Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Ujenzi wa Kituo cha Afya Hamai wamchefua Jafo

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, Chemba 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amechukizwa na kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha Afya Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba ambacho hakijakamilika ujenzi wa miundombinu ya Afya ilihali fedha za ujenzi zikiwa zimefikishwa kituoni hapo miezi kumi iliyopita.

Mhe. Jafo ameonyesha kuchukizwa kwake wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Afya inayoendelea kujengwa katika Halmashauri hiyo mapema leo hii. Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Jafo amesema Kituo cha Hamai kimepokea fedha tangu Januari 2018 lakin mpaka sasa ujenzi haujakamilika wakati vituo vingine vyenye mazingira magumu zaidi vimekwishakamilisha ujenzi tena kwa ubora wa hali ya juu.

Mhe Jafo aliongeza kuwa fedha zilizoletwa hapa ni sh milioni 400 nimeambiwa kuwa zimekwishatumika zote na inahitajika tsh mil 29 zaidi ili kukamilisha majengo haya; Nashindwa kuelewa ni kitu gani cha gharama kilichowekwa katika kituo hiki ambacho kimepelekea fedha hizo kwisha kabla ya ujenzi kukamilika. “Inakuwaje halmashauri zingine wametumia kiasi hicho cha fedha kukamilisha miundombinu yao lakini kwa chemba fedha hizo zisitoshe kukamilisha kituo kuna tatizo gani hapa” alihoji Jafo

Hakuna fedha itakayoongezwa katika kituo hiki cha Hamai nataka majengo yote yaliyojengwa hapa yakamilike haraka iwezekenavyo na kwa ubora unaotakiwa bila kuwa na sababu zingine zozote mkatafute fedha popote mkamilishe kituo hiki aliongeza Jafo. 

 Akizungumza na wananchi wa Hamai Mhe. Jafo aliwajulisha kuwa Halmashauri ya Chemba ni miongoni mwa Halmashauri zilizopata fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya vitatu na Hospital ya Wilaya kwa hiyo hatavumilia kuona fedha hizo zikitumika vibaya atasimamia sharia na atakayekwenda kinyume na maelekezo atachkuliwa hatua kali.
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwasili katika kituo cha Afya Hamai kukagua miundombinu ya afya inayoendelea kujengwa katika kituo hicho kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Mweshimiwa Rajabu. 
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo baada ya kukagua miundombinu ya afya katika kituo cha Afya Hamai, Chemba 
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati wa kukagua miundombinu ya afya katika kituo cha Afya Hamai, Chemba 
Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya afya iliyofanywa na Waziri wa TAMISEMI Wilayani humo. 



WAZIRI LUGOLA KUANZA ZIARA NDEFU MKOANI KAGERA KESHO, AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili mjini Bukoba Mkoani Kagera leo, kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku nane kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 

Waziri Lugola anatarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho Januari 2, 2019 mjini Bukoba kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye kuzungumza na Baraza la Askari na Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo mjini humo. 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, leo, Lugola amesema baada ya kuzungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake pamoja na kupokea changamoto zao, atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi utakaofanyika uwanja wa uhuru mjini humo ili aweze kusikiliza na kuzitatua kero mbalimbali zinazowakabili. 

“Nitafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru eneo la Mayunga hapa mjini Bukoba, ambapo utaanza saa 10:00 hadi 12:00 jioni, hivyo nawaomba wananchi wa mji huu wajitokeze kwa wingi kunisikiliza kile ambacho nimepanga kuwaambia na pia nitawapa nafasi wananchi waulize maswali bila woga, waniambie kero zao nami nitazitatua katika mkutano huo,” alisema Lugola. 

Pia Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo yake mbalimbali ambayo aliyatoa mwaka jana 2018 katika mikutano yake kama yalifanyiwa kazi na viongozi wa Taasisi anazoziongoza au yalipuuzwa, yakiwemo ya dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe. 

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma aligundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kulala akiwa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo wengi wao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea. 

