Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Taswira za Majengo mbalimbali ya Maktaba ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

0
0
 Majengo mbalimbali ya Maktaba ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambayo imefunguliwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Maktaba hio inauwezo wa kuchukuwa Wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja na uwezo wa kuhifadhi vitabu 800,000-PICHA NA IKULU






UJUMBE MKUBWA WA SEKTA BINAFASI ZA MAFUTA NCHINI UGANDA WAONYESHA NIA YA KUPITISHA BIDHAA BANDARI YA TANGA

0
0
UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda leo wametembelea Bandari ya Tanga huku wakionyesha nia yao ya kutumia Bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao kutokana na uwezo wa kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 30 mpaka 45 ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia shehena.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya ujumbe huo kutembelea Bandari ya Tanga ikiwemo maeneo yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.

Alisema kwamba lengo la ujumbe huo kutua mkoani Tanga ni kuangalia fursa eneo gani ambalo wanaweza kupitisha bidhaa zao kutoka nchini Uganda kwenda kwenye soko la nje kwa gharama nafuu zaidi na kupelekwa pia eneo ambalo litapokelea mafuta, Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga ya GBP na sehemu ambayo mafuta yanaposhushwa (Gati ya Meli za mafuta).

“Kwa kweli tunawashukuru TPA makao makuu na Serikali kutuletea ujumbe huu mkubwa wa sekta binafsi za mafuta za Uganda wakiwemo Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano ya Uganda jambo ambalo linatusaidia kutangaza fursa kubwa tulionayo Bandari yetu ya Tanga “Alisema.

Alisema msingi wake wa kutumia muda mfupi wakati wa upitishaji wa bidhaa msingi wake ni meli kwenye Bandari ya Tanga inakuja moja kwa moja inapata gati tofauti na maeneo mengine unalazimika kusubiri kwa kipindi cha wiki moja mpaka mbili ambapo kitaalamu wanasema dunia kwenye biashara za bandari na meli katika kila sh, mia moja mwenye meli anaingia gharama ya s h.65 akiwa bandarini.
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na Ujumbe Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na  kuvutiwa kuitumia Bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao kutokana na uwezo wa kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 30 mpaka 45 ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia shehena.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akisalimiana na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katika akiwa na baadhi ya wajumbe wakiwa eneo la  yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akitoa maelezo kwa  wajumbe hao wakati  wakiwa eneo la  yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

WAZIRI JENISTA AWAFUNDA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama amewapa somo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuwa mfano katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuwapa mwanga wananchi kuona mfano na kuiga na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowezesha kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.

Ameyasema hayo leo mkoani Arusha alipokuwa akizindua Kongamano la Mwaka liliwakutanisha Wataalam wa Maendeleo kutoka Wizara husika, Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri, Sekta Binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Waziri Jenista amesema kuwa katika maendeleo ya nchi yoyote Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni watu muhimu katika kuamsha ari ya wananchi katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla katika kulueta uchechembuzi katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.

Ameongeza kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi katika kuwawezesha wananchi kuchumi na kusema kuwa katika Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuna jumla ya mifuko.. inayotoa mikopo kwa waananchi ili kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara na kauanzisha viwanda vidogo vidogo katika maeneno yao na kuwataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuchukua mikopo hiyo na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuwa mfano kwa jamii.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akiangali moja ya vitabu vya Sera mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya kuzindua Kongamano la wataalam wa Maendeleo ya Jamii unaofanyika mkoani Arusha. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akiangali moja ya vitu mbalimbali inavyotengezwa na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya kuzindua Kongamano la wataalam wa Maendeleo ya Jamii unaofanyika mkoani Arusha. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka Taasisi za serikali Sekta Binafsi,  Mashirika yasiyo ya Kiserikali waliojumuika katika uzinduzi wa Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendela Mkoani Arusha. 
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea jinsia umuhimu wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii unavyoweza kuleta mabadiliko katika jamii wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendela Mkoani Arusha. 

