Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live

Muhimbili-Mloganzila yainyuka mabao 6 kwa nunge timu ya Albino United

0
0
Timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila (Mloganzila Sports Club) imeichapa mabao 6-0 timu ya Albino United ya Kibamba, mchezo uliyofanyika leo katika kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo chekundu jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo bao la kwanza lilifungwa dakika ya 18 kipindi cha kwanza na mchezaji machachari Jamal Msuya kutoka timu ya Mloganzila.
Wafungaji wa mabao mengine kutoka timu hiyo ya Mloganzila Sports Club ni Ashirafu Katenda, Edger Mtitu na Adam Kingwande wakati magoli mawili yalifungwa na Goodluck Manji.

Katika mechi hiyo wachezaji wa Mloganzila walionekana kumiliki mchezo na kuhakikisha timu yao inaibuka na ushindi mnono.Hadi dakika tisini timu ya Albino United haikuweza kutikisa nyavu za wapinzani wao ambao ni Mloganzila Sports Club.

Awali kabla ya kuanza kwa mechi hiyo Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Dkt. Mohamed Juma Mohamed amewapongeza wachezaji wote kwa kushiriki mchezo huo wa kirafiki ambao unadumisha umoja na kulinda afya.

Dkt. Mohamed amewaeleza wachezaji hao kwamba uongozi wa hospitali utaendelea kushirikiana nao bega kwa bega ili kuhakikisha michezo inaendelea kudumishwa.

Vilevile Hospitali ya Mloganzila imewapatia timu ya Albino United msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mafuta maalum ya kupaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) pamoja na vifaa vya huduma ya kwanza.

Naye Mwenyekiti wa timu ya Albino United Mohamed Kidunyo ameushukuru uongozi wa hospitali kwa kukubali kushiriki mchezo wa kirafiki sambamba na kuwapatia msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni muhimu katika kulinda ngozi zao hasa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).


Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Dkt. Mohamed Juma Mohamed akiwasalimia wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Muhimbili-Mloganzila na timu ya Albino United ya Kibamba jijini Dar es Salaam
Mchezaji wa timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Jamal Msuya akiifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo uliochezwa katika Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park , Kidondo chekundu jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Muhimbili tawi la Mloganzila akipiga kichwa katika mchezo muda mfupi baada ya timu yake kufunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza
Mmoja wa wachezaji wa timu ya Albino United akikokota mpira baada ya kuwatoka wachezaji wa timu ya Muhimbili tawi la Mloganzila.
Kapteni wa Timu ya Albino United, Suleiman Mussa akiwapatia maelekezo wachezaji wa timu yake wakati wa kipindi mapumziko.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Dkt. Mohamed Juma Mohamed akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji hao
Dkt. Mohamed Juma Mohamed akiwapatia wachezaji wa timu ya Albino United msaada wa mafuta maalum ya kupaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja vifaa vya huduma ya kwanza. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

MBUNGE 'SUGU' AMVALISHA PETE YA UCHUMBA HAPPYNESS MSONGA JIJINI DAR

0
0


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' leo amemvisha pete ya uchumba Happyness Msonga, shughuli iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiambatana na mbunge huyo kutoa mahari.


TFDA yajivunia kuipaisha Tanzania kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti,kuifanya nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hiyo

0
0
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema katika kipindi Cha Miaka mitatu imefanya mambo mbalimbali ya udhibiti wa usalama, ubora na usalama wa bidhaa za ndani na nje ya Nchi ikiwemo kutambulika kimataifa kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya ISO 9001: 2015.

Hii ni kutokana na mafanikio ya miaka mitatu ya utekelezaji wa kazi chini ya Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Adam Fimbo amebainisha hayo wakati akitoa ripoti ya miaka mitatu ya Mamlaka hiyo wakati wa ziara maalum ya Maafisa Mawasiliano na habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

"Kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, mnamo Mwezi Desemba 2018, TFDA imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vipodozi, ambapo hatua hii imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hii

Fimbo ameeleza kuwa, TFDA katika mikakati yake hiyo imeweka mifumo na taratibu za ndani za utoaji huduma na utendaji bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ISO 9001:2015 kwa huduma za kawaida na ISO 17025:2005 kwa huduma za maabara. 

Aidha, ameongeza kuwa huduma za TFDA hutolewa kwa kuzingatia viwango vya Mkataba wa Huduma Wateja kama ulivyorejewa mwaka 2016. "Mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18.

Pia tumesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Hii imetokana na kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara." Ameeleza Fimbo.

Aidha, Fimbo ameongeza kuwa TFDA imekuwa ikifanya tathmini na usajili wa bidhaa kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama, ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko."Kuwepo kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.

Pia tumeweza kusajili maeneo ya biashara za bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa lengo la kutambua maeneo ambayo bidhaa hizo zinazalishwa, kuhifadhiwa, kusambazwa na kuuzwa. Mfumo huu husaidia kuhakikisha kuwa maeneo husika yanakidhi vigezo ili kutoathiri usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa". Alieleza Fimbo.

Aidha ameongeza kuwa, TFDA katika kipindi cha miaka mitatu (2015/16 – 2017/18), imeweza kusajili jumla ya maeneo 25,630 ya biashara za bidhaa zinazodhibitiwa ikiwa ni pamoja na maeneo 9,000 yaliyosajiliwa mwaka 2016/17 na maeneo 5,606 mwaka 2015/16, hii ikiwa ni sawa na ongezeko la 60.5%.

Aidha, katika kipindi hiki, TFDA imeendelea kushuhudia kufikiwa kwa dira yake ya kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuvutia nchi mbalimbali kuja kujifunza mifumo iliyopo na kwenda kuitekeleza nchini kwao.

(mfano nchi za Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana, Mauritius, Lesotho na Bangladesh zinekuja kujifunza TFDA).
"Katika kipindi cha mwaka 2015/16 - 2017/18, Mamlaka imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika utekelezaji wa mipango kazi yake.

