Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: Rais Dkt Magufuli alivyochomekea Tanzanite Bridge liwe jina la daraja jipya la kisasa la selander


Balozi Seif akagua meli ya Sea Star

$
0
0

Meli Mpya ya Kampuni ya Usafiri wa Baharini ya Sea Star  yenye uwezo wa kubeba Mizigo Tani 1,400 na Abiria 1,500  imewasili Bandarini Zanzibar kwa ajili ya kuongeza huduma za Usafiri wa Baharini katika Mwambao wa Bahari ya Afrika Mashariki. Meli hiyo iliyopewa jina la Sea Star 1 itafuatiwa na Boti nyengine Mbili za Mwendo wa Kasi zinazotarajiwa kuingia Visiwani Zanzibar Mwezi Juni Mwaka ujao wa 2019.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mamlaka zinazosimmamia Usafiri wa Baharini alipata nafasi ya kukagua sehemu mbali mbali za Meli hiyo iliyopo Bandaini Malindi na kuridhika na Ubora wake. Meli hiyo yenye sehemu kubwa ya kubebea Mizigo, Vyumba vya Watu Mashuhuri { VIP} pamoja na Abiria wa kawaida itaanza na safari za Zanzibar-Pemba – Tanga, Zanzibar – Dar es salaa, Zanzibar – Mtwara na baadae kuendelea na safari za mbali kwa kuanzia Visiwa vya Comoro.


Safari ya Zanzibar - Dar es salaam huchukuwa muda unaokadiriwa wastan wa saa Tatu wakati safari ya Zanzibar – Pemba itachukuwa wastani wa saa Nne na Nusu. Akitoa Maelezo ya uwepo wa Meli hiyo Nchini Mwakilishi wa Kampuni ya Sea Star Mh. Salum Turky alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umejizatiti kutoa huduma bora za Usafiri wa Baharini kwa Wananchi wote.

Kepteni wa Meli Mpya ya Sea Star Nassor Abubakar akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Chumba cha Mawasiliano alipofika kuikagua Meli hiyo.
Balozi Seif na mwenyeji wake Mh. Salum Turky wakipumzika moja ya sehemu za VIP baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za Meli hiyo.
Mwakilishi wa Kampuni ya Sea Star Mh. Salum Turky wa Tatu kutoka Kulia akisisitiza azma ya Uongozi wa Kampuni hiyo kufuata Taratibu zote za usafiri wa Baharini wakatiu choba chao kitakapoanza kutoa huduma ya usafiri.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Uongozi mzima wa Sea Star juu kabisa ya Meli ya Kampuni hiyo baada ya kumaliza ziara ya kuikagua sehemu mbali mbali. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KAIRUKI ALIVYOSHIRIKI KONGAMANO LA SEKTA YA MADINI JIJINI BEIJING CHINA

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Fainali za mabingwa Afrika kwa vijana chini ya Miaka 17 (AFCON) yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania April 2019 yamefikia katika upangaji wa makundi.

Droo hiyo iliyochezeshwa jioni ya leo ikishuhuduwa na viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na viongozi kutoka Shirikisho la Mpira Wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na nchi washiriki waliofanikiwa kuingia katika fainali hiyo.

Fainali hizo zinahusisha timu nane zilizofanikiwa kufuzu na zitachuana kuweza kupata wawakilishi wawili kutoka katika kila kundi kwa ajili ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia la Vijana nchini Peru.Kwenye kupanga makundi hayo mwenyeji Tanzania ameangukia katika kundi la A akiwa na timu za Nigeria, Angola na Uganda.

Katika kundi B, kuna timu za Cameroon , Guinea, Morroco na Senegal.
Waangalizi kutoka CAF wameshakagua viwanja, mahospitali na hoteli kwa ajili ya timu zinazokuja nchini mwakani pamoja na waalikwa kutoka nchi mbalimbali.

YANGA YAENDELEZA UBABE WAKE, NINJA AMALIZA KAZI AIPA ALAMA TATU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kikosi cha Yanga kimeendeleza ushindi wake mfululizo na kujikita zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya AFrican Lyon.

