Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

Serikali Imedhamiria Kuwezesha Vijana kushiriki kilimo Biashara-Waziri Mhagama

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amesema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwezesha vijana kiuchumi kupitia kilimo biashara ili kuchochea ongezeko la ajira na kipato chao. 

Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, tayari wilayani Kigoma wameanza kutekeleza Mradi unaolenga kuwezesha vijana kushiriki katika shughuli za uchumi kupitia mafunzo ya ujuzi na ujasiriamali kwenye kilimo na ufugaji.

Akiongea katika ziara yake mkoani Kigoma wakati wa kukagua shughuli za utekelezaji za Baraza la Taifa la Biashara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amefafanua kuwa Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, wameanza utekekezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na chuo cha Maendeleo Kihinga.

“Nitoe wito watendaji wa Halmashauri na ngazi ya mkoa wa Kigoma waendelee kuwaunga mkono vijana hawa wanao shiriki katika Mradi huu wa Kilimo Biashara, na nawataka mtambue haya yote yanafanyika kwa sababu ya jitihada zinazofanywa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo ufadhili wa Mradi huu kutoka Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, unaunga jitihada zake za kuwezesha vijana” Amesisitiza Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akizindua Mradi wa Kuwawezesha Vijana Kushiriki katika Kilimo Biashara, Manispaa ya Kigoma, Mradi huo unalenga kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mafunzo ya ujuzi na ujasiriamali kwenye kilimo na ufugaji. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Kuwawezesha Vijana Kushiriki katika Kilimo Biashara, Manispaa ya Kigoma, Mradi huo unalenga kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mafunzo ya ujuzi na ujasiriamali kwenye kilimo na ufugaji. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Masuala ya Majadiliano ya Sekta ya Umma na Binafsi), Andrew Mhina juu ya ujenzi wa mabwawa ya Samaki kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuwawezesha Vijana Kushiriki katika Kilimo Biashara, Manispaa ya Kigoma, Mradi huo unalenga kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mafunzo ya ujuzi na ujasiriamali kwenye kilimo na ufugaji. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Masuala ya Majadiliano ya Sekta ya Umma na Binafsi), Andrew Mhina juu ya ukarabati wa mabanda ya kuku kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuwawezesha Vijana Kushiriki katika Kilimo Biashara, Manispaa ya Kigoma, Mradi huo unalenga kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mafunzo ya ujuzi na ujasiriamali kwenye kilimo na ufugaji. 


Shule tatu Kibamba zakabidhiwa visima

0
0
Joseph Zablon

Shirika lisilo la kiserikali la Time to Help limekabidhi visima vitatu kwa shule tofauti za wilaya mpya ya Kibamba, jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo kusaidia shule za msingi na sekondari nchini katika kukabili changamoto tofauti.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa shule za sekondari Kibwegere, Kibweheri na shule za msingi Kibwegere, leo Mkuu wa tasisi hiyo Kubilaty Talu alisema wametoa msaada huo baada ya kuombwa kufanya hivyo.

Alisema tasisi hiyo imelenga kuzisaidia shule mbalimbali nchini kukabili changamoto ya mahitaji ya maji na visima hivyo anaamini vitabadili mazingira na kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hizo tatu ambao pia walipewa zawadi za madaftari.awali Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya alisema visima hivyo vitasaidia mengi ikiwa ni pamoja na kulinda afya za watoto kutokana na uhaba wa maji hivyo pia kuwaepusha na magonjwa yanayotokana na uhaba wa maji safi na salama.

Katika risala ya wanafunzi wa sule hiyo hizo ambayo iliwasilishwa kwa mtindo wa ngonjera, wanafunzi wa shule hizo waliomba msaada wa vyumba zaidi vya madarasa kutokana na uhaba uliopo na wameshukuru kupata huduma ya maji.Walisema ukosefu wa maji safi na salama ulisababisha baadhi ya wanafunzi kuugua magonjwa ya matumbo mara kwa mara kutokana na kutumia maji ya kunywa yasiyo safi wala salama. 
Mlezi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu akifungua bomba la maji jana, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari Kibwegere ambacho kimejengwa na taasisi hiyo, Kibamba, Dar es Salaam.
Mlezi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu akifungua bomba la maji jana, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari Kibwegere ambacho kimejengwa na taasisi hiyo, Kibamba, Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kibwegere (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibweheri, Alexandra Ngonyani na Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya, wakimshukuru mlezi wa taasisi ya Time to help, Remziye Talu (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kisima kilichojengwa na taasisi hiyo katika shule ya sekondari Kibwegere
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibwegere wakipewa madaftari na zawadi zingine kutoka kwa wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help mara baada ya uzinduzi wa kisima cha maji katika Shule ya Sekondari Kibwegere, jana. Taasisi hiyo imekabidhi visima vya maji vitatu katika shule za sekondari Kibweheri , Kibwegere shule ya msingi Kibwegere.

