Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

WATENDAJI KATA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE WAPATIWA MKOPO WA PIKIPIKI

$
0
0
Hyasinta Kissima
Halmashauri ya Mji Njombe imekusudia kutatua changamoto ya upungufu wa vitendea kazi kwa watendaji wa Kata katika Halmashauri hiyo kwa kuwakopesha pikipiki.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya pikipiki hizo kwa watendaji wa Kata za Lugenge, Matola, Ihanga na Kifanya  Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Halmashauri ya Mji Njombe Abdulatif Mkata amesema kuwa lengo la Halmashauri kuwakopesha pikipiki hizo ni kutoa motisha kwa watendaji waliofanya vizuri katika utendaji wao wa kazi na kurahisisha utendaji kazi wa watendaji hao wa Kata kwa kuwa Kata wanazozisimamia ni kubwa na pikipiki hizo zitawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa urahisi kwa kuweza kufika kwenye Vijiji vya Kata na kufanikisha utoaji wa huduma kwa jamii kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa wanazitunza pikipiki hizo na kuhakikisha kuwa zinatumika kwa ajili ya ufuatiliaji wa mapato ya Halmashauri na usimamizi wa shughuli za maendeleo katika Kata zao.
“Kwanza natoa pongezi kwa kazi nzuri mlizofanya katika Kata zenu.  Pikipiki hizi tumewapatia kama mkopo ili muweze kuzitunza kwani utakapo maliza mkopo wewe ndio utakua mmiliki halali wa pikipiki hizi. Ni matumaini yangu kuwa sasa mtaenda kusimamia shughuli za maendeleo ya Kata kwa urahisi lakini kubwa zaidi kusimamia mapato ya Halmashauri kikamilifu.”Alisema Mwanzinga.
Khadija Lutumo ni Mtendaji wa Kata ya Lugenge Halmashauri ya Mji Njombe ambaye ni miongoni mwa watendaji waliokabidhiwa pikipiki hizo ambapo ameishukuru Halmashauri kwa kutoa motisha ya pikipiki  kwani itasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa vitendea kazi  na ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika Kata yake na kusimamia mapato kikamilifu kwani kwa kutumia pikipiki aliyokabidhiwa swala la usimamamizi litakuwa rahisi.
Halmashauri ya Mji Njombe imefanikiwa kununua pikipiki nne zenye thamani ya Shilingi milioni tisa laki 4 kupitia mapato ya ndani na imekusudia kuhakikisha kuwa katika siku za mbeleni watendaji wote watakaofanya vizuri katika maswala ya utendaji kazi na ukusanyaji mapato wanakopeshwa pikipiki  kwa kutenga  bajeti  na kuhakikisha Mazingira ya kazi ya watumishi wake yanaboreka siku hadi siku.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji Njombe ni miongoni mwa Halmashauri za Miji zinazofanya vizuri katika swala la ukusanyaji mapato na imejizatiti kuhakikisha kuwa kadri siku zinavyosonga mbele ikusanye zaidi ya malengo yaliyokusudiwa na kuibuka kinara  katika makusanyo ya mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga akimkabidhi funguo ya  pikipiki Mtendaji wa Kata ya Lugenge  Khadija Lutumo wakati wa utoaji wa mkopo wa pikipiki kwa watendaji wa Kata Halmashauri ya Mji Njombe 
 Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Halmashauri ya Mji Njombe Abdulatif Mkata akizungumza jambo wakati wa makabidhiano ya pikipiki hizo.Kushoto kwake ni watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Mji Njombe
Wajumbe wa Kamati ya fedha na wataalamu wa Halmashauri ya Mji Njombe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya pikipiki hizo.

Benki ya Exim yatoa Mil 10 kufanikisha maadhimisho siku ya takwimu duniani.