GAVANA SHILATU ATAKA MRADI WA MAENDELEO USIOKAMILIKA VYEMA USIPOKELEWE

0
0

Na Mwandishi wetu, Mihambwe 

Gavana Mihambwe, Emmanuel Shilatu amesisitiza jukumu kubwa la viongozi wa Serikali ni kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi unafanyika kwa kuhakikisha miradi inayopokelewa ni ile iliyokamilika vyema. 

Gavana Shilatu aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mkoreha ili kujionea hatua iliyofikiwa. *Tarafa ya Mihambwe tunatekeleza, Viongozi wote wa Serikali tuna jukumu kubwa la kuhakikisha tunasimamia na kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kuhakikisha miradi ya kimaendeleo inayokabidhiwa ina ubora unaolingana na thamani ya pesa. Hivyo mradi wa maendeleo usiokamilika vyema usipokelewe.”* alisema Gavana Shilatu. 

Gavana Shilatu alisifu hatua iliyofikiwa ya mradi huo wa ujenzi na kusisitiza madarasa hayo yakamilike haraka ili yaanze kutumika mara moja. *”Napongeza hatua iliyofikiwa. Kuanza kutumika kwa madarasa haya yatakidhi mahitaji yaliyopo ambayo yameongezeka kutokana na fursa ya elimu bure na bora ambayo Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli inatoa. Hivyo Madarasa haya yakamilishwe vyema mara moja na yaanze kutumika mapema iwezekanavyo.”* alisisitiza Gavana Shilatu

Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini

0
0

Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya leo amefanya mazungumzo na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Sahabu Isah kuhusu mambo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar-es-salaam, Naibu Waziri Manyanaya na mgeni wake wamezungumza masuala mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo uwekezaji wa uliofanywa na kampuni ya kuzalisha saruji ya Dangote.

“Tumefurahi kumuona balozi amekuja kututembelea na kufuatilia masuala ya uwekezaji yanayohusu nchi yake”. Amesisitiza Mhe. Manyanya. Mhe. Manyanya ameeleza kuwa kupitia kikao hicho wameweza kubalishana uzoefu katika masuala ya maendeleo ya nchi zote mbili.

Mhe. Waziri amemuhakikishia balozi huyo wa Nigeria kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi ya Nigeria katika masuala ya Uwekezaji na pia wizara yake iko tayari muda wowote kumokea endapo atakutana na changamoto yeyote. Mbali ya kumhakikishia uhsirikiano, mheshimiwa Manyanya pia alitoa shukran za serikali kwa uwekezaji uliofanywa na nchi ya Nigeria “sisi tunafurahi kumuona Dangote amewekeza, na tungependa uwekezaji wake uendelee ili watanzania waendelee kufaidika na uwekezaji huo”, aliongeza mhandisi Manyanya.

Kwa upande wake Mhe. Sahabu amehaidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina na nchi hizo mbili na amefurahishwa na hatua za serikali za kutatua changamoto za wafanyabiashara mbalimbali kutoka Nigeria waliowekeza nchini.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya kwenye kikao na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Sahabu Isah alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar-es-salaam. Mhandisi Manyanya na mgeni wake wamezungumza mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Kushoto (suti ya blu) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph Bchweishaija. 
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Stella Manyanya, kwenye picha ya pamoja na balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Sahabu Isah baada ya kumaliza mazungumzo yaliohusu uwekezaji wa nchi ya Nigeria nchini. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph Bchweishaija. 

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA WILAYA YA GEITA YA NZERA

0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Geita ya Nzera, Novemba 27, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara . Watatu kulia ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Mbunge wa Geita Vijijini, Jioseph Msukuma wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, Novemba 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzera wilayani Geita, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 28,2018

PROFESA MBARAWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MUKABUYE

0
0
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ameiagiza Kampuni ya KGG Investment Ltd & Tanafri Group Ltd inayojenga Mradi wa Maji wa Mukabuye kuhakikisha inakamilisha mradi huo ifikapo mwezi Disemba, 2018 ili wakazi wa Mukabuye na vijiji jirani wapate huduma ya majisafi na salama. 

