Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

Shonza awataka wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuimarisha Umoja wa Jumuiya

$
0
0


.
Na Anitha Jonas,Dodoma

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki wanaoshiriki Mashindano ya vyuo vikuu Kanda ya Afrika Mashariki kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu katika Michezo.

Mheshimiwa Shonza ametoa tamko hilo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mashindano hayo yatakayo dumu kwa wiki mbili nchini ambapo mashindano hayo yamehusisha vyuo takribani ishirini huku lengo la mashindano likiwa ni kuimarisha Umoja na Ushirikiano kwa wanachama wa umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

‘’Ninaimani na waamuzi watakaosimamia michezo yote katika mashindano haya kuwa watatenda haki na pale mtakapoona mwamuzi hakutenda haki basi kateni rufaa badala ya kuleta migogoro katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,’’alisema Mhe.Shonza.Kwa upande wa Mlezi wa Umoja wa Shirikisho la Michezo kwa Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Elifas Bisanda aliupongeza uongozi Chuo Kikuu cha Dodoma kwa maandalizi mazuri waliyofanya ili kufanikisha mashindano hayo ya Kimataifa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kanda Afrika Mashariki.

Pamoja na hayo nae Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Prof.Ahmed Ame aliwataka wanamichezo hao pamoja na kuja kushiriki mashindano hayo mara badaa ya mashindano wasisite kutembelea vivutio mbalimbali vilivyoko nchini hapa ikiwemo kutembelea vivutio kama mbuga za wanyama pamoja na Michoro ya Kondoa Irangi.
 
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiwataka wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki waliyoshiriki Mashindano ya Michezo ya Umoja huo kuimarisha Umoja na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alipokuwa akifungua Mashindano Kumi na Moja ya vyuo vya nchi wanachama leo jijini Dodoma(kushoto ) Rais wa Shirikisho hilo la Michezo kwa Vyuo Vikuu Vya Afrika Mashariki Cyriaco Kabagambe.
PIX 2
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyevaa tisheti ya kijivu na koti nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na wataribu wa mashindano hayo leo jijini Dodoma mara baada ya ufunguzi wa mashindano ya Kumi na Moja ya Michezo kwa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki,aliyevaa track suit nyeusi  ni Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Tafiti za Kisayansi Burundi Mhe.Theophile Ndarufatiye.
PIX 3
Wanamichezo ambao ni wanafunzi  kutoka  Vyuo Vikuu nchini Burundi wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati ufunguzi wa mashindano ya Michezo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
PIX 4
Wanamichezo ambao ni wanafunzi  kutoka  Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza hayupo pichani wakati ufunguzi wa mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo jijini Dodoma.


NKANA FC KUTUA LEO JIONI, SIMBA KUBADILI KIKOSI DHIDI YA KMC KESHO

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kikosi cha Nkana Fc 'The Devil' kinatarajia kutua leo usiku kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kimataifa wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya Simba utakaochezwa siku ya Jumapili Desemba 23 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa. 

Katika mchezo wa kwanza wa timu hizo uliishia kwa Simba kufungwa goli 2-1 uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Zambia. Taarifa ya kuwasili kwa kikosi hicho imetolewa na Ofisa Habari wa Klabu ya Simba Hajji Manara kuwa Nkana wataingia nchini usiku wa leo wakitokea Zambia kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano. 

"Nkana FC wataingia leo usiku wakitokea kwao Zambia kuja kuwakabili Simba kwenye mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika na watakuja kwa usafiri wa shirika la ndege la Kenya,kwahiyo leo usiku ndiyo watatua pale Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere," alisema Manara. 

Nkana ambayo inatumikiwa na mchezaji wa kitanzaia Hassan Kessy inatua kucheza mchezo huo wa marudiano ikiwa tayari na mtaji wa ushindi wa bao 2-1 waliouvuna kwenye mchezo wa kwanza waliocheza wakiwa nyumbani wiki iliyopita. Katika mchezo huo, Simba wanatakiwa wapate ushindi wa goli 1-0 au zaidi ili kuweza kuingia hatua ya makundi ya Klabu bingwa Afrika ila sare yoyote inamuondoa Simba kwenye michuano hiyo na kushuka mpaka Kombe la Shirikisho Afrika. 

