Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

MWIBA HOLDINGS YATOA GARI NA MAMILIONI KWA WMA KUENDELEZA UHIFADHI

$
0
0
Na  Ripota wetu,Meatu.

Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori (WMA) ya Makao,iliyopo wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,juzi imepatiwa msaada wa gari aina ya Toyota Land Crusser baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa utalii wna uwindaji na kampuni ya Mwiba Holdings limited.

Mkataba huo, ulisainiwa katika halmashauri ya Meatu, ambapo katika kipindi cha miaka mitano,Makao WMA itakuwa ikipata fedha wastani wa shilingi 600 milion kutoka sh 400 milioni za miaka mitano iliyopita.

Akizungumza katika makabidhiano ya gari hilo, lenye thamani ya sh 40 milioni, baada ya kusaini mkataba, Meneja wa Mwiba Holdings moja ya kamapuni ya Friedkin Conservation Fund, Mark Ghaui alisema wanatarajia ndani ya miaka mitano kuongeza watalii katika eneo hilo.

"tumetoa msaada huu wa gari, ili litumike katika doria za ulinzi wa wanyamapori na mazingira na tutaendelea kutoa misaada mingine ili kuhakikisha jamii pia inanufaika na uhifadhi"alisema kwa upande wake, Katibu wa Makao WMA, Robert Simon licha ya kushukuru msaada huo, pia alitangaza operesheni ya kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi.

Alisema wametoa mwezi mmoja kwa kaya zaidi ya 60 zilizovamia maeneo ya hifadhi ili kutoka na hivyo kuendelea kutunzwa kwa mazingira ya hifadhi hiyo.Alisema mkataba waliosaini, umeboreshwa kwani fedha za kila kijiji zimeongezeka kutoka wastani wa sh 25 milion hadi 27 milioni na kwa mwaka fedha zimeongezeka hadi kufikia 600 milioni.

Kaimu Mwenyekiti wa Makao WMA, Nzemo Gwesere alipongeza kampuni ya Mwiba kwa kusaini Mtakaba mpya na Makao WMA na kutoa gari kwa ajili ya ulinzi.

Alisema Makao WMA na serikali kwa ujumla katika miaka mitano ijayo itanufaika zaidi na uwekezaji wa kampuni hiyo kwani watalii wataongezeka.
Meneja wa kampuni ya Mwiba,Mark Ghaui (wapili kushoto) akiwa na meneja maendeleo ya jamii na Mahusiano ya Mwiba,Alfred Mwakivike (kushoto0 wakikabidhi funguo na kadi ya gari aina ya Landcrusser waliyotoa kwa hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Makao na viongozi wa jumuiya hiyoanayepokea ni Mwenyekiti ni Kaimu Mwenyekiti Nzemo Gwesere akiwa na Katibu wake Robert Simon .
Meneja wa kampuni ya Mwiba,Mark Ghaui (wapili kushoto)akiwa na meneja maendeleo ya jamii na Mahusiano ya Mwiba,Alfred Mwakibiki (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuwekeza shughuli za Utalii,katika hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Makao na viongozi wa jumuiya hiyo,Robert Simon Katibu na Kaimu Mwenyekiti Nzemo Gwesere jana


WAZIRI LUGOLA AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO WATANO SAKATA LA KUNASWA SARE ZA JESHI KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola
 
 
*Aagiza wachunguzwe, atoa maagizo mazito kwa Katibu Mkuu Mambo ya Ndani

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola amewasimamisha kazi vigogo watano wanaohusika na wakimbizi katika kambi ya Mtendele na Nduta mkoani Kigoma, baada ya kubainika uwepo wa sare za Jeshi zikiwa kwenye marobota ya nguo za misaada.

Akizungumza leo Januari 13,2019 , Waziri Lugola amesema kumebainika uwepo wa sare hizo kwenye marobota hayo ya nguo za misaada ambazo yalikuwa yanapelekwa katika kambi ya Wakimbizi Mtendeli na Kambi ya wakimbizi ya Nduta mkoani Kigoma.

Amefafanua katika kambi ya Mtendeli kumebainika kuwepo kwa sare za jeshi 1325 na katika kambi ya Nduta kumebainika uwepo wa sare 622 na hivyo kufanya jumla ya idadi ya sare zote kuwa 1947.

"Kwa Serikali hii inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli haiko tayari kuona tukio hilo linaachwa bila kuchukua hatua.Kama nguo hizo zimeweza kubainika maana yake kesho au kesho kutwa zinaweza kuingizwa silaha.Tulitarajia wahusika walitakiwa kubaini nguo hizo mapema kabla ya kuingia kwenye makambi hayo.

" Lazima tuhakikishe nchi yetu iko salama kwa kuhakikisha hakuna ambacho kinaingia nchini kwetu.Hivyo nimeamua kuchukua hatua za kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa kambi hizo za wakimbizi,"amesema Waziri Lugola wakati anazungumzia sare hizo.

Amewataja aliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Harson Mseke, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Wakimbizi upande wa Menejimenti ya Makambi na Makazi, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi anayeshughulikia Usalama na Operesheni.

Wengine ni Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Mtendeli John Mwita pamoja na Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nduta Peter Bulugu .Pia amesema Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani anatakiwa kumchukulia hatua Mratibu wa Wakimbizi Mkoa wa Kigoma Tony Laiza.

Akizungumzia zaidi tukio hilo la kubainika kwa sare hizo ,Lugola amesema tayari amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ndani ya siku mbili kuanzia kesho kuunda tume kuchunguza sare hizo na kisha baada ya siku 10 awe amempa taarifa ya uchunguzi na uwe umekamilika.

"Nimemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani kuunda timu maalum kuchunguza suala hili na ndani ya siku 10 awe amekamilisha ripoti na kunikabidhi,"amesema Lugola huku akifafanua uwepo wa sare hizo nchi ya Burundi inaweza kuwa na mawazo hasi kwa kudhani huenda Tanzania inawasaidia Wakimbizi kuunda jeshi jambo ambalo si kweli.

Waziri Lugola amefafanua kuwa siku za karibuni kulikuwa na mchakato wa kuwarudisha wakimbizi waliokubali kwa hiyari yao kurudi nchini Burundi na hivyo kubainika kwa sare hizo huweza kutafsiriwa kwamba walikuwa wanataka kuwapa sare hizo kwenda kufanya uasi.

" Lazima tuchukue hatua katika hili,nasubiri ripoti ya uchunguzi itakavyoeleza,"amesisitiza Waziri Lugola huku akiwataka WaTanzania kutoa taarifa zozote ambazo zitasaidia kuifanya nchi yetu kuwa salama .

Na kwamba hata kama kuna misaada inayotolewa na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya Wakimbizi walioko nchini isiwe sababu ya kutumika kuingiza sare za jeshi au silaha.

Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikiteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo hivi karibuni. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwa ajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.

Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto. 

MTANZANIA, MOHAMED MANSOUR AENDELEA TENA KULIWAKILISHA NA KULITANGAZA VYEMA TAIFA ANGA ZA KIMATAIFA

$
0
0
 Mtanzania, Mohamed Mansour Nassor anaetokea Zanzibar ambae anafanya masomo kiwango cha juu ya PhD katika fani ya Uchumi ambae pia ndio Raisi wa Umoja wa Vijana na Wanafunzi wa Nchi zote za Afrika(ASSAFSTU) katika Chuo Kikuu kwa Jina maarufu la Patrice Lumumba(RUDN University) ametunukiwa tunzo kubwa ya Kimataifa kwa Kuhamasisha vijana wa nchi za Afrika nchini Urusi.


