Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 24 | 25 | (Page 26) | 27 | 28 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights,Balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Tajammul Altaf akizungumza katika uzinduzi huo ambapo amasema amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na mfanyabiashara kutoka nchini kwake na jinsi Tanzania ilivyoweza kumpa ushirikiano na hatimaye sasa matunda yameonekana kwa kuzaliwa jengo la Uhuru Heights lenye hadi ya Kimataifa.Aidha amesema huo ni mwanzo tu na kuwataka wafanyabiashara zaidi kutoka Pakistan kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu mahali ambapo ukiwekeza matunda yanaonekana kutokana na amani na utulivu uliopo na ushirikiano wa serikali.
  Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights, Muhammad Owasi Pardesi akizungumza na wageni wakati wa uzinduzi wa jengo hilo na kutoa shukrani zake akisema sasa wakazi wa Dar es Salaam wataweza kununua nyumba kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya International Commercial (ICB) na kulipa kwa muda wa miaka 10 na kuishi katika miongoni mwa majengo marefu ya makazi yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam lililojengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Bilioni 40.
  Amesema Malengo ya kampuni ya Cosmos Group ni kuboresha miundo mbinu na maisha ya watu na hayo yamezingatiwa kwa kujenga jengo la Uhuru Heights.
  Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuingia mkataba wa kufanya biashara pamoja baina ya Cosmos, IBC Benki na Exim.
  MC katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Hegihts Taji Liundi.
  Muonekano wa Jengo la Uhuru Heights lililopo barabara ya Bibi Titi Mohammed liking'arisha jiji la Dar nyakati za usiku.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Wahandisi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani cha ndege yao aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilipata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida. 

  Matengenezo hayo yanafanyika katika uwanja wa ndege wa Kigoma yakisimamiwa na Mhandisi Righton Mwakipesile na Mhandisi Merkior Karwani.

  Uongozi wa ATCL umedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba yao inavyoonyesha punde kuanzia kesho tarehe 22/1/2013. 


  0 0

  MWENYEKITI wa kamati ya kuratibu Tamasha la kila mwaka la Pasaka, Alex Msama, amesema tukio hilo linalohusisha onyesho la muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi, ni la kila mtu kwani litaendelea kusaidia makundi mbalimbali yasiyojiweza na walemavu. 

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Msama alisema ingawa wao ni waratibu, lakini lengo hasa la tamasha hilo ni kupata kiasi cha fedha za kuwapatia watu wanaohitaji msaada, kama vile watoto yatima, walemavu wa aina mbalimbali na wale wanaokumbwa na majanga makubwa. “Hili ni tamasha lao, wao ndiyo wadau wakubwa kwa sababu wananufaika nalo. Kila mtu ni shahidi kuwa tumekuwa tukitoa misaada ya aina mbalimbali kwa makundi maalum ya watu. 

  Hata hivyo, ni vyema pia tukaweka wazi kuwa wanaowezesha haya yote ni watu wanaokuja kuunga mkono tukio hili linalofanyika kila mwaka,” alisema Msama. Kuhusu tamasha la mwaka huu, Msama alisema hawezi kulizungumzia kwa undani kwa sasa kwa vile bado wanaendelea na taratibu za kupata kibali chake na wakishafanikisha suala hilo, wataweka wazi kwa umma ili ujue. Katika tamasha la mwaka jana lililofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, waimbaji mbalimbali maarufu walipanda jukwaani na kutoa burudani safi. 

  Miongoni mwao walikuwa ni Rose Mhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival. Waimbaji wan je walioshiriki tamasha hilo ni pamoja na Rebeca Malope wa Afrika Kusini, Maryanne Tutuma, Solomon Mukubwa na Anastazia Mukabwa (Kenya), Faraja Ntaboba (Congo) na Ephraim Sekeleti.

  0 0

  Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakiwajibika katika onesho lake maalumu la kumtambulisha mwimbaji mpya wa bendi hiyo,Othumani Kambi (wa pili kulia). wengine ni Hassani Moshi (kushoto) Eddo Sanga na Juma Katundu,onesho hilo lililofanyika katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni,jijini Dar.
  Mashabiki wa bendi ya msondo ngoma music wakicheza kwa furaha wakati wa onesho maalumu la kumtambulisha mwimbaji mpya wa bendi hiyo,Othumani Kambi. Picha na www.burudan.blogspot.com.

