Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO SOPHIA KIZIGO AONGOZA OPERESHENI YA KUONDOA WAVAMIZI NDANI YA HIFADHI

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

KAMATI ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo imeamua kufanya operesheni maalumu ya kusaka na kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo kuna watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.

Akizungumzia operesheni hiyo Mkuu wa Wilaya Kizigo ameiambia leo, Michuzi Blog kuwa wameanza kuifanya juzi na jana (Desemba 4 na Desemba 5 mwaka 2018) ambapo mbali ya kamati ya ulinzi na usalama pia kulikuwepo na vikosi kazi na timu ya wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya hiyo na kwamba uamuzi huo wa kufanya msako umekuja baada ya doria ya kwanza iliyofanyika kwa njia ya anga (ndege) ambapo walijionea uharibifu uliofanyika kwenye hifadhi ya Ushoroba wa Selous , Niassa, Mbarang'andu , Kisungule na Kimbanda.

"Kwa kutumia usafiri wa anga ambao tumefanya kwenye maeneo mbalimbali ya hifadhi tumejionea namna ambavyo kuna uharibu wa mazingira.Hivyo jana tumeamua kufanya msako maalumu wenye lengo la kuwaondoa wavamizi ambao wanaharibu hifadhi hiyo,"amesema Mkuu wa Wilaya Kizigo.

Amesema katika kuhakikisha wanafanikiwa kwenye operesheni hiyo juzi na jana waliamua kwenda kwa miguu maeneo ambayo yamefanyiwa uharibifu na tayari kuna baadhi ya watu ambao wamewakamata kwa kutuhuma za kuharibu hifadhi ambapo pia amesema wapo watu ambao wanaingia kwenye msitu huo kwa ajili ya kufanya ujangiri kwa kuua wanyama.


KAMATI ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo wakiendelea kukamata vifaa mbambali vya watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo kuna watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.
Sehemu ya Kamati i ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo (wa pilia kulia) wakiwa kwenye operesheni maalumu ya kusaka na kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo kuna watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.
Baadhi ya Watuhumiwa waliokamatwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo  (hayupo pichani) walipokuwa wakifanya operesheni maalumu ya kusaka na kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Tanzania kuwakilishwa na waogeleaji wanne Mashindano ya Dunia China

0
0
Tanzania itawakilishwa na waogeleaji wanne katika mashindano ya dunia ya kuogelea yaliyopangwa kufanyika nchini China kuanzia Desemba 11 mpaka 16 eneo la Hangzhou Olympic and International Expo Center. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Asmah Hilal aliwataja waogeleaji hao kuwa ni Kalya Temba na Celina Itatiro kwa upande wa wanawake na Collins Saliboko na Hilal Hilal watawakilisha upande wa wanaume.

Asmah alisema kuwa kocha maarufu nchini, Alexander Mwaipasi na Mwenyekiti wa chama chao, Imani Dominick wataambatana na timu hiyo nchini China. Alisema kuwa Kayla na Celina wameondoka jana usiku wakati Collins ataungana na wenzake mjini Hangzhou akitokea Uingereza na Hilal atakenda China akitokea Dubai.

Alisema kuwa waogeleaji hao wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo ambayo pia yataambatana na mkutano mkuu wa Shirikisho la Mchezo wa kuogelea duniani (Fina) na kozi ya makocha, Mkutano Mkuu wa Fina na kozi ya makocha utaanzia kesho.  “ Ni matarajio yetu kuwa watafanya vizuri pamoja na changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo, mashindano yatakuwa magumu kwani waogeleaji nyota wa Dunia nao watakuwepo,” alisema Asmah.

