Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

RC RUVUMA AMWAGIZA DC TUNDURU KUKAMATA KWA MTINDO WA KATA FUNUA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akishiriki ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Frank Weston iliyopo Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
......................
Agizo la Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA la kuhakikisha wanafunzi wanaopaswa kuanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza wanakwenda shule limeanza kutekelezwa katika Mkoa wa RUVUMA. Ambapo Mkuu wa Mkoa huo Christine Mndeme amefanya ziara ya kukagua mapokezi ya wanafunzi wa darasa la kwanza, kidato cha kwanza na kukagua miundombinu ya madarasa katika Wilaya ya TUNDURU. Sambamba na kumpa maagizo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera kuwachukulia hatua wazazi ambao wameshindwa kuwapeleka watoto wa shule ” DC we kata funua “.

WAKULIMA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO NCHINI

$
0
0
SERIKALI imeziagiza Bodi zote zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo kuanza mara usajili wa wakulima wa mazao yote na zihakikishe zinawapa vitambulisho kwa ajili ya kuwatambua na wanapofanyika kazi zao ili iwe rahisi kuwahuduma.Hatua hii inalenga kuwatambua na kuwasaidia kuboresha kilimo chao ili waweze kupata huduma za uhakika  kwa ajili ya manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akifungua mkutanowa kitaifa wa mwaka wa wadau wa sekta ya Tumbaku Tanzania. Alisema hatua inalenga kuwatambua wakulima wote na maeneo ambayo wanalima ili kuwaondoa na kilimo cha kujikimu na kuelekea katika kilimo cha kibiashara na kisasa.

Hasunga alisema hadi hivi sasa ni Bodi ya Tumbaku pekee ndio imesajili wakulima na kuwapa vitambulisho. “Lazima tuanze kuwatambua wakulima wetu walipo, mashamba wanayolima na ukubwa wake na mazao wanayolima na kiwango mazao ambacho wanatarajia kuzalisha ” alisisitiza.

Hasunga alisema lazima shughuli ya kilimo ianzie kutambulika kama zilivotaaluma nyingine
Alisema kukosekana kwa takwimu halisi za wakulima , ukubwa wa mashamba yao na walipo kumesababisha kuwa vigumu huduma muhimu kwa ajili ya kuboresha kilimo kuwafikia na kusababisha wapatiwe huduma za kitaaalamiu ambao halizingani na mahitaji yao na wakati mwingine sio halisi.

Waziri hiyo wa Kilimo aliongeza kuwa nguvu kubwa lazima ielekezwe katika kuwasaidia wakulima kulima cha kisasa kwa sababu ndicho kinatoa ajira kubwa kwa Watanzania ambapo asilimia 65 ya wananchi wamejiari katika kilimo na asilimia 8 wanashughulika na biashara inayotokana na mazao ya kilimo.

Katika hatua nyingine Hasunga amegiza Bodi ya Tumbaku Nchini na wadau wa zao hilo kuhakikisha wanasaidia kuinua zao la Tumbaku ambalo limeshuka na kupoteza uongozi wa kuwa zao linaloingiza fedha nyingi za kigeni.

Alisema uzalishaji umeshuka kutoka tani 126,0000 kwa msimu wa mwaka 2010/11  hadi kufikia tani 54,800 kwa msimu 2018/19 na kuongeza kuwa hata wastani wa bei umeshuka kutoka wastani wa Dola 2.11   kwa msimu wa mwaka 201/11 na kufikia Dola 1.72 mwaka 2018/19. Hasunga alisema ni lazima Bodi ya tumbaku na wadau wengine kuja na mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo siku za nyuma lilikuwa likiongoza kuingiza fedha za kigeni nchini.

Alitaja mikakati ni pamoja na kutafuta wanunuzi wengine sehemu mbalimbali ili kuongeza ushindani wa bei na kumnufaisha mkulima na Taifa kwa ujumla. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Hassan Wakasuvi alisema kuwa moja ya mambo ambayo yatawezesha kuleta mabadiliko katika sekta ya tumbaku ni marekebisho ya Sheria ya tumbaku. Aliwataka wadau kuwa tayari kutoa maoni yao wakati ukiwaidia ili kuwepo na Sheria nzuri
 Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Hassan Wakasuvi akijitambulisha wakati wa mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini ambao umefanyika leo  mkoani Tabora
 Baadhi wa Wakuu wa Wilaya na wadau wa tumbaku nchini wakiwa katika mkutano wa Kitaifa wa wadau wa tumbaku leo Mkoani Tabora.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwashukuru wajumbe wa mkutano wa kitaifa wa wadau wa tumbaku kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Kikao hicho cha siku moja kilichofanyika mkoani humo leo. 
 Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za mkoa huo wakati wa mkutano wa kitaifa wa siku moja wa  wadau wa Tumbaku nchini leo .

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua  mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini leo mkoani Tabora uliokuwa ukijadilia masuala mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji. Picha na Tiganya Vincent

KIKAO CHA KAMATI YA NISHATI NA MADINI CHAFANYIKA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo Kamati imepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Wizara ya Nishati, pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo, Felister Mgonja.

 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo wamepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Wizara ya Nishati.

Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Subira Mgalu akiwa akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo Kamati hiyo imepokea na kujadili taarifa mbalimbali za Wizara ya Nishati

MWANAMITINDO MISS EL SALVADOR ATUA NCHINI, KUTEMBELEA HIFADHI ZA TARANGIRE NA NGORONGORO.

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga,Moshi .

MWANAMITINDO na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo amewasili nchini usiku wa kuamkia kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. 

Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira. 

Akizungumza na Waandishi wa habari Marisela ambaye ni raia wa nchi ya El Salvador aliyehamia Los Angels, Marekani amesema lengo la kuja nchini kutembelea vivutio vya utalii ni pamoja na kuangalia fursa mpya ipatikanayo katika sekta ya Utalii Duniani pamoja na kuvitangaza. 

Marisela ambaye ameongozana na mchumba wake pamoja na mama yake mzazi akaeleza nia yake ya kuja Tanzania ikiwemo kukuza uchumi kupitia utalii ,elimu kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania . Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna mghwira amesema hii ni fursa adhimu ambayo nchi nyingi zenye vivutio vya utalii zimekua zikitamani hasa kwa kutembelewa na watu mashuhuri Kwani kupitia kwao inasaidia kutangaza utalii Duniani. Mwenyeji wa ugeni huo ,Dennis Meela akaeleza namna alivyo fanya ushawishi kwa Mwanamitindo huyo hadi kuamua kuja Tanzania. 

Mwanamitindi huyo kesho (Januari 18) ataanza safari ya kwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambako atakaa hapo kwa siku moja na baadae kuelekea Ngorongoro ambako atashuhudia maajabu ya wanyama katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la ufa la Ngorongoro (Ngongoro Creator).” Mwanamitindo huyo anakuja kujifunza baadhi ya vivutio anavyotaka kuvitumia kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa akiwa ameongozana na na kundi la watu wanne akiwemo mama yake mzazi na mpenzi wake ambaye ni Mwanasheria nguli nchini Marekani. 

Baada ya safari ya siku mbili katika hifadhi hizo atarejea Moshi Januari 22 na kutembelea moja ya kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuona namna ya kuweza kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Mwaka jana Merisela ameshiriki mashindano ya ulimbwende nchini El Salvador na kufanikiwa kutwaa taji la hilo (Miss El Salvador 2018). 

Pia amewahi kushiriki mashindano ya Best National Costumes na kufanikiwa kushika nafasi ya pili ambapo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Brazili na ya tatu Panama. Merisela anamiliki Taasisi binafsi ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Marekani.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa na Mwanamitindo  na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM .
 
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza jambo na na Mwanamitindo  na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM 
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akimpokea Mwanamitindo  na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo,mara baada ya kuwasili nchini usiku wa kuamkia jana kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha. Marisela amewasili usiku wa jana katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shrike la ndege la KLM .

UJUMBE WA PEMBE KWA WASANII CHIPUKIZI WA VICHEKESHO NCHINI

$
0
0

Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MSANII wa vichekesho nchini aliyejizolea umaarufu kutokana na umahiri na uhodari wa kuchekesha Yusuph Kaimu 

a.k.a Pembe ametoa ujumbe kwa wasanii na waigizaji wa vichekesho ambao ni chipukizi kuwa wabunifu katika kazi zao kwa lengo la kuteka soko la sanaa hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki.

Pembe ametoa kauli hiyo leo Januari 17, 2019 wakati anazungumza na Michuzi Blog ambapo amefafanua kwa sasa wasanii wengi wa vichekesho wanafanya kazi kwa kuigana na hivyo kuwa ngumu kumtambua msanii kutokana na sauti anayotumia inatumiwa na wasanii wengi.

