Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110149 articles
Browse latest View live

UNAIDS yaangalia namna ya kusaidia kituo cha Matumaini

$
0
0
Mkurugenzi wa Kijiji cha Matumaini, SR Maria Rosaria akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng ya dawa mbalimbali wanazotumia kwa ajili ya watoto hao wanaolelewa kwenye kijiji cha Matumaini mjini Dodoma kinachoendeshwa na masista wa Kanisa Katoliki, Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Yesu alipotembelea kituoni hapo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akimkabidhi zawadi za ‘Pampers’ Mkurugenzi wa Kijiji cha Matumaini, SR Maria Rosaria alipotembelea kituo hicho kinachowalea watoto yatima wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akimsalimia mmoja wa watoto yatima anayelelewa kwenye kijiji cha Matumaini mjini Dodoma kinachoendeshwa na masista wa Kanisa Katoliki, Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Yesu alipotembelea kituoni hapo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Mkurugenzi wa Kijiji cha Matumaini, SR Maria Rosaria akimtambulisha Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng kwa baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Afya cha kijiji cha Matumaini alipotembelea kituoni hapo kuwatia moyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akisalimiana na Daktari wa zamu wa kituo cha Afya cha kijiji cha Matumaini, Dr. John Zephania alipotembelea kituo hicho kinacholea watoto yatima kinachoendeshwa na masista wa Kanisa Katoliki, Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Yesu wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akimbariki mtoto yatima anayelelewa kwenye kijiji cha Matumaini mjini Dodoma kinachoendeshwa na masista wa Kanisa Katoliki, Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Yesu alipotembelea kituoni hapo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani. Amembatana na Mkurugenzi wa Kijiji cha Matumaini, SR Maria Rosaria.
Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima anayelelewa kwenye kijiji cha Matumaini mjini Dodoma kinachoendeshwa na masista wa Kanisa Katoliki, Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Yesu alipotembelea kituoni hapo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mjini Dodoma.



MBOWE , ESTER MATIKO 'MAMBO MAGUMU' , WARUDISHWA TENA MAHABUSU

$
0
0
Kuna kila dalili Sikukuu ya Krismass, Mwaka mpya wakasheherekea wakiwa ndani.

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

KESI ya tuhuma za uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko na wenzao saba inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepigwa kalenda hadi Desemba 21 mwaka huu.

Aidha Mahakama hiyo imetoa ruhusa kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuendelea kuhudhuria michezo ya Afrika Mashariki nchini Burundi na pia imeruhusu Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, kumuuguza mkewe ambaye amejifungua kwa upasuaji hivi karibuni.

Mbowe na Matiko wataendelea kukaa mahabusu kwa muda usiojulikana pengine hadi mwakani, baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusimamisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washitakiwa hao kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana.

Hatua hiyo imetokana na upande wa Serikali kukata rufaa kupinga uamuzi ya Jaji Sam Rumanyika aliyesema kuwa rufaa ya kina Mbowe ipo mahakamani hapo kisheria na kwa maana hiyo, haina mamlaka ya kuendelea na usikilizwaji wa rufaa hiyo.

Akitoa uamuzi huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Jaji Rumanyika alisema DPP anapewa mamlaka ya kukata rufaa kwa uamuzi mdogo ambao haumalizi kesi chini ya kifungu cha sita cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa na kwamba kunapokuwepo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani, mahakama ya chini haiwezi kuendelea na shauri.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko pichani nyuma wakirejeshwa  mahabusu kwa muda usiojulikana .

Muslim: Madereva fuateni sheria za Usalama Barabarani

$
0
0
Na Chalila Chibuda, Blogu ya Jamii
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim amewataka madereva wa kufuata sheria za Usalama ili kuokoa maisha ya wasafiri. Muslim aliyasema hayo wakati alipofanya ziara katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa katika mwisho wa mwaka kumekuwa na ungezeko la wasafiri nchi nzima hivyo madereva wazembe hawawezi kuvumiliwa hata kwa uzembe wanaoufanya.

Aidha amesema kuwa wataofanya makosa kwa kujirudia watawanyanga leseni na kutakiwa kurudi darasani ili wakajifunze udereva. "Kazi ya Udereva lazima iheshimike kwa kila mmoja awafuate sheria zilizoekwa na ziko wazi katika kufanya abiria kuwa salama katika safari wanazozifanya"amesema Muslim.