FAIDA YA MAADHIMISHO NA MWENYEZI MUNGU

0
0


Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt. Barnabas Mtokambali amesema Mwenyezi Mungu anapenda maadhimisho kwa kuwa ni sehemu ya kujifunza, kumsifu, kujenga ushirika na kumtolea shukran. Dkt. Mtokambali amebainisha hayo Mjini Dodoma, kwenye sherehe za maadhimisho ya mchungaji Vangast Salum wa kanisa la TAG, kwa kutimiza miaka 40 ya wokovu na 36 ya huduma na kuweka wakfu kitabu.
Amesema moja ya sababu za maadhimisho ni kujifunza, akitolea mfano mchungaji Vangast Salum, amepitia hatua mbalimbali za maisha na kiuchungaji na kwamba maadhimisho pia yanajenga ushirika zaidi na Mwenyezi Mungu kwa kuwaleta watu karibu.

Kiongozi huyo wa juu wa kanisa la TAG Tanzania amesema kuwa sababu ya tatu ya maadhimisho ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa yote aliyoyafanya juu ya maisha ya mchungaji Vangast Salum kwa kipindi cha miaka 40 ya wokovu, na kumtaka kutoa shukran za kumsifu Mwenyezi Mungu.
Wakati huo huo Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt. Barnabas Mtokambali amepata fursa ya kuzindua vitabu 500 vya mafundisho ya dini na uzinduzi wa jengo la darasa na Ofisi ya mchungaji wa kanisa hilo eneo la Area D Mjini Dodoma.

MICHUZI TV: Mufti mkuu wa Tanzania apongeza jitihada za Rais Dkt Magufuli katika kuijenga nchi

MICHUZI TV: SHEKHE KIPOZEO ASEMA RAIS MAGUFULI ANASTAHILI SIFA NA KUOMBEWA DUA

HIZI NDIZO SALAMU ZA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU KWA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2019

MICHUZI TV: VIJANA WALIVYOOKOA BASI LA MWENDO KASI UBUNGO LEO

DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO

0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amezungumzia ziara ya kikazi ambayo imefanywa na Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa wilayani humo kwa lengo la kuangalia hali ya kilimo hasa kipindi hiki cha msimu wa kilimo kwa mwaka 2018 /2019.

Akizungumza na Michuzi Blog , Mkuu wa Wilaya Sophia Kizigo amesema Bashungwa akiwa kwenye wilaya hiyo alipata nafasi ya kuzungumza na wakulima kuhusu hali ya kilimo kwa mwaka huu, pia alipata nafasi ya kuangalia iwapo mbolea imefika kwa wakati au laa.

Kizigo amesema kwenye suala la mbolea, Naibu Waziri wa Kilimo alipata nafasi ya kwenda kwa wasambazaji wakubwa wa mbolea ambapo alikutambolea imefika kwa wakati na ipo ya kutosha na baada ya hapo akaenda kwawakulima ambako nako alikuta mbolea haina tatizo.

"Hata hivyo kwa wakulima wa tumbaku wao wamenunua na kuanza kuitumia mbolea bila tatizo, ila kwa wakulima wa mahindi wengi wao licha ya mbolea kufika kwa wakati wameshindwa kuinunua kutokana na changamoto yakifedha.Sababu kubwa ya kutokuwa na fedha ya kununulia imetokana na beiya mahindi kwa msimu uliopita kuwa chini kwani kilo ya mahindi ilifikia Sh.200.

