Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109992 articles
Browse latest View live

ATCL CABIN CREW


ASASI ZA VIJANA ZAHIMIZWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
Na OWM (KVAU), Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezitaka asasi mbalimbali zinazoshughulikia maendeleo ya vijana kuwa chachu ya maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la wadau wa asasi za maendeleo ya vijana nchini walipokutana kwa lengo la kukuza uelewa katika kutekeleza programu ya kuwawezesha vijana kati ya Ujerumani na nchi za Afrika (African – German Youth Initiative), Waziri Mhagama alisema kuwa, Serikali kupitia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana na Sera ya Taifa ya Ajira imekuwa ikihamasisha wadau mbalimbali kuanzisha Miradi na Programu zinazowawezesha vijana kupata ujuzi na uzoefu wa kuwaweza kujiajiri au kuajiriwa katika Sekta mbalimbali ili waweze kuchangia kwenye maendeleo ya nchi.

“Vijana ndio chachu kubwa ya maendeleo endelevu, hivyo ni vyema wakatumia fursa zilizopo kuleta mabadiliko yatakayo kuwa na tija na mchango kubwa katika maendeleo ya taifa.” alisisitiza Mhagama

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa vijana wanawezeshwa ipasavyo kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Pia alifafanua kuwa, Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau wanaoshughulika masuala ya maendeleo ya vijana katika kuwajengea ujuzi na uelewa vijana juu ya maendeleo. Hivyo aliipongeza Taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition katika kujenga ustawi na maendeleo endelevu kwa vijana ambao ndio wanufaika wa fursa ya programu hiyo ya mabadilishano ya vijana na Mataifa mengine.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa vijana nchini kufanya kazi kwa bidii na kuendelee kudumisha uzalendo, amani na utulivu.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa alieleza kuwa Programu ya mabadilishano ya vijana (Exchange Program) imekuwa na manufaa makubwa sana katika kuwajengea uwezo vijana kupitia fani mbalimbali zinazoleta mabadiliko ya chanya katika Taifa.

Naye, Mkurugenzi wa Tanzania Youth Coalition (TYC) Bw. Lenin Kazoba alisema kuwa kongamano hilo litakuwa na manufaa kwa vijana na asasi zinazoshughulikia maendeleo ya vijana kwa kuweza kujadili kwa pamoja fursa zitakazoleta maendeleo kwa vijana na jamii inayowazunguka.

Programu ya mabadilishano ya vijana kati ya Nchi ya Ujerumani na Tanzania ilizinduliwa rasmi tarehe 30 Juni, 2016 Mjini Bonn, Ujerumani na Waziri wa Uchumi wa Ushirikiano na Maendeleo Mhe. Gurd Muller ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ilikuwa moja kati ya Nchi Tatu (3) Barani Afrika zilizopewa heshima kubwa ya kuchaguliwa kutekeleza mradi huo kwenye hatua ya majaribio kupitia Tanzania Youth Coalition (TYC). Zaidi ya vijana 4,015 wamefaidika kupitia program hiyo kwa kupata ujuzi na uzoefu wa fani mbalimbali.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la wadau wa asasi za maendeleo ya vijana nchini walipokutana kujadili maendeleo ya vijana kupitia programu ya mabadilishano ya vijana (Exchange Program) kati ya Nchi ya Ujerumani na Tanzania. Kongamano hili limefanyika hoteli ya Morena Januari 16, 2019, Jijini Dodoma.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa kongamano la wadau wa asasi za maendeleo ya vijana nchini walipokutana kujadili masuala ya maendeleo ya vijana.
 Mkurugenzi wa Tanzania Youth Coalition (TYC) Bw. Lenin Kazoba akifafanua kuhusu programu ya mabadilishano ya vijana kati ya Nchi ya Ujerumani na Tanzania kwa wadau wa maendeleo ya vijana walioshiriki kongamano hilo lililofanyika Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wadau wa asasi zinazoshughulikia maendeleo ya vijana nchini wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kuhusu taulo za kike kutoka kwa Bi. Josephine Lyengi, alipokuwa akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na vijana. (Kulia) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa, (Kushoto) ni Mkurugenzi wa Tanzania Youth Coalition (TYC) Bw. Lenin Kazoba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa Taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition (TYC) mara baada ya kufungua kongamano hilo lililofanyika Jijini Dodoma. (Kulia) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa, (Kushoto) ni Mkurugenzi wa Tanzania Youth Coalition (TYC) Bw. Lenin Kazoba.

