Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live

MAGEUZI YA KILIMO YANAHITAJI USHIRIKIANO WA WADAU WOTE-HASUNGA

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Mageuzi ya kilimo nchini Tanzania yanapaswa kutiliwa mkazo na wadau wote wa sekta ya kilimo wakiwemo wananchi, wadau wa maendeleo na serikali kwa ujumla.

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 23 Novemba 2018 wakati akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro.

Mhe Hasunga alisema kuwa Sekta ya kilimo imeendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania kwani imekuwa ikichangia kwa Kiasi kikubwa katika kutoa ajira, kuchangia karibu nusu ya mauzo yote ya nje na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta fedha za kigeni.

Alisema kuwa Serikali imeendelea kuweka juhudi zake katika kuwezesha sekta ya kilimo kwa kufanya mabadiliko mbalimbali ya kisera yenye lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa sekta ya kilimo kukua.Pia serikali imezindua Mpango wa pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II) wenye lengo la kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa na inachangia katika maendeleo ya uchumi na kuongeza kipato cha mkulima mdogo.


Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Ndg Geofrey Kirenga akieleza mwelekeo wa jinsi SAGCOT itakavyoendesha shughuli zake wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018. 


Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.



NEWZ ALERT: KINONDONI YATAJA SABABU KUZUIA FIESTA VIWANJA VYA LEADERS, CLOUDS MEDIA WATOA YA MOYONI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imefuta kibali cha kufanyika kwa tamasha la Tigo Fiesta ambalo lilitarajiwa kufanyika leo Viwanja vya Leaders.

Sababu za kufuta kibali cha kufanyika tamasha hilo kwenye viwanja hivyo imetokana na Ofisi ya Ofisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo ya Kinondoni kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na wagonjwa waliolazwa hospitalini kutokana na matangazo yaliyoambatana na muziki unaopigwa kwa sauti kubwa.

Barua ya Ofisa Utamaduni wa Halmashauri ya Kinondoni ambayo nakala yake imekwenda kwa Mkurugenzi wa Clouds Media imeeleza kuwa kutokana na malalamiko hayo amefuta kibali kilichotolewa Novemba 22 mwaka huu cha kufanyika kwa Fiesta uwanja wa Leaders na kuihamishia uwanjwa Tanganyika Peakers-Kawe.

Baada ya barua hiyo , uongozi wa Kamati ya maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 umesema kwa masikitiko makubwa wanatangaza kusitisha tukio la kilele cha msimu wa Tigo Fiesta lililopaswa kufanyika leo Novemba 24 mwaka 2018 katika viwanja vya Leaders na kwamba sababu zilizotolewa kusitishwa kwa tamasha hilo zipo nje ya uwezo wao.

"Tunaomba radhi kwa madhara yoyote yatakayosababishwa na hili.Tunaambua fika wapenzi wa Tigo Fiesta Dar es Salaam na nje ya Dar waishajiandaa vema na tukio hili na zaidi walishanunua tiketi.Kwa walionunua tiketi kwenye Tigo pesa watarudishiwa fedha zao na wale ambao walinunua vituo vya mauzo wafike kwenye vituo hivyo watarudishiwa fedha zao.

"Mioyo yetu imejawa na shukrani,sisi Clouds Media Group ,Prime Time Promotions,Tigo Tanzania,TBL, na Tatu Mzuka tutazidi kuwashukuru Watanzania wote kwa kutuchagua na ahadi yetu ni kuendelea kuwatumikia.Pia tunatoa shukrani kwa Serikali na wadau wote ambao wamejitoa kwa hali na mali kufanikisha shughuli zote za Tigo Fiesta tangu kuanza kwa msimu hadi sasa,"umesema uongozi huo kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari.
 Taarifa kutoka  Afisa Utamaduni Manispaa ya Kinondoni
 Taarifa kutoka kwa Waandaji wa Tamasha la Fiesta.

Miaka 3 ya JPM Imechagiza Mageuzi Katika Sekta ya Anga

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum katika kipindi cha MORNING TALK cha Ebony Fm Mkoani Iringa kuhusu Utekelezaji wa Serikali katika Kipindi cha Miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli[/caption] Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ndani ya miaka mitatu imeweza kuleta ukombozi katika sekta ya anga kwa lengo la kuchagiza mageuzi katika sekta hiyo.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa kipindi cha Morning Talk cha redio Ebony Fm Mjini Iringa.Dkt. Abbasi amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli amekuwa akitekeleza yale yote aliyoyaahidi ambapo mpaka sasa anaendelea kutekeleza aliyoyaahidi katika sekta ya anga.