"Hivyo wengi hawajanunua ingawa tayari wameshapanda mahindi,ila kinachoonekana watanunua mbolea kwa ajili ya kukuzia mahindi.Tunafahamu Wilaya ya Namtumbo inaongoza kwa kilimo na hasacha mahindi ambayo mengi yanatoka wilayani kwetu,"amesema Mkuu waWilaya Kizigo wakati anaelezea ziara hiyo ambayo imefanywa na Naibu Waziri wa Kilimo Bashungwa.Pia amesema akiwa humo amepata nafasi ya kutembelea wakulima kwabaadhi ya kata na kujionea hari ya wakulima hao katika kuandaa mashamba yao ambapo wengi wao wameshapanda kwani tayari msimu wa kilimoulishaanza ndani ya wilaya hiyo.

Akizungumzia maandalizi ya kilimo wilayani humo ,Kizigo amesema amefurahishwa na juhudi ambazo zinafanywa na wakulima katika kuhakikisha wanautumia vema msimu huu kwa kuandaa mashamba mapemana kwamba wengi wao wameshapanda mbegu kwani msimu wa kilimo umeshaanza katika wilaya hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo akiwa ameambatana na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kwa pamoja wakitembelea mashamba ya mahindi katika vijiji mbalimbali kikiwemo kijiji cha Namanguli,kata ya Luchili wilayani Namtumbo.
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akimsikiliza mmoja wa wakulima alipokuwa akizungumza nae kuhusu suala la upatikanaji wa mbolea,masoko na namna kilimo cha mahindi kinavyokwenda,kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh Sophia Kizigo.
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akimsikiliza Afisa Kilimo wa Wilaya alipokuwa akizungumza nae kuhusu namna ya wakulima wa Mahindi wananvyoandaa mashamba yao na kwa kiwango gani wanavuna mazao yao,na kwamba Mkulima anatakiwa alime heka ngapi ili asipate hasara,ambapo Afisa huyo alieleza kuwa Mkulima ili asipate hasara katika kilimo chake anapaswa kulima heka nne ili apate faida.
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa pichani kulia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh Kizigo na wadau wengine wakikagua Shamba la mahindi katika kijiji cha Suluti kata ya Namtumbo.
Ukaguzi wa shamba la tumbaku katika kijiji cha Suluti kata ya Namtumbo
Wananchi walisimamisha msafara wa Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa katika kata ya Luchili kijiji cha Namanguli wakitaka wasikilizwe kero zao.
Ukaguzi wa maduka ya pembejeo kuangalia mwenendo wa biashara na bei elekezi kama inazingatiwa ulifanyika pia.

JUMLA YA WAZEE 264 WAPATIWA BIMA YA AFYA MERU

0
0
Na. Vero Ignatus Arusha

Jumla ya Wazee 264 katika Wilaya ya Meru mkoani Arusha wamepatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupata huduma za afya katika vituo mbali mbali vya afya hivyo kuboresha ustawi wa maisha ya wazee.

Akikabidhi Bima hizo kwa wazee wanaohudumiwa na kituo cha Huduma ya Wazee Sakila kilichopo wilayani hapo ,Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere alisema kuwa kadi hizo zitawawezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima kwa gharama nafuu.

Elizabeth Alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuwekeza kwenye afya za wazee kwani ni kundi muhimu katika jamii ambalo linapaswa kupawa kipaumbele kwenye huduma za kijamii.. "Ni muhimu kutunza kadi hizi muweze kufika nazo na kupewa matibabu ,tunawashukuru wadau kwa kujitoa kuhudumia wazee kwani serikali haiwezi kufanya kila kitu"

Alisema Mratibu wa kituo cha huduma ya wazee sakila, Hamphrey Mafie alisema kuwa wazee hao wanapaswa kutunza kadi hizo zitazowawezesha kupata huduma za afya bure bila kulipia . Mafie anaeleza kuwa shirika la Dorcas International limewawezesha wazee kupata bima za matibabu pamoja na zawadi za sikukuu za krismas na Mwaka mpaya ambapo wazee walipatiwa chakula,mavazi pamoja na mahitaji mengine .

Kwa Upande wake Mzee anayehudumiwa na kituo hicho Maria Solomon ameishukuru kituo hicho kwa kuwajali na kuwathamini kwani wazee hao walikua na changamoto ya matibabu kutokana na uwezo mdogo wa kifedha hivyo watapata fursa ya kutibiwa . 
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere akikabidhi Kadi ya Bima kwa Bi.Maria Solomon ,kadi hizo zimetolewa na Kituo cha Huduma ya Wazee Sakila

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Elizabeth Mohere akikabidhi Kadi ya Bima mmoja wa wazee kwenye kituo cha Huduma ya wazee Sakila .


