Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

CHUO CHA MISITU OLMOTONYI WAMFIKISHIA KILIO NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU

$
0
0
Watumishi wa Chuo cha Misitu cha Olomotonyi wamemuomba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ashughulikie changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo. 

Pia, watumishi hao wamesema wamekuwa hawapandishwi vyeo kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likishusha ari ya kufanya kazi kwa bidii.
Wameyasema hayo leo mbele ya Naibu Waziri Mhe. Kanyasu wakati alipokuwa akisikiliza changamoto za watumishi wa Chuo hicho jijini Arusha ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo .

Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wenzake, Mkufunzi wa Chuo hicho, Philipina Shao amesema kwa muda wa miaka 12 hajapandishwa cheo na kwa sasa anakaribia kustaafu. Mbali na malalamiko hayo, Watumishi hao wamemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Chuo hicho kimekuwa kama gereza kwa vile baadhi ya watumishi ambao wameonekana kufanya vibaya maeneo mengine huhamishiwa katika Chuo hicho kama adhabu. 

Wakizungumzia kuhusu watumishi hao ambao wamekuwa wakihamishiwa katika Chuo hicho kuwa wengi wao huwa wamebakiza miaka michache kustaafu, hivyo wanakuwa hawana mchango wowote kwa Chuo. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Watumishi wakati alipowatembelea leo katika Chuo cha Misitu cha Olmotonyi jijini Arusha ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aliposhika nyadhifa hiyo.( Picha na Lusungu Helela-MNRT) 
Makamu Mkuu wa Chuo cha Misitu cha Olmotonnyi Bw.Steve Kigwere akisoma taarifa mbele ya Naibu Waziri, Mhe. Kanyasu wakati alipotembelea leo Chuo hicho kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.( Picha na Lusungu Helela-MNRT) 
Mkufunzi wa Chuo cha Misitu Olmotony,Charles Giliba akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mhe, Kanyasu, wakati alipotembelea jana Chuo hicho kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi .( Picha na Lusungu Helela-MNRT) 


Kesi ya Wanaodaiwa kumuua Dkt. Mvungi yaanza kuunguruma upya

$
0
0
  Watuhumiwa sita wanaodaiwa kumuua aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr. Edmund Sengondo Mvungi wakitoka mahakamani  baada ya kusomewa mashatka yao leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Watu sita wanaodaiwa kumuua aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr. Edmund Sengondo Mvungi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la mauaji.

Washtakiwa hao ambao wamesomewa shtaka hilo Leo Novemba 22. 2018 na wakili wa Serikali Lilian Rwetabula mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Agustina Mbando kuwa ni, Msigwa Matonya(35), Mianda  Mlewa(45), Paulo Mdonondo(35), Longishu Losindo(34), Juma Kangungu(34) na John Mayunga(60).

Katika kesi hiyo, mpya ya mauaji namba 6, 2018,  washtakiwa hao wameshtakiwa kwa kosa la mauaji ya kukusudia  kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

 Mapema leo asubuhi, washtakiwa hao waliachiwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kuindoaa kesi hiyo chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya makosa ya jinai (CPA). Hatua hiyo imefikwa baada ya wakili wa  Serikali Nassoro Katuga kuiomba mahakama kufuta kesi hiyo kwa kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi  ya washtakiwa.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Lilian amedai, Novemba 3 mwaka 2013 huko Kibwerenge Msakuzi eneo la Mbezi, washtakiwa walimuua Dr Mvungi. Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji

Kabla ya kuahirishwa kesi hiyo, wa shtaka hao walidai kuwa, hiyo siyo kesi mpya,  llikuwa inaendelea kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sam Rumanyika lakini upande wa mashtaka wameamua kuindoa na kuileta upya hapa Kisutu.

Pia washtakiwa hao wameiomba mahakama iwaeleze upande wa mashtaka wakamilishe upelelezi kwa haraka kwani hakuna chochote kipya kwa sababu hakuna ushahidi mpya zaidi ya ule ule uliosomwa kwenye Committal( maelezo ya mashahidi). Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 6, 2018 kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Jumia yakabidhi luninga, kutoa bodaboda Ijumaa hii!