IBADA YA MKESHA WA MWAKA MPYA KANISA BAPTIST KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mchungaji wa Kanisa la Baptist Kinondoni,Samweli Kabonaki akiongoza ibada ya kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019 iliyoanza saa tatu usiku na kufika tamati saa sita usiku.

Kwaya ya vijana ya Kanisa la Baptist Kinondon  B  wakiimba nyimbo za kusifu na shangwe wakati wa mkesha wa mwaka mpya Dar es Salaam.

Wanakwaya wakitoa huduma  katika  mkesha wa mwaka mpya uliofanyika katika  kanisa la Baptist Kinondoni B jijini Dar es Salaam.

Waumini wa kanisa la Baptist Kinondoni B wakiendeleza sherehe za kuupokea mwaka 2019 na kuuaga mwaka 2018 leo  usiku kwenye ibada  ya kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019,iliyoanza saa 3 usiku na kufika tamani saa 6 usiku.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

VODACOM wagawa Tuzo Points Moshi mjini

$
0
0
 Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania wakiwazawadia wateja wa mtandao huo kutoka Moshi Mjini Tuzo Points pamoja na zawadi zinginezo. Wateja wa Vodacom hujipatia Tuzo Pointi pale wanaponunua salio au kufanya miamala kupitia M-Pesa. Pointi hizo zinaweza kubadilishwa kuwa fedha, salio au bando. Katika msimu huu wa sikukuu, Vodacom Tanzania inawazawadia wateja wao pointi za Tuzo zenye thamani ya shillingi Bilioni moja.


WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA, APOKEA MADARASA MAWILI YA SHULE YA SEKONDARI KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa jana Desemba 31, 2018 alizindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa pamoja na kupokea madarasa mawili yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa kwa udhamini wa Benki ya CRDB, iliyopo katika Kijiji cha Kilimahewa.

Waziri Mkuu aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kufanikisha kujenga tawi hilo ambalo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi wa Ruangwa kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki.

Kadhalika, Waziri Mkuu alisema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018. Wengine pichani ni kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa, Method Muganyizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay wakifungua pazia katika kibao kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018. Wengine pichani ni kutoka kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa, Method Muganyizi. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa yaliyojengwa na Benki ya CRDB, iliyopo katika Kijiji cha Kilimahewa, Ruangwa mkoani Lindi Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakiwa wameketi katika madeski pamoja na baadhi ya wanafunzi katika moja ya madarasa hayo yaliyojengwa na Benki ya CRDB. 

RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA SKULI YA MSINGI CHIMBA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi ya Chimba, Shehia ya Chimba ikiwa katika shamrashamra za Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar,ufunguzi huo umefanyika leo 1-1-2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuizungua Skuli ya Msingi Chimba Shehia ya Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba, uzinduzi huo umefanyika leo, 1-1-2019.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua moja ya Madarasa ya Mskuli ya Msingi Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba Shehia ya Chimba, akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya uzinduzi wa Skuli hiyo uliofanyika leo.1-1-2019, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu) 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Chimba Wilaya ya Micheweni Pemba akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, akielekea katika majengo ya Madarasa kwa ajili ya Uzinduzi wake ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu) .

MAJALIWA ASHIRIKI KATIKA DUA YA KUMSHUKURU MUNGU MKESHA WA MWAKA MPYA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa , mkesha wa mwaka mpya kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba Mungu aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa mkesha wa mwaka mpya, kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama saa wakati alipojumuika na ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa mkesha wa mwaka mpya kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba Mungu aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwake katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa , mkesha wa mwaka mpya kushiriki katika Dua ya kumshukuru Mungu kwa kuwajalia watanzania na viongozi wao kuumaliza salama mwaka 2018 na kumuomba Mungu aendelee kulilinda taifa letu na viongozi wake kwa mwaka 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI SHONZA AWATAKA WASANII KUJIJENGEA TABIA YA KUJIWEKEA AKIBA

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha

Naibu waziri wa Habarui, sanaa utamaduni na michezo Mhe. Juliana Shonza  amewataka wasanii wa Injili kjijengea tabia ya kujiwekea akiba ili punde wapatapo matatizo waweze kuyatatua kwa urahisi.

Ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizindua mfuko wa Tagoane LoanFund Jijini Arusha ambapo amepongeza uongozi wa Tagoane kufikia hatua hiyo. Ameyataka mashirikisho yote ya muziki wa Injili nchini Tanzania kuiga mfano nzuri wa Tagoane ili waweze kuwa na mashirikisho ambayo ni hai na yanayoleta mshindo kwenye jamii.

Amesema yeye kama mlezi wa wasanii wote nchi amewaomba waamke wachangamkie fursa na wasiwe wavivu kujifunza kutoka kwa wenzao waliofanikiwa .Amewataka wasanii kukaa kwa pamoja Kuonyeshe Uzalendo kwa nchi yao wajadili changamoto mbalimbali wanazozipitia na kutafuta namna ya kutazua changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake Rais wa Tagoane Taifa Dkt. Godwin Maimu amesema kuwa wanedhamiria kuanzisha mfuko wao wa Tagoane Loan Fund ambapo mpaka sasa umekuwa na wanachama ambao wameshachangia akiba zao zipatazo shilingi milioni kumi.Amesema mfuko huo unatarajiwa kuanza kutoa mikopo kwa wanachama wavhqngiaji kuanzia 2 januari 2019

maendeleo kama vijana hayawezi kuendelea ukiwa na jitihada za mtu mmoja mmoja bali balintunapounganisha nguvu zetu kwa pamoja mwisho wa siku tunapata kitu cha kuweza kutusaidia. Alisema Dkt Maimu

Naibu waziri wa Habari, sanaa utamaduni na michezo, Juliana Shonza akizungumza katika tamasha Tukuza Festival Genesis one katika hotem ya Corido Spring Jijini Arusha. Picha/habari na Vero Ignatus.
Naibu Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na michezo Juliana Shonza akipeana mikono na Rais wa Tagoane Dkt. Godwin Maimu mara baada ya kuzindua mfuko wa Tagoane Loan Fund Jijini Arusha.
Rais wa Mtandao wa wasanii wa Injili na Maadili Tanzania Dkt. Godwin Maimu akizungumza na wasanii mbalimbali waliohudhuria katika tamasha la Tukuza festival Genesis one Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Habari sanaa utamaduni na michezo Juliana Shonza akisalimiana na Mkurugenzi wa Newlife Band Fortunatus Mabondo(Hondo)
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni na michezo akipokelewa na kikundi cha ngoma cha jamii ya wamasai cha Meserani Jijini Arusha.



NHIF YAKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA TUNDURU

$
0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoa wa Ruvuma,umekutana na wanachama na viongozi wa vyama viwili vya msingi vya ushirika vinavyojihusisha na kilimo cha zao la korosho katika wilaya ya Tunduru.

Lengo ni kuhamasisha wanachama na viongozi wa vyama hivyo kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa ajili ya kupata huduma za matibabu pindi wanapoumwa kwa kuwa shughuli za kilimo zinahitaji mtu mwenye afya njema ambayo itamruhusu kuendelea na majukumu yake katika kipindi cha msimu wa kilimo.

Wanachama hao ni kutoka vyama vya Naluwale na Mumsasichema kata ya Muhwesi ambayo ni maarufu kwa uzalishaji mkubwa wa korosho wilayani hapa.Akizungumza na Wanachama hao kaimu Meneja wa mfuko huo Antony Mgima alisema, mpango huo unalenga kutoa huduma kwa mwanachi mmoja kwa gharama ya shilingi 78,600 ambapo mwanachama atapata fursa ya kuhudumiwa kuanzia ngazi ya zahanati,kituo cha Afya na Hospitali zote Nchini.

