Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

YANGA YAPELEKA VIJANA KOMBE LA MAPINNDUZI

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kikosi cha Yanga kimewasili Visiwani Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi lililoanza kutimua vumbi Januari Mosi 2019 na kufikiwa tamati Januari 13, 2019.

Kikosi hicho kinaongozwa na Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila akisaidiwa na Kocha wa timu ya Vijana Said Maulid 'SMG', daktari wa timu Edward Bavu, Meneja wa timu  Nadir Haroub "Canavaro" na  Mohamed Ali.

Yanga watashuka dimbani kesho saa 2.15 wakiumana na KVZ ukiwa ni mchezo wa kwanza kwenye mashindano hayo kwenye dimba la Amani Zanzibar. Wachezaji hao ni 


1. Maka Edward

2. Haji Mwinyi
3. Said Makapu
4. Matheo Anthony
5. Erick Msagati
6. Deo Mkami
7. Ibrahim Abrahaman
8. Ibrahim Ahmed
9. Deus Kaseke
10. Mustapha Seleman
11. Abuu Shaban
12. Ramadhan Mrisho
13. Mohamed Salumu
14. Cheda Hussein
15. Yasini Salehe
16. Salumu Mkama
17. Faraji Kilaza
18. Bakari Athman
19. Said Khasimu
20. Shaban Mohamed
21. Jafari Mohamed
22. Pius Buswita
23. Juma Abdul 

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZINDUA MRADI WA VITUO VYA UOKOZI NA UZAMIAJI VYA KMKM ZANZIBAR

0
0
BOTI ya Kisasa ya Uokozi na Uzamiaji ya Kikosi cha KMKM Zanzibar imezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Ali Mohamed Shein,.leo katika bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba, wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Vituo Vya Uokozi vya KMKM.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Boti ya Mradi wa Vituo vya Uokozi na Uzamiaji vya Kikiso cha KMKM Zanzibar,uzinduzi huo umefanyika katika, bandari ya Mkoani Pemba leo,2-1-2019.kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi Maalum. Mhe Haji Omar Kheri na kulia Mkuu wa KMKM Commodere Hassan Mussa Mzee.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza CDR.Hussein Ali Makame, akitowa maelezo kwa Rais wakati akitembelea Boti hiyo baada ya kuizindua leo katika Bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni shamrashamra za Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika Boti ya KMKM ya Uokozi baada ya kuizindua akiwa na Mkuu wa KMKM Commodore Hassan Mussa Mzee, (Picha na Ikulu) NO 5665///RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Hemed Suleiman wakiondoka katika eneo la Bandari ya Mkoa baada ya Uzinduzi wa Boto ya KMKM ya Uokozi na Uzamiaji.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua Kituo cha Mradi wa Uokozi na Uzamiaji cha KMKM Zanzibar, wakati wa shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza CDR. Hussein Ali Makame. akitowa maelezo ya kimoja ya vifaa vya Uokozi baada yya kukifungua Kituo cha KMKM Cha Mradi wa Uokozi na Uzamiaji katika Bandari ya Mkoani Pemba.(Picha na Ikulu).
JENGO Jipya la Kituo cha KMKM la Mradi wa Vituo vya Uokozi na Uzamiaji lilioko katika Bandari ya Mkoani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 

AZAM FC KUANZA NA JAMHURI LEO USIKU MICHUANO YA MAPINDUZI CUP

0
0
Na Ripota Wetu, Zanzibar.

MABINGWA watetezi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya  Jamhuri ya Pemba, mchezo utakaofanyika Uwanja Amaan, Zanzibar saa 2.15 usiku.

Kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa wa michuano hiyo mara mbili mfululizo, kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi kwenye Uwanja wa Dimani, tayari kujiweka sawa na mtanange huo unaotarajia kuwa mkali.

