Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: WAZIRI MKUU AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA MIKOA NA MA’RAS


MICHUZI TV: UJUMBE WA RAIS MAGUFULI KWA MAMLAKA YA MAPATO NCHINI

MICHUZI TV: HUU NDIO UWEKEZEJI WA CHINA NCHINI TANZANIA

WAZIRI KAKUNDA AZUNGUMZIA UWEKEZAJI WA CHINA, MKURUGENZI MTENDAJI TIC APONGEZA TAMKO LA RAIS

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema China ndio nchi pekee ambayo imeweka fedha nyingi zaidi kwa ajili ya uwekezaji ambapo fedha waliyoweka kwenye kuwekeza ni Dola za Marekani bilioni 5.8 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh.trilioni 12 huku akisisitiza umuhimu wa kujengwa kwa viwanda nchini ambako kutsaidia kuzalisha bidhaa nyingi ambazo zitauzwa nje ya nchi yetu.

Kakunda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati mkutano uliowakutanisha wawekezaji kutoka nchini China, maofisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta zinazojihusisha na uwekezaji nchini ambapo wametumia nafasi hiyo kujadili fursa za uwekezaji ambazo zipo nchini.

Akifafanua zaidi wakati anazungumzia ujio wa wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini kuangalia fursa za uwekezaji, amesema kuwa kwa sasa China ndio nchi ambayo imeweke fedha zake nyingi kwa ajili ya masuala ya uwekezaji ambao wamewekeza nchini.

"Nchi ya China au wawekezaji kutoka China ndio ambao wameka fedha nyingi sana katika maeneo ya uwekezaji.Wamewekeza kwenye viwanda vya aina mbalimbali, vimo viwanda vya saruji, viwanda vya kubangua kurosho na pia wapo pia kwenye uwekezaji katika eneo la ujenzi ambako nako huko wameweka fedha nyingi,"amesema Kakunda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania(TIC)Geoffrey Mwambe (kulia) akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Wang Ke wakati wa kongamano la uwekezaji ambalo limejumuisha wawekezaji wa nchi hizo mbili
 Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Uhusiano kati ya nchi zinazoendelea kutokana China Lyu Xinhua akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji kati ya wawekezaji wa China na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kushoto)akiandika kabla ya kuzungumza kwenye kongamano la uwekezaji ambalo liliwahusisha wawekezaji kutokana nchini China ambao wamefika nchini kuangalia fursa za uwekezaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi(TPSF) Godfrey Sembeye akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji baina ya wawekezaji waChina na Tanzania ambalo limefanyika leo jiiini Dar es Salaam.
 Baadhi ya  wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini wakiangalia fursa za uwekezaji wakimsikiliza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseoh Kakunda wakati wa kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania.wakimsiki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Wakuu wa Mikoa Simamieni Miradi ya Maendeleo Inayolenga Kuwapunguzia Umasikini Wananchi

CCM YATOA NENO MJADALA UNAONDELEA MTANDAONI KUHUSU DK.BASHIRU NA MEMBE

$
0
0
*Yawataka Watanzania wakiwamo wanaCCM kupuuza uzushi, uchonganishi na fitna
*Kamati Kuu kukutana Desemba 17 na 18 Dar, yazungumzia pia ushindi wa kishindo 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kuwa kimefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii  kuhusu wito ambao umetolewa na Katibu Mkuu wao Dk.Bashiru Ally kwa kada wa Chama hicho Benard Membe kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano.

Taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM Humphrey Polepole ambayo ameitoa leo Desemba 3 mwaka huu wa 2018 amesema kuwa wanatoa rai kwa rai kwa watanzania kuwa wito wa Katibu Mkuu ulikuwa ni wa kawaida wa kiongozi wa CCM kwa mwanachama wa CCM, hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea hasa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti yenye hila mbaya, wana CCM na Umma wa watanzania wanaombwa 
waupuuze.

"Chama Cha Mapinduzi kinawataka wana CCM na watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa na umoja, mshikamano na upendo zaidi katika kipindi hiki ambacho Rais Dk.John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM anandelea kutuongoza katika mageuzi makubwa ya kiuchumi na ya kimaendeleo kwa watanzania wote,"amesema Polepole kwenye taarifa hiyo.