Mamlaka katika kipindi cha 2017/18 itaendelea kutoa kipaumbele katika utekelezaji kwa ufanisi wa malengo mahususi nane (8) yaliyomo katika Mpango Mkakati mpya wa miaka mitano (5) yaani 2017/18 – 2021/22, ili kulinda afya ya jamii." Alieleza Fimbo.

Mafanikio mengine ni pamoja na kukamilika kwa jengo la Maabara na kufungwa kwa vifaa vya kisasa vya uchunguzi jijini Mwanza jambo ambalo limesaidia kusogeza huduma zaidi kwa jami.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Adam Fimbo akizungumza na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zake zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya kwa ziara kwa taasisi hizo pamoja na Hospitali kuangalia uwekezaji katika Sekta hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Meneja wa Maabara ya uchunguzi na bidhaa nyongeza wa TFDA Dkt Yonah Hebron akizungumza wanavyofanya uchunguzi wa dawa wakati Maafisa wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto wakiwa katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
Fundi sanifu wa Maabara Mkuu Oscar Kandege akizungumza namna wanavyofanya uchunguzi wa vifaa tiba kutokana na serikali ilivyowezesha kununua vifaa vya kisasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Sehemu ya Maabara ya uchunguzi.
Upimaji wa kifaa tiba kondomu unavyofanywa katika kuhakikisha mwananchi anapata bidhaa bora katika kulinda afya.
Mchunguzi wa Vifaa tiba wa TFDA Geovin Mgoyela Akizungumza na maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walipotembelea TFDA kuangalia uwekezaji uliofanywa na serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Kaimu Meneja wa Mikrobailojia Catherine Luanda akizungumza kuhusiana na uchunguzi wanaofanya wa dawa na vyakula wakati Maafisa Uhusiano wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto walipotembelea TFDA katika kuangalia uwekezaji uliofanywa katika Maabara hiyo katika utoaji wa huduma bora za kulinda walaji.

'YES WE CAN' YAIPA SIMBA USHINDI WA 3-0 DHIDI YA JS SAOURA, DK.MWAKYEMBE ATOA NENO KWA MASHABIKI WA SOKA TANZANIA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

YES We Can!Ndivyo unavyoweza kuuzungumzia ushindi wa timu ya Simba wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya JS Saoura katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Slaam.

Kabla ya mchezo huo uliofanyika jana jioni ya Januari 12,2019 ,Simba kupitia Msemaji wake Hajji Manara walizundua kampeni ya Yes we can ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili inasema Ndio Tunaweza kwa lengo la kuhakikisha wanashinda mchezo huo na ndicho kilichotokea.

Umahiri,umaridadi wa pasi, akili ya soka na kila aina ya udambwidambwi kwa wachezaji wa Simba ulitosha kuwafanya wachezaji wa timu ya JS Saoura kushindwa kumiliki vema mpira na hivyo wachezaji wa Simba kuonekana kuumiliki kila idara.

Dakika ya 45 mshambuliaji nyota wa Simba Emmanuel Okwi alipeleka shangwe,nderemo na vifijo kwa Simba na mashabiki wa soka nchini baada ya kupachika bao la kwanza.Uwanja mzima ulizizima kwa shangwe kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa Simba .Hivyo wakati wanakwenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja.

Katika mchezo huo wachezaji wa JS Saoura walionekana kutohimili stamina za wachezaji wa Simba kwani mara kwa mara walionekana wakianguka.
Kipindi cha pili cha mchezo huo kilianza kwa kasi huku kwa Simba wakiwa na hamu ya kutaka kuongeza mabao wakati JS Saoura nao wakionekana kutaka kusawazisha.

Hata hivyo kwa Simba ambao walioonekana kuendelea kulisakama lango la wapinzani wao. Kutokana na kusakata kabumbu vema Simba walifanikiwa kupata mabao mengine mawili kupitia kwa mchezaji wake Medie Kagere.
Hakika ushindi wa Simba uliwafanya mashabiki wa soka kuwa na furaha ambapo kila aliyeuzungumzia mchezo huo wameonesha kuwa na matumaini na timu hiyo kufanya vema kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Michuzi Blog ilipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe ambapo ameuzungumzia mchezo huo na kwamba ameridhishwa na kiwango cha Simba ambacho wamekionesha uwanjani hapo.

"Kwa leo mimi ni mshibaki wa Simba,na ikitokea kesho timu yetu nyingine ikacheza na timu ya nje ya Tanzania nitakuwa kwa timu ya nyumbani.Simba wamecheza vizuri sana leo," amesema Waziri Mwakyembe.

Alipoulizwa anatoa ujumbe gani kwa mashabiki wa soka nchini,Waziri Mwakyembe amejibu kuwa ni vema kuwa na uzalendo na timu za nyumbani zinapocheza na timu za nje."Tuwe wamoja timu zetu zinapocheza na timu kutoka nje.Ndio maana leo nilikuwa naishangilia Simba."

WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA WADAU WA UTEKELEZAJI MRADI WA KUENDELEZA TASNIA YA MBEGU NCHINI

0
0




Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 12 Januari 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa kuendeleza tasnia ya mbegu nchini. 

Katika Kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo I Jijini Dar es salaam pamoja na wadau kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu (TOSCI), na Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), vilevile walialikwa wadau kutoka Bill & Melinda Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience. 

Akizungumza katika kikao kazi hicho Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuongeza matumizi ya teknolojia ikiwemo mbegu bora. 

Alisema pamoja na mambo mengine serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli imjidhartiti katika kuhakikisha kuwa nchi inajitosheleza kwa mafuta ya kula na hivyo serikali inataka mradi huo kuondoa chanagmoto katika sekta ya mbegu kwa kuzalisha mbegu za mafuta hasa za alizeti na michikichi. 

Mhe Hasunga amewapongeza wadau kutoka Bill & Melinda Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania kutekeleza mradi huo.

WATENDAJI MKOANI SINGIDA WATAKIWA KUANZISHA VITUO VYA MKONO KWA MKONO KUOKOA WAATHIRIKA WA UKATILI

0
0

  Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akifungua kikao kazi cha kuandaa jumbe za kuelimisha jamii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku na wa kwanza kushoto ni Bw. Christopher Mushi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya wanao kaa mjini singida kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Bw. Christopher Mushi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii akitoa mada kuhusu Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.



