Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YAENDA SAMBAMBA NA UZINDUZI WA JENGO JIPYA LA KISASA LA OFISI YA NIDA

$
0
0


Afisa Usajili Msaidizi NIDA Bw. Makame Khamis Makame akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi namna hatua za awali za Usajili wa Vitambulisho vya Taifa zinavyofanywa.
Kaimu Mkurugenzi NIDA Zanzibar Bw. Hassan H. Hassan akielezea jambo kwa mgeni rasmi na ujumbe wake wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi za NIDA. Kulia ni Mh. Dkt. Khalid Salum Mohamed (Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi), wa pili kushoto ni Mh. Mohamed Aboud (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais) na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Arnold M. Kihaule.

Baadhi ya watumishi wa NIDA Visiwani Zanzibar wakiwa wenye nyuso za furaha wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jengo la Ofisi za NIDA wilaya ya Kati Dunga.



Mkurugenzi Mkuu NIDA, Dkt Arnold M. Kihaule akiiwasilisha taarifa ya ujenzi wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa Jengo la NIDA Wilaya ya Kati Dunga.



Mh. Dkt. Khalid Salum Mohamed akizungumza mbele ya wageni waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa Jengo la NIDA wilaya ya Kati Dunga.



Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi, Mh. Dkt. Khalid Salum Mohamed(katikati mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa NIDA wakati wa Sherehe ya uzinduzi wa Jengo jipya la NIDA wilaya ya Kati Dunga.

………………………..

Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Dkt Khalid Salum Mohamed amezindua jengo la ofisi ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wanaoishi Wilaya ya Kati Dunga – Tanzania Zanzibar.

Uzinduzi huo ulifanyika na kushirikisha wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zikiwemo Taasisi za Muungano.

Akihutubia kwenye sherehe hizo Waziri Dkt. Khalid Salum Mohamed amewataka wananchi na wadau muhimu katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA); kuhifadhi na kutunza miundombinu ya Mfumo wa Taifa na Utambuzi kwani taarifa zinazopatikana katika mfumo huo zitasaidia kupata takwimu sahihi ambazo zitaimarisha uchumi wa Nchi.

Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa juhudi zake za kuboresha mradi wa Vitambulisho vya Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kujenga Ofisi za Usajili katika Wilaya mbalimbali nchini, na kusisitiza umuhimu wa Vitambulisho hivyo kwa wananchi, Kiuchumi, Kijamii na Kiusalama.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Vitambulisho vya Taifa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Dkt. Anold Mathias Kihaule amesema, zaidi ya asilimia 96.5 ya wananchi wa Zanzibar wameshaandikishwa na zaidi ya asilimia 90 tayari wameshazalishiwa vitambulisho vyao.

Dkt Kihaule amesema kukamilika kwa jengo la ofisi ya usajili wilaya ya Kati Dunga limegharimu zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bil. 1.9 na kufanya mpaka sasa jumla ya kiasi cha Shilingi Bil 32 kuwa zimetumika katika kujenga majengo 13 nchi nzima ambapo kwa upande wa Zanzibar jengo hilo linakuwa ni la kwanza kukamilika katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa majengo ya ofisi za usajili.

Pia ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango wake mkubwa ilioutoa ikiwamo upatikanaji wa viwanja na kupatiwa msamaha wa kodi mbalimbali (exemption) ambazo zimesaidia kukamilika kwa jengo hilo linalotarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi 47,000.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imeahidi kuendeleza mikakati ya ujenzi wa majengo ya Ofisi ili kusogeza karibu zaidi huduma kwa Wananchi, ambapo katika awamu ya pili ya Ujenzi itakayoanza hivi karibuni itakuwa na ujenzi wa ofisi zingine tatu kwa Unguja na Pemba.

Awamu ya kwanza ya ujenzi mbali na Tanzania Zanzibar; maeneo mengine yaliyopata majengo ya Ofisi ni mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dar-es-salaam, Kibaha na Arusha.

Ujenzi wa Ofisi hizo umetokana na mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Korea Kusini kupitia Benki ya Exim Korea.

WIZARA YA YA KILIMO IPO KATIKA MAPITIO YA SIFA ZA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA – MHANDISI MTIGUMWE

$
0
0

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Rukwa


Wizara ya Kilimo ipo katika mapitio ya sifa za viongozi wa Vyama vya Ushirika nchini ili kupata viongozi watakao ongoza kwa weledi sekta ya Ushirika.

Dhana ya kuchagua viongozi wa ushirika wenye sifa ya kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati hivyo kuna kila sababu ya kuchagua viongozi wenye weledi na utashi katika utendaji.

