Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAAGIZA HATUA KALI KWA WATAKAOINGIZA MAFUTA YA MAGENDO

$
0
0
*Yazitaka mamlaka husika kudhibitiuingizwaji wa vyakula visivyokuwa na virutubisho

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuhakikisha zinachukua hatua kali dhidi ya watu wote watakaobainika wanaingiza nchini bidhaa za chakula na mafuta ya kupikia kwa njia za magendo.

Kadhalika, Waziri Mkuu aziagiza mamlaka husika kuhakikisha zinaendelea kudhibiti uingizwaji holela wa bidhaa mbalimbali za vyakula visivyokuwa na virutubisho yakiwemo mafuta ya kupikia na kutoa adhabu kali kwa wafanyabiashara watakaobainika kuingiza bidhaa hizo nchini.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Novemba 15, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Vullu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alihoji kuhusiana na suala la uagizwaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje kama unazingatia sheria iliyopitishwa na Serikali ambayo inayolazimisha vyakula na mafuta ya kula kuwekwa virutubisho. 

Waziri Mkuu amesema ipo sheria (Sheria ya chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219) inayohusu udhibiti wa vyakula yakiwemo mafuta ya kupikia ambayo inasimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na imeweka utaratibu wa kudhibiti uzalishaji, uagizaji, usambazaji pamoja na uhifadhi wa mafuta.“Sheria hiyo pia inataka vyakula vyote vikiwemo vile vilivyoagizwa kutoka nje ya nchi na vinavyozalishwa hapa nchini yakiwemo mafuta ya kupikia, lazima viwekewe virutubisho.Wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kulinda afya ya mlaji.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inakusudia kuanzisha kurugenzi au idara itakayosimamia fukwe zote nchini zikiwemo za bahari na maziwa ili kuziimarisha na kuzifanya ziwe miongoni mwa vivutio vya utalii nchini.Amesema kuimarishwa kwa fukwe hizo kutawezesha watalii kupata maeneo ya kupumzika mara wanapotoka kutembelea vivutio vingine vya utalii vilivyopo nchini kama mlima Kilimanjaro pamoja na mbuga mbalimbali za wanyama.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Kiteto Zawadi Koshuma aliyetaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kukuza utalii nchini kupitia fukwe zilizopo katika ukanda wa bahari na maziwa, ambazo zimeachwa bila kuendelezwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA MERERANI,AFUNGUA KIWANDA CHA KUCHENJUA MADINI YA GRAPHITE

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan amewataka wamiliki wa migodi na viwanda vya kuchenjua madini nchini kuzingatia haki na usalama wa wafanyakazi wao.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachotengeneza madini ya Kinywe (Graphite), Mererani Wilayani Simanjiro.Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Manyara.

“Pamoja na kuwekeza kupata pesa na kutoa ajira, kulipa kodi ni muhimu kuzingatia afya ya mfanyakazi kwa kumlinda kwa kumpatia vifaa vya usalama kazini pamoja na haki zao” alisema Makamu wa Rais.

Kiwanda cha Gomwanga Gem Ltd kinamilikiwa Mtanzania kwa asilimia 100%, kinazalisha tani 60 kwa siku na kimeajiri Watanzania 80 ambacho mpaka sasa kimezalisha tani 3730.Kwa upande mwingine Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairuki amesema kwa sasa Serikali imeweka zuio la kusafirisha madini ghafi mpaka yaongwezewe thamani hivyo amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuitikia maelekezo ya Serikali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa namna madini ya Tanzanite yanavyotambulika na kuwekwa kwenye madaraja yake na Mtaalam wa Madini Bw. Jaffar Ally Mohamed wakati alipotembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mererani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Meneja wa Kampuni ya Godmwanga Gem Ltd Bw. Andrew Mbando (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti (kulia) wakati alipotembelea kiwanda kinachomilikiwa na Mzawa kwa asilimia ambayo inachenjua madini ya Kinywe (Graphite). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka  jiwe la msingi la ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kiwanda cha Godmwanga Gems Ltd kinachochenjua madini ya Kinywe (Graphite), Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

SERIKALI YASAINI MKATABA WA MKOPO NAFUU WA SHILINGI BILIONI 440.703 PAMOJA NA MSAADA WA SH. BILIONI 45 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA.