Akizungumza kuelekea mchezo wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri,  Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Van Der Pluijm, alisema kuwa wanaingia na malengo ya kujaribu kutwaa taji hilo na kuendeleza rekodi nzuri waliyokuwa nayo kwenye ushiriki wao kila mwaka.

“Unapoenda kwenye michuano, hauendi tu kwa lengo la kushiriki au kujaza idadi ya timu, tunataka kushinda taji, tunapaswa kufanya hivyo kama tunavyofanya katika ligi mechi hadi mechi, tunajiandaa kila wakati hasa kujenga saikolojia na akili, hili ni jambo la muhimu sana kwa wachezaji wa Kitanzania,” alisema.

Huo utakuwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa timu hizo kukutana, mara ya mwisho kukutana ni kwenye michuano iliyopita na Azam FC kuichapa mabao 4-0, yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Bernard Arthur, kiungo Salmin Hoza, Yahya Zayd na Paul Peter.

Aidha timu hizo pia ziliwahi kukutana kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo mwaka 2012, na Azam FC kuandika rekodi ya kutwaa taji la kwanza kati ya manne ya Kombe la Mapinduzi, ikishinda mabao 3-1, yaliyofungwa na gwiji wa timu hiyo, John Bocco ‘Adebayor’, Mrisho Ngassa na Mrisho Ahmed aliyejifunga.

Azam FC ipo Kundi B la michuano hiyo, sambamba na timu nyingine za Yanga, Jamhuri, KVZ na Malindi.



Kikosi cha Azam FC

Article 1

0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Sulemani Jafo ameonyesha kukerwa sana na uzembe uliofanywa na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwa kusasua ujenzi wa kituo cha Afya Mikumi licha ya kupokea fedha tangu mwishoni mwa mwezi June 2018. 

Katika ziara hiyo ya kushtukiza watendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilosa inaonekana walidamka asubuhi ya leo na kupeleka mchanga zaidi ya Maroli sita pamoja na fundi aliyekuwa akichanganya mchanga huo ili ionekane kazi inaendelea lakini waziri Jafo aligundua janja hiyo na kutoa maagizo mazito kwa Uongozi wa Halmashauri hiyo. 

‘ Niwatake Mkurugenzi wa Kilosa, Mweka Hazina, Mkanga Mkuu wa Wilaya, Afisa Mipango pamoja na Mhandisi kuwasilisha barua zenu haraka sana Ofisi ya Rais Tamisemi za kujieleza kwanini msichukuliwe hatua kutokana na uzembe mlioufanya katika kituo hiki’ aliagiza Jafo. 

Aliongeza kuwa Mpaka sasa kituo hikinwapo katika hatua ya msingi wakati wenzao wa maeneo mengine waliopewa fedha wakati mmoja wakiwa katika hatua za umaliziaji. 

Ziara hiyo ya waziri Jafo Mkoani Morogoro amefanikiwa kutembelea ujenzi wa kituo cha afya Mikumi, ujenzi wa kituo cha afya Kidodi, pamoja na kutembelea eneo la Luhembe ambapo patajengwa daraja kubwa litakalo gharimu zaidi ya shilingi milioni mia nane.
Kifusi cha mchanga kilicholetwa muda mfupi kabla ya Waziri Suleiman Jafo kuwasili .
Waziri Suleiman Jafo akitembelea eneo la ujenzi kituo cha afya mikumi 
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi pamoja na Mbunge wa Mikumi Mh. Joseph Haule wakinuahidi waziri Jafo usimamizi wa makini wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mikumi 

MAJALIWA AWASILI SONGEA KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI RUVUMA

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uhakikishe kuwa vijana wote wanaomaliza darasa la saba kwenye kila Halmashuri za mkoa huo wanakwenda kuanza kidato cha kwanza. Aametoa agizo hilo leo (Jumatano, Januari 2, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasili kwenye uwanja ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema Halmashuri zote za mkoa huo zijikite katika kujenga madarasa ili wanafunzi wote waliofaulu ambao wanatakiwa kwenda sekondari waende. Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuahakikisha kwamba watoto wote wenye sifa za kupata elimu ya seondari wanapata elimu hiyo kote nchini hivyo juhudi za makusudi lazima zifanywe na kila Halmashauri ili kutimiza azma.