Hayo yameelezwa jana tarehe 8 Januari 2019 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakati akizungumza kwenye kikao kazi na maafisa wa Kilimo wa Wilaya za Mkoa wa Rukwa, Wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwemo mawakala wa pembejeo, wasindikaji, wawakilishi wa vyama vya msingi vya ushirika na wakulima, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Alisema kuwa mfumo wa ushirika ni nyenzo muhimu ambayo ukitumika vizuri itasaidia kuondoa umaskini wa wakulima hapa nchini na utaimarisha uanzishwaji wa viwanda kuleta tija katika kilimo hivyo ni lazima kuwa na juhudi za makusudi kuwa na viongozi wenye weledi.

Katibu Mkuu huyo katika ziara yake mkoani Rukwa alitembelea maduka na maghala ya mbolea yanayomilikiwa na kampuni za ETG, YARA na PREMIER na kujionea hali halisi ya upatikanaji wa mbolea ambapo amepongeza utoshelevu wa mbolea uliopo mkoani humo.

Akizungumzia swala la masoko ya mazao ya wakulima Mhandisi Mtigumwe alisisitiza kuwa ubora wa mazao ya wakulima ni suala la msingi kulizingatia ili kuweza kusaidia wakulima kupata masoko ya uhakika na kujiongezea kipato, kwani mazao bora yana ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kuhusu Milipuko ya visumbufu vya mimea, Mhandisi Mtigumwe alisisitiza kuwa ili kunusuru mazao ya wakulima nchini, hatua madhubuti zinaendelea kuchukuliwa ili kuweza kudhibiti wadudu wanaothiri mazao akiwemo Kiwavijeshi Vamizi (FAW). 

Hivyo, alitoa rai kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa na Makatibu Tawala wote nchini, kuwaagiza Maafisa Kilimo kufanya tathmini ya awali na kubaini maeneo ambayo kiwavijeshi vamizi ameanza kuonekana ili Wizara kwa kushirikiana na halmashauri ziweze kuchukua hatua za kudhibiti milipuko ya kiwavijeshi vamizi kabla hajasambaa zaidi na kuleta athari kubwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe

KUMBUKUMBU YA CASSIAN MALIMA

$
0
0

Ni kama zimepita siku kumi tu lakini tayari leo imetimia miaka 10 tangu Mpendwa wetu Cassian Kigeso Malima ulipotutoka ghafla jioni ya tarehe 9 Januari 2009 katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam na kupumzishwa katika kwenye makaburi ya Mwisenge, Musoma mjini tarehe 14 Januari 2009.

Muongo mmoja umepita lakini ungali unaishi kiroho maishani mwetu na tunajenga taswira ungekuwa na mwonekano gani, ungekuwa na madaraka gani na mengine mengi yanayoeleza mafanikio ya duniani. Hatuna budi kumshukkuru Mungu kwa zawadi ya uhai wako na  mapenzi yake yatimizwe.


Baba, wanao, ndugu, majirani na rafiki zako daima tutaendelea kukukumbuka kwa upole, ucheshi na uchapakazi wako wakati wa uhai wako, haiba ambayo haikubanduki kila tunapokukumbuka.


Tunamuomba Mungu wa Rehema aendelee kukupumzisha kwake katika amani ya milele tukiamini tutaonana siku ya mwisho. Amina.


1 Wathesalonike 4:13-14 (Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.).



KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Zao la Korosho lapata soko Nchini Algeria

WAZIRI JAFO AWAPOKEA KATIBU MKUU,NAIBU KATIBU MKUU MARA BAADA YA KUAPISHWA LEO IKULU

$
0
0
 Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo akizungumza wakati alipo  wa kuwakaribisha Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu walioapishwa leo Ikulu.
 Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt.Dorothy Gwajima akizungumza wakati alipokaribishwa ofisi ndogo za wizara mara baada ya kuapishwa leo Ikulu
 Picha ya pamoja(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
 Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo akizungumza  amempokea Katibu na Naibu Katibu wapya katika wizara hiyo baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais John Magufili leo, ambapo amewaasa kufanya kazi kwa weledi kwani wizara hiyo ni kubwa na ina mambo mengi.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Afya Dkt.Zainab Chaula aripoti kazini mara tu baada ya kuapishwa

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maemdeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya akizungumza wakati alipokaribishwa ofisi ndogo za wizara mara baada ya kuapishwa leo Ikulu
 Waziri wa Afya,Maendekeo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza Katibu Mkuu mpya wa Wizara yake Dkt.Zainab Chaula
 Dkt.Zainab Chaula akitoa salamu baada ya kukaribishwa Ofisi ndogo za Wizara hiyo,kushoto ni aliyekua Katibu Mkuu Dkt.Mpoki Ulisubisya
 Aliyekua Katibu Mkuu-Idara Kuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya akimkabidhi baadhi ya vitendea kazi Katibu Mkuu Mpya Dkt.Zainab Chaula kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara jihini Dar es Salaam

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkaribisha Katibu Mkuu Mpya wa Idara Kuu Afya Dkt.Zainab Chaula kwenye ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa
Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akitoa neno la ukaribisho wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya (hayupo pichani)


