Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

DAWASA YAWAKUMBUSHA WATEJA WAKE KULIPA BILI ZAO


MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB, IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyemtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Nsekela alikwenda kwa lengo la kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa aliyeambatana na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU THABO MBEKI NA WAZIRI WA MAENDELEO WA KIMATAIFA WA NORWAY IKULU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mhe.Thabo Mbeki Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Afrika linalohusu Udhibiti na Utakatishaji wa Fedha haramu kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es salaam.Novemba 28,2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza  na Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mhe.Thabo Mbeki Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Afrika linalohusu Udhibiti na Utakatishaji wa Fedha haramu kabla ya kuagana nae Ikulu Jijini Dar es salaam.Novemba 28,2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mhe.Thabo Mbeki Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Afrika linalohusu Udhibiti na Utakatishaji wa Fedha haramu(watatu kutoka kushoto) kutoka kulia kwa mhe.Rais Magufuli ni  Bw.Barrister Akere Muna,Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Dkt.Damas Ndumbaro,Bi Mojanko Gumbi (Wapili kutoka kulia )Wakili wa Mhe.Thabo Mbeki, na Balozi Zuhura Bundala (wakwanza kutoka kushoto) Ikulu Jijini Dar es salaam.Novemba 28, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mhe.Thabo Mbeki Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Afrika linalohusu Udhibiti na Utakatishaji wa Fedha haramu .Ikulu Jijini Dar es salaam.Novemba 28,2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Nicolai Astrup kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Novemba 28,2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Nicolai Astrup alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi  Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Nicolai Astrup kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Afrika mashariki Dkt.Damasi Ndumbaro,Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba pamoja na Balozi wa Norway nchini Elisaberth Jacobsen Novemba 28, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Nicolai Astrup , Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Afrika mashariki Dkt.Damasi Ndumbaro,Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba pamoja na Balozi wa Norway nchini Elisaberth Jacobsen Novemba 28, 2018. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA ABC YAWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA JAMII

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha.

Benki ya ABC tawi la Arusha imeendelea na juhudi za kuwekeza kwenye maendeleo ya jamii kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali ,kusaidia jamii kupata bima za afya ili kuharakisha maendeleo ya jamii ya Kitanzania.

Meneja wa Benji hiyo tawi la Arusha Magabe Nyambuche amesema kuwa kwa mwaka 2019 Benji hiyo imejipanga kutoa mikopo kwa Vikundi maalumu ikiwemo Vicoba na Sacco's ambao wamekua wakipewa mafunzo na Maafisa Wa Ustawi wa jamii ili waweze kunufaika na mikopo kwa kufanya shughuli za uzalishaji Mali.

Magabe alisema kuwa benki hiyo limekua karibu na jamii na kuwafikia wananchi walioko vijijini kupitia ubunifu wa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ambapo benki hiyo ilipewa tuzo ya Ubunifu.

"Kwa sasa tuna mawakala 250 ambao wanahakikisha kuwa wateja wetu wanafikiwa na huduma za kifedha popote pale walipo" Anaeleza Meneja hiyo

Hata hivyo benki hiyo imedhamini mkutano mkuu wa Wadau wa maendeleo ya jamii unaondelea jijini Arusha ikiwa ni juhudi mojawapo ya kuisaidia jamii ambayo hunufaika na Utaalamu wa Maafisa wa Maendeleo katika Vijiji na Mjini.

Pia wamejizatiti katika kuendelea kushirikiana na serikali kuharakisha maendeleo ya jamii kwa kutuma dhana ya uwezeshaji wa mikopo yenye masharti nafuu.


Meneja wa Benji ABC tawi la Arusha Magabe Nyambuche

MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI

$
0
0
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kumuandikia barua mkandarasi wa Kampuni ya Impesa di Construzioni anayejenga kituo cha ukaguzi wa pamoja (one stop inspection station) eneo la Manyoni mkoani Singida na Nyakanazi mkoani Kagera kurejea eneo la kazi na kuendelea na ujenzi.

Akizungumza katika kijiji cha Muhalala mkoani Singida wakati wa ukaguzi wa kituo hicho, Katibu Mkuu huyo amesema Serikali tayari imeshashughulikia madai ya mkandarasi huyo, hivyo hana sababu ya kutoendelea na ujenzi wa mradi huo. "Naagiza Mkandarasi huyu arudi eneo lake la kazi na kuanza kazi ya ujenzi wa mradi huu mara moja", amesema Mhandisi Nyamhanga.

