Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

LUKUVI ALIA HALMASHAURI KUSHINDWA KUSIMAMIA MABARAZA YA ARDHI YA KATA

0
0
Na Munir Shemweta, WANMM
Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema halmashauri zina wajibu wa kuayasimamia mabaraza ya ardhi ya Kata katika maeneo mablimbali nchini.

Kauli ya Lukuvi inafuatia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumeleza kuwa ofisi yake hairidhishwi na namna  Mabaraza ya Ardhi ya Kata yanayofanya kazi  na kubainisha kuwa baadhi yake yanaendeshwa na watu wasiokuwa na taluma ya sheria huku wakitoa hukumu za kisheria ambazo  baadhi yake hazieleweki.

Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kinondoni  wakati wa  mkutano wa kusikiliza migogoro ya ardhi kupitia Program ya Funguka kwa Waziri uliofanyika  uwanja wa shule ya msingi Bunju B jijini Dar es Salaam jana, Waziri Lukuvi alisema halmashauri kupitia kwa mwanasheria wake zinapaswa kujua maamuzi yote yanayotolewa katika Mabaraza ya Ardhi ya  Kata.

Alisema, pamoja na kilio cha wananchi wengi dhidi ya Mabaraza ya Ardhi ya Kata katika maeneo mbalimbali lakini upo utaratibu mzuri uliopangwa kuhusiana na Mabaraza hayo ingawa  yameachwa yajiendeshe yenyewe huku Halmashauri chini ya Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikiyaangalia bila kufuatiliwa.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kiondoni mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kuwasilisha migogoro yao ya ardhi  katika program maalum ya Funguka kwa waziri katika uwanja wa shule ya Msingi Bunju B.
 Mmoja wa wananchi wa Mabwepande akiwasilisha lalamiko lake la mgogoro wa ardhi kawa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika program maalum ya Funguka kwa waziri katika uwanja wa Shule ya Msingi Bunju B.

  Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuwasilisha malalamiko yao ya migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika program maalum ya Funguka kwa Waziri katika uwanja wa Shule ya Msingi Bunju B.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI

0
0
Na Tiganya Vincent, Tabora
WAJASIRIAMALI wadogo wadogo mkoani Tabora wameonywa kutotumia vitambulisho walivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuzia biashara za wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuwa chanzo cha ukwepeji kodi.

Onyo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akigawa vitambulisho 25,000 kwa Wakuu wa Wilaya saba za Mkoa huo na viongozi watatu wa Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora ikiwa ni uzinduzi wa zoezi hilo mkoani humo.

Alisema vitambulisho vilivyotolewa na Rais ni kwa ajili ya Wajasiriamali wadogo wadogo na sio vinginevyo na ambao ni wale biashara zao kwa siku zote 365 za mwaka mapato yao hayazidi shilingi  milioni nne.

Mwanri alisema ni kosa kuazimisha kitambulisho au kubeba bidhaa za wafanyabiashara wakubwa  na kuongeza kuwa atakayebainika atakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya Sheria ili achukuliwe hatua.

Aidha alisema Mkoa huo ulipatiwa vitambulisho 25,000 vilivyotolewa na Rais Magufuli hivi karibuni ambapo vimegawanywa kwa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Tabora na kila moja imepata vitambulisho 3125.
 Maandamano maalumu ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua rasmi ya kuwapatia vitambulisho yaliyoandaliwa na  Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora yakiingia kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora tayari kwa kugawiwa vitambulisho.
  Baadhi ya Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha)  kabla ya kuanza kugawa vitambulisho vilivyotolewa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wajasiriamali.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akimvisha kitambulisho Katibu Msaidizi wa Wajasiriamali Manispaa ya Tabora Ashura Rashid baada ya aaandamano maalumu ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua rasmi ya kuwapatia vitambulisho yaliyoandaliwa na  Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (wenye Tshirt ya Njano) akimkabidhi vitambulisho 6250 Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula (kushoto) kwa ajili kwenda kuwagawia Wajasiriamali wilayani kwake. Picha na Tiganya Vincent

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri Mhagama-Bilioni 16 zimetumika Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Kigoma na Dodoma.

