Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Rais Dkt Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Dkt. Irene Isaka


UKARABATI WA MIUNDO MBINU YA BARABARA JIMBO LA VUNJO KUREJEA JANUARY.

0
0
VUNJO-KILIMANJARO 

MBUNGE wa Vunjo, James Mbatia amesema kuanzia wiki ya pili ya mwezi Januari mwaka ujao, mitambo yote ya ujenzi wa barabara iliyokuwa imezuiwa na serikali ya Wilaya ya Moshi kuendelea na kazi za upanuzi wa barabara, itarejea kazini.

Alitangaza uamuzi huo mbele ya mamia ya wananchi, viongozi wa dini mbalimbali, madiwani na watendaji wa vjijiji waliohudhuria hafla ya siku ya wana Vunjo iliyofanyika Chuo cha Ualimu Marangu, Wilaya ya Moshi.

“Tumeingiliwa lakini tujipe moyo kwa sababu jambo lolote likipata msukosuko sana, ni jambo lenye heri. Mwezi wa 11 mwaka huu Rais (Magufuli) aliagiza kazi hii iendelee mara moja, kwa hiyo naomba nitangaze kwa niaba ya bodi ya VDF (Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo), wiki ya pili ya mwezi Januari 2019, vyombo vyote vinarudi kazi na kazi inaendelea,”alisema Mbatia

Wakati Mbatia anatangaza uamuzi huo, tayari upanuzi na ujenzi wa barabara hizo za vijijini katika Jimbo la Vunjo kwa kiwango cha changarawe, umezuiwa na serikali Wilaya ya Moshi.Mradi huo unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zitagharimu sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Eliona Kimaro alisema maendeleo ya mtu na utu wake na nguvu ya jamii ndivyo pekee vinavyoweza kuchochea kuleta maendeleo katika nchi yeyote ile.

“Nguvu ya jamii katika kuleta maendeleo na kutatua matatizo yao binafsi na ya serikali ni kinyume kabisa katika maendeleo kwa kanuni za kiuchumi.Zaidi Much, Kimaro alieleza: "Kufikiri kwamba nchi tu ndiyo inaweza ikaleta maendeleo ni makosa, ndio maana wanasiasa wengi wa Marekani wamekuwa wakisema ili uwe Rais wa nchi au kiongozi wa serikali lazima uwe na mawazo haya, kwamba unakwenda kuifanyia nini nchi na sio nchi imfanyie yeye,”alisisitiza 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa VDF ambaye ni Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao alisema dhamira ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni si kuboresha tu miundo mbinu ya barabara, bali pia kuna sekta za afya, elimu, maji na sekta ya mazingira.Alisema taasisi hiyo ndio mwanga wa alfajiri uliopewa jina la ‘ngatuni yetu’ ambayo inataka kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora, salama na pazuri pa kuishi, kwa vile itatekeleza jukumu hilo nchi nzima.
Mwenyekiti wa Tahsisi ya Maendeleo ya Vunjo (VDF) Askofu Mstaafu wa KKKT dayosisi ya Kaskazini ,Dkt Martin sham akizungumza wakati wa Sherehe ya siku ya Wanavunjo (Vunjo Day) iliyofanyika chuo cha Ualimu Marangu na kukutanisha wananchi na viongozi mbalimbali.
Mbunge wa jimbo la Munjo na Katibu wa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo (VDF) Mh James Mbatia akizungumza katika sherehe hizo ambas zinafanyika kwa mara ya kwanza Latina jimbo hilo na kukutanisha wenyeji wa Vunjo waishio nje na ndani ya jimbo hilo.
Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama ,Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Eliona Kimaro ambaye pia ni mwenyeji wa Jimbo la Vunjo akizungumza latina sherehe hizo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki katika sherehe hizo wakipiga makofi .

KIGAMBONI YAONGOZA UTOAJI VITAMBULISHO

0
0
Wilaya ya Kigamboni imeongoza katika utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali katika mpango wa kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuwa ya kwanza katika Mkoa wa Dar es salaam kuwafikia wafanybiashara wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sara Msafiri alipokutana na wandishi wa habari ofisini kwake  jana. Mkuu wa Wilaya amesema ofisi yake ilipokea vitambulisho elfu tano toka ofisi ya Rais-Tamisemi na vikiwa na lengo la kukusanya jumla ya shilingi Milioni mia moja lakini mpaka jana Desemba 28,2018 jumla ya shilingi milioni 94 sawa na asilimia 97 ya lengo.

  Mkuu wa Wilaya amesema  kuwa kiwango hicho kimefikiwa baada ya kuwa na mpango wa ushirikishwaji wa watendaji wa mitaa na wenyeviti ambapo waliweza kuwafikia wajasiriamali wengi katika mitaa yao.

