Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

Muhimbili wahitimisha huduma za afya kwa njia ya mkoba katika Hospitali ya Rufaa Lindi

$
0
0
Watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) ambao walikua wakitoa huduma za afya kwa njia ya mkoba katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE wamehitimisha huduma hiyo leo kwa kuwahudumia zaidi ya wagonjwa 1103 na kufanyia upasuaji wagonjwa 47.

Maeneo ambayo wataalam wa Muhimbili wamehudumia kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Sokoine ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho,watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya dharura, Radiolojia pamoja na magonjwa ya ndani.

Mbali na kutoa huduma hizo lakini pia watalaam wa Muhimbili wamewajengea uwezo kiutendaji wataalam wa hospitali hiyo pamoja na kuleta mabadiliko ikiwemo kuelekezwa jinsi ya kanzisha idara na kuzisimamia ili kuleta ufanisi katika utoaji huduma.

Akizungumza katika kikao cha tathimini ya utoaji huduma, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija amesema kuanzishwa kwa idara mbalimbali kutaleta mabadiliko makubwa katika kutimiza majukumu yao kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu.Hivyo amewataka watumishi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi kukubali mabadiliko ili kufikia malengo ya utoaji huduma bora.

‘’Hospitali hii ni ya rufaa, wananchi wanaitegemea katika kupata huduma hivyo lazima tutoe huduma bora na zenye viwango vya juu na yote yatafanikiwa endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake’’.amesisitiza Dkt. Shija.Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu amemsihi kiongozi wa hospitali hiyo kutowaonea aibu watumishi wanaokwamisha maendeleo ya hospitali.
Ameto wito kwa watumishi hao kutumia fursa zinazojitokeza ili kupata ujuzi Zaidi.

Mara baada ya kumaliza kutoa huduma katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi wataalam hao wataelekea Hospitali ya Ligula Mtwara kwa ajili ya kutoa huduma na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo. 

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija akizungumza katika kikao cha tahimini ya utendaji kilichohusisha wataalam wa MHN pamoja na wataalam wa hospitali hiyo. 
Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na wataalam wa Hospitali ya Sokoine wakimsikiliza Kaimu Mganga Mfawidhi katika kikao hicho.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu akielezea jambo katika kikao hicho. 
Katibu wa hospitali hiyo Boniface Lyimo akitoa neno la shukrani wakati wa kikao hicho. 
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na watalaam wa afya wa Idara ya Upasuaji mara baada ya kuanzishwa kwa idara hiyo kufuatia ushauri uliotolewa na wataalam wa MNH. 

MAJAJI WA MAHAKAMA KUU CHINA WATEMBELEA MAHAKAMA YA TANZANIA

$
0
0

Na Lydia Churi – Mahakama

Majaji watano kutoka Mahakama Kuu ya nchini China wameitembelea Mahakama ya Tanzania ili kujifunza namna mfumo wa utoaji haki wa Tanzania unavyofanya kazi na pia kubadilishana uzoefu kuhusu masuala yakisheria na utoaji haki.

Majaji hao kutoka jimbo la Zhejiang la nchini China pia wameitembelea Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kujifunza zaidi na kubadilishana uzoefu hasa kuhusu adhabu zinazotolewa na Mahakama kwa ajili ya kuirekebisha jamii.

Akizungumza na Majaji hao, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati amewaambia kuwa Mahakama ya Tanzania ni chombo huru kinachotekeleza majukumu yake kwa uhuru pasipo kuingiliwa na Mihimili mingine. Akizungumzia adhabu zinazotolewa na Mahakama katika kuirekebisha jamii hasa zile za kifungo cha nje, Msajili Mkuu alisema adhabu hizo hutolewa kwa mujibu wa sheria na kwa vigezo mbalimbali ikiwemo kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kufanya shughuli za uzalishaji ili kuisaidia jamii.

Alisema Mahakama ya Tanzania imekuwa ikishauri matumizi ya adhabu mbadala ikiwemo kazi za nje badala ya adhabu za kifungo gerezani. Kupitia adhabu hizi, wafungwa watatumika pia kufanya kazi za uzalishaji mali na kuisaidia jamii. Kwa upande wao, Majaji hao kutoka nchini China wamesema wamefika nchini kujifunza mfumo wa utoaji haki unavyofanya kazi na hasa kuhusu adhabu zinazotolewa na Mahakama katika kuirekebisha jamii kwa kuwa mfumo huo pia hutumiwa na Mahakama zao.

