Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES

$
0
0
Na Munir Shemweta, KOROGWE 

Serikali imeyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa hekari 12,915.126 ya kampuni ya Mohamed Enterprises yaliyopo korogwe mkoa wa Tanga. 

Uamuzi wa kufuta mashamba hayo unafuatia mapendekezo yaliyotolewa na halmashuri ya wilaya ya Korogwe kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu na baadaye maombi hayo kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wizara kwa nia ya kufutwa. 

Mashamba yaliyofutwa ni yale yaliopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge wilayani Korogwe mkoani Tanga. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba hayo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula alisema mashamba yaliyobatilishwa ni kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohamed Enterprises Mazinde wilayani Korogwe na kubainisha kuwa uamuzi huo unalenga kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za serikali kuzingatia masharti ya uwekezaji. 

Alisema, mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba ya Mohamed Enterprises, wizara ya ardhi ilifanya ufuatiliaji juu ya mambo ya halmashauri husika la kutoendelezwa mashamba na baada ya kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo kwa rais na kuridhiwa. 

Alisema, uamuzi huo wa Rais kuridhia ubatilishaji mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na Mohamed Enterprises unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji. 

Hata hivyo, Dk Mabula alisema mashamba ambayo hayajabatilishwa yamewekewa utaratibu kwa nia ya kuyaboresha kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho kwa nia ya kufanya vizuri. 

Ameitaka halmashauri ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la mashamba yaliyofutwa na kipaumbele kwa watakaopewa maeneo katika mashamba hayo ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mashamba hayo na sehemu itakayobaki atafutwe mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la serikali ni kuwa na uwekezaji wa viwanda.

Aidha, Dk Mabula alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela kwa kufanya kazi nzuri ya kufutilia na kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais John Pombe Magufuli alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wa Tanga. 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela aliwataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo. 

Alisema, ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya Mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi na uwekezaji. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Meneja wa Mashamba ya Mkonge ya Mohamed Enterprises ya Mazinde Korogwe mkoa wa Tanga Alhaji Imam Sheketo wakati alipofanya ziara katika mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019, kulia kwa waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.
Mkazi wa Mabogo Korogwe mkoani Tanga Said Mbazi Idawa akiwasilisha malalamiko yake wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula katika Mashamba ya Mkonge Korogwe mkoa wa Tanga.
aibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akiwasikiliza wananchi wa Mabogo Korogwe mkoa wa Tanga wakati alipotembelea mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019.
Meneja wa Shamba la Mkonge la Mohamed Enterprises lilipo Korogwe mkoani Tanga Alhaj Imam Sheketo akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela sehemu ya mashine za kutengeneza katani katika shamba lilipo eneo la Mabogo Korogwe Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa wakimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kuangalia eneo la mashine za kutengeneza katani katika shamba la Mohamed Enterprises lililopo Mabogo Korogwe mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-WIZARA YA ARDHI)

WATEJA 6 WAIBUKA WASHINDI WA SIMU SAMSUNG S9+ KWENYE MASTABATA YA NMB

$
0
0
SHINDANO la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata', leo limeendelea kuchezeshwa huku wateja sita wakijishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja.

Katika droo hiyo ya nne pia wateja 20 wengine wa benki hiyo wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- ambazo zitaingizwa kwenye akaunti zao moja kwa moja ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo. Droo hiyo ya nne iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imefikisha wateja 80 hadi sasa ambao wameshindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuchezeshwa droo ya leo, Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala alisema mbali na droo hiyo kupata washindi 20 wa shilingi 100,000/- kila mmoja, wateja 6 wengine wamejishindia simu aina ya Samsung S9+' kila mmoja yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/-.

Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.

Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano hilo.

Mtaalam kutoka kitengo cha Kadi cha NMB, Domitila Silayo (kulia) akiwasiliana na mmoja wa wateja wa NMB waliojishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kwenye droo ya nne ya Shindano la MastaBata. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo pamoja na Sophia Mwamwitwa wa NMB akishuhudia (kushoto). 



Meneja wa NMB Tawi la Mlimani City, akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika kwenye tawi lake.

Meneja kutoka kitengo cha Kadi cha Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa (kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Droo ya nne ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Semvua akisimamia droo hiyo na Domitila Silayo wa NMB (kushoto). 


Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala akizungumza na waandishi wa habari kufafanua wateja walivyojishindia zawadi anuai kwenye Masta Bata ya NMB.

Nkasi waitikia wito wa serikali katika kukikuza kilimo cha kahawa Mkoani wa Rukwa.

$
0
0
Wakulima katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wameitikia wito wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza zao la kahawa mkoani Rukwa na kuhakikisha wanalima zao hilo kwa wingi ili kubadili kipato chao na hatimae kushawishi wawekezaji wa kuchakata zao hilo kuwekeza Mkoani humo ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Zao la kahawa ni miongozi mwa mazao matano ya kimkakati yanayohimizwa na serikali ya awamu ya tano katika kuinua kipato cha wananchi pamoja na pato la nchi kwa ujumla.

Wakulima hao wakiongozwa na mkulima mzoefu wa zao hilo Elias Mwazembe alisema kuwa zao la kahawa linastawi katika mkoa mzima wa Rukwa hivyo aliushukuru uongozi wa Wilaya pamoja na Mkoa kwa kuendelea kuwasaidia pale wanapokwama mbali na changamoto aliyoipata mara ya kwanza alipolima katika hifadhi yam situ wa mfili na kuondolewa na serikali.

“Nilipoona kwenye Mkoa inakubali na kwenye wilaya ikabidi nije huku (Kijiji cha) Kalundi nikaanzisha kulima mwezi wa tatu nikaona ile kahawa inastawi vizuri kwahiyo nikaona hapa sio pa kuachilia niendelee na zao la kilimo lakini sikutulia niliendeleza hamasa kwa watu wengine kuwaambia kuwa zao la kahawa mkoani Kwetu linakubali ingawa changamoto ikawa mtu alikuwa anahitaji avune kwa mwaka huo huo nikasema mbegu iliyopo ni miaka miwili unaweza kuvuna kahawa na kwa umri nilionao nitavuna mpaka vitukuu,” alisema.

Nae Afisa kilimo wa Kijiji cha Kalundi Jiasi Muyunga alikiri kuwa kitendo cha mkulima huyo Elias Mwazembe kufika katika Kijiji hicho kumepelekea wakulima wengi kutaka kujihusisha na kilimo hicho cha kahawa baada ya kuona kuwa kinastawi vizuri katika Kijiji hicho na hivyo kutoka wito kwa maafisa ugani wenzie juu ya kuwasaidia wakulima na kuwakikishia kuwa zao hilo ndilo litakalokuwa mkombozi.

Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi alisema kuwa baada ya kubaini kwamba kata 18 zilizopo ufipa ya juu zenye eneo la hekta 48,000 kuwa zinafaa kulima zao hilo hal,mashauri ilianisha maeneo ya kuanza nayo huku wakishirikiana na kituo cha utafiti cha Tacri kilichopo Mbimba Wilaya ya Mbozi, ili kujua mbegu inayofaa katika maeneo hayo na hatimae kuwapeleka wataalamu na wakulima kwenda kujifunza.

“Mkulima ambaye tumemtembelea leo ndugu Mwazembe ni mmoja wa wakulima hao ambao nae alikwenda kujifunza Mbimba na baada ya kutoka huko aliendeleza juhudi za kufanya kilimo hiki cha kahawa na tunae mkulima mwingine yupo Kijiji cha Kakoma kata ya Namanyere nae pia mepanda kahawa karibu miche 500 na kitaluni ana miche karibu 12,000 na kuna taasisi zaidi ya sita ambazo tumepa miche iliyotokana na kilo 100 za mbegu ambapo kila kilo moja inatoa miche 4000, hivyo tunaamini baada ya miaka mitatu halmashauri itaanza kuona faida yake,” Alisisitiza.

Aidha Afisa kilimo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ocran Chengula aliwashauri wakulima wote wanaotarajia kuanza kilimo hicho cha kahawa kuhakikisha kuwa wanaandaa mashimo mapema na kuweka mbolea ili iweze kuchangayikana na udongo

“Tunatakiwa kuandaa mashimo mapema, kama unategemea kupanda mwaka huu maana yake unaze kuandaa mashimo mwezi wa nane ama wa tisa kwa kuchimba mashimo na kuweka mbolea ili mbolea iweze kuchanganyikana na udongo ikishaanza mvua mwezi wa kumi na moja ile miche inatakiwa ihamishwe kwenye mashamba ili mvua itakavyonyesha iweze kushika na kuwa na nguvu zaidi ya kuweza kukua,” Alifafanua.

Mkoa wa Rukwa unategemea kuwa na miche 1,040,000 ifikapo mwakani inayotokana na kilo 260 za mbegu za kahawa inayopandwa kwenye vitalu mwaka huu ili kuweza kuisambaza kwa wakulima na taasisi mbalimbali ikiwa ni kuhamasisha kilimo cha zao hilo pamoja na kuinua kipato cha wananchi, mkoa na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea kitalu cha mkulima wa kahawa Elias Mwazembe katika Ziara yake ya siku nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. 

HANDENI GIRLS HAPPY TO HELP OUT IN DOMESTIC CHORES

$
0
0
During school holidays most girls in rural areas in Tanzania spend their time helping out their parents with domestic chores. Handeni girls are not an exception. Actually they have been learning the rudiments of living since childhood, hence as teenagers they continue what their parents have taught them ungrudginly.

TAARIFA KUTOA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA).

