Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 25 | 26 | (Page 27) | 28 | 29 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,ACP ANTHONY RUTHA akikabidhi pikipiki kwa mkaguzi msaidizi wa Polisi,Joseph Matui kwa niaba ya maafisa wote wa Polisi ngazi ya Tarafa Mkoani humo.

  Na Juma Kapipi- Tabora

  Jeshi la polisi mkoani Tabora limepokea pikipiki 13 kutoka kwa Inspekta Jenerali Said Mwema zitakazosaidia harakati za kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika mkoa huo.

  Akikabidhi pikipiki hizo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, ACP Anthon Rutha amesema kuwa,pikipiki hizo zitagawiwa kwa wakaguzi wa kila tarafa wa wilaya za Igunga ,Uyui,Urambo ,Sikonge,Nzega na Tabora mjini kwa lengo la kusaidia ulinzi na usalama wa wananchi.

  Kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Tabora ametoa wito kwa wakaguzi wa kila tarafa kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na si kuzitumia kwa matumizi binafsi na kuwataka wazitunze vizuri kwani kwa kufanya hivyo , kunaweza kusaidia kudhibit uhalifu kwa wakati na kuimarsha amani mkoani hapa.

  Akipokea pikipiki hizo kwa niaba ya wakaguzi wa tarafa mkoani hapa mkaguzi msaidizi wa polisi Joseph Matui wa tarafa ya Tabora kaskazini amesema kuwa, pikipiki hizo zitawasaidia kufika maeneo ambayo wananchi wanahitaji kujua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na juu ya ulinzi na usalama wa mali zao.

  Matui amewataka wananchi kuonesha ushirikiano wa dhati kwa askari polisi kuwafichua waharifu wanaosumbua katika maeneo yao.

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Katibu Mkuu Mstaafu wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Kiafrika (OAU),Dr. Salim Ahmed Salim ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, mara baada ya Mh. Lowassa kutoa maonai yake mbele ya tume hiyo.

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kukusanya Maoni ya Katiba mpya,mara baada ya kutoa maoni yake.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Mjumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba mpya,Dk. Senkondo Mvungi mara baada ya kutoa Maoni yake.

  YAFUATAYO NI SEHEMU YA MAONI ALIYOYATOA MH. EDWARD LOWASSA:

  Kwanza ningependa kukupongeza wewe mwenyekiti Mh Jaji Warioba pamoja na tume nzima kwa imani kubwa ambayo Rais ameionesha kwenu, ni kwa kuwapa jukumu hilo zito na muhimu kwa nchi yetu.

  Wananchi pia wamekuwa na imani kubwa na wamejenga matumaini ya kila kitu kwa tume hii. Kutokana na hilo wamekuwa wakitoa maoni ambayo mengine hayahusiani na katiba, yaani siyo ya kikatiba.Pengine na mimi nitakuwa miongoni mwao, kwa hiyo naomba radhi mapema, iwapo maoni yangu haya mengine , yataonekana si ya kikatiba.

  Katiba yetu ya sasa ni nzuri, imetuongoza katika umoja na mshikamano wa kitaifa kwa muda wote huo.Lakini, kutokana na hali ya dunia ya sasa, ni vyema kuwepo na katiba mpya ili kuendana na hali halisi.

  Kuna mambo manne ambayo kwa imani na mtizamo wangu ningependa yawemo katika katiba yetu ijayo.

  1.ELIMU BURE

  Moja ya haki za mtoto ni kupata elimu. Ningependa suala la elimu bure ya sekondari liwemo kwenye katiba yetu. Katiba itamke wazi kuwa elimu ya sekondari ni bure.Nchi yetu bado ina idadi kubwa ya watu wake ambao ni masikini.

  Uwezo wao wa kipato ni mdogo.Naamini kabisa hili linawezekana na serikali inaweza kugharimia elimu ya sekondari ikawa bure. Hii itatoa nafasi ya kujenga taifa lijalo lenye idadi kubwa ya vijana watakaokuwa wamepata elimu ya sekondari.Wabunge wenzangu bila shaka wanalijua hili.