"Mpaka sasa nchi yetu inandege tatu aina ya Bombadia na Dreamliner moja na pia mwezi Desemba tunaleta AIRBUS mbili ili kuendeleza na kuchagiza mageuzi katika sekta ya Anga" amefafanua Dkt. Abbasi.Aidha, Dkt. Abbasi anaongeza kuwa "Leo hii Shirika letu la ndege limeongeza idadi ya abiria wanaotumia usafiri huo kwa mwezi kutoka 4000 hadi kufikia 36000".

Akizungumzia kuhusu Ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea, Dkt Abbasi amesema kuwa, kufikia mwaka 2019 Desemba kipande cha reli cha kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kitakuwa kimekamilika na treni ya kwanza ya umeme itatoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.Vile vile Dkt. Abbasi amebainisha kuwa Serikali imeanzisha mfumo wa kuleta mbolea na baadhi ya pembejeo kwa pamoja ili kuweza kusaidia kupunguza gharama na kusaidia maendeleo katika sekta ya kilimo.

"Wakulima waendelee kufanya kazi katika maeneo yako kwani Serikali inafanyia kazi changamoto zote ikiwamo ya masoko kwa lengo la kusaidia maendeleo katika sekta hiyo muhimu kwa Watanzania" ameongeza Dkt. Abbasi.

Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesema kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua kubwa ya kujenga nchi kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mbali mbali mikubwa ya maendeleo ikiwemo Mradi wa Kamuzalisha Umeme wa Stieglers.

WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewasimamisha kazi watumishi watatu wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya Jiji la Arusha kwa tuhuma ya kushirikiana na matapeli wa viwanja katika jiji hilo.

Aidha, Lukuvi ameagiza maofisa hao waliosimamishwa kazi kutokanyaga katika eneo la ofisi za Jiji mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika na maamuzi dhidi ya tuhuma zao yatakapotolewa.

Lukuvi alichukua uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Jiji la Arusha jana kufuatia kuwepo tuhuma nyingi za matapeli ya viwanja kushirikiana na baadhi ya maofisa wa ardhi wasiokuwa waaminifu kufanya utapeli kwa wamiliki halali wa viwanja.Maafisa ardhi waliosimamishwa kwa tuhuma hizo za kushirikiana na matapeli kudhulumu viwanja kwa wamiliki halali katika jiji la Arusha ni Elizabeth Mollel, Lassen Mjema na Zawadi Mtafikikolo.

Mbali na kusimamishwa kazi kwa watumishi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza maafisa Ardhi wa Jiji la Arusha kuhakikisha matapeli wote wa viwanja wanaoshirikiana na watumishi hao wasipatiwe huduma katika masuala yoyote ya ardhi kufuatia kuonekana kujihusisha na mipango ya utapeli wa viwanja kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha.

Katika ziara yake hiyo ya kushtukiza pamoja na kuelezwa na Afisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato uwepo wa watumishi wawili Lassen na Zawadi huku Elizabeth akiwa katika likizo ya uzazi, watumishi hao walipotea ghafla ofisini bila taarifa mara baada ya kuelezwa wanahitajika kwa waziri na hata pale walipopigiwa simu za mkononi hazikupatikana.

Kwa mujibu wa Lukuvi, watumishi hao wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na matapeli wa viwanja katika jiji hilo jambo linalotia mashaka utendaji wao wa kazi na kubainisha kuwa maafisa hao wamekuwa na tabia ya kufuatilia kesi zilizopo katika Mabaraza ya Ardhi kwa nia ya kuwasaidia matapeli.

SPIKA JOB NDUGAI AWEKA HADHARANI KILA KITU KUHUSU RAIS DK.MAGUFULI

$
0
0
*Ammwagia sifa kutokana na utendaji wa kutukuka
*Asema anaandika historia kuwa Rais mjenga nchi
*Ahoji Watanzania wanataka nini tena zaidi ya ....

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKATI Watanzania wa kada mbalimbali wakitoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli ambaye ametimiza miaka mitatu kwenye nafasi hiyo, Spika wa Bunge Job Ndugai ameamua
kuweka wazi kila kitu kuhusu Rais wetu.

Spika Ndugai amesisitiza utendaji kazi wa Rais Dk.Magufuli pamoja na timu yake yote ya Serikali ya Awamu ya Tano ni wa mfano usiopatikana kirahisi katika Bara la Afrika.Akizungumza na Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni ofisini kwake Mjini Dodoma,Spika Ndugai amesema Rais Magufuli pamoja na mambo mengi ambayo ameyafanya na kuleta heshima kwa nchi yetu ukweli ni kwamba uzalendo wake ni mkubwa na wa hali ya juu.

