Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi kwa wananchi waishio kwenye Mkoa wa Kaskazini kisiwani Pemba na kubaini kuwa yapo baadhi ya maeneo yana usikivu mdogo wa mawasiliano na mengine hakuna kabisa mawasiliano ya simu za mkononi

Nditiye aliambatana na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah ambaye ndiye chimbuko la ziara hiyo kwa kuuliza maswali Bungeni wakati wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu changamoto ya mawasiliano kisiwani Pemba.

“Zipo changamoto mbali mbali ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, wananchi wanapata tabu za kuwasiliana hasa nyakati za usiku hasa wakipata msiba au mgonjwa, tuliwasilisha changamoto hizi Bungeni ili ziweze kutekelezwa,” amesema Maida

Nditiye amebaini uwepo wa usikivu mdogo wa mawasiliano na ukosefu wa mawasiliano wakati wa ziara yake kwenye Shehia ya Kiungoni – Wingwi, Dodeani, Kiuyu Mbuyuni, Sizini – Chwaka, Tumbe, Kipande Konge na Makangale – Mnarani zilizopo kwenye Wilaya ya Micheweni pamoja na kwenye Shehia nyingine za Weni – Tungamaa – Machwengwe, Mtambwe, Mkanjuni na Kivumoni zilizopo kwenye Wilaya ya Wete

“Kuna maeneo ambayo minara ipo ila mawasiliano hayana nguvu na sehemu nyingine hakuna mawasiliano kabisa kutokana na jiografia ya Pemba, nimekuja na wataalamu wa kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), nimewaelekeza hili walifanyie kazi, raha yangu ni kuona wananchi wote wana wasiliana,” amesema Nditiye
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akiwasili kisiwani Pemba kukagua changamoto za mawasiliano. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah na wa kwanza kushoto ni Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Baucha
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyenyoosha mkono) akijadiliana na Shehia wa Sheha ya Kiungoni, Omari Khamisi Othman kuhusu eneo la kujenga mnara wa mawasiliano katika ziara yake ya kukagua changamoto za mawasiliano Pemba. Aliyevaa miwani akisikiliza kwa makini ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akiwa kwenye boti eneo la Makangale – Mnarani akikagua upatikanaji wa mawasiliano wakati wa ziara yake Pemba. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga



Watumishi OSHA Waaswa Kufanya Kazi Kwa Kuzingatia Maadili

$
0
0
Watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA ) wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi, sheria na kanuni zinazosimamia utumishi wa umma ili kufikia malengo yakutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge kama dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inavyoelekeza.

Akizungumza  kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa OSHA, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Bw. James Kajugusi amesema kuwa kikao hicho ni fursa pekee ya kutathmini utendaji wa wafanyakazi na kuangalia namna ya kuboresha ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Baraza hili la Wafanyakazi linasisitiza umuhimu wa watumishi kufanya kazi kwa maadili na nidhamu ya hali ya juu kama wakaguzi wa masuala ya Afya na Usalama  katika maeneo ya kazi ili muweze kuwa mfano wa kuigwa na Taasisi nyingine za Umma zinazofanya kazi zinazoshabihiana na za kwenu.”

Akifafanua Bw. Kajugusi  amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati, kuondoa uzembe, ubadhirifu pamoja na vitendo vyovyote vya rushwa mahala pa kazi, ikiwa ni pamoja na kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuongeza tija. Aliwaasa watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwa kuzingatia malengo yaliyopangwa kwa wakati husika ili kuchochea maendeleo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, akizungumza  kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, akimkaribisha  Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa Wakala huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Andrew Massawe, Jijini Dodoma.
 Sehemu ya washiriki wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) kinachofanyika  Jijini  Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi, (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
                                                          

SIMBA WAPASHA KIPORO CHA KMC, WATOKA NA USHINDI WA 2-1

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu ya Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Kinondoni Municipal Council (KMC) mechi iliyochezewa katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi ilichukua dakika 11 ya kupitia kwa mshambuliaji Adam Salamba kuiandikia vijana wa Msimbazi goli la kuongoza.