Na Anthony Ishengoma -Singida

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka watendaji wa serikali Mkoani Singida kuanzisha vituo vya Mkono kwa Mkono (One Stop Centres) ili waanga vitendo vya ukatili waweze kupata huduma kwa haraka tofauti na sasa wanapokumbana na mlolongo wa taratibu unaochangia kupotea kwa ushaidi.

Dkt. Lutambi amesama hayo leo mjini Singida wakati wa kikao chake na baadhi ya watendaji wa mkoa wake wanaotengeneza jumbe za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.

Aidha Dkt. Lutambi amewataka watendaji hao kutengeneza jumbe ambazo zitatoa elimu pamoja na mambo mengine itawawezesha waanga wa ukatili kupata mahali pa kukimbilia ndio maana amewaagiza kuanzisha vituo vya mkono kwa mkono kwa lengo la kuwapatia huduma ya haraka waanga hao.

Aidha alitaja urasimu na taratibu ngumu zinazojitokeza baada ya muanga wa ukatili kufika katika vituo vya polisi ambapo waanga wanalazimika kufuata PF3 pamoja na kufuata milolongo ya kumuona daktari jumbo ambalo lianasababisha baadhi ya waanga kukata tamaa na wengine kurubuniwa na kubadili mawazo hivyo kuacha vitendo hivyo viendelee kutokea.

‘’Muhanga wa ukatili anapofika polisi anadaiwa PF3 akifika hospitali anakuta Daktari wa zamu hayupo na wakati mwingine akifika polisi anaambiwa polisi wako doria jambo linalotoa mwanya wa kushawishiwa na watendaji wasio kuwa waadilifu na hatimaye kubadili mawazo’’. Aliendelea kusema Dkt. Lutambi.

Aidha Dkt. Lutambi pia amewataka ndugu pamoja na raia wema kushirikiana na madawati ya jeshi la polisi kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili kwa kutoa ushaidi mahakamani kwani kesi nyingi mahakamani zinakwama kutokana na kukosa ushahidi.

Kwa mantiki hiyo basi mewataka watendaji hao kuweka mifumo imara itakayowezesha watendaji na waanga wa ukatili kufanikisha kukomesha vitendo vya ukatili sio tu kwa Mkoa wa Singida bali pia Tanzania nzima.

Wakati huo huo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku wakati akiongea na vyombo vya habari ameutaja Mkoa wa Singida kuwa ni miongoni mwa mikoa mitano Nchini Tanzania inayoongoza kwa ukeketaji.

Ameitaja mila ya ukeketaji kama mojawaopo ya mila inayopaswa kuachwa kwa kuwa inaacha makovu ya kisaikoloijia kwa mtu anayepata kufanyiwa tohara lakini pia ina madhara katika suala zima la Afya ya uzazi kwani mlengwa anaweza kupoteza maisha wakati wa kujifungua.

Aidha Mkurugenzi huyo amewataka wananchi mkoa wa Singida kubadilika kifikra na kuacha vitendo vya ukatili ambavyo kwa mazingira ya ulimwengu wa kisasa hayana na nafasi tena.

Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inaendelea itaendelea katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa.

KAMPUNI YA MOOVN DRIVER YATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA HANANASIFU

0
0
KAMPUNI Ya usafirishaji abiria ya Moovn Driver kwa kushirikiana na umoja wa madereva wa mtandao (TODA), leo wametoa msaada wa vyakula na mavazi kwa kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Hananasifu, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa Umoja wa Madereva wa Mtandao (TODA), Fredy Peter, amesema kuwa msaada huo umelenga kuwapatia nafuu katika mazingira waliyomo na akatoa wito kwa makampuni na taasisi zingine ziige mfano huo kuwasaidia watu wenye mahitaji, hasa watoto wanaoishi kwenye vituo vya mayatima.
Baadhi ya wawakilishi kutoka kampuni ya usafirishai abiria ya Moovn Driver wakishirikiana na umoja wa madereva wa mtandao (TODA), wenye T-shirt nyeusi, wakimkabidhi msaada mwanamama Zainab Bakari ambaye ni mlezi wa kituo cha watoto yatime cha Maunga cha Hananasifu, Kinondoni, Dar.

 
Wakipeana mkono ikiwa ishara ya kufurahia kukutana na watoto yatima.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIVYONOGESHA USHINDI WA SIMBA SC HAPO JANA UWANJA WA TAIFA

0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wapenzi wa mpira wa miguu alipofika kushuhudia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Januari 12, 2019. Katika mechi hiyo Timu ya Simba ilishinda goli 3-0 dhidi ya JS Saoura.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia goli la pili la Simba, wakati akiangalia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, wakati alipowasili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kushuhudia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria, Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, wakati alipowasili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kushuhudia Mechi kati ya Simba SC na JS Saoura ya Algeria, Januari 12, 2019. Timu ya Simba iliibuka mshindi wa goli 3-0 dhidi ya JS Saoura. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


MAJANGILI WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KUKIONA -NAIBU WAZIRI AWESO.

0
0
Na Abdullatif Yunus - Kagera

Kutokana na ukosefu wa huduma ya Maji katika baadhi ya maeneo Nchini, ambayo miradi ya Maji kuharibiwa na kuhujumiwa na Majangili wa miundo mbinu ya Maji, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza Viongozi kuweka Ulinzi madhubuti kwa ajili ya kulinda wahujumu hao na pindi watakapobainika sheria ifuate mkondo wake.

Akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani Ngara jana Januari 12,2019, Naibu Waziri Aweso amesema Serikali imekuwa ikiwekeza pesa nyingi kwa miradi mbalimbali ya Maji hapa Nchini, lakini miundo mbinu ya miradi hiyo imekuwa ikiharibiwa na wakati mwingine kuibwa na wale alowaita Majangili wa Maji.

