Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA YAFUTA DHAMANA YA MBOWE,MATIKO KWA KUKIUKA MASHARTI KESI YA UCHOCHEZI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia dhamana Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana katika kesi ya uchochezi inayowakabili wao pamoja na viongozi wenzao saba wa chama hicho.

Uamuzi huo umetolewa leo asubuhi Novemba 23, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Akitoa uamuzi huo dhidi ya Mbowe na Matiko, Hakimu Mashauri amesema, kitendo cha washtakiwa hao kutokufika mahakamani bila ya kuwa na sababu za msingi ni kudharau amri za Mahakama kwa makusudi.

Akitoa uamuzi kuhusu mshtakiwa Mbowe, Hakimu Mashauri amesema, sababu zilizotolewa na mdhamini wake Novemba Mosi mwaka huu kuwa mshtakiwa huyo aliugua ghafla na kupelekwa nje ya nchi akiwa mahututi huku Wakili wake Peter Kibatala akieleza kuwa alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu si za kweli kwa sababu zinakinzana na taarifa alizotoa mshtakiwa mwenyewe.

Amesema, Mbowe katika maelezo yake alieleza kuwa alisafiri nchini Oktoba 28 mwaka huu kuelekea Washngton DC kuhudhuri mkutano wa Oktoba 30 na kwamba Oktoba 31, usiku alipotaka kusafiri kurejea nchini kwa ajili ya kesi hiyo iliyopangwa kuwepo Novemba Mosi, mwaka huu alishambuliwa na ugonjwa wa ghafla.

Alieleza kulingana na ugonjwa wake, madaktari waliokuwa wakimtibu, walimshauri asisafiri umbali mrefu kwa ndege lakini hata hivyo hati yake ya kusafiria inaonesha alisafiri umbali mwingine mrefu kwa kwenda Marekani kwa ndege na kitu kinachoonyesha kwamba alikuwa anadharau amri za mahakama kwa makusudi kwa sababu amezungumza mambo ya uongo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa chini ya ulinzi baada kufutiwa dhamana kwa kukiuka masharti ya dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili yeye na viongozi wenzake nane wa Chadema baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi saa saba mchana kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi kama kesi hiyo iendelee katika hatua ya usikilizwaji leo ama la.



SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WANANCHI WANAOHARIBU MIUNDOMBINU YA NJIA YA RELI

$
0
0
Serikali inawataadharisha wananchi wanaoharibu miundombinu ya njia ya reli kwa kuwa imeazimia kuwachukulia hatua kwa wanaojishughulisha na shughuli za kibinadamu ndani ya eneo la hifadhi ya miundombinu ya njia ya reli na kwa wanohujumu miundombinu hiyo kwa kuiba 
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa miundombinu ya njia ya reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Arusha akiwa kwenye stesheni ya treni ya Mombo iliyopo mkoani Tanga .
Nditiye ameyasema hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa Kasongwa akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama kuwa washirikiane na Shirika la Reli Tanzania (TRC), viongozi na wananchi wanaoishi maeneo inakopita reli hiyo na vyombo vya ulinzi na usalama kuilinda na kuitunza reli kwa kuwa reli ni uchumi na inachangia maendeleo ya taifa letu, tuilinde na tuitunze. “Ni marufuku kufanya shughuli yoyote ya kibanadamu ndani ya eneo la mita 30 kulia na kushoto mwa njia ya reli kwa kuwa kwa kufanya shughuli za kilimo au kibinadamu unasababisha udongo kuja kwenye njia ya reli na kuharibu miundombinu ya njia ya reli,” amesema Nditiye.
Pia ameongeza kuwa wapo baadhi ya wananchi wanahujumu reli yetu, wanafungua vifungashio ambapo inaweza kusababisha treni kuanguka kwa lengo la kutaka kuiba mataruma na reli yenyewe, viwanda vya chuma chakavu wafikie mahala watafute malighafi inayotakiwa.  Amesema kuwa treni ikirushiwa mawe wakati inatembea na ikitokea kioo kikapasuka, treni hiyo isimame na wananchi waishio eneo hilo wachukuliwe hatua.
Nditiye amesema kuwa hakuna Serikali makini inaweza kupuuza usafiri wa njia ya reli ambapo kwa kutambua hilo, Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano ameona afufue reli hii ambayo inatakiwa ianze kufanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018. Amefafanua kuwa reli ni usafiri wa gharama nafuu na starehe na itasaidia kuzuia uharibifu wa barabara kwa kusafirisha mizigo mizito
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa Kasongwa amesema kuwa watashirikiana na TRC kuhakikisha kuwa wanalinda rasilimali za reli, “reli ni rasilimali zetu,” amesema Kasongwa.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akisikiliza kwa makini taarifa kuhusu mataruma yanayohitajika kukarabati njia ya reli ya Korogwe – Mombo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Reli wa Shirika la Reli Tanzania Mhandisi Felix Nlalio (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye ziara ya kukagua reli hiyo mkoani Tanga. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa Kasongwa
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (mwenye kikoti cha njano) akipata maelezo kuhusu vifungashio vya mataruma ya reli vinavyohitajika kwa ajili ya kukarabati njia ya reli ya Dar es Salaam – Moshi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Reli wa Shirika la Reli Tanzania Mhandisi Felix Nlalio (aliyeinama) wakati wa ziara yake mkoani Tanga ya kukagua ukarabati wa reli hiyo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda  kiberenge kwa ajili ya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu ya njia ya reli ya Dar es Salaam – Moshi katika stesheni ya Mombo mkoani Tanga

