Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

DKT .PIMA ASEMA MSHIKAMO KATI YAO NA MADIWANI NDIO SIRI YA KALIUA KUFANYA VIZURI KWENYE ELIMU NA UKUSANYAJI MAPATO

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

UMOJA na kufanyakazi kwa ushirikiano miongoni mwa Watendaji na Madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Kaliua ndio sababu ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye mtihani wa darasa la saba , afya na ukusanyaji mapato mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani baadaya Watendaji wake kupongezwa kwa uchapaji kazi mzuri.Alisema kufanya vizuri katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi na kuwawezesha kuwa wa kwanza kimkoa na kutoa mwanafunzi bora wa kiume kitaifa na kuwa wa nne kitaifa katika ukusanyaji wa mapato na kushika nafasi ya nne kitaifa ni sababu ya uwepo wa mshikamano kati yao na Madiwani.

Dkt. Pima aliongeza kuwa hata kule kufanya vizuri katika mpango wa afya wa RBF na kuifanya Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kimkoa ni sababu ya ushauri kutoka Kamati ya Elimu , Afya na Maji.Alisema wao kama watendaji wataendelea kupokea ushauri mzuri kwa ajili ya kuendelea kulinda nafasi waliyopata.Kuhusu Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mitihani yake ya kumaliza Darasa la Saba , alisema wataendelea kuwa naye karibu ili aendelee kufanya vizuri kwa ajili ya kuwa kioo cha Kaliua.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele alisema Baraza la Madiwani linawapongeza Watendaji wote waliofanyakazi kwa bidii na kuiwezesha Halmashauri hiyo kufanya vizuri kimkoa katika elimu na kiafya na kuwa wa nne kitaifa katika ukusanyaji mapato.Aliagiza Watendaji katika Idara zilizofanya vizuri ni vema wakapongezwa na kupewa cheti kinachotambua mchango wao uliong’arisha Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua katika maeneo hayo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kaliua Magalena Sakaya alitaka kuanzishwa kwa zoezi la kuwashindanisha watumishi na wakuu wao wa idara katika Halmashauri ya Kaliua ili wanaofanya vizuri wapongezwe na wanaofanya vibaya warekebiswe ili kuendelea kuifanya Kaliua iwe ya kwanza sio tu kwa ngazi ya Mkoa hata kitaifa. 
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao kilichokuwa kikijadili taarifa za utekelezaji wa robo mwaka kilichofanyika jana.

KALIUA WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUWAONDOA MAAFISA UGANI OFISINI NA KWENDA KWA WAKULIMA.

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT,TABORA

HALMASHAURI ya Wilaya Kaliua imekamilisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kuwataka Maafisa Ugani kuondoka Ofisini na kwenda vijijini ili kuwasaidia wakulima katika uboreshaji wa kilimo chao kwa ajili ya maendeleo yao na taifa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima wakati akijibu hoja za Madiwani katika kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa za utekelezaji.

Alisema hivi katika Ofisi za Halmashauri hiyo wamebaki Maafisa Kilimo wawili ambao ndio wanashughuli na shughuli za makao makuu ya Halmashauri na kuratibu wa mambo mengine yanayohusu masuala ya kilimo kupitia wilaya.Dkt. Pima aliowaomba Madiwani kuhakikisha wanawasimamia na kufuatilia utendaji wao wa Maafisa hao katika Kata zao ili waweze kutoa huduma na ushauri mzuri kwa wakulima kwa ajili ya kuwafanya wazalishe mazao yenye tija na manufaa kwao na kwa Halmashauri yao.

Awali Mbunge wa Jimbo la Kaliua Magdalena Sakaya alisema Halmashauri hiyo sehemu kubwa inategemea kilimo kukusanya mapato yake ya ndani na kuwataka kuwa karibu na wakulima kwa ajili ya kushauri na kuwasimamia ili waweze na uzalisjai mzuri.Alisema msimu wa kilimo kilichopita wakulima hawakuweza kufanya vizuri kutokana na mazao yakiwemo mahindi kushambuliwa na wadudu na hivyo kujikuta wakiapata mavunoa hafifu kinyume cha matarajio yao.

Sakaya alisisitiza kuwa uwepo wa karibu wa Maafisa ugani hoa kwa wakulima kutawawezesha kujua mapema matatizo wanayokabiliana nao na kuyatatua.Upelekeji wa Maafisa kilimo vijijni ni mkakati wa wilaya hiyo wa kuinua kilimo na pia unatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa akiwa mkoani Tabora la kuwataka watendaji hasa wanahusika moja kwa moja na wananchi kuwafuata na kuwasaidia kutatua matatizo yao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele akifungua kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa robo mwaka wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani jana.

