Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: Najisikia faraja kuwa sehemu ya serikali awamu ya tano - DC Patrobas Katambi


MICHUZI TV: ANGA LOTE LA TANZANIA CHINI YA ULINZI WA RADA ZA KISASA ASILIMIA 100

MICHUZI TV: Gharama za matibabu vituo vya afya binafsi zajadiliwa (APHFTA)

Habari za UN KUTOKA NEW YORK, MAREKANI, Novemba 21, 2018

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 21.11.2018

MKAZI WA MBEZI JUU, DAR ES SALAAM, EMMANUEL NZUKI SHINDA BAJAJ PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA

$
0
0
Kumekucha Kwenye Promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa maana watanzania wanazidi kushinda bajaj kutokana na ubashiri wanaofanya kupitia timu ya ushindi.

Safari hii kambi ya timu ya ushindi imehamia hapa jijini Dar es salaam katika viunga vya Mbezi Juu ambapo kuna mshindi wa droo ya 57 Emmanuel Nzuki anayekabidhiwa bajaj baada ya ushindi.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa bajaj hiyo Nzuki alisema hakuamini kama anaweza kushinda maana mara kadhaa alikuwa anacheza mara nyingi lakini hakubahatika kumbe wakati wake ulikuwa haujafika kubahatika sasa ndio ameamini baada ya kuupokea ushindi huo

"Ama kweli nimeamini bahati ya mtu haipotei unajua vile nilikuwa nikiona wengine wakishinda nilijua labda wanaoshinda ni wale wenye kipato cha chini kabisa kumbe hata sisi wenye kipato cha kati inawezekana, siku ya leo yote naitumia kusherekea ushindi wangu" alisema Nzuki.

Aidha mshindi huyo aliongeza kuwa bajaj hiyo itaweza msaidia kuinua kipato chake na kuacha maisha ya kutegemea mshahara pekee. "Sikia nikwambie aisee ni kweli nina mshahara mzuri lakini bado bajaj hii itakuwa msaada mkubwa kwangu maisha ya kutegemea mshahara pekee ni magumu sana lakini kupitia bajaj hii naweza sasa boresha maeneo mengine mfano kulipia watoto wangu ada ya shule kuwasaidia ndugu na pesa nyingine naweza malizia malipo ya kiwanja changu na kuanza kujenga.

 Mshindi wa droo ya 57 Emmanuel Nzuki aliyekabidhiwa bajaj baada ya ushindi.

MAANDALIZI YA MBEZI FUN RUN YAKAMILIKA,CHAMA CHA RIADHA NCHINI (RT) CHATOA BARAKA

$
0
0
CHAMA cha Riadhaa nchini (RT), kimetoa baraka kwa wandaaji was mbio za kujifurahisha Mbezi Fun Run zilizopangwa kufanyika Desemba Mosi jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa RT, Willihelmi Gudagudai alisema RT imetoa kibali kwa wandaaji hao baada ya kufuata taratibu zote."Tumewataka baada ya tamasha lao, wawasiliane na RT ili mbio zao ziingizwe kwenye kalenda ya mwaka ya matukio ya RT."alisema.

Kwa upande wa waandaji hao kupitia kwa katibu Mbezi Fun Run Omary Kimbau alisema mandalizi ya mbio hizo yamekamilika kwa asilimia 90 mpaka Sasa, na kwamba kuanzia leo wataweka wazi vituo mbali mbali vya kujiandikisha kwa yeyote anayependa kushiriki.

"Kushiriki ni bure, hakuna kingilio chochote na mlango upo wazi kwa yeyote, ila kuna tisheti na beji kwa wakimbiaji, beji shilingi 10,000 na atakayependa kutumia fulani zetu bei ni shilingi 25,000."alisema.Kimbau alisema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbali mbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.

“Kama mnavyojua siku hiyo ya Desemba Mosi itakuwa ni siku ya ukimwi duniani hivyo pia tumemualika Waziri Ummy Mwalimu awe mgeni rasmi na tutafanya nae mazoezi ya pamoja, na pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu.“Damu salama inahitajika kwenye banki ya damu, kama haijanisaidia mimi itamsaidia ndugu yangu, jamaa au mtanzania yoyote yule, hivyo tumeona siku hiyo pia tuitumie kuchangia damu salama na pia kupima afya yetu kwa kupima maambukizi ya virusi ya ukimwi.”alisema.


