Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: WAKALA WA MISITU WATOA NENO BAADA YA VIDEO HII KUSAMBAA


RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN ATOA SALAMU ZA MWAKA MPYA 2019

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa salamu za Mwaka Mpya wa 2019, Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi  wa Zanzibar kuendelea kuidumisha hali ya amani na utulivu ambayo ndio msingi wa mafanikio yanayoendelea kupatikana hivi sasa na yatakayopatikana hapo baadae. Dk. Shein aliyasema hayo leo katika risala yake ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2019 aliyoitoa kupitia vyombo vya habari, Ikulu mjini Zanzibar.

Rais Dk. Shein alisema kuwa katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mwaka 2018 mafanikio makubwa yamepatikana ambayo yamechangiwa na kuwepo kwa amani, mshikamano, umoja na mapenzi yaliopo. Katika risala yake hiyo Rais Dk. Shein alieleza kuwa hali ya amani, umoja na mshikamano uliopo nchini ni jambo muhimu linalowavutia Washirika wa maendeleo ambao wanaridhika na jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ndio maana wanaiunga mkono katika mipango yake ya maendeleo.

Alisema kuwa hapana shaka kwamba iwapo amani, usalama na utulivu vitadumishwa na kufanya kazi kwa bidii Washirika wa Maendeleo watakuwa pamoja na Zanzibar katika kuisaidia ili kuweza kutekeleza malengo yaliyopangwa. Rais Dk. Shein alitoa shukurani kwa wananchi wote kwa kuunga mkono juhudiza serikali za kuiletea maendeleo Zanzibar na kueleza kuwa moyo wao huo wa umoja na mshikamano umewezesha kuimarisha vizuri hali ya uchumi wa Zanzibar.

Hata hivyo, Dk. Shein alitoa shukurani nyingi kwa wananchi wote kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuiletea maendeleo Zanzibar ambapo moyo wao huo wa umoja na mshikamano umewezesha kuimarisha vizuri hali ya uchumi wa Zanzibar. “Tukiwa tunaukaribisha mwaka mpya wa 2019, nachukua fursa hii kwa niaba ya wananchi wote  wa Zanzibar kuwashukuru kwa dhati  Washirika wetu wa Maendeleo kwa kuendelea kutuunga mkono, tunathamini mikopo, misaada na ushauri tulioupata kutoka kwao”, alisema Dk. Shein.

Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza kuwa wakati unakaribishwa mwaka 2019 ni wajibu wa kila Taasisi ya Serikali ikajipima namna inavyoendelea kutekeleza mambo yaliyoagizwa katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015-2020. “Nawakumbusha viongozi wenzangu viongozi wenzangu wote wa CCM tuliochaguliwa na wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, uliorudiwa mwezi Machi, 2016. Kadhalika jukumu hili wanapaswa walizingatie na wale wote niliowateua katika nyadhifa mbali mbali”,alisema Dk. Shein katika risala yake hiyo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAJUMBE WA NEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
WAJUMBE  wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Zanzibar wamesema CCM itaendelea kuisimamia Serikali ikusanye kwa wingi mapato bila kuruhusu uvujaji wa rasilimali fedha. Wamebainisha kuwa hatua hiyo itasaidia nchi kujitegemea na kuondokana na mfumo wa kutegemea baadhi ya fedha za wadau wa maendeleo zenye masharti yanayokwenda kinyume na Ustawi wa kijamii na Utamaduni wa wananchi wa Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe hao, Mjumbe wa NEC Ndugu Amini Salmin Amour huko katika Kituo cha ufugaji wa Kasa Mnarani Nungwi, ameeleza kwamba endapo Serikali itazidisha kasi ya usimamizi na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato Zanzibar itakuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa. Ndugu Amini ameeleza kwamba Sekta ya Utalii ni moja ya Taasisi muhimu zinazochangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia fedha za kigeni.

Alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Sekta ya Utalii na maeneo ya Uwekezaji kwa lengo la kushauri na kutoa maelekezo kwa baadhi ya sehemu zenye changamoto za kiutendaji. Aliipongeza Kamisheni ya Utalii Zanzibar kwa utendaji wao mzuri uliochangia kuimarika kwa taasisi hiyo na kufanikiwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa Ilani ya CCM.

Pamoja na hayo aliwasihi wananchi kuendeleza Utamaduni wa kufanya Utalii wa ndani ili wajionee vivutio mbali mbali vya utalii vilivyopo nchini pamoja na kufahamu historia na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa kupitia Sekta ya Utalii nchini.
 BAADHI ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakisoma machapisho mbalimbali yanayotolewa na Kamisheni ya Utalii hapo katika Kituo cha mawasiliano, Utafiti na Takwimu cha Kamisheni ya Utalii Zanzibar kilichopo  Uwanja wa Ndege wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Zanzibar.
 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakipatiwa maelezo juu ya huduma zinazopatikana katika ukumbi wa mikutano wa Holeli ya Kimataifa ya Verde iliyopo Mtoni Marine Unguja, katika ziara yao ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakikagua boti na vifaa vya kisasa vilivyopo katika Hoteli ya Kimataifa ya Verde huko Mtoni Marine Zanzibar.
 MKURUGENZI Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Miraji Ussi akitoa maelezo ya ramani ya ujenzi wa mradi mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika eneo la Makumbusho ya Kihistoria la Bihole lililopo Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakipatiwa maelezo juu ya Mradi wa Ufugaji wa Kasa uko Mnarani Nungwi, ambapo ni sehemu ya mradi unaoendeshwa na wananchi wakishirikiana na kamisheni ya Utalii Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NITAWAPUMZISHA WACHEZAJI WANGU KUNA MAKOMBE MUHIMU- ZAHERA MWINYI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KUELEKEA katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameweka msimamo wa kuwapumzisha wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza. Zahera  amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani  Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuelekea mashindano hayo,  atawapumzisha wachezaji baadhi ya wachezaji wake kutokana na kukabiliwa na mashindano mengi msimu huu. Zahera ameeleza kuwa kufuatana na uwepo wa mashindano hayo ni vema wakawapumzisha wachezaji kadhaa kwa ajili ya kuweka nguvu katika Ligi Kuu Bara.

"Kufuatana na nguvu yetu tulionayo (wachezaji) inatubidi tuangalie wapi tutapata faida, tupo na ligi kuu, tupo na Azam federation cup , Mapinduzi Cup na Sport Pesa. "Inabidi sisi kama Yanga tuwe na malengo kwenye kitu chenye manufaa kwetu tukiamua kuyataka makombe yote tunaweza kosa yote ivyo lazima baadhi ya wachezaji wapumzike kwaajili ya ligi na ASFC", amesema Zahera.

Mbali na hilo Zahera amefanya Kikao na wachezaji wa zamani wa Klabu hiyo kongwe na kumpongeza kwa jitihada kubwa anazozifanya za kuisaidia timu ingawa ipo katika kipindi kigumu.
Akizungumza kwa niaba ya wengine Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga Sunday Manara 'Computer'  amesema kuwa  wanampongeza Kocha na benchi zima la  ufundi na wako pamoja nao.

Sunday manara amesema akiwa kama mwanayanga na mchezaji wa zamani wa timu hiyo wanaendelea kuunga mkono jitihada zote zinazofanywa na Wachezaji wa timu yao wakiongozwa na kocha Zahera. Mbali na hilo Manara amesema mpaka sasa yanga itaendelea kufanga vizuri kulingana na mikakati thabiiti inayofanywa na uongozi wa timu hiyo.
Kocha Mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Dismas Ten.