Profesa Mbarawa ametoa maagizo hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mukabuye kwenye ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma. “Mradi wa Maji wa Mukabuye umeanza kutekelezwa Juni, 2018 na unategemewa kukamilika mwezi Aprili, 2019 kulingana na mkataba. Lakini mimi nataka mkandarasi akamilishe mradi huu mwishoni mwa mwaka huu ili wananchi hawa wapate maji haraka iwezekanavyo’’, amesema Profesa Mbarawa. 

“Hakuna sababu ya kusubiri mpaka mwakani mradi huu ukamilike, kama fedha zipo na tutamlipa mkandarasi kiasi kilichobaki. Sina mashaka na uwezo wa mkandarasi kwa sababu uwezo anao, kikubwa ni kuongeza bidii na kasi ya utekelezaji’’, aliongeza Profesa Mbarawa. Akisisitiza ziara yake imelenga kubaini na kutatua changamoto zote za miradi ya maji katika Wilaya ya Kibondo kwa kuwa Serikali imelenga kuwa karibu na wananchi na kutatua kero zao kwa wakati. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Paul Bura (kushoto) mara baada ya ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Mukabuye, wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye kisima cha IOM kilichopo eneo la Kumwayi kinachotumiwa na Mradi wa Maji wa Kibondo Mjini, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Mabamba/Mukurazi uliopo Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akizungumza na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo katika ofisi za wilaya, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akijibu maswali ya wakazi wa Kijiji cha Mukabuye kabla ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Mukabuye, wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma. 


GAVANA LUOGA ATOA PONGEZI MAALUM KWA WAFANYAKAZI BOT KUANDAA MIFUMO YA KUKUSANYA MALIPO YA SERIKALI

0
0

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, amewapongeza wafanyakazi nane wa Benki Kuu upande wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa mchango na uzalendo wa hali ya juu uliowezesha kusimikwa kwa mifumo ya kielektroniki ya kulipa mishahara na kukusanyia mapato ya serikali nchini.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi hao kwa kushirikiana na wataalam kutoka taasisi zingine za serikali katika kubuni, kutengeneza na kusimika mifumo ya kukusanya malipo ya serikali kielektroniki ya GePG na kulipa mishahara kupitia Benki Kuu ya Tanzania (GSPP) kati ya mwaka 2015 na 2018.

“Siku zote, Benki Kuu imekuwa ikihamasisha wafanyakazi wake kujituma katika kazi kwa weledi na ubunifu wa hali ya juu ili kuongeza tija na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea. Katika hili, tunawapongeza kwa kuwa mmetekeleza kwa vitendo falsafa hii kutokana na utendaji wenu uliotukuka. Hongereni sana!,” amesema Prof. Luoga.

Gavana Luoga alisema kwa kutumia wataalam wa ndani kusimika mifumo hiyo, sio tu kumeiwezesha serikali kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato, bali pia kumeliwezesha taifa kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kununua mifumo kama hiyo kutoka nje ya nchi.

Kushoto: Gavana wa BoT Prof. Florens Luoga akimpongeza Bi. Mota Cecilia Mlama kwa kazi nzuri. Kulia Prof. Luoga (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa BoT walioshirikiana na wataalam kutoka taasisi zingine za serikali kutengeneza mifumo ya kulipa watumishi wa umma mishahara kupitia Benki Kuu na kukusanya malipo ya serikali kielektroniki. Waliokaa wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Kened Nyoni na kulia ni Bi. Flora Mwaigomole, Meneja wa Rasilimali Watu. 

POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA

0
0

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola maesema licha ya kuwa Jeshi la Polisi linapambana usiku na mchana kuwaondoa askari wala rushwa lakini ana taarifa ya baadhi yao wanaendeleza tabia hiyo, hivyo dawa yao ipo jikoni inachemka.

