Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AVUNJA KAMATI YA UJENZI

$
0
0
Na Shani Amanzi, Chemba.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga amachukizwa na Wananchi na Wafanyakazi wa Serikali wasiokuwa wawijibikaji hasa pale wanapopewa majukumu na Serikali ikiwemo kuwekwa kwenye Kamati za shughuli za kimaendeleo katika jamii.

Mhe. Odunga aliyazungumza hayo alipotembelea kata ya Mrijo akiongozana na mkurugenzi wa Halmashauri, Katibu Tawala pamoja na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo. 

 “Nampongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuweka kipaumbele katika Afya na kutaka kila kata kuwe na Kituo cha Afya na sitakubali mwananchi au mtaalam yoyote akwamishe malengo hayo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa”, alisema.

Aidha Mhe.Odunga aliongeza kwa kusema mkumbuke wapo Wananchi ambao baadhi yao wapo macho na wanataka kushirikishwa katika kila jambo na inasikitisha sana Kamati hii ya Ujenzi inafanya mambo bila kuwashirikisha Wananchi na ninaamuru Kamati hii ivunjwe na kutaka Mkurugenzi ahakikishe anaunda nyingine mara moja kuanzia leo kwani wengi wao wananchi hawaiamini Kamati hii ikiwemo na upande wa manunuzi. 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus.H.Mashimba ameomba ushirikiano kwa Wananchi katika kuhakikisha Ujenzi wa Kituo cha Afya- Mrijo kinakamilika na kuipongeza Serikali katika kuweka kipaumbele Chemba katika Ujenzi wa Vituo vya Afya. 
 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga wa pilia kushoto akizungumza na wananchi (hawapo pichani)  baada ya kuitembelea kata ya Mrijo akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri (wa pili kulia) Mh.Dkt.Semistatus Mashimba  pamoja na Katibu Tawala Zahara Muhidin Michuzi (mwisho kushoto) sambamba na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019. 
 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza na baadhi ya Wananchi  alipotembelea kata ya mrijo akiongozana na mkurugenzi wa Halmashauri, Katibu Tawala pamoja na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019. 
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mrijo wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nano baada ya kuitembelea kata ya mrijo akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri, Mh.Dkt.Semistatus Mashimba  pamoja na Katibu Tawala Zahara Muhidin Michuzi sambamba na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilizopofikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo,Tarehe 12/1/2019. 


MAWASILIANO YA BARABARA YA DODOMA-MOROGORO YAREJEA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa, amewahakikishia wananchi na watumiaji wa barabara ya Morogoro-Dodoma kuwa mawasiliano ya barabara hiyo sehemu ya maingilio ya daraja la Dumila yamerudi kama ilivyokuwa awali.

Kauli hiyo ameitoa leo mkoani Morogoro, alipofika darajani hapo kujionea athari za mvua zilizosababisha kubomoka kwa daraja hilo na wananchi kushindwa kutumia barabara hiyo kwa takriban masaa saba. 

"Kama mlivyoshuhudia tangu asubuhi tumeanza kazi za kurudisha mawasiliano katika barabara hii, matengenezo yakamilika na wananchi tayari wameshaanza kutumia barabara", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, ameupaongeza Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Morogoro, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kampuni ya ujenzi ya Yapi Merkez na wadau wote waliojitokeza katika kuhakikisha wanashirikiana bega kwa bega ili kurudisha mawasiliano katika eneo hilo.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanakuwa imara, Serikali ipo katika mpango wa kuboresha barabara hiyo ambapo kwa sasa wataalam wanafanya usanifu wa barabara hiyo na pindi usanifu huo utakapokamilika basi ujenzi wake utaanza mara moja na wataanza na sehemu korofi.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, amesema kuwa uongozi wa mkoa ulifika eneo la tukio na kuanza kushirikiana na TANROADS mkoa kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea mapema.Amewataka wananchi kujitolea kupanda matete na magugu maji katika eneo hilo ili kuelekeza maji yanayopita katika mto huo kuelekea sehemu husika.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, amesema kuwa kazi zilizokuwa zikifanyika katika maingilio ya daraja hilo ilikuwa ni kuweka mawe makubwa na kokoto sehemu iliyobomoka.Amefafanua kuwa kutokana na sehemu hiyo kuwa na maji mengi na mchanga mwingi, wamefikiria kufanya usanifu wa daraja hilo utakaoleta suluhisho la kudumu.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Magari yakionekana kupita katika daraja la Dumila ambalo liliathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019, na kukata mawasiliano katika mkoa wa Morogoro na Dodoma kwa takriban saa 7.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati), mara baada ya kuwasili katika daraja la Dumila lililoathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019 na kuvunja maingilio ya daraja hilo mkoani Morogoro.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, akimueleza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, hatua zilizochukuliwa na wakala huo katika matengenezo ya maingilio ya daraja la Dumila lililoathirika na mvua zilizonyesha usiku wa tarehe 15/1/2019, mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitazama athari za mvua zilizonyesha na kuharibu sehemu ya maingilio daraja la Dumila, mkoani Morogoro.
Kazi za ujazaji wa mawe na kokoto zilizokuwa zikifanyika katika kurekebisha athari za mvua zilizonyesha na kubomoa maingilio ya daraja la Dumila, mkoani Morogoro. Daraja hilo liko katika hatua za usanifu wa kina wa kuongeza tuta la daraja hilo.

WILAYA YA CHEMBA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO

$
0
0
Na Shani Amanzi, Chemba

Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewaonya watu watakaotaka kufanya udanganyifu katika zoezi la ugawaji vitambulisho kwa Wajasiliamali Wadogo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwani watakuwa wamekwenda kinyume na taratibu. 

Dc Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anazindua zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasirimali Wadogo wilayani Chemba hivi karibuni katika Ukumbi wa Godown. 

