Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MAHOJIANO YA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT.ABBAS NA KITUO CHA REDIO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Na. Vero Ignarus, Arusha

Msenaji wa Serikali Dkt Abbas amesema serikaki inaendelea na ukarabati na ujenzi wa Zahanati na Vituo vya afya kwa nchi nzima kwani Mpango wa serikali ni kuhakikisha kila Wilaya ina hospitali

Amesema upatikanaji wa dawa umeongezeka kwa rikali kuongeza bajeti ya madawa kutoka bill.31 hadi bil. 280,ambapo Serikali inanunua madawa moja kwa moja kutoka viwandani na sio kwa madalali tena. Tiba za kibingwa zimeimarishwa sana katika nchi yetu hasa magonjwa ya Moyo,kupandikiza figo na matatizo yakutosikia hii imepelekea kupungua kwa idadi ya wagonjwa wakutibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wa sejta ya Elimu Dkt Abbas anesema Serikali inatoa fedha kiasi cha bil.29 kila mwezi kuwezesha elimu bure katika nchi yetu.Dkt.Abbas.Amesisitiza kuwa Migomo ya elimu ya juu imeshaisha katika awamu hii ya tano kwani fedha zinapelekwa kwenye vyuo kwa wakati ambapo kwa mwaka huu kiasi cha bil 137 kimeshapelekwa kwenye vyuo mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kwenye sekta ya Kilimo Serikali imeanzisha mamlaka ya udhibiti wa masoko kwa bidhaa za Tanzania, hii itawasaidia wakulima, wafanyabiashara kupata masoko yenye uhakika.June mwaka huu Serikali lizindua mpango mpya wa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji ili kumuwezesha mkulima kutotegemea mvua.


Dr. Hassan Abbas mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Tanzania.


KAKUNDA AITAKA VETA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA ZA KISASA

$
0
0
WAZIRI wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema ni vyema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuanza kuwekeza katika kubuni teknolojia za kisasa na kuzalisha mashine za kurahisisha shughuli za viwanda nchini.

Kakunda aliyasema hayo alipotembelea banda VETA katika Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere-Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema kutokana na mkakati wa serikali kwenda katika uchumi wa kati kupitia viwanda, VETA  inawajibu wa kuzalisha nguvu kazi yenye uwezo wa kubuni teknolojia ambazo zitarahisisha kufanya uchakataji wa malighafi zinazolishwa nchini.

 Kakunda amesema kuwa mali ghafi zikichakatwa nchini zitasaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa malighafi hizo na hatimaye kuwasiadia wakulima kunufaika na kilimo wanachokifanya.

“VETA mna nafasi kubwa nchini katika maendeleo ya viwanda na serikali inawategemea katika uzalishaji wa teknolojia na nguvu kazi ili kusaidia kusukuma maendeleo hayo,” alisema.

Maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda yanafanyika katika viwanja vya Sabasaba kuanzia tarehe 5 hadi 9 Desemba 2018.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda akiangalia Kibuda cha kuchakata mihogo wakati alipotembelea banda la VETA katika maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Joseph Kakunda akipata maelezo kutoka kwa Afisa habari wa VETA David Edward wakati alipotembelea banda la VETA katika maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda akiangalia bidhaa zinazozalishwa na VETA wakati alipotembelea maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili.

$
0
0
Equinor Tanzania inaona fahari kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi kumi na tatu miongoni mwa wanafunzi wake wengi inaowafadhili ambao wamekuwa wakichukua masomo ya shahada- ya pili (Uzamili) katika Geoscience and Engineering.

Wanafunzi wanaohitimu wamekuwa wakifadhiliwa chini ya programu ya ufadhili wa Equinor Tanzania unaojulikana kama Angola Tanzania Higher Education (ANTHEI). Programu hii ya ufadhili ya ANTHEI kutoka kwa Equinor ni programu ambayo inatoa ufadhili kamili kwa hadi kufikia wanafunzi kumi kila mwaka kusomea shahada ya pili katika masomo ya (Utafiti wa Petroli) Petroleum Geoscience na Uhandisi wa Petroli (Petroleum Engineering) katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Norway (Norwegian University of Science and Technology) (NTNU) kinachofanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Da es salaam (UDSM).
 
 Programu hii imeandaliwa kwa namna kwamba mwanafunzi atatumia mwaka mmoja nchini Norway na kukamilisha mwaka wa mwisho wa masomo ya shahada ya pili katika chuo cha UDSM. Kwa mujibu wa hati ya makubaliano iliyosainiwa na Equinor, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na NTNU mpango huu wa udhamini chini ya Equinor ulianza mwaka 2012 na utaendelea mpaka 2019.