Hata hivyo amesema ukaguzi huo katika kituo cha Ubungo ni wa kila hivyo hakuna gari basi bovu litalofanya safari likwa na ubovu. Amesema usafiri kwa abiria ni kuwasafirisha kwa Usalama na sio kuwaua au kusababisha ulemavu wa kudumu.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim akiwa katika kituo cha mabasi Ubungo kwa akiangalia ukaguzi mabasi katika kituo cha mabasi leo jijini Dar es Salaam.
Ukaguzi chini ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim akiangalia ukaguzi na unaofanywa na Askari wa Kikosi hicho Ibrahim Samwix wakati alipofanya ziara katika kituo cha mabasi ya Ubungo jijini Dar es  Salaam. 

KORTI YAAHIRISHA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAMKABILI MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Aziz, kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Akram ambaye alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, 2018 na kufunguliwa kesi namba 82/2018 anakabiliwa na mashitaka 75 yakiwemo ya kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018 ambapo Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile kuwa kesi hiyo leo Desemba 6, 2018 imekuja kwa
ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Kutokana na taarifafa hiyo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, 2018 kwa ajili ya kutajwa.Akram anakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na nyara za Serikali, mashitaka 70 ya kukutwa na silaha, mashitaka mawili ya kukutwa na risasi zaidi ya 6,496 na moja la utakatishaji fedha.

Inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu mshitakiwa akiwa maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, alikutwa na nyara za Serikali ambayo ni meno sita ya tembo yenye thamani ya dola za Marekani 45,000 sawa na Sh 103, 095,000, mali ya Serikali.Pia inadaiwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni mkoani humo Akram alikutwa na nyara za Serikali ambazo ni nyama ya nyati yenye uzito wa kilogramu 65, yenye thamani ya dola za Marekani 1,900 sawa na Sh 4,352,900 mali ya Serikali bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapoli nchini.

Katika mashitaka ya tatu hadi la 72, kwamba siku hiyo na eneo hilo hilo, mshitakiwa huyo alikutwa na silaha aina ya Pistol bila ya kibali cha mrajisi wa silaha.Inadaiwa katika mashitaka ya 73 kuwa, Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay mshitakiwa alikutwa na risasi 4,092 na katika mashitaka mengine ilidaiwa mshitakiwa alikutwa na risasi 2,404 bila kuwa na kibali.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo hayo ya Oysterbay, Akram alitakatisha USD 9,018 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kujihusisha na makosa ya uhalifu.
Pichani kati ni Mfanyabiashara  Akram Aziz anaetuhumiwa na kesi ya uhujumu uchum

MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

MSANII nguli nchini kwenye tasnia ya filamu ya maigizo Hashim Kambi ahimiza nidhamu iwe ni kipaumbele kwa wasanii wenye majina maarufu pamoja na chipukizi katika kukuza  tasnia hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia mienendo ya baadhi ya wasanii ambapo amesema hairidhishi na inasababisha wasanii kutopata nafasi kwenye masoko ya nje huku akitolea mfano nchi jirani kama ya Kenya.

Kambi amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya wasanii wa Tanzania na Kenya ambapo, wasanii wa nchi hiyo wanazingatia nidhamu kwa kiwango cha hali ya juu bila kujali ukubwa au udogo wa jina na wanaheshimiana katika kazi zao za sanaa.

Pia amesema wasanii wenye majina  huwapa kipaumbele wasanii wakongwe ambao ambao wapo kwenye tasnia kwa muda mrefu na kuona ni fursa adhim kwa wakongwe hao kuendelea kutoa mafunzo na ujuzi ili kuleta mapinduzi katika sekta ya  filamu nchini.

Kuhusu sanaa yake ya uigizaji wa filamu , Kambi amesema kwa sasa ameshiriki kwenye filamu ya hukumu ya Msanii Rammy ambayo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu janga la dawa  ya kulevya  ambalo linaonekana kushamiri na kusababisha athari kwa vijana wengi nchini.
Msanii wa nguli wa filamu hapa nchini Hashim Kambi akizungumza na wanahabari kuhusu uzinduzi wa filamu ya Rammy Garis inayoitwa  hukumu yangu leo Jijini Dar es Salaam ,  iitakayozinduliwa Desemba 15 mwaka huu katika moja ya ukumbi uliyopo City mall.

MJANE WA DAUD BALALI AINGIA KWENYE MGOGORO WA ARDHI MBWENI MAPUTO

$
0
0
*Wanaoishi maeneo hayo wamuangukia Waziri William Lukuvi, wamuomba aingilie kati *Diwani ajitosa kuzungumzia ukweli eneo hilo...adai wananchi wamevamia, waondoke

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANANCHI wa Mtaa wa Mbweni Maputo jijini Dar es Salaam wapatao 270 wamemuomba Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuingilia kati mgogoro wa ardhi wa eneo ambalo linadaiwa kuwa ni mali ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Daud Balali(sasa marehemu) ambalo baada ya kuwa pori na kichaka cha uhalifu waliamua kusafisha eneo hilo na kisha kuweka makazi yao.

Wakizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo katika eneo hilo la mtaa wa Mbweni Matupo jijini Dar es Salaam wananchi hao ambao wanadaiwa kuwa ni wavamizi wameeleza wazi kuwa ni kweli wao waliamua kusafisha eneo hilo baada ya kuwa kero kwa wananchi wa maeneo hayo ya Mbweni na walifanya hivyo baada ya kuona limekaa muda mrefu bila kuendelezwa huku wakidai wamefuatilia wizarani na kubaini halina mwenyewe kwani ni eneo ambalo halijapimwa ila wanachokiona kuna watu wameamua kutengeneza hati ili kujionesha kama wao ndio wamiliki.

Wamewaambia waandishi wa habari kutambua kuwa katika eneo hilo hadi sasa kuna watu karibu watano wamekwenda na kila mmoja anasema la kwake.Hata hivyo wananchi hao wakiomba kuoneshwa hati hakuna mwenye hati miliki huku wakidai kuwa kwa kuwa wao wanyongwe watu wenye uwezo wa kifedha wanatumia kama fimbo ya kuwanyanyasa na kutishia kwamba waondoke na kinyume na hapo nyumba zao zitabomolewa.
 Baadhi ya wananchi wa Mbweni Maputo jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha kuangalia namna ya kuomba msaada wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kuingilia kati kwani kwa sasa wanaishi maisha ya hofu
 Mkazi wa Mtaa wa Mbweni Maputo jijini Dar es Salaam Raphael Joseph akizungumzia mgogoro wa eneo ambalo wao wameamua kufanya makazi baada ya mrefu kudai lilikuwa pori ambapo wanamuomba Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuingilia kati ili haki itendeke kwani kuna watu wanawatishia kuwaondoa  kwa nguvu
 Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mbweni Maputo Costantine Malifa akionesha barua ya kampuni ya udalali ya Sums JKT ambayo inawataka wananchi hao kuondoka ndani ya siku 14 kuanzia jana.Hata hivyo amekataa kuitambua hiyo kwa mdaia suala la eneo hilo liko mahakamani ,hivyo hawezi kutoa usharikiano kwenye jambo analoona linakwenda kinyume na sheria
 Diwani wa Kata ya Mbweni Hashimu Mbonde(kulia)akitoa ufafanuzi kuhusu eneo hilo ambalo amedai mmiliki halali ni Anna Muganda ambaye ni mke wa aliyekuwa Havana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Daud Balali ambaye kwa sasa ni marehemu.

NANYAMBA SASA KUPATIWA MENEJA WAKE WA TANESCO

$
0
0
Na Veronica Simba – Mtwara
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameuagiza uongozi wa juu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuteua na kupeleka Meneja atakayesimamia Halmashauri ya Nanyamba wilayani Mtwara, ili pamoja na mambo mengine aharakishe zoezi la uunganishaji umeme kwa wananchi. Alitoa agizo hilo jana, Desemba 5 akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kilimanjaro, Waziri Kalemani alisema ukosefu wa Ofisi ya TANESCO katika eneo hilo, ni mojawapo ya sababu zinazochelewesha zoezi la kuwaunganishia umeme wananchi. “Najua hapa hakuna Ofisi ya TANESCO. Mtu wa kuwahudumia anatoka Tandahimba. Hivyo naagiza, kuanzia kesho awepo Meneja hapa ambaye atasimamia Nanyamba peke yake.”

Miongoni mwa majukumu makuu ambayo Waziri alielekeza yatekelezwe na Meneja atakayeteuliwa ni pamoja na kuhakikisha ndani ya siku 20 kuanzia kutolewa kwa agizo, wananchi wote waliolipia wawe wameunganishiwa huduma ya umeme. Pia, alisema Meneja husika atawajibika kumsimamia mkandarasi anayeunganisha umeme katika eneo hilo kuongeza kasi ya kazi ili kushawishi wananchi wengi zaidi kulipia na kuunganishwa.

Aliagiza Meneja husika kuhakikisha anawafuata wananchi mahala walipo badala ya kukaa ofisini akisubiri wao wamfuate ili kupatiwa huduma. Aidha, Waziri Kalemani aliwaahidi wananchi wa Mtaa wa Kilimanjaro kuwa watapatiwa umeme kupitia mpango wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutokana na uhalisia wa eneo hilo kuwa na sifa za kijiji zaidi badala ya mtaa kama ulivyoainishwa.