Mbali na hilo Uongozi wa Simba umesema kuwa utabadilisha kikosi kitakachovaana na wapinzani wao KMC kesho katika uwanja wa Taifa ili kuwapa nafasi wachezaji wengine kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Nkana FC ya Zambia.Simba kesho wanakibarua cha kucheza na KMC katika mchezo wa ligi kuu ikiwa ni kiporo chao kutokana na kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Manara amesema wanatambua wana kazi nzito ya kutetea ubingwa na kuweza kusonga mbele kwenye hatua ya makundi hivyo wamejipanga kuweza kupata matokeo."Tuna kazi ya kucheza na KMC kesho, tunawaheshimu wapinzani wetu na tunatambua ushindani uliopo ila tumejipanga kupata matokeo katika mchezo huo na tutabadili kikosi chetu.

"Tutawapa nafasi wachezaji wetu kwenye kikosi ili wengine waendelee na maandalizi dhidi ya Nkana FC ya Zambia, sapoti ya mashabiki ni muhimu katika hili," alisema.

Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara

MOMBO NA UTAMU WA NYAMA CHOMA YA MBUZI

$
0
0


Mombo ni eneo maarufu ambalo kwa sasa limezidi kujizolea sifa na umaarufu mkubwa kwa kuchoma nyama ya mbuzi, ambapo wasafiri wengi wanaotumia barabara kuu ya Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Kilimanjaro,Arusha wasafiri huwa wakisimama eneo hili na kupata nyama choma kama inavyooneka pichani, wauzaji wakiandaa nyama hiyo huku baadhi ya wasafiri wakijisevia.

WIMBO WA MWANZA WAWAPONZA DIAMOND NA RAYVAN WAFUNGIWA KWA MUDA USIOJULIKANA

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limetangaza kumfungia mwanamuziki Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) na Raymond Mwakyusa (Rayvan) kutokana na kitendo chake cha kupuuzia.

Basata imesema Diamond na Rayvan wamepuuzia na kuendelea kuutumia wimbo wa “Mwanza” maarufu kama Nyegezi katika shoo zake za Wasafi Festival na kuonesha dharau na  utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri.

Katika barua iliyotolewa leo mapema, Basata wameeleza pia kuwa wamewafungia wasanii hao kutokufanya shoo ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichojulikana kuanzia Desemba 18 2018.

Pamoja na hayo Basata wamefuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival kutokana na ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Utaratibu katika uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini.

SERENGETI BOYS KUSHIRIKI MASHINDANO NCHINI UTURUKI

$
0
0
TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inatarajia kushiriki mashindano maalumu ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) U17 mjini Antalya nchini Uturuki Februari mwakani.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Miguu Afrika (CAF) kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Ulaya UEFA yataanza Februari 22 hadi Machi 2, mwakani na yatashirikisha jumla ya timu 12 kutoka Afrika na Ulaya. 

Mbali na Serengeti Boys nchi nyingine za Afrika zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Angola, Morocco, Cameroon, Uganda, Nigeria, Senegal na Guinea ambazo zitaungana na timu 4 kutoka Bara la Ulaya. ‬Serengeti Boys itakwenda kwenye michuano hiyo ikitoka kutwaa ubingwa wa michuano ya U17 Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa penalti 6-5 dhidi ya Angola kufuatia sare ya bao 1-1, kwenye mchezo wa fainali juzi mjini Gaborone nchini Botswana. 

Katika dakika 120 za mchezo huo, Angola walitangulia kwa bao la Morais kabla ya Tanzania kusawazisha kupitia kwa Kelvin Pius dakika ya 78.Na baada ya mchezo huo, Nahodha wa Tanzania, Michael Morice alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi. Tanzania iliyo chini ya kocha Oscar Milambo ilifika hatua hii kwa ushindi wa matuta pia, ikiitoa Zambia kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 pia. 

Awali, katika mechi za Kundi B, Serengeti Boys ilizifunga Malawi 2-1 na Afrika Kusini 2-0 baada ya kufungwa 2-0 na Angola, hivyo kufanikiwa kuingia Nusu Fainali. Kikosi cha Serengeti Boys kinachojiandaa kwa fainali za Afrika za U17 Mei mwakani ambazo watakuwa wenyeji katika Jiji la Dar es Salaam. 
Nahodha wa timu ya Vijana Serengeti Boys Michael Morice akikabidhi kombe kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya U17 Kusini mwa Afrika (COSAFA) walipowasili Uwanja wa ndege jana. 
Wachezaji Michael Morice na Kelvin John wakiwa na tuzo zao.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

RC Wangabo Atoa Tahadhari Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kalambo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa tahadhari kwa uongozi wa wilaya ya Kalambo juu ya matumizi na ubora wa hospitali inayotarajiwa kujengwa katika wilaya hiyo ili kusijirudie makosa yaliyofanyika wakati wa ujenzi wa vituo vya afya vinavyoendelea ikiwemo kuchelewesha malipo kwa mfundi pamoja na kuachana na mafundi wasumbufu wanaochelewesha ujenzi.