“Nataka zoezi hili lisizidi siku saba na kuhakikisha mapato yanaenda vizuri bila kusahau kuhakikisha makundi ya Wajasirimali Wadogo wanapata ikiwemo wa Magenge ya chakula,Mitumba,Mafundi cherehani,Wasusi na wengineo wanaostahili katika Tarafa zote ikiwemo Mondo,Goima,Kwamtoro na Farkwa za Chemba”alisema Dc Odunga. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba alisema kuwa katika zoezi la awali walitambua Wajasiliamali 105 ambapo katika kata ya Chemba walipata Wajasirimali 35,kata ya Kidoka Wajasirimali 40,kata ya Paranga Wajasiliamali 30 na kuwa zoezi hilo limehakikiwa na Kitengo cha Biashara kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi pamoja na Maendeleo ya Jamii. 

Aidha Dkt.Semistatus H.Mashimba amesema” Kamati ya zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasiliamali Wadogo ilizungunga wilaya nzima katika kutoa elimu na kuhakikisha zoezi hili linakuwa endelevu na tulibaini kuna watu walitaka kufanya udanganyifu na tuliweza kutatua jambo hilo na kuhakikisha hali hiyo haitatokea tena” 

Jumla ya Vitambulisho vya Wajasirimali Wadogo 2750 kutoka Ofisi ya Rais –Tamisemi viligaiwa Mkoani ambapo walikabidhi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mhe.Odunga ambapo aliagiza Mkurugenzi Dkt.Mashimba kuratibu zoezi hilo la Ugawaji Vitambulisho kwa wilaya yake. 
 Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza wakati anazindua zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasirimali Wadogo wilayani Chemba hivi karibuni katika Ukumbi wa Godow,Dc Odunga amewaonya watu watakaotaka kufanya udanganyifu katika zoezi hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
 Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akigawa Vitambulisho kwa baadhi ya Wajasiliamali Wadogo,wakati wa uzinduzi wilayani Chemba hivi karibuni katika Ukumbi wa Godow,pichani kulia anaeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mh.Zahara Muhidin Michuzi
Baadhi ya Wajasiliamali Wadogo wadogo wakiwa wamejitokeza kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho hivyo. 

KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU AKABIDHIWA OFISI

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi akishuhudia makabidhiano rasmi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Katibu Mkuu mpya (Sera na Uwekezaji), Bi. Dorothy Mwaluko kutoka kwa  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Profesa, Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu  Tawala  mkoani Kagera. Katibu Mkuu Mwaluko kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejineti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akishukuru kwa ushirikiano aliokuwa anapewa wakati  akihudumu katika ofisi hiyo, kwa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi (katikati) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko (kushoto )
Aliyekuwa Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa  Makatibu Muhtasi wake,  pamoja na Katibu Mkuu mpya  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko (kulia), mara baada ya Profesa Kamuzora kumkabidhi ofisi rasmi. Picha na PMO

TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA (TFNC) INAJIVUNIA MIAKA MITATU YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Imeelezwa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Taifa limefanikiwa kuimarisha huduma za lishe ikiwemo kuongeza bajeti ya lishe kuanzia ngazi ya Mikoa na Halmashauri. 

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Vincent Assey wakati akiongea na maafisa habari/mawasiliano na uhusiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na taasisi zake kwenye kampeni ya "Tumeboresha Afya" .

"Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kuongeza fedha zinazotengwa kugharamia huduma za lishe kutoka shilingi 500 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka 5 iliyokuwa inatengwa mwaka 2015/16 hadi shilingi 1,000 mwaka 2018/19. 

Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Serikali imetumia shilingi bilioni 11. Hiki ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa katika historia ya utoaji wa huduma za lishe hapa nchini katika kipindi cha mwaka mmoja wa fedha" alisema Dkt. Assey.

Pia, amesema kwamba Serikali imeendelea kuimarisha huduma ya utoaji wa vidonge vya vitamini A ya nyongeza na dawa za kutibu minyoo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5. Huduma hii inatolewa mara mbili kwa mwaka. Hadi kufikia mwezi Juni 2018 asilimia 96 ya watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 nchini walipatiwa vidonge vya vitamini A ya nyongeza ili kuimarisha kingamwili dhidi ya magonjwa na kuboresha uwezo wa macho yao kuona vizuri

Aidha Dkt. Assey amesema kupitia viwanda, Serikali imefanikiwa kuboresha lishe za watanzania kwa kuviwezesha viwanda vinavyosindika vyakula kuongeza virutubishi muhimu ikiwemo Vitamini A na D kwenye mafuta ya kula, madini chuma na vitamini ya asidi ya foliki katika unga wa mahindi na unga wa ngano. 

Vitamini A huimarisha kingamwili inayosaidia kudhibiti magonjwa mwilini, vitamini D inasaidia kuimarisha afya ya mifupa. Madini chuma yanayosaidia kuongeza wingi wa damu mwilini na vitamini ya asidi ya foliki inayosaidia pia kuongeza damu mwilini na kuzuia tatizo la watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vikubwa, mgongo wazi na midomo iliyopasuka (mdomo sungura).