“Mtaa wa Kilimanjaro na vitongoji vyake mtaunganishiwa umeme wa REA ambao gharama yake ni shilingi 27,000 tu,” alisisitiza. Waziri Kalemani aliwasisitiza wananchi kuandaa makazi yao kwa ajili ya kuunganishiwa umeme ikiwa ni pamoja na kutandaza nyaya za umeme. Aidha, aliwashauri wale wasio na uwezo wa kugharamia utandazaji wa nyaya za umeme katika nyumba zao, kutumia kifaa mbadala cha Umeme Tayari (UMETA), ambacho huuzwa kwa bei rahisi ya shilingi 36,000 tu.

Hata hivyo, Waziri alibainisha kuwa Serikali imetoa vifaa hivyo 200 bure kwa ajili ya wananchi watakaowahi kujitokeza ili kuunganishiwa umeme. Katika ziara hiyo, Waziri Kalemani aliwasha umeme katika moja ya nyumba ya mwananchi aliyeunganishiwa. Pia, alitembelea na kukagua miradi ya umeme, kuzungumza na wananchi na kuwasha umeme katika maeneo mengine kadhaa ikiwemo Namambi.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kilimanjaro, Manispaa ya Nanyamba wilayani Mtwara, akiwa katika ziara ya kazi Desemba 5, 2018.
 Umati wa wananchi wa Mtaa wa Kilimanjaro, Manispaa ya Nanyamba, wilayani Mtwara wakishuhudia Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) akiwasha umeme katika nyumba ya mmojawao ambaye amekwishaunganishiwa huduma hiyo. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi Desemba 5, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa eneo la Namamba wilayani Mtwara, alipopita kukagua zoezi linaloendelea la uunganishaji umeme, akiwa katika ziara ya kazi, Desemba 5, 2018.

KIGOMA YAFUNIKA KAMPENI YA MNADA KWA MNADA KARIBU TUKUHUDUMIE YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA leo imeendelea na kampeni yake ya Mnada kwa Mnada karibu tukuhudumie mkoani Kigoma ambayo elimu ya watumiaji huduma pamoja na huduma ya utatuzi wa matatizo yatokanayo ya matumizi ya huduma za mawasiliano zinatolewa.

 Akizungumzia kampeni hiyo inayofanyika katika mnada uliopo Mwanga sokoni Manispaa ya Kigoma Ujiji meneja wa TCRA kanda ya kati Bw. Antonio Manyanda amesema kampeni hii inayohusisha TCRA, Jeshi la polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni, watoa huduma wa Airtel, Halotel, Tigo, TTCL vodacom, startimes, Ting, Continental na Digitek inalenga katika  kusogeza huduma kwa wananchi wa kawaida na kujipanga na watoa huduma jinsi bora zaidi ya kutatua matatizo ya watumiaji wa huduma za mawasiliano.

Bw. Manyanda amesema wananchi watatatuliwa matatizo yao yote bila gharama zozote na unataka wakazi wa Kigoma na maeneo mengine kujitokeza kwa wingi wanaposikia kampeni imefika katika mikoa yao.

TCRA ikishirikiana na wadau  wake inaendesha Kampeni ya Mnada kwa Mnada Karibu Tukuhudumie   ambayo itazunguka katika mikoa yote 31. Baada ya Kigoma mnada utahamia Mtwara Desemba 14, 2018
Katika Mnada huo wananchi wa Kigoma wamejitokeza kwa wingi katika kuweza kuhudumiwa wadau mbalimbali wa mawasiliano.

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro

Imebainika kuwa tafiti na machapisho mengi yanayofanywa na wanataaluma na wanafunzi katika Vyuo mbalimbali si tu zinasaidia kujenga taswira za vyuo bali zinapaswa kuwa sehemu ya kufanya elimu iwe nzuri na bora zaidi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 6 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Mhe Hasunga amewaagiza watendaji wa Chuo hicho sambamba na vyuo vingine nchini kufanya tafiti za kutosha katika tasnia ya ushirika na kuhakikisha kuwa Matokeo ya tafiti hizo yanawafikia walengwa. "Serikali nayo kwa upande wake imeweka na itaendelea kuweka mazingira rafiki zaidi yatakayosaidia kuimarisha dhana ya ushirika miongoni mwa jamii ya watanzania" Alisema

Alisisitiza kuwa moja ya kadhia inayovikumba vyuo mbalimbali nchini ni kutowekwa wazi kwa haraka machapisho na Tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza ili zijulikane katika sehemu mbalimbali Duniani.

