Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV : PAPII KOCHA AWAKUMBUSHA MASHABIKI ZAKE BABU SEYA...


MICHUZI TV : MASHABIKI WAMLILIA OMMY DIMPOZ USIKU WA FUNGA MWAKA NA KINGKIBA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI KIJIJI CHA NANDAGALA WILAYANI RUANGWA,APOKELEWA KWA SHANGWE

0
0



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UGANI WA KATA YA SASU WILAYANI KALIUA AINGIA MATATIZO KWA KUTOKUWEPO KITUONI KWAKE

0
0


NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemwagizwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kumchukua hatua Afisa Ugani wa Kata ya Sasu Amos Kafulila kwa kosa la kutokuwepo katika Kituo chake cha kazi bila ruhusa.

Alisema hatua hiyo inakwenda kinyume cha agizo la Mkoa la kuwataka watumishi wote wanaohusika na Kilimo kuwa karibu na wakulima kipindi hiki cha msimu wa kilimo ili kuwasaidia kulima kilimo cha kisasa. Mwanri alitoa agizo hilo juzi katika Kata ya Sasu wilayani Kaliua wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhamasisha kilimo bora ikiwemo kilimo cha pamba kwa kuzingatia Sheria na kununi 10 za zao hilo na kumkuta hayupo katika Kituo chake cha kazi.

Alisema Ofisi ya Mkoa ilishatoa maelekezo kuwa Maofisa Ugani wote katika kipindi hiki cha kilimo ,likizo zao zitaharishwa hadi hapo baadaye ili waende vijijini kuwasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija , lakini wapo baadhi yao wamekaidi na kuondoka katika maeneo yao bila hata kutoa taarifa kwa viongozi jambo ambalo ni utovu wa nidhamu. Mwanri alisema mkulima ni lazima asaidiwe kuondokana na kilimo cha kizamani cha kupata chakula cha kujikimu na badala yake azalishe ziada kwa ajili ya maendeleo yake na ujenzi wa viwanda nchini.

Alisema kimsingi Ofisi ya Mkoa haijazuia likizo ilichofanya ni kusogeza mbele ili Maofisa Ugani na watumishi wanaohusika na kilimo watumie kipindi hicho cha kilimo kuwasaidia wakulima kukabiliana na matatizo yanayorudisha nyuma maendeleo yao. Mwanri alisema Afisa Kilimo hakuajiriwa kukaa Ofisini bali ni kwenda kwa wakulima na kuwafundisha na kuwaelekeza mbinu sahihi za kilimo.

Alisema Afisa Ugani ambaye atakuwa na matatizo ambayo yanahitaji ruhusu ni lazima aombe kwa Mkurugenzi Mtendaji wake na kisha Mkuu wa Wilaya husika na Mkoa ufahamishe na sio kuondoka bila mamlaka ya juu kupewa taarifa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa ushauri jana kwa Mwenyekiti wa Halmashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele(kulia) juu ya kuunga mkono juhudi za wakazi wa kijiji cha Miti mitano za ujenzi wa Shule ya Msingi .Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima.

PAMBA FIFI ILIYOKUWA IMEBAKI WILAYANI URAMBO YAPATA UFUMBUZI NA TIGANYA VINCENT

0
0
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeagiza Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuhakikisha inanunua pamba iliyobaki Daraja B (fifi) ya wakulima wa Urambo ili kutowakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo hicho.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kufuatia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao hilo katika Kijiji cha Itengamatwi wilayani Urambo juu ya uwepo wa pamba ambao hadi hivi sasa iko katika maghala na wakulima hawajalipwa fedha.

Aliwataka wakulima kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa jitihada zinaendelea ili kuhakikisha pamba yao fifi(daraja B) ambayo hadi hivi sasa bado iko katika maghali ya kuhifadhi mazao inanunuliwa na Bodi ya Pamba Tanzana baada ya wanunuzi wa awali kusimamisha ununuzi na kuzima mashine.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wakulima kuzingatia kanuni 10 za kilimo cha zao hilo ili kuepuka kuzalisha pamba Daraja B ambalo ndio wakati mwingine linakuwa kigezo cha wanunuzi kuwapa bei mbaya na wakati mwingine kukataa kununua pamba yao.