$
0
0
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James (kulia) akiwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Alex Mubiru wakisaini mikataba ya makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu wa  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 ambapo fedha hizo zote zitatumika katika Mradi mkubwa wa umeme mkoani Kigoma, Bajeti Kuu ya Serikali, Kilimo pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo.
 . Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James (kulia) akizungumza na wanahabari (hawaonekani) pichani mara baada ya kusaini Mikataba hiyo ya mkopo wa masharti nafuu wa  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa wa Hazina jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Alex Mubiru 
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Alex Mubiru (kushoto) akizungumza na Wanahabari mara baada ya Benki hiyo kuikopesha Serikali ya Tanzania  jumla ya Shilingi bilioni 440.703 pamoja na msaada wa Shilingi bilioni 45 ambapo fedha hizo zote zitatumika katika Mradi mkubwa wa umeme mkoani Kigoma, Bajeti Kuu ya Serikali, Kilimo pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo. 

POLISI WILAYA YA TABORA INAMSAKA ALIYESABABISHA TAHURIKI KWA KUTUMA MESEJI YA UONGO KUHUSU KUTEKWA WATOTO

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

JESHI la Polisi Wilaya ya Tabora linaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza ujumbe wa uongo juu ya kutekwa wa wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi ChemChem uliosababisha taharuki kwa wananchi na kupelekea kuharibu mali za Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tabora (OCD) John Mfinanga wakati akitoa ufafanuzi kwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora kwenye kikao cha robo ya kwanza.Alisema ujumbe huo ulisababisha kuwepo na uvunjifu wa amani ambao ulitokana na baadhi ya raia kuanza kuwashambulia Polisi na mgari yao na kupelekea kupasuliwa vyoo.

Mfinanga alisema hadi leo ikiwa saa 30 zimeshapita hakuna mzazi aliyejitokeza kutoa taarifa juu ya kupotelewa na mtoto jambo linaonekana lilikuwa na uongo na lenye nia ya kuleta vurugu katika jamii.“Waheshimiwa Madiwani ni mzazi gani anaweza kukaa zaidi ya masaa 24 mtoto wake amepotea hatoi taarifa…tunamtafuta aliyesambaza meseji hiyo ili hatimaye tumfikishe anapostahili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria” alisema.

Aliwataka Madiwani kusaidia kuwaelimisha wapiga kura wao wanapotoa taarifa ziwe za kweli ili zisisababishe taharuki na fujo katika jambo.Katika hatua nyingine Kamanda huyo wa Wilaya ya Tabora alisema Jeshi la Akiba Mgambo lipo kisheria na liko kwa ajili ya kusaidia majeshi mbalimbali yanapokuwa na uhitaji katika kutekeleza majukumu yao.

ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKURUGENZI wa mfuko wa maendeleo ya jamii -TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema, bado zipo kaya maskini 6,048 sawa na asilimia 30 Tanzania Bara na Visiwani, ambazo hazijafikiwa katika utekelezaji wa mpango kunusuru kaya maskini .

Aidha , wale ambao wameshanufaika awamu ya kwanza ya mpango huo watafanyiwa tathmini, na wameandaa mkakati wa kuwapima kwa vigezo vya kuwa na hali nafuu kwa utaratibu ili watoke na wapishe wengine.

Akiweka bayana juu ya masuala hayo, wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, alisema maeneo ambayo hayakufikiwa ,utekelezaji utaanza mwezi april 2019 ,ili kukamilisha maeneo yote nchi nzima 16,048.#

Mwamanga alisema vijiji,sheia na mitaa 10,000 wameshavifikia hadi sasa .

Alifafanua, kuna kaya maskini ziliachwa kwenye mpango kwa sababu mbalimbali nao wataingizwa kwenye mfumo thabiti ili kuwa na rekodi sahihi kwa nchi nzima.

Hata hivyo ,alisema kaya ambazo zina wazee na wenye ulemavu wataendelea kuwasaidia ili kukidhi mahitaji yao ya msingi.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N'hunga alisema, serikali ipo katika hatua za mwisho za kisera kutatua changamoto ya muda mrefu kwa kaya ambazo hazikujumuishwa katika mpango .

Alifafanua ,kaya hizo hazikuweza kujumuishwa kutokana na kutofanyiwa dodoso na baadhi ya walio fanyiwa dodoso kukataa mpango kwa madai kwamba hauna manufaa kwao.

N'hunga alisema, kupitia madodoso hayo ,serikali ikajumuisha watu hao  kwenye mpango kupitia changamoto hizo ,kuboresha sera na utaratibu uliopo ili kupunguza changamoto hiyo Bara na Visiwani kwa lengo la kuwafikia watanzania maskini katika ngazi ya sheia,kata, mitaa na vitongoji .

Hata hivyo alieleza dhamira ya serikali zote mbili kufikia april 2019 kaya zilizopo kwenye vijiji,sheia na kata ambazo hazijafikiwa waweze kufikiwa .