Na ujumbe wake ulisema kama ifuatavyo:


Leo tarehe 12/01/2019 kwa uwezo wa Mungu nimefikia tena kutambuliwa Kimataifa na najivuna tumeendelea tena kulitangaza vyema Taifa letu la Tanzania katika anga za Kimataifa. 
Kwa heshima kubwa kwangu na kwa nchi yetu, nimetunukiwa Tunzo ya kufanya vyema sana katika kuhamasisha vijana wa Afrika nchini Urusi katika masuala ya Taaluma(Elimu) na Maendeleo ya Jamii(Community Development) kupitia Shirika la vijana wa Kiafrika lisilo la Kiserikali(NGO) la Youth of Large Exploit(YOLE) katika hafla yao iliofanyika mjini Moscow.
Kwa uwezo wa Mungu, pamoja na tunzo huu ya leo tayari inakua ni kwa mara pili kutambuliwa Kimataifa kwa mwaka huu wa 2019 tangu uanze ambapo pia mwezi huu wa Januari nilichapishwa na kutambuliwa Kimataifa kama Mtanzania maarufu zaidi katika Watanzania waliowahi kusoma vyuo vya Sovieti ya Urusi na Urusi katika jarida la Kimataifa(Encyclopedia) la Wahitimu wote wa kigeni waliosoma nchini Urusi yani SOYUZ Alumni. 

Lakini si hivyo tu Tarehe 11 Mwezi Novemba 2018 nilifikia hatua kubwa katika masuala ya uongozi Kimataifa ambapo nilichaguliwa kuwa Raisi wa Vijana wote wa Nchi za Afrika katika Chuo Kikuu Cha Urafiki Cha Watu Wa Urusi au maarufu kama Chuo Kikuu Cha Patrice Lumumba ambapo nafasi hii ndio kwa mara ya Kwanza inshikwa na Mtanzania tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki miaka ya 1960. 
Aidha licha ya hivyo bado, nimekua nikifanya kazi za uongozi kama Makamu Mwenyekiti wa Diaspora ya Watanzania nchini Urusi na nchi za CIS yani TADIRU na kama Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kiswahili Cha Moscow(CHAKIMO) chini ya Ulezi wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Urusi,Mheshmiwa Simon Marco Mumwi. Namshukuru sana mheshimiwa Balozi wetu na Ubalozi kwa ujumla kwa mwongozo, nasaha, usahuri na kunipa dira na kunipa msaada mkubwa katika majukumu yangu na harakati zangu.
Nawashukuru sana viongozi wa shirika la YOLE na pia Chama chetu Cha SOYUZ Alumni Association of Tanzania walioniamini ili kuwawakilisha Kimataifa kama Balozi wao. 

Napenda pia kuwashukuru Watanzania wote wanaounga mkono juhudi zangu na harakati zangu na kwa dua zao njema kwangu hasa kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania linaloongozwa na Raisi Makini kabisa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!
Ahsante sana!  





MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 14,2019

MAWAZIRI WATANO WATEMBELEA MRADI WA KUFUA UMEME STIEGLER'S GORGE

$
0
0
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akizungumza na baadhi ya Mawaziri pamoja na Makatibu wakuu waliofanya ziara jana ya kutembelea mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji kwa ajili ya kukagua Miundombinu Wezeshi ikiwemo maji, barabara, umeme pamoja na nyumba za watumishi kabla ya kumkabidhi Mkandarasi huyo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bwawa la kuzalisha Umeme.
Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Mkazi, Mhe. William Lukuvi akiwa ameshika moya nguzo za umeme zilizotengenezwa kwa zege yenye urefu wa mita 17 ambazo zimewekwa katika Pori la Akiba la Selous ili wanyama kama vile tembo na twiga waziweze kuziangusha wakati Mawaziri watano walipofanya ziara katika mradi huo wa kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Morogoro. Wengine wanaoangalia ni mawaziri na makatibu wakuu.
Mratibu wa Mradi wa Kufua Umeme wa Mto Rufiji, Mhandisi Justus Mtolela akizungumza na Mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali walioambatana na katika Pori la Akiba la Selous kabla ya kuanza kufanya ziara ya kukagua Miundombinu Wezeshi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akizungumza na Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kukagua Nyumba za kuishi watumishi wanaokuja kufanya kazi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji wakati Mawaziri hao walipofanya ziara jana Mkoani Morogoro ya kukagua Miundombinu Wezeshi kwa ajili ya Mkandarasi kuanza kazi.
Mratibu wa Mradi wa Kufua Umeme wa Mto Rufiji, Mhandisi Justus Mtolela akitoa maelezo kwa Mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali walioambatana nao katika Pori la Akiba la Selous wakati wakiangalia daraja amabalo linatakiwa kujengwa upya kutokana na daraja hilo kuwa na uwezo mdogo wa kuhimili mzigo mizito itakayoanza kusafirishwa na Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Morogoro.
Baadhi ya Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakikagua Nyumba za kuishi watumishi watakaokuja kufanya kazi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji wakati wa ziara iliyofanyika katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro
Baadhi ya Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakiangalia sehemu ya kujengwa Bwawa la kufua umeme katika mto Rufiji wakati Mawaziri hao walipofanya ziara jana katika Pori la Akiba la Selous Kanda ya Matambwe mkoani Morogoro
Eneo la Fuga ni sehemu ambayo mizigo itakuwa ikitelemshwa kwa njia ya reli itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi kufua umeme katika mto Rufiji katika Pori la Akiba la Selous katika Kanda ya Matambwe mkoani Morogoro.(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)





NA.LUSUNGU HELELA-MOROGORO

Serikali imesema maandalizi ya miundombinu wezeshi kabla ya kumkabidhi Mkandarasi aliyepewa kazi katika Mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji tayari imekamilika kwa asilimia themanini.

Miundombinu hiyo ni pamoja na maji, umeme, barabara pamoja na nyumba za kukaa wafanyakazi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mawaziri wa Wizara tano kutoka Nishati, Maliasili na Utalii, Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Fedha na Mipango baada ya kutembelea na kujionea miundombinu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imeshakamilika.


Ziara hiyo katika Pori la Akiba la Selous kanda ya Matambwe mkoani Morogoro iliongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ikilenga kukagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kumuwezesha Mkandarasi kuanza kusafirisha mizigo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Alisema kukamilika kwa miundombinu hiyo kutamuwezesha Mkandarasi huyo kuanza maandalizi ya awali ikiwemo kuanza kusafirisha mizigo kuileta katika maeneo ya ujenzi wa bwawa.Aliongeza kuwa kutokana na Mkataba uliopo Mkandarasi huyo ataanza kazi rasmi Juni 15 mwaka huu na ataukamilisha mradi huo ifikapo mwezi April 2022. 

Katika upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu alitoa tahadhari kwa wafanyakazi wanaokuja kufanya kazi katika mradi huo wasiende kupumzika vichakani kuna wanyama wakali kama vile Simba, Nyati pamoja na tembo.

" Wale wenye tabia ya kujipumzisha vichakani baada ya kufanya kazi chonde chonde jiepusheni na haya mazoea la sivyo mtaliwa na Simba.Aidha, Mhe.Kanyasu alitumia fursa hiyo kuiomba Wizara ya Utumishi kutoa kibali cha kuajiri Askari Wanyamapori zaidi ya 200 ambao watatoa ulinzi kwa Wafanyakazi wa mradi huo,

Ombi hilo linakuja kufuatia Askari wanyamapori 115 kutoka mapori mengine kuhamishiwa kwa muda katika Pori hilo katika kanda ya Matambwe kwa lengo la kuongeza nguvu baada ya askari 115 waliokuwepo kuonekana hawatoshi.

Hata hivyo , Mhe.Kanyasu alisema hatua za haraka zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja kutengeneza vyoo, malazi pamoja na maji kwa vile miundombinu iliyokuwepo katika Kanda hiyo ilikuwa na uwezo wa kuhudumia Askari Wanyamapori 85 tu lakini hadi hivi sasa kuna jumla ya askari 230.