 Jumla ya wahandisi wa Petroli wapatao 42 (Wahandisi wa Uzalishaji, Uhifadhi na wahandisi wa Uchimbaji) wahandisi 16 wa Utafiti wa Petrioli (Geology, Petrophysicis na Geophysics) na wahandisi 6 wa usimamizi wa miradi wameshasajiliwa mpaka sasa.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen akizungumza jana na waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo. 
Mhitimu, Bertha Ngereja akitoa shukurani zake kwa niaba ya wenzake kwa wafadhili Equinor Tanzania, ANTHEI, UDSM na NTNU kwa kuwawezesha kupata shahada ya pili ya masomo mbalimbali yanayohusu Mafuta na Gesi. Sherehe za mahafali zilifanyika jana kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.
Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dr. Mette H. Ottoy akizungumza jana na waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo.
Mhitimu, Masolwa Kasongi akipokea cheti cha kuhitimu shahada ya pili ya Geoscience and Engineering jana kwenye sherehe ya mahafali zilizofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.

TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
BODI ya Uhasibu na  Ukaguzi wa hesabu (NBAA) watoa Tuzo kwa Taasisi, Makampuni pamoja na mashirika yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2018 iliyofanyika Bunju jijini Dar es salaam.

Akipokea Tuzo hiyo Mhasibu  Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii Athuman Senzota amesema ni kwa Mara ya tatu wananyakua Tuzo hiyo ambapo  vilikua vyuo viwili kwenye kinyang'anyiro cha Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na Taasisi ya ustawi kuwa washindi wa pili huku nafasi ya kwanza kushika chuo cha Mzumbe.

Senzota ameeleza kuwa Tuzo hiyo waliyoipata inaonyesha jinsi gani Taasisi ya Ustawi wa Jamii ni waadilifu na wachapakazi wa hali ya juu  katika kutunza na kutumia pesa za Umma Kikamilifu kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha 2018.

Hata hivyo amefafanua kuwa waliweza kufikia viwango ambavo viliwawezesha kushinda Tuzo ambapo ili uweze kushinda Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi ilizingatia viwango vya uwasilishaji kufikia 75% ya Mapato kwa mwaka wa fedha 2018 .

Na Tuzo hiyo imekua chachu kwa Taasisi ya ustawi wa jamii  inayofanya tuendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa Mapato ili kusaidia jamii na maslahi kwa nchi kwa ujumla.
 Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii  Dkt. Zena Mabeyo  akipokea Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha katika nafasi ya Taasisi ya elimu ya juu na Vyuo vikuu  zilizoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) kwa mwaka 2018 jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii CPA Athuman Senzota akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushinda Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha kwa mwaka 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU

$
0
0
          Na.Khadija seif,globu ya jamii.

BODI ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) watoa Tuzo kwa Taasisi,Makampuni pamoja na mashirika yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2018 Bunju jijini Dar es salaam.

Akipokea Tuzo hiyo Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii Athuman Senzota amesema ni kwa Mara ya tatu wananyakua Tuzo hiyo ambapo vilikua vyuo viwili Kwenye kinyang'anyiro cha Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na Taasisi ya ustawi kuwa washindi wa pili huku nafasi ya kwanza kushika chuo cha Mzumbe.

Aidha,Senzota ameeleza kuwa Tuzo hiyo waliyoipata inaonyesha jinsi gani Taasisi yao ya ustawi wa jamii ni waadilifu na wachapakazi wa hali ya juu katika kutunza na kutumia pesa za Umma Kikamilifu kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha 2018.

Hata hivyo amefafanua kuwa Waliweza kufikia viwango ambavo viliwawezesha kushinda Tuzo ambapo ili uweze kushinda Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi ilizingatia viwango vya uwasilishaji kufikia 75% ya Mapato kwa mwaka wa fedha 2018 .

Na Tuzo hiyo imekua chachu kwa Taasisi ya ustawi wa jamii inayofanya tuendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa Mapato ili kusaidia jamii na maslahi kwa nchi kwa ujumla.
 Kaimu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii  Dr. Zena Mabeyo  akipokea Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha katika nafasi ya Taasisi ya elimu ya juu na Vyuo vikuu  zilizoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) kwa mwaka 2018 jijini Dar es salaam
Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii CPA Athuman Senzota akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushinda Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha kwa mwaka 2018.

WAZIRI KAKUNDA AWATAKA WAWEKEZAJI KUJITOKEZA KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI ZILIZOPO HAPA NCHINI.

$
0
0
Na Agness Francis, Glogu ya Jamii. 