Vilevile Serikali imewawezesha wazalisha chumvi kuongeza madini joto kwenye chumvi ili kutokomeza tatizo la upungufu wa madini joto mwilini. Kwa kudhibiti tatizo la upungufu wa madini joto mwilini Taifa linadhibiti kasi ya mimba kuharibika, watoto kufariki wakiwa tumboni, pamoja na kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na mtindio wa ubongo/taahira na ulemavu wa viungo. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe, Sikitu Saimon ameeleza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imeboresha vitendea kazi vya kutolea elimu ya lishe kwa umma kwa kutumia mfuko wa siku 1000, unaotumika katika ngazi ya jamii kuhamasisha matunzo bora ya mama mjamzito, mama anayenyonyesha, na mtoto mchanga kuanzia wakati wa kuzaliwa hadi anapotimiza umri wa miaka miwili.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Vincent Assey akielezea mafanikio ya lishe nchini katika miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe na Magufuli, wakati wa kampeni ya "Tumeboresha Sekta ya Afya" inayoendeshwa na maafisa habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na taasisi zake.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 17,2019

MKAZI WA ARUSHA AJISHINDIA GARI PROMOSHENI YA TBL KUMENOGA TUKUTANE BAA

$
0
0


Meneja wa huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumtafuta mshindi wa tatu wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. ambapo mkazi wa Arusha George Issaya (29) aliibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kutoka Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Adam Kefa, na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini ,Majid Bakari.
Meneja wa huduma za Masoko wa TBL,David Tarimo (wapili kushoto) akipofya kitufe cha Komputa wakati wa kumtafuta mshindi wa tatu na wa mwisho wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. ambapo mkazi wa Arusha George Issaya (29) aliibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kutoka Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Adam Kefa, Meneja wa huduma za Jamii wa Aim group, Aidan Mattaka na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini ,Majid Bakari.
Meneja wa huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo (kushoto) akiongea na George Issaya (29) mkazi wa Arusha mara baada ya kuibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Wakati Droo ya tatu ya promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa huduma za Jamii wa Aim group, Aidan Mattaka na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini, Majid Bakari.


Droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha, George Isaya (29) amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID. Isaya akiongea baada ya kupigiwa simu na Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema anayo furaha kufanikiwa kuwa miongoni mwa washindi kupitia promosheni hiyo kwa kujishindia gari mpya.

“Sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru TBL kwa kunifungulia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari “alisema kwa furaha. 





Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za magari 3 mapya ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka kumpata mshindi wa tatu wa zawadi kubwa ya mwezi ambayo ni gari mpya. Tunawashukuru wateja wetu kutoka nchini pote walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi uliopita”. alisema Tarimo.

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilikuwa inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi mbalimbali na hivyo TBL kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake.

Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, aliwashukuru wateja wote wa TBL kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.

TRC YARUHUSU MADEREVA KUTUMIA BARABARA ZA MRADI WA SGR BAADA YA MVUA KUBOMOA DARAJA


MANOTA AZIDI KUING'ARISHA KIMARA KWA KUTEKELEZA AHAADI ZAKE

VOA Swahili: Rais Uhuru Kenyatta atoa pole kwa Taifa

AZAM TV - MAGOLI YOTE: YANGA SC 3-1 MWADUI FC (TPL – 15/01/2019)

VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI MKOA WA KAGERA WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KULETA MAENDELEO

$
0
0
Na Sylvester Raphael,Kagera

VIONGOZI  wa madhehebu ya dini Mkoani Kagera wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais DkJohn Magufuli kwa kuchukua hatua na maamuzi yanayolenga kumuinua mwananchi mnyonge ili afaidike na raslimali za nchi yake.

Wametoa pongezi hizo jana Januari 16,2019 baada ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ofisini kwake kwa mazungumzo.

Hivyo wametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini na yenye manufaa kwa umma mfano ununuzi wa ndege, ujenzi wa Reli ya Kisasa na ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge pamoja na miradi mingine mingi ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza kwa niaba yao Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini amesema pia wanaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kudumisha amani, utulivu na mshikamano kwa Watanzania na kuendelea kutekeleza shughuli ambazo zinalenga maslahi mapana ya wananchi.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wa madhehebu ya dini walimweleza Mkuu wa Mkoa Gaguti kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali ya mkoa katika kudumisha amani na utulivu katika mkoa huo.

 Pia wameahidi wataendelea kuhamasisha wananchi kuchapa kazi kwa bidii kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa mkoa kama jina la mwaka 2019 kwa lugha ya Kihaya linavyohimiza kila mwananchi kufanya kazi likimaniisha kuwa kila mmoja atakula kwa jasho lake “Biluga Omumpiita”.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Gaguti katika mazungumzo hayo aliwahakikishia viongozi hao wa dini kuwa yeye binafsi pamoja na Serikali ya Mkoa wataendelea kushirikiana nao kwani wao ndiyo nguzo kuu ya amani katika mkoa.Pia viongozi wa dini ndio nguzo kuu ya maadili hasa kwa kuiunganisha Serikali na wananchi wake.

“Serikali tutaendelea kushirikiana na nyinyi kama ilivyo desturi ya Mkoa wetu wa Kagera na tunawategemea sana katika kuhakikisha mkoa wetu unaendelea kudumisha amani na utulivu kwani kila mara mnapokutana na waamini wenu mkahubiri kuhusu amani na utulivu sisi kwetu kazi inakuwa ndogo. 

"Pia mnapowahimiza wananchi wafanye kazi kwetu sisi Serikali inakuwa rahisi mno kuweka msukumo kwa wananchi," amesema Gaguti

Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Viongozi wa Madhehebu ya Dini waliokuwepo ni ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoriki la Bukoba Kilaini, Sheikh Aruna Kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera na Askofu Dk. Abedinergo Keshomshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania Dayosisi ya Kasikazini Magharibi.
Askofu Msaidizi Jimbo Katoriki la Bukoba akizungumza jambo mbele yaMkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti,huku Askofu DKt. Keshomshahara (KKKT) na Sheikh Aruna Kichwabuta wakimsikiliza.
Askofu Msaidizi Method Kilaini na Askofu Dkt. Keshomshahara Wakisikiliza na Kufurahia Jambo Kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti (hayupo Pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti (Kushoto) akimsikiliza Askofu Method Kilaini kwa Umakini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti (Kushoto) Akimsikiliza Sheikh Aruna Kichwabuta (Kulia) Askofu Method Kilaini na Askofu Dkt. Abednergo Keshomshahara wakisikiliza.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti akitoa neno kwa Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoani Kagera
Picha ya Pamoja Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa
Sheikh Aruna Kichwabuta (Kulia) Kwa niaba ya Wenzake akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti Mwongozo wa Namna Viongozi Madhehebu ya Dini Wanavyoshirikiana Mkoani Kagera
 

HASSAN GOBBOS: MCHEZAJI ALIYEMPISHA LEODEGAR TENGA KATIKA YANGA, MZIZIMA UNITED NA TAIFA STARS!

