Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

STARTMIMES YAJA NA LIPA TUKUBUSTI MSIMU WA KRISMASI

$
0
0

KUELEKEA msimu wa Krismasi kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya Startimes imekuja na promosheni kabambe kabisa Kwa wateja wao pendwa na kuwashauri  wale ambao bado hawajajiunga na familia ya StarTimes kuwa msimu huu wa siku kuu wanaletea ‘LIPA TUKUBUSTI’ambayo inawapatia faida nne Katika kila atakachonunua kutoka kwao ambapo kama kampuni  watawabusti au kuwaongezea wateja zaidi.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waigizaji maarufu wa Bongo Movie pamoja na wasanii wa Muziki wa kizazi Kipya.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja masoko wa Startimes Davis Malisa amesema kuwa Promosheni ya LIPA TUKUBUSTI kwa wateja wa StarTimes itawapa vifurushi vikubwa zaidi kila watakapolipia na kujiunga na vifurushi vyao vya kawaida kwa malipo ya mwezi Mzima. Hali kadhalika kwa wateja wapya watapatiwa Antena bure kila watakaponunua king’amuzi cha Antenna kwenye maduka na mawakala wa StarTimes.

“Vifurushi vyetu, kwa wateja wa Antenna Ukilipia kifurushi cha NYOTA kwa Tsh 8,000/= utapata kifurushi cha MAMBO kwa mwezi mzima, Ukilipia kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000/= tutakubusti hadi kifurushi cha Uhuru kwa mwezi mzima, na ukilipia Uhuru utapatiwa wiki moja bure" Ameeleza Malisa.

Aidha Malisa amesema kuwa
 kupitia promosheni hiyo wateja watanufaika kwa Kupata dishi bure kila watakaponunua luninga za Kidigitali za StarTimes za ukubwa wowote ule kuanzia Inchi 24, 32, 43 hadi ile Luninga Smati ya Inchi 55.

Kwa upande wa maudhui, Msimu huu wa Sikukuu StarTimes wamejipanga kuleta burudani hasa  Filamu Mpya kabisa za Bongo Movie Huku shindano la Bongo Star Search likiendelea, na kufikia hatua ya mchujo ndani ya Studio na shindano hilo linaendelea kuonekana Kila siku saa tatu Usiku kupitia chaneli ya StarTimes Swahili Pekee.

Kwa upande wake meneja maudhui wa Startimes Zamaradi Nzowa amesema kuwa, "Tuna furaha kubwa kuwaletea filamu za Bongo Movie Mpya kabisa kwa mwezi mzima wa Disemba, filamu ambazo zina mastaa tunawaowapenda na kuwafatilia kila siku. Ni wakati wa kutengeneza kumbukukumbu nzuri na wale tuwapendao na StarTimes inalifanikisha hilo. Sio hayo tu bali tunaleta Msimu mpya wa Coppa Italia kwa mara ya kwanza kupitia StarTimes pekee, utamshuhudia Cristiano Ronaldo na Juventus kuanzia Disemba 5 kupitia chaneli zetu za Michezo”. Ameeleza Zamaradi.

Pia Zamaradi amesema kuwa,   "Ligi ya Bundesliga inayoonyeshwa na StarTimes pekee, inaendelea sambamba na ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, huku zikichagizwa na Ligi ya EUROPA. Bila kusahau chaneli na vipindi vya watoto kama Jim Jam, POP na chaneli mpya ya ST Kids ambavyo vitahakikisha watoto wako wanakuwa na siku kuu ya kipekee.
Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
 Meneja Maudhui wa Startimes Zamaradi Nzowa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa tasnia ya Filamu pamoja na muziki wa kuhusu maudhui zitakazopatikana kwenye vifurushi vya Startimes wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen akizungumza kuhusu Startimes wanavyoshirikiana kwenye kuibua vipaji vya wasanii wachanga wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya kabambe kabisa awa wateja wao pendwa kwenye msimu huu wa Krismasi uliofanyiaka jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja

Mradi mkubwa wa kunoa bongo za ufundistadi wazinduliwa

$
0
0
Na Mwandishi wetu
MRADI mkubwa wa kufunza walimu wa wasimamizi wa mafunzo ya ufundi standi umezinduliwa kwa kufanyika kwa warsha itakayosaidia kutoa mwelekeo wa mradi .
Akizungumza katika warsha ya mradi huo wa BEAR ll unaofanyika katika nchi tano zikiwamo Tanzania na Uganda katika awamu yake ya pili, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Noel Mbonde akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo alishukuru serikali ya Korea na UNESCO kwa kusaidia kupatikana kwa elimu hiyo nchini.
Nchi zingine ni Ethiopia, Kenya, Madagascar, Tanzania na Uganda.
Alisema elimu hiyo itasaidia kuboresha na kuleta uwiano kati ya mafunzo ya ufundi stadi na matumizi yake katika viwanda nchini.
Alisema kuna malalamiko kwamba wahitimu wanashindwa kwenda sanjari na matakwa ya shughuli zao katika viwanda hivyo mradi huo ni msaada mkubwa.
Mradi huo wenye changio la dola za Marekani milioni 1.56 kwa kipindi cha miaka mitatu zinatarajiwa kusambazwa kwa mamlaka mbalimbali za mafunzo nchini yakiwemo mafunzo ya ufundi stadi zitakazowezesha wafundishaji kutoa mwanga unaotakiwa kwa mafundi stadi. Mamlaka hizo ni pamoja na TCU, Baraza la Ithibati (NACTE) nakadhalika.
Alisema mradi huo anaamini utatafuta tatizo la kutoa mafunzo kwa walimu wa ufundi na kuoanisha mahitaji ya viwanda.
Alisema ingawa awamu ya kwanza haikufika nchini Tanzania, awamu hii ya pili iliyoletwa nchini kwa miaka mitatu ina msaada mkubwa kwa watanzania ambao wanajiandaa kuwa nchi ya viwanda.
Pamoja na kushukuriwa, Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song amesema taifa lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba linawezesha elimu ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo.
 Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song akitoa salamu za serikali ya Korea Kusini wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde akizungumza kwa niaba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo wakati wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
 Sehemu ya wadau kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA pamoja wadau wa maendeleo walioshiriki uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.
Mgeni rasmi pamoja na washiriki wa uzinduzi wa mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi uliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 15,2018

BENKI YA BIASHARA YA DCB YAZINDUA UUZWAJI WA HISA ZAKE KUANZIA LEO

$
0
0
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa (kulia), akikabidhi hundi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka baada ya kununua hisa za benki hiyo muda mfupi baada ya DCB kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.Uzinduzi huu unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.