"Uzalendo mkubwa na wa hali ya juu ameounesha kama kiongozi wa nchi.Tuliwahi kupata ahadi na awamu zilizopita na hasa kutokana na zuluma iliyokuwa inafanyika kwenye madini ,lakini Rais wetu Dk.Magufuli yeye aliahidi kupitiwa upya kwa mikakata ya madini na kweli yote imefumuliwa na imeshonwa upya."Na hili eneo la madini lilikuwa eneo gumu ambalo haligusiki lakini yeye ameweza.Ameonesha uzalendo wa hali ya juu katika kuhakikisha rasilimali za nchi yetu zinanufaisha Watanzania wote,"amesema Spika

Ndugai wakati anazungumzia utendaji kazi wa Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu.Pia jambo moja ambalo Watanzania walikuwa wakililia sana kabla ya uchaguzi mkuu ambao umemuweka madarakani Rais Magufuli ni ilikuwa kupata kiongozi mwenye maamuzi."Tumepata Rais mwenye maamuzi, aidha unapenda au hupendi hiyo shauri yako lakini yeye ameshaamua.

"Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maamuzi.Ni kiongozi anayeamua kwa wakati na tunakumbuka huko nyuma kuna mambo yalikuwa yamenyooka na yanahitaji maamuzi kwa ngazi mbalimbali lakini hayakutolewa maamuzi.Sasa hilo limebaki historia,"amesema.Spika Ndugai amefafanua zaidi kuwa Rais Magufuli anapambana rushwa na ufisadi moja kwa moja."Katika hilo tunashuhudia hata baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) wakibadilishwa kwa kushindwa kwenda na kasi yake kulingana na taarifa alizonazo,"amesema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MICHUZI TV:Tamasha la Mziki Mnene E-fm lawatoa watu Njee/Ndani,Balaa.

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

$
0
0


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili wakala hiyo ianze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Akikabidhi kiwanja hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Musa Joseph amesema ujenzi wa Ofisi hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma.

Bw. Joseph amefafanua kuwa, kiwanja kilichokabidhiwa kina ukubwa wa ekari 5.7 na kuwataka TBA kuanza ujenzi mara moja ili kuwawezesha watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwahudumia wananchi wakiwa katika mji wa Serikali.

Bw. Joseph ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari imeshaingiza fedha kwenye Akaunti ya Wakala wa Majengo Tanzania kiasi cha shilingi 700, 000,000/=  ili kuiwezesha TBA kuanza ujenzi na kuongeza kuwa nia ya kufanya malipo mapema ni kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.

Akipokea kiwanja hicho, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania mkoani Dodoma, Mhandisi David H. Shunu ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini TBA na kuahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati na kwa kiwango bora. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akiwasisitiza Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha ujenzi wa ofisi kwa wakati katika Mji wa Serikali ili iweze kutumika kuwahudumia wananchi.
002
Afisa Ugavi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Deograsius Michael (kulia) akikabidhi hati ya makabidhiano ya kiwanja kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, Mhandisi David H. Shunu (kushoto) kwa lengo la kuanza ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali. Anayeshuhudia ni Afisa Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Benard Makanda.
003
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph (wa pili kushoto) akizungumza na Wataalam  wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kukabidhi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kutumia vifaa vilivyopo katika karakana zake kuchonga vipuli na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa mahitaji mbalimbali nchini.
Butiku alitoa ushauri huo wakati wa mahafali ya chuo cha VETA Dar es Salaam yaliyofanyika Novemba 23, 2018.
Alisema baada ya kutembea kwenye karakana mbalimbali na kuhojiana na walimu na wanafunzi, amebaini kuwa VETA ina rasilimali na hazina kubwa ya mashine na ujuzi wa walimu na wanafunzi ambao ukitumiwa vyema unaweza kuzalisha vitu vingi ambavyo kwa kiasi kikubwa bado vinafanywa na watu binafsi au kununuliwa kutoka nje ya nchi.
“nimejionea vifaa vingi ambavyo naamini vikitumika vizuri vinaweza kuleta manufaa makubwa sana kwa taifa, ifike mahali sasa vifaa mlivyonavyo katika karakana zenu viweze kutengeneza mashine nyingine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ” Alisema
Alitoa mfano wa karakana ya uchapaji ambayo alisema ikiimarishwa inaweza kufanya shughuli nyingi sana za uchapaji wa vitu mbalimbali kwa kuwa ina vifaa na wataalam muhimu vya kuweza kufanya shughuli hizo kwa ufanisi mkubwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu akizungumza kuhusiana na mpipango ya VETA katika kutoa ujuzi bobezi katika kupunguza uhaba mafundi katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam. 
 Mwakilishi wa waajiri kutoka kampuni ya PLASCO Fidelis Mashauri akitoa maelezo ya mchango wa VETA katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam Violeth Fumbo akitoa taarifa katika katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakionyesha umahiri wao katika  katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Jiji la Dodoma, Arusha vinara Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Arusha zimeibuka vinara katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2018/19.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati wa kutoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2018/19.