CULTURE AND GLOBALISATION WORKSHO @ LION HOTEL IN DAR ES SALAAM ON FEBRUARY 9, 2019

FILBERT BAYI: TANZANIA'S GREATEST- EVER ATHLETE WHO BROKE TWO WORLD RECORDS!!!

$
0
0
"Mh. Rais MAGUFULI anasisitiza sana uzalendo. Mtanzania aliyefanya jambo la kishujaa na kizalendo  lazma atajwe ili wananchi wamjue na wampongeze. Ndege ya Dreamliner 787-7 ilipopokelewa, waandishi waliandika kuhusu ndege hiyo tu bila kumtaja na kuandika historia ya Mzalendo, kijana wa Kinyakyusa, GEORGE JONAS, aliyeileta. Hii si sawa. Wazalendo hawa na historia zao lazma zijulikane....:"
PROF. P. KABUDI, Dodoma 30.8.2018.


1. Introduction

Over the years, TZ has produced many good athletes. However, the greatest of them all is none other than FILBERT SANKA BAYI who, in  spectacular and eye-catching ways, broke two World Records in 1974 and 1975! .

2. Birth, Early Days & Education:

FILBERT SANKA BAYI was born on 23.6.1953 in a small village of Karatu within sight of Mt Kilimanjaro. His parents were farmers-cum-cow herders hence when he was a kid, he used to take care of the goats and cows. 

In 1961, at the age of 6, BAYI started school whose location was 2 miles away from where his family lived. Every morning he had to run to school, then he had to go back for lunch and then he had to return to school for the afternoon classes. So, as a young boy, he was running about 8 miles a day and that built a lot of stamina in his body.

Throughout his years at school, BAYI continued to excel as an athlete immersing himself in competitions and working his way up to district and regional competitions.

3. Leaving Karatu for Dsm

BAYI left school in 1970 at age 17 and migrated to Dsm. While in Dsm, his running training was unique and very crude. In the crowded, high-humidity capital, he would pick up and sprint alongside a moving bus and rest when the bus was loading and unloading passengers. This was his daily routine in the morning and evening!.

4. National & International competitions:

In 1971, BAYI achieved a reasonably good personal best of 3:52:12 In the 1500 M.

BAYI competed in the annual East and Central African championships held in Dsm, TZ. On 3.12.1972, BAYI became a regional champion in the 1500 M. He won in an impressive time of 3:38:9, setting a new national record. He also beat his idol, the great Kenyan, Kip Keino.

5. BAYI's World Record in 1974

In 1974, the Commonwealth games were held in Christchurch, New Zealand. 21 year old BAYI, an athlete with an "Afro-hairstyle" and boyish looks, would compete in the 1500 M. BAYI, together with other Tanzanian athletes, left the country quietly. There was hardly any fanfare.!

The 1974 finals of the 1500 M at the Commonwealth games will loom in the minds of may truck enthusiasts for a very long time.

The date was February 2, 1974 and the stage was the men's 1500 M final. The home crowd, at the top of their voices, roared on their great hero, long-haired JOHN WALKER.

When all the competing athletes knelt down waiting for the starting pistol to be fired to start the race, the 21 year old Masai-boy from Karatu, Bongoland, alijifanya kama anajikuna vile and then he led from the start and continued at a blistering pace throughout the race to cross the finish line FIRST in a race that is often described as "the greatest middle distance event of all time". BAYI set a new world record of 3:32:16 smashing the previous world record set by JIM RYUN in 1967 in the US. The great JOHN WALKER came second.

What a sweet win for Tanzania! It was a glorious moment for our dear motherland, with one of our own putting us on the world map!.

Consequently, a huge crowd turned out at the DSM International airport, on 6.2.1974, to give BAYI, their triumphant hero, a deserved  rousing welcome back!.

It would take 5 more years for Great Britain's SEBASTIAN COE to break the record. Today, 45 years on, BAYI's phenomenal performance remains a Commonwealth record!. 

6. BAYI's World Record in 1975:

After setting a new world record in the 1500 M in 1974, BAYI was not done yet as he set another new world record a year later.

On Saturday night, in Kingston, Jamaica on 17.5.1975, leading, as usual, from start to finish, BAYI broke the world record in the Mile run! Two Villanova greats namely MARTY LIQUORI and EAMMON COUGHLIN, took turns chasing BAYI only to finish second and third respectively.

This was a world record performance that defied logic, a set of stopwatch numbers that hardly seemed real. Yet it stood there; irrefutable: a 3:51 Mile run by BAYI breaking JIM RYUN's 8 year world record of 3:51:1. 

BAYI did it despite a 23- hour plane trip from Bongo to Jamaica via Rome, London, Montreal and New York which landed him in Kingston, Jamaica just 48 hours before the race!.

7. Life after retirement:

BAYI is now the Secretary General of the Tanzania Olyimpic Committee.

On the other hand, the beginning of the new century witnessed retired Major BAYI and his wife commendably setting up a foundation "FILBERT BAYI FOUNDATION" intended to tap and develop athletic and educational youngsters.

BAYI opened the first iteration of FILBERT BAYI SCHOOL in a garage with just 7 children in attendance. It then developed into a large campus catering to thousands of students from nursery level up through primary school and into secondary school.

BAYI's complex lies in Mkuza, 50 miles from Dsm. 

8. What Next?

BAYI now intends to have a university.

More importantly, it is now 44 years since BAYI broke the Mile world record. Why can't we produce other BAYIs? Sadly, this is a jinx which, it seems, will take a miracle to break. There is a plethora of crippling challenges, from poor organization to poor funding, which bedevil any effort to MAke TAnzania Great Again (MATAGA) in this field!

In my view, as a country, we need to have a wholesome sports development agenda for the country where athletics and other  games are nurtured for good health, money and the glory of our nation.

KUDOS FILBERT SANKA BAYI- TANZANIA'S MOST DECORATED ATHLETE!

GCLA Kanda ya Kaskazini inajipanga kuanzisha Maabara ya vinasaba vya wanyama

$
0
0
Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango akiwatembeza maofisa  habari wa wizara na taasisi wa wizaravya afya wakati walipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa kampeni ya "Tumeboresha Sekta ya Afya"ambayo imeanza kwa mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Kilimanjaro.

NA WAMJW, ARUSHA

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini - Arusha, ipo mbioni kuanzisha Maabara maalum ya Vinasaba vya wanyama ambayo itasaidia kutambua asili ya mnyama ikiwemo wanyama waliopo ama waliokufa.

Akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa Uhusiano waliotembelea Kanda hiyo leo, Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango abainisha kuwa kwa sasa wapo katika ukarabati wa jengo ambalo Maabara hiyo itakuwepo. Awali ujenzi wa jengo hilo ulisimama baada ya ufadhili wake kukoma na hivyo kuilazimu Mamlaka kufanya ukarabati ili kujipatia sehemu ya kufanyia kazi.

"Maabara ya vinasaba vya wanyama ni muhimu sana. ukanda huu kutokana na kuwa na wanyama wengi na pia eneo la Kanda ya Kaskazini kuwa na watalii wengi ambao wanakuja kuona wanyama . Kwa sasa utaratibu unaendelea wa Kumalizia jengo hili na baadaye vitendea kazi kuwekwa "ameeleza Anyango.

Anyango ameongeza kuwa suala la kuwatunza wanyama ili waendelee kuwepo, Ni suala la msingi na Maabara itakapokamilika hakuna sampuli zitakazosafirishwa nje ya Kanda ya Kaskazini kwa uchunguzi.

"Pale hitaji litakapokuwapo kwa ajili ya uchunguzi wa wanyama hawa, baasi Kazi hii itafanyika hapa hapa Arusha." Alisema Anyango.Aidha, ametaja faida ambazo zitapatikana kwa Nchi ni pamoja na uwepo wa data zao kwa wanyama hao ikiwemo wanyama wanaolindwa Kimataifa kama Kifaru, tembo na wanyama wengine wengi ambao wapo hatarini kutoweka.

Maabara hii inatarajiwa kuwa ya kwanza Nchini na itakuwa ndio maabara Bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.Maabara hiyo itaweza kufanya uchunguzi kwa wanyama wote wakiwemo walio hai na waliokufa.

Aidha, wamemshukuru Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Rais Dk Joseph Pombe Magufuli kwa kutenga na kuridhia kiasi cha bajeti ya Shilingi Milioni 950 ya kwa ajili ya kumalizia jengo hilo.
Jengo la mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kaskazini-Arusha

RAIS JOSEPH KABILA: "MBONGO" ANAETAWALA WACONGOMANI DRC!!!

$
0
0
Rais JOSEPH KABILA ni raia wa Democratic Republic of Congo (DRC) lakini kwa kuwa amekulia Bongo kwa miaka mingi, basi ni dhahir shahir unaweza kumwita ni Mbongo! Ukweli huu unaakisiwa na usuli wa historia ya maisha yake.

JOSEPH alizaliwa tarehe 4.6.1971 eneo la Hewabora kijijini Fizi, Kivu Kusini huko Mashariki mwa DRC  ambapo alizaliwa pamoja na pacha wa kike aitwaye  JAYNET.

JOSEPH alianza masomo ya shule ya msingi huko DRC lakini alikuja kuendelea na masomo yake jijini Dar Es Salaam, Tanzania mwaka 1977 baada ya baba yake, LAURENT DESIREE KABILA na mama yake, SIFA MAHANYA, kuhamia Tanzania baada ya miaka mingi ya kuishi msituni huko Kivu wakiendesha uasi dhidi ya Rais wa wakati huo, marehemu dikteta MOBUTU SESE SEKO KUKU NGBENGU WA ZABANGA.