  0 0


  Na Anna Nkinda – Paris
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amesisitiza umuhimu wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kupewa chanjo kwa wakati, chakula chenye virutubisho na kuwafundisha kinamama jinsi ya kuwatunza kwa  kufanya hivyo nchi itakuwa inapanda mbegu nzuri na baada ya miaka michache taifa litakuwa na watoto wenye afya bora.
  Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ameyasema hayo jana wakati akiongea na wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu la nchini Ufaransa ambalo licha ya kutoa huduma mbalimbali za dharula pia linatoa huduma za afya kwa  watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
  Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema kuwa ili kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano Serikali kwa kushirikiana na shirika la GAVI Alliance kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa chanjo ya kuzuia magonjwa ya homa ya vichomi na uti wa mgongo  nchini Tanzania.
  “Taasisi ya WAMA imekuwa ikitoa vifaa tiba inavyochangiwa  na wadau  mbalimbali  katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati ambazo zimekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vitanda vya kulalia wagonjwa, mashine za kupumulia watoto wanaozaliwa wakiwa na matatizo.
  Pia kwa kushirikiana na shirika la AMREF International taasisi ya hii imetoa mafunzo kwa  manesi ambao wameweza kuwaelimisha watoto wa kike walioko mashuleni  jinsi ya kujiepusha na mimba za utotoni”, alisema Mama Kikwete.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhusiano na Oparesheni za Kimataifa za Shirika hilo Antoine Peigney alisema kuwa shirika hilo linafanya kazi za kukabiliana na majanga katika nchi 30 Duniani na limeajiri wafanyakazi 17000 pia  watu 20000 kutoka nchi hizo wanafanya kazi za kujitolea.
  Alisema kuwa Shirika hilo limekuwa likilisaidia Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania pale lilipoombwa kutoa msaada na kutoa mfano mwaka  2004, 2006 na 2009 lilitoa msaada katika mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na mwaka 2011 katika mkoa wa Manyara hivyo basi watafurahi zaidi kama watapata nafasi ya kufanya kazi na taasisi ya WAMA ili waweze kuwasaidia watanzania.
  Mama Kikwete ameambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Ufaransa kwa ajili ya mwaliko wa  ziara ya kiserikali ya siku tatu.

  0 0
 • 01/21/13--22:57: kumbukumbu
 • MAREHEMU MZEE ROBERT LUCAS JAKA

  Hatimaye siku , miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia mwaka mmoja (1) tangu ulipofariki mchana ule wa siku ya Jumapili, Januari 22 , 2012.

  Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe Kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.Tunakukumbuka kwa Upendo, Busara, na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na marafiki.

  Daima unakumbukwa sana na watoto wako wapendwa,wapendwa wajukuu zako, ndugu zako, wanajumuiya, majirani, jamaa na Marafiki zako wote.

  Tutaendelea kukukumbuka daima siku zote za uhai wetu, wakati huo huo tunakuombea Mwenyezi Mungu aendelee kuiweka roho yako mahali pema peponi.

  -RAHA YA MILELE UMPE EH BWANA NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE ROHO ZA MAREHEMU MZEE ROBERT JAKA IPUMZIKE KWA AMANI

  0 0

  The University of Dar es Salaam (UDSM), Center for Virtual Learning(CVL) is organizing a 5 days training to equip participants with the skills, knowledge and techniques for designing and developing good websites without even being experts by using Open Source Content Management System (CMS) called Joomla! CMS 2.5.8

  Joomla is an award-winning CMS, which enables people to build Websites, as well as Web based applications. A summary of course outline can be found from the College website: www.coict.udsm.ac.tz


  Target Audience

  • Individuals who would like to have their very own website.

  • Owner of an existing Joomla website built by another 3rd party.

  • SMEs and small businesses who wish to cut down the costs of web development projects and manage their own websites.

  • Individuals who wish to be self-employed in Website development


  • Web masters, website administrator, computer systems analysts, public relationship officers, communication officers and entrepreneurs.