Aidha, Mhandisi Nyamhanga, ameeleza kuwa jumla ya gharama za mradi wa vituo hivyo ni takribani shilingi bilioni 55, ambayo itahusisha gharama za ujenzi, usimamizi na fidia. Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa ujenzi wa kituo hicho unaenda sambamba na ujenzi wa kituo kingine eneo la Nyakanazi mkoani Kagera ambapo kituo kingine cha vigwaza mkoani Pwani kimeshakamilika na hivyo kutafanya jumla ya vituo vikuu vitatu vya ukaguzi vyenye umbali wa kilomita 500 kutoka kwa kila kimoja.
 Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Masige Matari, akitoa taarifa ya mradi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga,  wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (One Stop Inspection Station), katika kijiji cha Muhalala, wilayani Manyoni, mkoani humo.
 Muonekano wa baadhi ya nyumba za watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Polisi watakaoishi mara baada ya ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja kukamilika katika kijiji cha Muhalala, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga,  akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri  Adel alkhateeb, anayesimamia ujenzi wa barabara wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati alipoukagua mradi huo, Mkoani Tabora.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua moja ya boksi kalvati iliyojengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua moja ya boksi kalvati iliyojengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara  ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati Katibu huyo alipokagua mradi huo, mkoani Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKIWASILI ZANZIBAR AKITOKEA NCHINI KENYA ALIPOKUWA AKIHUDHURIA MKUTANO WA BLUE ECONOMY

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari (Blue Economy).
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM Zanzibar alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari(Blue Economy).
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi na Wazee waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume Zanzibar, akitokea Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu (Blue Economy) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Serikali na Binafsi, kuhusiana na ziara yake Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari,(Blue Economy) kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Waziri wa Kilimo Maliasi Mifugo na Uvuvi Zanzibar.Mhe. Rashid Ali Juma.akiwa katika ukumbi wa VIP Zanzibar. (Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari (Blue Economy).
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM Zanzibar alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari(Blue Economy).
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi na Wazee waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume Zanzibar, akitokea Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu (Blue Economy) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Serikali na Binafsi, kuhusiana na ziara yake Nchini Kenya alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari,(Blue Economy) kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Waziri wa Kilimo Maliasi Mifugo na Uvuvi Zanzibar.Mhe. Rashid Ali Juma.akiwa katika ukumbi wa VIP Zanzibar. (Picha na Ikulu) 

KITUO CHA UWEZESHAJI SEKTA YA USAFIRI WA KATI WAKUTANA KUJADILI SERA MBALIMBALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Mkutano wa Kituo cha Uwezeshaji wa Usafiri wa Kati (CCTTFA), kimekutana na wadau kutoka nchi tofauti katika Ukanda wa Jangwa la Sahara kujadili sera mbalimbali.


Mkutano huo utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba 28- 30 mwaka huu utazungumzia  mpango wa sera za usafiri wa Afrika eneo la kiuchumi jamii ya ushirikiano wa kamati ya usafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa CCTTFA, Capt Dieudonne Dukundane amesema mkutano huu unalenga kujadili masuala mbalimbali ya Kiuchumi kwa nchi washirika na kuhakikisha mafanikio yanafikiwa.

Amesema, CCTTFA ni kituo kinachokutanisha nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Jamhutri ya Kidemokrasia  Congo, Rwanda na Burundi na kukutana pamoja ni kwa ajili ya kufahamu Tanzania wanafanikiwaje kwenye sekta ya usafiri hususani Reli na barabara na hata sisi pia tunajifunza baadhi ya vitu kutoka kwao.

"Tumekutana katika mkutano huu wa siku tatu lengo letu likiwa ni kujadiliana na masuala mbalimbali pia wao wanakuja pia kujifunza Tanzania imefanikiwa kwa namna ipi kwenye sekta ya usafiri hasa kwenye reli na barabara ikiwemo na sisi wenyewe kujifunza baadhi ya vitu kutoka kwao,"amesema Dukundane.