MICHUZI TV: HII NDIO KAULI YA MBUNGE KINGU KWA RAIS DKT MAGUFULI

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MOROGORO (SUA) ASHINDA BAJAJ

$
0
0
Tangu ameanza kucheza SportPesa haikuchukua muda mrefu mpaka pale alipotangazwa kuwa ni mshindi wa Shinda Zaidi na SportPesa na kufanikiwa kushinda bajaj mpya kabisa kutoka timu ya ushindi.

Huyu ni Mgaya Hassan mshindi wa Droo Ya 43 yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu na mkoani Morogoro lakini ushindi wa bajaj umemkuta akiwa hapa jijini Dar es Salaam wakati akimalizia likizo yake kwa kaka yake.

Na Timu Ya Ushindi haikutaka Kumcheleweshea Ilimfuata mpaka Bunju Hapa Dar es salaam Nyumbani kwa Kaka Yake Na Kumkabidhi Bajaj. Akikabidhiwa bajaji ya ushindi Hassan alisema alianza kucheza na SportPesa baada ya kusikia kwenye redio na tv kuwa kuna bajaj zinatolewa na yeye moja kwa moja akijasajili na kuanza kutupia bashiri kwenye mechi mbalimbali hatimaye kufanikiwa kushinda.

"Mimi ni mwanafunzi nasoma SUA Morogoro taarifa hizi za ushindi zimenikuta hapa Dar es salaam wakati nikiwa likizo, nimefurahi sana maana wakati nacheza wanafunzi wenzangu waliniambia mimi siwezi kushinda kwa sababu naweka pesa ndongondogo waliamini kuwa wanaoshinda ni wale ambao hubashiri kwa pesa nyingi kumbe sivyo kila mtu ana nafasi ya kushinda maana mimi nilikuwa nacheza kwa elfu moja moja pekee sasa nimeshinda najua wakiniona ndio wataamini yani nina furaha sana" alisema Hassan

Aidha Hassan anasema bajaji hii itamkomboa kutoka kwenye maisha ya sintofahamu na kuingia kwenye maisha mazuri huku akitegemea kipato kitakachopatikana kutokana na bajaj kumsaidia kwenye mahitaji yake ya chuoni na nyingine kuwawezesha ndugu zake ambao hawako vizuri kiuchumi. 

"Daaah maisha ya chuo ni magumu sana unatoka chuo umechoka wakati mwingine huna pesa ya kula familia zetu nazo zinatoka katika mazingira ya kimaskini unajikuta huna cha kufanya lakini kwa ushindi huu wa bajaj ntaweza jikimu mimi mwenyewe maana kila siku ntakuwa na uhakika wa kupata chochote kutokana na bajaji hii" aliongeza Hassan.

Hassan aliwaomba wanafunzi wenzake wa vyuoni wale ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na zaidi kucheza na SportPesa maana wanaweza jikuta wakiandika historia mpya kwenye maisha yao na kumudu gharama ndogondogo zinazopatikana chuoni.

  Mgaya Hassan mshindi wa Droo Ya 43 yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu na mkoani Morogoro lakini ushindi wa bajaj umemkuta akiwa hapa jijini Dar es Salaam wakati akimalizia likizo yake kwa kaka yake.

MKAPA AWASILI UGANDA KUWASILISHA RIPOTI YA USULUHISHI YA MGOGORO WA BURUNDI KWA RAIS MUSEVENI

$
0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa Burundi akiwa katika chumba cha wageni maalum katika uwanja wa Ndege wa Entebbe leo. kulia ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, Brig Gen. Mkumbo, kushoto ni Msaidizi wa Rais Mkapa katika utatuzi wa mgogoro huo, Balozi David Kapya na anayemfuatia ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima. Mkapa aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe asubuhi ya tarehe 19 Novemba 2018 kwa ajili ya kuwasilisha ripoti ya mkutano wa upatanishi uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha kwa Mpatanishi Mkuu wa mgogoro huo Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni. 
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akimsikiliza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa Burundi. Rais Mkapa aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe asubuhi ya tarehe 19 Novemba 2018 kwa ajili ya kuwasilisha ripoti ya mkutano wa upatanishi uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha kwa Mpatanishi Mkuu wa mgogoro huo Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni. 
Mhe. Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mlima, Balozi Kapya na Bw. Makocha Tembele ambaye ni Katibu wa Rais Mkapa. 