Mashindano hayo ya 14 yatafanyika kwenye bwawa la kuogelea la mita 25 ambalo ni la kisasa zaidi limejengwa na kampuni ya Italia ya Myrtha Pools na linahamishika. Bwawa hilo la kuogelea limejengwa kwenye uwanja wa tenisi na litaondolewa na kuwekwa eneo la wazi ambalo litatumiwa na jamii.
Waogeleaji wa Tanzania, Celina Itatiro (wanne kutoka kushoto) na Kayla Temba (wa tatu kutoka kulia) katika picha ya pamoja na uongozi Chama cha kuogelea na nchini (TSA) na wazazi mara baada ya kuondoka jana kwenda Hangzhou, China kushiriki mashindano ya Dunia. Katikati ni kocha wa timu hiyo, Alexander Mwaipasi.

UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI

0
0
Na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania
Mahakama ya Tanzania iliingia mkataba na Shirika la Posta kuhakikisha kuwa huduma ya kusambaza nyaraka mbalimbali za Mahakama inatolewa kwa nchi nzima. Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni (The post at your door step) iliyoanzishwa na Shirika la Posta, umelipa jukumu la kukusanya na kusafirisha/kusambaza nakala za hukumu na nyaraka mbalimbali za Mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anuani zao na mahali walipo (Anuani za makazi).

Kwa kipindi kirefu kumekuwa na malalamiko miongoni mwa wananchi/wateja wa Mahakama juu ya usumbufu katika upatikanaji wa Nakala za hukumu na baadhi ya nyaraka za Mahakama, hali ambayo kwa namna moja au nyingine ilisababishwa kwa kutokuwa na taarifa sahihi za Mdaawa/Mteja na utaratibu stahiki wa ufikishaji wa nyaraka hizo. Mahakama ya Tanzania katika utekelezaji wake wa majukumu mbalimbali inawalenga wateja wake ili kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati na kuimarisha imani ya Wadau kwa Mahakama. Utoaji wa huduma kwa wateja pamoja na mambo mengine unajumuisha utoaji wa nyaraka mbalimbali kama nakala za hukumu, wito wa kuitwa Mahakamani (Sumons).

Aidha; nyaraka muhimu zinazosambazwa kupitia huduma ya Posta Mlangoni ni Nakala za Hukumu ‘Judgment’, ‘Summons’ wito wa Mahakama, Mwenendo wa shauri/mashauri ‘Proceedings’, Maamuzi ‘Rulings’,  Amri ‘Order’, Tuzo ‘Award’/ ‘Decree’. Akizungumza kabla ya utiani saini wa mkataba huo Aprili, 2018, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga alisema kuwa hatua hii ni mwendelezo wa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ili kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.
 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (katikati) akitia saini Mkataba wa utoaji huduma ya Posta mlangoni (The post at your door step), anayeshuhudia kulia ni Msajili Mkuu- Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati aliyeketi kushoto ni Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe, wanaoshuhudia (waliosimama) ni baadhi ya Viongozi/Maafisa kutoka Mahakama na Shirika la Posta.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe akitia saini Mkataba huo.
Makabidhiano ya Mikataba hiyo mara baada ya kuhitimisha zoezi la utiaji saini. Kulia ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na kushoto ni Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe.
 Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia) akiongea jambo mara baada ya utiaji saini wa Mkataba huo.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UHAMASISHAJI WA USAFI WA MAZINGIRA WILAYA YA CHEMBA WAFANYIKA

0
0
Na Shani Amanzi
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga amewataka Wananchi wa Chemba kujali afya zao kwa kufanya usafi wa mazingira kuanzia majumbani kwao ikiwemo  kuwa na vyoo bora ili kuzuia magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindu pindu.

Mhe.Simon Odunga ameungana sambamba na Rais wa  Awamu ya Tano Mhe ,Rais John Pombe  Magufuli  na kuridhia ,Tamko la Rais la kuhakikisha kaya zote katika Wilaya  ya Chemba zinakuwa na vyoo bora.