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UTUMWA MAMBO LEO BY AYOUB MZEE

LIVE: WASANII WA WASAFI FESTIVAL WAKIINGIA MTWARA

VIKUNDI 750 VYA WAKULIMA WILAYANI KISARAWE KUKABIDHIWA HATI MILIKI ZA ARDHI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

VIKUNDI vya wakulima 750 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani vinatarajia kukabidhiwa hati miliki za ardhi zitakazoweza kuwasaidia kupata mikopo katika taasisi za fedha.

Hayo yalibainika wilayani humo juzi katika Kijiji cha Zegero wakati wa mkutano wa mchakato wa kuanzisha jukwaa la wakulima unaoratibiwa na Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association kwa kushirikiana na Ofisi ya mkurugenzi wa halmshauri hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo Ofisa miradi wa shirika hilo, Said Simkonda alisema kati ya vikundi hivyo vitakavyopata hati hizo vikundi 250 ni vya watu wenye ulemavu ambavyo vimepata mashamba kwa ajili ya kufanya kilimo.Akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa jukwaa la wakulima alisema litakuwa ni chombo cha kuwakutanisha wakulima wote waliomo wilayani Kisarawe na mikoa ya jirani ili kuleta kilimo chenye tija.

Alisema mchakato huo umewahusisha wadau wa kilimo kutoka Kata ya Kurui, Mzenga, Mafizi, Vihingo, Marui na Chole na kuwa shirika hilo linaupongeza uongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kulidhia kuupokea mradi huo wa kilimo mnamo mwaka 2016.
Ofisa Miradi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda, akizungumza na wadau wa kilimo ambao ni wanachama wa shirika hilo kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Jukwaa la Wakulima wilayani Kisarawe mkoani Pwani pamoja na kukabidhiwa hati miliki za ardhi. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni.
`Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akitoa taarifa ya shirika hilo wakati wa mkutano huo.
Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akimkabidhi taarifa hiyo Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni.

WAFANYABIASHARA WA UTURUKI WAONESHA NIA YA KUWEKEZA KATIKA KIWANDA CHA NGUO SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki wameonesha nia na dhamira ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo mkoani Simiyu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 4000.

 Hayo yamebainishwa katika kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo ambaye aliambatana na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Uturuki kutoka makampuni saba ya nchi hiyo, katika kikao maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali na jumuiya ya wafanyabiashara ya mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Balozi Kiondo amesema Wafanyabiashara hao wanayo azma ya kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza nguo katika mnyororo mzima wa utengenezaji kutoka bidhaa ya awali ya pamba mpaka bidhaa ya mwisho kabisa, ambayo ni nguo kwa ubia(partineship) na Watanzania.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS amesema  mpaka sasa ni makampuni sita kutoka nchini humo yameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha nguo mkoani Simiyu na akaahidi kwenda kuwashawishi wafanyabiashara wenzake hivyo watakaporudi kwa mara nyingine  makapuni mengi yatakuja kuwekeza katika viwanda vya nguo.

