Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110102 articles
Browse latest View live

HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI KWENYE MAPOKEZI YA NDEGE YA PILI YA AIRBUS A220-300


DC NAMTUMBO AZUNGUMZIA ZIARA YA KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, AMSHUKURU KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amezungumzia ziara ambayo imefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo ambapo ameshukuru kwa kuchangia ujenzi wa madarasa manne kwa shule za sekondari Wilaya ya Namtumbo.

Ambapo Kizigo amefafanua mchango huo umekuja wakati muhimu hasa kwa kuzingatia kwamba mwaka huu wanatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wengi, hivyo kusababisha uhaba wa vyumba vya madarasa.

Akizungumzia ziara ya Katibu Mkuu huyo, leo Januari 12,2018 Kizigo amesema alianza ziara kwa kutembelea semina ya mafunzo iliyohusisha Waalimu wakuu wa shule zote za Msingi 110 zilizopo wilaya ya Namtumbo. 

"Semina hiyo ilihusu mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa takwimu unaolenga kusaidia kuwa na takwimu sahihi za shule za msingi nchini," amefafanua.

Aliwahimiza wazingatie mafunzo hayo ili iwe rahisi kwao kuutumia mfumo huo mpya.Pamoja na hayo aliwatia moyo na kuwataka wachape kazi kwani wao ndio wahandisi wanaotengeneza wataalam wa kila kada nchini.

Kizigo amewema Katibu Mku pia alitembelea Shule ya sekondari Nasuli ambapo akiwa hapo alipokea taarifa ya shule na kukagua majengo (Hostel na madarasa) yaliyojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R. 

Pia alipata nafasi ya kusalimia wanafunzi wa kidato cha sita mchepuo wa CBG na kuwahusia wazingatie masomo na baada ya hapo wakaenda kutembelea chuo kipya cha Ufundi VETA Namtumbo ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 kwa awamu ya kwanza.

"Katibu Mkuu alionyesha kuridhishwa na ujenzi wa chuo hicho.Ammpongeza mkandarasi kwa kumaliza kujenga kwa," amesema Kizigo wakati anazungumzia ziara hiyo ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo (kushoto kwake) na viongozi wengine waandamizi wakitembelea maeneo mbambali ya chuo kipya cha VETA Namtumbo,ambapo chuo hicho kimekamilika kwa 100% kwa awamu ya kwanza. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kipya cha VETA ndani ya Wilaya ya Namtumbo,ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kipya cha VETA ndani ya Wilaya ya Namtumbo,ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,Sophia Kizigo alipokuwa akielezea jambo kuhusu chuo kipya cha VETA Namtumbo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo alitembelea shule ya sekondari Nasuli kupokea taarifa ya shule na kukagua majengo (Hostel na madarasa) yaliyojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R. 
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh.Sophia Kizigo akisoma taarifa ya idara ya Elimu wilaya ya Namtumbo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo,ambapo pia alitumia nafasi hiyo kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu elimu katika wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Kizigo pichani kushoto mara baada ya kuwasili kwenye ofisi hizo.

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WACHIMBA MADINI NCHINI YASIKILIZA KERO ZA WACHIMBAJI WA MKOA DAR,PWANI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SHIRIKISHO la Vyama vya Wachimbaji wa Madini nchini (FEMATA) limefanya ziara ya kutembelea wachimbaji wa Mkoa Dar es salaam na Pwani ambapo wametumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa wachimbaji pamoja na kusikiliza kero na kutatua.

Ziara hiyo iliongozwa na Rais wa FEMATA John Bina akiwa ameambatana na uongozi wa chama cha wachimbaji Mkoa wa Dar es salaam na Pwani (DARCOREMA) ambapo pia ujumbe huo ulitembelea wadau wa sekta ya madini wakiwemo wazalishaji na wasambazaji wa vifaa vya wachimbaji vikiwemo Baruti na mitambo ya inayotumiwa na wachimbaji.

Kwa mujibu wa Bina wachimbaji kupitia vyama vyao hawana budi kutatua changamoto zao kupitia meza ya mazungumzo baina hao na Serikali.

Mojawapo ya kero zilizoonekana kukithiri Kwa wachimbaji ni pamoja na wengi wao kukosa mitaji na hivyo kulazimika kuingia ubia na wawekezaji wa Nje makubaliano ambayo Mara nyingi ukosa usawa kibiashara.

Pia Bina amesema tayari shirikisho limeandaa mpango wa namna ya kuwasaidia wachimbaji kutatua changamoto hizo.
 Pichani kati aliyevaa suti nyeusi ni Rais wa FEMATA akiwa wizarani akizungumza na viongozi wa chama cha wachimbaji Mkoa wa  Dar es salaam na Pwani. 
 Baadhi ya viongozi wa Shirikisho la wachimba madini nchini wakipata maelezo baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wachimbaji wa madini Mkoa wa Dar es Salaam
  Baadhi ya viongozi wa Shirikisho la wachimba madini nchini wakiwa kwenye moja ya eno la uchimbaji madini wakipata maelezo kwenye ziara yao kuwatembelea wachimbaji wa madini Mkoa wa Dar es Salaam.

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Rwegasira Mukasa Oscar (kushoto) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi katika kikao na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliongoza ujumbe wa Wizara katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019. Wengine katika picha, kuli ni Bw. Hamid Mbegu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Japahary Kachenje. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliwasilisha taarifa mbili katika kikao hicho. Taarifa ya kwanza ilihusu hatua zinazochukuliwa na Wizara katika mapambano dhidi ya Ukimwi na taarifa ya pili ilihusu namna Wizara inavyoshirikiana na mashirika ya kimataifa, kikanda na nchi mbalimbali katika kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya. 
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ukisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zinawasilishwa na Mhe. Naibu Waziri. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi walioshiriki kikao hicho. 
Mhe. Amina Mollel, Mbunge wa Viti Maalum akichangia jambo wakati wa kikoa kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Mhe. Masoud Abdallah akichangia jambo katika kikao hicho. 
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioshiriki kikao kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje. 
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Wizara ulioshiriki kikao hicho. 
Waheshimiwa Wabjumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi wakisalimiana na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kikao kuanza. 
Mhe. Allan Kiula, Mbunge wa Iramba Mashariki akisalimiana na Mhe. Naibu Waziri. 
Mheshimiwa Mbunge akibadilishana mawazo na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kuanza kikao. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Kimey akiongea machache na Mhe. Naibu Waziri kabla hawajaingia katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi. 

