Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

KOZI MPYA YA UCHAMBUZI YAKINIFU KUPITIA VIASHIRIA HATARISHI KATIKA MFUMO WA UTOAJI MIKOPO YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB), Patrick Mususa(kulia), akizungumza wakati wa kumkaribisha Meneja wa Usimamizi wa Taasisi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT), Nassor Omar,kuzindua Kozi mpya ya Uchambuzi yakinifu kupitia viashiria hatarishi katika Mfumo wa Utoaji Mikopo(The basics of Credit Risk Modelling) kwa Wakurugenzi Wakuu wa Mabaenki na Taasisi za Fedha,uliofanyika Dar es Salaam, jana.

CHUO KIKUU MZUMBE CHAANZISHA SAFARI YA MABADILIKO WEZESHI SEKTA YA AJIRA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka,akizungumza na Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe waliohudhuria warsha ya mabadiliko katika Sekta ya ajira kwa manufaa ya Jamii Afrika Mashariki (TESCEA) inayoendelea Morogoro.
Mwezeshaji wa warsha hiyo toka nchini Kenya Prof. Charles Kingsburry akifafanua kuhusu mradi huo kwa Waandishi wa Habari.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Taaluma) Prof. Ganka Nyamsogoro akiwasisitiza washiriki umuhimu wa warsha hiyo katika kubadili mbinu za ufundishaji.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika majadiliano.
Mratibu wa mradi wa TESCEA Dkt. Albogast Musabila akifafanua kuhusu mradi huo kwa Waandishi wa Habari.
Mwezeshaji toka Chuo Kikuu, Afrika Nazarene cha nchini Kenya Dkt. Kendi Muchungi akieleza umuhimu wa mpango huo na jinsi unavyoweza kunufaisha wasomi na Jamii zao.
Mratibu Msaidizi wa mradi wa TESCEA wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Jennifer Sesabo akitambulisha mpango wa mradi huo kwa Washiriki.
Washiriki wakifuatilia maelekezo yanayotolewa katika warsha hiyo inayoendelea Hoteli ya Morogoro.
Washiriki wa warsha ya TESCEA katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi. Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi wake mpya wa ‘TESCEA’ kimeendesha warsha ya kuwajengea uwezo wahadhiri katika mbinu bora za ufundishaji zinazosaidia wanafunzi kuweza kujiajirika pindi wanapohitimu masomo yao ya elimu ya juu .
 Akizungumza katika uzinduzi wa warsha hiyo inayoendelea katika hoteli ya Morogoro, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka amesema Chuo Kikuu Mzumbe ni mahiri katika kufundisha masomo ya biashara na menejimenti na sasa kinakwenda hatua ya mbele zaidi kwakuwaandaa wahitimu wa ndani na hata nchi nyingine kutengeneza ajira kabla ya kuhitimu masomo yao. 
Prof.Kusiluka ameeleza kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa waajiri dhidi ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini na kuonekana kutokuwa na ujuzi wa kutosha na umahiri katika fani walizosomea pindi wanapotaka kuajiriwa. Hivyo, Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo vikuu viwili kutoka Uganda (Uganda Martys na Gulu), pamoja na asasi za AFELT, LIWA, ASHOKA kutoka Kenya na INASP kutoka Uingereza, wameanza kwa kuwajengea wahadhiri ili kubadili mbinu za ufundishaji zitakazowawezesha wahitimu kuwa na maarifa, ubunifu na ujuzi zaidi kutambua na kutumia fursa zilizopo ili kutengeneza ajira au kuajiriwa. 
Kwa upande wake mwezeshaji wa warsha wa asasi ya umoja wa Vyuo vikuu vinavyofundisha mbinu zinazohitajika katika kuboresha ufundishaji Afrika Mashariki (AFELT) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Daystar cha Kenya Prof. Charles Kingsburry, amesema ni muhimu sasa kubadili mfumo wa ufundishaji unaowafanya wahitimu kujua vitu kulingana na elimu wanayofundishwa darasani pekee na kwa kutegemea mitandao ya intaneti na badala yake mbinu mpya za ufundishaji ziwajenge katika ubunifu ,maarifa,mbinu na stadi halisia zitakazowawezesha kujiajiri wao na kuweza kuajiri watu wengine. 
Hii ina lengo si tu la kuwafanya wahitimu kujua vitu tofauti bali kuwajenga kuwa watu tofauti wanaoleta mabadiliko chanya kwa jamii nzima na kujinufaisha wao na jamii zinawazunguka kupitia elimu waliyopata. Naye mwezeshaji mwingine toka Asasi ya AFELT na mhadhiri wa Chuo Kikuu, Afrika Nazarene cha nchini Kenya Dkt. Kendi Muchungi amesema wahitimu wa Vyuo Vikuu vyote vya Afrika Mashariki hawatofautiani na wamekuwa wakikosa uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa na hivyo kushindwa kuisaidia jamii katika suala la ajira kupitia elimu waliyopata,badala yake wamekuwa wakitegemea kuajiriwa. 
Hivyo ni imani yake kuwa mpango huo utaleta mabadiliko kwa wahadhiri wa vyuo vikuu katika ufundishaji na kunufaisha jamii nzima ya Afrika Mashariki kupitia wasomi wachache. Wakati huo huo mratibu wa Mradi wa ‘TESCEA’ kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,Dkt.Albogast Musabila amesema pamoja na lengo kuu la mpango wa mradi huo la kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri na kuajiri,Chuo Kikuu Mzumbe kwa ushirikiano na wadau wa Sekta ya ajira, wahadhiri na wanafunzi kimeanza mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kuandaa mapendekezo yatakayozingatiwa wakati wa kuboresha mitaala na kuanzisha mitaala mipya. 

TAG YAKIKABIDHI MIFUKO 500 YA SARUJI KWA RC ARUSHA

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)  limetoa mifuko 500 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari zenye uhaba wa madarasa licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Arusha.

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr. Barnabas Mtokambali  amekabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuziba pengo la upungufu wa madarasa,ambapo amesema kuwa kanisa hilo limeaona lishiriki katika maendeleo ya jamii kwa kusaidia ujenzi wa madarasa.

Alisema kuwa kanisa linatambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kutoa elimu kwa Watanzania hivyo wameamua kuungana na serikali kwa kutoa mifuko hiyo kama chachu ya maendeleo ya elimu katika mkoa wa Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kanisa la TAG limekua la kwanza katika kutoa msaada kwa serikali na kuwezesha ujenzi wa madarasa kwani ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa huku madarasa yakiwa machache.

Gambo alisema kuwa serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo wataendelea kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania.

“Taasisi za dini ni wadau wakubwa wa maendeleo ambao licha ya miradi ya kuhudumia wananchi bado wanaliombea taifa amani ambayo ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa” Alisema Gambo

Muumini wa Kanisahilo Danford Massawe alisema kuwa makanisa yanapaswa kuiga mfano wa kanisa la TAG katika kushirikiana na serikali katika masuala ya maendeleo ili kuharakisha maendeleo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dr.Barnabas Mtokambali akikabidhi mifuko 500 ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika halfa fupi iliyofanyika jana jijini  Arusha.Picha na Mahmoud Ahmed Arusha

WIZARA YAWAKUMBUSHA WADAU KUHUSU UMUHIMU WA KULINDA MFUMO WA FEDHA NCHINI, KUDHIBITI UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

WIZARA ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeandaa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya fedha nchini.

