Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

YANGA YAENDELEZA UBABE TPL, YAIFUNGA MBEYA CITY 2-1 SOKONE MBEYA

$
0
0
Na Ripota Wetu, Mbeya

Timu ya Yanga imeendelea kushikilia usukani wa ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mbeya City mechi iliyochezwa kwenye dimba la Sokoine Jijini Mbeya.

Yanga wamefanikiwa kuibuka ushindi huo na kufikisha alama 50 akiwa amecheza michezo 18 akishinda 16 na kutoa sare michezo miwili.Katika dakika ya ... Mshambuliaji wa Kimataifa Heritier Makambo anaiandikia Yanga goli la kwanza akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib baada ya madhambi kutokea nje ya 18.

Dakika ya 24, Mbeya City wanasawazisha goli kupitia kaa Msambuliaji wake Iddy Seleman 'Nado' na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao ili wapate goli la kuongoza.Makambo akiwa ndani ya eneo la hatari aliweza kuwainua mashabiki wa Yanga katika dakika ya 41 akiwapeleka wana jangwani hao mapumziko wakiwa wanaongoza kwa goli 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Mbeya City wakisaka goli la kusawazisha lakini umakini wao ukiwa mdogo na kushindwa kutumia nafasi walizozipata.Mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi Martin Sanya inapigwa Yanga anatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 2-1 akiendelea kushikilia rekodi ya kutokufungwa.Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto'  na Haruna Moshi 'Boban' wakiwania mpira na mchezaji wa Mbeya City  Mpoki Mwakinyuke wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto'  na Haruna Moshi 'Boban' wakiwania mpira na mchezaji wa Mbeya City  Mpoki Mwakinyuke wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Mchezaji wa Mbeya City Medson Mwakatundu akiwa anaoambana kuchukua mpira kutoka kwa Heritier Makambo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Introducing "Gogo" Official Video by Nabella Produced by Marco Challi

TAMASHA KUBWA LA MKESHA WA MWAKA MPYA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA

AKAUNTI HALALI ZA INSTAGRAM NA TWITTER ZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI KANGI ALPHAXARD LUGOLA

$
0
0
Baada ya kuwepo kwa akaunti feki ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambao ulikua unatoa taarifa mbalimbali kwa jamii kuhusu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ujumla, kuanzia leo Disemba 30, 2018, Wizara inatangaza rasmi kwa jamii, akaunti halali zilizosajiliwa kwa jina la Mheshimiwa Waziri Kangi Lugola, kama ifuatavyo; 
 officialkangi_lugola (Instagram) 
@kangi_lugola (Twitter) 

 Taarifa zote zitakazotolewa katika kurasa za akaunti hizi zitakua sahihi. 
Kwa hatua hiyo, Wizara inaendelea kutoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayejihusisha kwa kutumia jina la Kangi Lugola kusajili akaunti yoyote na kutoa taarifa za Waziri huyo kupitia akaunti feki hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 

 Aidha, Wizara inawaomba Watanzania waendelee kupata taarifa zake zaidi kupitia tovuti yenye anuani; www.moha.go.tz na twitter ya Wizara kwa akaunti ya Msemaji Mambo ya Ndani. 

 Imetolewa na: 
 Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali 
 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Rais Dkt. Magufuli ashiriki katika Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kanisani kwa ajili ya kushiriki Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30,2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30,2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa Amani na Masista wa kanisa katoriki na waumini wengine wakati wa Ibada ya jumapili ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30,2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na watoto wa kanisa katoriki wakati wa Ibada ya jumapili ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Paroko msaidizi Padre Asis Mendokta mara baada ya kuungana na waumini wengine katika Misa ya Maadhimisho ya sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Desemba 30, 2018.
PICHA NA IKULU

Waziri Hasunga aziagiza Bodi za Mazao nchini kuwasajili Wakulima wote

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amewaagiza Wakurugenzi wa Bodi za Mazao kuanza mara moja zoezi la kuwatambua na kuwasajili wakulima wa mazao yote nchini lengo likiwa kuwatambua ili kupanga mipango sahihi yenye kuongeza tija na uzalishaji katika mazao yote.

