Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde wakibadilishana taarifa ya mkutano kati ya Tanzania na Uganda uliojadili namna ya kuimarisha biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara na visivyokuwa vya kiforodha uliofanyika Mutukula, Uganda tarehe 19 Desemba 2018.




Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda
20 Desemba 2018

MAKALA MAALUM- MIAKA MITATU YA RAIS MAGUFULI MADARAKANI

VETA yaanzisha ushirikiano na Chuo cha Henan-China

$
0
0
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano kati yake na Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo lengo la kuboresha utoaji wa mafunzo kwa njia ya kutembeleana na kubadilishana ujuzi na maarifa kwa walimu na wanafunzi na shughuli zingine za kitaaluma.

Makubaliano hayo ya awali yaliafikiwa na kusainiwa leo (tarehe 20 Desemba 2018) kati ya Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu kwa upande mmoja na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dr. Pancras Bujulu kwa upande mwingine na kwamba yatafuatiwa na utiaji saini wa Waraka wa Makubaliano (MoU) siku za mbeleni.

Utiaji saini wa makubaliano ya awali uishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board), Peter Maduki, wawakilishi wa Chuo cha Henan na Wajumbe wa Menejimenti ya VETA.

VETA ina nia ya kuimarisha mafunzo katika sekta ya kilimo na miongoni mwa malengo yake ni kukiimarisha na kukiboresha chuo cha VETA Kihonda ili kiweze kubobea na kuwa kituo bora cha mfano katika mafunzo ya ufundi stadi kwenye sekta ya kilimo.

Kabla ya kusaini makubaliano, ujumbe wa watu sita kutoka Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo ukiwahusisha watendaji wakuu na wataalam mbalimbali umekuwepo nchini tangu Jumanne tarehe 18 Desemba 2018 ambapo ulifanya majadiliano na Menejimenti ya VETA Makao Makuu, ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt Pancras Bujulu na Jumatano, tarehe 19 Desemba 2018 ulitembelea ofisi ya VETA Kanda ya Mashariki, kisha chuo cha VETA Kihonda na kujionea karakana, mashine na vifaa mbalimbali vinavyotumika kufundishia fani ya Ufundi wa Zana za Kilimo (Agro-mechanics), mafunzo ambayo yanagusa sekta ya kilimo ambayo ndio mkondo wa chuo cha Henan.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu (wa pili kutoka kulia, waliokaa) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu (wa pili kutoka kushoto,waliokaa) wakisaini makubaliano ya awali ya ushirikiano kati yao. Wa kwanza kulia, waliokaa ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na wa kwanza kushoto waliokaa naye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan, Chen Yueying.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Pancras Bujulu (wa pili kutoka kulia, mstari wa mbele) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan cha Ufundi Stadi wa Kilimo, Profesa Dou Ruimu (wa pili kutoka kushoto, mstari wa mbele) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya awali ya ushirikiano kati yao. Wa kwanza kulia, mstari wa mbele ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Noel Mbonde na wa kwanza kushoto, mstari wa mbele naye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Henan, Chen Yueying. Wengine ni wajumbe wa Menejimenti ya VETA na Wawakilishi wa chuo cha Henan.

DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo amewaonya wananchi  wanaowashawishi wenzao kukataa ardhi ya vijiji vyao isipimwe na kupangiwa matumizi bora ya ardhi kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria .

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Hati ya Kimila ya maeneo ya malisho kwa uongozi wa Kijiji cha Endesh Kata ya Baray jana amesema utaratibu wa kupima na kupanga matumizi bora ya ardhi una baraka za serikali na unalenga kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji,wakulima na wawekezaji.