Pichani kati ni mwenyekiti wa bonaza hilo la Mbezi Run Fun Loraa George ‘Robelo’ alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mbio hizo ambazo anaeleza kuwa kwa asilimia 90 yamekamilika,kulia ni Katibu wa Mbezi Fun Run Omary Kimbau na kushoto ni mwakilishi kutoka kitengo cha afya Wilaya ya kinondoni Getruda Kafuko.
Katibu wa Mbezi Fun Run Omary Kimbau akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jana kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo  kwa asilimia 90 mpaka Sasa,na kuongeza kuwa vitakuwepo vituo mbali mbali vya kujiandikisha kwa yeyote anayependa kushiriki.

"Kushiriki ni bure, hakuna kingilio chochote na mlango upo wazi kwa yeyote, ila kuna tisheti na beji kwa wakimbiaji, beji shilingi 10,000 na atakayependa kutumia fulani zetu bei ni shilingi 25,000."alisema.Kimbau alisema mbio hizo zimeandaliwa na umoja wa wakazi wa Mbezi Beach zikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo na kusaidia kwenye changamoto mbali mbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.
Mkurugenzi wa ufundi wa mbio za Mbezi Fun Run Isihaka Mlawa akionesha kibali walichopewa mara baada ya kufuata na kukamilisha taratibu zote kutoka chama cha Riadhaa nchini (RT).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 22,2018


DC MURO ALETA SULUHU MGOGORO WA KANISA ULIODUMU KWA TAKRIBANI MIAKA 13 ARUMERU

$
0
0

Na. Vero Ignatus, Arusha

Mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 13 wa kanisa la AMEKI wilayani Arumeru kata ya Usariva umemalizika kwa pande mbili kukubaliana kwa kuondoa tofauti zao na kuamua kuwa na kanisa moja na uongozi mmoja

Akizungumzia mgogoro huo uliodumu kwa miaka 13 mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewapongeza viongozi kwa hatua kubwa waliyoifikia kwani kwa miaka yote hali ilikuwa nzito na mgogoro ulidumaza maendeleo ya kanisa ,ustawi wa wananchi,maendeleo ya shughuli za serikali katika wilaya hiyo.

"Mhe. Baba Askofu, Mhe. Msaidizi wa , Askofu nimesimama hapa kwa niaba ya serikali kuwapongeza kwa hatua kubwa mliyofikia, tumekuwa na changamoto za mgogoro uliodumu kwa miaka 13''alisema Jerry.Jerry amesema kuwa serikali itaendelea kusimama na kanisa la AMEKI kuwaunga mkono katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo sambamba na ukuaji wa kiroho na maendeleo ya waumini wao

'' Ndani ya miezi mitatu kama mkuu wa wilaya namshukuru sana Mungu kunifanya kuwa chachu ya kuwapatanisha viongozi hawa wa kanisa na leo wamekuwa wamoja na kanisa moja naamini sasa baraka zaungu zitaonekana''alisema Jerry .Sambamba na hayo amesema kwakuwa mgogoro umeisha,serikali inaanza kazi mara moja ndani ya wiki moja serikali itahakikisha kuwa inatatua changamoto zote ya maeneo yote ambayo yalikuwa ya kanisa

Baadhi ya Wachungaji na viongozi wa Makanisa ya Ameki nchini waliohudhuria ibada hiyo ya shukrani wakiwa na Baba askofu pamoja na makamu wa askofu katika ibada ya pamoja
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza katika la AMEKI mara baada ya pande mbili hizo kuondoa tofauti zao na kuamua kuwa wamoja na uongozi mmoja
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza Baba Askofu wa kanisa la Ameki lililopo Wilayani hapo kata ya Usariva mara baada ya kuondoa tofauri zao na kutangaza Amani


Baadhi ya waumini katika kanisa la Ameki waliohuduria katika Ibada ya shukrani baada ya mgogoto huo uliodumu zaidi ya miaka 13 kumalizika

TCRA yatoa elimu kwa wanafunzi na walimu Shule ya Sekondari Morogoro

$
0
0
Na Chalila Kibuda .