UONGOZI wa Benki ya DCB umetangaza rasmi kuanzia leo Novemba 12 mwaka huu kuanza hisa zake kwa wanahisa wa sasa na umma wa Watanzania kwa ujumla na kwamba uuzaji wa hisa hizo umegawanyika kwenye awamu mbili.

Wakizungumza leo wakati wanatangaza uuzaji wa hisa hizo jijini Dar es Salaaam uongozi wa benki hiyo umesema hiyo ni fursa ya kipekee ambayo wanahisa na watanzania wote wanatakiwa kuichangamkia na kwamba hisa moja itauzwa kwa bei ya Sh.265 ambayo ni cheni ya bei iliyopo kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE).

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara ya DCB Godfrey Ngalahwa amesema kuwa "Nachukua nafasi hii kuwataarifu kuwa uuzaji wa hisa za DCB unatarajia kuanza leo 12 Novemba 12, 2018. na kwamba Novemba 5, 2018, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ilitoa idhini ya uuzaji wa hisa kwa wanahisa wa sasa na umma wa Watanzania kwa ujumla.
"Dhana kubwa ni kuwaruhusu wanahisa waliopo kununua hisa na kutoa nafasi kwa wawekezaji wengine kununua hisa zitakazobaki. 

Uuzaji hisa za DCB umegawanywa katika awamu mbili, awamu ya kwanza itaanza leo hadi Desemba 3, 2018, ambapo hisa zitauzwa kwa wanahisa waliopo katika daftari la wanahisa. Aidha, kuanzia Desemba 4 hadi Desemba 18, 2018, hisa zote zitakazobaki zitauzwa kwa wanahisa waliopo na kwa wawekezaji wengine wasio wananhisa wa DCB. Kwa sasa, daftari limefungwa na mauzo ya hisa za DCB zilizopo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yamesimamishwa kuanzia November 7 kupisha uuzaji wa hisa,"amesema.

Kuhusu utaratibu wa kushiriki kwa wanahisa Profesa amesema wanahisa watakaoshiriki ni wale walioorodheshwa katika Rejista ya Wanahisa baada ya kufungwa kwa jalada ili kupata idadi ya hisa stahili, Novemba 7 mwaka huu na kusisitiza mwanahisa ana haki ya kununua hisa moja kwa kila hisa mbili anazomiliki.

Aidha amesema wawekezaji wengine wanatakiwa kujaza fomu kuonesha idadi ya hisa watakazonunua na baada ya awamu ya pili kukamilika, watagawiwa kwa mujibu wa utaratibu utakaowekwa na uongozi wa benki na maelekezo ya waraka wa matarajio.

Hivyo basi, wanahisa waliopo na wawekezaji wapya, wote wanaruhusiwa, kwa mujibu wa taratibu, kununua hisa zitakazobaki baada ya awamu ya kwanza kukamilika. Amefafanua malipo ya kununua Hisa za Haki yatafanyika kupitia matawi yote ya Benki ya Biashara ya DCB na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Akizungumzia mpango mkakati wa biashara ameseama kuwa kwa njia ya mashauriano, mwishoni mwa mwaka 2017, Benki ilikaa na kufafanua mpango wake wa biashara wa miaka mitano ambao utatekelezwa kwa awamu tatu na kwamba mafanikio yaliyopatikana kati ya Januari na Juni mwaka 2018 yametokana na kuweka msisitizo kwenye mabadiliko ya kiutendaji na kuhakikisha benki inapata faida.

"Kazi hii imekamilishwa ipasavyo na matokeo yake hadi Septemba 2018 benki imefanikiwa kupata faida ya TZS 1.4 bilioni. Mafanikio haya yametokana na kupungua kwa gharama za uendeshaji na kupunguza uwiano wa mapato na matumizi kutoka asilimia 104 mwaka 2017 hadi asilimia 81 mwaka 2018.Aidha, benki ilianzisha utaratibu wa kuboresha mtandao wa matawi na kutanua wigo wa bidhaa zilizopo na huduma kwa wateja ili kukuza mizania. Mikopo chechefu imedhibitiwa kwa kuanzisha mpango thabiti wa makusanyo ikiwa ni pamoja na kusuka upya idara ya mikopo,"amesema Ngalahwa.

Ameongeza benki hiyo inatarajia kufikia tarakimu moja ya mikopo chechefu mwishoni mwa mwaka 2019.Pia kuhakikisha benki inakuwa na wafanyakazi wenye maadili, utekelezaji wa programu ya mafunzo umefanyika na mchakato wa kuimarisha utamaduni wa utendaji unaendelea ambapo wafanyakazi wote wanahusika.Ameeleza mipango ya benki yao imekuwa kupata faida kabla ya kodi ya Sh.bilioni 1.8 ifikapo Desemba 2018.

 Katika kipindi hiki, mtaji wa benki unasimamiwa kwa uangalifu na ufanisi, huku hatua madhubuti za kukusanya mkopo na ufuatiliaji zinaendelea ili kupunguza mikopo chechefu huku tukizidi kukuza biashara.

"Mpango wa biashara uliorekebishwa wa miaka mitano unathibitisha matarajio ya benki kukuza mali zake kutoka Sh.bilioni 154.88 hadi Sh.bilioni 363.20 na amana za wateja kutoka Sh.bilioni 119.20 hadi Sh.bilioni 304.83. 