TAASISI YA SLYNN YA NCHINI UINGEREZA YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA MAHAKAMA YA TANZANIA

$
0
0

Na Mary Gwera, Mahakama
Taasisi ya Slynn ya nchini Uingereza imeahidi kushirikiana na Mahakama ya Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo kutoa Mafunzo kwa Waheshimiwa Majaji ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.
Akimzungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania mapema Januari 15, Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo inayojishughulisha na masuala ya Haki, Bi. Alison Fenney alisema kuwa lengo la ziara yao ni pamoja na kutaka kubaini maeneo ya ushirikiano. 
“Lengo la kutembelea Mahakama ya Tanzania ni pamoja na kujua taratibu mbalimbali za uendeshaji mashauri, kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi na vilevile kuona jinsi gani Taasisi inasaidia katika maeneo yatakayobainishwa,” alisema Bi. Fenney.
Katika msafara huo Bi. Fenney aliambatana na Majaji Wastaafu,  Lord Bonomy na Nic Madge pamoja na Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Catherine Cooke ambao kwa  pamoja walifanya mazungumzo na Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na ugeni huo, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma aliainisha baadhi ya changamoto ikiwa ni pamoja na baadhi ya wananchi kukosa huduma za Mahakama katika maeneo waliopo au kusafiri umbali mrefu kupata huduma hiyo kutokana na kukosa majengo.
“Tanzania ni nchi kubwa, hivyo kuna baadhi ya maeneo ambayo wananchi hawapati huduma ya Mahakama au hutakiwa kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo,” alieleza Jaji Mkuu.
Aidha, Jaji Mkuu aliongeza kuwa, idadi ya Majaji ni ndogo ukilinganisha na wingi wa mashauri yaliyopo ambapo alisema kuwa kila Jaji anasikiliza wastani wa kesi 400 kwa mwaka kiwango ambacho ni kikubwa.
Kufuatia changamoto hizi, Jaji Mkuu alieleza kuwa Mahakama iliona ni vyema kuandaa Mpango Mkakati ambao unatumika kama dira katika kutatua changamoto mbalimbali. 
Aliongeza kuwa Mpango Mkakati huo umejielekeza katika maeneo/nguzo kuu tatu (3) ambazo ni Utawala bora, Uwajibikaji na Usimamizi wa Rasilimali,  Upatikanaji na utoaji haki kwa wakati na Kurejesha imani ya jamii na ushirikishwaji wa wadau.
Taasisi ya Slynn iliyopo nchini Uingereza ina takribani umri wa miaka 30 inajihusisha na masuala ya haki na sheria na inafanya kazi  kwa karibu na Majaji na Taasisi za haki duniani ili kuboresha mifumo ya utoaji haki na uongozi wenye kufuata misingi ya sheria.
Ujumbe huo ambao utafanya ziara ndani ya Mahakama kwa siku tatu umejielekeza kujua zaidi jinsi gani Mahakama ya Tanzania inafanya katika suala zima la Usuluhishi ‘Mediation’ na masuala mengineyo. 
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyeketi mbele) akizungumza na Ujumbe kutoka Taasisi ya Slynn iliyopo nchini Uingereza, katika mazunguzo hayo walikuwepo pia Viongozi Wakuu wa Mahakama;  Jaji Kiongozi, Msajili Mkuu pamoja Naibu Msajili Mwandamizi –Mahakama ya Rufaa.

Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Sarah Catherine Cooke akizungumza jambo.

Jaji Mstaafu wa Mahakama  nchini Uingereza, Lord Bonomy (kushoto) akiongea jambo. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Catherine Cooke, kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama-Uingereza, Jaji Nic Madge. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania,  Prof. Ibrahim Juma (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wageni na baadhi ya Maafisa wa Mahakama  waliomtembele,  katikati ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Eliezer Feleshi, wa nne kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Catherine Cooke, wa pili kushoto ni Jaji Mstaafu wa Mahakama nchini Uingereza, Jaji Lord Bonomy, wa nne kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama nchini Uingereza,  Jaji Nic Madge wa tatu kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Slynn, Bi. Alison Fenney, wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati na wa kwanza kulia ni Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama ya Rufani (T), Elizabeth Mkwizu.
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati (wa nne kulia akiwaonesha Wageni kutoka Taasisi ya Slynn, Ukumbi wa Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Wageni hao walipata nafasi ya kutembelea kituo hicho na kujionea ‘Video Conference’ iliyofungwa katika kituo hicho, vilevile wageni hao walifanya mazungumzo na Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Eliezer Feleshi.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

Mjue Inayat Kassam aliyejitolea kuokoa maisha ya wananchi kwenye mashambulizi ya Riverside na Westgate

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
INAYAT Kassam ambae ni Mkurugenzi wa kampuni ya Scorpio Africa Ltd amejizolea umaarufu tena baada ya kuwa mmoja wa Watu waliojitolea kuokoa manusura wa shambulizi la Kigaidi la Westgate mwaka 2013 na kuendelea kupata sifa baada ya kujitokeza kwa mara nyingine  kuokoa Watu waliokuwepo eneo Riverside Nairobi, Kenya lililoshambuliwa na Magaidi wa Alshabaab jana.
Septemba 21 miaka 6 iliyopita wakati magaidi walipovamia Westgate na kuua watu 62 Inayat alijitokeza na kushirikiana na vyombo vya dola na kuwanusuru mamia ya watu.
Akiwa mkufunzi wa usalama na mjuzi wa kutumia silaha za moto alijitokeza tena jana eneo la Riverside na kushirikiana na vyombo vya dola kuwaokoa manusura.

Watu wengi wamemshukuru na kumwita shujaa wa Kenya kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA KAMPUNI YA TANZAPLUS

$
0
0
Waziri wa Madini, Doto Biteko tarehe 16 Januari, 2019 amekutana na kampuni  inayojishughulisha na uyeyushaji wa madini ya bati katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ya Tanzaplus katika Ofisi za Wizara ya Madini zilizopo jijini Dodoma.  Kikao chake  pia kilishirikisha Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Mhandisi Migodi Mkuu kutoka Tume ya Madini, Conrad Mtui pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Madini. 

Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kampuni ya Tanzaplus Minerals kwa kushirikiana na kampuni nyingine ya AIMGROUP kutambulisha teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa madini. Waziri Biteko aliitaka kampuni ya Tanzaplus kuendelea kufanya utafiti zaidi juu ya mfumo husika kwa kushirikisha wadau mbalimbali  kabla ya kuwasilisha pendekezo lake Serikalini.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akizungumza na watendaji wa kampuni inayojishughulisha na uyeyushaji wa madini ya bati katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ya Tanzaplus. Waliokaa kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini, Augustine Ollal, na Upendo Fatukubonye na Hamis Mhando ambao ni watendaji kutoka kampuni ya Tanzaplus.
 Mkurugenzi kutoka kampuni ya Tanzaplus, Hamis Mhando (kulia) akielezea  jinsi teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa madini inavyofanya kazi.
Wataalam kutoka Wizara ya Madini wakinukuu maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) 

MKURUGENZI IDARA YA URATIBU MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA MJI MPYA WA SERIKALI, IHUMWA, DODOMA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu  wa Mzinga Holdings Company, Meja Jenerali, Seif Makona ambaye ndiyo Mkandarasi anayejenga Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji mpya wa serikali akiteta na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, wakati Mkurugenzi Matamwe alipotembelea eneo la ujenzi wa ofisi hiyo, leo tarehe 17 Januari, 2019.
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akiangalia shughuli za ujenzi wa  Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji mpya wa serikali, Ihumwa, Dodoma, leo tarehe 17 Januari, 2019.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akiongea na moja ya mafundi kutoka Mzinga Holdings ompany wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa  Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji mpya wa serikali, Ihumwa, Dodoma, leo tarehe 17 Januari, 2019.
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akiongea na Mratibu Ujenzi Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka Mzinga Holdings Company wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa Ofisi hiyo,  katika Mji mpya wa serikali, Ihumwa, Dodoma, leo tarehe 17 Januari, 2019.

KAMATI YAPOKEA MAONI YA WADAU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengelwa akizungumza katika Kikao cha kukusanya maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa, kulia kwake ni Makamu Mwennyekiti wa Kamati hiyo, Najma Giga.
Wadau mbalimbali wakiwa wamejitokeza katika Kikao cha Kamati ya Bunge Katiba na Sheria kwa ajili ya kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Msekwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengelwa.

KIKAO CHA KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA CHAFANA

$
0
0

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mwanne Nchemba akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Jijini katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, katikati ni Katibu wa Kamati, Eunice Shirima na wa kwanza ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jason Rweikiza.
Naibu Waziri , Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara akifuatilia hoja za wajumbe wa Kamati Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Jijini katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo Kamati imepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu utendaji wa Tume ya Utumishi katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka 2018.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Jijini katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo wamepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu utendaji wa Tume ya Utumishi katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka 2018.

MAHAKAMA YAAMBIWA MBOWE AMESHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI KWASABABU ANAUMWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anayekabiliwa na kesi ya jinai namba 112 ya mwaka huu na wenzake nane, leo Januari 17,2019 ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi hiyo kwa kuwa anaumwa.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH). 

Wakili Mwita amedai kesi hiyo leo,ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini wamepata taarifa kutoka Magereza kuwa mtuhumiwa ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu anaumwa hivyo, ameiomba mahakama kuipangia tarehe nyingine kutokana na usikilizwaji wa rufaa ya dhamana ya washatakiwa Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko kwenye Mahakama ya Rufaa.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo mpaka Januari 31 mwaka huu.Mbali na Mbowe na Matiko, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu bara John Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa bunda, Esther Bulaya, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.


ZITTO ANANIUMIZA SANA KICHWA-SPIKA NDUGAI

$
0
0
*Akiri kumuonea huruma kwani bungeni yupo peke yake,amshangaa kupotosha umma

*Apigilia msumari kwa CAG Profesa Assad,asema asipofika atajua nani muajiri wake

Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ametoa msimamo wake kwa mara nyingine kuhusu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad kuwa lazima atafika kwenye Kamati ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Maadili huku akieleza kuwa moyo wake unapata taabu sana kwa Mbunge wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe.

Akizungumza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine Spika amemzungumzia Zitto kwa kueleza kuwa amekuwa akipotosha umma kuhusu kinga ya CAG."Kuna rafiki yengu mmoja yupo Uganda , kule Uganda CAG ni Ofisa wa Bunge,na Ofisa wa Bunge anaweza kumgomea Spika? Mihimili iko mitatu na niwahakikishie CAG hiyo tarehe 21 atakuja tu.

"Wengi ambao wanaongea kuhusu hili anajua wanatoka upande gani,wapinzani wengi wao wanawaza kupinga tu," amesema Spika Ndugai na kufafanua kama nchi kuna fedha nyingi zinatumika Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani kwa ajili ya kuitangaza nchi lakini anatoka Ofisa wa Serikali anakwenda nje kuisema nchi.

"Huwezi kutoka hapa halafu unakwenda kuisema nchi vibaya.Kazi yetu sote ni kuhakikisha nchi inakaa vizuri," amesema Spika Ndugai huku akisema anasikitishwa na namna Zitto anavyopotosha umma."Zitto amekuwa akinipa tabu sana ,niseme tu kutoka moyoni.Pale Bungeni inakuwa rahisi kuwafukuza wabunge wengine wanapofanya makosa maana hata ukiwafukuza wengine wapo lakini Zitto kwenye Chama chao mbunge ni mmoja.