Ohoooo....!

$
0
0
Ni Basi ama Daladala lenye nama za usajili T587  DGK likiondolewa kwenye mtaro mara baada ya kupoteza muelekeo mapema leo asubuhi maenEo ya Hospitali ya  Massana,Goba jijini Dar.Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa,watu wote walitoka salama,aidha chanzo cha basi hilo kupoteza muelekeo hakikujulikana mara moja.

WAZIRI MHAGAMA AWATAKA WATENDAJI KIWANDA CHA VIATU CHA KARANGA KUZALISHA KWA TIJA

$
0
0
NA. MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama amewataka watendaji wa kiwanda cha Viatu na bidhaa za ngozi cha Karanga Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuendana na Soko lililopo nchini.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki ili kukagua shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho na kujiridhisha na ubora wa bidhaa zinazozalishwa. “Niwatake watendaji kuweka mikakati madhubuti ya kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotatiwa”, Mhagama

Aidha Waziri aliwaasa watendaji wa kiwanda hicho kuendelea kutatua changamoto zinazowazunguka za kimfumo kwa kuzingatia sheria na taratibu za uendeshaji wa kiwanda hicho ili kuendana na ukuaji wa teknolojia na ushindani ulipo. “Nisingependa kuona kiwanda kinakwama kuzalisha bidhaa zenye ubora, hivyo ni vyema kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa kiwanda katika ufanisi wa hali ya juu”,alisisitiza mhagama.

Waziri alieleza kuwa, ili kuwa na wateja wa uhakika ni vyema kutumia mbinu za kujitangaza juu ya shughuli na bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia vyombo vya habari ili kuendana na soko lililopo nchini. Aidha waziri alieleza Mpango mkakati wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha Taifa katika eneo hilo la Gereza la Karanga na tayari eneo limetengwa kwa ajili ya ujenzi na kuboresha kiwanda kilichopo ili kuongeza uzalishaji kwa wakati na ubora unaotakiwa.

“Uwekezaji unalenga kuboresha kiwanda cha zamani kutoka kuzalisha pair 150 kwa siku na kuzalisha pair 400 kwa siku ingawa mpango mkakati uliopo ni kuwa na kiwanda kikubwa kitakachozalisha pair 4000 kwa siku”,alisisita Waziri Mhagama.

Naye Kaimu Mkuu wa Kiwanda hicho, Shalua Magandi alibainisha faida zinazotarajiwa kutokana na mradi wa kiwanda hichi ni pamoja na  uzalishaji wa ajira 5000 za moja kwa moja na zaidi ya ajira 4000 kutokana na shughuli za uzalishaji nchini, kuongeza Kodi kwa Manispaa, kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ngozi, kuongeza manufaa kwa mkoa pamoja na mikoa inayozunguka kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wananchi.

Kwa upande wake Afisa masoko wa kiwanda hicho Bw. Fredrick Njoka aliwataka Watanzania kuendelea kununua viatu vinavyotengenezwa kwa bidhaa za ngozi kwa kuzingatia ubora na bei nafuu kwa kuwa kiwanda hicho kinatumia mashine za kisasa kutoa nchini Italia ambao ndiyo wenye ujuzi wa hali ya juu na teknoloji ya kisasa ya utengenezaji wa mashine hizo.

“Wananchi msiogope kututembelea na kununua bidhaa zetu kwa kuzingatia zina ubora wa na bei nafuu, na tunapokea mahitaji ya kila aina kulingana na uhitaji wa wateja wetu”,alisema Njoka. Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba alieleza namna watakavyotekeleza maagizo ya waziri pamoja na kuhakikisha usimamizi mzuri wa shughuli za serikali.

“Nikushukuru kwa ziara yako inatukumbusha kuendelea kusimamia utendaji wenye tija kwa watumishi wa Serikali pamoja kuhakikisha kiwanda hiki kinazalisha bidhaa bora na kulingana na mahitaji ya wateja”, alisema Warioba. Kiwanda cha viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi kilizinduliwa rasmi Juni 3, 1977 na Rais wa awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere.Awali kilikuwa na ubia na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ambapo baada ya mabadiliko ya kuunganishwa kwa mifuko hiyo , kwa sasa kina ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza la Karanga lenye ubia na Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSSSF alipofanya ziara kiwandani hapo Januari 09, 2019 Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
 Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha Viatu cha Karanga, Shalua Magandi akisoma taarifa ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama alipotembelea kiwandani hapo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelekezo ya namna viatu vinavyopachikwa soli kutoka kwa Fundi Mkuu Msaidizi Kiwanda cha viatu Gereza la Karanga, George Komba wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelekezo kuhusu moja ya kiatu kilichotengenezwa kwa ngozi kutoka kwa Afisa Masoko wa kiwanda cha Viatu cha Karanga Bw. Fredrick Njoka wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokea maelezo kutoka kwa Fundi idara ya ushonaji Charles Botto kuhusu malighafi zinazotumika kutengeneza viatu vya ngozi katika kiwanda cha Viatu cha Gereza la Karanga.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika ziara kiwanda cha Viatu na bidhaa za ngozi cha Gereza la Karanga Wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa kiwanda cha viatu cha Karanga na watendaji wa Mfuko wa Hifadhi wa PSSSF na Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara yake katika kiwanda hicho.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

JE WAJUA NI JENGO GANI HILI.?

WANAFUNZI WA KIKE 235 MKOANI PWANI WAPATA MIMBA KIPINDI CHA MWAKA 2018

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
WANAFUNZI wa kike 235 wa shule za msingi na sekondari mkoani Pwani wamepata mimba katika kipindi cha mwaka 2018 ,hali ambayo ni mbaya. Kutokana na takwimu hiyo, kamati ya ushauri ya mkoa wa Pwani (RCC) imekemea vikali masuala ya mimba za utotoni ,na kuagiza sheria ichukue mkondo wake kwa wale ambao wamehusika kuwapa mimba wanafunzi hao.

Akizungumza kwenye kikao cha ushauri cha mkoa huo, ofisa elimu mkoa wa Pwani, Abdul Maulid alisema kati ya wanafunzi hao, 155 ni wanafunzi wa shule za sekondari. Alieleza, wanafunzi wengine 80 waliopata mimba katika kipindi hicho ni wa shule za msingi. "Mikoa ya wenzetu kama Kilimanjaro tujiulize kwanini wanafunzi hawapati mimba ,tushirikiane kupiga Vita tatizo hili ,"

"Madereva bodaboda, jamii ishirikiane na serikali kupambana na namba hii, bodaboda msiwe chanzo cha kupakia wanafunzi hawa na kuwarubuni kuwapa mimba "alisisitiza Maulid. Hata hivyo, alielezea, changamoto ya shule kuwa umbali mrefu, wanafunzi kukosa chakula mashuleni ni chanzo moja wapo cha wanafunzi kupata mimba. 