Baada ya masomo ya shule ya msingi, JOSEPH alisoma masomo ya jioni ya taasisi ya Zanaki katika shule ya sekondari ya wasichana ya Zanaki. Akiwa Zanaki, alikuwa pia akipata mafunzo ya kareti toka kwa Sensei MASSAWE aliyekuwa "Karate Spurring Partner" wake. Akiwa kijana, JOSEPH alipewa jina la utani la  "WAR BUS" kwani alipenda sana sinema za kivita na 'martial arts".  
 Miaka ya mwisho ya 1980s, JOSEPH alijiunga na Shule ya Sekondari ya Irambo ambako alisoma kidato cha tano na sita. Shule hiyo kuukuu iko jijini Mbeya ambayo sasa, kwa kumuenzi JOSEPH, imeweka kumbukumbu  yake ambapo njia aliyokuwa akipita kwenda madarasani toka bwenini, imewekwa bango "JOSEPH KABILA ROAD". Aidha, bweni alimokuwa akilala sasa limegeuzwa na kuwa darasa  "Form 11 B". Bw. SHAMBWEE SHITAMBALA, aliyekuwa CHADEMA na kisha kutimkia CCM na ambaye kwa sasa ni wakili wa kujitegemea jijini Mbeya, ni mmoja wa waalimu waliowahi kufundisha katika shule hiyo. 

Baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha sita, JOSEPH alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujinga Taifa. Mafunzo hayo ya lazima ya mwaka mmoja yalikuwa ni kwaajili ya kuwajengea uzalendo na ukakamavu vijana wa Kitanzania na yalianzishwa kwa mujibu wa "The National Service Act No. 16 of 1964 ('RE 2002)".

JOSEPH alijiunga na kambi ya KJ 834 MAKUTUPORA JKT "OPERESHENI VYAMA VINGI" 1992/93 ambapo alikuwa "D Coy" kwaajili ya mafunzo hayo. Kambini hapo, JOSEPH alikuwa ni kijana mkimya  na mtaratibu. Alipenda sana mafunzo ya kijeshi na hakuwahi kujongo hata mara moja. Aidha, alipenda sana kupata habari mchanganyiko na alikuwa akitembea na kiredio chake kidogo mkononi na alikuwa msomaji mzuri wa "novel".

Hapa Dar Es Salaam, Mzee LAURENT DESIREE KABILA na familia yake waliishi eneo la Kunduchi Kilongawima karibu na bahari. Kwa kuogopa kubambwa na vikaragosi vya dikteta  MOBUTU, mzee KABILA alikuwa akitumia jina feki la FRANCIS MTWALE au "Baba Cecy"(jina la mmoja wa watoto wake) na kudanganya kuwa yeye ni mfipa wa Sumbawanga!. 
Mwanzoni, maisha ya familia hiyo yalikuwa ni ya kubangaiza na "kuungaunga" sana na hii ilipelekea watoto wa mzee huyo kusoma shule chovu. Mkewe, SIFA MAHANYA alilazimika kulima vimbogamboga na kwenda kuuza sokoni kwani walikuwa hoehae sana huku wakiwa na watoto wengi. Bi SIFA, baada ya mmewe kuwa Rais wa DRC,  alikuja kuuelezea mwenyewe ufukara huo uliokuwa umetamalaki kwenye familia yao kwa muongo mingi ambapo tarehe 2.6.2006 alisema:
"If life in the bush in Kivu was difficult, in Tanzania it was much worse. We had nothing. I farmed a small field and sold my vegetables at the market like all poor African women".  
Mzee KABILA akiwa nchini Tanzania alikuwa akizunguka nchi mbalimbali kutafuta 'support" ya kumng'oa MOBUTU. Hapo Kunduchi Kilongawima, familia hiyo ilipata nyumba ambayo ipo mpaka leo na panajulikana kama "Kwa KABILA". Akiwa Kilongawima, mzee huyo  alikuwa maarufu kutokana na ucheshi na kupenda kujichanganya hasa na vijana. Alikuwa na Land Rover 104 yake nyeupe aliyokuwa akiitumia kubebea nyasi za ngombe alizokuwa akizichukua Mbuyuni njia ya Tegeta.

Baadhi ya watoto wa mzee KABILA wamezaliwa Dar As Salaam (ZOE(26.6.1979), CECYLIA na JOSEPHINE). Mmoja wa watoto wa Mzee KABILA aliyekuwa akipenda kwenda kupunga upepo baharini karibu na Kilongawima, alitokea kumpenda mvuvi mmoja mchovu Mzanzibar aliyekuwa akivua samaki mara kwa mara na wenzake katika eneo hilo. Baada ya maisha kuinyookea familia ya KABILA, mvuvi huyo kijana, baada ya kupata rizki mantashari hiyo toka kwa binti wa Mzee KABILA, kwa sasa ni milionea aliyeamua kurudi kwao Zanzibar anakomiliki moja ya  kumbi  kubwa za muziki Afrika Mashariki iliyoko kwenye eneo kubwa pembezoni ya Zanzibar. Mara kwa mara, "mvuvi" huyo hupenda  kupiga stori maskani iliyopo jirani na ukumbi huo akiwa na washkaji zake ambapo ukimuona huwezi kuamini kuwa ndio "owner" kwani wengi wanadhani inamilikiwa na Muitaliano!.

JOSEPH alimaliza mafunzo ya JKT mwaka 1993. Kwa kuwa amekaa Tanzania kwa miaka yote hiyo, anakicharaza Kiswahili kama Mbongo tofauti na WACONGOMANI ambao wengi mara nyingi wanaongea Kifaransa na Kilingala  huku lafudhi yao ya Kiswahili ikiwa na mushkeri. 

Si Mzee KABILA pekee aliyekuwa akitumia jina feki alipokuwa Tanzania bali hata wanawe, kama alivyokuja kukiri mkewe SIFA baada ya kurejea DRC. Hata JOSEPH hakuwa akiitwa JOSEPH KABILA kama ilivyo sasa bali alijulikana kama JOSEPH KABANGE, lengo likiwa kutotumia jina "KABILA lililokuwa maarufu Zaire/DRC.  


JOSEPH, baada ya mafunzo ya JKT, alienda Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Mzee KABILA, baada ya harakati za miongo mingi, hatimaye akafanikiwa, kwa msaada wa mataifa mbalimbali, kumng'oa dikteta MOBUTU na kuwa Rais wa tatu wa nchi hiyo tarehe 17.5. 1997.

Mwaka huohuo wa 1997 alimpeleka mwanae, JOSEPH, kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi Beijing, China kwenye Chuo cha PLA National Defence University na aliporejea mwaka 1998, alimteua kuwa Meja Jenerali.

Mzee KABILA aliuawa tarehe 16.1.2001 baada ya "kutandikwa shaba" na mmoja wa walinzi wake ambapo aliacha watoto 25 aliozaa na wanawake 7. Idadi hii ilithibitisha alichokisema Rais DR. MAGUFULI tarehe 17.10.2016 pale Karimjee Hall wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Meya wa zamani wa Dar Es Salaam, marehemu DIDAS MASABURI aliposema: "Ni jambo la kawaida kwa wanaume wa Kiafrika kuwa na wake wengi na watoto wengi. Hii idadi iliyotajwa hapa ya wake na watoto wake si sahihi, mi najua wapo wengi zaidi". 

Tarehe 26.10.2001, JOSEPH akamrithi marehemu baba yake na kuwa Rais wa nne wa DRC. Akiwa amezaliwa mwaka 1971, JOSEPH alikuwa Rais wa kwanza duniani kuzaliwa miaka ya 1970s na kwa umri wake wa miaka 30, akawa ndiye Rais mdogo kuliko wote duniani!. 

Tarehe 1.6.2006, Rais JOSEPH KABILA alimuoa Bi. OLIVE LEMBE DI SITA,  ndoa iliyofungwa kanisani na kufuatiwa na harusi ya kukata na shoka ambapo watu walikula kunywa hadi majogoo!.
Rais JOSEPH KABILA na "First Lady" huyo wana watoto wawili ambapo mmoja ni wa kike aitwae SIFA, na mwingine ni wa kiume aitwaye LAURENT DESIREE (ambayo yote ni majina ya wazazi wa Rais JOSEPH KABILA). 

Mwaka 2006, Rais JOSEPH KABILA alichaguliwa kuendelea kuwa Rais katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia toka nchi hiyo ipate uhuru toka kwa Ubelgiji mwaka 1960. 

Rais JOSEPH KABILA alichaguliwa tena kuwa Rais mwaka 2011. Kwa kuwa Katiba ya DRC iliyopitishwa tarehe 18.2.2006 inampa Rais mihula miwili tu ya kutawala, mhula wake wa miaka mitano ya mwisho uliisha mwaka 2016 baada ya kucheleweshwa, uchaguzi umefanyika tarehe 30.12.2018 ambapo yeye hakugombea bali alipiga kura. 

Tafakuri Tunduizi (Critical Thinking):

1. Je, iliwezekanaje Mcongoman JOSEPH kuhudhuria mafunzo ya JKT yaliyotolewa mahususi kwa vijana wa KITANZANIA?

2. Baada ya kuwatumikia wananchi wa DRC kama Rais, je "Mbongo" JOSEPH KABILA,   atarejea Kunduchi Kilongawima alikokulia? 

3. Je, uongozi wa Shule ya Sekondari ya Irambo ambayo imekuwa chovu una mikakati gani ya kuwatumia 'alumni wake hasa Mh JOSEPH KABILA ili kuikarabati? 

4. Je, ni kwanini watoto wakizaliwa, mara nyingi, hupewa majina ya babu na bibi zao? 

5. Je, ni sahihi kwa watoto  wazaliwao kuchukua majina ya wazazi wa baba tu? 

Tupia maoni yako. 