Lengo la warsha hiyo ni kuendelea kuwakumbusha wadau kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo wa fedha wa nchi yetu ili usitumiwe vibaya na wahalifu na watu wasio waaminifu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo kuhusu udhibiti wa utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Onesmo Makombe alisema tatizo la utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii.

Amesema ni kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili, uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidhaa bandia, ujambazi na uporaji

Aidha amebainisha madhara ya utakasishaji wa fedha haramu kuwa ni ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama. Madhara hayo pamoja na uhalifu kuendelea kushamiri kwa uhalifu na wahalifu kujiimarisha; wahalifu kuwa na nguvu kiuchumi.

Pia kuhatarisha utawala wa sheria na usalama kwani uhalifu unaposhamiri na makundi ya uhalifu yanapojiimarisha hupata nguvu na kujaribu kudhibiti vyombo vya au kushindana na vyombo vya dola; kuharibu ushindani wa kibiashara katika uchumi kutokana na wahalifu kuwa na mitaji inayotokana na fedha haramu.

Amefafanua madhara mengine ni wafanyabiashara halali hushindwa kuhimili ushindani; kushusha hadhi ya nchi kimataifa na kusababisha nchi kutonufaika na mfumo wa fedha wa kimataifa; kushusha imani ya wawekezaji na kusababisha uwekezaji kupungua.

"Na wawekezaji wapya kutotaka kuwekeza kutokana na kushamiri kwa uhalifu, wawekezaji huwa na hofu kuwa mitaji na mali zao havitakuwa salama; imani ya washirika wa maendeleo na jumuiya ya kimataifa hupungua na nchi huathirika kiuchumi; kushuka kwa hadhi ya taasisi za fedha na mfumo mzima wa fedha.

"Na nchi kushindwa kufikia malengo ya maendeleo kwani rasilimali huwa mikononi mwa wahalifu wachache badala ya kutumika kutekeleza ajenda pana ya maendeleo ya nchi," amesema Makombe.

Wakati huo huo Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu amewakumbusha washiriki wa warsha hiyo kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kutekeleza wajibu wao wa kisheria kwa uadilifu na uaminifu ili kusaidia katika kubaini wahalifu wanaoweza kutumia mfumo wa fedha wa nchi kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya kigaidi na kuhatarisha usalama wa nchi. 

Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka benki na taasisi zinazotoa huduma za kibenki na huduma ndogo ndogo za fedha.
Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini
Kamishna Msaidizi ,Huduma za Kompyuta Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Gilbert .R.Nyombi akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini alipokuwa akitoa mada juu ya kudhibiti fedha haramu.
Baaadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Mtaalamu kutoka FIU Kwa umakinimu.
Washiriki wakiwa katika Makundi kujadili mada zilizowashirishwa na wao kuchangia katika suala zima la utakatishaji fedha kutumia taasisi za kifedha. 
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe 
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe.

BANKA KUANZA KUVAA UZI WA YANGA FEBRUARI 8 MWAKA HUU.

$
0
0
Na Ripota wetu, blogu ya Jamii 

Uongozi wa klabu ya Yanga umebainisha Kiungo Mohammed Issa 'Banka' aliyekuwa akikipiga kandanda Mtibwa Sugar amebakisha wiki tatu amalize adhabu yake ya miezi 14 aliyofungiwa na FIFA kutokana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku za kuongeza nguvu akiwa mchezoni. 

Banka aliyesajiriwa na Klabu ya Yanga msimu huu 2018 -19 ambaye pia hajaitumikia hata mara moja timu hiyo kutokana na sakata hilo, ataanza rasmi kuvaa uzi wa Yanga February 08 2019 adhabu yake itakapokuwa imemalizika.

Uongozi huo unasema kuwa Mchezaji banka tangu mwezi uliopita aliruhusiwa kujifua na kikosi cha Yanga kujiweka sawa kabla adhabu yake haijamalizika na kurejea dimbani.Hata hivyo Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameeleza kuvutiwa na kiungo huyo akimsifu kuwa ni aina ya wachezaji anaopenda kufanya kazi nao.

Baada ya kocha huyo kufanya nae mazoezi kwa Muda mfupi amesema kuwa amebaini kiungo huyo atakuwa msaada mkubwa kwa kikosi cha Yanga ambacho sasa kimeweka dhamira ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

"Nimevutiwa sana na Banka ukimuona uwanjani mazoezini utagundua kwamba ni mchezaji ambaye licha ya kuwa nje kwa muda mrefu lakini alikuwa akizingatia nidhamu ya mwili, nilikuwa nahitaji sana mtu kama huyu katika timu yangu, " amesema Zahera

Vile vile kocha Zahera ameeleza kuwa katika mazoezi ya Yanga Banka ameonyesha uwezo mkubwa katika majukumu ya ukabaji, kuchezesha timu na hata kufunga vitu ambavyo vitaipa nguvu timu yake katika mzunguko wa pili.
Mchezaji Mohammed Issac Banka.

MABORESHO YA SERA YA MAENDELEO YA JINSIA KUKAMILIKA JUNI 2019

$
0
0
Maboresho ya Sera ya Maendeleo ya  Jinsia ya mwaka 2000 yanategemewa kukamilika ifikapo mwezi Juni mwaka 2019 ili kuwezesha hatua nyingine za ukamilishaji wa Sera hiyo na kuanza kutumika rasmi.

Hayo yamebainikia leo jijini Dodoma katika kikao kilichokutanisha wadau wa masuala ya jinsia kikosi kazi cha wadau wanaoshughulikia masuala  ya jinsia katika Wizara, Taasisi za Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.

Akifungua kikao hicho Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)  Bw. Patrick Golwike amesema kikao kazi hicho ni muhimu kwa kupeana mrejesho wa masuala mbalimbali yahusuyo jinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Ameongeza kuwa wadau wa nafasi ya muhimu na wajibu wa kutetea masuala ya kijinsia kwa kuunganisha nguvu kwa pamoja na Serikali na wananchi na kuwa suala  la usawa wa kijinsia  na uwezeshaji wanawake linawezekana endapo kutakuwepo na ushiriki wa pande zote husika.

Akielezea suala la marekebisho ya Sera ya Maendeleo ya Jinsia ya mwaka 200 Kaimu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa Serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikisha marekebisho hayo ili kuendana na mabadiliko katika jamii ambapo masuala mbalimbali yahusuyo jinsia yamekuwa yakijitokeza ikiwemo uwepo wa  kipaumbele kwa mahitaji ya wanawake katika mapambanao dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi ameeleza kuwa Mchakato wa maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Jinsia upo katika hatua ya mwisho ya kupata ushauri wa wadau ili kuanza kuipitia Sera hiyo na kuifanyia marekebisho kwa kushirikisha wadau wa masuala  ya jinsia.

Naye Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Jeshi la Mgereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila amesema Jeshi hilo linaendeleza jitihada za kuleta usawa wa kijinsia na imetekeleza maagizo ya kuanzishwa kwa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi hilo.

Ameongeza kuwa uazishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza unalenga kusaidia jeshi kuweka Mipango ya usawa wa jinsia, kupokea, kusikiliza, kufuatilia na kutoa uamuzi, ushauri, na mapendekezo kuhusu migogoro, malalamiko ya masuala ya kijinsia na changamoto zake.

Kamishna Tusekile amesisitiza kuwa Dawati la Jinsia katika Jeshi hilo linasimamia masuala yote ya kijinsia kwa kutoa elimu na ushauri kuhusu masuala hayo kwa wadau wa ndani na nje ya Jeshi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)  Bw.  Atupele Mwambene akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto amesema kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2018 jumla  ya Kamati za ulinzi kwa wanawake na watoto  3,605 zilianzishwa katika ngazi ya mikoa, wilaya, mitaa na vijijini na mpaka sasa jumla ya Kamati 10,988 zimeanzishwa nchi nzima.