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imeamua kutoa ufafanuzi kwa jamii ya Watanzania kuhusu hali ya ongezekeo la joto katika baadhi ya maeneo hapa nchini huku ikifafanua kwenye baadhi ya mikoa joto limefikia asilimia 34.

Taarifa ya TMA kwa vyombo vya habari ambayo imetoa leo jijini Dar es Salaam imesema kwa kawaida kipindi cha Oktoba hadi Machi kila mwaka jua la utosi linakuwa katika maeneo ya kizio cha kusini mwa dunia na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini, huwa na hali ya joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na miezi mingine. 

"Hapa nchini, vipindi vya jua la utosi vinafikia kilele kati ya mwishoni mwa Novemba na Desemba wakati jua la utosi likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena Februari wakati jua la utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa). Jua la utosi huambatana na hali ya Joto kali kwa sababu kipindi hicho ndipo uso wa dunia katika eneo tajwa huwa karibu zaidi na jua kuliko maeneo mengine. Hali hii hushuhudiwa zaidi kunapokuwepo na upungufu wa mvua ambazo zingesaidia katika kupunguza hali ya joto katika kipindi husika,"imesema taarifa hiyo ya TMA.

Imefafanua wastani wa joto kwa Novemba na Desemba ni nyuzi joto 31.5 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba. Hata hivyo, mpaka kufika mwishoni mwa Novemba 2018 joto limeshafika nyuzi joto 34. Katika baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dar es salaam, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba ambapo msimu wa mvua za Vuli unaendelea kukumbwa na mtawanyiko hafifu wa mvua hali ya fukuto inachangia katika hali ya joto japo vipimo vya nyuzi joto katika baadhi ya maeneo hayo ni vya wastani.

Imeongeza kuwa vipindi hivyo vya joto kali vinatarajiwa kupungua kadiri mtawanyiko wa mvua za vuli utakavyoimarika Desemba mwaka huu wa 2018 huku ikifafanua kuwa hata hivyo ikizingatiwa kuwa hali ya joto inatarajiwa kujirudia tena Februari 2019, wakati wa kipindi cha pili cha jua la utosi. Aidha, taarifa za mwenendo wa joto, zinaendelea kutolewa katika 

utabiri wa kila siku na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kwamba wanatoa mwito kwa wananchi kuendelea kufuatilia taarifa hizo na kuchukua hatua stahiki kila inapobidi.

KAMWELWE: SERIKALI INAMPANGO WA KUUNGANISHA TAA NA KADCO

$
0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Mhe. Isack Kamwelwe amesema Serikali ina mkakati wa kutunga sheria ya kuunganisha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)na Kampuni ya Maendeleo ya Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) ili kuunda Mamlaka ya usimamizi na uendeshaji wa Viwanja vya Ndege hapa nchini.

Waziri Kamwelwe alisema hayo alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAA katika Ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Kamwelwe alisema lengo la kuunganisha TAA na KADCO ni kuwa na Mamlaka kamili ili isimamie Viwanja vya ndege na kuhudumia ndege zote pamoja na kusimamia biashara za kimkakati kama mafuta ya Ndege na utoaji huduma katika Viwanja vya Ndege. 

Kamwelwe alisema “mafuta ya ndege hayadhibitiwi kama zinavyodhibitiwa nishati nyingine na EWURA. Kwa nini huku kwenye ndege msimamizi asiwepo? sasa ili kudhibiti hili mtakuwa mnauza mafuta ninyi na hii ni baada tu ya kuwa Mamlaka kamili,” alihoji .

Akizungumzia Jengo la III la abiria alisema kunahitajika Watumishi zaidi ya 600 hivyo lazima Serikali iangalie wanahitajika Watumishi wa aina gani ili kuijenga TAA katika sura mpya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw, Richard Mayongela alipokuwa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa LAPF Dodoma mapema leo.
 Wajumbe mbalimbali wa Baraza Kuu la Wafanyakazi walipokuwa wakifuatilia kwa umakini hoja zilizokuwa mezani  katika Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo.  

