Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

TRA YAKUSANYA TRILIONI 7.9 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6 YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

$
0
0
Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 7.9 kwa kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 7.8 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo amesema makusanyo ya mwezi Desemba, 2018 yaliongezeka kuzidi makusanyo ya miezi yote iliyopita kwa mwaka huu ambapo TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.63.

“Mbali na makusanyo hayo ya mwezi Desemba, katika mwezi Novemba, 2018 TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.21 na mwezi Oktoba, 2018, zilikusanywa jumla ya shillingi trillioni 1.29. Nachukua fursa hii kuwashukuru walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati”, alisema Kayombo.

Kayombo aliongeza kuwa, katika kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya walipakodi, uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania umeamua kwamba, kila siku ya Alhamisi itakuwa ni siku maalum kwa ajili ya Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa TRA kote nchini kuwasikiliza na kutatua changamoto za walipakodi.

“Pamoja na kutenga siku hiyo maalum, tumeanzisha Kituo cha Ushauri kwa Walipakodi kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambacho kipo katika Jengo la NHC kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Bridge kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuwa karibu na walipakodi.  Tumeanza kwa Dar es Salaam lakini vituo hivi vitaendelea kufunguliwa katika mikoa mingine nchini”, alieleza Mkurugenzi Kayombo.

Aidha, Kayombo amewakumbusha wamiliki wa majengo kote nchini kulipia Kodi ya Majengo ambayo viwango vyake ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000/= kwa kila sakafu ya ghorofa na shilingi 20,000 kwa ghorofa za wilayani na vijijini.

“Sambamba na kuwakumbusha wamiliki wa majengo kulipia kodi ya majengo, napenda kuchukua fursa hii kuwasisitiza wafanyabiashara wadogo wadogo kuchangamkia vitambulisho vya wamachinga ambavyo vinapatikana nchi nzima katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa shilingi 20,000/=. Vitambulisho hivyo ni maalum kwa wale tu ambao mauzo yao ghafi hayazidi shilingi 4,000,000/= kwa mwaka”, alisisitiza Kayombo.

Mkurugenzi huyo wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kusema kuwa, TRA imeanza kampeni rasmi ya usajili wa walipakodi wapya kote nchini kwa kuwapatia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) bure katika maeneo wanayofanyia biashara.
  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, katika Ofisi za TRA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, katika Ofisi za TRA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA BENEDICT LIWENGA).

NAIBU WAZIRI MASAUNI AKABIDHI MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI GEREZA LA KWAMNGUMI WILAYANI KOROGWE

$
0
0
Serikali imeyataka Magereza yote nchini kutumia Wataalamu na fursa zilizopo katika maeneo yao kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli  kutaka Jeshi la Magereza liimarishe shughuli za uzalishaji kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akikabidhi mashine za kufyatulia matofali katika Gereza la Kwamngumi Wilayani Korogwe mkoani Tanga  ikiwa ni jitihada za serikali kutatua makazi ya askari nchini

Akizungumza wakati anakabidhi mashine za kufaytulia tofali kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza mkoani Tanga, Naibu Waziri Masauni alitoa wito kwa magereza yote nchini kutumia fursa zinazowazunguka huku akiweka wazi jeshi hilo kuwa na nguvu kazi ya kutosha na wataalamu mbalimbali.

“Maagizo ya Mheshimiwa Rais Magufuli ni kuona mnatumia nguvu kazi mliyonayo ya wafungwa kuzalisha na kuweza kusimama kwa uwezo wenu wenyewe, jambo hilo linawezekaana nikiamini mna fursa kubwa ikiwemo ardhi, wataalamu na nguvu kazi,” alisema Masauni

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi, Emmanuel Lwinga, ameiomba serikali iwasaidie katika umaliziaji wa hatua za mwisho wa nyumba hizo zitakazojengwa kwani imekua ni changamoto kubwa pindi wanapofikia mwisho wa ujenzi.

Akiishukuru Serikali kwa kuletewa mashine hizo, Mkuu wa Gereza la Kwamngumi, Mrakibu wa Magereza, Christopher Mwenda amesema watahakikisha wanatumia nguvu kazi ya wafungwa waliyonayo kutengeneza matofali imara na ameahidi mazingira ya gereza hilo kubadilika pindi ujenzi wa nyumba hizo utakapokamilika.

“Sasa tumepata vitendea kazi, awali tulikua tunapata taabu kwani tumejenga nyumba nne na ofisi moja kwa kutumia matofali ya kufyatua kwa mikono, ila kwa mashine hizo naahidi kuongeza uzalishaji wa matofali na kukaribia kumaliza tatizo la makazi wa askari katika gereza hili,” alisema Mrakibu Mwenda.

Jumla ya nyumba kumi zinatarajiwa kujengwa ndani ya mwaka huu katika Gereza hilo ikiwa ni kupambana na changamoto za makazi kwa askari wilayani Korogwe.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Emmanuel Lwinga (kulia), moja ya mikono ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa ili kuweza kutumika kufyatulia matofali yatakayotumika kujenga nyumba za askari ikiwa ni juhudi za serikali kutatua changamoto ya makazi kwa askari, makabidhiano hayo yamefanyika leo wilayani Korogwe, mkoani Tanga.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kiraia), akisikiliza maelezo ya Ujenzi wa Nyumba za Askari kutoka  kwa mmoja wa askari anaosimamia ujenzi wa nyumba hizo. Pichani ni mashine alizokabidhi Naibu Waziri ikiwa ni juhudi za serikali kutatua changamoto ya makazi kwa askari, makabidhiano hayo yamefanyika leo wilayani Korogwe, mkoani Tanga. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiongozana na Viongozi wa Magereza Mkoa wa Tanga baada ya kuwasili Gereza la Kwamngumi wilayani Korogwe, Tanga  kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