UMEME UTATANDIKWA VIJIJI VYOTE JIMBONI KWANGU-MHE HASUNGA

0
0
Na Mathias Canal, Songwe

Serikali imesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (Rea).

Aidha, Serikali imetenga Sh1 trilioni kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa na nishati hiyo huku ikiendela na uwekaji wa umeme katika vijiji zaidi ya 13400.

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga amewahakikishia wananchi kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo hilo hivyo wananchi wanapaswa kuondoa wasiwasi na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Mhe Hasunga ameyasema hayo wakati wa mikutano yake katika kijiji cha Igale na Iyula A vilivyopo katika kata ya Iyula akiwa katika ziara ya kikazi jimboni humo iliyoanza juzi tarehe 22 Octoba 2018.Alisema kuwa upatikanaji wa umeme katika jimbo lake utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla wake.

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe wakifatilia mkutano wa Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Teknolojia ya mawasiliano ilivyowarahisishia wakulima upatikanaji mifuko ya PICS

0
0

Miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikirudisha nyuma maendeleo ya kilimo ni wadudu wanaobangua nafaka, pamoja na wakulima wengi kujikita katika upuliziaji dawa ya kuzuia wadudu hao bado haikuzuia wadudu kushambulia nafaka kavu kwa asilimia 100.

Kero hiyo ilisababisha wakulima kulazimika kuuza nafaka hizo kwa bei ya hasara ili mradi kukwepa usumbufu wa kupuliza dawa na wengine kuuza nafaka hizo kwa bei ya kupangiwa na wachuuzi wakihofia zitakapokaa muda mrefu zitapoteza ubora wake wa awali.

Kero hiyo iliwasumbua wakulima wengi katika nchi za Kiafrika, kabla ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Purdue cha Marekani ambacho kilifanya utafiti katika nchi za Afrika Magharibi na kisha kuanzisha teknolojia mpya ya kuhifadhi nafaka kwa kutumia mifuko maalumu ya tabaka tatu kwenye nchi ya Cameroon.

Wasomi wa chuo hicho walitengeneza mifuko hiyo maalumu ya kuhifadhi nafaka iliyopewa jina la Purdue Improved Crops Storage (PICS) ambayo ni mahususi kwa kuhifadhi nafaka kavu bila kutumia kemikali.“Tanzania teknolojia ya PICS ilianza mwaka 2014 ambapo kiwanda cha PEE PEE Tanzania Limited (TTTL) cha Tanga kilipata kibali cha kutengeneza mifuko hiyo.

“Wakati unaingia nchini, tayari mradi huo ulikuwa umeenea katika nchi za Afrika Magharibi na Mashariki ya mbali ukifanyika chini ya ufadhili wa Taasisi ya Melinda and Gates Foundation,” anasema meneja mradi wa PICS Tanzania, Ladislaus Ngingo.

MATUMIZI YA MIFUKO YA PICS

Ngingo anasema tofauti ya mifuko ya PICS na mingine ya salfeti ni kwamba ile ya PICS imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuhifadhia nafaka kavu bila kubanguliwa na wadudu kwa zaidi ya miezi sita na mkulima hatohitaji kupulizia dawa nafaka atakazohifadhi kwenye mifuko hiyo.

“Katika kipindi chote hicho nafaka zitaendelea kubaki katika ubora ule ule kama kwamba ndiyo zimetolewa shambani muda huo, mifuko hii ina nailoni mbili ndani ambazo ni nzito kila moja ina ‘macron’ 80 ambazo zina upekee katika kuhifadhi nafaka kavu,” anasema Ngingo.

Familiya kijijini Mnenia, Wilayani Kondoa ikitoa ushuhuda wa usalama wa mahindi yao. Yalihifadhiwa miaka miwili, na mifuko ya PICS.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Introducing "Basi" Official Audio by Hype Burton

Captain Aliyetoroka na NDEGE Kenya Apewa Mamilioni na JPM!

Dkt.BASHIRU AZINDUA KAMPENI YA KUTOKOMEZA UDUMAVU WA WATOTO KAGERA

0
0
Na Abdullatif  Yunus wa Globu ya Jamii, Kagera

Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally ameanzisha kampeni hiyo ya kutokomeza Udumavu wa watoto Mkoani Kagera, Desemba 26 wakati wa  ukaguzi wa kiwanda cha kuchakata Nyanya  ili kupata "Tomato sauce" Kiitwacho VICTOLIA EDIBLES LTD    Kilichopo eneo la Kafunjo Kata Butelankuzi Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.