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Temeke Bw.Gamaliel Mafie amesema wao kama mamlaka wamefurahia huo mpango kwa kuwa umewajumuisha watu ambao hawakuwa kwenye mfumo rasmi wa walipa kodi. Ameongeza kuwa hata wao wamepokea mpango huo kwa furaha kwa kuwa umepanua wigo wa walipa kodi kwa mpango wa kuchangia.

Akihitimisha kikao hicho, Mkuu wa Wilaya  ametuma ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili aweze kupatiwa vitambulisho elfu tatu (3000), kukidhi idadi kubwa ya wafanyabishara ambao bado hawajafikiwa mpaka sasa.
 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akimkabidhi kitambulisho cha mjasiriamali,Amina Rashidi jana  jijini Dar es Slaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Temeke,Gamaliel Mafie akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika jana  jijini Dar es Salaam.

Baada ya maafa RC Wangabo aunga mkono juhudi za wananchi kukarabati shule

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amechangia shilingi milioni tatu ili kuharakisha ukarabati wa ujenzi wa shule ya msingi Msia pamoja na shule ya sekondari Kipeta zote za bonde la ziwa rukwa, Wilayani Sumbawanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi katika kurudisha miundombinu ya shule hizo zilizoharibika baada ya upepo na mvua kali iliyonyehs amwanzoni mwa mwezi huu.

Kati ya fedha hizo shilingi milioni mbili zitatumika katika shule ya msingi Msia na shilingi milioni moja zitatumika kuikarabati shule ya sekondari kipeta ambapo zimebaki wiki mbili shule hizo kufunguliwa na wanafunzi kutakiwa kuendelea na masomo.

Mh. Wangabo aliwashukuru wananchi waliojitokeza kuchangisha fedha kwaajili ya ukarabati wa shule ya msingi Msia zilizofikia kiasi cha shilingi 5,595,000/= ambapo wananchi wa kawaida walichangia shilingi 5000/=, wafanyabiashara wadogo shilingi 20000/=, mfangabiashara wa kati shilingi 50000/= na wafugaji shilingi 100000/= ambapo fedha hizo zinatarajiwa kufanya ukarabati na ujenzi wa madarasa manane.

Awali akisoma taarifa ya harambee ya ukarabati wa shule Mtendaji wa kijiji cha Msia Andrew Sanga alieleza mikakati ya kijiji kuwa ni kuongeza vyumba vya madarasa vitatu, na ofisi moja ya walimu na msingi umeshaaza kujengwa, kukusanya michango kwa wananchi ambao bado kuchangia na hivyo kutimiza lengo la kujenga madarasa nane, ofisi mbili ndani kabla ya shule kufunguliwa mwanzoni mwa mwezi wa kwanza.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa mapungufu yaliyopo ni kama ifuatavyo, bati, madirisha, nondo, misumari, madirisha, milango na rangi, ili kukamilisha majengo tunayoendelea kuyajenga kwani shule hiyo yenye wanafunzi 866 ina uhitaji wa madarasa 22,” Alibainisha.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza kushoto)akionyeshwa maendeleo ya ujenzi wa madarasa unaoendelea ili kuhakikisha shule inapofunguliwa mwezi wa kwanza wanafunzi wanapata fursa ya kuendelea na masomo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akishiriki msingi wa ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Msia alipokwenda kuangalia ujenzi unaoendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo 
Kipeta Sekondari – Jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kipeta likiwa limeezuliwa paa. 

PROF. KABUDI ATEMBELEA IHUMWA ATOA MAAGIZO

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea eneo linapojengwa jengo la Wizara yake na kuagiza timu maalum kupiga kambi eneo hilo ili kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana huku wakizingatia viwango vya ubora katika ujenzi wa jengo hilo.

“Nataka ujenzi uharakishwe kama ambavyo Waziri Mkuu alivyogiza lakini viwango vya ubora katika ujenzi vizingatiwe” alisema Prof. Kabudi.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amemtaka mkandarasi anayejenga jengo la Wizara hiyo kuhakikisha anakusanya mahitaji yote yanayotakiwa eneo la ujenzi ili kufanikisha kasi ya ujenzi inaenda kama inavyotakiwa.

Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Katiba na Sheria unatarajiwa kukamilika mapema ifikapo tarehe 15 Januari 2019.

MAKONDA ATOA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA WAGONJWA, WAFANYAKAZI WA MUHIMBILI, ORCI NA HOSPITALI ZA RUFAA DAR

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa zawadi ya ng’ombe 20 kwa ajili ya mwaka mpya 2019 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na hospitali za rufaa za Temeke, Ilala na Kinondoni ikiwamo Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI). 

Zawadi hiyo imetolewa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hizo pamoja na wafanyakazi ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza kutokana na huduma bora ambazo wanazozitoa na hivyo kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.