Picha ya pamoja ya Viongozi wa Wizara na baadhi ya watumishi waliopo ofisi ndogo ya wizara hiyo
Picha zote na Wizara ya Afya

TAASISI YA WAJIBU YATOA MAONI SAKATA LA SPIKA WA BUNGE NA CAG

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

TAASISI ya WAJIBU inayojihusisha na masuala ya uwajibikaji hapa nchini imetoa maoni yake kuhusiana na tamko la Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad juu ya kauli aliyoitoa kwenye mahojiano na kituo cha redio cha idhaa ya Kiswahili ya Redio ya umoja wa Mataifa (UN Redio)

Kupitia taarifa yao waliyoitoa kwa vyombo vya habari WAJIBU wameeleza kuwa wakiwa miongoni mwa taasisi fikra za uwajibikaji nchini wameona ni vyema itoe maoni huru kwa kuzingatia maslai mapana katika uwajibikaji na utawala bora nchini kwa kuzingatia kuwa Bunge na CAG ni vyombo vinavyotambuliwa kikatiba.

Katika maoni yao WAJIBU wamesema kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa taasisi hizo mbili katika kusimamia rasilimali za Umma na kukuza uwajibikaji na utawala bora ni vyema busara ya hali ya juu ikatumika baina ya pande hizo mbili. Na kueleza kuwa dhana za uwajibikaji na utawala bora nchini vitaimarika iwapo tu kutakuwepo na uhusiano na mzuri kati ya taasisi zote za uwajibikaji na usimamizi nchini.

Aidha wameeleza kuwa taasisi hizo mbili zina umuhimu mkubwa hivyo zinatakiwa kushirikiana kwa karibu sana katika kuimarisha uwajibikaji na utawala bora nchini na wameshauri wananchi kutoa maoni yatakayoboresha na kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo.

WAJIBU wamesisitiza kutumika kwa busara za hali ya juu bila kuathiri uhuru wa kikatiba uliotolewa kwa mhimili Bunge na kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali.

Sakata la unyanyasaji wa kingono, lamuweka pabaya muimbaji R-kelly...

AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NCHINI Marekani, Mjini Phoenix katika kliniki ya shirika la afya la Hacienda mwanamke mmoja aliyekaa mahututi (Koma) kwa miaka 10 amejifungua mtoto wa kiume katika kliniki hiyo.

Shirika la utangazaji la CNN nchini humo limeripoti kuwa Disemba 29 mwanamke huyo ambaye hakujulikana kama mjamzito hadi alipoonesha dalili za kujifungua, alijifungua mtoto wa kiume na polisi wa wameanza uchunguzi kwa udharilishwaji huo wa kingono kwa kutaka vipimo kwa damu (DNA) kwa wanaume  wanaofanya kazi kituoni hapo na taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa na Sajent. Tommy Thomson ilisema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Imeelezwa kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa kuwa amedharilishwa kingono alikaa kituoni hapo kwa muda mrefu katika kituo hicho cha Hacienda akipatiwa matibabu baada ya kupata tatizo hilo miaka 14 iliyopita.

Aidha imeelezwa kuwa hali ya mtoto aliyezaliwa ni njema kabisa na ulinzi katika kituo hicho umeimarishwa hasa kwa wanaume ambapo hawaruhusiwi kuingia Hacienda bila kuambatana na wasaidizi wakike.

Kliniki hiyo imelaani vikali tukio hilo na tayari mkurugenzi mkuu Bill Timmons ameachia madaraka mapema Jumatatu.

Hacienda ni kliniki maarufu nchini Marekani kwa kuhudumia watu wenye magonjwa sugu, watoto wachanga na watu wenye ulemavu.

MAGAZETI YA LEO AL HAMISI JANUARI 10,2019

SERIKALI HAITAWAVUMILIA WANAOPOTOSHA WAKULIMA

$
0
0

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewataka Wakulima kutokusikiliza maneno ya barabarani ya wapotoshaji na badala yake waendelee kuiamini Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Gavana Shilatu aliyasema hayo Leo Jumatano Januari 9, 2019 alipokutana na kufanya kikao na  Wakulima wakubwa wa Korosho wanaoishi Kata ya Mihambwe.

Gavana Shilatu amewataka Wakulima kusimama imara na kuwapuuza wale wote wanaopotosha maana halisia ya zoezi la uhakiki wa Korosho kwa Wakulima.

*"Rais Magufuli ameonyesha nia ya dhati ya kutaka kumkomboa kiuchumi Mkulima wa Korosho. Zoezi la uhakiki linafanywa kuhakikisha Mkulima halisia ananufaika na jasho lake na sote tupuuze maneno  ya vijiweni. Serikali ipo kwa ajili ya kusimamia haki na jasho la Mkulima linamnufaisha Mkulima mwenyewe. Serikali haitawavumilia wanaopotosha Wakulima, wanaopotosha nia njema ya Rais Magufuli Kwa Wakulima."* alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu alitoa ufafanuzi ikiwemo kujibu maswali ya Wakulima wa Korosho wa Mihambwe waliyokuwa nayo. 