Akizungumzia suala la utoro shuleni, Waziri Mkuu amesema hilo ni moja kati ya maeneo yanayozorotesha juhudi kubwa za Serikali za kuwapatia watoto wa Tanzania elimu katika maeneo mengi nchini na lazima viongozi wa wilaya na mikoa wasimame imara ili kukomesha hali hiyo. Amesema viongozi wa ngazi zote katika mikoa na wilaya ndiyo hasa wanaoweza kumaliza tatizo la utoro wakishirikiana kwa karibu na wanavijiji ambao wanaishi na watoto hao na wanajua ni watoto wangapi hawaendi shule.

Hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kutoa maelekezo na miongozo itakayowabana watoto watoro pamoja na wazazi au walezi wao kwani wanayo mamlaka na uwezo wa kuchukuwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi. Akizungumzia zao la korosho , Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mkoa wa Ruvuma kuwaondolea hofu wananchi wanaolima zao hilo katika mkoa huo kwa kuwahakikishia kwamba Serikali inazo fedha za kutosha kununua korosho zote ziliyovunwa na wakulima.

Kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kubeba dhamana waliyopewa na Taifa ambayo ni pamoja na kusimamia ukusanyaji mapato ya Serikali kwa kishirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). "Halmashauri zote na wakuu wa wilaya wasimamie kwa dhati ukusanyuaji wa kodi."

Akiwa mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu kesho anatarajiwa kufungua soko la mazao la Lilambo katika wilaya ya Songea, kufungua ghala la mazao la Mgazini na kuweka jiwe la msini la ujenzi wa zahanati ya Luganga na kisha kuhutubia mkutano wa hadhara.

Keshokutwa Waziri Mkuu ataongoza kikao cha wadau wa zao la kahawa kitakachowashirikisha pia Waziri wa Kilimo na Mrajisi wa Ushirika. Wengine watakaoshiriki katika kikao hicho ni viongozi wa AMCOS, UNION na viongozi wa Bodi ya kahawa.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani  humo, Januari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakisalimiana  na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho  wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, Januari 2, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina, Mndeme. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, Januari 2, 2018. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Wakazi wa Dodoma watakiwa kuchangamkia fursa ujenzi wa Mji wa Serikali

0
0

Na Teresia Mhagama, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua amewaasa wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa za kazi za ujenzi zinazoendelea katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.

Katibu Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dodoma baada ya kukagua kazi ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati ambapo aliambatana na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Haji Janabi pamoja na wajumbe wa Kamati ya ujenzi huo wakiongozwa na Katibu wa Kamati, Maseke Mabiki.

Akiwa katika eneo hilo la ujenzi, Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amemweleza Katibu Mkuu kuwa, kazi za ujenzi zinaendelea usiku na mchana lakini kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa vibarua wa kutosha watakaoweza kuf anya kazi muda wote.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (aliyenyoosha mkono) akiangalia jinsi kazi za ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati unavyoendelea katika Mji wa Serikali jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga na kushoto kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Haji Janabi.
 Kazi za ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati zikiendelea katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma.
Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati unaoendelea jijini Dodoma . Wanaosikiliza ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (wa pili kushoto) na Wajumbe wa Kamati ya Ujenzi ya Wizara ya Nishati.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAENDELEO KATIKA UJENZI WA MJI WA SERIKALI IHUMWA DODOMA

0
0
 Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma  leo wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
 Muonekano wa jengo la Ofisi ya Rais,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma  kama linavyoonekana ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika katika muda uliopangwa.
  Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe akionesha kazi ya usimikaji wa miundombinu ya umeme inayofanywa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
 Mkadiriaji Majenzi kutoka  Vikosi vya Ujenzi vya Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bi Selemina Rutambanzibwa akieleza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara hiyo kwa Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma  Bw. Meshach Bandawe leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI NA MKEWE JANETH MAGUFULI WAMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU DKT. SALIM AHMED SALIM

