Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

UONGOZI WA JESHI LA MAGEREZA WAKUTANA NA BALOZI MSTAAFU LT. GEN.MSTAAFU MAKAKALA LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akimkaribisha  aliyekuwa Balozi Tanzania nchini Zimbabwe Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala mara alipowasili  Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Dar es Salaam leo Desemba 05, 2018 kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa Jeshi hilo  na kufanya mazungumzo na uongozi wa Jeshi la Magereza.
 Aliyekuwa Balozi Tanzania nchini Zimbabwe Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala (wa pili kulia) akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo  na baadhi ya viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza leo  Desemba 05, 2018 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dar es Salaam.
 Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Zimbabwe Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala akisalimiana na Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Nicas Banzi (2002-2007) walipokutana Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dar es salaam leo Desemba 05, 2018.
 Lt. Gen.Mstaafu Charles Makakala aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza leo Makao Makuu ya Jeshi hilo. Watatu kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza  Phaustine Kasike. Kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama na  Kamishna  wa Miundombinu ya Magereza na Uzalishaji, Tusekile Mwaisabila. Kushoto ni Kamishna wa Fedha na Mipango, Gedion Nkana na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Augustino Mboje. (Picha zote na Jeshi la Magereza).


Tanzania Kinara wa Kuvutia Wawekezaji Afrika Mashariki

$
0
0
Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Tanzania imeendela kuweka rekodi ya kuvutia wawekezaji kwa nchi zilizopo ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na mtaji wa uwekezaji wa Dola Bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda wenye uwekezaji wa dola za kimarekani 700

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Godffrey Mwambe amesema nchi ya Kenya inashika nafasi ya Tatu wakiwa na uwekezaji wa dola za kimarekani 670 na hivyo kuiweka Tanzania kuwa juu ya nchini zingine Afrika Mashariki.

Mwambe amesema kuwa Tanzania inaongoza kuvutia wawekezaji kutokana na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo hadi sasa imewekeza jumla ya miradi mipya 905 katika sekta mbalimbali nchini miradi ambayo itatengeneza ajira 115,055 kwa watanzania na kuleta tija na manufaa kwa taifa

Alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu TIC imeweza kuvutia wawekezaji na kuweza kuandikisha, mfano kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali ambavyo vimeweza kuongeza pato la Taifa.

Akifafanua zaidi anasema kuwa baadhi ya miradi mikubwa zaidi iliyowekezwa nchini ni pamoja na ikiwemo kiwanda cha Goodwill Ceremics Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kinachojihusisha na utegenezaji vigae na kimewekeza jumla ya dola za kimarekani milioni 53, huku kikitoa ajira za moja kwa moja 1500 kwa watanzania na ajira zisizo za moja kwa moja 3,000. 
 Mkurugenzi  Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Godffrey Mwambe akisisitiza  jambo kwa Waandishi wa Habari  (Hawapo  pichani), wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari  kueleza mafanikio ya TIC ndani ya Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano ulifanyika leo Disemba 5, 2018 katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO  Jijini Dar es Salaam. 
: Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TIC,Godffrey Mwambe (Kushoto) wakati wa Mkutano wake kueleza mafanikio ya TIC ndani miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.

EACH ONE TEACH ONE INITIATIVE 23RD NOVEMBER 2018

$
0
0
Each One Teach One is an initiative started by the UBA Foundation with the purpose of All UBA staff to get an opportunity to give back to the community in their own way. The initiative aims at helping under the privileged and young children, get vocational skills that may result in them making money.

UBA Tanzania through the UBA Foundation participated for the Each One, Teach One Initiative for youths in Africa. Through Each One Teach One initiative UBA staff voluntarily commit their time to their communities, teaching youth’s various activities such as foreign languages, photography, fashion design, martial arts, music and much more.
UBA Tanzania staff showing members of Mshikamano group from Yombo Vituka in Dar es salaam how to make buns (maandazi in Swahili, common bites used for breakfast and dinner) but these ones were with different taste with eggs, milk and a little flavour of vanilla essence teaching skills that may give them a head start in life.
The UBA Foundation is an arm of the bank which carries out some of the institution’s Corporate Social Responsibility. It was formed in 2011 and had given back to society part of its profits by way of helping the less privileged and vulnerable.