Mchezo huo wa 17 kwa mabingwa hao wa Kihistoria uliochezwa kwenye Uwanja wa Shekhe Amri Abeid Karume Jijini Arusha uliweza kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Mechi hiyo ilianza majira ya saa 10 Alasiri, ukiwa ni mchezo wa kasi ya kawaida kila timu ikimsoma mpinzani wake ila kwa Upande wa Yanga waliweza kuwatoa wachezaji wake wawili Jaffar Mohamed na Ramadhan Kabwili baada ya kupata maumivu kwenye Kipindi cha Kwanza.

Mabadiliko hayo Yanga waliyafanya kwa kumuingiza Deus Kaseke na Klaus Kindoki na mpaka mpira unafika mapumziko, kila upande ulikuwa haujaona lango la mwenzake.Kipindi cha Kilianza na African Lyon wakionesha kuhitaji zaidi alama tatu ili kuweka matumaini ya kutoka katika nafasi ya chini huku Yanga nae akitaka kuweka rekodi yake ya kutokufungwa.

Kupitia kwa Beki wake wa Kati Abdalla Shaibu 'Ninja' katika dakika ya 64 aliweza kuiandika Yanga goli la Kuongoza baada ya kuupiga kwa kichwa mpira wa adhabu ulipigwa na Ibrahim Ajib.African Lyon walindelea kusaka goli la kusawazisha na kupata alama moja lakini umakini wa safu ya ulinzi wa Yanga uliwanyima nafasi washambuliaji wake na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa kupoteza kwa goli 1-0.

Baada ya ushindi huo, Yanga imefikisha alama 47 wakiwa wamecheza michezo 17 wakishinda 15 na kutoa sare 2, akifuatiwa na Azam mwenye alama 40 akiwa amecheza mechi 16 huki mabingwa watetezi Simba wakicheza mechi 13 na wakisalia nafasi ya tatu kwa alama 30.

Katika mchezo huo uliochezwa Jijini Arusha uliweza kuonesha hamasa kubwa ya mpira wa miguu kwa mashabiki kujitokeza kwa viongozi wa kiserikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na aliyewahi kuwa Afisa habari wa Yanga na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro.
Kikosi cha Yanga.

MICHUZI TV: Rais Dkt Magufuli amwagiza waziri wa uchukuzi kufuatilia kwa kina meli zilizouzwa

Sekta ya usafirishaji inahitaji wataalam wengi -Nditiye

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

NAIBU Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema Serikali imejenga miundombinu ya usafirishaji yakutosha ambapo Chuo cha Usafirishaji (NIT) ndio watumiaji wa miundombinu hiyo.

Serikali haitegemei kutafuta watalaam kutoka nje kwa ajili kutumia miundombinu yetu katika ndege Boti pamoja na Reli.
Nditiye amekitaka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuhakikisha kinatoa mafunzo bora yatakayosaidia kupatikana kwa wataalamu wa kisasa wataofanya kazi hapa nchini katika sekta mbalimbali za usafirishaji.

Waziri Nditiye ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mahafali ya 34 ya chuo cha NIT yaliyofanyika katika viwanja Chuo hicho jijini Dar es Salaam.Amesema chuo hicho kikianza kutoa kozi ya marubani na wataalamu wa reli itaongeza wigo la watalaamu nchini.

"Rai yangu kwa NIT kuhakikisha kuwa kozi hizo zinaanza mapema hapo mwakani ili kuokoa fedha zilizokuwa zinatumika kusomesha marubani na wataalamu wa reli za kisasa nje ya nchi ambapo Serikali imekuwa gharamia kwa fedha nyingi"amesema Nditiye. Aidha Nditiye amewataka wahitimu kuhakikisha wanatumia maarifa na ujuzi waliyoupata wakiwa chuoni kuleta maendeleo ya kwao binafsi na taifa kwa ujumla kwa kujiajiri au kuajiriwa.
 