Katibu tawala msaidizi mkoani Pwani ,Abdulrahman Mdimu alisema, wanakabiliwa  na changamoto ya baadhi ya kaya maskini katika vijiji 86 ,mitaa 33 kutofikiwa kutokana na upungufu wa raslimali fedha .

Alitaja changamoto nyingine ni baadhi ya walengwa kukataa kuingizwa kwenye mpango kwa madai serikali haiwezi ikatoa fedha bure ,mitazamo hasi wakidhani kuwa kaya ikitambuliwa ni maskini ni kufedheheka.

Kamati hiyo ilitembelea pia ,mradi wa kutoa ajira ya muda -uvunaji wa maji ya mvua katika zahanati ya Disunyara kata ya Kilangalanga na kilimo cha bustani ,ambapo kaimu mratibu TASAF halmashauri ya Kibaha Vijijini Halima Bira, alisema mpango huo umekuwa mkombozi katika jamii .

Halima alisema ,mpango huo ulianza kutekelezwa 2012 na jumla ya kaya 7,250 zilitambuliwa na kati ya hizo kaya 5,600 kutoka vijiji 45 ziliandikishwa kwenye mpango.

Shuhuda wa utekelezaji wa mpango wa TASAF ,huko Disunyara Athumani Shabani alisema, ameweza kusomesha watoto ,wameibua miradi na wazee wananufaika kupitia mradi huo .
 Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N'hunga akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani. (picha na Mwamvua Mwinyi) 
 Kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii Ladislaus Mwamanga (mwenye suti ya rangi ya ugolo) na baadhi ya viongozi mkoani Pwani na halmashauri ya Kibaha Vijijini, wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kilimo cha bustani huko Disunyara Kibaha Vijijini. 

GST YAAGIZWA KUANDAA RAMANI ZA MADINI NGAZI ZA MIKOA, WILAYA

$
0
0
*Biteko asema wachimbaji sasa kuchimba kwa uhakika

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetakiwa kuandaa ramani zinazoonyesha madini mbalimbali katika ngazi ya Mikoa na Wilaya ili kuwapa nafuu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kupokea taarifa ya Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika nchi nzima kwa ushirikiano kati ya GST na Taasisi ya Jiolojia ya China.

Naibu Waziri Doto pia, ameitaka taasisi hiyo kuelekeza nguvu katika kuisaidia serikali katika kupata matokeo chanya katika shughuli za madini huku ikiongeza thamani ya kazi kutokana na utafiti huo na kuongeza kuwa, GST inaweza kutumia utafiti huo mkubwa kuandaa ramani za madini katika ngazi za Mikoa na Wilaya.

Akizungumzia manufaa ya tafiti huo kwa Tanzania, amesema baada ya muda si mrefu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji watahamia katika uchimbaji wa uhakika na siyo wa kubahatisha kwa kuwa utafiti huo unaonesha mahali sahihi ambapo shughuli hizo zinaweza kufanywa.

Amesema mbali na shughuli za madini, utafiti huo pia unaweza kutumika katika sekta za kilimo, maji na ujenzi wa barabara kwa kuwa unawezesha kutambua aina ya udongo unaofaa kwa shughuli hizo. 

Kutokana na umuhimu wa utafiti na kazi iliyofanywa na taasisi hizo mbili, Naibu Waziri Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuitumia taasisi ya GST katika shughuli za kitaalam ikiwemo kupata taarifa za utafiti zinazohusu sekta ya madini na kuongeza kuwa, sekta hiyo inao uwezo mkubwa wa kutekeleza wajibu wake.Aidha, Naibu Waziri Doto ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kutokana na ushirikiano huo iliyoutoa katika kutekeleza utafiti huo ambao umegarimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 4 na Laki Tano 
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akionesha taarifa ya utafiti wa jiokemia uliofanywa nchi mzima na Taasisi ya Jiolojia ya Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia ya China. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China Profesa Sun Xiaoming na Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mathias Absai.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya Jilojia ya China, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), na Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.
 Naibu Waziri Doto Biteko akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming Cheti cha kutambua mchango wake na kukamilika kwa utafiti wa Jiokemia uliofanywa nchini.

 Sehemu ya Wataalam kutoka Taasisi ya Jiolojia ya China, Wizara, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini wakifuatilia kikao hicho.

