Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 268 | 269 | (Page 270) | 271 | 272 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.

  Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.

  Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.

  Stars chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12 mwaka huu kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.
  …5,000/- NDIYO KIINGILIO CHA KUISHANGILIA STARS.

  Kiingilio katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe ni sh. 5,000 wakati tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu (Novemba 18 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

  Mbali ya kiingilio hicho cha sh. 5,000 ambacho ni kwa viti vya bluu na kijani, viingilio vingine ni sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.

  Tiketi zitauzwa katika magari maalumu katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, BMM Salon iliyopo Sinza Madukani, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama, na kituo cha mafuta Buguruni.

  0 0


  Kampeni ya Kili Nani Mtani Jembe inaendelea kuunguruma, mashabiki wa Simba na Yanga katika maeneo mbalimbali Tanzania wanachuana vikali kuhakikisha timu zao zinaibuka na kitita cha shilingi milioni mia moja Taslimu!!..

  Kilimanjaro Premium Lager inawakaribisha kushuhudia Bonanza kubwa la aina yake Jumapili hii tarehe 17 November 2013!, Mashabiki wa Simba na Yanga katika miji ya Tunduma na Morogoro watashindana katika michezo mbalimbali kama vile;
  Foos Ball!!
  Kuvutana kamba!!.
  Soka la wachezaji saba kila upande aka “Seven aside” nk,
  Nyama Choma na Burudani nyingine nyingi zitakuwepo…

  Pale katika Mji wa Tunduma; Bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika uwanja wa Mwaka!!. Kutumbuiza jukwaani watakuwepo High Class Band…. aka Wazee wa Mjini!.

  Na kule Mjini Morogoro – Mji Kasoro Bahari; Bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi “Kiwanja cha Ndege”!!. Jukwaani watatumbuiza…The Bikon Sound!.. aka Wazee wa Pamba!.

  Bonanza za Kili Nani Mtani jembe Tunduma na Morogoro zitafanyika Jumapili hii tarehe 17 November!, kuanzia saa nne asubuhi, Hakuna kiingilio na wote mnakaribishwa!.

  Je wewe ni shabiki wa Simba au Yanga???!!! Njoo usaidie timu yako kuibuka na mkwanja huu mnene wa Kampeni ya Kili Nani Mtani Jembe!

  0 0


  Ngoma maarufu ya kitamaduni ya Sri Lanka ijulikanayo kama 'Ves. Umaarufu wake ni kama Ndingala kwa wanyakyusa, mdundiko kwa Wazaramo, Mbwa Kachoka ama Msewe kwa Zanzibar, Kidumbak kwa Pemba, Ighoboghobo kwa Mwanza,Kuduwa kwa Iringa, Mdumange kwa Tanga, Sangula kwa Morogoro, Mganda kwa Songea, Linguchwu kwa Wamatumb na kadhalika...

  0 0

  Kundi la Black Warriors likiendelea kutumbuiza kwenye kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe Tour’ kwenye baa ya Tanzanite Park iliyopo Kimandoro, Arusha ambayo ipo kanda ya kaskazini na mashariki inayojumuisha pia mikoa, Kilimanjaro na Tanga ambapo mashabiki wa timu hizo wanatakiwa kuzipigia kura timu zao za Simba na Yanga ili zipate pointi nyingi zitakazowezesha kupata fedha nyingi.Jumla ya Tsh. 100Milioni kushindaniwa.
  Wadau wa Simba na Yanga wakionyesha furaha zao wakati wa timu ya kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe Tour’ ilipokuwa kwenye baa ya Tanzanite Park iliyopo Kimandoro, Arusha ambayo ipo kanda ya kaskazini na mashariki inayojumuisha pia mikoa, Kilimanjaro na Tanga ili kuhamasisha upigaji kura kwa mashabiki wa Simba na Yanga ili zipate pointi nyingi zitakazowezesha kupata fedha nyingi.Jumla ya Tsh. 100Milioni kushindaniwa.
  Mshereheshaji wa kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe Tour’, Pendo Robert akimvika jezi ya Simba, Frank James baada ya kushinda kwa kujibu maswali yanayohusiana na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwenye baa ya Tanzanite Park iliyopo Kimandoro, Arusha ambayo ipo kanda ya kaskazini na mashariki inayojumuisha pia mikoa, Kilimanjaro na Tanga ambapo mashabiki wa timu hizo wanatakiwa kuzipigia kura timu zao za Simba na Yanga ili zipate pointi nyingi zitakazowezesha kupata fedha nyingi.Jumla ya Tsh. 100Milioni kushindaniwa.

  0 0

  SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM (DAWASCO) LINAHIMIZA WATEJA WAKE WOTE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM, MIJI YA KIBAHA NA BAGAMOYO KULIPA BILI ZAO KWA WAKATI NA KABLA MWEZI HAUJAISHA.

  MTEJA ULIYETUMIA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA, NENDA SASA KALIPIE KABLA HUDUMA HIYO HAIJASITISHWA NA WAKAGUZI WANAOPITA NYUMBA KWA NYUMBA.