0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim hospitalini Jijini Dar es Salaam, alipomtembelea pamoja na Mkewe Janeth Magufuli ili kumjulia hali.Januari 2 ,2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiomba Dua Maalumu na Mama Janeth Magufuli pamoja na Mama Amne Salim (Mke wa Dkt.Salim) ya kumuombea Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim, walipomtembelea ili kumjulia hali Jijini Dar es Salaam. Januari 2 ,2019
PICHA NA IKULU

WAMACHINGA WAGOMBANIA VITAMBULISHO ARUMERU

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amezindua zoezi la utoaji wa vitambulisho Kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao mauzo ghafi Hayazidi Shilingi milioni 4.

Akizindua zoezi hilo la utoaji wa Vitambulisho ambalo limefanyika katika Halmashauri ya Arusha Dc eneo la Ngaramtoni na Halmashauri ya Meru katika eneo la Uwanja wa Ngaresero ambapo limehudhuriwa na mamia ya wafanyabiashara Ndogondogo ambao watanufaika na zoezi hilo ambapo Kwa kuanzia Wilaya itatoa zaidi ya vitambulisho elfu sita Kwa wafanyabiashara ndogondogo Wilayani Arumeru.

Awali Ndugu Muro akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo , Meneja wa mamlaka ya mapato nchini TRA Wilayani Arumeru Bwana Musa Sudi amesema wataendelea kutoa Elimu kwa wafanyabiashara ili waweze kutambua fursa zilizopo katika kufanya Biashara kupitia vitambulisho vya Magufuli hatua ambayo itawarahisishia ulipaji wa kodi pamoja na kuwasaidia kukua kibiashara.

Wakizungumza Kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi la utoaji wa vitambulisho hivyo , wakurugenzi wa Halmashauri za Arusha na Meru Ndugu Emanuel Mkongo pamoja na Dkt . Charles Mahela wamesema Halmashauri zimeweka utaratibu mzuri wa Kuwatambua wafanyabiashara pamoja na kuwaratibu ili waweze kutambuliwa na kuingizwa kwenye Mfumo rasmi ambao utatoa fursa ya wao kuweza kukua na kuepuka migongano ya mara Kwa mara katika kufanya biashara.
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amezindua zoezi la utoaji wa vitambulisho Kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao mauzo ghafi Hayazidi Shilingi milioni 4,kama aonekanavyo pichani DC Muro akimkabidhi mmoja wa machinga kitambulisho hicho,aidha zoezi hilo  limefanyika katika Halmashauri ya Arusha Dc, eneo la Ngaramtoni na Halmashauri ya Meru katika eneo la Uwanja wa Ngaresero ambapo limehudhuriwa na mamia ya wafanyabiashara Ndogondogo
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muroakimkabidhi mmoja wa machinga kitambulisho kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao mauzo ghafi Hayazidi Shilingi milioni 4,kama aonekanavyo pichani DC Muro 
 Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwa wamejitokeza kwa wingi wakisubiri kupewa vitambulisho hivyo,ambavyo vimeonekana kuwa umuhimu mkubwa kwao.

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro pichani katikati akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wafanyabiashra ndogo ndogo,mara baada ya kuzindua zoezi hilo la utoaji wa vitambulisho Kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao mauzo ghafi Hayazidi Shilingi milioni 4.

Dkt. BASHIRU AHITIMISHA ZIARA YAKE KAGERA KWA KUSULUHISHA MGOGORO WA VIGOGO NDANI YA CCM.

0
0
Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Mkoani Kagera, imehitimishwa Januari 02, 2019 kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.

