Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR IKULU LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar, akifungua Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara  Zanzibar katika ukumbi wa mkutano Ikulu Zanzibar, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.(Picha na Ikulu) 
 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wakulima wa Karafuu Zanzibar Ndg.Kassim Khamis Rashid, akichangia Mada, wakati wa Mkutano huo wa Taifa wa Baraza la Zanzibar, uliofanyika Ikulu Zanzibar, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani. 21/11/2018
 KATIBU wa Baraza la Vijana Ndg. Khamis Faraj, akiwasilisha Mada kuhusiana na Fursaza Ajira kwa Vijana za Kiuchumi, wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano Ikulu Zanzibar.
 MWENYEKITI wa Jumuiya ya ZATI Ndg. Seif Masoud Miskry,akichanga Mada wakati wa  mkutano wa Taifa wa Baraza la Biashara Zanzibar uliofanyika Ikulu Zanzichibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani, umefanyika leo 21/11/2018. 
 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenyeviwanda na Wakulima Zanzibar, Ndg Tofiq Salim Turky, akichangia wakati wa Mkutano huo wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa ZNBC Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
WAZIRI wa Fedha naMipango Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohammed akichangia wakati wa mkutano huo wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar,uliofanyika Ikulu Zanzibar, kulia Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)  

WAJASIRIAMALI 250 KUSHIRIKI MAONESHO YA SIDO KANDA YA KASKAZINI JIJINI TANGA

$
0
0
ZAIDI ya wajasiriamali 250 wamekwisha wasili Jijini Tanga kwa ajili ya  maonyesho ya Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO)Kanda ya  Kaskazini yanayotarajiwa kuanza kesho Nov 22 hadi 26 ambapo mgeni anatarajiwa  kuwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda

Hayo yamezungumzwa na Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga  Gladness Foya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya tangamano Jijini hapa  na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Foya alisema maandalizi yapo vizuri na tayari baadhi ya wafanyabaishara  toka Nchini Uganga na Burundi wamekwisha wasili kwa ajili ya maonyesho hayo  ambayo yanajumuisha mikoa ya Tanga,Kilimanjaro.Arusha na Manyara.“Tumekwisha anza pokea wageni na wapo zaidi ya wajasiriamali 250 wamekwisha  wasili na watatu toka Uganda na watano toka Burundi na tunatarajia kupokea  wageni zaidi katika maonyesho haya”Alisema Foya.

Awali akizungumzia maonyesho hayo Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella  alisema ni fursa kwa Watanzania na wananchi wa ndani ya jiji na nje  kujifunza namna Serikali ya awamu ya tano inavyotekeleza kwa vitendo uchumi  wa viwanda.Aidha alisema tayari taasisi za kifedha,wamili wa viwanda na wasindikaji  wamekwisha wasili Jijini hapa kwa ajili ya maonyeshoi hayo ambayo  yatawajenga katika nyanja hiyo ya uchumi wa viwanda na ujasiriamali.

“Tunaowageni wengi tumekwisha anza wapokea na zaidi ni fursa kwetu na  wajasiriamali maana watapata muda wa kuuza bishara zao na kuona bidhaa  zinazozalishwa na sido na wanaweza kuomba kutengenezewa labda niseme tu ni  fursa kubwa”Alisema Shigella.

Hata hivyo aliwaomba wafanya biashara kuyatumia maonyesho hayo ili kuweza  kujinufaisha kibiashara na namna ya kuweza kupata bidhaa bora toka shirika  hilo la Sido.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza kuhusiana na maonyesho hayo kushoto ni Mhasibu wa SIDO mkoani Tanga Janeth Kiwale
 Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga  Gladness Foya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kesho na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Mhasibu wa SIDO Mkoani Tanga Janeth Kiwale
Sehemu ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia mkutano huo

Dkt Abbasi Awataka Waandishi kufuata Sheria ya Habari

$
0
0

Na Grace Semfuko-MAELEZO

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amewataka waandishi wa habari kutumia haki na wajibu wao katika kulinda maadili yao ya uandishi na kutotumia taaluma yao kukejeli na kuchafua watu wengine

Amesema Sheria mpya namba 12 ya mwaka 2016 ya huduma za vyombo vya habari kifungu cha 7 ingawa inawapa Waandishi wa Habari kukusanya,kuhariri na kusambaza habari lakini haiwapi fursa waandishi hao kuandika habari ambazo zinachafua wengine.