Ameongeza kuwa Idadi ya Kamati zinazotakiwa kuanzishwa ni 21,500 na mpaka sasa ni asilimia 51 tu ya Kamati hizo ndio zimaenzishawa na kusema kuwa kuna changamoto kubwa katika uanzishwaji wa Kamati hizo katika ngazi ya Vijiji na Mitaa.

Bw. Mwambene amesema kuwa ili kuondoakana na changamaoto hizo Serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwezesha uanzishwaji wa Kamati hizo hasa katika ngazi za Vijiji na Mitaa na mpaka sasa mikoa yote imeanzisha Kamati katika ngazi hiyo.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)  Bw. Patrick Golwike akifungua kikao cha wadau wa masuala  ya kijinsia kilichofanyika jijini Dodoma kulia ni Mwakilishi wa Shirika la UN Women Bi Hoda Addou na kushoto ni Mkurugenzi wa  Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi (kushoto) akielezea juhudi za Wizara katika masuala ya jinsia na uwezeshaji wanawake wakati wa kikao kilichokutanisha wadau wa masuala ya kijinsia jijini Dodoma kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)  Bw. Patrick Golwike.
 Mwakilishi wa Shirika la UN Women Bi. Hoda Addou(kulia) akifafanua masuala  mbalimbali yanayofanywa na Shirika hilo kuhusu usawa wa kijinsia wakati wa Kikao kilichowakutanisha wadau wa masuala ya jinsia jijini Dodoma kushoto  ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)  Bw. Patrick Golwike.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia Jeshi la Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila (katikati) alielezea namna Dawati hilo linavyowasaidia wafungwa wanawake, familia za watumishi wa magereza na jamii iliyokaribu na magereza wakati wa Kikao kilichowakutanisha wadau wa masuala ya jinsia jijini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa masuala ya jinsia wakifuatilia mijadala na maoni yaliyokuwa yakitolewa na wajumbe katika kikao kilichowakutanisha wadau hao jijini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya kijinsia na uwezeshaji wanawake. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

WAZIRI MHAGAMA AKERWA NA SEKTA BINAFSI YA ULINZI KUONGOZA KWA MIGOGORO MAHALA PA KAZI

$
0
0
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, kuweka mpango Maalum wa kuhakikisha migogoro   katika sekta  binafsi ya Ulinzi haizalishwi tena kwa wingi kwani inasababisha kutumika vibaya kwa rasilimali muda kati ya mwajiri na Mfanyakazi hali inayopelekea kuchelewesha Maendeleo.    
         
Waziri Mhagama amebainisha sekta  nyingine zinazoongoza kuwa na migogoro mahala pa kazi   kuwa ni  Sekta  ya Ujenzi na Sekta  ya Elimu. Aidha, ameitaka Tume hiyo kufanya utafiti kwa sekta   zote zinazoongoza kwa migogoro ya kikazi ili kubaini chanzo cha migogoro hiyo na kuandaa Mkakati Maalum wa kuishughulikia.
Mhagama ameyasema hayo leo mjini Morogoro  tarehe 14 Januari,  2019, wakati wa kikao cha Baraza la  wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima.       
"Hii sekta  Binafsi ya Ulinzi kwa nini huko migogoro  haiishi? Nataka mpango wa kumaliza migogoro hiyo, shirikianane na Taasisi nyingine muweke mpango maalum utakao weza kutatua na kuhakikisha haizalishwi mogogoro  mingine" Alisisitiza Mhagama. 
Mhagama alifafanua kuwa Serikali ya Awam  ya Tano  inayoogozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiriakwa vitendo vya kupiga vita uzembe, ubadhirifu na vitendo vyote  Vya rushwa mahala  pa kazi.   
  "Nisisitize kazi ya Usuluhishi na Uamuzi ni  kazi ya heshima na pia ni  kazi ya wito. Hivyo wekeni mkazo kwenye suala la Usuluhishi ili kupunguza muda  na mlundikano wa  mashauri, pia bainisheni sekta  nyingine zenye migogoro  mikubwa. Elimu ni  vyema iendelee kutolewa kwa Wadau kuhusu Sheria za Ajira na mahusiano kazini." alieleza Mhagama. 
   
Awali akiongea katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Shanes Nungu alibainisha kuwa Tume hiyo itatekeleza maagizo hayo kwa kuboresha Mkakati Wa Mpango kazi Wa Tume ili kuwa na mpango mkakati kwenye mtazamo Wa kupunguza migogoro  na unaolenga kumaliza migogoro kwa nataka katika sekta  zinazoongoza kuwa na migogoro mahala  pa kazi.
 "Tumekuwa tunajitahidi kumaliza na kuipunguza migogoro ya kikazi, kwani tumefanikiwa kumaliza migogoro hiyo kwa asilimia 80 kwenye hatua ya Uamuzi na asilimia 77, kwenye hatua ya Usuluhishi" alieleza Nungu.        
              
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi  ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo  Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo kimefanyika kwa mujibu wa Agizo la Rais Na.1 la mwaka 1970. Baraza hilo   huiwezesha Tume kuboresha Huduma na masuala ya utatuzi Wa migogoro ya kikazi kwa njia ya Usuluhishi na Uamuzi.
 Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama  akiongea, wakati wa kikao cha Baraza la  wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hawapo pichani) kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro,  tarehe 14 Januari,  2019.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Shanes Nungu akiongea, wakati wa kikao cha Baraza la  wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro,  tarehe 14 Januari,  2019.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la  wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wakiwa katika kikao hicho kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro,  tarehe 14 Januari,  2019.
 Mmoja wa  wajumbe wa Baraza la  wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi akichangia hoja  katika kikao hicho kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro,  tarehe 14 Januari,  2019
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama  akiwa katikapicha ya pamoja na wajumbe wa  kikao cha Baraza la  wafanyakazi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na  waamuzi wa migogoro ya kikazi nchi nzima, mjini Morogoro,  tarehe 14 Januari,  2019.

CHUO CHA IFM WAONGEZA KOZI YA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA HIFADHI YA JAMII

$
0
0

Na Khadija Seif, Globu ya jamii
CHUO cha usimamizi wa fedha  nchini (IFM) kimeanzisha kozi ya shahada ya uzamili katika hifadhi ya jamii. Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea rasimu hiyo Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Emmanuel Mnzava amewapongeza  wawakilishi kutoka vyuo vishiriki Saba Muco, IFM, Ustawi wa Jamii, Tengeru, Udsm na kukiteua Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kuwa cha kwanza katika kuanzisha mtaala huo wa shahada ya Hifadhi ya Jamii chuoni hapo ikiwa ni shahada ya pili.

 Mnzava amefafanua kuwa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) kipo kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuboresha elimu na kuelekea uchumi wa viwanda chuo hicho kitaweza kuzalisha wafanyakazi watakaohitaji kulindwa hasa kwenye kipengele cha bima na mafao .

Amewaomba vyuo vishiriki kuchukua wakufunzi wabobezi watakaojiunga na mtaala huo ili kuleta wataalam wenye kuleta tija na maslahi kwenye nchi kwa ujumla ambapo mtaala umezingatia mahitaji na hivyo wasomi kupewa watapewa kipaumbele na ili kuongeza ujuzi zaidi .