HALI YA UHALIFU IMEPUNGUA IKILINGANISHWA NA MWAKA 2017 -KANDA MAALUMU DAR ES SALAAM

$
0
0
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE ATOA SALAMU ZAKE KWA WATUMISHI WAKATI WA KUFUNGA MWAKA 2018 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2019

$
0
0
Na ASP Deodatus Kazinja
Katika kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019  Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike ameelezea matarajio ya Jeshi hilo kwa mwaka 2019 kuwa ni pamoja  kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia katika kutoa huduma kwa wafungwa na mahabusu.
Matarajio mengine ni pamoja na  kumimarisha hali ya ulinzi na usalama magerezani ikiwa ni pamoja na kusimika mifumo ya kiusalama, kujenga kiwanda cha seremala mkoani Dodoma ili kuongeza na kuimarisha  utengenezaji wa samani, kujenga nyumba 100 mkoani Dodoma kwa ajili ya watumishi wa ofisi ya Makao makuu mkoani humo.
Aidha, Kamishna Jenerali Kasike ameongeza kuwa matarajio ya mwaka ujao ni  Kuanzisha ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu mkoani Dodoma, kuendelea kuhimiza ujenzi wa nyumba kwa njia ya kujitolea ili kupunguza uhaba wa nyumba za watumishi wa jeshi hilo, Pia amesema atahakikisha Shirika la Magereza (Magereza Corporation Sole) linapata Bodi ili kujiimarisha katika kufanya shughuli za kibiashara.
 Ameongeza kuwa Jeshi la Magereza litashirikiana na Idara ya mahakama katika kukamilisha maandalizi ya uendeshaji wa mashauri kwa mfumo wa kielektroniki wa ‘video conference’ ili kurahisisha utoaji wa haki kwa wafungwa na mahabusu kwa wakati. Kamishna Jenerali Kasike amehitimisha Salaam za Mwaka Mpya kwa kusisitiza suala la ufanyaji kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza Jeshi hilo na amewataka askari kubadili mtazamo wa kiutendaji na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. “Kila mmoja atimize wajibu wake kikamilifu kwa kutumia uweledi, ubunifu na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele”.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akizungumza na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza katika Baraza la kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019 leo Desemba 31, 2018 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
Baadhi ya maafisa, askari na watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakimsilikiliza  Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani)wakati wa Baraza la kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019 leo Desemba 31, 2018 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza wakiwa wamesimama kwa heshima kuwakumbuka watumishi mbalimbali wa jeshi hilo walioaga dunia kwa mwaka 2018. (Picha zote na Jeshi la Magereza)

TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mafanikio hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Adam Fimbo, alisema kuwa TFDA imepata mafanikio hayo makubwa kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, ambapo Desemba mwaka huu, imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imesaidia Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hiyo muhimu.

“Hii ni hatua kubwa kwa kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuvutia nchi mbalimbali kuja TFDA kujifunza mifumo iliyopo na kwenda kuitekeleza nchini mwao na sasa mifumo yetu imetambulika na kujulikana na nchi nyingi kwa mfano Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana, Mauritius, Lesotho na Bangladesh” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA

Sambamba na hilo, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA, aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka,

Akitolea mfano katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18, TFDA imesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Ikiwa ni kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA, alifafanua kuwa tathmini na usajili wa bidhaa hufanyika kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama, ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko. Kuwepo kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.


WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA

$
0
0
*Asema litahamasisha ukuaji wa uchumi na wananchi watahifadhi fedha zao 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa na kuushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuwa tawi hilo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 31, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuzindua tawi la benki ya CRDB, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamisha wananchi kutumia benki kwa kuhifadhi fedha zao. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwa sasa benki hiyo inatakiwa itoe mikopo midogo, ya kati na mikubwa kulingana na uhitaji wa wajasiriamali ndani ya wilaya hiyo kwa sababu mikopo itawawezesha wananchi waweze kukuza mitaji na kujikwamua kiuchumi. Pia Waziri Mkuu ameipongeza benki ya CRDB kwa kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za afya pamoja na elimu kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki hiyo nchini. 