 “Ntahakikisha kila kaya inakuwa na vyoo bora na kuvitumia  ,kwa kaya nyingine ambazo hazina vyoo naelekeza  kwa viongozi wenzangu na vijana  kama tulivyokubaliana  kuanzia 25/12/2018  kila kaya iwe na choo bora na kukitumia na kuagiza viongozi wotewanaohusika katika  ngazi zote za wilaya, Kata,Tarafa ,Vijiji na Vitongoji kusimamia kikamilifu agizo langu hili”aliongeza kwa kusema  hivyo Mhe.Simon Odunga.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus  Mashimba ameipongeza Wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto   na Msanii Mrisho Mpoto  kwa kuwa na ubunifu wa uhamasishaji ,kwani wilaya  ya Chemba wameitika kwa mwitikio mkubwa na kupokea ujumbe huo.

 Aidha Dkt.Mashimba amesema  “katika taarifa ya ya robo mwaka July,September jumla ya kaya 60,576 zilitembelewa kati ya hizo kaya zenye vyoo vya muda ni 47,487  sawa na asilimia 78.4 na kaya zenye vyoo vya kudumu ni 11,920 sawa na asilimia 19.7 na changamoto iliopo ni baadhi ya jamii kutoezeka  vyoo vyao,kwa imani ya kuogopa nyoka kuingia kwenye vyoo”
Naye Msanii Mrisho Mpoto amesema katika kampeni hii aliyoshirikiana na Wizara ya Afya ya kusema”Usichukulie Poa Nyumba ni Choo”wameweza kuzunguka Kata 10 ikiwemo Mondo,Jangalo,Goima ,Mrijo,Babayu,Kidoka ,Soya,Gwandi,Kelema na Chemba  wamefarijika sana kwani mwitikio wa wananchi ni mkubwa  bali kata moja tu ambayo ni ya Babayu imeonekana ina idadi kubwa ya kaya zisizo na vyoo.

Hata hivyo sheria ndogondogo za Halmashauri zinaendelee kutumika katika kuwabana wasio na vyoo pamoja na wasiokamilisha ujenzi wa wa choo bora,aidha kampeni hiy ya uhamasishaji wa mazingira imehitimishwa katika kata ya Chemba ambapo kampeni hiyi ilifanyika ndani ya siku tano kuanzia Tarehe 1 mpaka5/12/2018 ilipomalizika katika uwanja wa Godown,Chemba.

SERIKALI KUIMARISHA UHUSIANO NA NCHI YA FALME ZA KIARABU

0
0
 Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad  Masauni, akizungumza  wakati  wa  Hafla  ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam. Ambapo aliahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akichagua  tiketi ya mchezo wa bahati nasibu iliyoendeshwa  wakati  wa  Hafla  ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam.
 Naibu  Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni(wapili kulia) na Viongozi wengine wa Ubalozi wa Nchi ya Falme za Kiarabu wakimkabidhi  Ali Suleiman Ali ,zawadi ya tiketi ya ndege  kwenda nchini Dubai na kurudi baada ya kuibuka mshindi katika bahati nasibu iliyochezeshwa wakati  wa  Hafla  ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal (wapili kushoto), akiongozana  na  Balozi  wa  Nchi  ya  Falme za  Kiarabu hapa  nchini, Khalifa  Abdulrahman  Mohamed  Al- Marzooqi (watatu kushoto), Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni (wanne  kushoto)  na  wageni  waalikwa   wakitoka  nje  ya  ukumbi  baada  ya kumalizika  Hafla  ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Balozi wa Nchi ya Falme za Kiarabu ,Khalifa Abdulrahman Mohamed Al- Marzooqi (kulia), baada ya kumalizika kwa Hafla ya  Kusheherekea  miaka  47  ya  Siku  ya  Taifa   la  Nchi  ya  Falme  za   Kiarabu,  lililofanyika  katika  Ubalozi  wa  nchi  hiyo, jijini  Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

AWESO AFANYA ZIARA RUANGWA NA NACHINGWEA -LINDI

0
0
Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) leo amehitimisha ziara Ruangwa Mkoani Lindi kwa kukagua miradi ya Kitandi, Mihewe na Mbekenyera. Aidha Mheshimiwa Aweso amefanya ziara Wilayani Nachingwea kwa kukagua miradi ya Mtua na Chimbendenga.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipewa maelezo juu mitambo ya kusafisha maji ya mradi wa Mbekenyera - Ruangwa.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiongea na Mkazi wa Mtua alipokuwa akikagua mradi wa maji katika kijiji hicho wakati wa ziara yake aliyoifanya leo.
Naibu wa Maji Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa Chimbenenga Nachingwea wakati wa wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji.

