Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI

$
0
0

Siku ya Jumanne, tarehe 24 Septemba 2018, Mtanzania Gerald Bigurube alitunukiwa tuzo ya mwaka 2018 ya Ujerumani na Afrika (2018 German Africa Award). Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwake na Dr. Wolfgang Schäuble, Rais wa Bunge la Ujerumani Bundestag. Mwaka huu tuzo hiyo ilitolewa kwa watu wawili, mwingine akiwa ni Bw.

Bw. Gerald Bigurube ametumia kipindi cha miaka arobaini na nne katika Maisha yake kutunza wanyama pori na mazingira. Alipokuwa kiongozi wa TANAPA, Bw. Bigurube (miaka 66), alipambana dhidi ya ujangili, na alifanya juhudi za kuleta uwiano sawa baina ya utunzaji misitu na Wanyama pori kwa upande mmoja, na maisha ya wanadamu na maendeleo ya kiuchumi kw aupande mwingine. Bw. Bigurube ametoa mchango mkubwa kuonyesha jinsi utunzaji wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi vinavyotegemeana.

Kwa sasa, Bw. Bigurube anafanya kazi kama mkurugenzi mkaazi wa Frankfurt Zoolocal Society, taasisi ya kimataifa inayojihusisha na utunzaji wa mazingira, yenye makao yake mjini Frankfurt Ujerumani. Taasisi hiyo inafanya kazi kwa karibu na mamlaka za hifadhi nchini Tanzania, hususan katika kupambana na ujangili.

Ushirikiano wa mamlaka za Serikali ya Tanzania na Frankfurt Zoolocal Society umeiwezesha Tanzania kupata mafanikia katika utunzaji wa mazingira na kukabiliana na ujangili. Mpaka sasa, Tanzania imeweza kutenga maeneo takriban asilimia 32 ya ardhi yote kama hifadhi za taifa, na kuifanya kuwa ndiyo nchi yenye eneo kubwa zaidi la hifadhi barani Afrika.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Possi, amempongeza Bw. Bigurube kwa moyo wa uzalendo aliokua nao. Dkt. Possi pia amewahimiza wadau wa mazingira kuzidi kufanya kazi kwa karibu na Tanzania, haswa ukizingatia kwamba kazi ya Utunzaji wa mazingira inayofanywa na Tanzania pia ina manufaa kwa ulimwengu mzima.

Dkt. Possi alifafanua, juhudi za kutunza mazingira Tanzania zitafanikiwa zaidi iwapo kutakuwa kuna ushirikiano utakaoiwezesha Tanzania kupata teknolojia bora itakayorahisisha matumizi bora ya ardhi katika shughuli za binadamu, na kwa maana hiyo, nchi zilizoendelea na Taasisi mbalimbali za kimataifa zinapaswa kuzingatia kwamba masuala kama vile kilimo cha kisasa na upatikanaji wa uhakika wa nishati ni muhimu katika utunzaji wa mazingira.

ZAIDI YA SH. BILIONI TATU ZAPOTEA WILAYANI NYANGW’ALE

$
0
0

*Waziri Mkuu aagiza kuchukuliwa hatua kwa watumishi wote waliohusika
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyangw’ale waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu fedha ambazo zilitolewa na Serikali kugharamia miradi ya maendeleo wachukuliwe hatua.

Pia ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Gavana Matesa kwa sababu ameshindwa kutoa kwa mamlaka husika kuhusu taarifa za wizi wa fedha za maendeleo zilizotafunwa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Novemba 28, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nyangw’ale akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Geita.
Miongoni mwa miradi ambayo fedha zake zimepotea ni pamoja na sh. bilioni 1.2 za ujenzi ofisi ya halmashauri hiyo, sh. milioni 400 za ukarabati wa kituo cha afya Nyangw’ale, sh. milioni 611.230 za miradi ya maji.