Akizungumza katika machinjio ya Vingunguti, Mkuu wa Mkoa Makonda amewataka watumishi wa hospitali hizo kuongeza juhudi katika sehemu zao za kazi ili Mkoa wa Dar es Salaam uwe namba moja katika kutoa huduma mbalimbali za afya. “Idadi ya malalamiko imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na huduma za matibabu kuimarika,” amesema Makonda.

Pia, mkuu huyo wa mkoa ametoa zawadi ya ng’ombe 20 kwa Jeshi la Polisi na ng’ombe 20 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya 2019. Katika hatua nyingine, Makonda amesema kwamba Serikali itajenga machinjio ya kisasa na kwamba ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 8.5.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa machinjio ya Vingunguti wakati akitoa zawadi ya mwaka mpya ya ng’ombe 20 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Ocean Road, na hospitali za rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana na Mwananyamala. 
Baadhi ya wananchi na maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakimsikiliza mkuu wa mkoa kabla ya kutoa zawadi ya mwaka mpya. 
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed akimshukuru Mh. Makonda kwa kulipatia jeshi hilo zawadi ya mwaka mpya ya ng’ombe 20. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Mhe. Makonda na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bwana Makwaia Makani 
Mhe. Makonda akikagua ng’ombe ambao ametoa zawadi ya mwaka mpya kwa hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ). 
Baadhi ya ng’ombe wakiwa katika machinjio ya Vingunguti leo baada ya Mhe. Makonda kukabidhi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Maghembe. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) .

Mkandarasi Jengo la Wizara ya Nishati Atakiwa Kukamilisha Kazi ya Ujenzi kwa Wakati

0
0

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amemtaka mkandarasi anayetekeleza kazi ya ujenzi wa Jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa.

Akizungumza katika eneo la Ihumwa Waziri Kalemani amesema kuwa, ili kufanikisha utekelezaji wa kazi hiyo kwa wakati ni vyema mkandarasi huyo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akahakikisha kuwa vifaa vyote vinavyotakiwa katika kutekeleza kazi hiyo vinakuwepo katika eneo la kazi.

“Ni Lazima mkandarasi uhakikishe kuwa matofali, mchanga, simenti, mabati, kokoto, rangi, madirisha, nondo na vifaa vyote vinavyotakiwa hapa kwa ajili ya ujenzi vinapatikana kwa wakati wote katika eneo hili la ujenzi ili kuharakisha utekelezaji wa kazi hii kama ulivyopangwa na si vinginevyo”;

Akifafanua, Dkt. Kalemani amesema kuwa atakuwa akitembelea eneo hilo mara kwa mara kuona hatua za utekelezaji wa kazi hiyo na kuwaasa watendaji wa Wizara yake kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa karibu kazi husika ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hamisi Mwinyimvua amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anaongeza mitambo inayotakiwa katika kutekeleza ujenzi huo ili kuongeza kasi ya utekelezaji.

Ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati ni utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wizara zote kujenga majengo katika eneo hilo la Ihumwa unakojengwa mji wa Serikali unaojumuisha majengo ya Wizara zote.

NAMAINGO YAZINDUA MRADI WA ASALI MIZINGA 55000 KIBITI

0
0

Na Richard Mwaikenda, Kibiti.

TAASISI ya Namaingo, imezindua uwekezaji wa Mradi wa Mizinga ya nyuki wa asali 55000 wa wanachama wake katika Kijiji cha Kikale, wilyani Kibiti, Mkoa wa Pwani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jana kijiji hapo, Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Namaingo, Ignus Augustino, alisema mipango yao ni kila mwanachama kuwa atamiliki mizinga 50.

Uzinduzi huo ulifanywa mbele ya wananchama waliotoka Dar es Salaam pamoja na wanakijiji wa Kikale katika mabanda matatu yenye mizinga 200 ya kuanzia. Mizinga hiyo ipo ndani ya msitu wa miti ya mikoko inayoaminiwa kutoa daraja la kwanza la asali yenye kiwango cha kimataifa.

Augustino alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kuutekeleza mradi huo mkubwa ambapo hivi sasa tayari watalaamu wa kutengeneza malkia wapo eneo la mradi. Urinaji ukianza baada ya miezi sita Kila mzinga utakuwa unatoa kilo 20 za asali. Naye Mwenyekiti Msaidizi wa Namaingo, Elesia Mkuru, alisema baadhi ya wanachamama walikuwa 

hawaamini kuwa mradi huo utandinduliwa, lakini sasa wameshaona ukweli wa mambo.Aliipoongeza Serikali kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), kwa kuwaruhusu kuwekeza mradi huo katika misitu iiyopo mikoa ya Pwani, Iringa, Njombe, Dar es Salaam na Morogoro. Mwanachama wa Namaingo, Queen Ryoba, alisema kuwa wamefurahi sana kuona mradi huo umeanza 
Baadhi ya Wanachama wa Taasisi ya Namaingo wakiangalia moja kati ya mabanda ya ufugaji nyuki wa asali wakati wa uzinduzi Mradi wa Mizinga 55000 katika Kijiji cha Kikale, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Namaingo, Ignus Augustino, akiwaongoza wanachama kuangalia mizinga.
Wanachama wakiangalia baadhi ya mizinga