Kukamilika kwa mradi huo wa kufua umeme, Bwawa hilo la Rufijin litakuwa la nne kwa ukubwa kwa Afrika na la kwanza kwa Afrika Mashariki, Duniani ni la 60 katika ya mabwawa sabini makubwa.

SADC URGES ALL INCLUSIVEGOVERNMENT IN DRC

$
0
0
His Excellency Mr Edgar Chagwa Lungu, President of the Republic of Zambia says given the strong objections to the provisional results of the presidential election in the Democratic Republic of Congo (DRC), the Southern African Development Community (SADC) has called on all political leaders to consider a negotiated political settlement for an all-inclusive government.
And SADC encourages all stakeholders in the DRC elections to pursue a negotiated political settlement for a government of national unity. 

In his capacity as chairperson of the SADC Organ on Politics, Defence and Security, President Lungu says he has spoken to leaders of SADC and the International Conference of the Great Lakes Region (ICGLR).  

President Lungu has also spoken to the provisionally proclaimed winner, Mr. Felix Tsisekedi and other stakeholders within and outside of the DRC.

“SADC draws the attention of Congolese politicians to similar arrangements that were very successful in South Africa, Zimbabwe and Kenya where governments of national unity created the necessary stability for durable peace.”

“SADC therefore encourages all parties to enter into a political process towards a government of national unity in order to enhance public confidence, build bridges and reinforce democratic institutions of government and electoral process for a better Congo,” he said.

SADC has urged DRC authorities to swiftly resolve all elements of doubt that could undermine the fairly successive general election and pose a danger to the peace and stability of the country. 

SADC has taken note of the strong doubts cast on the poll outcome by Roman Catholic Church in the DRC which had deployed more than 40,000 monitors; the opposition Lamuka coalition, and other observers and therefore feels a recount would provide the necessary re-assurance to both winners and losers.

It is therefore imperative that at this very crucial moment, all DRC politicians commit to actions and processes that do not escalate tensions any further. 

SADC expresses solidarity with the government and the people of the DRC for organizing a relatively successful election that inspires hope that the country was on a path towards democratic consolidation.
   
____________________________
Issued by:                       

Amos Chanda
 SPECIAL ASSISTANT TO THE PRESIDENT
(PRESS AND PUBLIC RELATIONS)
 STATE HOUSE

Vodacom Tanzania yaongeza ushiriki wa Wasichana katika teknolojia kupitia #codelikeagirl

$
0
0
Vodacom Tanzania waongeza ushiriki wa wasichana katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM), kupitia mafunzo ya teknolojia ya ku-code yaliyodhaminiwa na kampuni hiyo ambapo awamu ya pili ya mafunzo yalichukua siku tano na kuona wanafunzi 59 wakihitimu mafunzo hayo yaliyofanyika katika taasisi atamizi ya Dar Teknohama Business Incubator (DTBI). 

Shirika la Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa linasema, 'ushiriki wa wanawake katika sayansi na teknolojia ni mdogo ukilinganisha na wanaume. Hivyo Code like a girl ni programu ya kimataifa yenye lengo la kuandaa Wasichana kuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira ya technolojia.

Kwa kushirikiana na DTBi, mafunzo haya yalijumuisha elimu ya lugha za kompyuta na utengenezaji wa programu kama HTML, CSS, GitHub and Bootstrap. Mafunzo yalitolewa kwa mfumo wa ushirikiano na yalijumuisha mafunzo ya kijamii pamoja na ku-code ili kuwawezesha kutengeneza tovuti zao wenyewe. Washiriki pia walipewa mafunzo ya kuwasilisha mada na mawasiliano.

"Tumefurahishwa na idadi ya wanafunzi waliohudhuria semina hii, wiki ilifana na mafunzo mbali mbali ya maisha, coding, mawasilisho, pamoja na mafunzo ya ujuzi wa mawasiliano. Mwishoni mwa juma, wasichana walikuwa wamiliki wa tovuti ambazo walitengeneza wao binafsi, "alisema Zaituni Ally, Mkuu wa kitengo kinachoangalia ufanisi wa shirika (Head of Organizational Effectiveness) akimuwakilisha Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom, Bi Vivienne Penessis.”Leo, mabadiliko ya kidijitali yanatokea kila mahali duniani, kwa hiyo, ni muhimu kuandaa wasichana kwa mabadiliko haya katika soko la ajira," aliongeza.

Akizungumza kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa DTBi Dr George Mulamula  anasema kuwa "Katika awamu ya kwanza ya mafunzo, tuliona kuwa idadi kubwa ya wanafunzi, hasa wasichana katika shule za sekondari wanafundishwa kwa nadharia badala ya vitendo kuhusiana na teknolojia ya Mawasiliano (ICT). Hivyo basi mkakati huu wa mafunzo haya una lengo la kuwawezesha Wasichana nchini kote kupata elimu ya ICT, lakini pia kuwasaidia kupata fursa mbalimbali katika mazingira ya teknolojia kama vile wenzao wa kiume, "aliongeza.

Lengo la Vodacom ni kutoa fursa kwa wasichana nchini kote kushiriki katika masomo ya STEM; kwani "Coding ndio nati na spana za dijitali siku zijazo. Kupitia mipango kama hii, tunatarajia kuona wasichana wengi katika sekta ya Teknolojia. Pia kuwasaidia vijana kupanua ujuzi wao kupitia teknolojia ili Kuleta maendeleo nchini Tanzania "alielezea Bi Zaituni.
 Mhitimu wa kidato cha nne, Diana Moshy, akiwasilisha tovuti iitwayo “WAW” waliyobuni yeye na kundi lake katika mafunzo ya Code like a girl, yaliyoendeshwa na Dar Teknohama Business incubator (DTBi) jijini Dar es Salaam. Code like a girl imedhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa lengo la kukuza ushiriki wa Wasichana katika kada za sayansi na teknolojia.
  Meneja wa Rasilimali na Maendeleo wa Vodacom Tanzania, Bi Immaculate Mwaluko akizungumzia kuhusu umuhimu wa teknologia kwa wasichana, katika programu ya Code like a girl, iliyofanyika Dar Teknohama Business incubator (DTBi) jijini Dar es Salaam. Code like a girl imedhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa lengo la kukuza ushiriki wa wasichana katika kada ya sayansi na teknolojia
Mkuu wa Ufanisi wa Shirika wa Vodacom Ms Zaituni Ally (katikati ) akimkabidhi cheti muhitimu wa mafunzo ya kuunda tovuti katika programu ya ‘Code Like a Girl’, Ms Fatuma Mniga ambaye ni mwanafunzi wa Shule Sekondari ya Kinondoni Muslim. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Teknohama Business incubator (DTBi), Dr. George Mulamula.

watanzania watakiwa kununua bidhaa za kwenye maduka yanayotambulika

$
0
0
WATANZANIA wameshauriwa kununua bidhaa kwenye maduka yanayotambulika na kuacha kuamini matapeli wanaotumia nembo za kampuni kubwa kuwahadaa.

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Kampuni ya Elite Computers yenye dhamana ya kusambaza bidhaa za Apple hapa nchini, wakati wa hafla ya kutambulisha simu mpya ya iPhone XR.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Aqil Kurji ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Elite Computers alisema pamoja na kwamba Apple inaaminika kwa kuzalisha bidhaa bora lakini kumekuwa na wajanja wachache ambao wamekuwa wakitumia nembo ya kampuni hiyo kwa kuwauzia watanzania bidhaa zisizo na ubora.

“Leo Elite Computers ambao ni wakala rasmi wa Apple nchini tumetambulisha simu mpya ya iPhone XR  ambayo tunaamini kuwa itaendana na mazingira ya Kitanzania kwa asilimia 100 kutokana na kuzingatia hali halisi.