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasialiano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Philip Mpango ( wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa ( wa pili kulia), Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Peter Msoffe (wa pili kushoto) katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimishwa jijini Dodoma hivi karibuni ambapo Benki ya Exim ilitoa kiasi cha Sh Milioni 10 kufanikisha maadhimisho hayo kupitia chuo kikuu cha UDOM.
 Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasialiano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (katikati) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Mil 10/-  kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Peter Msoffe (wa pili kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimimishwa jijini Dodoma hivi karibuni.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango,  akizungumza na waandishi wa habari alipohudhuria katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimimishwa jijini Dodoma hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo.

MAHAKAMA YAKWAMA KUSIKILIZA KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU

$
0
0
Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na mwenzake, sababu shahidi wa upande wa mashtaka ana dharura.

Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru Vitalis Peter amedai leo Novemba 13, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini wamepata taarifa kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika Kesi hiyo amepatwa na dharura.

Kutokana na hiyo, Hakimu Simba alisema kwa mtindo huu hii Kesi haitomalizika, watakuwa wanacheza tu."Wasa muwe mnaleta mashahidi Wawili Wawili ili mmoja akipata dharura mwingine anaendelea kwani hali kama hii imekwisha jitokeza zaidi ya mara nne au tano" amesema Hakimu Simba.

Wakati upande wa utetezi ukiwakikishwa na Wakili Alex Mgongolwa amewataka mashahidi wanaokwenda kutoa mashahidi katika Kesi hiyo wajulikane na kwamba upande wa mashtaka unapoona shahidi wanayemtafuta anahitilafu watafute mwingine.

Aidha hakimu Simba ameusisitiza upande wa mashtaka kupeleka mahakamani hapo mashahidi wawili wawili.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 27 na 28, mwaka huu ambapo utaendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.Katika kesi hiyo, Gugai na wenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, katika Mahakama hiyo.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Gugai ni kosa la kumiliki mali zilizozidi kipato chake halali, ambapo anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2005 na Desembea 2015.

RC TABORA AAGIZA POLISI KUFANYA DORIA MAENEO YA SHULE ZA MSINGI ILI KUDHIBITI UOVU DHIDI YA WATOTO

$
0
0
NA TTGANYA VINCENT,RS TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeamua kuweka ulinzi katika shule za Msingi za Manispaa ya Tabora nyakati za masomo ili kuzuia kusije kukatolekea kwa vitendo vyovyote vya kuwazulu na kuwateka wawapo shuleni.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kufuatia vurugu kubwa zilizotokea leo katika Shule ya Msingi Chemuchemu baada ya kuwepo kwa hisia ya watoto wawili kutekwa.

Alisema hadi hivi sasa hajajulikana kama kweli kuna watoto wa Shule hiyo waliotekwa na kupandishwa katika gari aina ya Noah.Mwanri alisema wamejaribu kufuatilia ili kujua ni watoto gani na majina yao ya watoto waliotekwa hakuyapata na wala hakuna mzazi aliyejitokeza kusema kuwa mtoto wake amepotea.

Alitoa wito kama kuna wazazi ambapo watoto wao wametekwa watoe taarifa kwa Polisi au katika Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ili hatua ziweze kuchukuliwa ikiwemo kuwatafuta.“Kuanzia sasa nimeagiza Polisi kuongeza Doria katika maeneo ya shule za Msingi ili kuwaondolea hofu wazazi…na kama mtu asifahamika ataonekana maeneo ya shule achukuliwe hatua” alisema.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema vurugu hizo zilitokana na wananchi kuwa bado na kumbukumbu ya wiki iliyopita ambapo mtoto wa miaka 6 alitekwa na kuwawa katika eneo la Tambuka Reli.Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kulifanyia uchunguzi matukio yote na kuwataka wazazi kuwa watulivu.

WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefanikiwa kupata dhamana baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi kuridhia wapate dhamana na kuwapangia masharti ya dhamana.