Katika Mkutano huo pamoja na mambo mengine, Dkt. Bashiru amehitimisha kwa kuwataka wajumbe wa Kikao hicho kusitisha mchakato na mgogoro uliokuwa ukifukuta ndani ya CCM, baina ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jasson Rweikiza pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba, Ndg. Murshidi Ngeze kuacha Mara moja kwani hauna tija wala faida ndani ya Chama, zaidi ni kuzorotesha Maendeleo.

Akirejea mgogoro huo kabla ya kusuluhisha, amenukuliwa akisema kuwa kumekuwepo na hali isiyokuwa ya kawaida kati ya Madiwani wanoumuunga mkono Mbunge na wale wanaomuunga mkono Mwenyekiti kuhusu wapi ijengwe Hospitali ya Wilaya ya Bukoba. 

Katibu Bashiru amethibitishia Kikao juu ya Kuomba radhi na Kukiri mbele ya Kamati ya Siasa kwa Mwenyekiti kuwa aliyumba kimaamuzi licha ya suluhisho kupatikana kuwa Hospitali ijengwe eneo la Kanazi kulingana na hoja za kitaalamu na Ukubwa wa eneo husika.

Kufuatia maelezo hayo Viongozi hao wawili Mbunge na Mwenyekiti wakapata nafasi ya kujieleza na kisha kumaliza tofauti zao za kisiasa huku Katibu Mkuu akimuomba Ndg. Rweikiza (MB) kurudisha malalamiko yake ndani ya Chama na sio Mhakamani kwa kile anacholalamika kuwa Ndg. Ngeze (Diwani Kata Rukoma) alimdhalilisha kwa kumtuhumu kuwa Mbunge Rweikiza alitoa Rushwa katika mchakato wa Uchaguzi. 

Tayari Mh. Rweikiza amekubali kurejea kwenye Vikao vya suluhisho na maadili ya Chama kulalamika upya, ingawa Dkt. Bashiru kaelekeza Viongozi hao kwenda kutoa ufafanuzi mzuri eneo la Ikimba ambalo baadhi ya watu walipotosha kuwa wametengwa kufuatia Hospitali kutojengwa eneo lao.

Aidha Dkt. Bashiru amepata nafasi ya kuwakaribisha rasmi madiwani waliorudi kutoka Vyama pinzani, huku kivutio kikubwa akiwa ni Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Kapteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Ndg. Kateme ambae baada ya kushindwa katika kinyanganyiro cha Uchaguzi katika Kara ya Kaibanja, alitimkia CUF na sasa ameamua kurejea kutokana na kuridhishwa na muundo wa Serikali iliyopo madarakani, na Utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza  wakati akihitimisha ziara yale leo Bukoba mkoani Kagera kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.
Baadhi ya Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa  katika Kikao chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.

ASKARI WANAOCHAFUA JESHI LA POLISI WAFUNGE VIRAGO MAPEMAAAA - LUGOLA

0
0
Na Abullatif Yunus wa Michuzi Blog,  Kagera. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola, ameanza Rasmi ziara yake Mkoani Kagera kwa kukutana na Idara pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo, na kisha kufanya Mkutano wa hadhara licha ya Mkutano huo kuchelewa kutokana na Majukumu yaliyokuwepo.

Mh. Kangi Lugola katika hotuba yake iliyojaa ufafanuzi wa Utekelezaji unaofanywa na Mh. Rais John Pombe Magufuli, katika Kusimamia Amani ya Nchi na Watanzania kwa Ujumla, na kuwa Mh. Rais hapendi kusikia Mwananchi yeyote akionewa, na kunyimwa haki kwa namna yoyote ile.

Sambamba na hilo Mh. Waziri Lugola, katika kuwakumbusha Watendaji na watumishi ndani ya Vyombo vya Ulinzi vya Usalama kuendelea kutenda haki na kulinda Amani bila kuchoka, isipokuwa wale wachache ambao wamekuwa wakichafua Vyombo vya Ulinzi kutafuta Kazi nyingine ya kufanya, akitolea mfano baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wanaofukuza Bodaboda, na kukamata Bodaboda Gulioni.