“Sifa kuu ya simu hii kwanza inadumu na chaji kwa saa 25 hadi 65 pia ina usalama kwani mteja atatumia uso wake kama paswedi(Face Id) na hivyo itarahisisha masuala ya wizi wa fedha kwenye simu jambo ambalo limekuwa likikemewa na serikali kwa muda mrefu hivyo iPhone XR ni ya kipekee ukilinganisha na matoleo yaliyopita.

“Kumekuwa na watu wengi wanaowadanganya watanzania kuwa ni mawakala wa Apple na badala yake wakiuziwa bidhaa hizo zisizo halisi wanakuja kulalamika kwetu jambo ambalo wanapaswa kuliepuka,” alisema Kurji.

Pia alifafanua kuwa mteja anaweza kupata matengenezo kwa kutembelea ofisi za Elite Computers zilizoko Upanga, Samora, Viva Towers, Seacriff village na Mwanza na kuongeza kuwa mteja anunuapo simu ghiyo atapata dhamana ya mwaka mmoja.

Upande wake Hussein Hassan ambaye ni mfanyabiashara wa simu nchini aliipongeza kampuni hiyo kwa kutamulisha simu hiyo ambayo alisema kuwa hiyo ni fursa kwa watanzania kununua simu hiyo ili kuondokana na ununuaji wa simu zisizo na kiwango mara kwa mara.

“Hili ni jambo la kupongezwa kwa kampuni ya Apple kwani simu hii inausalama na kama tulivyoelezwa hapa kuwa ina uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa zaidi ya dakika 30 bila kuharibika hivyo ni jambo la kupongezwa kwani sisi wengi shughuli zetu zimekuwa ni za pilikapilika.

“Hivyo ni bora ukajinyima lakini ukamiliki simu yenye usalama na uhakika zaidi na pia inayodumu na chaji kuliko kuepuka gharama matokeo yake unakuwa wa kununua simu kila wakati,” alisema Hussein.

Mara kwa mara serikali imekuwa ikitilia mkazo kwa watanzania kuhakikisha kuwa wananunua bidhaa bora ikiwamo kudai risiti huku pia ikisisitiza kuongeza usalama kwenye simu zao ili kuzuia wizi wa fedha unaoweza kutokea.

RAIS WA DKT. SHEIN AKIWAFARIJI FAMILIA YA MUASISI WA CCM ZANZIBAR BI.JOHARI YUSSUF AKIDA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, atowa mkono wa pole kwa Wanafamilia ya Marehemu Bi. Johari Yussuf Akida, aliyefariki wiki iliopita, katikati Mtoto wa Marehemu Bi. Shawana Buheti,anayefuata Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, walipofika katika makaazi yao Mwanakwerekwe kutowa mkono wa pole 13/1/2019.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimfariji Mtoto wa Marehemu Bi. Johari Yussuf Akida, muasisi wa CCM.katikati Bi.Shawana Buheti na kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar. Mama Mwanamwema Shein, walipofika nyumbani kwake Mwanakwerekwe Unguja kutowa mkono wa pole 13/1/2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia na kumpa mkono wa pole Ndugu wa Marehemu Bi. Johari Yussuf Akida,alipofika nyumbani kwao Mwanakwerekwe  na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,kutowa mkono wa pole 13/1/2019.(Picha na Ikulu)  

TFDA NA GCLA ZAJIDHATITI UDHIBITI MPAKANI NAMANGA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Namanga Arusha.

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) zimejidhatiti kulinda bidhaa za vyakula ,dawa, vipodozi pamoja na Kemikali katika kuhakikisha walaji wanapata huduma bora za bidhaa hizo.

Kulinda kwa bidhaa hizo ni pamoja na kuhakikisha Serikali haipotezi fedha kwa kuingiza bidhaa zisizo na ubora.

Hayo yamebainishwa katika kituo cha Namanga wakati wa Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo walipotembelea Kituo cha ukaguzi Namanga mkoani Arusha ikiwa ni Kampeni Tumeboresha Sekta ya Afya katika miaka mitatu ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika utekelezaji wa uwekezaji katika sekta hiyo.


Maafisa wa mpaka wa Namanga kati ya Tanzania na Kenya walieleza mikakati ya utoaji wa huduma za ukaguzi kutokana na serikali kuwekeza rasimali watu pamoja vitendea kazi katika kurahisisha utoaji wa huduma katika mpaka huo.

Meneja wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) Benny John amesema ofisi ya Kanda imeendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwemo udhibiti wa bidhaa za Chakula, dawa vipodozi na vifaa Tiba kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata kanuni na sheria zilizowekwa katika masilahi mapana ya kulinda wananchi katika utumiaji wa bidhaa hizo. iki
"Udhibiti wa bidhaa zinazoingia nchini umeongezeka kwa wafanyabiashara kulipa Kodi na tozo za Serikali na Hivyo kuongeza pato la Taifa" alisema Kaimu Meneja huyo.

Nae Mkaguzi wa Dawa wa TFDA mpaka wa Namanga Elia Nyeura amesema takwimu za shehena katika kituo cha Namanga zimeongezeka kutoka shehena 724 hadi kufikia shehena 1223 kwa mwaka 2016/2018."Kwa nia ya Rais wa awamu ya tano ya kuwa Tanzania ya viwanda, bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA na mamlaka zingine zilizosindikwa kwa kipindi cha miaka mitatu shehena zimeongezeka kutoka 429 hadi kufikia 640 kwa 2016 /2018 " amesema Nyeura na

Ameongeza kuwa, mamlaka imepunguza upotevu wa fedha za kigeni zinazotokana na bidhaa zisizofaa". Alisema.Hata hivyo amebainisha thamani ya bidhaa iliyokamatwa kuingizwa nchini kwa kutofuata utaratibu imepungua kutoka Milioni 630.3 hadi kufikia Milioni 24.7 kwa mwaka 2015/2018 .

Kwa upande wa Msimamizi wa Kituo cha Ukaguzi Namanga wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Michael Benarnd amesema kuwa kemikali bidhaa za kemikali zinazoingia na kutoka nchini lazima wazikague katika hicho pamoja na kuhakiki vibali vya usafirishaji wa bidhaa hizo.

Amesema kuwa mwaka 2016 walikagua mizigo ya Kemikali 1300 ikiwa 750 ya mizigo hiyo ilifuata utaratibu wa sheria sawa na asilimia 57 ya mizigo iliyofuta sheria , mwaka 2017 walikagua mizigo ya Kemikali 1450 ikiwa 1120 ya mizigo hiyo ilifuata utaratibu wa sheria sawa na asilimia 77.2 ya mizigo iliyofuta sheria na mwaka 2018 mizigo 1320 iliyofuata utaratibu 1237 sawa na asilimia 93.7.

Aidha amesema kuwa ofisi ya GCLA imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha kemikali zote zinafuata sheria ikiwa ni pamoja na kushirikisha wadau katika uapatikanaji wa taarifa.

Kaimu Meneja  TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John akionesha kielelezo cha ulinganifu wa bidhaa zilizoingia nchini (Istogram) kwa  Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Mpaka wa Namanga panapokaguliwa na  TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
Kaimu Meneja  TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John akizungumza na  Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Makao makuu ya TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
 Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza akizungumza katika kituo cha Namanga  wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya kwa kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika miaka mitatu.