Dkt Abbasi aliyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha Hallow Tanzania kinachorushwa na Radio Uhuru ya Jijini Dar Es Salaam alipokuwa akijibu maswali ya wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali Nchini.

“Sheria Mpya ya Habari inawapa fursa Waandishi kufanya kazi zao za kukusanya,kuhariri na kusambaza habari,sheria hii haijamnyima Mwandishi wa Habari kupata habari, lakini pia haijatoa fursa za kusambaza habari za kukejeli na kuchafua wengine, sheria itachukua nafasi yake kwa atakaebainika kufanya hivyo” alisema Dkt Hassan Abbasi Msemaji Mkuu wa Serikali.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Magufuli kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni sehemu ya kulinda maadili ya uandishi wa habari na kuvitaka vyombo vingine kuendelea kuheshimu,kulinda na kutetea maslahi ya Taifa.

Akihojiwa na Mtangazaji wa kipindi hicho Aggrey Manzi kuhusiana na baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii katika kuchafua wengine, Dkt Abbasi alisema sio sahihi kutumia mitandao hiyo katika kuona wengine hawafai, bali mitandao itumike kutangaza habari za Maendeleo.

MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI

$
0
0
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga ameyataka Mashirika hayo kuwajibika kwa wananchi kwa kuhakikisha wanatekeleza miradi wanayoiombea fedha kwa kushirikiana na Serikali.

Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati alipokutana na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani humo kwa lengo la kujitambulisha, kujadiliana na kujua changamoto zinazoyakabili Mashirika hayo katika kutekeleza majukumu yake.

Bi. Neema amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatakiwa kujiendesha kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchini na kuwa wazi, kuwajibika ila baadhi ya NGOs zimekuwa zikifanya kazi bila kuzingatia uwazi na uwajibikaji hivyo kupeleka upotevu wa rasilimali zilizoombwa kwa lengo la kuwaletea watanzania maendeleo.

Ameongeza kuwa lengo la mkutano huo na wadau wa NGOs mkoani Arusha ni kujadiliana na kupata namna bora za kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya NGOs nchini na kusema kuwa ana imani mkutano huo utatoka na majibu sahihi yatakayowezesha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha kutekeleza majukumu yake katika misingi ya uwazi na uwajibikaji.

Msajili huyo amesisitiza kuwa Serikali inatambua mchango wa Mshirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuwa inatoa ajira kwa watanzania na kusaidiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia Miradi mbalimbali katika Sekta za Afya, Mazingira na Kilimo na Sekta nyingine hivyo kuchangia katika kusogeza mbele gurudumu la maendeleo la taifa.
 Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha katika ziara yake ya kutembelea wadau hao, kutambua changamoto zao na kutoa maelekezo ya uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa fedha na uendeshaji wa miradi yao katika ngazi ya jamii.
 Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Utaratibu mkoa wa Arusha Bw. Moses Mabula akielezea namna Serikali ya mkoa unavyoratibu na kuyasimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ngazi ya Mkoa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga mkoani humo.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Baraka Leonard akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wa mkoa wa Arusha kushoto ni Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga na katikati ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Bw. Ismail Suleiman.
 Mwakilishi wa Shirika la the Girls Foundation of Tanzania Bi. Esther Happy Mariki akiuliza swali kwa Msajili wa NGOs katika kikao kilichowakutanisha Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arisha na Msajili wa NGOs wakati wa Ziara ya Msajili huyo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga mkoani humo
Baadhi ya wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha wakimsikiliza Msajili wa NGOs Bi. Neema Mwanga (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Msajili huyo mkoani humo kujitambulisha na kutambua changamoto za mashirika hayo nchini ili kukuza uwazi na uwajibikaji. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


Wadau wa Elimu Changamani baada ya msingi (IPPE) watakiwa kuboresha elimu katika shule zao ili kukuza kizazi chenye ujuzi