“Nikirudi nyumbani kama kiongozi wa wafanyabiashara nitawashawishi wengine pia waje wawekeze katika viwanda vya nguo,ombi langu kwenu ni kwamba ninahitaji Mfanyabiashara Mtanzania ambaye tutashirikiana naye katika uwekezaji huu(partinership), lakini niwahakikishie tu kuwa katika kiwanda tutakachojenga mashine na vifaa vyote vipo tayari kule Uturuki” alisema  Cengiz.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo unaotarajiwa kufanywa na Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki katika mkoa wa Simiyu.
 Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na  mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS( wa tatu kulia),  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede( wa pili kulia) na viongozi wa Serikali pamoja na wafanyabiashara wa mkoa huo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MASHINDANO YA VIJANA KUOGELEA KUFANYIKA DESEMBA 8 NA 9 MWAKA

$
0
0
Mashindano ya kuogelea kwa wachezaji yoso yamepangwa kufanyika Desemba 8 na 9 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga. 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji chipukizi kuanzia miaka 12 kushuka chini, yana lengo la kuibua vipaji vya waogeleaji kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali nchini na ya kimataifa. 

Inviolata amesema kuwa TSA kwa sasa inatafuta wadhamini wa kufanikisha mashindano hayo. Mwisho wa kuthibitisha ni Novemba 30. “Mashindano haya ni ya kuibua na kuendeleza vipaji, na pia yameandaliwa kwa ajili ya kupima uwezo wa waogeleaji chipukizi ambao wameibuliwa katika mashindano yaliyopita, tunaomba wadhamini wajitokeze,” alisema Inviolata. 

Amefafanua kuwa wanatafuta wadhamini kwa ajili ya kusaidia gharama za uendeshaji kwani siyo kazi rahisi mashindano hayo kufanyika bila sapoti kutoka nje.Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.

“Mashindano haya yatatoa fursa kwa waogeleaji ambao walishindwa kushindana katika mashindano ya wakubwa kutokana na kigezo cha umri, kwa vile TSA inatamnbua waogeleaji chipukizi, tumeamua kuandaa mashindano ambao yatawafanya waogeleaji wanaochipukia nao kujipima uwezo wao,”alisema. 

Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la waogeleaji waliochini ya miaka saba, waogeleaji wa miaka nane na tisa, 10 na 11 na 12. Washindi wa jumla katika kila kundi atazawadiwa kikombe wakati washindi wa kila shindano watapata medali.

Muhimbili yahudumia wagonjwa zaidi ya 1476 Ligula

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na watalaam wengine wa afya leo wamehitimisha utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara -Ligula- kwa kuhudumia wagonjwa 1476.

Kati ya hao, upasuaji mkubwa umefanyika kwa wagonjwa 54 na mdogo kwa wagonjwa 81. Baadhi ya upasuaji mkubwa uliofanyika ni kutoa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi, kutoa matezi ya koo na matezi ya nyama ya pua (mafindofindo, kutoa tezi dume pamojan na kutoa mtoto wa jicho. Maeneo ambayo wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Ligula wamehudumia ni magonjwa ya dharura, Radiolojia magonjwa ya ndani, afya ya kinywa na meno,watoto ,magonjwa ya pua,koo na masikio, magonjwa ya kike na uzazi pamoja na mfumo wa mkojo.

Utoaji wa huduma za afya umeenda sambamba na kuwajengea uwezo wataalam wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara ili waweze kutoa huduma bora za afya na kupunguza rufaa za kwenda Muhimbili. Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Dkt. Lobikieki Kissambu amewashukuru wataalam wa Muhimbili kwa kutoa huduma za afya katika hospitali hiyo na kueleza kuwa hospitali hiyo ina Daktari Bingwa mmoja tu hivyo ujio wa watalaam hao umewawezesha wananchi kupata huduma za kibingwa.

Utoaji wa huduma za afya kwa njia ya mkoba ni sehemu ya mpango mkakati wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ya kuhakikisha inatembelea Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini ili kushirikiana nao na kuwajengea uwezo katika kutoa huduma ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili.
Wataalam wa afya wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara-Ligula- wakiwahudumia wagonjwa wa macho kwa kutumia mashine maalum ya kupimia macho.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinywa na meno kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Frank Kessy (kulia) akishirikiana na Dkt. Dickson Sahini kumfanyia upasuaji mgonjwa mwenye uvimbe aina ya jipu lililotokana na magonjwa ya kinywa na meno.
Daktari Bingwa wa watoto Apansia Ndossa (kushoto) pamoja na muuguzi Dorcas Ndedya wakimuhudumia mtoto mchanga ambaye hakupumua vizuri baada ya kuzaliwa.
Daktari wa magonjwa ya dharura kutoka Muhimbili (kulia) akitoa maelekezo kwa watoa huduma wa kitengo cha magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Ligula jinsi ya kumpatia huduma mgonjwa mwenye shida ya kupumua.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Henrika Kimambo (kushoto) akimuhudumia mgonjwa mapema hii leo.