Kuhusu idadi ya wateja benki yetu imedhamiria kukuza mara mbili wateja wake mpaka 300,000 ifikapo mwaka 2022 huku ikiongeza masoko yake katika maeneo muhimu ya kimkakati,"amesema.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Profesa Lucian Msambichaka amesema anayo furaha kubwa kuzindua rasmi uuzaji wa hisa leo Novemba 12, 2018 na kusisitiza . Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa Watanzania kwa ujumla na kwamba hiyo ni fursa hii ni adimu kwa kuwa haitokei mara kwa mara ikizingatiwa kuwa mara ya mwisho, Benki ya DCB ilitoa fursa kama hii mwaka 2012.

"Kuhakikisha wananchi wengi wanapata fursa ya kuwekeza katika benki yetu, hisa hizi zitauzwa kwa bei punguzo ya Sh.265 sawa na punguzo la asilimia 22 ikilinganishwa na bei yake halisi iliyopo katika soko la hisa la Dar es Salaam ambayo ni TZS 340 kama ilivyonukuliwa tarehe 9th Novemba, 2018. Kila mwanahisa atapewa stahiki ya kununua hisa moja kwa kila hisa mbili alizonazo na mwekezaji mpya atatakiwa kuomba kununua hisa zitakazobaki. Uuzaji hisa za DCB umegawanywa katika awamu mbili, awamu ya kwanza itaanza leo hadi Desemba 3, 2018, ambapo hisa zitauzwa kwa wanahisa waliopo katika daftari la wanahisa. 

Aidha, kuanzia Desemba 4 hadi Desemba 18, 2018, hisa zote zitakazobaki zitauzwa kwa wawekezaji wengine wasio wanahisa wa DCB,"amesema.
Pia Profesa Msambichaka amesema Benki ya DCB inatarajia kuuza jumla ya hisa 33,913,948 ili kuongeza mtaji wa Sh. bilioni 8.9, mtaji huo utasaidia kuongeza uwezo wa benki sambamba na kuchochea ukuaji na mageuzi ya kibenki yatakayoifanya ijiendeshe kibiashara kikamilifu. Amesema benki ya DCB mpaka sasa ina jumla ya hisa 67,827,897 ambazo tayari zimeishanunuliwa na kulipiwa kikamilifu na kiasi cha mtaji uliolipiwa kuhusiana na hisa hizo ni Sh.bilioni 16.96. Utoaji huo wa hisa mpya utafikisha idadi ya hisa kwa ujumla kuwa 101,741,845.Bodi ya wakurugenzi itapitia kwanza maombi ya wanahisa waliopo kabla ya kugawa hisa kwa wengine walioomba kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Amesema wanahisa wa sasa na watarajiwa watafaidika na uwekezaji huu kutokana uuzaji wa hisa kwa bei pungufu ukilinganisha na bei ya soko huku wakiwa na kumbukumbu kuwa ni miongoni mwa fursa adimu zinazoweza kuwaongezea umiliki katika benki kwa kununua hisa mpya. Aidha, thamani ya kila mwanahisa inaweza kuongezeka kutokana na ukuaji wa bei ya hisa unaosukumwa zaidi na ukuaji wa biashara na nguvu ya hisa za benki katika soko la hisa. Vilevile mwanahisa atapata gawio kila mwaka kulingana na mwenendo wa kibiashara wa benki.

TWASHEREHEKEA MAISHA YA MAMA ma YOHANAMARIA KOKULAMUUKA MUTEMBEI

$
0
0
Tarehe hii mwaka jana, alfajiri alipoamka;
mawili akaongea, usingizini kurejea;
tukaita hakuitika; kumbe amehitimisha,
kwa kauli na vitendo, aliposema:“naba ndioo”,
kama anayetwambia kazi ameimaliza, 
kwamba saa ilishatimia, atavuka kwenda ng’ambo tupokee kishujaa. 
Mama amefaulu, hatulii, twashangilia.


Amebaki shujaa wetu kama Baba alivyokuwa.
Kushughulika na kuelekeza, mahitaji ya wanae kama Mwalimu stadi awezavyo darasa. 
Kila mwanae alijisikia amefika na kujiona muhimu kwake,
naye akawa rubani, kutuongoza safarini;
Akatujengea umoja, utuongozao mpaka kesho.
Ukidhihirika kwa jamaa pana, ya waume wa binti zake na wake wa wanae, 
watoto na wajukuu, vitukuu na vilembwe. 


Ukali twaukumbuka, alishikilia nidhamu,
hakutaka tupotee, kiimani, mila na desturi.
Alisimamia elimu na kuhimiza bidii, hakuwa na mzaha akisema waziwazi: 
afadhali msumbuke sasa faida mtaiona baadaye.
Aliiishi nidhamu, akawa mfano kwetu na wajao nyuma yetu.
Ya kwamba maisha bora ni bidii, kutokukata tamaa na kumtegemea Mungu.
Tunaposheherekea mwaka mmoja, twakumbuka ukarimu wake, 
Waliomtembelea hawakuondoka, bila chai, chakula na heri kuwaombea


Alithamini mila na desturi 
Akajiunga na kina mama, vyamani kijijini na mjini; 
Marafiki rika mbalimbali akawagusa watu wengi;


Alikuwa na elimu  
kuhimili changamoto,kujadili na wenye elimu mbalimbali bila kubaki nyuma
kipaji chake cha kumbukumbu kilikuwa kitabu cha historia, kilichoandikwa kwa umakini 
kukumbuka yaliyojiri, kwa habari za kijamii za furaha na huzuni, 
kwa habari za koo, za mila na desturi
Tunamshukuru Mungu tukisherehekea maisha yake. Alivipigana vita vizuri mwendo akaumaliza na imani akailinda.