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO
Wadau wa Elimu Changamani baada ya msingi (IPPE) nchini wametakiwa  kubuni mbinu mbalimbali zitakazosaidia kuboresha elimu katika shule zao na kusaidia kujenga kizazi chenye ujuzi,weledi na maarifa ya kupambana na changamoto mbalimbali za maendeleo zinazokabili jamii yetu kwa sasa.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu  Naibu Mkurugenzi Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt Honest Kapasika wa  Taasisi ya Elimu ya Watu wazima(TEWW) nchini wakati akifungua Semina ya siku moja kwa wadau hao leo Jijini Dodoma.
"Semina hii imekuja katika wakati muafaka, ni matumaini yangu kuwa mwisho wa semina hii mtajiwekea maazimio  ambayo kila mmoja anapaswa kufuata",Aliongeza Dkt Kapasika.
Aidha Dkt Kapasika ameeleza kuwa semina hiyo itajikita katika maeneo makuu manne ambayo  ni Kukuza uelewa wa taratibu mbalimbali za uendeshaji wa shule huria zenye programu za mpango wa elimu changania baada ya msingi, Pili zitachambua changamoto  mbalimbali zinazikabili utoaji wa mpango elimu changamani baada ya msingi ,Tatu itasaidi  kukuza uwezo wa wadau wa mpango wa elimu changamani bada ya msingi kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa mtaala wa elimu nje ya mfumo rasmi pamoja na elimu changamani baada ya msingi , Nne  itakuza uelewa wa mfumo wa upimaji na kutunuku vyeti kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi na mpango wa elimu changamani baad aya msingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Elimu Masafa (TEWW) , Baraka Kionywaki amesema  kuwa lengo hasa la semina hiyo ni kuhakikisha kuwa programu hizo zinatolewa katika ubora ambao Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inauhitaji na pia TEWW imeanza kufungia vituo ambavyo vinakiuka programu izo kwa kutoa programu zinazotolewa katika mfumo rasmi.
Nae Sister Erneta Mlelwa kutoka Chuo cha Ufundi Mariele  Namanga amesema kuwa watapokea maelekezo watakayopewa na TEWW ili kuboresha elimu na kukuza kiwango cha ufaulu katika vituo vyao kama inavyotakiwa.
 Kaimu  Naibu Mkurugenzi Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt Honest Kapasika Taasisi ya Elimu ya Watu wazima(TEWW)  akiwaonyesha wamiliki na wasimamizi wa shule huria mfumo wa mtaala kwa ajili ya elimu changamani baada ya Msingi (IPPE) leo Jijini Dodoma.
  Mkuu wa Idara ya Elimu Masafa (TEWW) , Baraka Kionywaki akizungumza na wamiliki na wasimamizi wa shule huria kwa ajili ya elimu changamani baada ya Msingi (IPPE) yenye lengo la kukuza uelewa juu ya uendeshaji wa programu za elimu ya sekondari  leo Jijini Dodoma.
 Wadau wa mpango wa elimu changamani baada ya msingi kutoka Mikoa 14 nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati akifungua Semina ya wadau wa elimu changamani baada ya Msingi (IPPE) kwa wamiliki na wasimamizi wa shule huria leo Jijini Dodoma.
: Kaimu  Naibu Mkurugenzi Taaluma Utafiti na Ushauri Dkt Honest Kapasika Taasisi ya Elimu ya Watu wazima(TEWW)  akiwa katika picha ya pamoja  na wamiliki na wasimamizi wa shule huria kwa ajili ya elimu changamani baada ya Msingi (IPPE) leo Jijini Dodoma. Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO

DKT SINARE YUSUPH AONGOZA KIKAO CHA SIKU MBILI CHA BODI YA WAKURUGENZI YA BARAZA LA KILIMO TANZANIA.

$
0
0


Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku mbili cha Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo kilichoanza leo Jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Baraza la kilimo Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akiwasilisha taarifa ya fedha kwa wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania, kikao hicho cha Bodi kitafanyika Dar es Salaam kwa siku mbili ikiwa ni kikao cha kawaida .
Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bw. Eneck Ndondole (kati kati) akichangia jambo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ubia wa Kilimo Tanzania, Baada ya Mratibu wa Mradi huo kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mradi huo kwenye kikao cha Bodi ya wakurugenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akiongoza kikao cha Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo, kikao hicho cha siku mbili kilichoanza leo jijini Dra es salaam pia kilihudhuliwa na wajumbe wa Bodi na Menejiment ya Baraza la Kilimo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Bi Janeth Bitegeko.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akiongoza kikao cha Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo, kikao hicho cha siku mbili kilichoanza leo jijini Dra es salaam pia kilihudhuliwa na wajumbe wa Bodi na Menejiment ya Baraza la Kilimo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Bi Janeth Bitegeko.

WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO

$
0
0


Na Felix Mwagara, MOHA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia, Kenya na Afrika Kusini katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, na kuwaambia ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao nchini upo vizuri.

Akizungumza katika kikao cha mabalozi hao waliofika ofisini kwake kwa nyakati tofauti leo, Lugola pia aliwaomba wawakilishi hao wa nchi zao hapa nchini waendelee kushirikiana na Wizara yake na nchi kwa ujumla.

Lugola aliwahakikishia Mabalozi hao kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. “Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Balozi wa Afrika Kusini, Thami Mseleku alisema akiwa nchini anajiona kuwa yupo nyumbani kwasababu nchi yake ina historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania. Hata hivyo, Balozi wa Italia, Roberto Mengoni alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza Wizara hiyo na pia alimuakikishia ushirikiano zaidi kati ya nchi yake na Tanzania.

“Hongera sana mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na pia nimefurahi kuja katika ofisini yako kufanya mazungumzo nawe,” alisema Balozi Mengoni. Naye Balozi wa Kenya Nchini, Dan Kazungu alisema Tanzania ni nchi yake na anajisikia furaha kuwepo nchini kwasababu alishawahi kufanyakazi miaka kadhaa iliyopita hapa nchini, hivyo nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Balozi wa Italia, Roberto Mengeni, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Italia. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Afrika Kusini, Thami Mseleku, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Afrika Kusini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Italia, nje ya jengo la ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, kabla ya kuagana na Balozi huyo baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya usalama wa nchi pamoja na ushirikiano kati ya Italia na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini humo leo 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Balozi wa Kenya, Dan Kazungu kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Kenya. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA JUKWAA LA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOANI TABORA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Novemba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Saidi Kanimba  kuhusu viatu vya ngozi vinavyotengenezwa   katika Halmashuri ya wilaya Uyui mkoani Tabora katika Maonyesho ya  Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yailyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sabuni za Kampuni ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora, Imani Matabula  (kulia)  katika  maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imani Matabula. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Imani Matabula  (kulia)  kuhusu sabuni zinazotengenezwa na Kampuni yake ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora katika maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chupa yenye ujazo wa nusu lita yA mkojo wa sungura wakati alipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wasindikaji wa Tabora katika maonyesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji katika Mkoa wa Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Kwa mujibu wa Mratibu wa Wajasiriamali hao, Bibi Ashura Mwazembe, mkojo wa Sungura unatumiwa kama mbolea ya mazao ya kilimo na pia ni dawa nzuri sana ya kuua wadudu waharibifu wa mazao. Lita moja ya mkojo huo inauzwa sh. 10, 000/=. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU ZANZIBAR LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimfungua mkutano huo wa Baraza la Biasha la Taifa Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu leo, 21/11/2018.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 21/11/2018.
BAADHI ya Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano huo leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu ) 

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE

$
0
0


5Y2A9391
Balozi mpya wa Norway nchini Tanzania Mheshimiwa Elisabeth Jacobsen amemtembelea Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ofisini kwake bungeni leo. Balozi huyo amempa Spika salamu mbalimbali kutoka serikali ya nchini kwake.
5Y2A93935Y2A9403

WANAFUNZI WA VYUO MBALIMBALI WAWASILI BUNGENI TAYARI KWA MAANDALIZI YA BUNGE LA VIJANA

$
0
0

Mkurugenzi idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Itifaki Ndugu Eliufoo Daniel akiwakaribisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ambao wamefika bungeni tayari kwa ajili ya kuanza bunge la vijana.

Afisa wa Bunge Idara ya Kamati Ndugu Michael Chikokoto akiwapa elimu jinsi Idara ya kamati inavyofanya kazi bungeni.
Wanafunzi mbalimbali waliokuja bungeni kwa ajili ya bunge la vijana wakipata picha ya pamoja mbele ya mlango wa kuingia ukumbi wa bunge.

MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU

$
0
0
 Leandra Gabriel na Karama Kenyunko Blogu ya jamii
SERIKALI imesema ipo katika mpango wa kutengeneza muongozo ambao utasaidia katika utoaji huduma kwenye hospitali binafsi ikiwemo suala la ongezeko la gharama ambazo zinawafanya wananchi wa kawaida kushindwa kupata huduma.

 Mkurugenzi  wa tiba kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema hayo leo Novemba 20.2018 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa 19 wa wadau wa afya na hospitali binafsi. Amesema kuwa muongozo huo utasaidia hospitali binafsi ambazo hutoa huduma  kwa gharama kubwa kuacha kuwabagua wagonjwa wa dharula kwani ni lazima afya ya mtu ije kwanza.

"Tunashughulikana  hospitali zenye  tozo kubwa kwa wagonjwa, kwani ni sawa kwao kuweka gharama zao kutokana na mfumo wa kutibu magonjwa maalumu, ni sawa kwa hospitali hizo kuwa na gharama zao ila kwa magonjwa ya dharura lazima huduma zitolewe bila kuangalia hadhi ya hospitali hizo" ameeleza Dkt. Gwajima.

Aidha amesema kuwa malengo ya kufanya mkutano huo ni kujadili juu ya kuimarisha utoaji wa huduma katika vituo vyao vya kutolea huduma. Dkt. Gwajima amesema kuwa sekta binafsi zinamiliki asilimia 40 za  utoaji wa huduma za afya nchini  na pia wanashiriki sana katika utoaji ajira na wao kama serikali wanatambua mchango wao na changamoto zao lazima wazifanyie kazi.
 Mwenyekiti wa chama cha wamiliki binafsi wa vituo vya afya nchini (APHFTA) Dkt. Kaushik Ramaiya (kushoto) wakifuatilia mjadala uliozinduliwa na Mkurugenzi wa tiba leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa mtendaji wa APHFTA Dkt. Samwel Ogillo. (Picha na Erick Picson, Blogu ya jamii)
Mkurugenzi wa tiba kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua mkutano wa 19 wa wanachama na wamiliki binafsi wa vituo vya afya leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa mtendaji  wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .
Afisa mtendaji  wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi.

Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo Meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na washiriki wa mkutano huo suala zima ni mashirikiano kati ya Tcra na wadau mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia walengwa ambao ni wananchi.

Amesema kuwa semina hiyo inatakiwa kuwa endelevu na watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwafikishia wananchi kwenye maeneo yao na tutarajie kuondoa changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi hususani ya wizi wa mtandao.“Natoa rai kwa TCRA kuhakikisha changamoto mbali mbali zinazoelekezwa kwao kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa kero na adha wanayokutana nayo wananchi katika maeneo mbali mbali hapa nchini tunashukuru sana sisi tumepata uelewa wa masuala haya ya channel zisizolipiwa na tunaahidi kutoa elimu kwa wananchi”alisema Mwakiposa

Aidha Baadhi ya washiriki mbali mbali walioshiriki katika semina hiyo wamepata uelewa ila wakaitaka Tcra kuenda mbele zaidi katika suala zima la utoaji wa elimu kwa wananchi sanjari na kutatua changamoto mbali mbali wanazokutana nazo walaji wa mamalaka hiyo.

DKT. MPOKI AKEMEA TABIA YA ABIRIA NA MADEREVA KUCHIMBA DAWA MAENEO YASIYOHUSIKA

$
0
0
NA WAJMW-DODOMA

Madereva wa mabasi yaendayo mikoani na abiria wametakiwa kuacha tabia ya kujisaidia “Kuchimba dawa” katika maeneo yasiyo rasmi ili kutunza na kuepuka uharibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja kusababisha magonjwa ya milipuko.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua mkutano unaojumuisha Maafisa Afya kutoka mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini pamoja na wadau wa mazingira, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Dkt. Mpoki amekemea tabia hiyo hatarishi kwa ustawi wa mazingira huku akiwataka maafisa Afya na wadau wa mazingira nchini kusimamia afua zilizowekwa zinaendelea kutekelezwa ili kulinda mazingira ambayo yanatuzunguka.