" Hivyo naamua kumuacha tu kwa kutumia busara lakini ukweli huko mbele ya safari nitachoka na niyamchukulia hatua.Bungeni pale watu wanashindana kwa hoja na inaungwa mkono na wabunge wengine."Ndio maana wabunge wakiunga mkono wanne ujue hilo jambo linatupwa na Zitto anakwama kwasababu hana wa kumuunga mkono katika mambo yake,"amefafanua Spika Ndugai.

Ameeleza kwa sasa wabunge wengine wako Dodoma wakiendelea na Kamati za Bunge lakini Zitto yupo Dar es Salaam anahangaika kwenye korido kuhusu kuupinga muswada wa vyama vya siasa." Muswada unaendelea kama kawaida, na ukifika Bungeni utapitishwa .Zitto alitakiwa kuwa kule ili atoe maoni yake ili yafanyiwe kazi,"amesema Spika.

Akifafanua zaidi kuhusu kumuita Mdhibiti na Mkagazi wa Hesabu za Serikali kwenye kamati, amesisitiza lazima aende kuhojiwa na kamati husika na nia njema tu kwani kabla ya kuchukua hatua lazima utoe haki kwa mhusika kupata nafasi ya kujieleza na asipofika atajua nani muajiri wake.

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA WAWEKEZAJI WENYE NIA YA KUFUNGUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NCHINI

$
0
0
Na Samwel Mtuwa - Dodoma

Waziri wa madini Mh Doto Biteko leo  Januari 17/2019 amekutana na wawekezaji wa kiwanda cha Nyakato Gold Refinery (NGR) ofisini kwake jijini Dodoma , wenye nia ya kufungua kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu kwa kiwango cha asilimia 99.5 kwa lengo la kuongeza thamani pamoja na kuboresha soko la dhahabu nchini inayotoka kwa wachimbaji wadogo na wakati. 

Kabla ya majadiliano kuanza waziri Biteko alipokea taarifa juu ya namna ya kiwanda hicho cha NGR kitakavyofanya kazi ya ununuzi na usafishaji wa dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wakati, ambapo baadhi ya mapendekezo yaliyowasilishwa na NGR ni juu ya matarajio ya usafishaji wa dhahabu kwa kiasi cha kg50 kwa siku na tani 1.5 kwa mwezi. 

Baada ya majadiliano hayo waziri amewataka wawekezaji hao kuandaa na kuwasilisha andiko la mpango mkakati wa wazi utakaonesha namna uendeshaji wa kiwanda hicho utakavyofanyika ikiwa pamoja na namna serikali itakavyofaidika na uwekezaji huo ndani ya sekta ya madini. 

Tanzania ni nchi ya nne barani afrika katika uzalishaji wa madini ya dhahabu ikiongozwa na nchi ya Ghana naAfrika kusini . 

Pichani waziri wa madini Mh Doto Biteko mwenye suti ya rangi ya Blue aliyekaa mbele akiwa ofisini kwake jijini Dodoma akiongea na wawekezaji wenye nia ya kufungua kiwanda cha kusafisha dhahabu kitakachojulikana kwa jina la Nyakato Gold Refinery (NGR), wengine waliyekaa upande wa kushoto mwekezaji mwenye asili ya India Vaya Rajendra, anayefuata pembeni upande wa kulia ni Baraka Ezekiel yeye ni muhamasishaji kutoka NGR, wengine waliokaa upande wa kulia katika sofa ni watendaji kutoka wizara ya madini pamoja na Tume ya Madini wakifuatilia majadiliano.

KAMATI YAPOKEA MAONI YA WADAU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
 Wadau mbalimbali wakiwa wamejitokeza katika Kikao cha Kamati ya Bunge Katiba na Sheria kwa ajili ya kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Msekwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mohamed Mchengelwa. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengelwa akizungumza katika Kikao cha kukusanya maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa, kulia kwake ni Makamu Mwennyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Najma Giga.

Tanzania kushiriki Maonesho ya Biashara ya Dunia ya EXPO 2020

$
0
0
Tanzania itashiriki Maonesho ya Dunia ya Biashara (Expo 2020 yatakayofanyika Dubai kuanzia mwezi Oktoba 2020 na kumalizika mwezi April 2021.

Uwekaji saini wa Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho hayo ulifanywa tarehe 16 Januari 2019 na Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

Kwa upande wa UAE, mkataba huo uliwekwa saini na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali.

Baada ya uwekaji saini wa Mkataba huo, Mhe. Balozi Mbarouk alieleza kuwa Serikali inayapa umuhimu mkubwa maonesho hayo kwa kuwa ni fursa adhimu ya kuitangaza Tanzania kwenye sekta za uwekezaji, biashara, viwanda, utalii na mila na utamaduni.

Aidha, Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020 alieleza kuwa amefurahishwa na hatua ya Tanzania kusaini Mkataba huo ambapo itatoa fursa kwa nchi kujiandaa mapema na taratibu nyingine za ushiriki.

Baada ya uwekaji saini wa Mkataba huo,` kitakachofuata ni utayarishaji wa simulizi ya maudhui ya maonesho (pitch story) ambayo inatakiwa kuthibitishwa na Kamati ya Kitaifa ya Tanzania ya DUBAI Expo 2020. Simulizi ya maudhui hayo yatahusu vipaumbele vya Tanzania kama vile maendeleo ya viwanda, miundombinu, masuala ya biashara na uwekezaji, utalii, kilimo, elimu, afya, sanaa na utamaduni. Simulizi ya maudhui pia itatumika katika kusanifu muonekana wa banda la maonesho la Tanzania.