"Wasanii wengi wanatumia sauti ya aina moja wakati wa kuigiza na hivyo kuwa ngumu kutambua anayechekesha kwa wakati husika.Hivyo ni vema wakabadilika na kuwa wabunifu kwa kila mmoja kuwa na sauti yake na staili yake ambayo itakuwa rahisi kutambua,"amesema Pembe.

Akizungumzia utofauti wa tasnia ya filamu kwa miaka ya zamani na sasa, Pembe amesema hapo nyuma wasanii walishandana na kuonesha vipaji vyao halisi vya kuigiza na kuchekesha na kwamba walikuwa na nidhamu ya 
kazi."Umahiri wa waigizaji wa zamani ulisababisha hata kufanya uwepo ushawishi uliosaidia kuvuta wadau wengi kuwa karibu na tasnia hiyo,"

Amewataja baadhi ya wasanii wa vichekesho ambao wamejizolea umaarufu kutokana na umahiri wao ni Senga,Bambo na Kingwendu ni wasanii ambao wamekuwa maarufu kutokana aina ya lafudhi zao za sauti zao ambazo 
walikuwa wanazitumia kwenye kuigiza na kwamba unaposikia sauti unajua tu huyo ni Bambo au huyo ni Kingwendu ama Senga.

Amesisitiza kupitia lafudhi zao wasanii hao wamekuwa mfano tosha na mpaka sasa wamebaki kwenye aina ya uwasilishaji wao wa sanaa huku akieleza kuwa hata pale ambapo watu wanapewa tuzo n vema kukawa na utaratibu wa kutambua waliofikisha sanaa hiyo hapo ilipofika.

KASI YA UJENZI MJI WA SERIKALI INARIDHISHA - WAZIRI MKUU

$
0
0
*Ataka kampuni ya Mzinga Holdings isimamiwe kwa karibu
*Ahimiza tarehe ya mwisho ni Januari 31, mwaka huu
ZIKIWA zimepita siku 20 tangu akague ujenzi wa mji wa Serikali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na ujenzi unaoendelea katika eneo la Mji wa Serikali lililoko Ihumwa.

Hata hivyo, amesema kampuni ya ujenzi ya Mzinga Holdings inahitaji kusimamiwa kwa karibu zaidi ili ikamilishe ujenzi wa majengo yake kabla ya Januari 31, mwaka huu. “Nitakuja kukagua kazi na kupokea funguo za ofisi siku hiyo,” amesema.

Ametoa kauli hizo leo mchana (Alhamisi, Januari 16, 2019) mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

Waziri Mkuu ambaye alianza kukagua ujenzi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais, ametembelea majengo ya wizara zote na kubaini bado kuna changamoto zinazojitokeza kutokana na utendaji wa mazoea miongoni mwa watumishi wa Serikali.

Akiwa katika jengo la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa meneja mradi, Bi. Selemina Rwehumbiza kwamba aliandaa certificate tangu tarehe 13 Januari lakini hadi sasa hajapata malipo. Alipofuatilia, alijibiwa na mshauri mwelekezi kwamba wamepokea certificate hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 16, 2019).

“Kama kazi hii muhimu ya Mheshimiwa Rais, na anayesimamia ni Waziri Mkuu inacheleweshwa hivi, je akija mwananchi wa kawaida huko ofisini kwenu atachukua muda gani kupatiwa huduma?,” Waziri Mkuu alimhoji Mshauri Mwelekezi wa mradi huo kutoka Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Hilary Msaki.

“Huu ni mfano halisi wa malalamiko yanayotoka huko nje kwamba Serikali haijibu barua za wananchi. Sasa nyaraka kutoka hapa Mtumba inachukua wiki nzima kwenda mjini, na mtu bado hajajibiwa. Sielewi ni kwa nini barua iende hadi mjini, wakati wakandarasi wako huku. Kwa nini ninyi msipokee hizo nyaraka na kuzikimbiza mjini kisha mrudishe majibu hapa site?”, alihoji Waziri Mkuu.

“Kuanzia sasa, kazi zote mpokee ninyi, na ninyi ndiyo mzipeleke huko mjini na kurudi na majibu hapa site kwa wateja wenu, kwani wakandarasi wote wako hapa,” alisisitiza.

Akiwa katika eneo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri Mkuu alielezwa na Waziri Ummy Mwalimu kwamba wana changamoto ya kutopatiwa taarifa za maendeleo ya mradi. “Tangu mradi unaze hatujapewa taarifa hata moja, wakurugenzi wapo wanakuja, lakini mshauri mwelekezi hatupi ripoti yoyote juu ya huu mradi,” alisema.

Alipohoji ni kwa nini taarifa hazitolewi, Waziri Mkuu alibaini kuwa hata watu wa TEMESA pia hawakuwepo kwenye zoezi hilo la ukaguzi. “Niliagiza TBA wahamie hapa, nao wameweka ofisi yao hapa hapa. Nimeulizia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wako wapi, nikaambiwa wako mjini. Ni kwa nini hawako hapa?” alihoji.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa tangi la maji lenye ujazo wa lita milioni moja, Waziri Mkuu alisema pamoja na spidi anayoihimiza, bado wakandarasi wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia ubora unaotakiwa (quality).

Alisema kwa ujumla kazi nyingi zimeboreshwa tangu alipokagua mradi huo Desemba 27, mwaka jana. Aliitaka TBA kwa kushirikiana na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Mkurugenzi wa Dodoma wawasimamie wakandarasi na hasa wale wa Mzinga ili kazi yao ikailike kwa wakati.

“Nimesisitiza katika kila site, zile kazi ndogondogo zisizohitaji ujuzi au ufundi mkubwa, zigawiwe kwa vijana ili kuongeza kasi lakini tuzingatie ubora wa kazi,” alisisitiza.

Desemba 27, mwaka jana, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali na kubaini kuwa baadhi ya wakandarasi hawaendi na kasi inayotarajiwa na Serikali. Siku iliyofuata aliitisha kikao cha Mawaziri wote, Makatibu Wakuu na wakandarasi wao ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini. Kikao hicho alikifanyia hukohuko Ihumwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Jengo la Wizara ya Maji wakati alipokagua ujenzi wa Mji wa Serikali  katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 17, 2019.  Wanne kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, Watano kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 17, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  ujenzi wa Jengo la Ofisi ya  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakati alipotembelea Ujenzi wa Mji wa Serikali kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma Januari 17, 2019. Watano kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo na watatu kulia ni Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Mji wa Serikali kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 17, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) wakati alipokagua ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara hiyo katika Mji wa Serikali unaojengwa eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 17, 2019. Wapili kulia ni  Waziri wa Elimu, Sayansi ya Tekinolojia, William Ole Nasha na kushoto ni Katibu  wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kuratibu Mpango  wa Serikali  wa Kuhamia Dodoma, Meshack Bandawe.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,  akizungumza na Saidi Kiwape (kushoto) ambaye ni fundi wa kusuka nondo wakati alipokagua ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara ya Nishati kwenye eneo la Ihumwa unapojengwa  Mji wa Serikali jijini Dodoma, Januri 17, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, watatu kulia ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujezi wa tangi la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja za maji  kwa ajili ya kuhudumia Mji wa Serikali unaojengwa katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 19, 2019.  Katikati ni Katibu wa Kikosi Kazi  cha kitaifa cha Kuratibu  Mpango wa Serikali wa Kuhamia Dodoma, Meshck Bandawe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mh. ABDULRABI(MB) "ALIYESUKUMIZIWA NDANI" NA MAHAKAMA KUU NA YA RUFAA KWA KUBAMBWA NA NYARA ZA SERIKALI!!!

$
0
0
Mh. ABDULRABI ALLY YUSUPH(71), ambaye alizaliwa siku ya IJUMAA, alikuwa ni mbunge wa Songea mjini baada ya kushinda ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa  mwezi Octoba 1985. 

Haikuwa ajabu kwake kujikita katika ulingo wa siasa kwani alikulia katika mazingira ya siasa ambapo baba yake, marehemu ABDULRABI YUSUPH, alikuwa Katibu wa kwanza wa TANU akifanya kazi kwa karibu kabisa na Mwalimu JK NYERERE. Kwavile, kwa mujibu wa Katiba yetu  mbunge hukaa kipindi cha miaka mitano, Mh. ABDULRABI alitarajia kuhudumu kwenye wadhifa huo wa ubunge hadi mwaka 1990, na ingewapendeza wapiga kura wake angeendelea kwa kipindi kingine.

Hata hivyo, hilo halikutimia kwani alikamatwa siku ya IJUMAA akiwa na nyara za tembo 105 ndani ya gari lake la ubunge aina ya Land rover. Kwa vile Katiba yetu haitoi kinga "immunity"  kwa mbunge atuhumiwapo kwa kosa la jinai,  baada ya upelelezi wa kina, Mh. ABDULRABI akashtakiwa na kufikishwa Mahakamani Kuu, Songea, kwa mara ya kwanza, siku ya IJUMAA.