*"Mambo Kama akaunti za Wakulima kutokufanya kazi, kuchanganya taarifa Kwa Mkulima ni baadhi tu ya changamoto ambazo kwenye zoezi la uhakiki zinarekebishwa. Nawasihi Wakulima kuwa wavumilivu."* alimalizia Gavana Shilatu.

Mpaka mwisho wa kikao Wakulima waliridhika na ufafanuzi na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha Kwa Serikali Kama desturi yao ilivyo.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi  ya Mtendaji kata ya Mihambwe kilihudhuliwa na Mtendaji Kata Mihambwe, Afisa Maendeleo kata ya Mihambwe, Serikali za Vijiji vilivyopo Mihambwe, Viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) wa Mihambwe pamoja na Wakulima wa Korosho.

UZALISHAJI SUKARI WAONGEZEKA TPC

$
0
0

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kulia) na Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakiwa ameshika sukari inayozalishwa katika kiwanda cha TPC kufuatia ziara waliyoifanya katika kiwanda hicho jana.
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kulia) na Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakiwa na uongozi nwa TPC,Bodi ya Sukari na Wataalamu wa Halmashauri.



Na Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Kiwanda cha Sukari TPC kimeongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 36,000 ambayo ilikua ikizalishwa mwanzoni kabla ya ubinafsishaji na kufikia tani 110,000 ikiwa ni juhudi za kutatua changamoto ya upungufu wa sukari ya majumbani nchini ambayo ni tani 100,005.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Utawala kiwanda cha TPC ,Jaffari Ally alisema hayo katika ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba pamoja na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda katika kiwanda hicho ambapo alisema kuwa bado wanaendelea na upanuzi wa mashamba na wanatarajia kuzalisha tani 120,000 .

Jaffari aliipongeza serikali kwa kuziba mianya ya biashara magendo ya sukari ambapo sukari zisizokidhi viwango zilizua zikiingizwa nchini na kushindanishwa katika masoko ya ndani hivyo kuathiri viwanda vya ndani.

“Wazalishaji wa sukari tunapenda kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuzibiti mianya ya uingizwaji holela wa sukari ,miaka ya nyuma soko lilichafuliwa na sukari iliyokua ikiingizwa nchini isiyokua na viwango na iliingizwa kwa njia ya magendo bila kulipiwa kodi wala ushuru ,sukari ambayo ilikua ikiathiri afya za watanzania tunaishukuru serikali kwa kuziba mianya” alisema Jaffari

Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mghumba baada ya kutembelea kiwanda cha sukari cha tpc yakiwemo mashamba mapya ya miwa ,aliwataka wawekezaji hao kupanua wigo wa kilimo cha miwa ili kuongeza uzalishaji wa sukari .

Omari alisema kuwa kuna fursa kubwa ya uwekezaji katika mashamba ambayo yanastawi miwa yaliyopo katika mikoa ya Pwani,Kigoma,Musoma ambapo kuna maeneo makubwa ya uwekezaji.

Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda alisema kuwa bado kuna fursa kubwa ya uwekezaji katika sukari ya viwandani ambayo ina soko kubwa ili kupunguza wimbi la kuagiza sukari ya viwandani kutoka nje ya nchi

NGOMA AFRICA BAND NA CD YAO MPYA AWAMU YA TANO HAPA KAZI

$
0
0
Si wengine ni ile bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ,inayoongozwa na mwanamuziki Kamanda Ras makunja wenye makao yao nchini Ujerumani,bendi hiyo iliyojizolea umarufu kila kona barani ulaya na kufanikiwa kuteka washabiki kwa kutumia muziki wao wa dansi wa bongo.

Ngoma Africa band ukipenda waite FFU ughaibuni au viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" mara hii wamepakua CD yao "Awamu Ya Tano Uwanjani" yenye nyimbo mbili za "Amkeni Kumekucha"  na "Awamu ya Tano Sasa Kazi"  nyimbo hizo ni utunzi na uimbaji wake Kamanda Ras Makunja akimshirikisha Chris-B  Bakotesa ambaye pia ni  solo gitaa na kundi zima la FFU wa Ngoma Africa band wakisindikiza kwa mdundo mzima wa Hapa Kazi Kumpigia Saluti na  kumuunga mkono Rais Magufuli.

Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC

$
0
0
Wafuasi wa Felix Tshisekedi awali walikusanyika nje ya makao makuu ya chama chake Limete, Kinshasa Jumatano


Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tume ya uchaguzi imesema.

Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Bw Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi wa urais mteule."

Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni.