0
0

Na. OWM, Kigoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji unaotekelezwa katika mkoa wa Kigoma na Dodoma, umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 16 hadi kufikia Desemba 2018.

Mradi huo ambao utekelezaji wake unajikita katika Uwekezaji na Biashara katika Halmashauri kupitia mfuko wa (SIFF), Kuimarisha minyororo ya thamani pamoja na kuimarisha majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, tayari umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara kwa Wakulima na wavuvi wa mkoani Kigoma.

Akiongea katika ziara yake mkoani Kigoma wakati wa kukagua shughuli za utekelezaji za Baraza la Taifa la Biashara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amefafanua kuwa Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na Mradi huo wameweza Kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji kwenye miradi midogo midogo inayochochea ongezeko la ajira na kipato.

“Nimetembelea Mwalo na Soko la Samaki la Kibirizi, hapa mkoani Kigoma nimeridhishwa jinsi Mradi huu ulivyoboresha miundo mbinu ya mwalo huu katika kuhakikisha wavuvi wanapunguza upotevu wa mazao ya samaki na dagaa. Niyaombe Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya yaendelee na mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha walengwa wa mradi huu wanaendelea kunufaika” Alisisitiza Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Biashara Manispaa ya Kigoma Ujiji, Festo Nashoni, juu ya Uboreshaji wa chanja za kuanika dagaa katika mwalo wa Soko la samaki la Kibirizi wakati akikagua shughuli za Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akiongea na wafanyabiashara wa Soko la Jioni la Mwanga, mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mfanyabiashara, Justina Damas, Soko la Jioni la Mwanga mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

MOHAMED ISSA 'BANKA' ARUHUSIWA KUANZA MAZOEZI BINAFSI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

Mchezaji Mohamed Issa 'Banka' ameruhusiwa kuanza mazoezi wakati akikaribia mwisho wa adhabu yake ya kufungiwa baada ya kubainika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya bangi. 

Banka baada kubainika kutumia dawa hizo alifungiwa kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Disemba 9,2017 na adhabu kumalizika Februari 8,2019. 

Pamoja na kuruhusiwa kuanza mazoezi Banka kucheza mchezo wowote ule zaidi ya kufanya mazoezi. Mchezaji huyo alifungiwa na Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Africa (RADO). 

Banka alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili katika dirisha la usajili la mwezi June akitokea timu ya Mtibwa Sugar lakini hakuweza kushiriki kwenye mchezo wowote kutokana na kufungiwa kutokushiriki masuala ya kimichezo ikiwemo kufanya mazoezi sehemu atakayoonekana na watu.Adhabu yake inatarajiwa kumalizika mwezi Februari mwakani na matarajio yake ni kujiunga na timu yake mpya.

MAJIBU YA RAIS MAGUFULI KWA JOHN MNYIKA

0
0
*Amuuliza anataka demokrasia ya aina gani?
*Amshangaa kwa kushindwa kusema ahsante 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameamua kujibu Mbunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam John Mnyika baada ya kutoa malalamiko ya kudai kwamba hivi sasa demokrasia imebanwa.

Mnyika baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara kutoka Kimara Stop over hadi Kibaha mkoani Pwani uliofanyka leo alitumia nafasi hiyo kutoa kilio chake kwa Rais Magufuli kudai demokrasia.

Hivyo Rais Magufuli pamoja na mambo mengine aliamua kumjibu Mnyika na kumuuliza anataka demokrasia ya aina gani huku akifafanua demokrasia ipo na ndio maana hata Mnyika amepata nafasi ya kuzungumza mbele yake na kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo wanachama wa vyama vyote wapo na wamechanganyika bila tatizo lolote.

"Tunafahamu hata Meya wa Jiji la Dar es Salam ni wa upinzani lakini anajua kuwa Ilani inayotekelezwa ni ya CCM.Tungekuwa wabaya tusingefanya mambo ya maendeleo Dar es Salaam ambako watu walikukataa lakini bado Serikali inaleta maendeleo bila kujali.