KUSOMOA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAWAFUNDA WANACHAMA WAKE KUHUSU UONGOZI NA UTAWALA BORA

$
0
0
 Mkufunzi kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Dkt Freddy Gamba akisisitiza jambo wakati akitoa mafunzo ya Uongozi na Utawala bora kwa wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania, ambapo wanachama hao wanatarajia kunufaika na mafunzo hayo kwa siku mbili yanayofanyika Dar es Salaam, huku lengo kuu ikiwa ni kuwajengea uwezo kiutendaji wanachama wa baraza katika taasisi wanazoziongoza. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko akisisitiza jambo kwa wanachama wa Baraza la Kilimo wanaoshiriki semina ya siku mbili ya Uongozi na Utawala bora, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo zaidi wa kiutendaji wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania ambao ni viongozi katika taasisi wanazoziongoza.
 Baadhi ya wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania ambao wanatoka kwenye Taasisi za TAMPRODA, SECO,  SUWA Farmers Association, Agri link Tanzania na Morogoro Rural Agro Dealers  Association, wakifuatilia mafunzo ya Uongozi na Utawala bora, mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika Dar es Salaam yameratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
 Mwenyekiti wa taasisi ya Morogoro Rural Agro Bw Michael Mpembwa akijadili jambo na washiriki wenzake na wa semina ya uongozi na uatawala bora, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji wanachama wa baraza la kilimo Tanzania.
Afisa Uhamasishaji Maendeleo ya wanachama na Uhusiano Kimtandao kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bw Khalid Ngasa na washiriki wengine wa semina ya siku mbili ya Uongozi na Utawala Bora, Semina hiyo imelenga katika kuwajengea uwezo zaidi wa kiutendaji wa wanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania ambao ni viongozi katika taasisi wanazoziongoza.

WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF

$
0
0
Na Lusungu Helela-Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko  wa Misitu Tanzania (TaFF) isimamie utekelezaji wa uanzishwaji wa  mradi wa viwanda  vya kusindika, kuchakata  na kufungasha asali katika mikoa inayofuga nyuki ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo   wakati alipokuwa akizindua  Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania uliofanyika leo jijini Dodoma.

Kufuatia agizo hilo, Waziri Kigwangalla ameiambia Bodi hiyo kuwa pamoja  na utekelezaji wa maagizo mengine aliyowapatia, suala la uanzishwaji viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali na bidhaa nyingine zitokanazo na ufugaji nyuki katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya liinapaswa kupewa uzito wa  juu kiutekelezaji.

Waziri Kigwangala ameongeza kuwa ni azma ya Serikali ya awamu ya tano kuifikisha Tanzania katika uchumi wa  kati ifikapo 2025 na kuwa suala hilo lina  umuhimu mkubwa  kwa wafugaji wa nyuki na uhifadhi mazingira..

Ameongeza kuwa endapo suala hilo la viwanda litafanikiwa , itasaida  kuchochea jamii  kuwa mstari wa mbele  kulinda misitu badala ya sasa jamii kujikita kwenye ukataji  miti ovyo hali inayotishia nchi kugeuka kuwa  jangwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza  na Wajumbe wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania  pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. 
 Mwenyekiti wa  Bodi ya pili ya Wadhamini  ya Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof. Romanus Ishengoma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Romanus Ishengoma  mara baada ya Waziri Kigwangalla  kuzindua  Bodi hiyo jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo,  Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)  wakimkabidhi kabrasha Mjumbe  wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Tuli Msuya (kulia)  wakati  Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

CDF YAPOKEA MILIONI 60 KUTOKA NETHERLAND KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA WANAWAKE NCHINI

$
0
0
SHIRIKA la utu wa mtoto nchini (CDF) limesaini makubaliano na ubalozi wa Nertheland nchini ambayo imetoa jumla ya shilingi milioni 60 zilizolenga kupunguza vitendo dhidi ya watoto na wanawake.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti amesema kuwa Netherland wamekuwa marafiki wazuri katika kuhakikisha wanawake na watoto wanaishi huru na hiyo ni kwa kutoa msaada ambayo inasaidia kupinga vitendo hivyo vya ukatili.

Mtengeti amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika programu jijini Dodoma katika Wilaya ya Mpwapwa na hiyo ni kutokana na hali ya juu ya ukatili jijini humo.Aidha amesema kuwa maeneo yatakayoangaliwa ni pamoja na kujua vyanzo vya matukio hayo, jinsi ya kufanya kazi na kamati ya kutokomeza matukio hayo na kuwajengea watoto na wanawake uwezo wa kutoa taarifa kuhusiana na matukio hayo.

Aidha amesema kuwa maeneo yatakayoangaliwa ni pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi, wanajamii katika kulinda haki za watoto na wanawake pamoja na wanaume katika kushiriki katika kulinda haki na kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya ukatili.

Pia amesema kuwa programu hiyo ni kubwa na wamefanya katika makao makuuu ya nchi ili kuweza kutoa taarifa sahihi kwa serikali ili kuweza kupunguza asilimia 40 za ukatili kwa wanawake.