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema vyombo vya dola visiwafumbie macho wahusika wa mimba hizo. Alisema, namba hiyo ni kubwa hivyo sheria ichukue mkondo wake na wafungwe miaka 30 jela ili iwe fundisho. Ndikilo anawataka ,wazazi na walezi kuacha kumalizana kesi za mimba za utotoni majumbani na kurubuniwa fedha ili kuwaachia huru wanaobainika kuwapa mimba watoto wao wakike. 

WAZIRI UMMY AWAONYA MADAKTARI NCHINI, AWATAKA KUACHA KUWA MADALALI WA MADUKA YA DAWA

$
0
0
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya madaktari nchini kuacha tabia za kuwa madalali wa maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili huku akiwaambia kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali. 

Huku akiagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka ya dawa litakalokuwa na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka binafsi. 

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani wa Tanga aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kauli hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walimsimamisha nje ya hospitali hiyo kabla ya kukutana nao. 

Wananchi hao ambao walikuwa wakisubiri kuingia hospitalini hapa walimueleza kero hiyo ambapo alisema mbali na kero hiyo aliwaagiza madaktari nchi nzima kuhakikisha wanazingatia mwongozo wa kutoa dawa au matibabu ili kuepusha lawama kwa wagonjwa wa kubadilishiwa dawa na kila daktari. 

Akiwa kwenye eneo hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupumzikia wananchi ambao wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao kabla ya kuingia hospitalini hapo ndipo wananchi hao walipoamua kumueleza kilio hicho ambacho kimekuwa kikiwaumiza muda mrefu sana na kumuomba akishughulikie. 

“Kwa kweli hii sio sawa kabla ya hapa nimepata wasaa wa kuzungumza na wananchi nje ya geti lakini kilio chao kikubwa ni kutokuridishwa na huduma tunazozitoa likiwemo suala la mgonjwa kuandikiwa dawa na kila daktari hii sio sawa naaagiza madaktari acheni kuwa madalali wa maduka ya dawa na sitaki kusikia hili siku nyengine “Alisema Waziri Ummy 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya waziri huyo Mmoja wa wananchi Mussa Jangwa alisema kwamba kwenye hospitali hiyo kumekuwa na changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni kila daktari anayeingia wodini anaandika dawa zake. 

Alisema kwamba hatua hiyo imepelekea kuingi gharama kubwa huduma bado ni changamoto kutokana na kutumia fedha nyingi kutokana na kuwepo kuandikiwa dawa kila wakati na kulazimika kwenda kununua 

“Mh Waziri tunashukuru kwa kuja na tungeomba viongozi wengine waige mfano wako hapa hospitali ya Bombo kuna tatizo kubwa sana unapo na mgonjwa wodini unapokuja daktari wa kwanza naandika dawa na mwengine akipita anaandika dawa kwenye zamu yake sasa mgonjwa hajui anunue zipo na ghamara zinakwenda “Alisema Mussa. 

Alisema wakati wanapoandikiwa dawa hizo wanaelekezwa duka la kwenda kununulia huku wakitumia fedha nyingi ndani ya siku nne jambo ambalo limechangia kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki kuingia gharama zisizokuwa za msingi huku mgonjwa akiwa bado hajatumia akizoandikiwa na hali yake ni mbaya. 

“Unapozungumzia jambo la afya ni uhai wa binadahamu nichukue fursa hii kukupongeza kutembelea hospitali hii isiwe ni wewe tu viongozi wote wafanye ziara kama wewe huduma za afya bombo bado changamoto kubwa sana “Alisema 

Naye kwa upande wake Pili Nzoya Alisema wakati mwengine daktari anaweza kupita wodini na kumuandikia mgonjwa dawa nyingi wakati ni za kununua na kila wakati wamekuwa wakifanya hivyo na kupelekea kuwepo kwa usumbufu mkubwa kwao. 

Awali naye mkazi mwengine Amina Mrisho alimueleza Waziri Ummy kwamba wamekuwa wakiandikiwa dawa wakati bado nyengine walizokuwa nazo hawajazimaliza kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu na kujikuta wakiingia hasara. 

Alisema kwamba jambo ambalo limekuwa likiwashangaza ni kuandikiwa dawa na daktari halafu wanabadilishiwa dawa nyengine jambo ambalo ni hasara kwao huku wagonjwa wao wakiwa kwenye hali mbaya na baadae mgonjwa anafariki. 

“Kwa mfano Mh Waziri umeandikiwa dawa leo za sh.40,000 kabla haujazimaliza unaandikiwa nyengine hili ni tatizo ambalo limekuwa likituumiza sisi wananchi tunaomba utusaidie “Alisema. 

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini walikuwa wanafanya kwa nia njema lakini kama tukiwabaini ambao walikuwa wanafanya kwa nia binafsi tutawachukulia hatua. 
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) akizungumza na watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati wa ziara yake ya Jimbo la Tanga kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita akizungumza katika ziara hiyo kulia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu anayefuatia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita mara baada ya kuwasili hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiwa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo wakitembelea maeneo mbalimbali kwenye hospitali hiyo 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati alipowasili kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akilakiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Saidi Nondo 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akisikiliza malalamiko ya wananchi nje ya geti la Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kabla ya kukutana na watumishi wa Hospitali hiyo 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo 
mmoja wa watumishi akiuliza swali kwa Waziri Ummy 
Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo wakimsikiliza Waziri Ummy 

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita

RAIS DKT. SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, alipowasili katika viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba, kuhudhguria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungua Mkono Wananchi akiwa katika gari Maalum ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, wakati akiingia katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwa Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea shatu ya Gwaride rasmin la maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliofadhimishwa kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride rasmin la Sherehe za Mapinduzi kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba. leo (Picha na Ikulu)

MKUU WA MKOA AWAAGIZA TRA KUTOFUNGA MADUKA YA WAFANYABIASHARA MKOANI KAGERA BADALA YAKE WAELIMISHWE ILI KULIPA KODI YA SERIKALI