Watumishi 13 Ulanga hatiani ubadhirifu wa Bil 2.9

0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

OFISI ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) imebaini matumizi mabaya ya fedha za serikali Sh. bilioni 2.98 katika halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wakuu wa idara wote waliohusika wavuliwe nyadhifa zao huku watumishi wengine waondolewe majukumu ili vyombo vya dola viendelee na hatua kwa mujibu wa sheria dhidi yao.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Twala za mikoa na Serikali za mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uchunguzi maalum uliofanywa kwa halmashauri ya wilaya hiyo.

Jafo alisema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi imefanya uchunguzi maalum katika halmashari 12 nchini ambazo ni Ulanga, Same, Mbulu, Meru, Itigi, Misungwi, Nyang’hwale, Serengeti, Bahi, mpwapwa, Morogoro Dc na Kibaha Tc ambapo katika halamasahuri ya Ulanga uchuguzi ulianza Novemba 13 hadi 23 mwaka huu.

Alisema uchunguzi huo ulifanyika kufuatia malalamiko ya wanachi mbalimbali pamoja na mbunge wa jimbo la Ulanga Mhe. Goodluck Mlinga kutokana na ubadhirifu uliokuwepo. Aidha alisema kiasi hicho kimebainika kupotea kutokana na matumizi mabaya ya fedha za serikali ambapo watumishi wasio waadilifu katika halmashauri hiyo walikiuka taratibu na kufanya manunuzi hewa na kutumia vibaya fedha kinyume na malengo yaliyopangwa.

“Halmashauri hii imekuwa ikifanya udanganyifu katika taarifa za miradi ya maendeleo taarifa za mfuko wa wanawake na vijana, kwa ujumla inausimamizi mbovu wa mapato na kuwa na udhibiti hafifu wa makusanyo na matumizi ya fedha za Umma”alisema Jafo. Jafo alisema kuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ulanga, Yusufu Daud Semguruka kwa nafasi yake ya afisa masuhuli alishindwa kusiomamia sheria ya fedha za serikali za mitaa katika kudhibiti na kuweka mifumo dhabiti ya kuhakikisha fedha ziko salama kuanzia makusanyo hadi matumizi yake.

“Hii ni pamoja na kushindwa kumsimamia mweka hazina wa halmashauri katika kutekeleza majukumu yake na kwa kushindwa kutekeleza majuku hayo amesababisha hasara halmashauri ya shilingi 2,980,172,763.60″alisema Jafo. Alifafanua kuwa Rajabu Siriwa,ambaye alikuwa ni mweka hazina wa halmasahuri hiyo alichangia kuhujumu mapato ya serikali kwa kuweka utaratibu ambao umeisababishia hasara serikali.

Alisema kuwa mweka hazina huyo aliidhinisha malipo ya sh. 225,586,400 nje ya bajeti bila idhini ya ofisi ya Rais Tamisemi ambapo malipo hayo yalihusisha posho ya safari ya mkurugenzi mtendaji Sh. 192,000,000. “Pia kukusanya mapato na kutoyapeleka benki, katika mfumo wa LGRCIS umeonyesha halmashauri ilikusanya fedha ambazo hazikupelekwa benki kabisa shilingi 760,686,732.43 fedha hizi hazijulikani matumizi yake halisi ni nini”alihoji Jafo.

Mtoto apotea mazingira ya kutatanisha Z’bar

0
0

MTOTO Manahil Mundhir Rashid mwenye umri wa miaka mitano (pichani), amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha eneo la Mkunazini mjini Unguja Visiwani Zanzibar.

Baba wa mtoto Mundhir Rashid, amesema kuwa mtoto wake alipotea Oktoba 14, mwaka huu baada ya kushuka kwenye basi wakati akitoka shule.

“Nipo kwenye mashaka ni zaidi ya miezi miwili sasa sijamuona mtoto wangu sijui yuko wapi na kwenye mazingira gani Mungu wangu.“Binafsi nina mashaka makubwa na usalama wa mtoto wangu na hata mimi na mke wangu. Tumejawa na hofu ni wapi alipo mtoto wetu,” amesema Rashid

Kutokana na hali hiyo amesema walitoa taarifa Kituo cha Polisi Madema mjini Unguja ambapo lilifunguliwa jalada ya uchunguzi namba MAD/R.B 8011/18.Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya polisi ilieleza kuwa tayari mtu mmoja ameshakamatwa Oktoba 17, mwaka huu katika Bandari ya Malindi, Zanzibar kwa kosa hilo la kudaiwa kutorosha mtoto.