$
0
0
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
JUMAMOSI Agosti 10, 1974 ni siku ambayo ina kumbukumbu ya pekee katika soka la Tanzania, kwani ndiyo siku soka la uhakika na la ushindani baina ya Simba na Yanga lilionekana kwa mara ya mwisho.
Ni mechi hiyo ambayo binafsi huwa ninaiita ‘Thriller’ ambayo ilichezwa pale Nyamagana, Mwanza.
Lakini MaendeleoVijijini inatambua kwamba, hiyo ndiyo siku ambayo beki mashuhuri namba nne wa Yanga, Mzizima United (timu ya Mkoa wa Dar es Salaam) na Taifa Stars, Hassan Gobbos maarufu kama ‘King Hassan wa Morocco’, aliamua kutundika daruga baada ya filimbi ya mwisho na kumkabidhi majukumu hayo beki msomi, Engineer Leodegar Chilla Tenga kwenye timu zote hizo.

Nilipata kufanya naye mazungumzo mwaka 2002 wakati akiwa mtumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) – sijui kama bado yuko pale – na aliniambia sababu za kuamua kutundika daruga zilikuwa kujikita zaidi kwenye kazi kwani umri nao ulikuwa unayoyoma!
Lakini anakumbuka vyema mchezo ule wa fainali baina ya Yanga na Simba pale Nyamagana jinsi ulivyokuwa na ushindani mkubwa.
“Tangu wakati ule sijaona mchezo wa Simba na Yanga wenye ushindani, zaidi utasikia majigambo tu kwenye vyombo vya habari na ukienda uwanjani unakuta hali iko tofauti kabisa,” alisema Gobbos ambaye siku hiyo kama kawaida yake alicheza namba 4 na akampisha Boi Idd.
Kikosi cha siku hiyo cha Yanga kilikuwa na Elias Michael ambaye aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Muhidin Fadhil, Ally Yussuf, Selemani Saidi Sanga, Hassan Gobbos/Boi Iddi 'Wickens', Omari Kapera, Abdulrahman Juma (nahodha), Bona Max Mwangi, Sunday Manara, Kitwana Manara, Gibson Sembuli na Maulid Dilunga, kikiwa kinanolewa na Tambwe Leya kutoka Zaire.
Simba wao waliwakilishwa na Athumani Mambosasa, Shaaban Baraza, Mohammed Kajole, Athumani Juma, Omari Chogo, Omari Gumbo, Willy Mwaijibe aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Kessy Manangu, Haidari Abeid 'Muchacho' (nahodha), Saad Ally aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Adamu Sabu, Abdallah Kibadeni, na Abbas Dilunga ‘Sungura’. Walikuwa wananolewa na Paul West Gwivaha.
Gobbos anakumbuka kwamba, hadi kufikia fainali Agosti 10, 1974, kulikuwa na ushindani mkubwa kwenye ligi hiyo iliyofanyika Mwanza kuanzia Julai 18 mpaka Agosti 10, 1974 katika Uwanja wa Nyamagana.
“Kwa matayarisho ya michuano ya mwaka huo Yanga tulikwenda kuzuru Brazil na Simba walikwenda Poland, na ndizo timu ambazo zilikuwa na vikosi imara zaidi msimu huo,” anakumbuka.
Msimu huo timu zilikuwa Yanga, Kazi Mara, Comworks Singida, Ntomoko Dodoma, Miembeni Zanzibar, Ujenzi Rukwa, Simba, Kaye ya Iringa, Ufundi Kigoma, Nyota Mtwara, Coast Stars ya Bagamoyo, Mwadui ya Shinyanga, Magunia Kilimanjaro, Madaraka Rubuma, Polisi Bukoba, na Jeshi Zanzibar.
Nyingine zilikuwa Jeshi Tabora, Rungwe Sekondari, Nyota Tanga, Jeshi Lindi, Jumuiya Arusha, na Mwatex.
Katika nusu fainali, Yanga iliifunga Miembeni ya Zanzibar mabao 2-1 huku mabao yote ya Yanga yakifungwa na mshambuliaji mwenye mashuti makali ambaye hajapata kutokea tena, Gibson Sembuli, wakati Salhina aliifungia Miembeni bao la kufutia machozi.
Simba yenyewe iliitoa Jeshi Tabora kwa mabao 3-0 ambapo Hilary wa Jeshi alijifunga katika jitihada za kuokoa na mabao mengine yalifungwa na Saad Ally na Adam Sabu.