Simba waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao na baada ya dakika tatu ikiwa ni  dakika ya 14, Said Ndemla anaiandikia goli la pili kwa shuti kali nje ya kumi na nane na kuzidi kudidimiza matumaini ya KMC kuondoka na ushindi kwenye mchezo.

Mpaka mapumziko, Simba walienda kifua mbele wakiwa wanaongoza kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Kocha wa KMC akifanya marekebisho kwa kuwatoa wachezaji wawili na kuingiza nguvu mpya.

Mpira ulikuwa wa kasi na kila mmoja akisaka goli na katika dakika ya 67,  KMC walifanikiwa kupata goli kupitia kwa mchezaji wake James Msuva na kupelekea matokeo yake kuwa 2-1.

Mpaka kipengya cha mwisho kinapulizwa Simba wanaibuka kidedea kwa  ushindi wa goli 2-1 na kufikisha alama 30 akisalia kwenye nafasi ya tatu akiwa nyuma ya Yanga mwenye alama 44 na Azam 40.

Kikosi cha Simba kimeweza kumuanzisha mchezaji wake mpya Koulbaly pamoja Haruna Niyonzima, Asante Kwasi na Jurko Murshid waliokosekana kwa muda mrefu.

Wadau wakutana kujadili mikakati mipya kukabili mimba za utotoni

$
0
0
WADAU mbalimbali katika sekta ya elimu wanaokutana mjini Morogoro, wametakiwa kujadiliana kwa kina kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na Ukatili wa Kijinsia kwa kuangalia taratibu zilizopo sasa za kukabiliana na hali hiyo ili kufanya maeneo ya elimu kuwa salama na chanzo cha mabadiliko ya kitabia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayira katika hotuba iliyosomwa na Afisa wa Elimu Afya Mashuleni wa Wizara hiyo, Bw. Avit Maro wakati akifungua mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo.
Mkutano huo ambao umeelezwa kuwa wa kuongeza kasi kwa sekta za elimu kukabiliana na mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya shule na vyuo ni wa kamati ya uratibu ya kitaifa na uthamini wa masuala hayo na unafanyika mkoa wa Morogoro katika hoteli ya Kingsway.
Msingi wa mkutano huo ni kutafuta mkakati wa pamoja wa kuweza kuhuisha sera hizo kulingana na hali ilivyo kwa sasa ili kuweza kukabili changamoto zilizopo.

 Afisa wa Elimu Afya Mashuleni wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Avit Maro akitoa hotuba ya kufungua mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro. Kulia ni Afisa wa Elimu Afya Mashuleni kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Avit Maro, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo (wa pili kulia) pamoja na Ofisa Utawala wa Elimu wa TAMISEMI, Jeanimina Mtitu (kushoto).
 Ofisa Utawala wa Elimu wa TAMISEMI, Jeanimina Mtitu akitoa salamu kwa niaba ya TAMISEMI wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
 Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Herman Mathias akizungumza jambo na washiriki wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
 Program Meneja wa kitaifa wa elimu ya afya shuleni wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Bw. Clement Mung’alo akisherehesha mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Washiriki wa mkutano wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAANET WAIOMBA SERIKALI KUTUNGA SERA JUU YA KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA POMBE

$
0
0
Na, Khadija Seif, Globu ya jamii
   MTANDAO wa Mashirika ya kupambana na matumizi mabaya ya pombe nchini (TAAnet) imetoa wito kwa Serikali kutunga sera juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika ya kupambana na Matumizi mabaya ya pombe (TAAnet) Sophia Komba amepongeza serikali kwa uamuzi waliochukua kutokana na kuzuia na kupiga maarufu juu ya uuzwaji na utumiaji wa pombe aina ya kiroba ambayo ilikua ikiua nguvu kazi ya vijana wengi Kwenye jamii kutokana na kuathirika kiakili na kimwili na kufanya vijana kuwa tegemezi na kutojihusisha na kujenga Taifa hasa kiuchumi.