Kesi yake ilivuta hisia kubwa si tu Songea bali nchi nzima. Wananchi toka maeneo mbalimbali ya Songea walikuwa wakifurika mahakamani kujua kinachojiri kwani kwanza haikuwa kawaida kwa kiongozi mkubwa kama yeye kushtakiwa na pili ilijengeka dhana kuwa majangili wa nyara za tembo ni Wasomali na wananchi wa hali ya chini.

Baada ya upande wa mashtaka na upande wa utetezi kumaliza kutoa ushahidi, Mh. ABDULRABI alitiwa hatiani na Mahakama Kuu tarehe 15 April 1988, siku ya IJUMAA, baada ya mahakama hiyo kuridhika na ushahidi usio na mawaa wa upande wa mashtaka na ikampiga "mvua" 9. Hiki kilikuwa kitu cha ajabu sana kwani wananchi wengi hawakutegemea mbunge kufungwa!. 

Baada ya kutolewa adhabu hiyo na Mahakama Kuu, Mh. ABDULRABI hakuridhika hivyo alikata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa nchini ambayo aliiwasilisha siku ya IJUMAA ambapo aliorodhesha sababu sita. Sababu yake kubwa ilikuwa kwamba- "Hizo nyara sio zake ila yeye alibambwa na nyara hizo  kwavile siku hiyo  "alikuwa ameamua kwenda-front mwenyewe kuwakamata majangili wa nyara za tembo". 

Mahakama ya Rufaa, baada ya kuisikiliza kwa makini rufaa hiyo, ilitoa hukumu tarehe 24 Machi 1989, siku ya IJUMAA. Katika hukumu hiyo, Mahakama hiyo ya juu 'ilimchinjia baharini" Mh. ABDULRABI, huku Mh. ROBERT KISANGA, mmoja wa majaji bora kabisa kuwahi kutokea nchini, akizikejeri sababu hizo 6 za rufaa, kwa niaba ya majaji wenzake, kwa kusema:
"We only wish to say that one needed very unusual courage to swallow such a fantastic story. The six grounds, raised by the appellant in his memorandum to the court, were totally devoid of substance". 

Mahakama hiyo ikaamua kuonesha mfano kwa mahakama zote nchini ambapo si tu haikukubaliana na hoja za Mh. ABDULRABI bali pia iliamua kumuongezea "mvua" toka miaka 9 hadi 12.!!! Mh. ABDULRABI, familia yake, ndugu na marafiki zake hawakuamini maskio yao na kubakia kububujikwa na machozi! Kwa hakika, ilikuwa ni siku ya uchungu mno kwao. 

Mh. ABDULRABI alianza kutumikia kifungo chake cha jela kwenye gereza la Songea. Baadae alihamishiwa gereza la Lilungu, Mtwara, siku ya IJUMAA na baadaye akahamishiwa Ukonga Dar Es Salaam na kisha gereza la Maweni, Tanga.

Kutokana na kipaji chake cha kuzaliwa cha uongozi, Mh. ABDULRABI alikuwa Mnyapala mkuu katika kila gereza alikohamishiwa na pia alikuwa ni Imamu wa kuswalisha waislam wote waliofungwa. Kwa hakika alikuwa ni mtu maarufu sana magereza yote aliyopitia.

Mh. ABDULRABI, akiwa anatumikia kifungo chake hicho, alipatwa na mikasa mingi. Mkasa wa kwanza ulikuwa ni wa kuachwa na mkewe miezi mitano tu baada ya kuanza kutumikia kifungo chake. 

Siku moja akiwa gereza la Lulindi, Mtwara, kiongozi mmoja Mlokole alimfuata na kumwambia amemsilimisha mkewe na kuwa Mlokole na mbaya zaidi akamuoa kabisa! Mh ABDULRABI alihuzunika na kupata uchungu sana kwani  alikuwa amezaa watoto 6 na mke wake huyo wa kwanza, ambapo baadhi ya watoto hao pia wakawa walokole wakati yeye ni "Swala 5"!.

Mkasa mwingine uliomkumba akiwa "lupango" ulitokea siku moja ya IJUMAA alipomsikia kiongozi mmoja wa zamani wa Bunge  la Jamhuri  ya Muungano alipolitangazia Bunge na Taifa kwamba: "aliyekuwa Mbunge wa Songea mjini(CCM) Bw. YUSUPH ALLY ANDULRABI aliyekuwa amefungwa, amefariki". Jambo hili lilimtia simanzi na uchungu usio na mfano na hadi leo haelewi ni kwanini  kiongozi huyo alitangaza hivyo!.

Mkasa mwingine ni pale akiwa "lupango", watoto wake walipotimuliwa shule kwa kukosa mtu wa kuwasomesha. Siku moja, Rais wa awamu ya pili, Mh ALLY HASSAN MWINYI alifanya ziara ya kitaifa huko Songea na akahutubia kwenye uwanja wa Majimaji.  

Huku Rais MWINYI akiendelea kuhutubia, dada yake Mh. ABDULRABI aliamua "kujitoa fahamu" na kwenda karibu kabisa na alipokuwa Mh. Rais MWINYI na akamwangukia miguuni huku akilia kwa uchungu! Kitendo hicho kiliwaudhi mno wanausalama ambao, kufumba na kufumbua, wakawa wamemkwida na kumbeba mzobemzobe hadi nje. 

Hata hivyo, baadae "Mzee Rukhsa", akiwa Ikulu ndogo, aliagiza mwanamke huyo apelekwe ili akatoe dukuduku lake. Alipofika Ikulu ndogo, dada huyo wa Mh. ABDULRABI alimweza "Mzee Rukhsa" kuwa anaishi na watoto 2 wa Mh. ABDULRABI na kwamba yeye ni fukara chokambaya asiye na nyuma wala mbele na kipindi chote alichokaa na watoto hao 2, "hakuna rangi aliyoacha kuiona" hivyo akaomba kusaidiwa. "Mzee Rukhsa", papo hapo, akaagiza CCM iwasomeshe watoto hao waliokuwa wadogo na kweli ikawasomesha hadi kidato cha nne.

Jambo lingine lililomkumba Mh ABDULRABI ni kukimbiwa na viongozi na marafiki zake karibu wote ambao zamani walikuwa wanakunywa wote na kufurahi kwa pamoja. Hili linamsononesha sana. Hii ndio mikasa aliyokumbana nayo.

Mh. ABDULRABI, akiwa anatumikia kifungo chake, alishuhudia na kushiriki kwenye mambo mengi mengine yakiwa si ya kawaida. Mfano mmoja mkubwa ni pale aliposhuhudia, kwa macho yake, kunyongwa kwa wafungwa 11 baada ya Rais MWINYI kutia saini hati zao za kuidhinisha wanyongwe baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya mauaji ya kukusudia na Mahakama Kuu na rufaa zao kutupwa na Mahakama ya Rufaa  . 

Baadhi ya watu wamekuwa wakitoa takwimu potofu kuhusu idadi halisi ya watu walionyongwa nchini toka tupate uhuru. Taarifa rasmi na sahihi ilitolewa bungeni tarehe 30/1/2008 na Mh. MATHIAS MEINRAD CHIKAWE, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba wa awamu ya nne kama ifuatavyo:
"Mh Spika, jumla ya watu 82 wamenyongwa kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu hii ya nne. Kati ya watu hao, 10 walinyongwa wakati wa awamu ya kwanza na 72 walinyongwa wakati wa awamu ya pili. Hakuna ambaye alinyongwa wakati wa awamu ya tatu na awamu ya nne..."

Mh. ABDULRABI si tu alishuhudia kunyongwa kwa watu hao 11 bali pia yeye alikuwa mmoja wa waliopewa kazi ya kusafisha vitanzi hivyo baada ya adhabu hiyo kutekelezwa.

Mh. Rais MWINYI alimsamehe Mh. ABDULRABI, muda mfupi kabla ya kuacha urais, akitumia mamlaka yake  kwa mujibu wa ibara ya 45 (1)(a) ya Katiba yetu isemayo:
"Rais anaweza kutoa msamaha kwa yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote.."

Mh. ABDULRABI aliachiwa ikiwa imebaki miezi 4 amalize kutumikia kifungo chake. Mh. ABDULRABI hakutumikia miaka yote 12 gerezani kwani kwa mujibu wa Kifungu cha cha 49(1),(2),(3) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 'RE (2002) mfungwa yeyote( isipokuwa aliyehukumiwa kunyongwa au kifungo cha maisha) hupata msamaha wa 1/3 ya kifungo chake. Mh. ABDULRABI alifungwa Aprili 1988 kwa kupatikana na nyara za serikali hivyo ukiondoa 1/3 ya miaka 12 unabaki na miaka 8. Hivyo, angetoka April 1996 kama asingepata msamaha huo wa Mh. Rais MWINYI.   

Mh. ABDULRABI akaachiwa siku ya IJUMAA na kwenda kuishi eneo lijulikanalo kama Mfaranyaki ambako alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo. 