Alisema, mpango huu wa sasa utasaidia sana kila mmoja kunufaika nao tofauti na hapo awali ambapo ni watumishi wa umma pekee yao ambayo walikuwa na sifa ya kuwepo katika mpango wa huduma za matibabu.

Kwa mujibu wake, mwanachama wa NHIF ana hiari ya kumlipia fedha kama michango kwa mtu yoyote ambaye anaona anastahili kuwemo katika mpango hasa ikizingatia kuwa, kwa sasa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeboresha sana huduma zake .

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera,ameitaka NHIF kuhakikisha wanawashirikisha viongozi wa vijiji na kata katika kuhamasisha wananchi wengi zaidi ili nao waweze kujiunga na mfuko huo badala ya kulenga wanachama na viongozi wa vyama vya ushirika.

WAKAZI DISUNYARA WATUMIA SH. 4,000 KUFUATA VIPIMO IKIWEMO CHA MALARIA UMBALI WA KM. 10 KWENDA NA KURUDI

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI 

ZAHANATI ya Disunyara, kata ya Kilangalanga Kibaha Vijijini, inakabiliwa na ukosefu wa maabara hali inayosababisha kufuata vipimo ikiwemo cha malaria na damu kituo cha afya Mlandizi ambako kuna umbali wa km kumi kwenda na kurudi na nauli ya pikipiki sh. 4,000.

Kutokana na hali hiyo wakazi wa eneo hilo wamejitolea kuanza ujenzi wa maabara ambapo mbunge wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu amechangia mifuko 30 ya saruji . 
 
Akichangia mifuko hiyo,alisema vipimo ni suala muhimu ambalo inahitajika nguvu ya pamoja kumaliza ujenzi huo. “Baada ya kusikia wananchi wameanza juhudi hizo ndipo nilipoguswa kuwaunga mkono ili kuendelea na ujenzi,alielezea Subira. 

Nae diwani wa kata hiyo, Mwajuma Denge alisema wananchi wanapata shida kufuata huduma ya vipimo umbali mrefu. Aliwaomba wadau kuendelea kujitokeza kuchangia ili kumaliza ujenzi huo waweze kupata japo vipimo vya awali karibu. Kwa upande wake mganga mfawidhi wa zahanati ya Disunyara ,Maimuna Yusuph alitaja tatizo la ukosefu wa chumba cha maabara kunasababisha akinamama wajawazito kwenda Mlandizi kufuata vipimo na wakati mwingine hushindwa kutokana na ukosefu wa nauli. 


Tatizo jingine ni vitanda vya kuzalia kwani kilichopo ni kimoja, kingine kibovu hivyo mahitaji ni vitanda vingine viwili ili kukidhi mahitaji. Mkazi wa Disunyara Mwajuma Juma alimshukuru Subira kwa kuwashika mkono ili kumkomboa mwanamke. Alisema endapo maabara hiyo ikikamilika itasaidia wakazi wenye mahitaji ya vipimo hasa akinamama na watoto.

Mbunge viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu akizungumza wakati alipokwenda kutembelea zahanati ya Disunyara, huko Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi) .

DKT. BASHIRU - WAWEKEZAJI WA KIUCHUMI WEKEZENI UCHUMI WA KIMATAIFA, NA WAKISASA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi –Taifa ameendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera Januari Mosi, 2019 kwa kutembelea Kiwanda cha Kusindika Kahawa cha TANICA kilichopo Bukoba Manispaa, Mkoani kagera na kuagiza Uongozi wa Kiwanda hicho kutafuta Masoko ya Kimataifa ikiwemo Nchi za nje kama vile China.

Akiwa katika Kiwanda cha TANICA Katibu Mkuu Dkt. Bashiru amekutana na kuzungumza na Bodi ya Usimamizi wa Kiwanda hicho na kuwataka Wasimamizi hao kuendesha kiwanda hicho katika mfumo wa Kitaasisi ya kibiashara inayojulikana Kimataifa, na kisasa zaidi, ili kuleta tija katika kile alichotaja kuwa ni Vita ya Kiuchumi, huku akishangazwa na Kahawa ya Kagera kushindwa kuuzika katika soko la Kimataifa kama China, wakati Uganda tayari wameweza kupenyeza hadi katika Soko hilo.