RAIS wa Zanzibar Dk. Shein Azungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani,Kangi Lugola Ikulu Zanzibar

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Shein, akiwa na Viongozi wa Wizara hiyo Katibu Mkuu Meja Jenerali.Jocob G.Kingu na Naibu Katibu Mkuu Ndg. Kailima Ramadhan, leo Ikulu Zanzibar Novemba 19/11/2018.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, alipofika Ikulu Zanzibar na Viongozi wa Wizara hiyo kujitambulisha rasmin kwa Rais wa Zanzibar Dk. Shein leo Ikulu Zanzibar.Novemba 19/11/2018(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola, walipofika Ikulu Zanzibar kuona na Rais wa Zanzibar Dk. Shein, kwa kujitamulisha na kufanya mazungunzo leo Ikulu Zanzibar, novemba 19/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizuingumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dk. Shein, novemba 19/11/2018.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Kangi Lugola, baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Zanzibar leo 19/11/2018.(Picha na Ikulu )
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Kangi Lugola, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 19/11/2018.(Picha na Ikulu )

MICHUZI TV:MBUNGE WA KASULU VIJIJINI AZUNGUMZIA HARAKATI ZA MAENDELEO JIMBONI KWAKE

Wajasiriamali Nchini Kuendelea Kunufaika na Urasimishaji wa Biashara

$
0
0
Wajasiriamali Nchini kuendelea kunufaika na Mpango wa Kurasimisha Biashara katika mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaniunua wajasiriamali hao. 

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe yanayolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kuongeza tija na kuchangia katika ujenzi wa Taifa, Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa lengo ni kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao. 

“Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Bunge kwa kuiwezesha MKURABITA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi hasa katika eneo la kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili warasimishe Biashara zao;’’ Alisisitiza Mgembe 

Akifafanua amesema kuwa mafunzo yakuwajengea uwezo Wajasiriamali hao yameendeshwa kwa siku 10 ambapo kila kundi lilikuwa na siku mbili za kujifunza mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali zikiwemo benki kama; CRDB Bank na NMB . 

Taasisi nyingine zilizoshiriki katika kutoa mada katika mafunzo hayo ni pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO, Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na wataalamu wengine wa ujasiriamali. 

Pia, alipongeza ushirikiano ulipo kati ya MKURABITA na Mkoa wa Njombe hali iliyosaidia katika kufanisha mafunzo kwa wajasiriamali na pia urasimishaji ardhi kwa wananchi ambapo baadhi yao wameweza kupata mikopo katika Taasisi za fedha na hivyo kuinua uchumi wao kutokana na kukua kwa shughuli za ujasiriamali walizokuwa wanafanya na hasa kutokana na mikopo waliyopata kutoka katika Taasisi za fedha zikiwemo Benki. 
 Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia  Mgembe akizungumza na sehemu ya wajasiriamali wa Halmashauri ya Mji wa Njombe wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biasharaza zao hali itakayowawezesha kuongeza tija na kupata mikopo katika Taasisi za fedha.hiyo ilikuwa Novemba 16,2018 Mkoani Njombe.

 Sehemu ya Wajasiriamali wa Halmashuri ya Mji wa Njombe wakimsikiliza Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia  Mghembe (Hayupo pichani)  leo mjini Njombe wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali wa  Halmashauri hiyo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kurasimisha Biashara zao.

 Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) Mkoa wa Njombe Bw. Stanley Sulle Akiwasilisha mada kwa wajasiriamali hao kuhusu taratibu za ulipaji kodi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kurasimishaji biashara zao na hivyo kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa kulipa kodi, Mafunzo hayo yameandaliwa na MKURABITA.



 Mmoja wa wajasiriamali  waliopata mafunzo ya kujengewa uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao Bi. Sesilia Mwalyego akizungumza katika mafunzo hayo leo Mjini Njombe, Mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao.

 Mmoja wa wajasiriamali walionufaika na urasimishaji wa Ardhi Bw. Bahati  Mtitu akionesha jinsi alivyoiweza kupanua na kukuza shughuli  zake za ujasiriamali  baada kurasimisha ardhi na kupata hati zilizomuwezesha kukopa katika Taasisi za fedha

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

MWANZA WAZINDUA MSIMU WA KILIMO CHA PAMBA KWA KUGAWA MBEGU

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA MISUNGWI

WANANCHI wa vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wametakiwa kulima kilimo chenye tija kitakachowanufaisha kiuchumi na kuondokana na umasikini.