Nyingine ni sh. milioni 536.119 za mpango wa malipo kulingana na huduma (EP4R), sh. milioni 125.914 za ushuru wa huduma, sh. milioni 31 za ujenzi wa ofisi ya mbunge na sh. milioni 109 za mfuko wa barabara.

“Wilaya ya Nyangw’ale ni mpya na Serikali imekuwa ikileta fedha nyingi lakini fedha zote zimetafunwa, Serikali ipo makini sana na moja kati ya vita kubwa ni dhidi ya mafisadi, wala rushwa ambayo ni endelevu hivyo tutashughulika na kila mmoja.

Tayari watu saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyangw’ale, Carlos Gwamagobe na wenzake wamekamatwa. Wizi unatisha Nyangw’ale wilaya inatia aibu tutawaondoa watu wote waliohusika na tutaendelea kuwakamata.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Sabasaba kilichopo Karumwa wilayani Nyang'hwale, Novemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wakati alipowasili kwenye Kiwanja cha Sabasaba  kilichopo Karumwa wilayani Nyang'hwale kuhutubia mkutano wa hadhara, Novemba 28, 2018.  

 Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Sabasaba  kilichopo Karumwa, Novemba 28, 2018.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

KITUO CHA KULEA WASICHANA (NHGO) CHAPOKEA MSAADA WENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILION 10 KUTOKA FCS

$
0
0
Kwa kuwa vijana ndio nguvu kazi ya taifa ni vema kuwajengea misingi mizuri ya kupenda kujitolea kwa ajili ya jamii yao, Na ndio maana Foundation for Civil Society imeweza kuandaa mashindano kwa ajili ya vijana kutoa stori zao za namna walivyoweza kijitoa katika kusaidia jamii na mwisho kuwapa zawadi wenye story nzuri zaidi.
Hayo yamesemwa mapema jana na Afisa Uhusiano, Biashara na Maendeleo wa Taasisi ya Foundation for Civil Society Martha Olotu wakati akiongea na waandishi wa habari kwa Niaba ya Mkurugenzi wa FCS Bw. Francis Kiwanga katika Jumanne ya Kutoa (Giving Tuesday), ambapo kwa mwaka huu wameweza kutoa misaada katika kituo cha New Hope for Girls Center kilichopo kimara jijini Dar es salaam.

Akielezea sababu za kuchagua kituo hicho afisa huyo amesema ni moyo wa upendo na wakujitolea alionao huyo Mama kwa kuwachukua mabinti wanaoishi katika mazingira hatarishi, Yatima, na walioterekezwa na familia zao na kuamua kuishi nao nyumbani kwake wakiwa ni kama sehemu ya familia yake na sio kama watoto ambao wapo kwenye kituo cha kulelewa.

Aliongeza kuwa mbali na tukio hilo la kuandaa mashindano kwa vijana, lakini pia kampeni hiyo ilitanguliwa na tukio la kijitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji wa damu katika Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha MOI ambapo watu 38 waliweza kijitolea damu.

Aidha aliendelea kusema kuwa wametoa misaada yenye thamani ya zaidi ya Milioni Kumi hii ikiwani FCS, wananchi mbalimbali, pamoja na mashirika mengine yaliyoguswa na tukio hilo, lakini kwa wafanyakazi wa Foundation for Civil Society wamejichanga na wametoa mashine ya Photocopy ikiwa ni kama njia ya kuacha alama katika kituo hicho.

Kwa upande wake Mama mlezi wa wasichana hao Bi. Consoler Eliya alisema kuwa sababu iliyomsukuma kufanya hivyo ni kutokana na ugumu wa maisha pamoja na mazingira hatarishi ambayo ameyapitia wakati akiwa msichana, Ikiwa ni pamoja na kupigwa sana, kukosa nafasi ya kusoma kutokana na magonjwa yaliyotokana na kipigo cha mara kwa mara.
Afisa Uhusiano, Biashara na Maendeleo wa Foundation for Civil Society Martha Orotu akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema jana jijini Dar es salaam katika siku ya Jumanne ya Kutoa (.Giving Tuesday).
Msichana Janeth Thobias ambaye ni miongoni mwa mabinti wanaolelewa katika kituo hicho akisoma Risala mbele ya wageni waalikwa mapema jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wasichana wa kituo cha New Hope for Girls Center wakiimba shairi mbele ya wageni waalikwa.

