Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Mhitimu Chuo cha Mipango Awaasa Vijana Kuchangamkia Fursa Mfuko wa Mikopo kwa Vijana


MOROGORO MARATHONI ILIVYOFANA BAADA YA KUFANYIKA KWA MARA YA KWANZA .

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Morogoro.

WANARIADHA Marko Joseph wa Singida na Amina Mohamed wa JKT –Arusha jana wamewek rekodi mpya baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa mbio za kilometa 21 kwa wananume na wanawake katika mashindano ya Mbio mpya za Morogoro Marathon 2018.

Joseph alifanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kutumia saa 1:05:50 akifuatiwa na mwanariadha Faraja Lazaro w JKT –A rusha aliyemaliza mbio hizo zilizoanzia na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri akituia saa 1:0:04.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na mwanariadha mkongwe Dickson Marwa aliyemaliza mbio hizo kwa kutumia saa 1:07:42 huku nafasi ya nne ikichukuliwa na mwanariadha Anthony Moya aliyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:07:42.

Kwa upande wa wanawake Amina Mohamed amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kutumia saa 1:21:47 akifuatiwa n Rozalia Fabiani liyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:23:59 huku Monica Nicolaus akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2:00:08.

Washindi wa Mbio za Kilometa tano wametangazwa Hashim Athuman (18:50:07) kwa upande wa wanaume huku kwa wanawake akishika nafasi ya kwanza Rosemary Mustapha kutoka mjini Magharibi Zanzibar (23:41:66).
Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Mbio za Morogoro Marathoni.
Baadhi ya Washiriki wa Mbio hizo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathoni .
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Kihanga akizungumza katika Mashindano hayo.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mbio za km 21 kwa wanawake Amina Mohamed zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa tatu wa mbio za km 21 kwa wanawake Monica Nicolaus zawadi ya king'amuzi cha DSTV.

Chuo cha Mipango cha Mpongeza Rais Magufuli kwa Utendaji Wake

KIGAMBONI INTERNATIONAL MARATHON 2018 YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva akikimbia za mbio KM 10 za Kigamboni mapema leo eneo la Fun City jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Ofisa Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando (kushoto).
Wakimbiaji wa KM 41 wakifukuza upepo katika mchuano mkali.
Kila mmoja akionyesha umahili wake wa kufukuza upepo katika mbio za Kigamboni International Marathon 2018 zilizofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam.

UN yahimiza mapambano dhidi ya UKIMWI

$
0
0
UMOJA wa Mataifa umesema jamii ina wakati mgumu wa kutengeneza mikakati ya kumaliza tatizo la UKIMWI ifikapo mwaka 2030 au la kizazi kijacho kitabeba mzigo mzito wa kuendelea kupambana na janga hili la kidunia. Tamko hilo limetolewa wakati inatambulika kwamba watu milioni 77 duniani wameambukizwa UKIMWI huku wengine milioni 35 wakiwa wamekufa kutokana na magonjwa nyemelezi. Kauli hiyo imetolewa juzi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, akikariri waraka wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye siku hiyo.

Alisema miaka 30 tangu kuanzishwa kwa siku ya UKIMWI duniani, bado hali ni tete na kwamba juhudi zozote tunazochukua sasa zinaweza kuonesha kama tutazika UKIMWI ifikapo mwaka 2030 au la. Alisema pamoja na dunia kupiga hatua kubwa katika kung’amua na kutibu ugonjwa huo, hatua zilizofikiwa bado hajazifikia nia ya dunia ya kuondokana na tatizo hilo.
Katibu Mkuu huyo alisema kwamba maambukizi mapya hayapungui kwa jinsi dunia inavyotaka huku baadhi ya maeneo yakiwa nyuma zaidi huku raslimali fedha zikizidi kupungua.