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TAA (MAB)  Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (pili kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa TAA Bw, Richard Mayongela (pili kulia) na Wajumbe mbalimbali  mara baada ya kufungua Mkutano wa 22  wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF , Dodoma mapema leo.

BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA

$
0
0




Na Said Mwishehe,Globu ya jamii



WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano chini Rais Dk.John Magufuli ikihimiza ujenzi wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati, uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi imara utakaotokana na viwanda.




Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na wahariri wa habari za uchumi na biashara kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini , Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobard Sabi amesema wanatambua Serikali imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025.


"NBC inaunga mkono dhamira hiyo kwa kuwawezesha wafanyabiashara katika sekta mbalimbali na mitaji ya kifedha. Kama mnavyofahamu kwamba NBC ni moja ya benki yenye mtaji mkubwa wa kuwawezesha wafanyabiashara wa kitanzania. Hivyo tutahakikisha tunashiriki kikamilifu katika kuwajengea uwezo wa Tanzania ili washiriki kwenye kujenga uchumi kupitia viwanda na hayo ndio moja ya malengo yetu kama benki yenye uwezo mkubwa kifedha,"amesema Sabi.




Kuhusu vipaumbele vya benki hiyo, amesema kuwa wameweka vipaumbele vitano na namna ya kufanikisha.Amesema kipaumbele chao cha kwanza ni mteja kuwa namba moja na safari ya kumuweka mtaja kuwa wa kwanza itakazia kwenye mabadiliko ya kitamaduni ya benki yao na kuelekea kwenye utoaji hasa katika maeneo ya malipo, ufunguaji na ufufuaji wa akanti, chaneli za kidigiti pamoja na ututatuzi wa malalamiko.


Pia kipaumbele namba tatu ni kuwa karibu na wateja wao kwani NBC inaamini kwamba bila ya wateja na wao hatutakuwepo. "Hivyo tutajikita katika kuhakikisha tunakuwa karibu na wateja wetu. Tutaboresha muonekano wa matawi yetu inayoendana na matakwa na mahitaji yao.




Tumeanza na tawi letu la Dodoma ambalo lina muonekano mpya na wa kisasa unaokidhi mahitaji ya wateja wetu. Tumeanza na ukarabati wa tawi letu la Dodoma kwa sasa, lakini mengine yatafuata,"amesema Sabi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akielezea mpango makakati wa miaka mitano wa benki hiyo  wenye lengo la kuboresha kwa kiwango kikubwa huduma za benki hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,  Theobald Sabi (kushoto),  akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mpango mkakati wa miaka mitano wa benki  hiyo wenye lengo la kufanya maboresho makubwa kwenye huduma zake. Kushoto kwake ni jopo zima la wakurugenzi wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,  Theobald Sabi (mbele),  akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mpango mkakati wa miaka mitano wa benki  hiyo wenye lengo la kufanya maboresho makubwa kwenye huduma zake. Walioketi ni baadhi ya wakurugenzi wa NBC.

WATANZANIA MNAOSOMA CHINA JITUMENI KWA AJILI YA MAENDEO YA TAIFA-BALOZI KAIRUKI.

$
0
0
 WATANZANIA wanaosoma nchini China wametakiwa kuwa chachu ya maendeleo, ubunifu,kujituma na kujitolea kwa manufaa ya taifa la Tanzania ikiwemo kuchangamkia fursa za maendeleo.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania nchini humo (TASAFIC) Desemba mosi mwaka huu.
Mkutano huo ulioandaliwa na Shirikisho la Watanzania wanaosoma China na Ubalozi wa Tanzania, ulilenga kuleta pamoja watanzania wanaosoma miji mbalimbali kama Dalian, Najing na Tianjing.