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki ya CRDB imekua na kupanua wigo wake wa kufikisha huduma kwa wateja na kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za fedha. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Jengo la Benki ya CRDB tawi la Ruangwa ambalo lilizinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Desemba 31, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kompyuta mpakato Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017, Omari Hassani Magoma baada ya kuzindua tawi la Benki hiyo la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta Mpakato 28 zilitolewa na Benki ya CRDB kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017 wilayani Ruangwa, Omari Hassan Magoma akionyesha Kompyuta Mpakato aliyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati Waziri Mkuu alipozindua tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta mpakato 28 zilitolewa na Benki ya CRDB kwa vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu .


UHURU MEDIA GROUP YAWAPA MOTISHA WAFANYAKAZI WAKE WOTE

$
0
0
*Mkurugenzi Mtendaji Mkuu atangaza uhakiki wa wafanyakazi nchi nzima
*Azungumzia kuanza kufanya tafiti kubaini wasomaji,wasikilizaji wa vyombo vyao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Faustine Sungura ameamua kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao.

Amesema motisha hiyo inakwenda sambamba na uhakiki wa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo huku akielezea namna ambavyo amefurahishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wote na hasa katika kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye amefanya mambo makubwa kwa mwaka 2018.

Akizungumza leo ofisini kwake Sungura amesema Desemba 28 mwaka huu wa 2018 amekutana na wafanyakazi wote kwa kada mbalimbali na alitumia sehemu hiyo kuelezea mikakati ya kampuni hiyo ambayo imedhamiria kufanya mambo makubwa.
 
"Tulipokutana na wafanyakazi kuna mambo mengi ambayo tumeyazungumza.Pia nilitumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya. Rais wetu amefanya mambo makubwa kwa mwaka huu yakiwamo ya kuboresha sekta ya anga, miundombinu kwa upanuzi wa barabara na ujenzi wa madaraja, umeme wa mto Rufiji ,ununuzi wa korosho, elimu bure na mambo mengine mengi ambayo yamefanyika.Hivyo wafanyakazi hawa wamekuwa wakiunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais,"amefafanua.

Ameongeza wafanyakazi wa Uhuru Media Group kwa mwaka huu wa 2018 wamefanya kazi kwa bidii, hivyo ameamua kuwapongeza kwa kuwapa motisha kwani kesho ni Januari moja ni vema wakauanza mwaka vizuri."Kila mfanyakazi aliyeajiriwa na wasioajiriwa lakini wanafanya kazi kwenye vyombo vya habari vya chama tutawapa motisha hiyo.Tutafanya kwa walioko Dar es Salaam na wa mikoani," amesisitiza.

Aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini."Nataka kumuona kila mfanyakazi uso kwa uso .Rais wetu aliamua kufanya uhakiki kwa watumishi wa Serikali ,nami namuunga mkono kwa kufanya uhakiki wa wafanyakazi wetu."amesema Sungura.
 MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group ambayo inasimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Faustine Sungura akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa motisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kama sehemu ya kuthamini mchango wao,aidha mbali ya kutoa motisha atatumia nafasi hiyo kufanya uhakiki wa wafanyakazi waliopo kwenye vyombo hivyo na iwapo kutakuwa na wafanyakazi hewa atawabaini na kuchukua hatua.
 MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura  akielezea mbele ya Waandishi wa habari leo Ofisini kwake jijini Dar,namna kampuni  hiyo inavyojipanga ,amesema kuanzia mwakani wataanza kufanya utafiti utakaochukua muda wa miezi mitatu na lengo ni kufahamu wasomaji wao,wasikilizaji wao na watazamaji wao wanataka nini."Pia Februari mwaka 2019 tutafanya 'uzinduzi laini' wa vyombo vyetu na Aprili 2019 tutafanya uzinduzi rasmi,ambapo ndio tutazungumza malengo na mikakati yetu.",alifafanua Sungura.
 MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Group Faustine Sungura akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi kutoka Idara ya Utawala,Banga Lucas kiasi cha fedha ikiwa ni sehemu ya motisha iliyotolewa kwa wafanyakazi wote wa  kampuni hiyo ikiwa kama sehemu ya kuthamini mchango wao.Picha na Michuzi Jr-MMG.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

ASKARI ALIYENUSURIKA KUUAWA NA MAJAMBAZI APANDISHWA CHEO

$
0
0


NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MMOJA wa askari watano waliotunukiwa vyeo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, kutokana na utendaji wao amesema kuwa alinusurika kupigwa risasi na jambazi wakati wakijiandaa kuwakabili katika eneo la Nyegezi,jijini Mwanza.