‘Serikali haitawaonea huruma wanaokwamisha juhudi za serikali kuhakikisha tunakua na vijiji vyenye ramani zinazotambulika kisheria na ambazo wananchi wamekubaliana namna ya matumizi ya ardhi katika shughuli za maendeleo,”amesema Mahongo

 Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalam wa ardhi wanaofika katika maeneo yao kwaajili ya kupima na kupanga matumizi bora ya ardhi kwamba ni jambo zuri ambalo lina faida kubwa katika kujipangia mipango ya maendeleo.
 Wafugaji wa jamii ya Wabarbaig katika Kijiji cha Endesh Kata ya Baray wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha wakiimba nyimbo za asili wakati wa hafla ya kukabidhiwa hati ya kimila yenye mpango wa matumizi bora ya ardhi na nyanda za malisho  iliyoandaliwa na Ujamaa Community Resouce Team(UCRT).
 Mkuu wa wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha,Theresia Mahongo(kulia) akiwa ameungana na Wanawake wa  jamii ya kifugaji ya Wabarbaig katika Kijiji cha Endesh Kata ya Baray  wakiimba nyimbo za asili.
 Mkuu wa wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha,Theresia Mahongo(kulia) akimkabidhi Hati ya Kimila Mwenyekiti wa Kijiji cha Endesh Kata ya Baray ,Geway Nanagi kutoka  jamii  ya kifugaji ya Wabarbaig  wakati wa hafla ya kukabidhiwa hati ya mpango wa matumizi bora ya ardhi na nyanda za malisho  iliyoandaliwa na Ujamaa Community Resouce Team(UCRT).
Mzee wa jamii  ya kifugaji ya Wabarbaig katika Kijiji cha Endesh Kata ya Baray wilaya ya Karatu,mkoa wa Arusha,Gidaulanda Marakwa akifurahia Hati ya Kimila iliyoandaliwa na taasisi ya Ujamaa Community Resources Team.Picha na Filbert Rweyemamu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZAZI WATAKIWA KUWA JIRANI NA WATOTO WAO ILI WASIJIINGIZE KATIKA MAOVU

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
WAZAZI nchini wametakiwa kuwa jirani na watoto wao jambo litakalosaidia kupunguza ndoa za utoto na kujiingiza katika vitendo viovu kama matumizi ya dawa za kulevya.

`Mwito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Temeke, Faisal Hassan wakati wa hafla ya kuzindua Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi.

" Mnajua wazazi ndio wanaochangia asilimia 70 ya watoto wao kujiingiza katika vitendo visivyofaa zikiwemo ndoa za utotoni kwa kuwa wao ndio walezi wa kwanza wa watoto hao" alisema Hassan.

Alisema katika suala la malezi ya watoto si la serikali peke yake bali ni la kila mmoja wetu hivyo uanzishwaji wa taasisi hiyo katika Kata ya Temeke ni hatua kubwa ya maendeleo pia itakuwa ni mkombozi kwa vijana kutokana na shughuli zake kujikita zaidi kusaidia vijana na kuwa Temeke ina changamoto kubwa kwa vijana kujihusisha na vitendo viovu.
 Diwani wa Kata ya Temeke,Faisal Hassan (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Hidaya Shomvi na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Matumbi, Khatibu Lindi.
 Baadhi ya watoto wanaosaidiwa na taasisi hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Msanii Hemed Mwelevu akitoa burudani wakati wa hafla ya uzindua Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam
 Bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa taasisi hiyo.
 Msanii Happynes Starley, akitoa burudani wakati wa hafla ya kuzindua Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu mpya wa Zanzibar wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT), Tunu Juma Kondo, amesema atahitumikia jumuiya hiyo kwa hekima na busara ili kutimiza kwa vitendo malengo ya CCM na Jumuiya hiyo. Amesema baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ametambua kuwa siasa ni hekima na busara hivyo katika utendaji wake atafanya kwa misingi hiyo kwa uadilifu mkubwa.

Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na wanajumuiya wa UWT katika ukumbi wa CCM kisiwandui,Naibu huyo alisema hakutarajia kushika nafasi hiyo na kwamba utaratibu wa chama ni mzuri wa kuwateua viongozi bila ya ubaguzi Katika maelezo yake Naibu huyo alisema CCM haina ubaguzi na kwamba inazingatia utendaji wa mtu na si vinginevyo akitoa mfano alisema kwa upande wake hakutarajia kuwa siku moja atapewa jukumu kama hilo.