Akitolea mfano wa ujenzi wa kituo cha afya cha Legeza Mwendo kilichopewa Shilingi milioni 700 na hatimae kufanikiwa kujenga majengo tisa, hivyo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa usimamizi wa mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanazitumia vyema Shilingi bilioni 1.85, fedha ambazo zimetengwa na serikali kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya.

“Utoaji wa fedha ofisi yako Mkurugenzi mmekuwa mnasuasua, malipo mnasingizia sijui mifumo mifumo, watu hawalipwi kule (kituo cha afya) Mwimbi imekuwa tabu karibu mwaka mzima, hata kule (kituo cha Afya) Legeza mwendo ilikuwa hivyo hivyo, nisingependa hili litokee, malipo lazima yaende vizuri, hata wale mama lishe walikuwa wanadai hawalipwi,” Alisisitiza.

Alisema kuwa kutokana na fedha hiyo iliyotengwa angependa kuona majengo mazuri yenye viwango ili kuupendezesha mji wa Matai ambao ni makao makuu ya wilaya hiyo.Maeyasema hayo katika ziara yake ya kuona maazimio ya eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kalambo ambapo kumekuwa na mvutano juu ya eneo la kuijenga hospitali hiyo huku maeneo kadhaa yakihitaji fidia wakati maelekezo ya fedha hizo si kwa nia ya kulipa fidia bali ni ujenzi huku zikiwa zimebaki siku chache Ofisi ya Rais TAMISEMI kurudisha fedha zake endapo fedha hizo zitakuwa hazijaanza kutumika kwaajili ya ujenzi uliokusudiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mh. Daudi Sichone alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa msukumo wake wa kusimamia miradi hiyo ya maendeleo pamoja na kuwasukuma wafanye haraka kutafuta ufumbuzi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya ili wananchi waweze kupata huduma bora na kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo (aliyetupa mgongo) akiangalia eneo ambalo linatarajiwa kujengwa hospitali ya Wilaya ya Kalambo. 

MICHUZI TV: Irene Uwoya afichua siri ya mafanikio yake,ahidi kusomesha albino


MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU WAKABIDHI SETI ZA JEZI KWA MICHUANO YA JIMBO CUP

$
0
0


IMG_4071
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akimkabidhi Seti ya Jezi Mwenyekiti wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Said Hassan, kwa ajili ya Michuano ya Vijana Mpira wa Miguu Jimbo la Tunguu, vilivyotolewa na Mbunge na Mwakilishi. kushoto Katibu wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Ndg. Ali Khatib Kisu, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4080
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akipata maelezo ya Bidhaa zinazotengenezwa na Vijana wa Kikundi cha Maendeleo cha Vijana Ubago Bi. Hawa Ali Mzee, akitowa maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Vijana hao, akiangali Shampoo wakati akitembelea kikundi hicho,kushoto Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Tunguu Ndg.Said Hassan.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4081
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, akiangalia Shampoo inayotengenezwa na KIkundi cha Vijana cha Maendeleo Ubago, akipata maelezo kutoka kwa Katibu Hamasa wa Kikundi hicho Bi. Hawa Ali Mzee, wakati alipotembelea kikundi hicho Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4100
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akiangalia moja ya nguo zinazozonwa na Kikundi cha Vijana na Maendeleo Ubago, wakati alipowatembelea Vijana hao katika Kituo chao kuangalia shughuli wanazozifanya za utengenezaji wa Shampoo, Sabuni. Lotion na mafuta ya mgando na ushoni wa nguo.(Picha na Othman Maulid)

MICHUZI TV: VIJANA WA KITANZANIA WAPATA JUKWAA LA KUUNGANISHWA NA WAWEKEZAJI

MICHUZI TV : Chaz Baba: Alikiba amenishangaza sana siku ya ndoa yangu...

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu UDOM Prof Mubofu

MHANDISI KAMWELWE ALALAMA NA UTOAJI HUDUMA WA ATCL, VIWANJA VYA NDEGE NCHINI

$
0
0
*Ameagiza ifikapo January 2019 hataki kuona matatizo hayo, ataka wajirekebishe.

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe amelalamikia huduma zinazotolewa kwa Wateja na Kampuni ya Ndege (ATCL) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini.

Akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya, Mhandisi Kamwelwe amesema huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo zimekuwa zikilalamikiwa na Abiria ambapo ametolea mfano uwepo wa Joto kali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Terminal 2).

