO, LOBILO na mkali wao, JEAN ADELARDE MAKU MAYANGA. MAYANGA, aliyeitungua SIMBA mechi ya Dsm, alikuwa mshambuliaji aliyekuwa akiogopewa bara zima la Afrika kwani alikuwa ni mshambuliaji mahiri sana mwenye sifa zote. Mashambulizi "yaliyosukumiwa ndani" ya 18 za SIMBA siku hiyo na washambuliaji hao wenye uchu mkali, hayakuwa ya nchi hiyo!!!.

5. TWINS wapewa majina ya OMAR MAHADHI:

OMAR MAHADHI "BIN JABIR", kipa hodari sana wa Mnyama SIMBA" na "Tanzania One" wa wakati huo, alifanya mambo makubwa sana ya kihistoria na kuwa shujaa wa SIMBA siku.

Katika mechi hiyo, MAHADHI alithibitisha kuwa CAF haikukosea kumchagua katika TIMU YA AFRIKA mwaka 1973 baada ya kumalizika kwa michuano ya "All Africa games" nchini Nigeria. Katika michuano hiyo, MAHADHI na MAULID DILINGA "MEXICO" wa YANGA walichaguliwa baada ya kuonesha uwezo mkubwa sana. Katika michuano hiyo, Taifa Stars ilitoka sare 0-0 na Nigeria A, ikaifunga Nigeria B 2-1, ikazifunga Ghana 1-0 na Togo 1-0. Katika hatua inayofuata, iliyochezwa kwa ligi tena, Taifa stars ilitoka sare 1-1 na Nigeria A, ikatoka sare na Misri 1-1 kabla ya kufungwa na Algeria 2-1 na kuondolewa mashindanoni. DILUNGA alifunga katika karibu kila mechi na kwa hakika YANGA haijawahi kuwa na namba 10 bora kama mtaalam DILUNGA! Uwezo mkubwa wa MAHADHI katika michuano hizo ndio uliopelekea achaguliwe Timu ya Afrika.

Katika mechi dhidi ya AS VITA, beki ya SIMBA ilikuwa ikikatika mara kwa mara na kama si uhodari wa MAHADHI basi SIMBA ingeweka rekodi ya kuwa timu ya Bongo iliyofungwa magoli mengi zaidi nje ya nchi!  Kwa wale waliomuona DAVID DE GEA wa MAN U akiokoa magoli ya wazi dhidi ya TOTTENHAM katika kipindi cha pili, jumapili ya tarehe 13.1.2019, wanapaswa kutambua kuwa MAHADHI yeye alifanya kama alivyofanya DAVID DE GEA  ila MAHADHI alifanya kwa vipindi vyote viwili kwani kila wakati alijikuta yuko uso kwa uso na akina MAYANGA, LOBILO na LOFOMBO!!! Hatimaye, AS VITA wakabahatisha kagoli kamoja kalikofungwa kwa umahiri wa hali ya juu na MAYANGA ambaye baada ya kukusanya kijiji, alijifanya kama anajikuna na kuachia atomic missile iliyogonga besela na kujaa wavuni! SIMBA ikatolewa kwa jumla ya mabao 2-0. Baada tu ya refa kupuliza kipyenga kumaliza mechi hiyo, MAYANGA alimkibilia MAHADHI na kumkumbatia na kumpa hongera kwa uhodari mkubwa aliouonesha!.

SADIQUE MUSIMBWA, mpenzi wa AS VITA, aliyefurahishwa sana na uwezo wa MAHADHI, na ambaye mkewe alijifungua watoto mapacha wa kiume masaa machache baada ya mechi hiyo, aliwapa 'twins' wake majina ya kipa huyo mahiri wa SIMBA ambapo mmoja alimwita OMAR na mwingine MAHADHI.

Magazeti yote ya michezo ya kesho yake jijini Kinshasa yalitamalaki picha za MAHADHI akikumbatiana na MAYANGA na picha za 'twins" hao!

Itapendeza sana iwapo "Twins' hao, ambao sasa wana umri wa miaka 41, wataushuhudia mtanange huo na baadae kuonana  na kupiga picha na viongozi na wachezaji wa SIMBA kama kumbukizi ya mambo makubwa aliyofanya kipa wao katika mtanange huo wa mwaka 1978.

Ili SIMBA isichezee kichapo leo, AISHI MANURA itabidi afanye walau robo ya mambo aliyofanya MAHADHI mwaka 1978!.

6. Mafanikio ya AS VITA:

AS VITA ni timu iliyoshiriki michuano mbalimbali barani Afrika hivyo ina uzoefu mkubwa:

6.1 AS VITA ilikuwa Mabingwa wa Afrika mwaka 1973;

6.2 AS VITA imeingia fainali ya ubingwa wa Afrika 1982 na 2014;

6.3 AS VITA iliingia fainali ya CAF CONFEDERATIONS CUP mwaka jana Disemba 2018 (AS VITA ilifungwa 3-0 na Raja Casablanca ugenini na yenyewe ikaitandika RAJA 3-1 "machinjioni" Stade de Martyr).

7. Mfumo wa AS VITA ni kushambulia tu:

SIMBA LUWALA/LUNYASI lazma itambue kuwa leo inakutana na "Mziki mnene" kwani timu ya AS VITA huwa haina hekaya za abunuwasi wala hadithi za Esopo za kupaki basi wao ni kushambulia tu muda wote ikiwa na wachezaji wenye mbio na stamina ya hali ya juu. Sifa yao kubwa ni upigaji vichwa ambapo 60% ya magoli yao ni ya vichwa hivyo SIMBA isiruhusu kabisa mipira ya faulu, krosi au kona. 