"Nashukuru UWT kwa kuridhia jina langu lipelekwe katika uongozi wa juu wa chama hivyo sina budi kuwashukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM,Dk.Bashiru Ally,kamati ya Halmashauri Kuu kwa kuniamini na wameonesha imani kubwa kwangu,"alisema Naibu Katibu Mkuu huyo Tunu aliwataka wanajumuiya hiyo kumpa ushirikiano katika utendaji wake na amewataka wakumbuke kuwa siku za mbele kuna uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kwamba wao ndio wapiganaji hivyo wanapaswa kushirikiana.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM Zanzibar  Khadija Kabir mara baada ya kuwasili Zanzibar  kwa mara ya kwanza toka alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akifurahia na wanachama wa UWT katika mapokezi hayo.
  NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akizungumza na wanajumuiya wa UWT katika ukumbi wa CCM Kisiwandui

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Taasisi ya Uongozi na REPOA wazindua programu mpya ya kuisaidia serikali kuwezesha sera bora za kiuchumi

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmari akifungua warsha ya kujadili programu mpya ya utafiti itakayoisaidia serikali kutunga na kutekeleza sera bora za kiuchumi na kuwezesha mazingira bora ya kufanya biashara. Programu hii inataratibiwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na REPOA.
  Baadhi ya washiriki ya warsha waliohuduria kwa ajili ya kufanya tathmini ya maeneo yatakayolengwa katika programu hii ili kuweza kuja na mpango utakaoakisi kuboresha hali ya utawala wa kiuchumi nchini. Warsha hii ili wahusisha washirika hamsini kutoka katika idara za sera, utafiti na mipango serikalini, wizara, taasisi zake na hata kutoka sekta binafsi.
 Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Bi. Jacqueline Mneney Maleko akitoa mawazo yake kuhusu programu hiyo mpya inayoratibiwa na Taasisi ya Uongozi na REPOA wakati wa warsha ya kujadili programu mpya ya utafiti itakayoisaidia serikali kutunga na kutekeleza sera bora za kiuchumi na kuwezesha mazingira bora ya kufanya biashara.
 Afisa Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Ukusanyaji wa Fedha (TRA) Bw. Kailembo Yahya akichangia mada kwenye warsha ya kujadili programu mpya ya utafiti itakayoisaidia serikali kutunga na kutekeleza sera bora za kiuchumi na kuwezesha mazingira bora ya kufanya biashara.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa kutoa mapendekezo ya programu mpya itakayotoa ushauri kwa serikali kwenye kuboresha sera za kiuchumi na mazingira bora ya kufanya biashara.
   Sehemu ya washiriki ya warsha hiyo wakijadiliana kwenye makundi wakati wa warsha ya kujadili programu mpya ya utafiti itakayoisaidia serikali kutunga na kutekeleza sera bora za kiuchumi na kuwezesha mazingira bora ya kufanya biashara.
 Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmari akiteta jambo na Mbunge wa Igunga Dkt. Dalali Kafumu wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na REPOA. 

RAIS MAGUFULI AAGA MWILI WA MAREHEMU PROF. EGID BEATUS MBOFU MAKAMU ALIYEKUWA MKUU WA CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)

$
0
0
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akitia saini katika kitabu cha Maombelezo cha Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)  mara baada ya kuwasili Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18,2018 Nchini Afrika Kusini. 
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)  , Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akimpa pole mjane Joyce Chamhuro (Mke wa Marehemu) pamoja na familiya ya Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM), Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na Wafiwa na Waombolezaji wengine mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM), Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Wafanyakazi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) pamoja  na Waombolezaji wengine mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Profesa Egid Beatus Mbofu  aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)  , Tabata Wilaya ya Ilala nyumbani kwa marehemu, aliyefariki dunia Desemba 18, 2018 nchini Afrika Kusini.

 Picha na Ikulu.

MICHUZI TV: MAKAMU WA RAIS AJITAMBULISHA KAMA MLEZI WA CCM MKOA WA PWANI

MICHUZI TV: ANGALIA WALIOFUKUZWA UANACHAMA CCM WALIVYOOMBA RADHI HALMASHAURI KUU

TASWIRA MWANANA ZA JIJINI DAR LEO BAADA YA MVUA YA LEO

$
0
0

 Wananchi wa Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam wakiwa katika kituo cha mabasi cha Mbagala kikiwa kimejaa maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na mikoa ya Pwani (Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Wananchi wakikatiza kwenye maji  yaliyojaa kituo cha mabasi Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam.