$
0
0
Ni kupitia zoezi la ‘Treasure Hunt’
Luninga hiyo inauzwa shilingi 570,000 mtandaoni lakini mteja auziwa kwa shilingi 5,700!
Ijumaa hii bodaboda yenye thamani ya shilingi 1,850,000/- itauzwa kwa shilingi 18,500 tu kwa mteja atakayeipata. 

 Jumia imetangaza kutoa pikipiki aina ya Skymark yenye thamani ya shilingi 1,850,000 kupitia zoezi la ‘Treasure Hunt’ siku ya Ijumaa ya kesho. Zoezi hilo litafanyika kupitia App ya Jumia kwenye simu za mkononi pekee ili kutoa fursa kwa kila mtu kushiriki muda na mahali popote walipo. Mshindi mwenye bahati atakayefanikiwa kuipata pikipiki hiyo atauziwa kwa bei ya punguzo la asilimia 99 ambayo ni sawa ni shilingi 18,500 tu!

Jumia inaendesha kampeni yake kubwa kabisa ya mauzo ya mwaka inayokwenda kwa jina la Black Friday. Kampeni hii ilizinduliwa Novemba 16 na itafikia ukomo mnamo Desemba 7. Tofauti na miaka mingine ambayo Jumia hufanya Black Friday kwa siku moja tu ya Ijumaa ya Novemba 23, mwaka huu wateja watafaidi ofa za Black Friday kwa Ijumaa nne mfululizo. Lengo kubwa la kampeni hii ni kuwarahisishia wateja na watanzania kwa ujumla kufanya manunuzi yao hususani kipindi cha msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya ambazo zipo njiani wiki chache zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey amefafanua kuwa, “zoezi la kuficha bidhaa mtandaoni ili wateja kuzisaka na kujishindia au ‘Treasure Hunt’, ni mojawapo ya vitu vichache vinavyoendelea katika kampeni hii ya Black Friday. Miongoni mwa ofa zinazopatikana ni pamoja na punguzo la bei mpaka asilimia 70 na mauzo ya bidhaa maalum kwa bei nafuu zaidi ndani ya muda mfupi ndani ya siku au ‘Flash Sales.”
Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey akizungumza na Wanahabari leo jijini Dar kuhusu ufafanusi  wa  “zoezi la kuficha bidhaa mtandaoni ili wateja kuzisaka na kujishindia au ‘Treasure Hunt’,alisema na kuongeza kuwa ni mojawapo ya vitu vichache vinavyoendelea katika kampeni hii ya Black Friday. Kijanga amebainisha kuwa Miongoni mwa ofa zinazopatikana ni pamoja na punguzo la bei mpaka asilimia 70 na mauzo ya bidhaa maalum kwa bei nafuu zaidi ndani ya muda mfupi ndani ya siku au ‘Flash Sales.”


HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI

$
0
0
Na Francis Godwin,Iringa

MWENYEKITI  wa  bodi ya  shirika la  umeme Tanzania  (TANESCO )  Dkt   Alexander Kyaruzi amesema  kuwa  hali ya  uzalishaji  wa  umeme  nchini  ni  nzuri na  kuwa   watanzania  wasitegemee  kuwepo  kwa mgao   wa  umeme  kwa  mwaka  huu.

Akizungumza  wakati  wa   hafla ya  uwashaji  umeme  kijiji  cha  Ndolezi katika  Halmashauri ya  mji Mafinga  Dkt  Kyaruzi  alisema  kuwa  pamoja na  kuwa  kipindi cha  kiangazi  kinakwenda  kumalizika ila hali ya maji  katika  vituo  vya uzalishaji  umeme  vya Kidatu na Mtera  ni  nzuri  na kuwa maji hayo yataendelea  kuongezeka  zaidi kwani msimu wa masika  unakaribia.

Kuhusu   kasi ya  usogezaji wa  umeme  katika  vijiji  ,vitongoji  na  maeneo ya  visiwa alisema  kuwa  kasi  inaendelea   vizuri na  kuwa  hadi  mwaka 2021  maeneo  yote ya  nchi umeme  utakuwa  umefika na  hakutakuwa na kijiji  wala  kisiwa  ambacho  wananchi  watakuwa  hawana  umeme .