Mkaguzi wa Dawa wa TFDA mpaka wa Namanga Elia Nyeura akielezea taarifa fupi kwa   Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo (hawapo pichani) walipotembelea Mpaka wa Namanga panapokaguliwa na  TFDA Kanda ya Kaskazini, Mkoani Arushai ikiwa ni Kampeni ya ‘ Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli. Anayefuatia ni Kaimu Meneja TFDA Kanda ya Kaskazini, Benny John
 Afisa Ukaguzi katika Kituo cha Namanga wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA, Michael Benarnd  akizungumza namna wanavyodhibiti uingiaji wa kemikali nchini katika kituo hicho, wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea kituo cha Namanga.

mkaguzi wa dawa wa TFDA kituo cha Namanga akiendelea na majukumu yake katika tukio hilo
 Afisa Ukaguzi wa TFDA akionesha Maabara hamishika wanavyotumia katika ukaguzi wa dawa,vifaa tiba pamoja vitendanishi katika kituo cha Ukaguzi wa pamoja cha Namanga. 
 Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kanda ya Kaskazini ya TFDA iliyopo mkoani Arusha.
Picha ya pamoja ya maofisa habari wa wizara,taasisi pamoja na maofisa wa kituo cha Namanga wakiwa nje ya kituo hicho mara baada ya kuona kazi zinazofanya kwenye kituo hicho

Ujenzi mradi wa umeme Rufiji kuanza mwezi Juni mwaka huu

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Pwani
Imeelezwa kuwa ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji utakaozalisha  megawati 2115 unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 mwezi Juni mwaka huu. Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani katika eneo utakapotekelezwa mradi huo wilayani Rufiji mkoani Pwani mara baada ya kukagua  kazi za ujenzi wa miundombinu wezeshi ya mradi huo ikiwemo barabara, umeme, maji na reli.

Katika ziara hiyo, Waziri wa Nishati aliambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constatine Kanyasu na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa. Viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo ni makatibu wakuu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya Mifugo na uvuvi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Dkt. Kalemani alisema kuwa,  mkandarasi  ambaye ni Arab contractors amepewa miezi 36 ya ujenzi wa mradi huo na miezi sita ya maandalizi hivyo inatarajiwa kuwa mradi utakamilika mwezi Aprili  mwaka 2022. Kuhusu ujenzi wa miundombinu wezeshi ya mradi, Dkt Kalemani alisema kuwa kazi za ujenzi wa miundombinu hiyo iliyoanza miezi tisa iliyopita imekamilika kwa zaidi ya asilimia 80 .

Aliongeza kuwa, ili kutekeleza mradi huo, jumla ya megawati 30 zitahitajika katika eneo hilo ambapo mpaka sasa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeshafikisha megawati 10 huku  mahitaji ya umeme kwa sasa yakiwa ni megawati 7. Hivyo,  aliiagiza  TANESCO kuendelea kuratibu kazi hiyo ili nishati hiyo isiwe kikwazo cha kuchelewesha utekelezaji wa mradi.

Aidha pamoja na kuzipongeza  taasisi zote zinazohusika na mradi huo,  alitoa wito wa kuendelea kushirikiana ili kukamilisha kazi ndani ya wakati na kwa ufanisi kwani mradi huo ni wa Serikali. Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliwapongeza TANESCO kwa kutekeleza kazi zao kwa ufanisi katika eneo hilo la mradi na  viongozi wa wizara ya nishati kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.

Alisema kuwa,  Wizara hiyo ilipewa kazi mbalimbali ikiwemo kupima eneo lote la mradi na kueleza kuwa wameshamaliza kupima maeneo mawili ya mradi huo ambapo eneo la kwanza ni litakalojengwa mitambo ya umeme lenye hekta 1402 ambalo mchoro wake umekamilika. Pia, Wizara hiyo  imepima eneo lenye hekta 4711 litakalojengwa nyumba za kudumu za wafanyakazi na kwamba wameshaweka alama katika maeneo hayo ambapo alimkabidhi Waziri wa Nishati michoro ya maeneo hayo ili taratibu nyingine za umiliki ziendelee. 

kwa upande wake,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  alisema kuwa,  Wizara yake inaendelea majukumu mbalimbali yatakayowezesha kuanza kwa mradi huo ikiwemo usafishaji wa sehemu itakayokuwa ni bwawa la kuhifadhia maji ya kuzalishia umeme. Aliongeza kuwa,  kazi hiyo wameigawa katika  blocks 30 na kwamba blocks 27 zimeshapata watu wa kufanya kazi hiyo na baadhi ya waombaji tayari wanaendelea na kazi husika.

Kuhusu ulinzi alisema kuwa, wanatoa ulinzi katika eneo hilo na kwa watu wote wanaofanya kazi za mradi na kwamba awali kulikuwa  na askari 115 lakini wameongeza askari wengine 115 ili kukidhi mahitaji na kueleza kuwa idadi hiyo itaongezeka kadri kazi zinavyoongezeka. Viongozi waliohudhuria ziara hiyo kutoka Wizara ya Nishati, ni Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia maendeleo ya nishati, Mhandisi Juma Mkobya na Kaimu Mkurugenzi Msadizi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Lusajo Mwakaliku.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tano kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (wa pili kulia) wakiangalia kazi ya urekebishaji wa miundombinu ya barabara katika eneo kutakapojengwa mradi wa umeme wa Rufiji. Wengine katika picha ni viongozi kutoka Wizara na taasisi mbalimbali za Serikali zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (wa pili kushoto) wakiwa katika eneo kunapojengwa nyumba zitakazotumiwa na mkandarasi atakayejenga mradi wa umeme wa Rufiji zilizopo katika eneo hilo la mradi.
 Baadhi ya nguzo za umeme za zege zenye urefu wa mita 14 ambazo zinatumika katika eneo la  mradi umeme wa Rufiji  ili kutoathiri maisha ya wanyama katika mbuga ya  Selou ambao huweza kuruka kwa urefu wa mita 12.
Miundombinu ya reli katika Kituo cha Fuga wilayani Rufiji mkoani Pwani ambayo inaboreshwa ili kuweza kutumika kushusha mizigo wakati wa utekelezaji wa mradi wa umeme wa Rufiji.

GULAMALI AZIDI KUIMARISHA SEKTA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KATIKA utekelezaji ahadi kwa wananchi kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mbunge wa jimbo la Manonga, Seif Gulamali ameendelea na uboreshaji wa miundombinu hususani katika sekta ya elimu na afya ili kuhakikisha wananchi jimboni humo wanakuwa na afya bora na wanapata elimu yenye tija.

Akizungumza na  blogu ya jamii Gulamali amesema, suala la elimu kwa sasa hali ni shwari kabisa hasa kwa wanafunzi wapya anaoanza kidato cha kwanza kwani  wanafunzi wamekuwa  wengi kuliko siku za nyuma na wamejipanga vyema katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimo bora na bure na mkakati uliopo sasa ni kuendelea kujenga Shule mpya na kuongeza madarasa katika Shule zilizopo, amesema kuwa  wanatarajia kuongeza shule mpya  katika  Kata za Kitangiri, Ugaka, Igoweko, Mwamala, na Tambarale ambako  Wananchi wameonesha ari ya Kuchangia Ujenzi na yeye kama Mbunge atawaunga mkono kwa kuhakikisha Shule zote zinakamilika kwa Wakati.

Amesema kuwa  shule mpya ya Ibologero iliyoanza kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwaka huu wamepewa jumla ya shilingi milioni 4.5 kwa ajili ya uendeshaji na shule ya Kitangiri imeshapokea shilingi milioni 3.5 kwa mwaka huu wakiwa wanapokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza.

Aidha amesema kuwa pesa zimetolewa kwa ajili ukarabati wa madarasa na vyumba vya madarasa katika vijiji vya Mpogolo, Ncheli, Moyofuko, Kitangiri pamoja na Mondo.

Pia huduma za umeme na maabara  pamoja na ofisi na nyumba za walimu katika kijiji cha Ngulu unaendelea na hiyo ni sambamba na   ukarabati wa bweni katika sekondari ya Ziba ambapo jumla ya shilingi milioni saba zimetolewa.

Aidha Gulamali  amesema kuwa  Zahanati ya Nkinga imeshapata huduma ya maji na hiyo ni baada ya Mbunge  na waganga wa tiba asili kuungana katika kuchangia uboreshwaji wa huduma ya maji pia amesema kuwa katika kijiji cha Ugaka ambako Zahanati inajengwa tayari wamepatiwa mifuko 50 ya saruji na shilingi milioni 9.