"Mnyika kero yake kubwa ilikuwa maji kila siku lakini Serikali imetekeleza kwa kutumia mabilioni ya fedha.Nilitegemea anaposimama hapa angesema ahsante kwa Serikali kwa kutatua changamoto ya maji lakini ameshindwa na sasa anazungumzia demokrasia,"amesema.Rais Magufuli wakati anamjibu Mnyika ameendelea kueleza kuwa "Mnyika anataka demokrasia ya aina gani, amekuja hapo na kwenye mkutano ambao Mwenyekiti wake ni wa CCM, vyama vyote vipo, anataka demokrasia ya aina gani?

"Amekuja hapa amezungumza yote ambayo anayataka sasa anataka demokrasia ya aina gani.Demokrasia ndio hii amezungumza lakini 
demokrasia ya kufanya maandamano na fujo hiyo kwangu hapana.Kwanza demokrasia nzuri imehamia Dodoma.Hata kuwa bungeni na kisha kufunga mdomo nayo ni demokrasia,"amesema.

Rais Magufuli amesema Serikal anayoingoza ni kwa ajili watu na amekabidhiwa kwa ajili ya kuwatumikia WAtanzania na hivyo ataendelea kuleta maendeleo na kwamba huu ni wakati wa kuitengeneza Tanzania yetu.

"Na katika kipindi hiki hizi fedha ambazo leo zinatumika kutengeneza barabara siku za nyuma zilikuwa zinakwenda sehemu nyingine.Msiniulize ziliuwa zinakwenda wapi?Tukazibi mianya ya upotoaji wa fedha . Tulipoingia tulianza kwa kuongeza ukusanyaji kodi na tukarekebisha bajeti ambapo fedha za maendeleo ni asilimia 40 wakati zamani ilikuwa asilimia 20,"amefafanua Rais Magufuli.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Kibamba  John Mnyika (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

UJENZI WA OFISI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE, IHUMWA, DODOMA WASHIKA KASI

0
0
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo kwenye Mji wa Kiserikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma. Ujenzi wa Ofisi hizo zinatarajiwa kumalizika ifikapo mwezi mosi mwakani. 
Mkandarasi Mkuu wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akielezea maendeleo ya ujenzi huo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo walitembelea eneo hilo 
Juu na Chini sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Mkandarasi Mkuu alipokuwa akiwaelezea maendeleo ya ujenzi huo. 
Juu na Chini Wakuu wa Idara na Vitengo wakijionea maendeleo ya ujenzi 

USILALAMIKE VYUMA VIMEBANA...FANYA KAZI ILI UVIBANUE -RAIS DK MAGUFULI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika kuwa vyuma vimebana kwani ukifanya kazi chuma hakitakubana bali utavibanua.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara inayoanzia Kimara hadi Kibaha mkoani Pwani ambapo Rais aliamua pia kuzungumzi wanaolalamika vyuma kukaza.

"Tusilalamike vyuma vimebana kwani ukifanya kazi vyuma hakitakubana utavibanua.Sasa watu watu wanatumia maneno ya kawaida vyuma vinabana kila wakati utasikia wanasema vyuma vimebana .Lazima niwaambie ukweli usipofanya kazi vitabana kweli kweli hadi utachoka mwenyewe, hakuna vya bure...

"Huo ndio ukweli ninafuu niwaeleze hata kwenye maandiko matakatifu yanasema asiyefanya kazi na asile na usipokula utakufa.Eti hakuna atakayekufa na njaa.Mimi nawaambia usipofanya kazi utakufa njaa kwani hakuna hakua vya bure.Hili la vyuma kukaza ni mambo ya siasa tu na bahati nzuri Watanzania wameshaelewa sana.

Wakati huo huo Rais Magufuli amesema kuwa hii seriakali si katali ila ni sehemu ya maendeleo ya watanzania, hivyo amewaomba Watanzania wa vyama vyote kujiamini kwamba tunaweza japo kwa miaka mitano na atakapomaliza muda wake waendelee na 
kutojiamini."Watazania tumechezewa na tumeliwa mno".
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

Cuba kuendelea kuimarisha huduma za kibingwa Muhimbili

0
0
Serikali ya Cuba imeeleza azma yake ya kuendelea kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika kutoa huduma bora za kibingwa sambamba na kuwajengea uwezo watalaam wa Muhimbili. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Cuba nchini Lucas Domingo Hernandez Polledo ambaye ameambatana na ujumbe kutoka Serikali ya Cuba ukiongozwa na Naibu Waziri wa kilimo wa nchi hiyo, Jose Miguel Rodriguez de Armas.