Alisema watanzania wanaoishi nchini humo wanapaswa kuangalia fursa za maendeleo kuwa wabunifu kujituma na kujitolea kwa manufaa ya taifa la Tanzania.“Ili Tanzania inufaike na mafanikio ya China Kiuchumi ni lazima kuwe na wataalamu wenye ujuzi na maarifa inayokwenda sambamba na teknolojia ya kisasa,”alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawakala wa elimu ya vyuo vikuu nje ya nchi, Global Education Link, Abdul Malik Mollel ameipongeza Tume ya Vyuo vikuu (TCU) kwa kuwa na utaratibu wa kuchunguza mawakala ili kudhibiti huduma hiyo.

“Tanzania tuna mawakala zaidi ya 60 , tunampa Balozi mzigo mkubwa wa kutamka leo mawakala ni matapeli…”alisema.Jumla ya wanafunzi 500 wameanza masomo katika mwaka wa masomo ya taaluma mbalimbali nje ya nchi hasa nchi za China, India, Malaysia na Ukraini chini ya wakala wa Global Education Link.Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza na wanafunzi wanaosoma china katika mkutano Mkuu wa shirikisho la jumuiya za watanzania wanosoma China ambapo aliwataka kuwa 
wabunifu,kujitolea kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji    Global Education Link,Abdulmalik Mollel akizungumza na wanafunzi wanaosoma china katika mkutano Mkuu wa shirikisho la jumuiya za watanzania wanosoma China uliofanyika katika  chuo cha  Shanyang Aerospece China
 Pichani ni Wanafunzi wakiwa katika mkutano Mkuu wa shirikisho la jumuiya za watanzania wanosoma China uliofanyika katika chuo cha Shanyang Aerospece China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Kwa  Mkurugenzi Mtendaji Global Education Link,Abdulmalik Mollel,Mkurungezi Mwenza,Zakia Nasor.

ZIARA YA MBUNGE, NEEMA YAWASHUKIA WANA KOROGWE VIJIJINI

$
0
0


MBUNGE wa Korogwe vijijini Mh. Timotheo Mnzava amewataka wananchi wa jimboni kwake kuwa na uthubutu wa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuipa nguvu serikali ili wapate kipaumbele katika kukamilisha miradi yao. 

Ameyazungumza hayo akiwa katika ziara yake ya kata 29 ndani ya jimbo hilo ambapo ilianza tarehe 1 Disemba na kutarajiwa kumalizika tarehe 15 Disemba 2018. 
Aidha kufuatia kero na changamoto za jimbo hilo kuwa nyingi, Mnzava amewaomba wananchi kuainisha vipaumbele ili kurahisha utatuzi wa kero hizo kuwa katika mtiririko unaofaa na kuepusha kugusa kila kero na hatimae kushindwa kuzimaliza kwa wakati. 
Aidha katika kata nne za Kalalani,Mashewa,Kizara na Foroforo ambazo tayari amezipitia, Mnzava ameahidi jumla ya Mifuko ya Simenti 270, ambapo katika mifuko hiyo 250 itatumika katika sekta ya afya na mifuko 20 katika sekta ya elimu pamoja na nondo 45 zitakazotumika kwenye ujenzi wa zahanati katika kata ya Foroforo. 
Aidha Mnzava amewataka wananchi kuondoa ukanda na ukabira ambao unapelekea kukwamisha shughuli za maendeleo ya korogwe vijijini na kuwaasa waishi katika misingi aliyoiachia baba wa taifa Mwalimu Nyerere juu kutanguliza utanzania na kuachanana tabia ya kubaguana kwa makabira. 
Aidha kufuatia ujenzi wa Hospitali ya wilaya inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni, Mnzava amewataka wanachi kuunga juhudi za rais wa awamu ya tano dkt. John Magufuli anzozifanya katika kuboresha sekta ya afya, elimu pamoja na miundombinu akiwa na lengo thabiti la kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025.

DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI

$
0
0


Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kumsimamisha kazi maramoja mfanyakazi wake mmoja katika Ofisi ya TRA mkoa wa Dodoma, DANIEL KINGU, kupisha uchunguzi wa kuhusika kwake na tuhuma zinazomkabili za kumbughudhi mfanyabiashara mmoja Jijini humo.

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye mitaa ya Jiji la Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa mfanyakazi huyo akishirikiana na watu wengine na kumtaka ampelekee shilingi laki 7 za kulipia mashine ya kutolea stakabadhi za kielektroniki (EFD Machine) la sivyo angefungiwa biashara yake.