Askari huyo WP 12415 Dominica Michael ambaye ametunukiwa cheo cha Koplo amesema wakati akizungumza na mtandao huu muda mfupi baada ya kuvishwa cheo hicho na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna kwa niaba ya IGP Sirro.

Alisema kuwa Februari 2017, alinususurika kuuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuwahiwa na jambazi lakini kwa ujasiri alitumia mbinu ya uaskari kuwahi kulala chini kabla jambazi huyo kufariki kwa kupigwa risasi na askari wenzake.

Koplo Michael alieleza kuwa usiku wa siku ya tukio hilo laambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwake, walipangwa kuwakabili majambazi huko Nyegezi, kumbe eneo walikopangwa aliwahiwa na jambazi mmoja bila kumuona ambaye alimlenga kwa bunduki .

“Kwanza nashukuru kwa kupata cheo hiki ambacho sikukitarajia ambacho kinatokana na viongozi kutambua mchango wangu katika kulinda usalama wa raia na mali zao.Maishani mwangu sitasahau tukio la Februari 19, 2017 ambayo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwangu nilinusurika kuuawa nikiwa kazini,” alisema Koplo Michael na kuongeza;

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna akimvisha cheo Konstebo WP. 12415 Dominica Michael Nnko cheo kuwa Koplo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro baada ya kujwatunukia vyeo hivyo. 

TAARIFA YA SHUKURANI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

DC Uyui Aja na Mikakati ya Kuwakwamua Wananchi Kiuchumi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Isaya Msuya amesema kuwa Wilaya hiyo imejipanga kutekeleza miradi ya kimkakati itakayosaidia kuwakwamua wananchi kiuchumi katika kipindi cha mwaka 2019. 

Akizungumza katika mahojiano maalum amesema kuwa miradi hiyo itajikita katika sekta za Kilimo, Ufugaji, Elimu, Afya ambapo itawawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi na kujiletea maendeleo . 

“ Tumelenga kujenga Mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Wilaya yetu ina ardhi yenye rutuba na wananchi wanao uwezo mkubwa wa kushiriki katika uzalishaji kupitia sekta hii ndio maana tumeamua kuweka mikakati ya kukuza uzalishaji na kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda”. Alisisitiza Mhe. Msuya 

Akifafanua amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji kitasaidia kuongeza uzalishaji wa mpunga pamoja na mazao mengine ya biashara yatakayochochea ustawi wa wananchi na kukuza uchumi kwa ujumla. 

Akizungumzia huduma za afya amesema kuwa Wilaya hiyo imepokea shilingi Bilioni moja na nusu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na tayari maandalizi ya ujenzi yameanza ambapo mradi huo utakapokamilika utakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo ya jirani. 

Alitaja miradi mingine inayotekelezwa katika Wilaya hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya katika jimbo la Igalula kilichogharimu milioni 400 ambapo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho kukamilika ili wananchi waanze kupata huduma. 

Kwa upande wa kituo cha Afya Utege kilichopo jimbo la Tabora Kaskazini Mhe. Msuya amebainisha kuwa kimekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo hali inayoonesha dhamira safi ya Serikali kuleta ustawi kwa wananchi kwa kuboresha huduma za afya. 