Pia hali ya unyanyapaa inazidi kuwa mbaya zaidi na huduma kwa wahitaji zikiwa za kibaguzi na kusababisha kutokuwapo kwa uwazi. Katibu mkuu huyo alitaka dunia kubadilika kuondokana na unyanyapaa na ubaguzi na kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kuudhibiti na kuumaliza ugonjwa huo. Akizungumza katika siku ya UKIMWI mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI na kusema UN ipo sanjari na juhudi za Tanzania.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng  kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na UN nchini alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akihutubia wananchi (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu kutoka wa wahisani wa maendeleo wa UKIMWI wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakiwemo wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dodoma, Maafisa wa jeshi la Polisi, wakazi wa jiji la Dodoma, Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali, viongozi wa dini pamoja wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wa maendeleo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kitaifa yalifanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Selcom shifts Tanzania to a cashless economy

$
0
0
Mastercard and Selcom have expanded their collaboration by signing a strategic partnership agreement to introduce a variety of payment solutions in the country, thus supporting Tanzania’s goal of becoming a cashless economy.

In collaboration with Selcom, Hub 255 has organized the first of its kind Hackathon that has brought together 44 hackers with different skill sets; designers, data scientists, technology and business developers that will showcase utilization of the Masterpass Quick Response (QR) payment Application Programming Interface (API).

The API allows for consumers to gain access to a wide variety of payment solutions that are accessible on mobile money platforms or via their bank. According to the Marketing Manager of Selcom, Sabrina Munir said Masterpass QR enables millions of micro, small and medium enterprises (MSMEs) across Africa to accept fast and secure digital payments for the first time.

She said the service addresses challenges previously faced by small business owners who were unable to afford point of sale infrastructure and were forced to transact in cash. As for consumers, this technology eliminates the need to carry cash or traditional bank cards. “Selcom is wholly Tanzanian-owned, with a vision to enhance financial inclusion across Africa through strategic partnerships and alliances to facilitate the seamless movement of funds electronically at all levels,” she said.
Winners of Tsh 1,000,000 during the Selcom Masterpass QR- Hackathon at HUB255 from the left Product designer UX/UI, Mbwana Habibu, joined by one of the judges Mercy Kitomari, Andorid Developer, Jackson Twalipo, Head of Software Development at Selcom, Rosario Arun and Back end developer, Athjuman Mwinami. Event has been sponsored by Abel & Fernandes Communications and Raha
1. First runner-up of Selcom Masterpass QR Hackathon at Hub255 (Sheria kiganjani) from left Advocate, Nabiry Jumanne, Developer- Peter Daniel, Judge- Mercy Kitomari, Head of Software Development at Selcom, Rosario Arun, Business Development Manager- Chris Bweno and Graphics Designer Justine Peterson. Event has been sponsored by Abel & Fernandes Communications and Raha. 
Second runner-up of Selcom Masterpass QR Hackathon at Hub255 (team locate) from left Software programme- Erick Justin, Judge- Mercy Kitomari, Business personell- Bavius Muganga, Head of Software Development at Selcom, Rosario.

PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI

$
0
0

Katika kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu kwa ufanisi zaidi taasisi ya Pamoja Foundation kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation imezindua hostel kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa shule za serikali.

Uzinduzi wa hostel hiyo uliogharimu jumla ya shilingi milioni 50 umefanywa leo na Diwani wa Kata ya Tuangoma Mohamed Suleiman kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Mbagala Ally Mangungu katika eneo la Mzinga wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hostel hiyo, Diwani wa Kata ya Tuangoma Selemani amepongeza ubunifu uliofanywa na taasisi ya Pamoja foundation kwa kuanzisha mradi wa kusaidia wasichana hasa katika masuala ya elimu na kuzitaka taasisi nyingine kushirikiana katika kusaidia masuala ya elimu ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.

Aidha, aliwaasa wananchi wengine kuiga mfano wa mwananchi wa eneo la Mzinga kwa kutoa eneo la wakfu kwa ajili ya kujengwa hostel hiyo ambapo alisema uamuzi huo utawezesha kujenga hostel nyingi na kubainisha kuwa eneo la Tuangoma ulipo mradi wa viwanja 20000 yeye kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Mbagala ataangalia namna ya kupata kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hostel kwa kuwa katika mradi huo kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya shule.

Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akifungua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli iliyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho. 
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam leo, hostel hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Kushoto kwa Diwani ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho. 
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman (kulia) akiangalia vitanda katika moja ya vyumba vya Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Wa pili Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho. 
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akikata utepe kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo  imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. 


DKT. ABBASI AWAPIGIA SIMU “LIVE” WAKURUGENZI SSRA, HUDUMA ZA WAKALA WA MELI KUFAFANUA HOJA ZA WANANCHI

$
0
0
Na Hassan Silayo - MAELEZO

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas ameendelea na utaratibu wa kuwapigia simu Wakuu wa Taasisi ili kujibu hoja za wananchi moja kwa moja katika ziara yake kwa vyombo habari inayoendelea nchini.