"Ndugu zangu hakuna nchi inaweza kuendelea bila kuwekeza kwenye utafiti hivyo ni lazima kuongeza jitihada na juhudi katika utafiti" Alisisitiza.Alisema kuwa Vyuo vikuu vinatambuliwa kama taasisi zilizobobea katika kufundisha, kujifunzia, kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri hivyo vinapaswa kutangaza matokeo ya Tafiti wanazozifanya.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Stashahada ya Uhasibu na Uongozi Ndg Methusela Piniel kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi bora kitaaluma ngazi ya Shahada ya Biashara na Uchumi Bi Diana Kibodya kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Prof Faustine K. Bee akitoa taarifa ya chuo hicho kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tarehe 6 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi sambamba na baadhi ya wahitimu kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma chuoni hapo tarehe 6 Disemba 2018.

TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU

$
0
0
Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya amekiri shirikisho hilo kuwa na majadiliano mbalimbali katika ngazi ya Utatu na Upili yaani Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kuhusu hoja ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi za jamii nchini. 

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro leo sanjari na vikao vyao vya kikatiba takribani kwa siku mbili, Nyamhokya amesema wajumbe wamekuwa na fursa ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ustawi wa Wafanyakazi nchini pamoja na kutoa tamko baada ya kuhudhuria kikao hicho rasmi cha utendaji wa maswala yanayotakiwa kufanyiwa utekelezaji.

Moja ya agenda zilizojadiliwa kwa undani ni swala la uunganiswaji wa wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mkanganyiko uliojitokeza baada ya serikali kutangaza kuanza kutumika kwa vikokotoo vya mafao ya pensheni kwa wastaafu wa mifuko ya PSSSF na NSSF kuanzia Agosti 8 2018.
Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya akizungumza na wanahabari mjini Morogoro leo, wakati wa kutoa tamko la Kamati ya TUCTA Taifa kuhusu mkanganyiko wa kikotoo cha mafao ya pensheni yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tannzania. Kushoto ni Makamu Rais wa TUCTA, Qambos Sulle, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Dk Yahya Msigwa (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Jones Majura. 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakimsikiliza Rais wa shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alipozungumza na wanahabari mjini Morogoro leo, wakati wa kutoa tamko la Kamati ya TUCTA Taifa kuhusu mkanganyiko wa kikotoo cha mafao ya pensheni yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania. 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakiimba wimbo wa 'Solidarity Forever' wakati wa mkutano huo. 

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini. Amewaagiza viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 6, 2018) alipofungua kiwanja cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam. Amesema iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika michezo UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza nchini.

Waziri Mkuu amesema thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani 80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.Amesema anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya 161.

Waziri Mkuu amesema ilani inaielekeza Serikali kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuifanya sekta ya michezo kutoa ajira hususan kwa vijana.“Pia naishukuru Osaka Rotary Club ya nchini Japan kwa msaada wao wa dola za Kimarekani 12,856 kwa kufadhili mashindano hayo ya sita ya mchezo wa Baseball.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball  kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto kwake ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto.  Kushoto ni Mkwe wa Jackie Robinson ambaye ni Muasisi wa mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson na wapili kushoto ni Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro Robinson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira huku Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto  (kushoto) akijiandaa kuuzuia wakati Waziri Mkuu alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmoja wa wadhamini wa Ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball, Dkt. Kazusue Konoike wakati alipofungua kiwanja hicho na  Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es slaam, Desemba 6, 2018. Katikati ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN, AZUNGUMZA NA BALOZI WA KOREA NCHINI TANZANIA IKULU LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana  na Mwakilishi wa Kampuni ya KOLON Nchini Tanzania Ndg.Teger  Lee, kushoto kwa Rais Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Korea Balozi Song Geum –young, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo,6-12-2018. (Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Korea, Balozi Song. Geum-young, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha  kwa Rais wa Zanzibar leo 6-12-2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Korea Nchini Tanzania Balozi Song Geum-young, alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar,leo 6-12-2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Korea Nchini Tanzania,Balozi Song Geum-young, baada ya mazungumzo yao yaliofanyika leo Ikulu Zanzibar,6-12-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akibadilishana mawazo na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Korea Nchini Tanzania.Balozi Song.Geum –young, wakati wakiagana baada ya kumaliza mazungumzo yao leo Ikulu Zanzibar.6-12-2018.(Picha na Ikulu)