Kwa upande wa balozi wa Netherlands nchini Jeroen Verheul amesema kuwa wanashiriki katika programu hizo ili kuhakikisha haki za wanawake nchini zinalindwa na wanafurahi kufanya kazi na shirika hilo na wana imani malengo ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake yatapungua kwa kiasi kikubwa.

CITI FOUUNDATION NA TAMFI WAZINDUA AWAMU YA TATU YA TUZO ZA WAJASIRIAMALI

$
0
0

Kwa mara ya tatu mfululizo, CITI Foundation ikishirikiana na Shirikisho la Asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha (TAMFI), jana wamezindua awamu ya tatu ya tuzo za wajasiriamali za CITI (CITI Micro entrepreneurship Awards – CMA).Tuzo hizi zinalenga kutambua mchango mkubwa wa wajasiriamali kwenye kuinua uchumi wa familia zao na jamii zinazowazunguka.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Citibank Tanzania, Bw. Joseph Carasso, tuzo za CITI zimeshamiri na katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na mafanikio makubwa kwa wajasiriamali wadogo na walio wabunifu. 

Mtendaji huyo alisema CITI inaamini kuwa wajasiriamali wadogo wenye ubunifu ndio wajasiriamali wakubwa wa kesho. Tunawathamini sana.Tuzo za wajasiriamali za CITI (CMA) zimekuwa alama kubwa ya utendaji wa kazi za Citi Foundation kwa zaidi ya muongo mmoja.

Tangu mwaka 2005, wakati zilipoanzishwa nchini Marekani tuzo za CITI, zimelenga kuleta mageuzi ya kiuchumi na fursa kwa wajasiriamali katika nchi zaidi ya nchi thelatini duniani kote.Hapa nchini katika awam,u ya tatu , CITI itatoa zaidi ya shilingi milioni 70 kwa washindi kumi na sita. Na tuzo hizi zitaweka alama na kutoa motisha kwa wajasiriamali na asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha.

Mtendaji mkuu Citi bank Tanzania joseph Carasso akizungumza. Mwingine ni wmenyekiti wa bodi ya Tamsi Joel Mwakitalu .

Mtendaji wa TAMFI Terry akielezea hafla ya uzinduzi wa tuzo 

Washiriki katika uzinduzi 

Naibu Waziri Dkt Kijaji Mgeni Rasmi Mahafali ya 11 ya Chuo Cha Kodi

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Kodi yatakayofanyika Novemba 17 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa Isaya Jairo amesema katika mahafali hayo Naibu Waziri atakabidhi zawadi kwa wanafunzi 14 waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali.

Profesa Jairo amesema kuwa wahitimu kwa mwaka huu ni 359 na idadi imekuwa ikiongezeka kila kila mwaka kutokana na ubora wa elimu wanayoitoa.Amesema mikakati ya Chuo ni kuwa Chuo Kikuu kutokana na mahitaji ya Kodi na kuwa Chuo pekee kinachotoa utaalam wa kodi katika Afrika Mashariki.

Profesa Jairo amesema wahitimu 74 watatunukiwa Cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki pamoja na wahitimu 33 watatunukiwa cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 142 stashahada Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 95 shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu 95 wengine shahada ya uzamili katika Kodi na wahitimu 15 Postgraduate Diploma.

Katika mahafali hayo Naibu Waziri Kijaji atatoa vyeti kwa wahadhiri waliofanya tafiti na kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya Kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Cha Kodi Profesa Isaya Jairo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mahafali 11 ya Chuo hicho yatakayofanyika Novemba 17 mwaka huu katika viwanja vya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

TIGO YAZINDUA PROMOSHENI YA ‘JIGIFTISHE’ AMBAPO SHILINGI MILIONI 600 ZITATOLEWA KWA WATEJA NA KUWAFANYA MAMILIONEA MSIMU HUU WA SIKUKUU

$
0
0

Wateja watakaoongeza salio au kuweka Pesa Kwenye Tigo Pesa au Kutumia huduma yoyote ya Tigo watapata nafasi ya kushinda zawadi nono za hadi TSH milioni 50!

Dar es Salaam, 15 Novemba 2018; Tigo Tanzania - kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, itawezesha wateja wake kuwa mamilionea baada ya kuzindua promosheni kubwa zaidi itakayogawa kiasi cha TSH milioni 600 katika msimu huu wa sikukuu.

Promosheni hiyo ya kipekee ya ‘JIGIFTISHE’ kutoka Tigo katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya itawafanya zaidi ya wateja 450 kuwa mamilionea ndani ya siku 45, kutokana na kutumia huduma za Tigo pekee. Ni rahisi na hakuna kujiunga kwenye promosheni hii.