Waziri Jafo amebainisha kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa kukusanya mapato ghafi yaani Fedha nyingi kuliko Halmashauri zote nchini; Jiji hilo limefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh Bil 14.4 kati ya bajeti yao ya kukusanya Tsh Bil 68.6. Makusanya hayo ni sawa na aslimia 21 ya  malengo waliyojiwekea.
Wakati huo huo Arusha inaongoza kwa kukusanyanya vizuri kiasilimia na imefanikiwa kukusanya mapatyo kwa asilimia 26 ya malengo waliyojiwekea; Hii ni kwamba Jiji la Arusha limekusanya kiasi cha Tsh Bil. 4.1 kati ya Tsh Bil.15.6 ya malengo yao ya makusanyo kwa mwaka wa Fedha 2018/19.
“Ieleweke wazi kuwa Jiji la Arusha ndio lililofanya vizuri kimakusanyo kwa mujibu wa asilimia lakini Jiji la Dodoma ndio lililokusanya Fedha nyingi zaidi kuliko halmashauri zote Tanzania alisema Mhe. Jafo.
Aliongeza kuwa kwa upande wa Halmashauri za Manispaa iliyofanya vizuri zaidi ni Manispaa ya Musoma  na kwa Halmashauri za Mji zimeongozwa na Mbinga na upande wa Halmashauri za Wilaya zimeongozwa na Kisarawe.
Mhe Jafo alitanabaisha kuwa kwa makusanyo hayo ukiyawekwa Kimkoa inaongozwa na Mkoa wa Simiyu ikifuatiwa na Manyara, kisha Lindi, Mara, Pwani, Arusha, Njombe,Dodoma, Mwanza na kumalizia na Geita.
Mhe Jafo aliweka wazi pia Halmashauri zilizofanya vibaya zaidi kwa kukusanya chini ni Halmashauri ya Wilaya ya Masasi DC, Nanyamba TC, Nanyumbu DC, Newala Dc,Tandahimba Dc,Songea Dc,Madaba Dc, Rorya na Morogoro Dc.

Na kwa Upande wa Mikoa iliyofanya vibaya kwa kukusanya mapato kidogo ni Mkoa wa Mtwara, Ruvuma na Kigoma. Waziri Jafo aliwakumbusha viongozi wanaohusika kuwa ukusanyaji wa mapato ndio kitakua kigezo cha kupimwa katika utendaji kazi wao hivyo kila mtu ajitathmini kulingana na mapato ya Halmashauri/Mkoa wake.
Kwa mwaka wa Fedha 2018/19 Halmashauri zilipangiwa kukusanya Tsh Bil. 735.6 kutoka kwenye vyanzo vyake vua ndani na hadi kufikia tar 30 Septemba.2018 Halmashauri zilikusanya jumla ya Tsh Bil 143.6 sawa na asilimia 20 ya makisio ya mwaka. Kwa mwaka wa fedha 2017/18 Halmashuri zilipangiwa kukusanya Tsh Bil. 687.3 na hadi kufikia septemba 30 mwaka 2017 ziliweza kukusanya Tsh. Bil 126.8 sawa asilimia 18 ya makisio ya mwaka.
“Kutokana na Takwimu hizo inaonyesha kwamba Halmashuri zimeongeza wingi wa mapato kwa kiasi cha Tsh Bil. 16.7 na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka kwa asilimia 2” alisema Jafo.