Aidha Dkt. Bashiru amefafanua kuwa Vita ya kiuchumi i wa Kitaifa na Uchumi wa kisasa ni ile hasa inayolenga kukidhi mahitaji ya Taifa kwanza, walengwa wakiwa ni Watanzania wenyewe kujikwamua Kiuchumi kutokana na fursa zinazowazunguka, huku akiagiza Uongozi wa Kiwanda hicho kuboresha miundo mbinu ya Kitekenelojia na kubuni miradi mingine zaidi kama Uvuvi, Mvinyo, Kusindika Ndizi n.k

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa TANICA Bwn. Linus R . Leopord Licha ya kubainisha baadhi ya mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Mei mpaka Oktoba Mwaka jana, ambayo ni pamoja Kuendelea kulipa madeni sugu ya Kiwanda hicho, wamefanikiwa pia kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni Nne,na huku wakiwa wameshachangia pato la Taifa zaidi ya shilingi Milioni Mia Nane, hakusita pia kuzitaja changamoto za Kiwanda hicho, ambazo ni pamoja na Uongozi uliopo madarakani kutishiwa Vifo na waliokuwa wafanyakazi na Viongozi walioachishwa Kazi, Kugushiwa kwa Nembo ya Kampuni na kusababisha Kuchafuliwa kwa Soko la Kahawa yao, Hali ya Mishahara na Ajira kwa wafanyakazi wenye Taaluma.

Awali Dkt. Bashiru amepata fursa ya kutembelea Bandari Ndogo ya Kemondo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na kuzungumza na Wananchi wa maeneo yale pamoja na Viongozi wa Serikali na Kichama. Miongoni mwa maelekezo aliyoyatoa ni juu ya Uongozi wa Bandari hiyo kuangalia upya namna ya Tozo inayolipwa getini kwa sasa, pia Tozo inayolipwa kwa Kampuni inayojihusha na Ubebaji mizigo, sambamba na Uvuvi haramu na kuutaka Uongozi husika kubainisha wahusika wa vitendo hivyo ili watiwe Nguvuni na sheria ichukue mkondo wake.
Dkt. Bashiru Kakurwa Akipata maelezo ya Bidhaa ya Kahawa kutoka kwa Rewina Peter (Afsa masoko - TANICA) mara baada ya kuwasili Kiwandani hapo.
Meneja Mkuu wa TANICA Bwn. Linus R. Leopord akitoa ufafanuzi Kwa Dkt. Bashiru namna ya kupeleka Bidhaa yao katika Soko la Kimataifa.
Pichani dkt. Bashiru akizungumza na wannchi katika Bandari ya Kemondo, pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Bwn. Murshidi Ngeze.
Wajumbe wa Bodi ya TANICA pamoja na Uongozi wakiwa wameketi Kikao na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru.

TANGAZO LA KIFO CHA CLEMENT THOMAS NDELEOKASI SHAYO

$
0
0
Selina Mushi wa Mlandizi Njia Panda JKT anasikitika kutangaza kifo cha mume wake mpendwa Clement Thomas Ndeleokasi Shayo  kilichotokea Alhamsi tarehe 29, Novemba 2018 katika hospitali ya Muhimbili - Mloganzila. 


Mazishi yalifanyika nyumbani kwa marehemu, Uparo-Kirua Vunjo Moshi, Kilimanjaro siku ya Jumanne tarehe 4 Desemba, 2018. Watoto wa marehemu, Frederick Clement Shayo na Regina Clement Shayo, pamoja na mama yao Selina Mushi na dada wa marehemu Clementina Thomas Shayo  wakishirkiana na famlia ya Mtika na ukoo wote wa Shayo, pamoja na familia ya Lesiaki Mushi wanatoa shukrani za dhati kwa wauguzi wa hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kwa juhudi zao za kujaribu kuokoa maisha ya mpendwa wao Clement. 