NHIF kuanza kampeni ya uandikishaji kijiji kwa kijiji

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akionyesha kitambulisho cha matibabu kupitia mpango wa Ushirika Afya kabla ya kukabidhi kwa wanachama waliojiunga kwenye kampeni ya uhamasishaji aliyoifanya katika Mkutano wa hadhara katika eneo la Kitangali Wilaya ya Newala.


Na Grace Michael, Tandahimba

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema unaanza rasmi kampeni ya uandikishaji ya kijiji kwa kijiji katika Mikoa ya Mtwara na Lindi ili kuwawezesha wananchi hao kuwa kwenye utaratibu mzuri wa kupata huduma za matibabu.

Imeelezwa kuwa, wananchi wamekuwa wakiingia katika umasikini mkubwa kwa kulazimika kuuza mali za familia kwa lengo la kupata fedha za kugharamia huduma za matibabu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga wilayani Tandahimba ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji walioambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika ziara yake ya kutembelea vituo vya huduma na uhamasishaji wa wakulima kujiunga na NHIF, kupitia Mpango wa Ushirika Afya.

“Nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri na wananchi wote walioko hapa, timu yangu inaanza rasmi kampeni ya kijiji kwa kijini kuanzia wiki ijayo kwa lengo la kumfikia kila mkulima aliyeko katika Mkoa wa Mtwara na Lindi ili wananchi hawa wawe kwenye mfumo bora wa kupata huduma za matibabu wakati wowote,” alisema Bw. Konga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi wa huduma za matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba. 

Alisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wote wako kwenye sekta ya kilimo hususan maeneo ya vijijini na kwa kutambua umuhimu wa kulitunza kiafya kundi hili, Mfuko ulianzisha mpango maalum unaojulikana kwa jina la Ushirika Afya unaowawezesha kujiunga na huduma za NHIF kwa gharama nafuu.

Akizungumzia upatikanaji wa huduma za matibabu, Mhe. Waziri Ummy, alisema kuwa Serikali imetengeneza utaratibu rahisi kwa wananchi wake juu ya upatikanaji wa huduma za uhakika za matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao una jukumu la kugharamia matibabu kwa wanachama wake.
Wananchi wa Kitangali wilayani Newala wakiwa katika mkutano wa uhamasishaji wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. 

“Hakuna sababu yoyote kwa sasa ya kushindwa kujiunga na NHIF, Serikali ya Awamu ya Tano imeboresha huduma na upatikanaji wa dawa kwa sasa ni mkubwa ambao unamwezesha kila mgonjwa kupata huduma anazozihitaji hivyo nawaomba wananchi wote mjiunge na NHIF ili muwe na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote hata ambao hamna fedha,” alisema Mhe. Ummy.

Alisema kuwa suala la kulinda afya za wananchi ni suala muhimu kutokana na ukweli kwamba bila ya afya njema ama uhakika wa matibabu hakuna shughuli zozote za maendeleo zinazoweza kufanyika. Kwa upande wa wananchi wamemhakikishia Mhe. Waziri kuwa wako tayari kujiunga na NHIF na kuunga juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Walitumia nafasi hiyo kumuomba Mhe. Waziri kufikisha salaam zao kwa Mhe. Rais Magufuli kuwa wanaridhishwa na utendaji kazi wake hivyo wako tayari kuhakikisha ndoto zake za kuifanya Tanzania kuwa na Uchumi wa Kati zinafikiwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya Ushirika katika Wilaya ya Tandahimba. 