“Mteja wetu awe salama!! na nitaendelea kufuatilia, lakini kuanzia muda huu Kingu aondoke ofisini, hatuwezi kuwavumilia watu wa jinsi hii hata kidogo kwa sababu kazi ya kuuza EFD machine si yake na anamwambia mteja aende ofisini kwake chumba namba fulani, anafanya haya mambo ndani ya ofisi ya Serikali, akitoka nje inakuwaje?” alihoji Dkt. Kijaji

Alisema hatasita kuchukua hatua hizo kwa wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Mapato popote walipo nchini wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja Msaidizi upande wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mustapha Mkiramweri alipofanya ziara ya kushitukiza katika mmoja wa mitaa Jijini Dodoma, kusikiliza kero za wafanyabiashara zinazoelekezwa kwenye Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Thomas Masese (kulia) alipokuwa akifanya ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara na kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akiwa na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), wakisikiliza malalamiko ya mteja kwa njia ya simu walipomtembelea ofisini kwake kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma, baada ya mfanyabiashara huyo kuilalamikia TRA kumlazimisha kununua mashine za kutolea stakabadhi ya kielektroniki (EFD Machine) .


PROF. MBARAWA AAGIZA UJENZI WA TENKI LA MAJISAFI SARANGA

$
0
0
Waziri wa Maji Mhe. Prof Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kuanza ujenzi wa tenki la Maji safi lenye uwezo wa kuhifadhi Maji kiasi cha lita za ujazo milioni tano katika eneo la Saranga jijini Dar es salaam.

Alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea katika maeneo ya Kimara Temboni na Saranga na kushuhudia changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji safi katika maeneo hayo iliyosababishwa na jografia ya milima na kupelekea kuwepo kwa msukumo mdogo wa Maji katika maeneo hayo. Hali hiyo ilikuwa ikisababisha baadhi ya wakazi hao kukosa huduma ya Maji.

“Niwahakikishie kuwa mtapata huduma ya Maji safi kwa masaa 24 na siku saba kwa wiki kama maeneo mengine kwa kuwa nimewaagiza DAWASA wajenge tenki la Maji safi lenye ujazo wa lita milioni tano ambalo lita sambaza Maji katika eneo lote la Saranga. Tayari wameshaanza kazi ya kutafuta mkandarasi na baada ya muda mfupi ujenzi utaanza” alisema Prof. Mbarawa

Aidha kwa upande wa Afisa mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amehaidi kutekeleza agizo la Waziri wa Maji kwa wakati ilikuendana na kasi na adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kumtua mama ndoo ya Maji kichwani kwa kuwafikishia huduma hiyo karibu zaidi  ilikuondokana na kero ya kufuata huduma hiyo kwa umbali mrefu. 

Hata hivyo Waziri Mbarawa ameigiza pia DAWASA kuweka mitandao wa Maji safi kwa Maeneo yote yasiyokuwa na mitandao kabisa ili tenki hilo la Maji safi likikamilika liweze kunufaisha wakazi wote wa eneo la Saranga.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Prof Makame Mbarawa akionesha jambo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ( wapili Kulia)  wakati alipotembelea maeneo la Saranga na Kimara Temboni na kuagiza kujengwa kwa Tenki la Maji litakalohudumia eneo hilo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wakati alipotembelea  maeneo ya Saranga na Kimara Temboni.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akielezea jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa wakati alipotembelea maeneo la Saranga na Kimara Temboni na kuagiza kujengwa kwa Tenki la Maji litakalohudumia eneo hilo.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

LIVE: MIAKA 19 YA CLOUDS FM NA JOSEPH KUSAGA


KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KIKAZI GEREZA KONDOA NA KING’ANG’A MKOANI DODOMA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na maafisa wa gereza la mifugo King’ang’a wilayani Kondoa mkoani Dodoma mara baada ya kuwasili gerezani hapo alipofanya ziara ya kikazi Desemba 3, 2018. 

