Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Habari za UN toka New York, Marekani, Novemba 22, 2018


Hasunga kufungua mkutano wa Baraza la Kilimo Tanzania.

$
0
0
Waziri wa kilimo Nchini Mh Japhet Hasunga anatarajia kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kisera wa Baraza la Kilimo Tanzania unaotarajiwa kufanyika Nov 26 na 27 mwaka huu jijini Dra es salaam wenye lengo kukusanya maoni ya yahusuyo Sera za Kilimo ili kuona namna zinavyoweza kufanyiwa marekebisho. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko imesema mkutano huo wenye kauli mbiu ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania unatarajiwa kuhudhuliwa na wadau wa sekta ya kilimo zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya nchi.

Bi Janeth alitaja mada zitakazowalishwa katika mkutano huo kuwa ni apmoja na mada kuu ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania, Fursa ya Sekta Binafsi Katika Utekelezaji wa ASDP II, Nafasi ya Vijana na Utekelezaji wa ASDP II ikiwa ni pamoja na Kuimarisha Ushirika kwa Faida ya Wazalishaji.

“ Kwetu Baraza la Kilimo Mkutano huu ni muhimu kwa sababu ndiko tunapopata changamoto za kisera zinazowakabili wadau wa kilimo nchini na kwenda kukaa meza moja na serikali na kuzifanyia kazi, ndio maana utaona tumewaalika wadau wote wa kilimo nchini,

“ Na tumegusa wadau wote wanaojihusisha na mboga mboga, maziwa, mifugo kwa ujumla, kilimo , Uvuvi na yeyote anayeguswa na sekta nzima ya kilimo tunaamini kwa kuwaweka pamoja wote hawa tutatoka na maazimio mazuri yatakayolenga kuendelea kuiboresha sekta ya kilimo nchini” alisema Bi Janeth Bitegeko Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Kilimo Tanzania.

Katika mkutano huo na vyombo vya habari ofisini kwake aliongeza kuwa “ Mambo yote yatakayojadiliwa katika mkutano huu ndio kipaumbele chetu kwa mwaka ujao 2019, kwasababu tumekuwa tukiyafanyia kazi na kumekuwa na matokeo chanya kwasababu sisi tumekuwa tukifanya kazi na serikali kwa karibu zaidi ndio maana unaona masuala mengi yaliyokuwa changamoto kwa wakulima kama vile tozo serikali imekwisha kuyafanyia kazi”.


Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku mbili cha Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo, kulia kwake ni Makamo Mwenyekiti Bi Jacqueline Mkindi . 
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akiwa katika moja ya vikao vya Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania. 

RC GAMBO AANZA ZIARA YA SIKU TATU YA UKAGUZI WA MIRADI MIKUBWA YA MAJI

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameanza ziara yake ya siku tatu katika wilaya za Arusha, Arumeru na Longido kukagua maendeleo ya Miradi Mikubwa ya Maji inayotekelezwa katika wilaya hizo.

Akiwa katika halmashauri ya Jiji la Arusha Gambo ametembelea mradi mkubwa wa Maji unaotekelezwa Jijini humo pamoja na baadhi ya kata za wilaya ya Arumeru.Gambo ameitaka Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafishaji Mazingira Jiji la Arusha AUWSA kuweka kipaumbele katika utunzaji wa vyanzo vya Maji vilivyopo katika mlima Meru ili kuhakikisha miradi hii inayotumia fedha nyingi inakua endelevu.

“Nimewahi kusikia wataalam wa Maji wakisema Vita ya Tatu ya dunia itahusisha kugombea maji, ninaomba sisi tuanze kujihami kwa kutunza vyanzo vyetu vya maji''alisema Gambo

Ameotaka bodi ya AUWSA kuandika andiko la mradi ambalo watalipigia debe katika Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia Mazingira ili kuweza kupata ufadhili wa kampeni hiyo ya utunzaji wa Vyanzo vya Maji. "Itakua haina maana kutumia kiasi kikubwa hivi cha fedha ikiwa baada ya miaka michache ijayo vyanzo vyote vitakauka” alisema Gambo"

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya alisema mradi huo utakamilika Juni mwaka 2020 na wanatarajia Arusha itanufaika na mradi huo kwa kuwa ukosefu wa maji utakua historia.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiangalia moja ya Visima ambavyo ni chanzo cha Maji yanayotarajiwa kuhudumia Jiji la Arusha.
Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto) akipokea maelezo ya mapito ya mtandao wa maji taka. 

Mafundi wa kampuni ya Cheil Engeneering wakiwa katika uchimbaji wa kisima kilichopo wilayani Arumeru
Miundo mbinu ya mfumo wa maji taka, mabwawa haya yanajengwa katika eneo la Terrat pembezoni mwa Jiji la Arusha. Mabwawa haya yanakadiriwa kuwa na uwezo wa kutibu takribaniita Milioni 22 kwa siku za Maji Taka.

MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA.