 Wahitimu wakiwa wametunukiwa shahada na Mgeni Rasmi katika mahafali ya 34 ya Chuo cha NIT yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wa Chuo cha Usafirishaji cha (NIT) wakiwa katika maandamano katika mahafali ya 34 ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza katika mahafali ya 34 ya Chuo cha Usafirishaji yaliyofanyika viwanja ni hapo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha NIT katika mahafali ya 34 yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

NITATUMIA UTAJIRI WANGU WOTE ILI MJE KUFANIKIWA BAADAE- DKT MENGI

$
0
0
Mlezi wa Serengeti Boys, Dkt Reginald Mengi amekutana na kikosi cha Srengeti Boys kilichotwaa ubingwa wa kombe la Cosafa, hivi karibuni nchini Botsw ana ili kuwapongeza. 

Hafla hiyo ya chakula cha mchana ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, Rais wa TFF Wallace Karia na wadau wengine wa Soka.

Katika hafla hiyo Dkt Mengi aliwapongeza kwa ubingwa huo huku akiitoa zawadi ya fedha kwa wachezaji na benchi zima la ufundi huku akiwaambia kuwa kutwaa kombe hilo ni moja ya safari nzuri ya kuelekea kutwaa ubingwa katika michuano ya Afcon inayotarajiwa kurindima mwakani hapa nchini.Mengi amesema hii ni historia kwa nchi na pia timu hii ya vijana kufanya vizuri kwenye Mashindano makubwa mawili ikiwemo kombe la Cosafa na kurejea na Kombe, hivyo wanastahili pongezi.

“Pia niipongeze serikali kwa sapoti kubwa wanayoendelea kuitoa katika timu yangu hii ya vijana, hivyo tutampatia kombe hili mheshimiwa Rais Magufuli kama zawadi ya krismasi, kwani tunajua atafurahia kwakuwa ni mmoja ya viongozi wapenda mafanikio", alisema Mengi.

Amewaeleza kuwa, ana zawadi kubwa zaidi kwa vijana hao, ila amewasihi kuwa kuwaambia vijana hao wa Serengeti Boys kuwa zawadi hii ya leo ameipunguza baada ya kushauriwa kuwa umri wao ni mdogo sana hivyo kwahoyo yeye kama Mlezi na ataendelea kuwa nao atatatumia mali zake zote ili ahakikishe huko badaye maisha yao yanakuwa mazuri.

Kwa upande wa Waziri Mwakyembe amesema Kombe hilo ni zawadi ya sikukuu ya Krisimas kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na ameahidi atazifikisha salam zao kwake pamoja kuahidi kwenda kumkabidhi kombe hilo.
Mlezi wa Timu ya Vijana Serengeti Boys Dkt Reginald Mengi akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na wadau wengine wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana hao iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akitoa pongezi kwa timu ya vijana ya Serengeti Boys iliyofanikiwa kurudi na Kombe kwenye mashindano ya nchi za ukanda wa kusini COSAFA, hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mlezi wa Timu ya Vijana Serengeti Boys Dkt Reginald Mengi akipokea kombe kutoka kwa Nahodha wa Serengeti Boys Abraham Morice na wakati wa hafla ya kuwapongeza Vijana hao iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

MRADI WA MFANO WA USIMAMIZI WA MAJI MTIRIRIKO SEKONDARI YA KINZUDI WAZINDULIWA DAR ES SALAAM

$
0
0


MGENI Diwani wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori wakati wa uzinduzi wa mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kwenye Shule ya Sekondari Kinzudi, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Pamoja naye ni Mratibu wa Mradi huo, kutoka Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Wilbard Kombe (kulia), Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Saimon Mpyana (wa pili kulia), Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) na Wataalam kutoka ARU na Halmashauri za jiji hilo. Mradi huo umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na kutekelezwa na wataalam wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU).  (Imeandaliwa na Robert Okanda)
MGENI Diwan wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda (wa tatu kulia) kwa niaba ya Mkuu wa  Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori akipata maelezo baada ya kuzindua mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kutoka kwa Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Kinzudi, Juma Mbwana iliyopo Goba Wilayani humo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Mratibu wa Mradi huo, kutoka Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Wilbard kombe (wa pili kulia), Mhadiri Msaidizi wa ARU, Saimon Mpyana (kulia), Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) na Wataalam kutoka ARU na Halmashauri za jiji hilo

Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) akimpatia maelezo Mgeni Rasmi, Diwani wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda alipotembelea maeneo mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kwenye shule ya Sekondari Kinzudi ulivyotekelezwa katika Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Disemba 18 2018.