Shukrani zao za pekee zinatolewa kwa Sista Agatha wa kituo cha Afya cha Mtakatifu Joseph, Luguruni Dar es Salaam, ndugu, jamaa na marafiki wote waliomhudumia Clement wakati wa kuugua kwake.  Marehemu aliugua akalazwa hospitali kwa muda mfupi na kuruhusiwa; kisha akapata stroke.  

 Kifo cha Clement kimekuwa mshtuko mkubwa kwa ndugu, jamaa, marafiki, na wote waliomfahamu Tanzania, Marekani na Canada. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe. Mwenyezi Mungu aipokee roho ya marehemu Clement katika Furaha ya Milele, Amina

FAMILIA YA DAUDI LIANA YATOA MSAADA WODI YA WAZAZI WILAYANI MWANGA

$
0
0

Familia ya Daudi Liana, Usangi-Mwanga Kilimanjaro wakitoa msaada wa mashuka kwa wodi ya wazazi ya hospitali ya Wilaya ya Mwanga, Usangi, Kilaweni.. Picha ya pamoja ya familia ya Daudi Liana wakiwa pamoja na uongozi wa hospitali ya wilaya ya Mwanga, Usangi KilaweniPicha ya pamoja ya familia ya Daudi Liana wakiwa pamoja na uongozi wa hospitali ya wilaya ya Mwanga, Usangi Kilaweni
Mmoja ya wanafamilia ya Daudi Liana wa Usangi-Mwanga Kilimanjaro akionesha moja ya misaada ya mashuka kwa wodi ya wazazi ya hospitali ya Wilaya ya Mwanga, Usangi, Kilaweni.

NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI

$
0
0

NA LUSUNGU HELELA-GEITA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewaonya wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi za Misitu nchini kuacha tabia ya kuwashambulia Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

Onyo hili linakuja ikiwa zaidi ya watumishi watano wa TFS katika mikoa ya Pwani, Tabora ,Kigoma pamoja Kilimanjaro wakiwa wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na wananchi wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

Aidha, Mhe.Kanyasu amepiga marufuku kwa watumishi wa TFS kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wananchi wanapobainika kutenda makosa."Watumishi wa TFS hamruhusiwi kumpiga Mwananchi mnapomkamata ndani ya Hifadhi au akiwa anasafirisha mazao ya Misitu kinyume na sheria, atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

Ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mgusu wilayani Geita mkoani Geita ikiwa ni ziara yake ya kutatua migogoro ya mipaka kwenye msitu wa Hifadhi Geita iliyopo baina ya Vijiji ambapo jumla ya hekta 4,462.95 zimefutwa kwa tangazo la Serikali.

Amesema shughuli za uhifadhi ni lazima zifanyike kwa ushirikishwaji kati ya wananchi na watumishi wa TFS." Uhasama unaozidi kujengeka kati yenu hauna tifa katika uhifadhi shirikianeni" amesisitiza Mhe.Kanyasu.Amewataka wananchi kuheshimu na kuzifuata sheria za uhifadhi ya Misitu nchini huku akiwataka watumishi kujiepusha na migongano kati yao na wananchi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Geita mkoani Geita akipewa maelezo na Meneja wa Misitu wa wilaya wa Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS) Fedy Ndandika wakati alipotembelea eneo la Manga lililokuwa limevamiwa na wakulima ambayo ni moja ya eneo la Msitu wa Hifadhi Geita
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mgusu, Halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani Geita akiwasisitiza wananchi umuhimu wakufuata sheria na kuacha tabia ya kuvamia Hifadhi za Misitu.
Mkazi wa kata ya Mgusu, Anaeli Mbokile akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwasilisha ombi la kumegewa eneo la Hifadhi ya Msitu Geita ili liweze kutumika kwa ajili ya malisho na makazi baada ya wakazi wa kata ya Mgusu idadi ya kuongezeka.
1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiteta jambo na baadhi ya wanachama wa CCM wakati alipomaliza mkutano wa hadhara katika kata ya Mgusu mkoani Geita. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA).