 Katika ziara hiyo Naibu Waziri Aweso ametembelea mradi wa Maji unaosukumwa kwa Nishati ya Umeme unaohudumia Vijiji vya Muhweza na Murugarama. Mradi huo Ulioanza Mwaka 2014, ni miongoni mwa Vijiji 10  chini ya programu ya Sekta ya Maji (WSDP) wenye gharama zaidi ya Shilingi Milioni 559.
 Pichani ni Mtoto Zainabu Mohammed Mkazi wa Muhweza akisuuza Ndoo kabla ya  Maji kama alivyokutwa na Kamera yetu.
 Pichani ni Bi. Zubeda Baraka Mkazi wa Muhweza Wilayani Ngara, akifurahia huduma ya Maji iliyosogezwa karibu baada ya kuteseka kwa muda  kufuata Maji umbali mrefu.
 Tanki la Maji la Mradi wa Vijiji vya Muhweza na Murugarama unaoendelea kujengwa na Unatarajiwa kuzinduliwa Machi mwaka huu unaogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 559.
 Pichani Mh. Aweso akiwa juu ya Tanki la Maji linaloendelea kujengwa likiwa katika hatua za mwisho licha ya kuanza kuhudumia mradi huo.
Mh. Aweso Naibu Waziri wa Maji akinawa mkono katika Tanki kwenye mradi wa Maji wa Muhweza - Murugarama alipotembelea mradi huo mapema Januari 12, 2019.
index
Naibu Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso (MB) akishiriki kazi ya kutandaza mabomba ya maji katika mradi huo unaotekelezwa katika vijiji vya  Kabalenzi-Kanazi
index
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na Kaimu Mhandisi wa Wilaya ya Ngara, Simon Ndyamukama kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kabalenzi-Kanazi.

TAARIF YA WITO KWA WADAU KUTOA MAONI KUHUSU MISWADA MITANO YA SHERIA

TPSC YATAKIWA KUTOA MAFUNZO YATAKAYOWAWEZESHA WATUMISHI WA UMMA KUBORESHA HUDUMA KWA WANANCHI

0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao makao makuu ya TPSC jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Henry Mambo, akieleza majukumu ya TPSC kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa TPSC cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Makao Makuu ya chuo hicho jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo na Mtendaji

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikagua daftari la mmoja wa wanachuo wa Chuo cha Utumishi alipowatembelea wanafunzi hao katika moja ya madarasa ya Kampasi ya Dar es Salaam. Dkt. Mwanjelwa ametumia fursa hiyo kuwaasa wanachuo hao kusoma kwa bidii ili wawe watumishi wa umma bora hapo baadae.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akijaribu kutumia mashine ya kupiga chapa (typewriter) inayotumiwa kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa TPSC alipotembelea moja ya darasa katika Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwahimiza wanachuo wa TPSC waliopo maktaba kutumia vema maktaba hiyo ya chuo kujisomea ili kuongeza uelewa wa masomo wanayosoma, alipoitembelea maktaba hiyo iliyopo Chuo cha Utumishi Utumishi wa Umma Kampasi ya Dar es Salaam.



Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kila mmoja kwa nafasi yake wametakiwa kutoa mafunzo bora yenye kuzingatia weledi, yatakayowajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa umma wanaopata fursa ya kujiendeleza katika chuo hicho ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa TPSC makao makuu na Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu majukumu ya TPSC na kujiridhisha na utendaji kazi wa chuo hicho.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza watumishi wa TPSC kuwa wabunifu kwa kuboresha mitaala itakayowaandaa vema watumishi wa umma, sekta binafsi na wananchi wanaohitimu katika chuo hicho ili waweze kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa. Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, katika ulimwengu wa sasa jamii inabadilika, uchumi unabadilika na siasa zinabadilika pia, hivyo amewataka watumishi wa TPSC wabadilike ili utendaji wao uwe wenye kujali matokeo na wenye tija.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa alipata fursa ya kutembelea madarasa ya Kampasi ya Dar es Salaam ili kujionea vitendea kazi na kuzungumza na wanachuo ambao walimueleza kuwa, wanaridhika na elimu inayotolewa hivyo watatumia elimu na ujuzi wanaoupata katika kulitumikia taifa.

Naye, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Henry Mambo amesema, TPSC ilianzishwa ili kusaidia zoezi la kujenga uwezo wa watumishi wa umma uwe wenye kujali matokeo katika kutoa huduma bora kwa umma na kuongeza kuwa, kwa sasa chuo kina matawi sita yaliyopo Dar es Salaam, Mtwara, Singida Tabora,Tanga na Mbeya.

Dkt. Mambo amefafanua kuwa, madhumuni makubwa ya kuanzisha chuo ilikuwa ni kuziba pengo lililokuwepo la kukosekana kwa chuo rasmi kinachoshughulikia mafunzo ya watumishi wa umma ili waendane na mabadiliko yaliyoletwa na maboresho katika utumishi wa umma na kuongeza kuwa lengo lingine lilikuwa ni kusaidia, kukuza na kuboresha stadi za wafanyakazi, kubadili mtazamo juu ya utendaji wa watumishi wa umma katika suala zima la utoaji huduma bora kwa umma unaolenga kukuza uchumi na kuondoa umaskini kupitia mafunzo ya muda mfupi na mrefu.

Dkt. Mambo ameainisha kuwa, tangu chuo kianzishwe mwaka 2000 kimeweza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 61,221 katika nyanja ya uongozi, menejimenti na utawala .Aidha, Dkt. Mambo amesema kuwa, chuo kimeruhusiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa sekta nyingine ikiwemo sekta binafsi iwapo wana mahitaji ya kupata mafunzo ya kuwawezesha kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ni Wakala wa Serikali iliyoanzishwa mwaka 2000 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1997. Kuanzishwa kwa Chuo cha Utumishi kunafuatia muungano wa Chuo cha Watumishi wa Serikali, Dar es Salaam (Civil Service Training Centre) na kilichokuwa Chuo cha Uhazili Tabora (Tabora Secretarial College). Chuo cha Utumishi wa Umma kipo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AHUDHURIA TAARAB YA KUADHIMISHA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KISWANI PEMBA

