Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

SCANIA WAZINDUA LORI LA 'NEW GENERATION' AMBALO NI RAFIKI WA MAZINGIRA, JANUARI MAKAMBA AWAPONGEZA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Scania Tanzania imezindua kizazi kipya cha malori kwenye sekta ya usafiri nchini huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano January Makamba akilisifu shirika hilo kwa kuzindua malori hayo ambayo ni marafiki wa mazingira.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo wa kizazi kipya cha malori ambayo mbali ya kuwa rafiki wa mazingira yemetengenezwa katika mfumo wa kuhakikisha dereva 

anakuwa salama hata inapotokea ajali pamoja na ulaji mdogo wa mafuta, Makamba amesema analipongeza Shirika la Scania Tanzania kwa kutambua dhana ya kutunza mazingira ambapo imeamua kuja na malori ambayo mfumo wake ni rafiki wa mazingira.

"Huko tunakoelekea iko haja ya kuhakikisha tunakuwa na vyombo vya usafiri ambavyo vitakuwa rafiki wa mazingira badala ya kuwa usafiri ambao unaharibu wa mazingira.Kuna baadhi ya vyombo vya usafiri vinatoa moshi mwingi ambao ni hatari kwa mazingira yetu, hivyo 

lazima tuwe na usafiri rafiki katika kuhakikusha tunakuwa salama zaidi,"amesema Makamba.Pia Makamba amesema dunia ikiwa ni pamoja na Tanzania inakaribia hatua ya kusonga mbele ambapo kuunganishwa kwa teknolojia mpya na mifano mbalimbali ya biashara inaleta ufumbuzi wa usafiri wa kudumu na utoandoa usafiri wa kawaida.
 Waziri was Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano January Makamba (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Lars Eklund wakati wa uzinduzi wa aina mpya ya malori ya Scania jijini Dar es Salaam.Wengine ni sehemu ya maofisa wa Shirika la Scania.
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano January Makamba (kulia) akisalimiana na moja ya wadau wa usafiri nchini wakati wa uzinduzi wa lori la Scania 'New Generation' .Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa malori mapya ya Shirika la Scania .Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Scania nchini Lars Eklund akizungumza wakati wa uzinduzi wa lori mpya ya Scania ambayo ni rafiki wa Mazingira na yenye kutumia mafuta kidogo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano January Makamba akiwa ndani ya Lori la Scania ikiwa ni ishara ya kulizindua rasmi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


NAIBU WAZIRI MIFUGO NA UVUVI AWAPONGEZA MIKOCHENI ENGLISH MEDIUM SCHOOL KWA NAMNA INAVYOWANDAA WANAFUNZI KIELIMU

$
0
0
Na Said Mwishehe.

UONGOZI na walimu wa Shule ya Mikochen English Medium ya jijini Dar es Salaam wamepongezwa kwa kuendelea kufavya vizuri kielimu ambapo imekuwa ya pili kiwilaya, tano kimkoa na 54 kitaifa katika kundi la shule zenye watoto chini ya 40 katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba.

Pia wamepongezwa kwa kuwandaa wanafunzi katika misingi ya dini na malezi bora wakiwamo wa hitimu wa elimu ya msingi ambao wamefanya mahafali ya grade seven ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Uvuvi Abdalah Ulega.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa mahafali ya shule hiyo ambapo pia viongozi na walimu wamepongezwa kwa namna wqnavyowaandaa wanafunzi katika kuhakikisha wanazingatia masomo.

Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Ulega, Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi kutoka Wizara ya Kilimo na Mifugo Zacharia Kera amesema anaipongeza shule hiyo kwani imepiga hatua kimaendeleo na hasa katika kuwaandaa wanafunzo wake kitaaluma.

Wakati wa mahafali hayo wazazi na walezi wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanashuhudia mahafali hayo huku mgeni rasmi akitumia nafasi hiyo kutoa pongezi pia kwa walimu waliofanikisha kuwajenga kielimu wanafunzi ambao wamehitimu shuleni hapo.