  Training fee:  Tsh. 500,000/= (excluding breakfast and lunch)

  Venue:  UDSM Kijitonyama Campus (Former TTCL Staff College), Dar Es Salaam

  Registration:Please register NOW through the College website: www.coict.udsm.ac.tz

  Certificate of attendance:  will be provided upon completion of the course.

  For more information contact us at saganda@udsm.ac.tz; Telephone: +255715471705


  0 0

  Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama wakiwa katika majadiliano ya wazi, yaliyohusu ulinzi wa amani, ujenzi wa amani na maendeleo, majadiliano hayo yamefanyika siku ya jumatatu na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, Tanzania kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu, Balozi Tuvako Manongi, imesisitiza Baraza hilo kuendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazolenga kurejesha amani ya kudumu katika DRC hususani eneo la Mashariki ya nchi hiyo.

  0 0
 • 01/21/13--23:18: Article 3


 • 0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa salamu zake kwenye hafla ya Usiku wa Tarangire iliyokuwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani na pia kumuaga aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Ndg. Martin Laiboki ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uhifadhi na Ekolojia TANAPA Makao Makuu, hafla hiyo ilifanyika katika Hifadhi ya Tarangire.
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo (wa pili kulia) akimkabidhi Kamba Ndg. Martin Laiboki kama ishara ya zawadi ya Ng’ombe aliyozawadiwa na Uongozi na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Tarangire kwenye hafla ya jioni ya kumuaga baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uhifadhi na Ekolojia TANAPA Makao Makuu, awali Ndg. Laiboki alikuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire.
  Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El – Saadat (katikati) akifungua Champaign kwenye hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini hapo ambapo Bendi hiyo FM Academia ilitumbuiza na pia iliimba kibao maalumu kinachohamasisha utalii wa ndani kwa watanzania.
  Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba/miwani), Mkuu wa Mkoa Manyara Elaston Mbwilo (kulia kwa Dr. Nchimbi) Uongozi na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Tarangire wakiserebuka kwa muziki wa Bendi ya FM Academia wakati wa hafla ya Usiku wa Tarangire iliyofanyika hifadhini hapo.
  Wanamuziki wa Bendi ya FM Academia wakionesha vitu vyao wakati wa Hafla ya usiku wa Tarangire iliyofanyika kwenye hifadhi hiyo ya Taifa.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika Viwanja vya Makaburi ya Mashujaa jijini Harare, walipohudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo yaliyofanyika jana jijini Harare Zimbwabwe.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kushoto akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alipomtembelea Ikulu ya Harare jana kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu Dkt. Landa John Nkoma kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare baada ya kumaliza mazungumzo yao. Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dkt. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita. Dkt. Nkomo alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare baada ya kumaliza mazungumzo yao. Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dkt. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita. Dkt. Nkomo alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.PICHA NA OMR.

  0 0

  TAARIFA ILIYOIKIA GLOBU YA JAMII HIVI SASA TOKA JIJINI MWANZA,INAELEZA KUWA KUNA HALI YA HATARI INAENDELEA HIVI SASA JIJINI HUMO KATIKA MTAA WA MISSION BARABARA IENDAYO AIRPORT,KUTOKANA NA WAENDESHA BODA BODA KUANZA KUANDAMANA KUPINGA PATROO INAYOFANYWA NA JESHI LA POLISI LA KUWAKAMATA WALE WOTE WASIOKUWA NA LESENI ZA KUENDESHEA VYOMBO HIVYO PAMOJA NA VIFAA VYA KUJIKINGA.

  JESHI LA POLISI LIMELAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI NA RISASI ILI KUZUIA GHASIA HIYO .

  "KWAKWELI HALI NI MBAYA SANA HAPA MWANZA HIVI SASA,KWANI RISASI ZINALIA KAMA VITANI,YAANI NIMO NDANI YA OFISI YANGU NA NAONA JINSI POLISI WANAVYOTUMIA NGUVU KUBWA KUPITA KIASI,YAANI NI RISASI TUPU NA NIMEJIFUNGIA NDANI YA OFISI." HIVI NDIVYO ALIVYOKUWA AKISEMA MTOA TAARIFA.