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Kanda ya Mashariki imesema kuwa mawasiliano lazima yafuate sheria kwa wadau wote ili kulinda ustawi wa Taifa.

Hayo ameyasema Meneja wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero wakati walipotembelea Shule ya Sekondari Morogoro kwa ajili ya utoaji wa elimu ya mawasiliano ,amemesema watumiaji wa mawasiliano wanatakiwa kufuata sheria ili kutumia mawasiliano hayo kwa malengo yaliyowekwa.

Amesema kutokana na sheria iliyopo kwa mawasiliano yanaweza kumgharimu mtu yeyote kwa kukipa faini au kifungo cha hadi miaka mitatu.
Odiero amesema ni makosa kutumia laini ya simu ambayo haijasajiliwa pamoja na simu moja kumiliki zaidi ya mtu mmoja.Amesema kuwa simu ya biashara ya fedha inatakiwa kutumika kwa biashara hiyo tu katika kuondoa usumbufu wa mawasiliano mengine.
 
Mkuu wa Sule ya Sekondari Morogoro Boniface Gonjo amesema elimu iliyotolewa na TCRA wameielewa na kuahidi kuwa mabalozi katika mawasiliano.
Amesema TCRA iendelee kuwafikia watu wote kwani watu wengi wanatumia mawasiliano lakini hawajui madhara ya matumizi mabaya ya mawasiliano



Mkuu wa Shule wa Sekondari ya Morogoro Boniface Gonjo akizungumza kuhusiana na Ujio wa TCRA katika Shule hiyo
Afisa Elimu Mkoa Rhoda Mursuli akizungumza umuhimu wa matumizi bora ya mawasiliano kwa ustawi wa taifa
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Morogoro wakisikiliza mada kwa wataalam wa TCRA namna bora ya matumizi ya mawasiliano.

MEYA MWITA AKUTANA NA UJUMBE WA WATU WENYE UALIBINO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MEYA  wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la kutetea haki na ustawi wa watu wenye ualbino la Under The Same Sun, tawi la Tanzania.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana shirika hilo lililowakilishwa na Ofisa Uraghibishaji Kondo Seif, limeomba fursa ya kukutana na  madiwani wa Mkoa wa Dar es salaam wanapokuwa kwenye vikao vya kazi, ili kuwaeleza masuala mbalimbali yanayohusu dhana nzima ya ualbino na changamoto zake.

Taarifa ya Ofisa Habari wa Ofisi ya Meya Christina wa Jiji la Dar es Salaam Christina amesema Mwagala Meya wa jiji
Meya Mwita aliridhia ombi la shirika la Under The Same Sun na kuahidi ofisi yake kusaidia kwenye jitihada za kumaliza madhila wanayoyapata watu wenye ualbino.

Itakumbukwa katika miaka ya 2006, Tanzania iligubikwa na habari za matukio ya mauaji na ukataji wa viungo vya watu wenye ualbino, na kutumia viungo vya miili ya watu hao  kwa imani za kishirikina, kwa kuamini kuwa watafanikiwa kwenye shughuli zao za kiuchumi.


Tangu wakati huo, shirika la Under The Same Sun limekuwa likizunguka maeneo mbalimbali nchini kutoa elimu kuhusu ualbino, jinsi unavyopatikana sambamba na kutoa ufadhili wa kielimu kwa watu wenye ualbino, ambapo zaidi ya wanafunzi 400 nchi nzima wanafaika kwa kulipiwa gharama za elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi vyuo vikuu.
 Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu akimuonesha  Mstahiki Meya Isaya Mwita picha mbalimbali zilizomo kwenye kitabu hicho  jumbe mbalimbali zinazo elezea walemavu hao
 Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu akizungumza jambo na Mstahiki Meya Isaya Mwita jumbe mbalimbali zinazo elezea walemavu hao
 Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu akimkabidhi Mstahiki Meya Isaya Mwita jumbe mbalimbali zinazo elezea walemavu hao

WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Mara
Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameuagiza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuvunja uongozi wa Mfuko wa Udhamini wa North Mara ( Bodi ya Wadhamini na Menejimenti) kwa kuwa umeshindwa  kusimamia  uendeshaji wa Mfuko kwa tija na kuandaa utaratibu mzuri  wa usimamizi  wa Mfuko huo ambao utakuwa na  manufaa kwa Taifa .