Baba huyo wa mtoto huyo aliwaomba wananchi kwa yeyote atakayemuona atoe kituo kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au awasiliane na baba mzazi wa mtoto huyo kwa namba ya simu 0773044899



SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA LATOA USHAURI KUHUSU VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Bima la Taifa Tanzania(NIC) limeshauri kwamba ufike wakati sasa kuwepo na sera ambayo itahimiza mashirika, taasisi na wadau mbalimbali kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vita ya dawa za kulevya nchini.

Ushauri huo umetolewa leo Desemba 28,2018 na Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) Israel Severe wakati wa tamasha la Kataa Mihadarati liloandaliwa na Taasisi ya Binti Filamu chini ya Mwenyekiti wake muigzaji maarufu wa filamu Ndumbagwe Misayo a.k.a Thea .Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo alikuwa Naibu Waziri Stella Ikupa.

"Shirika la Bima la Taifa Tanzania tumeamua kushiriki kwenye tamasha hilo kutokana na kutambua umuhimu wake kwa jamii.Tunajua moja ya jukumu letu ni kushughulika na mambo ya bima lakini kwetu ni muhimu zaidi kuona jamii tunayoihudumia inakuwa salama kiafya.Sote tunatambua athari za matumizi ya
dawa za kulevya, hivyo tumeamua kushiriki kikamilifu kwenye vita hii ili kukomesha dawa hizo nchini.

"Tunashauri ifike wakati kuwe na sera ambayo itazungumzia umuhimu wa mashirika na taasisi mbalimbali nazo kushiriki kwenye vita hii ya dawa za kulevya.Hivyo ni wakati muafaka kwa Serikali kuweka sera itakayokwa chachu kwa mashirika na taasisi zote kushiriki kwa vitendo na iwe ni wajibu wetu,"amesema Severe.

Kuhusu tamasha hilo , Severe amesema anaupongeza uongozi wa Binti Filamu kwa uamuzi wake wa kuandaa tamasha hilo lenye lengo la kutoa elimu kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwamo wao ambao wamedhamiria kwa dhati kukomesha dawa hizo nchini kwetu.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Bw. Israel Severe ambaye ni Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) kutokana na mchango wa shirika hilo katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival) lililoandaliwa na tasisi ya Binti Filamu inayoundwa na wasanii wa filamu, tamashahilo limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati Foundation jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi kutokana na mchango Mamlaka hiyo katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival) lililoandaliwa na tasisi ya Binti Filamu Foundation inayoundwa na wasanii wa filamu, tamashahilo limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es salaam.
Bw. Israel Severe ambaye ni Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) akizungumza katika tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.

TBC TAFUTENI USHAURI WA MAENEO KWA WAZAWA KABLA YA KUSIMIKA MITAMBO YENU

0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM,Lushoto -Tanga

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amewataka viongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC )kusikiliza ushauri wa wazawa wa maeneo wanayoenda kusimika mitambo yao pale wanapofanya utafiti wa maeneo yatakayofaa kulingana na Jiografia ya eneo husika.

Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo Wilayani Lushoto alipotembelea eneo lililowekwa mitambo ya TBC iliyoko katika eneo la Kwemashai kwa lengo la kutaka kubaini changamoto zinazosababisha kutokuwepo kwa usikivu kwa baadhi ya maeneo Wilayani hapo.

“Changamoto kubwa katika Wilaya hiyo ya Lushoto ni Jiografia ya eneo hilo kwani inamilima mingi sana kati maeneo yake yote hivyo ni vyema mkashirikiana na Halmashauri katika kuelekezana eneo abalo itakuwa na mlima mrefu zaidi kushinda yote ambao utawafaa kwakuweza kusimika mtambo wenu utakao rusha matangazo katika maeneo yote ya Wilaya hii,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo aliusisistiza uongozi wa TBC kanda ya Kaskazini kuhakikisha wanafanya utafiti huo haraka na kusimika mitambo hiyo mapema kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha inakamilisha usikivu kwa mikoa iliyoko karibu na maeneo ya mipakani kabla ya mwaka 2020 na ndiyo maana fedha za bajeti ya kuboresha usikivu zinatolewa kila mwaka.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Julianna Shonza akitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatia kabla ya kusimika mitambo ya usikivu kwa Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso (hayupo pichani) leo katika Kijiji cha Kwemashai alipotembelea eneo hilo walilosimika mitambo yao wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo iliyoko mitambo ya TBC kwa Kanda ya Kaskazini. 
Mtambo wa kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) uliyopo katika Kijiji cha Kwemashai Wilayani Lushoto ambapo Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Julianna Shonza alitembelea eneo hilo leo ikiwa ni ziara yake ya kukagua maeneo iliyopo mitambo ya TBC kufuatia changamoto ya usikivu katika maeneo hayo ya Kanda ya Kaskazini. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili kulia) akitizama mitambo iliyopo Lushoto, (watatu kulia)Meneja wa Shirika la Utangazaji Taifa Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso akimwonyesha mitambo ya kurushia matangazo ya TBC iliyoko katika eneo la Kijiji cha Kwemashai alipofanya ziara yake aliyoifanya leo ya kukagua maeneo yaliyisimikwa mitambo ya TBC kutokana na kuendelea kuwepo kwa kero ya usikivu katika eneo hilo.  
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiwashauri viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lushoto kuuendeleza uwanja wa michezo wa Sabasaba kwa kuomba wataalamu Wizarani wa kuwapa ushauri wa kiutalamu wa namna ya kuboresha uwanja huo alipotembea uwanja huo leo,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Lushoto Bw.Amiri Shekelata . 