The campaign of the foundation is ‘each one, teach one’ geared towards promoting human capacity development and effectively giving back to society. Being in the country for over 9 years now and desirous of doing more they decided to go a step further, thereby introducing the new campaign, which involves giving skills training to young people with the aim of making them self-reliant.
These skills have the potential of turning the participant into entrepreneur, especially as there is widespread demand for make-up skills, entrepreneurship, cooking skills in the society and photography. They could use the training to later open businesses on their own, eventually empowering them economically.

This intellectual capacity building cannot be financially quantified, when one considers the result of this capacity building on the individual. It is a contribution to humanity. UBA is not only focused in Dar es salaam and Dodoma, but has plans to extend similar programs to other parts of the country. UBA has been in the country for 9 years now and has been responding positively in its Corporate Social Responsibility.

maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda vya Tanzania kufunguliwa kesho jijini Dar

$
0
0
Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji,Joseph Kakunda (watatu kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara,Novatus Rutageruka (katikati)Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO nchini, Bw.Stephen Bainous Kargbo akitembelea maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda vya hapa nchini, maonesho hayo yatafunguliwa rasmi Desemba 6 kwaka huu.
Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji Joseph Kakunda akiangalia bizaa zinazotengenezwa na kiwanda cha Darsh,(katika) Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO nchini, Bw.Stephen Bainous Kargbo(kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo Biashara,Edwin Rutageruka.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mh Joseph Kakunda aliyeambatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara,Edwin Rutageruka akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino – NIDA Bi. Rose Joseph, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndani ya maonyesho Tatu ya Bidhaa za Viwanda.
Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye banda la NIDA ndani ya maonyesho ya Tatu ya Bidhaa za viwanda wakipatiwa elimu juu ya zoezi la usajili, umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa na taratibu za kufuata ili kukamilisha hatua za awali za usajili. (Picha na Emmanuel Massaka, MMG)
Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji, Joseph Kakunda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya maonesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yanayo funguliwa Desemba 6 kwaka huu ambapo kaulimbiu ya mwakaa huu Tanzania sasa tunajenga viwanda.

UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO

$
0
0


Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii


UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu kwa jina la ‘Mpemba wa Magufuli', 

umetakiwa Desemba 18 mwaka huu kutoa majibu ya kueleweka kuhusu upelelezi dhidi ya kesi hiyo umefikia wapi.Katika kesi hiyo, Yusuph na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh.milioni 785.6 milioni. Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu 

Mkazi Kisutu amesema hayo leo Desemba 5, 2018 baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika."Nawapa nafasi ya mwisho upande wa mashtaka hadi Desemba 18. Nataka mje na majibu upelelezi wa kesi hii umefikia kwenye hatua gani? Haiwezekani ichukue muda mrefu kukamilika upelelezi,” amesema Hakimu Simba. 

Mapema, Wakili wa Serikali Elia Athanas alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikwenda kwa ajili ya kutajwa na kwamba uandaaji wa nyaraka zote ambazo ni uendeshaji wa shauri pamoja na uchujaji wa washtakiwa upo katika hatua nzuri.

Kutokana na maelezo hayo Wakili wa utetezi Aloyce Komba alihoji ni nyaraka gani hizo na zimefikia hatua gani. Akijibu, Athanas amesema ni nyaraka za uendeshaji na usikilizaji wa shauri hilo pamoja na uchujaji wa washtakiwa kabla ya kuwasomwa maelezo ya mashahidi na vielelezo.

Kesi hiyo imeahirishwakesi hadi Desemba 18 mwaka huu itakapotajwa tena. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, katika tarehe tofauti kati ya Januari 2014 na Oktoba, 2016 wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, washtakiwa wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh.milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.

Katika shtaka la pili inadaiwa kuwa Oktoba 26, 2016 wakiwa Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam walikutwa na vipande 10 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 13.85 vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 30,000 (Sh 65.4 milioni ). Oktoba 27, 2016 wakiwa Tabata Kisukuru washtakiwa hao wanadaiwa walikutwa na vipande vinne meno ya tembo vyenye uzito wa 

kilo 11.1 vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 15,000 (Sh 32.7 milioni).
Pia inadaiwa Oktoba 29, 2016 walikutwa na vipande 36 vyenye thamani ya Sh294.6 milioni bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa Wanyamapori.