RAIS DKT.SHEIN AFUNGUA SKULI YA SEKONDARI NA MSINGI BWEFUM WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuifungua Skuli ya Seokndari na Msingi ya Bwefum Wilaya ya Magharibi B Unguja kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto Waziri wa Elimu na Mafunzio ya Amali Zanzibar Mhe. Rizi Pembe Juma,Skuli hiyo imejengwa na Kampuni ya Union Property Developers Ltd, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Kisasa ya Sekondari na Msingi ya Bwefum, Wilaya ya Magharibi B Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuwahutubia Wananchi na kuifungua rasmin Skuli hiyo.
(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkandarasi aliyejenga Majengo ya Skuli hiyo kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Quality Bulding Contractors Ltd. Mkurugenzi ,Mtendaji  Ndg. Shaib Said Ali, akitowa maelezo ya Majenzo ya Skuli hiyo yaliotengenezwa na Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Bwefum Kidatu cha Tatu Khamis Masoud.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, wakati Rais wa Zanzibar akitembelea moja ya Madarasa hayo alipotembelea baada ya kuifungua rasmin Skuli hiyo, ikiwa ni shamrashamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Bwefum Wilaya ya Magharibi B Unguja Masoud Mussa, Naifat Makame na Suleiman Sapu, wakiimba wimbo wa "Sisi Sote Tumegomboka " wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli yao, iliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,. Dk. Ali Mohamed Shein, Skuli hiyo imejengwa na Kampuni ya Union   Property Developers Ltd.

VIGOGO KAMPUNI YA VKP INVESTMENT FOUR YOUTH WAFIKISHWA KORTINI KWA KUJIPATIA MILIONI 300/- KWA NJIA YA UDANGANYIFU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 
Mkurugenzi wa kampuni  ya VKP Investment Four Youth, David Manot, mwanasheria wa kampuni hiyo Ernest Ngonyani na wenzao wanne wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa mashtaka 31 ya' kujipatia zaidi ya sh.milioni 300 kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la kula njama.

Washtakiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo pamoja na Manot ni, mfanyabiashara, Yona Kiita, Mkurugenzi wa masoko, Jane Isack, Afisa Masoko, Modikai Kilala na Meneja muendeshaji Juliana Kasambala. Mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando, imedaiwa na wakili wa serikali Ester Martin kuwa kati ya Januari 2016 na Desemba 2018 katika jengo la Mwalimu House lililopo Katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. 

Katika mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu washtakiwa wote hao wanadaiwa kati ya Novemba 21, 2017 na Aprili mahali hapo hapo, washtakiwa kwa nia ya kutenda kosa walijipatia fedha kupitia kampuni hiyo ya VKP investment for Youth kutoka kwa Anna Kavishe kwa kujifanya kuwa wangemuuzia kiwanja huku wakijua kuwa siyo kweli.

Washtakiwa hao wanadaiwa kupata kiasi tofauti tofauti cha pesa kutoka kwa Joel Olinda, Mlolu Chelehan, Shukuru Olomi, Emmanuel Mlambity, Agnes Joseph,  Christopher Mraha, Prowin Mtei, Mustapha Ngayoma,Chausiku Kinyehe, Issa Illy, Samson Ngayoma, Asha Mtangaza, Prisca Mrope Dotto Pangimoto, Nice Mohammed, Elizabeth Makombe na Elirehema Mangore.

Wengine ni, Mgaza William, Nataka Milivya, Joyce Chacha, Diana Mussa, Lucy Mpayo, Benson Mboya, Comfort Peter, Ilenedy Bongezi, Edwin Mwimbula, Emmanuel Messy, Azizi Mohammed na Anna Tarimo.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande hadi January 11, 2019 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutolewa maamuzi  juu  ya dhamana ya washtakiwa

TRA YAKUSANYA TRILIONI 7.9 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 6 YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 7.9 kwa kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Desemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 7.8 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo amesema makusanyo ya mwezi Desemba, 2018 yaliongezeka kuzidi makusanyo ya miezi yote iliyopita kwa mwaka huu ambapo TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.63.

“Mbali na makusanyo hayo ya mwezi Desemba, katika mwezi Novemba, 2018 TRA ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.21 na mwezi Oktoba, 2018, zilikusanywa jumla ya shillingi trillioni 1.29. Nachukua fursa hii kuwashukuru walipakodi wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati”, alisema Kayombo.

Kayombo aliongeza kuwa, katika kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya walipakodi, uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania umeamua kwamba, kila siku ya Alhamisi itakuwa ni siku maalum kwa ajili ya Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa TRA kote nchini kuwasikiliza na kutatua changamoto za walipakodi.

“Pamoja na kutenga siku hiyo maalum, tumeanzisha Kituo cha Ushauri kwa Walipakodi kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambacho kipo katika Jengo la NHC kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Bridge kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuwa karibu na walipakodi. Tumeanza kwa Dar es Salaam lakini vituo hivi vitaendelea kufunguliwa katika mikoa mingine nchini”, alieleza Mkurugenzi Kayombo.

Aidha, Kayombo amewakumbusha wamiliki wa majengo kote nchini kulipia Kodi ya Majengo ambayo viwango vyake ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000/= kwa kila sakafu ya ghorofa na shilingi 20,000 kwa ghorofa za wilayani na vijijini.

“Sambamba na kuwakumbusha wamiliki wa majengo kulipia kodi ya majengo, napenda kuchukua fursa hii kuwasisitiza wafanyabiashara wadogo wadogo kuchangamkia vitambulisho vya wamachinga ambavyo vinapatikana nchi nzima katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa shilingi 20,000/=. Vitambulisho hivyo ni maalum kwa wale tu ambao mauzo yao ghafi hayazidi shilingi 4,000,000/= kwa mwaka”, alisisitiza Kayombo.

Mkurugenzi huyo wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kusema kuwa, TRA imeanza kampeni rasmi ya usajili wa walipakodi wapya kote nchini kwa kuwapatia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) bure katika maeneo wanayofanyia biashara.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, katika Ofisi za TRA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, katika Ofisi za TRA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA BENEDICT LIWENGA).

UJUMBE KUTOKA MAREKANI WATEMBELEA LIFE AND HOPE MKOA WA PWANI

$
0
0
Ujumbe kutoka Chama Cha  Kisaikolojia Marekani umetembelea Kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani nchini Tanzania ili kujionea shughuli zinazofanywa na kituo hicho. Kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' kinajishughulisha na malezi ya watu walioathirika na aina zote za ulevi ikiwemo dawa za kulevya ambapo kipo mjini Bagamoyo.