0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Mhe.Balozi Ali Karume, wakifuatilia moja ya nyimbo ya kikundi hicho “Wakezi na Wakulima ” iliokuwa ikiimbwa na Msanii. Makame Faki, wakati wa hafla hiyo iliofanyika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwanachama wa CUF Mbunge Mstaaf Mussa Haji Kombo, baada ya kumaliza hafla ya Taraab rasmi ya kusherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tiborinzi Chakechake Pemba.kushoto Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe. Profesa Ibrahim Lipumba, wakiagana baada ya kumalizika kwa Taarab, jana usiku.12-1-2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Mhe. Balozi Ali Abeid Karume, baada ya kumalizika kwa hafla ya Taraab rasmin ya kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Chakechake Pemba,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Chakechake Pemba, wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa na Kikundi cha Taraab cha Taifa, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Waziri wa Vijana Michezo,Utamaduni na Sanaa.Mhe. Balozi Ali Karum, wa mwisho Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.
BAADHI ya Mawaziri Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wananchi wakiwa wamesimama wakati wa kupigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Taraab Rasmin ya kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar iliopigwa na Kikundi cha Taraab cha Taifa Zanzibar.
BAADHI ya Wananchi waliokuwa wakihudhuria hafla ya Taraab rasmin ya kusherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiwa katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi Pemba wakifuatilia hafla hiyo.(Picha Ikulu)
MSANII wa Kikundi cha Taifa cha Tarab Zanzibar Bi. Amina Abdallah, akiwa jukwaani akiimbo “Wimbo Umewashuka) wakati wa hafla hiyo ya musherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika Uwanja wa Tibirinzi Pemba jana usiku.(Picha na Ikulu)

WAZIRI LUGOLA, MWAKILISHI UNHCR WAJADILIANA MASUALA YA WAKIMBIZI WALIOPO NCHINI, JIJINI DAR LEO

0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) alipokua anamfafanulia wakati walipokuwa wanaagana mara baada ya kumaliza kikao chao cha kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, wapili kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa UNHCR, Zephania Amuiri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya, mara baada ya kumaliza kikao chao cha kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, na wapili kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa UNHCR, Zephania Amuiri. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya, ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, na kujadiliana masuala mbalimbali ya wakimbizi nchini.

Waziri Lugola pamoja na Mwakilishi huyo, pia walijadiliana masuala ya ushirikiano kati ya Serikali na Shirika hilo la Kimataifa kwa mujibu wa sheria zinazowaongoza.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Jumapili, Lugola alisema Wizara yake haiwezi ikafanikiwa kikamilifu katika masuala ya kuwahudumia wakimbizi nchini kama haitashirikiana ipasavyo na UNHCR.

“Licha ya kuwa baadhi ya wakimbizi wanaendelea kurudishwa kwa hiari nchini kwao Burundi, lakini katika kufanikisha zoezi hili, lazima tushirikiane ipasavyo kati ya Serikali pamoja na nyie UNHCR, naamini Wizara yangu itafanya vikao nanyi mara kwa mara ili kufanikisha zoezi hilo pamoja na mengineo yanafanikiwa,” alisema Lugola.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNHCR, Kapaya, alisema Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika lake vizuri, na jambo lolote la majadiliano linapotokea ujadiliana ili kuweka sawa ushirikiano huo. “Mheshimiwa Waziri mimi nakushukuru sana kwa kuniruhusu kuja kufanya mazungumza nawe, nimefarijika na haya madiliano na pia tutaendelea kushirikiana zaidi,” alisema Kapaya.

Katika kikao hicho Mwakilishi wa UNHCR aliambatana na Msaidizi wake Zephania Amuiri, na Waziri Lugola aliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara yake, Harrison Mseke

SERIKALI HAITABOMOA NYUMBA ZA WATU WALIOJENGA KATIKA MAKAZI HOLELA

0
0
Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kwamba Serikali ya awamu ya tano kuanzia sasa haitabomoa tena nyumba za wananchi waliojenga maeneo ya makazi yasiyo rasmi badala yake itarasimisha makazi holela.

Waziri Lukuvi amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa fursa kwa wananchi wote masikini waishio mijini waliojenga bila ya kufuata mipango miji na hawana hatimiliki za ardhi kufanyiwa urasimishaji wa makazi yao na wasibomolewe nyumba zao tena kwakuwa haikuwa ni makosa yao kujenga maeneo hayo.

Lukuvi ameyasema hayo alipokuwa wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara alipofanya ziara yake ya kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi kwa wakazi wa mji huo, ambapo amesema wananchi wote wachangamkie fursa hii iliyotolewa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwapa fursa ya kumiliki hati katika maeneo ambayo siyo rasmi kwa kurasimishiwa.

“Serikali ya awamu ya tano inajali sana wananchi wake kwakuwa zamani wananchi ambao hawakujenga kwa kufuata mipango miji wangebomolewa nyumba zao, lakini kwa sasa Serikali ya awamu ya tano imeanzisha mpango kurasimisha makazi holela na kuwapatia hati wananchi wote waishio mijini ili waishi katika makazi rasmi” Amesema Lukuvi.

Aidha, Lukuvi amewataka wananchi wote waishio mijini kuwa wazalendo kwa kurasimisha maeneo yao waweze kujipatia hati na ili walipe kodi ya pango la ardhi jambo ambalo litaiongezea Serikali mapato.

Lukuvi alipokuwa ziarani Simanjiro mwishoni mwa wiki aligundua kuwa wakazi wa mji wa Simanjiro walio na hatimiliki za ardhi hawazidi 1,000 wakati nyumba zilizopo ni nyingi zaidi ya idadi hiyo. Hivyo Waziri Lukuvi akawataka wachangamkie fursa hii ya kujipatia hati ili kuzipa hadhi nyumba zao.

“Nyumba isiyokuwa na hati haina thamani kwakuwa hata ukienda Benki kukopa pesa hawatakuuliza umejenga nyumba ya uzuri gani, lakini watakachotaka ni hati yako ya kumiliki ardhi ambacho ndio kitu kilicho na thamani zaidi kwako kuwa nacho” aliongeza Lukuvi.