Na ASP Deodatus Kazinja, Kondoa

Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza nchini watakiwa kujenga uhusiano mwema na viongozi wa kada tofauti tofauti nje ya Jeshi la magereza kwa lengo kuleta mshikamano na ushirikiano wa kiutendaji. Wito huo uliotolewa Desemba, 3 mwaka huu na Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na maafisa na askari wa magereza ya King’ang’a na gereza Kondoa wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Kamishna Kasike alisema kiongozi au askari wa magereza anayejifungia katika eneo lake tu ni vigumu kuwa na ushirikiano ulio mzuri na viongozi wenzake jambo ambalo lawezakukwamisha baadhi ya mambo ya kiutendaji ambayo yangetatulika kirahisi kama kungekuwa na uhusiano mzuri. “ Ukiwa kiongozi au askari wa kawaida jitahidini kutambua viongozi, watumishi wenzenu na jamii inayowazunguka, jenga nao uhusiano ulio mwema. Hakuna anayejitosheleza kwa kila jambo. Sote tunahitajiana kwa njia moja ama nyingine” alisisitiza CGP Kasike.

Kwa upande mwingine, CGP Kasike aliwataka maafisa na askari wote wa magereza nchini kudumisha nidhamu kazini. Alisisitiza kuwa nidhamu ndiyo nguzo kuu ya uaskari na nidhamu ndiyo chimbuko la utendaji ulio bora mahala pa kazi.

Aidha, Jenerali Kasike aliwafahamisha maafisa na askari katika magereza hayo kuwa maagizo ya Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ya kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa yanaendelea vizuri na kwa kuanzia tayari magereza 10 yameanishwa.

“Ninayo furaha kukufahamisheni kwamba katika agizo la kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa tayari magereza 10 yatakayozalisha mahindi, mpunga na maharage yameainishwa. Tunachokifanya sasa ni kutoa kipaumbele cha raslimali chache tulizonazo zielekee katika magereza hayo” alifahmisha CGP Kasike.

Kamishna Jenerali Kasike aliwataka maafisa na askari wote nchini kuwa wavumilivu na wastahimilivu wakati changamoto mbalimbali zinazowakabili wao binafsi na jeshi kwa ujumla zinatafutiwa ufumbuzi kwa zote serikali inazitambua na anayo matumaini kuwa zitatatulika hatua kwa hatua.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (mwenye miwani) akikagua maeneo ya mipaka ya gereza la mifugo King’ang’a inayodaiwa kuvamiwa na wananchi mbalimbali wakifanya shughuli za kilimo na ufugaji ndani ya eneo la gereza. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa gereza hilo Mrakibu wa Magereza Josephat Mkama.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akikagua mradi wa tofali za kuchoma wa gereza King’ang’a zilizoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari wa gereza hilo pamoja na gereza Kondoa. CGP Kasike alisisitiza kufyatuliwa kwa wingi kwa tofali hizo ili kukabiliana na uhaba wa nyumba katika vituo hivyo.

LUGOLA AWATAKA POLISI KUIMARISHA ULINZI MSIMU WA SIKUKUU; VIBAKA, MATAPELI NA MAJAMBAZI WAKAMATWE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kisorya, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Katika hotuba yake Lugola aliwataka Polisi nchini kuimarisha ulinzi kwa kuwasaka vibaka na majambazi katika msimu huu wa sikukuu. Pia aliwaagiza wawakamate watu wanaowatia mimba wananfunzi na wawafungulie mashtaka.

Na Felix Mwagara, (MOHA), Mara.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Polisi nchini liimarishe ulinzi wakati wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya na kuwataka wananchi kutokujisahau kwasababu ya sikukuu hizo.

Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kisorya, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, alisema msimu huu wa sikukuu vibaka, majambazi na matapeli hutumia sikukuu hizo kufanya uhalifu. Alisema Polisi wanapaswa kujipanga zaidi ili kuhakikisha sikukuu hizo zinasherekewa kwa amani kwa kufanya ulinzi kona zote za nchi ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa usalama na kuendelea kuijenga nchi yao.