Katika mahojiano na kituo cha Redio cha Jembe FM 93.7 mkoani Mwanza, 

Dkt. Abbasi alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dkt. Irene Isaka , ambaye alifafanua kuhusu Sheria mpya ya Hifadhi ya jamii.Dkt. Irene alisema kuwa baada ya kuunganisha Mifuko mafao yamezidi kuboreshwa ili mstaafu awe anapokea fao kubwa la mwezi.

Dkt. Isaka amesema kuwa mstaafu atalipwa fao la mkupuo la 25% na baada ya hapo fao la mwezi litakuwa kubwa zaidi tofauti na ilivyokua awali ambapo fao la mkupuo lilikuwa kubwa lakini fao la kila mwezi likawa dogo kumfanya mstaafu ashindwe kumudu maisha.

Aidha, Mkurugenzi wa SSRA ametaja faida zingine za Sheria mpya kuwa ni familia ya mstaafu kuendelea kulipwa kwa miaka mitatu baada ya mstaafu kufariki, fao la kuachishwa kazi, kuweka usawa katika kulipa mafao na kuwa hivi sasa wanaweka utaratibu wafanyakazi wapate mikopo ya nyumba kupitia pensheni zao.

Katika mahojiano hayo ya moja kwa moja na Kituo cha Jembe FM, Dkt. Abbasi pia alimpigia simu Mkurugenzi wa Wakala wa Hufuma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamisi kujibu hoja na masuala ya usafiri wa maji hasa ununuzi w meli mpya Ziwa Victoria ulipofikia.

Bw. Hamisi alielezea vema hatua ambazo Serikali imechukua na inaendelea kuzichukua kuboresha usafiri wa majini.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali akifanya mahojiano maalum na kituo cha Radio cha Jembe Fm cha Jijini Mwanza kuhusu miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Jembe FM 93.7 mkoani Mwanza, Jimmy Kagaruki akisoma maswali yaliyokuwa yakitumwa na waskilizaji yaliyohusumiaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.


ONGEZEKO WAHITIMU CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE NI MAFANIKIO- PROF KILLIAN

$
0
0
Na Zanab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yamefanyika jana kwa jumla ya wahitimu 1769 wametunukiwa katika ngazi mbalimbali.

Kwenye mahafali hayo wahitimu 1736 wametunukiwa digrii za awali katkka fani mbalimbali, 26 wakitunukiwa stashada ya uzamili katika elimu na 7 wakitunukiwa shahada ya umahiri.

Akitoa hotuba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es salaam Dkt Jakaya Mrisho Kikwete , Rasi wa Chuo Kikuu Kishirikishi Professa Bernadeta Killian amesema kuwa kati ya wahitimu wote wa mwaka huu wanaume ni 1255 na wanawake ni 514.

Amesema idadi ya wahitimu kwa upande wa digrii za awali ni kubwa ikilinganishwa na wahitimu wa miaka yote iliyopita, kwani wahitimu wa digrii za awali kwa mwaka 2017 ilikua ni 1443 ambalo ni ongezeko la wahitimu 239 na kufikia 1736 na wahitimu wa masomo ya sayansi kuongezeka mara mbili kutoka 231 kwa mwaka 2017 kufikia 472 kwa mwaka 2018.
Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dkt Jakaya Kikwete akitoa cheti kwa Mwanafunzi Bora wa kike kutoka kitivo cha Elimu Irene Loshiro wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yamefanyika jana ambapo jumla ya wahitimu 1769 wametunukiwa katika ngazi mbalimbali.
Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt Jakaya Kikwete akitoa cheti kwa Mwanafunzi Bora wa kiume kutoka kitivo cha Sayansi Mohamed Hassan wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) .
Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt Jakaya Kikwete akiwa na Mwanafunzi Bora wa kike kutoka kitivo cha ElimuIrene Loshiro na Mwanafunzi bora wa Kiume Kitivo cha Sayansi Mohamed Hassan wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) jana.

