Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

NEW ONLINE TANZANIAN VISA SERVICE


MICHUZI TV: Tazama uzuri wa Maporomoko ya Maji Malasusa wilayani Rungwe, Mbeya

MBUNGE AANZA KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTONI

$
0
0
Katika kuhakikisha tatizo la mimba za utotoni Mashuleni linatoweka Mkoani Ruvuma, Mbunge wa Viti maalum Mkoani humo Kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) Jackline Ngonyani Msongozi ametoa mifuko 50 ya Saruji katika shule ya sekondari Makita iliyopo Wilaya Ya MBinga kwa Ajili ya ukarabati wa Mabweni ili kuwapunguzia changamoto wanazokutana wanafunzi wakike pindi wanapokuwa wanarudi kutoka shule.
Attachments area

MICHUZI TV: Fedha za maendeleo tunayoyaona hazitoki mbinguni, ni kodi za wananchi-RC PAUL MAKONDA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA MJI WA SERIKALI ENEO LA IHUMWA JIJINI DODOMA

$
0
0

*Akuta baadhi ya wakandarasi wanasuasua, wengine wako vizuri
*Aitisha kikao cha Mawaziri, Makatibu Wakuu wote kesho saa 5 asubuhi
*Ataka leo jioni apewe taarifa ya kila taasisi inayohusika Ihumwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali lililoko Ihumwa na kubaini kuwa baadhi ya wakandarasi hawaendi na kasi inayotarajiwa na Serikali.

Waziri Mkuu ameamua kuitisha kikao cha Mawaziri wote na makatibu wakuu wote kesho (Ijumaa) saa 5 asubuhi ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini.Ametoa agizo kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 27, 2018) mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Mtumba lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

“Nimekagua maeneo yote na kukuta baadhi ya wakandarasi wanatakiwa kujenga majengo ya wizara nne hadi tano. Sijaridhika na baadhi ya kazi, nimeitisha kikao cha Mawaziri wote kesho ili tuangalie ni mkandarasi yupi anaweza kumudu hii kazi.”

“Nimebaini kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kama kokoto, nondo, matofali na kikao cha kesho kitahusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, viongozi wa Mkoa na Jiji la Dodoma, wakandarasi wote ili tukubaliane kazi hii inaisha lini,” amesema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma ramani ya Mji wa Serikali wakati alipokagua Ujenzi wa mji huo, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Mipango Miji katika jiji la Dodoma, William Alfayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na Kulia ni Katibu  wa Kikosi Kazi cha  Kuhamishia Shughuli za Serikali jijini Dodoma, Meshack Bandawe. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Katibu  wa Kikosi Kazi cha  Kuhamishia Shughuli za Serikali jijini Dodoma, Meshack Bandawe kuhusu Ujenzi wa Mji wa Serikali wakati alipokagua Ujenzi huo, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa jengo Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi ya kusuka nondo  kwa ajili ya nguzo za jengo la Ofisi za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018.  Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Msingi  wa jengo la Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati alipokagua Ujenzi wa Mji wa Serikali, eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Desemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Matangazo maalum ya Michezo Dira ya Dunia TV

Waziri Mhagama aitaja Mikoa 11 vinara kwa Mabaraza ya Biashara

$
0
0
Na OWM, Kigoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ameitaja mikoa 11 ambayo ilianzisha mabaraza ya Biashara na hadi sasa yako hai na kubainisha kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo la kuanzisha mabaraza hayo tu lakini utendaji wa Mabaraza hayo umekuwa siyo endelevu.

Waziri Mhagama ameitaja Mikoa hiyo 11 ambayo Mabaraza yake yako hai hadi sasa kuwa ni Dodoma, Kigoma, Tanga, Geita, Morogoro, shinyanga, Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Songwe na Mbeya. Aidha, Mhagama amebainisha kuwa Mikoa mingine ambayo mabaraza yake hayafanyi vikao inakiuka Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 unaosisitiza kuanzishwa kwa mabaraza hayo na utendaji wake kuwa endelevu.

Akiongea wakati wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma, Waziri Mhagama alifafanua kuwa Dhumuni kuu la kuanzisha mabaraza ya biashara hususani katika ngazi ya wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali na Sekta Binafsi katika kila ngazi ya utawala, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa ajili ya kukuza sekta binafsi ambayo ndio muhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.

“Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya Baraza la Taifa la Biashara katika ngazi ya Taifa lakini katika ngazi ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili kupunguza kero za wafanya biashara na wawekezaji” Amesema Mhagama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akisisitiza jambo wakati alipokutana na wajumbe wa Baraza la Biashara Mkoa wa Kigoma, wakati alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, Katibu Tawala wa mkoa huo, Rashid Mchata na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa Kigoma, Rashid Mchata, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Baraza la Biashara la mkoa huo, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC), Andrew Mhina akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo mkoani Kigoma, wakati Waziri alipofika mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akiongea na Mjasiriamali aliyekuwa akihudumiwa katika kituo cha Biashara (One Stop Business Center) wilayani Kigoma, wakati alipofika mkoani Kigoma kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Biashara la Taifa.

RAIS DKT.MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA VYAMA SHIRIKI IKULU


RAIS MAGUFULI AREJESHA KIKOKOTOO CHA ZAMANI KWA WASTAAFU....SHANGWE ZALIPUKA IKULU

$
0
0
* Asema kustaafu sio dhambi bali ni heshima kwa Taifa
* Asisitiza hakuna sababu ya kuwasumbua wastaafu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amerejesha matumaini mapya kwa wafanyakazi na kuagiza wastaafu wote nchini walipwe kwa kutumia kikotoo cha zamani cha asilimia 50.

Pamoja na hilo amesema kuwa kustaafu si dhambi bali ni heshima kwa Taifa.
Ametoa uamuzi huo leo hii Desemba 28, mwaka 2018 katika kikao chake kilichohudhuriwa na wadau wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii ,wafanyakazi na viongozi wa ngazi mbalimbali wa mifuko hiyo.

Baada ya Rais kutangaza kutumika kwa kikotoo cha zamani ukumbi wa Ikulu uligeuka kuwa sehemu ya shangwe ambapo nyimbo za mshikamano kwa wafanyakazi zilianza kuimbwa huku Rais akiwaambia "Wafanyakazi Hoyee...wafanyakazi ni muhimu katika kipindi hiki na lazima wapewe stahiki zao na fomuka nzuri ni ile ya kuboresha maslahi ya watu na sio kuwa na fomula inayotesa wafanyakazi."

Akifafanua wakati anatoa uamuzi huo Rais Mafuli amesema kwamba "kustaafu si dhambi bali ni jambo la heshima. Anayestaafu anastahili kuheshimiwa na Taifa hili na hivyo hatakiwi kupata shida , kikokotoo kilichokuwa kinatumika huko nyuma kitumike katika kipindi hiki cha mpito hadi mwaka 2023," amesema Rais huku akishangiliwa.

Amefafanua kuwa kwa takwimu alizonazo ni kwamba kwa kipindi cha mpito ambacho ni kuanzia sasa hadi mwaka 2023 watakaostaafu ni wanachama 58, 000 na hao walipwe kwa kikotoo cha asilimia 50 huku akisisitiza mifuko yote ilipe kama ilivyokuwa inalipa awali.

Ameongeza kuwa Serikali iliyopo madarakani imeweka mfumo imara wa ukusanyaji kodi na miongoni mwa walipa kodi wazuri ni wafanyakazi na hivyo lazima waendelee kulipwa kama zamani ndani ya kipindi hicho cha mpito .

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUFANYIKA JANUARI 10 NA 11, 2019 ZANZIBAR

REPSSI WAANZA KAMPENI KUMBANA NA TATIZO LA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

$
0
0
Na Mwandishi ,Mkuranga. 

Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na msuala ya Kisaikolojia nchini (REPPS) limeanza kufanya kampeni ya kupambana na tatizo la mimba na ndoa za utotoni baada ya tafiti nyingi kuonyesha bado tatizo hilo ni kubwa.

Takwimu za Democratic and Health Survey , zinaonyesha kuwa tatizo la mimba za utotoni nchini limeongezeka kutoka asilimia 23 mwaka 2010 hadi kufikia 27 mwaka 2016/17, kutokana na ukosefu wa huduma pamoja na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19.

Mkurugenzi Mkazi wa Repps, Tanzania Edwick Mapalala amesema kampeni hiyo wanaiendesha kwa kuzungumza na jamii kwenye vijiwe, shambani, maeneo ya masomo na mikusanyiko yote ili kufikisha elimu ya namna ya kuwalea na kuwatunza watoto kimaadili.“Tatizo la mimba na ndoa za utotoni lipo kwenye jamii yenyewe, wazazi na walezi wakijua umuhimu wa malezi bora tatizo hili halitakuwepo kabisa,” amesema.

Amesema kama watoto wa kike wataendelea kukatisha masomo yao kwa mimba na ndoa itakuwa vigumu kufikia ndoto ya Tanzania yenye viwanda kwa sababu nguvu kazi inayoachwa njiani ni kubwa.“Mtoto wa kike akipata elimu na kusoma kwa bidii atatimiza ndoto yake na kuja kuchangia maendeleo kwenye taifa lake,” amesisitiza.