Hatua hiyo imekuja baada ya washtakiwa kupitia mawakili wao kupeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu kwa kuwa washtakiwa wameshtakiwa chini ya sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo kesi hizo zinasikilizwa Mahakama Kuu.

Washtakiwa waliopata dhamana ni Ofisa wa Mazingira NEMC, Deusdith Katwale(38) na Mtaalam wa IT NEMC, Luciana Lawi(33) wote wakazi wa Ubungo Msewe, Katibu Muhasi wa NEMC (Sekretari), Edna Lutanjuka (51) Mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, Msaidizi wa ofisa Mwaruka Mwaruka (42) na Ofisa mazingira Nemc, Lilian Laizer (27) wote wakazi wa Ukonga Mombasa.

Washitakiwa hao Octoba31, Mwaka huu walisomewa mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa Mazingira.

Akiwasomea masharti sita ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama Kuu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando amewataka kila mshtakiwa kuweka fedha benki kiasi cha Sh. Milioni 13.3 au kuwasilisha mahakamani hapo hati ya mali isiyoamisha yenye thamani hiyo ya fedha.


MAKAMU WA RAIS AWASILI MERERANI TAYARI KWA ZIARA YA SIKU 5

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Mererani wilayani Simanyiro mkoani Manyara kwa ziara ya siku 5.

Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti, Wabunge pamoja Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi ambapo alipokea taarifa ya mkoa iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa.

Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Mkoa wa Manyara alimueleza kuongezeka kwa mapato katika mkoa huo sambamba kuongezeka kwa makusanyo mara baada ya kujengwa kwa ukuta.

“Miezi 10 kabla ya kujengwa kwa ukuta tulikuwa tunakusanya milioni 402 na miezi 10 baada ya ukuta tunakusanya bilioni 2.1” alisisitiza Mkuu wa Mkoa.

Makamu wa Rais ameushukuru uongozi wa mkoa kwa mapokezi mazuri na kuupongeza kwa hatua mbali mbali za kimaendeleo pamoja na kuboresha huduma za jamii ikiwemo huduma maalum kwa wazee.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Serikali pamoja na Chama mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa,wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara Ndugu Simoni Lulu.
Makamu wa Rais amewasili Mererani leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 5 ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Manyara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay na Mbunge wa Babati mjini Mhe. Vrajilal Jituson.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Hannang Mhe. Mary Nagu.

TRC YAJIVUNIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA RELI NCHINI , WASIFU JITIHADA ZA SERIKALI

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema linajivunia kuboresha miundombinu ya reli nchini ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kuboresha miundombinu hiyo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge Railways (SGR).

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa wakati anazungumzia miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli ambapo amesema shirika hilo lina majukumu ya kutoa huduma za usafiri wa abiria wa treni za mikoani na treni za mizigo ndani ya nchi na nje.

Pia amesma kwa sasa TRC imerudisha safari ya treni ya mizigo kutoka Dar es salaam mpaka Mji wa Kampala nchini Uganda, ambapo ikiwa na miradi miwili ambayo ni mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa uboreshaji wa reli ya kati pamoja na miradi midogo kama kurejesha njia ya Tanga, Arusha na Moshi na baadae Mtwara,Mbambabei na njia ya Singida.

Kadogosa amefafanua zaidi kuwa mapato yameongezeka kutokana na huduma zinazotolewa na TRC na kuboreshwa kwa huduma za shirika hilo kwa mwaka 2017/2018 na kufikia kiasi cha Sh.bilioni 36 tofauti na mwaka 2016/2017 ambapo kiasi cha fedha kilikua Sh. bilioni 23.

Pia amesema kuna miradi ya ujenzi wa miundombinu ya reli inaendelea kutekelezwa katika sehemu mbili za mwanzo zinazojumuisha Dar es salaam na Makutopora, kwa lengo la ifikapo 2021 Aprili , sehemu hizo mbili za mradi ziwe zimekamilika. Pia amesema katika ujenzi huo TRC limetoa zabuni kwa wakandarasi ambao ni ubia wa kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchi ya Uturuki na Mota Engil kutoka nchini Ureno.