MWENYEKITI MPYA BODI YA WAKURUGENZI BARAZA LA KILIMO TANZANIA AKABIDHIWA 'KIJITI'.

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akimkabidhi rasmi Uenyekiti wa Baraza hilo Bi Jacqueline Mkindi baada ya kuteuliwa na Bodi na kuthibitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt Sinare amemaliza muda wake baada ya kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 5.
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi Jacqueline Mkindi akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania baada kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti Mh Jitu Son na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko, Mkutano huo umefanyika Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi Jacqueline Mkindi akimkabidhi tuzo ya heshima ya utendaji uliotukuka katika Sekta ya Kilimo, Mwenyeki wa Bodi ya Baraza la Kilimo aliyemaliza muda wake Dkt Sinare Yusuph Sinare , kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Bi Janeth Bitegeko, tukio hilo limefanyika Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania.
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi Jacqueline Mkindi akimakabidhi tuzo ya heshima ya utendaji uliotukuka katika Sekta ya Kilimo, Mwenyeki wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya baraza la kilimo Bw Salum Shamte, tukio hilo limefanyika Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo Tanzania

Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Mh Jitu son ambaye kwa sasa ni Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, na Bw Julias Nyabicha wakifuatilia kwa makini kitabu cha mahesabu wakati wa Mkutano Mkuu wa wajumbe wa Baraza la Kilimo Tanzania uliofanyika Dar es Salaam, wengine kwenye picha ni sehemu ya wajumbe wa Mkutano huo.
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi Jacqueline Mkindi, kulia ni makamo wake Mh Jitu Son, kushoto ni mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Sinare Yusuph Sinare wakiwa kwenye picha na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania muda mfupi baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kilimo uliofanyika Dar es Salaam.

MICHUZI TV: IMANI ZA KISHIRIKINA ZATAWALA PAMBANO LA SIMBA SC DHIDI YA MBABANE SWALLOWS

UJENZI WA RELI KIPANDE CHA PILI MOROGORO HADI MAKUTUPORA SINGIDA WASHIKA KASI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Kilosa

ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha pili kuanzia eneo la Morogoro hadi Makutupora Singida, unazidi kushika kasi baada ya wakandarasi wa ujenzi wa reli hiyo kumaliza kazi muhimu.

Kazi hizo ni pamoja na uchukuaji wa sampuli za udongo, miamba kwenye milima itakayapasuliwa, kuchonga, kupasua na kujaza udongo kwenye njia za reli ya mwendokasi pamoja na kumalizia ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mataluma ya reli.

Hayo yalibainika kwenye ziara ya maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya Ador Tanzania kwa waandishi mbalimbali nchini, ili kujionea ufanyaji kazi wa ujenzi wa reli hiyo kuanzia Morogoro hadi Makutupora.

Ujenzi wa reli hiyo kwa kipande hicho, unajengwa na Kampuni ya Yepi Merkezi kwa gharama ya dola bilioni 2, ambapo Meneja Mradi huo katika Lot 2 inayotoka Morogoro Mpaka Makutupola, Dk. Husnis Uysa amesema wamekamimilisha mambo ya Msingi katika ujenzi huo.