Alisema azimo la Mkoa wa Tabora katika msimu wa kilimo cha zao ujao ni kila mkulima ni lazima azingatite kanuni kumi za zao hilo ikiwemo kuvuna kwa wakati na kuhifadhi katika hali ya usafi.Mwanri alisema hatua hiyo itasaidia kulinda ubora wa zao hilo na kumsaidia mkulima kupata Daraja A na kulipwa bei ya juu itakayompa fedha nyingi ambazo zitasaidia kuboresha maisha yake.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa somo kuhusu Sheria na kanuni 10 za kilimo cha pamba juzi katika kijiji cha Ugansa wilayani Kaliua jana .
Baadhi ya wakijiji wa Ugansa wilayani Kaliua wakisikiliza somo la Sheria na Kanuni 10 za zao la pamba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) jana .picha na Tiganya Vincent
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama akitoa salamu za Wilaya kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora aggrey Mwanri ili atoe somo kuhusu Sheria na kanuni 10 za kilimo cha pamba juzi katika kijiji cha Miti mitano

SHILINGI BIL. 222 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO-MAJALIWA

0
0

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222 zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kuwataka wakulima wawe na subira.

Amesema wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na uhakiki kisha watalipwa.”Fedha zipo, hakuna mkulima ambaye atapoteza haki yake wote watalipwa. Tunaendelea na uhakiki kwa wale wenye korosho nyingi ili kubaini kama hawajanunua kangomba.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Desemba 30, 2018) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Nandagala ‘A’ baada ya kufungua ofisi ya CCM kata ya Nandagala.Amesema baadhi ya watu wamekutwa na kilo zaidi ya 1,500 na wameshindwa kuonesha mashamba yao ya mikorosho, hali inayodhihirisha kwamba amenunua kupitia kangomba.

Waziri Mkuu amesema baadhi ya waliokutwa na korosho nyingi ni vijana wadogo ambao hawana hata uwezo kifedha hivyo Serikali itahakikisha inawakamata watu wanaowatuma.Amesema lengo la Serikali inayoongizwa na Rais Dkt. John Magufuli ni kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao, hivyo biashara ya kangomba lazima lidhibitiwe.Waziri Mkuu ambaye leo ameanza ziara yake kwa kikazi wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi amesema zoezi la ulipaji kwa wakulima wa korosho linaendelea, wakulima wawe na subira.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Doto Biteko Atoa Maagizo Mazito kwa Wachimbaji kokoto Dodoma

0
0


Na Nuru Mwasampeta

Kufuatia ziara ya Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoifanya hivi karibuni katika eneo la Ihumwa ambako ujenzi wa Mji wa Serikali unaendelea na kubaini uhaba wa kokoto katika ujenzi huo, leo Disemba 30, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akifuatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye maeneo yanayochimba kokoto hizo na kubaini madudu.

Naibu Mawaziri hao wamebaini machimbo ya kokoto yakiwa yamefungwa kwa madai kuwa wafanyakazi wako likizo, zikiwemo mashine za kusagia mawe hayo zikiwa zimeharibika kwa takribani miezi mitatu na hivyo kupelekea uzalishaji kusimama.

Akizungumza katika eneo hilo la machimbo, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema anashangazwa kuona kuwa watumishi katika mgodi wa kokoto wanakwenda likizo wakati mahitaji ya kokoto ni makubwa na soko la uhakika. “Mmechukua zabuni kwa ajili ya kusambaza kokoto kutoka kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),na kampuni ya MZINGA wenye uhitaji mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea halafu mnadai mko likizo,?” amehoji Biteko.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd , Biteko amemtaka mkurugenzi huyo aliyefahamika kwa jina la Joel Mchovu kuhakikisha kuwa, ifikapo Januari 2, 2019 kokoto ziwe zimezalishwa na kusambazwa kwa wahitaji kama walivyokubaliana ili ujenzi uendelee kwa kasi iliyokusudiwa.