$
0
0
ZAIDI ya washiriki 5000 kutoka mikoa ya Morogoro,Dodoma,Dar es Salaam ,Iringa na Zanzibar wanataraji kushiriki mbio mpya za Marathoni zijulikanazo kama “Morogoro Marathon 2018” zitakazofanyika katika mji wa Morogoro kwa mara ya kwanza Desemba 2 mwaka huu.

Miongoni mwa washiriki hao wamo pia wanariadha wanaoshiriki mashindano ya Kimataifa wa Tanzania na nchi jirani za Kenya ,Ethiopia na Sudani ya Kusini watakaochuana kuweka rekodi mpya katika riadha kutokana na hali ya hewa ya mji wa Morogoro.

Meneja Uhusiano na Masoko wa taasisi ya uwakala wa Michezo ya Itete “ITETE SPORTS AGENCY” ambao ndio waandaaji wa Mbio hizo ,Dixon Busagaga alisema tukio hilo litakuwa tukio la kwanza kubwa kuwahi kufanyika katika mkoa wa Morogoro na kukutanisha idadi kubwa ya washiriki.

“Kutokana na jiografia ya mkoa wa Morogoro kuwa lango la mikoa ya mikoa ya kusini na kupakana kwa ukaribu na baadhi ya mikoa ya nyanda za kati na Pwani ni wazi matazamio yetu litakuwa tukio kubwa kwa mkoa wa Morogoro”alisema Busagaga.“Tukio hili limebeba maudhui matatu makubwa ambayo ni ,uhamasishaji wa masula ya utunzaji wa Mazingira ,uhamasishaji katika masuala ya Afya pamoja na kutangaza vivutio vya utalii hasa vilivyopo kusini mwa nchi yetu . “alisema Busagaga .

Busagaga alisema hadi sasa vilabu zaidi ya 50 vya mazoezi “Jogging Clubs” kutoka mikoa ya Dar es Salaam ,Dodoma na Morogoro vimewasilisha maombi ya kushiriki katika tukio hilo pamoja na Vilabu zaidi ya 20 vya timu za mpira wa miguu za wachezaji wa zamani yaani Veterani.

“Tukio hili tunataka kulifanya la pekee,tutakuwa na siku mbili za tukio,siku moja kabla ya tukio kubwa la mbio,tutakuwa na shughuli za kuotesha miti zaidi ya 10,000 katika maeneo mbalimbali ya mji wa Morogoro”alisema Busagaga.

“Baada ya tukio hilo ,Timu za Veterani zitakazokuwa zimewasili na kujisalijili kwa ajili ya ushiriki wa Marathoni hiyo tumeandaa mashindano yao kwa jioni ya Desemba mosi ,ambapo washindi wa Bonanza hilo watakabidhiwa zawadi zao na mgeni rasmi siku ya tukio la Marathon.”alisema Busagaga



WIZARA YA MALIASIALI NA UTALII YAWATOA HOFU WATALII

$
0
0

Na. Vero Ignatus Arusha

Siku chache baada ya Benki kuu ya Tanzania kutoa ufafanuzi Juu ya Oparesheni ya Ukaguzi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Jijini Arusha ,Wizara ya Mali asili na Utalii imejitokeza na kusema Zoezi hilo halijaathiri shughuli za Kitalii

Naibu waziri wa maliasili na Utalii Constatine Kanyasu ameyasema hayo wakati lipotembelea taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwenye mkutano wake na wafanyakazi wa shirika la hifadhi za taifa(TANAPA) jijini Arusha na kusema watalii wanaendelea kupata huduma kwani zoezi hilo ni la kawaida na limelenga maslahi ya nchi.

Mara baada ya Mazungumzo hayo Naibu Waziri akiwa nje ya Ukumbi wa Mamlaka hiyo , amezungumza na Wanahabari kisha kugusia suala la oparesheni iliyofanywa na Benki Kuu hivi karibu Jijini hapa.Ameeleza kuwa zoezi hilo lililovishirikisha vyombo vya dola na halijaathiri uchumi katika sekta ya fedha za kigeni hasa kwa upande wa utalii kwa kuwa ni zoezi hilo la mara moja kuwahusisha wanajeshi ambao wanawajibu wa kulinda rasilimali za nchi yao.

'' Wanajeshi hawawezi kuathiri uchumi wa nchi hasa sekta ya utalii kwakuwa wanawajibu wa kulinda rasilimali zetu‘’alisema Kanyasu .Akiongelea suala la migogoro ya Ardhi na mipaka kwa baadhi ya mipaka amesema wizara yake imejipanga kukomesha changamoto hiyo ambayo imekuwa ikitumia fedha nyingi bila kupatiwa ufumbuzi.