Atakumbukwa daima na watoto Rhoda, Regina, Anders, Doris, Melissa, Alison, Aldin, Proscovia na Jovian; Wakwe wake na watoto wa kuwalea, wajukuu na vitukuu, ndugu,jamaa na marafiki,Daima tutamuenzi
Shukurani ya pekee itatolewa katika Kanisa la KKKT/NWD Usharika wa Kabale Bukoba, tarehe 18/11/2018

Wataalam wa afya Lindi wawashukuru Madaktari Bingwa kutoka Muhimbili

$
0
0
Wataalam wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE wanaendelea kunufaika na utaalam wa Madaktari Bingwa pamoja na wataalam wengine wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili huku wakiwashukuru kwa utaalam wao.
Watalaam hao kutoka Muhimbili wanawafundisha kwa vitendo jinsi ya kutoa huduma mbalimbali kwa usahihi na kwa ubora.
Maeneo ambayo wataalam wa hospitali ya Sokoine wananufaika ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara, magonjwa ya ndani, magonjwa ya dharura pamoja na Radiolojia.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa chakula na ini Godfrey Mchele amesema pamoja na kuwajengea uwezo wa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo upasuaji pia wanaangalia changamoto zinazowakabili na kuwashauri kitaalam.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija ameahidi kufanyia kazi ushauri na mapendekezo yanayotolewa na watalaam hao ambao wamebobea katika kutoa huduma za afya ili wajifunze na kuleta mabadiliko katika hospitali hiyo.
‘’Tuna shukuru uwepo wenu, tuna ahidi kufanyia kazi yale yote ambayo tunashauriwa na watalaam kutoka Muhimbili ili kusudi hospitali yetu ipige hatua katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi’. Amesema Kaimu Mganga Mfawidhi.
Watalaam wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwemo Madaktari Bingwa 11 bado wapo katika hospitali ya Sokoine kwa ajili ya kutoa huduma za afya na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo.
 Daktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa chakula na ini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Godfrey Mchele (kushoto) akiwafundisha Madaktari wa Kitengo cha Upasuaji cha Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE jinsi ya kuunganisha utumbo baada ya kukatwa.
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinywa na meno kutoka Muhimbili Kessy Frank (kulia) akimuelekeza Tabibu wa magonjwa ya kinywa na meno wa hospitali ya Sokoine Benard Mpepo namna ya kutoa dawa ya ganzi kwa usahihi kabla ya matibabu ya kinywa.
 Daktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa mkojo kutoka Muhimbili Edward Ogola akishirikiana na watalaam wa afya wa hospitali ya Sokoine kufanya upasuaji wa tezi dume.
 Mtaalam wa macho kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Elizabeth Mahende akimpima mgonjwa wa macho Bwan. Karim Wahedi ili kupata namba sahihi ya miwani itakayomsaidia kuona wakati wa kusoma na wakati anapotembea.

Wananchi wa mkoa wa Lindi wakisubiri kupatiwa huduma za afya na wataalam kutoka MNH kwa kushirikiana na wataalam wa hospitali ya Sokoine hii leo.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto  (katikati) na Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Mahmoud Mgimwa (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Awamu ya tatu ya tuzo za wajasiriamali za CITI (CITI Micro entrepreneurship Awards – CMA) yazinduliwa

$
0
0
Kwa mara ya tatu mfululizo, CITI Foundation ikishirikiana na Shirikisho la Asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha (TAMFI), jana wamezindua awamu ya tatu ya tuzo za wajasiriamali za CITI (CITI Micro entrepreneurship Awards – CMA).

Tuzo hizi zinalenga kutambua mchango mkubwa wa wajasiriamali kwenye kuinua uchumi wa familia zao na jamii zinazowazunguka.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Citibank Tanzania, Bw. Joseph Carasso, tuzo za CITI zimeshamiri na katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumekuwa na mafanikio makubwa kwa wajasiriamali wadogo na walio wabunifu.
Mtendaji huyo alisema CITI inaamini kuwa wajasiriamali wadogo wenye ubunifu ndio wajasiriamali wakubwa wa kesho. Tunawathamini sana.

Tuzo za wajasiriamali za CITI (CMA) zimekuwa alama kubwa ya utendaji wa kazi za Citi Foundation kwa zaidi ya muongo mmoja.

Tangu mwaka 2005, wakati zilipoanzishwa nchini Marekani tuzo za CITI, zimelenga kuleta mageuzi ya kiuchumi na fursa kwa wajasiriamali katika nchi zaidi ya nchi thelatini duniani kote.
Mtendaji mkuu Citi bank Tanzania joseph Carasso akizungumza. Mwingine ni wmenyekiti wa bodi ya Tamsi Joel Mwakitalu.
Washiriki katika uzinduzi
Mtendaji wa TAMFI Terry akielezea hafla  ya uzinduzi wa tuzo.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA




CGP KASIKE AFANYA ZIARA GEREZA LA WILAYA MAKETE, MKOANI JOMBE

$
0
0
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike akiwasili Gereza Makete tayari kwa ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe, Novemba 14,  2018.
 Mkuu wa Gereza Makete, SP. Aloyce Kayera(kushoto) akisoma taarifa ya Gereza mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo leo Novemba 14, 2018.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike akizungumza jambo alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya Makete Novemba 14, 2018. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
 Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza wakiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo askari hao wamempongeza Mkuu wa Jeshi hilo kwa uamuzi wake wa kutembelea magereza mbalimbali hapa nchini.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua maandalizi ya mashamba ya kilimo cha mahindi katika eneo la Gereza Ludewa mapema leo asbuhi Novemba 14, 2018  kabla ya kuelekea Gereza Makete kuendelea na ziara yake ya kikazi.
Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Veronica Kessy akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya Makete.