  ZOEZI LA USITISHWAJI WA HUDUMA YA MAJI LIMEANZA RASMI NA LITAHUSISHA WAKAZI WOTE WANAOHUDUMIWA NA DAWASCO.

  KUMBUKA PINDI UTAKAPOSITISHIWA HUDUMA HII GHARAMA YA KURUDISHIWA NI TSH 15,000/ = KWA WATUMIAJI WA MAJUMBANI NA TSH 50,000/= KWA TAASISI NA MAKAMPUNI. EPUKA USUMBUFU LIPIA HUDUMA HII SASA.

  MALIPO YAFANYIKE KUPITIA:

  LIPA BILI YA MAJI KUPITIA BENKI ZA CRDB- 01J1021921900, NMB-20103300047, BARCLAYS- 0014003711 NA BOA-02022460009; MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY NA EZYPESA; MAXMALIPO NA SELCOM; AKIBA MOBILE, EXIM MOBILE, NMB MOBILE NA TPB POPOTE; ATM ZA UMOJA SWITCH.

  LIPA BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE NA KWA WAKATI WOWOTE
  DAWASCO IMESOGEZA HUDUMA KARIBU NA MTEJA

  IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
  DAWASCO MAKAO MAKUU

  0 0
 • 11/18/13--02:29: MWANA FA ALONGA NA VIJIMAMBO
 • Mwanamuziki wa kizazi kipya anaefanya vizuri kwenye tasnia hiyo ya Bongo Flava, Mwana FA leo Jumatatu Novemba 18, 2013 alonga na Vijimambo aelezea historia yake kwa ufupi na kwanini yupo Marekani je yeye ni mfuasi wa Freemason? Je anamchumba? na kama anaye mchumba wake ni nani na lini wataaowa? kati ya Ali Kiba na Diamond nani anamkubali na mengene mengi MSIKILIZE

  0 0

   Mwezeshaji  Beda Msimbe  akiendelea  kuwanoa  wanahabari  wamiliki wa mitandao ya  kijamii nchini ambao  wanapatiwa mafunzo  na  TMF.
  Wanahabari  wa vyombo mbali mbali na  wamiliki wa mitandao  ya  kijamii (Blog) wakiendelea na mafunzo  yao ya siku nne  katika  ukumbi wa Dodoma  Hotel  leo,mafunzo  yaliyolenga  kuboresha uandishi wa mitandao ya kijamii
  Wanahabari  wakionyesha kufurahia mafunzo ya uandishi wa mitandaoni leo mjini Dodoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  MKURUGENZI wa Tamasha la Krismasi, Alex Msama amewataka wafanyakazi wake wa makampuni yake kutangaza uzalendo wa hali ya juu kwa sababu tamasha hilo nia yake ni kutangaza amani na upendo.
  Akizungumza na wafanyakazi wake hivi karibuni, Msama alisema tamasha hilo litakuwa na wageni wengi kutoka nchi mbalimbali sambamba na viongozi wa Tanzania.    
  Msama aliyasema hayo katika maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajia kufanyika Desemba 25 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baadaye mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro.
  “Kila mmoja mfanyakazi awe askari kwa mwenzake ili kufanikisha maendeleo ya Tamasha hilo ambalo litakuwa na dhamira ya kusaidia wanaoishi katika mazingira hatarishi,” alisema Msama.
  Aidha Msama alisema umakini utaongezeka zaidi katika suala la tiketi ambazo zitatoka nje ya Tanzania kwa sababu ya kukwepa wizi unaofanywa na baadhi ya wasilolitakia mema tamasha hilo.
  “Tunajipanga kutengeneza tiketi kutoka nje ya nchi ambazo zimepiga hatua zaidi kimaendeleo ili kukwepa wizi unaofanywa na wajanja wachache wasiolitakia mema tamasha hilo lenye lengo la kusaidia wenye uhitaji maalum,” alisema Msama.

  0 0

  Mkulima wa mbogamboga Bw. Kilalile Shamte akitoa elimu ya lishe bora kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu kuhusu umuhimu wa kula mboga za majani katika mlo wa kila siku. Wakati wa maonesho ya wakulima wadogo yaliyofanyika katika viwanja vya hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kujenga soko kwa wakulima wadogo na kuchochea ulaji wa lishe bora kwa Watanzania. Maonesho hayo yalidhaminiwa na Vodacom.
  Mkulima wa mbogamboga Bw. Kilalile Shamte, akitoa elimu ya lishe bora kwa baadhi ya Wateja waliojitokeza katika maonesho ya Wakulima wadogo wadogo yaliyokuwa na lengo la kutafuta soko kwa wakulima hao na kuchochea ulaji wa lishe bora kwa Watanzania. Pamoja nao katika picha ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu ambao ndio wadhamini wa maonesho hayo.
  Mkulima wa Matunda Bw. Asagwile Mwakilasa akitoa elimu ya lishe bora kwa baadhi ya Wateja waliojitokeza katika maonesho ya Wakulima wadogo wadogo yaliyokuwa na lengo la kutafuta soko kwa wakulima hao na kuchochea ulaji wa lishe bora kwa Watanzania. Pamoja nao katika picha ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu ambao ndio wadhamini wa maonesho hayo.