SERIKALI YAZISHAURI BENKI NCHINI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezitaka Benki nchini kushusha viwango vya riba za mikopo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi wakiwemo wakulima kunufaika na huduma za kifedha zinazotolewa na taasisi hizo za fedha kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua rasmi Tawi la Benki Azania, Sokoine, na kusisitiza kuwa Benki zina nafasi kubwa wa kuisaidia nchi kufikia azma yake ya kuwa ya viwanda ifikapo mwaka 2025 kwa kukuza mitaji na biashara za wananchi.

Alisema kuwa hivi karibuni Serikali imechukua hatua madhubuti za kiutawala na kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo katika soko zinapungua, ikiwemo Benki Kuu kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara, kushusha riba kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0.

"Tumepunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0, hatua ambazo zimesaidia kupunguza riba katika soko kutoka wastani wa zaidi ya asilimia 20 hadi asilimia 17" aliongeza Dkt. Kijaji

"kama haya yote yamefanyika, iweje benki ziendelee kutoza riba ya asilimia 17 kwa kisingizio cha kuogopa mikopo chechefu wakati Serikali kupitia Benki Kuu, imeanzisha kanzi data ya kuhifadhi na kutoa taarifa ya wakopaji (Credit Reference Bureau System)" alihoji Dkt. Kijaji
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya Azania, Sokoine, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Benki ya Azania, Sokoine Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya Azania, Bw. Eliud Sanga, baada ya kuhutubia katika ufunguzi wa tawi la benki hiyo la Sokoine Jijini Dodoma.


Tanzania kuwakilishwa na waogeleaji wanne Mashindano ya Dunia China

0
0
Dar es Salaam. Tanzania itawakilishwa na waogeleaji wanne katika mashindano ya dunia ya kuogelea yaliyopangwa kufanyika nchini China kuanzia Desemba 11 mpaka 16 eneo la Hangzhou Olympic and International Expo Center.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Asmah Hilal aliwataja waogeleaji hao kuwa ni Kalya Temba na Celina Itatiro kwa upande wa wanawake na Collins Saliboko na Hilal Hilal watawakilisha upande wa wanaume.

Asmah alisema kuwa kocha maarufu nchini, Alexander Mwaipasi na Mwenyekiti wa chama chao, Imani Dominick wataambatana na timu hiyo nchini China. Alisema kuwa Kayla na Celina wameondoka jana usiku wakati Collins ataungana na wenzake mjini Hangzhou akitokea Uingereza na Hilal atakenda China akitokea Dubai.

Alisema kuwa waogeleaji hao wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo ambayo pia yataambatana na mkutano mkuu wa Shirikisho la Mchezo wa kuogelea duniani (Fina) na kozi ya makocha, Mkutano Mkuu wa Fina na kozi ya makocha utaanzia kesho.

 “ Ni matarajio yetu kuwa watafanya vizuri pamoja na changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo, mashindano yatakuwa magumu kwani waogeleaji nyota wa Dunia nao watakuwepo,” alisema Asmah.

Mashindano hayo ya 14 yatafanyika kwenye bwawa la kuogelea la mita 25 ambalo ni la kisasa zaidi limejengwa na kampuni ya Italia ya Myrtha Pools na linahamishika. Bwawa hilo la kuogelea limejengwa kwenye uwanja wa tenisi na litaondolewa na kuwekwa eneo la wazi ambalo litatumiwa na jamii.
Waogeleaji wa Tanzania, Celina Itatiro (wanne kutoka kushoto) na Kayla Temba (wa tatu kutoka kulia) katika picha ya pamoja na uongozi Chama cha kuogelea na nchini (TSA) na wazazi mara baada ya kuondoka jana kwenda Hangzhou, China kushiriki mashindano ya Dunia. Katikati ni kocha wa timu hiyo, Alexander Mwaipasi.