Wakati huo huo amesema kuna Kampuni za wazawa 16 zinazoshiriki katika ujenzi wa reli ya kisasa kama Wakandarasi,Wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma, lengo likiwa ni kushirikiana kati ya wazawa na wageni katika kujifunza na kujiongezea ufanisi mkubwa ili kuleta maendeleo kwenye nchini yetu hususani Kwenye usafiri wa treni.

Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila

$
0
0
Na Neema Edwin

Maelfu ya watu wamejitokeza kupima afya zao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kisukari duniani, huku Mkurungezi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Lawrence Museru akiwataka Watanzania kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini kama wana tatizo la kisukari au matatizo mengine ya kiafya.

Katika maadhimisho hayo hadi kufikia saa 7:30 mchana leo, watu 1,150 wamejitokeza kufanya uchunguzi wa macho, uchunguzi wa afya ya kinywa na meno, uchunguzi wa magonjwa ya kisukari, homoni pamoja na shinikizo la damu.  

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Prof. Museru amesema kati ya watu wazima 100 takribani watu 9 wana ugonjwa wa kisukari na kati ya watu wazima 3 mmoja ana shinikizo la damu. “Tatizo ni kubwa kwani takwimu zinaonyesha kliniki ya kisukari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ina wagonjwa zaidi ya 6000 wanaoudhuria kwa mwaka,” amesema Prof. Museru.

Prof. Museru amesema kwamba moja ya vyanzo vinavyochangia kuongezeka kwa magonjwa yasioambukiza ikiwamo kisukari na presha ni ulaji usiofaa kama kula chakula kuzidi mahitaji ya mwili na hivyo kunenepa, kula mafuta na chumvi zaidi ya mwili, kutokula matunda na mbogamboga kiasi cha kutosha na kula nafaka zilizokobolewa.

Mkurugenzi huyo amesema matumizi ya pombe kupita kiasi, tumbaku na dawa za kulevya, kutofanya mazoezi na msongo wa mawazo pia yanachangia kuongezeka kwa magonjwa yasioambukiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Prof. Lawrence Museru akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kisukari ambayo huadhimishwa Novemba 14, kila mwaka. Maadhimisho hayo yanafanyika katika hospitali hiyo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
 Mmoja wa wananchi aliyejitokeza kuchangia damu katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani hospitalini hapo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Museru akionyesha umuhimu wa wananchi kuchunguza afya zao kwenye maadhimisho hayo.
Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma ya uchunguzi leo.


TAKUKURU YAWASHIKILIA VIGOGO WATANO MAKETE KWA TUHUMA ZA UPOTEVU WA FEDHA MILIONI 500/- , YUMO MKURUGENZI WA HALMASHAURI

$
0
0
Na Amiri Kilagalila ,Njombe 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) mkoani Njombe inawashikilia watumishi watano wa Halmashauri ya Makete akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Francis Namaumbo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha zaidi ya Sh.milioni 500.

Akizungumza leo Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe Chalse Nakembetwa amesema kuwa upotevu wa fedha hizo umetoka katika makusanyo ya Julaihadi Semptemba ambapo yalikuwa ni zaidi ya Sh.bilioni moja huku taarifa zikionesha kuwa zaidi ya Sh.milioni 500 zimepotea na wahusika wakishindwa kutoa maelezo ya kutosha baada ya kuhojiwa na taasisi hiyo.

Amesema katika uchunguzi Takukuru imebaini wizi na ufisadi unaofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Makete zaidi ya Sh.milioni 5.69 sawa na asilimia 46 zilizokusanywa kwa utaratibu wa POS kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2018 hazijulikani zilipo.