"Changamoto zilikua ni nyingi katika utayarishaji wa mtaala huu lakini kamati iliweza kufanya kazi nzuri na Mia ambapo leo tumeweza kupata mawazo Bora katika kuelekea uchumi wa viwanda naamini tutaweza kuzalisha wataalam wengi wenye weledi na waliotukuka"alisema mnzava

Kwa upande wake Mkuu wa kitivo katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) Baghayo Saqware amesema Muungano huo wa vyuo vishiriki Saba umeunda mtaala ambao utaleta tija kwa wataalam hususani kwenye ngazi ya bima ,sera na kiutendaji.

Aidha, Saqware amesema mtaala huo utaweza kukidhi mahitaji ya soko hasa katika hifadhi za jamii na  kuleta tija na manufaa kwa kuwepo kwa wataalam wengi. "Napendekeza kwa upande wa (NACTE)kupitisha mtaala huo mapema ili mafunzo yaweze kuanza rasmi "alisema Saqware.

Muwakilishi kutoka chuo kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) Nassor Nassor amepongeza chuo cha usimamizi wa fedha( IFM) kwa kuuona mchango wa vyuo vishiriki katika kuwasilisha mawazo na maoni na hatimae kufanyia kazi ipasavyo na kuletwa rasmi kwa rasmu ya mtaala huo wa shahada ya uzamili katika hifadhi ya jamii.

"Naamin mapendekezo mengine yataweza kufanyiwa kazi ili kuleta chachu ya Maendeleo katika sekta ya hizo hasa kukuza taaluma nchini "alisema Nassor.
Makamu Mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) Dkt. Emmanuel Mnzava na Mkuu wa kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii cha chuo hicho Kidadi Mashawishi baada ya kupokea rasimu hiyo ya mtaala wa shahada ya uzamili katika hifadhi ya jamii jijini Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Emmanuel Mnzava akipokea rasmu ya mtaala mpya wa kozi ya shahada ya uzamili katika Hifadhi ya Jamii kutoka kwa mwakilishi wa vyuo vishiriki Saba leo jijini Dar es Salaam

WIZARA YAZINDUA USHIRIKIANO MAMLAKA KUU SEKTA YA SHERIA

$
0
0
Na Sheiba Bulu
Wizara ya katiba na Sheria imezindua ushirikiano wa Mamlaka Kuu za Sheria nchini zitakazokaa pamoja kubainisha uwezo na changamoto zinazoikabili sekta ya sheria nchini na kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa sekta hiyo na hivyo kutoa mchango stahiki kwa taifa.
Ushirikiano huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) na kuhudhuriwa na Jaji Mkuu Mhe. Prof Ibrahim Juma na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome.
Akizindua ushirikiano huo Prof Kabudi amewataka wajumbe wa ushirikiano huo kufahamu kuwa wajumbe wote kwa ujumla wao wanajenga nyumba moja na wautumie ushirikiano huo kama chachu na hivyo kuleta tija na ufanisi kwa sekta ya sheria nchini ili iweze kutoa mchango wa kweli kwa Taifa.
“Sekta hii ni moja, wote hapa mnajenga eneo moja, tumieni ushirikiano huu kama chachu ya kuleta tija na ufanisi kwa sekta hii na muwe huru kushauri na kuzungumza ili kuifanya sekta ya sheria ambayo ni sekta mtambuka kutoa mchango wa kweli kwa taifa hili,” alisema Prof. Kabudi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma ameipongeza Wizara kwa  kuanzisha ushirikiano huo hasa ikizingatiwa kuwa sekta ya sheria ndio mama wa sekta zote nchini kwani sekta zote zinatumia sheria kujiendesha.
Amesema Ushirikiano ulioanzishwa utawezesha kuwepo kwa mashauriano baina ya mamlaka za sheria ili pamoja na mambo mengine utawezesha kuwa na msimamo mmoja juu ya masuala mbalimbali na pia utawezesha kutumika kama njia ya haraka ya kutatua changamoto mbalimbali katika sekta na kwa nchi kwa ujumla.
“ nipongeze kwa kuzindua ushirikiano huu, ni kitu kizuri kitawezesha kufanyika kwa mashauriano kwa pamoja na kutoka na msimamo mmoja kama timu, ushirikiaano huu unaweza kutumika kama njia ya haraka ya kutatua jambo na hivyo kutoa ushauri wa haraka kwa sekta husika kwa taifa na hata kwa uongozi wa nchi,” alisema Prof. Juma.
Ushirikiano huo unaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Mwenyekiti na wajumbe wake ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Katiba na Sheria, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria- Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwandishi Mkuu wa Sheria, Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakili Mkuu wa Serikali na Kabidhi Wasii Mkuu.
 
 Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Shria Prof. Sifuni Mchome aliesimama akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria nchini uliozinduliwa na Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Prof. Palamagamba Kabudi jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza wakati akizundua ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni  Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa mamlaka za sheria nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi.
Wajumbe wa ushirikiano wa mamlaka kuu za sheria nchini katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma baada ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es salaam leo

MGALU ACHANGIA MIL. 43 KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII NA KIMAENDELEO PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu, amechangia shughuli za maendeleo katika wilaya mbalimbali mkoani hapo, iliyogharimu sh. milioni 43 kwa kipindi cha mwaka mmoja. Aidha amekabidhi vifaa vya ofisi vyenye thamani ya milioni 5, kwa ofisi za jumuiya ya UWT katika kata zote 133 kimkoa ili kurahisisha utendaji kazi na kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Akitolea ufafanuzi juu ya utekelezaji wa shughuli zake za kibunge wakati wa baraza la UWT mkoa, Subira alisema moja ya majukumu yake ni kuunga mkono juhudi za serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kushiriki shughuli za kijamii.  Alisema kati ya mambo alitoshiriki kuweka mkono wake ni pamoja na kujitolea mifuko ya saruji kwenye ujenzi mbalimbali katika sekta ya afya na elimu. 

Hata hivyo Subira alieleza, katika kutekeleza ilani kwenye sekta ya nishati alianzisha kampeni ya zima vibatari ,washa taa kwa kuchangia taa za solar akiambatana na uongozi wa UWT Mkoa wa Pwani . "Taa hizo nilizigawa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu hususan katika mashule kwa lengo la kuboresha elimu bora kwa wanafunzi na zahanati kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa huduma za kiafya ikiwemo wadi za kujifungulia, uboreshaji wa afya za mama wajawazito ,watoto na kurahisisha huduma za afya kwa makundi maalum". 

"Pia niliambatana na mrs. Barbara Wentworth wa Wentworth Foundation na kutembelea shule ya sekondari Mandela na kukabidhi vitaulo yaani PADS kwaajili ya wanafunzi wa kike;"alifafanua Subira.  Subira alibainisha, taulo hizo ni za mwaka mzima kwa kila msichana, kwa wasichana 500, huo ni msaada mkubwa na utasaidia kuboresha mahudhurio yao darasani ,amekabidhi maboksi ya vitabu na kuahidi kujenga maktaba. 

Mbunge huyo, ambae pia ni naibu waziri wa nishati alisema kwamba, licha ya majukumu hayo amefanya ziara wilaya mbalimbali kukagua miradi ya ujenzi wa nishati ya umeme na kuwasha umeme katika maeneo mbalimbali ya mkoa. Anaipongeza na kuishukuru  serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais dkt.John Magufuli kwa jitihada za kuondoa changamoto ya ukosefu wa umeme kwenye baadhi ya maeneo. 