Katibu Mtendaji wa   Kituo cha Uwezeshaji wa Usafiri wa Kati (CCTTFA),  Capt Dieudonundne Dukane akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mkutano huo utakaofanyika kuanzia Novemba 28- 30 mwaka ukiwa na lengo la  kujadili masuala mbalimbali ya Kiuchumi kwa nchi washirika na kuhakikisha mafanikio yanafikiwa.

Washiriki wa mkutano wa mwaka wa  kituo cha Uwezeshaji wa Usafiri wa Kati (CCTTFA) wakiwa katika picha ya pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

UNICEF identifies youth role in SDG

$
0
0
By Our Reporter

Young citizens in Tanzania can play a significant role to enable the country realize its Vision 2025, the global Sustainable Development Goals and Agenda 2063.

Speaking in Dar es Salaam on Tuesday during World Children's Day celebrations , United Nation Children's Fund (UNICEF) Representative Ms. Maniza Zaman said youth of Tanzania should be encouraged and engaged in realizing of the country’s development objectives.

Ms. Maniza who was addressing over 100 young men and women from different schools and higher learning institutions from all over the country at an event organized at the Bank of Tanzania Conference Facilities said that Tanzania’s children under the age of 18 have their hopes and dreams in life, just like adults and, that these aspirations should not only be encouraged to blossom but also to benefit the country’s development agenda.

The Oxford University educated Ms. Maniza said that if every boy and girl is given a fair chance and the opportunity to be heard in life as well as supported accordingly, then chances are that they will be successful and make significant contribution to the country’s struggle for development.

“Let us encourage them to make the right choices and pursue the paths to make those choices a reality in their lives. This will surely help them achieve their goals in life as well as significantly contributing to the country’s major development goals,” said Ms Maniza.

During the event five young Tanzanians shared their aspirations, dreams, and narrated their stories on how they chose their path in life, bringing them to some encouraging achievements.

The five included Brigitte Lyimo, Miss Tanzania 2012 and now an activists for the rights of young people with albinism in Tanzania, an activist for youth rights from Arusha Raphael Dennis and an IT and engineering student at the University of Dar Es Salaam Witness Mtui.


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 27/11/2018

CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
SERIKALI ya China kupitia ubalozi wake nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es saalam wameandaa semina maalumu ambayo imelenga kujadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na kuimaimarisha masuala ya biashara.

Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo naibu Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya amesema kuwa semina hiyo imeandaliwa na Serikali ya China chini ya ubalozi wa nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya kujenga uhusiano pamoja na kujenga na kuimarisha mahusiano ya kibiashara.

Manyanya amesema kuwa semina hiyo imelenga kupanga mikakati ya kushirikiana baina ya nchi hizo mbili pamoja na faida kwa nchi hizo za Tanzania na China ambazo zimekuwa na uhusiano bora kwa muda mrefu na ameeleza kuwa Tanzania ina rasilimali za kutosha na mahusiano hayo yatasaidia sana katika kufikia malengo ya nchi ya kufikia uchumi wa kati 2025. Amesema kuwa agenda ya viwanda wana malengo ya kuongeza rasimali hasa za kilimo, madini nakadharika.

Pia amesema kuwa semina hiyo ambayo wazawa wanashiriki itakua chachu ya kufungua milango katika sekta ya viwanda. Pia amesema kuwa, "Katika kuwainua wazalishaji (wakulima) tutatoa elimu kuhusiana na masoko na ukuaji wa viwanda nchini na tutahakikisha wanajihusisha na  kilimo chenye tija  na ninawahakikishia kuwa watanufaika  na mikakati inayofuata  na kutambua namna ya kufanya kilimo kitakachowasaidia" ameeleza Manyanya.
 Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi. Stellah Manyanya akizungumza wakati wa akifungua  semina hiyo iliyoshirikisha wadau wa biashara kutoka Tanzania na China.
Balozi wa China nchini Wang Ke akizungumza  wakati wa semina hiyo ya kuimarisha uhusiano ambapo amesema kuwa wapo bega kwa bega na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha malengo ya kufikia uchumi wa kati 2025 yanafikiwa.
Baadhi wa washiriki wa semina wakifuatilia mjadala huo ambapo wadau mbalimbali wa kiuchumi wamekutana na kubadilishana mawazo juu ya namna bora ya kukuza uchumi.
 Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Stellah Manyanya na Balozi wa China nchini Wang ke wakiwa  kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa biashara wa hapa nchini na kutoka nchini China.
(Picha na Agnes Francis, Blogu ya Jamii.)


SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA WAANDAA MKAKATI WA KITAIFA KUSIMAMIA TAKA NCHINI.

$
0
0

Na.Khadija Seif, Globu ya jamii.

SHIRIKA la umoja wa mataifa linalojishugulisha na mazingira (AGENDA) limezitaka nchi zilizopo katika Ukanda wa Jangwa la Sahara kutunga sera zakusimamia ukusanyaji wa taka Ngumu ili kulinda afya ya mazingira.

Wito huo umetolewa Leo jijini Dar es salaam katika mkutano wapili wa wadau wa kuandaa mkakati wa kitaifa wakusimamia taka Tanzania(AGENDA) ambapo imewashirikisha Taasisi ,Wizara na Mamlaka mbalimbali za serikali,Makampuni binafsi na wawakilishi wa asasi za kirai.

Akizungumza na wanahabari Kiongozi wa shirika hilo kwa Ukanda wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Prof. Abdrahman Bary amesema kushindwa kuhifadhi Takataka kumeleta madhara mengi kwa nchi zinazoendelea na kwa sasa mapambano yanaendelea katika kudhibiti uzalishaji wa taka. 

Aidha Bary ameeleza kuwa usimamizi bora wa taka ngumu ni muhimu kwa afya ya jamii,usalama na Mazingira bora kwa ujumla.Hata hivyo amefafanua kuwa baadhi ya matatizo yanayolikabili jiji la Dar es salaam ni pamoja na ongezeko la kiwango cha juu cha idadi ya watu pamoja na uwezo mdogo kifedha wa kudhibiti taka.

Kwa upande wa Msimamizi wa mradi kudhibiti takataka ngumu Prof. Jamidu Katima kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema linakadiriwa kuzalisha tani 4600 za taka kwa siku huku taka nyingi zikiwa hazipelekwi sehemu za kuhifadhia takataka (dampo) hivyo kuhimiza mamlaka husika kusimamia taratibu za uhifadhi, Kusafirisha na kutupa taka ili kulinda mazingira

Katima amesema mkakati huo unalenga kuona nchi zinazoendelea zinapambana katika kudhibiti taka Ngumu pamoja na uzalishaji wa taka Ngumu, kutumia taka kama vyanzo vya uzalishaji mbolea, taka zinazoweza kurejelewa zirejelewe huku wakizalisha Ajira kwa vijana wao kupitia uhifadhi taka wakisasa.

Vilevile Katima amewapongeza shirika la Mazingira UN kutupatia Msaada wa kifedha kuwezesha uandaaji wa mkakati wa kusimamia taka.
 Msimamizi wa mradi kudhibiti takataka ngumu Prof. Jamidu Katima kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa pili wa wadau wa Kuandaa mkakati wa kusimamia Takataka
Washiriki katika Mkutano wa pili wa wadau wa Kuandaa mkakati wa Kitaifa wa kusimamia Taka nchini uliofanyika jijini Dar es salaam ulioandaliwa na Shirika la kudhibiti na kusimamia Taka (AGENDA) 

UZINDUZI KONGAMAO KA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII

BENKI YA NBC YACHANGIA DAMU MPANGO WA TAIFA DAMU SALAMA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Blogu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa benki ya  NBC Theobald Sabi amesema kuwa kama wadau wa kijamii na maendeleo wanawajibu wa kuchangia damu kwa wahitaji wa damu kote nchini. Akizungumza wakati wa uchangiaji wa damu  kupitia mpango wa taifa wa damu salama Mkurugenzi mtendaji wa NBC Sabi amesema kuwa watu wenye uhitaji wa damu ni wengi na uchangiaji ni mdogo hivyo wakiwa wafanyakazi wa benki ya NBC wamechangia na wataendelea kuchangia  damu ili iweze kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Amesema kuwa mpango wa taifa wa damu salama damu inayohitajika ni unit 600000 mpango mkakati wao ni kukusanya unit 375,500 kwa mwaka sawa na asilimia70. Kwa upande wake Mkurugenzi wa hazina na masoko ya fedha wa NBC Peter Nalitolela amesema kuwa benki ya NBC kupitia idara yao waliona umuhimu wa kuchangia damu na kushawishi wafanyakazi na wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuchangia damu ambayo itawasaidia watu wenye mahitaji maaalumu.