Kuhusu Wananchi wanaowakaribisha Raia wasio Watanzania na Wahamiaji haramu amewatahadhalisha wenye kufanya hivyo waache Mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha Usalama wa Nchi yetu, ikiwa ni sambamba na wale wanaofanya shughuli za magendo.

Katika Mkutano huo wa hadhara Mh. Waziri Lugola amepata nafasi ya kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa Wananchi nakuahidi kuzishughulikia ndani ya muda mfupi kabla hajaondoka Mkoani Kagera.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Kangi Lugola akizungumza na Wananchi waliohudhuria kumsikiliza katika Uwanja wa Mayunga Mjini Bukoba. 
 Bi Sauda Amiri (34) Mkazi wa Bukoba Manispaa, Akitoa kero yake kwa Mh. Lugola juu ya Uonevu aliofanyiwa kwa kuchomewa Nyumba yake pamoja na kufyekewa shamba lake la miche ya nyanya 1500.
 Sehemu ya Umati uliojitokeza katika Viwanja vya Mayunga Bukoba kumsikiliza Mh. Kangi Lugola Januari 2, 2019.
Picha na Abullatif Yunus wa Michuzi Blog,  Kagera.


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Atoa msaada baada ya kufuraishwa na huduma MuhimbiliAtoa msaada baada ya kufuraishwa na huduma Muhimbili

0
0
Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam ametoa msaada wa vifaa tiba aina ya (suction machines) kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kusaidia wagonjwa wenye matatizo katika mfumo wa hewa baada ya kuvutiwa na huduma nzuri za matibabu alizopatiwa mtoto wake.

Mashine aina ya suction inatumiwa na wataalam wa afya kwa ajili ya kunyonya makohozi mdomoni, puani na katika koo la mgonjwa kwa lengo la kumpatia mgonjwa tiba iliyokusudiwa. Msaada huo una thamani ya shilingi 800,000 na umetolewa leo na mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, Bi. Elizabeth Amandus kutokana na huduma nzuri ambayo alipatiwa mtoto wake Februari 28, 2018 baada ya kumfikisha Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Bi. Elizabeth alisema alijifungua mtoto wake katika hospitali nyingine, huku akiwa hajatimiza umri unaotakiwa (njiti) na kupewa rufaa ya kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Wataalam wa Muhimbili walinipokea vizuri, nikahudumiwa mimi na mtoto wangu hivyo nimeamua kutoa msaada wa mashine hizi mbili ili ziwasaidie watoto wachanga wanaoletwa hapa,” amesema Bi. Elizabeth.

Akipokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa hospitali hiyo, Sista Zuhura Mawona amesema msaada huo umewatia moyo na kwamba wataendelea kufanya kazi kwa juhudi kubwa. “Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, natoa shukrani kwa Bi. Elizabeth kutokana na kutambua juhudi zetu za kutoa huduma bora kwa wagonjwa, ametutia moyo kuchapa kazi kwa bidii zaidi,” amesema Sista Mawona. 

Mkurugezi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sista Zuhura Mawona akipokea msaada wa mshine ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo kwenye mfumo wa hewa kutoka kwa Bi. Elizabeth Amandus baada ya mtoto wake kupatiwa huduma nzuri za matibabu na wataalam wa hospitali hiyo.
Mkurugezi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sista Zuhura Mawona akizungumza baada ya kupokea msaada huo leo kutoka kwa Bi. Elizabeth Amandus.
Sista Mawona akiwa katika picha na baadhi ya wataalam wa Muhimbili pamoja na ndugu wa Bi. Elizabeth. 