“Ndiposa tukakutana na Simba kwenye fainali na kwa hakika kila timu ilikuwa imara mno,” alisema Gobbos wakati huo akikumbuka mechi hiyo ya aina yake.
Inakumbukwa kwamba, siku hiyo Uwanja wa Nyamagana ulifurika watu isivyo kawaida. Mashabiki walitoka sehemu mbalimbali za nchi - Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Dar es Salaam, Tabora, Shinyanga, Kigoma, Morogoro, Mara na Kagera. Hao ni licha ya wale waliotoka kwenye vitongoji vya Mwanza. Ilipofika saa 10.30 jioni hapakuwa na nafasi ya kukaa mtu hapo uwanjani, ingawa wengine walikuwa wanaendelea kumiminika.
Mchezo ulianza kwa nguvu ingawa Yanga walianza pole pole kidogo wakijaribu kuusoma mchezo wa Simba. Baada ya dakika tano tu matokeo ya nguvu hizo yalionekana. Saad Ally wa Simba aliumia baada ya kugongana na Gibson Sembuli wa Yanga na akatolewa nje. Adamu Sabu aliyeingia badala yake, aliwafurahisha wapenzi wa Simba, kwani aliifungia goli timu yake katika dakika ya 16.
Katika pambano hilo, golikipa wa Yanga, Elias Michael aligongana na Willy Mwaijibe wa Simba katika dakika ya 70 na wote wawili wakakimbizwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Nafasi zao zilichukuliwa na Muhidin Fadhil kwa upande wa Yanga na Kessy Manangu kwa upande wa Simba.
Yanga walijaribu sana kukomboa goli hilo lakini walipata taabu kwani ukuta wa Simba ulikuwa imara sana. Kadiri mchezo ulivyoendelea watu walidhani Yanga isingepata hata goli moja na kwamba, siku hiyo ingefungwa tena, kwani hadi mapumziko matokeo yalikuwa ni yale yale ya goli moja kwa Simba na Yanga wakiwa na gurudumu.
Katika dakika ya 87 ya mchezo, yaani dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika, mambo yalibadilika. Ilikuwa ni golikiki, ambapo mlinzi wa Yanga, Ally Yussuf, alipiga mpira kuelekea golini kwa Simba. Mpira huo ulipita juu ya vichwa vya wachezaji kadhaa wakiwemo Abdallah Kibadeni wa Simba na Gibson Sembuli na Sunday Manara.
Mpira huo uliambaa ambaa kuelekea goli la Simba ambako Kitwana Manara, aliyekuwa amebanwa mno na beki wa Simba ambaye hakutaka mchezo, Omari Chogo 'Chemba', licha ya kuwa ameupa mgongo mpira huo aliruka na kupiga kichwa kushoto kwake.
Moja kwa moja mpira huo uliingia kwenye 'anga' za nambari tisa wa Yanga, Gibson Sembuli, aliyeujaza wavuni kwa shuti kali la ugoko, lililoingilia kwenye kona ya kushoto na kumuacha kipa Athumani Mambosasa, aliyekuwa ametoka kumkabili mchezaji huyo, akiwa hana la kufanya zaidi ya kuutumbulia macho mpira huo ukitinga wavuni kuandika goli la kusawazisha kwa Yanga. Hivyo, hadi mwisho wa dakika 90 za kawaida za mchezo matokeo yalikuwa 1-1.
Goli hilo likabadilisha kabisa sura ya mchezo. Watazamaji ambao walianza kuondoka uwanjani wakidhani Yanga wameshindwa walirudi tena uwanjani kuangalia mchezo. Dakika 90 zilipokwisha ubao wa matokeo ukasomeka Yanga 1 Simba 1 na ndipo dakika 30 zilipoongezwa ili kupata mshindi.
Katika dakika ya saba ya muda wa nyongeza, mlinzi Ally Yussuf wa Yanga aliipangua ngome ya Simba na kutoa pasi ya juu kwa mchezaji wa kiungo wa Yanga, Sunday Ramadhan Manara, aliyefunga goli la pili kwa kichwa. Goli hilo likawa la ushindi kwa Yanga baada ya Simba kushindwa kusawazisha kwa dakika 23 zilizokuwa zimesalia.
“Ilikuwa mechi ngumu mno, haijapata kutokea,” alisema Gobbos, ambaye mwaka huo pia alikuwemo kwenye kikosi cha Tanzania Bara kilichotwaa Kombe la Chalenji.