MAMA FATMA ABEID KARUME IS ONE OF TEN EXTREMELY UNIQUE FIRST LADIES ON THE PLANET!!!

$
0
0
There have been only TEN FIRST LADIES on the planet who are extremely unique because they were married to Presidents and later gave birth to Presidents!

Although there are seven continents of the world namely AFRICA, EUROPE, ASIA, SOUTH AMERICA, NORTH AMERICA, AUSTRARIA and ANTARCTICA but 70% of these unique First Ladies hail from Africa, the world's second largest continent. Oh AFRICA my motherland!.

Betterstill, one of them is none other than our very own MAMA FATMA ABEID AMAN KARUME who is also a member of the Board of Trustees of YANGA, the most successful team ever in Tanzania!.

Hereinbelow is a list of that rare breed of women:

1. FATMA ABEID AMAN KARUME:

She is the Co- mother of our nation as she was the wife of the First President of Zanzibar, the late ABEID AMAN KARUME who served as the First President of Zanzibar from 12.1.1964 to 7.4.1972 when he was assasinated. MAMA FATMA, on the 1st November 1948, birthed AMAN ABEID KARUME who went on to become the 6th President of Zanzibar and served from 8.11.2000 to 3.11.2010.

2. MAMA NGINA JOMO KENYATTA:

She was the third wife of the first President of Kenya, the late JOMO KENYATTA who served from 12.12.1963 to 22.8.1978. On the 26th October 1961, at 11.10 AM at Aga Khan Hospital, Nairobi, MAMA NGINA gave birth to  UHURU MUIGAE JOMO KENYATTA, the sixth child of the late founding President. UHURU is the fourth and current President of the Republic of Kenya.

3. SIFA MAHANYA:

She saw her husband, the late LAURENT DESIREE KABILA, rise to power, after having moved from Zaire to Tanzania in mid 1970s, and become the 3rd President of DRC on 17.5.1997 before he was assasinated by his bodyguard on 16.1.2001. Ms SIFA gave birth, on 4.6.1971, to JOSEPH KABILA who is the fourth and current President of DRC.

4. RUTH WILLIAMS KHAMA:

She was the wife of Botswana's First President, Sir SERETSE GOITSEBENG MAPHIRI KHAMA who was President between 1966 and 1980 hence she served as the inaugural First Lady. Her son, IAN SERETSE KHAMA, born on 27.2.1953,  served as the fourth President of Botswana from 1.4.2008 to 1.4.2018. 

5. SENA SABINE MENSAH:

She was the First Lady of Togo for 38 years as her husband, the late ETTIENE GNASSINGBE EYADEMA who was the fourth President of Togo from 1967 to 2005, died in office in 2005 paving way for her son, FAURE ESSOZIMNA GNASSINGBE EYADEMA, born on 6th June 1966, to become the fifth President of Togo. 

6. PATIENCE DABANY:

She was the First Lady of Gabon for 42 years before her husband, the late El Hadji OMAR BONGO ENDIMBA, the second President of Gabon who served from 2.12.1967 to 8.6.2009, died in 2009 and her son, ALI BONGO ONDIMBA took over on 16.10.2009 as the third President of Gabon.

7. ADELINE SYLVIA EUGENIA ANA YEBOAKU AKUFO ADO:

She was the wife of the fourth President of Ghana, His Excellency EDWARD AKUFO-ADO who served from 31.8. 1970 to 13.1.1972 when he was deposed in a coup d'etat and later mother to His Excellency NANA AKUFO-ADO, born on 3.1944, who is the current President of Ghana.

8. ABIGAEL JOHN ADAMS:

She was the wife of the second US President, the  late JOHN ADAMS, who served from 1797 to 1801. She is considered as one of the most intelligent First ladies the world has ever seen. During their courtship and marriage, ABIGAEL and JOHN exchanged over 1,100 letters, many filled with intellectual discussions on government and politics and not udakuz!. Her eldest son, JOHN QUINCY ADAMS, served as the sixth US President from 1825 to 1829. ABIGAEL died in 1818, seven years before her son became President.

9. YUK YOUNG-SOO:

She was the wife of the third South Korean President, PARK CHUNG- HEE who served from 1963 to 1979 when he was assasinated  and the mother of Her Excellency Ms.PARK GEUNE-HYE, born on 2.2.1952,  who served as the eighteenth President of South Korea from 2013 to 2017. First Lady YUK YOUNG -SOO is the only First Lady to have given birth to a female President. 

10. BARBARA GEORGE BUSH:

She was the First Lady of the United States  from 1989 to 1993 as the wife of the 41st US President GEORGE HEBERT BUSH. Among her sixteen children is GEORGE WALKER BUSH, born on 6.7.1946, who served as the 43rd US President from 2001 to 2009.

NB: MAMA MARIA GABRIEL JULIUS NYERERE, who served as the inaugural First Lady of Tanganyika & Tanzania, would have joined the above unique club had her son, Hon. CHARLES MAKONGORO NYERERE, been elected by CCM as its presidential candidate since he was one of 42 CCM stalwarts who had collected nomination forms in 2015.

SARAH SIMBAULANGA: MWANAMKE WA KWANZA "BANDIDO""KUPIGA PESA NDEFU" KATIKA HISTORIA YA MABENKI NCHINI!!!

$
0
0
Saa 7 kamili mchana, siku ya jumapili ya tarehe 1.11.1987, Watanzania, kila pembe ya nchi, walipigwa butwaa na kushikwa na bumbuwazi kubwa baada ya Radio Tanzania Dar Es Salaam kutangaza, katika taarifa ya habari, kwamba mwanamke aitwae SARAH MARTIN SIMBAULANGA (35) mfanyakazi wa NBC alikuwa amekwapua mamilioni ya fedha na alitoroka nchini akiwa na watoto wake watatu na laaziz wake, Mfanyabiashara TOROHA MOHAMED TOROHA(40).

Tukio hilo la kipekee na la aina yake liliwaacha midomo wazi wananchi hasa kwavile enzi hizo halikuwa jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa "mpigaji" wa kiwango cha kutisha cha fedha!.

Tukio hilo liliongelewa mno sehemu mbalimbali hasa maofisini, majumbani, mashuleni, makambini, masokoni, mahotelini, vilabuni nk huku wengi wakimlaani vikali mwanamke huyo na kusikitika nchi kuibiwa fedha hizo. Kwa wengi, ilikuwa ni simanzi kubwa sana na haikushangaza basi pale Mkutano Mkuu wa Baraza la Kuu la Vijana uliokuwa ukifanyika Singida kutoa wito kuwa uongozi wote wa juu wa NBC "Ufyekelewe mbali"!.  

Ofisi ya DCI, mara moja, ilituma taarifa  (Interpol) nchi mbalimbali ili zisaidie kuwakamata "mabandido" hao.

Hatimaye, majira ya saa 9 alasiri, siku ya Ijumaa, tarehe 13.11.1987, Bw. TOROHA akabambwa kwenye ofisi ya magari ya Toyota jijini Nairobi, Kenya akiwa kwenye mishemishe ya ununuzi wa magari.

"Mandata" walipombana aeleze kuhusu aliko Bi. SARAH, Bw. TOROHA hakuwa na namna zaidi ya kuwapeleka chumba na. 322 cha hotel maarufu ya Jacaranda. "Mandata" hao, wakiwa na TOROHA, waliingia chumba hicho kininja na kumkamata Bi. SARAH kiulaiiini!.

Jijini Dar Es Salaam, NBC ilimfukuza kazi Bi. SARAH kwa kutoonekana kazini kwa siku 5 mfululizo. Aidha,   kamatakamata ilianza ambapo wafuatao walikamatwa na kuhusishwa na wizi huo: Bw. ROMANIUS PETER NDANZI(43), Mdhibiti wa Fedha za Kigeni, NBC "Foreign Branch",  Bw. ERNEST JOHN MWENEWANDA(40), Meneja mauzo KLM, HAROON DAUD(35), Mfanyabiashara. Washtakiwa hawa, tarehe 19.11.1987,  walifikishwa Kisutu kwa "Pilato" Mh. JUMA MUSTAPHA JIBREA. Waliomba dhamana wakanyimwa. Wakakata rufaa Mahakama Kuu.  Tarehe 5.1.1988, Jaji LUHEKELO KYANDO, aliwanyima dhamana na kueleza, kwa uchungu na uzalendo, kwamba:
"Kiini cha kesi hii ni moja ya matukio ambayo yameshtua sana umma kuona kwamba mamilioni ya fedha yanaibwa. Ni maoni yangu kuwa itakuwa kinyume na hisia za jamii ikiwa mahakama itachukua msimamo tofauti na usiokuwa na mwelekeo wa hisia sahihi kuhusu vitendo hivi".

Msimamo huu uliakisi kilichoelezwa na aliyekuwa Waziri wa sheria, Mama JULLIE MANNING, tarehe 17.1.1976, kwamba: "Ingawa Mahakama hazipendelei upande wowote, hiyo haina maana kwamba zisijali nini kinatokea nchini".

Serikali ilituma Kenya Hati ya kuomba SARAH na TOROHA warudishwe nchini(Extradition) kwani nchi hizi zina makubaliano hayo ya aina hiyo. Hati hiyo iliwasilishwa na SP PETER MWANGI mahakamani saa 2.30 asubuhi ijumaa, tarehe 15.1.1988 mbele ya Hakimu Mwandamizi, Mh JOSEPH MANGO na kisha maombi hayo yakaanza kusikilizwa.


Tarehe 29.1.1988, mahakama hiyo ikatoa uamuzi kuwa, kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa, SARAH arudishwe  Tanzania kujibu mashtaka lakini ikamuachia huru TOROHA. Baada tu ya kuachiwa, mbio alizotimua TOROHA, hata USAIN BOLT angesubiri!.