EALA WINS IN SOCCER, BEATEN IN VOLLEYBALL AND NETBALL AS GAMES ENTER DAY 5

0
0
East African Legislative Assembly, Bujumbura, Burundi, 6th December, 2018: The East African Legislative Assembly posted mixed results as the Games entered Day 5 in Bujumbura yesterday.

In football, EALA got off to a good start by defeating Parliament of Kenya 2-1 in an entertaining match at the Centre Technique, Ngagara in Bujumbura. Ahmed Mwapambe and Wycliff Ketto scored the all-important goals for the victors while Senator Cleophas Malala reduced the deficit for the Parliament of Kenya.

Both teams started the game on a high note with end to end action. Striker, Senator Kipchumba Murkomen, could have given his team an early lead but failed to latch on to a pass by Hon David Gikaria. On the opposite side, star striker, Ibrahim Jamal upon receiving a pass from Hon Julius Maganda beat the defence but shot wide with the goalkeeper Rogers Okwiri beaten. The EALA striker was, however, carried off the pitch with a suspected collar bone injury after a collision with a Parliament of Kenya player.

Ahmed Mwapambe was later to beat Rogers Okwiri to give EALA the lead after tapping in the ball, moments after Kenya’s goalkeeper blocked a rasping shot by

Hon Kim Gai. In the second half, EALA resumed forcefully with the striking force making constant raids on the Parliament of Kenya backline. It paid off when Wyclif Ketto beat the defense line to unleash a block-buster in to the roof of the net for the second goal.

In other games of the day, Parliament of Uganda (women) won Parliament of Kenya by 3 Sets to 0. The victors won the first two sets 25-13 before taking 25-17 win to seal the lead.

In the second women’s match of the day, Parliament of Kenya beat EALA 3 sets to 0 (25-10) (25-5) and (25-19). In men’s volleyball, Parliament of Burundi beat EALA 3 sets to 0 scoring (25-16), (25-22) and (25-16). In netball, Parliament of Kenya won EALA 44-12 in a one-sided match.

More games are expected on December 6 as Burundi and Uganda play in the first netball match before Parliament of Kenya lock horns with Parliament of Tanzania in the second match.

Later in the afternoon, the Parliament of Uganda will face off with Parliament of Burundi in football inn the first match, before EALA takes the field to battle out with Parliament of Tanzania.
The Chief Guest, Senator Prof Sam Ongeri is introduced to Hon Dr Damas Ndumbaro, EALA player by captain, Hon Pierrre Claver Abega. EALA beat Parliament of Kenya 2-1.
Hon Julius Maganda with ball goes past Allan Opiyo of the Parliament of Kenya as Hon Gideon Gatpan races alongside.
EALA 's Hon Kim Gai jumps to block a shot from Parliament of Kenya player during the match. EALA lost by 3 sets to 0 to Parliament of Kenya.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Desemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Apson Mwang’onda, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Bw. Apson Mwang’onda amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kumuona na kuzungumza naye na amempongeza kwa uongozi mzuri unaochochea kasi ya maendeleo hususani katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Bw. Apson Mwang’onda ameitaja baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo kuwa ni mradi wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Power Project) na Ujenzi wa madaraja na barabara ambazo licha ya kurahisisha usafiri zitasaidia kuondoa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

“Mabadiliko ni makubwa sana ambayo yametokea, kuna miradi mikubwa mingi inafanyika sasa hivi, kwa hiyo mabadiliko ni makubwa kusema kweli na yote hayo ni kwa manufaa ya nchi, kwa hiyo nachoweza kusema amefanya kazi kubwa kwa maendeleo ya nchi” amesema Bw. Apson Mwang’onda.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Tano ili itekeleze mipango yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Taifa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Desemba, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, alipomtembela Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, wakati wanaagana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA VITANDA NA MASHUKA VYENYE THAMANI YA TSH. MILIONI 1O, KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

0
0


Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi akimkabidhi Mashuka na Kitanda Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) ni Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua) na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (alievaa tai rangi ya bluu) akimkabidhi Kitanda na Mashuka Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum (kulia) Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi na (kushoto) Meneja Uhusiano Faraja Kaziulaya kutoka Dar es Salam.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (alievaa tai rangi ya bluu) akimkabidhi Kitanda na Mashuka Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum (kulia) Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi na (kushoto) Meneja Uhusiano Faraja Kaziulaya kutoka Dar es Salam.
Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua) na Mdau wa mambo ya afya akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Vitanda na Mashuka kwaajili ya huduma za Kujifungulia katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja jengo la Dodoma.  