 

Tanzania ina chakula cha ziada na imejitosheleza- Waziri wa Kilimo Hasunga

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Kwa mliganisho wa mahitaji na uzalishaji nchi ina ziada ya tani 3,013,515 na imejitosheleza kwa asilimia 123 na 120 mtawalia ambapo uzalishaji katika msimu wa 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa tani 15,900,864 na 16,172,841 mtawalia ambapo mahitaji ya chakula yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 13,159,326, na 13,300,034 kwa mwaka wa ulaji 2017/2018 na 2016/2017 mtawalia. 

Uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa uzalishaji wa 2017/2018 ulifikia tani 16,981,974 zikiwemo tani tani 9,537,857 za mazao ya nafaka na tani 7,354,117 mazao yasiyo nafaka, kiwango ambacho kimeiwezesha nchi kutosheleza mahitaji yake ya chakula ya tani 13,569,285 katika mwaka 2018/2019 kwa kiwango cha utoshelevu (Self Sufficiency Ratio-SSR) cha asilimia 124. 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 2 Januari 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma.

Alisema Uzalishaji wa mahindi katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa ni tani 6,273,150; 6,680,758 na 6,148,699 mtawalia, wakati mahitaji yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 5,462,390; 5,407,499 na 5,202,405 katika miaka ya ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017, Ambapo ziada ya tani 810,760(2018/2019); 1,273,259(2017/2018) na 946,284(2016/2017) zilipatikana.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma tarehe 2 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).



Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) yatuma orodha ya Waamuzi wa Tanzania watakaochezesha mechi za kimataifa wakiwa na beji ya FIFA.

$
0
0
Katika orodha hiyo wapo waamuzi wa katikati na Waamuzi wasaidizi wa Kiume na wa Kike.

Aidha wapo pia waamuzi watakaochezesha soka la Ufukweni.

Waamuzi wa katikati Wanaume 
1NASSORO Mfaume Ali
2SASII Hery Ally
3MWANDEMBWA Emmanuel Alphonce
4SAANYA Martin Elifhas

Waamuzi Wasaidizi

1CHACHAFerdinand
2KINDULI Mgaza Ally
3LILASoud Iddi
4KOMBA Frank John
5MKONO Mohamed Salim
6HAULE Mbaraka Haule

Waamuzi wa Soka la Ufukweni 

1MSILOMBO Jackson Steven
2MWAMBONEKO Geofrey Tumaini

Waamuzi wa katikati Wanawake 

1KABAKAMA Jonesia Rukyaa
2CHIEF Florentina Zabron

Waamuzi wasaidizi Wanawake

1MDUMA Hellen Joseph 
2WAMALAGrace
3BALAMAJanet Charles
4MTWANA Dalila Jafari

TAMKO LA WIZARA KULAANI VITENDO VYA UKATILI WA WATOTO MAJUMBANI

$
0
0

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalaani na kukemea vikali vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyoendelea kujitokeza nchini. Vitendo hivi vinafanywa na kuhusisha ndugu na walezi wa karibu wa wataoto hivyo kuzua hofu kubwa kwa watoto na jamii kwani vinaathiri malezi na makuzi ya awali ya watoto kwa kutozingatia haki zao za msingi.

Mapema wiki hii, imeripotiwa mwalimu wa shule ya msingi jijini Dodoma (jina limehifadhiwa) ambaye anatuhumiwa kumfungia mtoto mdogo ndani ya kabati kwa kipindi kirefu na kusababisha afya ya mtoto huyo kudhohofika. Mwalimu huyo anatuhumiwa pia kumfanyia vitendo vya ukatili mama mzazi wa mtoto huyo kwa kumpiga na kumsababishia maumivu mwilini yaliyopelekea binti huyo na mtoto wake kulazwa.