‘Wateja wa Tigo watakaoweka pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, kuongeza salio au kununua simu janja kwenye maduka yote ya Tigo au kutumia huduma zozote za Tigo katika kipindi hiki cha sikukuu watapata fursa ya kujishindia TSH milioni 1 kila siku au TSH milioni 10 kila wiki. Pia kutakuwa na zawadi kubwa za TSH milioni 15, TSH milioni 25 au TSH milioni 50 zitakazotolewa mwishoni mwa promosheni hii ya JIGIFTISHE!’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Akibainisha vigezo vya ushiriki katika promosheni hiyo ya JIGIFTISHE, James Sumari, Mkuu wa Bidhaa za Huduma za Tigo Pesa wa Tigo alisema kuwa ili kupata fursa ya kushinda, wateja wa Tigo wanahitaji kununua kifurushi chochote kwa njia yoyote (ikiwemo kupitia *147*00#, *148*00# au kuongeza muda wa maongezi kwa njia ya kielektroniki, kadi au kupitia Tigo Pesa) au kufanya miamala ya Tigo Pesa kupitia *150*01# katika msimu huu wa sikukuu.

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (kushoto), Meneja Uhusiano wa Tigo Woinde Shisael (kati) pamoja na Balozi wa promosheni ya Tigo Jigiftishe, Lucas Mkenda almaarufu Joti (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wote watakaotumia huduma za Tigo katika msimu wa sikukuu fursa ya kushindania jumla ya shilingi 600 milioni. 
Mkuu wa Masoko wa Tigo, Tarik Boudiaf (kushoto), Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (wa pili kushoto), Balozi waTigo Lucas Mkenda almaarufu Joti (katikati), Meneja Mawasiliano Woinde Shisael (wa pili kulia) pamoa na Mkuu wa Bidhaa za Tigo Pesa, James Sumari (kulia) wakizindua promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wa Tigo fursa ya kushinda hadi TSH 50 milioni katika msimu huu wa sikukuu.

CBA BANK NA VODACOM WAFANYA PROMOSHENI YA PILI YA SHINDA NA M-PAWA

$
0
0
CBA Bank na Vodacom wamefanya promosheni ya pili ya Mpawa iliyoibua washidi wengine 200 walioweka amana na Mpawa , Ambao watajishindia mara mbili ya kiasi walichohifadhi kwenye Mpawa. 

Promotion hii ilizinduliwa tarehe 8 mwezi wa kumi na moja, Draw ya leo inafanya idadi ya washindi kuwa 430, Ambapo washindi 400 wamejishindia mara mbili ya amana zao walizohifadhi kwenye Mpesa, na washindi 30 ambao walikopa na kurejesha kabla ya wakati wamejishindi Shilingi TZS 100,000/= kila mmoja. 
 
Jumla ya washidi 1296 wanategemea kupatikana katika kipindi hiki cha wiki sita za kampeni. Zawadi kubwa zitakazotolewa kwenye droo kubwa wiki ya sita zitakua ni kitita cha Milioni 10 taslimu na Bajaj tano.

Promosheni hii inaonyesha jitihada za CBA Bank na Vodacom kuleta muamko wa kifedha na kuhimiza Watanzania kuwa na tabia ya kuweka akiba. Akizungumza wakati wa uzinduzi kutoa zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CBA Julius Konyani alisema “M-PAWA ni bidhaa inayoendelea kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa Watanzania hasa wale wamiliki wa biashara ndogo wanaoweka akiba na na kupata riba na Pia kupata mikopo inayowasaidia katika kuendeleza na kukuza biashara zao”.

Promosheni hii ya Shinda na M-PAWA itaendeshwa kwa muda wa wiki sita kuanzia Novemba 2018 hadi nusu ya Desemba 2018. Meneja Masoko wa Vodacom Huduma za kifedha Noel Mazoya alisema “Wateja watakaoomba mkopo na kurudisha mapema watakuwa na nafasi ya kuopoa zawadi ya shilingi 100,000 kwa wateja 15 kila wiki na Jumla ya wateja 96 watashinda kwa wiki sita. 
 
Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika CBA Julius Konyani(katikati), na muwakilishi kutoka Vodacom Tanzania Noel Mazoya, katika katika uzinduzi rasmi wa Promosheni iliyopewa jina la Shinda na M-PAWA. ilifatwa na kutangazwa kwa washindi 400 waliongezewa mara mbili ya salio lao, na watu 30 zaidi waliochukua mikopo na kulipa kwa wakati walijishindia 100,000 tshs kila mmoja.