  Ukweli katika majimbo yetu wazazi wamekuwa wakishindwa kulipia karo ya shule kwa watoto wao. Wabunge tumekuwa tukibeba mzigo huo japo kidogo. Kwa hiyo, kifungu cha ELIMU BURE KWA SEKONDARI, kiwepo kwenye katiba.

  2.ADHABU YA KIFO-DEATH PENALT

  Katiba ya sasa haisemi wazi kuhusu adhabu ya kifo.Inazungumzia tu haki ya uhai.Ibara ya 14 ya katiba hii ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 inatamka kiujumla tu kuwa KILA MTU ANA HAKI YA KUISHI NA UHAI WAKE KULINDWA.

  Lakini , haki hiyo inanyang'anywa na kifungu nambari 196 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16(penal code ,cap 16), kinachotamka kuwa adhabu ya kifo(death penalty or capital punishment) kwa kosa la mauaji ya kukusudia.

  Adhabu hiyo hiyo pia utolewa kwa kosa la uhaini.Sasa mapendekezo yangu mimi ni kwamba kuwe na ibara katika katiba mpya inayotamka wazi kuwa HAKUTAKUWA NA ADHABU YA KIFO HAPA NCHINI HATA KWA KOSA LA KUKUSUDIA AU UHAINI.

  3.MATUMIZI YA FEDHA KATIKA UCHAGUZI

  Katika sehemu nyingi hapa nchini mwananchi kama hana fedha hawezi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.Katiba mpya iwe na ibara inayofafanua ni kiasi gani cha fedha ambacho mgombea anaruhusiwa kutumia katika kampeni.Iainishe ni matumizi gani ya lazima ambayo mgombea hawezi kukwepa kutumia fedha katika kampeni zake, mfano kuwakusanya wapiga kura kwenda kupiga kura gharama hizo nani azibebe.

  Katiba ifafanue rushwa ni nini kwenye chaguzi hizi.Au tuwe na mfumo wa PROPORTIONAL REPRESENTATION ,vyama viwe ndiyo vinaingia kwenye chaguzi kuwania majimbo na siyo wanachama,huko kila mtu atakuwa anapigania chama chake kupata kura nyingi ili wapate viti vingi zaidi, pengine hii itasaidia kuondoa kikwazo cha mtu kuwa na uwezo wa kifedha ndiyo aweze kuwania uongozi.

  4.ARDHI

  Kwa mwanadamu, kunyang'anywa haki ya kutumia ardhi ya nchi aliyozaliwa ni sawa na kunyanng'anywa haki ya uraia wake. Katiba hii ya sasa inawapa nguvu wakulima katika suala la ardhi, na kuwasahau wafugaji.

  Wafugaji wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, wamekuwa wakitangatanga kutafuta malisho ya mifugo yao, ile ardhi waliyokuwa wanaimiliki wakiondoka kutafuta malisho huku nyuma imekuwa ikimilikishwa watu wengine, wakulima au wawekezaji, hili kwakweli si jambo jema .

  Tumeshuhudia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.Kwa hiyo, mimi ningependa katiba hii mpya impe mfugaji haki katika suala la ardhi kama.Ardhi ya wafugaji ilindwe, ifafanuliwe kikatiba haki yao hiyo. Kuwe na hali ya 50,50 situation kati ya mfugaji na mkulima katika suala zima la umiliki wa ardhi,kikatiba!

  0 0

  By Hassan Abbas, Addis Ababa

  All is now set for President Jakaya Kikwete to showcase the country’s endeavors in promoting governance in political, economic, corporate and socio-economic areas under the African Union governance assessment instrument-the African Peer Review Mechanism (APRM).

  According to the program of events released by the Continental APRM Secretariat in the meetings which take place in the margins of the AU Ordinary Summit here, Presidents of Tanzania, Jakaya Kikwete and his Zambian neighbor, Michael Sata will be reviewed.

  The review of the two countries which is scheduled to be on 26 January, 2013 will be preceded by APRM preparatory meetings which start here today with the 59th meeting of the APRM Panel of Eminent Persons. A meeting of Ministers coordinating APRM processes in their countries will take place on Friday.