Mh. ABDULRABI, kwa kupata msamaha huo wa Rais, amekuwa mmoja wa wafungwa viongozi/watu maarufu waliopata msamaha wa Rais kwa mujibu wa Katiba. Baadhi ya wengine ni ISMAEL ADEN RAGE (Rais Kikwete), NGUZA VIKING@BABU SEYA na mwanae JOHNSON NGUZA@ PAPII KOCHA (Rais Magufuli), AGNES DORIS LIUNDI (Rais Nyerere) na ASHA MKWIZU (Rais Mwinyi).  

Kama ionekanavyo maeneo mengi ya makala hii hapo juu, siku ya IJUMAA ni ya kipekee sana kwa maisha ya Mh. ABDULRABI na mama yake mzazi aliyefariki mwaka 2011 aliwahi kumsihi amshukuru Mungu kila siku ya Ijumaa kwani ina historia ndefu kwa maisha yake. Cha ajabu hata leo hii makala hii ya kumhusu Mh. ABDULRABI  imeandikwa IJUMAA!!!.  

Mh. ABDULRABI kwa sasa "amefulia" akiishi kwenye nyumba chakavu ya urithi pamoja na wake wawili ambao ni mama ntilie, na watoto kadhaa. Kwavile umri umekimbia,  kwasasa anawategemea mama ntilie hao kwa kila kitu. 

Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum

$
0
0

NOTES ON FIXED ACCOUNT.


·        Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum

·        Riba hadi asilimia 12 kwa mwaka kwa mteja mwenye amana ya kuanzia Milioni 5 kwa kipindi cha miaka miwili na kuendelea

·        Ni fursa nzuri kwa Mstaafu  anayepokea pensheni yake badala ya kununua gari alipendalo awekeze TPB Bank

·        Mtu yeyote anaweza akafungua akaunti hii na kuwekeza

·        Riba inalipwa kila baada ya mwezi, miezi mitatu mpaka sita kulingana na matakwa ya mteja.


GROUP ACCOUNT

Katika kutambua uwepo wa makundi mbali mbali ya watu, kujali mahitaji yao ya huduma za kifedha na adha wanazozipata katika kupata huduma za kibenki, TPB Bank ina akaunti maalum kwa vikundi.  Vikundi rasmi na visivyo rasmi.


Vikundi kama vile, vikundi vya wafanyakazi, vikundi vya ndugu, vilabu vya michezo mbali mbali, wasuka nywele, wasuka mikeka, wavuvi, mafundi seremala, vikundi vya kidini, vikundi vya sehemu ya kazi n.k.


WAZIRI MKUU AIAGIZA NHC KUONGEZA NGUVUKAZI KATIKA UJENZI WA MJI WA SERIKALI

$
0
0
Na Farida Ramadhani na Peter Haule - Dodoma
 Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, amemuagiza Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa Ofisi mpya ya Wizara ya Fedha na Mipango kutoka Shirika la Nyumba la Taifa, kuhakikisha anaongeza rasilimali watu ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa .

Majaliwa, ametoa agizo hilo wakati wa  ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi mbalimbali za Wizara katika mji wa Serikali eneo la Ihumwa Jijini Dodoma. Alisema kuwa  zimebaki siku 21 pekee kukamilisha ujenzi huo na  lengo la Serikali ni kuona kazi hiyo imekamilika ifikapo Januari 31 mwaka huu, na akaonesha hofu yake iwapo ujenzi utakamilika kwa wakati kwa kuwa hakulidhishwa na nguvu kazi iliyopo.

“Mimi ninapokuta watu wachache huku kukiwa na kazi zisizohitaji kusubiri siku mbili kama kazi ya kuweka bimu, natarajia kuona watu wangekuwa wanaendelea kufanya kazi hizo”, alisema . Aidha alisema kuwa Mawaziri kutembelea ujenzi unaoendelea na kuona ubora wa jengo ni  jukumu lao na wanauwezo wa kuonesha kuridhika au kutoridhika na ujenzi huo.

Ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu kuhakikisha mazingira ya eneo la Wizara linapandwa miti  kulingana na ramani ya majengo ya muda na yakudumu. Alisema kama watumishi waliopo ni wachache mkandarasi aongeze vijana ili ujenzi ukamilike mapema kwa kuwa kuna mafundi wengi Mkoani Dodoma na nje ya mkoa huo wanaotafuta kazi.

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameahidi kusimamia maagizo ya Waziri Mkuu na kuhakikisha jengo linakamilika kwa wakati kwa kuwa hadi sasa asilimia 95 ya vifaa vyote muhimu vya ujenzi vimenunuliwa.

Akizungumzia suala la kuongeza nguvu kazi, Dkt. Kijaji, amesema Wizara itahakikisha Mkandarasi anaongeza nguvu kazi kwa haraka  kutoka mtaani au Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili ifikapo Januari 31 Wizara ikabidhiwe jengo rasmi. Dkt. Kijaji alieleza kuwa Wizara ipo tayari kuhamia katika jengo hilo Februari mosi mwaka huu.

Naye Mhandisi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Elisante  Olomi, anayesimamia ujenzi wa ofisi za Wizara hiyo, amesema ujenzi unaendelea vizuri na mpaka sasa umekamlika kwa asilimia 75, huku akiahidi kuongeza mafundi wakutosha kwa kuwa wapo wengi na wamekuwa wakiomba kazi katika maeneo hayo ya ujenzi. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitoa maagizo ya ukamilishwaji wa Ujenzi wa ofisi ya Wizara ya fedha na Mipango katika Mji wa Serikali, Ihumwa Dodoma, kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto), alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
 Mhandisi Elisante Olomi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) namna ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango unavyoendelea, Ihumwa Jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katika), akiendelea na ukaguzi katika  eneo la mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia), akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Suzan Mkapa, katika ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo unaoendelea, Ihumwa Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Fedha na Mipango, Alfred Dede (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya mipaka ya eneo la Wizara hiyo  kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia), katika Mji wa Serikali  Ihumwa Jijini Dodoma, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bi. Suzan Mkapa na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Grace Sheshui wa Wizara hiyo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

MADINI KUWEKA MSUKUMO MIRADI YA LIGANGA, MCHUCHUMA

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Ludewa
Wizara ya Madini imesema itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kuweka msukumo ili kuhakikisha  kwamba miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na ule wa Chuma Linganga inaanza kutekelezwa.
Kauli hiyo ilitolewa Januari 16 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za madini mkoani Njombe  na kuona namna ya kutatua changamoto  zinazohusu Wizara ya Madini   katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema miradi hiyo ni moja ya miradi ya kimkakati ambayo Taifa linatarajiwa kunufaika kwa kiasi kikubwa, hivyo kutokana na umuhimu wake, wizara ya madini itashirikiana na wizara hiyo kuhakikisha hatua zaidi zinapigwa ili hatimaye miradi hiyo ianze kutekelezwa kwa kuwa imechukua muda mrefu.
Aliongeza kuwa, ni miradi mikubwa ambayo taifa linatarajiwa kunufaika nayo  kupitia ajira  na kuongeza pato la nchi huku akiyataja madini ya chuma kuwa  moja ya malighafi muhimu kwa uchumi  wa Tanzania ya viwanda  na kusema kuwa, kama taifa, linautolea macho mradi huo na kwamba serikali imedhamiria kuutekeleza.
Aliongeza kwamba, katika Serikali ya Awamu ya Tano, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anayo imani kubwa  kuwa  miradi hiyo itaanza huku  serikali ikitegemea  kupeleka  maendeleo  kwa wananchi kupitia miradi husika.

 “Wizara yetu ndiyo inatoa leseni za madini na tayari tulishatoa leseni ya Makaa ya mawe mchuchuma kwa hiyo nimefika kuangalia changamoto ambazo ziko upande wa wizara yetu kuweza kuzitatua ili tutoke hapa. Miradi hii tumeisikia miaka mingi ni wakati sasa tunataka ianze.” alisisitiza Nyongo. 
Aliongeza kuwa, ikiwa wizara ndiyo inatoa leseni za madini,  inaowajibu wa kujua yule aliyepewa leseni kama anaifanyia kazi na kuongeza, “Sisi tuliotoa leseni lazima tuangalie tuliyempa leseni amekwama wapi  lakini pia tujue  miradi hii inaanza lini? Makaa ya mawe na chuma vyote vinahitajika kwa taifa. Tunatambua makaa ya mawe ni madini ambayo yana tija kwa uchumi kwa nchi,” alisema Nyongo.