WAZIRI LUKUVI ABAINI UJANJA UKWEPAJI KODI YA ARDHI MOSHI

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ATAMBULISHWA BUNGENI, JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alipomkaribisha Bungeni jijini Dodoma leo. Nsekela alimtembelea Spika Ndugai kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyemtemebelea Bungeni, jijini Dodoma leo kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ujumbe wa Benki ya CRDB uliomtembelea Bungeni jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipungua wakati alipotambulishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, kwa Wabunge jijini Dodoma leo.


MBARAWA AVUNJA MIKATABA YA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI YA LINDI NA KIGOMA

$
0
0

Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amevunja mikataba miwili inayohusu kandarasi ya ujenzi wa miradi ya maji kwa kampuni mbili za kimataifa. 


Kampuni hizo ni Overseas Infrastructure Alliance (India) Pvt. Ltd yenye mkataba Na. ME-011/2011-2012/W/05 iliyokua inatekeleza Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Lindi mjini na kampuni ya Spencon Services Ltd yenye mkataba Na. ME-011/2011-2012/W/05 iliyokua inatekeleza Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Kigoma mjini. Mikataba hiyo imevunjwa kutokana na uzembe wa wakandarasi hao kuchelewa kukamilisha miradi.

Profesa Mbarawa amefafanua kuwa mikataba ya wakandarasi hao imevunjwa kutokana na kufilisika kifedha na kusababisha kukosa uwezo wa kumalizia kazi ndogo iliyokuwa imebaki na kukamilisha miradi hiyo, kulikopelekea wananchi wa maeneo hayo kutopata huduma ya majisafi na salama kwa muda mrefu kinyume na matarajio ya Serikali hivyo kuvunjwa kwa mikataba.

Amesema hatua hiyo inatokana na miradi hiyo kuchukua muda mrefu kukamilika pamoja na juhudi za viongozi wa juu wa Serikali, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri mwenyewe kwa nyakati tofauti.

Mkandarasi wa mradi wa maji wa Lindi mjini kampuni ya Spencon Services Ltd ilipaaswa kukamilisha mradi toka Tarehe 17 Machi, 2015 kwa mujibu wa mkataba wa awali ikashindwa na kuongezewa muda hadi Tarehe 1 Desemba, 2015 lakini mpaka kufikia leo mradi huo haujakamilika. Naye mkandarasi wa mradi wa maji Kigoma mjini kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance (India) Pvt. Ltd ilipaswa kukamilisha Tarehe 17 Machi, 2015 kwa mujibu wa mkabata wa awali, na ikaongezewa muda hadi Tarehe 23 Desemba 2015. Mradi huo haujakamilika mpaka sasa ukiwa umefikia asilimia 87 ya utekelezaji.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akiwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu kuvunja mikataba ya Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Maji ya Mkoani Kigoma na Lindi.



ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA .

MKURUGENZI wa mfuko wa maendeleo ya jamii -TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema, bado zipo kaya maskini 6,048 sawa na asilimia 30 Tanzania Bara na Visiwani, ambazo hazijafikiwa katika utekelezaji wa mpango kunusuru kaya maskini . 

Aidha , wale ambao wameshanufaika awamu ya kwanza ya mpango huo watafanyiwa tathmini, na wameandaa mkakati wa kuwapima kwa vigezo vya kuwa na hali nafuu kwa utaratibu ili watoke na wapishe wengine.

Akiweka bayana juu ya masuala hayo, wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, alisema maeneo ambayo hayakufikiwa ,utekelezaji utaanza mwezi april 2019 ,ili kukamilisha maeneo yote nchi nzima 16,048.#

Mwamanga alisema vijiji,sheia na mitaa 10,000 wameshavifikia hadi sasa .
Alifafanua, kuna kaya maskini ziliachwa kwenye mpango kwa sababu mbalimbali nao wataingizwa kwenye mfumo thabiti ili kuwa na rekodi sahihi kwa nchi nzima. Hata hivyo ,alisema kaya ambazo zina wazee na wenye ulemavu wataendelea kuwasaidia ili kukidhi mahitaji yao ya msingi. 

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga alisema, serikali ipo katika hatua za mwisho za kisera kutatua changamoto ya muda mrefu kwa kaya ambazo hazikujumuishwa katika mpango . 

Kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii Ladislaus Mwamanga (mwenye suti ya rangi ya ugolo) na baadhi ya viongozi mkoani Pwani na halmashauri ya Kibaha Vijijini, wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kilimo cha bustani huko Disunyara Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi) 


Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani. (picha na Mwamvua Mwinyi) .