Ameagiza kuwaondolea usumbufu Abiria wanaosafiri ambapo amesema abiria hao lazima wasikilizwe uhitaji wao.Pia ametaka kuendeleza ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Songwe kutokana na kutoridhishwa na ujenzi wa Kiwanja hicho kinachotegemewa kutua Ndege mpya. Pia kuhusu sakata la Fastjet, Mhandishi Kamwele amesema kuwa Kampuni hiyo tayari ilipewa agizo la kujirekebisha hivyo walipewa siku 28 ambapo zikiisha imeelezwa hatowezo kufanya biashara hapa nchini, na hatoweza kufanya biashara sehemu nyingine mpaka alipe madeni ya Serikali.

Ameagiza Rubani wote na Watendaji wa SUMATRA kutokwenda likizo kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuhakikisha uhitaji bora wa usafiri kwa abiria. Amesema hakuna atakayeongeza bei ya nauli katika usafiri.Amesema Ndege za AirBus za ATCL kuwasili Desemba 23, 2018 kama ratiba haijabadilika ambapo amesema tayari imetuma Crew wakiwemo Rubani nchini Canada kwa mafunzo. Uwanja wa Ndege Terminal 3 kukamilika mwezi May mwakani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, Richard Mayongela amemuahidi Waziri Kamwele kushughulikia changamoto zote ambazo zimelalamikiwa kwa Mamlaka hiyo katika utoaji huduma ifikapo January Mosi, 2019 ka ilivyoagizwa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandishi Isack Kamwelwe akizungumza na Mejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini baada yakurejea kutoka kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Richard Mayongela akitoa ufafuzi kwenye kikao cha pamoja baina ya Menejimenti ya Mamlaka hiyo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo ameahidi kutatua changamoto ambazo zimetajwa katika Mamlaka hiyo.

Sehemu ya Menejimenti ikimsikiliza Waziri alipokuwa anazungumza.

EXCLUSIVE MICHUZI TV : Madabida alonga kusamehewa na wenzie watatu...

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 19,2018


WAZIRI MBALAWA AKAGUA MIRADI YA MAJI WILAYANI BAGAMOYO

$
0
0
Na  Karama Kenyunko Globu ya jamii.
SERIKALI  imesema hivi karibuni itahakikisha inamaliza kabisa tatizo kubwa la ukosefu wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani linatokana na ukosefu wa miundombinuz ya usambazaji.'
'
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema hayo leo Desemba 18.2018 alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Waziri Mbarawa pia amewahakikishia wakazi wa Kiembeni, Kata ya Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani kuwa watapelekewa majisafi na salama na mpaka sasa tayari mradi utakaogharimu Sh. Bilioni 116 uko tayari na umeanza katika eneo hilo.

amesema, katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwasasa uzalishaji wa maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam umefikia lita bilioni 14 kwa mwezi.

Amesema kufuatia tatizo hilo la usambazaji ndio maana serikali kupitia mradi wake wa tanki la bagamoyo ulioanza mwaka jana iliamua kujenga tanki la maji la lita Bil. 6 ambalo litasaidia katika usambazaji kwa maeneo yote ya Bagamoyo na vitongoji vyake  ambao unatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Waziri Mbarawa ameongeza kuwa, kwa siku jiji la Dar es Salaam lina uwezo wa kuzalisha lita milioni 502 za maji na mahitaji kwa mwezi ni lita bilioni 14, lakini changamoto ni usambazaji.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo juu mradi mkubwa wa maji wa ujenzi wa Tanki ambao utakapoisha utamaliza kero zote za maji Katika Wilaya ya Bagamoyo mjini na vitongoji vyake, wakati wa Wizara ya kukagua miradi ya maji Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani iliyofanyika leo Desemba 18.2018 mradi huo ulioanza mwanzoni mwa mwaka jana unatarajiwa kumalizika mwaka huu mwishoni. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA CBA NA VODACOM WAKABIDHI ZAWADI ZA BAJAJI 5 KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHINDA NA M- PAWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
BENKI ya CBA kwa kushirikiana kampuni ya simu ya Vodacom wamekabidhi zawadi kwa washindi wake wa promosheni ya shinda na M- pawa katika tawi la benki ya CBA kijitonyama jijini Dar es salaam, na hiyo ikiwa ni baada ya kudumu kwa promosheni hiyo kwa muda wa wiki 6.

Akizungumza katika makabidhiano hayo mwakilishi wa Mkurugenzi wa benki ya CBA Julius Konyani amesema kuwa  promosheni hiyo ililenga kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma  za kibenki na kuwawekea mazingira ya kujiwekea akiba huku ikiwapa changamoto ya kurudisha mikopo yao kwa wakati pindi wanapochukua mikopo.