Filamu ya Uwoya, Red Light kuonyeshwa kesho Ijumaa

$
0
0

Baada ya uzinduzi wa Msimu wa Siku kuu na promosheni kutoka kwa Kampuni ya Star Media (T) Ltd, ambapo walitangaza rasmi nia yao ya kuisadia Bongo Movie kwa kununua filamu kadhaa na kuzionyesha kupitia chaneli yao ya Kiswahili, sasa filamu hizo zinaanza kuruka katika chaneli hiyo ya Kiswahili.
Ili kurejesha ladha ya filamu za nyumbani maarufu kama Bongo Movie, ambayo kwa muda mrefu watazamaji wameikosa. Msimu huu wa Siku kuu StarTimes wataonyesha jumla ya filamu 25 katika kipindi cha mwezi mzima wa Disemba.
Kwa wiki hii ya kwanza ya mwezi Disemba miongoni mwa filamu zitakazoonekana kupitia chaneli ya StarTimes Swahili ni Red light ambayo imemshirikisha mlimbwende Irene Uwoya ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini. 
Filamu hiyo inamuelezea kijana wa miaka 27 ambaye baba yake aliuwawa na rafiki yake huku mkewe akipona, kisa kikiwa ni pete ya utajiri. Mama na kijana wake wanaamua kuhama mji na kwenda kuishi sehemu nyingine ambako wanakutana na kijana anayewapatia habari kuhusu muuaji wa baba wa familia yao. Hivyo wanasafiri kumtafuta muuaji huyo na mwishoni wanakuta akiwa amefariki hivyo wanaichukua pete ya utajiri ambayo ilichukuliwa baada ya mauaji ya baba yao, na kuwa matajiri tena.
Filamu nyingine zitakazoonekana wikendi hii ni Agent Bavo na Akili Kichwania ambayo imemshirikisha mshekeshaji Haji Salum maarufu kama Mboto. Hii ni katika kuongeza chachu kwa wadau wengine kujitokeza na kusaidia ukuaji wa soko la filamu ndani ya nchi.
Wateja wa StarTimes wataweza kutizama filamu hiyo kwa kulipia kifurushi cha mwezi mzima cha Nyota kwa TSH 8000 tu upande wa Antenna na Tsh 11000 kwa upande wa Dish. Katika msimu huu wa Siku kuu kila watakapolipia kifurushi cha NYOTA watabustiwa hadi kifurushi cha MAMBO upande wa Antenna na SMART upande wa Dish.

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA STULI NA MEZA ZA MAABARA SHULE YA SEKONDARI MWANTINI

$
0
0
Benki ya NMB imetoa msaada wa Stuli 32 na meza 8 za maabara zenye thamani ya Shilingi milioni tano ili kusaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi katika shule ya Sekondari Mwantini iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 

Msaada huo umekabidhiwa leo Ijumaa Desemba 6,2018 na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko. 

Katamba alisema msaada huo wa stuli na meza ni sehemu ya ushiriki wa benki hiyo katika maendeleo ya jamii akibainisha kuwa changamoto za sekta ya elimu nchini kwa NMB ni jambo la kipaumbele kutokana na kwamba elimu ni uti wa mgongo wa taifa lolote duniani. “NMB tulipokea maombi kuwa mnahitaji stuli na meza za maabara,tulifarijika na kuamua kuja mara moja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya elimu kwa watoto wetu katika shule hii”,alieleza. 

“Tunatambua kuwa kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka,kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni,tutaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wetu kuhakikisha changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi”,aliongeza Katamba. Hata hivyo alisema kwa mwaka 2018,NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu hivyo kuifanya benki ya NMB kuwa benki ya kwanza kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote nchini. 
Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko wakati wa zoezi la kukabidhi stuli 32 na meza 8 za maabara kwa ajili ya shule ya sekondari Mwantini.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa ALAT taifa,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam ambaye pia ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje wakipokea moja kati ya stuli 32 kutoka benki ya NMB. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Manonga,Baraka Ladislaus na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwantini.
Picha ya pamoja wakati wa makabidhiano ya stuli na meza za maabara katika shule ya sekondari Mwantini. 

BENKI YA UBA YABORESHA HUDUMA ZA KIMTANDAO KWA KUZINDUA MAGIC BANKING

$
0
0
Ikiwa ni jitahada za kuendelea kuwa benki bora Barani Afrika kwa huduma za simu za mkononi na kuendelea kuendana na jinsi mtandao unapokuwa haraka na kuwa na bidhaa na huduma zilizo bora kabisa, benki ya UBA Tanzania leo imetangaza kuzindua huduma nyingine bora ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70# kwa hapa Tanzania.