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AHIMIZA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA KULIPA KODI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Mwita Wairata amewasisitiza wafanyabiashara na wenye Viwanda nchini kulipa kodi ya maendeleo ili Serikali iwe na uwezo wa kufanya miradi ya kimaendeleo ambayo itasaidia wananchi wengi.

Waitara ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa kuelekea katika kilele cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) ambapo amesema ili Serikali iongeze ufanisi katika kuhudumia jamii wafanyabiashara na wawekezaji katika maenneo mbalimbali wanapaswa kulipa kodi ya mapato ambayo pamoja na kusaidia uongezwaji wa miradi ya maendeleo pia itaboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

Amesema chama hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi wa Taifa na kuunga mkono juhudi za Seikali ya Awamu ya tano ya Rais Dk.John Magufuli inayosisitiza uchumi wa Viwanda.“Wafanyabiashara lipeni kodi ya maendeleo, Kodi ndio itatufanya kuwawekea mazingira mazuri ya uwezeshaji na hatimaye mfanye biashara zenu kwa ufanisi mkubwa, sisi tutaendelea kuwawezesha kwani chama chenu ni muhimu sana katika kukuza ustawi wa kijamii,"amesema Waitara.

Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara (wa pili kushoto) akisalimiana na  Mkuu wa Kitengo cha Biashara benki ya KCB Masika Mkulu.Wa kwanza kushoto ni Kaimu Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo Octavian Mshiu.

MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE ,ESTER MATIKO WAPELEKWA MAHABUSU YA SEGEREA

$
0
0



*Ni baada ya Mahakama kuwafutia dhamana baada ya kuvunja masharti

Na Karama Kenyunko blogu ya Jamii

MWENYEKITI  wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wamepelekwa mahabusu katika gereza la Segerea ambako watakaa mpaka pale rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mbowe na Matiko kufutiwa dhamana yao dhidi ya kesi  ya uchochezi inayowakabili  pamoja na viongozi saba wa chama hicho.

Kutokana na uamuzi huo,  Wakili Peter Kibatala anayewatetea washtakiwa hao alitoa taarifa ya kukata rufaa na akaomba kupatiwa nakala ya uamuzi huo mdogo. Pia aliomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo kusubiri rufaa watakayoifungua washtakiwa hao Mahakama Kuu itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi kama kesi hiyo iendelee kusikilizwa

Katika uamuzi wake, Hakimu Mashauri amesema Wakili Kibatala alitoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa chini ya kifungu cha 161 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hakimu Mashauri amesema kifungu hicho kinasema amri zote zinazotolewa ni lazima zitakatiwa rufaa mahakama Kuu kwa marejeo kufuatia taarufa hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 6 , mwaka huu kwa ajili ya kutajwa wakati wakisubiri rufaa hiyo isikilizwe na kutolewa maamuzi.

Katika rufaa yao, iliyowasilishwa chini ya hati ya dharura katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Wakili Kibatala kwa niaba ya washitakiwa  alidai kuwa wana sababu nne za kupinga uamuzi ikiwemo mahakama haijawapa nafasi wadhamini ya kujieleza kwa mujibu wa sheria.

Pia alidai Mahakama imekosea kuwafutia dhamana washitakiwa kwa sababu Novemba 12, mwaka huu Mbowe na Matiko walifika mahakamani bila kukamatwa na kuwa chini ya ulinzi.

Alidai masharti ya dhamana waliyopewa washitakiwa ni kinyume na sheria.

Mbali na Mbowe na Matiko, washtakiwa wengine Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa bunda, Esther Bulaya, katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji. 

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester  wakiwa tayari kupelekwa mahabusu katika gereza la Segerea ambako watakaa mpaka pale rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA CHAMA CHA WATAALAMU WA FIGO TANZANIA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Mkutano wa Tano wa Chama Cha Wataalamu wa Figo Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar, leo 23/11/2018, na kuhudhuriwa na Wataalamu wa Maradhi ya Figo kutoka Tanzania na Nje ya Tanzania.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mtaalam wa Kampuni ya Harsh Pharmaceuticals Limited ya Dar es Salaam,Ndg. Augustino Mbunda, akitowa maelezo ya Mashine ya kusafishia Figo, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Chama Cha Wataalamu wa Figo Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Karume Hoteli ya Zanzibar Beach Resout Mazizini Zanzibar kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na kushoto Mwenyekiti wa  NESOT. Dr. Onesmo Kisanga, wakati akitembelea maonesho hayo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe Balozi Seif Ali Iddi na kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamah Rashid Mohammed, wakimsikiliza Mtaalamu wa Kampuni ya Harsh Pharmaceuticals Limited Ndg. Augustino Mbunda, akitowa maelezo ya Dawa zinazotumika kwa Wagonjwa waradhi ya Figo wakati akitembelea monesho kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Chama Cha Wataalam wa Figo Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Karume Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Profesa Mohammed Janabi,kulia wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya ufunguzi huo, na kushoto Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na Dr. Mohammed Jidawi Mshauri wa Waziri Afya Zanzibar.(Picha na Ikulu ).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