Tanzania inakuwa miongozi mwa nchi washiriki zipatazo 100 ambazo tayari zimesaini Mkataba wa Ushiriki tangu Dubai ilipochaguliwa kuwa mwenyeji wa maonensho hayo.Wengine walioshuhudia uwekaji saini wa Mkataba huo ni Bw. Ali Jabir Mwadini, Kansela Mkuu, Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai; Bi Samira Ahmed Diria, Afisa Ubalozi; na kwa upande wa DUBAI EXPO 2020 ni Bi Manuela Garcia Pascual, Mkurugenzi wa Washiriki wa Kimataifa na Bi. Esther Omondi, Meneja wa Nchi/Afisa dawati la Tanzania.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.
17 Januari 2019


Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakiweka saini Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Biashara ya Dunia (Dubai Expo 2020. Uwekaji saini huo ulifanyika Dubai jana Januari 16, 2019.

Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakionesha Mkataba mara baada ya zoezi la kuweka saini kukamilika.

Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wao.

Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakibadilishana mawazo mara baada ya zoezi la kuweka saini kukamilika.

WATENDAJI WA NEC WAKAGUA VITUO VITAKAVYOTUMIKA KUPIGIA KURA KATIKA UCHAGUZI MDOGO KATA YA BITURANA WILAYANI KIBONDO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe (suti nyeusi), Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe Dk. Gabriel Chitupila na baadhi ya Maafisa wa NEC  wakiangalia orodha ya majina ya Wapiga Kura iliyobandikwa nje ya Kituo cha Kupigia Kura kilichojengwa katika eneo la wazi la uwanja wa Mpira wa Magereza  katika Kata ya Biturana wilayani Kibondo. Kata hiyo inafanya uchaguzi mdogo wa Udiwani Januari 19, 2019.
 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo Dk. Gabriel Chitupila akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe (suti nyeusi) kuhusu maandalizi ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Biturana mara baada ya kutembelea Kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Nengo wilayani humo.
 Baadhi ya wakazi wa Kata ya Biturana katika Halmashauri ya wilaya ya Kibondo wakikagua majina yao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililowekwa wazi katika eneo lao. Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata ya Biturana utafanyika Januari 19 mwaka huu ukihusisha vyama 3 vya Siasa.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe (suti nyeusi), Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo Dk. Gabriel Chitupila na baadhi ya Maafisa wa NEC wakikagua vituo vya kupigia Kura katika Kata ya Biturana wilayani humo itakayofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani Januari 19, 2019.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe akizungumza na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi (hawapo pichani) watakaosimamia uchaguzi mdogo wa udiwani Katika Kata ya Biturana wilayani Kibondo Januari 19 mwaka huu. Picha na NEC – Kibondo.

WAZIRI WA KILIMO AIAGIZA BODI YA TUMBAKU KUHAKIKISHA TUMBAKU YOTE ITAKAYOVUNWA MSIMU HUU INAUZWA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisiitiza jambo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi - Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri akitoa taarifa ya Mkoa huo mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kabla ya kufungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 
Mzee Hassan Wakasuvi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi ya Tumbaku akitoa maelezo ya awali kuhusu Tumbaku wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Shinyanga (KACU) na baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi - Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora leo tarehe 17 Januari 2019. 


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Tabora


Bodi ya Tumbaku nchini imeagizwa kuhakikisha kuwa Wakulima wote wa zao hilo wanasajiliwa katika mfumo unaoeleweka kwani hilo ni lengo la haraka la Wizara kwa taasisi zote la kuwasajili wakulima wote nchini ili kujua kiasi cha maeneo wanayolima.

Hayo yameelezwa leo tarehe 17 Januari 2019 na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ndogo ya Tumbaku katika ukumbi wa Mwanakiyungi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Mhe Hasunga ameitaka Bodi ihakikishe kwamba tumbaku yote itakayovunwa msimu huu inauzwa ifikapo Juni 2019 sambamba na kuagiza masoko kuwahi kuanza msimu huu ili kurahisisha kuanza mapema maandalizi ya zao hilo msimu wa 2019/2020.

Vilevile Waziri Hasunga ameagiza upatikanaji wa pembejeo kwa wakati. “Hili linaenda sambamba na utekelezaji wa Agizo la Mhe: Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) - Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuhakikisha unakuwepo utaratibu wa kumwezesha mkulima anajitegemea kwa pembejeo ili aache kuwa tegemezi wa mikopo ya mabenki” Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga alisisitiza kuwa lazima Bodi kutilia mkazo malengo ya muda mrefu kwenye Tumbaku ambayo ni pamoja na utafutaji wa masoko (mhakikishe mnapata wanunuzi wengine wapya ifikapo 2022), Kuhakikisha kuwa kwa ubia au ushirikiano uliopo kijengwe kiwanda kipya cha kuchakata tumbaku ili kutoa ushindani wa gharama za uchakataji wa tumbaku nchini, Kuongeza ubora wa zao kutoka asilimia 87 ya sasa hadi asilimia 92 ifikapo June 2022 na Kuongeza mbegu mpya na bora za tumbaku ili kuweza kupenyeza katika masoko ya nchi zingine kama China n.k.