Pamoja na  umeme    huo  wa maji na  gesi  ambao  unatumika  kwa sasa bado  alisema  shirika  limeendelea  na uvumbuzi  wa  vyanzo  vingine  vya  umeme kama  umeme wa  joto ardhi  ambao tafiti  zinaonyesha  baadhi ya  mikoa kama  mkoa  wa Mbeya  kuwepo  kwa  umeme   huo .

"  Tunategemea  miaka  mitano mbele  kuwa na umeme  utakaozalishwa   kupitia  joto  ardhi   hivyo  bado  nchi  itaendelea  kuwa  na  uhakika  wa  umeme baada ya  kuwa na  vyanvyo  tofauti  tofauti "  alisema  Dkt  Kyaruzi

Alisema  kuwa maeneo    Ziwa  ngozi  mkoani  Mbeya  ni  eneo la kwanza  ambalo  wamefanikiwa  kufanya  utafiti na  kuonekana  lina weza  kuzalisha  umeme  wa  joto  ardhi na  tayari  wamempata  mkandarasi  wa kufanya  zoezi la  uchimbaji  wa eneo hilo .
 Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Ali  Hapi mwenye  suti  nyeusi na mkurugenzi wa bodi ya Tanesco Dkt Alexander Kyarusi kulia  wakiwasha  umeme  kijiji cha Ndolezi Mafinga mkoani Iringa
 Mkuu wa  mkoa wa Iringa Alli Hapi  akisikiliza kero za  wananchi juu ya umeme wilayani Mufindi jana
 Mwenyekiti wa  bodi ya Tanesco Dkt Alexander Kyaruzi (kushoto) akifuatilia taarifa ya meneja wa Tanesco Mafinga  wakati wa uwashaji  umeme kijiji cha Ndolezi
Wananchi Mufindi wakitoa kero zao kwa  mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi  wakati wa  kuwasha umeme kijiji cha Ndolezi Mafinga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

VETA kuratibu mashindano ya ubunifu wa ufundi stadi, sekta isiyo rasmi

$
0
0
Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yamezinduliwa rasmi tarehe 14 Novemba 2018 huku Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikipewa jukumu la kuratibu mchakato wa mashindano katika makundi mawili ambayo ni Wabunifu wa Ufundi Stadi na Wabunifu wa kutoka Sekta Isiyo Rasmi, hivyo kupata majina matano ya kila kundi kuingia kwenye fainali.

Akizindua mashindano hayo sambamba na Mwongozo wa Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia, kwenye Ukumbi wa Kambarage, Nyerere square jijini Dodoma, Waziri wa sayansi na teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema mashindano hayo yataongozwa na kaulimbiu ya “Kukuza Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda,” na yatahusisha makundi mbalimbali ya wabunifu wa kisayansi, teknolojia katika maeneo na nyanja mbalimbali nchini kote, ambapo kilele chake kitakuwa Januari 2019.

Alisema ili nchi yetu iweze kunufaika na matokeo ya ubunifu, uvumbuzi na maarifa asilia, kuna umuhimu wa kuwahamasisha wagunduzi, wabunifu na wamiliki wa maarifa asilia.

“Kwa hiyo, mashindano haya yatasaidia kuibua vipaji na kuhamasisha uendelezaji wa teknolojia na ubunifu utakaoweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo endelevu ya viwanda, kuongeza tija ya uzalishaji wa malighafi, kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuboresha shughuli nyingine za kiuchumi. Kutokana na kutambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu, Wizara yangu ina mpango wa kufanya mashindano haya yafanyike kila mwaka ili uibuaji wa vipaji vya namna hii uwe endelevu,  ” alisema.

Aliongeza kuwa Mwongozo wa Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia utakuwa ni nyenzo ya kuongeza ufanisi wa taasisi zinazoshughulikia masuala ya ugunduzi, ubunifu na umiliki wa maarifa asilia.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

RC MTWARA: SERIKALI IMELIPA TSH BILIONI 4.6 KWA WAKULIMA 4871 NA KUKUSANYA TANI 130,111 ZA KOROSHO

MTIBWA SUGAR KUTUMIA UWANJA WA AZAM COMPLEX MICHUANO YA SHIRIKISHO AFRIKA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Klabu ya Mtibwa Suga ya Turiani Morogoro inayowakilisha Tanzanaia katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwa msimu wa 2018/2019 wanatarajia kutumia Uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa nyumbani.

Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi November 27 na 28 mwezi huu Mtibwa Sugar wamepangiwa kucheza dhidi ya Nothern Dynamos ya Usheli sheli.Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kupeperusha bendera kimataifa katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya Norhen Dynamo ya Shelisheli.

"Tumebeba dhamana ya watanzania katika michuano hiyo kazi yetu kubwa ni kuweza kupata matokeo hilo ndilo jukumu ambalo nimewapa wachezaji wangu, wote wanalitambua hilo," alisema. Mtibwa Sugar wanaingia kwenye michuano hiyo baada ya kukamilisha adhabu yao ambayo walipewa ya kutoa faini baada ya kushindwa kupeleka timu kwenye michuano hiyo nchini Afrika kusini kutokana na Ukata. 

Wana tam tam wanatarajia kuanzia uwanja wa nyumbani katika kutupa karata yao ya ushiriki wao katika michuano hiyo na uongozi wa juu wa klabu hiyo kupitia kwa msemaji wao Thobias Kifaru tayari umethibisha kuwa watatumia uwanja wa Azam Complex,Chamazi katika michuano hiyo kwa michezo ya nyumbani. 

“kila mmoja anajua tunatumia uwanja wa Manungu kama uwanja wetu wa nyumbani pia tunautumia uwanja wa Jamhuri kwa michezo miwili tu ya ligi kuu dhidi ya Simba na Yanga lakini katika michuano hii ya kimataifa tumeshindwa kutumia viwanja hivi viwili kutokana na viwanja vyote viwili kutokidhi hadhi ya kimataifa ya michuano hiyo hivyo tumeamua kuutumia uwanja wa Azam Complex uliopo Mbande ,Mbagala, hivyo tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi” Kifaru 

Mtibwa Sugar wamepangiwa kucheza dhidi ya Nothern Dynamos ya Usheli sheli katika kombe la shirikisho na baada ya mchezo huo wa jijini Dar es saalaam wana tam tam watasafiri kuelekea Usheli sheli kwa ajili ya mchezo wa pili wa marudiano na mchezo wa marudiano utachezwa kati ya Desemba 4 au 5.

Rais Magufuli amteua Dkt. Lutengano Mwakahesya kuwa Mwenyekiti wa PBPA


Mashindano ya Riadha kwa Wanawake "Ladies First" Kufanyika Dar

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Mkenyenge (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24-25 Novemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JICA) Bw. Toshio Nagase na kushoto ni Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha nchini (RT) Bi. Ombeni Zavala.
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JICA) Bw. Toshio Nagase akifafanua  jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24-25 Novemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Mkenyenge na kushoto ni Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha nchini (RT) Bi. Ombeni Zavala.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha nchini (RT) Bi. Ombeni Zavala akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24-25 Novemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Mkenyenge na kulia ni ni Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JICA) Bw. Toshio Nagase.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JICA) Bw. Toshio Nagase (wa pili toka kushoto) wakati wa kutangaza mashindano ya riadha kwa wanawake yanayoitwa “Ladies First” yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24-25 Novemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM- Dar es Salaam.

Dereva Boda Boda anayekimbiza kwenye Bongo Star Search

$
0
0
“…sikuwa nafahamu, aliniambia usaili unafanyika Club Next Door wahi uende ukajaribu bahati yako huwezi jua. Akaniongezea na Tsh 2000.”