ASKARI WA JWTZ AUA ASKARI MWENZIE NA RAIA HUKU ASKARI MAGEREZA AKIJIUA KWA KUJIPIGA RISASI - RUVUMA

0
0
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma SACP Gemini Mushy amesema kuwa mnamo disemba 27 majira ya jioni Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) katika kambi ya Chandarua iliyopo Wilayani Songea Mkoani Ruvuma askari aitwaye Ssgt Juma Uwesu Mkele akiwa kazini pamoja na raia Veronika Kayombo waliuawa kwa kupigwa risasi na askari wa JWTZ aitwaye Sgt Batisin Philip Samda akitumia bunduki aina ya SMG.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma SACP Gemini Mushy amesema kuwa askari Magereza aitwaye Adam Kunwa ambaye ni mganga katika Zahanati ya ya Gereza la Kitai lililopo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma akiwa lindoni alijiua kwa kujipiga Risasi kichwani na kufariki na upelelezi wa polisi unaendelea ili kuweza kubaini nini chanzo

Wateja wengine 20 wa NMB washinda 100,000 kila mmoja

0
0
DROO ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', imefanyika tena kwa mara ya pili Ofisi Kuu za Benki ya NMB jijini Dar es Salaam ambapo wateja 20 wengine wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja.

Akizungumza katika droo hiyo ya pili leo, Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo alisema washindi hao 20 wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo ya pili ya shindano hilo, na wamebahatika baada ya kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.

Akifafanua zaidi Bw. Achayo alisema washindi hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kuibuka washindi.Droo hiyo ya pili iliyofanyika leo inakamilisha jumla ya idadi ya wateja 40 ambao hadi sasa wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja huku ikiendeshwa kwa wazi na wateja wakipigiwa simu kuarifiwa ushindi wao na baadaye fedha hiyo kuingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mshindi.

Aidha aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea.Alisema takribani wateja 200 wa NMB ambao watafanya malipo kwa mfumo wa 'NMB Mastercard au 'NMB Masterpass' watakuwa kwenye uwezekano wa kujishindia zawadi za fedha, simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari iliyolipiwa ya mapumziko kwenda Dubai.
Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo akizungumza jana kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Meneja Mahusiano Selcom Sebastian Msuya akifuatilia zoezi hilo.
Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo akizungumza jana kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Meneja Mahusiano Selcom Sebastian Msuya na Meneja NMB Kitengo cha Kadi, Stephene Jilala (kulia) wakifuatilia zoezi hilo.
 

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMENI YA “Twende9teen” JIJINI DAR LEO

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na baadhi ya watoto na wazazi waliofika katika Tamasha la “Twende9teen” lilioandaliwa na Benki ya CRDB kupitia akaunti za “Junior Jumbo” na “Young Money Teens”, lililolenga kuwahamasisha wazazi na walezi kuwafungulia watoto wao akaunti na kuwawekea akiba ili kutimiza ndoto za watoto wao hususani katika nyanja ya elimu, Tamasha hilo limefanyika leo katika viwanja vya Mlimani City, jijini Dar es salaam ambapo Watoto walipata fursa ya kucheza michezo mbalimbali iliyoandaliwa kwa ajili yao. Walioketi kushoto ni Naibu Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts pamoja na Esther Kitoka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na baadhi ya watoto na wazazi waliofika katika Tamasha la “Twende9teen” lilioandaliwa na Benki ya CRDB kupitia akaunti za “Junior Jumbo” na “Young Money Teens”, lililolenga kuwahamasisha wazazi na walezi kuwafungulia watoto wao akaunti na kuwawekea akiba ili kutimiza ndoto za watoto wao hususani katika nyanja ya elimu, Tamasha hilo limefanyika leo katika viwanja vya Mlimani City, jijini Dar es salaam ambapo Watoto walipata fursa ya kucheza michezo mbalimbali iliyoandaliwa kwa ajili yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Esther Kitoka wakishiriki kuwafunguliwa watoto zawadi za pipi, katika Tamasha la “Twende9teen” lilioandaliwa na Benki ya CRDB kupitia akaunti za “Junior Jumbo” na “Young Money Teens”, lililolenga kuwahamasisha wazazi na walezi kuwafungulia watoto wao akaunti na kuwawekea akiba ili kutimiza ndoto za watoto wao hususani katika nyanja ya elimu, Tamasha hilo limefanyika leo katika viwanja vya Mlimani City, jijini Dar es salaam ambapo Watoto walipata fursa ya kucheza michezo mbalimbali iliyoandaliwa kwa ajili yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akijaza fomu ya kuweka hela kwenye akauti ya Junior Jumbo katika gari maalum la Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Twende 9nteen JJ leo katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimuuliza swali mmoja wa watoto katika Tamasha hilo.