Mhadhiri Msaidizi wa ARU, Given Mhina (kushoto) akimpatia maelezo Mgeni Rasmi, Diwani wa Kata ya Goba, Muslima Mwenda namna mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua na jinsi yanavyoweza kutumiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kinzuri baada ya kuzindua mradi wa mfano wa usimamizi wa maji mtiririko, kwenye shule ya Sekondari Kinzudi, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Disemba 18 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

MKOA WA ARUSHA WAPATA ENEO LA UJENZI WA KITUO KIKUU CHA MABASI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Mkoa wa Arusha unakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na kituo cha mabasi chenye hadhi ya kisasa,kwani kilichopo sasa kinakabiliwa na ufinyu hali iliyoilazimu  Halmashauri ya Jiji la Arusha kuja na mkakati wa kujenga kituo kikubwa cha mabasi chenye hadhi ya Kimataifa,kinachotarajiwa kujengwa katika Kata ya Olasiti iliyopo nje kidogo ya jiji hilo .

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipotembelea Eneo litakapojengwa Kituo hicho ambapo amewataka viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa kila mwananchi aliepisha eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho analipwa fidia inayokadiriwa ni ni zaidi ya shilingi bilioni 1.7.

Gambo amesema kuwa mkoa wa arusha hauna standi inayoendana na hadhi ya jiji hilo na kuweza kufanya tathmini upya ya eneo hilo ili kuanza mchakato wa kuwalipa wale wanaostahili ili kuondoa sintofahamu ya kuwalipa watu wasio husika hali ambayoimekuwa ikisababisha malalamiko na migogoro mingi isiyo na tija kati ya wananchi na serikali yao.

“Hakikisheni mnapitia upya mchakato wa kuwalipa wananchi na ikiwezekana kila moja asimame kwenye eneo lake ili kuhakikisha mnamlipa mtu anayestahili kulipwa na sivinginevyo ili kuepusha migogoro isiyo na tija kati ya serikali na wananchi”alisisitiza mkuu huyo wa mkoa.
Viongozi wa mkoa wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo walipotembelea eneo litakapojengwa Kituo kikuu cha mabasi mkoani hapa eneo la Olasiti nje kidogo ya jiji la Arusha (Picha na a Ahmed Mahmoud  Arusha)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Hali ya hewa isiwe kisingizio cha kuchelewesha miradi ya umeme vijijini- Mgalu

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Njombe
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaosambaza umeme  vijijini kutochelewesha utekelezaji wa miradi hiyo kwa kisingizo cha mabadiliko ya hali ya hewa kama vile uwepo wa mvua. Aliyasema hayo wilayani Makete mkoani Njombe  wakati alipokuwa akikagua kazi ya usambazaji umeme vijijini inayotekelezwa kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza.

“ Kabla ya Serikali kuwakabidhi kazi hii ya usambazaji umeme vijijini, mlishafanya upembuzi wa maeneo mnayoenda kufanyia kazi na mnayafahamu vizuri, hivyo basi, iwe Jua au mvua, tunataka kuona kazi hii inaendelea kutekelezwa ili wananchi wengi wapate huduma ya umeme,” alisema Mgalu