Ameeleza kuwa wanaendelea kujipanga ili kuhakikisha kila mwaka wanakusanya damu kwa kuwa mahitaji ya damu inayokusanywa haitoshelezi mahitaji. Pia Afisa wa uhamasishaji wa mpango wa taifa wa damu salama kanda ya Mashariki Fatuma Mjungu amesema kuwa wanashukuru benki ya NBC na kuwataka waendelee hivyo hivyo kwani mahitaji ya damu ni makubwa sana.

Na amewataka wadau wengine kujitokeza katika uchangiaji wa damu kwa kuwa mahitaji ya damu ni makubwa sana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Benki hiyo kushiriki katika uchangiaji damu iliyofanyika katika viwanja vya NBC jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa NBC Peter Nalitolela akizungumza kuhusiana na Kitengo chao cha kuratibu uchangiaji damu kutokana na mahitaji kuwa makubwa kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya NBC jijini Dar es Salaam.
 Mwananchi akichangia damu baada ya kuwakuta wafanyakazi wa NBC wakiendelea na uchangiaji damu
 Wafanyakazi wakijisajili kwa ajili ya uchangiaji damu kupitia mpango wa Taifa wa Damu Salama.

DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imefanikwia kuunganisha wateja wapya 2881 katika mfumo mpya wa ugawaji maji ambao umekamilika kujengwa kwenye miradi tofauti ya Mamlaka hiyo.

Kazi hiyo iliyoanza Oktoba Mosi mwaka huu imeweza kufanikisha kuunganisha wateja wapya na inaendelea kwa kasi kwenye maeneo tofauti ya Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Akielezea maunganisho hayo mapya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya amesema kuwa mpaka sasa maunganisho mapya yanaendelea kwa kasi katika maeneo ya Salasala, Kilimahewa na Kinzudi, Kiluvya, Kiluvya madukani, Gogono, Hondoro na Kiamba pamoja na  Bagamoyo- Kiembeni.Amesema, lengo ni kuunganisha wateja wapya 60,000 (Elfu Sitini) katika eneo la Salasala na wateja 100,000 (laki moja) katika eneo lilipo kati ya Kiluvya na Mbezi.

"Wateja wapya 2881 wameshaunganishwa maeneo yaliyopo, idadi ikiwa 1624 kwa Salasala- Kinzudi, Kiluvya- Mbezi 1111 na Bagamoyo 146 hivyo bado kunwa uwezekano wa wateja wengi zaidi kuendelea kuunganishwa,"amesema.

Amesema Katika kuhakikisha kuwa maji yalioongezeka yanawafikia wananchi wengi zaidi hasa katika maeneo ambayo zamani hayakuwa na mtandao wa mabomba, miradi mikubwa na midogo imetekelezwa ikiwemo uoanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini kukiwa na  ujenzi wa matenki ya maji matano yenye ujazo wa kati ya lita milioni 5.0 na 6.0 pamoja na ulazaji wa mtandao wa mabomba.

Msuya amesema, maeneo hayo yote yanapata maji kutoka katika mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini na ili kuharakisha kazi ya uunganishwaji wa majisafi kwa wananchi wote, wananchi wanakumbushwa kuwa uunganishwaji mpya unatolewa kwa Mkopo.Aidha, ameeleza kuwa DAWASA itagharamia vifaa, uchimbaji wa mtaro na mabomba ya maji yataunganishwa katika malipo ambayo mteja atarerejesha ndani ya muda wa miezi sita.

Matenki hayo  yamejengwa katika maeneo ya Changanyikeni, Salasala,Wazo, Mabwepande na Bagamoyo na katika maeneo yote ya miinuko ili kuwezesha maji kufika katika maeneo mengi Zaidi kwa msukumo mzuri na mradi huo umetekelezwa na serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya Exim ya India.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoa pongezi kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa kufanikisha uunganishwaji wa Wateja wapya 2881 katika mfumo mpya wa ugawaji maji ambao umekamilika kujengwa kwenye miradi tofauti ya Mamlaka hiyo.

MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA MAJI WA NYAMTUKUZA WILAYANI NYANG’HWALE

$
0
0



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Kamuyaga Ibuga (kushoto) wakati alipotembelea Mradi wa Maji wa Nyamtukuza wilayani Nyang’hwale,  Novemba 28, 2018
PMO_0086-min
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea chanzo cha Maji katika  Mradi wa Maji wa Nyamtukuza wilayani Nyang’hwale, Novemba 28, 2018
PMO_0043-min
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitazama wingi wa Maji katika tangi  wakati alipotembelea Mradi wa Maji wa  Nyamtukuza wilayani Nyang’hwale Novemba 28, 2018.  Kulia ni Waziri wa Nisahati na Mbunge wa Chato, Medard Kalemani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA

$
0
0

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili wafanyakazi watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bado haujakamilika. 

Wakili wa Serikali, Jenipher Massue aamedai hayo leo Novemba 28.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando wakati kai hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa, 

"Mheshimiwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa upelezi bado haujakamilika tu naomba tarehe ya kutajwa" amedai wakili Massue.
Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 12, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. 

Katika kesi hiyo wafanyakazi hao wanakabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa Mazingira.

Washtakiwa hao ni Ofisa wa Mazingira NEMC,Deusdith Katwale(38) na Mtaalam wa IT, Luciana Lawi(33) wote wakazi wa ubungo Msewe, Katibu Muhasi wa NEMC (Sekretari), Edna Lutanjuka (51) Mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, Msaidizi wa ofisa Mwaruka Mwaruka (42) naOfisa mazingira Nemc, Lilian Laizer (27) wote Wa kazi wa Ukonga Mombasa na Ofisa mazingira wa Nemc, Magori Wambura (38) mkazi wa Bombambili. 

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwamo la kula njama, mawili ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kusababisha hasara ya Sh.Milioni 160



Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Septemba 27, 2016 na April Mosi,2018 jijini Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.

SERIKALI SAIDIENI KUINUA TASINIA YA MAVAZI NA MITINDO-KASIKANA COLLECTION

$
0
0
Mbunifu wa Mavazi na Mitindo Kasikana Collection ameiomba Serikali kuipiga jeki tasinia hiyo kama tasinia nyingine zinavyothaminiwa, kwani hata hii nayo inaitangaza Nchi .

Palozi wa Palestina Atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
 Mkuu wa huduma za Sheria na Katibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maulid Kikondo akimwelezea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kutembelea ukarabati wa wodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam
  Baba wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua Hamis Daud akimwelezea Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli maendeleo ya mtoto wake baada ya kufanyiwa upasuaji huo alipofanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kutembelea wagonjwa wodini leo Jijini Dar es Salaam
 Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akielezea namna wagonjwa wa moyo wanavyofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na kupatiwa matibabu ya karibu katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa balozi wa Palestina nchini  Mhe. Hamdi Mansour AbuAli alipotembelea chumba cha ICU wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam 
 Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli akizungumza na menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ambavyo Palestina itashirikiana na taasisi hiyo katika masuala mbalimbali ya afya ya moyo baada ya kufanya ziara kuangalia huduma zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli baada ya kufanya ziara kuangalia huduma zinazotolewa na taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Pcha na: Genofeva Matemu - JKCI

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SOKO LA KALANGALALA

$
0
0
*Azitaka halmashauri zingine nchini ziige mfano wa Mji wa Geita
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaameweka jiwe la msingi mradi ujenzi wa soko kuu la  Kalangalala katika Mji wa Geita na kuzitaka halmashauri zingine nchini kuiga. Pia, amesema wajasiriamali waliokuwa wakifanya shughuli zao katika eneo hilo kabla ya  ujenzi watakuwa wa kwanza kupewa maeneo ya kufanyia biashara. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Novemba 28, 2018) baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa soko la Mji wa Geita.

Amesema ni vema halmashauri zote zikaiga mfano wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kujenga masoko ya kisasa ili wajasiriamali wapate maeneo ya kufanyia kazi zao. “Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaondolea wananchi kwa kuboresha na kuimarisha huduma za jamii.” Hivyo, Waziri Mkuu amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel kwa kuwa mbunifu na msimamiaji mzuri wa miradi ya maendeleo. Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji viongozi wa aina yake, ambao si wabadhilifu bali wanajali thamani na maslahi ya wananchi katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi  Gabriel ameahidi kulinda heshima ya wananchi wa mkoa huo kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Amesema atasimamia kikamilifu ujenzi wa miradi ya maendeleo, ukiwemo ujenzi wa soko la kisasa ambalo litakapokamilika wajasiriamali watafanyakazi muda wote hadi usiku. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Geita, Adolf Ritte amesema ujenzi wa mradi huo umegawanyika katika awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa soko lenye majengo makubwa mawili yenye thamani ya sh. bilioni 1.9. 