PSSSF YATOA ELIMU KWA JISHI LA POLISI ZANZIBAR JUU YA FAIDA ZINAZOPATIKANWA KATIKA MFUKO HUO

$
0
0
 Meneja wa PSSSF Zanzibar Issa Sabuni akitoa elimu kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi juu ya faida zinazopatikanwa katika  mfuko huo baada ya kuunganishwa na mifuko mengine na kua  mifuko mmoja wanye kuleta faida kwa  Wafanyakazi Wastaafu.
  Afisa Maendeleo PSSSF Hamza Msangi akitoa Mafunzo kwa Jeshi la Polisi faida zinazopatikanwa katika Mfiko huo katika ghafla iliofanyika katika ukumbi wa Polisi  Ziwani Mjini Unguja.
 Msaidizi Kamishna wa Polisi Zanzibar F C Shilogile  akitoa shukurani kwa Maafisa wa PSSSF kwa kuwapatia Mafunzo Wafanyakazi wake katika ghafla iliofanyika katika ukumbi wa Polisi  Ziwani Mjini Zanzibar,( kulia) ni Meneja wa PSSSF Zanzibar Issa Sabuni.

Baadhi ya Askari wa jeshi la Polisi waliohudhuria katika Mafunzo hayo yaliofanyika katika  Ukumbi wa Polisi Ziwani Mjini Unguja.

Picha na Abdalla Omar  Maelezo – Zanzibar.

WAZIRI MKUU AAGIZA VYOO NA MIFUMO YA MAJI VIWANDANI VIKAGULIWE

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, katika ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Usafi wa Mazingira Shirika la Plan International Dodoma Rachel Stephen, kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, katika ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018, kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Mohammed Bakari, , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi funguo ya gari mshindi wa kwanza katika usafi Mkuu wa Wilaya ya Njiombe Ruth Msafiri, kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, katika ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Maafisa Afya wa mikoa nchini, wakati alipofungua rasmi mkutano wa maafisa hao kwenye ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018.

KUPATA MATOKEO NI NJIA NZURI YA KUWANIA UBINGWA- PLUIJM

$
0
0

BAADA ya ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Van De Pluijm amesema kwa timu yake kupata matokeo ni njia nzuri ya kwenda kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ushindi huo unaihakikishia Azam FC nafasi ya kuendelea kubakia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 33 wakiwa  wamecheza mechi 13 bila kupoteza hata huku wakitoa sare michezo 3 na kushinda michezo 10 ya Ligi Kuu.


Pluijm amesema, anaona fahari kubwa sana kwa vijana wake kucheza kwa kujituma na kupata matokeo ambayo anayahitaji hasa kwenye ligi kuu na kielekea kwenye mbio za kuwania ubingwa.


Akizungumzia mechi za ligi kuu, Pluijm amesema  matokeo yao ndani ya Uwanja yanatokana na wachezaji kufuata maelekezo na kujituma ndani ya uwanja.

"wachezaji wangu wanapokuwa uwanjani wanakuwa na uwezo wa kutafuta matokeo kwa juhudi kubwa sana na  hilo ni jambo la kujivunia hasa kwa kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi wanazozicheza,"amesema Pluijm.

"Bado tuna kazi ya kuendelea kutunza rekodi kwa kuwa kuna michezo mingi hasa ukizingatia timu zimeongezeka kwa sasa," alisema.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC izidi kuwa kinara wa ligi ikiwa na pointi 33 wakifuatiwa na Yanga ambao wana pointi 29

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kitapumzika kwa siku tatu kabla ya kuanza mazoezi Jumatatu kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Stand United utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Desemba 4, mwaka huu saa 1.00 usiku.