SERIKALI, VODACOM FOUNDATION WASHIRIKIANA KUOKOA MAISHA YA WANAFUNZI VISIWA VYA UKEREWE

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Mpina (wa pili kushoto) akipokea moja ya jaketi maalum la kujiokole (life jacket) kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia ikiwa ni moja ya vifaa mbalimbali vya uokoaji vilivyotolewa na taasisi hiyo mwishoni mwa wiki hii mjini Ukerewe. Waziri Mpina alitangaza kuanza kwa ujenzi wa bweni kwaajili ya wanafunzi wanaoishi upande wa pili wa kivuko ambapo taasisi ya Vodacom Foundation iliahidi kutoa vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Bw Cornel Magembe (wa kwanza kushoto) na muasisi wa taasisi ya Sukos Kova Foundation, Bw Suleiman Kova.

ILI kuokoa zaidi ya wanafunzi 1300 wanaosafiri kwenye maji kila siku asubuhi kwenda shule katika visiwa vya Ukerewe jijini Mwanza, Waziri wa Uvuvi na Mifugo Luhaga Mpina amesema serikali itajenga bweni ili wanafunzi hao waishi shuleni. Waziri Mpina alitangaza uamuzi huo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vya uokozi majini vilivyotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Sukos Kova Foundation ambao pia wametoa mafunzo ya uokozi na kujikinga na majanga kwa wanafunzi, walimu, wavuvi na wakazi wengine wa visiwa hivyo.

Msaada huu unajumuisha makoti ya kujiokolea 1,568, vifaa vya kuzimia moto 21, mablanketi ya kuzimia moto 21, pamoja na vifaa vya kutolea huduma ya kwanza 21 ikiwa na malengo ya kusaidia shule za sekondari na msingi kuwa na utayari wa kukabiliana na majanga au maafa mbalimbali pindi yanapotokea. Pia simu za redio 8 pamoja na suti za majini 20 zimegawiwa kwa viongozi wa fukwe za maji.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Mpina akikabidhi mtungi wa kuzimia moto (fire extinguisher) kwa wawakilishi wa shule ya sekondari Mibungo baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya uokoaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia mwishoni mwa wiki hii mjini Ukerewe. Waziri Mpina alitangaza kuanza kwa ujenzi wa bweni kwaajili ya wanafunzi wanaoishi upande wa pili wa kivuko ambapo taasisi ya Vodacom Foundation iliahidi kutoa vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao. Wanaoshuhudia ni muasisi wa taasisi ya Sukos Kova Foundation Suleiman Kova na Bi Rosalynn Mworia.

“Nawashukuru sana Vodacom Tanzania Foundation kwa msaada huu ambao utawaweka salama wanafunzi wa shule hizi, lakini pia wakazi wa hapa wanaangukia katika wizara yangu maana wao ni wavuvi, kwa maana hiyo nina jukumu kubwa la kuwasaidia, na hivyo natangaza kwamba serikali itajenga bweni moja ili wanafunzi waanze kuishi hapo shuleni,” alisema Waziri Mpina.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi. Rosalynn Mworia aliunga mkono juhudi za serikali kwa kuahidi kwamba taasisi yake itanunua magodoro na vitanda kwa ajili ya bweni hilo pindi litakapokamilika.

“Tumefurahishwa sana na uamuzi wa serikali wa kujenga bweni hilo, maana hii itaokoa vipaji vingi ambavyo vingeweza kupotea aidha kwa kukata tamaa maana usafiri wa kwenda shule ni mgumu, au kutokea kwa majanga ya majini, hivyo basi pindi bweni hilo litakapokamilika sisi tutaleta vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao,” alisema Mworia.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akipokea radio za upepo (Radio Calls) kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia ikiwa ni moja ya vifaa mbalimbali vya uokoaji vilivyotolewa na taasisi hiyo mjini Ukerewe ili kukabiliana na majanga ya majini. Waziri Mpina alitangaza kuanza kwa ujenzi wa bweni kwaajili ya wanafunzi wanaoishi upande wa pili wa kivuko ambapo taasisi ya Vodacom Foundation iliahidi kutoa vitanda na magodoro kwa ajili ya wanafunzi hao. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Bw Cornel Magembe (wa kwanza kushoto) na muasisi wa taasisi ya Sukos Kova Foundation Suleiman Kova. 