Aidha, amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa juhudi na weledi mkubwa ili kuzalisha kiasi kinachotosheleza mahitaji vinginevyo oda zitahamishwa na kupewa kampuni za zinazozalisha kokoto zilizopo Chalinze ambazo zinaonesha uwezo mkubwa katika uzalishaji wa kokoto.

Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng (wa pili kushoto), akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Wa pili kutoka kulia) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (wa Kwanza kushoto) walipofanya ziara katika machimbo hayo ili kujionea kinachoendelea, wa kwanza kulia ni Afisa Madini wa Mkoa wa Dodoma mhandisi Jonas Mwano. 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika machimbo ya kokoto ya kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde na kushoto ni msaidizi wake Kungulu K. Masakala 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, akitoa tamko la Serikali kwa wachimbaji wa kokoto alipofanya ziara kujionea kinachoendelea katika machimbo hayo baada ya kubainika uhaba wa kokoto katika eneo la ujenzi wa ofisi za Serikali Ihumwa jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) pamoja na Naibu Waziri Ofisi  ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde (Kulia) wakiangalia moja ya kifaa kinachotumika katika kuchoronga mawe kwa ajili ya kokoto ambacho kwa sasa hakifanyi kazi kutokana na kuharibika. Katikati ni Fundi wa mashine katika mgodi wa WADI Gao Peng .

MICHUZI TV: MASHABIKI WAMLILIA OMMY DIMPOZ USIKU WA FUNGA MWAKA NA KINGKIBA


VOA Swahili: Wakongo wapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria

MICHUZI TV: PAPII KOCHA AWAKUMBUSHA MASHABIKI ZAKE MAMBO YA BABU SEYA...

Ohoooooooo....

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 31,2018

NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

0
0


NA LUSUNGU HELELA-MWANZA.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya  Kome  na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.
Kauli hiyo ameitoa  wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya  Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza  Naibu Waziri hiyo kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji  tozo kubwa hata kama mtu ana eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa lengo la kupata msaada zaidi.

Amefafanua kuwa mtu anayemiliki hekari moja  anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa hekari moja  kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.
Mmoja wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na serikali iweze kupata mapato yake.

Kaimu Meneja wa TFS Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo hizo na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi ya misitu.

Kanyasu amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja  kulipa tozo hizo kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi ili waweze kuilipa pesa hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akizungumza na  wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
2
 Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake  kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wa kutatua kero za  wananchi wanaoishi ndani ya  Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha  Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Kisaba na Bugombe
3
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama, Thomas Sabuni, akizungumza  na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa lengo  kutatua kero za wananchi wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika eneo la Kome mchangani.
4
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akiteta jambo na Meneja wa Shamba la Buhindi , Ayoub Kigongwira wakati wa  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Michuano ya Emirates FA Cup ndani ya DStv kuanzia Januari 2019

0
0
Wateja wa DStv wanauanza mwaka kwa kicheko baada ya kutangazwa rasmi kuwa DStv itaonyesha michuano maaruya ya Emirates FA Cup kupitia chaneli za SuperSport kuanzia tarehe 4 Januari 2019. Hii inamaana kuwa mechi za mzunguko wa tatu sasa zitaonekana katika kisimbuzi cha DStv

Akizungumzia kurejea kwa michuano hiyo katika chaneli za SuperSport, Mkurugenzi wa MutliChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema “Lengo letu ni kuwa mstari wa mbele katika kutoa burudani ya soka bora duniani kwa wateja wetu wa DStv hivyo, kuanzia tarehe 4 Januari 2019, wateja wetu wataweza kufurahia michuano ya Kombe la Emirates maarufu kama FA Cup kupitia chaneli za SuperSport zizopatikana ndani ya vifurushi vya DStv"

Amesema kuwa muda wote MultiChoice imahakikisha kuwa wateja wake wanapata burudani ya hali ya juu na ndiyo sababu wamekuwa wakiongeza maudhui mapya kila uchao katika vifurushi vya DStv. 