Serikali yakifikiria Kiwanja cha Ndege Bukoba

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwelwe (kulia) leo akimsikiliza Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Bi. Doris Uhagile (katikati), akimpa maelezo mbalimbali wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye kiwanja hicho. Mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyangu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwelwe akipita eneo la ukaguzi wa abiria na mizigo la Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, leo alipofanyua ziara ya kikazi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushari (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Bi. Doris Uhagile (katikati) leo akiwa eneo la ukaguzi wa tiketi za abiria ambapo alitoa maelezo ya namna mashirika ya ndege yavyohudumia abiria kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwelwe. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya TAA, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema.

SERIKALI inafikiria kufanya upanuzi na urefushaji wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Bukoba licha ya changamoto zilizopo, ili kiruhusu kutua kwa ndege kubwa zaidi. Hayo yamesemwa leo (jana) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu ya taasisi zilizopo chini ya Wizara yake, ambapo kiwanja hicho kipo chini ya Mamlala ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Mhe. Kamwelwe amesema bado Kiwanja hicho kinakabiliwa na changamoto endapo kitaongezwa lazima baadhi ya nyumba za Ibada, hospitali na nyumba za kuishi watu zitalazimika kuondolewa ili kupisha upanuzi huo. “Ukiangalia upande mmoja unamakazi ya watu na upande mwingine ni Ziwa Viktoria na mwingine kuna Mlima, hivyo bado tunafanyia kazi hizi changamoto na endapo zitatatuliwa basi miundombinu hii itaboreshwa zaidi kwa kuwa tayari lipo jengo zuri na lenye mfumo mzuri wa maji taka na mifumo mingine mbalimbali,” amesema Mhe. Kamwelwe.

Hata hivyo, amesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) litaongeza safari zake mara mbili kwa siku wenye Kiwanja cha ndege cha Bukoba, kutokana na kuwa na abiria wengi kwa sasa. Mhe. Kamwelwe amesema kwa sasa ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inakuja mara moja kwa siku kwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.

“Kwa sasa abiria wameongezeka zaidi nimeelezwa kuwa kwa mwaka ilikuwa kiwanja kinaweza kuhudumia abiria 28,000 pekee, lakini sasa ni zaidi ya 45,000 kwa mwaka, hivyo inaonesha ni kiasi gani wanavyoongezeka na ndio maana ninasema kutakuwa na uwezekano wa kuongeza safari za ATCL na iwe mara mbili kwa siku balada ya sasa mara moja,” amesema Mhe. Kamwelwe. Amesema serikali tayari imenunua ndege mbili aina ya Airbus 220 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 zitakazowasili nchini Desemba 18 na 23, 2018 tayari kwa safari za maeneo mbalimbali.

Ndege hizi zinaweza kutua kwenye viwanja vya ndege vya daraja la 4C, ambapo kwa sasa ni Songwe na Mwanza, na baada ya ukarabati kukamilika kwenye kiwanja cha Mtwara na kuboreshwa kwa Kigoma, pia itaweza kutua; hali kadhalika pia itatua kwenye viwanja vya Kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA), ambavyo ni daraja la 4E.

Kiwanja cha Ndege cha Bukoba kinajengo la kisasa la abiria, ambalo lilizinduliwa Desemba 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, ambapo mbali na ATCL ndege nyingine zenye ratiba maalum zinazotua ni pamoja na Precision, wakati nyingine zinakuwa zimekodiwa bila kuwa na ratiba maalum kama Auric.

OPERESHENI MIKOA YA KUSINI: JESHI LA POLISI LAKAMATA SHEHENA YA SILAHA NA MILIPUKO NDANI YA MWEZI MMOJA

$
0
0
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, katikati akiwa amenyanyua silaha aina ya AK 47 zilizopatikana katika Operesheni maalum ya kupambana na uhalifu iliyofanyika kuanzia Octoba mwaka huu mpaka Novemba mwaka huu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, katikati akiwa amenyanyua Bomu moja (1) la kurushwa kwa mkono (Hand Grenade – Defensive) lililoko mkono wa kulia na milipuko mingine iitwayo Explosive – Gel V6 iliyokamatwa katika Operesheni maalum ya kupambana na uhalifu iliyofanyika kuanzia Octoba mwaka huu mpaka Novemba mwaka huu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, katikati akionyesha mbolea aina Ammonium Nitrate na Potassium Nitrate zinazotumika kutengenezea milipuko mbalimbali, mbolea hizo zilipatikana katika Operesheni maalum ya kupambana na uhalifu iliyofanyika kuanzia Octoba mwaka huu mpaka Novemba mwaka huu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. (Picha na Jeshi la Polisi).