“Hili tatizo la kuwepo vibaka na kuwafanya wananchi waishi kwa wasiwasi nchini, sasa napenda niwaambie nyie wananchi wa hapa Kisorya, na Tanzania kwa ujumla, Jeshi lipo imara, hao vibaka pamoja na majambazi wote, sasa hawana nafasi, nawaagiza polisi kufanya msako mkali kuwakamata matapeli, vibaka na majambazi wanaojitokeza hasa kipindi hiki cha maandalizi za sikukuu za krismasi na mwaka mpya, “ alisema Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkazi wa Kijiji cha Nambubi, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati mwananchi huyo ambaye alikuwa anawawakilisha walemavu jimboni Mwibara wakimuumba msaada Mbunge huyo. Lugola alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Katika hotuba yake Lugola aliwataka Polisi nchini kuimarisha ulinzi kwa kuwasaka vibaka na majambazi katika msimu huu wa sikukuu. Pia aliwaagiza wawakamate watu wanaowatia mimba wananfunzi na wawafungulie mashtaka.

Pia Lugola aliwataka wananchi watoe taarifa polisi iwapo wataona dalili zinazoashiria uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ili Jeshi la Polisi liweze kuzifanyia kazi mapema taarifa hizo. Aidha, Lugola aliwataka Polisi nchini kuwakamata watu wanaowarubuni wanafunzi pamoja na kuwatia mimba, wawafungulie mashtaka haraka iwezekanavyo kutokana na tatizo hilo kushika kasi nchini na kuwafanya wanafunzi kukatisha masomo yao.

“Wananchi wa Kisorya, tatizo hili ni la nchi nzima, na mara kwa mara nalikemea na kuwapa maagizo polisi kuwakamata watu wanaoharibu watoto wadogo wa shule kwa kuwatia mimba, nawataka polisi muwe wakali sana kuhusu hilo, hakuna kucheka na mtuhumiwa, kamateni wekeni rupango na apelekwe mahakamani mtuhumiwa ili kukomesha tatizo hili sugu hapa nchini,” alisema Lugola.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, alikiri tatizo hilo kuwa sugu wilayani humo, hata hivyo alimuahidi Waziri Lugola watalishughulikia na wahalifu wote watakamatwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (wapili kulia), akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alipokua anajibu maswali ya mbalimbali ya wananchi katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Nambubi, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani humo, Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Katika hotuba yake, Lugola aliwataka Polisi nchini kuimarisha ulinzi kwa kuwasaka vibaka na majambazi katika msimu huu wa sikukuu. Pia aliwaagiza wawakamate watu wanaowatia mimba wananfunzi na wawafungulie mashtaka.

“Mheshimiwa Waziri, matatizo ya wananfunzi kutiwa mimba hili lipo wilayani hapa, ila siku za nyuma tuliwahi kumkamata mwalimu ambaye alimtia mimba mwanafunzi na baadaye akasingizia kuwa mimba hiyo siyo yake na alipigwa na mwanafunzi mwenzake, hivyo tupo wakali kuhakikisha tunalimaliza tatizo hilo kwa kuwakamata na kuwapeleka mahakamani watuhumiwa,” alisema Bupilipili. Pia katika mkutano huo, Waziri Lugola aliwataka wananchi wa jimbo lake waanze maandalizi ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ili kuepuka janga la njaa lisije likawakumba endapo hawatalima. Hata hivyo, kijiji hicho alichokitembelea, kwa mujibu wa taarifa ya mipango yao ya kilimo walisema kuwa wana upungufu mkubwa wa mbegu za mazao mbalimbali hasa zao la pamba.

“Nimeagiza maafisa ugani waje kuangalia upungufu wa mbegu za pamba na kutatua kero hii kutokana na taarifa yenu ya mpango wa kilimo ya mwaka 2018/2019, na pia nasisitiza zaidi mlime mazao ya chakula kwa wingi,” alisema Lugola.