Aidha amesema migogoro baina ya Hifadhi na Wananchi,Naibu waziri anasema hakuna mtu ama taasisi inayonufaidika na Migogro hiyo na imekuwa ikichochewa na makundi machache na tayari serikali imekwisha anza kuchukua hatua.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Jumla ya Vijiji mia tatu tisini na mbili vitanufaika na zoezi la upimaji wa matumizi bora ya ardhi lenye lengo la Kupunguza

Migogoro ambapo tumepanga billion 2.5 kwa miradi midogo midogo kuweza kuweka nguvu kwa wananchi kuondoa misuguano isiyo na lazima ambayo inaathiri kiasi kikubwa shughuli za uhifadhi.


Naibu Waziri Wizara ya Mali asili na Utalii Constatine Kanyasu

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI

$
0
0
Na Richard Mwaikenda-Dar .

WANAFUNZI waliomaliza Kidato cha Nne, wametakiwa kuachana na tabia ya kupoteza muda kusubiri kurithi mali za wazazi wao, bali wajitambue kwa kufanya kazi kwa bidii kujiletea maendeleo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Makongo Juu, Dar es Salaam hivi karibuni.

“Kila mmoja ajitambue kivyake,, simama wewe kama wewe, jitambue wewe ni nani, ukijiami kama unaweza na utaweza kweli. Mkome kutegemea kurithi mali za baba zenu,” aliwaaasa Mwamfupe.

“Msiruhusu ndoto zenu zife, hata kama mtakumbana na mazingira magumu majumbani kwenu, mzishikile msiruhusu ndoto zenu zife, Kawaida wewe ndiyo unaamua kuwa tajiri au masikini , utajiri uko kichwani kwako,” alisisitiza Mwamfupe huku akipigiwa makofi na wanafunzi.

Mwamfupe, hakusita kujitolea mfano yeye kuhusu maisha yake ya ujana, ambapo aliwaeleza kuwa licha ya utajiri wa babake, lakini yeye aliamua kujitegemea tangu akiwa anasoma na kwamba alipokuwa ana miaka 19 alinunua gari aina ya Toyota Corola (Mayai).Pia, kupitia kipaji chake cha kucheza mpira na ngoma za asili kilifanya kwa mara ya kwanza apande ndege kwenda Romania kuiiwakilisha Taifa katika Tamasha la Ngoma. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe (Kulia), akimsikiliza mmoja wa wanafunzi aliyekuwa akijieleza jinsi atakavyokabiliana na maisha baada ya kumaliza shule..
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo hayo
Mkuu wa Kitengo cha Vijana cha Taasisi hiyo, Harrison Edger akiwa tia moyo wanafunzi hao.

DKT. NDUGULILE – “SEKTA YA AFYA NCHINI INAKUWA KWA KASI”

$
0
0
Sekta ya afya inakua kwa kasi huku huduma muhimu za afya kwa sasa zikiwa zinapatikana hapa hapa nchini”

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile alipokua akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) iliyopo katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro jana Novemba 22, 2018.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Sekta ya Afya imepewa kipaumbele cha hali ya juu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu mageuzi makubwa ndani ya sekta ya afya yameanza kuonekana huku huduma za matibabu ya kibingwa yakiwa zikipatikana hapa hapa nchini.

“Tunasimama hapa kifua mbele tukiona mabadiliko katika hali ya upatikanaji wa dawa kuimarika zaidi, bajeti ya dawa imeongezeka toka Shilingi Bilioni 30 mpaka Shilingi Bilioni 270 yaani mara tisa zaidi ndani ya miaka mitatu” alisema Mhe.Naibu Waziri na kuendelea “Tumeboresha vituo vya afya takribani 300, huku Mkoa wa Kilimanjaro ukiwa na Vituo 8 vilivyoboreshwa vilivyogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 na kwa mwaka huu 2018 Serikali imeanza kujenga Hospitali za Wilaya 67 nchini”

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya Hospitali mpya za Rufaa za Mikoa ili ziweze kutoa huduma za kibingwa, kupunguza msongamano wa wagonjwa na ucheleweshwaji wa huduma katika Hospitali za rufaa za kanda.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisoma nyaraka za matibabu za Bi. Mary Nyange (kulia) anayepatiwa huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akihojiana na Bw. Longini Mtalo, Mteknolojia kutoka kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC huku akiwa ameshika sampuli ya kiungo bandia kilichotengenezwa na kituo hicho. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua benki ya damu zilizopo katika jokofu Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC. 


UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI

$
0
0


Naibu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Elias John Kwandikwa amewataka wakazi wa mikoa ya Mwanza na Geita kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazojitokeza wakati wa ujenzi wa daraja litakalounganisha eneo la Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.

Amesema maandalizi kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo la aina yake hapa nchini yako katika hatua ya usanifu wa kina hivyo ujenzi wake utaanza mara baada ya mkandarasi wake kutangazwa na linatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 3.2, litakapokamilika. “Hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kazi ya ujenzi iwe nyepesi na wale watakaopata fursa za ajira fanyeni kazi kwa weledi, bidii na nidhamu” amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika miradi ya maendeleo ya muda mrefu hivyo ni jukumu la wananchi kujiandaa na kubaini fursa za kiuchumi na kijamii na kuzitumia. Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya amesema daraja hilo litakuwa na njia nne za kupitisha magari, njia ya waenda kwa miguu ambapo pia litakuwa na kina kitakachoruhusu meli kupita chini ya daraja hilo.