Amefafanua makusanyo hayo yalikuwa ni sehemu ya Sh.1,245,632,633 yaliyokusanywa katika kipindi tajwa .Kutokana na uchunguzi huo Takukuru Mkoa wa Njombe inawashikiria baadhi viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa ajili ya uchunguzi.

SIMBA SC KUITOA KIMASOMASO TANZANIA KWENYE MICHUANO YA AFRIKA...

MICHUZI TV: Polisi Mbeya watoa Somo Kwa Madereva wa Serikali..

Mchezo mpya wa Supa Tano wazinduliwa Tanzania

$
0
0

 • Kwa shilingi 1,000 tu mchezaji anaweza kushinda hadi 10,000,000/- kila baada ya dakika 10

Kampuni ya The Network inayosimamia michezo ya namba nchini Tanzania leo imezindua mchezo wa namba ujulikanao kama Supa Tano ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni 10,000,000/- kila baada ya dakika 10.

Huu unakuwa ni mchezo pekee kwa sasa nchini Tanzania ambapo mshindi anaweza kupata kiasi kikubwa ndani ya dakika kumi tu. Mchezo wa Supa Tano pia unakuwa ni mchezo pekee wenye kutoa fursa nyingi zaidi za ushindi hapa nchini.
Meneja wa Fedha wa The Network,Bwana Jacob Millinga, amesema ‘Supa Tano ni mchezo mpya wa namba ambao wachezaji wanaweza kucheza viwango mbalimbali kati ya shilingi 1000 mpaka 20,000. Mchezo unatoa nafasi ya kushinda hadi mara 10,000 ya dau uliloweka, ambacho ni kiasi kikubwa kuliko mchezo wowote Tanzania’ anasema Kupitia Supa Tano mchezaji anapata nafasi nyingi zaidi za ushindi, kwani kila namba anayolinganisha analipwa kuanzia namba 2, 3, 4 au namba 5 kwenye droo za kila dakika 10, na wakati huo huo kila shilingi 1000 yake inampa nafasi ya kuingia kwenye SupaMzuka Jackpot siku za Jumapili na Jumatano.

‘Mchezaji anacheza kupitia simu yake ya mkononi kwa kutuma shilingi 1,000 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 551551 ikifuatiwa na kumbukumbu namba ambazo zitakuwa namba zake 5 za bahati kati ya 0-9, na kama ameshinda anatumiwa kiwango cha pesa cha ushindi wake moja kwa moja kwenye namba yake ya simu’ alifafanua balozi wa Supa 5, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa.

Mchezo wa Supa 5 unaendeshwa kwa uwazi na usimamizi wa serikali kupitia Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Matokeo yote ya washindi na zawadi walizoshinda yatawekwa kwenye tovuti ya: www.supatano.co.tz.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwakilishi wa Bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), amesema mchezo wa Supa 5 unaongeza fursa nyingine za ushindi kwa watanzania lakini ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa ustaraabu bila kutumia pesa ya matumizi muhimu kwenye mchezo huu.
 Meneja wa Fedha wa kampuni ya The Network. Jacob Millinga akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa mchezo wa namba ujulikanao kama Supa Tano ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni10,000,000/- kila baada ya dakika 10,uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar
‘Mchezaji anacheza kupitia simu yake ya mkononi kwa kutuma shilingi 1,000 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 551551 ikifuatiwa na kumbukumbu namba ambazo zitakuwa namba zake 5 za bahati kati ya 0-9, na kama ameshinda anatumiwa kiwango cha pesa cha ushindi wake moja kwa moja kwenye namba yake ya simu’ alifafanua balozi wa Supa 5, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa kwa Wanahabari leo jijini Dar.
 
 Balozi wa Supa 5 Adam Mchovu akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari namna ya kucheza mchezo huo wa namba ujulikanao kama Supa 5 kupitia simu ya mkononi,ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni10,000,000/- kila baada ya dakika 10,uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar
Uzinduzi wa Mchezo wa namba ujilikanao kwa jina la Supa 5 ukiwa tayari kuzinduliwa rasmi na wananchi kuanda kuucheza mchezo huo kwa njia ya simu zao za Kiganjani.

MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI

$
0
0
Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo  kikuu cha Dodoma ( UDOM)kitivo cha elimu amekwama nauli ya kufika chuoni  baada ya wazazi  wake kutamka bayana kuwa hawana uwezo hata  ya kupata nauli ya kumsafirisha  binti yao kufika chuoni .
Bahati  Njete (21) mkazi wa Minazini wilayani Namtumbo amechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma  huku  wazazi wake hawana  uwezo  hata wa kumpatia  nauli ya kufika  chuoni  ili  akaendelee  na masoma yake.
Akiongea  na Ofisa ustawi wa jamii wilaya ya Namtumbo Irene Kitula ofisini kwake  Bahati alisema  wazazi wake wanahali ngumu za kimaisha na mafanikio aliyoyapata ni kutokana na misaada ya wasamaria wema  ambao walijitolea kwa hali na mali kumsaidia toka kidato cha kwanza  hadi cha sita.
Aidha  Bahati alidai kumaliza elimu ya sekondari katika sekondari ya kata Narwi  iliyopo wilayani Namtumbo na kisha kuchaguliwa kuendelea na masomo kidato cha sita katika shule ya sekondari ya  Igowole  iliyopo mkoa wa Njombe.
Ofisa  ustawi wa jamii alimfikisha mwanafunzi huyo mpaka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Namtumbo ili apatiwe kibali cha kuomba kuchangiwa fedha  kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufika chuoni  na zimsaidie akiwa chuoni pia.
Kwa  mujibu wa  mwanafunzi mwenyewe Bahati  alidai kusoma katika mazingira magumu kulingana na hali ngumu za wazazi wake lakini anawashukuru  wasamaria wema walioweza kumchangia kwa hali na mali mpaka kufikia hapo alipofikia .
Hata hivyo anaendelea kuwaomba wasamaria wema hao wasichoke  kumsaidia  bali waendelee kumsaidia kupitia namba yake ya simu 0718792037 ili aweze  kutimiza ndoto zake  za maisha baada ya kumaliza chuo.

MWANAHABARI WA RELI TV BEN MWANANTALA NA SUZAN MAMKWE WAMEREMETA

$
0
0
 Mwandishi machacahri wa wa Shirika la Reli Tanzania Ben  Mwanantala akiwa na mkewe Suzan Mamkwe baada ya kufunga.ndoa katika  kanisa la Mwenge Parokia ya Mwenge jijini Dar es salaan na kufuatiwa na mnuso wa nguvu katika ukumbi  wa Mwenge Hall. Globu ya Jamii inatoa hongera sana kwa Ben ambaye ni mfano wa kuigwa kwa wanahabari wa kwenye taasisi za umma kwa weledi wake na kujituma,
 Ben mwanantala na Suzan Mamkwe katika mnuso wao baada ya  kumeremeta
Ben mwanantala na Suzan Mamkwe wakiwa na furaha kwa kumeremeta

DC MURO AZISAKA MILIONI 400

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani Arumeru linamsaka aliyekuwa mweka hazina ( Muhasibu ) wa halmashauri ya meru Ndg. Emmanueli Joram na Michael Palanjo aliyekuwa mhudumu wa kawaida akapewa kazi ya wakala wa kukusanya mapato ya halmashauri kwa tuhuma za ubadhilifu wa ya shilingi Milioni 364 Fedha Za Miradi ya TASAF kwa halmashauri ya Meru, uku Shilingi milioni 119,674,285 zikiwa pia hazionekani katika akaunti ya halmashauri ya Meru zikiwa ni fedha za makusanyo ya ndani ambazo hazijapelekwa benki na hazijulikani zilipo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za halmashauri hiyo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. JERRY MURO ambapo amefanya ziara yake ya kushtukiza katika Halmashauri hiyo na kubaini kiasi hicho cha fedha kupotea na ameshangazwa na upotevu huo kuchukua muda mrefu bila uchunguzi.