Amesema tayari wameshaleta vifaa ambavyo zaidi ya magari 3,085, ambayo ipo katika eneo la mradi, huku pia kambi za mafundi na wafanyakazi kujengwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkata, Kilosa na Makutupora.
Meneja mradi wa Standard Gauge kipande cha Morogoro hadi Makutupora kwa upande wa Shirika la reli nchini(TRC), Injinia Faustin Kataraia akiwaeleza Waandishi wa Habari namna mradi huo utakavyoungana na ule wa kutoka Dar mpaka Ngerengere.
Meneja Mradi wa SGR katika Lot 2 inayotoka Morogoro Mpaka Makutupola, Dk. Husnis Uysa akizungumza na Waandishi w ahabari juu ya hatua zilizochukuliwa katika kutekeleza Mradi huo. 
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliotembelea mradi wa SGR Kutoka Morogoro mpaka Makutupora wakiangalia mashine ya kusagia kokoto
Sehemu ya Makandarasi wakiendelea na ujenzi wa tuta kutoka Morogoro mpaka Makutupora Singida.
Mtambo wa kusagia Kokoto ukiwa umefungw akatika moja ya vituo vya kazi katika tuta la Morogoro kama unavyoonekana.

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA UKAGUZI UWANJA WA MBINU ZA MEDANI KILIMANJARO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamis Issah (kushoto), wakati alipofanya ziara ya Ukaguzi katika eneo la mafunzo ya mbinu za medani Kilelepori wilayani Siha mkoani Kilimanjaro leo 28/11/2018. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na wanafunzi wanaopata mafunzo kwa ngazi ya Uofisa pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo katika Shule ya Polisi Moshi eneo la Kilelepori wilayani Siha mkoani Kilimajaro leo 28/11/2018. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na baadhi ya Wakufunzi wa Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro wakati alipofanya ziara ya Ukaguzi Leo 28/11/2018. Picha na Jeshi la Polisi.

MICHUZI TV: STARTIMES YAZINDUA CHANELI YA 'StarTimes ON', BONGO STAR SEARCH KUNUFAIKA...


MICHUZI TV: MAMLAKA HUSIKA ZIINGILIE KATI UNYANYASAJI WA KINGONO VYUONI - CDF

RELI TV: MIAKA 3 YA JPM NA UBORESHAJI WA SEKTA YA USAFIRI WA RELI IKIWEMO UJENZI WA SGR TANZANIA

Michuzi TV: Wajasiriamali wapata dola 480,000 kutoka UBA, TEF

VOA Swahili: Duniani Leo November 28, 2018

Michuzi TV Exclusive: Mtangazaji nyota Millard Ayo aweka wazi siri ya mafanikio yake

IKULU: HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI KWENYE UFUNGUZI WA MAKTABA YA CHUO KIKUU (UDSM)

MBATIA AWEKA WAZI ALICHOTETA NA RAIS MAGUFULI WIKI CHACHE ZILIZOPITA.

$
0
0

Kilimanjaro.

MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia amewamegea siri wananchi wa mji mdogo wa Himo juu ya mazungumzo yake na Rais Dk. John Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Alidai alikwenda kumueleza malalamiko ya wananchi kuhusu amri ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi ya kusitisha ujenzi wa barabara na kusababisha hasara ya mabilioni ya shilingi.

“Haya yote nimemueleza Mheshimiwa Rais (Magufuli) niwe mkweli, nilibahatika hapo katikati Mheshimiwa Rais akaniita akasema hivi, narejea sauti ya Rais aliniambia na ameshaagiza ofisi zake na wengine wameniita Dodoma, barabara za wana Vunjo atachangia yeye binafsi kama John Pombe Magufuli, pili serikali yake itachangia na tatu atakuja kama Amiri Jeshi Mkuu kufungua barabara hizi yeye mwenyewe kama John Pombe Magufuli,”alisema

Mbatia alikuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Makuyuni katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya ghalani. 

Mradi wa upanuzi na ujenzi barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe unaodaiwa kusisitishwa katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zilikuwa zigharimu Sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) wa mwaka huu.
 Mbunge wa jimbo la Vunjo ,Mh James Mbatia akizungumza wakati wa mkutano wake uliofanyika katika Mji Mdogo wa Himo. 
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mh ,James Mbatia wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni hapo. 
 Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akifanya dua na baadhi ya viongozi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani Mji Mdogo wa Himo.