Siku ya jumanne, saa 6 mchana, tarehe 2.2.1988, SARAH alikabidhiwa kwa maafisa wa Tanzania mpakani Namanga na kukimbizwa "wanguwangu" na magari 5 ya polisi hadi Dar Es Salaam.

SARAH alifikishwa mahakama ya Kisutu saa  tatu asubuhi, siku ya Jumatano, tarehe 10.2.1988 chini ya ulinzi mkali. Mahakama hiyo ilikuwa imefurika mno huku barabara ya Bibi Titi ikifungwa kwa muda kwani wananchi wengi walitoroka makazini kwenda kumuona SARAH anafananaje na kusikia aliwezaje kuiba kitita chote hicho!.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mh. JOSEPH MASANCHE, Bi. SARAH alisomewa mashtaka 5 na SSP EDWIN ABRAHAM MAN. Bi. SARAH alikuwa akitetewa na Dr. MASUMBUKO ROMAN LAMWAI, mmoja wa mawakili bora kabisa kuwahi kutokea nchini.

Bi. SARAH aliushangaza umati uliofurika, pale bila kupepesa macho, kutingisha pua wala kutikisa maskio, alipokiri mashtaka yote 5! Hakimu MASANCHE nae pia alipigwa butwaa na ikabidi amuulize kama ameelewa vizuri mashtaka ambapo "alikomaa" na kusema anaelewa na anakiri ni kweli alitenda makosa hayo!. 

Mh MASANCHE, baada ya kusikiliza pande zote 2 kuhusu adhabu, akasoma hukumu iliyochukua robo saa tu ambapo alimuhukumu SARAH kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa na makosa yote kwenda pamoja hivyo angetumikia miaka 7 tu na pia akamuamuru arudishe fedha hizo mara moja. Mh MASANCHE alin'gaka- "Hakuna kitu kibaya kama wizi wa fedha za kigeni ambazo Taifa linazihitaji sana".

Upande wa mashtaka haukuridhika na adhabu hiyo "kiduchu" hivyo ukakata rufaa Mahakama Kuu kuomba adhabu hiyo iwe kwa kufuatana na sio kwa pamoja. Aliyekuwa Jaji Kiongozi, Mh. NASSOR MZAVAS ndiye aliyesikiliza rufaa hiyo huku jamhuri ikiwakilishwa na Bw. KULWA SATO MASSABA na Dr. LAMWAI akimuwakilisha SARAH. 


Saa 4 asubuhi, Ijumaa ya tarehe 19.2.1988, Mh MZAVAS alitoa hukumu. Baada ya kuisoma hukumu hiyo kwa dakika 45, huku umati ukisubiri kwa hamu, Mh. MZAVAS "aliinama na kujifanya kama anajikuna" kisha "akampiga SARAH mvua 28"! SARAH hakuamini macho yake na kubaki amebun'gaa!  Mh. MZAVAS akamalizia- "Hii ni hasara ya kiuchumi ambayo inaiathiri nchi. Fedha hizo kidogo za kigeni nchi ilizofaulu kujiwekea akiba kwa kujikidhi sana, ndio inalolifanya kosa la kuiba fedha za kigeni kutisha. Wizi huu ulipotangazwa na RTD, Mahakama pia ilisononeka na kufadhaika sana kwa kuibwa kwa fedha hizo za kigeni kwani Mahakama nayo ni sehemu ya jamii".


"Upigaji" huu ulikuwa umepangwa na wapenzi hao wawili, SARAH na TOROHA. TOROHA alikuwa ni kijana mtanashati aliyezaliwa  Mbegani, Bwagamoyo mwaka 1948. Baba yake aliwahi kufanya kazi Ikulu na kisha akawa Afisa wa ubalozi Japan na Uholanzi miaka ya mwanzoni ya Uhuru na alikuwa na uwezo wa kifedha. Mwaka 1967, baada ya kuzinguliwa na siasa ya Ujamaa ambapo  nyumba yake ilitaifishwa, aliacha kazi na  kutimkia Ujerumani  na kufanya biashara ya mkahawa na duka la vinyago.  

Mwaka 1979, Bw. TOROHA, akiwa kijana wa miaka 31, alimuoa Mkenya, Bi. ELIZABETH WANJIRU na wakaishi Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Kenya.

TOROHA alikuwa akija nchini mara mojamoja hivyo akaanza urafiki na Bi. SARAH aliyekuwa binti mdogo mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Zanaki jijini. SARAH, baadaye, aliajiriwa NBC na kupanda vyeo hadi kuwa Msimamizi, Idara ya Fedha za Kigeni.

TOROHA aliingia nchini tarehe 11.10.1987 na kufanya "mchongo wa upigaji" na "Mpango wa kando" wake, Bi. SARAH. Ili kufanikisha dili la upigaji na kusepa nje ya nchi bila kushtukiwa, Bi. SARAH alishirikiana na maafisa wasio waaminifu wa "Immigration" na kubadili majina yake na ya wanawe na kupata "passports" mpya tarehe 28.10.1987. "Passport" ya SARAH yenye Na. 220130 ikawa na jina KHADIJA ALI MKIMBAU. "Passports" za wanawe zikawa na majina mapya 1.HAPPINESS SIMBAULANGA-(JAMILA ISMAEL HASSAN), 2. SIMBA SIMBAULANGA- (HALFAN ISMAIL HASSAN), 3. BLANDINA SIMBAULANGA-(JENIPHER ISMAEL HASSAN). 

Kisha, SARAH "akapiga" hundi za kusafiria 1,100 zenye thamani ya $ 390,000 na hundi 200 zenye thamani ya  £ 20,000. Fedha hizo 'alizipiga' mara 3 kati ya tarehe 19.10.1987 na 29.10.1987. Kwa wakati huo, hizo zilikuwa ni fedha nyingi sana. Baada ya mchongo kukamilika, SARAH na TOROHA walichukua vyumba 2 katika hotel maarufu sana ya Skyway  iliyokuwa makutano ya Ohio na Samora. Chumba kimoja kilikuwa chao na kingine cha watoto wa SARAH ambako walilala kwa usiku mmoja wa Ijumaa, tarehe 30.10.1987. Usiku wa Ijumaa hiyo, SARAH na TOROHA walienda ukumbi wa White House "kushangilia ushindi" ambako bendi ya Marquis du Zaire chini ya Babu Seya iliwapagawisha vilivyo!.

Tarehe 31.10.1987, TOROHA, kin'gast chake SARAH na watoto wake 3 walikwea pipa la ATC kwenda Kenya. Walipotua tu Jomo Kenyata International Airport, wakatumia hundi zenye thamani ya $ 2700 kununua tiketi 5 za KLM na wakaenda Amsterdam na kisha London. Wakiwa London UK, walifanya "transactions" nyingi "Baclays bank"  na   tarehe 2.11.1987 wakanunua tiketi 5 za KLM ili waondoke kuelekea Kenya tarehe 5.11.1987. Tarehe 3 na 4 ilikuwa ni "kujirusha" tu nchi ya Malkia ile Kazi na Bata!.

Tarehe 5.11.1987 walikwea KLM na kufika Kenya tarehe 6.11.1987. Nchini Kenya walifanya matanuzi na manunuzi ambapo TOROHA alitumia $ 260,000  kununua magari (mini-bus 4 na pick up 1) na yote akayasajiri kwa jina la SARAH. TOROHA, alipokuwa akitaka kununua magari mengine ndipo aliponyakwa na mamwela katika ofisi za Toyota tarehe 13.11.1987! .

Huu ndio mkasa wa Bi. SARAH MARTIN SIMBAULANGA @KHADIJA ALLY MKIMBAU uliokuwa wa aina yake na wa kipekee!

MH: JULIE MANNING: MWANAMKE MTANZANIA WA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUSOMEA SHERIA NCHINI MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NA REKODI LUKUKI!!!

$
0
0
1. Usuli:

Tanzania imebarikiwa kuwa na wanawake hodari na wachapakazi walioliletea heshima na mafanikio makubwa Taifa letu. Hata hivyo, weledi, utumishi uliotukuka, uzalendo pamoja na historia yake ya kipekee isiyo na mfanowe, ni vitu vinavyomtofautisha kabisa Bi. JULIE CATHERINE WILLIAM MANNING na wanawake wengine nchini!.

2. Asili ya BI.JULIE:

Bi.JULIE ni mmoja wa watoto 10 wa marehemu Dr. WILLIAM MANNING ambaye alikuwa chotara kwani baba yake alikuwa mzungu aliyemuoa Mwafrika Mmalawi(Bi. REBECCA MWALE). Bi. JULIE nae ni chotara kwani baba yake(Dr. WILLIAM), aliyezaliwa mwaka 1910, alimuoa mwanamke wa Msumbiji, Bi. MARIA REGINA ambaye ni mama yake Bi. JULIE.

Dr. WILLIAM na Bi. MARIA walifika Kyela, Mbeya zamani na kuishi  kwenye nyumba ya serikali kwani Dr. WILLIAM alikuwa akihudumu kama daktari kwenye hospitali ya wilaya .

3. Masomo:

Dr. JULIE amesoma shule ya msingi Kissa ambayo ilikuwa katika eneo kati ya wilaya ya Kyela na Tukuyu. Shule hii ilikuwa ni ya masista. 

Baada ya kumaliza elimu ya msingi, Bi. JULIE alifaulu vizuri hivyo akachaguliwa kujiunga na shule ya sekondari  ya wasichana ya "Tabora Girls" huko Tabora, shule ambayo ilianzishwa mwaka 1928 ikiwa shule ya msingi na baadaye kubadilishwa na kuwa ya sekondari.