$
0
0
 Na Sylvester Raphael
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti awaagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera (TRA) kuanzia Januari 11, 2019 kuacha tabia za kufunga biashara za wananchi kwasababu ya kodi badala yake wajikite katika kutoa elimu na kuwaelimisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa utashi bila kushurutishwa pia waweke mkakati wa kuwapata walipakodi wapya.
 Maagizo hayo yalitolewa na Mkuu wa Mkoa Gaguti katika kikao cha Baraza la Wafanyabiashara kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Bukoba Januari 11, 2019 ambapo aliwaita wafanyabiashara hao kuwasikikiliza kero zao ili kuboresha ulipaji wa kodi katika Mkoa wa Kagera ikiwa ni pamoja na kufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi kwa mwaka 2018/2019 kwa asilimia 100%.
 Kabla ya Mkuu wa Mkoa kutoa maagizo hayo aliwapa nafasi wafanyabiashara kuchangia namna bora ya kuhakikisha kodi inakusanywa kwa asilimia 100% katika Mkoa wa Kagera na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafikiwa ili kodi rafiki ilipwe katika mazingira mazuri ya kufanya biashara bila bughudha zozote.
 Wafanyabiashara waliopata nafasi ya kuchangia katika kikao hicho walilalamika juu ya utendaji kazi wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa wanakusanyatu kodi bila kutoa elimu na hawajengi mazingira mazuri yakuwasikiliza wafanyabiashara ili walipe kodi kwa utashi hasa katika Mkoa wa Kagera jambo ambalo limepelekea wafanayabisahara wengi kufunga biashara zao.
 Mara baada ya kuwasikiliza Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa anataka katika Mkoa wa Kagera kuwe na mazingira mazuri ya wafanyabiashara kufanya biashara zao  na kulipa kodi bila kushurutishwa na kila mfanyabiashara atambuliwe ili kuwa na takwimu sahihi za wananchi wote wanaojishughulisha na biashara.
 Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa siku kumi na nne kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwatumia Viongozi na Watendaji katika ngazi za Kata hadi Vijiji kuwatambua wafanyabiashara wote wawe wakubwa au wadogo ili kuwe na takwimu sahihi ya mkoa kuhusu wananchi wanaojishughulisha na biashara kwani  katika Mkoa wa Kagera ulipaji kodi ni asilimia 0.4% tu.
 Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliitaka TRA Mkoa wa Kagera kutanua wigo katika kukusanya kodi hasa kodi za majengo na ardhi. Pia aliwataka wafanyabiashara kuwa wakweli katika kutoa takwimu zao za biashara ili wasikwepe kodi na wala wasionewe. Mwisho Gaguti aliitangaza tarehe 25 hadi 30 Machi, 2019 kuwa itakuwa wiki ya Kagera na kuwaomba wananchi katika Sekta zote kushiriki kuutangaza Mkoa wa Kagera katika wiki hiyo.
 Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustine Kamuzora aliyehudhuria kikao hicho aliwahakikishia Wafanyabiashara kuwa sasa uongozi wa mkoa umejipanga kuondoa vikwazo vyote vinavyorudisha juhudi za wafanyabiashara kusonga mbele ambapo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inataka kuona kila mwananchi anatajirika katika nchi yake mahali popote alipo.
 Profesa Kamuzora alisema kuwa atahakikisha anaimarisha Mabaraza ya Wfananyabiashara ya Wilaya na Mkoa ili kuhakikisha Sekta binafsi inashirikiana na Serikali kikamilifu katika kuchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla
 “Jana wakati nimefika hapa mkoani niwauliza wenzangu kuwa mkoa wetu hivi leo unacheza ngazi gani ya ligi nikaambiwa unacheza ndondo cup, wakati ule sisi Kagera ndiyo tulikuwa tunawika na kucheza Premiere League lakini sasa Ndondo? Hapana! Jambo hili inaenda mbali hadi kwenye maendeleo sisi hatutakiwi kuwa ndondo tunatakiwa Premiere.” Alisissitiza Katibu Tawala wa Mkoa Prof. Kamuzora
Mara baadaya kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Kagera kumalizika Mkuu wa Mkoa na Ktibu Tawala wa Mkoa pamoja na viongozi wengine walitemblea baadhi ya Wafanyabiashara katika Mtaa wa One Way na Soko Kuu Manispaa ya Bukoba kusikiliza Changamoto wanazokumbana nazo ili kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na kulipa kodi stahiki kwa utashi.

PICHA: GWARIDE LA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA MAPINDUZI LEO

$
0
0
 KIKOSI cha Bendera cha JWTZ kikipita mbele ya Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakitowa heshima kwa mwendo wa Pole wakati wa bwaeride la kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba leo.
 GADI ya kwanza ya Gwaride rasmi la kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakipita kwa mwendo wa Pole mbele ya jukwaa la Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
 KIKOSI cha JWTZ Wanawake wakitowa heshima kwa mwendo wa polepole wakitowa heshima mbele ya Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
 KIKOSI cha Askari wa FFU wakipita kwa mwendo wa pole mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Dk. Ali Mohamed Shein.
  KIKOSI cha Jeshi la Polisi Wanawake wakitowa heshima wakati wakipita jukwaa kuu Uwanja wa Gombani Pemba.
 ASKARI wa Kikosi cha KMKM Wanawake wakitowa heshima wakati wakipita Jukwaa Kuu Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba wakati wa gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 ASKARI wa Kikosi cha KMKM wakitowa heshima wakiwa katika mwendo wa kasi wakati wa maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Uwanja wa Gombani Pemba.
 ASKARI wa Chuo cha Mafunzo wakipita kwa mwendo wa kasi wakitowa heshima jukwaa kuu, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
ASKARI wa Kikosi cha JKU wakitowa heshima kwa mwendo wa Kasi mbele ya Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein. (Picha na Ikulu)

TANZANIA YATAFUTA SOKO LA UTALII UHOLANZI

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Tanzania yatafuta Soko la Utalii Uholanzi


Taasisi za Serikali na kampuni binafsi mbalimbali za utalii zipo nchini Uholanzi kushiriki maonesho ya utalii ya kimataifa kwa lengo la kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.

Maonesho hayo maarufu kama Holday Fair 2019 (Vakantiebeurs2019) yalianza tarehe 9 Januari na yatakamilika tarehe 13 Januari 2019, hufanyika kila mwaka katika mji wa Utrecht na kushirikisha taasisi mbalimbali kutoka duniani kote.