Kera amesema amefurahishwa na namna ambavyo wanafunzi wa shule hiyo wakiwamo wahitimu wa shule ya hiyo ambavyo wameandaliwa vema na kwamba wamejengwa kwenye misingi imara ya kielimu.
Mkuu wa shule ya msingi   Mikocheni English Medium, Zuwena Khamis Omar akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mahafali dalasa la saba yaliyo fanika mikocheni jijini Dar es Salaam. Shule hiyo imekuwa ya  pili kiwilaya, tano kimkoa na 54 kitaifa.
Sehemu ya wazazi na walezi wakiwa katika mahafali ya darasa la saba katika Shule ya Mikochen English Medium iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa katika mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika katika Shule ya Mikochen English Medium ya jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Zacharia Kera akizungumza na waandishi wa habari katika mahafali ya darasa la saba ya shule Mikocheni English Medium ambapo amewataka wahitimu kuwa na nidhamu, bidii na kutanguliza uzalendo katika yale watakayokuwa wakifanya ili kufikia malengo yao. (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG).
Sehemu ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya dalasa la saba katika shule ya Mikochen English Medium iliyopo jijini Dar es Salaam.

ITS ALL ABOUT GETTING TOGETHER.

$
0
0
Stokhom Sweden karibuni kweny get together party ya Christmas tusherehekee pamoja na familia zetu kwa kiingio cha kr 200 kwa wakubwa, watt weny miaka 13-18 ni 100kr na miaka 6-12 ni kr 50 na chini ya miaka 5 free.

Hii itaambana ta na kinywaji kimoja bure na misosi ya kitanzania tutakuwa na buffé ya vyakula vya kitanzania!! Lipia sasa kuweka booking yako na familia tusherekee pamoja!!

@mamambila_openkitchen_sweden👩‍🍳🇸🇪 akishirikiana na Active Chef issa 🇸🇪👨‍🍳

WAFANYAKAZI WA WIZARA YA AFYA SIERRA LEONE WAFANYAZIARA YA KUJIFUNZA MASWALA YA RASLIMALI WATU ZANZIBAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla kulia akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya ya Sierra Leone waliofika Zanzibar kwa ajili ya kujifunza maswala ya Raslimali watu,hafla iliofanyika katika  ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
 -Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Afya ya Sierra Leone waliofika Zanzibar kwa ajili ya kujifunza maswala ya Raslimali watu,hafla iliofanyika katika  ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
 Mkuu wa Msafara Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Sierra Leone David Banya akizungumza kuhusiana na safari yao ya kuja Zanzibar kwa ajili ya kujifunza maswala ya Raslimali watu,hafla iliofanyika katika  ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na ziara ya Wafanyakazi wa Wizara ya Afya ya Sierra Leone waliofika Zanzibar kwa ajili ya kujifunza maswala ya Raslimali watu,hafla iliofanyika nnje ya   ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MKUTANO WADAU WA MAENDELEO ,MAAFISA WA SERIKALI NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Na. Estom Sanga-DSM 

Mkutano wa siku tano utakaojadili utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza jijini Dar es salaam baada ya kukamilika kwa ziara katika maeneo ya utekelezaji wa Mpango huo katika mkoa wa Mwanza na kisiwa cha Unguja. 

Mkutano huo unaowashirikisha Wadau wa Maendeleo wanaochangia utekelezaji wa Mpango huo,Maafisa wa Serikali kuu na baadhi ya halmashauri na Wafanyakazi wa TASAF hufanyika kila baada ya miezi sita kwa kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango na kuona mfanikio na changamoto za utekelezaji kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi kubwa iliyoko mbele ya Mfuko huo,Wataalamu, Wadau wa Maendeleo ni kuhakikisha kuwa maelekezo ya Serikali ya kuweka utaratibu mzuri wa kuwashirikisha walengwa katika kufanyakazi kupitia Mpango wa Ajira ya Muda unazingatiwa kwa ukamilifu. 

Bwana Mwamanga amesema licha ya mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Mpango huo unaojumuisha takribani Kaya za Walengwa zipatazo Milioni Moja na Laki Moja , bado kuwa idadi kubwa ya Wananchi walioko nje ya Mpango ambao wamekuwa wakiomba kujumuishwa ili nao pia waweze kunufaika na sera hiyo ya serikali ya kupambana na umaskini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akimkaribisha Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bw. Mohamed Muderis (aliyeketi) kuzungumza kwenye mkutano wa Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa Serikali na TASAF jijini Dar es salaam.


Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia, Bw. Mohamed Muderis (aliyesimama) akizungumza na Wadau wa Maendeleo, Maafisa wa Serikali na TASAF (hawapo pichani) mwanzoni mwa mkutano unaojadili utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini DSM.


Picha ya chini na juu ni baadhi ya Wadau wa Maendeleo , Maafisa wa Serikali na TASAF wakiwa kwenye mkutano unaojadili utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulioanza leo jijini DSM.

Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi (mbele) akiwa katika mkutano wa Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa Serikali na TASAF ambapo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulioanza leo jijini Dar es salaam.


KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA>>>>

Viwanda vya dawa vinahitaji watalaam wa Kemia na Biolojia

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi amesema viwanda vya dawa vinahitaji watalaam wenye msingi wa Masomo ya Kemia na Biolojia. Profesa Kambi ameyasema hayo leo wakati wa utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia katika matokeo ya kidato cha Nne na Sita kwa mwaka 2018 iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda ambapo vitajengwa viwanda vya dawa hivyo kunahitajika wabobezi wa katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa ajili ya kuendesha viwanda hivyo. Aidha amesema kuwa masomo hayo wanatakiwa wanafunzi kujituma zaidi ikiwa na wazazi kuwatia moyo wa kufanya vizuri katika masomo ya sayansi. Profesa Kambi amempongeza mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuanzisha tunzo hizo kwani inawatia moyo wanafunzi kuendelea kuvutika katika kusoma masomo ya Kemia na Biolojia.

Nae Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa wamekuwa wakitoa tunzo kwa wanafuzi kwa kuwapa cheti pamoja na Fedha. Amesema kwa huu jumla ya wanafunzi waliopata cheti na fedha ni 24 na walimu wanne wa masomo hayo. Wanafunzi hao wamepata kuanzia sh.500000 hadi 350 kwa wakwanza hadi wa tatu.  Amesema katika matokeo hayo shule za serikali ni Nne ambazo zimetoa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa mwaka 2018.

 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akizungumza wakati wa utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita mwaka 2018 iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

 Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza kuhusiana utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita mwaka 2018 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Esthehellen Jason akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akimkabidhi Cheti  Mwanafunzi aliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha Nne katika Masoko  Biolojia na Kemia Liliani Katabalo katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam.
 Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia kwa kidato cha Nne.

KUSOMA ZAIDO BOFYA HAPA

MICHUZI TV: Chin Bees avuliwa nguo jukwaani/Country Boy kolabo na Harmonize.

MICHUZI TV: NDUNGULILE AWAPA NENO TFDA


MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI YAFANA ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema si jambo jema hata kidogo wala haipendezi kwa wana jamii kuona inawatenga, kuwanyanyasa, kwa kuwatendea matendo maovu Watu wenye ulemavu ambayo ni kinyume na Haki za Binaadamu. Alisema Watu wenye ulemavu wanahitaji kutunzwa, kuthaminiwa na kuenziwa utu wao kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na Sheria ya Watu wenye Ulemavu.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani sherehe zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa  Sheikh Idriss Abdull Wakil uliopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar. Alisema Serikali ya Mapinmduzi ya Zanzibar imekuwa ikisikitishwa juu ya hali ya kinyama inayokiuka misingi ya Haki za Binaadamu inayofanywa na Watu wasiokuwa na maadili wala huduma kwa kuwafanyia vitendo viovu Watu wenye ulemavu pamoja na Wanawake na Watoto.