Anaitwa Julius Macha mkazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam ambaye ni miongoni mwa washiriki 17 waliongia katika kambi ya Bongo Star Search jijini Dar es Salaam. Alifanikiwa kufikia hatua hiyo baada ya kupita kwenye usaili wa Dar es Salaam kati ya tar 12 na 14 mwezi Oktoba na kuwa kati ya wawakilishi 10 wa mkoa wa Dar es Salaam.
Julius anaimba muziki wa miondoko ya Rap na ndiye mshiriki pekee kati ya wote 17 wa msimu huu ambaye anafanya hivyo. Anaeleza kuwa amepokelewa vizuri na majaji wote pamoja na mashabiki wa Msimu wa tisa wa Bongo Star Search. 
“Nilipofika kwa majaji sikuwa na uoga nilionyesha kujiamini, nikafanya muziki wangu na wakanikubali nikawa nimepita kwenye top ten ya Dar es Salaam. Siku iliyofuata tukaingia kwenye mchujo wa nchi nzima ambapo nashukuru pia nilifanikiwa kupita na kuingia kwenye kumi na sita bora”, alisema James.
“Siku ya usaili sikuwa nafahamu, nilikuwa naendelea tu na kazi zangu za kila siku. Kuna mama mmoja ambaye ni mteja wangu huwa nambebea mizigo yake kuelekea Coco Beach, tukiwa njiani akaniuliza Vijana wangu huwa wanasema unaweza kuimba, hivi unajua kuna usaili wa BSS unaendelea? aliniambia usaili unafanyika Club Next Door wahi uende ukajaribu bahati yako huwezi jua, nikakubali na akaniongezea Tsh 2000 ya kunisaidia.” Julius
Julius alifika kwenye usaili na pikipiki ambayo anadai sio mali yake, na muda wote alikuwa anatoka nje ya ukumbi wa usaili kwenda kuhakikisha usalama wa chombo hicho cha moto. Kwa sasa Julius anasema ameirudisha pikipiki hiyo kwa mmiliki wake huku akijaribu kuielekea ndoto yake ya kuwa mwanamuziki, na anayo matarajio makubwa kupitia Bongo Star Search atafanikiwa kuifikia ndoto hiyo.
Julius Macha aliperform wimbo ‘Habari ndo hiyo’ wa msanii maarufu wa kizazi kipya Mwana FA na kuvutia wapiga kura wengi ambao hupiga kura kupitia App ya StarTimes ON inayopatikana Play Store na App Store, kwa sasa Julius ndiye anayeongoza kwenye chati za kura. Bongo Star Search inaonekana kupitia chaneli ya ST Swahili kila siku saa 3 Usiku.

Coppa Italia ndani ya StarTimes kuanzia Disemba

$
0
0
Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza ujio wa ligi ya Coppa Italia katika king’amuzi chake kuanzia tarehe 4 Disemba mwaka huu. Ligi hiyo itakuwa ikionekana kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee. Taarifa hiyo imetolewa na Idara ya Mawasiliano ya kampuni hiyo siku ya Jumatano.
StarTimes wamepata haki za kuonyesha michuano hiyo kwa Miaka mitatu yaani kuanzia msimu huu hadi ule wa 2020/21 na itakuwa ikipatikana katika lugha mbalimbali ikiwemo lugha adhimu ya Kiswahili.

Coppa Italia ni moja kati ya michuano yenye ushindani wa hali ya juu na msisimko wa aina yake barani Ulaya kwani huzikutanisha timu 16 zinazocheza katika ligi kuu ya nchini Italia maarufu kama Serie A, daraja la kwanza Serie B na Serie C ili katika mzunguko wa kwanza kutafuta timu 8 ambazo zitaungana na timu 8 za juu katika msimamo wa ligi kuu (Serie A) ili kucheza hatua ya 16 bora.

“Mpira wa kiitalia ni moja ya soka zinazovutia sana kutazama ndio maana tumewaletea wateja wetu kandanda hili la kusisimua. Pia ni katika mwendelezo wetu wa kuhakikisha hatuishiwi soka hata pale wengine wanapokaukiwa. Pia Italia kuna timu nyingi na bora ambazo zitashiriki katka Coppa Italia, Mfano Juventus, timu za jiji Milan, Napoli na AS Roma ambazo zitashiriki”. Sam Gisayi, Afisa Mahusiano wa StarTimes.