Wananchi wakikatiza kwenye maji  

NAIBU WAZIRI SIMA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS KATIKA MJI WA SERIKALI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Sima (Mwenye tracksuit) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi  wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali kutoka kwa Mhandisi Simeo Machibya ambae ni Meneja Msimamizi wa Mradi kutoka Vikozi vya Ujenzi.  Sima ameridhishwa na kasi ya Ujenzi huo na kumwagiza mkandarasi kujenga kwa wakati, ubora na kuzingatia viwango vinavyokubalika.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Sima (Mwenye tracksuit) akishiriki katika shughuli za ujenzi kwa kuchanganya mchanga katika ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais unaondelea katika Mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.

WAKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO,MAAFISA UTUMISHI WAANDAMIZI WAJENGEWA UWEZO MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na SHIVYAWATA wametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakurugenzi wa Sera na Mipango na Maafisa Utumishi Waandamizi juu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Peter Kalonga amesema kuwa masuala ya Watu wenye Ulemavu ni mtambuka, hivyo ili kuifikia jamii jumuishi ni vyema kuhakikisha masuala ya wenye Ulemavu yanajumuishwa vyema katika mipango mkakati wa kila sekta.

“Sera ya Taifa ya huduma na maendeleo kwa Watu wenye Ulemavu pamoja na Sheria ya Watu wenye Ulemavu zinasisitiza ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali za kijamii.” Alisema Kalonga. Aliongeza kuwa, Nchi yetu iliridhia Mkataba wa Kimataifa wa haki za Watu wenye Ulemavu wa mwaka 2006 unaotoa tafsiri ya mambo mbalimbali kuhusu haki za Watu wenye Ulemavu na kupelekea kutungwa Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 ili kufanikisha utekelezaji wa mkataba huo na kukuza haki za watu wenye ulemavu nchini.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Peter Kalonga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo wakati wa mkutano wa kuwajengea uelewa Wakurugenzi na Maafisa Utumishi Waandamizi ngazi ya Wizara juu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika Disemba 21 na 22, 2018 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bi. Ummy Nderiananga akiwasilisha mada juu ya ujumuishwaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Josephine Lyengi akelezea jambo kuhusu ukondoishwaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza hotuba ya Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Peter Kalonga (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Peter Kalonga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Maafisa Utumishi Waandamizi na Wawakilishi kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA). PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Taasisi ya Governance Links yakabidhi miradi ya mfano Jijini Mwanza

$
0
0
Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu Mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) wakati wa zoezi la kukabidhi matenki ya kuvuna maji ya mvua yaliyojengwa kupitia mradi huo katika Shule za Msingi Mabatini A na B zote za Jijini Mwanza, hii leo Disemba 21, 2018.

Mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulibuniwa na taasisi ya Governance Links Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ukilenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko.
Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki ya mfano ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B Jijini Mwanza, umegharibu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa wakati wa mvua.
Utekelezaji wa Mradi wa majaribio wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulianza mwezi Otoba 2017 na unafikia tamati mwezi huu Disemba 2018 huku kukiwa na matarajio makubwa ya mradi huo kuwa endelevu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania imekabidhi manteki mawili ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B, yaliyojengwa kupitia mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience).


Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki hayo ya mfano umegharimu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine Jijini Mwanza zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa cha maji wakati wa mvua.



Kasongi amesema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) unaolenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko.



Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, wanafunzi Mariam Thomas (Mabatini B), Rayton Mandalu (Mabatini A) pamoja na Rhoda Madaraka (Mabatini B) wamesema uvunaji wa maji ya mvua umewasaidia kupata maji ya kutosha kwa ajili ya usafi wa madarasa, vyoo, kumwagilia miche ya miti na hivyo kuwaondolea adha iliyokuwepo awali.

Tazama BMG Online TV hapa chini
Mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience)

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye kikao cha kwanza na Watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mnyepe aliwataka Watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa kufuata miongozo na kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na uzalendo. Mkutano huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura. 