Kwa mujibu wa Majaji hao, China inazo fursa nyingi za kuwaendeleza wanasheria kitaaluma na hivyo wametoa wito kwa Mahakama ya Tanzania kutumia fursa hizo katika kuwaendeleza watumishi wake kama ambavyo nchi nyingine zimekuwa zikifanya.
Pichani ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati akiwa katika mazungumzo pamoja na Wahe. Majaji kutoka Mahakama Kuu Zhejiang iliyopo Jamhuri ya Watu wa China walipotembelea Ofisi ya Mhe. Msajili Mkuu, Novemba 16, 2018. 

SERIKALI YATOA SH. BILIONI 83 KUIMARISHA ELIMU

$
0
0
*Ni kuanzia Julai hadi Oktoba mwaka huu, kwa msingi na sekondari
*Waziri Mkuu aonya wanaoshiriki wizi wa mitihani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kati ya Julai na Oktoba, mwaka huu, Serikali imetoa jumla ya sh. bilioni 83.2 ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule nchini.

Waziri Mkuu amesema, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 38.6 zilipelekwa kwenye shule za msingi na shilingi bilioni 44.6 zilienda kwenye shule za sekondari ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa elimumsingi bila malipo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Novemba 16, 2018) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 13 wa Bunge. Bunge limeahirishwa hadi Januari 29, 2019.

“Katika kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule nchini, Serikali inapeleka fedha za elimumsingi bila malipo moja kwa moja shuleni. Kwa mfano, katika kipindi cha Julai hadi Oktoba, 2018 shilingi bilioni 38.6 zilipelekwa katika shule za msingi na shilingi bilioni 44.6 kwenye shule za sekondari,” amesema.

Amesema tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango wa elimumsingi bila malipo, uandikishaji wa watoto wa darasa la awali na darasa la kwanza umeimarika na kwamba kumekuwepo na mwenendo mzuri wa ufaulu kwenye mitihani ya kumaliza darasa la saba. 
 

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa .

Rais Magufuli Mgeni Rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri Bonde la Mto Nile

$
0
0
Jonas Kamaleki, MAELEZO, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuri atakuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Bonde la Mto Nile zilizopo kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maji, Prof. Makae Mbarawa amesema Mkutano huo utapitia utekelezaji masuala mbali mbali ya miradi, utapokea taarifa ya utendaji, hali ya ulipaji wa michango ya kila mwaka kwa nchi wananchama na tathmini ya watumishi wa Sekretarieti ya NELSAP.

Mkutano huo ambao utafanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22, 2018 utawashirikisha mawaziri wa Maji na wawakilishi kuto nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani ya Kusini na Uganda.Prof. Mbarawa amesema kuwa Mkutano huu utatanguliwa na vikao vya wataalamu ambavyo ni vya kiutendaji na vitaanza tarehe 20 hadi 21 Novemba, 2018 Jijini Dar es Salaam.

“Ushirikiano wa Nchi za Bonde la Mto Nile ni wa muda mrefu, umeanza tangu miaka ya 1960 na ilipofika tarehe 22 Februari, 1999 nchi wanachama ziliunda Taasisi ya Mpito ya Bonde la Mto Nile iitwayo Nile Basin Initiative-NBI. Taasisi hii ilianzishwa Dar es Salaam, na sasa inaelekea kutimiza miaka 20,”alisema Prof. Mbarawa.

Bonde la Mto Nile ni ukanda wote wa eneo la Bonde la Mto huo kuanzia Ziwa Victoria hadi Bahari ya Mediterania ambapo Tanzania iko sehemu ya juu ya Bonde la Mto Nile ambako Mto Mara, Simiyu na Mto Kagera inamwaga maji katika Ziwa Victoria ni sehemu ya Bonde hilo. Mto Nile ni mrefu sana Duniani kwa kuwa na urefu wa kilomita 6,695.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za Bonde la Mto Nile zinazoshirikiana katika kusimamia na kuendeleza Raslimali za Maji za Bonde la Mto huo chini ya mwavuli wa NBI.