Iwapo matokeo hayo yatathibitishwa, Bw Tshisekedi atakuwa mgombea wa kwanza kabisa wa upinzani kushinda uchaguzi wa urais tangu DRC ilipojipatia uhuru.

Bw Tshisekedi yuko kwenye muungano wa kisiasa aliyekuwa mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation) Vital Kamerhe UNC ambapo walikuwa wamekubaliana kwamba Tshiskedi atagombea wadhifa wa rais naye Kamerhe awe waziri mkuu iwapo muungano wao utashinda urais.

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 18.Mgombea wake aliyemteua kuwakilisha muungano tawala Emmanuel Ramazani Shadary amemaliza wa tatu.

Martin Fayulu ambaye awali alikuwa mgombea wa pamoja wa muungano wa upinzani kabla ya Tshisekedi na mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation) Vital Kamerhe kujiondoa kutoka kwenye muungano huo na kuunda muungano wao wawili, alimaliza akiwa nafasi ya pili.


TIMU YA MAAFISA HABARI WIZARA YA AFYA WASHUHUDIA UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYIKA SEKTA YA AFYA,WAIPONGEZA SERIKALI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zake iko katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya kwa kuangalia uwekezaji katika Sekta ya Afya katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza  kwenye Kampeni hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Gaudensia Simwanza amesema ziara hiyo katika Hospitali na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya ni kuangalia uwekezaji katika utoaji huduma bora za Afya kwa wananchi,kuhakikisha kuna nguvu kazi imara ya uzalishaji katika Sekta ya viwanda.

Amesema kuwa serikali imewekeza sehemu kubwa ya vifaa na mitambo katika hospitali na hali iliyofanya serikali kuokoa fedha nyingi kutibu wagonjwa nje ya nchi.

Simwanza amesema kuwa Hospitali ya MOI imekuwa na vifaa katika kila idara na kurahisisha utoaji huduma za Afya ambazo ni bora kutokana na Serikali kutilia mkazo uwekezaji wa vifaa tiba,mitambo, Dawa pamoja na vitendanishi.

Nae Afisa Habari wa MOI Patrick Mvungi amesema kuwa MOI itaendelea kutoa huduma bora kutokana na Serikali kuwekeza mashine mbalimbali zilizo kuwa changamoto,ambazo zilikuwa zinasababisha wagonjwa kupewa rufaa.

Mvungi ameipongeza serikali katika uwekezaji uliofanyika Hospitalini hapo pamoja na ujenzi wa majengo ya kisasa na kulaza wagonjwa kwenye 340 vitanda.Amesema katika ununuzi wa vifaa wamenunua Darubin ya kisasa ya sh.bilioni Moja.

Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kissenge amesema serikali imenunua mtambo wa sh.Bilioni Tatu na kufanya Taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma bora za Afya ndani na nje ya nchi.

Kissenge amesema kuwa Taasisi hiyo ni kati ya Taasisi 25 zinazotoa huduma za matibabu ya Moyo katika nchi za Afrika.Amesema magonwa ya Moyo yanatokana na wananchi kushindwa kufanya mazoezi pamoja hali ya ulaji wa vyakula.

Kissenge amesema kuwa nchi ya Thailand wananchi wake wanatumia baiskeli zaidi kuliko magari hali hiyo ni tofauti na hapa nchini ambao wanaona kutembea na magari ni ufahari. 
 Sehemu ya kufanyia  uangalizi wa magonjwa ya mwili wa binadamu kwa kutumia mitambo hiyo ambayo imenunuliwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli katika Hospitali ya MOI. 
 Daktari wa Hospitali ya MOI Ngina Mitti Akizungumza na waandishi wa habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
Daktari Bingwa wa Picha za MRI Rahma Hingora akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya katika Hospitali ya Mifupa (MOI) Jijini Dar es Salaam.

 Mgonjwa wa Figo Magesa Masigi akizungumza namna ya huduma za Afya zilizoboreshwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Muuguzi mwandamizi wa Kitengo cha Figo Moroa Nyamatara akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maduka ya MSD Betia Kaema akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
 Duka la MSD lilopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limejngwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
 Afisa Habari wa MOI Patrick Mvungi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Mafanikio ya Miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika uboreshaji wa upatikanaji wa vifaa katika Hospitali hiyo
 Jengo la MOI lilojengwa kwa udhamini wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
 Daktari Bingwa wa Hospitali ya MOI Hamis Shaban akizungumza na waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
 Meneja Uhusiano wa NHIF Akizungumza na wagojwa katika Hospitali ya MOI kuhusiana na utumiaji wa bima ya Afya katika Hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
 Jengo la Watoto katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo limejengwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pembe Magufuli.
Moja ya mtambo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI Ulionunuliwa kwa sh.bilioni tatu katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Maafisa Kilimo na ugani watakiwa kuwafuata wakulima mashambani kutoa elimu ya viwavi jeshi vamizi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza maafisa ugani wote wa mkoani humo kuhakikisha wanawafikia wakulima kwenye mashamba yao na kuwapa elimu ya kukabiliana na wadudu aina ya viwavijeshi vamizi ambao wanaonekana kuanza kuleta athari katika wilaya ya Nkasi.