Mratibu wa Safari hiyo, Dkt. Amanda Clinton kutoka  Chama Cha  Kisaikolojia Marekani, (American Psychological Association) amesema wamefurahishwa na hali waliyoikutam katika kituo hicho na kwamba wametoa ahadi ya kushirikiana na kituo hicho.m Alisema ni jambo la kufurahisha na kutia faraja kuona vijana wamekubali kukaa kwenye kituo ili kubadilisha tabia zao.

Aliongeza kuwa, nia thabiti huanza kwa muhusika wa tatizo kisha hatua inayofuata ni kupata mtu atakaemsaidia kuondoaa tatizo husika.lisema kwa mazingira aliyoyaona katika Kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' ana imani kuwa vijana hao watabadilika kitabia na hatimae kutimiza ndoto zao za kimaisha mara tu watakaporejea nyumbani.

Alifafanua kuwa, tayari nia imeonyeshwa na vijana hao, huku mtu wakuwasaidia yupo ambae ni Mkurugenzi wa kituo hicho cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji hivyo wana kila sababu ya kujivunia kutokana na maamuzi yao ya kujirekebisha kitabia. Aliendelea kusema kuwa tatizo la dawa za kulevya ni kubwa duniani hivyo jamii inapaswa kuchukua tahadhari na endapo athari imepatikana katika familia, na jamii kwa ujumla kila mtu ana wajibu wa kutoa msaada hata wa mawazo ili kusaidia wale walioathirika na dawa za kulevya.

Dkt. Amanda ambae ni mtaalamu wa saikolojia, alisema ili uweze kumsaidia mtu aliye athirika kisaikolojia kwanza unapaswa kumthamini na kumuona ni mtu muhimu katika jamii ili kile utakachomwambia aweze kukuelewa na kukubali mawazo yako. Msafara huo wa watu 15 kutoka Chama Cha  Kisaikolojia Marekani (American Psychological Association) umefurahia mazingira ya wanayoishi vijana hao na kusema hali hiyo inawanya wajione ni watu wenye thamani mbele ya jamii.

Awali akiwakaribisha wageni hao, Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji, amesema amefarijika na kufurahishwa kwa kufika ugeni huo ambao umefungua njia ya mafanikio ya kituo hicho. Bhanji alisema zipo changamoto kadhaa zinazokikabili kituo hicho ikiwemo ufinyu wa eneo na uelewa wa jamii kuhusu kituo hicho.

Alisema ili kufanikisha malezi ya vijana hao kituoni ushirikiano unahitajika kutoka kwa jamii, serikali na wadau mbalimbali ili kuwa kitu kimoja katika kusaidia vijana walioathirika na dawa za kulevya. Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha kuwatenga vijana walioathirika na dawa za kulevya na badala yake wake nao chini kujadilinamna ya kuwasaidia kutoka hapo walipo.

Alisema Kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' kinatoa fursa kwa wazazi na walezi kufika kupata ushauri na kuona namna gani ya kuwasaidia vijana ili warejee katika hali yao ya kawaida na hatimae walitumikie taifa lao.

Kwa upande wao vijana wanaopata huduma ya malezi katika kituo hicho wamesema wana matumaini ya kurejea katika hali zao za kawaida na kurudi katika familia zao kuendelea na maisha ya kawaida kama ilivyo kwa watu wengine. Aidha, walitumia nafasi hiyo, kuwaasa vijana kuacha makundi yenye vishawishi vya ulevi kwa ulevi wa aina yoyote humpelekea mtu kupoteza kabisa thamani kwenye jamii.

Waliongeza kuwa, utumiaji wa dawa za kulevya humfanya mtu kila pesa anayopata haitoshi hali inayopelekea kuuza kila kitu chake na vitu vya wenzie ili tu afanikishe uvutaji wa dawa za kulevya. Wakiongea kwa uchungu vijana hao wamesema wapo walipoteza mali zao, kazi zao, familia zao kwasababu ya matumizi ya dawa za kulevya
Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji (kulia) akisalimiana na kiongozi wa msafara huo mara tu walipowasili katika kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Dkt. Amanda Clinton (kushoto).
 Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevywa cha Bagamoyo mkoa wa Pwani Sober House, Al Karim Bhanji, akitoa taarifa fupi ya kituo hicho kwa wangeni kutoka Marekani  walipotembelea kituo hicho jana.
Mmoja  wa wameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya akitoa ushuhuda
 Mmoja  wa wameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya akitoa ushuhuda
 Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' na wageni wake.
Mkurugenzi wa kituo cha Life and Hope ''Sober House Bagamoyo'' Al-karim Sadrudin Bhanji, akiwa katika picha ya pamoja vijana wake wanaopata huduma katika kituo hicho huku wakiwa na furaha.(Picha na Emmanuel Massaka, MMG)

MUBASHARA KUTOKA IKULU LEO: RAIS MAGUFULI KATIKA HAFLA YA KUWAAPISHA VIONGOZI WALIOTEULIWA

TIBOROHA AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MISHAHARA KWA WACHEZAJI YANGA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kampeni za Uchaguzi wa Yanga zimeendelea kwa wagombea kunadi sera zao na kuwataka wanachama kuwapa ridhaa ya kuiongoza Klabu hiyo.Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, leo amezindua rasmi kampeni zake za kuwania nafasi ya mwenyekiti katika klabu hiyo

Katika uzinduzi wa kampeni yake, Tiboroha ameweza kuanika vipaumbele vyake iwapo atapatiwa ridhaa na wanachama basi ataanza na mikakati ya muda mfupi ambapo ni kuhakikisha wachezaji wanalipwa mishahara yao kwa wakati na hilo na katika uongozi wake changamoto hiyo haitajitokeza.