Taasisi za Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanznaia (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Kwa upande wa kampuni binafsi ni into Africa Eco Travel Ltd, Migada Adventures, Mbalaget Tented Camp Ltd, Kili Fair Promotions Ltd, East Africa Camps na Makasa Tanzania Safaris.

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju amesema kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo kwa mwaka 2019, waandaji kwa mara ya kwanza wametoa nafasi kwa Balozi za nje zilizopo nchini humo kutangaza pia fursa za biashara na uwekezaji.

Balozi Kasyanju ambao Ubalozi wake unashiriki katika maonesho hayo alieleza kuwa maonesho hayo yataenda sanjari na Vakantiebeurs Travel Congress, Vakantiebeurs Consumer Day na Vakantiebeurs Trade Day ambapo washiriki watapata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.

Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo utasaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake. 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma, Tanzania

11 Januari 2019

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (mwenye miwani) akiwa na washiriki wengine katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa yanayofanyika nchini Uholanzi kuanzia tarehe 9 hadi 13 Januari 2019. 
Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya uwekezaji nchini.
Banda la Tanzania linatia fora kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watu wanaotaka kupata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii nchini. 
Wageni katika banda la Tanzania. 
Balozi Kasyanju na washiriki wenzake wakiwa katika badna la Tanzania tayari kuanza kazi ya kuuza vivutio vya utalii nchini Uholanzi. 

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KIGOMA YATEKETEZA SHEHENA YA NGUO ZINAZOFANANA NA SARE YA JESHI.

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

KAMATI ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma imeteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo.

Akiongea na wananchi baada ya kuteketeza nguo hizo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwaajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.

Alisema Viongozi wa serikali ya Wilaya walipata taarifa kutoka kwa mkuu wa makazi ya wakimbizi kuna nguo zimeingizwa kambini zinazofanana na sare za jeshi kwaajili ya kuwagawia wakimbizi kama msaada wa nguo.
"Baada ya kupata taarifa wakazifanyia kazi kwa haraka na wakafanikiwa kuzidhibiti na hakuna mkimbizi hata mmoja aliyefanikiwa kupewa"alisema

Anga amewataka wananchi kuacha tabia kutumia nguo zinazofanana na sare za kijeshi kwani ni kosa la kisheria,pia amewataka wale wenye nguo zinazofanana na sare hizo kuzisalimisha katika vyombo vya usalama kama kwenye vituo vya polisi.

"Ni marufuku kuvaa,kusambaza na kuagiza nguo zinazofanana na sare za jeshi ni kosa la kisheria ukipatikana umevaa au kusambaza utachukuliwa hatua kali za kisheria"alisema.Alisema hatua za awali walizochukua mpaka sasa ni wamefungua jalada la uchunguzi,pia wamemkamata mkurugenzi wa shirika lililoungiza hizo,pia wametekeza nguo hizo.

Jumla ya vipande 1947 vya nguo zinazofanana na sare ya jeshi zimeteketezwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa katika kiwanja cha mpira cha kawawa kilichopo eneo la Ujiji.
Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikiteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwa ajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.




Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto. 
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kuongoza zoezi la kuteketeza nguo zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa katika makambi ya wakimbizi.
Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kigoma ikishusha shehena ya nguo zipatazo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo,kwa ajili ya kuchomwa moto. 
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akiongoza zoezi la kuteketeza nguo zinazofanana na sare za jeshi zilikamatwa katika makambi ya wakimbizi.
Umati wa wananchi wakishuhudia nguo zinazofanana na sare za kijeshi zikiteketezwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa katika viwanja vya kawawa eneo la ujiji,mkoani Kigoma

TANZANIA YATAFUTA SOKO LA UTALII UHOLANZI

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (mwenye miwani) akiwa na washiriki wengine katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa yanayofanyika nchini Uholanzi kuanzia tarehe 9 hadi 13 Januari 2019.

Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya uwekezaji nchini

Banda la Tanzania linatia fora kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watu wanaotaka kupata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii nchini.

Wageni katika banda la Tanzania.

Balozi Kasyanju na washiriki wenzake wakiwa katika badna la Tanzania tayari kuanza kazi ya kuuza vivutio vya utalii nchini Uholanzi.


Taasisi za Serikali na kampuni binafsi mbalimbali za utalii zipo nchini Uholanzi kushiriki maonesho ya utalii ya kimataifa kwa lengo la kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.

Maonesho hayo maarufu kama Holday Fair 2019 (Vakantiebeurs2019) yalianza tarehe 9 Januari na yatakamilika tarehe 13 Januari 2019, hufanyika kila mwaka katika mji wa Utrecht na kushirikisha taasisi mbalimbali kutoka duniani kote.

Taasisi za Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanznaia (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Kwa upande wa kampuni binafsi ni into Africa Eco Travel Ltd, Migada Adventures, Mbalaget Tented Camp Ltd, Kili Fair Promotions Ltd, East Africa Camps na Makasa Tanzania Safaris.

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju amesema kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo kwa mwaka 2019, waandaji kwa mara ya kwanza wametoa nafasi kwa Balozi za nje zilizopo nchini humo kutangaza pia fursa za biashara na uwekezaji.

Balozi Kasyanju ambao Ubalozi wake unashiriki katika maonesho hayo alieleza kuwa maonesho hayo yataenda sanjari na Vakantiebeurs Travel Congress, Vakantiebeurs Consumer Day na Vakantiebeurs Trade Day ambapo washiriki watapata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.

Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo utasaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, Tanzania
11 Januari 2019 

MBARAKA MWISHEHE: 40TH DEATH ANNIVERSARY OF THE MOST MULTI-TALENTED TANZANIAN MUSICIAN OF ALL TIME

$
0
0
1. Background:

Today, 12.1.2019, marks the 40th death anniversary of the one and only, MBARAKA MWARUKA MWISHEHE, the man himself, who tragically passed away in a car accident on 12.1.1979 in Mombasa, Kenya.

2. Birth, Early Days & Education :

The late MBARAKA was born on 26.6.1944. He was the  second born in a family of 12 children. His father, MWISHEHE MWARUKA,  was from the Luguru tribe and was fortunate to go to school and later became a clerk. He was a resident of Mzenga, Kisarawe. The reason why the MWARUKA's family was based in Mzenga and not in Morogoro was because as a young man, MBARAKA's grandfather got a posting in Kisarawe where he went on to become a chief. While in Kisarawe, the new Chief  married 9 wives with whom he sired more than 50 children.

The late MBARAKA developed an interest in music at a very young age.