MFUMO MPYA WA KUTOLEA HUDUMA ZA KIBENKI WAZINDULIWA ZANZIBAR

0
0


Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dk,Sira Ubwa Mamboya akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dk,Sira Ubwa Mamboya akisisitiza jambo alipotoa hotuba ya Ufunguzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katibu Mkuu Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar akitoa hotuba na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkurugenzi mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidh akitoa hotuba katika hafla ya Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutolea huduma za Kibenki uliofanyika katika Makao makuu ya PBZ Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja Ikiwa Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

MKESHA WA KUOMBEA TAIFA//SHANGWE ZA MWAKA MPYA 2019


MTANZANIA ATAMBA KATIKA KICK BOXING NCHINI CHINA, AMTWANGA MCHINA KWA KNOCK OUT

0
0
Na Sultani Kipingo
Mwanafunzi Mtanzania anayesoma nchini China Isaack Ibrahim Emmanuel  juzi ameibuka kidedea katika mchezo wa kick boxing baada ya kumpiga kwa KO Mchina Zi xiǎo yún yǔ katika Mjini Jillin.

Isaack,  ambaye anasomea uhandisi wa Madawa (Pharmaceuticals engineering) katika Chuo Kikuu cha Liaoning jijini Shenyang, ameushangaza umati mkubwa wa Wachina baada ya kucheza kwa ustadi na hatimaye kumgaragaza Zi ambaye hajawahi kupigwa hata mara moja.

Mpambano huo wa Kg 60 umempa umaarufu mkubwa Isaack kiasi kwamba hata waandaaji wa mapambano wameanza kupigana vikumbo kumtaka acheze mapambano zaidi. Akiwa na uwezo wa kutumia kwa kasi ya ajabu miguu na mikono yote, wataalamu wa mchezo huo wamemtabiria makubwa kijana huyu wa kutoka Mwanza.
Akiongea na michuzi tv kwa njia ya mtandao, Isaack amesema yuko fiti kupambana na yeyote na popote huku akiendea na Masomo bila wasi. 
 Isaack Ibrahim Emmanuel akimenyana na Mchina Zi xiǎo yún yǔ katika Mjini  Jillin.
 Isaack Ibrahim Emmanuel akimpa kibano  Mchina Zi Xiǎo Yún Yǔ katika Mjini Jillin.
 Isaack Ibrahim Emmanuel akitangazwa mshindi dhidi ya  Mchina Zi Xiǎo Yún Yǔ katika Mjini Jillin.

MC PILIPILI kwa mara ya kwanza amtambulisha mchumba wake hadharani//Mkesha wa Mwaka mpya 2019

KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAPIGWA KALENDA TENA

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KESI ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na wenzao saba inayonguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepigwa kalenda hadi Januari 17, 2019. Mbowe na Matiko watandelea kusota rumande hadi tarehe tajwa kufuatia Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washtakiwa hao kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 26, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Wakili wa upande wa mashtaka Profesa Abdallah Safari amehoji  Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani. Profesa Safari alihoji kuhusu rufaa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kueleza kuwa shauri limeitwa kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kueleza hayo, Profesa Safari alimuuliza  Wakili Kadushi kama rufaa waliyoikata ilikuwa chini ya hati ya dharura na kama hawakufanya hivyo ni kwa nini...? Katika majibu yake Wakili Kadushi ameeleza kuwa hakuna uhalali wa kisheria kuhusu swali hilo mahakamani hapo, labda lingeulizwa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 17, 2019 huku akisema swali hilo la rufaa wakalihoji Mahakama Kuu.Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya  na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu  

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16,  mwaka huu maeneo ya  Dar es Salaam.

Atoa msaada baada ya kufuraishwa na huduma Muhimbili

0
0
Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam ametoa msaada wa vifaa tiba aina ya (suction machines) kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kusaidia wagonjwa wenye matatizo katika mfumo wa hewa baada ya kuvutiwa na huduma nzuri za matibabu alizopatiwa mtoto wake. Mashine aina ya suction inatumiwa na wataalam wa afya kwa ajili ya kunyonya makohozi mdomoni, puani na katika koo la mgonjwa kwa lengo la kumpatia mgonjwa tiba iliyokusudiwa.