WAZIRI wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amefungua rasmi leo kituo kikubwa cha maonyesho ya viwanda vitatu chini ya uwekezaji wa raia kutoka China vilivyoajiri watanzania Mia tisa kilichopo Tameko  Keko Jijini Dar es Salaam. 

WAZIRI Kakunda amezungunza wakati wa uzinduzi huo  katika kituo cha maonesho ya viwanda kilichopo Tameko maeneo ya Keko ambapo amewapongeza Wawekezaji hao raia wa kutoka nchini China kwa kuwa na ushirikiano mzuri waliouonesha hapa nchini

Waziri Kakunda amesema  zipo fursa nyingi  za uwekezaji kama viwanda vya mazao ya korosho, miwa, pamba, na alizeti, viwanda vya  Nguo, viatu vya ngozi hivyo basi amewataka wawekezaji wazidi kujitokeza kwa wingi katika kuwekeza na Dodoma ambao ni mji  Kuu wa Tanzania badala ya kuishi Dar es  Salaam tu ."Vile vile nawahakikishia kuwa wote mitaji mnayowekeza Tanzania itakuwa salama hakutakuwa na muingiliano wa kusababisha biashara yenu kuwa mbovu" amesema Waziri Kakunda. 

Aidha amesema kuwa Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania imejitahidi kuboresha  maeneo ya  viwanda vya uwekezaji, pamoja na mahakama ya biashara kwa mtu yoyote atakaeuwa na malalmiko ya unyanyasaji anakaribishwa kutoa malalmiko. 

Pia Waziri huo amemalizia kwa kusema kuwa "tunajua wenzetu mmetuzidi katika uhandisi tunawakaribisha muendelee kujitokeza katika ujenzi wa mabarara, madaraja na majumba"amesema Waziri Joseph Kakunda.
 Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji Joseph Kakunda akizungumza na wadau mbalimbali wa Viwanda pamoja na biashara waliojitokeza katika ufunguzi wa kituo kikubwa cha maonesho ya viwanda vitatu vya China kilichopo keko jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau mbalimbali waliofika katika hafla ya ufunguzi wa kituo cha maonesho ya viwanda vitatu vya China kilichopo keko jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji, Joseph Kakunda(wa tatu kutoka kulia)  akishirikiana na wawekezaji mbalimbali wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha maonesho ya viwanda vitatu vya China kilichopo keko jijini Dar es Salaam.
Wawekezaji kutoka wakiwa katika picha ya pamoja.

WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR KUYAFUNGIA MACHINJIO YASIYO NA VIWANGO

$
0
0
Na Khadija Khamis –Maelezo
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imeahidi  kusimamia na kudhibiti ubora wa machinjio ya ng’ombe na yatakayobainika hayana kiwango cha kufanya kazi hiyo yatafungiwa ili kuhakikisha wananchi wanapata chakula kilicho salama kwa afya zao.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea machinjio ya Kinyasini,Donge  Muwanda na Mahonda  katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kuangali mazingira na ubora wa machinjio hayo.

Amesema juhudi za Serikali kupitia Wakala wa Chakula na Dawa ni kuhakikisha wananchi wanapata chakula kilichoandaliwa katika ubora unaostahiki ambao utamlinda mtumiaji asipatwe na madhara.  

Alisema Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar walianzisha kanuni ya kuwataka wananchi wanaosafirisha nyama ya ngombe kwa ajili ya biashara kutumia gari maalum za kusafirisha kutoka machinjioni kwa lengo la kulinda usalama wa chakula hicho

Dkt. Khamis amezitaka taasisi zinazosimamia suala la uingizaji wa ngombe ikiwemo Idara ya Mifugo, na Kilimo Wakaguzi pamoja na vyombo vya ulinzi kuwa na mashirikiano ya pamoja ili kuhakikisha ngombe hawachinjwi katika mazingira hatarishi.

Diwani wa Wadi ya Mahonda Haji Fadhil Mkadam amewaomba Wakala wa Chakula na Dawa kuwasaidia kumaliza ujenzi wa chinjio lao liweze kuanza kazi  ili kuepuka usumbufu na kuvunja sheria ya kuchinja ngombe katika sehemu zisizorasmi.
 Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Chakula na Dawa Dkt Khamis Ali na Mkaguzi wa Chakula Dkt. Faki Mohd Haji wakikagua Chinjio la Kinyasini linalomilikwa na Abdalla Mohd walipofanya ziara ya kuangalia mazingira ya machinjio ya mkoa Kusini Unguja.
 Mmiliki wa Chinjio la Kinyasini Abdalla Mohd akiwaeleza wakaguzi juhudi anazochukua katika kuhakikisha mazingira ya sehemu yake ya kazi yanakuwa salama na wananchi wanapata kitoweo kilicho bora kwa afya zao
 Wakaguzi wa Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Khamis Ali wakiangalio chinjiola kisasa la Donge Muwanda  walipofanya ziara ya kuangalia hali ya mazingira ya machinjio ya Mkoa Kaskazini Unguja.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Chakula na Dawa Dkt. Khamis Ali akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara ya kukagua machinjio matatu ya Mkoa Kaskazini Unguja.PICHA NA RAMADHANI ALI - MAELEZO ZANZIBAR