Amesema licha ya kutoa taarifa mara kwa mara kuwataka askari hao kufanya kazi kiuhadilifu kwa kuacha tabia ya kuomba rushwa lakini baadhi ya askari hao hawajamuelewa hivyo atapambana nao mpaka Jeshi hilo litakapokuwa safi.

Lugola amesema anapokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi kuwalalamikia baadhi ya Polisi kufanya matukio hayo ambayo hayakubaliki lakini anawataka askari polisi hao wajue kuwa kati ya maagizo aliyopewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kupambana na rushwa ndani ya Wizara hiyo, hivyo hawezi kumuangusha hata siku moja.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Namibu, Kata ya Neruma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola alisema baadhi ya polisi wanalichafua Jeshi hilo kutokana na tamaa zao, hivyo ameendelea kusisitiza kuwa, Serikali ya Magufuli ya awamu ya tano siyo ya kuchezewa.

“Jeshi la Polisi linalinda usalama wa raia na mali zao, linapambana na rushwa katika mambo mbalimbali yakiwemo ya ardhi hapa kijijini, hivyo ndugu wananchi mnapopata migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi na mengineyo akikisheni mnatoa taarifa polisi ili muweze kusaidiwa,” alisema Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akifurahi jambo wakati alipokua anasalimana na Diwani wa Kata ya Nyamihyolo, Mgendi Patrick, wakati Waziri huyo alipopokelewa na mabango na wananchi wa Kijiji cha Mahyolo, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambayo yalikua yana ujumbe mbalimbali. Lugola aliwataka wananchi wa Kijiji hicho wafanye shughuli za maendeleo bila kuvunja sheria za nchi. Pia alitoa onyo kwa baadhi ya askari kuiacha tabia hiyo haraka iwezekanavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahyolo, Clifford Bwire, alipokua anajibu maswali kuhusu ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Mahyolo iliyopo Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, kutokuendelea licha ya kua wananchi wa kijiji hicho walichanga fedha. Pia Lugola aliwataka wananchi wa Kijiji hicho wafanye shughuli za maendeleo bila kuvunja sheria za nchi. Pia alitoa onyo kwa baadhi ya askari ambao wanaomba rushwa kwa wananchi kuiacha tabia hiyo haraka iwezekanavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano iliyopo Kijiji cha Namibu, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Bunda, Mkoani Mara, wakati Waziri huyo alipofanya ziara shuleni hapo kwa ajili ya kuwasalimia wanafunzi hao pamoja na uongozi wa shule hiyo. Lugola yupo katika ziara ya kuhamasisha maendeleo na pia kuwapa elimu ya ulinzi na usalama jimboni kwake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI

0
0
Na Asteria Muhozya, Songea 

Serikali imesema haijaruhusu uchimbaji wa Madini katika Mto Muhuwesi na kwamba tayari Wizara ya Madini ilikwishakutoa maelekezo yapatayo matano ambayo wahusika wanatakiwa kuyafanyia kazi ili itoe maamuzi. 

Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea, wakati akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ambaye alimwomba Waziri asimamishe uchimbaji huo na kwamba tayari Mkoa umezuia shughuli hizo kuendelea kwa kuwa ndiyo chanzo cha maji mkoani humo na kwamba, alifanya hivyo ili kulinda miundombinu ya barabara. 

Waziri Kairuki alimweleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa, wizara ilitoa maelekezo kwa wahusika kwamba wanatakiwa kuwasilisha barua ya ridhaa ya Waziri wa Maji, ridhaa ya Wakala wa Barabara nchini (TANROAD), ridhaa ya Bodi ya Bonde la Mto Ruvuma/Pwani na Kusini ili wizara ijiridhishe kabla ya kutoa maamuzi. 