Mhandisi Rubirya amesisitiza umuhimu wa wananchi wenye maeneo yatakayotumika kupisha ujenzi huo kutoa ushirikiano ili kuharakisha kazi hiyo. Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua kivuko cha Kigongo-Busisi na kuagiza Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi kuhusu usalama na matumizi sahihi ya utumiaji wa vivuko.

Amezungumzia umuhimu wa TEMESA kuweka mifumo ya kielektoniki ili kuwezesha waendesha vivuko, wakusanya mapato na wasimamizi kuwa na mawasiliano ya pamoja na hivyo kuwezesha vivuko kuwa na abiria na mizigo inayokubalika wakati wote. Mkuu wa kivuko cha Kigongo –Busisi Mhandisi Abdala Atiki amesema kivuko hicho kwa sasa kinahudumiwa na Mv- Mwanza na Mv- Misungwi ambapo zaidi ya abiria elfu sita na mia tano huvushwa kwa siku.

Zaidi ya mikoa 12 nchini ina maeneo yenye mahitaji ya vivuko ambapo takriban vivuko 30 vinatoa huduma nchini kote.

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya (katikati), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) eneo litakapojengwa daraja jipya linalounganisha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, daraja hilo litakuwa na urefu wa KM 3.2 kulia ni mkuu wa kivuko cha kigongo-busisi mhandisi Abdala Atiki. 
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya (watatu kushoto), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (wapili kushoto) eneo litakapojengwa daraja jipya linalounganisha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, daraja hilo litakuwa na urefu wa KM 3.2 (kulia) ni mkuu wa kivuko cha Kigongo-Busisi mhandisi Abdala Atiki.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (mwenye miwani), akiwasikiliza wanafunzi ambao ni abiria wa kivuko cha Mv- Mwanza kinachotoa huduma kati ya Kigongo-Busisi mkoani Mwanza alipokagua shughuli za uendeshaji wa kivuko hicho.

Mashindano ya kuogelea ya Chipukizi kufanyika Desemba 8 na 9

$
0
0

Mashindano ya kuogelea kwa wachezaji yoso yamepangwa kufanyika Desemba 8 na 9 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji chipukizi kuanzia miaka 12 kushuka chini, yana lengo la kuibua vipaji vya waogeleaji kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali nchini na ya kimataifa.

Inviolata amesema kuwa TSA kwa sasa inatafuta wadhamini wa kufanikisha mashindano hayo. Mwisho wa kuthibitisha ni Novemba 30. “Mashindano haya ni ya kuibua na kuendeleza vipaji, na pia yameandaliwa kwa ajili ya kupima uwezo wa waogeleaji chipukizi ambao wameibuliwa katika mashindano yaliyopita, tunaomba wadhamini wajitokeze,” alisema Inviolata.

Amefafanua kuwa wanatafuta wadhamini kwa ajili ya kusaidia gharama za uendeshaji kwani siyo kazi rahisi mashindano hayo kufanyika bila sapoti kutoka nje. Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.

“Mashindano haya yatatoa fursa kwa waogeleaji ambao walishindwa kushindana katika mashindano ya wakubwa kutokana na kigezo cha umri, kwa vile TSA inatamnbua waogeleaji chipukizi, tumeamua kuandaa mashindano ambao yatawafanya waogeleaji wanaochipukia nao kujipima uwezo wao,”alisema.

Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la waogeleaji waliochini ya miaka saba, waogeleaji wa miaka nane na tisa, 10 na 11 na 12. Washindi wa jumla katika kila kundi atazawadiwa kikombe wakati washindi wa kila shindano watapata medali.

Wachezaji mbalimbali chipukizi wa kuogelea wakiwa katika matukio tofauti 

TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini

$
0
0


Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini imedhamiria kuendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali nchini ili waweze kuzalisha na kukuza biashara zao na kuchangia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. 

Akizungumza leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valley Mutakyamirwa amesema kuwa dhamira yao ni kuendelea kujenga uwezo kwa wajasiriamali hao ili waweze kuchangika katika kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya wanachama wa Taasisi hiyo. 