Tumbaku ni miongoni mwa mazao makuu matano ya kimkakati ya biashara katika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe: Dkt. John Joseph Pombe Magufuli – Rais waJamhuri ya Muunganowa Tanzania. Mazao hayo ni Tumbaku, Kahawa, Pamba, Korosho, na Chai. Takwimu zinaonesha kwamba kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 hadi kufikia mwaka 2016 tumbaku imekuwa na mchango mkubwa kuliko mazao mengine makuu ya biashara kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni. 

“Natambua juhudi mnazofanya katika hifadhi ya mazingira. Lakini mnatakiwa muongeze juhudi kwani taarifa zinaonesha kuwa hadi kufikia msimu wa kilimo uliopita wa 2017/2018 wastani wa miti iliyopona baada ya kupandwa na wakulima ni asilimia 40.46 tu, kiwango hiki hakiridhishi maana kiko chini mno” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema Ili uzalishaji wa tumbaku uwe katika mtazamo wa kibiashara wataalam mnapaswa kuwaelimisha wakulima ili waelewe kwa dhati umuhimu wa kuzingatia taratibu za kilimo cha tumbaku (Compliance). 

Alisema kuwa Baadhi ya wakulima katika vyama vya msingi vya ushirika wameshindwa kulipwa malipo yao kutokana na vyama kuwa na madeni yasiyokuwa wazi na yasiyolipika. Hali hii imesababishwa na ubadhirifu wa baadhi viongozi na watendaji wasio waaminifu katika ushirika, utoroshaji na ulanguzi wa tumbaku. 

Moja ya maeneo yanayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na masuala yanayohusu hatua za kutatua changamoto za kulikomboa zao la tumbaku na kulipa sifa zinazohitajika katika soko la dunia. Mfano wa masuala hayo ni pamoja na Wingi na ubora wa zao, Kuongeza tija, Malipo stahili kwa wakulima, Utunzaji wa Mazingira na Kuzuia utumikishwaji wa watoto.

Kupitia mkutano huo Waziri wa Kilimo amebainisha kuwa Serikali iko thabiti kusimamia uendelevu na uzalishaji wenye tija wa zao la tumbaku kama zao mojawapo la biashara la kimkakati. Ni kwa msingi huo, Serikali inaendelea na jitihada za kupata ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili tasnia ya tumbaku.

“Tarehe 28-30/12/2018 niliwaita viongozi wa Bodi za mazao ikiwa ni pamoja na Bodi ya Tumbaku na kuwapa malengo ya muda mfupi (Januari - Juni, 2019) na mrefu (Julai - Juni, 2022) ni pamoja na nyie wadau katika nafasi zenu mshirikiane ili kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa” Alisisitiza

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri alisema kuwa mkutano huo maalumu wa mwaka wa wadau wa Tumbaku ni mkutano ambao upo kwa mujibu wa sharia ya sekta ya Tumbaku Na 24/2001 kifungu cha 49 cha marekebisho ya sheria yam waka 2009 ambao imeweka ulazima wa wadau kukutana walau mara moja kwa mwaka kujadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta hii na kutatua changamoto zilizopo na kukubaliana utaratibu wa ugharamiaji wa majukumu ya pamoja ambayo yameainishwa na sharia ya sekta ya Tumbaku.

Alisema uwepo wa mkutano huo umekuwa miongoni mwa mikutano yenye tija kwa kukutanisha madau wote na kuwa na mikakati ya pamoja, kuongeza ufanisi wa masoko ya Tumbaku, na uhai wa kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa pamoja.

Kwa upande wake Mzee Hassan Wakasuvi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi ya Tumbaku akitoa taarifa ya utangulizi wakati wa mkutano huo alizitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Tumbaku kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa mkakati utakaotekeleza na shirikishi wa uhifadhi wa mazingira, kuchelewa kwa upatikanaji wa mikopo ya pembejeo kwa ajili ya kununua pemebejeo za kilimo.

Zingine ni utaratibu wa upatikanaji wa bei ya zao la Trumbaku katika kuhakikisha kuwa bei inapatikana mapema na kwa wakati, kushuka kwa mahitaji ya Tumbaku katika soko la Dunia, Kushuka kwa ubora wa Tumbaku ambao unachangiwa na masuala mbalimbali, Vita dhidi ya matumizi ya Tumbaku Duniani na kuboreka kwa bei ya pembejeo.

Sambamba na hayo pia ameishukuru serikali kwa mchango wake kwenye sekta ya Tumbaku kwa ushirikiano inaouonyesha katika suala la kuhakikisha kuwa wanapatikana wasambazaji wa pembejeo za kilimo na kufanikiwa kupunguza bei ya pembejeo za kilimo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

KIKAO CHA WADAU WANAOTEKELEZA MPANGO MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO JIJINI DODOMA

KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI IMALIZIE MAZUNGUMZO YA SHILINGI BIL.345 ZA UTALII KUSINI

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge  Ardhi, Maliasili na Utalii imeishauri Serikali imalize mazungumzo na Benki ya Dunia juu ya hatma ya mkopo wa mradi wa kukuza utalii kwa upande wa kusini baada ya Benki hiyo kuonesha kusuasua kufuatia Serikali ya Tanzania kusimamia uamuzi wake wa kuanzisha Mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji.

Hatua hiyo inakuja baada ya serikali ya Tanzania kukopa jumla shilingi bilioni 345 kutoka Benki ya Dunia ili kukuza utalii katika maeneo ya Kusini kupitia mradi ujulikanao kama Resilient Natural Resource Management for Tourism Growth ( REGROW)

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti Kamati hiyo, Mhe .Nape Nnauye baada ya Kamati hiyo  kufanya ziara katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni moja ya ziara ya  kutembelea ukanda wa kusini kwa ajili ya kuona mkopo huo umefikia wapi na namna mradi huo unavyotekelezwa.