Gulamali amesema kuwa  zaidi ya shilingi milioni 52 za mfuko wa jimbo zimetolewa kutokana na maombi aliyopokea kutoka kwenye kamati  husika za ujenzi na amesema kuwa ana imani kuwa viongozi  wa vijiji watasimamia kwa ufanisi na mapema mwaka huu atajiridhisha kupitia ziara yake atakayoanza hivi karibuni.

Mbunge wa jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Gulamali.

UJENZI WA OFISI YA WAZIRI MKUU KWENYE MJI WA SERIKALI, IHUMWA DODOMA WASHIKA KASI

$
0
0
 Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji wa Serikali, Ihumwa, linaloendelea kujengwa na Mkandarasi  Mzinga Holding Company, tarehe 13 Januari, 2019, Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya  Ulizi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka akikaribishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali watu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Nigel Msangi, alipofika kukagua shughuli za Mkandarasi Mzinga Holding Campony, anayejenga jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mji wa serikali Ihumwa Dodoma.,   Mkandarasi huyo yupo chini ya Wizara ya Ulizi, mwingine ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA-JKT, Kanali Rajab Mabele, tarehe 13 Januari, 2019.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ulizi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka akipata maelezo kutoka kwa Mratibu Ujenzi jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu wa  Mkandarasi Mzinga Holding Company, Kapteni, Erick Siara wakati alipofika  kukagua shughuli za Mkandarasi huyo katika mji wa serikali, Ihumwa , Dodoma, Mkandarasi huyo yupo chini ya wizara ya Ulizi,   tarehe 13 Januari, 2019.
Mmoja wa mafundi wa Mkandarasi Mzinga Holding Company, akijenga sehemu ya ukuta wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu, katika mji wa serikali, Ihumwa  Dodoma,   tarehe 13 Januari, 2019.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI  MKUU)

MAWAZIRI WATANO WATEMBELEA MRADI WA KUFUA UMEME STIEGLER'S GORGE

$
0
0
NA.LUSUNGU HELELA-MOROGORO
Serikali imesema maandalizi ya miundombinu wezeshi kabla ya kumkabidhi Mkandarasi aliyepewa kazi katika Mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji tayari imekamilika kwa asilimia themanini. Miundombinu hiyo ni pamoja na maji, umeme, barabara pamoja na  nyumba za kukaa wafanyakazi.

Kauli  hiyo imetolewa jana na Mawaziri wa Wizara tano  kutoka Nishati, Maliasili na Utalii, Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,  Fedha na Mipango baada ya kutembelea na kujionea miundombinu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imeshakamilika.

Ziara hiyo katika Pori la Akiba la Selous kanda ya Matambwe mkoani Morogoro iliongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ikilenga kukagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kumuwezesha Mkandarasi kuanza kusafirisha mizigo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Alisema kukamilika kwa miundombinu hiyo kutamuwezesha Mkandarasi huyo kuanza maandalizi ya awali ikiwemo kuanza kusafirisha mizigo kuileta katika maeneo ya ujenzi wa bwawa. Aliongeza kuwa kutokana na Mkataba uliopo Mkandarasi huyo ataanza kazi rasmi Juni 15 mwaka huu na ataukamilisha mradi huo ifikapo mwezi  April 2022. 

Katika upande wake  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu alitoa tahadhari kwa wafanyakazi wanaokuja kufanya kazi katika mradi huo wasiende kupumzika vichakani kuna wanyama wakali kama vile Simba, Nyati pamoja na  tembo. " Wale wenye tabia ya kujipumzisha vichakani baada ya kufanya kazi chonde chonde jiepusheni na haya mazoea la sivyo mtaliwa na Simba.

Aidha, Mhe.Kanyasu alitumia fursa hiyo kuiomba Wizara ya Utumishi kutoa kibali cha kuajiri Askari Wanyamapori zaidi ya 200 ambao watatoa ulinzi kwa Wafanyakazi wa mradi huo. Ombi hilo linakuja kufuatia Askari wanyamapori 115 kutoka mapori mengine kuhamishiwa kwa muda  katika Pori hilo  katika kanda ya Matambwe kwa lengo la  kuongeza nguvu baada ya askari 115 waliokuwepo kuonekana hawatoshi.

Hata hivyo , Mhe.Kanyasu alisema  hatua za haraka zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja  kutengeneza  vyoo, malazi pamoja na maji kwa vile miundombinu iliyokuwepo katika Kanda hiyo ilikuwa na uwezo wa kuhudumia Askari Wanyamapori 85 tu lakini hadi hivi sasa kuna jumla ya askari 230.

Kukamilika kwa mradi huo wa kufua umeme, Bwawa hilo la Rufijin litakuwa la nne kwa ukubwa kwa Afrika na la kwanza kwa Afrika Mashariki, Duniani ni la 60 katika ya mabwawa sabini makubwa.
 Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akizungumza na baadhi ya Mawaziri pamoja na Makatibu wakuu waliofanya ziara jana ya kutembelea mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji kwa ajili ya kukagua Miundombinu Wezeshi ikiwemo maji, barabara, umeme pamoja na nyumba za watumishi kabla ya kumkabidhi Mkandarasi huyo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bwawa la kuzalisha Umeme.
 Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Mkazi, Mhe. William Lukuvi akiwa ameshika moya  nguzo za umeme zilizotengenezwa kwa zege yenye urefu wa mita 17 ambazo zimewekwa katika Pori la Akiba la Selous ili wanyama kama vile tembo na twiga waziweze kuziangusha wakati Mawaziri watano walipofanya ziara katika mradi huo wa kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Morogoro. Wengine wanaoangalia ni mawaziri na makatibu wakuu.
 Mratibu wa Mradi wa Kufua Umeme wa Mto Rufiji, Mhandisi Justus Mtolela akizungumza na Mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali walioambatana na katika Pori la Akiba la Selous kabla ya kuanza  kufanya  ziara ya kukagua Miundombinu Wezeshi katika mradi  wa kufua umeme wa mto Rufiji.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akizungumza na Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya  kukagua Nyumba za kuishi  watumishi wanaokuja kufanya kazi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji wakati Mawaziri hao walipofanya ziara jana Mkoani Morogoro ya kukagua Miundombinu Wezeshi kwa ajili ya Mkandarasi kuanza kazi.
 Mratibu wa Mradi wa Kufua Umeme wa Mto Rufiji, Mhandisi Justus Mtolela akitoa maelezo kwa Mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali walioambatana nao katika Pori la Akiba la Selous  wakati wakiangalia daraja amabalo linatakiwa kujengwa upya kutokana na daraja hilo kuwa na uwezo mdogo wa kuhimili mzigo mizito itakayoanza kusafirishwa na Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Morogoro.
 Baadhi ya Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakikagua Nyumba za kuishi  watumishi watakaokuja kufanya kazi katika mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji wakati wa ziara iliyofanyika katika Pori la Akiba la Selous  mkoani Morogoro.

  Baadhi ya Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakiangalia sehemu ya kujengwa Bwawa la kufua umeme katika mto Rufiji wakati  Mawaziri hao walipofanya ziara  jana katika Pori la Akiba la Selous  Kanda ya Matambwe  mkoani Morogoro.
Eneo la Fuga ni sehemu ambayo mizigo itakuwa ikitelemshwa kwa njia ya reli itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi kufua umeme katika mto Rufiji katika Pori la Akiba la Selous katika Kanda ya Matambwe  mkoani Morogoro



(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)

RC Wangabo ashtushwa baada ya kuona vijiji vitatu vinachangia shule ya msingi moja

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa Kata ya Paramawe yenye vijiji vitatu vya Lyazumbi, Paramawe ‘A’ na ‘B’ kuchangia shule moja ya msingi huku shule hiyo ikiwa na upungufu wa madarasa ya kuwahifadhi wananfunzi 1400 wa shule hiyo iliyopo wilayani Nkasi.