Amesema kuwa atahakilisha anajenga na kuimarisha taasisi hiyo kwenye masuala ya Kiuchumi ikiwemo kubadilisha mfumo wa uendeshaji na tayari kuna kampuni mbili zimeshafunguliwa kwa ajili ya uwekezaji zilizo chini ya jina la Yanga

“Tukienda katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji mtu wa kwanza niliyemfikiria ni Mwenyekiti wangu Yusuf Manji kwani ninaamini anaweza kutusaidia kwa sasa nataka aje kuwekeza ili apate faida tofauti na zamani,” amesema Tiboroha

“ Nashangaa kuna watu wanasema mimi nina ugomvi na Manji ila sio kweli nina ushahidi hapa katika simu yangu nimewasiliana nae tena mara kwa mara kwahiyo hayo ni maneno tu yanaongelewa mtaani,” ameongezea.

Pili , Tiboroha amesema atafanya juhudi za haraka kuirudisha klabu kwa wanachama na mashabiki wake. Pia amesema  atafanya kazi ya kuimarisha matawi, atajenga mara moja misingi ya uwekezaji na biashara, kuimarisha na kujenga mifumo ya klabu na kushirikisha wadau wote.

Tiboroha amefanya uzinduzi wake makao makuu ya klabu hiyo na kuwatambulisha  baadhi ya wajumbe wanane aliombatana  nao, ambao ni Ally Msigwa, Christopher Kashililika, Dominic Francis na Salim Rupia. Wengine ni Arfat Hadji, Said Barala na Peter Simon ambao wote ni wagombea katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.

Yanga inafanya uchaguzi wa kujaza nafasi Januari 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi ukiwa ni wa kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu katika nyakati tofauti.
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dr Jonas Tiboroha akiwa ananadi sera zake wakati wa uzinduzi wa Kampeni Makao Makuu ya Klabu ya Yanga leo Jijini Dar es  Salaam.

WANANCHI WALIOVAMIA ENEO KATA YA PANGANI WATAKIWA KUONDOKA MARA MOJA-RC PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MKUU wa Mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wananchi waliovamia eneo lenye ukubwa wa hekari 500 ,Pangani huko Kibaha na kujigawia viwanja waondoke mara moja .

Aidha amelitaka jeshi la polisi kumkamata mtu yoyote atakayekutwa kwenye eneo hilo na wale waliouziwa kwenda polisi ili wahusika ambao ni matapeli waweze kukamatwa kwani eneo hilo linamilikiwa kihalali.

Ndikilo aliyasema hayo alipotembelea eneo hilo ambalo linamilikiwa na mtu anayefahamika kwa jina la Seamens na maeneo mengine yenye ukubwa wa hekari 500 yanayomilikiwa na watu wengine wawili ambao hawajaendeleza kwa kipindi kirefu hivyo wananchi kuamua kujigawia viwanja kinyume na taratibu. 

Alieleza, wananchi hao wanapaswa waondoke ili halmashauri ifanye utaratibu wa kulirudisha eneo hilo serikalini baada ya mmiliki wake kushindwa kuliendeleza na kuwa pori, na sehemu ambayo watu wanauwa na kutupwa .

"Kuna watu 18 ambao wanajifanya ndiyo viongozi na wamewagawia watu maeneo, hatua 30 kwa 30 kwa kila mtu na eneo hilo wahalifu wamelifanya eneo hilo kwa ajili ya kupumzikia baada ya kufanya uhalifu au wanapowateka watu au kuwaua"alifafanua.

“Tunajua kuna mahitaji makubwa ya ardhi lakini si kwa utaratibu huu mchakato unaendelea tutapeleka mapendekezo kwa waziri wa ardhi nyumba na makazi naye atapeleka kwa Rais kwa ajili ya kufuta umiliki kisha Halmashauri litapanga utaratibu na kuwagawia wananchi kutegemeana na mahitaji ya viwanja na mipango miji ,” alibainisha Ndikilo.

Aliitaka hiyo kamati iliyounda na kuwauzia watu wawarudishie fedha wale waliowauzia kwani wamewatapeli na serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hilo kwani mara baada ya kurudi litapangiwa utaratibu kwani kwa sasa mji huo unapangwa ili kuelekea kuwa Manispaa 

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alisema kuwa wananchi hao kutoka maeneo mbalimbali ya Kibaha na Dar es Salam waligawana maeneo hayo ambayo yanamilikiwa na watu watatu.

Alieleza, mtu wa kwanza eneo lake lina ukubwa wa hekari 300 ,mwingine 200 na wa tatu 500 ambapo wananchi waliamua kugawana viwanja kinyume cha sheria .Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka alisema eneo hilo lina wamiliki hivyo ni vema kukaa nao na kuangalia mipango miji ya serikali katika kuupanga mji wa Kibaha.

NAIBU WAZIRI AWATAKA BODI YA UTALII KUTUMIA WATU MAARUFU KUTANGAZA VIVUTIO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WIZARA ya Maliasili na Utalii imewaagiza bodi ya Utalii nchini (TTB) kutumia fursa ya watu maarufu na mashuhuri nchini ili kuweza kujitangaza zaidi. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu wakati alipokutana na menejimenti ya TTB jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa fursa kubwa ya kutangaza vivutio vya kitalii nchini ni kuwatumia watu maarufu kwakuwa wanakuwa na wigo mpana na ushawishi kwa jamii za watu mbalimbali wanaokuwa wanawafuatilia. Kanyasu ametolea mfano wa baadhi ya wachezaji wa mpira wa miguu wanaocheza soka la kulipwa nje ya ukanda wa Afrika na hata wale waliokuwa ndani ya ukanda kuwatumia ili kufanikisha adhma ya kufikia watalii milioni 2 ifikapo 2020.