“ Tunataka tujiridhishe na approval kutoka katika maeneo hayo na vikipatikana vyote, nitafanya uamuzi. Kwa sasa ipo ridhaa ya bodi ya bonde la mto Ruvuma,” alisisitiza Waziri Kairuki 

Pia, akifafanua kuhusu kusimama kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya Uranium unaofanywa na Kampuni ya Mantra Tanzania Limited, waziri Kairuki alisema kuwa, kampuni hiyo iliomba kusisitisha shughuli zake kwa kipindi cha miaka mitano kutokana na bei ya madini hayo kushuka katika soko la dunia na kwamba , suala hilo bado linafanyiwa kazi kitaalam na kiuchumi hivyo, bado serikali haijatoa majibu kuhusu suala husika. 
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) na Mkuu wa MKoa wa Ruvuma Christina Mdeme (kulia ) wakichanganya kokoto katika Kituo ch Umahiri Songea wakati wa ziara Kairuki kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
Sehemu ya jengo la Kituo cha Umahiri Songea katika hatua zake za ujenzi
Afisa Madini Mkazi wa Songea Abraham Nkya akieleza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Angellah Kairuki alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Waziri wa Madini ANgellah Kairuki akiteta jambo na AFisa Madini Mkazi Mkoa wa Ruvuma Abraham Nkya wakati wa ziara ya Waziri Kairuki kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea. Wa Pili Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mdema , Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Madini Gladness Mkambaita na wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini, Andrew Eriyo. 


ZAIDI YA WANANCHI 500 BUTIAMA WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA YA KINYWA CHA MENO.

0
0
Na Frankius Cleophace Mara.

Zaidi ya wananchi wanao kadiliwa kufikia miatano wamejitokeza kupata huduma ya kinywa na meno katika wilaya ya Butiama mkoani Mara kupitia huduma ya Madkatari Bingwa wa Afya ya Kinywa na meno.

Imelezwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wemekuwa Wakiungua ugonjwa wa kinywa na meno jambo ambalo linahatarisha maisha yao ambapo pia Tatizo Sugu la fizi hupelekea kutokea kwa Magonjwa mengine ikiwemo Magonjwa ya moyo na sukari.

Hayo yamebainishwa na Rais wa chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania Daktari Ambege Jack Mwakatobe wakati wa utoaji huduma hiyo kwa wananchi wa Wilaya ya Butiama ,Mwitongo mkoani Mara

Daktari Mwakatobe amesema kuwa uwepo watatizo hilo ndio chanzo kikubwa cha kupelekea kutoa huduma hiyo ambapo waliamua kufanyia wilayani Butiama ikiwa lengo nikumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na uwepo wa changamoto ya ukosefu wa watalamu wa Tatizo hilo katika hospitali za wilalaya.

“Tulishwahi kuja awali tukagundua kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa kutoa hudma ya matatizo ya Fizi ndio maana tumeamua kuja kutoa huduma hii ambapo novemba 28 tunamkutano wetu wa madaktari Bingwa.” Alisema Mwakatobe.
Mkuu wa wilaya ya Butiama Anarose Nyamubi akiongea na baadhi ya waginjwa wa maeneo katika eneo la madaktari bingwa wa Kinywa na meno wanapotoa huduma.
Madaktari bingwa wa kinywa na Meno wakiendelea na matibabu ikiwemo kungoa Meno katika eneo la Mwitongo Wilayani Butiama Mkoani Mara.
Baadhi ya wananchi wakipatiwa elimu jinsia ya kutunza vinywa na Meno.
Wanafunzi wa Sekondari wa Sekondari wakipatiwa elimu ya kutunza Kinywa na Meno.

VIONGOZI WAANDAMIZI WA JUMUIYA ZA CCM WASHIRIKI MKUTANO NCHINI NAMIBIA

0
0
 Katibu Mkuu UWT Queen Mlozi akiwasilisha mada kwenye moja ya mkutano wa siku tatu uliofanyika hivi karibuni  Nchini Namibia
Nikiwa na picha ya pamja na Makatibu Wakuu wa Jumuia za Chama Cha Mapinduzi Ndg. Erasto Sima( Wazazi) na Ndg. Raymond Mwangwala (UVCCM) kabla ya kuanza kushiriki mkutano huo hivi karibuni nchini Namibia.