WAZIRI LUGOLA AANZA ZIARA JIMBONI KWAKE MWIBARA, AWAHAMASISHA WANANCHI KUANZA MAANDALIZI YA KILIMO

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Mkazi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao ndani ya Jimbo lake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Afisa Tarafa ya Kenkombyo, Rebeca Mdodo alipokua anatoa taarifa ya Tarafa yake kwa Waziri Lugola, kabla ya Mbunge huyo hajaanza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Lugola ameanza ziara jimboni humo leo akisikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERIKALI YATEUA MAGEREZA KUMI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS JPM

$
0
0
Serikali imeteua jumla ya magereza kumi nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli la kulitaka Jeshi la Magereza litumie rasilimali watu ya wafungwa kuzalisha mazao kwa ajili ya biashara na chakula badala ya serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa agizo hilo katika Gereza la Kwamngumi wilayani Korogwe ,mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema utekelezaji huo unaenda sambamba na uteuzi wa magereza kumi ya kilimo nchini na akiweka wazi uwapo wa mpango maalumu wa kutathmini na kupima mpango mkakati huo kwa kila gereza.

Aliyataja magereza hayo kuwa ni Songwe (Mbeya), Kitai (Ruvuma), Ludewa (Njombe), Mollo (Rukwa), Kitengule (Kagera) ambayo yameteuliwa kulima mahindi, mengine ni Idete na Kiberege (Morogoro) yaliyoteuliwa kulima mpunga huku Kitete (Rukwa), Kitengule (Kagera) na Gereza la Arusha yakiteuliwa kulima maharagae

“Tunahitaji matumizi sahihi ya rasilimali watu na ardhi tuliyonayo katika magereza yetu itumike ipasavyo kwa shughuli za uzalishaji ili tuweze kutekeleza amri ya Mheshimiwa Rais, huku lengo la wizara kupitia jeshi la magereza ni kuweza kuwekekeza fedha kwa kulitumia shirika la uzalishaji mali lililopo ndani ya jeshi hilo na ikiwezekana hapo baadae tuweze kutafuta wateja watakaonunua mazao yatakayozalishwa katika mashamba hayo,” alisema Masauni


Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Gereza la Kwangumi, Christopher Mwenda, alisema wao kama uongozi wa gereza hilo wamejipanga vizuri katika utekelezaji wa aguzo hilo huku akiiomba wizara kuongeza vifaa vya kilimo ili waweze kuzalisha kwa kiwango kikubwa zaidi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa tofali linalotengenezwa na wafungwa ikiwa ni mpango wa uongozi wa gereza la Kwamngumi kukabiliana na changamoto ya makazi kwa askari, Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo,Christopher Mwenda, lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa nyumba iliyojengwa na matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamngumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo, Christopher Mwenda. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia tofali ambazo zimetengenezwa na wafungwa wa Gereza la Kwamngumi, ambazo hutumika kujengea nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji na kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa Kaunda suti), na ujumbe alioongozana nao wakipita mbele ya nyumba iliyojengwa kwa kutumia matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamgumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Dkt. Mwakyembe azindua Kampeni ya Uzalendo na Utaifa 2018, yenya kauli mbiu “Kiswahili uhai wetu,Utashi wetu”Dkt. Mwakyembe azindua Kampeni ya Uzalendo na Utaifa 2018, yenya kauli mbiu “Kiswahili uhai wetu,Utashi wetu”

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo  kwa wadau wa Wizara hiyo katika  hafla fupi  ya Uzinduzi wa Uzalendo na Utaifa iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam .
 Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa  Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akiongea jambo na wadau wa Wizara hiyo (Hawapo katika picha) katika  hafla fupi ya Uzinduzi wa  Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao  ndio Wadhamini Wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka  huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8  Disemba  2018 Jijini Dodoma, akieleza jambo kwa wadau wenzake waliofika kuunga mkono uzinduzi wa kampeni hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa,  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi(kulia) akimvalisha nembo inayoashiria uzalendo Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao ndio wadhamini wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka  huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8  Disemba  jijini Dodoma.
 Wadau wa Sanaa kutoka katika sekta binafsi taasisi za Serikali wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea  katika  hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.

SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amerasimisha bandari bubu nne mkoani Tanga kati ya bandari bubu 48 zilizopo mkoani humo wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu hizo na kupata taarifa ya utendaji kazi wa bandari ya Tanga. Nditiye amerasimisha bandari bubu ya Moa iliyopo Wilayani Mkinga, Kigombe (Muheza), Kipumbwi na Mkwaja zilizopo wilayani Pangani.

Nditiye amesema kuwa amerasimisha bandari bubu hizo nne tu kati ya bandari bubu 48 zilizopo mkoani Tanga kwa kuwa zipo mbali na bandari ya Tanga, zipo mipakani na nchi za jirani, kusogeza huduma karibu na wananchi na kuiwezesha Serikali kukusanya tozo na kodi mbali mbali kwa ajli ya kutoa huduma kwa wananchi. 