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWANAMKE APAMBANA NA JAMBAZI MWENYE SILAHA AKIMUOKOA MUMEWE

$
0
0
Na Felix Mwagara, (MOHA) MARA.
Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Kata ya Nyamihyolo, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Busimba Malegesi amemuokoa mumewe asiuawe na jambazi mwenye silaha ambaye alivamia katika nyumba yao na kuanza kumshambulia mwanaume huyo kwa kumkatakata mapanga mwili mzima.

Busimba alimrukia jambazi huyo kiunoni na kumuangusha chini na kufanikiwa kumnyang’anya panga pamoja na tochi ambazo alikua nayo wakati anamshambulia mumewe aitwaye Samson Malegesi (62).

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 7:30 usiku wa kuamkia Ijumaa wakati familia hiyo ikiwa imelala ndipo jambazi huyo alivunja mlango na kuingia moja kwa moja chumbani kwa wanandoa hao na kuwasha tochi kumsaka Malegesi na baada ya kufanikiwa kumuona alianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga kichwani, mikononi, kwenye mbavu na kusababisha damu nyingi kumwagika.

Wakati jambazi hilo akiendelea kumshambulia Malegesi, mkewe alikua naye anapambana kwa kumzuia asimshambulie mumewe, lakini jambazi hilo lilizidiwa baada ya mwanamke huyo kupata nguvu zaidi na kufanikiwa kumuangusha chini na kuhakikisha silaha aliyoishika mkononi akinyang’anywa kwa urahisi kutokana na kubanwa kwa juu na mwanamke huyo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo, Busimba Malegesi (katikati), alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Mgonjwa huyo amelazwa katika Hospitali ya Kibara, Wilayani humo akiendelea kupewa matibabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kulia ni Muuguzi wa hospitali ya Kibara, Godliver Josephat, ambapo mhonjwa huyo amelazwa akipatiwa matibabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akiingia Hospitali ya Kibara Wilayani Bunda kumwangalia mgonjwa aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Wilayani humo, Mkaguzi Boniface Mwalupale. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA

$
0
0
Shirika la Agape la Mjini Shinyanga limefanya Kongamano kwa wanafunzi 400 wa shule za msingi na sekondari katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi na ujinsia ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na wanafunzi wa shule nane zilizopo katika kata hiyo,limefanyika katika Uwanja wa Kijiji cha Singita ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mary Maka. 

Wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo ni kutoka shule za msingi Nzagaluba, Manyada, Busanda, Shabuluba pamoja na Shingida ambapo za sekondari ni Samuye, Usanda na Shingita. 

Kongamano hilo lililoanza kwa maandamano lilienda sanjari na Mdahalo wenye mada ‘Nini Manufaa/faida ya elimu ya afya ya uzazi na ujinsia’ pia lilitawaliwa na michezo na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi hao vyote vikilenga kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. 
Wanafunzi wa shule mbalimbali katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiandamana kuelekea katika uwanja wa kijiji cha Singita kata ya Usanda ambapo pamefanyika kongamano kwa ajili ya kutoa elimu afya ya uzazi na ujinsia ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga akielezea lengo la kongamano la wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kata ya Usanda ambalo limelenga kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi na ujinsia ili .kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.
Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mary Maka akiwasisitiza wanafunzi/watoto kutoa taarifa kwa viongozi na vyombo vya dola pale wanapofanyiwa vitendo vya kikatili.

BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU

$
0
0
Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu imefika na kufyeka mazao mbalimbali yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu na ndani ya Mita 60 kutoka kwenye mto huo katika eneo la Ruvu Darajaji mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema kuwa zoezi hilo ni muendelezo wa operation ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na kujenga makazi yao ndani ya Mita 60 kutoka Mto huo ili kulinda chanzo hicho cha maji. 

"Sasahivi maji yamepungua katika Mto huu nilikuwa naongea na ndugu yangu CEO wa DAWASA aliniambia kwamba mitambo yake sasa inaungua kwasababu kina cha maji kimepungua sana na maji yanapungua kwasababu watu wanalima hivyo michanga inaingia kwenye mto kina kinapingua" -Ngonyani.