Aidha, Waziri Kairuki amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuruhusu fedha za Keng'anya Enterprises Ltd ( KEL) kuendelea kulipwa  hadi hapo vyombo vya uchunguzi vitakakapobaini na kuelekeza vinginevyo, huku Mkuu wa Mkoa wa Mara akitakiwa kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.

“Kwa kuwa Keng'anya Enterprises iliomba kupata PL 303/95 kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ya Madini, hivyo malipo ya mrabaha wa asilimia moja yanayopokelewa kutoka kwenye mgodi kwa mujibu wa mkataba wake ni halali,” alisisitiza Kairuki.

Waziri Kairuki  alitoa  maagizo hayo Novemba 21, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ambaye alielekeza kufanyika uchunguzi wa Mfuko wa North Mara Community Trust  Fund, baada  ya baadhi ya wananchi wa Nyamongo Wilayani  Tarime kulalamika juu ya jamii kutofaidika na mfuko huo na badala yake kunufaisha baadhi ya watu wachache.

Rais Magufuli alitoa maelekezo ya kufanyika kwa uchunguzi wa mfuko huo wakati wa ziara yake Mkoani Mara tarehe 4 hadi 8 Septemba, 2018.

Mbali na agizo la kuuvunja uongozi wa mfuko, Waziri Kairuki aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwachunguza na kuwachukulia hatua za kisheria wajumbe wa bodi ya wadhamini, menejimenti ya mfuko na yeyote atakayethbitika kujihusisha na ufujaji na matumizi mabaya ya fedha za mfuko.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akieleza jambo. Kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kulia)
Sehemu ya Watendaji kutoka Wizara ya Madini, Uongozi wa Mkoa  wa Mara wakifuatilia kikao hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANUFAIKA WA TASAF CHATO WAIBUKIA KWENYE UFUGAJI

$
0
0
Na Richard Bagolele - Chato
Baadhi ya wanufaika wa mpango wa TASAF awamu ya tatu Wilayani wameendelea kujiongezea kipato kwa kufuga aina mbalimbali za mifugo.
Baadhi ya wanufaika wamesema kupitia ufugaji wameona ndio njia pekee ya kwao kujikwamua na hali ngumu ya maisha ambayo walikuwa nayo kabla ya kuingia kwenye mpango wa TASAF 3 wa kunusuru kaya masikini.
Bi Sugwa Bushuwandama mkazi wa kijiji cha Mkungo kata ya Bukome Wilayani hapa anasema kupitia mpango wa TASAF 3 kwa kipato kidogo anachopata hivi sasa anao mbuzi 12 ambao mara kwa mara amekuwa anauza na kununua mahitaji mengine ya familia kama vile chakula.
“mwezi uliopita niliuza mbuzi wawili nilienda kufanya manunuzi mnadani ambapo nilinunua gunia la mahindi la shilingi elfu 40 na nguo za wanangu” alisema Bi Sugwa huku akitabasamu.
Kwa upande mwingine wanufaika hao wanasema kupitia miradi ya ufugaji wa Ng’ombe na mbuzi kwao imekuwa ni rahisi kutokana na urahisi pindi wanapotaka kuuza au kubadili kupata bidhaa nyingine kama vile chakula pindi familia zinapokuwa kwenye ukata.
Bi Lega Amos mkazi wa kijiji cha Nyambiti kata ya Nyamirembe ambaye ana mbuzi 17 amesema baada ya kuanza kunufaika na mpango wa TASAF 3 alianza kununua mbuzi wawili lakini hadi sasa kupitia ufugaji huo ameanzisha mradi wa kukaanga samaki na kuuza kwenye soko la kijijini hapo lakini pia ameweza kujenga nyumba ndogo ya tofali za tope na kuezeka kwa bati.
  Bibi  Sigwa Bushuwandama mkazi wa kijiji cha Mkungo kata ya Bukome kupitia mpango wa TASAF 3 ameanzisha ufugaji wa Mbuzi na Kondoo kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato cha familia yake yenye watoto watano
 Bwana Mapinduzi Elkana (kulia) baada ya kuanza kunufaika na mpango wa TASAF 3 aliamua kuchimba kisima na kuanza kuuza maji kwa wakazi wa kijiji cha Mkungo ambapo kwa siku anakadiria kuuza ndoo 40 sawa na sjhilingi 4000 kwa siku.
 Bibi Tekla Mashine mkazi wa kijiji cha Kanyama kata ya Ilemela baada ya kuanza kunufaika na mpango wa TASAF 3 alianza kufuga mbuzi mradi ambao umemwezesha kuweka umeme wa jua kwenye nyumba yake na kupeleka watoto 6 shule ya msingi na sekondari.
 Bibi Nyamarwa Justine mkazi wa kijiji cha Kanyama kata ya Ilemela Wilayani Chato mbali na ufugaji wa mbuzi ameweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu na matarajio yake ni kukamilisha ujenzi huo mwaka 2019.
Bi Maria Jacob mkazi wa kijiji cha Nyang’omango kupitia mpango wa TASAF 3 ameweza kununua vyombo vyua kisasa kwa ajili ya matumizi ya familia yake.