4. Chuo Kikuu:

Bi.JULIE alifaulu vizuri sana masomo yake na akawa na nia ya kuwa mwanasheria na wakati huo wa ukoloni hakukuwa na Chuo kikuu hapa nchini. Bahati nzuri, tarehe 25.10.1961, mwezi takribani mmoja kabla ya uhuru, kikazinduliwa Chuo Kikuu kipya jijini Dar Es Salaam . Chuo hicho kilikuwa na kitivo kimoja tu ambacho kilikuwa ni Kitivo cha Sheria. Chuo hicho kilikuwa ni "affiliate" ya Chuo Kikuu cha London na ndicho pekee kilichokuwa kinatoa kozi ya  shahada ya sheria kwa nchi za Afrika Mashariki. Kitivo hicho kilizinduliwa na Mwalimu JK NYERERE, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, ambaye alisema:

"My Government is so pleased that the law faculty is open before independence day. Dar Es Salaam is the only place where East Africans can get training in Law. It is not by accident that we started with a Law college. An essential part of national philosophy must be a Legal profession of great integrity which not only knows the formalities of Law but also understands the basic philosophy which underlies our society.."
Bi. JULIE alichaguliwa kujiunga na chuo hicho akiwa ni mmoja wa wanafunzi 13 wa kwanza wa Kitivo hicho cha Sheria walipotoka Tanganyika, Kenya na Uganda. Bi JULIE alikuwa ni mwanamke pekee kwenye Kitivo hicho. Hivyo, Bi. JULIE akawaameweka rekodi pacha ambapo alikuwa Mwanafunzi wa kwanza Mwanamke Tanganyika na pia Mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kusomea shahada sheria.

Mkuu wa kwanza wa Kitivo hicho cha Sheria alikuwa ni Profesa Arther Brain Weston. Chuo hicho kilikuwa mtaa wa Lumumba ambapo jengo la Chuo hicho lilitolewa na TANU na Chuo kilikuwa na "Academic staff" 6 tu akiwemo Mganda 1. Kutokana na uhaba wa majengo, Mwalimu JK NYERERE alimfanyia mpango Bi. JULIE na hivyo akawaanaishi Ikulu. Mkenya SAMUEL KIVUITU, aliyekuja kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Kenya, ndiye alikuwa Kiongozi wa wanafunzi hao. Kuanzishwa kwa Kitivo hicho cha Sheria ndio ilikuwa chachu ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1970, eneo la Mlimani.

Bi. JULIE alimaliza shahada ya sheria mwaka 1963 na kuweka rekodi pacha nyingine ya kuwa Mwanamke Mtanzania wa kwanza kupata shahada ya sheria na pia Mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kupata shahada hiyo chuoni hapo!. 
Kwa hakika, ni rekodi ya kujivunia sana!.

5. Kuwa Mwandishi wa Sheria:

Baada ya kumaliza masomo yake, Bi. JULIE aliajiriwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kama Mwandishi wa Sheria, hivyo akaweka rekodi ya kuwa Mwanamke wa kwanza Mtanzania msomi kufanya kazi hiyo.

6. Kufiwa na Baba yake:

Tarehe 28.4.1971, Bi.JULIE alifiwa na baba yake, Dr. WILLIAM MANNING, aliyekuwa akijivunia sana mafanikio hayo makubwa ya mwanae. Dr. WILLIAM, aliyefariki kutokana na ugonjwa wa asthma, alizikwa hukohuko Mbeya. Bi. JULIE aliendelea kuchapa kazi kwa bidii ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi marehemu baba yake aliyeamini kuwa kazi ni msingi wa maendeleo. 

7. Kuteuliwa Ujaji:

Mwaka 1973, Bi. JULIE MANNING aliweka rekodi nyingine pacha pale alipoteuliwa na Rais JK NYERERE kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Tanzania. Bi. JULIE akawa Mwanamke wa kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kuwa Jaji!. Uteuzi huu ulitikisa Afrika Mashariki nzima ambapo gazeti la tarehe  7.5.1973 liliipa habari hiyo kipaumbele kwenye ukurasa wa kwanza: "WOMAN MADE JUDGE!!!!".

8. Kuteuliwa Uwaziri:

Mwishoni mwa Octoba, 1975, Bi. JULIE aliitwa Ikulu na Rais JK NYERERE ambaye alimjulisha kwamba amemteua kuwa  Mbunge wa Taifa, kwa kutumia moja kati ya nafasi 10 alizonazo Rais chini ya Katiba.

Aidha, Jumapili ya tarehe 9.11.1975, Rais NYERERE alimteua Bi. JULIE kuwa Waziri wa Sheria. Bi. JULIE na Bi. TABITHA IJUMBA MWAMBENJA SIWALE, ambaye katika Baraza hilo jipya la Mawaziri aliteuliwa kuwa Waziri pia, ndio wanawake wa kwanza kuwa Mawaziri kamili nchini. Hii ni kwasababu katikati ya miaka ya 1960s, Bi. TITI MOHAMED aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni na Bi. LUCY LAMECK kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Afya. Kabla ya uteuzi huo wa Bi. JULIE, hakukuwa na Waziri wa Sheria. Kwa hakika ilikuwa ni heshima kubwa sana kuamini wa na Baba wa Taifa na kupewa wadhifa mkubwa kama huo. 

Tarehe 21.12.1975, Bi. JULIE 'alilimwa' barua na Mh. ABRAHMAN BABU. Mh. BABU alikuwa amewekwa kizuizini gereza la Ukonga ambapo yeye na wenzake pamoja na waliokuwa wakishikiliwa Zanzibar, walidaiwa kuwa walihusika na mauaji ya marehemu Rais ABEID AMAN KARUME yaliyotokea tarehe 7.4.1972.

Mh. BABU aliandika barua hiyo baada ya tahariri ya gazeti la Daily News la tarehe 18.11.1975 kueleza: "Maharamia wateswe ili wakiri makosa yao! . 

Ndipo BABU akaandika:
" Mwandishi wa tahariri haelewi kuwa ikiwa leo tutakubali maharamia wateswe, kesho itakuwa zamu ya wahariri kuteswa. Rais NYERERE anakasirishwa sana na utesaji na umwagaji damu. Sasa akifa akaja kurithiwa na mtu mwenye maadili ya Pakashume, ikiwa Mrithi huyo atarithi taasisi zilizopotoka kimaadili basi maadili yote ya kisiasa na kijamii yatakuwa ya  kipakashume, ikiwa atarithi taasisi zilizopotoka kimaadili. Kwavile sasa Wizara ya Sheria imepata Waziri, tuna imani haki itatendeka..".  

Hizi zilikuwa changamoto za mwanzo alizokumbana nazo Mh. Waziri JULIE MANNING ambazo zilimsaidia kumkomaza haraka. 

Bi. JULIE alikuwa Waziri wa Sheria hadi 1983. 

9. Kuteuliwa Kamishna wa Tume ya Uchaguzi

Bi.JULIE aliweka rekodi nyingine pale alipoteuliwa kuwa miongoni mwa Makamishina 7 wa kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo alikuwa Mwanamke pekee. Makamishina wengine walikuwa ni Mh. LEWIS MAKAME, MARK BOMANI, AUGUSTINO RAMADHANI, SOLOMON LIANI, BEN LOBULU na MASAUNI YUSUPH MASAUNI.

Tume hii iliundwa na Mh. Rais kwa mujibu wa Kifungu cha 74 cha Katiba ya Tanzania, 1977. 

10. Kuteuliwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini:

Bi. JULIE aliteuliwa kuwa mmoja wa makamishina wa Tume ya Kurekebisha sheria nchini, kazi ambayo amelifanya kwa miaka mingi.

11. Mjumbe wa Taasisi ya Dini

Bi. JULIE, si tu kwamba amebobea kwenye mambo ya siasa tu bali pia mambo ya dini na ni Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya "Young Women Christian Association of Tanzania".

12. Kupewa Medali na Rais JM KIKWETE:

Ijumaa ya tarehe 9.12.2011, kulifanyika hafla kubwa ya kukata na shoka ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru. Moja ya matukio makubwa siku hiyo ilikuwa ni utunuku wa Tuzo na Medali kwa Watanzania waliotoa mchango mkubwa katika Taifa hili kwa utumishi wao uliotukuka. Bi. JULIE  alikuwa mmoja wa waliotunukiwa medali ya aina yake siku hiyo na Rais wa awamu ya nne, Mh. Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE!.

13. Kupewa Tuzo na Rais KIKWETE ya kuwa Mwanamke wa kwanza kusomea sheria:   

Tarehe 25.10.2011, Kitivo cha Sheria, Udsm, kiliandaa kumbukizi ya miaka 50 ya kuanzisha kwa Kitivo hicho: "Golden Jubilee Celebrations of the Faculty of Law:-25th October 1961-25th October 2011.

Kumbukizi hilo lilikuwa la aina yake ambapo wanafunzi wote waliosoma Kitivo hicho toka kinaanzishwa walialikwa. Aidha, zilitolewa tuzo mbalimbali. Majina ya Wanafunzi wote Bora wa Kitivo hicho toka kinasnzishwa tarehe 25.10.1961 (First Class Honours Degree Holders) ambao walipata GPA ya 4.4-5.0 yalitangazwa, miongoni mwao ni:

1. Mutula Kilonzo (Kenya)
2. Hassan Boubacar Jallow (Gambia)
3. Dr. Ringo Tenga (TZ)
4. Dr. Masumbuko Lamwai (TZ) 
5. Dr. Asha Rose Migiro (TZ)
6. Eric Ng'imaryo (TZ)
7. Prof. Palamagamba Kabudi (TZ)
8. Prof. Hamudi Majamba (TZ)
9. Steven Mosha (TZ & Uganda).