RC Chalamila awataka wamachinga mkoani Mbeya kujiendeleza kibiashara

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka wamachinga mkoani humu kujiendeleza na kuwa wafanyabiashara badala ya kupenda kuendelea kuwa wamachinga. Chalamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na HabariLeo kutolea ufafanuzi uamuzi wake wa kuwataka wamachinga waondoke kwenye maeneo yasiyokuwa rasmi.

Aliwataka wamachinga hao kutambua kuwa umachinga wao unapaswa kuwa kwa miaka mitatu na zaidi ya hapo wanapaswa kuanza kulipa kodi zote stahiki. 

Alisema.“Kuna mijadala inaendelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa nimewafukuza wamachinga mkoani kwangu sasa swali ni kuwa kama wao ni wapangaji unawafukuzaje, maana wanasema wamachinga wamefukuzwa, 

Ni vema wakafahamu kuwa umachinga haupaswi kuwa sifa ya kudumu, machinga sahihi inatakiwa uwe mabadiliko ya kuelekea kuwa mfanyabiashara wa kati katika eneo moja tulivu katika maduka.“ 

Pia Mkuu huyo wa Mkoa aliitaka ofisi ya Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoani humo kufuatilia ukuaji wa biashara za wamachinga hao ikiwa ni pamoja na kuwapatia elimu ya maarifa na ujuzi za biashara. 

Lakini pia alisisitiza kuwa anawapenda na anata kuona wananufaika na hivyo katika kutimiza adhma hiyo aliwataka kuwa na Saccos ya pamoja itakayowasaidia kupata mikopo kwa bei nafuu na hivyo kujipatia faida.

Alisema“Rais Dk John Magufuli anawapenda Machinga wote nchin, na amekuwa akitutaka viongozi kutowabughudhii na hivyo siye mkoani hapa tunaendelea kuzingatia maelekezo ya Mh Rais kwa utaratibu maalumu"

Aliwataka, wamachinga wote kutumia vema misamaha ya rais yenye nia njema kwa kufuata utaratibu na kukua katika biashara.

“Tuwafundihse Machinga kulipa kodi hata kama ni kidogo, ili kesho wakiwa wafanyabiashara wa Kati au wakubwa wawe tayari wamejenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari" alisema Rc Chalamila.

Dkt. Abbasi Awapiga Msasa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa

0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwasalisha mada kuhusu umuhimu wa Mawasiliano ya Kimkakati katika kuisemea Serikali wakati wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Leo Jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaonesha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa jarida Maalum utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli Leo Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akichangia Mada baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kuwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Mawasiliano ya Kimkakati katika kuisemea Serikali wakati wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Leo Jijini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mdeme akichangia Mada baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kuwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Mawasiliano ya Kimkakati katika kuisemea Serikali wakati wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Leo Jijini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi akisoma jarida Maalum utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli Leo Jijini Dodoma.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Theresia Mbando akisoma jarida Maalum utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt. John Magufuli Leo Jijini Dodoma.

Wajasiriamali wajitokeza kushiriki maonesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini

0
0
Wajasiriamali wakiwa na bidhaa zaa mbalimbali katika maonesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa  rasmi jana  jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji Stella Manyanya (hayupo michani)
Wajasiriamali wakiwa na bizaa mbalimbali katika maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji Stella Manyanya (hayupo michani) (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

KIPINIDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MICHUZI TV: MTOTO ATUPWA DAMPO MBEYA...