3. Dropping Out of School:
One day in 1965, MBARAKA made up his mind to drop out of school and take a bus to Dsm to pursue a career in music. He was a Form 3 student at Mzumbe Sec School.

On that day when Morogoro Jazz band musicians were taking a break outside their club, a young boy with a familiar face came by with a huge bag.

With the pep talk that ensued between the two parties, the musicians managed to convince young MBARAKA to sleep over at the club as he sorted out his future.

At that time  the band didn't have a rhythm guitarist yet they were preparing for a show. They succeeded to convince this novice to stay with them and  abandon his dreams of going to Dsm. They agreed to pay him a monthly salary of Tzs 120. One week later, there was a competition in Dsm and one of the invited bands was Morogoro Jazz Band. The gifted MBARAKA outshined all his colleagues assisting his band to win the competition. Consequently, his monthly salary was instantly raised from TZS 120 to TZS  250!. 

In 1970, Morogoro Jazz Band travelled to Osaka, Japan for an Expo as part of the Tanzanian cultural team. Others in the team were Mzee MORRIS NYUNYUSA, DSM University Theatre group and Mzee MAYAGILO with Tanzania Police Brass band. It was a historic trip as many people from different countries heaped praises on Morogoro Jazz Band.

MBARAKA's guitar strumming style made him one of the best soloists of his time. He was an exceptional guitarist. At one point, he would play like Dr NICO, at another point, he would play like FRANCO. He was a hybrid of the 2 guitar greats from Africa. The technique earned him a huge following. He was exceptional as he played the solo, wrote songs and also sang.

In 1971, he met a beautiful young girl named Ms AMNE KADRIBAKSH SHAHDAD and the two became lovers. On 17.3.1972, the two lovebirds tied the knot. Their marriage was blessed with two issues of the marriage namely MASIKU and TAJI.
In 1973, MBARAKA formed his own band, ORCHESTRAR SUPER VOLCANO which was very popular.

4. MBARAKA hit songs:

Some of MBARAKA's hit songs, which are still very popular todate, were:

3.1 Shida
3.2 Makao Makuu Dodoma
3.3 Twawapongeza Wanasoka
3.4 Vijana na mapenzi
3.5 Ntamtuma mshenga
3.6  Mtaa wa 7
3.7 Dr KLERUU
3.8 Safari sio kifo
3.9 Moro yapendeza
3.10 Maonesho Japan

5. Leaving Bongo for Kenya

The gifted MBARAKA, in 1973, like many other Tanzanian artists at the time, switched his base from Tanzania to Kenya where there were better recording  studios as well as a bigger music market.

6.  MBARAKA's death:

MBARAKA died on 12.1.1979 at 1.55 AM when the white Peogeot 404 he was travelling in, belonging to his friend OMAR ABDI  who was driving the car, rammed into a stationery lorry near Kigonya church, Mombasa, Kenya. He did not die instantly but at the hospital out of excessive loss of blood and lack of a donor at that moment. He was only 35 years old. It was a dark day for Tanzania and East African music.

In the said car, MBARAKA was with two companions who died on the spot. MBARAKA's body was transported to the border by friends and relatives and it was received by officials from the Tanzanian Ministry of Culture.

MBARAKA was buried at Mzenga, Kisarawe. His grave, which was in a dilapitated state, was repaired by the late CAPT JOHN KOMBA before he died in 2015.

R.I.P MBARAKA MWISHEHE: EAST AFRICA's MOST PROLIFIC ALL- ROUND POP MUSICIAN, A CROONER PER EXCELLENCE!!!

MECHI YA SIMBA NA JS SAOURA YAUSIMAMISHA MSAFARA WA NAIBU WAZIRI KWA MUDA

$
0
0
Msafara wa Naibu waziri wa Maji Jumaa Aweso waonyesha uzalendo kwa kuungana na mashabiki wa timu ya Simba na Taifa kwa ujumla, kutazama mechi ya Simba dhidi ya JS Saoura akiwa njiani kuelekea Mara baada ya kumaliza Ziara yake katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa.

Msafara huo umelazimika kusimama kwa Muda katika Kiwanja cha Hill top mjini Kayanga Wilayani Karagwe huku Mh. Aweso akishindwa kujizuia kuonyesha mapenzi yake dhahili kwa timu ya simba.
Naibu waziri wa maji Juma Aweso akishindwa kujizua wakati wa timu ya Simba ilipofunga goli la tatu timu dhidi  ya Js soura

WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA KONDOA WAPATA NEEMA

$
0
0

Na Peter Haule, WFM, Kondoa

WANAFUNZI wote 3,287 waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma, wanatarajia kuanza masomo baada ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, kutoa msaada wa mabati 1080 ya kuezekea vyumba 20 vya madarasa.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa kipaumbele chake kikubwa ni elimu na anataka kila mwanafunzi aliyefaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo anapata fursa hiyo ya kusoma.

"Tumeamua kutumia mfuko wa Jimbo, zaidi ya sh. 20m zimetumika kununulia mabati haya na niombe Mkurugenzi wewe ndiye mwenye watendaji mpaka ngazi ya vijiji na vitongoji ambako shule zetu zipo, mabati haya yafikishwe kwenye kila shule ili inapofika mwisho wa mwezi Februari, 2019, watoto wote waanze kusoma" alisema Dkt. Kijaji

Aidha, Dkt. Kijaji amewapongeza viongozi na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa jitihada zao za kukuza elimu na kufanikisha Wilaya hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 ambapo shule nane kati ya kumi zilizofanya vizuri katika Mkoa wa Dodoma, zinatoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

"Tunakwenda kwenye Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kuwapeleka wanaKondoa wasio na elimu ndio maana tumefanya mapinduzi makubwa katika wilaya yetu kutoka kuwa ya mwisho kielimu katika Mkoa wa Dodoma miaka mitatu iliyopita hadi kuwa na shule 8 zilizofanya vizuri kati ya 10, kimkoa" aliongeza Dkt. Kijaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bi. Hildegard Saganda, wamesema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka baada ya kuwa na wasiwasi wa namna ya kuwawezesha zaidi ya wanafunzi elfu 3 kupata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa uliokuwa ukiikabili Halmashauri ya Wilaya hiyo.