Watoto 10 wapandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

$
0
0


Madaktari bingwa wa masikio, pua na koo pamoja na wataalam wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watoto 10 waliopandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Wataalam hao leo wamewaona watoto hao wodini ili kujua maendeleo ya afya zao baada ya kupandikizwa vifaa hivyo. Kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo kutoka Misri, Prof. Lobna El Fiky, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili (aliyembeba mtoto) Kushoto ni mtaalam wa vifaa vya kusaidia kusikia kutoka Misri, Mohamed El Disouky na mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na wengine ni wazazi wa watoto hao. Wazazi wa watoto hao wametoka mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Kilimanjaro, Songea na Tanga. Hadi sasa idadi ya watoto waliopandikizwa vifaa hivyo imefikia watoto 21.
Watoto waliopandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia wakiwa wodini baada ya kupatiwa huduma hiyo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo kutoka Misri, Prof. Lobna El Fiky akifuatilia maendeleo ya mtoto aliyepandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam kutoka Misri. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Sufiani Baruani. Wengine ni wataalam wa magonjwa ya masikio, pua na koo.
Mmoja wa wazazi wa watoto waliopatiwa huduma hiyo akizungumza na Prof. Lawrence Museru wa Muhimbili kuhusu maendeleo ya afya ya mtoto wake. Kushoto ni Prof. Lobna El Fiky.

MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA AVUTIWA NA MAFANIKIO YA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI KUPITIA TASAF.

$
0
0

NA Estom Sanga- DSM

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem amefanya ziara katika mtaa wa Mamboleo,halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini DSM na kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

Akizungumza na Walengwa hao baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kukuza kipato chao, Dr. Ghanem amesema jitihada waliyonyesha Walengwa hao ya kuuchukia Umaskini ,itaendelea kuungawa mkono na Benki hiyo ya Dunia ambayo amesema ni rafiki mkubwa wa Serikali ya Tanzania.

Dr.Ghanem ametoa rai maalum kwa Walengwa hao wa TASAF kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji mali na kutumia mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo kwani amesema ni dhahiri kuwa serikali ya Tanzania inawajali na imeonyesha utayari wa kuboresha maisha ya wananchi. Aidha Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo Bi. Bella Bird, amesisitiza kuwa taasisi hiyo kubwa ya fedha Duniani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kufadhili Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha utekelezaji wake.

Akizungumza kwenye Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ameelezea mafanikio makubwa ambayo Mfuko huo umepata tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 18 iliyopita hususani katika nyanja za elimu,afya,maji, na uchumi. Bw. Mwamanga amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana yametokana pia na usimamizi wa Karibu wa viongozi wa Serikali katika ngazi zote za utekelezaji ambapo wamekuwa wakiwahamasisha wananchi kutumia vizuri fursa hiyo ili waweze kuinua kiwango chao cha maisha na kutokomeza umaskini kwa kasi kubwa zaidi.

Benki ya Dunia pamoja na taasisi nyingine za Kimataifa imekuwa ikichangia fedha kugharamia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao kwa sasa unahudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja Tanzania Bara, Unguja na Pemba,Mpango ambao umekuwa chachu ya maendeleo kwa Kaya za Walengwa .Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem (watatu kulia) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa na Walengwa wa TASAF katika eneo la Mamboleo,Temeke kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Baadhi ya walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Mamboleo-Temeke jijini DSM wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa WB kanda ya Afrika Dr. Hafez Ghanem na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga kulia kwa Makamu huyo wa Rais wa WB.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Dr. Hafez Ghanem akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi ambao wazazi wao wako katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF.
Makamu Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr.Hafez Ghanem,akivishwa skafu alipowasili kwenye mtaa wa Mamboleo,wilayani Temeke jijini DSMalipokutana na Walengwa wa TASAF.

MICHUZI TV: UHAKIKI UMEKAMILIKA TUNAANZA KUGAWA FEDHA LEO-WAZIRI WA KILIMO JAPHET HASUNGA

MICHUZI TV:DED -NEWALA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA SEKTA MBALIMBALI KATIKA SERIKALI AWAMU YA TANO


UMOJA WA ULAYA (EU) WAKABIDHI VIFAA KWAAJILI YA MAABARA YA KISASA TAEC

$
0
0
Na, Vero Ignatus Arusha 

Umoja wa Ulaya (EU) umerithishwa na ujenzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) ikiwemo uwekaji wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh, bilioni 2.3. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara hiyo, Meneja Mradi na Usalama wa Masuala ya Mionzi, kutoka EU, Genevieve Lizin alisema umoja huo umerithishwa na kazi nzuri ya uwekaji vifaa uliofanywa na serikali. 