Ametoa agizo hilo jana tarehe 29 Disemba 2018 wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Mhe. Hasunga amesema ili kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya kilimo na kuandaa mipango madhubuti ya kuendeleza mazao yote ni vyema kuwatambua Wakulima wote nchini na kuongeza kuwa Wakulima wa zao la korosho wametoa funzo kubwa kwa Wizara yake kufanya jambo kama hili katika mazao mengine hapa nchini.

Itakumbukwa kuwa wiki tatu zilizopita, Waziri Hasunga alitoa agizo kwa Bodi ya Korosho agizo kuandaa daftali maalumu la kuwatambua Wakulima wa korosho kote nchi ambapo moja ya taarifa ambazo zitajumuishwa katika daftali hilo ni pamoja na Jina Kamili la Mkulima, Mkoa, Wilaya, Kata na Tarafa anayotoka.Mambo mengine ni pamoja na Kitongoji, Mtaa au Jina la Kijijini anapotoka, mahali lilipo shamba pamoja na ukubwa wa shamba lake.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa mipango sahihi ya kuwaendeleza Wakulima kuanzia kwenye kilimo chenyewe hadi kufikia katika hatua ya kuvuna, kuhifadhi na kulifikia soko ni vyema kuwa na mfumo maalumu wa kanzi data (Database) ya kuwafahamu ili kushughulikia mahitaji yao kisasa na kwa haraka zaidi.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akifatilia mkutano wa Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao, uliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018.
Wenyeviti wa Bodi za Mazao pamoja na Wakurugenzi wa Bodi hizo za Mazao,  wakifatilia mkutano wa kazi ulioongozwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) kwenye ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma jana tarehe 29 Disemba 2018.

AZAM YAJIZATITI KUTETEA UBINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi Azam FC, imepangwa kundi moja na Yanga kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2019 inayotarajia kufanyika kuanzia Januari 1 hadi 13 mwakani Visiwani Zanzibar. 

Azam FC ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo ikibeba mara mbili mfululizo, mbali na kupangwa Kundi B pamoja na Yanga, kundi hilo pia lina timu nyingine za Malindi, KVZ na Jamhuri ya Pemba. 

Mabingwa hao wataanza kampeni ya kuanza kutetea taji kwa kupambana na Jamhuri, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar Januari 2 mwaka huu saa 2.15 usiku kabla ya Januari 5, kukipiga na Yanga. Aidha, Azam FC itamaliza hatua ya makundi kwa mechi mbili dhidi ya KVZ (Januari 7, 10.15 jioni) na kufunga dimba Januari 9 kwa kumenyana na Malindi saa 2.15 usiku. 

Baada ya hapo, Azam FC itasubiria hatua ya nusu fainali itakayohusisha timu mbili zitakazoshika nafasi mbili za juu kwa kuwa na pointi mbili kwenye makundi yote mawili na washindi wa mechi hizo mbili wataingia fainali itakayopigwa kwenye Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba. 

Kundi A la michuano hiyo linahusisha timu za Simba, KMKM, Mlandege na Chipukizi. Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, imesema kuwa zawadi kwa mshindi wa kwanza itaongezwa kutoka shilingi milioni 10 hadi kufikia shilingi milioni 15 ikiwa ni pamoja na medali za dhahabu pamoja na kombe. Mshindi wa pili naye naye atapata shilingi milioni 10 badala ya milion 5 iliyokuwa ikitolewa awali, na medali za fedha. 