  APRM is mandated to periodically review progress on good governance through wide consultations of the people at the national level and then a country is finally reviewed by its peers-the rest of the African Heads of States and Governments for constructive discussions on how to move ahead.

  The President Jakaya Kikwete confirmed his participation in the review meeting after a meeting with officials from the APRM Tanzania- a local secretariat of the Continental wide body at State House in Dar es Salaam on Thursday last week in Dar es Salaam.

  “I thank you for a very good work done in coordinating the process in Tanzania. Now I’m more than confident of attending the peer review Forum to present the views of my fellow Tanzanians,” said the President after meeting the officials of the APRM Tanzania National Governing Council and its Secretariat.

  Briefing the President on the process in Tanzania last week, the Minister of Foreign Affairs and International Cooperation, Bernard Membe whose Ministry coordinates the process in Tanzania, said the review of Tanzania was objective one.

  “The report has highlighted the best practices we have in various areas of governance and the challenges that we are facing which should be resolved,” said Minister Membe.

  Tanzania signed the Memorandum of Understanding (MoU) to join the APRM on the 26th May, 2004 and secured formal admission into the process on the 8th July 2004. On the 1st February, 2005 the Tanzanian Parliament ratified the APRM Memorandum of Understanding.

  0 0

  Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki akiogea na viongozi wa PPF Pensheni Fund wakati walipotembelea TSN kufahamiana na kujifunza mambo mbalimbali katika makutano ya barabara za Nelson Mandela na Nyerere Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw.Steven Alfred,Meneja wa Kanda, Mbaruku Magawa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
  Msanifu kurasa wa gazeti la HabariLeo, Ephraim Mwaluvinga (kulia) akiwaonesha jinsi maadalizi ya gazeti yanavyofanywa kwa ugeni kutoka PPF ulipotembelea chumba habari cha gazeti hilo Dar es Salaam jana.
  Mhariri wa Magazeti ya wikiendi ya DailyNews, Ichikaeli Maro akiukaribisha uongozi wa PPF ulipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo. Katikati ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki.
  Fundi Mitambo wa TSN, Rashid Singandole, akieleza jinsi mitambo ya uchapaji ya Standard Printers inayomilikiwa na TSN inavyofanya kazi, kwa uongozi wa PPF uliotembelea kiwanda hicho. Kuanzia kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji,Steven Alfred, na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo,Bi. Lulu Mengele.
  Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki (kulia) akiueleza jambo ugeni wa PPF baada ya kutembelea mitambo ya kampuni hiyo muda mchache kabla ya kuondoka.

  0 0
 • 01/22/13--14:29: Article 13


 • 0 0
 • 01/22/13--14:30: KIJIWE CHA UGHAIBUNI
 • .

  0 0


  Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika mapema jioni ya leo ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba mjini Mwanza.

  Brandts alisema wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

  Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.

  “Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.

  Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.

  Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwaonesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.

  “Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza na Mabalozi wanaziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa ( hawapo pichani) katika mkutano huo uliofanyika siku ya Jumanne, Ban Ki Moon alianisha vipaumbele vyake kwa mwaka 2013, miongoni mwa vipaumbele hivyo lipo suala la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo alisema mwaka huu wa 2013 lazima uwe na mtazamo mpya katika kukabiliana na hali ya DRC

  0 0


  The emerging problem in Mtwara, should not be confused with the African natural resource curse, but rather a new pattern of African awakening in which citizens are rising up to demand what belongs to them in an effort to get out of the poverty . The government of the day must not turn a deaf hear or even politicize the issue in Mtwara. It must re-examine itself carefully, and respect people’s will to save its self. 


  The culture of secrecy in which contract details are negotiated and signed in the darkness by rogue public officials, has particularly imposed heavy economic burden upon the people of Tanzania which has led us to this point.  Mtwara saga is certainly a product of phony contracts which has presented the government of Tanzania with a golden opportunity to review its investment and economic policies that seems to be repressive, deceptive, and not progressive to its people. 