“Kuna watu wengine nimeshawahi kuwaona kwenye basi wanatupa taka ovyo na mabasi mengine yanasimama porini ili abiria wajisaidie, hii tabia siyo nzuri na inatakiwa ikemewe kwa nguvu zote, Idara ya Kinga Pamoja na wadau wao wanakuja na mpango mkakati wa kuondoa kabisa dhana ya watu kusimama kujisaidia porini, "sisi tunatakiwa kuwa msitari wa mbele kupiga marufuku mabasi kusafiri bila kuchafua mazingira”.

Dkt. Mpoki amesema ni aibu kubwa kwa taifa kuona watu hawafuati kanuni za usafi huku akiwataka Maafisa Afya kuhakikisha wanafanya kazi kwa nguvu ili ionekane kuwa kero kwa watu wengine na watakaobainika kuchafua mazingira wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa neno mbele ya Maafisa Afya wa Mkoa, Halmashauri pamoja na Wadau wa Mazingira leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akikagua maonesho ya vyoo baada ya kufungua kikao cha Maafisa Afya wa Mkoa, Halmashauri pamoja na Wadau wa Mazingira leo jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete. 
 Maafisa Afya wa Mkoa na Halmashauri wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano wao uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dodoma katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete wenye lengo la  kusisitiza umuhimu wa mazingira.
 Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya katika baada ya kikao cha  Maafisa Afya wa Mkoa, Halmashauri pamoja na Wadau wa Mazingira kilichofanyika leo jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

SPIKA NDUGAI AWAPA SOMO WABUNGE BUNGE LA VIJANA JIJINI DODOMA

$
0
0

Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma 

Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka wabunge Bunge la Vijana, kutumia mafunzo ya Bunge hilo kwa weledi wa kutosha juu ya uendeshaji wa Bunge na kuwa mabalozi wazuri watakaporejea vyuoni.

Spika ameyasema leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Bunge la Tano la Vijana ukiwa na lengo la kuwaandaa Vijana kuwa viongozi bora wa baadaye lakini pia kuwa na mijadala inayofika mwisho bila kugombana.Mkutano Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa kuwajengea uwezo wabunge awamu ya pili (LSP II) na kufanyika katika ukumbini wa Pius Msekwa.

Spika amesema kuwa mkutano wa Bunge hili ambao umejumuisha vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya juu , lina lengo la kuwawezesha Vijana hao kutumia mijadala zaidi na viongozi wao wawapo vyuoni badala ya kukimbilia migomo katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.

Aidha Spika amebainisha kuwa, shabaha ya Bunge hilo ni kuwawezesha vijana kuelewa taratibu za uendeshaji wa Bunge,kuwafundisha Vijana Utamaduni wa kuvumiliana kwa kubishana kwa hoja na kuheshimu wengine kuwaelimisha Vijana juu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii na Taifa kwa ujumla na kuwafundisha vijana umuhimu wa kufikia maamuzi baada ya mjadala wa pamoja.

Spika amewaomba wabunge kutumia mafunzo ya Bunge hilo kuwa na weledi wa kutosha juu ya uendeshaji wa Bunge na kuwataka kuwa mabalozi wazuri watakaporejea vyuoni. Akimkaribisha Ndugai, Spika wa Bunge hilo Zephania Sane amesema kuwa matarajio yao ni kujifunza jinsi Bunge linavyofanya kazi hususan ya kupitisha miswada na kutungwa Sheria za Nchi.Mhe.Sane amesema kuwa Vijana wapo pamoja na Rais John Magufuli na wanamuunga katika kila anachokifanya kwa mustakabali wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Bunge hilo ambalo linafanyika kwa muda wa siku tano, limejumuisha Vijana 60 kutoka Vyuo vya Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP),Chuo Kikuu cha Dodoma,Chuo cha Biashara Tawi la Dodoma (CBE) Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro na Chuo Kikuu cha Uhasibu Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Bunge la Vijana mwaka 2018 linalofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma kulia kwake ni Spika wa Bunge la Vijana Mhe. Zephania Sane na kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Ashiruna Mhunzi 
Mapambe wa Bunge akiongoza msafara wa Spika wa Bunge la Vijana kuingia Ukumbini kwa ajili ya kuanza Kikao cha Kwanza cha Bunge hilo kwa mwaka 2018 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. 
Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiapa kushika nafasi hiyo mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Ndugu Alphonsina Ambrosi. Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018 unaendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Vijana mwaka 2018 wa wakila kiapo cha utii mbele ya Spika wa Bunge hilo la vijana, Mhe. Zaphania Sane.wengine ni Makatibu Kamati wa Bunge hilo.