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura akizungumza wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018. Kulia ni Katibu Mkuu, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi(kulia) akichangia jambo wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani).



Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani)wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliopo jijini Dodoma tarehe 21 Desemba 2018.

PILIKAPILI ZA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUELEKEA SHEREHE ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

$
0
0

 Wakazi  wa mkoa  Dar es Salaam na  baadhi  wageni  mbalimbali waliwasili kutoka mikoani kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya wakiwa kwenye pilipilika za kununua mahitaji mbalimbali kwenye Soko la Karikoo   leo. (Picha na Emmanuel Massaka, MMG)
 Wakazi  wa mkoa  Dar es Salaam na  baadhi  wageni  mbalimbali waliwasili kutoka mikoani kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya wakiwa kwenye pilipilika za kununua mahitaji mbalimbali kwenye Soko la Karikoo   leo.(Picha na Emmanuel Massaka, MMG)
 Sehemu ya umati wa watu uliofurika katika mtaa wa Congo katika soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam kwajili ya maandilizi ya Sikukuu za Chrismas na Mwaka Mpya wa 2019.
 Sehemu ya Wakazi wa Dar es Salaam wakichagua nguo na viatu  katika Mtaa wa Congo- Kariakoo.

MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

$
0
0
*Ahimiza ushiriki wao kwenye ujenzi wa viwanda
*Aahidi kutoa milioni 700/- Chuo cha Polisi Dar


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ametoa maagizo kwa vyombo vya ulinzi na salama kujipanga kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za uchumi ikiwemo ujenzi wa viwanda nchini.

Ametoa kauli hiyo leo Desemba 21, 2018 jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo ya maofisa wa Polisi na wakaguzi wasaidizi wa jeshi hilo zilizofanyika viwanja vya Chuo cha Polisi ambapo amesisiiza umuhimu wa vyombo vya ulinzi kujikita kwenye shughuli za kiuchumi.

"Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama jipangeni kushiriki kwenye kujenga uchumi wa nchi yetu.Hakuna ubaya kuwa na kiwanda cha kutengeneza viatu, maji na nafaka.Sioni sababu ya kila mara jeshi la polisi kupewa mchele kutoka kwa watu binafsi.Jeshi la Magereza mnao wafungwa ambao wanapaswa kulima na kuzalisha chakula cha kutosha ambacho mnaweza kukigawa kwa taasisi nyingine,"amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dk.Magufuli ameahidi kutoa Sh.milioni 700 kwa lengo la kuboresha Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam na kutaka fedha hizo zitumike vizuri na kinyume na hapo zitageuka kuwa kaa la moto huku akisistiza ameamua kutoa fedha hizo kwa lengo la kulinda heshima na hadhi ya chuo hicho.

"Fedha hizo nitazitoa kabla ya Ijumaa ya wiki ijayo , kubwa zaidi fedha hizo zitumike kwa malengo ambayo nimeyakusudia.Nimekusikia Mkuu wa Chuo hichi cha Polisi Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)Anthony Rutta ukiomba Sh.milioni 700 nitakuletea ili parekebishwe na kupendeza .Najua sisi Serikali tunahamia Dodoma lakini hapa chuoni lazima pawe pazuri na pakuvutia.

"Kwa Jeshi la Magereza niliamua kutoa fedha ili kujengwe nyumba z askari lakini hazikujengwa , wakati mwingine unapata shida kwasababu unatoa fedha zijengwe nyumba lakini hazijengwi.Nimeshatoa maagizo hizo fedha zifuatiliwe ili nijue zilikopotelea,"amesema Rais Magufuli.
 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Viongozi wa Majeshi na Serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018 

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGA KOZI YA MAAFISA NA WAKAGUZI WA JESHI LA POLISI KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Viongozi wa Majeshi na Serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Saimon Sirro akizungumza mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe.Ahmad Masauni akizungumza mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omary Mahita akitoa salamu zake mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Paredi ya Maafisa na Wakaguzi wahitimu wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
Paredi ya Maafisa na Wakaguzi wahitimu wa Jeshi la Polisi ikipita mbele ya Mgeni rasmi Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
Wahitimu Maafisa na Wakaguzi wa Jeshi la Polisi wakiapa kiapo cha Utii na Uadilifu mbele ya Mgeni rasmi Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018
 Maafisa na Wakaguzi wapya wa Jeshi la Polisi wakitoa salamu ya heshima walipopita mbele ya Mgeni rasmi Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba


MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ ALIPA MILIONI 259.5/- ILI KUKWEPA KIFUNGO CHA KWENDA JELA MIAKA 20

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MDOGO wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Azizi amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya Sh.milioni 259.5 au kwenda jela miaka 20 jela baada ya kukiri mashtaka 73 ya kukutwa na nyara za Serikali.