Katika hatua nyingine itakuwa imeandika rekodi ya kuwa timu pekee iliyofanya hivyo, na timu pekee kulitwaa mara nyingi taji hilo ikifanya hivyo mara tano na itakuwa imeiacha Simba iliyolitwaa mara nne.
MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi Azam FC

UJENZI MJI WA SERIKALI WAENDELEA KUSHIKA KASI


MICHUZI TV: HIVI NDIVYO ALI KIBA ALIVYOZIKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE JIJINI DAR

MAJALIWA ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU NDEJEMBI JIJINI DODOMA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini, Pancras Ndejembi, nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Bibi Leah Pancras Ndejembi, Mjane wa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PMO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Edna Ndejembi ambaye ni binti Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi Job Lusinde wakati alipowasili nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia Desemba 29, 2018. Kushoto ni Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa na Waziri Mstaafu, William Kusila.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na waombolezaji nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa maremu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AMJULIA HALI MAMA YAKE MZAZI BIBI. SUZANA MAGUFULI ANAYEPATIWA MATIBABU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Wasaidizi wake wakimuombea Mama yake Mzazi Bibi. Suzana Magufuli anayepatiwa Matibabu Jijini Dar es Salaam,Desemba 30, 2018. Bibi Suzana Magufuli anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa.PICHA NA IKULU



WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MTWARA AKIWA NJIANI KWENDA RUANGWA

$
0
0



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kwenda Ruangwa, Desemba 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Jilly Elibariki Maleko wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kwenda Ruangwa, Desemba 30, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bibi Rehema Madenge.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akislimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kwenda Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido

$
0
0

Na Anitha Jonas – WHUSM,Namanga -Arusha.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Mhe.Juliana Shonza ameuagiza uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini kukamilisha ujenzi wa kituo cha kurusha matangazo kinachojenga Makao Makuu ya Wilaya ya Longido ndani ya wiki moja.

Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hilo leo Wilayani Longido alipotembelea kituo cha kurusha matangazo ya TBC kinachojengwa Wilayani hapo kwa lengo la kutatua kero ya kukosekana kwa usikivu wa matangazo ya TBC ambapo wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakisikiliza radio za nchi jirani na hiyo imewafanya kukosa taarifa zenye ukweli na uhakika za ndani ya nchi.

“Chumba hichi cha kuhifadhi busta na mitambo mingine ni kidogo sana na ujenzi wake siyo wa kuchukua muda mrefu hakikisheni mpaka Januari 10,muwe mmekamilisha ujenzi wa Kituo hichi wananchi wa Longido wanakiu kubwa ya kutaka kusikia matangazo kutoka chombo hichi cha serikali chenye habari za ukweli na uhakika na hii ni haki yao,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo aliwasisitiza viongozi hao wa TBC kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho cha kurushia matangazo kinajengwa kwa kutumia vifaa imara kwani serikali ilitenga bajeti yenye fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha usikivu unaboreshwa katika maeneo ya mipakani na malengo ya serikali ni kabla ya mwa 2020 kero hii ya usikivu iwe imekwisha.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kurushia matangazo Longido ndani ya wiki moja kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw.Gerald Uisso (hayupo pichani) alipotembelea eneo hilo leo lilopo katika ofisi za Wilaya ya Longido,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Bw.Jumaa Mhina. 
Meneja wa TBC Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso (wa kwanza kulia) akimwonyesha Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (katikati) nyumba ambayo imejengwa kwa ajili ya kuweka busta za kurushia matangazo pamoja na mitambo leo alipotembelea eneo hilo Wilayani Longido linapojengwa mitambo hiyo kwa lengo ya kuthibiti changamoto ya usikivu wa matangazo ya TBC,wa (kwanza kushoto) ni Katibu Tawala Wilaya ya Longido Bw. Toba Nguvila. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Fundi Mitambo wa TBC Mhandisi Christopher Mkama akitoa maelezo kuhusu hali ya usikivu kwa eneo la Namaga alipotembelea kituo hicho cha kurusha matangazo ya TBC kilichopo Namanga leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kufuatiliaji wa usikivu kwa Kanda ya Kaskazini . 

STEMPU ZA KIELEKTRONIKI ZA USHURU WA BIDHAA KUANZA KUTUMIKA JANUARI, 2019

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa kama vile sigara, mvinyo, pombe kali pamoja na bia zitaanza kutumia rasmi stempu za kielektroniki Januari, 2019 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na Mbeya ambapo mfumo wa stempu hizo umeshafungwa kwenye mitambo ya uzalishaji.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ufungaji wa mfumo huo katika Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema kuwa mfumo huo mpya unaondoa mfumo wa zamani wa stempu za karatasi.