Lugola anaendelea na ziara jimboni kwake akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kisorya, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Katika hotuba yake, Lugola aliwataka Polisi nchini kuimarisha ulinzi kwa kuwasaka vibaka na majambazi katika msimu huu wa sikukuu. Pia aliwaagiza wawakamate watu 3 wanaowatia mimba wananfunzi na wawafungulie mashtaka. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Article 1

REPOA YAWANOA WATENDAJI WA NGAZI YA KATI WA SERIKALI NAMNA BORA YA KUTUMIA MATOKEO YA UTAFITI ILI KULETA MAENDELEO YA HARAKA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Masuala ya Uchumi na Maendeleo (REPOA) , Dkt Donald Mmari akitoa taarifa ya utangulizi kabla ya mgeni rasmi kufungua mafunzo ya siku tano yaliyoanza Desemba 3, 2018 mjini Morogoro kwa Watendaji wa ngazi ya kati wanaohusika na mipango na sera katika Wizara na Idara za serikali yakiwa na lengo la kuangalia namna bora ya kutumia matokeo ya utafiti mbalimbali unaofanywa na watafiti ili kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii na taifa.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi .
Watendaji wa ngazi ya kati wanaohusika na mipango na sera katika Wizara na Idara za serikali pamoja na watafiti baadhi yao wa Taasisi ya Utafiti ya Masuala ya Uchumi na Maendeleo (REPOA) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mgeni rasmi Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro, Noel Kazimoto ( kati kati walioketi ) kufungua mafunzo ya siku tano yaliyoanza Desemba 3, 2018 mjini Morogoro yakiwa na lengo la kuangalia namna bora ya kutumia matokeo ya utafiti mbalimbali unaofanywa na watafiti ili kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii na taifa na ( wapili kushoto) ni Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt Donald Mmari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Masuala ya Uchumi na Maendeleo (REPOA) , Dkt Donald Mmari ( wapili kutoka kulia ) akifurahia jambo na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano yaliyoanza Desemba 3, 2018 mjini Morogoro baada ya kufunguliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Noel Kazimoto ( hayupo pichani) yakiwa na lengo la kuangalia namna bora ya kutumia matokeo ya utafiti mbalimbali unaofanywa na watafiti ili kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii na taifa .

IJA KUNOA WANASHERIA, MAWAKILI SEKTA YA UMMA

$
0
0
Na Ibrahim Mdachi, Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto

Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kimeitisha kongamano maalum la wadau, kupitia na kutolea maoni mtaala wa mafunzo elekezi kwa Mawakili na Wanasheria wa Sekta ya Umma. Akizindua kongamano hilo jijini Dodoma, mwishoni mwa wiki iliyopita kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mick Kiliba, alisema kwa ujumla mafunzo yatakayotolewa na IJA yanalenga kujenga uwezo kwa wanasheria wapya wa Serikali.

Bw. Kiliba alisema kuwa Mafunzo hayo yanalenga kujua mifumo ya uendeshaji wa shughuli za kiserikali, uongozi na utumishi wa umma. Kwa lengo la kuwaandaa waajiriwa wapya wa kada ya sheria kutoa utumishi ulio bora na uliotukuka.

Alisema kuwa, matarajio ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utawala Bora kupitia Mafunzo haya ni kuona kila Mwanasheria aliyeajiriwa katika Utumishi wa Umma anafahamu ipasavyo; majukumu yake ya kazi. Aliongeza kuwa ni wajibu wa Mwanasheria kujua wajibu wake kama Mtumishi wa Umma, Muundo wa Serikali na Utunzaji wa siri za Serikali hali kadhalika kuiva kimaadili na kinidhamu.

“Itakumbukwa kuwa, waraka Na.5 wa mwaka 2011 wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, unaelekeza kutolewa kwa mafunzo elekezi kwa Watumishi wapya katika Utumishi wa Umma,” alieleza.
Aidha, kongamano hili ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Chuo cha IJA wa 2018/19 - 2022/23 ambapo Chuo cha IJA kilishirikiana na Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya Umma kama vile Mahakama ya Tanzania na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Miongoni mwa masuala muhimu yanayoangaziwa katika mtaala huo ni pamoja na kuwawezesha waajiriwa wapya kuelewa namna ya kuendesha shughuli za serikali, kuelewa sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.

Chuo cha IJA kimekasimiwa madaraka ya kuandaa na kutoa mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiriwa wote wa kada ya sheria katika sekta ya Umma nchini.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images