MAGWIJI WA KARATE WA OKINAWA WAWAAGA WANA-JUNDOKAN KWA " SAYONARA PARTY"

$
0
0
Ma- Masters wa Karate toka mitindo tofauti walihudhuria ufungaji wa sherehe ya chama cha Jundokan kilichotimiza miaka 65 na kuwakusanya wanachama wake toka nchi 30 ikiwemo na Tanzania iliyowakilishwa  na sensei Fundi Rumadha kwenye Asato Royal Orion Hotel, Naha,Okinawa,Japan. 
 Meza kuu magwiji wa karate ngazi ya juu kabisa wa Jundokan So Honbu.Masters: Kancho Yoshihiro Miyazato mwenyekiti wa Jundokan pia ni mtoto wa Eiichi Miyazato, Yasuda sensei, Kinjo sensei, Gima sensei, Higa sensei, Nakada sensei(USA), Renee sensei(France), Merriman sensei(USA) na Gsodam sensei ( Austria).
 Sensei Rumadha Fundi akiwa na Meitatsu Yagi kulia  wa  Meibukan Goju Ryu ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chojun Miyagi sensei, Meitoku Yagi mwanzilishi wa Meibukan Goju Ryu, kati ni master wa Okinawa Kobudo.
 Master Tetnosuke Yasuda Dan 10, umri wa zaidi miaka 94 akiwa na sensei Fundi Rumadha
 Sensei Rumadha akiwa Mwenyekiti wa Jundokan ambae pia ni mtoto wa mwanzilishi wa chama hicho master Eiichi Miyazato, pia ndie aliyekuwa mwalimu wa sensei Bomani mwanzilishi wa tawi la Jundokan Tanzania 1973.
Katika ufungaji wa sherehe hizo, pia walitunukiwa shahada au Dan wale wote waliopita mitihani yao asubuhi kabla ya sherehe. Ngazi ya juu kabisa katika shere hii kutunukiwa Dan,  ni Master Rony Kluger toka Israel aliyefuzu na kupewa shahada ya dan ya 9 na kuwa na cheo cha "Hanshi". pichani hapo Master Kluger akifanya kata ya Tensho.

Wananchi wazuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakidai shule

$
0
0
Wananchi wa kitongoji cha Senje, kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo wamefanikiwa kuuzui msafara wa mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo na kumuomba kuwawezesha wapate ushirikiano wa kujenga shule ili watoto wao waweze kusoma.

Wananchi hao wameeleza kuwa shule ya msingi iliyopo karibu ni kilomita saba kutoka katika kitongoji hicho ambapo shule hiyo ipo katika kijiji cha Samazi huku watoto hao wengi wadogo wakishindwa kufika katika shule hiyo kutokana na umbali.

Kitongoji hicho cha Senje ambacho ni kipya kimeanza kukaliwa na wananchi na kuonesha maendeleo baada ya kuanza kujenga vyumba viwili vya madarasa, kuchimba shimo la choo pamoja na kuwa na mabati kwaajili ya kuezeka majengo hayo huku wakiwa na suluhisho la dharura kwa kumlipa posho mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne ili aweze kuwafundisha watoto wao.

Kwa upande wake Mh. Wangabo alisema kuwa shule hiyo inayojengwa katika kitongoji hicho itaanza kuwa shule shikizi ya shule ya msingi samazi hivyo watoto hao wataanza kusoma shule ya awali, darasa la kwanza hadi la tatu kasha watahamia katika shule ya msingi samazi wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Aliongeza kuwa ili vyuma hivyo vianze kutumika ni muhimu kuwa na ofisi ya mwalimu na nyumba ya mwalimu ili halmashauri iweze kuunga mkono kwa kumleta mwaalimu na watoto waanze kusoma na kuwashauri kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo ili waweze kupewa mwaalimu haraka iwezekanvyo kwakuwa serikali ya wamu ya tano isingependa kuwaona watoto hawaendi shule.

“Kata pamoja na kijiji watasimamia hii, mkurugenzi utafuatilia kuhakikisha kwamba mtendaji wa kijiji na kata watasimamia ujenzi ule unaoendelea pale, lazima nyumba ya mwalimu isimame na ofisi ya mwali isimame na wakati huo muendelee kujipanga kuna swala la madawati watoto wasije wakakaa chini, vyoo ni uhimu ili wanafunzi watumie vyoo sio kwenda kwenye vichaka, shule haiwezi kuanza bila ya vyoo, tutaneza milipuko,” Alisisitiza.

Katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa Mkuu wa mkoa alimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya kalambo kuhakikisha wanaunga mkono kwa kununua mbao za kupaulia huku ofisi yake ikichangia bati za ofisi ya mwalimu pindi itakapokamilika.

Katika msafara huo ambao aliwepo mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura nae aliwataka kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo hauishii kwenye madarasa mawili tu na hatimae kuiachia serikali mzigo wa kuendelea kujenga shule hiyo wakati kitongoji hicho hakikuwahi kuwepo.

“Serikali sasa hivi ina utaratibu wa kusajili, kama hujatimiza vigezo huwezi kusajiliwa shule, hata mkiwa mmejenga vyumba viwili lazima mujenge ili mtoto akimaliza la kwanza, la pili, la tatu anaendelea, lakini wengine wakijenga vyumab wanaishia viwili tu halafu watoto wanaanza kusomea chini ya miti hatutaki,” Alibainisha.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na wananchi wa kitongoji cha Senje, Kijiji cha Samazi, Wilayani kalambo mara baada ya msafara wake kuzuiwa na wananchi hao wakidai kujengewa shule. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimkabdhi fedha mwalimu wa kujitolea katika kitongoji cha Senje, Kijiji cha Samazi anaewafundisha watoto wa kitongoji hicho ambao wapo mbali na shule ya msingi jambo lililowapelekea wazazi wa watoto wa kitongoji hicho kumlipa mwanafunzi huyo aliyemaliza kidato cha nne kuwafundisha watoto. 

DSTV YAZINDUA KAMPENI MPYA YA SIKUKUU 'NI MUDA WA KUKIWASHA NA DSTV'

$
0
0
    Na Khadija seif,globu ya jamii.