Mwanafunzi Editha Fabian kutoka Bwiro Sekondari alisema wamefurahishwa na uamuzi wa serikali maana utawafanya wasome kwa bidii zaidi, “tutakuwa katika mazingira salama, hatutachoka maana muda mwingi tutautumia kusoma badala ya kuwa safarini huku tukiwaza kuzama majini,” alisema Editha.

Waziri Mpina pia aliziomba taasisi zote mbili kuandaa mpango mkakati endelevu wa miaka mitatu ili kutoa elimu ya majanga kwa wakazi wa kanda ya Ziwa Victoria, “mkifanya hivi mtafikia watu wengi zaidi na pia kutakuwa na uendelevu wa juhudi zenu za pamoja, tafadhali kaeni chini miliangalie hili kwa kina zaidi,” aliongeza Waziri Mpina.

ESRF yafanya darasa la wazi kuhusiana na mfumo wa kidigitali kuelekea tanzania ya viwanda

$
0
0
Mtaalamu wa Masuala ya Kidigitali, Profesa Louis Henry Fourie, akiwasilisha mada iliyohusu mchango wa kidigitali katika Maendeleo ya Viwanda akihusisha fursa zinazopatikana katika Kilimo, Elimu, Biashara na Uwasilishaji wa Huduma wakati wa darasa la wazi lililofanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora akichangia hoja wakati Darasa la Wazi lililohusu Mchango wa Kidigitali katika Maendeleo ya Viwanda likihusisha  fursa zinazopatikana katika Kilimo, Elimu, Biashara na Uwasilishaji wa Huduma. Darasa hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Maarifa na Ubunifu, Margareth Nzuki akichangia hoja wakati Darasa la Wazi lililohusu Mchango wa Kidigitali katika Maendeleo ya Viwanda likihusisha  fursa zinazopatikana katika Kilimo, Elimu, Biashara na Uwasilishaji wa Huduma. Darasa hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mtaalamu wa Masuala ya Kidigitali, Profesa Louis Henry Fourie na katikati ni Dkt. Oswald Mashindano.
Mshiriki akichangia hoja wakati Darasa la Wazi lililohusu Mchango wa Kidigitali katika Maendeleo ya Viwanda likihusisha  fursa zinazopatikana katika Kilimo, Elimu, Biashara na Uwasilishaji wa Huduma. Darasa hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Masuala ya Kidigitali, Profesa Louis Henry Fourie(wapili kushoto),akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Darasa la Wazi lililohusu  Mchango wa Kidigitali katika Maendeleo ya Viwanda likihusisha  fursa zinazopatikana katika Kilimo, Elimu, Biashara na Uwasilishaji wa Huduma.Wengine mstari wa mbele ni Dkt. Oswald Mashindano(wakwanza kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Maarifa na Ubunifu, Margareth Nzuki (watatu kushoto) na Profesa Mascalena . Darasa hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.

MICHUZI TV: Rayvanny:Wasafi Festival Morogoro imenifanyia maajabu

INTRODUCING: Mwasiti Featuring Roma - Fall in love (Official video)

Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho

$
0
0
Kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inanunua korosho yote ya wakulima inatimia kabla ya kipindi cha masika hakijashika kasi, uongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji umewatoa hofu wakulima wote wa mikoa ya kusini kuwa serikali inao uwezo wa kununua na kihifadhi korosho yote itakayonunuliwa.

Hakikisho hilo limetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija wakati anahitimisha siku ya kwanza ya oparehseni ya ukaguzi wa maghala kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara. 
“Ziara ya ukaguzi wa maghala inatokana maagizo ya kikao cha tathmini ya Operesheni Korosho kilichoitishwa na Mwenyekiti wake Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, ambapo pamoja na mambo mengine kilibaini ufinyu wa maeneo ya kuhifadhia korosho kutoka kwa wakulima” anasema Prof. Buchweishaija. 