Hukumu hiyo imetolewa leo mahakamani hapo ambapo Akram amefanikiwa kulipa faini kwa kulipa fedha hizo, hivyo amekwepa kifungo cha kwenda jela miaka 20 jela.Hata hivyo Mahakama imeamua kuitaifisha nyara hizo na kuwa mali ya Serikali na kuamuru silaha zote ziwe chini ya Polisi hadi mshitakiwa atakapokamilisha taratibu za kisheria za kumiliki silaha.

Akram alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Oktoba 31,2018 akikabiliwa na mashitaka 75 katika kesi namba 82/2018 ikiwemo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018 lakini kwa mujibu wa sheria alifutiwa mashitaka hayo na kusomewa upya mashitaka 73 ukitoa ya utakatishaji fedha na meno ya tembo.

Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri aliyetoa hukumu hiyo amesema katika mashitaka ya kukutwa na nyama ya nyati, mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh. 43,529,000 na katika makosa 72, yaliyobaki kila moja atatakiwa kulipa Sh milioni tatu.Katika mashitaka hayo 72, jumla ya faini aliyotakiwa kulipa Akram ni Sh.milioni 216. Alisema mshitakiwa akishindwa kulipa faini hiyo atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela.

Awali kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kadushi akisaidiana na Wakili wa Serikali Wankyo Simon aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa adhabu kali kutokana na uzito wa makosa hayo ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo hivyo na kuomba Mahakama itaifishwe nyara zote iwe mali ya Serikali.Hata hivyo mshitakiwa alidai anasumbuliwa na shinikizo la juu la damu na kwamba ni mkosaji wa kosa la kwanza, ana watoto 10 wanaomtegemea
pamoja na mama yake mzazi ambaye ni mzee. 

WIZARA YA ELIMU YAPIGA MAARUFUKU KUSAMBAZA NYARAKA ZA SERIKALI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

$
0
0
PICHA 1-min
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza na washiriki wa Wizara hiyo (hawapo Pichani) waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamekamilika leo mkoani Morogoro.
PICHA 2-min
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamefungwa leo mkoani Morogoro.
3-min
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu.
.............................
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema ni kosa kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini ya Mamlaka husika, hivyo ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria kwa watumishi watakaobainika kusambaza nyaraka hizo.
Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifunga semina ya mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu kwa baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo na kusisitiza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa serikali asiyefahamu kuwa kutoa nyaraka za serikali bila idhini ni kosa la jinai.
“Kumekuwa na usambazaji wa nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini na kwa bahati mbaya wakati mwingine unakuta nyaraka imewekwa mhuri wa siri lakini bado unaikuta huko, watumishi wa serikali lazima watambue kuwa kuna utaratibu wa kutoa nyaraka za serikali na kuna sheria ambazo zinawabana wale wote wanaotoa taarifa hizo bila kuidhinishwa”alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.
Mhe. Ole Nasha amewataka watumishi hao kutambua kuwa hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya kazi bila kuwa na kumbukumbu au nyaraka hivyo amewataka kuhakiksha utunzaji mzuri na salama wa nyaraka hizo kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha utendaji wa majukumu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu, Moshi Kabengwe amesema mafunzo hayo yametolewa ili kusaidia watumishi kufanya kazi ambazo zitaleta tija kwa jamii inayohudumiwa na kuondoa changamoto ambazo zimebainika katika utoaji wa huduma.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tano na yameshirikisha watumishi zaidi ya 50 kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Makao Makuu, Vyuo vya Ualimu vilivyopo Morogoro na baadhi ya watumishi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images