“Nimekuja kufanya ziara katika viwanda hivi ili kujiridhisha kama kweli mfumo huu wa stepu za kielektroniki umefungwa na nimejionea mwenyewe mfumo tayari umefungwa katika viwanda vyote nilivyotembelea. Hivyo, tunaachana na mfumo wa zamani wa stempu za karatasi na kwa sasa tunaendelea kufunga mfumo huu mpya wa stempu za kielektroniki kwenye mikoa mingine ambayo haitaanza katika awamu hii”, alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa lengo la kuweka stempu za kielektroniki kwenye bidhaa hizo ni kupata idadi halisi ya uzalishaji wa bidhaa ili kutoza kodi stahiki na kuondoa dhana ya kusema kwamba TRA inawaonea wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa hizo kwa kutoza kodi isiyoendana na uzalishaji.“Lengo la kuweka stempu hizi za kielektroniki ni kupata kiasi halisi cha uzalishaji wa bidhaa hizi ili kila upande uridhike yaani mzalishaji alipe kodi sahihi na sisi TRA tutoze kodi stahiki bila kupingana wala kugombana na wateja wetu”, alisema Kichere.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania Rupa Suchak amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha serikali kufunga mfumo huo wa stempu za kielektroniki kwa sababu serikali itaongeza mapato na wafanyabiashara wataongeza uhiari wa kulipa kodi.“Ninaishukuru sana serikali yetu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuleta mfumo huu mpya ambao utaongeza mapato na kupanua wigo wa kodi lakini pia kwetu sisi wafanyabiashara tutaongeza uhiari wa kulipa kodi”, alisema Rupa.

Uwekwaji wa stempu za kielektroniki katika bidhaa nyingine kama vile juisi, maji ya chupa, bidhaa za muziki na filamu (CD\DVD\Tape) zitafuata kwa tarehe ambayo itatangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania hapo badae.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akikagua bidhaa katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam ambapo Januari, 2019 Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa zitaanza kutumika rasmi katika bidhaa hizo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bi. Rupa Suchak.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (katikati) akizungumza na watendaji wakuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa.

KIBITI ILIVYOJIPANGA NA ULINZI KATIKA SIKUKUU YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2019

$
0
0
Na Linda shebby , KIBITI

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji ni tulivu na salama hadi sasa hii ni kutokana na jitihada za jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na mshikamano wa wananchi.

Kamanda Lyanga amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo amesema"Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote kwa kusherehekea vyema sikukuu ya Krismas mnamo Desemba 25 mwaka huu ambapo wananchi wa Rufiji walisherehekwa kwa utulivu na amani".

Aidha alisema kuwa anapenda kuwajulisha kuwa jeshi la polisi litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wadau wote ili katika sherehe za kumaliza mwaka 2018 tuendelee kuwa na usalama kwa raia wote pamoja na mali zao.

"Niwatahadharishe kuwa katika kusherehekea kila mmoja azingatie sheria za nchi kwani kuvunja sheria kwa kigezo cha furaha ya kumaliza mwaka ama kwa sababu yoyote ile ikiwemo kufanya vitendo vya kihalifu mathalani kuchoma moto matairi barabarani au mitaani , ulipuaji wa fataki, baruti, kuendesha vyombo vya moto , shughuli za disko toto na ulevi wa kupindukia havitavumilika kwani vinaweza kuwa chanzo cha madhara mbalimbali kwa binaadamu pia natoa rai kwa kila kaya kuimarisha ulinzi katika makazi yao"alisema Lyanga.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na kuimarisha ulinzi na kufanya doria na misako katika kipindi hiki cha sikukuu kwa kutumia askari waendao kwa miguu, pikipiki na magari katika miji na barabara zote kuu.

"Tunaomba wananchi mtuunge mkono kwa maslahi mapana ya taifa letu"alisema Kamanda Lyanga.