Msaada huo una thamani ya shilingi 800,000 na umetolewa leo na mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, Elizabeth Amandus kutokana na huduma nzuri ambayo alipatiwa mtoto wake Februari 28, 2018 baada ya kumfikisha Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

 Elizabeth alisema alijifungua mtoto wake katika hospitali nyingine, huku akiwa hajatimiza umri unaotakiwa (njiti) na  kupewa rufaa ya kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi. “Wataalam wa Muhimbili walinipokea vizuri, nikahudumiwa mimi na mtoto wangu hivyo nimeamua kutoa msaada wa mashine hizi mbili ili ziwasaidie watoto wachanga wanaoletwa hapa,” amesema Bi. Elizabeth.

Akipokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa hospitali hiyo, Sista Zuhura Mawona amesema  msaada huo umewatia moyo na kwamba wataendelea kufanya kazi kwa juhudi kubwa. “Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, natoa shukrani kwa Elizabeth kutokana na kutambua juhudi zetu za kutoa huduma bora kwa wagonjwa, ametutia moyo kuchapa kazi kwa bidii zaidi,” amesema Sista Mawona.
 Mkurugezi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sista Zuhura Mawona akipokea msaada wa mshine ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo kwenye mfumo wa hewa kutoka kwa Elizabeth Amandus baada ya mtoto wake kupatiwa huduma nzuri za matibabu na wataalam wa hospitali hiyo.
 Mkurugezi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sista Zuhura Mawona akizungumza baada ya kupokea msaada huo leo kutoka kwa  Elizabeth Amandus.
Sista Mawona akiwa katika picha na baadhi ya wataalam wa Muhimbili pamoja  na ndugu wa Elizabeth. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

NISHATI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS KUWEZESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO

0
0
Na Veronica Simba – Geita
Wizara ya Nishati inatekeleza mkakati wa kuwaunganishia umeme wa uhakika wachimbaji wadogo wa madini kote nchini, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufulu kuiwezesha sekta hiyo izalishe kwa tija kwa manufaa yao binafsi na ya Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu, kinachomilikiwa na kampuni ya Padalu, kijijini Lumasa, Chato; Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa eneo hilo, Dkt Medard Kalemani, alisema serikali imefunga transfoma tano zenye uwezo wa KVA 400 hadi 1,000 ili kuwawezesha wachimbaji wadogo wa Geita kuzalisha kwa tija.

“Umeme huu mkubwa utawawezesha wachimbaji kuchimba , kuchenjua na kuongeza thamani dhahabu yao ili kuiongezea thamani, iwapatie faida na waweze kulipa kodi na mrabaha serikalini,” alisema.

Akieleza zaidi, Waziri Kalemani alisema yako maeneo mkoani humo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo lakini akabainisha kuwa utaratibu wa kufunga transfoma nyingine tano zenye uwezo uleule, unafanyika ili kuyafikia maeneo ya wachimbaji yaliyosalia ikiwemo Mbogwe na Nyakafuru.
 Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (kushoto) na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia), wakifungua kitambaa maalum kilichofunika jiwe la msingi la kiwanda cha uchenjuaji dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita, kuashiria uzinduzi rasmi. Hafla hiyo ilifanyika Januari 2, 2019.
 Msimamizi wa Kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita, Abel Lucas (kulia), akitoa maelezo jinsi kinavyofanya kazi kwa Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani pamoja na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, na ujumbe waliofuatana nao, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda hicho, Januari 2, 2019.
 Msimamizi wa Kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita, Abel Lucas (kushoto), akitoa maelezo jinsi kinavyofanya kazi kwa Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili – kulia), wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda hicho, Januari 2, 2019.
 Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (katikati), akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), walipowasili kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo Chato Geita, Januari 2, 2019. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Msafiri Mtemi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo jimboni mwake, Chato Geita, Januari 2, 2019.
Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo jimboni humo, Chato Geita, Januari 2, 2019.
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images