SPORTPESA WAZIDI KUWAWEZESHA VIJANA ,EMMANUEL NZUKI AJINYAKULIA BAJAJI KWENYE PROMOSHEN SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA

$
0
0
Kumekucha Kwenye Promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa maana watanzania wanazidi kushinda bajaj kutokana na ubashiri wanaofanya kupitia timu ya ushindi. Safari hii kambi ya timu ya ushindi imehamia hapa jijini Dar es salaam katika viunga vya Mbezi Juu ambapo kuna mshindi wa droo ya 57 Emmanuel Nzuki anayekabidhiwa bajaj baada ya ushindi. 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa bajaj hiyo Nzuki alisema hakuamini kama anaweza kushinda maana mara kadhaa alikuwa anacheza mara nyingi lakini hakubahatika kumbe wakati wake ulikuwa haujafika kubahatika sasa ndio ameamini baada ya kuupokea ushindi huo.

 "Ama kweli nimeamini bahati ya mtu haipotei unajua vile nilikuwa nikiona wengine wakishinda nilijua labda wanaoshinda ni wale wenye kipato cha chini kabisa kumbe hata sisi wenye kipato cha kati inawezekana, siku ya leo yote naitumia kusherekea ushindi wangu" alisema Nzuki. Aidha mshindi huyo aliongeza kuwa bajaj hiyo itaweza msaidia kuinua kipato chake na kuacha maisha ya kutegemea mshahara pekee. 

Sikia nikwambie aisee ni kweli nina mshahara mzuri lakini bado bajaj hii itakuwa msaada mkubwa kwangu maisha ya kutegemea mshahara pekee ni magumu sana lakini kupitia bajaj hii naweza sasa boresha maeneo mengine mfano kulipia watoto wangu ada ya shule kuwasaidia ndugu na pesa nyingine naweza malizia malipo ya kiwanja changu na kuanza kujenga. 

Mshindi huyo wa droo ya 57 aliwasisitiza watanzania kuacha woga na kujaribu bahati na SportPesa maana hata yeye wakati anaambiwa acheze hakuamini kama angeshinda lakini sasa tayari amefanikiwa kushinda na anamiliki bajaj yake aliyoshinda na SportPesa. 

Kwa upande wa SportPesa Meneja Uhusiano Bi Sabrina Msuya alisema prom0sheni yetu ni kwa mitandao yote ya simu na mteja anaweza kushiriki kupitia simu yake ya mkononi kwa kupiga * 150*87# na kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kupitia AirtelMoney, MPESA, TigoPesa na Halopesa kisha kuweka ubashiri wake.