Akiwa katika ukaguzi huo katibu Mkuu wa CCM Dr.Bashiru Ally amewaaka viongozi wote  wa Chama  na serikali kuendeleza kampeni hii ili kupunguza udumavu wa watoto Mkoa wa Kagera "Kagera ni Mkoa wenye  vyakula vingi vya asili na ardhi yenye rutuba ya kustawisha mazao mengi kama Ndizi ,Mahindi, Mihogo hivyo haipaswi kuwa na ongezeko kubwa la watoto wadumavu "amesema Katibu Mkuu wa CCM Dr.Bashiru Ally Mkuu 



Aidha amewasisitiza viongozi wa dini zote kushirikiana kwa pamoja kuelimisha Watanzania namna yakupata lishe bora ili kutokomeza Udumavu wa watoto hasa Mkoa wa Kagera.

Ziara hiyo fupi ya Katibu Mkuu wa CCM Dr.Bashiru Ally ameongozana na Mbunge wa CCM  Bukoba Vijijini na Katibu wa wabunge wa Chama hicho  Mh.Jasson Rweikiza (MB), Ziara hiyo imesababisha Katibu kuzuru eneo la Kanazi na  kukagua eneo ambapo kitajengwa Kituo cha Afya ya Wilaya ya Bukoba.

Akizungumza mbele ya wananchi amewataka Wanakagera  na Watanzania wote kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli kwa juhudi anazozifanya za kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa kati na kuendeleza kampeni ya Tanzania ya Viwanda

 Mh.Jasson Rweikiza (MB), Mkurugenzi wa Kiwanda cha Victoria Edibles Ltd akitoa maelezo ya mitambo, pembeni ni Mh. Dk. Bashiru Ally Katibu wa CCM - Taifa
 Sehemu ya kiwanda Cha kuchakata Nyanya Victoria Edibles ltd kilichopo Kafunjo Bukoba, Kagera.
Mh. Bashiru, na Mh. Rweikiza wakikagua eneo ambapo Hospitali ya Wilaya ya Bukoba inatarajiwa Kujengwa

MAMBO YA UBUNGO BUS TERMIBAL MPYA, WAHI DUKA MAPEMA

0
0
East Afrika Commercial and Logistics Center ni kituo cha biashara kinajengwa eneo la Ubungo bus terninal kuanzia Januari 19 hadi Juni 20, 2019. Kutakuwa na maduka yapatayo 2600 - 2800 ambayo yatauzwa kuanzia USD 50'000 hadi 100'000 na unakuwa na umiliki wa miaka30. Biashara za aina  zote zitapatikana. huduma za benk na ofisi za serikali TRA. uhamiaji n.k.yaani a ONE STOP CENTER. Kwa maelezo fika Ubungo plaza ground floor at main entrance utakuta model ya jengo na ofisi za EA Comercial and  Logistics Center
...



JENERALI MABEYO ATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI KUHUBIRI AMANI