Komba ameeleza kuwa matumizi mabaya ya pombe inajumuisha pombe za aina zote za kisasa pamoja na za kienyeji ambazo  zina madhara kwa jamii kutokana na kusababisha ajali barabarani, familia kutengana, kusababisha magonjwa kama shinikizo la damu , kisukari, na madhara mengine ya kiafya.


Amesema kuwa "Pombe ya kienyeji inaathiri afya ya watumiaji na watengenezaji kutokana na maandalizi ya kilevi hicho kuwekwa viungo ambayo ni hatarisha kiafya  na kupelekea afya zao kuwadhaifu " amesema Komba .Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama cha Afya jamii (TPHA) Dk. Mashombo Mkamba amesema jamii inaathirika sana kutokana na matumizi mabaya ya  pombe na Kwa sasa hata baadhi ya wajawazito wanajihusisha na unywaji wa pombe tatizo linalopelekea hata kizazi kitakachozaliwa kuathirika sehemu za ubongo .
Mwenyekiti wa Mtandao wa kudhibiti matumizi mabaya ya pombe (TAAnet, Sophia Komba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu athari zitokanazo na matumizi ya pombe uliofanyika katika ofini kwao leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya jamii (TPHA) Dk.Mashombo Makamba akizungumza na waandishi wahabari kuhusu magonjwa yanayoshamiri kwa sasa na matumizi ya pombe kuwa kisababisho kikubwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI WA DARAJA JIPYA NA BARABARA UNGANISHI TOKA AGA KHAN HADI COCO BEACH

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kwenye sherehe za kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick kufunua pazia kuashiria   kuwekwa kwa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana  na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Cho Tae-ick   baada ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana  na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe baada ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wanashuhudia.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakipata maelezo toka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Robert Mfugale kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selanderna Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018    
 Hili ndilo eneo la  Mradi wa Ujenzi wa Daraja Jipya la Selanderna Barabara unganishi ya Km 6.23 toka Hospitali ya Aga Khan hadi ufukwe wa Coco Beach kama linavyoonekana jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2018. Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Robert Mfugale, toka hapo eneo la ufukweni hadi sehemu ya baharini  itajengwa barabara unganishi juu ya tuta la mita 600 kabla ya daraja kuanza na kuishia kwenye ncha ya ardhi kule ambako ndiko CoCo Beach. PICHA NA IKULU

TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’

$
0
0
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation linatarajia kufanya matamasha makubwa matatu jijini Dar es Salaam katikaa wilaya za Ilala, Temeke na Kinondoni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga, inayofanyika sambamba na kutoa burudani.

Hii ni kuunga mkono hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli siku ya tar 21 Juni 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega alisema tamasha hilo litapambwa na wasanii Shilole, Man Fongo, Belle 9, Dully Skykes pamoja na Chege Chigunda.

Alisema burudani hiyo itaanza siku ya Ijumaa Desemba 21, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala, na siku ya Jumamosi Desemba 22, Kampenii hizo zitafanyika Wilaya ya Ilala katika Uwanja wa Karume huku fainali za burudani hizo kumalizikia Jumapili Desemba 23, Wilayani Temeke katika Viwanja vya Mbagala Zakhem.

“…Hadi tunavyozungumza leo, Kampeni hii imetembelea Mikoa yote ya Tanzania Bara na Miji mashuhuri na Wikiendi hii ni zamu ya Jiji la Dar Es Salaam. Katika Kampeni za mikoani, tumefanya kazi na Wasanii wawili maarufu, Shilole na Man Fongo.


Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia matamasha matatu makubwa ya kampeni za ‘Rudi Nyumbani Kumenoga’ yatakayoanza Desemba 21, Kinondoni Uwanja wa CCM Mwinjuma- Mwananyamala, Desemba 22 Ilala katika Uwanja wa Karume na Desemba 23 Wilaya ya Temeke viwanja vya Mbagala Zakhem. Kushoto ni Afisa Masoko wa TTCL, Mohamed Shaaban pamoja na Afisa Masoko wa shirika hilo, Bi. Aurelia Boniface (kulia).
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, wakiwa katika mkutano huo.  


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: TAA NATAKA KUONA MABADILIKO IFIKAPO JANUARY 2019 - MHANDISI KAMWELWE


Rukwa wapokea vifaa vya kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto

$
0
0

Mradi wa uzazi salama Mkoani Rukwa umekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi 211,145,850/= kwa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa ili kuvisambaza katika vituo 198 vya kutolea huduma za afya, ikiwa ni muendelezo wa jitihada na dhamira yao  ya kuhakikisha wanashirikiana na Mkoa katika kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Mkoa.

Mradi huo unaoundwa kwa ushirikiano wa mashirika matatu ya Plan International Tanzania, AFRICARE na JHPIEGO kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada umekabidhi vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vifaa vya upasuaji kwa kinamama wajawazito, vifaa vya kumsaidia mtoto mchanga na mama kupumua, vifaa vya kuwasaidia watoto njiti, majokofu ya kuhifadhia damu na vifaa vya kufanyia tathmini ya hali ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanaratibu kufanyika kwa siku ya afya kwa mwaka mara moja kwa kila kijiji na kuwataka wakuu wa wilaya wasimamie zoezi hilo. Na kuwaomba wanaume, wazee na viongozi wote wa dini pamoja na vijiji kutambua jukumu la afya ya uzazi na mtoto pamoja na familia ni la wote na sio la kinamama na wanawake peke yao.

“Viongozi wa serikali katika ngazi za vijiji na kata wanao wajibu wa kuhakikisha akina mama wanahudhuria katika vituo vya afya pindi wanapojigundua ni wajawazito kwa huduma na ushauri wa kiafya. Tuwe mstari wa mbele kuelimisha wengine hasa vijana wetu kuhusu afya ya uzazi na kuwasisitiza kushiriki katika matukio mbalimbali yahusuyo afya kama huduma rafiki kwa vijana na siku ya afya ya kijiji “village health day” yanayoratibiwa na mradi wa Uzazi Salama.”
Wakuu wa Wilaya za Sumbawanga, Kalambo na NKasi (kushoto) wakiweka saini mkataba wa usimamizi wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) katika hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya “JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA” katika Mkoa wa Rukwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa pili toka kulia) akipewa maelezo ya kitaalamu juu ya matumizi ya vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi Salama na mmoja wa wawakilishi wa mradi huo (wa kwanza Kulia).
Baadhi ya Vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi salama Mkoa wa Rukwa kwa Ofsi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: VIWAVIJESHI VYAWATESA WAKULIMA WA MAHINDI MBEYA

MICHUZI TV: RAIS MAGUFULI: TUNATAKA TANZANIA IWE KAMA ULAYA

HOSPITAL YA WILAYA YA MBINGA INAKABILIWA NA CHANGAMOTO NNE

$
0
0

Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga Mkoni Ruvuma inakabiliwa na changamoto kubwa nne zinazopelekea kushindwa kutoa matibabu bora kwa wananchi. Akizungumza na Ruvuma TV on line Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo Dkt Nicholas Kapunga , amesema kwa sasa tiba wanazotoa haziwafikii walengwa ipasavyo hivyo anaiomba serikali isaidie kutatua changamoto hizo ili waweze kutoa huduma za matibabu bora kwa walengwa. Kwa undani wa habari hii tizama video yake. 

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM TAIFA AKUTANA NA KAMATI YA SIASA MKOA WA PWANI

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge  wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Francis Koka pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Kibaha mjini Bi. Azilongwa Bohari pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya utambulisho kama Mlezi wa Chama hicho mkoa wa Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Ramadhani Maneno (kulia) akimtambulisha Mlezi wa CCM mkoa huo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kujitambulisha rasmi kama Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Taifa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kujitambulisha rasmi kama Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha.

Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto

$
0
0


Mradi wa uzazi salama Mkoani Rukwa umekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi 211,145,850/= kwa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa ili kuvisambaza katika vituo 198 vya kutolea huduma za afya, ikiwa ni muendelezo wa jitihada na dhamira yao ya kuhakikisha wanashirikiana na Mkoa katika kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Mkoa.

Mradi huo unaoundwa kwa ushirikiano wa mashirika matatu ya Plan International Tanzania, AFRICARE na JHPIEGO kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada umekabidhi vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vifaa vya upasuaji kwa kinamama wajawazito, vifaa vya kumsaidia mtoto mchanga na mama kupumua, vifaa vya kuwasaidia watoto njiti, majokofu ya kuhifadhia damu na vifaa vya kufanyia tathmini ya hali ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanaratibu kufanyika kwa siku ya afya kwa mwaka mara moja kwa kila kijiji na kuwataka wakuu wa wilaya wasimamie zoezi hilo. Na kuwaomba wanaume, wazee na viongozi wote wa dini pamoja na vijiji kutambua jukumu la afya ya uzazi na mtoto pamoja na familia ni la wote na sio la kinamama na wanawake peke yao.

“Viongozi wa serikali katika ngazi za vijiji na kata wanao wajibu wa kuhakikisha akina mama wanahudhuria katika vituo vya afya pindi wanapojigundua ni wajawazito kwa huduma na ushauri wa kiafya. Tuwe mstari wa mbele kuelimisha wengine hasa vijana wetu kuhusu afya ya uzazi na kuwasisitiza kushiriki katika matukio mbalimbali yahusuyo afya kama huduma rafiki kwa vijana na siku ya afya ya kijiji “village health day” yanayoratibiwa na mradi wa Uzazi Salama.”

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa pili toka kulia) akipewa maelezo ya kitaalamu juu ya matumizi ya vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi Salama na mmoja wa wawakilishi wa mradi huo (wa kwanza Kulia). 
Baadhi ya Vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi salama Mkoa wa Rukwa kwa Ofsi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo. Wakuu wa Wilaya za Sumbawanga, Kalambo na NKasi (kushoto) wakiweka saini mkataba wa usimamizi wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) katika hafla fupi ya  uzinduzi wa Kampeni ya “JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA” katika Mkoa wa Rukwa.

Serikali Yaipongeza MUWSA kwa kuwa Mamlaka Bora ya Maji Mashariki na Kusini mwa Afrika

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof.Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuipongeza Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi  kuwa Mamlaka bora ya maji  Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika leo Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo  Joyce Msiru.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof.Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuipongeza Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi  kuwa Mamlaka bora ya maji  Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika leo Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Joyce Msiru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa  Mazingira Mjini Moshi  Joyce Msiru (Kushoto) akizungumza mara baada ya kupokea pongezi za Serikali kwa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi  kuwa Mamlaka bora ya maji  Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika leo jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo. (Picha na: Shamimu Nyaki - WHUSM)


MAVUNDE AFANYA ZIARA YA GHAFLA TIC KUFUATILIA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amefanya ziara ya ghafla kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwa lengo la kufuatilia maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambayo aliyatoa Desemba 4 mwaka huu.

Baadhi ya maagizo hayo ni pamoja na uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa wawekezaji kupitia Mfumo wa Mahala Pamoja 'One Stop Facilitaion Centre', ambapo Waziri Mkuu baada ya kupata maelezo kuna mambo hakukubaliana nayo na hivyo akatoa maagizo.