Naye Mbunge wa Simanjiro Mheshimiwa James Ole Millya ambaye amehamia CCM akitokea Chadema amemshukuru Mhe. Lukuvi pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwajali wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo makubwa na kusimamia suala la wananchi wa kawaida kupata fursa ya kumiliki ardhi kutoka kwa wawekezaji wakubwa ambao walikuwa hawayaendelezi mashamba yao kwa muda mrefu.

Simanjiro ndio wilaya inayoongoza kwa wamiliki wa mashamba makubwa walio na hati na hata wengine wasio na hati rasmi. Kwa sasa wamiliki wa mashamba walio na hati rasmi wanafika 158 yaliyo na hekari zaidi ya 120,000 ambapo wasio na hati ni zaidi ya hao, hivyo Waziri amenza utaratibu wa kufuta mashamba makubwa 55 yanayomilikiwa kwa kuwa wamiliki wake wamekiuka masharti ya umiliki.
Waziri Lukuvi

Top Natural Pain Killer


Miaka 40 bila Mbaraka Mwinshehe Mwaruka

0
0
Na John Kitime.

Jumanne, 27 Juni 1944, vita ya pili ya dunia ilikuwa bado inaendelea sehemu nyingi za dunia huko Morogoro siku hiyo alizaliwa mtoto wa pili wa Mzee Mwinshehe Mwaruka. Mzee Mwinshehe Mwaruka alikuwa karani katika mashamba ya mkonge na hatimaye alikuja kupata watoto 12. 

Mzee Mwaruka alikuwa Mlugulu lakini mke wake alikuwa Mngoni. Mtoto aliyezaliwa siku hiyo alipewa la Mbaraka. Kutokana maelezo ya familia, babu yake Mbaraka alikuwa wa kabila la Wadoe wa Bagamoyo na alipelekwa Mzenga akawe Jumbe wa huko na wakoloni. Alipofika huko mzee huyo alioa wake tisa na kupata watoto zaidi ya hamsini akiwemo baba yake Mbaraka, Mzee Mwinshehe Mwaruka. 

Mbaraka Mwinshehe alililewa vizuri na kupelekwa shule, talanta yake ya muziki ilijitokeza zaidi alipoanza sekondari. Alianza kushiriki katika maonyesho ya Morogoro Jazz tangu akiwa shule, wakati huo alikuwa akipiga filimbi wakati bendi hiyo ikipiga nyimbo za mtindo wa ‘kwela’. Mtindo huu wa kwela ulitoka Afrika ya Kusini, na ulipata umaarufu kutokana na wapulizaji mahiri wa filimbi na saxaphone kama Spokes Mashiyane. Uchezaji wa muziki huu wa kwela uliitwa Jiving. 

Vijana walitengeneza makundi mengi ya kucheza jiving wakati huo na hasa katika shule za sekondari. Jiving ilikuwa ni mtindo wa kundi kuimba na kucheza kwa ‘steps’ zilizoigwa kutoka kwa wasanii wa Afrika ya Kusini zikisindikizwa na muziki wa filimbi. Kwa zama hizi unaweza kulinganisha jiving na Kwaito.

Kila wikiendi Mbaraka alishiriki katika maonyesho ya Morogoro Jazz Band akiwa anapiga filimbi, wakati huo akiwa bado shule. Ili kuhudhuria maonyesho haya Mbaraka alilazimika kutoroka bwenini kwake usiku siku za maonyesho. Hatimae siku moja iligundulika kuwa kuwa yeye na wenzie kadhaa walikuwa wametoroka usiku, kesho yake walipewa adhabu ya kupigwa viboko mbele ya wenzao. Mbaraka aligoma  adhabu hiyo na siku moja baadae aliacha shule. 

Hiyo ilikuwa mwaka 1965.
  Mbaraka aliacha shule na mawazo yake yakiwa ni kuondoka Morogoro na kuelekea Dar es salaam kutafuta bendi ya kujiunga, lakini alipopita kwenye jengo la klabu ya Morogoro Jazz Band ili kuwaaga, wanamuziki waliokuwepo walimshawishi apumzike kwanza pale kwenye klabu ajifikirie uamuzi wake wa kuhamia Dar es Salaam. Kesho yake wanamuziki walipofika klabu walishangaa kumkuta Mbaraka akifanya mazoezi ya gitaa kwani walikuwa wakimfahamu kama mpiga filimbi.

 Kwa kuwa wakati huo walikuwa na shida ya mpiga gitaa la rhythm walimsihi aachane na mipango ya safari ya Dar es Salaam na abaki kwenye bendi kama mpiga rhythm, akakubali. Wakati huo katika bendi ya Morogoro ni wapiga tarumbeta, saxaphone na gitaa la solo pekee ndio waliokuwa wanalipwa mshahara kwa mwezi, wengine wote walipewa posho kidogo kila lilipopigwa dansi, hivyo Mbaraka nae akaingia katika mfumo wa kupewa posho kwa kazi yake. Siku moja Moro Jazz walialikwa Dar Es Salaam kwa ajili ya mashindano na bendi ya Kilwa Jazz, kulikuwa na utamaduni wakati huo wa bendi kualikana kufanya mashindano, lakini kabla ya kuondoka Mbaraka aligoma kwenda kwa kuwa alikuwa halipwi mshahara, wazee wa bendi wakakubali kumlipa shilingi 120 kwa mwezi, mpiga solo ambaye alikuwa akilipwa shilingi 150  akaja juu na akagoma kwenda Dar kwa kusisitiza kuwa kwa taratibu za bendi hiyo, mpiga rhythm hastahili malipo. 

Bendi ikawa katika sintofahamu na hasa kwa kuwa kulikuwa na huo mwaliko wa mashindano. 
Hatimae  Mbaraka akasema safari iendelee yeye angepiga solo, basi bendi ikaamua kwenda Dar ikiwa na mashaka kwani Kilwa Jazz Band wakati huo ilikuwa ni bendi maarufu yenye nyimbo nyingi zilizopendwa nchini, na wao walikuwa wakienda bila mpiga solo.