  What is happening in the Democratic Republic of Congo or even in Niger Delta is quite different to what is happening Tanzania. DRC and Niger Delta have militants, factions and separatists in all out war, fighting their governments.  Mtwara residents are on the contrary, waging a different type of war, a peaceful war that can never be defeated by the mightiest army on the face of the planet. And in the wake of rather stunning revelation of inflated cost of the pipeline ($1.2Billion) from the actual price of $600million, their strength has grown and there nothing the government can do but back down and address the mistakes made


  Sand oil discovery in Canada brought economic boom to Alberta residents and Canadian economy as a whole. High school graduates working in the oil industry are earning in excess of $120 an hour which is considered average pay. Albertans are enjoying their natural wealth. Oil companies are investing -giving back- heavily on Alberta’s social programs and causes. 

  On the contrary, Tanzanian residents in Nyamongo; one of the gold rich regions in Africa are much poorer than they were before the Gold mining companies camped on their land. Water sources are polluted; animals are dying and the residents are silently suffering unknown ailments


  Poverty and joblessness are the order of the day, while small scale mining that sustained the community for decades has literally collapsed, yet foreigners have the leverage to be employed as dump truck drivers. Thousands of jobless Nyamongo residents capable of driving forklifts can only standby and watch heavy dump trucks driven by Kenyans, South- Africans, Australians and Canadians move gold-sand from the land that once belonged to them. An obvious problem the government has neglected  


  Legitimate economic reasons are to blame for Mtwara protests. People in the south see natural gas has the only viable way out of poverty. They have seen the problems in Tarime, and are no-longer interested in promises. 

  All they need is action that will improve their lives. The government must not make a mistake of overlooking, politicizing, or even attempting to quell the protests using force. Instead, the government needs a cautious approach to determine the root cause of the problem it is


  Logical government will raise various hypothetical scenarios as to why people in southern Tanzania do not want natural gas to leave their land. In retrospect, various theories will emerge in this self re-examination process.  The government will come into terms with the fact that, this is a new era. 

  An era of internet-citizens, mainly youth that have found a new sense of confidence and self- approval. The government will discover a new generation that no-longer wants to complain and blame others for their misery; a generation that fear no tear-gas, water cannons or bullets. A generation that does not want handouts from foreign entities, rather, wants to sustainably liberate themselves from their ruins of poverty through their God given resources and talents. 


  A new generation that wants jobs, better education, better healthcare and improved infrastructure. We are referring to the generation that knows quite well, that Chinese don’t love them but their wealth. Mtwara people have realized that in the real world, there aren’t always an ending to fairy tales and acts of deception, and that any guarantee of happily ever after, must begin with them; a new awakening. And as long as their grievances are not addressed, the government will never be at ease. 


  They have realized that they must stand on their own and take care of themselves and not rely upon promises they have been hearing for the past fifty some years. Honorable Mwakyembe, Kagasheki, Magufuli and Muhongo are invariably known to be top performers in the current government. Notwithstanding, as long as these leaders are surrounded by indiscipline civil servants, and crooked politicians, architecting the diversion of important national economic projects for their selfish gains, these top performers will remain hostages of the goons, that seem to be in the government’s radar. 


  Citizens of the internet that communicates through text messaging and social networks have been awakened from their sleep and are literally unstoppable. They are no longer interested in political propaganda and the so called CHINESE Aid shrouded with corruption. They know what they need and when they need it. Mtwara is a contagious polity awakening the government must reckon with 


  Mungu Ibariki Tanzania

  0 0

  Na Willy Sumia, Katavi

  JESHI la polisi mkoani Katavi limetakiwa kubadili utendaji kazi wake ili kujenga imani ya ushirikiano baina ya jeshi hilo na wananchi katika juhudi za kuutokomeza uhalifu mkoani humo.

  Hayo yalibainishwa jana na wananchi wa kata ya Kawajense katika mkutano wa hadhara wa polisi jamii uliofanyika katika eneo la Bar ya Web Site iliyoko jirani na shule ya msingi Nyerere katika kata hiyo mjini Mpanda ambapo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi alikuwa akitoa elimu ya polisi jamii kwa wananchi.