Huduma hii ya Magic Banking itamfanya mteja kwa kutumia simu yake ya mkononi kuweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hii ya Magic Banking, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Huduma za Kimtandao UBA Bank Tanzania Asupya Nalingigwa alisema kuwa mbali na huduma ya Magic Banking kufanya kazi kwenye simu aina yeyote ile lakini huduma hii ni salama, ya haraka na nafuu na mteja haitaji kuwa na salio ili kufanya miamala. ‘Huduma ya Magic Banking inamfanya mteja kuweza kufanya miamala ya hadi TZS 1 milioni kwa siku kwa kutumia UBA Secure Pass ambayo inaongeza usalama kwa mtumiaji,’ alisema Nalingigwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji UBA Tanzania Usman Isiaka alisema kuwa huduma ya Magic Banking itamfanya kila Mtanzania mwenye simu iliyosajiliwa kufungua akaunti papo hapo. ‘Mteja anayetumia simu ya mkononi bila kujali anatumia mtandao ngani wa simu anaweza kufungua akaunti na sisi kwa kupiga *150*70# bila gharama yeyote.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akizungumza waandishi wa habari, Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya benki huduma ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70#. Kushoto ni Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akimuelekeza Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella jinsi ya kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa kuzindua huduma ya UBA Magic Banking ambayo mteja anaweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.


HARMONIZE ATOA PARANAWE YA KUFUNGIA MWAKA WA 2018

$
0
0
Na Baba Faisal

MWENAMUZIKI maarufu kwenye muziki wa kizazi kipya ambaye anafanya kazi zake chini ya Lebo ya WCB Rajab Abdul Kahali a.k.a

Harmonize ameamua kuachia wimbo wake mpya wa Paranawe ambao tayari umeanza kuwa gumzo kwenye vituo mbalimbali vya redio pamoja na mitandao ya kijamii.

Unajua kwanini wimbo huo umeanza kuwa gumzo ?Ukweli ni kwamba licha ya wimbo huo kuwa una siku mbili tangu kuachiwa rasmi na msanii huyo umekuwa gumzo kwasababu Harmonize kupitia wimbo huo amethibitisha yeye ni moja kati ya wasanii bora kutokana na aina ya staili yake anayotumia katika kuimba na nyimbo zake.

Kikubwa ambacho kimeongeza ladha ya wimbo wa Paranawe ni pale ambapo ameamua kumshirikisha Rayvany ambaye kwa hakika sauti yake imefanikiwa kupenya kwenye masikio ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.Hivyo Harmonize a.k.a Konde Boy ameamua kumpa nafasi Rayvany katika wimbo huo.

Ni jana tu ndio Harmonize ameachia wimbo huo ambao tayari umeshika kasi mtaani.Kama unavyojua tena kwenye bodaboda huko mtaani tayari wameshaweka kwenye flash zao na kilichobaki wanasikiliza mdundo huo wa Paranawe kama sehemu ya kuwa na watu wa kwanza kuusikiliza.

HALMASHAURI WILAYA YA KALIUA, WADAU WA MAENDELEO WAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI

$
0
0
Na Editha Shija, Tabora

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wilayani humo wamejipanga kumaliza kero ya maji kwa wananchi ambayo imekuwa ya muda mrefu katika maeneo karibu yote wilayani humo.

Akizungumza na Michuzi Blog ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Dk.John Pima alibainisha kuwa ushirikiano mzuri wa watendaji na wataalamu wa halmashauri umechochea kasi nzuri ya ukusanyaji mapato, hivyo kumewezesha miradi mingi ya maji kutekelezwa kwa asilimia 100.

Amesema kuwa mfuko wa programu ya maji umekuwa chachu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo na wana uhakika katika kipindi kifupi kijacho tatizo la maji litapungua kwa kiasi kikubwa kama si kumalizka kabisa.Pima ameongeza kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya upatikanaji maji , ametaja miradi ya maji iliyotekelezwa kwa asilimia zote ni ujenzi wa mantenki mawili ya kuvunia maji mvua yenye ujazo wa lita 50,000 yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Uyowa na Mkindo na ujenzi wa tenki La chini ya ardhi lenye ujazo wa Lita 10,0000 lililojengwa katika Shule ya Sekondari ya Kaliua.

Miradi mingine iliyokamilishwa ni ukarabati wa visima virefu 4 katika vijiji vya uhindi viwili Songambele(1) Mwendakulima (1) pamoja na tenki moja la kuvunia maji ya mvua lenye ujazo wa Lita 50,000 katika zahanati ya kangemeAliongezea kwa kusema kuwa mradi mingine ni wa tenki la chini lenye ujazo wa Lita 10,0000 uliojengwa na kampuni ya FUM katika zahanati ya Nyasa huku kampuni ya wachina ya CHICCO iliyokuwa ikitengeneza barabara ya kaliuwa -Kazilambwa ikiwajengea miradi mitano ya maji.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amewataka wananchi watunze miradi hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kuwaondolea kero ya maji ya muda iliyokuwa inawakabiri.
 