Aidha amesema kuwa kutokana na wakulima hao wanaolima kando ya Mto kwa kutumia mbolea za chumvi chumvi kunapelekea usalama wa maji hayo kupotea kwa watumiaji hivyo watu wafuate sheria ili kulinda maji ya Mto huo.

"Tumeamua kusimamia sheria hatutawabakisha, leo tunafyeka mazao yote yaliyopo ndani ya Mita 60 lakini kinachofuatia nyumba ambazo zipo ndani ya Mita 60 zenyewe pia tutazifanyia kazi"- Ngonyani.

Afisa  Maji  Bodi ya Maji Bonde la wami/Ruvu Simon Ngonyani (wa kwanza kulia) akiongoza zowezi la kufyeka mazoo mbalimbali yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu leo mkoa wa Pwani..(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Muonekano wa mazoo yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu mkoa wa Pwani.
Ufyekaji wa mazao yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu mkoa wa pwani ukiendelea.
Muonekano wa mto Ruvu uliopo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

TCAA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA USAFIRI WA ANGA DUNIANI JIJINI DAR

$
0
0
Bango lenye Kauli Mbiu,' HAKUNA NCHI ITAKAYOBAKI NYUMA' ikiwa ni ujumbe wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wafanyakazi na wananchi walioungana katika kilele cha maadhimisho ya  Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta (wa piku kulia) akipokea maandamano katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta (wa kwanza kushoto) akipandisha bendera ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi na wananchi wakimshangilia Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta alisema kuwa Tanzania kama mwanachama hai wa ICAO, imeendelea kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo ili kukuza sekta na kuifanya itoe mchango wake kikamilifu.

 Alisema jitihada za TCAA za kuboresha miundombinu pamoja na raslimali watu zimeanza kuzaa matunda. Matokeo mazuri ya ukaguzi uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) mwaka 2017 kuhusu uwezo wa Tanzania katika kusimamia na kudhibiti usalama wa sekta ni udhibitisho tosha ambapo matokeo ya ukaguzi yaliyotolewa Septemba 2017 yalionyesha uwezo wa Tanzania wa kudhibiti sekta umeongezeka toka 37.8 (2013) hadi asilimia 64.35 (2017). Alama hizo zinaifanya Tanzania kuwa juu ya kiwango cha wastani wa asilimia 60 kilichowekwa na Shirika hilo.

TRA YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA UANDAAJI VITABU VYA HESABU

$
0
0

Na Veronica Kazimoto ,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa jumla katika tuzo za uandaaji wa hesabu bora mwaka 2017 zinazotolewa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere, amewaasa wahasibu nchini kuwasaidia wateja wao kuandaa vitabu vya mahesabu kwa kufuata viwango vya kimataifa ili kuepuka kufanya marekebisho ya vitabu hivyo na kupotea kwa kodi.

Amesema taasisi nyingi zimekuwa hazijui kuandaa vitabu vya mahesabu na wakati mwingine hulipua katika kuviandaa ambapo matokeo yake vimekuwa vikikataliwa na kutakiwa kurudia mahesabu hayo hali ambayo inafanya kazi hiyo kuwa ngumu na wakati mwingine inaleta mashaka. Kichere amesema siri ya ushindi wao ni ushirikiano mzuri walionao kama mamlaka ikiwa ni pamoja na kutoa muda wa ziada wa kazi ili kuweza kukidhi viwango vya kimataifa na kama taasisi ya kukusanya mapato lazima ifanye hivyo.

“Tumefurahi kupata tuzo hii inayoonyesha kuwa, tunatengeneza mahesabu yetu kwa kufuata taratibu na viwango vya kitaifa katika uandaji wa vitabu vinavyohusiana na fedha. Tumekuwa na ushirikiano mzuri na wahasibu wetu ambao mara zote wamejitolea muda wao ili kukidhi vigezo hivi vya kimataifa,” amesema Kichere. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ambaye alikuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hizo, aliwaambia wahasibu kuwa, imani yake ni kwamba, siku tatu walizokutana wamezitumia vizuri kwa kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu kwa undani.

Amesema kuwa amefurahishwa na namba ya wahudhuriaji wa mkutano huo wa wahasibu ambayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka jambo ambalo limewawezesha kujadili kwa undani changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utendaji wa kazi zao. Kabla ya ushindi huo wa jumla, TRA ilipata ushindi wa kwanza katika kipengele ya kushindanisha Taasisi za Serikali ambapo Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lilikuwa la pili na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ilikuwa ya tatu.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji akimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (wa tatu kulia) akiwa ameshikilia tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (wa tatu kulia) akiangalia kwa makini tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam. 