Akifafanua zaidi kuhusu miradi hiyo alisema kuwa, mradi wa Makaa ya Mawe unatarajiwa kuzalisha umeme ambao mbali ya kuuza kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), umeme huo unatarajia kutumika katika kuzalisha madini ya Chuma Liganga.
 “ Mpango ni Liganga kutumia megawati 250 kwa shughuli zake za kuzalisha chuma na megawati 350 zitauzwa Tanesco kuzalisha umeme,” aliongeza. 
Akifafanua sababu za kuchelewa kwa miradi hiyo, alisema ni kutokana na changamoto za kimkataba ambazo bado ziko katika majadiliano katika ngazi za juu na kuitaja baadhi ya mikataba hiyo kuwa ni  kuwa ni pamoja na mikataba ya upunguzaji wa kodi.
Aliongeza kuwa, wizara ya madini ikiwa ni wizara ambayo inasimamia Sheria ya Madini, imelenga kuhakikisha kwamba miradi hiyo mikubwa inaanza ili hatimaye iweze kuwanufaisha watanzania na taifa.
Akielezea suala la fidia kwa wananchi waliopisha miradi hiyo, alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ludewa kwa kutenganisha suala la miradi hiyo na fidia  ambapo alisema kwamba taratibu za juu zikikamilika, wananchi watalipwa fidia  na hivyo kuwataka kuwa na subira na kuwa tayari kupisha utekelezaji wa miradi hiyo.
Awali,  Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Christopher Ole Sendeka alimweleza waziri umuhimu wa wizara ya madini kujielekeza  kwenye kupata taarifa halisi kuhusu tafiti zilizofanyika awali kuhusu  akiba iliyopo ya madini ya chuma  Liganga na Makaa ya Mawe mchuchuma. 
Aidha, aliongeza kuwa, mbali na chuma na makaa ya mawe mkoa huo unayo madini mbalimbali ikiwemo dhahabu ambayo bado haijachimbwa kwa kiasi kikubwa.
Miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na Chuma Liganga, inatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Group Ltd, ya China.
Pia, akiwa mkoani humo, Naibu Waziri alitembelea mgodi wa Kokoko Kokoto wa Nyakamtwe Quary, ambapo alitoa changamoto kwa mmiliki wa mgodi huo kuongeza kasi ya uzalishaji na kuwa wabunifu kutumia fursa  za miradi mikubwa ya ujenzi  inayotekelezwa na serikali ikiwemo ya ujenzi wa reli ili kokoto hizo ziweze kutumika.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akimsikiliza Meneja wa mgodi wa Kokoto wa Nyakamtwe Quary, uliopo mkoani Njombe   alipoutembelea wakati wa ziara yake hivi karibuni. Mhagama ni mmoja wa wanufaika wa ruzuku iliyotolewa awali na Serikali  kwa wachimbaji wadogo . Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Ruth Msafiri.
 Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mhandisi Paschal Malesa, akimweleza jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati alipotembelea mradi wa Liganga uliopo Wilayani Ludewa mkoani Njombe. Naibu Waziri Nyongo alitembelea kujua maendeleo ya utekelezaji mradi huo ikiwemo kujua changamoto ambazo  ziko upande wa Wizara inaweza  ili izifanyie kazi kuhakikisha kwamba mgodi huo unatekelezwa kama ilivyopangwa.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiangalia makaa ya katika mgodi wa Liganga alipoutembelea hivi karibuni. Naibu Waziri alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujua changamoto za utekelezaji wa mradi huo. Anayemweleza jambo ni Mtalaam kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mhandisi Paschal Malesa.
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akimsikiliza akimweleza jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake mkoani humo.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitoka katika Ofisi za Wilaya ya Ludewa  tayari kwa ziara ya kutembelea katika mgodi wa Liganga kwa ajili ya kujionea changamoto za utekelezaji wa mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakifuatilia kikao baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka. (hayupo pichani) Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri. 

RC Wangabo aishauri Wizara ya Kilimo kujenga vihenge eneo la viwanda la Kanondo

$
0
0
Katika hali ya kuupendezesha mji wa Sumbawanga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameishauri wizara ya kilimo nchini kuona namna ya kuhamisha mradi wa ujenzi wa vihenge kutoka katikati ya mji wa Sumbawanga na kuhamishia katika eneo maalum lililotengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwaajili ya ujenzi wa maghala na viwanda ili kuutanua mji na kujenga vihenge hivyo kwa nafasi.

Amesema kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)tayari wamekwishanunua eneo la ekari 24.6 lenye thamani ya shilingi 298,938,000 lililopo katika eneo maalum lililotengwa kwaajili ya viwanda vidogo, maghala na hotel lililopo Kijiji cha Kanondo, Kata ya Ntendo, Manispaa ya Sumbawanga ambapo mpaka sasa viwanja vilivyouzwa katika eneo hilo ni asilimia 35.

“Sisi tungependa kama mkoa wa Rukwa eneo hili liwekezwe, kwasababu tuna uchumi wa kati wa viwanda, lakini sasa naona bado tunapenda maeneo yet utu, sasa huku nani atakuja aendeleze? Kwakweli huu mradi uje kujengwa huku ntashauriana na wizara ya kilimo Waziri tuone namna ya kuleta huku, kwasababu hapo mnapotaka kujenga ni eneo dogo” Alisema.

Ameyasema hayo alipotembelea eneo hilo maaluma la uwekezaji wa maghala lililililonunuliwa na NFRA miaka miwili iliyopita huku likiwa limeachwa wazi bila ya matumizi yoyote. Kwa upande wake Kaimu meneja wa NFRA Mkoa wa Rukwa James Marwa alisema kuwa mradi wa vihenge ulianza kabla ya kununuliwa kwa eneo hilo, hivyo ili kuhamisha mradi huo lazima eneo hilo jipya lipimwe upya.

Nae Afisa Mipango miji wa Manispaa ya Sumbawanga Thadeo Maganga amesema kuwa hatachoka kuendelea kuwahamasisha wadau mbalimbali kufika katika eneo hilo ili kuona umuhimu wake na kuweza kuwekeza kwa maslahi ya Manispaa, Mkoa nan chi kwa ujumla. Ujenzi huo wa Maghala na Vihenge vya kisasa (Silos) utajengwa katika maeneo nane ya kanda saba za wakala ambapo ujenzi huo utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Mradi huo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi umeanza kujengwa katika Manispaa ya Songea (Ruvuma), Dodoma, Mpanda (Katavi), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara) ambapo Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga James Mtalitinya akionyesha ramani ya viwanja vilivyotengwa kwaajili ya uwekezaji wa viwanda vidogo na maghala katika eneo la Kanondo, kata ya Ntendo Manispaa ya Sumbawanga km 5 kutoka Sumbawanga mjini, mbele ya timu ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. 
 Bango la ramani ya Viwanja vya Kanondo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joachim Wangabo akionyesha ubovu wa maghala yaliyopo katika ofisi za NFRA katikati ya mji wa Sumbawanga. 

MRADI WA MAJI WA BILIONI 4.9 WAENDELEA KUHUJUMIWA NAMTUMBO

$
0
0
Na Yeremias   Ngerangera, Namtumbo.
Mradi wa  maji katika kijiji cha Likuyusekamaganga  wilaya  ya Namtumbo mkoani Ruvuma  umeingia   dosari tena  na kumfanya  mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia  kizigo  kuendesha zoezi la kupiga kura za siri ili kumbaini  wanaohujumu  mradi huo  baada ya  hivi karibuni  vifaa vyenye thamani  ya shilingi  milioni 500  kuteketezwa  kwa  moto  na  tukio hilo kurudia tena  siku ya  jumatatano  wiki hii na kuchoma mabomba  ya mradi huo

Mwakilishi wa kampuni  ya Elegance Developers Company Ltd  ya Dar  es salaam inayojenga mradi huo  Mhandisi  Felician Kavishe  alisema vifaa  vyenye thamani  ya shilingi milioni 500 vilichomwa  moto    na watu  wasiojulikana  hivi karibuni lakini tukio hilo hilo  limejirudia  tena kwa kuchoma  mabomba  ya kusambazia  maji ambayo  thamani  yake bado haijajulikana.

Aidha kavishe alionesha  wasiwasi  wake kwa  wafanyakazi  wa kampuni  hiyo kuendelea kutekeleza  mradi huo  katika  mazingira  ya  hofu  zilizojaa mioyoni mwao juu ya matukio  ya mara kwa mara  ya kuchoma  vifaa  na mwisho  wa  yote akadai isije  wakachomwa  na wafanyakazi  wa kampuni hiyo.

Kaimu Mtendaji wa kata ya Likuyuseka Petro Nyoni  alidai kitendo  cha mkuu wa wilaya hiyo kuendesha  zoezi la kupiga  kura za siri kwa wananchi wa kijiji  hicho  linaweza  kuwa suluhisho  la kumalizika  kwa tatizo hilo kutokana  na wananchi hao kuwajua watu wanaofanya hujuma hiyo  kwa kuwapigia kura za siri za  ushindi .