Sambamba na mechi za michuano ya kombe la FA za mzunguko wa tatu zitakazoanza Januari 4 2019, wateja wa DStv pia wataendelea kuburudika na ligi kubwa za soka zinazotamba duniani ikiwemo ligi kuu ya Uingereza maarafu kama PL, ligi kuu ya Italia Seria A, michuano ya ligi kuu ya Hispania {La Liga} na ligi ya mabingwa Ulaya maarufu kama EUFA Champions League bila kusahau maudhui mengineyo mengi zikiwamo filamu na tamthilia mpya kutoka nje na ndani ya Tanzania na vipindi vya watoto.

Mechi hizi za michuano  ya kombe la FA zitakuwa zikipatikana mubashara kupitia chaneli za Supersport ndani ya DStv. Idadi ya mechi zitakazoonekana mubashara zinatofautian kulingana na aina ya kifurushi huku baadhi ya mechi hizo zikionekana katika kifurushi cha chini cha DStv Bomba kwa Sh 19,000.

Kwa wateja wanaotaka kujiunga na DStv, bado wanaweza kunufaika na ofa inayoendelea ya msimu wa sikukuu ambapo kwa gharama ya Sh.79,000 tu!  Mteja anapata seti kamili ya DStv. Pia kupitiamtandao wa bongoshop.dstv.com mteja anaweza kupata maelekezo ya ziada ya namna ya kujiunga na DStv ikiwemo kuunganishwa na mawakala na mafundi wa DStv popote alipo.

WAZIRI KALEMANI AWATAKA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME KUELEZA MIPANGO KAZI YAO KWA VIONGOZI

0
0
Na Veronica Simba – Ukerewe
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchini kote, kuwasilisha mipango-kazi yao kwa viongozi na wawakilishi wa wananchi wa maeneo wanakofanyia kazi ili waweze kuielewa hivyo kusimamia utekelezaji wake.
Alitoa maagizo hayo jana, Desemba 30, 2018 wilayani Ukerewe akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ofisini kwa Mkuu wa Wilaya, Colonel Magembe, Waziri Kalemani alifafanua kwamba viongozi na wawakilishi wa wananchi ndiyo wanawajibika kuisemea serikali, hivyo wanapaswa kuifahamu kwa kina miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, waweze kuwaeleza wananchi.

“Hili ni agizo kwa wakandarasi wote wa miradi hii nchi nzima, wapatieni viongozi wa maeneo mnayofanya kazi mipango-kazi yenu, wajue nini mnatekeleza, kwa namna gani na kwa kipindi gani ili nao wasaidie kuwaelimisha wananchi wao,” alisisitiza Waziri.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chabilungo wilayani Ukerewe, Desemba 30, 2018 kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa pili-kulia) akikata utepe kabla ya kuwasha rasmi umeme katika Shule ya Msingi Chabilungo wilayani Ukerewe, Desemba 30, 2018, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme. Kulia ni Mkuu wa Wilaya, Colonel Magembe na kushoto ni Mwalimu anayefundisha shuleni hapo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akimweleza dhamira ya ziara yake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Colonel Magembe (kushoto) pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alipowasili wilayani humo Desemba 30, mwaka huu, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MABONDIA WAPIMA UZITO KUZIPIGA DESEMBA 31 UWANJA WA KINESI

0
0
Mabondia Azizi Uliza na Ramadhani Shauri wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Desema 31, 2018 mpambano wa kufunga mwaka na kufungua mwaka. Aliyekuwa wa kwanza kabisa kuingia katika viwanja vya las Vegasi Mabibo kwa ajili ya kupima uzito ni Azizi Uliza aliyeingia uwanjani kwa shangwe na ndelomo uku akisindikizwa na wapambe wake pamoja na vigoma.