JWTZ YATANGAZA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI MADAKTARI WA BINADAMU NA FANI NYINGINE ZA TIBA

$
0
0

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.
      Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji  ya sasa na siku zijazo.
      Watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifatazo:-
a.           Daktari Bingwa wa Meno    -  Dental Surgeon
b.          Daktari Bingwa     -       Specialist Neurasurgeon
c.           Mkemia   (Chemisist)
d.          Mteknolojia Msaidizi (Maabara) - Assistant Laboratory Technician.
e.           Tabibu msaidizi     -  Assistant Clinical officer.
f.            Katibu wa Hospitali  - 
g.          Msaidizi wa kumbukumbu.  – Medical Records (Certificate)
h.          Daktari           - Medical Doctors.
j.      Afisa Muuguzi  -  Registered Nursing Officer. 
k.     Fundi sanifu vifaa tiba  -  Bio Medical Engineer.
l.      Tabibu   - Clinical Assistant  (Certificate).
m.    Mteknolojia msaidizi -  Laboratory Assistant (Certificate)
n.     Mfamasia -  Pharmacist  (Degree)
o.     Mtoa tiba kwa vitendo  - Physiotherapist  (Diploma)
p.     Afisa Muuguzi msaidizi  - Assistant Nursing officer

Sifa za kuandikishwa Jeshini ni zifuatazo:-
a.    Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
b.    Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist
c.     Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.
d.    Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri
e.    Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.
f.     Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).
g.    Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi.
h.    Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

       Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika Kambi yaJenerali Abdallah Twalipo, Mgulani    Dar es Salaam tarehe              17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.
Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa usafiri, chakula na malazi.
Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao. 
JIUNGE NA JWTZ UJIFUNZE MENGI, UONE MENGI NA UFAIDI MENGI

WAZIRI LUGOLA AMSWEKA SELO AFISA MTENDAJI KWA KUTAFUNA FEDHA ZA WANANCHI MWIBARA

$
0
0
Na Ripota Wetu, MARA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemsweka ndani Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, kwa kosa la kutafuna fedha za wanakijiji wilayani humo.

Waziri Lugola ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo alitoa maamuzi hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi hao uliofanyika kijijini hapo leo, baada ya kuwataka wananchi wenye malalamiko, maswali pamoja na ushauri watoke mbele ili aweze kuwasikiliza wananchi hao.

Baada ya agizo hilo, zaidi ya wananchi kumi walijitokeza na kuuliza maswali pamoja na kutoa kero zao, ndipo watu saba kati ya waliotoka mbele wakiwa wamepanga foleni walitoa tuhuma mbalimbali kuhusiana na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Wilbard Malea kutafuna fedha zikiwemo fedha za maendeleo ya kijiji pamoja na za faini kutokana na mashtaka yanayowasilishwa na wananchi kwake kwa ajili ya usuluhishi pamoja na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mkazi wa Kijiji hicho, Simon Joseph alimtuhumu katika mkutano huo, Mtendaji huyo alimfuata katika kikundi chao cha Muungano cha kuweka na kukopeshana alisema anaomba kukopa fedha shilingi 91,000 na kijiji kitarudisha fedha hizo, lakini mpaka leo hajazilipa na hakutumwa na Serikali ya Kijiji bali alisema uongo ili ajipatie kwa njia ya udanganyifu.

Pia Happyness Tabonwa mkazi wa kijiji hicho, alimlalamikia mtendaji huyo amechukua mbuzi wake watatu baada ya kushindwa kulipa shilingi 50,000, akaamua kuwakamata mbuzi hao na baada ya kumpeleka elfu 50 anayoidai Mtendaji huyo akashindwa kuwarudisha mbuzi hao kwa kuwa alishawauza na pesa kazitafuna.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimuuliza maswali Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Wilbard Malea, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijji hicho, leo. Mtendaji huyo alikiri kutafuna fedha za wanakijiji hao na aliahidi kuzirudisha. Hata hivyo, Lugola alimsweka ndani Mtendaji huyo kutokana na kosa hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 52 MUHIMBILI

$
0
0
 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd akimkabidhi madawati 52 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. John Rwegasha kwa ajili ya wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu hospitali hapo. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akishuhudia tukio hilo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga. Msaada huo una thamani ya Tsh. 10 milioni.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikagua madawati hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Muhimbili, John Rwegasha, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kabla ya NMB kukabidhi msaada wa madawati hayo kwa uongozi wa Muhimbili.
 Mkazi wa Kurasini jijini Dar es Salaam, Mariam Shaban akiishukuru Muhimbili pamoja na NMB kwa kuwapatia madawati hayo ambayo watayatumia kusubiri ndugu na jamaa  wakati wakipatiwa matibabu na wataalam wa afya. Pia, Bi. Mariam amemweleza Naibu Waziri jinsi wataalam wa Muhimbili walivyompokea vizuri mgonjwa wake na kuanza kumpatia matibabu kwa wakati.
Dkt. Ndugulile akizungumzia huduma za afya zinazotolewa na Muhimbili baada ya kukagua madawati hayo leo.