TCRA yawasaa vijana kutumia Teknolojia ya mawasiliano katika kujiletea maendeleo

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 MKURUGEZI wa Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Frederick Ntobi amewaasa vijana kutumia fursa za kiteknolojia za kisasa kubuni vitu mbalimbali vitakavyosaidia maendeleo ya  kiuchumi.

Akizungumza katika Maonesho ya Mawasiliano yaliyofanyika viwanja vya Posta, Ntobi amesema teknolojia za kisasa zikitumiwa vizuri zinaweza kubadili kubadili mwenendo wa uendeshaji wa shughuli za kiuchumi nchini.

Amesema  maonyesho ya kwanza ya Mawasiliano yaliyoandaliwa na Kampuni ya Aecco Cunsulting kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kitivo cha Tehama jiji hapa.

Amesema Maonesho hayo yanalenga kukuza biashara na kuongeza mwanya wa ubunifu na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

"Maonesho haya yatasaidia vijana kujitangaza lakini  wabadilike kutoka matumizi ya Tehama ya kuwasiliana mambo ya hovyo na badala yake watumie mawasiliano yenye tija ili kuibua ajira na kukuza uchumi wa mtu mmoja moja na hatimaye uchumi kwa taifa" amesema Ntobi

Ntobi TCRA inahimiza kampuni zote za sekta ya mawasiliano kutoa fursa kwa vijana kupata mafunzo kazini ili wawe wabobezi katika masuala ya Tehama.

Ubunifu wa vijana wetu wakiwa katika kampuni  unaweza kuleta maendeleo katika sekta ya mawasiliano kwani sasa tunakwenda  kwenye uchumi wa  viwanda hivyo vinahitaji rasilimali watu wenye ujuzi wa kuendesha mitambo kwa njia ya teknolojia ya kisasa"amesemaNtobi.

Ntobi ametoa rai kwa watoaji mafunzo katika katika vyou kuwa elimu na maarifa wanayotoa kwa wanafunzi  iwe chachu ya kujenga uwezo na ubunifu katika utendaji wa maisha yao.

Naye Meneja Mradi wa Aecco Jacqueline Buretta amesema wanatambua mchango wa mawasiliano katika kukuza uchumi wa viwanda hivyo maonyesho hayo ni muhimu na yako katika muda mwafaka

"Nia yetu ni kuendeleza ushirikiano na wadau wa sekta ya mawasiliani katika kuhakikisha kuwa na nafasi ya kuonesha bidhaa za mawasiliano kwa nia yabkuonesha umma upana wa sekta ya mawasiliano,"

 Hata hivyo amesema Maaendeleo ya ubunifu katika sekta ya mawasiliano haitofanikiwa bila ushuriki wa vyuo vikuu.

 Picha ya pamoja.
 Mkuu wa Chuo, Ndaki ya Tehama Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dkt. Mussa Kissaka akizungumza kuhusiana na utoaji wa elimu katika Chuo hicho katika masuala ya Tehama.
 Meneja wa Mardi AECCO na Waandaji wa maonesho Jucqline Buretta akizungumza kuhusiana na maonesho yaliyofanyika Jijini Dar Salaam.
 Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Fredrick Ntobi na Afisa Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano Mabe Masasi wakiwakabidhi muongozo wadau wa mawasiliano.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Fredrick Ntobi akizungumza wakati akifungua Maonesho ya Mawasiliano yaliyofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKABIDHI HATI MILIKI NA KIBALI CHA UJENZI KWA AUWSA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi hati miliki Mhandisi Humphrey Mwiyombela, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA), wakati wa makabidhiano hayo ya hati miliki na kibali cha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya kanda ya mamlaka hiyo hafla hiyo imefanyika leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya hati miliki na kibali cha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya kanda ya mamlaka hiyo hafla hiyo imefanyika leo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya hati miliki na kibali cha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya kanda ya mamlaka hiyo hafla hiyo imefanyika leo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa na wale wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira wa Arusha (AUWSA) wakifuatilia makabidhiano hayo ya hati miliki na kibali cha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya kanda ya mamlaka hiyo hafla hiyo imefanyika leo.

PONGEZI KWA Saddy Kambona

$
0
0
Tunampongeza Saddy Kambona kwa kufanikiwa kumaliza masomo yake ya shahada ya Uzamili(Masters) katika fani ya Sheria aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Novemba 13, 2018. Katika Sherehe za Mahafali iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
  Saddy Kambona
 Mzee Hamisi Kambona, baba mzazi, akimvalisha taji mwanaye Saddy Kambona ikiwa ni ishara ya kumpongeza katika Sherehe ya Mahafali iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Sherehe hiyo iliandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Novemba 13, 2018.
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live




Latest Images