Ujumbe huo umetembelea Muhimbili leo kwa lengo la kuangalia utendaji kazi wa hospitali pamoja na utendaji kazi wa watalaam wa afya 17 wa nchini Cuba ambao wapo Muhimbili kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma. Awali, wakiwa katika mazungumzo na uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Balozi Polledo ameupongeza uongozi wa Muhimbili kwa utoaji bora wa huduma za matibabu na kueleza kuwa amekua akipata mrejesho mzuri kutoka kwa wataalam wao na kusisitiza kwamba ushirikiano huo haunabudi kudumishwa.

 “Tunapenda ushirikiano huu uendelee kwa faida ya nchi zote mbili na endapo mkihitaji tuwaongezee wataalam wengine zaidi tupo tayari kuwapatia,” amesema Balozi Polledo. Balozi Polledo pia ametumia fursa hiyo kuwataka wataalam hao wa Cuba kuzidisha juhudi katika utendaji kazi kwa kuwa uwepo wao Muhimbili unawakilisha Serikali ya Cuba hivyo wanapaswa kuwa mabalozi wazuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Miquel Rodriquez de Armas wakati walipoitembelea hospitali hiyo kuona huduma mbalimbali za matibabu zinazotolewa na wataalam wa nchi hiyo kwa kushirikiana na wataalam wa Muhimbili. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Muhimbili, Makwaia Makani, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dkt. Sufiani Baruani, Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mohamed Kamal Mohamed, Kaimu Mkurungezi wa Huduma za Uuguzi  Muhimbili, Sista Zuhura Mawona na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. John Rwegasha.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mh. Miquel Rodriquez de Armas, Afisa katika Ubalozi wa Cuba nchini Tanzania, Sultan Hamud Said, Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo na wengine ni ujumbe wa Naibu Waziri huyo kwa pamoja wakimsikiliza Prof. Museru.
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Lucas Domingo Hernandez  Polledo akizungumza na baadhi ya wataalam wa Cuba, huku akiwataka kuongeza bidii zaidi ili kutoa huduma bora za kibingwa katika hospitali hiyo. Wengine ni wataalam wa afya wa MNH.
Daktari Bingwa wa Mapafu na Wagonjwa Mahututi, Dkt. Paulina Chale wa Muhimbili akizungumza na Balozi Lucas Domingo Hernandez Polledo (wa nne kulia) wakati alipotembelea wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum. Wengine ni baadhi ya wataalam wa Muhimbili na  Cuba.
Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Miquel Rodriquez de Armas akisisitiza jambo wakati akizungumza na wataalam kutoka Cuba ambao wanashirikiana na wataalam wa Muhimbili kutoa huduma za matibabu katika hospitali hiyo. Kushoto ni Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Muhimbili, Makwaia Makani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwa katika picha ya pamoja, Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Miquel Rodriquez de Armas (kushoto) na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo (kulia). Wengine ni baadhi ya wataalam wa Muhimbili na maofisa walioambatana na ujumbe huo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV:Waitara awakana wapinzani,ampongeza Rais Magufuli

RAIS DKT.MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI UPANUZI WA BARABARA YA KIMARA – KIBAHA

0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata Utepe  na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai mara baada ya kufunua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Roberth Mfugale akitoa maelezo ya mradi wakati wa hafla  ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Kibamba  John Mnyika (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Ubungo Said Kubenea (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

WANACHAMA NANE YANGA WACHUNGUZWA, NI KUHUSU UCHAGUZI WA JANUARI 13

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo ametaja majina nane ya wanachama ya Yanga wanaodaiwa kuwakwamisha uchaguzi wa Yanga ambao umepangwa kufanyika Januari 13.