MADAKATARI BINGWA MAGONJWA YA MOYO KUTOKA SAUDI ARABIA WAMALIZA KAMBI YA MATIBABU

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea ngao kutoka kwa Dkt. Jameel Alata ambaye ni mkuu wa msafara wa wataalamu wa afya kutoka mradi wa Little Heart wa nchini Saudi Arabia ambao walikuwa katika Taasisi hiyo kati ya tarehe 2-8 Desemba, 2018 kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ambayo iliandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Taasisi ya misaada ya MUNTADA ya Uingereza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya Tanzania.
Baadhi ya madaktari kutoka mradi wa Little Heart kutoka Saudi Arabia ambao ni mradi wa afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao makuu yake mjini London nchini Uingereza wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza madaktari hao baada ya kumalizika kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya kuzaliwa nayo iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Madaktari hawa walikuwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete kati ya tarehe 2-8 Desemba kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ambayo iliandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Taasisi ya misaada ya MUNTADA ya Uingereza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya Tanzania.
Mufti Abubakari bin Zuberi akimkabidhi Katibu Mkuu wa Taasisi ya Dhi Nureyn Bw. Shams Elmi Obsiye ngao ya kuipongeza Taasisi hiyo kutokana na kuwa kiunganishi kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mradi wa Little Heart wa nchini Saudi Arabia ambao walifanya kambi ya matibabu ya moyo na kutibu watoto 70 na watu wazima wawili wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo kuanzia tarehe 2-8 Desemba, 2018. Kambi hii ya matibabu ya hisani iliandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Taasisi ya misaada ya MUNTADA ya Uingereza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya Tanzania.

TASWA YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA MAPENDEKEZO YA KATIBA YAKE

$
0
0
KAMATI ya Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), imekamilisha Rasimu ya Kwanza ya Mapendekezo ya Katiba ya chama hicho na itaanza kutolewa kwa wadau mbalimbali leo Jumapili Desemba 9, 2018 kwa ajili ya kujadiliwa.

Hatua ya kuandaa rasimu hiyo ya kwanza imefanywa na Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA kwa kuangalia Katiba za vyama mbalimbali duniani vinavyohusiana na waandishi wa habari za michezo na pia kupitia muongozo kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), ambacho TASWA ni mwanachama.

Pia Kamati imechambua Katiba ya sasa ya TASWA na kupokea maoni kutoka kwa waandishi wa habari za michezo kuhusu maeneo yenye upungufu kwa nia ya kuiboresha.Maeneo mbalimbali yamefanyiwa kazi katika rasimu hiyo baadhi yakiwa ni sifa za mwanachama, wajibu wa mwanachama, muundo wa uongozi, sifa za viongozi na pia ukomo wa uongozi.

Pia kuna mapendekezo katika rasimu hiyo ya kuanzishwa kamati mbalimbali kwa nia ya kuisaidia Kamati ya Utendaji.Kutokana na hali hiyo, Kamati imepanga hatua ya kwanza baada ya kuitoa rasimu hiyo leo, itapokea maoni binafsi ya wadau kwa njia ya email (katibataswatz@yahoo.com), kisha itakutana na wahariri wa habari za michezo, waandishi waandamizi na waandishi chipukizi kwa kadri mtakavyotaarifiwa.

TAASISI YA ULINGO WAFANYA USAFI SOKO LA MWANANYAMALA, WAHIMIZA WANAWAKE NCHINI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

$
0
0
Na Said Mwishehe Globu ya Jamii

TAASISI Ulingo ambayo inajihusisha na kusimamia wanasiasa wanawake wa vyama vyote nchini imefanya usafi kwenye Soko la Mwananyamala jijini Dar es Salaam huku ikitumia nafasi hiyo kuwahimiza wanawake wanaofanya kazi katika shughuli mbalimbali kuhakikisha wanashiriki kugombea nafasi zenye maamuzi.

Mbali ya kuhimiza wanawake kushiriki kugombea nafasi zenye maamuzi, pia wamekemea tabia ya vitendo vya rushwa ya ngono ambapo wamesema wanaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekuwa mstari wa mbele kukomesha vitendo vya rushwa ikiwamo rushwa ya ngono.