KAMPUNI  ya MultiChoice Tanzania imetangaza ofa Kabambe kwa wateja wake na  kwa wale wanaojiunga na huduma zao kupitia kampeni yake maalum inayokwenda kwa jina la  "Ni muda wa Kukiwasha na DSTV."

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo,Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema wateja wao sasa watapata burudani zaidi za kusisimua kupitia soka,filamu,Tamthilia,Katuni na vipindi mbalimbali vya watoto vitakavyoiletea familia pamoja na kuimarisha upendo.

Aidha Mria ameeleza kuwa mara kwa mara wamekuwa wakiwatunuku wateja wao wa zamani na wapya zawadi na ofa Kabambe huku wakiendelea kupata burudani ya uhakika muda wote kwani kwa mwaka huu wamekua wakitoa mfululizo wa zawadi kwa wateja wote.

Kwa upande wa Mkuu wa Mauzo wa Kampuni hiyo Salum Salum amefafanua ofa hiyo ni zawadi ya kufunga mwaka kwa wateja wapya wa Dstv kwani katika kipindi cha miezi miwili wataweza kuunganishwa kwa gharama ya shilingi elfu 79 tu  na kupewa kifurushi cha Bomba cha mwezi mmoja bila malipo ya ziada.

 Vilevile mbali na kuongezwa kwa chaneli na maudhui kedekede kwa wateja pia kwa wale ambao hawajajiunga hawajasahauliwa na kwa sasa watapata ofa hiyo Kabambe ya Kujiunga kwa gharama nafuu zaidi ya hapo wapate kifurushi cha mwezi mmoja bila malipo ambayo ni zawadi ya sikukuu kwa wateja wetu alisema Salum Salum .
 Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Ni muda mzuri Kukiwasha na DSTV   utakaowapa fursa wateja wao kupata burudani zaidi za kusisimua kupitia soka,filamu,Tamthilia,Katuni na vipindi mbalimbali vya watoto vitakavyoiletea familia pamoja na kuimarisha upendo.
 Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania Salum Salum akifafanua kuhusu ofa hiyo Kabambe msimu huu wa sikukuu  itakayowapa fursa wateja wao kupata burudani zaidi za kusisimua kupitia soka,filamu,Tamthilia,Katuni na vipindi mbalimbali vya watoto vitakavyoiletea familia pamoja na kuimarisha upendo.

MIUNDOMBINU YA RELI YABORESWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU SERIKALI YA AWAMU YA TANO- KADOGOSA

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii.

Shirika la reli nchini (TRC) katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli wameboresha sekta ya Miundombinu ya reli pamoja na kujenga reli ya kisasa "standard Gauge Railways " (SGR). 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa shirika la reli nchini(TRC) Masanja Kungu Kadogosa amesema shirika hilo lina majukumu ya kutoa huduma za usafiri wa abiria wa treni za mikoani pamoja na treni za mizigo ndani ya nchi na nje ya nchi. 

Amesema kwa sasa TRC imerudisha safari ya treni ya mizigo kutoka Dar es salaam mpaka Mji wa Kampala nchini Uganda, ambapo ikiwa na miradi miwili ambayo ni Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na Mradi wa uboreshaji wa reli ya kati pamoja na Miradi midogo kama kurejesha njia ya Tanga,Arusha na Moshi na baadae Mtwara,Mbambabei na njia ya Singida. 

Na Kadogosa amefafanua zaidi kuwa Mapato yameongezeka kutokana na huduma zinazotolewa na TRC na kuboreshwa kwa huduma za shirika kwa mwaka 2017/2018 na kufikia kiasi cha bilioni 36 tofauti na mwaka 2016/2017 ambapo kiasi cha pesa kilikua bilioni 23. 

Aidha, ameeleza Mradi unaendelea kutekelezwa katika sehemu mbili za mwanzo zinazojumuisha Dar es salaam,Makutopora kwa lengo la ifikapo 2021 mwezi wa pili , sehemu hizi mbili za Mradi ziwe zimekamilika. Na katika ujenzi huo shirika la reli (TRC) limetoa tenda kwa wakandarasi ambao ni ubia wa kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchi ya Uturuki na Mota Engil kutoka Ureno.

Sanjari na hilo kuna Kampuni za wazawa 16 zinazoshiriki katika ujenzi wa reli ya kisasa kama Wakandarasi,Wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma, lengo likiwa ni kushirikiana kati ya wazawa na wageni katika kujifunza na kujiongezea ufanisi mkubwa ili kuleta maendeleo Kwenye nchini yetu hususani Kwenye usafiri wa treni amesema Kadogosa.



Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli (TRC) 
Masanja Kungu Kadogosa  

akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa taarifa kuhusu maboresho yaliyofanywa pamoja Miundombinu ya Reli Katika miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano.

BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA.

$
0
0
BAADA ya mjadala wa muda mrefu hatimaye Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga limeamua rasmi eneo la Mwakidila lililopo Kata ya Tangasisi kuwa sehemu sahihi ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya Tanga ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.5

Awali hospitali hiyo ilitarajiwa kujengwa katika kata ya Masiwani ambapo tayari jengo la utawala la ghorofa moja lilikwisha jengwa ambalo linadaiwa kugharamia kiasi cha shilingi Milioni 700.Mjadala uliibuka ndani ya kikao hicho cha baraza hilo ambapo madiwani walipingana eneo gani linaweza kuwa sahihi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo mchakato wake unadaiwa kuanza tangu mwaka 2005.

Akizungumza Mwenyekiti wa baraza hilo Mstahiki Meya Mustafa Seleboss alisema kweli yapo maeneo matatu yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo kila eneo linachangamoto zake huku akibainisha umuhimu wa hospitali hiyo kujengwa katika eneo hilo la Mwakidila.Aidha alisema Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha shilingi Milioni 500 kati bilini 1.5 toka Serikali kuu kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itaondoa sitofahamu ya kutokuwepo kwa Hospitali hiyo ndani ya Wilaya.