Rai hiyo ilitolewa jana katika Kijiji cha Seeke wilayani Misungwi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akizindua msimu mpya wa kilimo cha pamba kwa kugawa mbegu za zao hilo pamoja na kamba za vipimo vya kupandia kitaalamu.Alisema wakulima walime kilimo cha kisasa cha kibiashara, wazingatie masharti na kanuni kumi bora za kilimo, wakifanya hivyo wataongeza uzalishaji na kupata maendeleo ya kiuchumi na kipato.

Mongela alisema kwa kuwa serikali imewaletea mbegu kwa wakati wajitume na kulima kwa bidii kwani bila kujibidisha itawawia vigumu kupata mavuno mengi na kuonya wanaume kuacha tabia ya kukaa kwenye vijiwe vya kahawa badala yake wajikite kwenye kilimo.Aliigiza Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuhakikisha inasambaza kwa wakati dawa za viuadudu (viautilifu), vikipungua taarifa itolewe mapema na kuwataka maofisa ugani watoke ofisini waende vijijini wakawasaidie wakulima kwa kuwapa elimu.

Pia aliwataka wakulima ambao hawajakata masuke (miti ya pamba) msimu uliopita kuhakikisha ifikapo Novemba 20 wawe wameyakata na kuyachoma moto kwa kuwa ni chanzo kikubwa cha kuzalisha wadudu.“Pamba ni uchumi wa aina yake na ni muhimu tugeuke turudi tuikotoka tutajirike kwa kuwa mbegu zimeletwa mapema tulime na kupanda kwa wakati.Pia maofisa ugani tutoke twende tukawaelimishe wakulima wapande kwa mistari, wafundishwe jinsi ya kupulizia dawa,”alisema Mongela.

Aidha, afisa kilimo wa Wilaya ya Misungwi, Majid Kabyemela msimu huu wameweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa pamba kwa kubadili mbegu ya UK-91 ambayo uzalishaji wake unaonekana kushuka na wamesambaza tani 350 za mbegu mpya aina ya UKM-08.Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Misungwi Ratifa Malimi alisema siasa ni uchumi hivyo akawashauri wakulima kukipa kilimo cha pamba kipaumbele na wakifaya hivyo watakuwa wameitendea haki ilani ya uchaguzi ya CCM na kufanya maendeleo yasogee baada ya mivutano ya kisiasa.
Mkulima wa Kijiji cha Seeke wilayani Misungwi Charles Faya akipokea mbegu za pamba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela kuashiria kuanza kwa msimu wa kilimo cha zao hilo. Picha na Baltazar Mashaka

SAVE THE CHILDREN YAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA

$
0
0
Shirika la Save The Children limekutana na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika mafunzo ya siku moja kwa ajili ya kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Novemba 19,2018 katika ukumbi wa Good Shepherd mjini Kahama, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.

Akifungua mafunzo,Macha aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.Alisema katika wilaya ya Kahama,halmashauri za Msalala na Ushetu zinaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni kutokana na mila na desturi kandamizi,umaskini,tamaa za mwili,mazingira pamoja na maendeleo ya teknolojia ambapo simu za mkononi zimekuwa zikiongeza tamaa kwa wanafunzi.

“Waandishi wa habari mna nafasi kubwa katika vita hii ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa mnawafikia watu wengi zaidi kupitia habari zenu,Lazima wadau wote tushirikiane kutokomeza changamoto hizi ili watoto wetu wawe salama”,alisema.Aidha Macha aliwataka wananchi kuzingatia utawala wa sheria na kwamba serikali itaendelea kuwachukulia sheria watu wote wanaoshiriki kuwafanyia ukatili watoto.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children kwa ajili ya kukutana na kupanga mikakati ya kutokomeza ndoa na mimba za utotoni. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima - Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu- Malunde1 blog.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akielezea lengo la shirika hilo kutoa mafunzo kwa waandishi yaliyolenga kukutana na wanahabari na kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.
Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron akielezea miradi inayotekelezwa na shirika hilo ambayo ni elimu,ulinzi wa mtoto na mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.