KAMISHNA WA FIU AWAPA SOMO WATUMISHI WA TASISI ZA FEDHA

$
0
0
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeandaa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya fedha kwa lengo la kuendelea kuwakumbusha kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo wa fedha wa nchi yetu ili usitumiwe vibaya na wahalifu na watu wasio waaminifu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo juu ya udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema tatizo la utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili, uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidhaa bandia, ujambazi na uporaji n.k. 

Aidha aliainisha madhara ya utakasishaji wa fedha haramu kuwa ni ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama. Madhara hayo pamoja na uhalifu kuendelea kushamiri kwa uhalifu na wahalifu kujiimarisha; wahalifu kuwa na nguvu kiuchumi; kuhatarisha utawala wa sheria na usalama (threaten peace, stability and rule of law) kwani uhalifu unaposhamiri na makundi ya uhalifu yanapojiimarisha hupata nguvu na kujaribu kudhibiti vyombo vya au kushindana na vyombo vya dola; kuharibu ushindani (ruin competitiveness) wa kibiashara katika uchumi kutokana na wahalifu kuwa na mitaji inayotokana na fedha haramu, wafanyabiashara halali hushindwa kuhimili ushindani; kushusha hadhi ya nchi kimataifa (erosion of country’s integrity) na kusababisha nchi kutonufaika na mfumo wa fedha wa kimataifa; kushusha imani ya wawekezaji na kusababisha uwekezaji kupungua na wawekezaji wapya kutotaka kuwekeza kutokana na kushamiri kwa uhalifu, wawekezaji huwa na hofu kuwa mitaji na mali zao havitakuwa salama; imani ya washirika wa maendeleo na jumuiya ya kimataifa hupungua na nchi huathirika kiuchumi; kushuka kwa hadhi ya taasisi za fedha na mfumo mzima wa fedha; na nchi kushindwa kufikia malengo ya maendeleo kwani rasilimali huwa mikononi mwa wahalifu wachache badala ya kutumika kutekeleza ajenda pana ya maendeleo ya nchi.

Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu amewaasa na kuwakumbusha washiriki wa warsha hiyo kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kutekeleza wajibu wao wa kisheria kwa uadilifu na uaminifu ili kuendelea kusaidia katika kubaini wahalifu wanaoweza kutumia mfumo wa fedha wa nchi kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya kigaidi na kuhatarisha usalama wa nchi. 

Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka benki na taasisi zinazotoa huduma za kibenki na huduma ndogo ndogo za fedha. 
Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini.
Kamishna Msaidizi, Huduma za Kompyuta Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Gilbert .R.Nyombi akizungumza na Watumishi wa Taasisi Mbalimbali za kifedha nchini alipokuwa akitoa mada juu ya kudhibiti fedha haramu.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Mtaalamu kutoka FIU Bw. Girbert R. Nyombi.
Washiriki wakiwa katika Makundi kujadili mada zilizowashirishwa na wao kuchangia katika suala zima la utakatishaji fedha kutumia tasisi za kifedha.
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe 
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe

Ujumbe wa “Niache Nisome” kutawala katika “T-shirt” za wananfunzi Rukwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza Wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wananfunzi wa shule zote za serikali katika halmashauri za mkoa huo zinaandikwa ujumbe wa “Niache Nisome” kwa herufi kubwa mbele ya flana zao za shule ili kuufikisha ujumbe huo kwa wale wote wenye nia na dhamira ya kukwamisha masomo ya wanafunzi hao kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutapunguza idadi ya wanafunzi wa kike kupata mimba pamoja na kumaliza utoro kwani ujumbe huo utawalenga wazazi pamoja na vijana wenye tabia ya kuwanyemelea wanafunzi wa kike na kuwalaghai kwa kuwanunulia chipsi pamoja na kuwapakiza bure katika usafiri wa pikipiki maarufu kama Bodaboda ili waweze kuwapa mimba na hatimae kukatisha masomo yao.
“shule zote ziandikwe maneno “niache Nisome” Mkurugenzi kama kuna “T-shirt” imeandikwa maneno mengine zifutwe, ziandikwe “Niache Nisome” tena ziwe na herufi kubwa nzuri, ujumbe huu ufike mbali, ujumbe kwa watanzania, ujumbe wa watu wote wa mkoa wa Rukwa “Niacheni Nisome” Msitusumbue, vichipsi chipsi vile hakuna kwa Watoto wa kike, sijui bodaboda, utoro utoro, “Niacheni Nisome””, Alisema.
Aliyasema hayo alipotembelea katika shule ya sekondari Kate, iliyopo Kata ya Kate, Wilayani Nkasi na kupokea taarifa ya shule hiyo iliyoonyesha ufaulu mzuri kwa wananfunzi wa kidato cha sita na ufaulu mbovu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne jambo lililopelekea Mkuu wa Mkoa kushtushwa na hali hiyo ya wanafunzi kuwa katika shule moja na kuwa na ufaulu tofauti.
Halikadhalika alielezea kuwa kitendo cha wanafunzi wa kidato cha kwanza kushindwa kufika shuleni kwa wakati na kuwa watoro ni sababu mojawapo ya kupelekea kushindwa mitihani ya kidato cha pili kutokana na kuwakuta wanafunzi wenzao wakiwa wamekwishapiga hatua katika masomo na ukizingatia kuwa lugha ya kufundishia ni ya kigeni hivyo hupelekea mwanafunzi huyo kushindwa kuwa sawa na wanafunzi wenziwe na hatimae kukata tamaa, hali inayopelekea kushindwa kidato cha nne.
Kwa upande wake makamu mkuu wa shule ya sekondari Kate alisema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika shule hiyo, wa kiume ni 144 na wa kike ni 155 na kufanya jumla yao kuwa 299 huku walioripoti wa kiume wakiwa 27 na wa kike 19 na kufanya jumla yao kuwa 46 na hivyo wanafunzi 253 bado kuripoti shuleni hapo tangu shule kufunguliwa tarehe 7.1.2019.
Wiki ya Kwanza ya Ufunguzi wa Shule za Sekondari na mahudhurio ya Kidato cha Kwanza katika Shule za Sekondari alizozitembelea Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.

Shule
Waliopangiwa
Walioripoti
1.
Shule ya Sekondari Kate
299
46
2.
Shule ya Sekondari Chala
100
37
3.
Shule ya Sekondari Korongwe beach
50
17
4.
Shule ya Sekondari Kala
153
38
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kate. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (wa pili toka kushoto mstari wa nyuma) katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Kate waliovalia fulana zilizoandikwa "Niache Nisome" pamoja na viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya na Jimbo. 

JUMA THOMAS ZANGIRA: MTANZANIA WA KWANZA NCHINI KUSHTAKIWA KWA UJASUSI

$
0
0


Moja kati ya kesi kubwa za kihistoria nchini Tanzania ni ile kesi ya UJASUSI (ESPIONAGE) iliyomhusu Bw. JUMA THOMAS ZANGIRA ambayo ilirindima nchini mwaka 1977. Hii ilikuwa ni kesi ya aina yake iliyowaacha wananchi wakiwa hawaamini maskio yao kwani hii ilikuwa ni kesi ya kwanza ya ujasusi nchini.

Siku ya Jumapili, tarehe 25.9.1977, Radio Tanzania Dar Es Salaam, katika taarifa yake ya habari saa mbili usiku, ilieleza kwamba Bw ZANGIRA atapelekwa mahakamani kesho yake, jumatatu. Hata hivyo, RTD haikutaja atapelekwa mahakama ipi. Kwavile wananchi walizoea kwamba washtakiwa wa makosa ya jinai hupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jumatatu asubuhi watu wengi walijazana mahakamani hapo kujionea wenyewe  Mshtakiwa ZANGIRA yukoje na kusikiliza alifanya vipi ujasusi huo.