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani 
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akipitia taarifa kwenye kikao hicho
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza katika kikao hicho

ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

CHAMA cha Madaktari bingwa wa watoto nchini kimefanya kongamano lake la kwanza la kisayansi kwa watoto wachanga likiwa na kauli mbiu ya "Kila pumzi ni ya thamani" likiwa na malengo ya kufundisha watumishi wa afya jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga ili kupunguza vifo vya watoto walio chini ya mwezi mmoja. 

Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa. Lawrence Museru amesema kuwa Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi mmoja na asilimia kubwa ya watoto hao huwa ni njiti na takwimu zinaonesha kuwa asilimia 13-17 ya watoto wanaozaliwa nchini huwa njiti. 

Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikiripoti programu mbalimbali ambazo lengo lake ni kupunguza vifo vya watoto wachanga na wale walio chini ya miaka 5, programu hizo ni pamoja na zile za kumsaidia mtoto kupumua baada ya kuzaliwa pamoja na kupanua huduma za watoto wachanga kwa kujenga wodi za watoto wachanga katika hospitali za Wilaya na Halmashauri pamoja na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kuhusiana na namna ya kuwahudumia watoto wachanga na programu hizo zimesaidia sana katika kupunguza vifo vya watoto wachanga. 

Aidha amesema kuwa kuanzishwa kwa wodi za watoto wachanga itasaidia pia kutatua changamoto ya matibabu kwa watoto hao na maboresho yanayoendelea kufanyika yatasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuhakikisha watoto wachanga hasa njiti wanapata huduma bora zinazostahili. 


WAZIRI LUKUVI ABAINI UJANJA UKWEPAJI KODI YA ARDHI MOSHI

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amegundua ujanja unaofanywa na baadhi ya wananchi wa Moshi mkoani Kilimanjaro wa kutochukua hati miliki za ardhi kwa lengo la kukwepa kulipa kodi ya ardhi.

Kufuatia hali hiyo Lukuvi ameagiza takriban hati 5,000 ambazo hazijachukuliwa katika Wilaya hiyo kuchukuliwa na wahusika na watakaoshindwa kuzichukua watafikishwa mahakamani kwa kosa la kukwepa kulipa kodi. Katika Manispaa ya Moshi Jumla ya viwanja 15,000 vimepimwa na kati ya hivyo ni hati 10,168 tu ndizo wamiliki wake wamejitokeza kuzichukua.

Aidha, Waziri Lukuvi amemuagiza Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi katika wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha ifikapo februari mwaka ujao (2019) anasitisha kesi za migogoro ya ardhi na kuanza kujikita katika kusikiliza kesi za wamiliki wa ardhi wasiolipa kodi ya ardhi ili kuiwezesha serikali kupata mapato.

‘’Wote wasiolipa kodi iwe waliokuwa na hati ama wasio na hati lakini wanaishi katika maeneo ya mijini yaliyopangwa ikifika februari 2019 watafikishwa mahakamani na tutahakikisha wanadaiwa kuanzia kipindi walichomilikishwa na wakishindwa nyumba zao zitapigwa mnada’’ alisema Lukuvi

Akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo zaidi ya 150 waliojitokeza kuwasilisha kero zao za ardhi kwa Waziri Lukuvi katika program maalum ya Funguka kwa Waziri leo (jana), alisema katika ziara yake wilayani Moshi amebaini kuna hati zipatazo 5000 huku baadhi yake zikiwa na zaidi ya miaka 18 hazijachukuliwa na wahusika ambapo kwa mujibu wa Lukuvi wengi wao hawataki kuzichukua kwa kuogopa kulipa kodi ya ardhi.

MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia)  akimwapisha , Mbunge wa Simanjiro, James Millya, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 15, 2018. 
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (Kulia) akimwapisha Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 15, 2018. 
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia)  akimwapisha mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chacha, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 15, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi baada ya  Mbunge huyo kuapishwa, bungeni jijini Dodoma, Novemba 15, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul baada ya mbunge huyo kuapishwa, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 15, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Iramba Magaharibi, Mwigulu Nchemba kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JUMIA TANZANIA YAZINDUA KAMPENI KUBWA YA MAUZO YA MWAKA ' BLACK FRIDAY'

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MTANDAO wa Jumia Tanzania umezindua rasmi kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.

Black Friday imekuwa inafanya mauzo ya bidhaa tofauti kwa bei nafuu kutoka kwa wauzaji mbalimbali mtandaoni na kwa kupitia Jumia Tanzania itadumu kuanzia Novemba 16 hadi Desemba.Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo ya Black Friday, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James amesema kuwa, kwa kawaida Black Friday imekuwa inafanyika kila mwaka ifikapo Novemba 23, lakini kwa mwaka huu itakuwa kila Ijumaa na itaanzia Novemba 23 mpaka Desemba 07 mwaka huu.

James amesema, tofauti na siku za kawaida za Black Friday kutakuwa na ofa nyingi zaidi na mapunguzo makubwa ya bei kwa bidhaa zote mpaka kufikia asilimia 70 na hii katika kuhakikisha wateja hawapitwi kunufaika na maununuzi ya bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara tofauti wanaoaminika kwenye mtandao wa Jumia."Ukiachana na ofa na mapunguzo ya bei, kutwakuwa na vocha za bure za manunuzi kuanzia shilingi 5,000 mpaka 80,000, mauzo ya bidhaa ya muda mfupi katika siku (flash sales) na kuogesha zaidi Black Friday kutakuwa na 'Treasure Hunt' kila Ijumaa ambapo bidhaa itafichwa kwenye mtandao wa Jumia," amesema James.