Hivyo Mavunde amefanya ziara ya ghafla TIC ili kujionea namna shughuli hizo zinavyoendeshwa hasa katika Idara ya Kazi. Akiwa TIC amezungumza na maofisa kutoka Wizara/Taasisi/Idara/Mamlaka mbalimbali wanaotoa huduma kwa wawekezaji ,kupitia mfumo wa Mahala Pamoja na kuwakumbusha kuwa wao ni sehemu ya uchakataji wa vibali na leseni mbalimbali za wawekezaji, hivyo waongeze kasi katika kutekeleza majukumu yao ili huduma husika zipatikane kwa wakati sahihi.

Aidha ,baada ya mazungumzo hayo Mavunde amefanya kikao kazi kati yake na Kamishna wa Kazi Tanzania Gabriel Malata, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe na Ofisa Kazi Mfawidhi ndani ya Mfumo wa Huduma za Mahala Pamoja TIC, Emiliana Rweyendela.Ziara ya Naibu Waziri inakuja takribani wiki mbili tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea TIC na kukutana na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TIC na kutoa maagizo ya kufanya maboresho mbalimbali ya utoaji wa huduma bora kwa wawekezaji ndani ya Mfumo wa Mahala Pamoja.

Imeelezwa kuwa tangu Waziri Mkuu atembelee TIC kituo hicho chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji kimefanya kikao na Kamishna wa Kazi Tanzania, Kamishna Mkuu wa TRA, Kamishna wa Uhamiaji Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kwa pamoja walikubaliana kuboresha mifumo ya utoaji wa vibali, kutoa elimu kwa umma juu ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kupata vibali husika na kufanya kazi kama timu ili kushauriana zaidi katika utoaji wa vibali mbalimbali kwa wawekezaji.

Pia kama sehemu ya kazi za kila siku, kituo kinaendelea kushughulikia changamoto za uwekezaji kwa kushirikiana na wadau husika ili kufikia lengo la kuwa na mazingira bora ya uwekezaji nchini yatakayowezesha kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya Wananchi na Taifa kiujumla.

WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA

$
0
0
KATIKA hospitali ya Muhimbili kuna moja ya wodi inayojulikana Sewa haji, mwanzilishi na mdhamini wa hospitali hiyo anajulikana kama Sewa Haji Paroo.

Sewa Haji Paroo raia wa India, alizaliwa mwaka 1851 na kufariki 1891 huko visiwani Zanzibar na kuacha historia kubwa katika maeneo ya Zanzibar na Bagamoyo kwa msaada aliokuwa anautoa kwa jamii hizo hasa kwa kujenga huduma za jamii kama shule, hospitali na visima.

Sewa Haji alikuja Tanzania mnamo mwaka 1851 huko Bagamoyo na mwaka 1897 aliweka makazi yake Zanzibar ambapo alifanya biashara na kuwa mmoja ya wafanyabiashara wakubwa visiwani humo.

Sewa Haji paroo ndiye mwanzilishi na ndiye aliyedhamini ujenzi wa hospitali ya Sewa Haji kama ilivyojulikana kwa kipindi hicho na kwa sasa inajulikana kama hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es saalam, hospitali hiyo ilikuwa ikitoa huduma kwa wananchi wa kipato cha chini bure kabisa na kwa sasa Sewa Haji ni moja moja kati ya wodi maarufu katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Pia Sewa Haji Paroo alidhamini miradi mingi zikiwemo shule, misikiti na miradi ya mingi ya kijamii huko Bagamoyo na alikuwa rafiki mzuri wa wakristo na kutoa misaada.

Hospitali ya taifa Muhimbili ilianza miaka ya 1910 hadi 1920 ikijulikana kama Sewa Haji na kufikia mwaka 1956 iliitwa hospitali ya Princess Magreth na baada ya uhuru 1961 ilijulikana kama Muhimbili hospitali na baadaye kuitwa Muhimbili medical centre mnamo mwaka 1976 na baadaye kuitwa Hospitali ya taifa Muhimbili.