WAHUKUMIWA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA VIPANDE VITANO VYA MENO YA TEMBO NA UHALIFU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu wakulima wawili na mfanyabiashara mmoja kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande vitano vya meno ya tembo na kuongoza uhalifu.

Washtakiwa waliohukumiwa ni Amiri Fransis (44), mkulima Mkazi wa Tanga, Jairab Rashid (33), mkulima na Ibrahim Mkande (30) ambaye ni mfanyabiashara.

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 19 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa Jamhuri uliowasilishwa mahamani hapo pamoja na vielelezo vinne ikiwemo hati ya tathimini ya nyara za Serikali.

Hakimu alisema washtakiwa walikuwa wanatuhumiwa na makosa mawili ya kuongoza mtandao wa kiarifu na kukutwa na nyara za Serikali, Mahakama imewakuta na hatia, ambapo watatumikia kifungo cha miaka 20 jela.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Shaidi amesema, makosa haya ni makubwa sana, yanapelekea kuharibu utalii wa Taifa zima."Nyie ni wabinafsi sana m nataka kujinufaisha kibinafsi kwa Mali ambazo zinasaidia Taifa zima" amesema Hakimu Shaidi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

WENGI WANUFAIKA NA SEMINA YA UFUGAJI WA KISASA WA KUKU KUTOKA KUKU PROJECT,JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kuku Project Bw. Geofrey Kayenga akifungua Semina kwa ajili ya ufugaji wa kisasa wa kuku kwa wafugaji na ambao wanahitaji kuanza na wanaofuga kuku, alisema kuwa lengo kubwa la semina hiyo ilikuwa ni kuhamasishana na kubadilishana ujuzi wa ufugaji wa kuku kwa ujumla na kuwapa njia za kisasa za ufugaji wa kuku, Chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam.
Bi. Beatrice Kanemba Meneja Mawasiliano wa Kuku Project, akielezea kwa ufupi juu ya Kuku Project ambapo ilianza mwaka 2014, alisema kuwa malengo yao yalikuwa ni kuona sekta ya ufugaji inakuwa rasmi,watu kufanya ufugaji kama biashara,kutumia teknolojia ya mitandao ya kijamii kutoa elimu ya ufugaji wa kuku ili kuwafikia watu wengi zaidi. aliongeza kuwa baadhi bidhaa walivyonavyo ni pamoja na Vifaa vya kisasa vya ufugaji na vifaranga wa iana zote ya kuroirer pamoja na ushauri wa ufugaji wenye tija na usimamizi wa mabanda na masoko ndani na nje ya nchi. 
Bw. Deusdedit Nestory, Mkuu wa Kitengo cha Kuku Manispaa ya Kinondoni akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Ufugaji ambapo pamoja na kuhimiza wananchi kufanya shughuli zao kwa vikundi ili kuwarahisishia kupata mikopo na kufanya kazi kwa urahisi lakini pia wanatoa elimu ya ufugaji wa kuku kwa wananchi kuanzia ngazi ya Kata lengo likiwa ni kuboresha sekta ya ufugaji wa kuku.
Baadhi ya watu mbalimbali walifika katika semina hiyo wakiendelea kufuatilia masomo mbalimbali juu ya ufugaji wa kuku wa kisasa.

WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA NA MENEJIMENTI YA TASAF.

$
0
0
Na Estom Sanga-DSM 

Wadau wa Maendeleo na menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- wamekutana jijini DSM kwenye Ofisi Ndogo za Mfuko huo Kujadili pamoja na mambo mengine maandalizi ya zoezi la kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini litakalofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao. 

Utaratibu huo wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini hufanyika mara mbili kwa mwaka na hujumuisha Maafisa wa Serikali na wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi ambao hupata fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo na kukutana na Walengwa na Viongozi wa Maeneo ya Utekelezaji wa Mpango. 

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF imekuwa ikitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN- ulioanza mwaka 2012 katika baadhi ya Halmashauri za Wilaya kwa majaribio na kisha kutekelezwa nchini kote kufuatia mafanikio ya majaribio yaliyofanyika katika wilaya za Bagamoyo, Kibaha, Chamwino na Mbarali mkoani Mbeya. Kwa sasa Mpango huo unanufaisha Kaya takribani Milioni Moja na Laki Moja Tanzania Bara ,Unguja na Pemba ambako walengwa hupata ruzuku ya Masharti hususani katika nyanja za elimu na afya na ile isiyokuwa ya Masharti kwa lengo la kuboresha maisha ya walengwa . 