Mkuu wa wilaya hiyo aliwaambia wazee wa kijiji hicho kuwa serikali imeleta  bilioni 4.9 kutatua changamoto ya maji na kuelekeza  lawama  zake  kwa  wazee wa kijiji hicho kwa kulifumbia macho tatizo  hilo la uchomaji moto  wa vifaa vya mradi vinavyoletwa na mkandarasi huku wa zee  hao wakibaki kimya alisema mkuu wa wilaya hiyo.

“Wazee  huo ni  ujinga  kuendelea  kuacha  kudhibiti  tatizo hili ambalo mliweza kulitatua wazee wa kijiji  hiki lakini mkaendelea  kubaki  kimya na matukio  yanaendelea  kutokea  huku  wazee  wa kijiji  mpo” alisema  Mkuu wa wilaya hiyo.

Hata hivyo mkuu wa wilaya aliendesha   zoezi la kupiga kura za siri  kwa wananchi  wa kijiji hicho kuwataja  watu wanaojihusisha  na matukio  ya uchomaji moto  vifaa vya mradi huku matokeo ya kura hizo zikabaki kuwa siri kwa hatua za uchunguzi zaidi.   
 Mhandisi  mshauri Nashoni Charles  kutoka kampuni  ya Norplan  Tanzania Ltd ya Dar es salaam alisema  kitendo  cha kuendelea kuchoma  vifaa   kinaiingizia hasara  kampuni  lakini pia kitafanya  kampuni hiyo  kutumia muda mwingine kwenda kununua vifaa  , huku muda wa  mkataba wa utekelezaji wa mradi huo upo palepale.
 Kwa  mujibu wa mhandisi  mshauri wa kampuni  hiyo Nashon  alidai mradi huo  wa maji  wa Likuyumandela  umefikia  asilimia 60 kwa sasa  katika  utekelezaji wake  na unategemea kuhudumia watu 13,319 kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kukamilika kwake.

Kaimu  Mhandisi wa maji wa Halmashauri  ya wilaya ya Namtumbo Salumu Nachundu  alidai mradi unatekelezwa chini ya progamu  ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP)kupitia program ndogo ya maji  na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP)

Balozi Seif aongoza Mahafali ya 35 Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameushauri Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kutumia Programu za kutayarisha Walimu Tarajali watakaowaandaa Wanafunzi wa Skuli za Msingi na Sekondari kuwa na Stadi na maadili ya kujiendeleza kupitia mfumo wa Elimu Huria na Masafa.

Alisema uwepo wa Chuo hicho  unaendelea kutoa matumaini kwa Mtoto wa Kitanzania anayeanza Darasa la kwanza kuwa na uhakika wa kupata Elimu hadi ngazi ya Chuo Kikuu ikiwa na maana halisi ya Elimu endelevu kama haki ya Binaadamu.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo wakati akiwahutubia Wahitimu wa Mahafali ya 35 wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania {Open University} yaliyofanyika hapo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Alisema Elimu Huria na Masafa inajitanabahisha kama Mfumo wa kisasa na mahiri katika kutoa Elimu na mafunzo yenye ubora unaokubalika  na kutambulika Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ukizingatia taratibu na kukidhi Vigezo vya ithibati vya Mamlaka husika.

Balozi Seif aliukumbusha Uongozi wa Chuo hicho kwamba katika jitihada zake za kutekeleza majukumu yake ni vyema ukaendelea kujikita katika kauli mbiu isemayo elimu bora na nafuu kwa wote kwa mujibu wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014.

Alieleza kwamba Kanuni za Chuo hicho katika masuala ya Udahili, kufundisha, kujisomea pamoja na kutathmini Maendeleo ya Wanafunzi ni fursa pekee itakayoweza kuisaidia Taifa kuongeza kiwango cha Udahili kwa Wananchi wake katika Elimu ya juu.

Balozi Seif alisema kwa mujibu wa Takwimu za Benki ya Dunia, Uchumi wa Kati na wa Viwanda hauwezi kufikiwa au kuwa endelevu pasipo kuwa na kiwango cha udahili katika Elimu ya juu cha angalau kufikia asilimia 23%.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kiwango cha Tanzania kama zilivyo Nchi za Burundi na Madagaska hivi sasa kimefikia asilimia 4%  kikiwa chini kutokana na sababu zilizobainishwa kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo 2014.

Balozi Seif  alisema huo ndio mfumo ambao unahitaji kuhuishwa na Mfumo wa Elimu huria na masafa ili Elimu ifikie kuwa  Haki ya Msingi ya kila Mwananchi kama ilivyo haki nyengine zote za Binaadamu.

Alisema Serikali imekusudia kuleta Mapinduzi ya Kiuchumi ili kuibadili Tanzania iwe Nchi ya Uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025, mbapo Sekta ya Elimu na mafunzo kwa mujibu wa Dira ya Maendeleoya Taifa na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo inatarajiwa kuleta Maendeleo ya haraka.

Alifahamisha kwa kutambua kuwa Elimu ni haki ya Msingi ya Binaadamu Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kubeba wajibu wa kutoa Elimu ya Msingi na Sekondari biya ya malipo kwa Watoto wote waliofikia umri wa kwenda Skuli, uamuzi ambao pia umefanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Balozi Seif  ameunga mkono rai iliyotolewa na Uongozi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kuwa mamlaka  husika hususan Wizara ya Elimu, Tume ya Vyuo Vikuu, Baraza la Elimu na Ufundi pamoja na Chuo Kikuu Huria Tanzania zishirikiane katika kubuni taratibu zitakazotekeleza azma ya Serikali kama ilivyoainishwa ndani ya Sera ya Elimu.

Alielezea matumaini yake kwamba Chuo hicho kitaendelea kuwa chemchem ya Elimu inayotiririka kila pembe ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kunufaisha pamoja na kukinaisha Watanzania wengi zaidi.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kukipatia eneo la ujenzi wa Ofisi Chuo hicho ili kijenge Kituo chake cha Pili kwa ukubwa Nchini Tanzania Jamii ikiamini kuwa uwepo wao Zanzibar utasaidia kudumisha Muungano.

Akizungumzia suala la Wahitimu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema ni vyema kwa Vyuo Vikuu vya Tanzania kuunda Jumuiya ya Wahitimu { Alumni Associations} zenye nguvu ili kupata nafasi ya kuwashirikisha Wahitimu kwenye Maendeleo ya Vyuo vyao.

Alisema maendeleo ya Vyuo Vikuu vingi mashuhuri Duniani yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na Wahitimu wake ambao wengine hunyookewa kimaisha na kuwa Matajiri wakubwa katika Jamii zinazowazunguuka.

“ Wengi wetu hapa kwenye Meza kubwa tumesoma kwenye Vyuo vya hapa Nchini lakini sifikirii kama Vyuo vyenyewe vina habari na sisi”. Alisema Balozi Seif.

Aliwaomba Watitimu wote waliopata elimu Chuo hicho kusaidia kuchangia maendeleo yake kwa njia tofauti ikiwemo mawazo, ubunifu, ufadhili kwa Wanafunzi maskini pamoja na kufadhili tafiti mbalimbali za Chuo.

Akitoa Taarifa ya Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Elifas Tozo Bisanda alisema utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano {TEHAMA} katika ufundishaji umewezesha kupatikana kwa ongezeko kubwa la Vituo vya Mitihani  33 katika maeneo yote Tanzania Bara na Zanzibar.

Profesa Elifas alisema ongezeko hilo la Vituo vha Mitihani limesaidia kuibua Wataalamu wengi waliohamasiska kupata Taaluma zaidi ya Elimu Huria na Msafa kwenye chuo hicho kinachofikia Miaka 25 sasa tokea kuasisiwa kwake Mnamo Mwaka 1994.

Alisema Jumla ya Wahitimu Elfu 3,053 wa ngazi ya Shahada, Stashahada na Astashahada wamefanikiwa kukamilisha mafunzo yao mwaka huu na kuifanya idadi ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kufikia 39,934 toke kuanzishwa kwake.

Alisema inapendeleza kuona wanafunzi wa Chuo hicho kwa sawa wanatoka sehemu mbalimbali za Dunia hasa katika Mataifa ya Bara la Afrika hali iliyokifanya Chuo hicho kuimarisha vituo vya nje kaika Nchi za Kenya, Namibia, Zambia, Ghana na mazungumzo yanaendelea kufungua Kituo chengine Nchini Ethiopia.

Mapema akitoa salamu za Uongozi wa Chuo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Rwekaza Makandala alisema Chuo hicho kimelenga kuwa na Maabara ya Tafiti zote ili kiwe sehemu ya Taifa ya Mabadiliko ya Uchumi.

Profesa Ujenzi huo wa Mabara unakwenda sambamba na Mpango Mkakati ulioanza Mwaka 2018-2019 na 2020 – 2022 unaokusudia kujenga uwezo wa Kitaaluma kwa Mwanafunzi popote alipo kwenye Kituo chake.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania alizishukuru na kuzipongeza Serikali zote mbili Nchini Tanzania kwa kusimamia Mikakati inayochangia Maendeleo ya Chuo hicho Huria Nchini.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza na Wahitimu hao Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Riziki Pembe Juma kwa Niaba ya Waziri pacha mwenzake wa Elimu Sayansi na Teknolojia wa Tanzania alisema Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimesaidia kujenga uwezo wa kukidhi mahitaji ya Serikali.