WADAU WA JINSIA WAKUTANA MJINI MOROGORO KUFANYA MAPITIO SERA YA TAIFA YA JINSIA

$
0
0
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii inakutana na wadau wa masuala ya Jinsia kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Taifa ya Jinsia ili pamoja na mambo mengine iweze kuwa na masuala ya wanawake waishio vijijini lakini pia kuzingatia makundi mengine maalumu hususani vijana na watu wenye mahitaji maalum.

Akiongea wakati wakufungua kikao kazi na wadau wa sera ya jinsia kutoka Wizara za serikali na mashirika yasiyo ya Kiserikali Kaimu Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi Grace Mbwilo amewataka wadau hao kufanya mapitio ya sera hiyo lakini pia kuangalia namna bora ya kutatua changamoto zinazomkabili mwanamke wa kijijini.

Aidha Bi. Mbwiro pia amewataka wadau hao kuangalia masuala mengine katika jamii akisema ni mengi mno hivyo kuzingatia vipaumbele vya masuala ya jinsia kwa wanawake  akisema kundi hilo katika jamii bado linachangamoto ambazo zinalifanya kuendelea kubaki katika nyanja tofauti.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi Grace Mbwilo katikati akiongea na wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Taifa ya Jinsia leo Mkoani Morogoro.
 Wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Jinsia katika kikao  kikazi cha wadau wadau wa Jinsia kinachoratibiwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii leo Mkoani Morogoro.
 Wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Jinsia katika kikao  kikazi cha wadau wadau wa Jinsia kinachoratibiwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii leo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Jinsia katika kikao  kikazi cha wadau wadau wa Jinsia kinachoratibiwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii leo Mkoani Morogoro.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MSD NA AGA KHANI WAKUBALIANA KUFANYA KAZI PAMOJA

$
0
0


MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, wa Taasisi Aga Khan, Sulaiman Shahabuddin wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya Kiutendaji jijini Dar es Salaam Desemba 20 2018. Wanaoshuhudia (kulia) ni Meneja Msaidizi wa Kisheria wa Hospitali ya Aga Khan, Kieran Kitojo na Mwanasheria Mkuu wa MSD, Christopher Kamugisha. (Imeandaliwa na Robert Okanda)

MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya utiliaji saini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji na Taasisi ya Taasisi Aga Khan. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Hospital ya Aga Khan, Lucy Kwayu.
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, wa Taasisi Aga Khan, Sulaiman Shahabuddin wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wandamizi wa Taasisi waliohudhuria hafla hiyo.

RC Wangabo awatahadharisha wataogushi taarifa ili kupewa vitambulisho vya wajasiliamali

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewatahadharisha wafanyabiashara watakaogushi taarifa kwa nia ya kupatiwa vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.

Amesema kuwa jukumu lake ni kuvikabidhi kwa wakuu wake wa wilaya ili nao kuvifikisha kwa wakurugenzi na hatimae kuwafikia walengwa wa vitambulisho hivyo na kuongeza kuwa wajasiliamali waondoe shaka juu ya idadi ya vitambulisho hivyo kwani vikiisha vitaagizwa vingine na hakuna atakaekosa.

“20,000/= kwa kila kitambulisho, lakini kwa mtu yeyote yule ambae atakuwa “amefoji” ambae atapewa kitambulisho bila ya kustahili atanyang’anywa kitambulisho hicho na 20,000/= hazitarudi, kwahiyo nitoe angalizo kwa hawa wajasiliamali wadogo wadogo wazingatie hizo taratibu ambazo zimewekwa,” Alisisitiza.

Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vitambulisho hivyo 25,000, kwa wakuu wa Wilaya tatu za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi zenye halmashauri nne, hivyo kila halmashauri kupatiwa vitambulisho 6,250.
 Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (Kulia) akikabidhi vitambulisho vya wajasiliamali kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.
 Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (Kulia) akikabidhi vitambulisho vya wajasiliamali kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akisaini hati ya kupokea vitambulisho kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo muda mfupi kabla ya kupewa vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji isiyozidi shilingi milioni nne.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images