 “Mbali na kushinda fedha za ubashiri wake ambazo huingizwa papo hapo kwenye akaunti ya mteja mara baada ya kubashiri kwa usahihi michezo aliyoweka, mteja anaweza kujishindia zawadi mbalimbali kama Bajaji, Simu janja(Smartphone), Jersey za Simba na Yanga pamoja na safari ya kwenda Hispania na Uingereza kushuhudia mitanange ya ligi zinazoendelea nchini humo” 

“Michezo anayoweza kushiriki ni pamoja na Jackpot (yenye mechi 13 ambayo kwa sasa ni zaidi ya shilingi milioni 394 yaani karibia milioni 400, hii ni Jackpotyenye kiasi kikubwa kuliko Jackpot zingine zozote nchini, pia mteja akibashiri kwa usahihi mechi kuanzia 10 hadi 12 anajipatia bonus kama zawadi” “Napenda kuwahamasisha watanzania wote kwamba washiriki na waendelee kubashiri na SportPesa kwani kuna mambo mbalimbali yanaendelea na wategemee mazuri zaidi kutoka kwetu”.

Upasuaji wa kuunganisha mifupa ya fuvu la uso wafanyika Muhimbili

$
0
0
Wataalam wabobezi wa upasuaji wa kinywa mataya na uso (Oral & maxillofacial surgeons) wa Hospitali ya Taifa 


Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wenzao wa Marekani kwa mara ya kwanza kupitia Hospitali ya umma nchini, wamefanya upasuaji wa ubingwa wa kuunganisha mifupa ya fuvu kwa mgonjwa aliyepata ajali na sura yake kuharibika.

Upasuaji huo ambao ulifanywa na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Kansas City na Chuo Kikuu cha Missouri nchini Marekani, ulifanikiwa kurejesha sura ya mgonjwa huyo katika hali yake ya kawaida.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso, Dkt. Daud Shaban amesema upasuaji mwingine uliofanyika unahusisha wagonjwa waliokuwa na uvimbe mkubwa sehemu ya taya na uso. Amesema pia wataalam wenzake walifanya upasuaji wa kutengeneza taya jipya kwa mgonjwa aliyepata ajali na taya lake kuharibika ambapo wamechukua kipande cha mfupa kutoka kwenye sehemu ya kiuno chake na kukiunganisha na taya ili kulikamilisha upasuaji huo.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Doraha Kiwale (kulia), Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso, Dkt. Daud Shaban wa Muhimbili (katikati) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso, Dkt. Baraka Kileo wa Muhimbili wakifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe chini ya shingo ya mgonjwa ambao umeziba mshipa mkubwa wa kupeleka damu kwenye ubongo. Wa pili kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, mataya, na Uso, Prof. Thaer Raifallah kutoka Hospitali ya Kansas City na Chuo Kikuu cha Missouri huko Marekani akishiriki kwenye upasuaji huo. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Kinywa, Mataya na Uso wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Daud Shaban akizungumza na mwandishi wa habari kuhusu upasuaji wa kinywa, mataya na uso ambao unafanywa na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya Kansas City na Chuo Kikuu cha Missouri nchini Marekani. 
Wataalam wa wakiendelea na upasuaji katika hospitali hiyo.


USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA

$
0
0
Na Karama Kenyunko Blogu ya Jamii.
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili, washtakiwa Harbinder Sethi  na James Rugemarila umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa,   washtakiwa wameshindwa kufikishwa mahakamani hapo kwa sababu ya kuwepo kwa shida ya usafiri. 

Wakili wa serikali Emmanuel Nitume ameeleza  hayo Leo Novemba 22,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na pia washtakiwa wote wanaokabiliwa na kesi hiyo hawapo kwa sababu kuna shida ya usafiri." Amesema Nitume.

Wakati wakili huyo wa serikali akieleza hayo, afisa mmoja wa Magereza aliyekuwemo mahakamani humo aliongeza kuiambia mahakama kuwa washtakiwa hawajaletwa kwa sababu kuna shida ya magari.

Kufuatia melezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi  Desemba 6, mwaka huu.

Katika kesi hiyo,Washtakiwa Sethi na Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kusababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

HASUNGA AWATAKA WATAALAMU WIZARA YA KILIMO KUONGEZA UFANISI ILI KUWA NA TIJA KATIKA UZALISHAJI

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga ameshangazwa na miradi mingi iliyopo katika wizara ya kilimo huku ikiwa na uchache wa manufaa.