Kufuatia utekelezaji wa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini, Walengwa wa Mpango huo wameonyesha mabadiliko makubwa hususani katika uboresha ya makazi ,uanzishaji wa miradi ya kiuchumi huku suala la mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka kwenye Kaya hizo shuleni na kwenye vituo vya afya yakiboreshwa zaidi. 

Serikali kupitia TASAF kwa sasa iko katika maandalizi ya Awamu ya Pili ya utekelezaji wa Mpango huo ambayo mkazo maalum utawekwa kwa Walengwa kufanya kazi na kuibua miradi itakayowaondolea kero kwa kushirikiana na Wataalamu walioko kwenye maeneo yao huku pia mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye shughuli za uzalishaji mali ili waweze kukuza uchumi wao na hivyo kupunguza umaskini .
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga (katikati) akimsikiliza kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bw. Mohamed Muderis (mwenye miwani).
Wadau wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF (picha ya juu na chini wakiwa katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini DSM.
Menejimenti ya TASAF akiwa katika mkutano na Wadau wa Maendeleo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mfuko huo kujadili masuala ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo jijini DSM.

MAHAKAMA YAMUONYA 'MC' MAARUFUU NCHINI

$
0
0
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.

MAHAKMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 19.2018 imemuonya mshereheshaji maarufu nchini, Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda kwa kitendo chake cha kusafiri bila ya ruhusa ya Mahakama.

Onyo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi dhidi ya mshtakiwa hiyo ilipoitwa mahakamano hapo kwa ajili ya kutajwa.

Hatua hiyo imefikiwa badaada ya wakili Kishenyi kuieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba mara ya mwisho kulikuwepo na amri ya mahakama ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa kusafiri bila ruhusa ya mahakama.Wakili Kishenyi akaongeza, kwa sababu mshtakiwa amejitokeza mwenyewe akumbushwe masharti ya dhamana.Kufuatia maelezo hayo, wakili anayemtetea Luvanda, Jebra Kambole alidai hana pingamizi kuhusu mshtakiwa kukumbushwa masharti ya dhamana na akaomba radhi kwa yaliyotokea na kwamba mambo hayo hayatajirudia tena.

Hakimu Shaidi alimwambia mshtakiwa kuwa kila kitu kinanidhamu yake, hata katika kesi na kufika mahakamani kuna nidhamu yake lakini kitendo cha wewe kusafiri bila kuitaarifu mahakama siyo kitu kizuri, ukitaka kusafiri toa taarifa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 18, mwaka huu na akamuonya mshtakiwa huyo afuate utaratibu.Katika kesi hiyo, MC Luvanda pamoja na kampuni yake, Home of Company Limited. wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania huku Luvanda akishtakiwa kwa kosa la kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Inadaiwa kuwa kati ya Februari 24 na Septemba 2018 katika jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alianzisha na kutumia mtandao wa www.mcluvanda.com ambao haukuwa na kikoa cha .tz.Aidha imedaiwa,mshtakiwa huyo alitoa Huduma ya online kupitia online TV ifahamikayo kama MC Luvanda pasipokuwa na kibali toka TCRA.

Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala mashuleni

$
0
0
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ipo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ‘syllabus’ ya elimu nchini ili wanafunzi waanze kufundishwa maana ya kodi tangu wakiwa wadogo.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa uelewa mdogo katika masuala ya kodi ambao unachangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi hasa wanaoanzisha biashara kuona ulipaji kodi ni mzigo.

 Akizungumza katika mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Rose Mahendeka alisema mchakato huo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzanian Associate kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel and Fernandes Communications, yalilenga kuwakuelimisha jamii kuhusu masuala ya kodi. Aidha, Mahendeka alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutoelewa umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi katika biashara zao.

“Wafanyabiashara wengi hawana uelewa wa kodi ila tupo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ya elimu waanze kupata wakiwa wadogo kabisa kule mashule ili waanze kupata uelewa wakiwa wadogo kabisa kwamba nini maana ya kodi, inahusu nini na jinsi gani kodi inalipwa Tanzania, tunaamini kwa njia hiyo watu wengi wataelewa,” alisema.


Afisa Elimu Mkuu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Rose Mahendeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara, Kwigaya Mito akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communications, Fatma Fernandes akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzania Associates kwa lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara wa kati na wadogo kuhusu sheria za kodi na umuhimu wa kulipa kodi.
Mshauri wa masuala ya Kodi, Petro Francis akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
Mwanzilishi wa Taasisi ya The Tanzania Associates, Lucy Minde akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.