Hata hivyo, wananchi hao waliula wa chuya kwani kisheria Ujasusi ni kosa kubwa ambalo ni lazma lisikilizwe na Mahakama Kuu na lazma wawepo Wazee wa Baraza  kumsaidia Jaji kama yalivyo makosa mengine makubwa kama vile mauaji au uhaini . Ni kwasababu hiyo basi, Bw. ZANGIRA, jumatatu ya tarehe 26.9.1977 alifikishwa Mahakama Kuu, na si Kisutu, toka gereza la Ukonga akiwa amefungwa pingu chini ya ulinzi mkali.

Kutokana na upekee wa kesi hii, ilibidi Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) aiendeshe mwenyewe badala ya Mawakili wa Selikali walio chini yake. Aidha, kutokana na ukweli kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya aina yake, ikabidi isikilizwe na Jaji Mkuu, Mh. FRANCIS NYALALI mwenyewe. Mh. NYALALI alisaidiwa na wazee wa Baraza ambao ni  Bw. ZUBEIR ALLY, Bw. HUSSEIN ZAMANI na Bw. SIMBA SALUM. Kesi hiyo iliendeshwa kwa kasi ambapo ndani ya siku 10 tu hukumu ikatolewa.

Siku hiyo ya kwanza saa 3 asubuhi, DPP MEELA alimsomea Bw. ZANGIRA mashtaka 3: 

Shtaka la 1 lilikuwa ni kukusanya habari kisha kuzitoa kwa mzungu aishie Uingereza aitwaye JOHN WILSON kwa nia ya kuvuruga usalama wa nchi yetu na kwamba taarifa hizo zingeweza kutumiwa na mataifa ya nje yanayoichukia Tanzania kuvuruga usalama wa nchi. Kosa la 2 ni kumpatia Bw JOHN WILSON habari ambazo zingeharibu jitihada za TANU na vyama vya ukombozi vya SWAPO, FRELIMO, PAC, ANC na ZANU na kosa la 3 ni kutoa taarifa za OAU kwa JOHN WILSON. Mashtaka haya yote matatu yalidaiwa ni kinyume na Kifungu cha 9(1)(a) na 9(2)(1) vya Sheria ya Usalama wa Taifa, 1970. 

Mshtakiwa ZANGIRA, aliyekuwa akitetewa na wakili THOMAS MKUDE wa lililokuwa Shirika la Sheria Nchini (TLC), alikana mashtaka yote hayo 3 ambayo ilidaiwa  aliyatenda kati ya mwaka 1971 na Julai 1977. 

DPP, ambaye aliileza Mahakama kwamba Bw. ZANGIRA ni Afisa Uhusiano wa hoteli ya Kilimanjaro aliyekuwa pia Afisa Usalama wa Taifa,  aliita mashahidi 8. 

Shahidi wa kwanza alikuwa ni SASP ALI JUMA GUGURU. Kwa ujumla, maelezo ya mashahidi hao 8 yalikuwa ni kwamba tarehe 27.7.1977, Bw GUGURU alipokea habari za ujasusi na akamtuma Sajin ABDALLAH kuchunguza  nani anatumia sanduku la posta 3900 DSM. Sajin ABDALLAH akatumia mbinu za medani na kugundua kwamba anayelitumia si mwingine bali ni Bw. ZANGIRA hivyo wakaanza kumfwatilia nyendo zake kwa karibu . 

Siku tatu tu baadaye, yaani tarehe 29.7.1977, saa 2 asubuhi, Bw ZANGIRA aliondoka nyumbani kwake akawa anaenda "mdogomdogo" ofisini kwake kwa kupitia posta bila kujua kuwa alikuwa anafanyiwa "surveillance" kali ya nyendo zake!.

Bw. ZANGIRA alipofika posta akafungua sanduku lake la barua na kutoa barua moja aliyoikuta. Kufumba na kufumbua akanyakwa na polisi!

Bw. ZANGIRA alikiri kuwa barua hiyo ni yake na ilipofunguliwa ilikuwa na £ 150. Barua hiyo ilikuwa imeandikwa na JOHN WILSON wa PARKSIDE, DERRY HILLS, CALNE, WITS, UK ikimtaka Bw. ZANGIRA atafute na kumpa habari juu ya namna uhusiano kati ya China na Tanzania unavyoharibu uhusiano wa Tanzania na majirani. Pia ilimtaka aeleze kuhusu vyama vya ukombozi ambavyo makao yake makuu yako Dar Es Salaam. Aidha, ilimtaka kutotumia jina lake halali na kwamba atalipwa £ 150 kwa mwezi na akileta habari zaidi ataongezewa.

Nyumba ya Bw  ZANGIRA ilisachiwa na kisha ofisi yake nayo ilisachiwa ambapo zilipatikana barua 33. Barua zote hizo zilipokelewa mahakamani kama vithibiti.

Barua ya kwanza kuandikwa iliandikwa tarehe 29.11.1971 na ikafuatiwa na zingine tarehe 18.2.1972, 29.2.1972, 11.3.1972, 25.3.1972 na 12.4.1972. Barua hizo zilizungumzia mambo mbalimbali ya ujasusi huku zikionesha ZANGIRA alitumiwa £485.

Aidha, baadhi ya barua hizo zilitoa pongezi kwa Bw ZANGIRA kwa kazi nzuri anayofanya na zingine zilimlaumu baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu. Pia, Bw ZANGIRA alitakiwa kutoa taarifa kuhusu mambo ya OAU na ziliko kambi za wapigania uhuru hapa nchini na kuulizia iwapo Rais NYERERE alikuwa akipendwa na wapigiania uhuru na ni nani nchini angekuja kuchukua nafasi yake. 

Bw ZANGIRA alitakiwa pia kutoa taarifa kuhusu ofisi zote za ubalozi na maeneo zilipo na ni zipi zinawaunga mkono Wapigania uhuru. Barua hizo pia zilionesha alikuwa akipokea fedha mara kwa mara na aliwahi kumwandikia Bw. JOHN WILSON akimtaka ampe fedha za kujenga nyumba na kununulia gari kwani alikuwa amefanya kazi kubwa ya kupeleka taarifa hizo nyeti na alijibiwa kwamba apeleke "Account No." yake na avute subira. Mwisho, barua zilionesha alisafiri kwenda  Kenya (22.7.1974) na Chileke, Malawi(7.4.1976) ambako alitajiwa na JOHN WILSON hoteli za kufikia na watu wa kukutana nao.

Baada ya kesi hiyo kusikilizwa mfululizo kwa siku 4 na upande wa mashtaka kufunga kesi yao, Ijumaa, tarehe 30.9.1977 ikawa zamu ya Bw ZANGIRA kutoa utetezi wake.

Mh NYALALI alimueleza kwamba anayo haki ya kujitetea baada ya kula kiapo ambapo akimaliza kujitetea ataulizwa maswali  au anaweza kuchagua kutoa utetezi bila kuapa ambapo hataulizwa swali na Jaji NYALALI, DPP Meela wala Wazee wa Baraza.

Bw ZANGIRA alichagua kutoa utetezi bila kuapa, hivyo hakuulizwa maswali.

Katika utetezi wake, Bw ZANGIRA alikiri kuwa barua hizo zote ni zake na kwamba ni kweli alikuwa akimpelekea habari Bw JOHN WILSON ila alifanya hivyo kama mwandishi wa habari kwani habari hizo zilikuwa ni za kawaida tu na zilipatikana magazetini. Aidha, alidai kwamba habari alizokuwa akituma zilikuwa za mambo ya biashara tu.