“Naiagiza TPA kuhakikisha kuwa bandari bubu nne nilizorasimisha zinafanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2019 na wahakikishe kuwa watumishi wa TPA na TRA wanakuwepo kwenye bandari hizo pamoja na ofisi zote za Serikali zinazohitajika ikwemo Jeshi la Polisi,”.

Pia ameitaka TPA kwa kushirikiana na TRA itoe elimu kwa wateja kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ya Serikali kwa kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa ni kidogo ukilinganisha na athari wanazopata wananchi na wafanyabiashara kwa kuhatarisha maisha yao kwa kukwepa kodi na kutumia bandari bubu kupitisha mizigo na bidhaa nje ya bandari rasmi zilizopo na kupita maporini. 

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea shukrani za Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Moa, Rambazo A. Mohamedi (wa kwanza kushoto) kwa kurasimisha bandari bubu ya Moa kuwa bandari rasmi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa bandari ya Tanga, Percival Salama

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya utendaji kazi wa Bandari ya Tanga kutoka kwa Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama (aliyesimama katikati) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua bandari hiyo

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu upakuaji wa mafuta melini kutoka kwa Nahodha Andrew Matilya wakati wa ziara yake ya kukagua bandari ya Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akipokea taarifa kuhusu bandari bubu ya Moa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Yona Mark wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu mkoani Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokutana na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu (watatu kulia)  na baadhi ya Watendaji wa Baraza hilo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 24, 2018.  Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,  Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi,  wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Baraza, Suleiman Malela na kulia ni Mchumi wa Baraza, Erad Mushi. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu kabla ya mazungumzo  yao yaliyowashirikisha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mainuna Tarishi na Watendaji wa Baraza. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 24, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZAIDI YA MADEREVA 1600 WAPATIWA MAFUNZO ARUSHA

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha

Madereva wa mabai ya kubebea abiria katika mkoa wa Arusha wamepatiwa mafunzo ilihali wengine waki3ndelea na mafunzo

Akizungumza Mrakibu wa polisi Joseph Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha amesema lengo kuu ni kuhakikisha kuwa madereva wote wanapata elimu na wanatoa huduma inayoendana na elimu waliyoipata

Tangia kuanzishwa kwa mafunzo ya madereva miezi minne iliyopita madereva 1600 wamehitimu mafunzo wa magari ya kubeba abiria (PSV)kupitia chuo cha Veta pamoja na chuo rafiki wa NIT cha Moden driving vyote vya mkoa wa Arusha.

"Pamoja na mapambano hayo ya ajali za barabarani ni lazima kuhakikisha kuwa wapo madereva wenye weledi" alisema Bukombe. Aidha amesema mafunzo haya yamesaidia sana kwani mkoa hapo pamekuwa salama bila Ajali ."Tangia tumeanzisha mafunzo takribani miezi minne iliyopita kwa mkoa wa Arusha tupo salama, na ukikuta ajali imesababishwa na bodaboda na siyo magari ya abiria" alisema Bukombe

Mara baada ya kuona ajali zimeongezeka jeshi la polisi liliendesha ukaguzi wa leseni na kugundua kuwa madereva wengi wana leseni lakini hawana vyeti, kwahiyo yamkini wanazipata leseni kwa njia wanazozijua wao."Sisi tukasema hawawezi kuendelea na leseni walizonazo badala yake warudi darasani kwenda kusoma ili waweze kupata vyeti"alisema.



Mrakibu wa Polisi Joseph Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha .


WAZIRI MWAKYEMBE ATEMBELEA BANDA LA WAJASIRIAMALI WA TABORA

$
0
0


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kulia)  akitizama mboga za majani zilizokaushwa na kuhifadhiwa  katika paketi kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka kikundi cha Amka Group cha Tabora Mjini kushoto ni Mjasiriamali wa kikundi hicho Bi.Anna Shango ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora (wapili kulia) ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda uwanja wa Jeshi.
PIX 3
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati)  akitizama viungo vya mbalimbali vya chakula vilivyosagwa na kuhifadhiwa  katika vikopo kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka Wilaya ya Uyui ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.
PIX 5
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kushoto)  na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri wakifurahia maziwa yanayotengenezwa na Neema Brand mjasiriamali mdogo wa Mkoa huo leo walipotembelea Maonesho ya wajasiriamali waliyoshiriki maonesho  ya Jukwaa la Fursa za Biashara  katika uwanja wa Jeshi linaloendelea Mkoani hapo,kushoto ni Bi.Sameera Sumar mmilikiwa biashara hiyo.
PIX 7
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto)  akitizama  zulia lillofumwa kwa mikono na Mjasiriamali  Bw.Hassan Rashid (kulia) kwa kutumia mikono  na mifuko ya sandarusi iliyokwisha kutumika na nzuri  leo  alipotembelea maonesho ya wajasiriamali  waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.