Tanzania Kinara Ukuaji Uchumi Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika

PANITA WAZUNGUMZIA MAZURI YALIYOFANYIKA MWAKA 2018 KATIKA LISHE, WATOA USHAURI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


JUKWAA la Lishe Tanzania (PANITA) limesema kuna mambo kadhaa mazuri ambayo yamefanywa kwa mwaka huu 2018 katika eneo linalohusu lishe nchini Tanzania huku likitoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha eneo la lishe linapewa kipaumbele zaidi kwa mwaka ujao wa 2019.

PANITA limetoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya Michuzi Blog kutaka kufahamu ni mambo gani mazuri ambayo yamefanyika katika eneo la lishe kwa mwaka huu 2018 ambao umebakisha siku moja ya kesho kumalizika.

Uongozi wa PANITA pamoja na mambo mengine mazuri ambayo yamefanywa na wadau wa masuala ya lishe nchini, umesema kwa mwaka huu 2018 wamefurahishwa na ongezeko la bajeti iliyotengwa kwa ajili ya lishe toka Sh.bilioni 11 kwa mwaka 2017/18 mpaka Sh.bilioni 14 mwaka 2018/19.Pia wamezungumzia kufurahishwa na kusainiwa kwa mikataba ya kutekeleza afua za lishe kati ya wakuu wa mikoa na Makamu wa Rais kupitia Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imeongeza uwajibikaji wa Lishe katika ngazi zote.

"Tukiri kwa mwaka huu kuna mambo mengi mazuri ambayo yamefanyika na kuonesha jitihada za dhati katika kuhakikisha eneo la lishe kwa Watanzania lipata nafasi ya kuwepewa kipaumbele.Kumewepo na mikutano ya mipango na bajeti za lishe iliyoshirikisha pia asasi imeongeza umiliki wa mipango.Pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuahidi kutunga sheria ya kubana,"amesema.

Uongozi wa PANITA umefafanua Waziri mkuu aliahidi kushawishi Bunge kuwe na sheria ya kubana fedha za lishe zisitumike vinginevyo.PANITA imetoa mwito umefika wakati kuwa na vyanzo vya fedha vya ndani katika 
kushughulikia suala la lishe ili kupunguza utegemezi wa wafadhili

.Pia wameshauri Serikali kujenga nyumba za kunyonyeshea ili kuwapa nafasi ya kunyonyesha watoto vizuri hususani miji yenye foleni.

VIDEO' INAYOSAMBAA MITANDAONI YAWAIBUA TFS

$
0
0
*Yaomba radhi wasafiri, yafafanua utaratibu kusafirisha mazao ya misitu
*Pia yamzungumzia Ofisa wake wa Misutu, kumchukulia hatua za kinidhamu 


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA Wakala wa  Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  umepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii na wadau  mbalimbali  zinazohusisha  namna  Ofisa  Misitu  wa Wilaya  ya  Korogwe mkoani Tanga ambavyo alikuwa akitekeleza majukumu ya kusimamia Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni
zake za  mwaka 2004.

Ofisa huyo  alikuwa akitekeleza  majukumu hayo kwa mujibu wa  kifungu cha 93 (Powers of officers with respect to offences) inayompa mamlaka Ofisa Misitu au Ofisa wa Jeshi  la  Polisi  kukagua,  kukamata  na  kuzuia  mazao  yanayodhaniwa  kupatikana  kinyume  na sheria.

Kwa kukumbusha tu leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na video inayosambaa kwa kasi kubwa ikionesha namna ambavyo wananchi wanalalamikia kitendo cha Ofisa Misutu akilumbana na abiria baada ya kulisamamisha gari na kubaini kuna vitanda vimebebwa.Hivyo kukaibuka malumbano ambayo yamechangia TFS kuamua kutoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari.

Taarifa ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) iliyotolewa leo Desemba 30,2018 imesema uongozi wa  TFS  umefanya uchunguzi wa haraka na kubaini  kuwa abiria mmoja  alikuwa akisafirisha  vitanda  viwili vipya  kwa  basi. Vitanda hivyo vililipiwa  ushuru wa Serikali kupitia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) na kupewa stakabadhi halali ya Desemba 26, 2018 katika kituo cha Mkata, Handeni Mkoani Tanga.