Alisema Umoja huo umeamua kutoa vifaa hivyo kwaajili ya kudhibiti masuala ya mionzi ndio maana wametoa ili kudhibiti masuala ya mionzi katika nchi za Afrika. "Maabara hii ni ya kisasa na hakuna mfano wake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla hivyo tumeridhika na kazi waliyofanya Taec katika zoezi la uwekaji vifaa ambavyo sisi tumevitoa "
 Mkurugenzi Mkuu Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala akizungumza na Meneja Mredi kutoka Jumuiya ya nchi za Ulaya Genevieve Liz pamoja na wageni wengine alioonhozana nao. 
Denis Mwalongo Mkuu wa Idara ya Mionzi, mashine za kuhakiki vifaa vya mionzi katika mwili wa binadamu akiwaonuesha wageni hao kutoka Umoja wa Ulaya jambo 
Dkt Wilbroad Muhogora mwenye (shati la draft) Mtafiti wa Tume akifafanua jambo kwa wageni kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na, waandishi wa habari

VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Mtwara

WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema serikali imeshaanza uhakiki wa wakulima wanaodai malipo ya korosho ambapo jumla ya vyama vya msingi 35 vimeshahakikiwa na malipo yameanza kufanyika.

Hayo aliyasema jana mkoani Mtwara wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu opereshe korosho inayoendelea katika mikoa inayolima korosho kuhakikisha wakulima wote wanauza korosho zao kwa serikali kwa bei ya Sh. 3,300.

"Tulitenga vyama 50 vya awamu ya kwanza na ndani ya siku mbili tumehakiki taarifa za wakulima kwenye vyama 35 kwa kuangalia majina yao, kiasi cha korosho walichoingiza kiasi cha fedha wanazotakiwa kulipwa na taarifa za akaunti zao na hivi ninavyoongea tayari wameanza kulipwa kuanzia sasa kupitia akaunti zao binafsi," alisema Hasunga.

Alitaja halmashauri ambazo vyama vyao vimehakikiwa kuwa ni pamoja na Halmashauri ya Newala (5) Wilaya ya Newala (5) Wilaya ya Masasi (5) Nanyumbu (2) Lindi (5) Tunduru Ruvuma (5).Kuhusu malipo ya kitaasisi ikiwemo ushuru wa halmashauri alisema inaanda mwongozo wa kuangalia namna ya kuwalipa na kwamba malipo yatafanyika baada ya korosho kubanguliwa na kuuzwa.

"Ili kulipa malipo ya makato yote lazima tujue tumeuza korosho kwa bei gani kisha kama ni asilimia zinakatwa kulinga na bei tuliyouzia," alisisitiza.Makato hayo ya kitaasisi huwa yanalipwa kwa Halmashauri ambayo huchukua asilimia tatu ya bei elekezi, wasafirishaji wa korosho, watunza maghala pamoja na vyama vikuu vya ushirika ambavyo hukata Sh. 53 katika kila kilo moja ya korosho kwaajili ya vifungashio.

Hasunga yupo mikoa ya kusini tangu siku moja tu baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo ili kujionea zoezi la uingizaji korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hazitoki na kuuzwa baada ya serikali kuweka msimamo wa kununua korosho zote za wakulima nchini.

Alisema kwasababu serikali ndiyo mnunuzi wa korosho hivyo inalazimika kulipa tozo ambazo walikuwa wanalipa wanunuzi wengine."Kwa agizo la Rais fedha zote zitapelekwa kwa wakulima bila makato yoyote kwasababu tunaangalia wakulkma kwanza na wengine watalipwa baadae" alisema.
Waziri wa Kilimo , Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kutoa Malipo ya korosho kuanzia leo Novemba 17 mwaka 2018 kama ilivyoagizwa na Rais Dr.John Pombe Magufuli.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wametoka kuokota korosho katika Mashamba ya shule kwa ajili ya kukusanya ziende kuuzwa kwenye Maghala.