“Kwa hiyo wateja wetu wanao uhakika wa kumtazama Cristiano Ronaldo, Edin Dzeko, Gonzalo Higuain, Paulo Dybala na sasa kuna tetesi msweden Ibrahimovich atarejea kwenye klabu ya AC Milan hivyo burudani itaongezeka maradufu”. Aliongeza

Mbali na Coppa Italia, mwezi Disemba StarTimes watakuwa na michuano ya Club World Cup ambayo kwa kuanzia tarehe 12 kupitia chaneli zao za michezo. Kwa mara nyingine tena wateja wake wana nafasi ya kuwashuhudia Mabingwa Real Madrid wakijaribu kutetea taji lao, ila mara hii watahijati kufanya hivyo bila Cristiano Ronaldo.

StarTimes pia wanaendelea kuonyesha ligi ya Bundesliga pamoja na ile ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, na wiki ijayo kutakuwa na raundi nyingine ya EUROPA ligi ambayo nayo huonyeshwa kupitia StarTimes Pekee katika chaneli zao za michezo. Na wateja hutakiwa kulipia aidha kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000/= tu au SMART kwa Tsh 21,000/= pekee.

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI LA NCHI ZA BONDE LA MTIO NILE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu katika kusimamia matumizi endelevu ya maji ya Mto Nile kwa ustawi wa kiuchumi wa nchi zote.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 22, 2018) wakati akifungua mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile zilizopo Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.
Amesema nchi wanachama hazina budi kuimarisha ushirikiano ili ziweze kusimamia vizuri matumizi endelevu ya maji ya Mto Nile pamoja na kushughulikia changamoto zinazolikabili Bonde la Mto Nile. 
Waziri Mkuu ametaja baadhi ya changamoto zinazolikabili Bonde la Mto Nile kuwa ni pamoja na kushindwa kufikia makubaliano ya kuanzisha Kamisheni ya Kudumu ya Bonde la Mto Nile. “Kwa takribani miaka 10 sasa tumeshindwa kufikia makubaliano.”
Amesema, sambamba na changamoto hiyo nchi wanachama zimekuwa zikichelewa sana kutoa michango yao ili kuziwezesha taasisi zao kutekeleza ipasavyo majukumu yao, jambo ambalo si tu linachelewesha maendeleo bali linatishia usalama wa maji katika Bonde la Mto Nile.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu ametoa mapendekezo mbalimbali ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwenye Bonde la Mto Nile pamoja na kusaidia nchi wanachama kupata maendeleo.

Moja ya mapendekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu ni pamoja na nchi wanachama kutoa elimu kwa wananchi wake kuhusu matumizi sahihi ya maji na umuhimu wa kutunza vyanzo vyake ili kuhakikisha kunakuwepo na matumizi endelevu ya maji.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri  la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Novemba  22, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri  la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Novemba 22, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. George Lugomela (kulia) kuhusu mashine ya kutambua uwepo wa maji ardhini  kabla ya kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena, Novemba 22, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama burudani ya ngoma  wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri  la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu, Novemba 22, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa Makame na watatu kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Afrika ya Mashariki,  Balozi Dkt.  Augustine Mahiga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YASAINI MKATABA NA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

$
0
0
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesaini Mkataba na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wa kuanza rasmi ujenzi wa ofisi katika mji wa serikali, Ihumwa jijini Dodoma. Mkataba huo umesainiwa ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za serikali Makao Makuu ya Nchi. 

Kabla ya kusaini mkataba huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, amesema ujenzi wa ofisi hiyo ni hatua muhimu ya kutimiza mpango wa serikali na maelekezo ya Mhe. Dkt. Magufuli ya kuhamia Dodoma kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi. Dkt. Ndumbaro ameitaka TBA kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa ofisi hiyo kwa wakati na kwa kiwango bora ili kuwawezesha watumishi wa ofisi yake kutoa huduma kwa wananchi katika mazingira mazuri.

Kwa Upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini ofisi yake na kuwapa kazi ya ujenzi wa ofisi hiyo. Arch. Mwakalinga ameahidi kufanya kazi ya ujenzi huo kwa weledi mkubwa kwani wana vitendea kazi vya kisasa vinavyojitosheleza ikiwa ni pamoja na wataalam wa kutosha watakaowezesha kukamilisha jengo hilo kwa kiwango bora na kwa wakati. Aidha, Arch. Mwakalinga ametoa wito kwa wakuu wa taasisi nyingine kuitumia Wakala wa Majengo Tanzania katika ujenzi wa majengo mbalimbali kwani wako tayari muda wote kutoa huduma kwa kiwango bora.

Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa ni sehemu ya mwendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za serikali jijini Dodoma aliyoyatoa tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akisaini Mkataba na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga wa kuanza rasmi ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga wakipeana mikono kabla ya kukabidhiana Mkataba wa kuanza rasmi ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga wakionyesha Mkataba wa kuanza rasmi ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa jijini Dodoma.

JWTZ YAPOTEZA WENGINE WATATU DRC, AFRIKA YA KATI

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama mnavyofahamu linashiriki Ulinzi wa Amani ndani na nje ya Bara la Afrika.

JWTZ linasikitika kuwataarifu kwamba limewapoteza wapiganaji wake watatu (3) waliofariki kwa tarehe tofauti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kati (CAR) wakiwa kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani baada ya kushambuliwa na vikundi vinavyosadikiwa kuwa ni vya waasi.           

Mashujaa wetu waliouwawa ni Koplo Mohamed Mussa, Koplo Erick Masauri John na Praiveti Musa Shija Machibya.  Miili ya marehemu hao tayari imepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuhifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Heshima za mwisho kwa mashujaa wetu hao zitatolewa katika sehemu ya kuagia Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kesho tarehe 23 Novemba 2018 kuanzia saa 2.30 asubuhi.  Vyombo vya Habari na Wananchi wanakaribishwa tuungane katika kuaga mashujaa wetu.

Mungu azilaze Roho za Mashujaa wetu mahali pema Peponi, Amina.

JUKWAA LA TISA LA BIASHARA KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KUFANYIKA JUMAMOSI ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali  (katikati )akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Jukwaa la Tisa la Biashara baina ya Serikali na Sekta Binafsi litakalofanyika siku ya Jumamosi 24/11/2018 katika Ukumbi wa Sheih Idrisa Abdul Wakil hafla iliofanyika Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar. 
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano na Waandishi wahabari kuhusiana na Jukwaa la Tisa la Biashara baina ya Serikali na Sekta Binafsi litakalofanyika siku ya Jumamosi 24/11/2018 katika Ukumbi wa Sheikh  Idrisa Abdul Wakil hafla iliofanyika Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.
-Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali akisisitiza jambo wakati akijibu Maswali mbalimbali alioulizwa katika mkutano na Waandishi wahabari kuhusiana na Jukwaa la Tisa la Biashara baina ya Serikali na Sekta Binafsi litakalofanyika siku ya Jumamosi 24/11/2018 katika Ukumbi wa Sheikh  Idrisa Abdul Wakil hafla iliofanyika Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO WA BUNGE LA VIJANA MWAKA 2018

$
0
0
 Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiongoza Kikao cha Pili cha Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018. Mkutano huo wa Bunge la Vijana unafanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Waziri wa Kazi na Ajira katika Bunge la Vijana, Mhe. Victoria Ngowi akijibu  swali la mbunge wakati kikao cha Bunge la Vijana kikiendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Bunge la Vijana kutokea upande wa Upinzani, Mhe. Julius Mtatiro akiuliza swali Bungeni wakati kikao cha Bunge hilo la Vijana kinachoendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Mwanasheria Mkuu wa  Serikali katika Bunge la Vijana, Mhe. Shabir Bigirwa akijibu  maswali ya wabunge wakati kikao cha Bunge la Vijana kinachoendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Wabunge wa Bunge la Vijana wakimsikiliza Waziri wa Elimu katika Bunge hilo Mhe. Riziki Bakari wakati akijibu swali la Mbunge katika kikao cha Bunge hilo la Vijana kinachofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MOI YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA WA KUONDOA UVIMBE KWENYE MISHIPA YA DAMU YA UBONGO

$
0
0
NA KHAMISI MUSSA
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imefanikiwa kufanya upasuaji kwa mara ya kwanza hapa nchini kuondoa vivimbe katika mishipa ya damu ya ubongo (Aneurysm) ya mgonjwa. Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Alhaji Dkt. Hamisi Shabani.(pichani) amesema kwamba kabla ya hapo wagonjwa walikuwa wanafanyiwa upasuaji huo nje ya nchi kwa gharama kubwa isiyopungua shilingi za kitanzania milioni 100.