Baara ya Saa moja Bondia Ramadhani Shauri naye akaingia na shangwe na ndelemo, vifijo zaidi ya mwenzake hata hivyo nani zaidi ya mwenzie itajulikana katika uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar es Salaam ambapo pambano hilo litapigwa kwa Raundi 10.

Akizungumzia mpambano huo, Promota  Josepher Nyilawila kutoka Kampuni ya Ijuka Sports amesema kuwa ulizi utakuwa ni wa kutosha, amesema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali ambapo Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazichapa na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' naye Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni.

Amesema mapambano yote hayo yatakuwa kwa kingilio cha Tsh 6000 na kwa V.I.P 10, 000 ambapo utashuhudia mapambano yote
Bondia Mussa Msabaha kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Makubi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kufunga mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika viwanja vya Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki Picha na Super D Boxing News
Bondia Azizi Uliza akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kufunga mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika uwanja wa kinesi uliopo Shekilango akizipiga na Ramadhani Shauri mpambano wa Raundi kumi.
Wasichana wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kufunga mwaka utakaofanyika Desemba 31 katika viwanja vya Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki

WAMILIKI WA MAABARA BINAFSI WASIOFUATA KANUNI KUCHUKULIWA HATUA KALI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
WAMILIKI wa maabara na vituo vya afya nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao mara moja bila shurti kabla ya Januari 15 2019 kwa kuhakikisha wanakamilisha vigezo vyote vya umiliki maabara hizo kwa kuwa muda wa kutoa elimu umepita na sasa ni muda wa kazi tu.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa  Tiba wa Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto na Mkurugenzi wa bodi ya usajili wa maabara Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa hadi kufikia Septemba 2018 bodi ya usimamizi wa maabara binafsi ilitambua jumla ya maabara 641 zinazojitegemea na maabara 719 zilizoshikizwa kwenye vituo vya tiba vya watu binafsi vya ngazi mbalimbali.

Amesema kuwa kutokana na baadhi ya wamiliki wa maabara binafsi hasa zilizoshikizwa kutofuata maadili ya uwajibikaji kisheria kufikia Septemba 20, bodi kupitia ziara yake imebaini kuwa kati ya vituo vya tiba 1731vya  watu binafsi vyenye maabara ndani ni maabara 1012 sawa na asilimia 58 pekee ndizo zilizotimiza wajibu wake wa kujiandikisha kwenye bodi ya usimamizi wa maabara binafsi na kutekeleza matakwa ya kisheria.

Amesema kuwa wamiliki ambao hawatatekeleza wajibu wao wa kumiliki maabara hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo pamoja na faini au vyote kwa pamoja.
Mkurugenzi wa  Tiba wa Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto na Mkurugenzi wa bodi ya usajili wa maabara Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa sheria ya umiliki wa maabara binafsi za Afya.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maabara Binafsi za Afya akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliohusu utekelezaji wa sheria ya umiliki wa maabara binafsi za Afya uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya Afya jijini Dar es Salaam. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

STEMPU ZA KIELEKTRONIKI ZA USHURU WA BIDHAA KUANZA KUTUMIKA JANUARI, 2019

0
0
Na Veronica Kazimoto
Bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa kama vile sigara, mvinyo, pombe kali pamoja na bia zitaanza kutumia rasmi stempu za kielektroniki Januari, 2019 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na Mbeya ambapo mfumo wa stempu hizo umeshafungwa kwenye mitambo ya uzalishaji.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ufungaji wa mfumo huo katika Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema kuwa mfumo huo mpya unaondoa mfumo wa zamani wa stempu za karatasi.