“ Wajasiriamali hawa ni wanachama wetu hivyo jukumu letu ni kuhakikisha kuwa tunashirikiana nao katika kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ambayo tunashirikiana na Serikali katika kuona namna bora yakuzitatua “; Alisisistiza Mutakyamirwa 

Akifafanua amesema kuwa, Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali ikiwemo kujenga miundombinu, kupunguza kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kutoka asilimia 20 hadi 18 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya Serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya wajasiriamali kufanya biashara. Aliongeza kuwa Warsha hiyo inawasaidia wajasiriamali hao kufanya tathmini ya shughuli wanazofanya na kuja na mikakati ya pamoja itakayoasaidia katika kuimarisha Biashara hapa nchini. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valency Mutakyamirwa akizungumza na washiriki wa warsha ya siku mbili kuhusu uwezeshaji wa wanachama wa Taasisi hiyo leo Jijini Dodoma ikilenga kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja yakuzitatua. 
Meneja Mradi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bi. Veneranda Sumila akisisitiza kuhusu umuhimu wa semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa TPSF leo Jijini Dodoma wakati wa hafla yakufungua warsha hiyo. 
Mratibu kutoka Taasisi ya Best Dialogue Bi. Manka Kway akizungumzia umuhimu wa Maktaba ya Mtandaoni inayoleta pamoja taarifa za wajasiriamali wa Tanzania ikiwemo tafifi mbalimbali zinazofanyika zikilenga kuchangia katika kukuza biashara hapa nchini. 
Muwezeshaji wa masuala ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Patrokil Kanje akizungumzia namna wajasiriamali wa Tanzania wanavyoweza kukuza na kuendeleza biashara zao kwa kutumia mbinu za kisasa wakati wa warsha ya wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi. 
Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wachimbaji wa Madini na Nishati Tanzania (TCME) Bw. Gerald Mturi akizungumzia umuhimu wa semina hiyo kwa wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi. 

DKT. NDUGULILE AZIDI KUZISISITIZA NGOs KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA TAIFA

$
0
0
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezidi kuyasisitiza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa na Serikali
katika kutekeleza miradi ya Maendeleo nchini.

Ameyasema hayo mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya siku tatu kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali katika sekta ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.  Dkt. Ndugulile amesema kuwa nia ya Serikali sio kuyabana Mashirika hayo ila kuyaratibu ili yaweze kufanya kazi katika mazingira mazuri ambayo yatawezesha kuwa na mgawanyiko mzuri wa rasilimali katika maeneo mbalimbali nchini.

Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameutaka uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuweka vipaumbele na kuzielekeza NGOs sehemu za kwenda na sio kuziweka NGOs nyingi mahala pamoja.  Dkt. Ndugulile pia amezitaka NGOs kufanya kazi katika misingi ya uwajibikaji na kufuata Sheria na taratibu za nchi ili kuendeleza ushirikiano kati yao na Serikali katika kuchangia juhudi za wananchi kupata Maendeleo jumuishi.  “Unakuta sehemu moja zimerundikana NGOs nyingi na mkoa huo huo maeneo mengine hakuna NGOs hata moja” alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mgwira amesema Mkoa wake unapambana na changamoto mbalimbali katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii na kuiomba Wizara kushirikiana nao ili kutatua changamoto zinazoukabili mkoa wake.  “Nikushukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kutukumbuka kuja kututembelea ila naomba mtuangalie kwa jicho la tatu katika kutatua changamoto zetu hapa mkoani” Alisisitiza Mhe. Anna.

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Best Magoma amesema huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii zinazingatiwa na kuangaliwa kwa ukaribu ili kuendelea kumuwezesha mwananchi kufaidika na huduma hizo.  Msisitizo huu kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufuata vipaumbele
vya taifa umekuja baada ya Serikali kuyataka Mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo nchini.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu kufuatilia utekelezaji wa sera na programu katika Sekta ya Afya na
Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mgwira (kulia) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo kuhusu kuwaelekeza wadau wa NGO kupanga utekelezaji wa miradi yao kwa kufuata vipaumbele na kuwapangia sehemu sahihi wadau hao kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni ili kuleta usawa katika mgawanyo wa rasilimali kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza Mzee wa miaka 98aliyejulikana kwa jina la Daniel Mzava alipotembelea Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile  kimjjulia hali mmoja wa Mtoto aliyekuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi wakati wa ziara yake Hospitalini hapo.  Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

mkutano wa mwaka Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI) wafanyika jijini Dar

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw Hisham Hendi akitoa mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali katika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Nyuma ni Mkurugenzi wa Muendeshaji wa kampuni ya FSDT, Bi Irene Mlola na Mwenyekiti wa DTBi, Bw Mihayo Wilmore. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Universal Communication Service Access Fund (UCSAF), Peter Ulanga akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI) uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema jana. Mkutano huu umelenga kujadili ukuaji wa uchumi wa kidijitali. 
  Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw Hisham Hendi akichangia mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali kaatika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Universal Communication Service Access Fund (UCSAF), Peter Ulanga
 Mshauri wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI, Bw Anael Ndosa, akichangia mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali kaatika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

WATU 80 WAMEFARIKI KWA KIPINDUPINDU HADI SASA, VIFAA VYA LIFESTRAW SULUHISHO KUOKOA JAMII

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

WAZIRI wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amezindua huduma ya maji safi na salama kwa jamii mradi unaotekelezwa na kampuni ya Lifestraw nchini ambayo imezindua vifaa maalumu na vya kisasa ambavyo huchuja na kusalimisha maji vyema kabisa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Ummy amesema kuwa Lifestraw wanastahili pongezi  kwa hilo walilolifanya na ni njia ya kufikia malengo ya kufikia asilimia 80 ya kutoa huduma ya maji safi na salama katika jamii.