Amesema kupitia kampeni hiyo wanayoiendesha kwa ushirikiano na Shirika lililo chini ya Kanisa la Roman Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam (PASADA), vijana wameweza kupewa elimu ya afya ya uzazi na kujitambua itakayowasaidia kufikia ndoto zao.Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Parang’andam Felisian Magulu amesema kupitia kampeni hizo jamii inapata ufahamu wa madhara ya mimba kwa watoto na kujua namna ya kupambana na tatizo hilo.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkuranga, Dunia Mabufu alikiri kuwepo kwa kampeni za aina hiyo kunasaidia katika kubadilisha fikra za wengi zinazoendeshwa na mila na desturi kandamizi dhidi ya wasichana na wanawake.
Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni.
Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni
Baadhi ya vijana wa boda boda waliochangia mjadala wa kupinga ndoa na mimba ya utotoni.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA VYAMA WASHIRIKI NA WATENDAJI WAKUU WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongozi wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipoongea na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii  baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  (hawapo pichani) na viongozi wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongozi wengine waandamizi   katika picha ya pamoja na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018.

PICHA NA IKULU

MKUTANO WA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Baadhi ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari waliohudhuria katika Mkutano kuhusiana na Mabadiliko ya Teknolojia Ulioandaliwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)wakishirikiana na Tume ya Utangazaji Zanzibar.katika ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni mjini Unguja.
Mhandisi Mkuu wa Utoaji Leseni za Mawasiliano TCRA Andrew Kisaka (aliesimama)akitoa maelezo kuhusu Mabadiliko ya Teknolojia katika mkutano uliowashirikisha Wamiliki wa Vyombo vya Habari uliofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni mjini Unguja.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Khadija Bakari Juma akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano kuhusiana na Mabadiliko ya Teknolojia Ulioandaliwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)wakishirikiana na Tume ya Utangazaji Zanzibar.katika ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

VIONGOZI NA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIKATABA

$
0
0
Mtaalam Manunuzi,Bw. Jones Mapunda kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama, akitoa mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba kwenye ukumbi wa kitengo hicho.
Baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania na Watumishi wakiwa katika mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama.
Mtaalam Manunuzi,Bw. Jones Mapunda kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama, akitoa mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba kwenye ukumbi wa kitengo hicho kwa viongozi na Watumishi wa Mahakama. (Picha na Magreth Kinabo).
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama, Mhe. Zahra Maruma akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama.
Mtendaji wa Mahakama ya Rufaa, Bw. Solanus Nyimbi akifunga mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama.

MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI

$
0
0
*Aagiza wakae na wakandarasi wao na kupima kama watamaliza kazi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la tenki la maji la kutolea huduma katika ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba badala ya ukumbi wa Hazina kama alivyokuwa amepanga awali.

Akiwa Ihumwa, Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri wafike kwenye maeneo ya ujenzi wa ofisi zao, watathmini uwezo wa wakandarasi wanaojenga majengo ya wizara na pale watakapojiridhisha kuwa uwezo wao ni mdogo, wawabadilishe mara moja.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Desemba 28, 2018) akiwa kwenye kikao cha kazi (site meeting) na mawaziri 15 na manaibu mawaziri katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.“Mawaziri mliopo na makatibu wakuu wote kaeni na wakandarasi wenu hapa site ili waeleze kazi hii itakamilishwa lini. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi hii inakamilishwa kwa wakati,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa mrejesho Mawaziri juu ya changamoto alizokutana nazo jana alipofanya ukaguzi wa ujenzi kwa kila wizara. “Nataka Mawaziri ambao ofisi zao zinajengwa wa watu wa Mzinga, wakae nao na kutathmini uwezo wao na kama mtaona hawawezi, mkabidhi kwa mkandarasi mwingine,” amesema Waziri Mkuu.