"Mbati haya yatapelekwa kwenye shule ambazo wananchi wamejenga maboma na zimefikia hatua ya lenta ambazo ni Busi, Kikore, Changaa, Kalamba, Itaswi, Kwadelo, Hondomairo na Loo" alifafanua Bi. Hildegard Saganda

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa, ameelezea kuridhishwa kwake na namna Ilani ya CCM inavyotekelezwa katika wilaya yake katika nyanja mbalimbali na kumpongeza Dkt. Ashatu Kijaji kwa jitihada zake za kuiletea Maendeleo wilaya hiyo.
Afisa Elimu Sekondari wa Hamashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bi. Hildegard Saganda, akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, muda mfupi kabla Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, kabla ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Bw. Alhaji Othman Gora, akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipokabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya hiyo. Kulia ni Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
Mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yaliyokabidhiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza takribani 3287 waliofaulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo kati ya Shule za Msingi kumi bora zilizoongoza kwa ufaulu Mkoani Dodoma kwenye mtihani wa darasa la saba, shule nane zinatoka katika Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akieleza umuhimu wa kuweka kipaumbele katika elimu kwa ujenzi wa taifa wakati akikabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bw. Mustapha Semwaiko (wa pili kushoto), mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, wakishuhudia kukabidhwa mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko, akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) baada ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kulia) pamoja na viongozi na maafisa wa Halmashjauri ya Wilaya ya Kondoa wakizungumza jambo baada ya hafla ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.(Picha na Peter Haule- Wizara ya Fedha na Mipango).

DR. AGGREY: MGHANA MAHIRI ALIYEACHA HISTORIA TANZANIA HADI "KUPEWA" MTAA JIJINI DAR

$
0
0
 DR.JAMES EMMANUEL KWEGYIL AGGREY, aliyezaliwa mwaka 1875 na kufariki takribani miaka 100 iliyopita, ni Mghana ambaye kamwe hatasahaulika katika historia ya nchi yetu, ingawa takriban 90% ya Wabongo hawajawahi hata kumsikia!.

DR. AGGREY alikuwa ni Mwalimu mahiri aliyeheshimika duniani kote. Tarehe 15.5.1895, akiwa Mwalimu-kijana wa miaka 20 tu, alifanya mtihani pamoja na waalimu wenzake wengine 119 kutoka mikoa yote nchini Ghana uliotungwa Uingereza. Dr. AGGREY aliibuka kinara ambapo alitunukiwa cheti na Malkia kilichoandikwa- "This Certificate of Distinction, qualifies you, without further examination, to teach in any school in any British colony". Dr. AGGREY alikuwa Mwafrika wa kwanza  kutunukiwa tuzo hiyo na Malkia!.

DR. AGGREY, kutokana na weledi wake wa kipekee, aliteuliwa kuwa mjumbe wa "Phelps-Stokes Fund Commission" iliyoundwa kuangalia namna kuwaendeleza Waafrika kielimu. Tume hiyo iliundwa kutokana na Mmarekani Bi. CAROLYINE PHELPS STOKES, aliyefariki 1909,  kuacha kitita cha fedha na wosia uliosema- "I bequeath $ 1,000,000 to my trustees to be used for the education of Negros, both in Africa and the United States". Tume hiyo ilizuru mataifa 10 ya Afrika ambapo ilikuja Tanganyika na Zanzibar na kukaa toka Machi 1924 hadi April 1924. Dr. AGGREY alikuwa Mwafrika pekee kwenye Tume hiyo katika kipindi hicho ambapo ubaguzi wa rangi ulikuwa umetamalaki duniani kote. Hata kuwa mjumbe katika Tume hiyo ilikuwa ni kwa mbinde!.

Wajumbe wa Tume hiyo walipowasili nchini walifikia NEW AFRICA HOTEL, moja ya hoteli kubwa 2 nchini wakati huo. Katika hali ya kusikitisha, Dr. AGGREY alikataliwa katakata kupewa chumba kutokana na kuwa mweusi na hivyo ikabidi akatafute hoteli Kariakoo!.

Ubaguzi huu ulimuhuzunisha sana lakini haukumkatisha tamaa. Akiwa Kariakoo, alijichanganya sana na Watanganyika na kupelekea kujuana na KLEIST SYKES, Mtanganyika msomi aliyekuwa akiongea Kiingereza na Kijerumani kwa ufasaha na mjuzi wa mambo mengi ambaye asili yake ilikuwa Afrika ya Kusini.  

DR. AGGREY "alimpiga shule na kumpa nondo kali" Bw. KLEIST juu ya umuhimu wa kuanzisha chama kwa minajiri ya kupigania haki za Watanganyika. "Shule"hiyo ilimuingia vilivyo Dr. KLEIST, kama alivyokiri mwenyewe baadae, na hatimaye yeye na wenzake wakaanzisha chama cha AFRICAN ASSOCIATION (AA) mwaka 1929. AA ilibadilishwa na kuwa TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION mwaka 1948. AA ndiyo ilikuwa chimbuko la TANU iliyoundwa tarehe 7.7.1954.    


Tume ilipotoka hapa nchini ilikwenda Belgium Congo kuendelea na jukumu la kuwaendeleza waafrika. Baada ya kazi ya siku nzima ya kwanza, Gavana MARTIN RUTTEN aliialika Tume hiyo Ikulu kwaajili ya "dinner". Gavana huyo mbaguzi alichukia sana kumuona mtu mweusi kwenye Tume hiyo hivyo akamuamuru Dr. AGGREY asikanyage ndani bali abaki getini!. Dr. AGGREY akakaa hapo getini na walinzi kuanzia saa 1 hadi saa 8 usiku "dinner" hiyo ilipoisha na "hakuna rangi aliyoacha kuiona" kwani kulikuwa na kibaridi kikali na mbu wengi!.  


Figisufigisu hizi za ubaguzi hazikumkatisha tamaa bali zilimuongezea morali zaidi wa kuwasaidia Waafrika wenzake kielimu. Tume hiyo ikaenda Angola ambako nako masaibu ya ubaguzi  "hayakumuacha salama" na yaliendelea kumkumba ambapo ilibidi tu "apambane na hali yake". Kuna siku alionja "joto la jiwe" aliposukumizwa nje ya treni kwavile tu ni mweusi na hivyo kuumia mguu wa kulia na mkono wa kushoto na kulazimika kuchelewa mhadhara wake wa elimu!.

Tume hiyo, baadae, ikaenda Afrika ya Kusini ambako Dr. AGGREY alitoa Hotuba Bora kabisa kuwahi kutolewa na Mwafrika katika karne ya 20.  Dr. AGGREY, kwa ufupi, alisema kuhusu elimu:

"By education I don't simply mean learning. I mean the training of the mind, in morals and in a hand that helps to make one socially efficient. Not simply the 3 Rs, but the 3 Hs ie the Head, the Hand and the Heart. No race or people can rise half slave, half free. The surest way to keep people down is to educate the men and neglect the women. If you educate a man you simply educate an individual but if you educate a woman, you educate a family."