SAMSUNG WAFUNGUA DUKA JIPYA LA KUUZA BIDHAA ZAKE DAR

$
0
0
*Viongozi wazungumzia ubora wa bidhaa zao, waipongeza Serikali
*Watakaonunua bidhaa kwao kuingia kwenye droo kila siku

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

DUKA kubwa la kisasa linaouza bidhaa za aina mbalimbali za Samsung zenye viwango vya hali ya juu katika ubora limefunguliwa Posta katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Uzinduzi wa duka hilo umefanyika leo Desemba 24 mwaka 2018 ambapo viongozi wa ngazi mbalimbali wa kampuni ya Samsung ndani na nje ya Tanzania pamoja na baadhi ya wananchi wa Jiji hilo wameshuhudia uzinduzi huo uliokwenda sambamba na punguzo la bei pamoja na droo mbalimbali za kujishindia zawadi kwa wanaonunua bidhaa zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo jengo la Askari Posta Mpya jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson amesema Samsung ni bidhaa kubwa duniani na yenye ubora wa uhakika.

“Tumeamua kufungua duka hili eneo la Posta mpya jijini Dar es Saam kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa zetu zinapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.Hatutaki watu wanaohitaji bidhaa za Sumsung wasumbuke kuzipata.
“Tunayo maduka mengi nchini ikiwemo jijini Dar es Saalam lakini umuhimu wa duka hili unatokana na ukweli kwamba kuna bidhaa zote za Samsung ambazo mteja anahitaji kununua kutoka kwetu,”amesema.
1
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la vifaa vya Samsung Posta jijini Dar es salaam leo kulia ni Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung na kushoto ni Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson, , Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung na Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung wakiingia dukani mara baada ya kukata utepe wakati wa uzinduzi huo.
3
Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Graysonmara baada ya kuzinduliwa kwa duka hilo.

PROF. KABUDI AAHIDI KUKISAIDIA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO

$
0
0
Na Ibrahim Mdachi, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) ameahidi kukisaidia Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kuwa anatambua mchango wake katika utoaji mafunzo ya Sheria nchini.

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya 18 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Novemba 23 alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa Chuo hiki katika kutoa mafunzo ya sheria kwa ngazi ya Stashahada na Astashahada na katika kutoa mafunzo endelevu katika fani mbalimbali za sheria.

“Ninaahidi kutimiza wajibu wangu kwa kutoa msaada pale mtakapohitaji na nitakapoona sina budi nitatoa msaada huo hata kama hamjaleta rasmi hitaji lenu kwangu.” Alisema Prof. Kabudi.Akiendelea kuhutubia hadhara ya Wahitimu, Watumishi wa Chuo na Mahakama Wazazi na Walezi wa wahitimu, Prof. Kabudi aliongeza kuwa wahitimu wa chuo hiki wamekuwa mfano kwa jamii kwa uadilifu na maadili kutokana na malezi wanayopata chini ya usimamizi wa Mahakama ya Tanzania.

Alipongeza Uongozi wa Chuo kwa jitihada unazozifanya katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na namna unavyoweza kuzikabili na kuweza kutekeleza jukumu lake la utoaji wa mafunzo sambamba na utekelezaji wa miradi mbalimbali.Sambamba na hayo aliwaasa na kuwasisitizia Wahitimu na juu ya kujiendeleza katika fani ya Sheria ambayo huhitaji kusoma kwani sheria na kanuni hubadilika kila mara na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Mhe. Prof Kabudi aliwataka Wahitimu hao kuendelea kusoma vitabu kwa wingi kwani itawasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku.Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji, Prof. Paul Kihwelo alisema kuwa Chuo kimeendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa Watumishi wa Mahakama ili kuwajengea uwezo zaidi.

“Kwa kutambua umuhimu wake kwa Mahakama ya Tanzania pamoja na kuwajengea uwezo wa utafiti watumishi wake, Chuo kimeendesha mafunzo yaliyowajumuisha Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani Tabora ili kuwajengea uwezo wa namna wanavyopaswa kusikiliza mashauri katika ngazi zao,” alieleza Mkuu huo wa Chuo. 
Mhe. Waziri, mgeni rasmi (aliyeshika kipaza sauti) akiongoza sherehe za Mahafala ya ‘IJA’ Lushoto.
Waziri wa katiba na Sheria akipewa maelezo ya jinsi mfumo wa Kielektroniki wa Menejimenti ya Mafunzo ‘Training Management Information System (TMIS)’ unavyofanya kazi, Mhe. Waziri alizingua rasmi mfumo huo ambao utakuwa ukitoa taarifa ya Mafunzo mbalimbali na kuwezesha kujua ni Watumishi wangapi wa Mahakama waliopatiwa Mafunzo na ambao hawajapata mafunzo.
Meza Kuu katika picha ya pamoja na sehemu ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria.
Meza kuu ikiongozwa na Mhe. Mgeni rasmi (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria.