Akiongea na waandishi wa habari, Dkt.Shabani amesema kwamba aina hii ya upasuaji unahitaji darubini na vifaa tiba maalum ili kufanikisha upasuaji huo. "Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutupatia vifaa vyote ambavyo ni muhimu ili kufanikisha upasuaji huu.Na kuanzia sasa wagonjwa kama hao hawatapelekwa tena nje ya nchi watafanyiwa hapa nchini kwa gharama nafuu isiyozidi shilingi milioni 10".Naye Angel Msangi (37) ambaye ni mgonjwa wa kwanza kufanyiwa aina hii ya upasuaji alisema kwamba anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa kuwa mgonjwa wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa aina hiyo kwa mafanikio kwani asingemudu gharama za upasuaji nje ya nchi.

"Pia nawashukuru Madaktari wa Taasisi ya Mifupa MOI kwa kuniwezesha kunifanyia upasuaji huu na kuwashukuru wauguzi wa Taasisi hii kunifanyia upasuaji huu na sasa nina uhakika wa kuishi kwani nilikuwa nasumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu na nikiweka kitu nakuwa sijui nimekiweka wapi, nikiwa nimekula nasahau kama nimekula, kwa hiyo kwangu ikawa ni shida tayari".

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akimuelekeza Angel Msangi kufanya mazoezi ili ajiridhishe mgonjwa wake wakwanza aliye fanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe katika mishipa ya ubongo kujiridhisha kama amepata nafuu apate kumpa ruhusa ambapo upasuaji huo ulichukua muda wa saa 6. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSS)
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehem ndogo iliyotumika kuondoa uvimbe huo

Angel Msangi akizungumza jambo na waadishi wa habari leo katika Taasisi ya Mifupa MOI, Dar es Salaam. wa pili kulia ni Askari wa jeshi la Polisi CCP Moshi, Julius Msangi ambaye ni mume wa Angel Msangi na wa kwanza kushoto ni Dkt, Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI

$
0
0
 NA WAMJW- DAR ES SALAAM. 
BARAZA Tiba asili na Tiba mbadala nchini limetoa elimu kwa wakunga wa jadi  kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama kwenye kituo cha afya kilichopo karibu ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Hayo yamesemwa na Msajili wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini Dkt. Ruth Suza wakati wa semina na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa tiba  asili na tiba mbadala nchini. 

Amesema kuwa wakunga  wa jadi nchini wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuhakikisha wamama wajawazito wanawahimiza kujifungulia katika vituo vya afya kwa usalama wa maisha ya mama na mtoto. "Tunapita kuwaelimisha Wakunga wa jadi kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama kwenye kituo cha afya kilichopo karibu ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi" alisema Dkt. Suza. 

 Dkt Suza amesema jumla ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala 19912 wamesajiliwa na Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini ili kuweza kutoa huduma hizo kwa kufuata sheria na taratibu. "Pamoja na waganga wa tiba asili na tiba mbadala 19912 kusajiliwa pia tumesajili vituo vya tiba asili na tiba mbadala 19  kutoa huduma za afya nchini" alisema Dkt. Suza. 
 Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk.Edmond Kayombo akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu taratibu na hatua za usajili wa waganga,dawa na vituo vyakutolea huduma leo jijini Dar es Salaam, (kushoto ni)Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
 Mratibu wa Taifa tiba asili na tiba Mbadala Dkt.Liggyle Vumilia wa Wizara ya Afya akizungumza na waandishi habari na wadau mbalimbali juu hatua walizozichukua kwa watoaji huuduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
 Mfamasia Baraza la  tiba asali na tiba  Mbadala wa Wizara ya Afya,Ndahani Msigwa akizungumza na wadau mbalimbali wa afya kuhusu sheria,kanuni na taratibu za utoaji huduma za tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu wa wandau mablimbali wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmond Kayombo.

MAANDALIZI YA MBIO ZA MBEZI FUN RUN YAKAMILIKA, CHAMA CHA RIADHA CHATOA BARAKA

VOA SWAHILI: Duniani Leo Novemba 22, 2018

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images