Balozi Seif alionya kwamba katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia unaowakumba pia Watu wenye Ulemavu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuchukuwa hatua kali na za kisheria dhidi ya wale wanaobainika kujihusisha na Vitendo hivyo viovu. “ Serikalio haitamvumilia wala kumuonea aibu mtu ye yote atakayebainika kutenda jambo hilo ovu”. Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Aliviagiza Vyombo vya Ulinzi, usalama pamoja na vile vya Sheria kutolifumbia jicho suala hilo na badala yake kuchukuwa hatua zinazofaa kwa mujibu wa Sheria zinavyoelekeza ili kukomesha vitendo hivyo. Balozi Seif  alisisitiza kwamba ni wajibu wa Wananchi na Wana Jamii wote kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha  ili kukabiliana na kadhia hii inayotishia ustawi wa Watu wenye Mahitaji Maalum ambao wanastahiki na wao kuishi kwa amani na upendo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.
Balozi Seif Kulia akimkabidhi Zawadi Bibi Jouaquiline Mohan Mwakilishi wa Shirika la Umojawa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kazi kubwa ya usimamizi wa Mpango wa usajili wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapongeza Vijana Walemavu  wasioona Awena na Jamila baada ya kusoma utenzi katika mahadhi yaliyoleta ladha kwenye sherehe hizo.
Baadhi ya washiriki wa kilele cha maadhimisho ya ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani zilizofanyika hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Muhimbili tawi la Mloganzila yaadhimisha siku ya Ukimwi Duniani kwa kutoa huduma ya upimaji wa afya bure

$
0
0
Muhimbili tawi la Mloganzila yaadhimisha siku ya Ukimwi Duniani kwa kutoa huduma ya upimaji wa afya bure. Mamia ya wananchi leo wamejitokeza kupima afya zao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo hospitali hiyo imefanya zoezi la upimaji bure pamoja na kutoa ushauri nasaha.

Akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yamefadhiliwa na kampuni ya HETERO Laboratories, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema takwimu zinaonesha kuwa kila watanzania mia moja watu 4.7 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 kati yao wameathirika na Virusi vya Ukimwi na takribani watanzania 1.4 milioni wanaishi na Virusi vya Ukimwi.

Pia kwa mujibu wa Shirika la afya duniani -WHO-, watu milioni 37 duniani wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi huku vijana wakiendelea kuwa kundi lililoko hatarini zaidi kuambukizwa VVU hasa barani Afrika.

Akielezea kuhusu mafanikio ya utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Magandi amesema Muhimbili hutoa huduma za VVU katika kliniki zake za wagonjwa wa nje kila siku ambapo wagonjwa 3,534 wanahudumiwa, huku Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila ikihudumia takribani wagonjwa 70.
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akifungua maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambapo Muhimbili-tawi la Mloganzila imeadhimisha siku hiyo leo kwa kutoa huduma ya upimaji bure.
 Baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kwa ajili ya kupata huduma wakimsikiliza Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Amina Mgunja akitoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ukimwi.
 Wauguzi wa Muhimbili wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MBEYA CEMENT YATOA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa LafargeHolcim na Mbeya Cement Company Limited nchini Ilse Boshoff akizungumza na waandishi wa habari katika semina elekezi kwa waandishi wa habari kuhusiana na utayari wao wa kusaidia maendeleo nchini, sambamba na nia yao ya kutoa gawio kwa serikali pamoja na ubora na uimara ya saruji inayozalishwa na kampuni hiyo yenye makao makuu jijiji Mbeya wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari iliyofanyika Ofisini kwao jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa Saruji Mark Chilambe akitoa mafunzo hayo ambapo ameeleza namna anavyozalisha saruji sambamba na utunzaji wa mazingira na amesema kuwa saruji wanazozalisha huuzwa kwa asilimia 8 nchini na nyingine husafirishwa nje ya nchi.
 Mafunzo yakiendelea 
Uongozi wa LafargeHolcim ukiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo yaliyofanyika ofisini kwao jijini Dar es Salaam.