Amesema kuwa kuanzia mwezi Januari hadi leo watu 4406 wameugua kipindupindu  na kati yao watu 80 walipoteza maisha na tatizo hilo halisababishwi na kula kinyesi pekee pia ni kutokana na ukosefu wa maji safi na vyoo, pia amesema kuwa asilimia 60 ya wagonjwa wa nje (OPD) wanaotibiwa katika hospitali hukutwa na magonjwa yanayotokana na kukosa maji safi na salama, matumizi yasiyo sahihi ya vyoo na unawaji wa mikono mara baada ya kutumia vyoo.

Aidha amesema kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya maji wanahakikisha kuwa maji yanayosambazwa yanawekwa kinga maalumu ya kuua vijidudu katika maeneo yote na hasa yale yanayokumbwa na ugonjwa wa kipindupindu ikiwemo Mikoa ya Dar es salaam,  Pwani,  Arusha, Manyara na Singida.

Vilevile amewapongeza Lifestraw kwa kutumia teknolojia ambayo imethibitishwa na mamlaka husika nchini kuwa vifaa hivyo vinaweza kuua vijidudu kwa asilimia 99.999 na kuyaacha maji yakiwa salama kabisa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Lifestraw nchini Fatma Mahsen amesema kuwa uzinduzi huo wa vifaa vya kuhifadhia maji ni mkakati wa kusaidia jamii katika kuhifadhi maji safi na salama kwa  matumizi ya jamii.

Fatma amesema vifaa hivyo ni salama na huhifadhi maji kwa usalama na hudumu kwa muda mrefu na watahakikisha wanasimamia hilo ili kila mwananchi anapata huduma ya maji safi na salama ili kuweza kufanikisha malengo ya kufikia asilimia 80 ya kutoa huduma ya maji safi na salama na kutokomeza kabisa mlipuko wa magonjwa yanayotokana na ukosefu wa maji safi hasa kipindupindu.

Pia Benjamin Filskov kutoka Water Mission Tanzania amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa watu bilioni 2.1 wanakosa maji kwa mwaka na zaidi ya watu 842,000 hufa kila mwaka kwa kukosa maji safi na salama hali inayosababishwa na mlipuko wa magonjwa hasa kipindupindu.

Imeelezwa kuwa katika mradi huo unaojumuisha nchi 20 ikiwemo Tanzania utasaidia kuboresha huduma za upatikanaji wa maji safi na salama na hadi sasa asilimia 61 ya huduma hiyo ya kutumia vifaa maalumu kwa ajili ya kuhifadhia maji imefanikiwa katika maeneo mbalimbali.

TFDA YATOA ELIMU YA KUANZISHA VIWANDA KWA WASINDIKAJI WADOGO WA VYAKULA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Na James Ndege - Shinyanga
TFDA inaendesha mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali wadogo wa usindikaji wa vyakula mkoani Shinyanga ikiwa ni mojawapo ya mikakati yake ya kuwezesha ukuaji wa Sekta ya  viwanda nchini kwa wasindikaji 100 wa mkoa huo  kuanzia tarehe 22 – 23 Novemba 2018 katika Ukumbi wa SIDO Mkoa, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Jasinta Mboneko kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Zainab R. Telack ambaye aliwaasa wasindikaji wa vyakula hao kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ili waweze kukidhi vigezo muhimu vya kisheria na kuzalisha bidhaa bora, salama na zenye ufanisi ili kukidhi soko la ndani na nje ya nchi jambo litakalochangia ukuaji wa uchumi wa nchi lakini pia kulinda afya ya jamii kwa kuwa TFDA ipo karibu na kundi hili muhimu katika uanzishaji wa viwanda nchini kwa kutatua changamoto zao.
“Kafanyeni kazi zenu kwa kufuata mafundisho mtakayopewa, tunawategemea kwamba ninyi mtakuwa mabalozi wazuri kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wengine, kwenye Mkoa wetu tumejipanga kuhakikisha kwamba kila mmoja anafanya shughuli zake zilizo halali, hakuna ujanja ujanja kwenye Serikali ya awamu hii ya Awamu ya  Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Nadhani ninyi nyote mmeona kwenye vyombo vya habari kilichotokea Kahama kwa Wafanyabishara wasiotaka kufuata sheria.
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akifungua mafunzo ya siku mbili tarehe 22 – 23/11/2018 kwa Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Shinyanga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Zainab R. Telack katika Ukumbi wa SIDO wa Mkoa wa Shinyanga. Kulia, ni Mkaguzi Mkuu wa Chakula wa TFDA, Lazaro Mwambole na kushoto ni Mwenyekiti wa mafunzo hayo Juma Nyankanga
Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Justin Makisi akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo (hawapo pichani). Kushoto, ni Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko na kulia ni Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe
Sehemu ya wasindikaji wa vyakula wa mkoa wa Shinyanga wakifuatilia mada zilizotolewa na TFDA katika mafunzo hayo.
Sehemu ya picha ya pamoja baina ya Mgeni Rasmi, Watumishi wa Serikali na Wasindikaji wa chakula wa mkoa wa Shinyanga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BREAKING NEWZZZZZ:MAHAKAMA YA KISUTU YAFUTA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO

$
0
0
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta dhamana ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mining Ester Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 23.2018 dakika chache zilizopita na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

TUTAWALETEA HABARI KAMILI BAADAE KIDOGO.


BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN

$
0
0
Uongozi wa Chuo cha Kimataifa cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman umekusudia kuanzisha chuo chengine kipya cha Kimataifa Visiwani Zanzibar kitachopewa jina la American and Europe of  East Africa kwa lengo la kutanua Sekta ya Elimu ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini humo Dr. Muneer Moh’d Al – Naamany alitoa kauli hiyo wakati Ujumbe aliouongoza wa Chuo hicho ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Dr. Muneer Moh’d Al – Mastar alisema Zanzibar lazima iwe kituo cha Elimu katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika kitakachomjengea uwezo wa ajira ya kuaminika mahali popote Duniani Mwanafunzi aatakayemaliza masomo yake kwenye Chuo hicho.

Alisema mazingira ya kumfinyanga Mwanafunzi katika muelekeo wa chuo hicho kinachokusudiwa kuanzishwa Zanzibar unatokana na uzoefu wa miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Chuo chao chenye Wahadhiri kutoka pembe zote za Dunia wanaofundisha kwenye Taasisi yao.

Mkuu huyo wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Oman mwenye Asili ya Zanzibar alimueleza Balozi Seif kwamba Uongozi wa Chuo chake umefikiria Mpango huo kwa nia ya kuirejeshea hadhi yake Zanzibar kuwa Kituo cha masuala mengi katika enzi zilizopita hasa harakati za Biashara na usafiri uliokuwa ukiunganisha Dunia.

Naye kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman Dr. Ahmed Al – Naamany alisema mfumo wa ufundishaji utakaotumika utampa uwezo Mwanafunzi kuendelea na masomo yake hata akiwa nje ya Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na Uongozi wa Chuo cha Kimataifa cha Sayansi na Biashara  cha Nchini Oman uliofika Ofisini kwake Vuga kwa mazungumzo ya kuataka kuanzisha Chuo Kikuu Visiwani Zanzibar.
 Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini humo Dr. Muneer Moh’d Al – Naamany wa Pili kutoka Kulia akielezea msimamo wa Uongozi wa Chuo chake kutaka kuanzisha Chuo Kikuu Visiwani Zanzibar.
 Dr. Muneer Moh’d Al – Naamany akisisitiza jambo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
 Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman Dr. Ahmed Al – Naamany akimueleza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma aliyeshiriki mazungumzo hayo fursa zitakazopatikana katika mafunzo yatakayotolewa na Chuo hicho.
  Dkt. Muneer Moh’d Al – Naamany akifafanua zaidi malengo ya Chuo chake mbele ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA

$
0
0
Na Munir Shemweta, Babati
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepiga marufuku halmashauri zote nchini kupima viwanja kwa shinikizo la wamiliki wa mashamba makubwa na kusisitiza kuwa kazi hiyo inapaswa kufanywa na  halmashauri ambazo ndizo zenye jukumu la kupanga miji nchini.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singu wilaya ya Babati mkoani Manyara Lukuvi alisema uamuzi wowote wa kupima viwanja unatakiwa kuratibiwa na halmashauri husika kwa kuzingatia mipango miji na si vinginevyo kwa kuwa mwenye  dhamana ya kupanga miji ni halmashauri. Agizo la Waziri Lukuvi linafuatia kuelezwa na halmashauri za wilaya ya Babati kuhusu mpango wa kupima viwanja katika eneo la shamba la Singu Estate linalomilikiwa na kampuni ya Agric Evolution Ltd .

Lukuvi ameziagiza halmshauri za Mji na ile ya wilaya ya Babati kuainisha mipaka na kupima eneo la vijiji vya Singu, Sigino na Daglailoy vilivyopo kata ya Singu wilaya ya Babati sambamba na kuvipatia hati vijiji vyote na kubainisha kuwa zoezi la kugawa viwanja katika  shamba linalomilikiwa na kampuni ya Agric Evolution ltd litafanyika baadaye kwa utaratibu utakaopangwa.

Lukuvi alisema ameamua kusitisha ugawaji viwanja baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu sambamba na baadhi ya wawekezaji kununua mashamba katika maeneo ya mjini kwa nia ya kuzishawishi halmshauri kupima viwanja badala ya halmashauri kupima kulingana na mipango yake. " kumekuwa na mtindo wamiliki wa mashamba wanachukua maeneo ambayo wanaona yanakaribia kuwa miji kwa lengo la kupima viwanja na kuwalambisha asali  watendaji wa halmashauri ili malengo yao yatimie" alisema Lukuvi.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singu wilaya ya Babati mkoani Manyara wakati wa ziara ya siku moja kutatua mgogoro  wa ardhi baina ya wananchi na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago.
 Mbunge wa jimbo la Babati Paulina Gekul akitoa shukuran kwa  Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi kwa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 baina ya wananchi wa Singu na Endasago na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago.