Wakizungumza leo mapema asubuhi wakati wa kufanya usafi kwa kufagia maeneo yanayozunguka soko hilo la Mwanayamala ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, wadau mbalimbali wa taasisi hiyo wakiongozwa na viongozi wao wamesema wao kama taasisi inayosimamia wanasiasa wanawake wamekuwa na jukumu la kuendelea kuhamasisha wanawake nchini unapotokea uchaguzi washiriki ili wawe sehemu ya nafasi za maamuzi.
Makamu Mwenyekiti wa Ulingo Nancy Mrikaria akishiriki kufanya usaifi na wanachama wenzake kwenye soko la Mawananyamala kama maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake ambapo kilele chake kitafanyika Desemba 10 mwaka huu.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Bi Saumu Rashid akibandika kipeperushi chenye ujumbe wa kuhamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya maamuzi na kupinga ukatili dhidi ya wanawake katika moja ya kuta za soko la Mwananyamala wakati wanachama wa taasisi hiyo walipofanya usafi sokoni hapo leo. 
Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya wanachama wa Taasisi ya Ulingo wakishiriki kufanya usafi katika soko la Mwananyamala ambapo pia wamewahamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya kufanya maamuzi.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Bi Saumu Rashid akishiriki kufanya usafi katika soko la Mwananyamala pamoja na wenzake.
Mmoja wa wanachama wa Taasisi ya Ulingo Salma Masoud akibadika kipeperushi chenye ujumbe wa kuhamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya maamuzi na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake katika moja ya bajaji katika soko la Mwananyamala.


Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya

$
0
0
Mtumishi wa Wizara ya Afya kitengo cha maabara na mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma Mbwana Saidi Mbela , ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tigo Jigiftishe na kukabidhiwa zawadi yake jijini Da es Salaam.

Mbela anakuwa ni mshindi wa tatu wa zawadi ya shilingi milioni 10 ambayo hutolewa kila wiki kwa mshindi mmoja kupitia Promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe. Milioni 10 ya kwanza ilichukuliwa na David Mmuni huku ya pili ikienda kwa Iyaka Seifu Muinga.

Mbela aliungana na washindi wengine wanne ambao ni washindi wa kila siku ambao walikabidhiwa shilingi milioni moja moja .Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyika eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam, Mbela alisema alipigiwa simu kuwa ameshinda akiwa likizo jijini Dar es Salaam ambapo alikuja kumtembela shangazi yake.

“Niliamua kutumia likizo yangu kuja jijini Dar es Salaam kumsalimia shangazi yangu. Nilipofika tu nyumbani kwake Chamazi, nikapigiwa simu ya kuambiwa kuwa nimekuwa mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10,” anasema. Mbela aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusema kuwa atatumia fedha hizo kumalizia nyumba yake.
 Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa kwanza kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Shadya Bakari (kulia) wa Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo
 Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa tatu kulia) akipongezwa na washindi wa kila siku wa shilingi milioni moja moja pamoja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika halfa iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam 
 Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Theresia Philipo (wa kwanza kulia) akilia kwa furaha wakati akikadihiwa  mfano wa yenye thamani ya shilingi milioni moja na Shadya Bakari (wa kwanza kushoto) kutoka Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA NA TUZO MBILI ZA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2017

$
0
0

Na Peter Haule. WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50) linalohusika na masuala ya utawala, na Fungu ishirini na tatu (Vote 23) la Mhasibu Mkuu wa Serikali yamepata tuzo ya mshindi kwa nafasi ya pili na tatu katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, taaluma ya Uhasibu inamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kwa kuwa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wanahusika moja kwa moja katika suala la utawala na uongozi kupitia mipango, kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali na pia kuweka mazingira bora ya uwekezaji kuelekea katika maendeleo ya uchumi wa viwanda hivyo kuwa na tija katika agenda hiyo ya Taifa.

“Ni wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania inakua na uchumi wa kati ifikapo 2025, jambo hili haliwezi kufikiwa na Serikali pekee bali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao wanaweza kutumia taaluma yao na kuishauri Serikali kwa njia mbalimbali, ikiwemo mijadala inayotokana na mikutano ya mwaka ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu”, alieleza Dkt. Kijaji.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akielezea kuhusu taaluma ya Uhasibu kuwa nia muhimu katika maendeleo ya Viwanda   na kutimiza ndoto ya Serikali ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mwaka wa Wahasibu na kugawa tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa washindi wa mwaka 2017, katika Kituo cha  Uhasibu na Ukaguzi eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akimkabidhi tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23, Bw. Aziz Kifile, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
hasibu mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango fungu 50, Bw. Mwita Wambura (katikati) akiwa amenyenyua tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (katikati), Mhasibu Mkuu wa Fungu 50 Bw. Christopher Nkupama (wa pili kushoto), Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23, Bw. Aziz Kifile, na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa na furaha baada ya kupokea tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 


Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images