KAZI INAKWENDA VIZURI MRADI WA RELI YA KISASA KUTOKA DAR MPAKA SINGIDA MAKUTUPORA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Dodoma

Kazi inakwenda vizuri. Ndivyo unavyoweza sema kuhusu mradi wa reli ya kisasa marufu ya Standard Gauge kutokana na Shirika la Reli(TRC) kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kumsimamia mkandarasi Yepi Merkezi kwa ukaribu mkubwa.

Michuzi Blog imetembelea mradi huo, kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora, ambako kuna vipande viwili vya mradi huo vinavyotekelezwa na mkandarasi huyo, kujionea kuna mabadiliko makubwa  kuhusu ujenzi huo tofauti na watu wanavyozungumza katika Mitandao ya Kijamii na Vijiweni.

Hii inatokana na kuwepo kwa madai ya kuwa hakuna kazi inayofanyika, ambapo iko wazi kabisa kuwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kazi imefanyika kwa zaidi ya asilimia 36, ambapo sehemu zilizobakia ni ndogo na zinazoweza kufanyiwa kazi kwa uharaka na mkandarasi.

Pia, inaelezwa hata baadhi ya malighafi nyingi zinapatikana kwenye eneo la mradi iwe kipande cha Morogoro hadi Makutupora au Dar es Salaam hadi Morogoro, ambapo imerahisisha upatikanaji wa marighafi.

Akizungumza na Michuzi Blog Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Injinia Masanja Machibya, amesema hakuna malighafi yeyote inayozalishwa nje, bali mahitaji yote muhimu yanapatikana kwenye eneo la mradi.

Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Injinia Masanja Machibya, akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu mradi huo unavyoendelea katika Lot 1 inayotoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.
Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini (TRC), Injinia Masanja Machibya,akiwaonesha Wanndishi wa Habari mfano wa Reli ya SGR itakavyokuwa katika kiwanda cha kuzalisha Mataluma ya Reli hiyo.
Mafundi Wakiendelea na Ujenzi wa Madaraja na karavati katika eneo la mradi wa SGR eneo la Lot 1 Kisarawe.

Mataluma ya Reli yakiwa yameweka kwa ajili ya kutandikwa juu ili kujenga mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC),
Sehemu ya Wakandarasi wakiendelea na upandaji nyasi kwa ajili ya kuzuia Mmomonyoko wa udongo  kwenye tuta la kukatisha reli ya SGR.
Mafundi chuma wa mradi wa SGR Kutoka Yap Markenz wakiendelea na kazi ya kujenga Madaraja ya kupachika katika yard ya Shaurimoyo Jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, BASHUNGWA ATEMBELEA NFRA APONGEZA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA

$
0
0

Na Mathias Canal-NFRA, Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea na kujionea shughuli zinazofanywa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo Mhe Bashungwa amekagua ujenzi wa Maghala na Vihenge vya Kisasa (Silos) ambapo ameipongeza serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa mradi huo utakaoongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka.

Akizungumza na wafanyakazi wa NFRA mara baada ya kuzuru katika ofisi hizo zilizopo Mtaa wa Relini-Kizota Mhe Bashungwa alisema kuwa uongozi imara wa Dkt Magufuli umepelekea Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland kusaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ametoa rai kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Bi Vumilia L. Zikankuba kuweka msisitizo zaidi katika utoaji elimu kwa wakulima kuhusu njia bora za kuhifadhi mahindi ili wakati wanapotafuta soko waweze kupata soko imara na tija kutokana na nafaka hiyo.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa 
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA Bi Vumilia L. Zikankuba


Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu nchini Tanzania ya Mwaka 2017 (THDR) inayozungumzia  “Sera ya Kijamii Katika Muktadha wa Mageuzi ya Kiuchumi”, ina mchango mkubwa katika kuchambua masuala yanayohusu maendeleo ya binadamu na nafasi yake katika uandaaji wa mipango ya maendeleo, utengenezaji wa bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
Alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu wakati wa uzinduzi wa ripoiti hiyo mjini Dodoma jana.
“Kwa mtazamo wangu, dhana hii ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi sio tu kwamba ni dhana sahihi bali pia inaendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 – 2020/21.’ Alisema Dk. Mpango .
Aidha, alisema dhana ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi ni dhana ambayo imekuwa ikizingatiwa katika mipango ya ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka mmoja mmoja pamoja na miongozo ya uandaaji wa bajeti za serikali.
Dk. Mpango alisisitiza kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kujenga uchumi jumuishi, kutokuacha mtu yeyote nyuma katika mchakato wa maendeleo na kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya uchumi, serikali ya Tanzania imetoa umuhimu mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii ili kuinua hali za watu wake.
Waziri Mpango alisema kwamba sekta ya afya, elimu na miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli ya kisasa ni sehemu ya juhudi zinazofanya kuwezesha uchumi jumuishi.
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa nne kulia) akikata utepe kuzindua Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya (kulia) pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu (wa tatu kulia).
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Dkt. Phillip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly ambao ni wafadhili wa ripoti hiyo akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali bara na visiwani, ESRF, Umoja wa Mataifa pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma walioshiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Watumishi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wapewa mafunzo ya OPRAS

$
0
0

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt Evaristo Longopa amesema, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya utendaji wa Kazi ( OPRAS) utasaidia sana katika kuwapima watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Dkt. Longopa ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya uwezeshaji kuhusu mfumo wa OPRAS kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mafunzo hayo yaliwahusisha Manejimenti, Mawakili wa Serikali na watumishi wa kada nyingine na yalifanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Jijini Dodoma.

Katika mafunzo hayo, pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuelimishwa Sheria na Nyaraka mbalimbali zilizoanzisha OPRAS pia walielimishwa kuhusu umuhimu wa kila mtumishi katika utumishi umma wa kujaza fomu ya OPRAS kila mwaka kwa kushirikiana na Mkuu wake wa Kazi na kwamba zoezi hilo linatakiwa kufanyika kwa uwazi.

“ Katika vikao vyetu vya menejimenti, tulikubaliana kwamba, upo umuhimu wa zoezi la upimaji na tathmini ya utendaji kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Zoezi hili litatusaidia sana katika kujipima na kuwapima walio chini yetu ilikufikia malengo ambayo Ofisi yetu imejiwekea na hatimaye malengo ya Serikali kwa ujumla”. Akasema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya OPRAS kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikakali. Mafunzo hayo yalihusisha Menejiment, Mawakili wa Serikali na Watumishi wa kada nyingine . Walioketi nyuma ni wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Zainabu Kutengezah na Bi. Shomi Mongi.
Bi. Susan S. Kalele ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Raslimali watu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akitoa maelezo kwa Menejiment kuhusu mfumo wa OPRAS
Wakili wa Serikali Bi. Juliana Mnisi akiuliza swali kwa wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Bi Dorina Kalumna akitoa maelezo kwa watumishi wenzie jinsi ya kufikia ukokotoaji wa alama ambazo mtumishi na kiongozi wake wanakuwa wameafikiana wakati wa ujazaji wa fomu ya OPRAS.
habari na picha kwa hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

MAJALIWA USO KWA USO NA HAMIS MGEJA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga aliyehamia CHADEMA, Hamis Mgeja ambaye alijumuika na  maelfu ya mwananchi waliojitokeza kwenye Kiwanja cha  Sabasaba cha Karumwa wilayani Nyang'hwale  kumsikiliza Waziri Mkuu alipohutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita, Novemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye Kiwanja cha Sabasaba kilichopo Karumwa wilayani Nyang'hwale Novemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images