HASUNGA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MOROGORO ASISITIZA UMUHIMU WA MBEGU BORA

$
0
0

Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo-Morogoro

Imebainika kuwa malighafi nyingi zinazozalishwa kwa ajili ya viwanda nchini zinatokana na sekta ya kilimo ambayo inategemewa na watanzania kwa zaidi ya asilimia 75.

Hayo yamebainishwa tarehe 24 Novemba 2018 na Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipambanua katika usimamizi madhubuti wa ujenzi wa viwanda hivyo wananchi wanapaswa kuzalisha kwa wingi mazao mbalimbali katika sekta ya kilimo kwani uhai wa viwanda vingi vinategemea zaidi sekta ya kilimo.

Alisema kuwa Wizara ya kilimo itasimamia kwa weledi uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora na kwa wingi ili wakulima waweze kunufaika katika uzalishaji wenye tija ili kuondokana na uzalishaji wa mazao kwa ajili ya chakula pekee badala yake kuzalisha kwa tija kilimo cha kibiashara.

“Katika viwanda tutakavyozalisha zaidi ya asilimia 60 ya malighafi zitakazotumika zinazalishwa hapa nchini, hivyo tunawajibu wa kutoa malighafi zinazotosheleza viwanda tunavyovianzisha” Alikaririwa Mhe Hasunga


Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua ghala la kuhifadhia mbegu la Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt Sophia Kashenge.(Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo). 

Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt Sophia Kashenge akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga mfuko wa mbegu za alizeti zinazozalishwa na ASA wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018. 

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua ghala la kuhifadhia mbegu la Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018. 

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua mbegu mbalimbali zinazozalishwa na Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018. 

TIMU YA BUNGE YATAKA KURUDI NA UBINGWA

$
0
0

TIMU ya Bunge Sport Club imeendelea na mazoezi makali katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya michezo ya Wabunge wa Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Desemba mosi mwaka huu Jijini Bujumbura nchini Burundi.

Gazeti hili limefika katika uwanja wa Jamhuri jana asubuhi na kushuhudia timu hiyo ikiendelea na mazoezi makali ambapo kwa upande wa Soka ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi ambaye ni Mbunge wa Wawi,Ahmed Juma Ngwali.Kwenye Netiboli timu hiyo ilikuwa ikicheza mchezo wa kirafiki na Chuo cha Mipango huku Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula akionesha ufundi mkubwa wa kufunga mabao.

Aidha wakimbiaji wake, Daniel Mtuka, Yosepha Komba, Zubeda Sakuru nao walikuwa wakifanya maozezi ya kukimbia kujiweka sawa na mashindano hayo.Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini hapa,Kocha Mkuu wa timu ya Soka,Venance Mwamoto alisema wamejiandaa kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuwatoa kimasomaso Watanzania.Mwamoto ambaye ni Kocha mchezaji na Mbunge wa Kilolo, alisema kwa sasa timu za Taifa zimekuwa zikifanya vibaya katika mashindano mbalimbali hivyo akawataka Watanzania kuamini kwamba timu ya Bunge la Tanzania itawafuta machozi kwa kufanya vizuri.

“Hivi karibuni tumefanya vibaya kwa timu yetu ya Taifa kwa kufungwa na Lesotho pia timu ya Vijana nayo ilipoteza mategemeo yapo kwetu niwaahidi Watanzania hatutawaangusha,”alisema Mwamoto.Kuhusiana na maandalizi ya mashindano hayo,Mwamoto alisema wameweka kambi ya zaidi ya wiki tatu pamoja na kucheza michezo miwili ya kirafiki ili kuangalia mapungufu ya timu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.



Naibu Waziriu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na mchezaji wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge , Dk. Angelina Mabula akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Chuo cha Mipango wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya timu . Bunge Queens inajiandaa na michezo ya Mabunge ya Jumuia ya Afrika Mashariki itakayofanyika Bujumbura Burundi kuanzia Desemba mosi mwaka huu
Mchezaji wa timu ya Bunge ya Netbal, Agness Marwa akimiliki mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo.

Kocha wa timu Netiboli, Eleonora Mongi (mwenye mpira) akizungumza na wachezaji wake.
Wachezaji wa mpira wa Miguu wa Bunge FC ‘Ndugai Boys’ wakifanya mazoezi Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mahsriki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao.