Harakati zake
MaendeleoVijijini inatambua kwamba, harakati za Hassan Gobbos katika kutandaza ndinga zilianza alipokuwa darasa la tano, Mundemu Middle School, maili 12 kutoka Dodoma mjini. Akiwa shuleni hapo aliiwakilisha wilaya ya Dodoma katika mashindano ya kikombe cha Magwaya yaliyotumika wakati huo kupata wachezaji waliounda timu ya mkoa wa Dodoma (Central Province) kwa ajili ya michuano ya Sunlight Cup (sasa Taifa Cup). Wilaya nyingine zilizoshiriki zilikuwa Kondoa na Mpwapwa.
Mwaka 1963, Gobbos alichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, Dodoma Sekondari, na mwaka huo huo, kutokana na kile alichokielezea mwenyewe kuwa ni kujiendeleza kimpira, Gobbos alijiunga na timu ya Young Africans ya mjini Dodoma. Ikumbukwe kwamba zamani Simba (wakati huo Sunderland) na Yanga zilikuwa na matawi yake katika mikoa mbalimbali ambayo nayo yalichukua majina hayo hayo.
Uzoefu alioupata wakati wa Magwaya Cup ulimuwezesha kupata namba ya kudumu (nambari tano) kwenye timu ya mkoa wa Dodoma ambao aliuwakilisha katika mashindano ya Sunlight Cup lililoshindaniwa kwa mara ya mwisho mwaka 1963, kabla ya kubadilishwa na kuwa Taifa Cup, ambapo pia aliuwakilisha mkoa huo hadi mwaka 1966.
Akicheza kwa utulivu na kuutumia vizuri urefu wake Hassan Gobbos aliweza kufagia hatari nyingi kabla hazijasababisha madhara langoni wakati wa enzi zake. Alikuwa kiboko cha washambuliaji.
Mwaka 1964 alipokuwa kidato cha pili, Hassan Gobbos aliiwakilisha timu ya Taifa ya Vijana iliyokwenda Malawi kuadhimisha Uhuru wa nchi hiyo, Julai 6. Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa kimataifa kwa mwanasoka huyo. Pia aliuwakilisha mkoa wa Dodoma katika riadha, hasa mbio za mita 400 kupokezana vijiti (relay) na kuruka juu.
Januari 1967, Hassan Gobbos alijiunga na Young Africans ya Dar es Salaam baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari mwaka 1966 mjini Dodoma, wakati huo huo akiwa mwajiriwa bandarini. Haukupita muda viongozi wa soka mkoani Dar es Salaam wakawa wamemmulika mchezaji huyo, ambapo alikuwemo katika orodha ya wachezaji wa mkoa wa Dar es Salaam waliochaguliwa kuuwakilisha mkoa katika michuano ya Taifa Cup mwaka 1967.
Baada ya mwaka 1964, Hassan Gobbos alipata fursa tena ya kuvaa jezi ya taifa mwaka 1968 alipochaguliwa kuchezea timu ya wakubwa, Taifa Stars. Tangu mwaka huo hakuivua jezi hiyo nambari nne kwenye timu ya taifa hadi mwaka 1974 alipoamua kutoweka kabisa uwanjani.
Hassan Gobbos bado anayakumbuka sana mashindano ya kuwania Kombe la Chalenji ya mwaka 1970 yaliyofanyika mjini Nairobi, Kenya, hususan mchezo wa mwisho dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars. Baada ya kuzishinda Uganda na Zanzibar, Kenya na Tanzania Bara zilitoka sare ya bao 1-1. Hata hivyo, Kenya walichukua kombe kwa wingi wa mabao.
"Wenzetu Kenya walikuwa ndiyo kwanza wamerejea kutoka Ujerumani Magharibi kujiandaa kwa mashindano hayo. Walicheza mchezo tofauti na sisi na walikuwa na stamina ya hali ya juu sana," alieleza Gobbos.
Maoni ya mchezaji huyo wa zamani kuhusu hali ya kandanda nchini ni kwamba, imeshuka. Sababu kadhaa alizozitaja kuhusiana na kuporomoka kwa kiwango cha soka nchini ni pamoja na kukosekana mara kwa mara kwa vifaa vya michezo, kukosa michezo ya kutosha ya kimataifa ya majaribio wakati timu zetu zinapojiandaa na michuano ya kimataifa na pia kukosekana kwa miundombinu pamoja na programu za maendeleo ya mchezo huo.
"Kwa mfano enzi zetu, Yanga ilikwenda Brazil na Simba ilikwenda Poland kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ya taifa mwaka 1974, achilia mbali michezo ya kimataifa," alisema.
Pia alitoa wito kwa klabu kubwa hapa nchini kuacha mtindo wa kuwarubuni wachezaji kutoka timu nyingine, hasa za mikoani, ambapo inaonyesha dhahiri kwamba wengi wa wachezaji hao wamekuwa wakiishia kukaa benchi na hivyo vipaji vyao kufa haraka, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linarudisha nyuma maendeleo ya soka.
"Mchezaji yeyote yule wa kurubuniwa kwa fedha huwa hana ari anayopaswa kuwa nayo mchezaji uwanjani na anaweza pia akarubuniwa na klabu nyingine pinzani kuihujumu klabu anayoichezea. Badala ya kunyang'anyana wachezaji, ni vyema klabu zote zirejeshe mpango wa zamani wa kuwaandaa vijana chipukizi kuwa wachezaji wa baadaye," aliongeza.
Wachezaji waliomfurahisha enzi zake walikuwa Kitwana Ramadhan Manara 'Popat' au 'Mtafutaji magoli', Leonard Chitete na Omari Kapera, ambaye kwa utani alimwita 'Jeuri'.
Kwa wachezaji wa nje alivutiwa sana na Johan Cruyff mshambuliaji nambari 10 wa Uholanzi na beki nambari mbili Ben Kusi wa Asante Kotoko na timu ya Taifa ya Ghana, Black Stars.
“Huyu Kusi tulicheza naye katika Klabu Bingwa Afrika mwaka 1969 na 1970,” alisema.
Makala haya yameandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com, simu 0656-331974. Kama utayatumia kwa namna yoyote ile ni lazima utoe credit kwa mwandishi Daniel Mbega au MaendeleoVijijini Blog.