  ALIENDELEA KUSEMA "WATU WANAKIMBIA HUKU NA KULE NA WATU WA BODA BODA WAMEFUNGA BARABARA KWA MAWE,YAANI NI BALAA TUPU HAPA MAKONGORO ROAD.WADAU MNIOMBEE RISASI ISIPITE DIRISHANI IKANIKUTA KWENYE MEZA YANGU. MUNGU IBARIKI TANZANIA.JAMANI AMANI IDUMISHWE" 

  HIVYO NDIVYO MAMBO YALIVYO HIZI SASA,NA TUTAENDELEA KUJUZANA KADRI TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.

  0 0
 • 01/22/13--04:43: SHUKURANI
 • Familia ya Marehemu Siraju Juma Kaboyonga (pichani) inatoa shukurani zake za dhati kwa wote walioshiriki kwenye msiba na mazishi ya mpendwa wao Siraju Juma Kaboyonga aliyefariki tarehe 18/12/2012 na kuzikwa tarehe 20/12/1012 katika Makaburi ya Kisutu Dar es salaam.

  Tunatoa shukurani za dhati Kwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete - Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais mheshimiwa Gharib bilal ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………kwa taasisi, makampuni, ndugu, jamaa na marafiki kutoka Tabora, Mwanza Dodoma na kwingineko ambayo kwa aina ya pekee walijitolea kwa hali na mali kufanikisha mazishi ya mpendwa wetu.

  Ni vigumu kutaja kila mtu ILA Kwa uchache tunapenda kutoa shukurani za pekee Kwa NSSF, PPF, PSPF, TEA, SSRA, Ofisi ya Makamu WA Rais, Mfuko WA pembejeo, mheshimiwa Malima na Sheikh Yusufu wa Masjid Kuba.

  Tunamwomba mwenyezimungu awaongezee pale mlipotoa na awajalie upendo wenu uzidi daima dumu. Yote yaliyotokea ni mapenzi ya Mwenyezimungu mwingi wa Rehema mwenye Kurehemu.

  Tunamwomba mwenyezimungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Arobaini ya marehemu itasomwa nyumbani kwake Sinza Mori tarehe 26/01/2013 saa saba mchana.
  Wote mnakaribishwa kwenye shughuli ya arobaini Inshallah.

  INNA LILAH WAINA ILAH RAJIGHUUN


  0 0


  Kapteni  Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8 Q300 Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22.Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.


   Marubani   wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es Salaam leo asubuhi.

  Hii ni baada ya wahandisi wa shirika hilo kukamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani. Ndege hii aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilisitisha safari zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele katika chumba cha marubani kupata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida, imeanza tena safari za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
  Abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa ndege wa Kigoma, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam.

  0 0
 • 01/22/13--11:53: iPhone 4S - 16GB For Sale

 • iPhone 4S - 16GB For Sale (Almost like brand new)

  I am selling my iPhone 4S which I only used for three months before getting iPhone 5.
  It is white, well looked after and no scratch marks whatsoever. Just like new. It comes in its original box with charger.
  I live in the UK. The phone has been shipped and is now in Dar. You won’t pay until you have seen the phone. If interested get in touch.
  Price: Tsh 990,000
  The first person to see it will buy.

  0 0

  Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Hair Industry ltd James Walwa - Jimmy (kulia) akimkabidhi mbunifu wa mavazi nchini,Ally Rehmtullah tiketi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Afrika Mashariki katika mkutano wa 'The Economics of the Africa Fashion Industry' utakaofanyika nchini Marekani mwezi wa Februari. Tanzania Hair Industry ltd ambao ndio watengenezaji wa nywele maarufu aina ya Darling ndio wadhamini wa safari ya mbunifu huyu kwenye mkutano huo wa kihistoria utakaofanyika katika Kikuu cha Havard nchini Marekani.

  0 0
 • 01/22/13--12:09: Kali TV Online This week...

 • 0 0

  KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner aliyemtembelea leo, Januari 22, 2013, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. kwa ajili ya mazungumzo maalum ya kikazi.
  KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na mgeni wake, Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko.
  KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, baada ya mazungumzo yao, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2013. Wapili kulia ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0
 • 01/22/13--13:22: Article 18


older | 1 | .... | 24 | 25 | (Page 26) | 27 | 28 | .... | 3278 | newer