Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA

$
0
0
Na Sixmund J. Begashe
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi, amesema Mkoa wa Singida unatarajia kuwa wa mfano nchini kwa upande wa maendeleo yatakayo letwa na wafanya biasha wadogo wadogo wajulikanao kama wa Machinga.
Mh Nchimbi ameyasema hayo kwenye shughuli ya kuwatunuku vyeti vya mafunzo ya MKURABITA pamoja na kukabidhi vitambulisho  vilivyo tolewa na Mh Rais Dr Magufuli kwa wafanya biasha wadogo zaidi ya mia sita walio udhuria mafunzo maalumu ya ujasiria mali yaliyoendeshwa na Taasisi ya MKURABITA Mkoani Singida.
Katika zoezi hilo Dr Nchimbi aliwaeleza wajasiria mali hao kuwa Vitambulisho hivyo ni ishara tosha kuwa Mh Rais Magufuli anaupendo mkubwa dhidi ya watanzania wote hasa wananchi wenye vipato vya chini na walie wanyonge hivyo ipo haja kubwa kwa wamachinga nao  kuonesha kupokea heshma hiyo kwa kufanya kazi kwa bidi ili waje kuwa wafanya biasha wakubwa na walipa kodi wazuri. 
" Heshma aliyotupa Mh Rais Dr John Pombe Magufuli sisi Mkoa wa Singida kupitia ninyi wafanya biasha wadogo wadogo ni kubwa sana, hivyo tunapashwa kuitendea haki heshma hii kwa kuhakikisha tunafanya biashara zetu kwa weledi mkubwa na juhudi ili tupande na kuwa wafanya biashara watakao lipa kodi kwa maendeleo zaidi ya Mkoa wetu na nchi kwa ujumla."Dr Nchimbi alisema
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akionesha mwonekano wa vitambulisho vilivyo tolewa na Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano  kama Wamachinga Mkoani Singida, pembeni yake ni Meneja wa TRA Mkoa wa Singida Bw Apili Mbaruku.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akiwakabidhi vitambulisho maalumu vilivyo tolewa na Mh Rais Magufuli kwa wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano kama Wamachinga Mkoani Singida.
Baadhi ya wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano kama Wamachinga Mkoani Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkua  wa Singida Dr Rehema Nchimbi (ayupo pichani)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Tume yatangaza Uchaguzi mdogo katika Kata za Biturana, Kibondo na Mwanahina Meatu

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa kata mbili utakaofanyika tarehe 19 Januari 2019 sanjari na uchaguzi mdogo wa Jimbo la Temeke na Kata 46 za Tanzania Bara uliotangazwa awali.

Akitoa taarifa kwa umma Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne), Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji (Rufaa) Mbarouk Salim Mbarouk amezitaja kata hizo kuwa ni pamoja  na Mwanahina iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Shinyanga  na Kata ya Biturana katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma. 

“Fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya  tarehe  21  hadi tarehe 27, Disemba mwaka huu. Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe  27, Disemba mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 28, Disemba mwaka huu hadi tarehe 18 Januari 2019  na Siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 19  Januari 2019,” alisema Jaji Mbarouk.

Jaji Mbarouk aliongeza kwamba Uchaguzi wa Kata hizo ambao unafanyika kutokana na kujiuzulu uanachama kwa madiwani waliokuwepo awali utafanyika pamoja na uchaguzi wa Jimbo la Temeke na Kata 46 za Tanzania Bara, kama ilivyotangazwa hapo awali.

Akitoa wito kwa vyama vya siasa, Jaji Mbarouk alisema “Tume inapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo”.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU WAKABIDHI SETI ZA JEZI KWA MICHUANO YA JIMBO CUP