Kipekee, Wizara inawapongeza wanajamii wote walioibua tukio hili na kuwezesha Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya uchunguzi ili Sheria iweze kuchukua mkondo wake. TunaaminiJeshi la Polisi watafanya upelelezi wa tukio hili kwa weledi mkubwa ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.Matukio ya ukatili wa watoto yanapotokea majumbani yanarudisha nyuma jitihada za Serikali za kulinda na kuendeleza haki na ustawi wa watoto katika ngazi ya familia ambayo ndio kitovu cha jamii wakiwemo na watoto.

Kufuatia kitendo hicho kilichofanywa na mwalimu wa shule ya msingi ambaye ni mlezi wa watoto, Wizara inawataka wazazi, walezi na jamii kuzingatia wajibu wa ulinzi wa watoto ili kuwahakikishia usalama wao katika maeneo ya majumbani, shuleni, mtaani, njiani na katika jamii kwa ajili ya kutekeleza lengo la kupunguza matukio ya ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/2022.

Aidha, Wizara inatoa rai kwa jamii na wananchi wema kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuepuka makosa ya kisheria yanayoweza kutokea kwa kusambaza, kuchapisha na kupiga picha za watoto ambao ni wahanga wa ukatili na kuziweka wazi kinyume na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009.

Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mtoto aliyefanyiwa ukatili huo. Tunawaomba wanajamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kufichua vitendo vyote vya ukatili dhidi ya watoto vinavyojitokeza katika maeneo yao. Aidha, katika kipindi hiki ambapo uchunguzi unaendelea kufanyika tunaomba pawe na utulivu na uvumilivu ili kutoa nafasi kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi kwa makini na Sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)
02/01/2019

MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI ATOA TAKWIMU ZA BEI ZANZIBAR.

$
0
0

Meneja Uchumi Benki kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele Lugobi akijibu maswali yalioulizwa katika hafla ya Utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.


Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika hafla ya Utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Abdul-rahman Msham katikati akitoa maelezo kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.kulia ni Afisa Mwandamizi Mkuu Benki kuu Tawi la Zanzibar Malik Ali Suleiman na kushoto ni Afisa Uchumi na Biashara (Zura)Omar Ali Yussuf
Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA)Dkt.Suleiman Simai Msaraka akitolea ufafanuzi maswala mbalimbali yalioulizwa katika hafla ya Utoaji wa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kushuka kutoka asilimia 4.4 kwa Mwezi wa Novemba hadi asilimia 3.5 kwa mwezi wa Disemba hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.

Makala maalum ya Dira ya Dunia TV 01/01/2019

Vituo vya Mafuta Vyakumbushwa Kuweka Mabango Yanayoonyesha Bei

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

 
Vituo vya mafuta nchini vimekumbushwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kwa wateja na kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kaimu M
kurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Nzinyangwa Mchany wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu bei kikomo za mafuta aina ya petroli zilizoanza kutumika leo januari 2, 2019.

“Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja, adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika”, alisema Mchany.

Mchany ameongeza kuwa mabango hayo yanatakiwa kuonesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika ili wateja waweze kuwa na uwanja mpana wa kuchagua wapi pa kununua.Aidha, Mchany ametoa rai kwa wateja kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Kwa upande mwingine wauzaji wa mafuta ya petroli wamekumbushwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na wanunuzi wametakiwa kuhakikisha wanapokea stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Amefafanua kuwa Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kudhibiti watoa huduma wasio waaminifu pale ambapo wanunuzi wa mafuta watakuwa na malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, pia stakabadhi hizo zitasaidia kurahishisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na nishati mafuta.

Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote zimepungua ambapo kwa mwezi Januari 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa Shilingi 141/lita (sawa na asilimia 5.80), Shilingi 212/lita (sawa na asilimia 8.69) na Shilingi 167/lita (sawa na asilimia 7.03).

Vilevile, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa Shilingi 140.81/lita (sawa na asilimia 6.09), Shilingi 212.12/lita (sawa na asilimia 9.14) na Shilingi 166.02/lita (sawa na asilimia 7.40).
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images