Kwenye ziara hiyo Prof. Buchwaishaija pamoja na Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) Ludovick Nduhiye na maafisa wengine waandamizi wa wizara hiyo walifanikiwa kukagua maghala ya korosho kwenye wilaya za Mtwara, Mtama, Masasi na Nachingwea na kubaini kuwa maghala makuu na yale ya uhifadhi yana nafasi ya ziada kuhifadhi korosho zaidi ya tani elfu arobaini na nane.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Prof. Joseph Buchwaishaija (mwenye Kaunda suti), akisisitiza jambo kwa mwakilishi wa ghala la kuhifadhi korosho la OLAM Theophil Nandonde wakati alipofanya ziara ya kukagua maghala ya kuhifadhi korosho mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija, akipokea maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya OLAM inayomiliki maghala ya kuhifadhi korosho eneo la bandari ya Mtwara. Pembeni ni Naibu Katibu Makuu wa Wizara hiyo sekta ya viwanda Bw. Ludovick Nduhiye. 
 Meneja wa Bandari Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdulkarim  Salim akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Joseph Buchwaishaija wakati wa ziara yake ya kukagua maghala ya kuhifadhi korosho kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi. Kwenye ziara hiyo Serikali imefanikiwa kupata nafasi ya ziada ya kuhifadhi korosho zaidi ya tani elfu arobaini na nane. 
Mwakilishi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Sunshine kilichopo Mtama, Lindi akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Pof. Joseph Buchwaishaija alipotembelea kiwanda hicho ili kubaini uwezo wake wa kubangua korosho. (Picha na Idara ya Habari)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RC MBEYA APOKEA MSAADA WA MIFUKO 140 YA MBOLEA AINA YA UREA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chamilla(kushoto)pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini,Paul Nchinika wakipokea  mmoja wa mfuko wa mbolea kati ya 140 ya Urea kwa ajili ya vikundi vya kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani humo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya GSM Tanzania Matina Nkurlu(kulia)
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chamilla(watatu kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Paul Nchinika wakimshuhudia Maria Mwamulungu(kushoto) ambaye ni mmoja wa kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani humo akipokea moja ya mfuko kati ya 140 ya mbolea aina ya Urea kwa niaba ya wenzake kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu(kulia)
Wakina mama wanaounda vikundi vya kujishughulisha na kilimo mkoani Mbeya,Wakiimba nyimbo za furaha pamoja na  Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa GSM Tanzania,Matina Nkurlu(katikati) baada ya kukabidhiwa msaada wa mifuko ya mbolea 140 aina ya Urea.

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA AL NAKHIL YA DUBAI IKULU ZANZIBAR

$
0
0
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameikaribisha Kampuni ya Al Nakhil kutoka nchini Dubai kuitumia fursa ya kuja kuekeza  hapa Zanzibar katika sekta ya utalii.

Dk. Shein alitoa maelezo hayo wakati alipofanya mazungumzo na Sheikh Ali Rashid Lootah Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Nakhil kutoka nchini Dubai Ikulu mjini Zanzibar. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo wa Kampuni kubwa ya ujenzi ya Al Nakhil ya nchini Dubai kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kutoa ushirikiano wake mkubwa na kuweka mazingira mazuri katika kuhakikisha azma ya Kampuni hiyo inafikiwa. 

Dk. Shein alimueleza Mwenyekiti huyo kuwa Zanzibar ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya Utalii na iko tayari kutoa ushirikiano wake kwa Kampuni hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ina uzoefu na uwezo mkubwa katika harakati hizo. Aidha, Rais Dk. Shein alimueleza Mwenyekiti huyo juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii sambamba na hatua zilizofikiwa katika kuhakikisha idadi ya watalii imeongezeka.

Hivyo, Rais Dk. Shein aliendelea kusisitiza haja ya kuanzishwa kwa usafiri wa anga hasa kwa kutumia Kampuni ya ndege ya Emirates ambapo kati ya Zanzibar na Dubai, ambapo hatua hiyo itaimarisha na kuongeza idadi ya watalii na kuwasaidia wafanyabiashara na wasafiri wengine.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Nakhil ya Dubai, Sheikh. Ali Rashid Lootah, akiwa na Ujumbe wake,Mohammed Rashed na Masoud Mbarouk, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar, leo 3/12/2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Nakhil ya Nchini Dubai, Sheikh.Ali Rashid Lootah, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 3/12/2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Al Nakhil ya Nchini Dubai, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo.Sheikh. Ali Rashid Lootah,kulia kwa Sheikh.Ali ni Ndg.Mohammed Rashed.(Picha na Ikulu) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TIMU YA UHAKIKI WA WAKULIMA WA KOROSHO YAONGEZEKA, BIL 35 ZIMESHALIPWA-WAZIRI HASUNGA

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Timu ya wataalamu wa Uhakiki wa wakulima wa Korosho imeongezeka katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kutoka 11 mpaka kufikia timu 20 ili kuongeza uharaka wa uhakiki kwa ajili ya malipo ya wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo tarehe 3 Disemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CBT Mkoani Mtwara kutoa ufafanuzi juu hali ya ununuzi wa korosho.