Aidha, Prof. PALAMAGAMBA AIDAN MWALUKO KABUDI alipewa Tuzo maalum ya kipekee kwani GPA yake ya 4.9 ndiyo bora kuliko zote toka Kitivo hicho kianzishwe. Pia, ilibainika kuwa licha ya Kitivo hicho kuwa kikongwe kuliko vyote chuoni hapo, lakini ni wanafunzi wachache mno waliopata "First Class" na wanafunzi wa mwisho waliipata mwaka 1992!. Hii ni tofauti na vitivo vingine ambako "First Class" ni za  kumwaga!.

Siku hiyo ya kipekee ya utoaji zawadi, Bi. JULIE  alitunukiwa na Dr. GHALIB BILAL Tuzo ya kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kupata shahada ya sheria katika Kitivo cha Sheria hapa nchini! 

Huyu ndiye Bi. JULIE CATHERINE WILLIAM MANNING, Mwanamke mwenye rekodi nyingi na historia ya kipekee aliyetunukiwa medali kutokana na utumishi uliotukuka kwa nchi yake.      

WAZIRI LUKUVI ATOA HATI MILIKI ZA KIMILA KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA MAPOGOLO

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa hati kwa mmoja ya mwananchi wa kijiji cha Mapogolo wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mapogolo waliohudhulia mkutano wa kutoa hati miliki.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA

ZAIDI ya Kaya 200 za wafugaji wa kabila la Wamasai na Wamang’ati wamemilikishwa ardhi katika kijiji cha Mapogolo wilayani Iringa, hatua iliyoelezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwamba “itamaliza migogoro ya wakulima na wafugaji na kukuza utanzania.”

Kaya hizo zilikabidhiwa hatimiliki za ardhi za kimila juzi katika hafla iliyohusisha ugawaji wa jumla ya hati 2,404 za mashamba kwa wananchi wa kijiji hicho kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Hati hizo zimetolewa kupitia mradi wa Urasimajishaji Ardhi Vijijini (LTA) unaotekelezwa kupitia mpango wa Kupunguza Njaa na Utapiamlo (Feed The Future) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

“Leo tumeshuhudia makabila mbalimbali, wakiwemo ndugu zetu wamasai na wamang’ati wakipata ardhi katika ardhi ya wahehe. Hii ndio Tanzania, haina ubaguzi, mtu yoyote ana uwezo wa kufanya shughuli yoyote ya kimaendeleo mahali popote ili mradi havunji sheria,” alisema.

Alisema watanzania hawatarajii tena kusikia ugomvi baina ya wakulima na wafugaji katika kijiji hicho kwani mradi huo umeyawezesha makundi hayo kumiliki ardhi watakayoitumia kwa maendeleo yao endelevu katika jamii.

Mmoja wa wafugaji wa kabila la wamasai aliyemilikishwa ardhi katika kijiji hicho, Liwau Shang’ali aliwashukuru wenyeji wa kijiji hicho kwa kuikaribisha familia yake kijijini hapo akisema; “kama isingekuwa hivyo nisingewe kupata na kumiliki kisheria zaidi ya ekari saba za ardhi.”

Baada ya kupata shamba hilo, alisema hatarajii kuepeleka mifugo yake kwenye mashamba ya watu wengine kwa kuwa shamba alilonalo linaweza kukidhi mahitaji ya mifugo yake kama ataliendeleza na kufuga kisasa baada ya kupata elimu.

Pamoja na kupata kipande hicho cha ardhi aliishukuru serikali ya kijiji kwa kupitia mradi huo kutenga eneo kubwa la malisho kwa ajili ya wafugaji akisema uamuzi huo unaongeza usalama wa mifugo yao, utalinda mashamba ya wakulima na hatimaye kukuza amani na ushirikiano miongoni mwao.

Awali Mkurugenzi wa LTA, Tressan Sulivan alisema mpango wa matumizi bora ya ardhi na upimaji ardhi una manufaa makubwa katika kupunguza umasikini na njaa katika jamii hasa za vijijini.

Alisema wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wanawake na wanaume wana haki ya kupata, kutumia, kumiliki na kugawa ardhi ili mradi wafuate sheria na taratibu zilizowekwa.

Sullivan alisema kwa kupitia mradi huo uelewa wa haki za wanawake na jamii katika kumiliki ardhi umeongezeka na umesaidia kuwahamasisha kutumia nafasi waliyopewa kuomba ardhi ambayo ni rasilimali muhimu katika kukuza kipato chao.

Katika kijiji hicho alisema mradi uliwezesha uandaaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi na kukarabati masijala ya ardhi na kutoa mafunzo juu ya haki za ardhi na matumizi ya rasilimali ardhi kiuzalishaji ili kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Alisema waliopata hatimiliki za kimila wanaweza pia kuzitumia kama dhamana mahakamani na katika taasisi za fedha kupata mikopo itakayowawezesha kushughulikia changamoto walizonazo.

Alisema jumla ya vijiji 36 kati ya vijiji 133 vya wilaya hiyo vimenufaika na mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2015 na ambao utakamilika mwakani, 2019.

Mmoja wa wanawake walionufaika na mpango huo, Sakina Mlelwa alisema wanafurahi kuona mila na desturi zilizokuwa zikiwanyima haki ya kumiliki ardhi katika jamii zao zinapoteza nguvu zake mbele ya sheria mbalimbali za ardhi. 

“Tumeelimishwa jinsi sheria hizo zinavyoondoa tofauti za umiliki wa ardhi baina ya mwanamke na mwanaume, jamii inajua na imeanza kuuona umuhimu wa mwanamke kutobaguliwa katika umiliki wa ardhi,” Mlelwa alisema.

Alisema tatumia kipande chake cha ardhi chenye ukubwa wa heka tatu kutafuta mikopo atakayoitumia kuwekeza katika shughuli za kilimo na ufugaji.

WANANCHI VISIWANI ZANZIBAR WACHANGAMKIA HUDUMA KWENYE BANDA LA MAONYESHO LA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0

Wananchi wa Tanzania Zanzibar wameendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma za Usajili Vitambulisho vya Taifa zinazotolewa na NIDA wakati wa maonyesho yanayoendelea sambamba na maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar. Pamoja na huduma za Usajili, huduma nyingine zinazoendelea kutolewa kwenye banda hilo ni uchukuaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa waliokamilisha taratibu za Usajili na uhakiki, elimu kuhusu Vitambulisho vya Taifa na  matumizi mapana ya Vitambulisho hivyo katika huduma mbalimbali nchini. 

Sherehe hizo ambazo huambatana na Maonyesho ya Biashara ya kimataifa ambayo yanafanyika katika viwanja vya Maisara vilivyopo mjini Unguja, hufanyika kila mwaka ifikapo Januari. Maonyesho hayo ambayo yameanza tarehe 2/01/2019 yameendelea kuwavutia wananchi wengi kufika katika banda la NIDA; ambapo zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa limeonekana kuwagusa wananchi wananchi wengi wakiwemo wale ambao hawakujisajili. 

Wakizungumza baada ya kupata huduma kwenye banda hilo, wananchi wengi wameisifu NIDA  kwa kuwasogezea huduma pamoja na kufanya kazi mpaka muda wa usiku na kutoa fursa kwa wananchi wengi kushiriki na kuweza kunufaika na huduma hiyo.Mamlaka inaendelea kuwakaribisha wananchi wote wanaoishi visiwani Zanzibar kuendelea kufika katika banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ili kuweza kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali za Usajili na Utambuzi zinazotolewa na Mamlaka. Huduma hizo hutolewa kuanzia mida ya saa 4 asubuhi hadi saa 4 usiku kila siku wakati wa maonyesho. 
Afisa Usajili NIDA Salma Shaban Abdallah, akiwapatia maelezo baadhi ya wageni wakazi wanaoishi Visiwani Zanzibar walipofika kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na NIDA katika banda la Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Maisara mjini Unguja.
 Baadhi ya wananchi visiwani Zanzibar wakiwa katika banda la NIDA wakati wa siku ya maadhimisho ya Mapinduzi wakijionea na kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NIDA katika banda hilo. Zoezi hilo limefanyika wakati wa Maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Maisara.
 Afisa usajili NIDA Salma Shaban Abdallah, akijaza taarifa za mmoja wa wananchi wakati wa kukamilisha zoezi la kumpatia Kitambulisho cha Taifa mwananchi huyo aliyefika katika banda la NIDA kuchukua kitambulisho chake cha Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Maisara visiwani Zanzibar.
Afisa Habari NIDA Zanzibar, Bw. Said S. Said akiwafafanulia jambo  wananchi waliofika kutembelea banda la maonyesho la NIDA wakati maonyesho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisara Zanzibar.