“Nimekuja kufanya ziara katika viwanda hivi ili kujiridhisha kama kweli mfumo huu wa stepu za kielektroniki umefungwa na nimejionea mwenyewe mfumo tayari umefungwa katika viwanda vyote nilivyotembelea. Hivyo, tunaachana na mfumo wa zamani wa stempu za karatasi na kwa sasa tunaendelea kufunga mfumo huu mpya wa stempu za kielektroniki kwenye mikoa mingine ambayo haitaanza katika awamu hii”, alisema Kichere.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akikagua bidhaa katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam ambapo Januari, 2019 Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa zitaanza kutumika rasmi katika bidhaa hizo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho  Rupa Suchak.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (katikati) akizungumza na watendaji wakuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Shonza: Wasanii Jiungeni na Mfuko wa TAGOANE kujikwamua Kiuchumi

0
0
Na Anitha Jonas, WHUSM, Arusha
Naibu  Waziri  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa  wasanii kujitokeza na kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE LOAN FUND.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Jijini Arusha  alipokuwa akizindua Mfuko Mkopo wa TAGOANE  LOAN  FUND katika Tamasha la Tukuza Festival  lililoandaliwa na Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE).
 “Tumekuwa tukishuhudia wasanii wengi wenye majina makubwa wakikosa fedha hata za matibabu  hili limekuwa ni suala lisilo pendeza hivyo ni vyema wasanii mkajiunga katika mfuko huu ambao utawasadia kupata mikopo yenye riba nafau na bima ya afya kupitia hili mnaweza kujikwamua kiuchumi  na kujifunza kuwekeza kwa maisha ya baadae ,“alisema Mhe.Shonza.
Kwa Upande wa Rais wa TAGOANE  Dkt.Godfrey Maimu alifafanua kwamba mfuko huo haubagui msanii kwani  msanii yeyote anayetaka kujiunga anaruhusiwa  kwani lengo la mfuko huo ni kuimarisha umoja wa wasanii na kuhakikisha maisha ya msanii yanaenda kubadilika badala ya msanii kuonekana ni mtu tegemezi  na wakuomba kusaidiwa hata kwenda studio kurekodi.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  akitoa wito kwa wasanii wote nchini kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha, alipokuwa akizindua mfuko huo ambapo amesisitiza kuwa  wasanii wa makundi yote wanaweza  kujiunga.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  aliyejifunika mgorori mwekundu wa kimasai akicheza na wanakwaya wa jamii ya Kimasai kutoka kanisa la KKKT Meserani  alipowasili kuzindua Mfuko wa Mkopo  unaoratibiwa na TAGOANE  (TAGOANE LOAN FUND) leo Jijini Arusha.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza  (aliyeketi watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) mara baada ya kuzindua Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha,(aliyeketi wapili  kulia) ni Rais wa Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) Dkt. Godfrey Maimu.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Juliana Shonza  (nyuma wapili kushoto) akicheza wimbo  Hapa Kazi Tu  uliyokuwa unaimbwa na Msanii Isack Chalo leo Jijini Arusha,mara baada ya uzinduzi wa  wa Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND). 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

IGP SIRRO AZINDUA RASMI CHAMA CHA WASTAAFU WA JESHI LA POLISI (TARPOA)

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wastaafu wa Jeshi la Polisi (TARPOA) Kamishna Mstaafu CP Suleiman Kova (Kushoto), akimkabidhi zawadi Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii Mussa Ali Mussa kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, katika sherehe za Uzinduzi Rasmi wa chama hicho zilizofanyika mwishoni mwa juma katika bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.
Mgeni Rasmi Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa Ali Mussa kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, akiwaongoza aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu IGP Said A. Mwema (kulia) na kamishna mstaafu suleiman Kova ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wastaafu wa Jeshi la Polisi (TARPOA) katika zoezi la kukata utepe wakati wa sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Chama hicho zilizofanyika mwishoni mwa juma katika bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.
Baadhi ya Wastaafu wa Jeshi la Polisi ambao pia ni Wanachama wa Chama cha Wastaafu wa Jeshi hilo TARPOA wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Chama hicho kilichoanzishwa mwaka 2006 na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Mstaafu Said Mwema. Picha na Jeshi la Polisi.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images