Ameeleza kuwa mbinu nyingine ya kuweza kujitangaza zaidi ni kuwapa mialiko watu mashuhuri hususani wakimbiaji wa riadha wa kimataifa ili kuja kushiriki katika mbio mbalimbali zinazokuwa zinafanyika Mkoani Arusha. “Kuutangaza utalii ni gharama kubwa sana ila lazima utumie fedha nyingi ili uweze kuingiza fedha zaidi, tunafahamu ufinyu wa bajeti kwa upande wenu ila tutajitahidi na kushirikiana nanyi katika kuhakikisha utalii unakuwa siku hadi siku,” amesema Kanyasu.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TTB Devotha Mdachi amesema kuwa wameshafanya mazungumzo na baadhi ya watu mashuhuri akiwamo Mbwana Samatta na Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ili kuwa mabalozi wa hiari kwa kututangazia vivutio vya nchini. Amesema mbali na hilo pia wana watu wengine tayari wameshakuwa mabalozi wa hiari akiwamo Yusuph Poulsen ambaye ni kijana mwenye asili ya kitanzania na wengine kutoka China na maeneo mengine.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akizunguma na wanahabari sambamba na kutoa maagizo kwa bodi ya utalii nchini TTB wakati alipotembelea ofisi zao

MWANRI AAGIZA UCHUNGUZI KWENYE UJENZI WA TENKI LA MAJI KATIKA KIJIJI CHA IBELAMILUND WILAYANI UYUI

$
0
0
Na Tiganya Vincent, Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesitisha kwa muda siku mbili kuendelea na ujenzi wa tenki ya ujazo wa lita laki tatu uliokuwa ukiendelea katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui baada ya kuzuka utata wa idadi ya nondo zilizokuwa zikitakiwa katika mzuko wake ambao unasababisha uduni wa ubora.

Hatua hiyo inalenga kutuma timu ya wataalamu ambao watakaochunguza kama ujenzi wake umezingatia maagizo yaliyopo kwenye ramani ya ujenzi na uko katika ubora unaotakiwa.

Mwanri ametoa kauli hiyo wilayani Uyui baada ya kauli za wataalamu kutofautiana na idadi ya nondo ambazo zimeshawekwa katika tenki hilo zikisubiri umwagaji wa zege

Alisema katika maelezo ya mkandarasi na takwimu zilizopo katika ramani zilionyesha kuwa tenki hilo lingechukua nondo 170 kukamilisha mzunguko lakini baada ya kuziheshabu zilikutwa 125.

Mwanri alisema ili kuepuka kujengewa tenki lililo chini ya kiwango ni vema wataalamu wapitie na kudhiirisha kuwa idadi ya nondo zilizosukwa katika tenki hilo zitatoa tenki bora.

Alisema likijengwa tenki chini ya kiwango cha matakwa ya michoro ya kihandisi linaweza kusababisha Serikali kupata hasara na kuwa na uwezekano kutokea maafa kama likipasuka kutokana na kutokuwa na ubora uliokusudiwa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alimtaka Mhandisi Mshauri wa mradi huo akiwa kama msimamizi Mkuu wa Serikali katika ujenzi wa mradi huo  kuhakikisha kazi inayofanyika inakuwa na ubora unaotakiwa na inalingana na fedha zilizolipwa.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema timu hiyo halitachukua muda mrefu ili kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unaendelea na  kukamilika kwa muda ulipangwa.

Katika hatua nyingine Mwanri aliwataka wakazi wa maeneo yote ambayo mradi hiyo ya kuleta maji kutoka ziwa Victoria inatekelezwa kuhakikisha wanalinda vifaa vya Wakandarasi kwa kuwafichua watu wachache wenye tabia mbaya za wizi ili kutokuwa kikwazo cha kukamilisha mradi kwa wakati.

Alitoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya uwepo wa wizi wa nondo na saruji katika mradi wa  ujenzi wa tanki la Nzega mjini.

Mwanri aliwaagiza Polisi kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuhusika na kuhujumu mradi kwa kuiba vifaa vya wakandarasi,

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Said Ntahodi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuwapelekea mradi wa maji katika Wilaya ya Uyui kutoka ziwa Victoria.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuwapunguzia adha ya kutafuta maji kwa watumishi na wananchi wa  maeneo ambayo mradi huo utapita na hivyo kuwapunguzia gharama za kutumia fedha nyingi kutafuta maji.

Ntahodi alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuwafikishia shukurani zao kwa Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwaondolea shida ya maji wakazi wa Isikizya na maeneo mengine ya Uyui.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Tabora(TUWASA) Mukama Bwire alisema kuwa jumla ya vijiji 33 vilivyopo kando kando ya barabara kutoka Nzega hadi Tabora watanufaika na huduma ya maji safi na salama mara baada ya kukamilika mradi huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (aliyechumaa) akipima upana wa nondo zilizotandazwa chini ya mradi wa ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui wakati wa ziara yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutembelea mradi wa maji wa ziwa Victoria.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akiwa ameshika nondo zilizoleta utata kabla ya kuanza zoezi za kuzihesabu ili kuona kama idadi yake inawiana na ile iliyopo katika mchoro wa ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui wakati wa ziara yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutembelea mradi wa maji wa ziwa Victoria.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akipima upana wa nondo zilizosukwa kwenye  mradi wa ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui wakati wa ziara yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutembelea mradi wa maji wa ziwa Victoria.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akiwa katika zoezi la kuhesabu nondo nyembamba zilizosukwa kwenye mradi wa ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui wakati wa ziara yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutembelea mradi wa maji wa ziwa Victoria. Picha na Tiganya Vincent
 Nondo za ujenzi wa tenki la maji katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui ambazo zimesababisha mashaka na kumfanya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kusitisha kwa muda wa siku mbili kuendelea ya ujenzi hadi hapo timu ya wataalamu kutoka Mkoani watakaidhinisha kuwa idadi yake inalingana na zile zilizopo katika michoro.

TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii. 

KATIKA mchakato  wa kuendelea kwa michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC)  Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  imetangaza kuwa itafanya droo ya Kombe hilo siku ya kesho Januari 10 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Hababari katika ofisi za TFF jijini Dr es Salaam. Afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo amesema, droo hiyo itakafanyika katika Makao Makuu ya Azam Tv, iliyopo Tabata majira ya saa 5 asubuhi na itahusisha raundi ya 4 zenye timu 32 na raundi ya 5 itakayohusisha timu 16.

Ndimbo amesema timu zilizobaki katika hatua hiyo ni  Young Africans SC, Azam FC, Lipuli FC, Mtibwa Sugar, KMC, Coastal Union, Kagera Sugar, Mbeya City, Stand United, JKT Tanzania.