Aliongeza kuwa, wakandarasi hao wanapaswa kuwa na mipango mbalimbali  ya utekelezaji wa kazi kulingana na hali ya hewa ya maeneo wanayofanyia kazi ili kuweza kusambaza umeme katika vijiji vyote walivyopangiwa na Serikali ifikapo Juni 2019. Awali, Mkuu Wilaya ya Makete, Veronica Kessy, alimweleza Naibu Waziri kuwa, jumla ya vijiji 29 vimepangwa kuunganishiwa umeme kupitia mradi wa REA III mzunguko wa kwanza ambapo mkandarasi anaendelea na kazi ya usambazaji umeme vijijini, ingawa uongozi wa Wilaya hiyo umekuwa na wasiwasi na kasi yake katika usambazaji umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe ikiwa ni ishara ya wananchi katika Kijiji cha Bulongwa wilayani Makete kuanza kupata huduma ya umeme. Kulia kwake ni  Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronica Kessy.
 Baadhi ya nguzo za umeme zilizosimamishwa katika Kijiji cha Usungilo wilayani Makete mkoani Njombe ambapo kijiji hicho kitapata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza.
 Wananchi katika Kijiji cha Usungilo wilayani Makete, wakimsikiliza NaibuWaziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) wakati alipofika kijiji hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

$
0
0
Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda
20 Desemba 2018
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde wakibadilishana taarifa ya mkutano kati ya Tanzania na Uganda uliojadili namna ya kuimarisha biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara na visivyokuwa vya kiforodha uliofanyika Mutukula, Uganda tarehe 19 Desemba 2018.

Mbunge Mabula atoa Milioni 22 ujenzi wa soko la Mlango Mmoja uanze haraka

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ametoa shilingi Milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya soko la Mlango Mmoja iliyoteketea kwa moto miezi mitatu iliyopita. Mabula aliyasema hayo jana baada ya kuwatembelea wafanyabiashara wadogo (machinga) katika soko hilo na kubainisha kwamba fedha hizo kutoka mfuko wa jimbo zitasaidia ujenzi wa paa lote.

Mwenyekiti wa soko hilo, Jackson Kayoza alisema kulingana na tathmini iliyofanyika, shilingi Milioni 98 zinahitaji kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyoungua moto hivyo alimshukru mbunge Mabula kwa mchango huo. Mmoja wa machinga katika Soko la Mlango Mmoja ambaye pia bidhaa zake zilitekeketea kwa moto, Isaack Julius, alisema mchango wa mbunge Mabula uwe chachu kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuhakikisha inakamilisha kiasi cha fedha kinachohitajika ili ujenzi huo uanze mara moja.

Septemba 28, 2018 majira ya alfajiri, ajali ya moto ilizuka katika Soko la Mlango Mmoja na kusababisha meza 83 za wajasiriamali, maduka 23 na vyoo vitatu kuteketea ambapo hasara yake haikujulikana mara moja.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (katikati), akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
Tazama BMG Online TV hapa chini

NAUFUNGA MOYO - SUPER KAMANYOLA UTUNZI WAKE ALLY CHOKI


VULLU ATOA MSAADA WODI YA UZAZI KISARAWE NA SARUJI MIFUKO 80 KUKARABATI ZAHANATI NA SHULE

$
0
0



NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE 

MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Zainab Vullu ametoa msaada wa mapazia mazito yanayotumika kusaidia kuweka usiri kwa akinamama wanaokwenda kujifungua katika wodi ya uzazi hospital ya wilaya ya Kisarawe.

Msaada huo unaelezwa kuwaondolea kero waliyokuwa wakiipata akinamama hao kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wakikataa kujifungua hospitalini hapo kwa kuhofia kukosa faragha wakati wa kujifungua. 

Mbali ya msaada huo pia ametoa mifuko 80 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya ,zahanati na shule vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh.milioni mbili. 

Akitoa msaada huo ,Zainab alieleza kipindi cha nyuma akinamama wanaojifungua walikuwa wanakaa sehemu ambayo haijazibwa jambo ambalo limemsukuma kujitolea mapazia hayo. “Faragha inaanza tangu pale anapoanza kutafutwa mtoto hadi anapozaliwa lazima usiri uwepo,” alifafanua Zainab.
Nae mkuu wa wilaya ya Kisarawe ,Jokate Mwegelo alimshukuru mbunge huyo na kudai suala la ukosefu wa mapazia hayo ilikuwa ni changamoto kwa akinamama wanaojifungua. 