Akitoa taarifa kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harisson Mwakyembe, Singo amesema kuwa Waziri alipokea majina ya watu wanaosababisha kukwamishwa kwa uchaguzi huo na wamekuwa wanafanya vikao vingi vya siri ili kuhakikisha haufanyiki.

Amesema, majina hayo yamefikiwa kwa Waziri na raia wanaopenda soka liende mbali na liwe na maendeleo na tayari majina hayo yamepelekwa kwenye vyombo vya usalama ili wafanye uchunguzi na wakibainika wachukuliwe hatua.

"Waziri umeyachukua majina hayo na kuyapeleka katika vyombo husika vya serikali na kama watabainika ni kweli hatua kali zitachukuliwa dhidi yao," amesema Simgo.Singo amesisitiza kuwa, tayari kauli ya mwisho ya Serikali wameshaitoa ya Uchaguzi wa Yanga ufanyike Januari 13 sasa wanachama hawa wanakuwa wanapinga suala hilo wakidai kuwa hawautambui uchaguzi huo kutokana na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira Nchini (TFF) na wakisisistiza kuendelea kumtambua aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji.

Majina ya watu hao yaliyowekwa hadhani ni pamoja Mustapha Mohammed, Edwin Kaisi, Said Bakari, Shaban Omary, Kitwana Kondo, Boazi Ikupilika, Bakiri Makere na David Sanare.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo

MAJALIWA AKUTANA NA BODI YA TCCIA PIA AKUTANA NA MAWAZIRI PAMOJA KAMISHINA WA UHAMIAJI NA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Kazi alichokiitisha cha kujadili namna ya kuondoa kero zinazowapata wawekezaji  kuhusu upatikanaji wa vibali vya Kazi na Uhamiaji. Kikao  hicho kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Desemba 19, 2018, kiliwahusisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni (watatu kushoto) ,  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,  Anthony Mavunde (watatu kulia), Kamishina wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala (wapili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geofrey Mwambe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya TCCIA, Ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Desemba 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB achaguliwa kuwa mwenyekiti wa umoja wa Mabenki Tanzania

0
0
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernerd Kibese (wa pili kulia) akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Mabenki Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartted , Sunjay Rughani, na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Tusekelege Mwaikasu-Jounde.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernerd Kibese akifurahi jambo na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartted , Sunjay Rughani. Katikati ni Mwenyekiti Mpya wa Umoja huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela 
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernerd Kibese akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanachama wa Umoja wa Mabenki Tanzania, baada ya kikao chao kilichofanyika jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Katika kikao hicho kulifanyika uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu wake ambapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliibuka mshindi na kuchukua kijiti cha Mwenyekiti wa Umoja huo, huku nafasi ya Makamu ikichukuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartted , Sunjay Rughani.

HOTUBA YA RAIS DKT.MAGUFULI WAKATI WA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI BARABARA YA KIMARA - KIBAHA. KM 19.2

MAGAZETI YA LEO AL-HAMISI DESEMBA 20.2018


Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy

0
0
Na Grace Michael, Nachingwea

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa mpango wa Ushirika Afya ndio njia pekee na ya kisasa inayomwezesha mkulima kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote na kuepukana na upotevu wa fedha nyingi kwa kulipia gharama za matibabu.

Amesema kuwa ili mkulima aweze kunufaika na fedha anazozipata kutokana na kuuza mazao yake ya biashara ni lazima awe na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Ameyasema hayo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma pamoja na uhamasishaji wa wananchi na wakulima kujiunga na mpango wa Ushirika Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu kwa gharama nafuu.

“Ndugu zangu wana Nachingwea, nafahamu kabisa mmeweka mipango mingi kwenye fedha zenu mtakazopata kutoka kwenye mazao mliyouza lakini niwaombe sana katika vipaumbele vyenu suala la Ushirika Afya liwe ni miongoni mwake, kuwa ndani ya mpango huu kunakusaidia wewe na familia yako kutokupoteza fedha zako unapopatwa na magonjwa,” alisema Mhe. Ummy.