Katika mechi yao dhidi ya AL AHLY nchini Masri, AS VITA ilicheza muda mrefu na wachezaji 10 baada ya mchezaji wao CHARLES KALONJI kutolewa dk 36. AL AHLY, licha ya kuwa na numerical advantage, ilisumbuka sana na ikafanikiwa kupata bao la kulazimisha dk ya 65 na penati ya kimazabe dk ya 79 hivyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

8. Jean Mac Makusu Mundele @ MUNDENDE!!!

Mshambuliaji huyu mahiri wa AS VITA na timu ya taifa ya DRC ndiye kipenzi cha manazi wa AS VITA. Ni mchezaji mwenye umbo dogo lakini mjanja sana na mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu. Yeye "husukumia ndani magoli ya aina zote yaani ya kichwa, mguu wa kulia, mguu wa kushoto na hupenda sana kufunga magoli ya "Tikitaka".

MAKUSU alikuwa mfungaji bora wa pili kwenye CAF Confederations Cup 2018.

9. AS VITA HAIFUNGWAGI NYUMBANI:

Moja ya sifa kubwa ya timu hii ni kutofungika katika uwanja wake wa nyumbani, Stade de Martyr. Hii imepelekea manazi wa DC MOTEMA PEMBE kuwatania AS VITA kwamba walizika nyani 100 wakati wa kujenga uwanja huo( nyani huliwa sana na wacongoman).

9.1 Katika mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi ya DRC, AS VITA haijafungwa hata mechi moja uwanja wa nyumbani.

9.2. AS VITA haikufungwa hata mechi moja katika mechi za nyumbani kwenye CAF CONFEDERATIONS CUP 2018.

9.3 AS VITA haijafungwa hata mechi moja nyumbani kwenye hii Champions league msimu huu.


JE, MNYAMA SIMBA "ATATOKA" LEO?

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) jinsi maji yanavyovunwa katika Mtambo wa Ruvu Juu - Ruvu Kibaha - Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakiwa wamefika katika mtambo wa Ruvu Juu ikiwa ni ziara kwa ajili ya kujifunza baadhi ya mambo mbali mbali. 
Ziara ikiendelea.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya mashine za maji eneo la Ruvu Juu walipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza. 
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaongoza Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya kusafisha maji enwalipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza. 
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akitoa maelezo. machache. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakionyeshwa mitambo ya mashine za maji.
Meneja wa DAWASA Kibaha - Pwani, Crossman Makere akitoa ripoti mbele ya Wakurugenzi Bosi ya DAWASA mara baada ya kutembelea ofisini hapo. 
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakiwasili katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba, Ubungo kujionea walipofikia. 
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange. 
Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe na Kibaha injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kufika eneo la Minarani Kisarawe, Pwani kujionea ujenzi wa tanki la maji. 
Mafundi wakiendelea na kazi. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange akiwa na Wajumbe wa Bodi wakitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yahusuyo miradi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kujifunza wanavyofanyakazi. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi wa maeneo yanayozunguka miradi ya maji ikiwemo miundo mbinu kuweza kuitunza ili iweze kudumu. Jenerali Mstaafu Mwamunyage akiwa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA wameanza ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi mbalimbali ya mamlaka hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

 Akizungumza baada ya kumaliza siku ya kwanza Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kuwapatia maji safi na salama. "Niwaombe wananchi watunze miundo mbinu ya maji maana ujenzi wake ni gharama sana tofauti na wao wanavyofikiria wanapoona maji yamewafia majumba," amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange. Ziara hiyo ilianzia katika chanzo cha maji cha Mto Ruvu Juu, Ofisi ya DAWASA ya Kibaha, Tenki la Kibamba lenye ujazo wa lita Milioni 10 na ujenzi wa tanki la Kisarawe lenye ujazo wa Lita Milioni sita. 

Katika ziara yake Mwamunyage ametembelea pia Ujenzi wa mradi wa bomba la maji kutoka Kibamba (Bomba kuu la kusafirisha maji kutoka Ruvu juu) hadi Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha maji Lita Milioni 4 kwa siku na wananchi mbalimbali wa maeneo ya Kisarawe watafaidika na maji. Amesema kuwa, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa tenki hilo na kama wakandarasi wataendelea hivyo kufikia mwezi Septemba mwaka huu ujenzi utakua umekamilika. 

Katika mradi huo Jenerali Mstaafu Mwamunyange ametembelea tenki la maji lenye ukubwa wa lita milioni 10 kwenye eneo la Kibamba na kuoneshwa pampu nne za kusukumia maji hadi Kisarawe. Kazi zingine zinazoendelea kutekelezwa na Mamlaka hiyo kwenye mradi wa Kisarawe ni ujenzi wa bomba la kusafirishia maji lenye kipenyo cha inchi 16 urefu wa Km 15.65, mabomba ya kusafirisha na kusambaza maji kwenda kwenye maeneo ya Viwanda lenye urefu wa Km 5.15 na kipenyo cha inchi 12 na lingine likiwa ni urefu wa Km 8 na kipenyo cha inchi 8.9 Ujenzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji lenye ukubwa wa Lita milioni 6 katika eneo la Mnarani Kisarawe na ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba. Maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni kata ya Kisarawe, Kata ya Kazimzumbwi pamoja na maeneo ya Kiluvya, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya viwanda.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images