"I am proud of my colour and whoever is not proud of his colour, is not fit to live. Keep your temper and smile. That is what JESUS CHRIST meant when he told men to turn the other cheek".

"I have no time for revenge, that is not African. Some white people ought to be transformed to Negros just for a few days so as to feel what we feel and suffer what we suffer. I prefer to be a spokesman of my entire country: Africa, My Africa!".

"My fellow Africans I don't care what you know, show me what you can do. Many of you who get educated don't work, but like to drink. You see white people drink and think you can drink too. You imitate the weakness of white people but not their greatness. You won't imitate the whiteman working hard!".

"If you play only the white notes on a piano, you get only sharps; if only the black keys, you get flats. But if you play the two together, you get harmony and beautiful music".

Baada ya kutoa hotuba hiyo, umati mkubwa uliokuwepo ulimbeba msobemsobe huku SMURTZ MCNAMARA, Kiongozi wa "White settlers, akitamka- "Damn his colour, He is a Saint!". 

Kwa miaka mingi, hotuba hiyo ya kihistoria iliyosheheni "madini" lukuki, imekuwa ikinukuliwa na viongozi wengi duniani akiwemo marehemu Nelson Mandela, ambaye wakati akigombea urais,  tarehe 2.2.1994, aliulizwa akishinda atawachukulia hatua gani  makaburu waliomtesa kwa miaka 27, nae akajibu "My answer is very short: let me quote from one of the speeches of my idol, Dr. JAMES AGGREY, " I have no time for revenge. That is not African".

DR. AGGREY alikuwa mjuzi wa mambo mengi na "Hobby" yake kubwa ilikuwa ni kusoma vitabu vya kila aina hadi usiku wa manani. Alipokuwa akisinzia, alichukua kitambaa akachovya maji ya baridi na kujifunga kichwani na kuweka miguu kwenye karai la maji ya baridi! Aidha,  DR. AGGREY alikuwa anaongea "Queens English" ya hali ya juu na alipelekea Waziri Mmarekani, Mh. HEC BRYANT aseme: "He is dark as dark, but very few in America can use English as he can!".

DR. AGGREY alifariki dunia mwaka 1927 na kuzikwa North Calorina, Marekani alikokuwa akiishi na kufundisha.
Nchini Ghana, kwa heshima ya Dr. AGGREY, picha yake iliweka kwenye moja ya noti za nchi hiyo (5 Cedi Bill)! Hii ilikuwa ni ajabu sana kwani marais wengi wa Afrika hupenda "kuuza sura kwenye noti!.  

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya nchini yetu, mtaa mmoja jijini ukapewa jina lake kama kumbukumbu "MTAA WA AGGREY". Mtaa huo uko maeneo ya Kitumbini kuelekea Kariakoo jijini Dar Es Salaam.

Huyu ndiye DR. JAMES EMMANUEL KWEGYIL AGGREY, Mghana mahiri mwenye mchango mkubwa katika historia ya nchi yetu.

SIMBA SC YATIKISA KLABU BINGWA AFRIKA, YAINYUKA BILA HURUMA JS SAOURA YA ALGERIA 3-0

$
0
0
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa Timu ya Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa kwanza katika Kundi D baada ya kuifunga JS Saoura goli 3-0.

Simba wakiwa wako katika uwanja wa nyumbani wa Taifa walianza kwa kasi kulisakama lango la JS Saoura na ilichukua dakika 45 kwa Mshambuliaji Emanuel Okwi kuandika bao la kuongoza kwa shuti kali baada ya ‘kuwapinduapindua’ mabeki wa JS Saoura kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.

Okwi aliyekuwa katika kiwango cha juu leo, alifunga bao hilo akitoka kukosa bao la wazi baada ya kugongesha nguzo ya juu akiwa tayari amemtoka beki anatazamana na kipa.    

Simba Walifanya mabadiliko dakika ya 34 wakimtoa Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ baada ya kuumia nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mwenzake, Meddie Ksgere kutoka Rwanda. 

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kurudi na nguvu mpya na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yote yakifungwa na Kagere Goli la pili akifunga dakika ya 51 akimalizia pasi ya Okwi ambaye mabeki wa JS Saoura na lingine akifunga tena dakika ya 67 kwa mara nyingine akimalizia pasi nzuri ya Okwi.

Nahodha wa Simba John Bocco amesema mwitikio wa mashabiki Uwanjani umewapa morali kubwa hali iliyowafanya wapate nguvu na kushinda  mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura.

Bocco amesema mashabiki wanaumuhimu na nguvu kubwa wakiwa Uwanjani anafurahi kuwaona namna wanavyokuwa begakwabega na timu yao."Tunachoangalia sisi ni pointi tatu bila kujali nani anafunga na nani anakosa, makosa yapo na kwenye mpira mengi yanatokea ila sapoti ya mashabiki inatupa nguvu ya kupambana," alisema Bocco.

Mechi nyingine ya Kundi D inachezwa  Saa 4:00 usiku wa leo Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria kati ya wenyeji, Al Ahly dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Baada ya mchezo wa leo, Simba SC itasafiri kuwafuata AS Vita mjini Kinshasa Januari 19, wakati JS Saoura watakuwa wenyeji wa Ahly Januari 18 nchini Algeria.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Hassan Dilunga/Muzamil Yassin dk65, Jonas Mkude, John Bocco/Meddie Kagere dk37, Emmanuel Okwi/Shiza Kichuya dk86 na Clatous Chama.
 Moja ya heka heka iliyotokea kwenye lango la JS Saoura wakati Kipa wa timu hiyo, Khaled Boukacem akichuana  na Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi wakati akijaribu kutafuta namna kukwamisha mpira wavuni. 
 Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akishangilia moja ya bao alililofunga kwenye mchezo wa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam, Simba iliondoka na ushindi wa bao 3-0
 Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akishangilia moja ya bao alililofunga kwenye mchezo wa Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam, Simba iliondoka na ushindi wa bao 3-0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa akishuhudia mtanange huo baina ya Simba SC dhidi ya JS Saoura ya Algeria, mchezo uliomalizika jioni hii katika Uwanja wa Taifa.
 
 





Viewing all 110102 articles
Browse latest View live




Latest Images