Amesema kuwa wakulima wengi hawana elimu ya kukabiliana na wadudu hao hasa kujua aina ya dawa ya kutumia ili kuwaua na wasiendelee kuharibu mazao na kuongeza kuwa ni wakati wao sasa maafisa ugani kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi kupata matokeo bora ya mavuno kwa kutoa elimu ya kukabiliana na wadudu waharibifu na magonjwa.

“Kitu cha kufanya ni maafisa ugani wote na maafisa kilimo wote washuke kwenda kwenye mashamba, wakague na kutoa ushauri wa moja kwa moja, dawa zipo zinapatikana wanaanzia dawa gani inayofuata ni ipi, ili tuweze kuwasaidia wakulima waweze kuokoa haya mahindi, DC hawa watu wasimamiwe washuke asibaki mtu kwenye ofisi zao,” Alisisitiza.

Ameyasema hayo baada ya kuona athari ya viwavi jeshi alipotembelea shamba la mkulima wa mahindi Alex Ndenge katika ziara yake ya kuangalia maendeleo ya kilimo kwa wakulima na changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo upatikanaji wa pembejeo pamoja na mashambulizi ya wadudu na magonjwa ya mazao Wilayani Nkasi.

Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Mkoa wa Rukwa Ocran Chengula alifafanua namna ya kupambana na wadudu hao na kutoa tahadhari kwa wakulima kuwa na tabia ya kupanda kwa kipindi kimoja na sio kupishana kwani hali hiyo hupelekea wadudu hao kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kufuata mimea teke.

“Kuna sumu nyingine ukipiga inakuwa kwenye mmea, kwasababu huyu (mdudu) anatoa kinyesi kwahiyo ile sumu inaingia kwenye mmea kwahiyo anapokula anapata madhara anakufa, kwahiyo katika hatua za kwanza tunashauri (dawa aina ya) Duduba na hatua ya pili tunashauri dawa inaitwa “systemic” japo zina majina tofauti tofauti ni amjina ya kibiashara ila itumike hiyo baada ya kuona kwamba wameshaanza kutoa huu uchafu” Alieleza.

Kwa mujibu wa Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Emanuel Sekwao amesema kuwa viwavijeshi vamizi hao wameshaathiri kwa asilimia 2 mpaka 5 kutegemea eneo lakini bado haijafikia hatua ya wadudu hao kuharibu mimea kiasi cha kushindwa kuzaa.

Katika kipindi cha mwaka 2018/19 mkoa unalenga kulima jumla ya hekta 599,345.45 za mazao mbalimbali, kati ya hizo hekta 517,482.15 ni za mazao ya chakula na hekta 81,863.3 za mazao ya biashara.  Kutokana na eneo hilo mkoa unategemea kuzalisha jumla ya tani 1,817,171.84 za mazao ya chakula na biashara. Katika kiasi hicho tani 1,680,701.6 ni za mazao ya chakula na tani 136,470.25 ni za mazao ya biashara.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) akiwa pamoja na mwenye shamba hili Alenx Ndenge (kulia) pamoja na wataalamu mbalimbali wakiangalia namna viwavijeshi vamizi wanavyoanza kushambulia mimea ya mahindi wilayani Nkasi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) akiwa pamoja na mwenye shamba hili Alenx Ndenge (kulia) pamoja na wataalamu mbalimbali wakiangalia namna viwavijeshi vamizi wanavyoanza kushambulia mimea ya mahindi wilayani Nkasi.