Amesema uamuzi huo  wa Serikali wa kutaka kufungua Utalii wa Kusini ni wa muhimu sana hata endapo mazungumzo hayo yanayoendelea yatakwama Serikali ifikirie mbadala wake lengo likiwa ni kuongeza mapato yatokanayo na utalii.

Katika mradi huo Hifadhi za  Mikumi, Ruaha, Udzungwa pamoja na Pori la Akiba la Selous zinatarajiwa kunufaika kupitia mkopo huo  lengo likiwa ni kufanya ukanda wa kusini kuwa lango la Utalii kama ilivyo kwa ukanda wa kaskazini.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ameishauri Serikali kuwa endapo fedha za  mkopo huo zitapatikana iandae utaratibu wa kuufanya mradi huo uwe wa kibiashara badala ya ilivyo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha hizo yamejikita katika uhifadhi zaidi.

Amesema fedha  inayowekezwa ni  nyingi na italipwa na watanzania sasa ni vizuri itakapowekezwa itoe matokeo yaliyokusudiwa ambayo yatafanana na thamani ya mkopo wenyewe.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla amesema kumekuwa na mashaka kidogo kutoka kwa Wafadhili ambao wanatukopesha  pesa hizo baada ya kuona  mradi wa kufua umeme katika mto Rufiji unatekelezwa.

Amefafanua kuwa Wafadhili hao wanahofu kuwa kutakuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira na hivyo mradi wa Regrow utashindwa kutekelezwa kwa vile  kivutio katika Pori la Akiba la Selous kitabadilika sura yake. Ameelezea kuwa  Serikali imefanya  jitihada za kuhakikisha kuwa  mazingira ndani ya Pori hilo hayataharibiwi na hivyo mradi wa Regrow unaweza ukaendelea kama ilivyopangwa.

Amesema moja ya hatua zilizochukuliwa na serikali ni kuvihamisha viumbe ambavyo vilikuwepo  katika eneo linapotarajiwa bwawa kujengwa, Hivyo viumbe hao wataendelea kuwepo na wanaweza kurudi katika eneo lao la awali. Aidha,Mhe.Kigwangalla amesema hata kama itatokea viumbe hao wakapotea kutokana na ujenzi wa bwawa hilo basi viumbe na mimea iliyokuwepo katika eneo hilo vitarudishiwa kwa sababu tayari imechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye maabara ya vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo hapa nchini kikiwemo  Chuo kikuu Cha Dar es Salaam pamoja na Sokoine.

"Tumewaeleza kuwa mashaka yao hayawezi kuzuia huu mradi na bila shaka wametuelewa hivyo tunasubilia uamuzi wa mwisho wa kuamua wanatukopesha au hawatukopeshi" amesema Mhe.Kigwangalla. Pia amesema katika mradi huo yatachimbwa mabwawa makubwa  matatu ambayo yatatumika kama vyanzo vya maji kwa wanyama waliopo katika bonde la Mto Rufiji

Akizungumzia manufaa ya mkopo huo , Waziri Kigwangalla amesema utatumika kujenga miundombinu mbalimbali  ikiwemo barabara pamoja na viwanja vya ndege ambavyo vitakuwa vichocheo vikubwa katika kukuza na kuendekeza utalii kwa ukanda wa kusini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye ( wa tatu kushoto) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakipewa maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki kuhusiana na bwawa  lenye viboko wengi katika Hifadhi hiyo liitwalo Mwanambogo wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea kwa ajili ya kujionea mradi wa kukuza utalii kusini wa Regrow ulipofikia na namna unavyotekelezwa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Constantine Kanyasu.( Picha na Lusungu Helela)
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki ( wa kwanza kushoto)/akitoa Maelezo kwa  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye, ( wa pili Julia)  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla ( wa kwanza kulia)pamoja na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) kuhusu uwanja wa ndege unaotarajiwa kuboreshwa na utakuwa na urefu wa kilomita 2.2 unatekekelzwa  kupitia Mradi wa kukuza utalii kwa upande wa kusini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla ( wa nne kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi jana mara baada ya Kamati ya Bunge ya Kudumu,Ardhi, Maliasili na Utalii kuondoka katika Hifadhi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe.Nape Nnauye wakizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dkt.Hamis Kigwangalla pamoja na Mjumbe wa Kamati hiyo Dkt.Steven Kiruswa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye ( wa tatu kushoto) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakifurahia jambo mara baada ya kutembelea ziwa la viboko vinavyojulilika Bean a bears kama maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki kuhusiana na bwawa  lenye viboko wengi katika Hifadhi hiyo liitwalo Mwanambogo wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea kwa ajili ya kujionea mradi wa kukuza utalii kusini wa Regrow ulipofikia na namna unavyotekelezwa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Constantine Kanyasu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe.Nape Nnauye ( wa pili kushoto) Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla ( wa tatu kushoto) wakiwa pamoja na viongozi wengine wakizungumza mara baada ya kkuhitimisha ziara katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro.