BODA BODA WANAVYOHATARISHA MAISHA YAO BARABARANI

$
0
0
Bodaboda wachuuzi wa mkaa wanavyohatarisha usalama barabarani kwa kubeba mizigo kupita kiasi na kuhatarisha afya zao kwa kukaa juu ya tenki la mafuta kama wanavyoonekana katika picha tofauti, barabara ya Morogoro, eneo la Kibaha Mailimoja Dar es Salaam jana. Picha zote na Joseph Zablon 

MICHUZI TV: WAKALA WA MISITU WATOA NENO BAADA YA VIDEO HII KUSAMBAA

VOA SWAHILI: Duniani Leo December 31, 2018


Habari za UN: Matukio ya mwaka 2018

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 31/12/2018

RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA MWAKA MPYA KWA WANANCHI

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 1,2019

DC Chongolo, Msuya Waaga Mwaka 2018 kwa Kueleza Mafanikio ya Serikali

$
0
0
Na. Frank Mvungi

Wakuu wa Wilaya za Kinondoni, Daniel Chongolo na Wilaya ya Uyui, Gift Msuya kwa pamoja wamepongeza Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha mwaka 2018 ambazo zilizolenga kuboresha huduma za jamii na kuinua maisha ya wananchi.

Akizungumza leo katika mahojiano maalum na Idara ya Habari-MAELEZO, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2018, wananchi wameshuhudia uboreshaji wa miundombinu ya barabara, madaraja, vituo vya afya, Elimu, ujenzi Reli ya kisasa, Zahanati na ujenzi wa Hospitali mpya za Wilaya zipatazo 67.

"Ujenzi wa reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) hapa nchini utawezesha kufungua sekta mbalimbali ikiwemo uchukuzi, kukuza biashara kati ya Tanzania na mataifa ya jirani, kufungua uwekezaji ambao utachochea kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi na ustawi wa wananchi", ameeleza Chongolo.
Akifafanua kuwa katika Wilaya ya Kinondoni, barabara zenye urefu wa kilomita 58.2 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami na baadhi zimeshakamilika.

Ametaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika eneo la Mabwepande pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Kigogo vitaimarisha na kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi wa maeneo hayo.Kwa upande wa maji katika Wilaya ya Kinondoni amebainisha kuwa upatikanaji wa maji unatarajiwa kufikia zaidi ya asilimia 90 kutokana na maboresho na uwekezaji ulifanyika katika miundombinu ya maji.

Akizungumzia Wilaya ya Longido ambayo amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya, Chongolo amesema kuwa kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani Wilaya hiyo ilikuwa na Kituo cha Afya kimoja lakini hivi sasa vimejengwa vituo vya afya vinne vilivyojengwa katika Kata za Kitumbeine, Namanga, Engarenaibor na Olmoti.

Alibainisha kuwa upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani humo unatarajiwa kufikia asilimia 130 kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya maji.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Isaya Msuya, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa Shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ambapo tayari maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa na wa kihistoria yameanza.

Akizungumzia mikakati yakuwawezesha wananchi katika Wilaya hiyo, Msuya amesema tayari Serikali imeendelea kuwajengea mazingira wezeshi wananchi wa Uyui na mkoa wa Tabora kwa kuimarisha usafiri wa anga ambapo ndege za ATCL zimekuwa zikifanya safari za mara kwa mara mkoani Tabora jambo linalochochea maendeleo na ustawi wa wananchi kwa kufungua fursa za kukuza uchumi.

Ametaja miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini wa kufua umeme kutoka Mto Rufiji, Barabara, madaraja, vivuko, na ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuwa ni mafanikio makubwa kwa ujenzi wa uchumi na utoaji huduma bora kwa wananchi.

Aidha, amepongeza hatua ya Mhe. Rais kuwatambua wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga kwa kuwapatia vitambulisho maalum vinavyowawezeshakufanya biashara bila kubugudhiwa hali itakayowainua kiuchumi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato.

Wakuu hao wa Wilaya wameeleza kuwa kuwa katika mwaka 2019 wanatarajia kuendelea kutekeleza ahadi za Serikali ili kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi ikiwemo kuweka mazingira bora ya uwezeshaji kuichumi na utoaji wa huduma za jamii.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images