RAIS DKT. SHEIN ATUNUKU NISHANI ZA MAPINDUZI NA UONGOZI ULIOTUKUKA VIWANJA VYA IKULU ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma kitabu cha Orodha ya Viongozi na Wananchi wanaotunukiwa Nishani katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Viongozi Mhe. Omar Ramadhan Mapuri, hafla hiyo ya kutunuku Nishani ilifanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishaji ya Vikundi vya Uhamasishaji wa Bendi ya Safari Trippers ya Marehemu Marijan Rajab, akipokea Mwakilishi wa Familia Ndg Ismail Issa Michuzi, alikuwa Katibu na Mpiga Trumpet Dar International, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishaji ya Utumishi Uliotukuka Mwakilishi wa Marehemu Mussa Haji Foum, alikuwa Mwandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali vya Redio. akipokea kwa niaba ya Familia Mtoto wa Marehemu Bi.Inat Mussa Haji, hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Ushujaa ya kujitolea kupiga mbizi katika pango la maji dimani kuchukua sampu ya mchanga ili kuweza kupata wingi wa maji Ndg. Ali Ameir Mwalim, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Nishani ya Ushujaa Mwananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja Ndg. Muhammad Haji Muhammad, kwa ujasiri aliouonesha kumuyokoa mwananchi aliyeingia katika kisiwa na kumuokoa akiwa hai.hafla hiyo ya kutunuku Nishani za Mapinduzi katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa ameshimama wakati ukipigwa wimbo la Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, kwa ajili ya Kutunuku Nishani za Mapinduzi kwa Viongozi na Wananchi kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 RAIS Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi , akisalimiana na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume, alipowasili katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, kuhudhuria hafla ya kutunukiwa Nishani Viongozi na Wananchi.
 BAADHI ya Viongozi Wastaaf na Wawakilishi wa Marehemu wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar wakisubiri kutunukia Nishani za Mapinduzi na Utumishi Uliotukuka,
 BENDI ya Brassband ya Jeshi la Polisi Zanzibar ikitowa burudani wakati wa hafla ya Utuaji wa Nishaji ya Mapinduzi na Uongozi Uliotukuka, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
BAADHI ya Viongozi wa Serikali wakiwa wamesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar,wa kwanza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud,Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mama Fatma Karume na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mhe Zuberi Ali Maulid.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Nondo, baada ya kumaliza hafla ya Kutunuku Nishani za Mapinduzi na Uongozi Uliotukuka, kushoto Katika Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiteta na Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mzee. Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, wakati wa hafla ya kutunuku kwa Nishani za Mapinduzi na Uongozi Uliotukuka.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wawakilishi wa Familia za Marehemu waliowakilisha katika kupokea Nishani kwa niaba ya familia.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wananchi waliotunukiwa Nishani ya Mapinduzi na Uongozi Uliotukuku, baada ya hafla ya kukabidhiwa Nishani hizo katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
 BAADHI ya Wananchi na Viongozi Wastaaf waliotunikiwa Nishani ya Mapinduzi na UYongozi Uliotukuka wakitoka katika viwanja vya Ikulu Zanzibar baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kutunukiwa Nishani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. (Picha na Ikulu)

Dkt. Kalemani aridhishwa na kasi ya uboreshaji wa kituo cha umeme cha Zuzu

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameeleza kuridhishwa kwake na kasi ya kampuni ya KEC ya nchini India ambayo imepewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika Kituo cha kupooza umeme cha Zuzu, Dodoma ambacho kinachoongezewa megawati 400 mbali  ya megawati 48 za sasa.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo leo jijini Dodoma baada ya kufanya ziara ya kukagua vituo mbalimbali vya kupooza umeme ikiwemo cha Msalato, Mnadani na Zuzu ambapo aliambatana na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wizara ya Nishati.

Hata hivyo, Dkt Kalemani ameeleza kuwa, mkandarasi huyo anapaswa kukamilisha kazi hiyo mwezi januari mwakani ili kuweza kuboresha zaidi hali ya upatikanaji umeme jijini Dodoma ambapo kazi ya uunganishaji umeme kwa wananchi inaendelea na hivyo kuongeza matumizi ya nishati hiyo muhimu.

Dkt. Kalemani amesema kuwa,  mkandarasi huyo anafanya kazi tatu ambazo ni kushusha umeme kwa kV 400 katika kituo hicho, kujenga kituo cha kupoza umeme cha uwezo wa megawati 400 na kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali mkoani Dodoma.

Ameongeza kuwa, mkandarasi huyo alianza kazi hiyo mwezi Machi mwaka 2018 ambapo gharama ya mradi huo ni Dola za Marekani milioni 53 ambazo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).

Aidha, baada ya kukagua vituo hivyo vya kupooza umeme, Dkt Kalemani amewaagiza TANESCO kuhakikisha kuwa kila kituo kinakuwa na fundi sanifu atakayekuwa kituoni kwa masaa 24 ili inapotokea hitilafu ya umeme, iweze kutatuliwa kwa haraka.

Vilevile, Dkt Kalemani ameagiza kuwa, kila kituo kiwe na vifaa vya ziada vya umeme badala ya kusubiri kuagiza vifaa hivyo mara linapotokea tatizo hali inayopelekea wananchi kukosa umeme na kueleza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu atakagua utekelezaji wa agizo hilo na Meneja ambaye hatatekeleza, atachukuliwa hatua.

Aidha ametoa agizo kwa TANESCO kuweka walinzi katika miundombinu ya umeme kwani kumekuwa na matukio ya baadhi ya wananchi kuhujumu miundombinu hiyo kwa namna mbalimbali ikiwemo kukata nguzo za umeme na pia ametoa wito kwa wananchi kuwa walinzi wa miundombinu husika.