Nyingine ni Singida United, Alliance FC, African Lyon, Biashara United, Boma, Namungo, Mbeya Kwanza, Friends Rangers, Majimaji FC, Dodoma FC, Pamba SC, Rhino Rangers, Reha FC, Dar City, Polisi Tanzania, Mashujaa, Transit Camp, The Mighty Elephant, Cosmopolitan, Kitayosce, La Familia FC, Pan African

Ameongeza, mshindi atakaeibuka katika mashindano  hayo ataipeperusha bendera na  kuwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, ambapo mwaka jana Mtibwa Sugar ndio waliibuka kidedea wa michuano hiyo.

WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO WAKIENDELA KUJIPATIA KIPATO CHA SIKU

$
0
0
Wafanyabiashara wakifanya biashara katika kituo cha mabasi Feri jijini Dar es Salaam   (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS KATIBA SHERIA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA AWEKA JIWELA MSINGI FARAJA LA KIBONDEMZUNGU ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akitoa hotuba ya Uwekaji wa jiwe la msingi  Daraja la Kibondemzungu   Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Kulia yake  ni Waziri wa  Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dkt,Sira Ubwa Mamboya  na kushoto yake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud  Jumbe.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya Kitaalam kuhusiana na Ujenzi wa Daraja la Kibondemzungu   Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.   
 Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya  Uwekaji wa Jiwe la Msingi  Daraja la Kibondemzungu   Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.  
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dkt,Sira Ubwa Mamboya katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi  Daraja la Kibondemzungu   Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
 Daraja la Kibondemzungu lililowekewa jiwe la msingi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman Wilaya ya Magharibi B Unguja.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR. 

TANESCO YAWAHIMIZA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KWENYE VIWANDA, UMEME BORA NA WA UHAKIKA UPO WA KUTOSHA

$
0
0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limewahimiza wananchi kuwekeza kwenye viwanda kwani hivi sasa umeme bora na wa uhakika upo, Meneja Miradi wa Shirika hilo, anayeshughulikia uzalishaji (Generation) Mhandisi Stephene S. A. Manda (pichani juu) amesema leo Januari 9, 2019.Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea utekelezaji wa miradi ya umeme Kinyerezi II wa Megawati 240 na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I wa Megawati  185.“Mradi wa Kinyerezi namba II wa Megawati 240 umekamilika, kwa hivyo ombi letu kwa wote ambao wanaweza kuwekeza kwenye viwanda wawekeze kwani umeme wa uhakika na wa kutosha  upo.” Alisema na kuongeza.Licha ya mradi huo wa Kinyerezi II Mradi mwingine ni wa upanuzi wa Kinyerezi I unaozalisha megawati 150 ili ufikie Megawati 335 kwa kuongeza Megawati 185.“Itakapofika Agosti 2019 jumla ya umeme utakaokuwa unatoka Kinyerezi pekee ni Megawati 575 kwa hivyo ni umeme wa kutosha, kama ni kulisha Dar es Salaam, basi Dar es Salaam nzima Kinayerezi inaweza kuibeba.” Alitoa hakikisho.Kwa hivyo uwezo wa kuhakikisha viwanda vinapata kile vinavyopasa kupata kuhusiana na umeme TANESCO imejipanga vizuri na tunaomba sana wawekezaji wawekeze, kiwanda si lazima kiwe kikubwa sana, hata cha kukoboa na kusaga nafaka na vile vya kukamua matunda ya kutoka Tanga na kwingineko. Alisema Mhandisi Manda.Alitoa wito kwa watanzania kuuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kujenga uchumi wa kati na wa viwanda kwani inawezekana kwa vile umeme upo, ulio bora na wa uhakika.
 Picha ya dron ikionyesha muonekano wa sasa wa mitambo ya kufua umeme wa gesi Kinyerezi II jijini Dar es Salaam. Mradi huo umekamilika na unafua umeme wa Megawati 240.
Meneja Miradi wa Shirika hilo, anayeshughulikia uzalishaji (Generation) Mhandisi Stephene S. A. Manda, akiwa kwenye chumba cha udhibiti mitambo (control room) cha kituo cha kufua umeme wa gesi Kinyerezi II leo Januari 9, 2019.


 Mhandisi Stephene S. A. Manda (katikati), akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Miradi wa kampuni ya Jacobsen Elektro Ingar Tollum Andersen (kulia) na Mtaalamu wa kusimika mitambo kutoka kampuni hiyo, Markku Siren wakati alipotembelea kuona maendeleo ya mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I leo Januari 9, 2019.

 Picha ya dron ikionyesha muonekano wa sasa wa mitambo ya kufua umeme wa gesi Kinyerezi II jijini Dar es Salaam. Mradi huo umekamilika na unafua umeme wa Megawati 240.
  Picha ya dron ikionyesha muonekano wa sasa wa mitambo ya kufua umeme wa gesi Kinyerezi II jijini Dar es Salaam. Mradi huo umekamilika na unafua umeme wa Megawati 240.
 Mhandisi Manda akiwa juu kabisa ya jengo la utawala la Kinyerezi II, akifafanua kukamilika kwa mradi huo ambapo amesema kazi iliyobaki ni kuimarisha bustani na kusafisha njia.
 Jengo la utawala Kinyerezi II kama linavyoonekana leo Januari 9, 2019.
 Jengo la karakana na ghala la vifaa.
 Mhandisi Manda akionyesha moja ya mashine mpya zilizoko kwenye karakana ya Kinyerezi II.
 Meneja wa Kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi II, Mhandisi Ambakisye Mbangula, akiwa kwenye karakana ya kituo hicho leo Januari 9, 2019.
 Meneja wa Kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi II, Mhandisi Ambakisye Mbangula, akiwa na mwangalizi wa karakana hiyo.
Mhandisi Manda akifafanua jambo kwenye chumba cha udhibiti mitambo (Control room) cha Kituo hicho.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA ATOA MAAGIZO KWA NSSF, AKERWA NA TABIA YA NENDA RUDI KUFUATILIA MAFAO