$
0
0
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa Vya Michezo kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Jimbo hilo vilivyotolea na Mbunge na Mwakilishi kufanikisha michuano hiyo, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akikabidhi Seti 10, zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo,kwa ajili ya Michuano ya Vijana ya Mpira wa Miguu wa  Jimbo la Tunguu Zanzibar. hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akimkabidhi Seti ya Jezi Mwenyekiti wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Said Hassan, kwa ajili ya Michuano ya Vijana Mpira wa Miguu Jimbo la Tunguu, vilivyotolewa na Mbunge na Mwakilishi. kushoto Katibu wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Ndg. Ali Khatib Kisu, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akipata maelezo ya Bidhaa zinazotengenezwa na Vijana wa Kikundi cha Maendeleo cha Vijana Ubago Bi. Hawa Ali Mzee, akitowa maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Vijana hao, akiangali Shampoo wakati akitembelea kikundi hicho,kushoto Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Tunguu Ndg.Said Hassan.
 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, akiangalia Shampoo inayotengenezwa na KIkundi cha Vijana cha Maendeleo Ubago, akipata maelezo kutoka kwa Katibu Hamasa wa Kikundi hicho Bi. Hawa Ali Mzee, wakati alipotembelea kikundi hicho Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja.
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akiangalia moja ya nguo zinazozonwa na Kikundi cha Vijana na Maendeleo Ubago, wakati alipowatembelea Vijana hao katika Kituo chao kuangalia shughuli wanazozifanya za utengenezaji wa Shampoo, Sabuni. Lotion na mafuta ya mgando na ushoni wa nguo.(Picha na Othman Maulid)

BONDIA RAMADHANI SHAURI AJIFUA KUMKABILI AZIZI ULIZA DESEMBA 31 KINESI

$
0
0
Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' akimfanyika mazoezi ya kukaza misuri ya tumbo bondia Ramadhani Shauri anaejiandaa kuzipiga na Azizi Uliza Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki.
Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' kushoto akimsimamia bondia Ramadhani Shauri kupiga beg wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki.
Bondia Ramadhani Shauri kushoto akipiga beg uku akiwa kasimamiwa na Abdallah Seif 'Kamanyani' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki.
Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' kushoto akimwelekeza bondia Ramadhani Shauri kupiga ngumi iliyonyooka wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki. Picha na Super D Boxing News'

APPOINTMENT OF NEW CCBRT CEO

MultiChoice yafunga mwaka na waandishi Msasani Beach Club

$
0
0
Kampuni ya MultiChoice Tanzania, imefanya sherehe ya kufunga mwaka na kuwashukuru waandishi wa habari kwa ushirikiano wa kikazi waliokuwa nao katika kipindi cha mwaka huu wa 2018.
Sherehe hiyo ya kuwashukuru waandishi  ilifanyika Msasani Beach Club iliyopo katika fukwe za bahari ya Hindi, Kawe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa sherehe hiyo na waandishi, Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria alisema ‘Tunayofuraha kubwa kujumuika pamoja na waandishi kutoka vyombo mbali mbali ambavyo kampuni yetu ya Multichoice imekuwa ikishirikiana nanyi katika kipindi cha mwaka huu wa 2018. Tunapenda kutoa shukrani zetu dhati na zaidi kutegemea ushirikiano wenu katika kipindi cha mwaka ujao”.  

Sherehe hiyo ya kufunga mwaka na waandishi pia ilienda sambamba na mtanange mkali baina ya timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania na timu ya chama cha waandishi wa habari za michezo maarufu kama TASWA FC ambapo waandishi hao waliweza kuibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 2 -1 dhidi ya MultiChoice. 
 Baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiburudika kwa vinywaji katika sherehe ya Media Day iliyofanyika Msasani Beach Club mwishoni mwa wiki.
 Meneja Masoko Alfa Mria akizungumza katika hafla hiyo wakati akitangaza zawadi.
 Meneja Uajiri wa Multichoice Tanzania Tike Mwakitwange akimvisha nishani kapteni wa timu ya TASWA FC Bw. Majuto Omary mara baada ya mchezo wa timu hiyo na DSTV FC kwenye hafla ya Dstv Media Day iliyofanyika kwenye ufukwe wa Msasani Beach Club Kawe jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Meneja wa Fedha Multichoice Tanzania Bw. Godfrey Bwana akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku katika hafla ya Dstv Media Day iliyofanyika mwishoni mwa wiki Msasani Beach Club Kawe jijini Dar es salaam.
 Meneja Msoko Alfa Mria aliyekuwa refa wa mchezo kati ya DStv na TASWA akitoa kadi ya njano kwa mmoja wa wachezaji wa timu ya TASWA FC baada ya kucheza vibaya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Ruvuma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira  Mgalu, amewataka wataalam katika Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwa makini katika kazi ya upangaji wa vijiji vinavyopaswa kupelekewa umeme kwenye wilaya zenye majimbo mawili ya uchaguzi ili kuepusha malalamiko ya kupendelea upande mmoja wa Wilaya. Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akikagua miradi ya usambazaji umeme vijijini katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo Wilaya hiyo ina Jimbo la Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini.

Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya kupata malalamiko kuwa, Vijiji vingi vya Tunduru Kaskazini ndivyo vimesambaziwa umeme huku Tunduru Kusini ikiwa na Vijiji vichache. Aidha, Naibu Waziri aliagiza kuwa, kazi ya upangaji wa Vijiji vinavyotarajiwa kupelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali ishirikishe viongozi wa ngazi mbalimbali katika maeneo ili kuondoa malalamiko katika miradi hiyo.

Vilevile alisema kuwa, wataalam hao wahakikishe kuwa hawaruki Vijiji na badala yake kila kijiji kinachopitiwa na mradi kisambaziwe nishati ya umeme. Kuhusu kazi ya uunganishaji Wilaya ya Tunduru  kwenye umeme wa gridi,  Naibu Waziri alisema kuwa, wilaya hiyo itaanza kupata  umeme huo kuanzia mwezi Machi mwakani baada ya kuvuta umeme kutokea wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi, (hawapo pichani) kabla ya kuzindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Hanga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Namtumbo, Eng. Edwin Ngonyani na kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Mfaume.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Mtakanini, wilayani Namtumbo mkoani  Ruvuma.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi baada ya kuwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Mchuluka wilayani Tunduru mkoani  Ruvuma.
Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Hanga, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati alipofika kijijini hapo kukagua  mradi wa usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme katika Kijiji hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar salaam leo Desemba 18, 2018
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally akiongea kabla ya ufunguzi wa  kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018.
 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiendesha  kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018

PICHA NA IKULU

JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUMUOKOA MTOTO MCHANGA MKOANI MWANZA

$
0
0


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kutumia kikosi chake kabambe na jasiri, tumefanikiwa kumuokoa mtoto mchanga mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja hadi tatu aliyekua ametupwa na kuachwa bila msaada na mwanamke/mtu asiyefahamika huko mtaa wa Mwambani Wilayani Ilemela, kitendo ambacho ni kosa la Jinai.

Tukio hilo la kikatili limetokea tarehe 17.12.2018 majira ya saa 20:30hrs usiku, hii ni baada ya mtoto huyo kufungwa nguo mwilini mwake kisha kutupwa bila msaada wa aina yoyote. Ndipo kikosi chetu cha askari kilichokuwa doria chenye umakini wa hali ya juu kilipata taarifa na kufanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kumkuta mtoto huyo akiwa hai akilia sana akiwa ametupwa uwanjani hapo na mwanamke/mtu asiyefahamika. 


Baada ya Mtoto huyo kuokolewa amepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na uhifadhi, hali yake inaendelea vizuri. Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza, tunaendelea na upelelezi pamoja na msako mkali wa kumtafuta mwanamke/mtu aliyehusika katika kutenda ukatili huu ili aweze kukamatwa na kufikishwa  katika vyombo vya sheria, ili baadae iwe fundisho kwa wengine.

Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa onyo kwa baadhi ya wanawake wenye tabia kama hizi za kinyama kuwa waache kwani ni kosa la jinai lakini pia ni kinyume na haki za binadamu. Hivyo endapo mtu atabainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 
Vilevile tunawaomba wananchi pindi wanapomwona jirani yake ni mjamzito alafu baada ya muda ghafla ujauzito wake unapotea na mtoto haonekani watoe taarifa polisi ili tuweze kujiridhisha juu ya usalama wa mtoto.

Imetolewa na;
Jonnathan Shanna – ACP
Kamanda wa Polisi (M) Mwanza.


18 December, 2018.

Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu

$
0
0
Serikali imewaasa wananchi kutoa taarifa za kuwepo wahamiaji wanaoishi maeneo mbalimbali  nchini kinyume na sheria  za nchi ili raia wema waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na salama huku ikiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa waadilifu katika maeneo yao ya kazi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kauli mbiu ya Uhamiaji Unaozingatia Utu

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Naibu Waziri Masauni amesema ni lazima wananchi washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wahamiaji haramu wanaoishi maeneo mbalimbali nchini.