Bw ZANGIRA alieleza zaidi kwamba zamani alikuwa akifanyakazi Subuzani Tours & Safaris, Arusha ambapo kazi yake ilikuwa kuwapeleka watalii mbugani. 

Alieleza kuwa mwanzoni mwa 1971 alifanya kazi ya kumpeleka mtalii mmoja aitwae WILTSHIRE mbuga ya Mikumi. Bw WILTSHIRE alimwambia kuwa ana rafiki yake yuko UK anatafuta mwandishi hivyo yeye akasema yuko tayari hivyo akampa Bw WILTSHIRE "Contacts" zake. Baada ya miezi michache ndipo alipoanza kupokea barua toka kwa JOHN WILSON.

Bw ZANGIRA alieleza kwamba alikuwa akilipwa kwa habari zote alizokuwa akizipeleka toka 1971 hadi 1977 na kwamba alipigwa bumbuwazi aliposhtukia anakamatwa asubuhi ya tarehe 29.7.1977 mara tu baada ya kuchukua barua kwenye sanduku lake la posta toka kwa JOHN WILSON.    

Baada ya ZANGIRA kutoa utetezi wake, Jaji NYALALI aliwaeleza kwa kifupi wazee wa Baraza mlolongo wote wa kesi hiyo ili waweze kutoa maoni yao. Baada ya hapo, Wazee hao wa Baraza walitoa maoni yao ambapo wawili (SIMBA SALUM na HUSSEIN HAMIS waliona mashtaka yamethibitishwa wakati Mzee ZUBERI ALLY aliona mashtaka hayakuthibitishwa).

Mh NYALALI akaahirisha kesi hiyo na kuahidi kutoa hukumu Jumatano ya tarehe 5.10.1977. Siku hiyo, tofauti na ilivyokuwa siku ya kwanza, umati mkubwa ulifurika Mahakamani hapo kuanzia saa moja asubuhi na ulinzi ulikuwa umeimarishwa vilivyo.

Mh. NYALALI aliisoma hukumu hiyo ambapo alimtia hatiani Bw ZANGIRA kwa makosa yote 3 aliyoshtakiwa nayo. Mh NYALALI alisema:

"JOHN WILSON alikuwa ni Jasusi aliyekuwa akitumiwa na mataifa fulani ili kuangamiza usalama wa Taifa letu. Utetezi wa Bw ZANGIRA kwamba alikuwa anamtumia WILSON habari za biashara hauna mashiko. Hizo habari hazikuwa za kumfaa Mfanyabiashara yeyote bali Haini SMITH na Kaburu VOSTER wa Afrika ya Kusini. Vilevile, kama ni habari za biashara ni  kwanini ZANGIRA atakiwe kutumia jina bandia?. Tanzania ni moja ya nchi zilizo mistari wa mbele Kusini mwa Afrika hivyo kitendo cha ZANGIRA kutoa siri za vyama hivyo na za OAU ni sawa na Uhaini".

Baada ya kutiwa hatiani, DPP MEELA aliiomba Mahakama imwadabishe Bw ZANGIRA kwa kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine hasa ukizingania umuhimu wa Tanzania katika ukombozi kusini mwa Afrika.   

Nae MKUDE, wakili wa ZANGIRA, aliiomba Mahakama imuhurumie mteja wake kwani hilo ni kosa lake la kwanza na anategemewa na nduguze.

Mh NYALALI, baada ya kusikiliza "Aggravating & Mitigating factors" hizo, alitafakari kwa kina kisha akamuhukumu Bw ZANGIRA kwenda jela miaka 20.

Huyo ndiye JUMA THOMAS ZANGIRA, Mtanzania wa kwanza kushtakiwa na kutiwa hatiani kwa ujasusi.

DKT. ZAINAB ATINGA OFISI KUU, WIZARA YA AFYA JIJINI DODOMA.

$
0
0
Na WAMJW - DODOMA

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainab Chaula leo amekutana na Wakurugenzi wa idara na Wakuu wa Vitengo wa wizara hiyo tangu alipoapishwa siku chache kushika nafasi hiyo, akitokea TAMISEMI.

Katika kikao hicho Dkt. Chaula amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi hiyo, huku akihimiza kila mmoja kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa weledi ili kulinda taaluma zao. "Tujiandae kufanya kazi kama timu moja katika kutekeleza sera na miongozo ya sekta ya afya na kuhakikisha dhamana tuliyopewa tunaitumikia kadri inavyowezekana".Alisisitiza Dkt.Chaula

Hata hivyo Dkt.Chaula alimshukuru Katibu Mkuu aliyeondoka Dkt.Mpoki Ulisubisya kwa mifumo mizuri aliyoiweka na kuahidi kuendeleza kwa kuanza na changamoto zilizopo.Aidha,aliwataka wakurugenzi hao kutimiza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa kujituma, huku akiwatoa hofu kuwa ofisi yake iko wazi muda wote na yeyote mwenye wazo zuri la kujenga asisite kumuona, kwani lengo ni kuboresha Sekta ya Afya

"uwezo wa kufanya kazi tunao hivyo.mabadiliko ni vitendo, tufanye kazi kwa matokeo". Alisema Dkt. Chaula .Wakati huo huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ametembelea ujenzi wa mji mpya wa Serikali Ihumwa na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akipokea nyaraka za makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ulisubisya Mpoki leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi baada ya Kikao cha kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula.
Kikao chaWakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya kikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakimpokea Katibu Mkuu mpya Dkt. Zainab Chaula leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akiteta jambo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma, katika kikao na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya, Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi, pamoja na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya baada ya kikao kifupi cha ukaribisho wa Dkt. Chaula.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, akiwaonesha namna ya ufuatiliaji ili kuboresha Ujenzi wa Mji mpya wa Serikali Ihumwa wakati alipotembelea ujenzi wa TAMISEMI ili kujifunza, Wakwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima, anaefuata ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi na Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula pindi walipokutana kwenye ziara ya kutembelea ujenzi wa Wizara ya Afya katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakwanza Kushoto) akibadilishana mawazo na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Watatu kulia) pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi
Ujenzi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ukiendelea kwa kasi katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.

UTARATIBU WA KUSAJILI DAY CARE.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.

Badala ya kuendesha shule za kulea watoto kinyemela huko mitaani, makala haya yatakueleza namna ambavyo unaweza kufanya kusajili  na hivyo ukaendesha shughuli hii kihalali.


Ifahamike kuwa ni  kosa la jinai kuendesha kituo au  shule ya kulea watoto  bila usajili. Kanuni ya 4( 1 ) ya Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka 2012,  zinasema kuwa mtu hataendesha kituo cha kulea watoto wadogo isipokuwa kama anamiliki cheti halali cha usajili. Kwahiyo epuka kuingia katika kosa hili kwa kusajili kituo chako.Makala yatakuwa yakitafsiri Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, pamoja na Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka 2012.


SIFA ZINAZOHITAJIKA KABLA YA KUOMBA USAJILI.


1.Eneo ambapo  kituo kitajengwa litatakiwa kukaguliwa na afisa afya wa eneo husika na kutoa ripoti ya kuridhisha kuwa panafaa kwa ajili ya kulelea watoto. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya  4(3).


2.  Kama eneo/jengo ambapo utaendeshea kituo ni la kupanga basi hakikisha una mkataba wa pango ambao hauko chini ya miaka mitatu.  Kanuni ya 4(4).