  Wananchi hao walilalamikia vitendo vya baadhi ya askari wa jeshi hilo kutoa siri ya watoa taarifa kwa wahalifu na hivyo kujenga chuki na kuhatarisha usalama wa watoa taarifa na hivyo kudhoofisha juhudi za kupambana na uhalifu mkoani humo.

  Wakizungumza wananchi hao waliwasihi viongozi wa jeshi hilo ngazi ya wilaya kuiga utendaji kazi wa aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya hiyo na baadaye kupelekwa mkoani kuwa aliweza kupambana na uhalifu hadi akafanikiwa kuondoa wimbi la ujambazi lililokuwa limeota mizizi wilayani Mpanda.

  Akizungumza katika mkutano huo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari aliwasihi wananchi kutokukata tamaa kwa changamoto ndogo ambazo zinaweza kutatuliwa na yeye mwenyewe tena kwa muda mfupi sana, wanachopaswa kufanya kuanzia sasa ni kumpa taarifa ni askari gani anafanya huo mchezo mchafu wa kiuaji.

  Alisema anachoomba kwa wananchi ni kumpa taarifa kwa njia ya simu kwa namba alizozitoa au kumuona popote watakapokutana naye kuhusu matukio ya kuvujisha siri wanazotoa kwa jeshi la polisi ili aweze kuchukua hatua haraka na kwa wakati ili Katavi iendelee kuwa salama bila majambazi.

  0 0


  Na Anna Nkinda - Paris

  Ushirikiano wa pamoja baina ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na wadau wa maendeleo nchini umeiwezesha taasisi hiyo kuwasaidia na kuwainua wanawake kiuchumi ambao wameweza kujishughulisha na kazi za ujasiriamali na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

  Pia Taasisi hiyo imeweza kutoa ufadhili wa masomo kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi jambo ambalo limewafanya watoto hao wapate elimu sawa watoto wengine wenye wazazi na kuimarisha afya za mama wajawazito na watoto.

  Hayo yamesemwa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipotembelea Taasisi inayoshughulika na masuala ya watoto (France Parrainages) kiliyopo mjini Paris ambacho kinafanya kazi na Kituo cha Ufaransa cha kuwaangalia watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Partage Tanzania inayohudumia watoto yatima katika mkoa wa Kagera.

  Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAMA alisema kuwa Taasisi hiyo imeweza kujenga shule ya Sekondari ya WAMA – NAKAYAMA iliyopo Rufiji Mkoani Pwani ambayo ina wanafunzi 247 ambao ni watoto yatima na matarajio ya baadaye ni kuwa na wanafunzi 780.


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Ladislaus Mwamanga,alipowasili katika Ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili kuhusu Mpango wa Taifa wa Kujenga Uelewa kwa Wajumbe wa kamati za Uongozi na menejment za Tasaf ili kunusuru kaya Maskini,iliofanyika huko Hotel ya Zanzibar beach Resort Mazizini.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili kuhusu Mpango wa Taifa wa Kujenga Uelewa kwa Wajumbe wa kamati za Uongozi na menejment za Tasaf ili kunusuru kaya Maskini,iliofanyika huko Hotel ya Zanzibar beach Resort Mazizini.
  Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Warsha ya Siku mbili kuhusu Mpango wa Taifa wa Kujenga Uelewa kwa Wajumbe wa kamati za Uongozi na menejment za Tasaf ili kunusuru kaya Maskini,iliofanyika huko Hotel ya Zanzibar beach Resort Mazizini.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Ladislaus Mwamanga,alipofungua Warsha ya Siku mbili kuhusu Mpango wa Taifa wa Kujenga Uelewa kwa Wajumbe wa kamati za Uongozi na menejment za Tasaf ili kunusuru kaya Maskini,iliofanyika huko Hotel ya Zanzibar beach Resort Mazizini. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).

  Tuzo hiyo utolewa kwa wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na Flaviana amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba, Flaviana alishinda tuzo nyingine ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.

  Flaviana kwa ambaye kwa sasa anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo New York nchini Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi.