TUMETOA ELIMU YA KUTOSHA KWA WANANCHI JUU YA UPOKEAJI WA FEDHA ZA KOROSHO-Mkurugenzi Newala.

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii,Newala ,Mtwara.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae amesema tangu kutangazwa kwa operesheni korosho ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Newala wamezunguka  Wilaya nzima kutoa elimu kuhusu nini kifanyike kupitia agizo la Rais Magufuli kuwa Serikali itanunua Korosho yote nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Wilayani Newala Chimae amesema kuwa  wamezunguka kwa wananchi kutoa elimu juu ya namna zoezi hilo litakavyoendesha ikiwa ni pamoja na kuwataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia zoezi hilo kwa makini hili kusitokee malalamiko yoyote.
"Sambamba na zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima pia tumetoa maagizo kwa watendaji wa mitaa na kata kusimamia zoezi la uingizaji wa korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hakuna korosho inayoingia kutoka nje ya mitaa au kata zao ili kudhibiti korosho za magendo zinazoingizwa kutoka nchi jirani," alisema Chimae.

amesema kuwa Halmashauri ya Newala ni moja ya Halmashauri zinazopakana na nchi jirani ya Msumbiji ambapo kwa upande wa majirani zetu kwa sehemu nao wanalima zao la Korosho hivyo wamejipanga kwa kila namna kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Kuwa hakuna korosho kutoka nchi jirani itakayopenya nchini kupitia milango ya Wilaya hiyo.

amesema kuwa tayari askari wa JWTZ Wamejipanga katika Maghala na wameimarisha ulinzi kwa kukagua na kulinda korosho hili isije mtu akatokea akatia doa wilaya yake kwa kufanya vitu tofauti na maagizo ya Rais.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  Mafanikio yaliyopatikana katika Wilaya hiyo kwa kipindi hiki cha Miaka Mitatu ya Serikali ya  awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae
Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Newala linavyoonekana kwa nje

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI NA CGP KASIKE WATEMBELEA KIWANDA CHA SAMANI CHA JESHI LA MAGEREZA CHA ARUSHA KILICHOTEKETEA KWA MOTO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akiwasili leo Novemba 17, 2018 katika Kiwanda cha samani cha Magereza Arusha kukagua sehemu mbalimbali ambazo moto umeteketeza sehemu ya kiwanda hicho. Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.

Na Lucas Mboje, Arusha

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike leo wametembelea Kiwanda cha Samani cha Arusha, mali ya Jeshi la Magereza ili kujionea athari mbalimbali iliyosababishwa na ajali ya moto iliyotokea juzi Novemba 16, 2018.

Akizungumza eneo la tukio Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu amesema kuwa ni vyema taasisi mbalimbali nchini pamoja na wananchi wakachukua tahadhali za majanga ya moto ili kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza kufuatia majanga hayo.

Amesema kuwa Wizara yake itaendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vifaa vya kisasa ili liweze kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza. Aidha, Katibu Mkuu huyo, Meja Jenerali Kingu amelitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha kuwa linafanya jitihada za haraka za kurejesha shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho ikiwemo kufanyia matengenezo baadhi ya mashine zilizoteketezwa na moto.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu(kulia), wakiangalia moja ya mashine mbalimbali ambazo zimeteketezwa na moto katika kiwanda cha Samani cha Magereza Arusha. Chanzo cha moto huo inasemekana ni hitilafu ya umeme ndani ya kiwanda hicho.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amevishukru vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha sambamba na wananchi waliojitokeza kusaidia katika uzimaji wa moto huo ambao umeunguza sehemu ya kiwanda hicho.

“Nawashukru sana Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Arusha, Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kwa kazi kubwa waliyoifanya siku ya tukio kwani niliarifiwa kuwa moto ulikuwa mkubwa lakini tunashukuru Mungu hatimaye uzimaji ulifanikiwa pamoja na hasara iliyojitokeza”. Alisema Jenerali Kasike.

Akizungumzia chanzo cha moto huo na hasara iliyojitokeza, Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme ambayo ilisababisha kuteketea kwa baadhi ya mashine za kiwanda hicho pamoja na uharibu wa nyaraka mbalimbali za ofisi katika jengo la utawala.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati). Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango, Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana ambaye ni Kiongozi wa Kamati Maalum ya kuchunguza tukio hilo.

Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Phaustine Kasike ameunda Kamati maalum ya Maafisa watano kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambayo itachunguza chanzo cha moto huo pamoja na kuwasilisha taarifa kamili ya hasara iliyojitokeza. Tume hiyo itaongozwa na Kamishna wa Fedha na Mipango wa Jeshi hilo, Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana.

Kiwanda cha samani cha Magereza Arusha kilimikishwa rasmi kwa Jeshi la Magereza mwaka 1973 baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967 ambapo tangu kipindi hicho kiwanda hicho kinajishughulisha na utengenezaji wa samani mbalimbali za ofisi na samani za majumbani. Pia kiwanda hiki hutumika kuwafundisha na kuwarekebisha wafungwa ili wamalizapo vifungo vyao waweze kujitegemea kupitia ujuzi waliojifunza.

HASUNGA AWATAKA WATENDAJI KUSIMAMIA UBORA WA KOROSHO

$
0
0

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametaka watendaji wa Bodi ya Korosho na Waendesha maghala kusimamia kwa weledi ubora wa korosho ili fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya kununua korosho za wakulima katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma zitumike ipasavyo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo tarehe 16 Novemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Alisema kuwa baada ya wananchi katika maeneo mbalimbali kusikia kuwa serikali imeanza kuwalipa wakulima wa korosho yamejitokeza matukio ya kuwepo kwa korosho chafu zilizotunzwa kwenye maghala tangu msimu wa mwaka jana 2016/2017 zikiwa hazipo katika ubora unaotakiwa wa daraja la kwanza ilihali korosho za madaraja mengine hazijaanza kununuliwa.

“Nadhani wanafanya hivi ili wafaidike na hela za serikali, jambo hili hatuwezi kukubaliana nalo kwani tayari tumeshakamata Tani 20 za korosho chafu kutoka kwenye ghala la Olam za Chama cha Ushirika cha Mnyawi Amcos kilichopo Nanyamba pamoja na Mbembaleo Amcos ambapo gunia tano za korosho chafu zimepatikana” Alisema
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JESHI USU LA WANYAMAPORI NA MISITU ENEO LA FORT IKOMA SERENGETI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wadau wote wa uhifadhi hususan jeshi letu USU kuhakikisha kuwa wanatekeza kwa azma moja nia njema ya Serikali ya kuhakikisha usalama wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na misitu.

Makamu wa Rais ametoa rai hiyo leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi Usu la Wanyamapori na Misitu iliyofanyika katika eneo la Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.

“Vilevile, nitoe rai kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya uhifadhi kuheshimu sheria za nchi, kutoa ushirikiano kwa jeshi usu na kuwa raia wema kwa kujiepusha na kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya uhifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.” alisema Makamu wa Rais.

Utalii umekuwa moja ya vyanzo vikubwa vya kuliingizia Taifa fedha za kigeni kwa asilimia 25% na pato la Taifa kwa asilimia 17% pamoja na kutoa  ajira rasmi na zisizo rasmi.

Mfumo huu mpya wa kusimamia maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na misitu utasaidia kumaliza ujangili kabisa.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Nape Nnauye amesema wanatambua ukubwa wa tendo hili la uanzishwaji wa jeshi la Usu kwa faida ya nchi, kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho.

“Tunaamini kwamba pamoja na ujasiri na uzalendo lakini operesheni za jeshi hili zitafanyika kuzingatia ubinadamu ili tuwafanye wananchi waone umuhimu wa rasilimali hizi ushirikiano wao katika kuzilinda na kuzitunza ni muhimu” alisema Mwenyekiti huyo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Jeshi USU la Wanyamapori na Misitu likipita kwa ukakamavu mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara. 
 Jeshi  USU la Wanyamapori na Misitu likionyesha picha za Viongozi wakubwa wawili Mwalimu Julius K. Nyerere (kulia) kama ishara ya mpambanaji wa kusimamia rasilimali zetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kama mtekelezaji katika kuhakikisha rasilimali zetu zinalindwa na kufaidisha Wananchi wa Tanzania  na picha za wanyama zinaashiria wanyama wakubwa watano ambao ndio kivutio zaidi duniani na wamekuwa kwenye hatari ya kutoweka wakati wa sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo zilizofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi bendera Mkurugenzi Mkuu wa Hifahi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi kama ishara ya uzinduzi na kuanza kufanya kazi rasmi kwa jeshi la USU leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Jeshi  USU la Wanyapori na Misitu iliyofanyika Fort Ikoma Serengeti mkoani Mara.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE LA CHINA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanyika nchini hivi sasa chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano. 