TUSIMAMIE WAKANDARASI WANAOJENGA MJI WA SERIKALI DODOMA

$
0
0
Manaibu Mawaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua kiwanja kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo ambapo Serikali imetoa shilingi bilioni moja kwa kila Wizara na kuelekeza kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu Wizara zote ziwe zina majengo yake ya ofisi kwenye mji wa Serikali uliopo Ihumwa mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akiambatana na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na wataalamu wa Wizara hiyo wametembelea na kukagua eneo lenye ukubwa wa ekari 6.3 ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo Ihumwa mkoani Dodoma ambalo litagharimu jumla ya shilingi bilioni 1.120 na litajengwa na Vikosi vya Ujenzi, tawi la Dar es Salaam.
Kwandikwa amesema kuwa Serikali imetupa dhamana kubwa ya kuwa wakandarasi na kusimamia majengo ya Wizara zote, sisi kama Wizara tujenge vizuri kweli kweli ili tuwe mfano wa kuigwa na Wizara nyingine na tusimamie wakandarasi wengine wa JKT, NHC ambao wamepewa jukumu la kujenga ofisi za Wizara nyingine kwa kuwa sisi ndio wenye dhamana ya kusimamia wakandarasi wote nchini kama lilivyo agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa kassimu Majaliwa. Ameongeza kuwa tuko tayari kukesha na kukesha ili kuhakikisha kuwa tunafanya kazi usiku na mchana.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Mawasiliano Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (hayupo pichani) kuhusu eneo linalojengwa ofisi ya Wizara kwenye mji wa Serikali, Ihumwa, Dodoma.
Katibu Mkuu Mawasiliano, Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (wa kwanza kulia) akifafanua  jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya kukagua eneo linalojengwa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto)  wakisikiliza taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Barabara Wizarani Mhandisi Hapiness Mgalula kuhusu mipango ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakitembea kukagua eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ZANZIBAR ATILIANA SAINI NA MAKAMU WA RAIS WA HOSPITALI YA NANJING DRUM TOWER ZANZIBAR

$
0
0
 Katibu mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla kushoto akitiliana saini na Makamu wa Rais wa Hospitali ya Nanjing Drum Tower ya China Yu Cheng Gong kuhusiana na Mradi wa kuchunguza Kansa ya Shingo ya kizazi,hafla iliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
 Katibu mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla kushoto akibadilishana hati ya  saini na Makamu wa Rais wa Hospitali ya Nanjing Drum Tower ya China Yu Cheng Gong kuhusiana na Mradi wa kuchunguza Kansa ya Shingo ya kizazi,hafla iliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar. 
Mkurugenzi Tiba Hospitali ya Mnazi Mmjoa Dkt,Juma Salum, Mbwana kulia akikabidhiwa mashuka na Katibu wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar ZSTC Ali Hilal Vuai yaliotolewa msaada na shirika hilo kwa Hospitali mbalimbali za Wilaya Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

NSSF TPB KUENDELEZA MAHUSIANO MAZURI YA KIBIASHARA KWA TAASISI HIZO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Dar es
Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi wamekutana  leo jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo ili kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kwa Taasisi zao.


Wakuu wa Taasisi hizo  walikutana katika ofisi ya NSSF Makao  Makuu na walizungumza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha  mahusiano ya biashara baina ya Taasisi hizo mbili ambazo zimekuwa zikifanya huduma kwa muda mrefu.


Katika mazungumzo hayo Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ndugu William Erio alimuahidi Mkurugenzi mtendji wa TPB aendelee kutarajia biashara yenye tija


Nae Mkurugenzi mkuu wa TPB  Sebastia Moshingi amesema  atawashawishi wastaafu wote wa NSSF waliokuwa wakilipwa pensheni zao kupitia Shirika la Posta wafungue Akaunti TPB ili waweze kufaidika na huduma mpya ya kulipa wastaafu wa NSSF ambapo mstaafu atalipwa pensheni yake moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Benki hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi  wakiwa katika picha ya pamoja na kupeana mikono mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya ushirikiano wa huduma baina ya Taasisi wanazoziongoza
 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi  pamoja na watendaji wamashirika yote mawili wakiwa katika kikao cha kujadili huduma watakazoshirikiana.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi  wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mashirika wanayo yaongoza.

MICHEZO YA UBASHIRI YABADILISHA MAISHA YA WATU WENGI.

$
0
0
MENEJA uhusiano wa Kampuni ya michezo ya kubashiri (SPORTPESA) Sabrina Msuya ameeleza mafanikio ya kampeni ya shinda zaidi na sportpesa kutoka Bajaji 100 kushindaniwa mpaka kufikia Bajaji 26 zilizobakia kwa sasa kutokana na mwitikio mkubwa kwa wabashiri mwaka huu.