INTRODUCING "NAJIDAI" OFFICIAL VIDEO BY TID Ft. Q CHILLAH


Introducing "Ololufe" official video by OneSix

BODI YA MISHAHARA YATAKIWA KUTOFANYA KAZI KIMAZOEA KATIKA KUTEKELEZA JUKUMU LAKE

$
0
0
Watumishi na wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wametakiwa kutofanya kazi kimazoea katika kutekeleza jukumu lake la msingi la kuishauri Serikali namna bora ya kuoanisha na kuwianisha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuwavutia na kuwabakiza watumishi katika Utumishi wa Umma ili waweze kuwahudumia vizuri wananchi katika Taasisi za Umma.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya Mishara na Masilahi katika Utumishi wa Umma  makao makuu ya bodi hiyo, wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu majukumu ya bodi na kujiridhisha namna bodi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, yeye ni muumini wa ufuatiliaji hivyo atakuwa akifanya ziara za kushtukiza katika ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kujiridhisha na utendaji kazi wa bodi hiyo, hivyo amewataka watumishi hao kubadilika na kuachana na utendaji kazi wa kimazoea ili bodi hiyo iwe na tija na manufaa kwa watumishi wa umma nchini.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, pamoja na kuwataka watumishi na wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa uzalendo, uaminifu na uadilifu lakini pia amewataka kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kuisadia Serikali ya Awamu ya Tano kutimiza azma yake ya utoaji motisha kwa watumishi wa umma ili waweze kuwa na ari ya utendaji kazi. 
Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewataka wajumbe wa bodi ambao ni wastaafu na wazoefu katika utumishi wa umma, kila mmoja kwa nafasi yake kutoa mchango utakaowezesha bodi kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa wakati, na kuongeza kuwa, yeye binafsi anaamini kwa uzoefu wa wajumbe wanaounda bodi hiyo, Serikali itapata ushauri bora wa kuoanisha na kuwianisha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma nchini.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Mariam G. Mwanilwa amesema kuwa, lengo la kuanzishwa kwa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ni kuwa na chombo kimoja cha kuoanisha na kuwianisha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma ili kuwa na mfumo endelevu unaoondoa malalamiko kuhusu masilahi miongoni mwa watumishi wa umma kwa lengo la kuwavutia na kuwabakiza watumishi katika Utumishi wa Umma.
Bibi Mwanilwa ameeleza kuwa, hivi sasa bodi inafanya utafiti wa hali ya masilahi na uhusiano wake na mifumo ya upimaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma na kuongeza kuwa, utafiti huo unafanywa ili kubaini uhusiano uliopo kati ya utoaji wa motisha mbalimbali na utendaji wa kazi kwa lengo la kuwavutia na kuwabakisha watumishi wa Umma. 
Bibi Mwanilwa amefafanua kuwa, kwasasa hatua inayoendelea katika utafiti huo ni uchambuzi wa taarifa za utafiti huo, hivyo bodi inatarajia kuwasilisha taarifa hiyo serikalini ifikapo mwezi Februari, 2019.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald S.B. Ndagula amesema bodi yake inamtambua Dkt. Mwanjelwa kama mlezi, hivyo amemhakikishia kuwa, imepokea nasaha, ushauri na melekezo aliyoyatoa na ameahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo yote.
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 36 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na kuundwa kwa Hati ya Rais iliyotolewa kwenye Tangazo la Serikali Na. 162 la tarehe 3 Juni, 2011.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi na wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea  ofisini kwao makao makuu ya bodi jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Mariam G. Mwanilwa, akieleza  majukumu ya Bodi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi  na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald S.B. Ndagula akifafanua majukumu ya bodi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi  na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi na Wajumbe wa Bodi hiyo ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

BREAKING NEWZZZZZ: BOT YAHAMISHA BENKI M KUWA SEHEMU YA AZANIA BANK LIMITED

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Benki Kuu ya Tanzania imekamilisha Mchakato wa ufumbuzi na madeni ya iliyokuwa Benki M na kuyahamishia katika benki ya Azania Limited, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibesse amesema leo jijini Dar es salaam.

Dkt. Kibesse amesema kuwa Benki kuu ya Tanzania kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 59(4)cha sheria ya mabenki na Tasisi za fedha ya mwaka 2006 mchakato wa kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M umekamilika na madeni yakee kuchukuliwa na benki nyingine kama njia ya ufumbuzi wa matatizo.

"Hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(20)(h) cha sheria ya Mabenki na Tasisi za fedha ya mwaka 2006 ,benki kuu imeamua kuhamisha kwa mujibu wa sheria (aquisition by Operation of the law) mali na madeni yote ya bank M kwenda Azania Bank Limited "

Naibu Gavana huyo amesema kwa sasa Benki kuu, Azania Bank Limited na wadau wengine wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kukamilisha mchakato wa uhamishaji wa mali na Madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Limited.
Amesema wateja wenye amana na wadai wengine wa Bank M watataarifiwa tarehe ya kuanza kupata huduma za kibenki kupitia Azania Bank Limited.Wateja wenye mikopo wanatakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na Mikataba yao.

alimaliza kwa kusema kuwa Benki Kuu inawaakikishia kuwa Azania Bank Limited itakuwa na Mtaji na Ukwasi wa kutosha kuweza kuwahudumia wateja wake na wateja wapya kutoka Bank M baada ya kuchukua Mali na Madeni ya benki hiyo hivyo Azania Bank inatarajiwa kuwa na mtaji wa Bilioni 164.  
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ,Dk .Bernard Kibesse akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kuhamisha amana zote za Benki M na Madeni yake kwenda Benki ya Azania.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ,Dk .Bernard Kibesse akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kuhamisha amana zote za Benki M na Madeni yake kwenda Benki ya Azania.
 Mkurugenzi wa Benki ya Azania Katikati Mwenye Tai Nyekundu akiwa na wadau wengine wa Masuala ya Kibenki waliohudhuria Mkutano wa BOT na Waandishi wa Habari
 Mwandishi wa Habari Kutoka Gazeti la Nipashe, Beatrice Moses akiuliza Swali kwa Gavana juu ya Mchakato wa kuhamishwa kwa benki hiyo.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano huo ulikuwa ukitangaza maamuzi ya kuhamisha Benki Mkwenda Azania Bank.

RAIS WA GABON ALI BONGO SASA AREJEA NCHINI MWAKE

$
0
0
Na Ripota, BBC 

RAIS wa nchi ya Gabon Ali Bongo ameamua kurejea nchini kwake ikiwa ni moja tu tangu kufanyika kwa jaribi la kimapinduzi la kutaka kumuondoa madarakani.

Bongo mwenye umri wa miaka 59 amerejea nchini mwake akitoa nchini Morocco ambapo alikuwa amekwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu na amekaa nchini humo kwa miezi miwili.Hivyo amerejea nchini kwake baada ya jeshi kufanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya Serikali yake.Rais huyo akiwa kwenye mkutano mkuu wa kiuchumi nchini Saudi Arabia alipatwa na Kiharusi.

Taarifa kuhusu Rais Ali Bongo ambayo imetolewa leo Januari 15,2019 na Shirika la Habari la Uingereza(BBC) inaeleza kuwa kwa sasa yupo nchini kwake.Rais huyo baada ya kuwepo kwa utata kuhusu hali yake Desemba mwaka jana aliamua kutangaza kupatwa na kiharusi.

Kwa mujibu wa BBC ni kwamba wiki iliyopita, jeshi nchini humo lilizima jaribio la mapinduzi ya Serikali na kumkamata kiongozi wa kundi hilo na pia kuwaua wanajeshi wawili waliokuwa wamevamia kituo cha redio ya taifa.

Inaelezwa wanajeshi hao walisema walihisi hotuba ya Bw Bongo ya Mwaka ilidhihirisha kwamba kiongozi huyo alikuwa amepoteza uwezo wake wa kuliongoza taifa hilo.Mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu Julien Nkoghe Bekale alitangaza mabadiliko katika baraza la mawaziri.Katiba ya Gabon inasema mawaziri ni lazima wale kiapo mbele ya Rais.
RAIS wa nchi ya Gabon Ali Bongo

WABUNGE UINGEREZA WAJIANDAA KUPIGA KURA YA KUKUBALI AU KUKATAA MPANGO WA THERESA MAY KUJITOA UMOJA WA ULAYA

$
0
0
Na Ripota Wetu, BBC

IMEELEZWA Wabunge nchini Uingereza wanajitayarisha kupiga kura iwapo kuunga au kutounga mkono mpango wa Theresa May wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Kura hiyo inayotajwa kuwa ni Kura yenye umuhimu ambayo itafanyika baadaye leo Januari 15, 2019 wakati mjadala wa siku tano kuhusu Brexit ukikamilika na kwamba May amewataka wanasiasa kuunga mkono mpango wake au kuhatarisha "kuwavunja moyo raia wa Uingereza".

Kwa mujibu wa Shirika la Habari nchini Uingereza(BBC) ni kwamba wabunge wake mwenyewe wakitarajiwa kujiunga na wa vyama vya upinzani kupiga kura dhidi ya mpango huo.Hata hivyo inatarajiwa mpango huo hautofaulu.Pia wabunge watapata fursa ya kutoa mapendekezo ya marekebisho ambayo yanaweza kuunda upya mpango huo kabla ya kura kuanza 19:00 kwa saa ya GMT.

Inaelezwa kuwa Waziri Mkuu aliwahotubia wabunge wake Jumatatu jioni katika jitihada za mwisho kujaribu kupata uungwaji mkono kwa mpango wake unaojumuisha mpango wa kujitoa kwa misingi ya ambavyo Uingereza itajitoa kwenye Muungano wa Ulaya na tangazo la kisiasa kwa uhusiano wa siku zijazo.

Awali, katika Bunge la wawakilishi, alisema: "Hauko imara kabisa lakini wakati historia itakapoandikwa, watu watatazama uamuzi wa Bunge hili na watauliza, 'Je tuliwajibika kuhusu kura ya taifa hili kujitoa katika EU, tuliuchunga uchumi wetu, usalama na muungano au tuliwavunja moyo raia wa Uingereza?'"

Hata hivyo May alijaribu kuwashawishi wabunge kuhusu mpango wenye mbadala wenye mzozo wa kuepuka kurudishwa kwa ukaguzi wa mipakani kati ya Uingereza na Ireland. 
 
 

KUSOMA ZAIDI  BOFYA BBC Swahili
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live


Latest Images