Kwa upande wake msimamizi wa mfuko wa Tasaf Ndg. Bonifasi Mwilanga mbali na kukiri kufahamu kwa ubatilifu huo amekiri pesa hizo zimetumika kinyume cha utaratibu katika matumizi yake.

Pia kwa upande wao baadhi ya viongozi wa Halmashauri hiyo akiwemo Mkurugenzi Ndg. Emmanueli Mkongo na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ndg. Wille Njau wamelezea jitihada walizozichukua ikiwa ni pamoja na kuunda kwa tume ya uchunguzi juu ya upotevu wa fedha hizo.

Dc Muro amewaagiza wakuu wa idara zote katika Halmashauri hiyo kutosubiri taarifa za fedha za idara zao na badala yake ni kufatilia kila Juma kimaandishi ili kutotoa mwanya wa upotevu wa pesa za umma.

Waziri Mwakyembe akutana na Uongozi wa MISA –TAN kujadili maendeleo katika Sekta ya Habari.

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN kuhusu maendeleo ya sekta ya Habari leo Jijini Dodoma.

 Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari ya MISA – TAN Bibi.Salome Kitomary (Kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) wakati Taasisi hiyo ilipokutana nae leo Jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugeni Msaidizi Idara ya Habari Bw. Rodney Thadeus.

 Mkurugeni Msaidizi Idara ya Habari Bw. Rodney Thadeus akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) kuzungumza na  Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA – TAN leo Jijini Dodoma.

 Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN  Wakili James Marenga akizungumza wakati wa kikao kati ya taasisi hiyo na  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) kuhusu maendeleo ya sekta ya Habari leo Jijini Dodoma.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake.

MFAHAMU MICHAEL KEARNEY KIJANA ALIYEMALIZA CHUO AKIWA NA MIAKA 10 PEKEE

$
0
0


MICHAEL Kearney raia wa Marekani ndiye kijana pekee aliyevunja rekodi ya kumaliza chuo akiwa na umri mdogo kabisaa wa miaka 10 na kuwa mwalimu wa chuo kikuu akiwa bado kijana.

Michael alizaliwa Januari 18, 1984 familia yake ikinukuliwa na jarida la Chuo cha San Marin ilieleza kuwa Michael alianza kufundishwa na wazazi wake kabla ya kwenda shule na hiyo ni baada ya kuona namna anavyokuwa na kichwa chepesi na akili zilizopitiliza katika kuelewa mambo, imeelezwa kuwa hata dada yake Michael aitwaye Maeghan alimaliza chuo akiwa na miaka 16 pekee.

Imeelezwa kuwa akiwa na miezi minne pekee Michael alitamka neno la kwanza na akiwa na miezi 10 alijifunza kusoma na alipofika miaka 4 alifahamu na kujua hesabu akiwa hajaanza shule kabisa.

Akiwa na umri wa miaka 6 alienda shule ya San Marin kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kijiunga na elimu ya juu.

Akiwa na miaka 10 Michael alipata shahada yake ya kwanza katika fani ya Anthropolojia, na alipofika miaka 14 alipata shahada ya uzamili katika chuo cha Middle Tennesse mwaka 1999 na baadaye kufundisha katika chuo hicho na alipofikia miaka 18 tuu alipata shahada ya uzamivu (PHD) Katika fani ya Sayansi ya kompyuta na kuendelea kufundisha katika chuo hicho.

MTI MREFU AFRIKA HUU HAPA

$
0
0
KASKAZINI Mashariki mwa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kuna mti mrefu kuliko yote Afrika. Mti huo wenye kilometa 81.5 unapatikana katika moja ya bonde la mlima huo.