Ametoa shukrani hizo jana jioni (Ijumaa, Novemba 16, 2018) alipokutana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China, Bw. Cai Dafeng ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma. “Tunaishukuru Serikali ya China kwa sababu tumepokea misaada na mikopo ya gharama nafuu na kuendeleza miradi mbalimbali kama vile mradi wa umeme wa Kinyerezi, awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar,” alisema. 

Alisema Serikali ya China imekuwa pia na mahusiano ya muda mrefu na Serikali ya Tanzania na hasa kwenye sekta ya afya ambapo kuna wanafunzi wengi wa Kitanzania ambao wako China wakisomea udaktari na masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). “Tuna mahusiano mazuri kwenye sekta ya afya na sasa hivi tuna madaktari 20 ambao wanasoma huko na wengine wanasomea masuala ya TEHAMA. Pia tuna mahusiano mazuri baina ya Bunge la Tanzania na China,” alisema. 

Waziri alisema Tanzania imejipanga kuinua uchumi wake kupitia ujenzi wa viwanda na sekta nyingine kama utalii kutokana na vivutio vilivyopo nchini kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama za Serengeti na visiwa vya Zanzibar. “Nimefurahi kusikia kuwa hivi karibuni tutapata idadi kubwa ya watalii kutoka China,” alisema. Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China, Bw. Cai Dafeng alisema amefurahishwa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inavyoendelea kubadili hali ya uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli. 

Alisema China itaendelea kuiunga mkono Tanzania kwenye masuala ya kiuchumi na haiko tayari kuona ikiingiliwa masuala yake ya ndani na mataifa kutoka nje. Akizungumzia kuhusu masuala ya uwekezaji baina ya Tanzania na China, Bw. Cai alisema China itaendelea kuyahimiza makampuni ya nchi hiyo ili yawekeze zaidi nchini Tanzania kwenye maeneo mbalimbali kama vile ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. “China inataraji kuongeza uwekezaji kwenye kilimo, nishati na miundombinu,” alisema. 

Kuhusu elimu, Bw. Cai alisema Serikali ya nchi hiyo inaangalia uwezekano wa kuanzisha masomo ya lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili Watanzania wengi zaidi waweze kujifunza lugha hiyo. Kuhusu afya, alisema China itaendelea kutuma madaktari wake ili waje kutoa huduma kwa Watanzania na inatamani kuona mahusiano baina ya mtu mmoja mmoja kutoka nchi hizo mbili ikiendelea kukua.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China Cai Dafeng, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma Novemba 16, 2018. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akutana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China Cai Dafeng, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma Novemba 16, 2018. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mahagama, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China Cai Dafeng, ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma Novemba 16, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 

PAPII KOCHA, KHADIJA KOPA NA BI CHAU WANOGESHA SAUTI YA MWANAMKE JIJINI MBEYA

TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha 

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi na kuondoa malalamiko kutopata huduma stahiki

Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo iliyowashirikisha watendaji wa mitaa,Kata, Wakuu wa vituo vya polisi,waalimu wakuu wa shule sanjari na watumisha wa idara za serikali wilayani hapa Meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.
Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini Fransis Msungu akiongea kwenye semina iliyowashirikisha watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu kutoka halmashauri za jiji na wilaya ya Arusha sanajri na wakuu wa vituo vya polisi wilayani hapa iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha zote na  Mahmoud Ahmad,Arusha. 
Muwasilishaji kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini Tcra Janny Kaaya akitoa mada wakati wa semina ya watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu na wakuu wa vituo vya polisi walioshiriki semina hiyo kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa picha na mahamoud ahmad wa globu ya jamii arusha 
Katibu tawala wa wilaya ya Arusha mjini David Mwakiposa akifunga semina hiyo iliyowashirikisha Halmashauri za jiji la Arusha na wilaya ya Arusha iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Rose jijini hapa picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Arusha. 