Magazeti Yasiyohuishwa Kufutwa

Benki ya Exim yazindua kampeni ya ‘Deposit Utokelezee na Exim’

$
0
0

 Benki ya Exim Tanzania leo imezindua rasmi kampeni yake inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam leo inawawezesha wateja wa benki hiyo kupata viwango vya riba vya kuvutia hadi asilimia 10.5 ikiwa watafungua akaunti ya amana maalum (fixed deposit) au kuweka kwenye akaunti zao za amana maalum kiasi kisichopungua Sh 50m/- kabla ya Desemba 31 mwaka huu..

"Kampeni hii inalenga kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa watanzania. Kwa kuzingatia viwango vya ushindani tunavyowasilisha kupitia kampeni hii, wateja wetu watakuwa na uwezo wa kunufaika na riba ya hadi 10.5% kwenye amana zao, " Alisema Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda wakati hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kampeni hii inakuja ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' (Exim at Work Today, for tomorrow) unaoendana na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwa wateja na jamii inayoizunguka.

Bi Kaganda aliongeza, "kama benki, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wateja wetu, ili kuhakikisha wanakua na ustawi mzuri sasa na hata baadae. Kupitia akaunti zetu za muda maalum (Fixed deposit) mteja anaweza kuongeza kiasi kikubwa cha pesa huku akiwa na uhuru wa kuchagua aina ya muda anaotaka. Tunaamini kwamba kesho yako bora inaanza leo.’’

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997, Benki ya Exim imefanikiwa kujitanua maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo kwasasa ina matawi yake kwenye mikoa 13 nchini ikiwa ni pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na Mtwara. Pia matawi yake yapo kwenye nchi za Comoros, Djibouti na Uganda.


Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni mpya ya benki hiyo inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa (corporate) wa benki hiyo Bw Shrikant Ganduri (kushoto) na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji
Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo Bw Arafat Haji (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni mpya ya benki hiyo inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na Exim’ iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi. Wengine ni pamoja na Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes Kaganda (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa (corporate) wa benki hiyo Bw Shrikant Ganduri.

Watalaam wa afya Muhimbili waanza kutoa huduma Hospitali ya Rufaa Mtwara

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kutoa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara, Ligula ikiwa ni moja ya mkakati wa MNH wa kuwajengea uwezo wataalam wa afya wa hospitali za rufaa za mikoa nchini ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula Dkt. Lobikieki Kissambu amesema wataalam hao watatoa huduma katika maeneo mbalimbali ikiwemo upasaji, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara pamoja na magonjwa ya ndani.Amesema ujio wa wataalam hao utasaidia kupunguza gharama ambayo hospitali imekua ikitumia kusafirisha wagonjwa wanaopata rufaa kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi kwa mwezi hutoa rufaa kwa wagongwa 10 hadi 20 hivyo hutumia takribani shilingi milioni 300 kwa mwaka kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa hao.‘’Wataalam hawa kutoka Muhimbili watatusaidia kuwajengea uwezo wataalam wetu hasa ukizingatia hospitali ya Ligula ina upungufu mkubwa wa Madaktari Bingwa mpaka sasa hospitali hii ina Daktari Bingwa mmoja tu, lakini pia ujio huu utatusaidia kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa ambao wanapata rufaa ya kwenda kutibiwa Muhimbili. Amesema Mganga Mfawidhi.

Hata hivyo amesema katika kukabiliana na ukosefu wa Madaktari Bingwa hospitali hiyo imewapeleka shule Madaktari watatu ambao wanasomea ubingwa katika upasuaji, mifupa pamoja na koo, sikio na pua. Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka Muhimbili Geofrey Marandu amesema mbali na kutoa huduma za afya lakini pia watawajengea uwezo watalam hao na kuhakikisha huduma hizo zinakua endelevu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara Dkt. Lobikieki Kissambu (kulia) akizungumzia ujio wa wataalam wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushoto ni Daktari Bingwa kutoka Muhimbili Innocent Mosha.
Baadhi ya wagonjwa wakisubiri kupatiwa huduma katika hospitali hiyo mapema hii leo.
Watoa huduma katika Idara ya magonjwa ya dharura wa hospitali ya Ligula wakielekezwa na Daktari kutoka Muhimbili namna ya kumuhudumia mgonjwa ambaye amezidiwa.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho kutoka Muhimbili Judith Mwende (kushoto) akiangalia maendeleo ya mgonjwa wa macho ambaye alifanyiwa upasuaji wa macho mwezi wa tatu mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 
Mtaalam wa kupima usikivu kutoka MNH, Sista Theresia Uisso akimuelekeza mgonjwa namna ya kuishi kulingana na tatizo linalomkabili, kushoto ni Madaktari wanafunzi wakifuatilia.