“Kiukweli kabisa tunajivunia kama SportPesa, kwa kupitia promosheni hii tumefanikiwa kubadili maisha kwa Watanzania kupitia ushindi wao wa ubashiri wa matokeo amesema Msuya"

Pia ameeleza kuna Mabadiliko mengi kati ya hayo ni washindi wamenunua viwanja na wengine wamejenga nyumba kwa kupitia bajaj wanazoshinda kupitia promosheni hii inayoendelea na wengine wanawalipia ada watoto zao ambalo ndiyo jambo la msingi kuona watu wakiendelesha familia zao kupitia ubashiri wao.

Vilevile Promosheni hii inatoa ajira kwa Watanzania, kwani wapo baadhi ya washindi ni waajiriwa wanaposhinda bajaj wanawapa watu wawafanyie biashara, hivyo utaona ni jinsi gani hapo tumehusika katika kuajiri.Na washindi wa mwaka huu wametoka Mikoa ya Mara,Dar es salaam,Morogoro,Mwanza,Kigoma na Tanga ambao washindi wa mwaka jana walitokea Mkoa wa Kahama,Newala,Arusha.

Sportpesa imewasaidia Watanzania kujifunza mbinu za kufanya biashara kwani kabla ya kushinda bajaj hizo walikuwa hawafanyi biashara zozote, lakini wanaposhinda wanaanza kujifunza kufanya biashara kwa kupitia hizo bajaj.

BOHARI YA DAWA (MSD) YAPATA BODI MPYA YA WADHAMINI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ` (Mb.) leo amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) ambayo mwenyekiti wake ni Dr.Fatma Mrisho. 

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni pamoja na Bi. Uphoo Swai, Dkt. Eliamini Sedoyeke, Bw. Ahmed Shaaban Kilima, Bw. Mwemezi Elnathan Ngemera, Bw. Lubengo Hilary Nyang’ula, Prof. Eligius Francis Lyamuya na Dkt. Marina Daula Njelekela ``huku mjumbe mwingine wa Bodi hiyo akitegemewa kuteuliwa hivi karibuni.

Mhe. Ummy amewataka wajumbe wa bodi hiyo, kufanya kazi kama timu moja kwa kutumia taaluma na weledi wao ili kuhakikisha wanasimamia vyema utendaji wa shughuli za Bohari ya Dawa na kufikia viwango bora vya ufanisi zaidi katika ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

Aidha amewasihi wajumbe hao kuhakikisha MSD inajiendesha kibiashara, sambamba na kuzingatia taratibu za kitaalamu zinazohusiana na usimamizi na udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na maelekezo ya sheria ya manunuzi ya umma.

Waziri Ummy ameielekeza bodi hiyo kuhakikisha Bohari ya Dawa inajiendesha vyema kifedha na shughuli zake kuendeshwa kwa gharama nafuu, kuziba mianya yote ya rushwa, wizi na ubadhirifu wa aina yoyote ile, upatikanaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi vyenye ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa na mwisho kusimamia, kuboresha na kudumisha matumizi ya tehama ili kuleta tija katika utekelezaji wa majukumu ya Bohari ya Dawa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ` (kushoto), akimkabidhi vifaa vya kazi Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Udhamini ya Bohari ya Dawa (MSD), Dkt.Fatma Mrisho baada ya kuizindua rasmi Dar es Salaam leo.
` Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo.
Mjumbe wa bodi hiyo, Dkt.Marina Njelekela, akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa bodi.`
Baadhi ya maofisa wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.

UPANUZI WA BANDARI GATI NAMBA MOJA WAFIKIA ASILIMIA 100

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umefikia hatua nzuri baada ya kukamilka kwa upanuzi wa gati namba moja kwa asilimia 100 huku meli ya kwanza ikitarajiwa kutia nanga wiki moja ijayo ikishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.

Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdediti Kakoko, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa Sh. bilioni 336.7 wa upanuzi wa bandari hiyo.

Amesema upanuzi huo umeiongezea uwezo gati hiyo yenye urefu wa mita 192 wa kubeba meli kubwa mbili za tani 45,000 hadi tani 60,000 kwa wakati mmoja kutokana na kuongezewa kitako cha upana wa mita 11.5 kinachobebwa na nguzo imara za zege zilizochimbiwa mita 70 chini ya bahari.