DC WILAYANI NZEGA AWAAGIZA MAOFISA KILIMO KWENDA VIJIJINI KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA

$
0
0
Na Editha Shija -Tabora

MKUU wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora Godfrey Ngupula amewaagiza wataalamu wa kilimo wote waliopo katika wilaya hiyo kwenda vijijini kwa ajili ya kuwapa wakulima elimu ya kilimo bora na mbegu imara zinazofaa katika kipindi hiki cha kilimo.

Akizungumza na Michuzi Blog ofisini kwake jana Ngupula amesema mtaalamu atakayekutwa ofisini atakiona cha moto kwani huu wakati si wa kumuuacha mkulima aendelee kufanya kilimo cha mazoea na kisichokuwa na tija bali kimnufaishe mkulima na maisha yake.

Amesema kuwa kipindi hiki cha mvua ambapo maandalizi ya kilimo ndio yanaanza wataalamu wa kilimo hawapaswi kukaa maofisini kwani ni wakati wa kuhamishia ofisi zao mashambani na siyo mjini huku akiwataka maofisa tarafa na watendaji wote na vijiji na kata kushirikiana kwa karibu zaidi na wataalamu wa kilimo ili kuhakikisha wakulima wanapata elimu 
itakayowasaidia kuongeza uzalishaji mkubwa wa mazao.

Sambamba na hayo mkuu huyo amemalizia kwa kufafanua kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa na kwamba kitasimamiwa vizuri na wakulima wakaelimishwa ipasavyo na kuachana na kilimo kisichokuwa bora,kwani maisha yao yatabadilika na Mapato ya halmashauri yataongezeka.

WANATAALUMA YA UNUNUZI NA UGAVI WAPEWA SOMO

MWENYEKITI WA HALMASHAURI WILAYA YA NZEGA ATOA ONYO KWA WATENDAJI WANAOTAFUNA FEDHA ZA MAPATO

$
0
0
Na Editha Shija, Tabora

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora Kiwele Michael Bundala ametoa onyoa kali kwa watendaji wa Vijiji na Kata watakaobainika kutafuna fedha za mapato wanayokusanya kutoka katika vyanzo mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Ametoa onyo hilo jana wilayani hapa baada ya kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo kutowasilisha fedha za mapato kwa wakati ambapo amesema halmashauri inakusanya fedha nyingi kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali lakini nyingi zinaingia mifukoni mwa baadhi ya watu.

Pia amesisitiza kuwa watendaji wote wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinakusanywa katika maeneo yao na kuletwa kama zilivyo na kwamba kuanzia sasa Mtendaji yeyote atakayebainika kutafuna fedha za mapato au kujihusisha na vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kutimuliwa mara moja.

Amewasisitiza 'kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata kanuni,taratibu,na sheria huku akionya kuwa Serikali haina fedha za kuhamisha mtumishi mzembe anayeshindwa kutekeleza majukumu yake. Hata hivyo Mwenyekiti huyo amewataka madiwani wa kata zote kufuatilia kwa ukaribu watendaji wao na kuhakilisha fedha zote zinazokusanywa na kuwasilishwa ipasavyo.

 

MICHUZI TV: WAZIRI MKUU ATOA TUZO KWA WANAFUNZI WALIOSHIRIKI SHINDANO LA HUAWEI

MICHUZI TV: SSRA YAMJIBU MBUNGE ESTER BULAYA

MICHUZI TV :KIWANJA KINACHODAIWA CHA DAUD BALALI CHAZUA UTATA, MBWENI

AWESO ATUMBUA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji ameendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani
Lindi kwa kutembelea miradi ya maji ya Likwaya, Rutamba na Namangale
iliopo Halmashauri ya Lindi vijijini.

Pia aliongea na wananchi na kuwasikiliza kero zao zinazohusu sekta ya maji.
Aidha, Mheshimiwa Aweso alitembelea miradi ya Nangumbu na Michenga
iliopo Wilayani Ruangwa na kutoa maagizo.

Katika ziara hizo Naibu Waziri alionesha kutoridhishwa na mwenendo wa
jumuiya zinazosimamia miradi ya maji na kulazimika kuivunja jumuiya ya
watumia maji ya Rutamba baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wao.
 Mheshimiwa Aweso Naibu Waziri wa Maji akisalimiana na wakazi wa
Likwaya Lindi Vijijini.
BC207579-A0D8-471A-877B-DE869128926C-min
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua ujenzi wa kilua cha
kuchotea maji Nangumbu Ruangwa
A1F6C4C2-1510-4288-AF36-D1F2C832CE03-min
Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso akiongea na wananchi wa
Rutamba Lindi Vijijini.
64ED4CD2-83B6-4BB0-82A6-8A9782517536-min
Naibu Waziri wa Maji akifungua koki ya maji kujiridhisha kama mradi
unafanya kazi Rutamba.