UTUMISHI YAUNGA MKONO KWA VITENDO KAMPENI YA MAKAMU WA RAIS YA KULIFANYA JIJI LA DODOMA KUWA KIJANI KWA KUPANDA MITI

0
0
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeunga mkono kwa vitendo kampeni iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti katika ofisi yake inayojengwa Ihumwa jijini Dodoma kwenye mji wa serikali.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro mara baada ya watumishi wa ofisi yake kukamilisha zoezi la upandaji wa miti katika mji wa serikali Ihumwa, eneo ambalo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inajengwa ili kutoa huduma kwa umma. Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo ni endelevu na kuongeza kuwa, Ofisi yake itahakikisha miti hiyo inatunzwa kwa kuimwagilia maji ili hatimaye kuwe na mandhari ya kijani pindi ofisi yake itakapokamilisha ujenzi wa jengo kubwa.

Naye, mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Menyeaichi Koka ameongeza kuwa, watumishi wa Ofisi ya Rais – Utumishi wameitikia wito wa Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kupanda miti ili kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani na kuishukuru menejimenti ya ofisi kwa kusimamia vema zoezi hilo ambalo kila mtumishi amelifanya kwa hiyari na kwa moyo mkunjufu.

Bi. Koka ahaidi kuwa, atahakikisha mti alioupanda anauhudumia vizuri kwa kuumwagilia maji ya kutosha ili uweze kustawi vizuri na kuwa ni miongoni mwa miti iliyopandwa na kufanikiwa kukua vizuri na hatimaye kuchangia jiji la Dodoma kuwa kijani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua kampeni za kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani Julai 21, 2017 kwa kuongoza zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza kuhusu ofisi yake kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani iliyozinduliwa na  Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kukamilisha zoezi la upandaji miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathew Kirama akishiriki katika zoezi la upandaji miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akishiriki kuchimba mashimo kwa ajili kupanda miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiwa tayari kupanda miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma ili kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Julai 21,2017. 

MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UENDELEZAJI MIJI YA KIMKAKATI KATIKA JIJI LA DODOMA

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma na kukagua ujenzi wa maegesho ya malori makubwa katika eneo la Nala na uboreshwaji wa mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangalijijini Dodoma.

Pia amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi andelee kutenga maeneo ya mapumziko ili wananchi wapate sehemu za kukutana na kubadilishana mawazo baada ya kumaliza kufanya kazi. Waziri Mkuu amekagua maeneo hayo leo (Jumamosi, Desemba 29, 2018) ambapo ameupongeza uongozi wa jiji la Dodoma kwa kubuni wazo hilo na kusema kwamba ni muhimu kwa miji mikubwa kutenga maeneo ya kwa ajili ya mapumziko.

Amesema lazima jiji la Dodoma lipangwe kisasa na amewataka wahandisi wahakikishe maeneo ya mapumziko yatengwa na yanatumika kama ilivyokusudiwa. Pia amemtaka Mkurugenzi wa Jiji, Kunambi aendelee kusimamia ujenzi wa kimkakati ndani ya jiji hilo. ”Hatuwezi kuwa tumejaza nyumba kila eneo, watu hawana mahali pa kupumzika na kukutana na marafiki zao plan ya Chinangali Park ni nzuri, Jiji la Dar es Salaam plan ya awali kulikuwa na maeneo ya mapumziko lakini watu wa Idara ya Ardhi waliyauza.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amekagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na utekelezwaji wa agizo lake baada ya kutembelea eneo hilo na kukuta uzio umebomolewa na sasa kuna bustani iliyojengwa kwa ajili ya mapumziko na pia barabara imefunguliwa na wananchi wanaendelea kuitumia kama ilivyokuwa awali.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uboreshaji wa Mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangali jijini Dodoma, wakati alipokagua Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika Jiji hilo, Desemba 29, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Gowin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma, wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Watatu kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji hilo, Desemba 29, 2018. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .


SUPER NYAMWELA NA UBUNTU WAFUNIKA NIGERIA

0
0
Na Mwandishi Wetu,Calabar, Nigeria

Mnenguaji nyota wa muziki wa dansi Mtanzania, Hassan Mussa 'Super Nyamwela' na bendi yake Ubuntu Traditional juzi alifanikiwa kuwachengua maelfu ya watu waliofurika katika shamra shamra za tamasha la kimataifa Calabar Carvinal Festival, linalofanyika mjini Calabar nje kidogo ya jiji la Abuja nchini Nigeria.

Nyamwela na bendi yake walitumia fursa ya dakika tatu walizopewa na waandaji wa tamasha hilo Serikali ya Nigeria kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ili wasalimie tu na kuangusha shoo ya nguvu iliyofanya washangiliwe kwa nguvu.

Maelfu ya watu waliojipanga pembezoni mwa barabara za mji wa Calabar waliwashangilia wasanii hao kwa namna walivyoamsha dude na kusababisha gumzo.

Ubuntu ilitumia nafasi hiyo kuonyesha watanzania wamekuja Calabar kwa ajili ya kutangaza utamaduni wa Tanzania na si kutalii hivyo kipande cha shoo hiyo ni sehemu ndogo ya makubwa waliyojiandaa kuyafanya siku ya kupanda jukwaani rasmi ambayo ni leo usiku wa Jumamosi Desemba 29.

Hii ni mara ya pili kwa Nyamwela na bendi yake ya Ubuntu kushiriki tamasha hilo ambalo linashirikisha nchi zaidi ya 60 duniani.Kwa Tanzania ni Ubuntu pekee ndiyo imepata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka kwa udhamini wa serikali ya Nigeria ambayo imekuwa ikilitumia kutangaza utalii wa nchi yake.

Tamasha hilo lilianza rasmi Desemba 4 mwaka huu na linatarajia kufikia tamati Januari 4 mwaka 2019.
Mnenguaji nyota wa muziki wa dansi Mtanzania, Hassan Mussa 'Super Nyamwela' na bendi yake Ubuntu Traditional juzi alifanikiwa kuwachengua maelfu ya watu waliofurika katika shamra shamra za tamasha la kimataifa Calabar Carvinal Festival, linalofanyika mjini Calabar nje kidogo ya jiji la Abuja nchini Nigeria.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia onesho hilo

Matukio Katika Picha Maendeleo ya Ujenzi wa Mji wa Serikali

0
0
Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akikabidhi fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme za Wizara zote kwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi.Peter Mwaisabula walipokutana wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka. Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhi fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme za Wizara zote kwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi. Peter Mwaisabula (katikati) walipokutana wakati wa zoezi la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018.Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka na kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda. Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo jijini Dodoma. Aliyevaa tisheti ni Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe. Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akielezea jambo alipokuwa akikagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuitaka TBA kuwa na Ofisi katika eneo unapojengwa Mji wa Serikali ili kuharakisha huduma za ushauri kwa Makandarasi wanaoendelea na ujenzi wa Ofisi za Wizara mbalimbali leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda. Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe (kulia) akielezea jambo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu na Bunge) leo jijini Dodoma.


TAMASHA KUBWA LA MKESHA WA MWAKA MPYA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA,KIINGILIO BURE

0
0

Tamasha kubwa la mkesha wa kufunga 2018 na kufungua mwaka 2019 linatarajiwa kufanyika Desema 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkesha huo utakaokuwa wa aina yake unatarajia kumdondosha Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka nchini Nigeria anaejulikana kwa jina la Chris Shalom, anayetamba na wimbo wake maarufu uitwao 'my beautifier' na nyingine nyingi.

Pamoja Na Chris Shalom pia waimbaji wengine mbalimbali mahiri kutoka hapa nchini akiwemo Jesica Honore, Goodluck Gosbert, Joel Lwaga Na John Lisu wanatarajiwa kutumbuiza katika mkesha huo.

Mkesha wa mwaka 2019 umeandaliwa na Nabii (prophet) Clear Malisa wa Passion Java ministry, kutoka ubungo kibangu jijini Dar es Salaam.Waigizaji/wachekeshaji na watu maarufu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa pia kuwepo akiwemo Pastor Kuria kutoka show ya churchchill nchini Kenya.

Katika tamasha hilo hakuna kiingilio na usafiri utatolewa kwa watu wote katika vituo vyote vikubwa vya usafiri Dar es Salaam.Mkesha wa mwaka 2019, umedhaminiwa Na Clouds media group, Elishadai shopping center Na Fair Travel adventures.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images