$
0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na baadhi ya Wanachama wa NSSF waliofika kwenye ofisi za NSSF Ilala/Temeke leo kufuatilia madai yao mbalimbali kufuatia maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii(SSRA), watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Chama cha waajiri uliofanyika Desemba 28, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam. Waziri Mhagama akiwa ameambatana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio amefanya ziara leo katika ofisi za Ilala,Temeke na Kinondoni kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Rais na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo Wanachama hao wakati wa kufuatilia madai yao kwenye ofisi hizo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio,wakati alipofanya ziara leo ya kutembelea ofisi za Ilala,Temeke na Kinondoni kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Rais na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanachama katika ofisi hizo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Uongozi wa NSSF wakimsikiliza mmoja wa Wanachama akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa kufuatilia madai yao ya mafao. 
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tusiime,Nobert Kamugisha ambaye amekwenda  kufuatiia madai yake kwenye Ofisi za NSSF Ilala Boma leo,akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo mbele ya  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Baadhi ya Wanachama wa NSSF wakiwa kwenye Ofisi za Ilala Boma wakifuatilia madai yao mbalimbali,walipokuwa wakimsikiliza  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),William Erio akitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo madai ya Wanachama wa shirika hilo,mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama .

Baadhi ya Wanachama wa NSSF wakiwa kwenye Ofisi za Ilala Boma wakifuatilia madai yao mbalimbali,walipokuwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Uongozi wa NSSF wakiwasikiliza baadhi ya Wanachama wa shirika hilo waliofika kufuatilia madai yao mbalimbali katika ofisi za shirika hilo zilizopo Ubungo Plaza,jijini Dar.

======  ======  ========

WAZIRI JENISTA MHAGAMA ATOA MAAGIZO KWA NSSF, AKERWA NA TABIA YA NENDA RUDI KUFUATILIA MAFAO 

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge, Kazi ,Vijana na Ajira) Jenista Mhagama ameutaka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuhakikisha wanalipa mafao ya wastaafu kwa wakati huku akiwataka watumishi wa mfuko huo kufanya kazi kwa kujituma ya kuhudumia wastaafu nchini.

Mhagama ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ofisi za NSSF za Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia iwapo maagizo ya Rais Dk.John Magufuli ya kuwalipa wastaafu ambao wanadai mafao yao kama yameanza kutekelezwa ama la. Akiwa kwenye ofisi hizo Waziri Mhagama amesema, ameshuhudia maagizo ya Rais Magufuli yameanza kutekelezwa na NSSF lakini bado kuna baadhi ya changamoto ambazo lazima zipatiwe ufumbuzi. 


Amesema,moja ya changamoto ni tabia ya nenda rudi kwa wastaafu na wanapowaambia waondoke wanaondoka na fomu zao badala ya kuacha zishughulikiwe."Tabia hii ya nenda rudi sasa iwe basi na nimeshatoa maagizo ya kuwepo kwa mabango yenye namba za simu zote kwa kuwekwa wazi,"amesema.

"Waziri Magufuli amesisitiza umuhimu wa mafao ya wastaafu kushughulikiwa kwa wakati na kama watumishi hawatoshi kwenye ofisi hizo za Ilala na Temeke basi walioko makao makuu wahamishiwe kwenye ofisi hizo ili kutoa huduma kwa wanachama wao"."Ni vema NSSF wakahakikisha wanatoa huduma bora kwa wanachama, Kipaumbele lazima kiwe kuwahudumia wanachama wetu ambao ni wastaafu kwani wamefanya kazi kwa heshima, wao ni mashujaa na lazima washughulikiwe kishujaa badala ya kuwasumbua,"amesema Waziri Mhagama.

Amesema kuna baadhi ya watumishi wa NSSF wamekuwa na kauli za hovyo kwa wanachama wao na hivyo kutoa maagizo kwa kuwataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kujituma kama sehemu ya kuenzi kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli ya kuwapigania wastaafu nchini.

Pia amesema kuna mameneja ambao wanataka kuonwa kwa apointiment na hivyo ametaka tabia hiyo iachwe mara moja na kwamba hata yeye ofisini kwake wanaohitaji kumuona wanakwenda bila apointment.Waziri Mhagama amewataka NSSF kufanya mabadiliko ya kimfumo ya kiutendaji kwa lengo la kuleta ufanisi wa kuwahudumia wanachama wao na kwamba anachotaka kuona ni kwamba kuna kuwa na urahisi wa kulipwa kwa mafao."Kuwe na malipo jana, yaani kwa maana ya kwamba wakati mwanachama anakuja NSSF tayari akute utaratibu wa kushughulikia malipo yake ulishafanyika kabla na anapokuja ni kuchukua fedha zake na kuondoka,"amefafanua Waziri Mhagama.

Wakati huo huo, Waziri Mhagama amesema kuna baadhi ya watu wasiowaaminifu wanatumia kipindi hiki kutaka kufanya udanganyifu ili walipwe mafao kwa kupeleka nyaraka za uongo na hivyo amewataka wenye
tabia hiyo watambue watachukuliwa hatua."Kuna baadhi ya watu wanakwenda na vielelezo feki ili wapewe mafao na NSSF, tutaanza kuja na askari kanzu kwa ajili ya kuwakamata watu wa aina hiyo ambao kimsingi wanataka kufanya utapeli.Pia kwa NSSF lazima mboreshe mfumo wenu ambao utabaini wale wanaotaka kufanya utapeli wa fedha hizi za wanachama,"amesema.

MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI

$
0
0
 Rais wa mtandao wa wasanii wa Injili na Maadili Dkt. Godwin Maimu akizungumza katika Tamasha hilo lililofanyika Buza Jijini Dar es salaam Buza Kipera
 Picha ya Viongozi wa Mtandao wa wasanii wa Injili na maadili wa pili kutoka kulua ni Rais wa Tagoane Taifa Dkt. Godwin Maimu, aliyrpo kushoto kwake ni Katibu mkuu Mchungaji Lucy, wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu mwenza Silvanus Mumba akifuatiwa na Makamu wa Rais Tagoane, Florah Sungura. 
 Mchungaji mwenyeji Tamasha lilipofanyika Apostal Israel Popapo kutoka  Jijini Dar es salaam, katika  kanisa la ETERNITY GOSPEL CHURCH, Buza Kipera
 Uimbaji ukiendelea kama inavyoonekana katika picha kafika kanisa la ETERNITY GOSPEL CHURCH Buza Kipera
 Picha ya pamoja ya wasanii mbalimbali wa Injili waluohudhuria katika tamadha hilo lililopewa jina la Madhabahu ya shukrani