Kamishna wa Maadili Jaji Nsekela Atembelea Klabu za Maadili Shule za Sekondari Dodoma

WADAU WATAKIWA KUTEKELEZA KANUNI MPYA ZA NGOs KUDUMISHA MISINGI YA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

$
0
0


Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Kiserikali (NGOs) wametakiwa kutekeleza Kanuni Mpya za Sheria namba 24 ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2002 ikiwa ni lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika misingi ya uwazi na uwajibikaji.

Hayo yamebainika jijini Dodoma wakati wa mahojiano kati ya waandishi wa habari na Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Baraka Leornard wakati wa kikao baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini wanaotekeleza Sera zinazosimamiwa na Wizara.

Bw. Baraka ameongeza wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wamepitishwa katika Kanuni mpya ili kuwa na uwelewa wa kutosha katika utekelezaji wa Kanuni za utendaji wa mashirika hayo kwa ajili ya kutambua nini kinatakiwa kufanya na nini hakitakiwi kufanyika ili kuepuka kukinzana na Sheria, Kanuni na taratibu husika.

Amesisitiza kuwa mara baada ya kikao hicho Wadau watakuwa na uelewa mkubwa wa Kanuni hizo ambao utawasaidia kuweza kutekeleza wajibu wao bila kukiuka Kanuni zozote ambazo zinaenda na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2002. 


Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Neema Mwanga (katikati) akizungumza na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa kikao baina ya Wizara na wadau hao wanaotekeleza Sera zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Baraka Leornard na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali BI. Tausi Mwilima. 
Wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao baina ya Wizara na wadau hao wanaotekeleza Sera zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW .


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


MAAFISA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUTHAMINI MIRADI INAYOFANYWA NA SERIKALINI

$
0
0

Na. Edward Kondela

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Maafisa Ununuzi na Ugavi nchini kutambua na kuthamini miradi mbalimbali inayofanywa na serikali, kwa kuthaminisha miradi hiyo na thamani halisi ya fedha inayotumika katika miradi.

Prof. Gabriel aliyasema hayo leo (05.12.2018) Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mada kuhusu uvumbuzi na ufanisi bora kwa Maafisa Ununuzi na Ugavi kutoka maeneo mbalimbali nchini, wakati wa siku ya ufunguzi wa kongamano la Tisa la mwaka la maafisa hao.

“Katika ujenzi wa miradi mikubwa tunayoishuhudia kwa sasa nchini, fedha zinatumika, lakini jinsi gani sasa vifaa vinanunuliwa, malighafi zinanunuliwa ni jambo kubwa sana, kuna haja ya wahusika katika tasnia hii wawe wabunifu kadri iwezekanavyo na wawe ni watu wa kuleta mabadiliko”. Alisema Prof. Gabriel.

Katibu mkuu huyo aliwataka maafisa hao kuwa wavumbuzi na kufanya kazi kwa ufanisi katika masuala ya ugavi na usambazaji bidhaa ili kuisaidia serikali, kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika kujenga miradi mbalimbali ili iwe na tija kwa taifa.

Aidha, Prof. Gabriel aliwataka Maafisa Ununuzi na Ugavi, kubadili mienendo yao ambayo haiwaletei tija katika ufanisi wa kazi, pamoja na kujiongezea thamani katika jamii kwa kufanya kazi kwa ufanisi ili waweze kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada kwa Maafisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani) katika kongamano la Tisa la mwaka la maafisa hao. 
Baadhi ya Maafisa Ununuzi na Ugavi wakisikiliza mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) 
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akisikiliza kwa makini michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na Maafisa Ununuzi na Ugavi (hawapo pichani), mara baada ya kuwasilisha mada kwa maafisa hao juu ya uvumbuzi na ufanisi bora katika masuala ya ugavi. 