Katika mkutano huo pia Waziri Hasunga amesema kuwa timu ya wataalamu tayari imewasili mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza uhakiki wa wakulima wa korosho kuanzia leo tarehe 3 Disemba 2018 ambapo mkoa wa Pwani utakuwa mkoa wanne kuhakikiwa ukiungana na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Alisema kuwa hadi kufikia tarehe 1 Disemba 2018 jumla ya vyama vya ushirika 212 vilikwisha hakikiwa kati ya vyama 504 vilivyopo katika mikoa hiyo mitatu ya kusini.Aidha, Vyama 157 vimekwishalipwa fedha zao kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na korosho nchini.

Mhe Hasunga alisema kuwa tayari Bilioni 35,540,709,854 zimekwishalipwa kwa wakulima wa korosho ambapo kilo Milioni 10,769 za korosho zimekwishalipiwa.Mhe Hasunga ameviambia vyombo vya habari kuwa idadi ya wakulima ambao wameshalipwa mpaka tarehe mosi Disemba ni wakulima 34,938

Amefafanua zaidi kwa kusema kuwa katika mkoa wa Lindi tayari Bilioni 12.7 zimelipwa ilihali katika Mkoa wa Ruvuma ni Bilioni 4.9 na Mkoa wa Mtwara ni Bilioni 17.9Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CBT Mkoani Mtwara kutoa ufafanuzi juu hali ya ununuzi wa korosho Tarehe 3 Disemba 2018. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hazina jijni Dodoma, Desemba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya Makatibu  Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipofungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. 
  Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua  Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. 
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda baada ya kufungau Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala  wa Mikoa  kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba  3, 2018. Wengine  pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo,  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), George Mkuchika na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MICHUZI TV: NIKKI MBISHI atema cheche/hakuna msanii wa HipHop zaidi yake.

Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa

$
0
0
Na. Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa lugha ni kielelezo na  sehemu  muhimu ya utambulisho wa taifa  lolote duniani. Hayo ameyasema jana Jijini Dodoma  katika Hafla  ya  kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
“Taifa lolote lisilo na utamaduni wake ni taifa mfu, na sisi tunajivunia kwa kuwa na utamaduni hai ikiwemo lugha yetu ya Kiswahili” alisema Dkt. Mwakyembe Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa  lugha ya Kiswahili ni kitambulisho cha utamaduni wa Mtanzania , kwa kuwa ndiyo lugha inayowaunganisha watu katika shughuli mbalimbali za Kijamii, Kisiasa na kiuchumi. Dkt. Mwakyembe anazidi kufafanua kuwa takribani lugha elfu sita (6000) huzungumzwa kila siku  duniani  ambapo  lugha ya Kiswahili  ni miongoni mwa lugha 10 zinazoongelewa kwa wingi.
“Mafunzo haya ni mwanzo tu mwa mambo mengi mazuri ambayo Wizara yangu imepanga kufanikisha na ukizingatia kampeni ya mwaka huu ya Uzalendo na Utaifa ina kauli mbiu inayohamasisha kukuza lugha yetu ambayo ni Kiswahili Utashi Wetu, Uhai Wetu” alisema Dkt. Mwakyembe.
Naye Kaimu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bibi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na  wataalamu wa lugha ya Kiswahili ( Hawapo katika picha),  jana Jijini Dodoma katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma..
 Mhitimu ambaye ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Chikole ya Jijini Dodoma Bibi. Neema Mkobalo akisoma risala  kwa mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison  Mwakyembe (Wa tatu kulia) katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa  na  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia)  akimkabidhi cheti  mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi ya  wataalamu wa lugha ya Kiswahili  Mwalimu  wa Shule ya Msingi Chikowa  Bibi. Theresia Lejale jana Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia)  akimkabidhi cheti  mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi ya  wataalamu wa lugha ya Kiswahili  Mwalimu wa  wa Shule ya Msingi Vikonje  Bw. Emmanuel Mzumya jana Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images