Amesema kuwa wataalamu mbalimbali waliopo katika wizara hiyo wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa weledi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza tija katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.Waziri Hasunga ameyasema hayo tarehe 21 Novemba 2018 wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kikiwa na dhumuni la kufahamiana ambapo washiriki wamepata fursa ya kueleza namna ambavyo kilimo kinaweza kuimarika na kuwanufaisha wakulima nchini.“Lazima tuendelee maana rasilimali watu zipo, wasomi wazuri wapo na tafiti zipo hivyo hatuna sababu ya kushindwa kufanikiwa kwenye sekta ya kilimo” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Kuna watu wamepewa rasilimali kubwa kwa ajili ya kuzifanyia kazi lakini ufanisi wao na tija katika utendaji ni mdogo sana jambo hili halikubaliki lazima tubadilike” Kwa upande wake Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akichangia katika kikao hicho alisema kuwa tarehe 4 Juni 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alizindua programU ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) huku kukiwa bado kuna mapungufu makubwa kwenye ASDP awamu ya kwanza.
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya kilimo).
Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akielezea muundo na majukumu ya wizara ya kilimo kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018.

KUMBUKUMBU YA MZEE SABINUS KWEKA

$
0
0
KUZALIWA 30/12/1935     KIFO 22/11/2004

Umetimiza miaka kumi na nne tangu ulipoiaga dunia Novemba 22, 2004 Baba yetu,Rafiki yetu,Mshauri wetu na Mpendwa wetu. Pamoja na kwamba hatupo nawe kimwili, busara na miongozo yako bado tunaiishi hasa ile ya kupendana kama ulivyotupenda sisi. Tunatazamia kwa hamu wakati Mungu atakapotimiza ahadi yake ya kufufua wafu siku isiyojulikana
Unakumbukwa sana na sisi wanao, JANE, FESTO, EUGENIA, ELIZABETH, CECILIA NA THADEI, Dada yako mpendwa SR.DEVOTHA KWEKA C.D.K wana – kata wote wa Narumu,ukoo wote wa Kweka,Ndugu, jamaa na Marafiki wote.
“Raha ya milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa milele Umwangazie apumzike kwa amani........................AMINA”

WAKULIMA WA KOROSHO WA TUNDURU MKOANI RUVUMA WATUMA SALAMU KWA RAIS MAGUFULI

HASUNGA AKABIDHIWA RASMI OFISI, DKT TIZEBA ASHAURI MAZITO KUHUSU KILIMO

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Aliyewahi kuwa Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba ambaye ni Mbunge wa Buchosa Mkoani Mwanza leo tarehe 22 Novemba 2018 amemkabidhi rasmi ofisi Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu mawaziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba na Mhe Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, na Wakuu wa idara na Vitengo.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mhe Dkt Tizeba amempongeza Mhe Hasunga kwa kuteuliwa kuhudumu katika nafasi hiyo ambapo amesisitiza kusimamiwa kwa weledi huduma za ugani ambazo kwa kiasi kikubwa hakuna jambo la kujivunia katika eneo hilo kutokana na mgawanyo wa kimajukumu kuwa katika wizara mbili ya kilimo na TAMISEM jambo ambalo linapunguza ufanisi wa kiweledi.

Alisema kuwa wizara inapaswa kuendelea kusomesha wataalamu mbalimbali nchini wakiwemo wa ugunduzi na utafiti ili kuongeza tija ya kilimo na utoaji elimu kwa wakulima na kuongeza uwezo wa uzalishaji wa wananchi sambamba na Taifa kwa ujumla.
Mbunge wa Buchosa Mkoani Mwanza Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Kulia) akifurahi jambo pamoja na Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi Jijini Dodoma leo tarehe 22 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya kilimo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi Jijini Dodoma leo tarehe 22 Novemba 2018. 
Picha ya pamoja waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb), Mbunge wa Buchosa Mkoani Mwanza Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Naibu mawaziri wizara ya kilimo Mhe Omary Mgumba na Mhe Innocent Bashungwa, na Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wote wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi Jijini Dodoma leo tarehe 22 Novemba 2018. 

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images