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hamis Dikupatile alisema, serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha mazingira ya kutolea huduma lakini bado jitihada zinapaswa kufanywa na kila mmoja. Mganga mkuu wa halmashauri ya Kisarawe, Jonathan Budenu alibainisha kutokana na changamoto hiyo baadhi ya akinamama walikuwa wakikataa kujifungulia hapo kutokana na hali hiyo.

MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Zainab Vullu akikata utepe,kulia ni MKuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo

WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WANAFUNZI waliosoma Shule ya Msingi ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro kuanzia mwaka 1958 wanatarjiwa kushiriki tamasha la kuchangia uboreshaji wa miundombinu mbalimbali shuleni hapo litakalofanyika Desemba 27 mwaka huu.

Ushiriki wa wanafunzi hao ni matokeo ya ombi la mwalimu mkuu wa shule hiyo Christina Lyari la kuwaomba wananchi, wadau na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kujitokeza katika tamasha hilo la aina yake.

Lyari alisema wakati umefika kwa kila aliyepita shule hiyo kurudisha fadhili kwa kusaidia kuboresha miundombinu.“Tunahitaji kukarabati majengo kama ofisi ya walimu, maktaba, choo cha walimu, uwekaji wa madirisha ya aluminiamu na kununua komputa na viongine vingi hivyo ujio wanamwanga ni muhimu,” alisema.

Aidha Mwalimu Lyari alisema amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa shule hiyo imetengeneza viongozi, wataalam, watafiti, wanasiasa na wajasiriamali wengi wanaoweza kutatua changamoto nyingi zilizopo kama wakishirikishwa ipasavyo .Akizungumzia ziara hiyo mmoja wa wahitimu wa Shule ya Msingi Mwanga na aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Dk. Abu Mvungi alisema wameamua kufanya ziara hiyo kama moja ya sehemu ya kuonesha walipotoka.

“Nampongeza mwalimu kwa kuonyesha moyo wa dhati, ushirikiano na ushirikishaji wa katika suala zima la kutumikia jamii, suala hili lina umuhimu mkubwa na linahitaji kuungwa mkono na kuendelezwa na sisi tutamuunga mkonon kwani Mwanga ndio mwanga wetu,” alisema.

Alisema shule hiyo ni mkombozi wa maisha yake hivyo hawezi kuisahau hivyo kuwataka wale wote waliosoma Shule ya Msingi Mwanga kujitokeza.
Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Barabara mkoa wa Dar es Salaam (Tanroads), Haruni Msuya alisema hawezi kuisahau shule hiyo kwani ndio msingi unaomwezesha kuendelea kuitumikia jamii 

Wengine waliosoma shule hiyo ni Profesa Abdulkareem Mruma, Daktari Bingwa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Omary Salehe, Mliki wa Mabasi ya Chakito, Meraji Kidundi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Richard Mziray na wengine wengi.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwanga mkoani Kilimanjaro Christina Lyari akionesha mazingira ya shule hiyo ambayo wanafunzi waliosoma hapo kuanzia mwaka 1958 wanatarajia kushiriki tamasha la kuchangia fedha kwa akili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwanga Christina Lyari akiwa ofisini kwake

MBOWE, MATIKO KULA KRISIMAS, MWAKA MPYA WAKIWA RUMANDE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KESI ya tuhuma za uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko  na wenzao saba inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepigwa kalenda hadi Januari 3 mwakani.

Mbowe na Matiko wataendelea kusota mahabusu hadi Januari 3 baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washitakiwa hao kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana.

Wakili wa Serikali Simon Wankyo akisaidiana na Wakili wa Serikali alidai mbele ya hakimu mkazi mkuu Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea mahakamani hapo na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo.
Hata hivyo wakili Faraja Mangula amedai kuwa wakili wa washtakiwa hao Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura na kuiomba mahakama ipange Januari 4, mwakani.