“Serikali ya Tanzania inaheshimu haki za kila mtu na ndio maana tumeingia mikataba mbalimbali ya kimataifa yenye kulinda utu wa kila raia awe raia au mgeni aliyepo nchini, lakini hatutokuwa tayari kuona wahamiaji wasiofuata sheria za nchi wakiingia nchini kinyume na  taratibu zilizowekwa,” alisema Masauni
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akizungumza wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefamyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.
Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akisikiliza  maelezo  juu  ya  historia  ya  mabadiliko  ya  Pasi za Kusafiria  kutoka kwa mtaalamu wa pasi hizo,  Sajini  wa  Uhamiaji, Vedasto  Rweikiza(kulia), wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akipokea zawadi  kutoka  kwa  Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Salma Panja(kulia),  baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho  wakati wa Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), wakiangalia pasi ya kusafiria walipotembelea mabanda ya maonyesho wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefamyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

THE BILLIONAIRE CLUB: Reginald Mengi on his journey to riches

CCM YAWASAMEHE NA KUWAREJESHEA UANACHAMA RAMADHANI MADABIDA NA WENZAKE WATATU

$
0
0
Kwa kauli moja Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne ambao walitenda makosa hayo wakiwa Wenyeviti wa CCM ngazi ya Mikoa na Wilaya. 

Waliosamehewa na kurejeshewa uanachama ni; 
1.   Ndg. Ramadhani Rashid Madabida (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam).
2.   Ndg. Erasto Izengo Kwirasa (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga).
3.   Ndg. Christopher Mwita Sanya (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara).
4. Ndg. Salum Kondo Madenge (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni). 
 Pichani ni wanachama hao waliosamehewa wakiwa wamesimama mbele ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally na mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa  Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam 
Pichani ni wanachama hao waliosamehewa wakimshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally  mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa  Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam 
PICHA NA IKULU

Tamasha la Tigo Fiesta 2018 ‘kuipagawisha’ Dar Jumamosi

$
0
0
Zaidi ya wasanii 40 ‘Machampioni ‘kutoa burudani ya kufunga mwaka.


Mkuu wa Kitengo cha  Huduma za  Masoko wa Tigo William Mpinga (wa pili kulia) akiwa na mratibu wa Tamasha la Tigo Fiesta 2018 Gardner Habash (wa tatu kulia) pamoja na baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 litalaofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam Jumamosi.
????????????????????????????????????
Msanii  Nedy Music (wa kwanza kushoto)  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika katika viwanja vya Posta jinjini Dar es Salam Jumamosi.  Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za  Masoko wa Tigo Masoko William Mpinga akifuatiwa na Mratibu wa tamasha hilo Gardner G Habash kutoka Clouds Media Group akifuatia na msanii Chege

PIC 3
Msanii Dogo Janja (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salam Jumamosi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za  Masoko wa Tigo William Mpinga akifuatiwa na Mratibu wa tamasha hilo Gardner G Habash kutoka Clouds Media Group
PIC 4
Msanii wa muziki wa kizazi kipya TID, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha kuhusu ushiriki wake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es siku ya Jumamosi. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za  Masoko wa Tigo William Mpinga

SHAMTE AMEWATAKA VIJANA KUTUMIA FURSA ZINAZOJITOKEZA HAPA NCHINI KUENDELEZA BIASHARA ZAO

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
MWENYEKITI wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Salum Shamte amewataka vijana wasomi, wabunifu, wavumbuzi kutumia fursa inayotolewa na Shirika la Angel  Investors (Wawekezaji Malaika) ambalo limekuja nchini kuwafikia Watanzania kwa kutoa mitaji kwa Wafanyabiashara wadogo ili kupiga hatua.

Shamte ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi maalumu wa ufunguzi wa Ofisi ya Taasisi inayohudumia Vijana ambao ni wavumbuzi, wabunifu wanaoanza biashara ambapo watasaidiwa na Taasisi ya World  Business Angel Investment  Forum (WBAF) ambayo limejikita kupeleka huduma za kifedha  kwa Vijana hao. Aidha Shamte amesema kuwa asilimia  kubwa ya vijana hapa nchini wana ukosefu wa ajira pamoja na kupata mtaji wa kujiendeleza  katika biashara.