WAKUU WA MIKOA, WILAYA NA WAKURUGENZI SIMAMIENI UWAJIBIKAJI-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wahakikishe wanasimamia vizuri uwajibikaji na utowaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo yao bila ya woga. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amemtaka kila mtumishi wa umma nchini awajibike katika kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi, wabadhilifu, wavivu na haitosita kuwachukulia hatua.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza na watumishi, viongozi wa mkoa, wilaya ya Geita na taasisi za umma katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mji Geita.“Watumishi fanyeni kazi kwa bidii na msitarajie kuundiwa tume pale mnapofanya vibaya, ukiharibu kazi tunakushughulikia hapo hapo na huu ndio msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.”

Waziri Mkuu aliwaeleza watumishi hao kuwa wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi na pia watambue dhamana kubwa waliyonayo, ambayo ni kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza watumishi wa umma hususani Wakuu wa Idara wahakikishe wanakuwa na kitabu cha Ilani ya Uchanguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili wapate muelekeo wa utekelezaji washughuli zao.

Waziri Mkuu amesema kitabu cha Ilani ya uchanguzi cha CCM 2015/2020 kina maelekezo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kila idara inatakiwa kuangalia maelekezo yaliyotolewa kuhusu idara husika na kuyafanyia kazi.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba yeye kwa kushirikiana na viongozi wenzake watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo ameyatoa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. Kulia ni Mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MZAZI AFURAHI KUUAWA KWA MWANAE.

0
0

JOSEPH MPANGALA,MTWARA.

Mwanamke Mmoja aliyejulikana kwa Jina la Ndilikuli Matupa Mkazi wa kijiji cha Mkangaula Kata ya Namalenga wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara ameshukuru wananchii wenye hasira Kali kwa Kumchoma Moto Kijana wake Abdallah Hussein Mahona kwa Tuhuma za Kuhusika na matukio Kadhaa ya Ukabaji,Unyang'anyi na Mauaji.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 12 asubuh mwanzoni mwa wiki hii ambapo marehemu alihusishwa na kuwajeruhi watu wawili ndipo wananchi wenye hasira wakamtafuta na kumchoma moto mpaka kifo chake.

Akiongea katika eneo la Tukio ambalo Marehem Abdallah Hussein amechomwa mama yake Mzazi Bi Ndilikuli Matupa anasema alilazimika kulala nyumba za stareh {Disco}ili kuepuka kuuawa na Mwanae ambapo mara kadhaa amekuwa akimtishia Kumuua.

“Sina Masikitiko yoyoyote Mzazi Mimi,Nimepona kwa chukuchuku kila siku Mwenye disko mtu mkubwa kama Mimi nilikuwa nawaacha wajukuu wangu Mmoja wa Marehem Mmoja wa kaka yake mimi nakwenda kwenye disco ilihali mimi sio mtu wa disco yaan kukimbia Kifo”alisema Bi Ndilikuli Matupa ambaye ni Mama wa marehem.

Hata Hivyo Bi Ndilikuli ameongeza kuwa sio mara ya kwanza kwa Marehem mwanae Kumtishia kumuua kwa kumtuhumu kuwa ni Mchawi kutokana na Mtoto wa Marehemu Kuumwa kwa kipindi cha Muda Mfupi.

“Kwanza kifo Cha kwanza kabisa nilitaka kuuwawa kutokana na Mtoto wake Yupo hapa Mohamed Kuumwa tu Mudy nikataka kuuwawa nikasema huyu anaumwa tu sio kwa kumroga mimi nimroge mimi kwa sababu gani”Alisema Mama wa Mzazi wa Marehem.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mkangaula kata ya Namalenga tarafa ya Lulindi wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamekusanyika kutazama mwili wa marehem Abdallah Hussein Mahona aliyechomwa Moto kwa Tuhuma za Ukabaji na Unyang’anyi.
Mabaki ya mwili wa marehem Abdallah Hussein mahona ambaye ameuwawa kwa kuchomwa moto na wananchii wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuwa kibaka ambapo wananchii wa kijiji hicho walikusanyika kwa ajili ya Kuutazama.


MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAPOKEA MAJALADA NANE YA GUGAI YENYE MAJINA TOFAUTI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imeelezwa kuwa aliyekuwa mhasibu wa Takukuru Godfrey Gugai anayekabiliwa na mashtaka ya kumiliki Mali zisizolingana na kipato chake pamoja na wenzake watatu, anamiliki hati nane za umiliki wa ardhi zikiwa na majina mawili tofauti.

Hayo yameelezwa jana Novemba 27, 2018 na Afisa msajili msaidizi wa hati  wa Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Joanitha Kazinja ambaye ni shahidi wanne wa upande wa mashtaka wakati Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.  Shahidi huyo ambaye kazi yake ni kusajili hati na miamala mingine  inayofanyika chini ya kifungu 334 cha Wizara ya ardhi amesema, miamala inayofanyika ni pamoja na rehani na kubadilisha hati ya umiliki wa ardhi pamoja na kutunza kumbukumbu na kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya masuala ya ardhi.

Akiongozwa na wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU Awam Mbangwa, shahidi Kazinja amesema Gugai ndiye mmiliki wa kwanza wa ardhi kutoka Oktoba, Mosi 2004 na hiyo ni pamoja na kiwanja namba 225 kitalu namba 6 kilichopo Jkt Mbweni Manispaa ya Kinondoni na alipata hati yake kwenye ofisi ya msajili 19 Mei, 2009. Shahidi ameeleza kuwa amemtambua Gugai kuwa mmiliki wa ardhi hizo kutokana na Gugai kukiri na kuweka saini katika maelezo katika hati hiyo ya umiliki.

Majina ya umiliki katika hati hizo  yanaonesha kuwa takribani hati 6 zinaonesha umiliki wa Godfrey John Gugai na hati mbili za umiliki wa ardhi zikionesha jina la John Baptist Gugai. Kufuatia maelezo hayo, Shahidi Kazinja aliomba mahakama kutoa  majalada 8 ya umiliki wa ardhi ya mshtakiwa  Gugai kama sehemu ya kielelezo katika kesi hiyo, ambapo mahakama ilipokea majalada hayo nane.

Akijibu maswali yalioulizwa na wakili Seni Malimi kuhusiana na majina tofauti yaliyopo kwenye hati ambayo ni Godfrey John Gugai na John Bapstist Gugai shahidi Joanitha Kazinja amesema kuwa hawafahamu tofauti iliyopo ila amesoma majina hayo kutokana na kumbukumbu zilizopo. Hakimu Simba amehairisha kesi hiyo hadi kesho saa tano asubuhi.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine ni, George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera ambao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai. Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.
Mhasibu wa Takukuru Godfrey Gugai anayekabiliwa na mashtaka ya kumiliki Mali zisizolingana na kipato chake pamoja na wenzake watatu, anamiliki hati nane za umiliki wa ardhi zikiwa na majina mawili tofauti kiwa anatoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

KATIBU MKUU NYAMHANGA AKAGUA DARAJA LA KAVUUU

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, amekagua daraja la kavuu lililokamilika kujengwa katika barabara ya Majimoto-Inyonga yenye urefu wa KM 130.

Katibu Mkuu  amesema kuwa lengo la ujenzi  wa daraja hilo ni kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji kwa mkoa wa Katavi. Daraja hilo lenye urefu wa mita 85.344 limegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 kwa gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 2.718

Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa kwa sasa daraja hilo limeanza kutumika kwa magari yasiozidi tani 30 na hivyo kufanya  kupunguza urefu wa KM 135 endapo mwanachi hatapitia Mpanda. "Nimeridhishwa kwa kukamilika kwa daraja hili kwani ilikuwa ni kero kwa wananchi wa wilaya hizi kuzunguka umbali mrefu na gharama za usafiri kupanda", amesema Mhandisi Nyamhanga.