Mh. Riziki alisema Serikali zote mbili Tanzania ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zinathamini Mchango wa Chuo hicho kwa kuimarisha Sekta ya Elimu Nchini.

Waziri Riziki Pembe alisisitiza kwamba kusudi la Serikali ni kukiwezesha Chuo hicho kuwa mfano Bora wa Chemchem ya Elimu kwa kukisaidia kuunganisha Vituo vyote vya Mitihani kutumia Mkonga wa Taifa Mawasiliano ili kupunguza Gharama pamoja na kuwajengea uwezo zaidi wa Kitaaluma Wanafunzi wake.
 Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania {Open University} wakiwa katika  Gwaride Maalum  wakiingia katika Uwanja wa Mahafali  yao ya 35 yaliyoshirikisha katika wale wa Kiwango cha Shahada, Stashahada na Astashahada  yaliyofanyika hapo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Rizirki Pembe Juma kwa Niaba ya Pacha mwenzake Waziri wa Elimu Sayansi wa Tanzania akitoa salamu kwenye Mahafali ya 35 ya Chuo Kikuu huria Tanzania.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania hapo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani.
 Wahitimu wa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wakitafakari baada ya kutawadhwa rasmi ufaulku wao wa Udokta.
 Baadhi ya Wahitimu mbalimbali wa Shahada, Stashahada na Astashahada wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa Mahafali yao.
 Baadhi ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kutoka Visiwani Zanzibar wakitafakari mambo mbalimbali baada ya kumaliza mafunzo yao ya ngazi mbalimbali katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambae pia Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanda Peter Pinda akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Welezo Mheshimiwa Saada Mkuya Salum baada ya kupokea Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Picha na – OMPR – ZNZ.

JAJI KAIJAGE : WANANCHI JITOKEZENI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA 3 ZA TANZANIA BARA

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wapiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa kata tatu utakaofanyika kesho (Jumamosi: 19.01.2019) kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi kilichobaki kabla ya  Uchaguzi Mkuu ujao.

Akisoma risala kuhusu uchaguzi huo Jijini Dar es Salaam leo (Tarehe 18.01.2019) Mwenyekiti wa Tume, Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage amesisitiza kwamba watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Jaji Kaijage alizitaja kata zenye uchaguzi kuwa ni pamoja na Kata ya Magomeni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam, Kata ya Mwanyahina katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu na Kata ya Biturana katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma.

“Kesho Jumamosi tarehe 19 Januari, 2019, ni siku ya Kupiga Kura katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata tajwa.  Jumla ya Wapiga Kura 26,282 katika Vituo vya Kupigia Kura 69 watahusika na uchaguzi huu mdogo wa Udiwani,” alisema.

Jaji Kaijage amewaasa viongozi wa vyama vya siasa, wagombea, wafuasi wao na wananchi kwa ujumla wajiepushe na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu wakati wa uchaguzi.

“Pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi, malalamiko hayo yawasilishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Jaji Kaijage amesema kwamba upigaji kura utafanyika katika vituo vilevile vilivyotumika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuongeza kwamba vituo vitafunguliwa kuanzia saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni.

“Iwapo wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari, ambao wamefika kabla ya saa kumi jioni na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura.  Mlinzi  wa kituo cha kupigia kura, atasimama nyuma ya Mpiga kura wa mwisho aliyekuwepo kituoni kabla ya saa 10 jioni. Mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya muda huo,” ameelekeza Jaji Kaijage.

Licha ya kusisitiza kwamba watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Kata husika na wana kadi ya mpiga kura, Jaji Kaijage alisema kwamba Tume imeruhusu matumizi ya vitambulisho mbadala.

“…..Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 62(a) cha Sheria  ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, imeruhusu wapiga kura ambao  wamepoteza kadi zao za kupigia kura au zimeharibika au zimechakaa watumie mojawapo ya vitambulisho vifuatavyo; Pasi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),” amesema Jaji Kaijage.

Alifafanua kwamba mpiga kura ataruhusiwa kutumia vitambulisho hivyo, kwa sharti kwamba jina lake liwemo katika orodha ya Wapiga Kura katika kituo anachokwenda kupiga kura na lifanane kwa herufi, maneno na tarakimu na majina yaliyopo katika kitambulisho mbadala.

Jaji Kaijage alisema kwamba Tume imewaelekeza watendaji wa uchaguzi vituoni wawape kipaumbele wagonjwa, watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali, wanawake wajawazito au wenye watoto wachanga na wazee.

Pia ameelekeza kwamba mpiga Kura mwenye ulemavu wa kutoona, ataruhusiwa kwenda kituoni na mtu atakaemchagua mwenyewe  kwa ajili ya kumsaidia  kupiga kura.

“Wapiga kura wanatakiwa kuondoka vituoni  baada ya kupiga kura na wajiepushe na mikusanyiko au mikutano katika maeneo ya vituo vya kupigia kura..,” ameagiza.

IDARA YA URATIBU MAAFA YARIDHISHWA NA HATUA ZA KUREJESHA HALI DARAJA LA DUMILA

$
0
0
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akikagua sehemu ya kingo za daraja la Dumila, ambalo hivi karibuni kingo za daraja hilo ziliathirika kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Kamati ya Usimamizi wa  maafa  ya mkoa na wilaya  zilichukua hatua ya kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kwa wakati.
 Muonekano wa mawe yaliyowekwa katika Daraja la Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro, ikiwa ni hatua ya kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ya  kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kuweza kupitika. Daraja hilo liliathirika  kingo zake kutokana  na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa juzi.
 Vyombo vya Usafiri, ikiwa ni magari, pikipiki na baiskeli pamoja na watembea kwa miguu wakipita  katika Daraja la Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro, baada ya kingo za daraja hilo zilizo kuwa zimeathiriwa na mvua  kujengwa kutokana na  mvua zilizonyesha wilayani Kilosa juzi.  Hatua hiyo ilifanywa kwa wakati na kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro .
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akimsikiliza Mratibu wa Kurejesha Hali Daraja la Dumila, Mhandisi wa TANRODS- Morogoro, Deogratius, akimueleza hatua walizochukua katika kurejesha hali ya  hilo ambalo hivi karibuni kingo za daraja hilo ziliathirika kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Kamati ya Usimamizi wa  maafa  ya mkoa na wilaya  zilichukua hatua ya kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kwa wakati.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Kilimanjaro Marathon yazinduliwa rasmi Moshi

$
0
0
Mbio maarufu za Kilimanjaro  Premium Lager Marathon 2019 zimezinduliwa rasmi kimkoa katika viwanja vya Kibo Palace Homes, Mjini Moshi  kwa kushirikisha viongozi mbalimbali, wadhamini, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA), waandaaji wa mbio hizo na wadau mbalimbali.

Akizindua mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira aliwapongeza wadhamnini na waandaaji wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager 42km, Tigo-21km Grand Malt 5km  na wadhamini wengine wa meza za maji kwa kazi nzuri na kusema wamezifanya mbio hizi ziwe maarufu zaidi na pia wameendelea kuutagaza Mkoa wake wa Kilimanjaro. 

Mkuu huyo wa Mkoa aliipongeza Kilimanjaro Premium Lager kwa kutoa hamasa kwa watanzania ambapo mwanaume na mwanamke wa kwanza kumaliza mbio za kilometa 42 atapata Sh milioni 1.5 kila mmoja na wa pili watapata Sh milioni 1 kila mmoja. “Hii iwe changamoto kuwafanya watanzania wakimbie kwakasi zaidi ili washinde hata zawadi nyingine kubwa zinazotolewa na waandaaji.

Alitoa wito kwa wafanya biashara kutumia fursa hii vizuri kwani wakati huu wa Kilimanjaro Marathon ndio muda wa kufanya biashara tofauti tofauti. “Wenye mahoteli anzeni kufikiria kutoa ofa mbalimbali ili washiriki watenge muda zaidi wa kukimbia lakini pia kufanya utalii na wenye mabaa na makampuni mbalimbali mnaweza kuandaa promosheni ya wiki nzima kutangaza biashara zenu 

Alipongeza wadhamini wengine wakiwemo KK Security, Keys Hotel, Kilimanjaro Water, TPC Sugar, Simba Cement, AAR, Kibo Palace, Barclays Bank na Precision Air na waandaaji  Wild Frontiers, Deep Blue Media na Executive Solutions ambao ni waratibu wa kitaifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL, Mwamba Stanslaus alisema Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kudhamini mbio hizo kwa miaka 17 sasa kutokana na weledi na uzoefu mkubwa wa waandaaji ambao wamefanya mbio hizo ziwe maarufu sana na moja ya matokeo makubwa nchini huku mwaka huu kauli mbiu ikiwa ‘Mbio ya Watu.’