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea kuhubiri amani ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na mshikamano. 
Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama na Serikali, ambapo alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo kwa Taifa lolote duniani. 
"Suala la amani na utulivu ni la msingi sana katika nchi yetu, kwa vile kila mwananchi ana dini yake tunaamini kuwa viongozi wa dini zote kwa kuwa wanasikilizwa sana  na waumini  wakiweka msisitizo katika suala la amani, amani itatawala na kutakuwa na utulivu" 
“Utulivu huu tunauhitaji sana ili tupate maendeleo,  kama  viongozi wetu wa kisiasa wanavyosisitiza kuwa tudumishe amani na utulivu  tupate maendeleo, bila utulivu watu wakiwa wanahaingaika hakuna maendeleo kwa sababu hakuna shughuli mtu anaweza kufanya kama hana amani na utulivu, hivyo hataweza pia kuleta maendeleo yake, familia, jamii na Taifa kwa ujumla" alisema Jenerali Mabeyo 
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema vitendo vingi vya uvunjifu wa amani na uhalifu ikiwemo ukataji wa mapanga na mauaji ya vikongwe na yanachangiwa na watu kukosa hofu ya Mungu; hivyo nyumba za ibada(makanisa na misikiti) zinapojengwa kwa wingi zitakuwa msaada mkubwa sana kwa watu kuwa na hofu ya Mungu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema jamii inayoamini uwepo wa Mungu haiwezi kuwa na vitendo vya kisasi, kukatana mapanga na mauaji ya vikongwe huku akiwaasa Watanzania kukaa kwa amani na upendo bila kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha amani. 
Akibariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu amewataka Watanzania kupendana na kuacha roho ya ubinafsi na visasi. 
Aidha, Askofu Sangu ametoa wito kwa viongozi na waumini kufanya nyumba za ibada zibaki nyumba za sala kama yanenavyo maandiko matakatifu na kamwe zisitumike kama majukwaa la wanasiasa. 
" Palipo na msamaha pana umoja, uelewano na usawa lakini palipo na  kisasi hapana maendeleo; nyumba ya ibada isitumike kama jukwaa la Wanasiasa alisisitiza Muhashamu Askofu Sangu.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jeneral Venance Mabeyo akipokea mkono wa Heri ya Krismasi kutoka kwa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
 Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu akimshuhudia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati akitia saini kama shahidi katika Hati ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya, katika ibada ya kubariki na kutabaruku  kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakiwa katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
 Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo(kulia) wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na viongozi wengine wakiwa na katika picha ya pamoja na watoto wenye ualbino wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Lamadi, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.

MICHUZI TV: PATCHO MWAMBA afunguka kubaniwa kwa muziki wa Dansi

MICHUZI TV: PATCHO MWAMBA afunguka kwa kubaniwa muziki wa Dansi, Ashukuru Mwakyembe kuingilia kati

Fastjet inayumbishwa na madeni ya zaidi ya Bilioni Sita - TCAA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKA  la Ndege la Fastjet linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni Sita na Mamlaka zinazotoa huduma ya usafiri wa Anga pamoja na Wasambazaji, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)  Hamza Johari  amesema.
Bw. Johari ameweka bayana kuwa shirika la Fastjet lina matatizo makubwa yanayofanya lisiendelee kutoa huduma ya  usafiri wa anga. Amesema kuwa walivyotoa siku 28 ya kufunga huduma za shirika hilo walikuwa wamejiridhisha kutokana na madeni ya shirika hilo pamoja na kumiliki Ndege ambayo haina uhakika wa kufanya safari za anga.

Johari amesema kuwa shirika hilo lilikuwa linamilikiwa na Mwingereza na baada ya kuondoka wazawa wakanunua hisa akiwemo Mwenyekiti Mtendaji wa shirika hilo Laurence Masha ambao walianz kuanza kuendesha shirika hilo. Aidha ameeleza kuwa baada ya kupata matatizo hayo Meneja Usimamizi wa Ndege hizo alijiuzuru na ndiye aliyekuwa  anajua masuala ya Ndege hivyo Mamlaka haiwezi kuruhusu Ndege kuruka bila kuwepo kwa mtu huyo.
Aidha amesema kuwa taarifa ya kuleta Ndege zilizotolewa na Mwenyekiti Mtendaji Laurence Masha Desemba 22 mamlaka ilikuwa haina taarifa badala yake taarifa imewafikia Desemba 24 na bado wanaifanyia kazi. Pia amesema kuwa moja ya masharti waliyowapatia ilikuwa ni kupatikana kwa Meneja mwenye utaalamu wa masuala ya Anga ambapo Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet Laurence Masha alimteua Meneja wa Shirika hilo Laurence Masha kuwa Meneja usimamizi.

Johari amesema sharti lingine ilikuwa ni kuandika andiko la biashara ikiwa upatikanaji wa fedha za uendeshaji wa Shirika. Mkurugenzi Mkuu huyo wa TCAA amesema kuwa kuzuia kwa shirika hilo kufanya biashara ya usafiri wa Anga ni kuipendelea ATCL ni maneno tu kinachotakiwa kwa kila shirika kufuata sheria zilizowekwa kwa ajili ya Usalama wa abiria wanaotumia usafiri wa anga.
"Hakuna ugomvi shirika la Fastjet kufuata matakwa ya sheria kwa maslahi mapana ya abiria pamoja na kulipa madeni" amesema Johari
.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)  Hamza Johari  

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live


Latest Images