WANANCHI WA CHANGANYIKENI WAANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA RUVU CHINI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kolobelo akiwa ametembelea moja ya nyumba iliyounganishiwa maji kutoka katika mradi waupanuzi wa huduma ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA).


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo ametembelea miradi ya upanuzi wa huduma ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) inayohusisha ujenzi wa matenki na upanuzi wa mtandao. 


Miradi hiyo itanufaisha Manispaa za Kinondoni na Ubungo na Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo ukiwa unahusisha matenki matano yenye ujazo wa Lita Milioni 6.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhandisi Kalobelo amesema mradi huu ulio mbioni kukamilika umeanza kuonesha manufaa kwa wananchi wa Changanyikeni kuanza kupata maji.

Mhandisi Kalobelo amesema, matarajio ya serikali ni kuona wananchi wanapata maji safi na salama na maji ni rasilimali adimu wananchi wanatakuwa watunze miundo mbinu.Amesema, kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wa Goba, Wazo, Changanyikeni na Salasala ya kukosa maji kwa muda mrefu ila kumalizika kwa miradi hii mikubwa iliyowezeshwa na serikali kupitia Wizara ya Maji wananchi wataanza kunufaika baada ya kuyasubiri maji kwa muda mrefu.

" mradi huu ni wa awamu ya kwanza, kuna mradi wa pili ambao serikali tayari imepata hela kutoka Benki ya Dunia utakaowanufaisha wananchi walio maeneo ambayo hajayanufaika na mradi kwa kwanza," amesema Mhandisi.Amesema kuanzia siku ya Jumatatu Novemba 26, tenki la maji la Changanyikeni litaanza kupokea maji na kufikia Jumatano wananchi watakuwa tayari wameshaunganishiwa maji.

Amewapongeza DAWASA kwa jitihada wanazozionyesha kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji na ametoa rai kwa wananchi wajiunge kwenye mradi huu ili wapate maji safi na salama.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kolobelo (kushoto) akipata maelezo ya mradi kutoka Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprina Luhemeja (wa pili kushoto) akiwa sambamba Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji na Mjumbe wa Bodi ya DAWASA Mhandisi Nadhifa Kemikimba, Mkurugenzi wa Miradi wa DAWASA Mhandisi Lydia Ndibalema.
Wakiwa katika moja ya pampu za kuvuta maji.

MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya ameziagiza taasisi za udhibiti wa bidhaa,chakula na dawa nchini kuhakikisha zinakuwa karibu na wajasiriaamali ili kuweza kuwasaidia badala ya kuwakamata kwa kigezo cha kutokufanya vizuri. 

Hayo ameyazungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Kanda ya Kaskazini ya SIDO alipokuwa akiwahutubia wajasiriamali hao na kusema wataalamu wa taasisi hizo wanapaswa kutoa elimu ya kuwajengea uwezo badala ya kutoza faini. 

Aidha alisema wajasiaramali wengi nchini hasa wadogowadogo bado hawajakuwa na uwelewa mpana wa namna ya kuweka mpangilio mzuri wa maswala mazima ya shughuli zao hivyo wanahitaji kuelimishwa. “Tunao wataalamu toka TBS,TFDA na taasisi nyingine za udhibiti lakini wanatakiwa kuelimisha zaidi badala ya kuwafungia baadhi ya wajasiriamali au kuwatoza faini na haya sio malengo ya Serikali”Alisema Manyanya. 

Manyanya alisema lengo la Serikali hadi kufikia 2025 kufikia katika uchumi wa viwanda jambo ambalo linahitaji nguvu ya ziada ikiwa pamoja na kuwaelimisha wajasiriamali hao na kuwawezesha kimitaji. Hata hivyo aliwataka wajasiriamali wote Nchini kuhakikisha wanaimarisha ubora wa viwango wa bidhaa zao wanazozalisha ili kuendana na ushindani wa soko na kuongeza ubunifu ili waweze kuuza katika nchi za Afrika Mashariki. 
Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya akizungumza wakati akifungua maonyesho SIDO ya Kanda ya Kaskazini yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Joyce Meru
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Joyce Meru akizungumza katika ufunguzi huo
Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya kulia akipata maelezo kutoka kwa Banda la Tanga Fresh.

Viewing all 110144 articles
Browse latest View live




Latest Images