TANZIA: NYOTA WA ZAMANI WA YANGA NA TAIFA STARS HASSAN GOBBOS AFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mchezaji nyota wa Zamani wa klabu ya Yanga, Mzizima United na Taifa Stars, Hassan Goebles (Gobbos) amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa katika kundi la Whatsapp la wafanyakazi wastaafu wa Mamlaka ya Bandari, mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza. Tutajulishana zaidi mara habari kamili za ratiba zitapopatikana

KAULI YA DC MUHEZA YAMNUSURU MKUU WA IDARA YA ARDHI KUTUMBULIWA

$
0
0
Na Munir Shemweta, MUHEZA
Kauli ya Mkuu wa wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga Hajjat Mhandisi Mwanaasha Tumbo kuwa idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Muheza haina mtendaji wa sekta ardhi anayeweza kuvaa viatu vya ukuu wa idara iwapo anayeshikilia sasa nafasi hiyo Salehe Kang'e ataondolewa imemnusuru mkuu huyo wa sekta ya ardhi kutumbuliwa katika nafasi yàke.
Kauli hiyo inafuatia Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kueleza kuwa Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri hiyo hafai kuwa mkuu wa idara kutokana na kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi ya ardhi.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Bakari Mhando alimuomba Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutomuondoa katika nafasi hiyo mkuu huyo wa Idara na kubainisha kuwa mapungufu aliyoyaonesha atahakikisha yanarekebishwa ndani ya mwezi mmoja.
Akiwa katika ziara ya kustukiza katika halmashauri ya wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga tarehe 15 Januari 2019 Dk Mabula alionesha kuchukizwa na mkuu huyo wa idara kushindwa kusimamia ukusanyaji kodi ya ardhi ikiwemo kutoa hati za madai kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi katika wilaya ya Muheza.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Ardhi halmashauri ya wilaya ya Muheza Kang'e ambaye amebakiza mwaka mmoja kustaafu kazi, halmashauri ya wilaya yake imeingiza viwanja 3000 katika mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya kielektronik na mashamba 1009 lakini imetoa hati moja ya madai kwa wadaiwa wa kodi ya ardhi.
Dk Mabula alisema alichotegemea baada ya kuingizwa viwanja na mashamba kwenye mfumo huo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektronik mkuu wa idara ya ardhi angehakikisha wadaiwa wote sugu wanafuatiliwa ili walipe kodi lakini kinyume chake kazi hiyo haijafanyika na ni mdaiwa mmoja tu aliyepelekewa hati ya madai.
Alisema msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inakusanya mapato yakiwemo ya kodi ya ardhi ili kuweza kusaidia shughuli za maendeleo ambazo haziwezi kupatikana iwapo serikali haitakuwa na makusanyo mazuri ya kodi.
" Haya yote yanayofanyika ununuzi wa ndege ujenzi wa SGR bila ya kukusanya kodi hayawezi kufanyika na siku zote Rais wa Janhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amekuwa akisisitiza ukusanyaji kodi,  people are not serious" alisema Dk Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa mwezi mmoja kwa Mkuu huyo wa Idara ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Muheza  kuhakikisha wadaiwa wote wa kodi ya ardhi wanapelekewa hati za madai na watakaokaidi wafikishwe katika mabaraza ya ardhi na ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Kaskazini ifuatilie utekelezaji wa agizo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajjat Mhandisi  Mwanaasha Tumbo alisema,  baada ya maelekezo ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alihakikisha utekelezaji  unafanyika na matunda yameanza kuonekana katika baadhi ya maeneo ya  sekta ardhi ikiwemo uingizaji wamiliki wa viwanja na mashamba katika mfumo na amemuahidi Dk Mabula kuwa suala la hati za madai nalo atalisimamia kikamilifu ilii liweze kutekelezwa.
Alisema, changamoto kubwa inayoikabili halmashauri ya wilaya ya Muheza ni kukosekana watendaji wa sekta ya ardhi wenye uwezo mkubwa wa kusimamia masuala ya ardhi na kubainisha kuwa mbali na mkuu wa idara aliyepo sasa lakini halmashauri hiyo haina watendaji wa kutosha.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halamashauri ya Wilaya ya Muheza Salehe Kang'e wakati wa ziara ya kushtukiza kufuatilia maagizo aliyoyatoa katika halmashauri hiyo jana. kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajjat Muhandisi Mwanaasha Tumbo.
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajjat Muhandisi Mwanaasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimpa maelekezo Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halamashauri ya wilaya ya Muheza Salehe Kang'e alipofanya ziara ya kushtukiza katika halmashauri hiyo jana.

DKT. NDUMBARO ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA MAREHEMU ALHAJI SHEHU SHAGARI UBALOZI WA NIGERIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Nigeria hapa nchini kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Alhaji Shehu Shagari kilichotokea tarehe 28 Desemba 2019. Dkt. Ndumbaro alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Nigeria hapa nchini Mhe. Dkt.Sahabi Isa Gada. Tukio hilo limefanyika jijini Dar Es Salaam katika Ubalozi wa Nigeria hapa nchini.  
Balozi Gada akimwelezea jambo Dkt. Ndumbaro wakati wa mazungumzo.
Sehemy ya Maafisa wa Ubalozi wa Nigeria nchini wakisikiliza
Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Gada na maafisa wa Ubalozi huo.
Dkt. Ndumbaro akiagana na Balozi Dkt. Gada. 

QNET YAIPONGEZA CAF,KLABU ZA MPIRA WA MIGUU AFRIKA KATIKA MASHINDANO YA MPIRA YA CAF 2018

$
0
0
Kampuni inayoongoza ya mauzo ya moja kwa moja QNET, na mbia katika ligi ya mabingwa ya CAF, Kombe la Shirikisho la CAF na kombe la Super Cup imewapongeza Shirikisho la Soka Afrika, CAF na vilabu vyote vinavyoshiriki katika mashindano yote ya klabu ya CAF mwaka 2019. 

QNEt imekaribisha ushirikiano wake na CAF, katika mwaka 2018 na inaelezea fahari yake katika mpira wa miguu wa Afrika. 

Ushirikiano kati ya kampuni ya QNET na CAF ni sehemu ya juhudi za QNET za kukuza michezo Afrika na dunia kote.Kwa kweli, kama ilivyo katika michezo, QNET inaongozwa na ari ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu pamoja na shauku wakati inapofanya biashara zake kila siku. 

Ushirikiano huu ni fursa nyingine kwa QNET kuwa karibu na wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs), walaji na wateja ambako QNET inaendesha shughuli zake tangu zaidi ya muongo mmoja iliopita. 

Meneja Mkuu wa QNET wa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, Biram Fall amesema kwamba, “Mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka mzuri kwa mpira wa miguu barani Afrika. Katika QNET tunaona fahari sana kujihusisha na CAF na ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu barani. Falsafa ya biashara yetu inashikilia mwenendo wa mpira wa miguu, ambao kimsingi ni ufanyaji wa kazi katika timu, ushirikiano, shauku na kufanyakazi kwa bidii. 

Tunawawezesha wajasiriamali katika bara zima la Afrika na tumejikita katika kusaidia wengi zaidi waweze kufanikiwa. Vilevile ni heshima kwetu kudhamini mashindano haya maarufu na yanayoheshimiwa sana, na tusingeweza kupata mshirika bora zaidi kuliko Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuweza kufanikisha lengo hili. Mwaka 2019 unaonekana kutia matumaini zaidi na QNET itakuwa katika upande wa CAF kwaajili ya kuhakikisha utendaji bora zaidi”. 

Katika mwaka 2019, QNET itakuwepo zaidi viwanjani ikiwa na uhamasishaji, matukio zaidi kwaajili ya kuhamasisha mashabiki kuongeza nguvu kazi ya mauzo ya QNET na wawakilishi wa kujitegemea (IRs). 