Kwenye mpambano huo Mbaraka alilipiga vizuri sana gitaa la solo na Moro jazz ikashinda. Mbaraka akapandishwa mshahara hadi shilingi 250 kwa mwezi, kiwango ambacho kilikuwa juu sana wakati huo. na kuanzia hapo mpaka alipoacha bendi na kwenda kuanzisha bendi yake Super Volcano, Mbaraka akawa mpiga solo mkuu wa Morogoro Jazz Band.

Upigaji wake wa gitaa, mpaka leo bado ni darasa zuri sana kwa mpigaji anaetaka kujiendeleza katika upigaji wa gitaa la solo. Hata kwa kufanya mazoezi nyimbo zake nyingi alizorekodi ni zoezi kubwa sana kwa mtu anayetaka kujiendeleza katika upigaji wa gitaa la solo. Katika vipindi vyake vya kuanzia Morogoro Jazz hadi Super Volcano alipitia staili nyingi za upigaji wa gitaa lake la solo, baadhi ya staili za bendi ya Morogoro kama Sululu, Likembe, Masika Zolezole na kadhalika, zote zilionyesha upigaji tofauti kwa kila mtindo, haikuwa kubadili jina tu la staili, tofauti na bendi nyingi ambazo hubadili majina ya mitindo bila kubadili muziki wenyewe. 

Hivyo staili ya upigaji wa solo katika staili ya Likembe ilikuwa tofauti na  Masika Zolezole. Kipindi hicho wapenzi wa muziki walikuwa wakifunga safari kwenda Morogoro kufaidi wiki endi ya muziki kutoka kwa mojawapo ya bendi kubwa zilizokuwa katika mji huu, aidha Cuban Marimba, au Morogoro Jazz.

Siku ya Januari 12, 1979 ulimwengu wa muziki Tanzania ulitikisika kwa simanzi baada ya kusikika kifo cha Mbaraka Mwinshehe, mpiga gitaa muimbaji, mtunzi na kiongozi wa bendi wa miaka mingi na ambaye bendi yake ilikuwa imepiga kila wilaya ya nchini Tanzania. Taarifa ziliingia jioni ya siku ile kupitia redio ya Taifa kuwa nguli huyu alifia katika hospitali katika jiji la Mombasa nchini Kenya muda wa saa 1:55 jioni kufuatia ajali ya gari. 

Siku hiyo ya tarehe 12 Januari 1979 mchana muda wa saa saba, Mbaraka akiwa katika  mitaa ya Mombasa ndani ya gari aina ya Peugot 404 nyeupe iliyokuwa katika spidi kali gari lake liligongana na lori. Watu wakakimbilia kungalia ajali, na mara moja watu wakamtambua Mbaraka  aliyekuwa kiti cha mbele upande wa abiria. 

Maelezo ya baadaye yalimtambulisha dreva huyo kuwa alikuwa rafiki wa Mbaraka na mkazi wa Moshi aliyeitwa Omari Abdi, kuna maelezo mengine kuwa Abdi pia alikujafia hospitalini, na abiria aliyekuwa kiti cha nyuma alifariki palepale. Mbaraka alikuwa amebanwa miguu na lile gari lililokuwa limebonyea, lakini alikuwa bado hai, baada ya kuondolewa alikimbizwa hospitali. 

Wanamuziki wa KItanzania waliokuweko Mombasa, wakiwemo wanamuziki wa bendi ya Super Volcano ya Mbaraka mwenyewe na wale wa Jamhuri Jazz Band walitaarifiwa kuhusu ajali ya mwenzao, ambaye baada ya kutolewa alipelekwa katika Makadara. Mbaraka alifariki masaa machache baadae kutokana na kuvuja mno damu.

Muda si mrefu Mbaraka Mwinyshehe akafariki. Mbaraka alifariki 12 Januari 1979 akiwa na umri mdogo wa miaka 35 tu. Kwa kuwa mpaka wa Kenya na Tanzania ulikuwa umefungwa wakati huo kutokana na mgogoro kati ya serikali za nchi hizi mbili, mwili wa Mbaraka ulisafirishwa mpaka mpakani na kupokelewa na ndugu marafiki na Maafisa wa Wizara ya Utamaduni. Leo tumetimiza miaka 40 toka kifo cha nguli huyu aliyezikwa Mzenga Kisarawe. 

Nyimbo zake bado zinaendelea kufurahiwa na watu wengi. Album yake ya mwisho ambayo aliihangikia akiwa na ndoto ya kumaliza shida zake kwa kupata vyombo vipya ilikuwa na wimbo ulioitwa Shida. Kati ya maneno katika wimbo ule ni… Kila siku shida shida mpaka siku ya mwisho…. Mungu Alaze pema Mbaraka Mwinshehe Mwaruka
Mbaraka Mwinshehe hatimae alizikwa Mzenga Kisarawe
Mbaraka Mwinshehe alikuwa Kati ya watoto hao kumi na mbili, ni yeye na wadogo zake Zanda na Matata ndio waliweza kuja kuwa wanamuziki, Zanda alikuwa mwimbaji, akiimba pia nyimbo za kizungu katika bendi ya Morogoro na Matata alikuwa mpiga drum pia bendi hiyohiyo.

MIAKA 100 YA ASTRONOMIA: KuunganikaKuchuguzanaKuuelewaUlimwenguwetu NA MASAA 100 YA ASTRONOMIA

0
0
Dr N T Jiwaji (Mwenyekiti ASSAT) 11 Januari 2019 

 Mwaka huu 2019 Muungano wa Kimataifa wa WanaAstronomia (International Astronomical Union – IAU) unasheherekea miaka mia tangu uundwe (1919-2019), ili kuunganisha nguvu za wanaAstronomia wa kila sehemu ya Dunia kuunganika kuchunguza, kuelewa na kuendeleza fani ya Astronomia kwa ajili ya kufaidi matokeo yake.

Hapa Tanzania tunausheherekea mwaka huu kama shughuli za MIAKA 100 YA ASTRONOMIA zikiongozwa na Chama cha Astronomia na Sayansi ya Anga Tanzania (Astronomy and Space Science Association of Tanzania – ASSAT) katika makao yake Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na leo tarehe 11 Januari 2019 tuna zindua sherehe hizo.