RPC PWANI APEWA VITISHO NA WATU WASIOJULIKANA,AWAPA SALAMU ATAZIDI KUPIGA KAZI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 

KAMANDA wa jeshi la polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa anadaiwa kutishiwa na watu wasiofahamika kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuwa watamhamisha kwenye mkoa huo kutokana na kuzuia kuingiza bidhaa za magendo kwenye bandari bubu. Licha ya kitisho hicho amesema,hawezi kulegeza uzi kwani shughuli hizo zinasababisha nchi kukosa mapato kwa kukwepa ushuru.

Akizungumza kwenye kituo cha polisi wilaya ya Bagamoyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kufanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali ikiwemo madumu ya mafuta ya kula 4,311 ya lita 20 kila moja na mafuta ya dizeli madumu 52 kwenye oparesheni zinazoendelea mkoani humo.

 "Kwa siku za hivi karibuni mimi pamoja na watendaji wenzangu akiwemo ofisa upelelezi wa mkoa tumekuwa tukitumiwa jumbe za vitisho kupitia simu"“Nitafanya kazi kwa maelekezo ya mkuu wa mkoa, IGP na Rais hivyo siko tayari kufanya kazi kwa maelekezo ya watu wengine ambayo ni kwa maslahi ya mtu binafsi bali kwa maslahi ya nchi"

“Sitishwi na mtu wala sms eti watatuhamisha ama watatupeleka Mlingotini waambieni meseji zao tunazo ,tunazifanyia kazi na tumechukua namba za hawa tuliowakamata kutokana na operesheni hizi kama ni miongoni mwao tutawachukulia hatua kali "alieleza Nyigesa.
 Nae mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema lazima vyombo vinavyohusika vifuatilie jambo hili ikiwa ni pamoja na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA).

" Kila mamlaka hapo inapaswa kuhakiki bidhaa hizo ili kujiridhisha kuwa  bidhaa hizi zimeingizwa nchini kwa kufuata taratibu ??na ile ya chakula na dawa kuangalia kama mafuta hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu"alisema Ndikilo.
Katika msako huo pia vifaa vya ujenzi marumaru katoni 200, friji 16, pikipiki moja isiyokuwa na namba bangi kete 512 na pombe ya moshi lita 16 vilikamatwa na watuhumiwa 17 wanaotuhumiwa kuhusika na matukio hayo wanashikiliwa.

MELI YA KUREKODI MTETEMO YA KINA KIFUPI CHA MAJI YAWASILI ZANZIBAR

$
0
0


Na Mwashungi Tahir ,Maelezo

Mkurugenzi wa Uwezeshaji Mamlaka ya Udhibi wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Omar Zubeir Ismail alisema SeriKali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na utafiti wa mafuta na Gesi Asilia kwa njia ya mtetemo kwa kitalu cha Pemba Zanzibar.

Hayo ameyasema leo huko Bandarini Malindi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuwasili meli kubwa ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye kina kifupi cha maji. 

Aidha alichukua nafasi kwa kuwajuilisha wananchi kazi ya utafiti wa mafuta na gesi Asilia kwa njia ya mtetemo bado inaendelea kwa upande wa kina kifupi cha maji (TRANSITION ZONE 2D SEISMIC SURVEY) katika maeneo ya visiwa hivyo.

“Nachukua nafasi hii kuwajuilisha wananchi kwamba suala la uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ni la muda mrefu na linaweza kufika hadi miaka kumi kukamilika nawaomba muendelee na kazi zenu za kawaida”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema tumuombe Mungu tufanikiwe suala hili kwani likifanikiwa ni la wote kwa maendeleo ya nchi yetu na vizazi vyetu vya hapo baadae. Pia alisema meli zitakazotumika katika zoezi la mtetemo kwa kina kifupi cha maji tayari zimeshawasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Meli kubwa itakayotumika kurekodi taarifa za mtetemo kwa kina kifupi cha maji wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo ya Unguja na Pemba ya Stanford Bateleur ikiwa imefunga gati Bandari Malindi ikiwa tayari kuanza kazi hiyo wiki ijayo. 
Nahodha wa meli ya Stanford Bateleur Raul Mendoza akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu meli hiyo inavyofanyakazi ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji 
Mkurugenzi Uwezeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa utafutaji na Uchimabaji wa Mafuta na Gesi AsiliaOmar Zubeir Ismail akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa meli ya Stanford Bateleur inayorekodi mtetemo katika kina kifupi cha maji. PICHA NA RAMADHANI ALI MAELEZO .

Viewing all 110108 articles
Browse latest View live




Latest Images