Amesema kuwa umefika wakati wa kila Kijiji katika kata hiyo kuhakikisha wanaanza ujenzi wa shule shikizi ili kuweza kuisaidia mzigo wa wananfunzi uliopo katika shule hiyo mama iliyopo katika Kijiji cha Paramawe ‘A’ na hatimae shule hizo shikizi zitakazoanzishwa katika vijiji hivyo ziendelezwe na kusajiliwa na kuwa shule kamili.

Ameyasema hayo wakati alipoitembelea kata hiyo ili kujionea maendeleo ya elimu ya shule ya msingi ambapo Kijiji cha Lyazumbi tayari kimeshajenga madara matatu yaliyokamilika pamoja na vyoo na ofisi ya walimu huku Kijiji cha paramawe ‘B’ kikikosa shule hiyo shikizi na hatimae kuwapeleka Watoto wa katika shule ya msingi Paramawe ‘A’.

“Muanze kujipanga sasa hivi, Mkurugenzi tuma watu waje wakae huku waone namna gani ya kuwasaidia hivi vijiji vitatu namna gani ya kuondokana na changamoto hii ya msongamano ya Watoto kwa kuhakikisha kwamba kila Kijiji kinakuwa na shule yake ya msingi na kwa kuanzia wawe na shule shikizi, weka mkazo mkubwa kumaliza ile shule ya msingi Lyazumbi na isajiliwe na hawa paramawe ‘B’ watafute eneo la kujengea shule hiyo,” Alisema

Aidha, katika kubainisha vigezo vya shule ya msingi kukamilika na kuweza kusajiliwa, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Missana Kwangula alivitaja vigezo vinne vinavyopelekea shule ya msingi kusajiliwa na kufafanua kuwa vigezo hivyo vimewekwa baada ya Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kubaini kuwa shule nyingi zikianzishwa kama shikizi na kusajiliwa huwa haziendelezwi na wananchi na hivyo kuupa mzigo serikali.

“Sasa hivi ili shule ya msingi isajiliwe lazima iwe na vitu vya msingi vinne, cha kwanza vyumba visipungue saba kwa maana ya darasa la kwanza mpaka la saba na cha pili kuwe na walau nyumba moja ya mwalimu kwasababu mwalimu mkuu lazima akae shuleni, lakini cha tatu lazima kuwe na vyoo vya makundi matatu vyoo vya wanafunzi wavulana na wasichana na vyoo vya walimu na cha mwisho ni viwanja vya michezo na hasa mpira wa miguu na “netball””, Alisema.

Shule Shikizi ya Kijiji cha Lyazumbi ina wanafunzi 375 wa darasa la kwanza hadi la tatu hali iliyomelekea Mtendaji wa Kijiji hicho Elizabeth Alex kuomba msaada wa nguvu za wananchi, serikali pamoja na wadau wa elimu nchini kusaidia ujenzi wa kumalizia shule hiyo.

MWANACHUO NCHINI MISRI AFUKUZWA CHUO KWA KUMKUMBATIA MWANAUME HADHARANI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MWANAMKE mmoja nchini Misri amefukuzwa chuo baada ya kuonekana akimkumbatia mwanaume katika moja ya video iloyosambaa katika mitandao.

Binti huyo amefukuzwa katika chuo cha Al -Azhar akishutumiwa kujidharilisha yeye na chuo baada ya kuonekana akimkumbatia mwanaume huyo katika video ambayo ilichukuliwa katika chuo cha Mansoura nchini humo.

Baraza la nidhamu la chuo cha Al- Azhar lililokaa siku ya jumamosi liliamua kumfukuza Chuo binti huyo, Msemaji wa baraza hilo Ahmed Zarie alieleza vyombo vya habari.

Imeelezwa kuwa video hiyo imeleta picha mbaya kwa chuo hicho kitu ambacho hakiruhusiwi aidha imefahamishwa kuwa kukumbatiana baina ya mwanamke na mwanaume ambao hawajaolewa sio maadili wala taratibu za jamii ya taifa hilo.

Kwa upande wa kijana aliyeonekana kwenye video, msemaji wa baraza hilo amesema kuwa watakaa leo jumatatu na kufanya maamuzi dhidi yake. 

Chanzo: Daily Mail

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKABIDHI MAGARI 10,PIKIPIKI 35 KWA LENGO LA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali nchini huku akisisitiza Serikali ya Awamu ya Tano imejikita kuboresha sekta ya huduma ya afya kwa Watanzania.

Magari na pikipiki amekabidhi leo Januari 14, 2019, Mwalimu amesema tukio hilo la kukabidhi rasmi Magari 10 na Pikipiki 35 kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo ni muhimu . 

"Kama mnavyofahamu bado nchi yetu inakabiliwa na janga la ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukoma. TB ni hatari kwani inasababisha vifo, na Ukoma husababisha vifo na ulemavu wa kudumu. TB pia inaongoza kusababisha vifo vingi miongoni mwa wananchi wenye VVU," amefafanua Waziri Mwalimu.

Ameongeza kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa TB wapatao 154,000 ambao kati yao ni 44% (69,818) tu ndio waliogunduliwa. Changamoto kubwa ni jinsi ya kufikishia wananchi wote huduma za kufanya uchunguzi na upimaji pamoja na kuwapatia elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo.

Ameongeza Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa inafanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa ugonjwa wa TB na kwamba mojawapo ya juhudi hizo ni pamoja na ununuzi wa mashine za kupima vinasaba vya Kifua Kikuu kitaalamu Gene-Xpert.

Ambapo zimeongezeka kutoka 64 mwaka 2015 hadi 210  Disemba 2018 na kufanya 85% (158/186)  ya Halmashauri zote nchini kuwa na  mashine hizi zinazoweza kupima TB kwa haraka na kwa ufanisi zaidi. 

"Mashine hizo hutoa majibu ndani ya saa 2 tofauti na kipimo cha Hadubini ambazho huto majibu baada ya saa 48. Lengo ni hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wilaya zote ziwe na mashine hizi. Kipimo hiki cha Gene-Xpert hutolewa bure," amesema.

Waziri Mwalimu amesema Serikali hiyo imepeleka huduma ya kifua kikuu sugu karibu kwa wananchi, huduma ambayo wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani ilikuwa inapatikana katika hospitali moja tu ya Kibong’oto lakini kwa sasa inapatikana katika vituo 81 katika mikoa 23. 

"Ni katika kuongeza juhudi hizi, Serikali kupitia Wizara imenunua magari 10 na pikipiki 35 tunazozikabidhi leo kwa lengo la kuhakikisha Waratibu hawa wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.

" Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538. Jumla ni  milioni 778. Mikoa inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa. 

"Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo ," amefafanua.

Pia amesema magari hayo na Pikipiki zinazokabidhiwa kwa uongozi wa mikoa vitasaidia katika usimamizi wa shughuli za Mpango, kuhakiksha wagonjwa wa TB na Ukoma wanapatiwa elimu, wanagunduliwa na kupatiwa matibabu.

 Amesema vyombo hivyo vitatumika kwa shughuli zinginezo za mikoa na wilaya zinazolenga kumfikishia huduma bora za afya mwananchi. Ametoa rai yake kwa uongozi wa Mikoa inayopatiwa vyombo hivyo vya usafirishaji vitumike kwa shughuli iliyokusudiwa kuimarisha huduma za Kifua Kikuu na Ukoma.

Amesisitiza vyombo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo na wanaamini kwamba Mikoa hiyo itaongeza kwa kasi ugunduzi wa wagonjwa wa Kifua Kikuu na kutokomeza ugonjwa wa Ukoma katika mikoa yenu. 