Akijibu hoja hiyo wakili Saimoni alidai wanaiachia mahakama ipange tarehe itakayoona inafaa kusikilizwa kwa shauri hilo.Hakimu Mashauri amesema kuwa Januari 4 mwakani atakuwa na kazi nyingine hivyo amehairisha kesi hiyo hadi Januari 3 mwakani.Baada ya kuelezwa hayo Mbowe na Matiko waliwatakia wafuasi wao heri ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya wakiamini hawawezi kutoka gerezani kwa kipindi hiki.

Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya  na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, jijini Dar es Salam.

Wanawake wanavyoshiriki ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

$
0
0


Na Maura Mwingira , Ihumwa Dodoma

Mama Regina (55) ni kati ya akina mama takribani kumi, ambao ni sehemu ya vibarua wanaoshiriki kwa kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za kubeba zege katika eneo la Ihumwa inapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eneo hili la Ihumwa na ambalo lipo takribani kilometa 17 kutoka Dodoma Mjini, limetengwa maalum kuwa Mji wa Kiserikali ambapo kunajengwa Majengo ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. 

“Karibu habari za kazi” ananisalimia mama huyu ambaye anajitabulisha kama Mama Regina wakati nilipomsogelea mahali alipokuwa akichota maji kutoka kwenye simutanki kubwa lililopo eneo la Ujenzi.“ Unataka kunipiga picha” ananiuliza Mama Regina, baada ya kuniona nimeshika Kamera. Ni kamjibu kama yuko tayari na ananiruhusu kumpiga picha”.

Ninapomuuliza kuhusu kazi yake, Mama Regina kwa tabasamu kubwa ananijibu “ Ninamshukuru Mungu, nimefika leo asubuhi na nikabahatika kupata nafasi ya kufanya kazi kwenye ujenzi huu, ninashukuru sana tunafanya hivi kwa ajili ya ada za watoto” anasema Mama Regina kwa furaha kubwa.Furaha ya Mama Regina ya kupata nafasi ya kushiriki kazi ya ujenzi inajithihirisha wazi wazi usoni mwake ni furaha pia inayonekana kwa wamamawegine wanaobeba zege

Anajitishwa ndoo yake ya maji kichwani na kuniambia . “ Mimi nakaa kijiji kingine mbali kidogo na eneo hili la ujenzi, kwa hiyo ilinipasa kufika mapema asubuhi na nikapata nafasi, Kwa kweli nina mshukuru Mungu”
Mwandishi wa habari hii alikuwa miongoni mwa Maafisa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokwenda jana ( Alhamisi) kuangalia na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo hilo la Ihumwa.
Akina Mama wakiwa bega kwa bega na  vibarua wenzao wanaume katika  kubeba zege linalotumia kwa ujenzi wa msingi na nguzo  za jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika eneo la Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma
IMG_4604-MACHINE
Kazi ya  uchanganyaji zege ikiendelea katika eneo la ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ihumwa.( Picha na Habari kwa Hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali)
IMG_4647
Mama Regina akijitwika ndoo ya maji na  kuipeleka kunakoojengwa Msingi. Mama Rejina anasema anamshukuru Mungu kwa  kupata fursa ya kushiriki  ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama ilivyo kwa akina mama wengi, Anasema  kazi hiyo anaifanya kwaajili ya  watoto wake ( ada)
-PICHA 3
Maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiangalia na kukagua maendeleo ya ujenzi wa  msingi na usimikaji   wa nguzo mwenye kofia nyekundu ni Injinia  Shadrack Ng’wiza  kutoka Kampuni ya Ujenzi  ya Corporation Sole ( Works Superntent) kutoka Mwanza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

KABUDI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

$
0
0


Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongoza Kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Wizara jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Ndg. Amon Mpanju.
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiongoza Kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Wizara jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Ndg. Amon Mpanju.
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake.
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images