Matukio mbalimbali ya kimataifa yameandaliwa na IAU katika kuusheherekea mwaka. MASAA 100 YA ASTRONOMIA ni mojawapo ya shughuli ambapo wanaastronomia Duniani kote wanahamashisha jamii wakiwemo watoto, wanafunzi, waalimu, wafanyakazi, vijana, wazee na wote kwa ujumla kuelewa na kufurahia na kushughulika katika mambo ya Astronomia na kuelewa sayansi ya asili.

Masaa 100 hayo ni kuanzia tarehe 11 hadi 14 Januari ambapo mamilioni ya watu wanaalikwa kutazama angani kwa macho au kwa kutumia darubini na kuangalia, kufurahia na kuelewa maajabu ya Ulimwengu wetu.  Anga ni moja hiyo hiyo kwa watu wote Duniani na ndio inatuunganisha binaadamu wote.

Leo hii tarehe 11 January 2019, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimepanga tukio hili kuzindua shughuli zetu za MIAKA 100 YA ASTRONOMIA na kualika watu washiriki kwa pamoja katika MASAA 100 YA ASTRONOMIA kwa kuangalia anga.

MGAO WA MAJI WAZO KUWA HISTORIA - LUHEMEJA

0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imewahakikishia wananchi wa Kata ya Wazo kupata maji kuanzia leo usiku.

Akizungumza mbele ya wananchi hao na Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kulikuwa na changamoto kidogo ila kwa sasa wananchi wote waliokuwa kwenye mtandao wa maji wa zamani wataanza kupata maji kuanzia saa 2 usiku.

Luhemeja amesema, mradi huu wa sasa una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni sita kwa sasa tofauti na ule wa zamani uliokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita elfu sitini na kupelekea mgao wa maji kwenye maeneo mengi.

“Kuanzia sasa hivi hakutakuwa na mgao wa maji kwenye maeneo yote yaliyo na mtandao wa maji, mradi huu una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni sita na hivyo tatizo la maji kwa Kata ya Wazo, Madale na maeneo mengine limekwisha,”amesema Luhemeja.

Akielezea maeneo ambayo hayajafika mradi kutokana na kutokuwepo kwa mtandao wa maji, Mhandisi Luhemeja amesema kuna fedha takribani Bilioni 115 zimeshapatikana kwa ajili ya kusambaza mabomba yenye urefu wa Kilometa zaidi ya 1000 katika maeneo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kuna fedha bilioni 115 zimeshatengwa tayari zipo kwenye mchakato wa manunuzi pia tunakaribia kusaini mkataba na mkandarasi ambaye tumeshampata na nitawakaribisha wenyeviti wote kuja kushuhudia ikiwemo na Wakuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,”amesema Luhemeja.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo amesema katika serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli miradi mingi imekuwa ikitekelezwa na wananchi wawe na subira na wameshaahidiwa maji kutoka kuanzia usiku wa leo.

Chongolo amesema, yeye binafsi anaamini kuwa Mtendaji Mkuu wa DAWASA sio mwanasiasa hawezi kudanganya kazi imefanyika na inaonekana ya kutoka uzalishaji wa maji lita elfu sita hadi milioni sita kwa lisaa.

Ameongezea na kusema, atakuja kufuatilia maji kama yanatoka siku ya kesho kutwa (Jumanne) na kujionea kwa machi yake.DAWASA wamedhamiria kufika asilimia 95 Ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kufikia Desemba mwaka huu.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza mbele ya wananchi wa Tegeta Wazo na kuwahakikishia maji safi na salama kufikia leo usiku.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wakati alipotembelea Tenki la maji la Wazo na kuwahakikishia Watapata maji kama walivyoahidiwa na Afisa Mtendaji wa DAWASA
Busta Pampu zilizofungwa kwenye tenki la maji la Wazo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea tenki la maji la Wazo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea mradi wa tenki la maji la Tegeta Wazo lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni sita.

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI OFISI YA MAKAMU WA RAIS IHUMWA DODOMA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kulia) mara baada ya kuwasili katika eneo linalojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Kamati ya Taifa ya Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe (kulia) mara baada ya kuwasili katika eneo linalojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya kina juu ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ukiendelea kwa kasi nzuri Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo akielezea namna jengo la ofisi ya Makamu wa Rais litakavyokuwa mara baada ya ujenzi kukamilika katika eneo la Ihumwa, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya kina juu ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua  maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma akiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua  maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma akiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo 
 Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ukiendelea kwa kasi nzuri Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa kumbukumbu  mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ihumwa Dodoma  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwagilia maji mti wa kumbukumbu  mara baada ya kuupanda katika eneo ambalo  Ofisi ya Makamu wa Rais inajengwa Ihumwa Dodoma  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ukiendelea kwa kasi nzuri Ihumwa Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Halotel yatoa Shukurani kwa wateja wake jijini Mwanza

0
0



Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Katika kusherehekea miaka mitatu tangu kuanza kutoa huduma zake hapa nchini, kampuni ya mawasiliano ya simu Halotel imefanya tamasha kubwa na la wazi liitwalo “Shukrani Music Concert” katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Tamasha hilo limefanyika Januari 12, 2019 ambapo watumiaji wa mtandao wa Halotel walijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo simu za mkononi. Aidha kampuni hiyo pia ilitoa mashuka 50 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure na mengine 50 katika Kituo cha Afya Bwisya wilayani Ukerewe.

Makamu Mkurugenzi wa Halotel tawi la Mwanza linalojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara, Francis Mafuru alisema kampuni hiyo iliyoanza kutoa huduma zake hapa nchini Oktoba 15, 2015 pia imetumia zaidi ya shilingi Milioni Sita kununua madawa na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya Bwisya pamoja na Hospitali ya Sekou Toure.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo akimkabidhi mwakilishi wa Mgangwa Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bwisya, Cosmas Wanzara (kushoto), mashuka yaliyotolewa na kampuni ya Halotel.
Tamasha hilo lilipambwa na burudani kali kutoka kwa msanii Mr. Blue a.k.a BlueByser.
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live




Latest Images