AWESO AFANYA ZIARA RUANGWA NA NACHINGWEA -LINDI

0
0
Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) jana  amehitimisha ziara Ruangwa Mkoani Lindi kwa kukagua miradi ya Kitandi, Mihewe na Mbekenyera. Aidha Aweso amefanya ziara Wilayani Nachingwea kwa kukagua miradi ya Mtua na Chimbendenga.
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipewa maelezo juu mitambo ya kusafisha maji ya mradi wa Mbekenyera – Ruangwa.
IMG_8213
 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiongea na Mkazi wa Mtua alipokuwa akikagua mradi wa maji katika kijiji hicho wakati wa ziara yake aliyoifanya jana IMG_8254
Naibu wa Maji Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa Chimbenenga Nachingwea wakati wa wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji.

TRA YAWATAKA MAWAKALA FORODHA KUHAKIKISHA NAMBA ZAO ZA UTAMBULISHO WA MLIPAKODI (TIN)

0
0
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imewataka Mawakala wa Forodha wote kuhakakisha wanafanya uhakiki wa namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza na kuisaidia mamlaka hiyo kukusanya mapato mengi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani wa mamlaka hiyo, Abdul Zuberi katika Semina iliyowakutanisha na makampuni ya mawakala wa forodha iliyojadili masuala mbalimbali ya kodi na ushuru wa forodha.

Amesema kuwa mawakala hao wanatakiwa kuhakiki TIN zao kutokana na kuwepo mkanganyiko kuwa na zaidi TIN hali inayowapa shida ya kutambua idadi ya mawakala wanaotakiwa kulipa kodi.“ Kuna watu wana TIN zaidi ya moja wanazitumia bila kufanyiwa uhakiki na wengine wanazifanyia udanganyifu inatupa tabu kuwatamabua hivyo ni vema mkazifanyia uhakiki,” amesema.

Amebainisha kuwa TRA mawakala watakaobainika kutumia TIN zaidi ya moja bila kuzifanyia uhakiki watachukuliwa hatua za kisheria.Amesisitiza kuwa mawakala wa forodha watakaofanya uhakiki wa TIN zao watapatiwa cheti cha utambulisho ili kuondokana usumbufu wakati wa kuwakagua.

Ameongeza kuwa mawakala wanatakiwa kuwasilisha taarifa sahihi za mapato yao kwa mwaka pamoja kulipa Kodi ya Ongezeko la Mapato (VAT).

RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mfumo wa rada ya kuongozea ndege nchini unaojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). 

Akizungumza na wanahabari waliofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo, Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa amesema ujenzi wa jengo hilo umekamilika na ufungaji wa vifaa unaendelea hivyo ifikapo Desema 21 wataweza kufanya majaribio. 

"Kama mnavyoona wanahabari kila kitu kimeshafanyika tunachomalizia ni mitambo midogo midogo inayotarajia kukamilika ifikapo wiki ijayo na tufanye majaribio ili kuona ni wapi pa kurekebisha au tuongeze kitu gani?," amesema Mwakisasa.

Nae mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye amesema mara baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, mfumo huo utaimarisha zaidi ulinzi wa anga la Tanzania. Amesema kwa kiasi kikubwa rada hiyo pamoja na zile zitakazojengwa Mwanza, Songwe na Kilimanjaro zitasimamiwa na TCAA ikiwamo kuziongoza ili kuhakikisha ulinzi unaimarishwa zaidi. 

Jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo wa rada liliwekwa Aprili 2, 2018 na Rais John Magufuli na utagharimu Sh67 bilioni zikijumuisha mfumo wa rada uliojengwa katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.
Jengo lililofungwa rada mpya kwa ajili ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. 
Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yanayohusu ujenzi huo. 
Mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye akieleza machache juu ya ujenzi huo wa rada mpya. 
Wanahabari waliofanya ziara katika mnara wa kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images