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wananchi watakaokuwa wanakwenda kununua bidhaa mbalimbali kwenye soko hilo. “Pia Halmashauri ya Mji nayo itanufaika kwa kuongezeka kwa mapato yake ya ndani. Ajira zitakazozalishwa sokoni hapo ni takribani 200. Faida nyingine ya mradi huu ni kumaliza mgogoro wa maeneo ya kufanyia biashara katika mji wetu.” Mapema leo Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Mji Geita kwenye eneo la Magogo na kisha alikwenda katika eneo la Bombambili kwa ajili ya kukagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi za CCM mkoa wa Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kiwanda cha Kuchenjua Dhahabu cha Nyamigogo wilayani Nyang'hwale Novemba 28, 2018. Wapili kulia ni mmiliki wa kiwanda hicho, Hussein Nassoro Amali ambaye pia ni Mbunge wa Nyang'hwale. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constatine Kanyasu, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. Watatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Saidi Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha Kuchenjua Dhahabu cha Nyamigogo wilayani Nyang'hwale Novemba 28, 2018. Kushoto kwake ni mmiliki wa kiwanda hicho, Hussein Nassoro Amali ambaye pia ni Mbunge wa Nyang'hwale.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo maalum la kuhifadhi na kusafisha Maji machafu wakati alipozindua Kiwanda cha Kuchenjua Dhahabu cha Nyamigogo wilayani Nyang'hwale Novemba 28, 2018. Wapili kushoto ni mmiliki wa kiwanda hicho, Hussein Nassoro Amali ambaye pia ni Mbunge wa Nyang'hwale. Kushoto ni Mke wa Mbunge huyo, Ashura Muhoja.

WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN

$
0
0


Na Asteria Muhozya, Chunya

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amewataka Maafisa Madini nchini kuhakikisha wanafanya kaguzi za mara kwa mara katika maeneo ya wachimbji wadogo ikiwemo kutoa elimu ya uchimbaji, masuala ya afya na usalama kazini ili kuongeza tija katika shughuli hizo.

Waziri Kairuki aliyasema hayo Novemba 27, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Chunya kinachojengwa na Mkandarasi kampuni ya SUMAJKT.

Alisema, wachimbaji wadogo wanatakiwa kulelelewa ili watoke katika uchimbaji mdogo wa madini kwenda uchimbaji wa Kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa, na kueleza kuwa, ili kufikia azma hiyo elimu ya mara kwa mara kwa wachimbaji ni muhimu ikatolewa kwani itawezesha serikali kupata mapato kutokana na kufuata uchimbaji sahihi.

Pia, aliwataka Maafisa hao kuhakikisha kuwa wanatatua migogoro katika maeneo yao kwani suala hilo litawezesha uzalishaji zaidi na kupelekea serikali kunufaika na shughuli hizo, ikiwemo ongezeko la ajira na ustawi wa jamii.

Vilevile, Waziri Kairuki alieleza kuwa, pamoja na kwamba katika Mwaka wa Fedha 2018/19 wizara yake imepangiwa kukusanya shilingi bilioni 310, lakini kama anataka makusanyo hayo yafikie shilingi bilioni 500 na kuongeza kwamba, Maafisa madini watapimwa kutokana na ukusanyo huo wa maduhuli.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia ramani ya jengo la Kituo cha Umahiri Chunya litakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake. Jengo hilo linajengwa na Mkandarasi SUMAJKT. 
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akisikiliza jambo kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Chunya. Wengine ni Wataalam kutoka Ofisi za Madini Mbeya na Chunya, wataalam kutoka Wizara ya Madini, na uongozi wa Wilaya ya Chunya. 
Sehemu ya jengo la Kituo cha Umahiri Chunya likiwa katika maendeleo ya ujenzi wake. 
Sehemu ya viongozi wa Wilaya, viongozi wa Ofisi za Madini Mbeya na Chunya pamoja na wadau wa madini wilayani humo wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki (hayupo pichani). 

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images