Konyani amesema kuwa; "Mikopo yetu ina riba ndogo sana kwani lengo la  kufanya promesheni hii  hasa ilikua ni kuwawezesha kiuchumi wateja wetu, pia promosheni hii ilikua na lengo la kutoa shukrani na kuwazawadia wateja  wetu katika msimu huu wa sikukuu na tumefurahi washindi wetu wamekuwa ishara ya mafanikio yetu katika lengo hili" Ameeleza Konyani.

Aidha amesema kuwa benki ya CBA kwa kushirikiana na Vodacom wataendelea kutoa na kuboresha huduma ya M-pawa na kuwafikia watanzania wengi zaidi wakiwemo wakulima na wajasiriamali ambao watapewa mikopo midogo hadi ya shilingi laki tano ili kuweza kuwapa nguvu katika shughuli zao za kiuchumi wanazozifanya.
Washindi wa bajaji kupitia promosheni ya shinda na M -pawa wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi kutoka benki ya CBA na Kampuni ya simu ya Vodacom.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa benki ya CBA Julius Konyani (kushoto)akimkabidhi kadi ya bajaji bi. Mariam Barawa mmoja kati ya washindi watano waliojishindia bajaji hizo kupitia promosheni ya shinda na M- Pawa,  jijini Dar es salaam. Kulia ni meneja masoko wa huduma za kifedha kutoka kampuni ya Vodacom Noel Mazoya. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TANZANIA KINARA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA VIJANA NCHI ZA SADC

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TANZANIA imetajwa kuwa kati ya nchi tano ndani ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC ambazo zinatoa kipaumbele kwa masuala yanayohusu vijana.

Hayo yameelezwa katika mkutano wa vijana toka nchi za SADC uliofanyika mjini Windhoek, Namibia kati ya tarehe 13 na 15 Disemba 2018 ambapo mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Michezo, Vijana na Huduma za Umma wa Namibia, Mheshimiwa Erustus Uutoni ambaye alieleza nafasi zilizopo kwa  vijana katika ukanda huo.

Sambamba na hilo Uutoni alieleza namna viongozi akiwemo Mwalimu Julius Nyerere walivyotumia vizuri ujana wao kuleta uhuru kwenye nchi za kusini mwa Afrika, na kutoa Wito kwa Vijana wa nchi 16 za SADC kutumia vema ujana kwa maendeleo ya uchumi, siasa na jamii zao.

 Uutoni alieleza kuwa wakuu wote wa chi za SADC wapo tayari kusaidia vijana kufikia ndoto zao wakiwa katika nafasi nzuri kuliko wageni wanaoingia na kupora fursa za vijana na
Aliitaja Tanzania kama msambazaji mkuu wa madawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa nchi zote za SADC na kueleza kuwa Vijana wana nafasi kubwa sana katika maendeleo ya viwanda hasa vya vifaa tiba.

Kwa upande wake Mratibu wa masuala ya jamii na maendeleo ya watu SADC Bi. Duduzile Simelane alieleza kuwa Tanzania imekuwa na utaratibu mzuri wa kufungua fursa za kiuongozi kwa vijana, Lakini pia wizara inayohusiana na masuala ya vijana imewekwa chini ya ofisi ya waziri mkuu na ikiwa na naibu waziri ambaye ni kijana( Hapa akimaanisha Naibu Waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Anthony Mavunde).
Wawakilishi kutoka Tanzania, wakiwa kwenye mkutano wa SADC 2018 uliofanyika Windhoek Namibia, kutoka kushoto ni Charangwa Makwira akifuatiwa na Francis Daudi, Aziza Ngalupia na wa mwisho kulia ni Ernest Seko. 

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

INTRODUCING : Mwasiti Featuring Roma - Fall in love (Official video)

MKAZI WA SENGEREMA AMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI

$
0
0

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mama Madina Mbunda ambaye ni mkazi wa Katunguru wilayani Sengerema ametoa pongezi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyoendelea kuboresha sekta ya afya ikiwemo ukarabati wa Vituo vya Kituo Afya kama vile Katunguru na kutaka aendelee kuwa Rais hata baada ya muda wake kumalizika.

Mama Mbunda alitoa kauli hiyo jana baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kufanya ziara katika Kituo cha Afya Karume kilichopewa shilingi Milioni 400 na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa majengo matano mapya ambayo ni nyumba ya mtumishi, maabara, wadi ya wazazi, jengo la upasuaji pamoja na jengo la kuhifahia maiti kupitia mfumo wa “Force Account”.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images