Rais Dkt.Magufuli Mgeni Rasmi makabidhiano ya mfumo wa mawasiliano ya simu (TTMS

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

RAIS John Pombe Magufuli kesho anatarajia kuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) unaosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), ambao pamoja na mambo mengine mfumo huo utahakiki mapato yote ya watoa huduma za mawasiliano na kugundua mawasiliano ya simu ya ulaghai.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alisema shughuli za kiuchumi zinazohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) zimeongezeka na zinaendelea kuongezeka kwa kasi nchini hivyo kunahitajika kuwepo kwa mifumo mahiri ya usimamizi kama huo. 

Amesema mfumo huo ambao ulianza kufanya kazi rasmi Oktoba mosi 2013, pamoja na mambo mengine umewezesha upatikanaji wa takwimu za mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje ya nchi pamoja na kutambua mapato na takwimu za miamala ya fedha mtandaoni. 

"Mfumo huu utawezesha kusimamia kwa ufanisi ubora wa huduma za mawasiliano na hivyo kuboresha viwango vya huduma hizo, utatambua taarifa za laini ya simu na namba tambulishi za kifaa cha mawasiliano," amesema. 

Aliongeza kuwa kazi nyingine za mfumo huo, utaweza kubaini na kufungia simu zenye namba tambulishi zilizonakiliwa pamoja na kutoa takwimu zinazohusiana na matumizi ya data na jumbe fupi. 

"Mfumo huu unaweza pia kusimamia shughuli nyingi zaidi kutokana na mazingira na mabadiliko ya teknolojia mpya zinapojitokeza aidha mfumo huo wa TTMS ni chombo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na kijamii nchini," amesema. 

Hata hivyo amesema katika makabidhiano hayo zaidi ya viongozi na wananchi mbalimbali ambao ni wadau wa sekta ya mawasiliano wapatao 1500 wamealikwa kuhudhuria shughuli hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na makabidhiano ya mfumo wa mawasiliano

WAKAZI WAZO NA VITONGOJI VYAKE WAPATA MAJI, WAZIRI MBARAWA AWAPA DAWASA KONGOLE

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kuwasambazia maji wananchi wa Kata ya Wazo na vitongoji vyake ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotoa jumapili Jan 13, 2019. DAWASA imewekeza na imejenga tanki kubwa lenye uwezo wa kihifadhi lita milioni sita itakayofanya wakazi wa kupata maji kwa kipindi chote bila mgao. 

Akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza kazi na kuwapatia wananchi maji, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amewaomba wasimamizi wa vizimba (Maduka ya kuuzia maji) kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo na si tsh. 100 kama ilivyokuwa awali. "Leo mnafurahi kufunguliwa maji ila naomba muuze maji tsh. 50 kwa ndoo, sitaki kuona wananchi wanalalamika eti bei kubwa, mimi ndiyo msimamizi naomba mtekeleze mkumbuke na kulipa ankara zenu za maji ili DAWASA waweze kuwahudumia vyema," amesema. 

Mwishoni kwa wiki iliyopita DAWASA kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja mbele ya wananchi akiwemo Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, aliwaahidi wakazi wa kata ya Wazo na vitongoji vyake kuanzia wiki hii maji watapata bila mgawo wowote.
 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akishuhudia utokaji wa maji eneo la Kata ya Wazo mara baada ya kukamilika kwa tanki kubwa litakalowapatia maji kwa kipindi cha mwaka mzima bila kukatika. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji.  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji huku akitoa maelekezo ya kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo tu.  Maji yakitoka. 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akipata maelezo toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. 

MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI AKUBALI MWITO WA SPIKA NDUGAI

$
0
0
*Asema uhusiano kati ya CAG na Bunge ni muhimu, akiri hakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad amekubali mwito wa Spika wa Bunge 

Job Ndugai la kumtaka kufika kwenye Kamati ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Januari 21, 2019 ili ahojiwe na kamati hiyo.

Spika Ndugai alitangaza kumuita Profesa Assad kwenye kamati hiyo baada ya kudai kuwa amelidhalilsha Bunge kutokana na kauli yake ambayo ameitoa nchini Marekani ya kwamba Bunge ni dhaifu.

Akizungumza leo Januari 17, 2019 Profesa Assad amesema Ofisi ya CAG na Bunge ni taasisi ambazo lazima zimefanye kazi zake kwa karibu sana na kwamba anaamini kuwa mpaka sasa ana mahusiano mazuri na yenye tija na si tu kwake na Spika bali ni Bunge zima la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Pia mimi na wakaguzi wangu tumekuwa tukifanya kazi vizuri pamoja na kuaminiana kati yetu na wenyeviti na wajumbe wa Kamati zote za Bunge "amesema Profesa Assad na kuongeza kuwa uhusiano kati CAG na Bunge ni 
wenye umuhimu katika kutekeleza majukumu yake kikatiba na mantiki hiyo ni lazima uenziwe na kudumishwa na yanayotokea hivi sasa hayafurahishi bali yanasikitisha.

Aidha Profesa Assad amesema katika mahojiano yake yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kudhalilisha Bunge hata kidogo na kufafanua maneno kama udhaifu na mapungufu ni lugha ya kawaida kwa wakaguzi katika kutoa maoni ya utendaji wa mifumo ya taasisi mbalimbali.

Hata hivyo amesema kuwa ni wazi kwamba watu wengine wanaweza 
kuchukua tafsiri tofauti ya maneno kama hayo. "Hivyo naitikia mwito wa Janauari 21".
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha)leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,(MMG)
Viewing all 109992 articles
Browse latest View live




Latest Images