Aidha, amewataka Wakala wa Barabara (TANROADS) kuendelea kuifanyia matengenezo barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe ambacho itarahisisha kupitika kwa wakati wote. Naye Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, amemueleza Katibu huyo kuwa kazi za uwekaji wa kitanda  cha chuma katika daraja hilo ulifanywa pamoja na wahandisi wa ndani ikiwa ni lengo la kuongeza uwezo na uelewa katika ujenzi wa madaraja yanayotumika hasa nyakati za  dharura.

Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Nyamhanga, yupo katika ziara ya kikazi mkoani Katavi  ikiwa ni lengo la kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na sekta yake hususani barabara, madaraja na kiwanja cha ndege.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga,  akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, kuhusu kuifanyia matengenezo barabara ya Majimoto-Inyonga yenye urefu wa KM 130 kwa kiwango cha changarawe, mkoani humo.
 Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), kuhusu ukamilikaji wa Daraja la Kavuu linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani humo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoka kukagua kingo za Daraja la Kavuu linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani Katavi. Daraja hilo limekamilika na limeanza kutumika kwa magari yasiozidi tani 30.
Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa mita 85.344linalounganisha Wilaya ya Mlele na Mpwimbwe mkoani Katavi. Daraja hilo limegharimu kiasi cha shilingi  bilioni 2.718.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI WA GEITA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita  kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. Kulia ni Mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,  Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA

0
0
Na WAMJW- Muheza, Tanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kwa kufanya tafiti nzuri zinazoisaidia serikali katika mabadiliko ya sera ya afya kwenye matibabu ya ugonjwa wa Malaria

Dkt. Ndugulile amtoa pongezi mara baada ya kutembelea katika kituo cha tafiti cha ya ugonjwa wa Malaria Nirmi kilichopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.  “Serikali tunajivunia kuwa na taasisi hii, katika udhibiti wa ugonjwa wa Malaria tumepiga hatua kubwa, tumepunguza maambukizi ya Malaria kwa zaidi ya asilimia 50, tulikuwa na asilimia 14 sasa hivi tuna asilimia 7. Kwa juhudi ambazo tunaenda nazo katika tafiti hizi naamini kiwango cha maambukizi kitaendelea kushuka.” Alisema Dkt Ndugulile.

Licha ya kunufaika na tafiti hizo, Serikali imejiwekea malengo ya kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria nchini, Dkt Ndugulile amesema kuwa Serikali imejiwekea mikakati mbalimbali ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria kwa kutoa vyandarua, dawa za kuuwa vimelea vya Malaria, kila mgonjwa kupimwa ugonjwa wa Malaria pamoja na kunyunyizia dawa katika makazi ili kuuwa mazalia ya mbu. Aidha Dkt. Ndugulile ameipongeza taasisi hiyo ya Nimr kwa kutambulika na mashirika ya kimataifa kutokana na tafiti inazozifanya kuwa na ubora wa hali ya juu. “Niwapongeze kwa tafiti zetu kutambulika kimataifa, siyo tuu kwa kutusaidia katika mabadiliko ya sera bali pia 

“Tafiti zetu zinatambulika kimataifa, hivi sasa kituo hiki kinatambulika na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutokana na tafiti mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa Malaria, kwa hiyo nawapongeza wote kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya” alisema Dkt Ndugulile.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia sampuli za mbu katika maabara ya Taasisi ya Nimr Muheza, Tanga.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo (kushoto)  alipotembelea kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu Nirmr.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia vifaa vya zamani vilivyotumika kufanya tafiti katika kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu Nirmr Amani Muheza.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia lililokuwa jengo la posta ya zamani kabla ya uhuru ambalo lipo katika ofisi za Nimri Amani, Muheza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisoma kitabu cha tafiti za zamani katika kituo cha tafiti Nimr Amani, Muheza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA PALESTINA PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuonyesha viungo vya chai kutoka Zanzibar Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) wakati wa kumkabidhi kama zawadi, Mheshimiwa Balozi wa Japan alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Rais)
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images