Ameongeza lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020 tunawaibua na kuwapatia matibabu asilimia 70 ya watu wanaougua TB kutoka asilimia 48 ya hivi sasa.

Waziri Mwalimu amesema kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma ni malengo ya Serikali kutokomeza ugonjwa huo katika Wilaya 20 zilizobakia ambazo ni Liwale, Mkinga, Nkasi, Lindi DC, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga Manispaa, Kilombero, Mafya, Pangani, Mvomero, Masasi, Chato, Mpanda TC, Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Ulanga, Morogoro DC na Kilwa DC.

Ametumia nafasi hiyo shukurani kwa  Mfuko wa Dunia (GF – ATM) kwani, fedha hizo ni sehemu ya mfuko huu wa mzunguko wa 2018 – 2020.
Baadhi ya piki piki kati ya 35 na Magari 10 yatakayosambazwa katika mikoa mbalimbali, zilizokabidhiwa leo jijini Dar na Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa uongozi wa mikoa kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ipasavyo. 

Mikoa 10 inayopatiwa Magari ni Pwani, Songwe, Ilala II, Kilimanjaro, Lindi, Kagera, Tabora, Mtwara, Ruvuma na Rukwa na Pikipiki 35 zinatolewa kwa Halmashauri 35 ambazo ni Nzega Mjini, Urambo, Kasulu, Ujiji Manispaa, Ngara, Kyerwa, Mkalama, Itigi, Msalala, Kishapu, Bariadi, Same, Mbarali, Kyela, Mbulu, Hanang, Chato, Mbozi, Ileje, Kilolo, Chamwino, Amana, Madaba, Wanging’ombe, Ilemela, Mpanda, Kalambo, Nanyumbu, Mtwara, Mbagala, Mburahati, Tanga Jiji, Muheza, Kilombero na Gairo.

Magari haya 10 yamegharimu kiasi cha Sh.Milioni 611,869,741 na Pikipiki 35, zilizogharimu Sh.milioni 167,042,538

 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu moja ya piki piki kati ya 35 zitakazosambazwa katika mikoa mbalimbali kwenye hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.
 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata ufunguo wa moja ya gari kati ya 10,yatakayosambazwa katika mikoa 10 ,hafla  ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar.Waziri Ummy amekabidhi magari 10 na pikipiki 35 kwa mikoa mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Waratibu wanawatumikia wananchi kwa kwenda kuhakikisha kama huduma zinawafikia kwa wakati.
 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye moja ya magari hayo kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi waandamizi wa mikoa mbalimbali leo jijini Dar.
  WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha pamoja na viongozi waandamizi wa mikoa mbalimbali waliokabidhiwa Piki piki 35 na Magari 10 leo jijini Dar.

BREAKING NEWS: MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA KIKATIBA ILIYOFUNGULIWA NA VYAMA PINZANI

$
0
0


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeitupilia mbali kesi ya kikatiba  iliyofunguliwa na viongozi wa vyama vya upinzani. ikiongozwa na kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo,  Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu CUF Bara Joram Bashange, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma ya CUF.Salim Biman ya kupinga muswaada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa uliochapishwa na gazeti la serikali ili kujadiliwa bungeni. 

Uamuzi huo umetolewa leo Januari 14, 2019 na Jaji Dr Benhajj Masoud ambaye amesema ameridhika na mapingamizi mawili ya awali yaliyowasilishwa na mwanasheria mkuu wa serikali.
Kupitia jopo la mawakili wa serikali sita, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipinga kesi hiyo kusikilizwa kwa vile waombaji waliunganisha maombi mawili kwa wakati mmoja yenye mtazamo na madhara tofauti.

Wananchi kata ya Kala wamlilia RC baada ya kukosa mawasiliano ya simu na radio

$
0
0
Wananchi wa kata ya Kala yenye vijiji vitano iliyopo katika wilaya ya Nkasi wamefikisha kilio chao cha kukosa mawasiliano ya simu kwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ili aweze kuwasaidia kutatua kero hiyo ambayo inakwamisha maendeleo ya kata

Kilio hicho kimetolewa wakati wa kusoma risala ya maendeleo ya kata na msoma risala Felix kapoze alipokuwa akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo kwa muda mrefu jambo linalokwamisha utendaji kazi pamoja na kufanya mawasiliano kuwa magumu.

“Changamoto nyingine kubwa ilipo hapa Kijijini kutokuwapo kwa mtandao wa simu, hii inapelekeana kukwama kwa taarifa nyingi hasa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hivyo tunaiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa itusaidie kupatikana kwa mtandao wa simu ili kurahisisha mawasiliano,” Alifafanua.

Halikadhalika jambo hilo liliungwa mkono na mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini Desderius Mipata wakati akielezea changamoto hiyo na hatua alizochukua kuhakikisha kuwa mawasiliano hayo yanapatinaka na hatimae kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za maendeleo katika kata hiyo.

“Hawa wananchi ni pekee ambao hawazungumzi na wenzao katika taifa na katika jimbo, juhudi nilizozifanya kama kiongozi wa jimbo ni kuitaka wizara ihakikishe kwamba tunapata mtandao, tunashukuru mungu wametusikiliza na sasa wanajenga minara miwili katika Kijiji cha kilambo cha mkolechi na Kijiji cha Kala, wanasema Kala itazungumza wantuambia katika kipindi kisichozidi miezi miwili,” Alibainisha.

Nae Wangabo aliwahakikishia wananchi wa kata hiyo kuwa mawasiliano yataimarishwa “Tutaimarisha hayo mawasiliano na juzi nilikuwa naongea na waziri wa ujenzi alikuja pale ofisini na tuliongea swala hili la minara ya mawasiliano, uzuri wameshaanza kufanyia kazi, kwahiyo tutaongeza nguvu kule ili mitandao ya mawasiliano ifanye kazi n ahata radio nkasi iweze kuwafikia huku,” Alisema.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (kushoto) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mpasa, Kata ya Kala mwambao wa ziwa Tanganyika Wilayani Nkasi
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpasa, Kata ya Kala mwambao wa ziwa Tanganyika Wilayani Nkasi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akiongea na mlemavu wa miguu aliyesimamisha msafara wa Mkuu huyo ili kumsalimia katika kijiji cha mlambo kilichopo katikati ya Kijiji cha Mpasa na Kingombe vilivyotengwa kwa kilometa 34 na hakuna mawasiliano ya simu wala radio katika Kata ya Kala  Wilaya ya Nkasi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akisalimiana na mlemavu wa miguu aliyesimamisha msafara wa Mkuu huyo ili kumsalimia katika kijiji cha mlambo kilichopo katikati ya Kijiji cha Mpasa na Kingombe  Kata ya Kala  Wilaya ya Nkasi.

Wafanyakazi wa Taasisi ya JKCI waadhimisha sherehe ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akikata keki ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 katika sherehe iliyofanyika  hivi karibuni kwenye  hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mchekeshaji Bob Shaw kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani akitoa burudani kwa wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 iliyofanyika  hivi karibuni kwenye  hoteli ya Protea Court Yard Sea view jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wageni waalikwa wakicheza mziki wa iyokote uliokuwa ukipigwa na bendi ya Cocodo African Music wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 iliyofanyika  hivi karibuni kwenye  hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania Veronica Romwald kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima  Asha Mwakyonde  kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha East Africa Oliver Nyeriga  kutokana na mchango wa kituo hicho  wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru Baraka Loshiraa kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view  iliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha  shukrani mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo  Regina Kumba kutokana na mchango wa gazeti hilo wa kutoa  elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view  iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wakurugenzi watano wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifungua Champaign wakati wa  sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo Septemba 5, 2015 iliyofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Protea Court Yard Sea view  iliyopo jijini Dar es Salaam. Picha na JKCI
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images