"Mteja mwenye bahati atakayefanikiwa kuitafuta na kuipata atauziwa kwa bei yenye punguzo la asilimia 99, na baadhi ya zawadi zitakazokuwepo kuanzia Ijumaa hii ni luninga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 32 inayouzwa kwa shillingi 570,000 mtandaoni na itafichwa na kuuzwa kwa 5,700 kwa mteja atakayeipata, "amesema.Aidha, ameongeza kuwa lengo kuu la Jumia ni kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa urahisi na haraka mahali popote naa muda wowote walipo na mteja atakayenunua bidhaa kupitia Jumia itakayozidi thamani ya 200,000 atapelekewa bure mpaka alipo kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa upande wa washiriki wa Black Friday, Kutoka kampuni ya Skymark Meneja wa Kampuni hiyo, Nishit Modessa amesema kuwa wameamua kushirikiana na Jumia Tanzania baada ya kuona ni wazo zuri sana baada ya kuletewa na wakaamua kutoa pikipiki ili wateja wa Jumia washindanie.

Miodessa amesema, huu ni mwanzo wa ushirikiano wao ila wanategemea kuendelea kushirikiana nao zaidi katika kuuza bidhaa zao ambazo ni pikipiki na bajaji kupitia njia ya mtandao.
 Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James  akizungumzia  uzinduzi  rasmi wa kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka inayojulikana kama BLACK FRIDAY inayolenga kuwawezesha watanzania kufanya manunuzi kwa ajili nya msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya kupitia mtandao wa Jumia Tanzania, kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma Jumia Tanzania Kijanga Geofrey.
 Meneja wa Kampuni ya Skymark Nishit Modessa akielezea ushiriki wao kwa mara ya kwanza katika mauzo makubwa ya mwaka yanayofanyika kupitia kampuni ya Jumia Tanzania na kuamua kushirikiana nao kwa kutoa pikipiki na wateja washindanie, Kushoto ni  Meneja Masoko wa Jumia Tanzania Albany James. 

Uvuvi haramu ziwa Tanganyika wakusanya milioni 90 ndani ya mwezi mmoja

$
0
0
Operesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika kanda ya Kasanga, mkoani Rukwa imefanikiwa kukusanya shilingi milioni 90 ndani ya mwezi mmoja ikiwa ni adhabu mbalimbali kwa wavuvi waliokiuka sheria za uvuvi na.22 ya mwaka 2003 pamoja na sheria ya mazingira na.20 ya mwaka 2004.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa operesheni hiyo Geofrey Salaka wakati akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo baada ya kutembelea katika soko la samaki la kasanga na kuongea na maafisa wa operesheni hiyo.

Salaka alisema kuwa mbali na kuwatoza faini hizo pia wamefanikiwa kutoa elimu na kuwahamasisha wavuvi wadogowadogo kulipia leseni zao za uvuvi na leseni za vyombo wanavyovitumia kwa shughuli za uvuvi kama sheria inavyotaka huku akielezea changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu hayo.

“Changamoto tunazozipata ni pamoja na kukumbana na fujo kutoka kwa wananchi utoroshwaji wa samaki na mazao ya uvuvi kwenda nje ya nchi, kuwepo raia wa kigeni wakijihusisha na shughuli za uvuvi, hali ya hewa, upepo mkali, mvua na mawimbi ziwani,” Alisema.

Kwa upande wake Mh. Wangabo alipongeza juhudi hizo za kuhakikisha mapambano dhidi ya uvuvi haramu hayarudi nyuma ili kutunza na kuhifadhi samaki na mazingira katika ukanda wa Ziwa pamoja na Ziwa lenyewe na kusisitiza elimu iendelee kutolewa kwa wavuvi ili washiriki katika kutunza mazingira.

“Tuendelee kuwaelewesha wavuvi, vinginevyo wataendelea kuharibu rasilimali ya taifa letu, na hii ni kwaajili yetu sisi na vizazi vinavyokuja, tukivua katika hali ambayo haina uvuvi endelevu tutawafanya hawa samaki mwishoni watakwisha, wakiisha hawa watu watakwenda wapi, maisha yao yanategemea hapa lakini hawajui hilo, wanataka waharibu mpaka kambi sijui watalala wapi,” Alisema.

Na kuongeza kuwa atahakikisha anafanya mkutano na wananchi na wavuvi hao ili kuweza kuwaelimisha juu ya madhara yanayoweza kujitokeza kama uvuvi haramu utaendelea kutekelezwa bila ya usimamizi wowote.

Operesheni hiyo ilianza tarehe 19.10.2018 na Miongoni mwa zana zilizokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na Injini za boti 10, mitumbwi 48, magari 9 ya kusafirisha samaki, pikipiki 4 zilizokuwa zinasafirisha samaki, samaki wachanga kilo 2050, nyavu 250 za makila chini ya nchi tatu pamoja na nyavu 20 za timber (monofilament nets).

KUMBUKUMBU YA BIBIANA ( NKAMALI ) KWEKA

$
0
0

KIFO 16/11/2001

BIBIANA (NKAMALI) PETER BASI KWEKA


Bibi yangu mpendwa na somo wangu pia.Leo umetimiza miaka 15 tangu ulipoitwa mbinguni kwa BABA. Hatuna cha kusema,tumebaki kushukuru tuu kwani hata miaka ulioishi ilizidi ile ya Upendeleo.


Tunakumbuka sana  uzuri wako,Ucheshi,Usafi na Ufanyakazi wako bila kusahau jina lako (BIBI SHAMBA). Kweli ulikuwa mfano wa kuigwa.   Unakumbukwa sana na mimi somo wako JANE, WAJUKUU WOTE WA KWA BASI SARONGA,  MTOTO WAKO WA PEKEE ALIYEBAKI DUNIANI SR.DEVOTA KWEKA CDNK,  WA KWEKA WOTE WA NARUMU, WA –ULOMI WOTE WA USWAA- MACHAME, NDUGU, JAMAA  NA MARAFIKI ,MISA YA KUMUOMBEA IMEFANYIKA LEO ASUBUHI KWENYE KANISA LA MKOLANI- MWANZA.


RAHA YA MILELE UMPE EEEH  BWANA . . . . 



Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images