DC MSHAMA AKABIDHI SHAMBA PORI MIKONONI MWA WANANCHI WAKATI AKISUBIRI TARATIBU NYINGINE KUCHUKULIWA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MKUU wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama amesema ataandika ombi la kufuta hati ya shamba la mmiliki Siemens, lililopo kata ya Pangani, kutokana na kuwa pori na kugeuzwa jalala la kutupwa miili ya marehemu pamoja na kutumika kwa uhalifu. 

Hatua hiyo inakwenda pamoja na kuwakabidhi wananchi kulitumia kwa masharti ya kulima mazao ya muda mfupi wakati serikali ikiendelea na taratibu za kupima viwanja na kuuza kwa gharama nafuu. 

Akitoa maamuzi hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Assumpter alisema ifikie mwisho kujaza viwanja na mashamba pori wilayani hapo. Assumpter alitoa rai kwa wamiliki wenye mashamba na viwanja pori kuanza kuyaendeleza na kama watakaidi wananchi wakiyavamia ataruhusu wagawiane maeneo. 

"Hii ni salamu tuu, mwenzio akinyolewa wewe anza kutia maji, wananchi wamechoshwa kulinda maeneo ya watu, kama mmeyashindwa yaacheni"alifafanua Assumpter. Awali diwani wa kata ya Pangani, Agustino Mdachi aliomba serikali ,kuangalia namna ya kufuta umiliki wa mashamba ambayo hayaendelezwi na kusababisha kutumika vificho vya wahalifu .

Alisema, kwa kipindi cha miezi sita miili zaidi ya kumi zimeokotwa kwenye mtaa huo ambapo kati yao wengine walinusurika kifo na kuokolewa na wengine wakiwa wamefariki dunia. Nae mwenyekiti wa mtaa wa Pangani Jitihada Ndiali alisema maeneo hayo yamegeuzwa dampo au sehemu ya kutupia maiti pia madereva bodaboda kuporwa pikipiki zao kisha kutupwa .

Kwa upande wa wananchi akiwemo Lillian Godfrey alimpongeza mkuu wa wilaya kwa maamuzi yake. Alisema, wamekubali kulima mazao ya muda kama mihogo, mbaazi, maharage na mbogamboga hadi hapo serikali itakapofanya maamuzi ya moja kwa moja.

MAHAKAMA YAANZA KUSIKILIZA KESI KWA MTANDAO

$
0
0

Na Magreth Kinabo-Mahakama ya Tanzania

Mahakama ya Tanzania kwa mara ya kwanza imeanza kuendesha kesi kwa kutumia mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya picha za video yaani ‘Video Conferencing’ kwa kutumia vitendea kazi vyake yenyewe kwa kumsikiliza shahidi akiwa nchini Ufaransa.

Kesi hiyo imesikilizwa leo katika kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania kilichopo Kisutu jijini Dar es Salam na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara Mhe. Lugano Mwandambo. Hatua ya kuanza kusikilizwa kwa kesi kupitia mfumo huu ni hatua ya mafanikio katika Maboresho ya Utoaji wa Huduma za Mahakama kwa wakati na kwa viwango kumfikia mteja.

Kesi hiyo ya madai namba 6 ya mwaka 2017 iliyosikilizwa kwa njia picha za video inayohusu mdai ambaye ni kampuni ya Sogea Saton anayeidai zaidi ya shilingi bilioni 3.8 Bank of Africa. Aidha kupitia mfumo huo wa Video Conferencing, shahidi huyo aliweza kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji na Mawakili wa upande wa mdai ambao walikuwa ni Dilip Kesaria na Veronika Mwanajengwa, wakati mawakili wa upande wa utetezi walikuwa ni Peter Swai na Rosan Mwambo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 2, mwakani.

Mahakama ya Tanzania imeamua kutumia Tehama ili kurahisisha utoaji wa haki kwa wakati na pia kuokoa muda na kupunguza gharama kwa wananchi wanaofika Mahakamani kutafuta haki zao. Aidha, mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya picha za video (Video Conferencing) ulioanza kutumiwa na Mahakama ya Tanzania katika kusikiliza mashauri Mahakamani tayari umefungwa katika Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam na Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya.

Mpango uliopo ni kufunga Mfumo huu kwenye Mahakama Kuu zote nchini pamoja na chuo cha Uongozi wa Mahakama kilichopo Lushoto mkoani Tanga.