Amesema baada ya mkandarasi kukabidhi gati hiyo siku chache zijazo atakabidhiwa na kuanza kazi ya upanuzi wa gati namba mbili inayotarajiwa kukamilika Machi mwakani na upanuzi utaendelea hadi kufikia gati namba saba.

Akizungumzia ujenzi wa gati ya magari (RoRo Berth) pamoja na yadi ya kuegesha magari amesema mradi huo ulitakiwa uwe umekamilika lakini mkandarasi alikutana na changamoto ya kuwepo kwa udogo mbaya na hivyo kulazimika kutafuta udogo mzuri na kuujaza na kwamba ujenzi unatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa Juni mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdediti Kakoko, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Fredy Lihundi, akifafanua jambo
Wakandarasi wanaofanya upanuzi katika Bandari ya Dar es Salaam, wakijadili jambo katika mradi huo na viongozi wa TPA.
Mtambo wa kuchimba kina cha Bahari ukimwaga mchanga nje ya bahari katika Bandari ya Dar es Salaam.

TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA

$
0
0

   NaEmmanuel Masaka,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini Tanzania(TFDA) imefungua mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Afrika jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Kanda kwa nchi za Afrika, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wachunguzi wa Maabara .

Dk.Ndugulile ameeleza kwa sasa duniani kumekuepo na usugu mkubwa  kwenye baadhi ya vyakula ambavo haviivi vizuri au  walaji wa nyama na mayai kutochunguza kwa makini kama kuna asilimia yoyote ambayo italeta madhara Kwenye miili yao pindi watakapokula vyakula ambavo si salama kwa afya zao.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya dawa na chakula ( TFDA)Adam Fimbo amefafanua zaidi kuwa lengo la mafunzo hayo si tu  kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara bali pia kutoa elimu kwa jamii jinsi gani wanatakiwa kuepuka vyakula ambavo vitaleta madhara baadae katika miili yao.

Fimbo amesema washiriki wa mafunzo hayo wapo 30 na nchi ambazo zinazoshiriki ni 22.Baadhi ya nchi hizo ni Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Chad, DRC, Egypt, Kenya,Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria, SieraLeone, South Africa, Sudan, Uganda,  Tanzania na Zimbabwe.


Pia amewasisitiza  washiriki kuzingatia mafunzo hayo kwa ajili ya kunusuru na kupunguza kabisa uwezekano wa baadhi ya magonjwa ambayo si ya lazima endapo tutaweza kuyapatia ufumbuzi mapema .
Naibu waziri wa Afya maendeleo Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Africa, leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Adam fimbo akizungumza na waandishi wa habari (hawapi pichani) leo jijini Dar es Salaam katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za africa.

Makamu Mkurugenzi wa Maabara kutoka Nigeria Dkt.Flosade Oluwabamieo akifafanua jambo mbele washiliki wa mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa leo jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya washiriki wakimzikiliza Naibu Waziri wa Afya Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndungulile (hayupo pichani) alipokua akifungua mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Africa, leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

BANC ABC YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WATEJA WAKE

$
0
0
Na Pamela Mollel,Arusha

Banc ABC katika kuwajali wateja wake wa maeneo mbalimbali hapa nchini imeanzisha huduma maalumu ya kutumia satellite ili kuwafikia kwa haraka zaidi

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivi karibuni, Meneja wa Benki hiyo Magabe Nyambuche alisema pamoja na kuboresha huduma za kibenki pia wameanzisha huduma hiyo ya satelite itakayokuwa na uwezo wa kuwafikia hata wateja wavijijini

Alitaja mikoa ambao kwa sasa wanatoa huduma hiyo ya satellite ni Arusha,Dar es salaam,Dodoma na Mwanza.Alisema kuwa katika msimu huu wa sikukuu ya Chrismas wanatoa zawadi kwa wateja wote watakao weka pesa kwenye account(fixed account)watapata riba papo kwa papo.Pia aliwataka wananchi kujiunga na benki hiyo kwakuwa huduma zake ni nzuri .

Meneja wa Banc ABC tawi la Arusha, Magabe Nyambuche akizungumza jijini Arusha leo.

MICHUZI TV : OPERESHENI YA UVUVI HARAMU YAPAISHA MAPATO YA SERIKALI KUU, SAMAKI WAONGEZEKA

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images