Spika wa Bunge wa Bunge , Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Bunge la Vijana mwaka 2018 Mhe. Zephania Sane kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge hilo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Mhe. Ndugai alikuwa mgeni ramsi na alifungua Bunge hilo la Vijana.

KIKAO KILICHOWAKUTANISHA WADAU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI MKOANI ARUSHA NA MSAJILI WA NGOs

Kumi kufanyiwa upasuaji wa mafindofindo Mtwara

$
0
0

Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wataalam wa afya wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara-Ligula- leo wanawafanyia upasuaji wagonjwa 10 wenye matatizo ya mafindofindo.

Matibabu hayo ya kibingwa hayafanyiki katika Hospitali ya Ligula kutokana na ukosefu wa wataalam waliobobea katika maeneo ya pua, koo na masikio.
Daktari Bingwa wa upasuaji pua, koo na masiko kutoka Muhimbili Willybroad Massawe amesema wanawafanyia upasuaji watu wazima pamoja na watoto na kwamba upasuaji huo umeanza kufanyika leo.

‘’Tumeanza kufanya upasuaji huu leo asubuhi na lengo letu ni kumaliza wagonjwa wote kumi leo hii’’ amesema Dkt. Massawe. Kwa mujibu wa mtaalam huyo ugonjwa wa mafindofindo unasababishwa na maambukizi ya mara kwa mara katika njia ya hewa na kwa wengine unatokana na mzio (allergies) zilizokithiri.

Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanzisha programu ya kutoa huduma kwa njia ya mkoba ili kujenga uwezo wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini hasa katika maeneo yenye wataalam lakini wanahitaji kuongezewa ujuzi zaidi katika fani mbalimbali ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili. 

Daktari Bingwa wa upasuaji pua, koo na masikio Willybroad Massawe akimtoa mgonjwa matezi ya koo na matezi ya nyama ya pua (mafindofindo), upasuaji huo umefanyika leo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara-Ligula.
Mtaalam wa usingizi (nusu kaputi) Dkt. Amon Kingu (kushoto) pamoja na watalaam wengine wa Hospitali ya Ligula wakiwamuandaa mgonjwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. 

Tanzania yashinda Tuzo ya Utalii nchini Urusi

$
0
0


Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii duniani nchini Urusi kwa mwaka 2018 (The Best Destination to the World in the Category of Exotic Destination 2018).

Leo tarehe 21 Novemba 2018, Balozi wetu nchini Urusi Mhe. Maj. Gen. (Mst). Simon Mumwi atapokea Tuzo hiyo kutoka Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine” jijini Moscow kwa niaba ya nchi. 

Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “National Geographic Magazine” lililoshirikisha wapiga kura 263,000 kwa njia ya mtandao.

Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka saba tokea mwaka 2011, raia wa Urusi kupitia jarida hilo wanaichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii. Mwaka 2011, Zanzibar ilipata tuzo ya ‘Star Travel’ kama eneo bora zaidi la utalii wa ufukweni katika bara la Afrika na mwaka jana, Tanzania ilipata tuzo ya NGT na Tanzania ilishinda nafasi ya pili katika tuzo hiyo katika kundi la eneo bora la utalii duniani.

“National Geographic Traveller Awards” (NGT Awards) ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii nchini Urusi na hutolewa na Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine”.

Mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wetu Urusi, Wizara za Utalii za Tanzania Bara na Zanzibar, na Taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.Kupitia juhudi hizi, idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kutoka Urusi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, idadi hiyo imeongezeka kutoka watalii 4,021 mwaka 2012 hadi watalii 10,060 mwaka 2017. 

Wizara kupitia Ubalozi wetu itaendelea kuongeza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na tunategemea kwa kushirikiana na wadau wengine katika juhudi hizi, idadi ya watalii kutoka Urusi wanaokuja nchini itaongezeka zaidi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
21 Novemba 2018

RC Mwanri Amvunja Mbavu Waziri Mkuu "Nchi inakata roho"

DAS CHEMBA ALONGA

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images