Kesi ikiendeshwa kwa njia ya Mtandao- ‘Video Conferencing’ kwa mara ya kwanza katika kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania kilichopo Kisutu jijini Dar es salaam. Kulia pichani ni Shahidi namba tatu , Stela Janot akitoa ushahidi wake akiwa nchini Ufaransa. 
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara Mhe.Lugano Mwandambo akiendesha kesi kwa njia ya Mtandao ‘Video Conferencing’ aliyekaa mezani (katikati amevaa tai )katika Kituo cha Mafunzo cha Kisutu. Kushoto ni Makarani wa Mahakama Martha Cosmas na Fortunata Barnabas.

NAIBU WAZIRI CONSTANTINE KANYASU AMPA MKANDARASI SIKU 30 KUKAMILISHA JENGO LA MALIASILI NA UTALII DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe .Constantine Kanyasu ametoa siku 30 kwa mkandarasi wa SUMA JKT, aliyepewa kazi ya kujenga jengo la ofisi ya wizara hiyo katika mji wa serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma, kuhakikisha jengo hilo linakamilika ndani ya siku hizo alizopewa
Amemshauri Mkandarasi huyo kufanya kazi usiku na mchana ili aweze kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ndani ya siku hizo 30. 

Ametoa rai hiyo mara baada ya kutembelea eneo hilo la ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara hiyo linalotarajiwa kugharimu shilingi bilioni moja za kitanzania katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma. 

Aidha, Mhe.Kanyasu ameitaka kandarasi ya SUMA JKT ihakikishe inajenga jengo hilo kwa umakini, umahiri na viwango vya ubora wa hali ya juu vinavyokwenda sambamba na hadhi ya Wizara yenye mchango mkubwa kwenye pato la Taifa. Pia, Mhe.Kanyasu ameielekeza SUMA JKT wakati ikiendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo iwe inatoa taarifa kila siku kwa kila hatua inayofikia katika Ujenzi wa jengo hilo kwa Uongozi wa Wizara. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo mara baada ya kutembelea eneo ambalo jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii litakapojengwa ndani ya siku 30 katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma kwa kandarasi ya SUMA JKT litakalogharimu bilioni moja.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Bw. Lusius Mwenda mara baada ya kutembelea eneo ambalo jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii litakapojengwa ndani ya siku 30 katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma kwa kandarasi ya SUMA JKT litakalogharimu bilioni moja.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akioneshwa eneo na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Bw. Lusius Mwenda mara baada ya kutembelea eneo ambalo jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii litakapojengwa ndani ya siku 30 katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma kwa kandarasi ya SUMA JKT litakalogharimu bilioni moja. (Picha zote na Lusungu Helel 

WAZIRI LUGOLA ATOA AGIZO KWA WANANCHI AMBAO HAWAJAPATA KITAMBULISHO CHA TAIFA NCHINI

$
0
0
Na Felix Mwagara, (MOHA), MARA. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nansimo, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola amesema katika Mkoa na mikoa mingineyo zoezi la kujiandikisha lilishakamilika ila wale ambao hawakuandikishwa kipindi kile ambacho Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanaandikisha wananchi mitaani, wanapaswa kwenda katika ofisi Wilaya za Mamlaka hiyo ili waweze kujiandikisha. 

“Wapo ambao kipindi kile NIDA wanaandikisha wananchi mitaani hawakuwepo hilo nalijua, na pia kuna wale ambao kipindi kile zoezi la kuandikishwa linafanyika walikua hawajafikisha miaka 18, hao wote ambao hawajaandikishwa wanapaswa sasa kwenda kujiandikisha haraka iwezekanavyo katika ofisi za NIDA katika Wilaya zao,” alisema Lugola. 

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara aliongeza kuwa, zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye hapa nchini, ni kosa bwa kama wewe ni raia akaamua kukaidi ikiwa Rais Dk John Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote nchini. 

“Ndugu wananchi wa Mwibara na kote nchini, kupata kitambulisho ni jambo kubwa la nchi hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote na tusilichukulie kirahisirahisi tu, na ninawaambia baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali,” alisema Lugola.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (aliyemshika mtoto), akitoka mkutanoni baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimpongeza mwanachama mpya wa CCM, Andrea Mutesigwa (kulia) ambaye amerudisha kadi ya Chadema katika Mkutano wa Wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Katika mkutano wake na wananchi hao, Lugola aliwataka Watanzania ambao hawajajiandikisha waende kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa. 



Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images