  Tangu ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa aking’ara katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya sita katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza.  Ameweza kushiriki katika maonyesho ya mavaz mengi Ulaya na Amerika huku akitoa misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika mbali katika fani hiyo.

  Kwa sasa Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.

  Maria alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo alikuwa nayo muda mrefu.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,Bibi Liz Lioyd ambaye alimtembelea ofisini kwake magogoni leo.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,Bibi Liz Lioyd (pili kulia)pamoja na maofisa wengine wa Benki hiyo ambao walifika ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni kwajili ya mazungumzo ya kikazi.Picha na Chris Mfinanga.

  0 0


  Habari za Mchana. Pole na Majukumu.


  Napenda kuwahabarisha vijana wenzangu kupitia blog yako tukufu kuwa University of Dar es salaam, Wametoa fursa za nafasi za kazi zaidi ya 50 katika fani mbalimbali. Kwa kijana yeyote atafute Gazeti la Daily news ya leo ukurasa wa 20,21,22.Au abonyeze hapa


  Nawatakia mafanikio mema kwa wale wote watakaoomba.

  Wenu Mdau

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Sinde Warioba, wakati tume hiyo ilipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuchukua maoni yake binafsi ikiwa ni sehemu ya kuchangia maoni ya katiba mpya. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akitoa maoni yake kwa Viongozi wa Tume ya katiba mpya, iliyofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni sehemu ya jukumu la tume hiyo la kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa maoni ya Katiba mpya.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akitoa maoni yake.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, Jaji Augustino Ramadhan,  wakati Tume hito ikiondoka Ikulu baada ya kupokea maoni ya Mhe. Makamu leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa tume ya Kukusanya maoni ya Katiba Mpya, baada ya mazungumzo yao ya kupokea maoni yaliyofanyika leo Januari 23, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na ujumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan. Mheshimiwa Makamu wa Rais amepata fursa ya kukutana na Tume hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


  Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba kabla ya kumruhusu Mheshimiwa Makamu Wa Rais kutoa maoni yake, alimuelezea namna tume hiyo inavyofanya kazi na namna zoezi zima la kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja lilivyofanyika na kisha akaeleza kuwa, tume hiyo inaendelea na zoezi hilo kwa kukutana na makundi maalum sambamba na mtu mmoja mmoja kufuatia umuhimu wa hoja ambazo tume inakutana nazo na hivyo kuhitaji ufafanuzi.   Katika muktadha huo, Jaji Warioba sambamba na kumpa fursa ya kuchangia maoni yake mengine anayopenda alimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais kujikita zaidi katika suala la Muungano kufuatia yeye kuwa na uzoefu wa kiuongozi katika serikali zote mbili yaani ya Muungano sambamba na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.  Akizungumzia suala la Muungano Makamu wa Rais Dkt. Bilal ameieleza Tume kuwa yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni sababu ya kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na kuipambanua kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia.   Pia alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili  umesaidia kujenga na kudumisha udugu, amani na utulivu baina ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa kipindi cha miaka 49 sasa.  Tanzania imechangia kitu kikubwa katika historia, kudumisha Muungano wa mfumo wa serikali mbili kati ya nchi mbili, kubwa na ndogo, jambo ambalo kwa nchi nyingine za Afrika wameshindwa. Kumekuwepo na nchi nyingi ambazo ziliungana na kushindwa kudumu kama tulivyo sisi. Hatuna haja ya kujifunza mfumo mpya wakati tulionao umeweza kudumu, « alisema.  Katika ujumbe wa tume uliofika kuchukua maoni ya Mheshimiwa Makamu wa Rais ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Profesa wa Sheria Palamagamba Kabudi, Ndugu Simai Said, Ndugu Assa Rashid, Ndugu Sasmir Kyuki, Ndugu Salum Athuman, Ndugu Juma Mzalau na Mratibu wa Tume hiyo Ndugu Ramadhan Kailima.