 Wananchi wa vijiji vya Endasago na Dudiye vilivyopo wilaya ya Babati mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati wa ziara ya siku moja kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi akifurahia jambo na mbunge wa jimbo la Babati Paulina Gekul (kulia) wakati wa ziara ya siku moja kutatua mgogoro wa ardhi  baina ya wananchi na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago. Co Ltd.(Picha zote na Wizara ya Ardhi)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

REA AWAMU YA III MZUNGUKO WA PILI KUNUFAISHA VIJIJI VILIVYOSALIA KUANZIA JUNE 2019

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

MWELEKEO wa mradi wa wakala wa umeme vijiji (REA III )mzunguko wa pili unatarajia kuanza June 2019 ,ili kuvifikia vijiji ambavyo vimesalia katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya kwanza.
 Aidha mradi wa ujazilizi unatarajiwa kuanza mwezi machi mwakani huku mradi wa peri -urban utakaohusisha mkoa wa Pwani na Dar es salaam unategemewa kupata mkandarasi Januari mwaka huo na umeshatengewa sh.bilioni 83.

Naibu waziri wa nishati, Subira Mgalu alieleza hayo katika kikao cha madiwani cha kata kwa kata kilichofanyika Lugoba Chalinze, mkoani Pwani ,wakati akitolea ufafanuzi utekelezaji unavyoendelea wa miradi ya umeme vijijini na mipango ya miradi hiyo ya kimkakati .

Alisema, kwa jitihada zote hizo za serikali kutekeleza miradi ya vijijini tayari vijiji 4,702 vimeshafikiwa hadi sasa . Subira alisema maeneo yote iliyolengwa wakandarasi wanaendelea na kazi. Kwa mujibu wake ,mkoa wa Pwani katika REA awamu ya III vipo vijiji 150 ,ambapo baadhi ya vijiji vimeshawekwa miundombinu na vingine mita .

Alilielekeza shirika la umeme (TANESCO) kuendelea kusambaza umeme kwenye maeneo ya wananchi pasipo kusubiri utekelezaji wa mradi wa REA. "Serikali inafanya kazi ,nia yetu ni ushindi na sio ushindi tuu katika chaguzi zinazokuja bali tuwe na majibu ya namna tunavyotekeleza ilani vijijini na vitongojini" alisisitiza Subira.

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ,Saidi Zikatimu aliiomba serikali kuwa, vijiji vinavyopitiwa na umeme vifikie vitongoji vyake na kufikia vijiji ambavyo tangu dunia iumbwe havina umeme. Diwani wa kata ya Miono ,Juma Mpwimbwi alieleza bado kuna tatizo la ukosefu wa umeme kijiji cha Mkwajuni na Makaomakuu ambapo tangu wapimiwe nguzo hawajapelekewa vifaa wala kuandaa miundombinu .

Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Serikali imedhamiria kujenga Vituo vya Polisi 65 katika wilaya mbalimbali nchini ikiwa ni juhudi za kukabiliana  na uchakavu na upungufu wa vituo vya polisi nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Polisi cha Songe ambacho ndio kituo kikuu katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga
Alisema Serikali inatambua changamoto za vituo vya polisi ikiwemo uchakavu, udogo wa majengo katika vituo mbalimbali nchini na iko katika mpango wa kujenga vituo vya polisi 65 ili kuwepo na ulinzi thabiti wa raia na mali zao.
“Serikali inatambua changamoto ya vituo vya polisi hasa katika wilaya mpya nchini, ikiwepo uchakavu wa majengo, kwahiyo uko mkakati maalumu wa kujenga vituo vya polisi 65 nchi nzima ili kuweza kukabiliana na matukio ya kiuhalifu, lengo la serikali ni kuhakikisha raia wake na mali zao zinakua salama na matukio ya kiuhalifu yanapungua na kutoweka kabisa,” alisema Masauni
Alisema Serikali pia inakaribisha nguvu za wananchi na wadau mbalimbali ambao wako tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi huku akipongeza baadhi ya maeneo nchini ambako vituo vya polisi vimejengwa kwa ushirikiano wa michango ya wananchi na serikali.
 Naibu  Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akiwaongoza  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  kuingia  Kituo  cha  Polisi  cha  Songe, ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga .Picha  na  Wizara  ya Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi 
 Naibu  Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga . Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo na Kulia ni Katibu  Tawala  wa  Wilaya  hiyo,  Warda  Abeid.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo  akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga . Kulia ni  Katibu  Tawala  wa  Wilaya  hiyo, Warda  Abeid.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi , Edward Bukombe, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani, ) kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga . Picha  na  Wizara  ya Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images