Alisema kwa mwaka huu, Kilimanjaro Premium Lager imejiandaa vizuri kwani itatoa zawadi zenye thamani ya Tsh milioni 20 ambapo mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 42 kwa upande wa mshiriki mwanaume na mwanamke watapata tsh milioni 4 kila mmoja lakini pia imetoa ofa ya milioni tano kwa watanzania watakaomaliza wa kwanza na wa pili ambapo mwanaume wa kwaza na mwanamke watapata sh milioni 1.5 kila mmoja na wa pili watapata Sh milioni 1 kila mmoja.

Alisema mbio maarufu zakilometa 5 maarufu kama Fun Run, zinazodhaminiwa na Grand Malt pia zitafanyika ambapo watu wa rika zote wanaruhusiwa kushiriki. “Hizi ni mbio za kujifurahisha kwa hivyo watu wa rika zote wanakaribishwa kushiriki ili pia iwe kama sehemmu ya mazoezi huku wakipata kinywaji chao cha Grand malt chenye afya tele,” alisema na kuongeza kuw ambi hizo zimeendelea kuwa maarufu.  

Kwa upande wake, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Lilian Mwalongo alisema: “Tigo tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio maarufu za Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo. Tukiongoza sokoni kwenye mageuzi ya maisha ya kidijiti yakiwamo masuala ya fedha, tunafurahi kwa mara nyingine tena kuwezesha usajili na malipo kwa washiriki kwenye mashindano hayo yajayo kupitia kwa huduma zetu kamilifu za fedha - Tigo Pesa.  

Alisema kwamba kwa miaka kadhaa sasa, Tigo Pesa imethibitishwa kuwa bora zaidi na mfumo wa kuaminika wa malipo kwa wanariadha wote wenye nia kutoka sehemu yoyote nchini.  “Zaidi ya hapo, tunakaribisha kila mmoja kwa ajili ya kupata kumbukumbu za mashindano hayo na kutumia wengine kupitia mtandao wenye kasi zaidi Tanzania wa 4G+,” akasema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kili Marathon Race John Addison, kuna mipango ya kusisimua kwa ajili ya mbio hizo za mwaka huu, ikiwa ni pamoja na wikiendi ya sherehe itakayokuwa ikifanyika mjini Moshi, bustani mwanana ya Kilimanjaro Lager kwenye uwanja mbio zitakakomalizikia pamoja na ubunifu mwingine kadhaa kama picha kwa ajili ya njia maalumu kwa kila mshiriki wa marathion na half marathon.

“Washiriki waendelee kujisajili kupitia mtandao na kufanya malipo kwa kutumia credit card kupitia  www.kilimanjaromarathon.com  au kupitia TIGO Pesa -  Pigal *149*20# kisha fuata maelekezo,” alisema na kuongeza kwamba washiriki wajisajili mapema ili kuepuka usumbufu kwani usajiliutafungwa Februari 7,2019 au nafasi zitakapojaa.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mbio maarufu za Kilimanjaro  Premium Lager Marathon 2019 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Kibo Palace Homes, Mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira  (wa pili kushoto) na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania, Mwamba Stanslaus wakionesha nembo ya Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2019 ili kuashiria uzinduzi wa mbio hizo kimkoa. Wengine kutoka kushoto ni , Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo, Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimajaro Livingstone Mtacha, mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Jaffar Kiongo, Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippy Warioba, Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kibo Palace Patricia Maina na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Kibo Palace Homes Mjini Moshi.

KIKAO CHA MAWAZIRI KUHUSU BOMBA LA MAFUTA KUFANYIKA KAMPALA WIKI IJAYO

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Kikao cha Tatu (3) cha mawaziri wa sekta zinazohusika na utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kinatarajiwa kufanyika Januari 25, mwaka huu jijini Kampala.

Kikao hicho kitakachotanguliwa na vikao ngazi ya wataalamu na baadaye ngazi ya makatibu wakuu wa Wizara husika, kitaongozwa na Mawaziri wenye dhamana ya nishati, ambao ni Dkt. Medard Kalemani (Tanzania) na Mhandisi Irene Muloni (Uganda).

Akizungumza jana, Januari 17, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati jijini Dodoma, wakati wa kikao cha maandalizi kilichoshirikisha timu ya Tanzania inayohusika na usimamiaji wa utekelezaji wa mradi husika; Waziri Kalemani alitoa rai kwa wajumbe wote kufanya kazi kwa ushirikiano, kujituma na weledi wa hali ya juu ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati kwa faida ya Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, alisema anayo imani kubwa na kila mjumbe wa timu husika kwamba kuteuliwa kwao kuwa sehemu ya timu hiyo kumetokana na sifa zao kiutendaji na utaalamu, hivyo akawataka kutomwangusha Rais John Magufuli na Taifa kwa ujumla katika kutekeleza jukumu walilopewa.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, akichangia mjadala katika kikao hicho, alisema Ofisi yake imejipanga kutoa ushauri wote wa kisheria katika kuhakikisha mikataba mbalimbali inayoingiwa baina ya Tanzania na Uganda katika utekezaji wa mradi husika, inafuata misingi yote ya kisheria kwa manufaa ya Taifa.

Awali, akiwaongoza mawaziri, viongozi na wataalamu mbalimbali kupitia na kujadili ajenda za kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua alisema, hadi kufikia Desemba 2018, kazi mbalimbali za awali zimekamilika zikijumuisha tafiti za udongo, miamba na maji katika eneo la kituo cha kupokea, kuhifadhi na kusafirishia mafuta.

Aidha, alitaja kazi nyingine iliyokamilika kuwa ni tafiti za udongo, miamba na maji katika mkuza wa bomba pamoja na maeneo ya vituo vya Mradi; Stadi za mazingira na kijamii (ESIA); Tathmini za mali na utwaaji wa ardhi katika mkuza na maeneo ya kambi za utekelezaji Mradi pamoja na usanifu wa awali wa Mradi.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia na Serikali ya Jamhuri ya Uganda zilisaini Mkataba wa makubaliano, Mei 26, 2017 ambao umeweka misingi ya utekelzaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Tangu kusainiwa mkataba huo, Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT) imefanya vikao mbalimbali vya majadiliano na Timu ya Uganda katika miji ya Dar es Salaam na Arusha (Tanzania) pamoja na Kampala Uganda.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (mwenye miwani-katikati), akiongoza kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kulia kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (mwenye miwani-katikati), akiongoza kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kulia kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Kutoka kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, akifafanua jambo wakati wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mussa Sima wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, akiwaongoza mawaziri, viongozi na wataalamu mbalimbali (hawapo pichani) kupitia na kujadili ajenda za kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.e
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA QATAR OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Spika wa Bunge Job Ndugai (Mb) akizungumza na Balozi wa Qatar nchini  Abdullah Jassim Al-Maadadi Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Qatar nchini Abdullah Jassim Al-Maadadi akimueleza jambo Spika wa Bunge Job Ndugai (Mb) alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
   Spika wa Bunge Job Ndugai (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi wa Qatar nchini Abdullah Jassim Al-Maadadi mara baad ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Job Ndugai (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi wa Qatar nchini Abdullah Jassim Al-Maadadi mara baad ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. PICHA NA BUNGE

KAMATI YA KUDUMU YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA KUSIMAMIA OFISI ZA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA YATEMBELEA OFISI YA RAIS

$
0
0
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa  Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  kwa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa,kulia Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Panya Ali Abdallah, akifuatilia taarifa hiyo wakati ikiwasilishwa katika ukumbi mdogo Ofisi ya Rais Ikulu.
 MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar. Mhe. Panya Ali Abdallah, akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar.
WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar, wakifuatilia Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi  Gavu.wakati akiwailisha taarifa hiyo kwa Kamati katika ukumbi wa Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar. (Picha na Ikulu)

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA MRADI WA KUWEZESHA UMILIKISHWAJI ARDHI (LTSP) MKOANI MOROGORO

$
0
0
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (mb) akisisitiza jambo wakati akitoa maelezo ya utangulizi kwa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira katika mji wa Ifakara kabla ya kuanza kutembelea maeneo ya mradi. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Nape Nnauye (mb)
 Mratibu wa mradi wa kuwezesha Urasimishaji Ardhi (LTSP) Godfrey Machabe akitoa taarifa za mradi kwa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
 Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Nape Nnauye (mb) akiuliza jambo juu ya uandaaji wa ramani ya kijiji kutoka kwa afisa mipango miji wa wilaya ya Kilombero baada ya kamati hiyo kufika katika ofisi za LTSP.
 Kamati ikiwa katika ofisi ya afisa ardhi mteule wa wilaya ya Kilombero ambaye ndiye msajili wa hati za hakimiliki za kimila wakioneshwa jinsi hati hizo zinavyosajiliwa.

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images