  0 0

  On January 23, U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt met with President of Zanzibar, His Excellency Dr. Ali Mohamed Shein at the State House in Zanzibar. Accompanying the Ambassador at the meeting were the Tanzania Country Directors for U.S. Government agencies: Sharon Cromer from the United States Agency for International Development (USAID), Karl Fickenscher from the Millennium Challenge Corporation (MCC), Brian Rettmann from the President's Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR), Elizabeth O'Malley from the Peace Corps, and Zanzibar Affairs Officer Jefferson Smith. Pictured left to right are U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt, President of Zanzibar, His Excellency Dr. Ali Mohamed Shein, and Chief Secretary Abdulhamid Yahya Mzee.

  0 0
 • 01/23/13--04:14: yale yaleee.....
 • Michuzi,

  Mimi ni mdau wa blog hii tangu imefunguliwa nataka nipeleke ujumbe kwa wadau wote pale geti la kuingilia standi ya ubungo ni hatari sana kuna vibaka amabao ukiingia umebeba mizingo hasa miwili lazima wakusachi na watatimiza azma yao. Ngoja niwape kisa changu cha kusikitisha sana: Weekend iliyopita nikitokea dar kuja Arusha nilifika pale na bajaj mishale ya saa 12 kasorobo.

  Hapa vibaka wanasoma kila anayeingia. Nililipa bajaji na kurudishiwa chenji nikafunga mfuko wangu wa nyuma vizuri nikaaza kuhangahika na mizingo yangu. Kumfikia anayekagua tiketi lilikuwa ni kosa nikahisi kupapaswa makalio kucheki mfuko umeshafunguliwa na pesa inachungulia niligeuka ghafla kijana aliyekuwa nyuma yangu akema kwa uungwana sana " angalia mzee kuwa makini" nikamwangalia anayekagua tiketi nikaona yupo attention anasikiliza nikawa na amani nikamwamini kijana na nikafunga mfuko wangu vizuri kabisa kwani wakati huo nikahisi kwamba labda nilisahau kufunga mfuko wakati natoa nauli ya bajaj nikaendelea mbele mara mtu (mmoja watu kwenye hiyo foleni) akaniambia kama kwa kunisaidia; pitia mlango wa kushoto; nikijaribu huku nasukumana na mizingo yangu mlango hauzunguki kufungua.

  Mara sauti nyingine ikatoka nahisi hii ni ya mkaguzi pitia gei la mkono wa kulia.Kweli nikapita kiulaini kabisa. Kabla sijapiga hatua mbili mbele nikakumbuka je mfuko wangu bado uko salama? salaleeeeeeee! pesa yangu yote 155,000/= imeondoka!Baada ya kuomba wasamalia waiangalizie mizigo yangu nihangahike kutafuta hela ya nauli tena nilirudi pale geti nikwambia wamba nyie kama waangalizi wa hapa mmehusika kuibiwa hela zangu akanijibu...

  kama uliona mfuko wa nyuma umefunguliwa kwanini usibadilishe mfuko mwingine nikagundua kuwa kumbe mechi yote jamaa alikuwa naishuhudia.

  Wadau kaeni chonjo na hapo mlangoni usithubutu weka pochi au pesa mfuko wa nyuma na mbaya zaidi ukitoa nauli wanakuwa wanakuchora.Wakaguzi wa tiketi ubungo bus stand wanashirikiana na wezi.

  Wako mdau,

  Emma Kanindo
  Arusha.

  0 0

   
  Golikipa wa timu ya Black Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
   Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
   Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
   Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
   Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
   Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.
  Sehemu ya umati wa mashabiki wa timu ya Yanga wakifuatilia kwa makini mtanange uliokuwa ukiendelea uwanjani hapo.Kwa picha zaidi Bofya JIACHIE BLOG.

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya vifaa 100 vya kubebea taka vyenye thamani ya sh milioni 3.5,kutoka kwa Meneja Mikopo wa BankABC, Eugenia Shayo (wa pili kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye Ofisi ya Meya,Kinondoni jijini Dar leo.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yusuph Mwenda akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.

older | 1 | .... | 25 | 26 | (Page 27) | 28 | 29 | .... | 3282 | newer