QNET inaendelea kuongeza uwepo wake katika bara zima la Afrika, ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kusaidia watu kubadili historia zao vyema zaidi. Ukiachilia mbali ushirikiano wa kimichezo, QNET pia ni kampuni ambayo inajihusisha na majukumu ya kijamii, kutoa kwaajili ya maendeleo endelevu ya jamii katika kanda zote ambako inaendesha shughuli zake. Katika mwezi Novemba, kampuni ya QNET ilitunikiwa tuzo ya mwaka ya e-commerce CSD Company na Kituo cha Uwajibikaji kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa).
Pichani kulia shoto ni Meneja Mkuu wa QNET wa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, Biram Fall akiwa na mchezaji bora  (Afrika) wa zamani 20o1 kutoka nchini Senegal El Hadj Diouf

Watu watatu wajishindia jumla ya 1,500,000/= Promosheni ya Tusua Ada na Omo.

$
0
0
Meneja wa Sabuni ya Omo, Upendo Mkusa(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya kwanza, Muzdalifa Hamadi Haji pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” inayoendelea katika Supermakert ya Choppies Mlimani City.Droo ya kwanza ilichezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarkert ya kubwa tatu tofauti ambayo ni Choppies,Game Mlimani City na Shoppers Mikocheni, washindi watatu walijishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/= kila mmoja.
Meneja wa Sabuni ya Omo, Upendo Mkusa(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya kwanza, Gift Obed Ondara pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” inayoendelea katika Supermakert ya Shoppers Mikocheni.Droo ya kwanza ilichezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermakertn ya kubwa tatu tofauti ambayo ni Choppies,Game Mlimani City na Shoppers Mikocheni na washindi watatu walijishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/= kila mmoja.
Meneja wa Sabuni ya Omo, Upendo Mkusa(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya kwanza, Isabela Sango Luhanga pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” inayoendelea katika Supermarket ya Game Mlimani City.Droo ya kwanza ilichezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarket ya Choppies,Game Mlimani City na Shoppers Mikocheni na washindi watatu walijishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/= kila mmoja.
WASHINDI watatu kutoka katika maeneo tofauti ya jijini Dar es Salaam wamejishindia jumla ya pesa taslimu Shilingi 1,500,000/= ikiwa ni shilingi 500,000/= kila mmoja katika promosheni ya Tusua Ada na Omo inayoendelea katika Supermakert kubwa ya Game, Choppies Mlimani City na Shoppers Mikocheni,Masaki na Mbezi. Washindi hao walipatikana mara baada ya kununua Omo na kuingia rasmi kwenye droo kubwa inayochezeshwa katika Supermakert hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Omo, Upendo Mkusa kwanza aliwapongeza washindi wote watatu wa droo ya kwanza na kuwaomba kama wana watoto wanasoma pesa hizo wakazilekeze katika kuwasaidia watoto wao katika sekta ya kuwaendeleza kielimu.

Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Sabuni ya Omo wanatambua kama jamii ya Watanzania imetoka katika kipindi cha Siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya hivyo wakaona ni jambo jema kuungana na wanafamilia katika kipindi hiki cha watoto kwenda shule kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupitia promosheni hii.

Alisema Upendo, katika Promosheni hii ya Tusua Ada na Omo jumla ya Shilingi milioni sita (6,000 000/=) zitatolewa kwa washindi 12 ikiwa kila mmoja atajishindia pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=).

Alisema Upendu ushiriki uko wazi kwa kila mtu lakini lazima uwe na umri zaidi ya miaka 18, ni lazima ununue Omo 1kg moja ziwe pakti mbili au 500gm pakti ziwe nne au 3.5kg pakti moja,ambapo mshiriki utapewa kuponi ya itakayoingizwa kwenye droo itakayochezesha kila jumamosi ya juma hilo. Mwisho Upendo aliwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya pesa hiyo kwani ushiriki na ushindi wake uko wazi.

Nikufanya manunuzi ya Omo katika Supermakert ya Game,Choppies au Shoppers Mikocheni, Msaki au Mbezi tayari unaweza kujishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/=.

TANZIA:BABA MZAZI WA MSANII ALIKIBA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Baba mzazi wa wasanii wa bongofleva nchini Ali kiba pamoja na Abdul kiba Mzee salehe Kiba amefariki leo alfajiri  katika hospital ya Taifa Muhimbili alipokua akipatiwa matibabu.

Taarifa za awali zianeleza kuwa msiba huo utakuwa karikaoo nyumbani kwa marehemu Mzee salehe kiba.

Taratibu za Mazishi bado zinaendelea kupangwa na wanafamilia ili kuupumzisha mwili wa Mzee kiba mahali pema.

Uongozi wa Michuzi Media Group unatoa pole kwa familia ya Mzee kiba na kwa wale wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu.

TUTAWALEZA TAARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA MSIBA HUU.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN

RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA

$
0
0
 Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

RAIA wa Pakistani, Muhammad Hasnaih Hyderi leo Januari 17,2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutaka kumpa rushwa Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Imedaiwa na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru), Pascal Magabe akisaidiana na wakili, Leornad Swai kuwa, Januari 15, 2019 huko katika Mgahawa wa Best Bite uliopo ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitenda kosa.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza imedaiwa, siku ya tukio mshtakiwa alitoa rushwa ya Sh. milioni mbili kwa Talib Kombo ambaye ni Ofisa wa TRA)  ili kumsaidia asilipe kodi kubwa.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande Kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kuwa na wadhamini wawili kutoka ofisi yoyote inayotambulika na Serikali watakaosaini bondi ya Sh.milioni tano kila mmoja.

Pia Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria na haruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es  Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.Kwa mujibu upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umeisha kamilika na kesi hiyo itatajwa Januari 31 mwaka huu
MtuhumiwaRAIA wa Pakistani, Muhammad Hasnaih Hyderi leo Januari 17.2019 akifikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutaka kumpa rushwa afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images