KIKAO KAZI CHA KUPITIA RASIMU YA TAARIFA YA NCHI CHINI YA MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU CHAFANA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon Mpanju (aliyesimama) akifungua kikao kazi cha kupitia rasimu ya taarifa ya nchi chini ya mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za watu wenye ulemavu, kulia kwake ni Kaimu Kamishna Idara ya walemavu ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Josephine Lyenga. Wengine ni Afisa Mipango Mwandamizi Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Walemavu Bw. Abushir Said Khatib (kushoto) Mwingine ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Haki za Binadamu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya. Kikao hicho cha siku mbili kimeanza leo (6/12/2018) kinafanyika Morena Hotel Mkoani Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kazi cha kupitia rasimu ya taarifa ya nchi chini ya mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za watu wenye ulemavu wakimsilikiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon Mpanju alipokuwa anafungua kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Amon Mpanju akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha kupitia rasimu ya taarifa ya nchi chini ya mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za watu wenye ulemavu.

0468

JESHI LA MAGEREZA LAFANYA MAADALIZI YA UZINDUZI WA DAWATI LA JINSIA LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa hotuba  katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini leo Desemba 06, 2018  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika  Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Tike Mwambipile akichangia mada katika mafunzo  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo wa Magereza yote nchini  yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Bwalo Kuu la Magereza ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia  mafunzo  kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati hilo kutoka  Magereza yote nchini yanayofanyika katika Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam  ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi hilo. Uzinduzi huo utafanyika Desemba  07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es salaam.
 Mtoa Mada kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mapunda  John ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya jinsia kwa Waratibu na Watendaji  wa Dawati la Jinsia kutoka  Magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, amesema CCM imendelea kusimamia kwa ufanisi sera za maendeleo kwa jamii bila kujali itikadi za kisiasa. Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Watendaji wa Baraza la Manispaa Mjini, huko Sebleni katika mwendelezo wa ziara yakeb ya kukagua miradi mbali mbali iliyotekelezwa na manispaa chini ya mfumo wa Ugatuzi.

Dk.Mabodi ameeleza kwamba mipango endelevu inayotekezwa na Serikali za mitaa kwa lengo la kuimarisha huduma muhimu za kijamii katika nyanja za afya,elimu,uvuvi,ufugaji,kilimo na ujasiriamali ni kwa ajili ya wananchi wa rika zote bila ya kubaguliwa. Ameeleza kuwa Serikali Kuu imeamua kupeleka madaraka katika Serikali za Mitaa kwa lengo kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi.

Ameeleza kwamba utekelezaji mzuri wa mipango iliyomo katika ugatuzi ndio litakuwa ni chimbuko la utengenezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025, iliyokuwa bora na inayoendana mahitaji halisi ya wananchi. Pamoja na hayo amewasihi Watendaji wote waliotolewa Serikali Kuu na kupelekwa Serikali za mitaa kuendelea kuwa wazalendo wenye kujituma kwa moyo mmoja katika kuhudumia jamii.

Kupitia ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo, aliitaka Manispaa hiyo kuhakikisha miradi mbali mbali inayotelezwa inakuwa ndio vipaumbele halisi vya wananchi husika katika maeneo yao na inakuwa na viwango vinavyokubalika kisheria.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi  akielekea  katika ukaguzi wa ujenzi wa jengo la kisasa la machinjio ya kuku katika Soko la Darajani.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akipokea maelezo juu ya maendeo yaliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la soko la kuku darajani.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akikagua shamba la mboga mboga la kikundi cha shehia ya Nyerere iliyopo katika Wadi ya Amani ambao wanajishughulisha na kilimo na wanasaidiwa na Manispaa ya Majini katika kazi zao.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Afisa  Muunguzi  Ashura Amour Mwinyi (kulia)  wa Kituo cha Mamama  Wajawazito na Watoto cha Sebleni akielezea huduma za Afya zinazotolewa bure katika kituo hicho zikiwemo za kipimo cha Ultra Sound.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akipewa maelezo ya mashine maalum ya kusaga taka taka za kutengenezea mbolea ya mimea huko katika kikundi cha ujasiriamali kilichopo Shauri Moyo Zanzibar , katika ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na Manispaa ya Mjini chini ya ugatuzi.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110149 articles
Browse latest View live




Latest Images