Katika ziara hiyo pia Waziri wa Nishati alizungumza na wafanyakazi wa TANESCO katika kituo cha kupoza umeme kilichopo mjini Dodoma ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kazi wanazofanya, alionya kuwa, katika mwaka 2019, mfanyakazi atakayeonekana amefanya uzembe utakaopeleka kukosekana kwa umeme, atachukuliwa hatua.
 Baadhi ya mitambo ya umeme katika kituo cha kupooza umeme cha Zuzu jijini Dodoma.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO katika kituo cha Mjini Dodoma mara baada ya kukagua miundombinu ya umeme katika Kituo hicho. Wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.
 Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani kuhusu mitambo ya umeme katika kituo cha kupoza cha Mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya kupooza umeme katika eneo la zuzu Jijini Dodoma.

Wanafunzi watoro na wazazi wao kusakwa na kukamatwa huku hostel ikibadilishwa matumizi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Nkasi kuhakikisha anawatumia watendaji wa kata na vijiji pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuhakikisha wanawasaka na kuwakamata wanafunzi watoro pamoja na wazazi waoili kuhakikisha wanafunzi wote wanafika shule.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa fundisho kwa wazazi ambao kwa makusudi wanaacha watoto wao kutokwenda shule huku akipigia mfano faida ya elimu kwa kuwataja viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo yeye mwenyewe pamoja na wataalamu waliozingatia elimu na matokeo yake wamefanikiwa kimaisha.

“Kuna wanafunzi 173 watoro, hawajafika shuleni, sasa Mkurugenzi fuatilia shule yako, mkuu wa wilaya tumia watendaji wa vijiji, wa kata, kamati yako ya ulinzi, sakeni wanafunzi wote kamateni wazazi wao mpaka walete watoto wao shule, hatubembelezani hapa,”Alibainisha.

Ameyasema hayo alipotembelea shule ya sekondari Korongwe Beach katika Kijiji cha korongwe, kata ya Korongwe Wilayani Nkasi ili kujionea mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza pamoja na ujenzi wa madarasa ambapo wanafunzi 50 wamepangiwa kuanza kidato cha kwanza huku 17 tu wakiwa wameripoti na shule ikiwa na jumla ya wanafunzi 383.

Awali akitoa taarifa ya shule hiyo Mwalimu Mkuu wa shule Nicomedi Ntepele amezitaja changamoto za shule hiyo ikiwemo utorowa rejareja na wa kudumu, ukosefu wa madarasa na nyumba za waalimu, ofisi za waalimu na maji.

“miongoni mwa changamoto tulizonazo hapa shule ni pamoja na utoro wa wanafunzi wa reja reja na wa kudumu, ukosefu wa madarasa, pia wazazi kutokuwa na uelewa kuwaleta Watoto wao kuishi hostel, uhaba wa maji eneo la shule, ofisi za walimu kutokamilika hivyo tunaomba changamoto hizi kufanyiwa kazi ili tufanye kazi kwa ufanisi,” Alimalizia.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Missana Kwangula aliamua kubadilia matumizi ya hosteli ya wanafunzi wa kike kutumiwa na wanafunzi wa kiume baada ya Wangabo kumtaka ajibu maombi ya mwanafunzi Ibrahimu Musa ambaye pia ni kaka mkuu wa shule hiyo juu ya kujengewa hosteli  baada ya Mkuu wa Mkoa kutoa nafasi kwa wanafunzi kuuliza maswali.

“Wanafunzi tunatembea umbali mrefu hasa Watoto wa jinsia ya kiume, sisi tulikuwa tunaomba ndugu Mkuu wa Mkoa uweze kutujengea sisi pia hosteli ili na sisi tuweze kukaa bweni nasi tuweze kufanya vizuri katika masomo yetu,”Alisema

Katika shule hiyo ya Korongwe Beach Sekondari kuna hosteli ya wanawake iliyojengwa kwa msaada wa watu wa Japan (JAICA) pamoja na serikali ya Tanzania, hosteli ambayo kwa mujibu wa taarifa ya mwalimu mkuu wa shule haijawahi kutumika tangu kumaliziwa kwake, ndipo Mkurugenzi aliposema.

“Hosteli ile ilipojengwa ilikuwa ni kwaajili ya kuawasaidia Watoto wa kike kwasababu ndio wanachangamoto zaidi, lakini kwasababu hosteli ile hawaingii walengwa ambao wako hapa, tuna uwezo tu wa kuibadilisha matumizi na uiandika hosteli ya wavulana kuliko kujenga hosteli nyingine, tutakapobadili matumizi ninyi Watoto wa kike msige kuidai tena wakati ipo sasa hamuingii,” Alimalizia.

Shule ya Sekondari Korongwe Beach ina wanafunzi 383 na kushika nafasi ya kwanza kiwilaya katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018. Na wanafunzi 50 wamepangwa kuanza kidato cha kwanza huku 17 wakiwa wameripoti shuleni.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images