Amewataka wakandarasi wahakikishe wanaongeza idadi ya vibarua ili kazi hiyo iweze kwenda haraka. “Wizara iliyofanya vizuri kuliko zote ni ya Utumishi, wao wako hatua nzuri. Kwa maana ya uchapaji kazi, eneo nililokuta lina wafanyakazi wengi ni magereza,” amesema.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipowasili kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma, unapojengwa Mji wa Serikali kukutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu, Desemba 28, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine  Mahiga, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini  Dodoma unapojengwa mji wa Serikali, Desemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa Mji wa Serikali, Desemba 28, 2018.  Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa mji wa serikali, Desemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
 

BENDI YA UBUNTU TRADITIONAL KUTUWAKILISHA TAMASHA LA KIMATIFA NCHINI NIGERIA

$
0
0
Mwandishi Wetu, Calabar

Mnenguaji nyota wa muziki wa dansi nchini Hassan Mussa 'Super Nyamwela'leo anatarajia kuliongoza kundi lake binafsi la Ubuntu (Ubuntu Tradional Band) katika tamasha la kimataifa la utamaduni litakalofanyika nchini Nigeria katika mji wa Calabar nje kidogo ya jiji la Abuja.

Hii ni mara ya pili kwa Nyamwela na bendi yake ya Ubuntu kushiriki tamasha hilo ambalo linashirikisha nchi zaidi ya 60 duniani.

Kwa Tanzania ni Ubuntu pekee ndiyo imepata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka kwa udhamini wa serikali ya Nigeria ambayo imekuwa ikilitumia kutangaza utalii wa nchi yake.

Tangu kuwasili kwa Ubuntu mjini Calabar, hofu imeanza kutanda kwa makundi mengine wapinzani wake ambayo mwaka jana yalishindwa kufua dafu mbele ya Nyamwela na wenzake.


Tamasha hilo lilianza rasmi Desemba 4 mwaka huu na linatarajia kufikia tamati Januari 4 mwaka 2019.
Wasanii wa Bendi ya Utamaduni ya Ubuntu (Ubuntu Traditional Band), ikiongozwa na Hassan Mussa maarufu Super Nyamwela, katika picha ya pamoja wakijiandaa kutumbuiza katika Tamasha la Kimataifa (Calabar Carnival Festival) linalofanyika  Mjini Calabar, nchini Nigeria jana. Picha na Esther Mbussi.

WAITARA AZITAKA HALMASHAURI ZOTE KUTEKELEZA MPANGO WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI NCHI NZIMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara amezitaka Halmashauri zote kutekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi nchi nzima kwenye Halmashauri zao bila ya kutumia kisingizio cha ukosefu wa bajeti za kufanya vikao vinavyohusu utoaji wa majina ya mitaa 

“Suala la gharama halipo, tumieni vikao vyenu vya kawaida, vya kisheria kutaja majina ya mitaa, suala la anwani za makazi na postikodi iwe ajenda mahususi ya ulinzi na usalama”, amefafanua Waitara 

“Wakurugenzi wote wa Halmashauri zote nchi nzima waliopo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI wahakikishe kwamba wanatoa maelekezo mahususi kwa watendaji wote na kuhakikisha kuwa wanatoa majina ya mitaa,” amesema Waitara. Pia amewaelekeza Makatibu Tawala wote Tanzania Bara wahakikishe Halmashauri zote zinatekeleza mpango wa anwani za makazi na postikodi

Waitara ameongeza kuwa mpango huu unatuwezesha kujitambua na kuwatambua watu wetu wanakoishi, na nini kilichowaleta eneo hilo kama ni biashara, uwekezaji na ni muhimu kwa ulinzi na usalama wa raia. Pia amesema kuwa suala la anwani za makazi na postikodi litawasaidia viongozi wao wenyewe kuwatambua wananchi, kuwezesha ukusanyaji wa kodi na kufikisha huduma za Serikali kwa wananchi

“Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anataka watanzania walipe kodi, jambo hili likitekelezwa, watanzania watalipa kodi na mpango huu wa kuwatambua wananchi utasaidia kuongeza mapato ambayo yataleta maendeleo ya taifa letu na kujenga miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu,” amesema Waitara.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mwita Waitara wakiwa wanatoka kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema (hayupo pichani) wakati wa ziara yao wilayani humo ya utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi

 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mwita Waitara akizungumza na viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Sengerema na Buchosa (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi wakiwa Nyehunge, Mwanza. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi na wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole

 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Sengerema na Buchosa (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu utekelezaji wa mpango wa anwani za makazi na postikodi yaliyofanyika Nyehunge, Mwanza. Wa nne kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mwita Waitara na pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi

 Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mwita Waitara (wa tatu kushoto) kuhusu kituo cha telesenta wakati wa ziara yao Wilayani humo

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi James Kilaba akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mwita Waitara (wa pili kushoto) kuhusu kituo cha telesenta wakati wa ziara yao wilayani Sengerema.  Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Kipole.

MKAZI WA MBEYA AJISHINDIA MIL 32/- BAADA YAKUBASHIRI MECHI 12 KATI YA 13 ZA JACKPOT, SPORTPESA

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 28/12/2018

Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images