NA.VERO IGNATUS

Mtandao wa wasanii wa Injili na maadili Nchini(Tagoane) wanafanya Tamasha leo la kutoa shukrani kwa Mungu kwa kuwapa ulinzi na Kibali tangia kuanzishiswa kwa mtandao huo

Akizungumza  katibu mkuu mtendaji  Tagoane Taifa Silvanus Mumba amesema kuwa Tamasha hilo wamelipa jina la Tukuza Festival Madhabahu ya shukrani ambapo wananzia Jijini Dar es salaam ndipo wataelekea mikoa mingine

Amesema lengo kuu ni kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea tangia kuanzishwa kwa mtandao huo sambamba na mafanikio yaliyopatikana ya kuwaleta waimbaji wa pamoja.

Silvanus amesema kuwa hadi sasa wamekuwa na  Mafanikio Makubwa tangia kuanzishwa kwa TAGOANE, wameweza kusaidia Watoto Yatima, wameutangaza Utalii wa ndani wameweza kusaidia Vifaa vya matibabu katika  Hospitali Mount Meru sambamba na kusaidia Vijana Elimu juu ya ujasiliamali,

Akielezea matazamio waliyonayo ni  kuweza kuwasaidia wasanii Kuwa na UCHUMI imara kupitia Mfuko wa TAGOANE LOAN FUND, Kuwa na Wasanii walio Tayari kujito kwaajili ya Jamii na makundi Maalumu Kama Wazee, Yatima, wajane, vilema, na Wagonjwa

Amesema kuwa  wanaendelea Kuwa na Utaratibu wa Kuibua vipaji Mashuleni kwa Kushirikiana na Taasisi ya waalimu wa shule BinafsiTanzania (TPTU) Lakini pia Kujiunganisha na wadau wa Maendeleo Kama SIHAONE TUNAPENDANA Ltd

Tunapenda kuwaambia Wasanii wote, wakristo walio Kwenye sekta ya Sana, kujiunga na TAGOANE kwasababu ndio Pahala sahihi amvako wataweza kujiweka Akiba na kukopa inapohitajika, Kupata Fursa ya Mafunzo ya ujasiliamali na Sheria ya hatimiliki, Elimu juu ya Ubunifu Lakini pia Watajitolea kwa jamii pia ifaidike kupitia yeye

Mikoa mingine ambayo wanatazamia kufanya Tamasha hilo ni pamoja na Dodoma, Morogoro, kwa sasa wameanza na Jiji la Dar es salaam mikoa mingine wataendelea kutoa taarifa ,  lengo kuu ni Kumpelekea Mungu Shukurani za pekee kwa Kuisimamisha Tagoane Kuwa ya Mfano. 

Dkt.Zainab Chaula aripoti wizara ya afya

$
0
0
Picha ya pamoja ya Viongozi wa Wizara na baadhi ya watumishi waliopo ofisi ndogo ya wizara hiyo
Waziri wa Afya,Maendekeo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza Katibu Mkuu mpua wa Wizara yake Dkt.Zainab Chaula(picha na Wizara ya Afya).
Dkt.Zainab Chaula akitoa salamu baada ya kukaribishwa Ofisi ndogo za Wizara hiyo,kushoto ni aliyekua Katibu Mkuu Dkt.Mpoki Ulisubisya 

Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akitoa neno la ukaribisho wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya (hayupo pichani)
Aliyekua Katibu Mkuu-Idara Kuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya akimkabidhi baadhi ya vitendea kazi Katibu Mkuu Mpya Dkt.Zainab Chaula kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara jihini Dar es Salaam
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkaribisha Katibu Mkuu Mpya wa Idara Kuu Afya Dkt.Zainab Chaula kwenye ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK,ALI MOHAMED SHEIN ATUNUKU NISHANI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI WA SERIKALI YA ZANZIBAR

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Bw.Said Bakari Jecha katika Hafla ya Kutunuku Nishani iliofanyika katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Utumishi uliotukuka Bi Fatma Mohamed Said katika Hafla ya Kutunuku Nishani iliofanyika katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria katika Hafla ya Kutunuku Nishani iliofanyika katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi na watunukiwa wa Nishani katika Hafla ya Kutunuku Nishani iliofanyika katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Serikali Yashinda Kesi Dhidi ya Wanaharakati Kuhusu Kanuni za Maudhui Mitandaoni

$
0
0

Na: Beatrice Lyimo, MAELEZO

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imehukumu kwamba Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo hakukosea wala kukiuka Katiba kwa kutunga Kanuni za Maudhui Mitandaoni za mwaka 2018.

Hayo yamejidhihirisha baada ya Mahakama hiyo kusikiliza na hatimaye kuitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, Bodi ya Wadhamini wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetea Haki za Binadamu Tanzania (Human Rights Defenders Coalition) dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Katika shauri hilo walalamikaji wameshindwa kuthibitisha jinsi gani Kanuni hizo zitakavyo athiri haki za msingi za Walalamikaji katika masuala ya uhuru wa habari na mawasiliano ya mitandaoni.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa leo Januari 9, 2019 Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, imekubaliana na hoja za Mawakili wa Serikali kuwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni zimetungwa kwa mujibu wa sheria na kupelekea Mahakama hiyo kutupilia mbali shauri hilo.

Shauri hilo liliendeshwa na mawakili kutoka Ofisi Mpya ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao ni Bibi Alesia Mbuya, Bw. Ladislaus Komanya, Bw. Sylvester Mwakitalu, Bw. Johanes Kalungura, Bw. Killey Mwitasi, Bw. Abubakar Mrisha na Bibi Neisha Shao ambapo upande wa walalamikaji waliwakilishwa na mawakili Fulgence Masawe, James Marenga na Jeremia Mtobyesa.

Kwa hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Septemba 4, 2018, sasa ni rasmi madai ya kwamba Kanuni hizo zinabana uhuru wa habari na kwamba zilitungwa kimakosa yaaanguka rasmi.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images