Alifafanua kuwa gharama atakayotumia mkulima huyo kujiunga na Ushirika Afya ni ndogo sana ikilinganishwa na kugharamia huduma za matibabu kwa fedha taslimu hali ambayo imesababisha wananchi wengi kuingia kwenye umasikini kwa kuuza mali zao ili wapate fedha za kujitibia. 

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi fomu 1,000 kwa Kiongozi wa Vyama Vya Ushirika wilaya ya Nachingwea.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi kadi kwa Mwanaushirika aliyejiunga na mpango wa Ushirika Afya.
 Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi. Rukia Muwango akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Benard Konga wakifuatilia maelezo ya Mhe. Waziri.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mhe. Hassan Masala.
 Wananchi wilayani Nachingwea wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akielezea upatikanaji wa huduma za matibabu.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Zaidi ya wanafunzi 4,000 hatarini kukosa masomo wilayani Ilemela

0
0

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG.


Zaidi ya wanafunzi 4,000 waliohitimu darasa la saba mwaka huu na kufaulu, wako hatarini kukosa fursa ya kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.


Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula aliyasema hayo jana wakati akipokea mifuko 100 ya saruji kutoka benki ya Diamond Trust (DTB).


Dkt. Mabula alisema wanafunzi 8,350 wamefaulu mtihani wao wa darasa la saba lakini kuna upungufu wa vyumba 84 vya madarasa hivyo wenye uhakika wa kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza ni wanafunzi takribani 4080. Wilaya ya Ilemela ilishika nafasi ya kwanza kwa ufaulu mkoani Mwanza na kitaifa nafasi ya sita.


Hivyo Dkt. Mabula alisema mifuko hiyo ya saruji kupitia taasisi yake ya The Angeline Foundation inayoshirikiana vyema na Halmashauri ya Ilemela, itasaidia kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha wanafunzi waliofaulu wanapata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza ambapo aliwahimiza wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo.


Naye Meneja wa DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor alisema benki hiyo itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii katika Mkoa Mwanza hususani katika sekta ya elimu na afya.

Kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu, Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor, Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula pamoja na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita.
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula akishiriki zoezi la kupanda miti iliyotolewa na Benki ya "DTB" katika Shule ya Msingi Kitangiri C
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu (kushoto), Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor ( wa pili kulia) na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini
Benki ya Diamond Trust (DTB) yamuunga mkono Mbunge wa Nyamagana

MICHUZI TV:Shangwe za wananchi kumpongeza Rais Magufuli, upanuzi wa barabara kimara-kibaha hapo jana.

TAA YAAHIDI KUBORESHA HUDUMA KUANZIA JANUARI 2019

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, ameahidi kufanya Maboresho makubwa katika Miundombinu ya Viwanja vya Ndege Tanzania na katika kuhamasisha kasi ya utendaji ya wafanyakazi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.

Hayo ameyazungumza mbele ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu katika jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Awali Waziri Kamwelwe alianzia ziara yake Katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe na kubaini kwamba njia ya kuruka na kutua ndege imejegwa chini ya kiwango na mkandarasi lakini pia alipotua JNIA alibaini pia baadhi ya changamoto.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Kamwelwe ametoa maagizo kwa TAA kwamba kuanzia Januari mwakani kuwe na mabadiliko katika namna ya utendaji.
“Nawaomba ndugu zangu kuanzia Januari mwakani mbadilike na kama mtu hata badilika basi tutamtoa. Malalamiko ya watu mimi nayapokea na ninayafanyia kazi, kwa maana hiyo ni vyema pia muyafanyie kazi”, alisema Mhandisi Kamwelwe.  
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea kukagua miundombinu mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

2-min
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na Menejimenti na Waandishi wa Habari baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela.
3-min
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) jana akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya inayotoa huduma kwa abiria na mizigo ya Swissport Tanzania, Bi. Sarah Mlawa (kushoto) na Fliora Temba, alipokuwa akikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
4-min
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) akimsikiliza Msimamizi Kitengo cha Mitambo, Bw. Gregory Kosamu (wa pili kushoto) aliyekuwa akielezea mifumo ya Kiyoyozi ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Roichard Mayongela na kushoto ni Kaimu Meneja Matengenezo na Huduma za Kiufundi, Bi. Diana Munubi.

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images