VIJIJI VYOTE NCHINI KUPATIWA HUDUMA ZA MAJI SAFI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote wakiwemo wa wilaya ya Nachingwea wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, hivyo amewataka wananchi waendelee kuiamini.
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Novemba 17, 2018) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namatula ‘A’ na kijiji cha Mtua ambao waliosimamisha msafara wa Waziri Mkuu wakati akiekea Kata ya Kilimarondo wilayani Nachingwea.

“Serikaliya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini vikiwemo vijiji vya wilaya ya Nachingwea ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo.”

Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.

Amesema mbali na huduma ya maji, pia Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya ya Nachingwea. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Pia Waziri Mkuu ameesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Awali, Waziri Mkuu alimkabidhi Mwenyekiti wa kijiji cha Mpiluka saruji tani mbili na nusu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi Mpiluka.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Mtua, wilayani Nachingwea, Anthony Makota   ambaye alisoma taarifa kuhusu matatizo yanayokikabili kijiji hicho mbele ya   Waziri Mkuu ambaye alisimama kijijini hapo kuwasalimia wananchi, Novemba 17, 2018 . Kulia ni Mbunge wa Nachingwea, Hasan Masala.  (Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu)
 Wananchi wa kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia  mkutano wa hadhara kijijini hapo Novemba 17, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea, Novemba 17, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia upinde aliopewa na wazee wa kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea ikiwa ni ishara ya kumtakia ulinzi wakati wote anapotimiza majukumu yake ya kulitumikia taifa.  Alikuwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kijijini hapo, Novemba 17, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Bw. Haji Nangase ambaye ni mwanachama maarufu wa chama cha siasa cha ADC baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea  Novemba 17, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAFO AKEMEA MILA YA KUTAKASANA KISIWA CHA UKARA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo amekemea mila ya wafiwa kutakaswa kwa kufanya tendo la ndoa na mtu mwingine ili kuondoa mkosi kwenye kisiwa cha Ukara kwa kuwa wanaweza kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) na ugonjwa wa Ini. 

Waziri Jafo amekemea tabia hiyo inayoendelea kisiwani humo kwasasa baada ya watu wengi kufiwa na wenza wao kutokana na ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama miezi michache iliyopita na kupoteza watu wengi.

Katika ziara yake maalum ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la ujenzi wa majengo yenye hadhi ya hospitali katika eneo la Ukara, Waziri Jafo amesema zoezi hilo limeanza rasmi leo na kuagiza ujenzi huo ukamilike ndani ya miezi mitatu. Amesema amepata taarifa kwamba wafiwa wanafanya mapenzi na watu wengine ili watolewe mikosi kitendo ambacho ametahadharisha kwamba kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo kutokana na watu wao kuambukizwa nagonjwa yakiwepo gonjwa la UKIMWI na Ugonjwa wa Ini yaani Hepatitis B.

Jafo amewataka wale ambao bado hawajafanya kitendo hicho cha kutakaswa wasijaribu kabisa kwani kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amemuhakikishia waziri Jafo kwamba watasimamia ipasavyo ujenzi huo na kukamilika ndani ya miezi mitatu ili adhima ya Rais Magufuli ya kuwasaidia wananchi wa Ukara katika sekta ya afya iweze kutimia.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akiwa na viongozi wenzake wakishiriki na wananchi kushusha vifaa vya ujenzi kutoka katika meli kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali kisiwa cha Ukara.
2
.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akitoa maagizo viongozi wa Mwanza.
3
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo
4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wakielekea kisiwa cha Ukara.

MAJALIWA AWASALIMIA WANANCHI WA KIJIJI CHA NYAMATULA WILAYANI NACHINGWEA

$
0
0


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Nachingwea wakati  alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea kwa ziara ya kazi wilayani humo, Novemba 17, 2018.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  
PMO_0104
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nyamatula wilayani Nachingwea akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo, Novemba 17, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Lindi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, Novemba 17, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakiitazama ngoma ya Nsolopa iliyotubuizwa na Kikundi cha Mshikamano wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea mkoani Lindi, Novemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>