3. Utatakiwa kuthibitisha uwezo wa kifedha kuwa unaweza kuendesha kituo.

4. Hakikisha eneo lina vifaa vya kutosha kwa ajili ya michezo ya watoto. Hii ni kutoka kifungu cha 47(1)( c ).


5. Muombaji/waombaji wawe na akili timamu.


6. Uthibitisho kuwa baada ya kupewa cheti cha kuendesha kituo hautatoa, kuuza, kukodisha  kituo au cheti chako kwa mtu mwingine yeyote.

                   
KUSOMA  ZAIDI  

sheriayakub.blogspot.com



KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUOTESHA MITI YA MATUNDA JUU YA KABURI.

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga,Moshi 

Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utunzaji wa Mazingira lijulikanalo kama LEPAJE limezindua kampeni ya uoteshaji wa miti ya matunda juu Makaburi kwa lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya uharibifu wa mazngira nchini kwa kubadili wafu kuwa mti wa matunda.

Katika kampeni hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi huu katika kijiji cha Kifuni juu kata ya Kibosho Umbwe wilaya ya Moshi vijijini,mkoani Kilimanjaro,tayari miti ya matunda ya Parachichi imeoteshwa katika makaburi matano ya mfano huku makaburi zaidi ya 200 yakitaraji kuoteshwa kupitia kampeni hiyo.

Leonard Massawe ni mkurugenzi wa Shirika la Lepaje anasema katika kijiji hicho wamekubaliana kuotesha miti ya matunda ya muda mfupi na yanayopendwa na jamii ambayo yatakuwa tayari kuliwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Kwenye maeneo yetu haya ya baridi tumeamua kuotesha ,miti ya matunda ambayo yanastawi vizuri na ambayo yanapendwa zaidi na jamii yetu ya huku,tumeotesha Parachichi za kikonyo ,hata hivyo kampeni hii inahitaji kuungwa mkono na Serikali ,Wanahabari,viongozi wa Dini,taasisi za elimu na jamii kwa ujumla”alisema Massawe.

Amesema Makaburi matano ya mfano yaliyooteshwa miti ya matunda ni ya familia yake akiwemo mama yake mzazi na kaka zake wawili akieleza kuwa kampeni hiyo ni rahisi huku akisisitiza jamii kuinga mkono ili kufikia lengo.

“Kuishawisi jamii kuotesha miti ya matunda juu ya kaburi inahitaji ujasiri mkubwa ,mimi nimeotesha mti wa tunda la Parachichi kwenye kaburi la Mama yangu mzazi ili iwe mbegu ya utunzaji wa mazingira Duniani”alisema Masawe.Alisema muda umefika kwa jamii ya Wachaga kubadili mtazamo wa kuotesha majani yajulikanayo kama “Isale” na badala yake waoteshe miti ya matunda muda mfupi tu baada ya kumzika ndugu yao.

Alisema mwaka 2019 ni mwaka wa kubadili wafu kuwa Matunda katika mkoa wa Kilimanjaro huku akiitaka jamiii katika makaburi ya ndugu zao hata kama walizikwa miaka mingi iliyopita na kwamba hali hiyo itachangia kuboresha hali ya hewa kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Mmoja wa wananchi katika kijiji hicho Lucia John amesema uoteshaji wa miti a matunda katika kaburi pia utasaidia kuimarisha afya kwa jamii lakini pia utachangia uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa kuuza matunda na mengine yanaweza kusafirishwa nje ya nchi.

Hii ni kampeni ya 32 kwa shirika lisilo la kiserikali la kuhifadhi mazingira ambapo awali limefanya kampeni za kuotesha miti katika wilaya za mkoa wa Kilimanjaro kupitia mchezo wa riadha iliyojulikana kama Lepaje Marathon.




KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WADAU WA MAENDELEO WACHANGIA MIFUKO 500 YA SARUJI ARUSHA

$
0
0
Na Vero Ignatus Arusha
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)  limetoa mifuko 500 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari zenye uhaba wa madarasa licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Arusha.

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr.Barnabas Mtokambali  amekabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuziba pengo la upungufu wa madarasa,ambapo amesema kuwa kanisa hilo limeaona lishiriki katika maendeleo ya jamii kwa kusaidia ujenzi wa madarasa.
Alisema kuwa kanisa linatambua juhudi zinazofanywa na serikali katika kutoa elimu kwa Watanzania hivyo wameamua kuungana na serikali kwa kutoa mifuko hiyo kama chachu ya maendeleo ya elimu katika mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kanisa la TAG limekua la kwanza katika kutoa msaada kwa serikali na kuwezesha ujenzi wa madarasa kwani ufaulu umeongezeka kwa kiasi kikubwa huku madarasa yakiwa machache.
Gambo alisema kuwa serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo wataendelea kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania.
“Taasisi za dini ni wadau wakubwa wa maendeleo ambao licha ya miradi ya kuhudumia wananchi bado wanaliombea taifa amani ambayo ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa” Alisema Gambo
Muumini wa Kanisahilo Danford Massawe alisema kuwa makanisa yanapaswa kuiga mfano wa kanisa la TAG katika kushirikiana na serikali katika masuala ya maendeleo ili kuharakisha maendeleo.
1.Picha Wakwanza kushoto ni mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God nchini Tanzania Dkt. Barnabas Mtokambaki akimkabithi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mifuko 500 ya Saruji.

DC SAME AAGIZA MASHAMBA YENYE MIRUNGI ING'OLEWE,WANAKIJIJI WAKUBALI

$
0
0

Na Ripota Wetu,Blog ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro,Rosemary Staki Semanyule, ametoa maagizo kwa wanavijiji kuhakikisha mashamba matano ambayo yamebainika kuwa na mirungi katika Kijiji cha Rikweni ndani ya Kata ya Tae ing'olewe.

Ametoa maqizo hayo baada yankubainika kuwa na kuna mashamba ya mirungi walipokuwa kwenye ziara ya kamati ya Usalama na wataalamu iliyofanyika katika kijiji cha Rikweni Kata ya Tae. 

Akifafanua zaidi Mkuu wa Wilaya hiyo ya Same amesema lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua uchimbaji barabara lakini wakao a kuna kuona mashamba ya mirungi na kuamua kuenda kung'oa mirungi kwa msaragambo ambayo wenye mashamba hayo wamekuwa sugu na kuyaacha bila kung'oa. 

Hivyo ameagiza hadi Januari 11, 2019 mashamba matano yaliyobaki na mirungi yawe yameng'olewa ambapo pia amewataka viongozi wa vijiji kusimamia na kuwa wakishindwa kung'oa, basi wananchi watang'oa badala yao.

" Ili kujenga uzalendo wa kila mmoja kusimamia sheria. Kwani nao hawatoi taarifa kuhusu wahalifu.Tumepunguza mirungi toka vijiji 46 hadi 8 sasa. Navyo ni watu wachache, na tutahakikisha tunaimaliza kaabisa," amesema.

Ametoa mwito kuwa vijiji/vitongoji vya Tae, Belle, Mmeni, Irete, Kisesa, Makasa na Vudee kuondoa mirungi michache iliyobaki na kwamba hakuna watakaemuacha salama.

" Same isiyo na mirungi, inawezekana"
 Baadhi ya wanavijiji wakihakikisha mashamba matano ambayo yamebainika kuwa na mirungi katika Kijiji cha Rikweni ndani ya Kata ya Tae inang'olewe.
 Baadhi ya wanakijiji wakijadiliana jambo .

MAGAZETI YA LEO JUMANNEJANUARI 15,2019

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images