Mkurugenzi Mkazi wa Angel Investors  Tanzania (Wawekezaji Malaika), Sabetha Mwambenja amesema kuwa tayari wamesha fanya mazungunzo na Sekta ya Umma na Binafsi ikiwamo Vyuo vya Elimu ya Juu na Ufundi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Mtakatifu Joseph, Chuo Kikuu cha Tumaini, VETA, COSTECH, Taasisi yaTeknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Kilimo cha Sokoine, (SUA), Chuo cha All Makhoum cha Mbezi Beach na  Hatamizi za Tehama (Incubators).
Mkurugenzi Mkazi wa Angel Investors  Tanzania Dkt Sabetha Mwambenja akifafanua ujio wa taasisi hiyo wakati wa ufunguzi huo wa ofisi ya WBAF hapa nchini, kuwa ni kutaka kuinua Vijana wasomi katika suala zima la kujiajiri kwa kuwawezesha namna ya kupata mtaji ili kujikwamua kiuchumi  wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi hizo hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania Salum Shamte akisistiza suala la Vijana waso kutumia fursa inayotolewa na Taasisi ya World Business  Angels Investment  Forum (WBAF)  lililojikita kutoa huduma za kifedha kwa Vijana wasomi, wabunifu, wavumbuzi wanaoanza biashara  kupiga hatua na kuwa wafanyabiashara wakubwa, leo katika ufunguzi wa ofisi ya taasisi ya WBAF Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Biashara na Maendeleo nchini Ghana Ibrahim Awal  ambaye pia ni mkulima amehudhuri ufunguzi huo wa ofisi ya WBAF hapa nchini wakati wa hafla ya ufunguzi wa ofisi hizo hapa nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam..
  Mkurugenzi Mkazi  Angel Investors  Tanzania Dkt Sabetha Mwambenja (kushoto) na Mwenyekiti WBAF  Baybars Altuntas (kulia) wakionyesha mafaili kuashiria ufunguzi wa ofisi ya WBAF hapa nchini umeshakamilika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

MUCHUZI TV: TFDA YAPEWA TUZO YA KIMATAIFA


Irene Uwoya alivyotoa zawadi katika siku yake ya kuzaliwa

$
0
0

Na.Khadija seif,globu ya jamii
KATIKA kusherehekea siku yake ya  kuzaliwa Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya  amefanya dua ya  Kuwarehemu watu maarufu waliotangulia mbele ya haki.

Akizungumza wakati wa kutoa neno la shukrani kwa watu ambao wamejumuika nae kwenye sherehe hiyo ikiwemo  watu wenye ulemavu na wasiojiweza Irene amesema amefanya hivyo ili kurudisha fadhila kwa watu  ambao siku zote wamekua wakitazama kazi zake pamoja na kununua .


Uwoya ameeleza kuwa ni muhimu kuwasaidia watu wasiojiweza na kuwapatia mahitaji ili waweze kujisikia faraja na kuona wasanii wapo pamoja nao na kwa Leo ameweza Kula nao chakula pamoja na kuwapatia zawadi."Hakuna kitu kikubwa kama fungu la Kumi kwani sio hiyari na mafanikio yangu ni kutokana na kutoa sadaka kwa wingi hakuna  uchawi wowote bali ni kufanya sadaka kwa wingi na kumuomba mwenyezi mungu "alisema Irene uwoya




Kwa upande wa Mlezi wa kituo kinachowalea watoto yatima Almadina center kilichopo Tandale Yusra Mohamed ametoa pongezi kwa Irene Uwoya kwa kuwafariji watoto hao pamoja na walemavu kwani ni wasichana wachache wenye maono kama yake kuwapa nafasi watu hao kujumuika nao pamoja .

Hata hivyo watoto wameshukru na kufurahi siku ya Leo japo imekua ni mara chache kupatiwa misaada na kusubiri siku za sikukuu. Watoto Hawa ni wa kwetu sote tuwasaidie na kushirikiana nao katika kuwalea na kuwakuza katika maadili mema na yanayompendeza mwenyezi mungu.

Pia kwa upande wa Kiongozi wa Wasanii wa filamu ambae pia ni mtu wa karibu wa Irene uwoya, Steve Nyerere amempongeza Irene kwa kujumuika na watu hao na kuwashauri wasanii wengine waige mfano na kuwaenzi na kuwaombea dua kwa wingi watu waliofanya mazuri hapa nchini .


HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE

$
0
0
*Pia wanne warejeshewa uanachama wao, yumo Madabiba

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

HALMASHAURI KUU ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), imetangaza kuwa mwanachama wake mpya Abdallah ,Mtolea ameteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam.

Kwa kukumbusha tu Mtolea kabla ya kujiunga CCM alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi(CUF) lakini siku za karibuni aliamua kujiondoa kwenye chama hicho na kujiunga na CCM ambapo 
aliweka wazi amefurahishwa na jitihada za Rais Dk.John Magufuli katika kuwatumikia watanzania wote.

Akizungumzia maazimio ya Halmashauri Kuu, Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Alli amesema leo kuwa Mtolea amepitishwa kugombea ubunge kupitia chama hicho katika uchaguzi wa ubunge. "Kwa kauli moja 
Halmashauri Kuu imepitisha jina la Abdallah Ali Mtolea kugombea ubunge kwenye jimbo hilo la Temeke."amesema Dk.Bashiru.

Wakati huo huo Dk.Bashiru amesema kuwa Halamshauri Kuu imempa kalipio kali mwanachama wao Hasnal Muruji kutokana na kukiuka maadili ndani ya chama hicho.Aidha Dk.Bashiru amezungumzia uamuzi wa Halmashauri Kuu wa kuwarejeshea uanachama wanachama wake wanne akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida.Wengine waliorejeshewa uanchama aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa, aliyekuwa 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Chistopher Sanya huku aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akiendelea kuwa chini ya uangalizi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari alipokuwa akizungumza nao leo Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam,kuhusu yaliyojiri katika vikao vikuu viwili vya chama ambavyo ni Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) vilivyofanyika kati ya tarehe 17 na 18 Desemba, 2018 Jijini Dar es Salaam.Vikao hivyo vimeongozwa na Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Mkuu Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally kwenye mkutano wake na Waandishi hao uliofanyika leo Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Afya apokea Hati ya TFDA ya Ubora wa Mifumo ya Udhibiti Dawa

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa TFDA ni Taasisi ambayo inafanya vizuri na kufanya nchi kuwa kifua mbele katika masuala ya udhibiti wa Mifumo ya Dawa katika kulinda wananchi. Mwalimu ameyasema hayo wakati akipokea Hati TFDA ya Ubora wa Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa TFDA baada ya kufanyiwa tathimini na Shirika la Afya Duniani (WHO) imepanda ngazi ya Tatu ya  Udhibiti wa Mifumo ya Dawa na kuwa nchi ya kwanza kwa nchi Afrika kufikia ngazi hiyo. Ummy amesema kati asilimia 100 ni asilimia 30 ndizo zimefikia ngazi ya Tatu na zilizofikia ngazi  ya Nne ni nchi zilizoendelea. Amesema kubuniwa kwa kufanyika kwa  tathimini taasisi za udhibiti duniani ili ziwe na mifumo inayowezesha kudhibiti dawa inayopaswa na hivyo kuhakikisha dawa zinazosambazwa kwenye soko na zilizo bora, salama na zinazotibu watu.
 

Aidha amempongeza TFDA kwa hatua waliyofikia katika kuweka Tanzania kwenye ramani kwa kufikia ngazi ya Tatu kwa nchi Afrika kuwa taasisi bora.

"TFDA ni Taasisi ambayo inafanya vizuri katika suala la udhibiti wa dawa na hiyo ni kulinda watumiaji dawa" Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu Adam amesema kuwa mchakato wa kufikia hatua hiyo ulikuwa mrefu na kuahidi kuendelea kufanya vizuri na kupanda ngazi ya Nne
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata Utepe ya Hati TFDA ya Ubora wa ngazi ya Tatu ya Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati hafla ya kupokea Hati ya  Mamlaka ya Chakula  na Dawa (TFDA)kufikia ngazi ya Tatu ya Ubora wa Mifumo ya Udhibiti wa Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Adam Fimbo akizungumza kuhusiana na TFDA kufikia ngazi ya Tatu ya Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TFDa wakati wa hafla ya kupokea Hati ya TFDA ya Ubora wa Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

BREAKING NEWS:BASATA YAWAFUNGIA WASANII DIAMOND PLATNUMZ NA RAYVAN KUTOFANYA SHOO NDANI NA NJE YA NCHI KWA MDA USIOJULIKANA

Uwanja wa Ndege Mtwara Kugharimu Shilingi Bilioni 55

Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images