Imefafanua katika kutekeleza  majukumu  yake,  Ofisa  wao alimtaka  abiria  huyo  kuonesha  hati  ya Kusafirishia  bidhaa  hizo  kwa  mujibu  wa  Kanuni  za  Misitu  Kifungu  cha  13, sehemu ndogo ya 4 ambayo inakataza mwenye chombo chochote  cha usafiri kusafirisha mazao ya  misitu  ambayo  hayana  hati  ya  usafirishaji  ambapo  abiria  huyo  hakuwa  nayo. 

WAZIRI MPANGO ATOA TAARIFA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI 2018/2019

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 katika kipindi cha Julai-Novemba, 2018), ambapo alisema Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi tano zinazokua kwa kasi kiuchumi Barani Afrika, wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.

MKAZI WA TARIME AJISHINDIA MILIONI 10 ZA TIGO JIGIFTISHE

$
0
0

Mkazi wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen, ameibuka mshindi wa wiki katika promosheni ya Tigo Jigiftishe na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10.

Stephen anakuwa mshindi wa sita wa zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga, Jane Jisandu wote wa Dar es Salaam pamoja na Mbwana Mbela mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma na Flora Somba wa Morogoro.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake wilayani Tarime mwishoni mwa wiki, mshindi huyo aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusena itamsaidia kutimiza baadhi ya malengo yake kwa urahisi. “Naishukuru promosheni hii kwa kunipatia Sh 10m/-. Fedha hii imekuja muda muafaka kwa kuwa itanisaidi kulipa ada za shule kwa watoto wangu na pia itanisaidia kupanua mradi wangu wa ufugaji wa kuku. Natarajia pia kuanza ujenzi na fedha hii itakuwa nia ya msaada mkubwa kufanikisha lengo hili,” alisema

Stephen alisema alifanikiwa kushinda zawadi hiyo kutokana na kutumia huduma za Tigo Pesanikiwa bni pamoja na kutumua pesa, kukunua vifurushi mbali mbali nakuongeza kuwa ilikuwa vigumu kuamini kuwa amejishindia kiasi hicho pesa kwa urahisi alipopigiwa simu kuambiwa kuwa ni mshindi .Kwa upande wake Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya, alimpongeza Styephen kwa kuibuka mshindi na kuwataka watu kuendelea kutumia huduma za tigo ili waweze kuingia katika droo ambazo wanayo nafasi ya kujishindia shilingi milioni 50,25 na 15

Kuweza kujishinda mamililioni katika promosheni ya Tigo Jigiftishe ni rahisi sana, haina makato ya pesa wala kujiunga, ukitumia huduma zetu za tigo unaibuka mshindi” alisema Mainoya.

Mkazi wa Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya Sh 10m/- kutoka kwa Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya baada ya kuibuka mshindi wa wiki katika promosheni ya Tigo Jigiftishe katika hafla fupi ya kumkabidhi zawadi yake iliyofanyika Tarime mwishoni mwa wiki. 
Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya (kulia) akisisitiza jambo kwa  mshindi wa zawadi ya Sh 10m- katika promosheni ya Tigo Jigiftishe Ahia Stephen (kati kati) muda mfupi kabla ya kumkabidhi zawadi yake katika hafla fupi iliyofanyika Tarime mkoani Mara. Kushoto Meneja wa Tigo Mkoa wa Mara Abdillahi Luhorera 
Mshindi wa zawadi ya wiki ya sh 10m/-katika promosheni ya Tigo Jigiftishe kutoka Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen (katikati)akifurahia mfano wa hundi muda mfupi baaba ya kukabidhiwa zawadi yake wilayani Tarime mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Tigo Mkoa wa MaraAbdillahi Luhorera na kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya 
Mshindi wa zawadi ya wiki ya sh 10m/-katika promosheni ya Tigo Jigiftishe kutoka Tarime Mkoani Mara Ahia Stephen (kushoto) akiwapungua wakazi wa mji mdogo wa Tarime waliofika katika viwanja vya stendi ya Tarime kushuhudia akikabidhiwa zawadi yake. Kushoto ni Meneja wa Tigo Mkoa wa MaraAbdillahi Luhorera. 
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images