  0 0

  Viongozi na wasomi mashuhuri wa vyama na taasisi nyeti barani Afrika wanakutana kwenye kongamano la siku mbili kujadili na kupendekeza sera zinazotekelezeka na kuzingatia mazingira ya Afrika ili kuchochea mabadiliko na kuleta maendeleo.

  Kongamano hili limeandaliwa na taasisi za Club de Madrid kwa kushirikiana na UONGOZI Institue. Kongamano litaendeshwa kwa uenyekiti wa marais wastaafu na wanachama wa Club de Madrid, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Festus Mogae rais mstaafu wa Botswana.

  Dhumuni kubwa la kongamano hili ni kutoa fursa kwa viongozi wa Afrika kuchambua mapungufu na vikwazo vya maendeleo Afrika na kupendekeza mifumo mbadala itakayoweza fungua kurasa mpya wa mchakato wa maendeleo.

  Kongamano hili litazinduliwa na mkutano mfupi asubuhi ya tarehe 19, Novemba katika hoteli ya Serena ambapo viongozi kadhaa wa kiserikali, sekta binafsi na vyama vya kijamii wapatao 80 wamealikwa. Mkutano utaongozwa na majadiliano yenye mad ‘Leading Change for Transformation: Experiences from African Leaders’ . Marais wastaafu Benjamin Mkapa na Festus Mogae watatoa uzoefu wao katika kuongoza nchi na mapambano ya kukuza na kuboresha uchumi.

  0 0


  0 0

   Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ukipita leo katika 'mkeka' wa barabara, ulipokuwa ukitokea wilayani Namtumbo kwenda wilayani Songea mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana yuko katika ziara mkoani Ruvuma, kukagua utelekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua, barabara hiyo ni miongoni mwa barabara kadhaa zilizojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwaondolea wananchi kero ya kusafiri kwenye barabara mbovu.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za ujenzi katika Zahanati ya Mahilo wilayani Songea mjini .
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwenye shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya maabara katika shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
   Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wai Ruvuma, kuondosha gogo kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Mahilo, Songea mkoani Ruvuma.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na waasisi wa CCM wilaya ya Songea mjini, kutoka kushoto ni Mzee Hashimu Gawaza na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mzee Clemenci Nyoni ambao walikaa kikao cha kwanza na Mwalimu Nyerere tarehe 12 Agosti 1957 wakati wa harakati za kuikomboa nchi,anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
   Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Wazee hao.

  0 0


  0 0

  Gari la kubeba Wagonjwa la Hospitali ya Manispaa ya Kinondoni likitafuta namna ya kupita kwenye Msongamano wa magari yaliyokuwa yamesimama nila mpangilio kwenye makutano ya barabara ya Shekilango, eneo la Sinza Afrikasana.
   hakuna gari inayoweza kusogea hata kwa hatua moja, maana magari yamesimama bila hata mpangilio.
   wengine ndio wanazidi kutania.

  0 0

   Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Zimbabwe wakiwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ers Salaam.
  Mkuu wa msafara wa timu ya taifa ya Zimbabwe ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Shirikisho la Soka la Zimbabwe (ZIFA), John Phiri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili.
  Meneja wa timu ya taifa ya Zimbabwe, Patrick Mutesva akiwa katika picha ya pamoja na mtangazaji wa Radio One, Omary Katanga (kushoto).
  Nahodha wa timu ya taifa ya Zimbabwe, Simba Sithore akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo huo..
  Wachezaji wa Zimbabwe wakipanda basi la wachezaji.(Picha na Habari Mseto Blog).

  0 0

  Novemba 17, 2013 ilikuwa siku ya furaha sana kwa Beatrice Mroki (kushoto) kwa kupata sakrementi yake ya Kipaimara baada ya kuhitimu mafunzo ya miaka miwili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Ukonga jijini Dar es Salaam. Pichani ni Beatrice akigonganisha glasi na msimamizi wake Neema Steven wakati wa tafrija maalum ya kumpongeza iliyofanyika katika ukumbi wa Samunge Ukonga Mazizini.
   Hapa ilikuwa Kanisani wakisubiri kupokea Kipaimara katika KKKT Ukonga

   Baada ya Kipaimara baba na mama yake Beatrice wakilamba picha na Binti yao.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 11/18/13--07:14: Article 11

 • 0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiteremka katika ndege ya Serikali alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba,akiwa katika ziara ya wiki moja kisiwani huko.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi mbali mbali na Wanancchi, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba,akiwa katika ziara ya wiki moja kisiwani huko.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi mbali mbali na Wanancchi, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba,akiwa katika ziara ya wiki moja kisiwani huko.


older | 1 | .... | 268 | 269 | (Page 270) | 271 | 272 | .... | 3270 | newer