WAZIRI MKUU AWATAKA WANANCHI WAJENGE MABWENI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka wananchi kwenye Kata ya Mnacho wilayani Ruangwa washirikiane kujenga mabweni katika shule ya sekondari Mnacho ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembelea umbali mrefu kwenda shuleni hapo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 19, 2018) wakati alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni, ambalo ujenzi wake unagharimu sh. milioni 92.4 ikiwa ni mchango uliotolewa na wadau wa elimu.

“Bweni hili likikamilika litawapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kuja shuleni hususani wanaoishi vijiji vya mbali kwa sababu wataishi hapa, jambo ambalo litachangia kuongeza ufaulu wa watoto wetu.” Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi waishio katika Kata hiyo na za jirani washirikiane na kuanzisha mradi wa ujenzi wa mabweni mengine kwa kuwa hilo moja lililojengwa na wadau halitoshi kulingana na idadi ya wanafunzi.

Amesema yeye yuko tayari kuendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye mipango yao yote ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata yao, lengo likiwa ni kuhakikisha mikakati ya Serikali ya kuboresha huduma za jamii inatimia. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao washirikiane na walimu kufuatilia maendeleo ya taaluma kwa watoto wao shuleni na kujiridhisha kama wanafanya vizuri darasani na iwapo watabaini changamoto waweze kuzitatua kwa pamoja.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Mnacho wilayani Ruangwa, David Mwakalobo wakati alipokagua ujenzi wa bweni hilo Novemba 19, 2018 . Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandirwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa chumba cha upasuaji katika Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abubakar Abbas Rugwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa Novemba 19, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandirwa, kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Dkt. Mahela Njile na kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abubakar Abbas Rugwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

JENISTA MHAGAMA ATOA VYETI KWA WAHITIMU WA PROGRAMU YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO (FEMALE FUTURE PROGRAMME)

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii .

CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanya mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme). 

ATE wamefanya mkutano huo wakishirikiana na Shirikisho la vyama vya waajiri nchini Norway (NHO) wenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake kwa ajili ya kushika nafasi za juu za uongozi na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye bodi mbalimbali na kushiriki katika maamuzi. 

Akifungua Mkutano huo, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema mkutano huu mkubwa wa mwaka wa uongozi kwa wanawake unaenda samamba kabisa na juhudi za nchi yetu katika kuhakikisha idadi ya wanwake kwenye nafasi zao za juu za uongozi inazidi kuongezeka pia wanawake kuwa na idadi kubwa ya uwakilishi katika bodi za wakurugenzi za makampuni mbalimbali. 

"Serikali ya awamu ya tano imeendelea kusimamia na kuhakikisha kunakuwa na uwiano mzuri wa viongozi wanawake ndani ya serikali na jumuiya mbalimbali , makampuni ya kibiashara nchni na katika kufanikisha hili serikali imeanzisha mpango mkakati wa kitaifa kwa ajii ya maendeleo ya usawa wa kijinsia ambapo upo kwenye dira ya maendeleo ya Taifa 2025"amesema Jenista. 

Jenista amesema, programu hiyo ni fursa kwa wanawake wa wakati nujao na mafunzo hayo wakiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika nyanja mbalimbali, kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi kijacho. 

Amesema, kwa mwaka 2017 idadi ya wanawake katika bodi mbalimbali za taasisi za serikali iliongezeka na kufikia 117 kutoka 114 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na wanaume ambapo walipungua toka 526 mwaka 2014 hadi 352 mwaka 2017, aidha katika miaka hiyo idadi ya wanawake majaji imeongezeka na kufikia 39 kati ya majaji 95, wakati mwaka 2012 majaji wanawake walikuwa 34 kati ya 97. 
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizunguzma wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizzungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme). 
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Arafa wakati mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme). 
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ma Wwtu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa cheti kwa moja ya wahitimu Bahati Minja wakati mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi kwa mwaka 2018 uliombatanisha mahafali ya pili ya programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future Programme).

Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images