Kulingana na utafiti uliofanywa na mwanazuoni Adreas Hemps toka Chuo kikuu Bayreuth nchini Ujerumani akinukuliwa na jarida la Biodeversity and Conservation ambalo limeeleza kuwa Andreas aligundua mti huo miaka 20 iliyopita katika hifadhi hiyo na baadaye kati ya mwaka 2012 na 2016 alikuja na wataalamu wenzake na kuupima urefu wake ambapo kutokana na vipimo hivyo walikadiria umri wa mti huo ni kuanzia miaka 500 hadi 600.

Mti huo unaojulikana kwa jina la Colossus umevunja rekodi ya dunia kwa urefu wake na uliwahi kufananishwa na mti aina ya Sydney uliopo Limpopo Afrika Kusini ambao ulikufa mwaka 2006.

Pia fahamu kuwa mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu zaidi duniani kwa milima isiyo na safu na una kilele chenye mita 5895 kutoka usawa wa bahari ukiwa na vilele maarufu vya Kibo na Mawenzi.

WAZIRI NDALICHAKO AZINDUA MWONGOZO NA MASHINDANO YA UBUNIFU JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo amezindua mwongozo na mashindano ya ubunifu kitaifa mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi Waziri Ndalichako amesema lengo la mashindano hayo ni kutambua na kuendeleza fikra za wabunifu kwa lengo la kuongeza ajira.

Prof. Ndalichako amesema katika kuimarisha uchumi wa viwanda lazima matumizi ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaimarishwe kwa lengo la kuongeza tija viwandani na kwenye biashara.

“Kutoka na umuhimu wa mashindano haya naielekeza Idara ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kila mwaka, ili kukuza ujuzi, wabunifu kwa maendeleo ya viwanda,” alisisitiza Waziri Ndalichako.Mashindano hayo yameshirikisha Makundi mbalimbali ya kijamii zikiwemo Shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi Stadi, Sekta isiyo rasmi, Vyuo vya ufundi wa Kati, Vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi za utafiti na Maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa kuzinduliwa kwa mwongozo huo ni jambo kubwa na la kihistoria ikizingatiwa kuwa nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda.Serukamba amesema bila Sayansi, Teknolojia na ubunifu nchi haiwezi kufanikisha malengo yake, hivyo ameiomba Serikali ihakikishe inawekeza fedha nyingi.

“Kama hatutawekeza fedha za kutosha kwenye Sayansi, Teknolojia na Ubunifu hatuwezi kufanya kitu, hivyo tuwekeze fedha za kutosha ili tujiletee Maendeleo kwa haraka,” amesema Mhe. Serukamba.Kauli mbiu ya mashindano hayo ni “Kukuza Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda.”
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Huduma za Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba Mwongozo wa ubunifu mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dodoma.
Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizra ya Elimu na Teknolojia wakifurahia mara baada ya Mwongozo na Mashindano ya ubunifu kuzinduliwa.
Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba wakionesho mwongozo wa Ubunifu mara baada ya Kuzinduliwa leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akimkabidhi mmoja wa wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Dodoma Mwongozo wa ubunifu mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dodoma

DKT. MWANJELWA AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE ILI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA UMMA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) ameahidi kushirikiana na watumishi wa ofisi yake kupanga mikakati endelevu itakayowezesha kutoa huduma bora kwa umma na kuhakikisha ofisi hiyo inakuwa na mtazamo chanya katika kuwahudumia wananchi.

Dkt. Mwanjelwa ametoa ahadi hiyo leo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. Dkt. Mwanjelwa ameomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa watumishi wa ofisi yake kwani kila mtumishi ana mchango na umuhimu wake katika kuboresha utuoaji wa huduma kwa umma.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri mwenye dhamana ya utumishi na utawala bora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 10 Novemba, 2018 na kumuapisha tarehe 12 Novemba, 2018.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Dorothy Mwaluko, akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi, mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. 
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images