Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Waziri wa Nishati afanya mazungumzo na washirika wa maendeleo

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amekutana na washirika wa maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati ili kujadiliana nao kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo miradi wanayoifadhili na miradi mipya inayohitaji fedha za uwekezaji.

Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Nishati na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt Hamisi Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu,  Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi na watendaji kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Baadhi ya washirika wa maendeleo waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Ubalozi wa Ujerumani na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania.

 “Serikali haiwezi kufanya kazi peke yake hasa katika kutekeleza mipango ya muda mrefu ya kuzalisha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 na mipango ya muda  mfupi ya kuzalisha megawati 5000 ifikapo mwaka 2020,” amesema Dkt. Kalemani.

Amesema kuwa, washirika hao wanahitajika katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya usambazaji na usafirishaji umeme ambapo ameeleza kuwa sehemu kubwa ya nchi ina miundombinu ya umeme ya kV 33 na 132kV lakini kwa sasa msisitizo unawekwa katika kupata fedha ya kujenga miundombinu ya msongo wa kV 220 hadi kV 400 ili kupeleka umeme mwingi na wa uhakika kwa wananchi.

Ameongeza kuwa,  kwa sasa uwezo wa mitambo ya kufua umeme ni megawati 1500 lakini bado inahitajika mitambo itakayozalisha megawati 3500 ili kuweza kufikia megawati 5000 ifikapo mwaka 2020,  hivyo zinahitajika juhudi za pande zote mbili ili kuweza kufikia lengo husika.

Dkt Kalemani pia, amewaeleza washirika hao kuwa, Tanzania bado ina fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji ambapo kuna vyanzo vya maji vinavyoweza kuzalisha megawati 4700 lakini kwa sasa zinazalishwa megawati chini ya 600 kwa kutumia chanzo hicho.

Kuhusu umeme wa makaa ya mawe amesema kuwa, Tanzania ina mashapo ya makaa ya mawe ya kiasi cha tani 1.2 bilioni lakini hazijaanza kuzalisha umeme hivyo eneo hilo pia linahitaji ushirikiano ili makaa hayo yatumike katika kuzalisha umeme.

Aidha, amewaeleza washirika wa maendeleo kuwa, Tanzania ina upepo wenye kasi ya 8-9 kilometa kwa sekunde ambao unaweza kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 5000 lakini kwa sasa umeme wa upepo unaozalishwa nchini ni chini ya megawati 1.

Vilevile amewaeleza kuhusu fursa za uwekezaji katika uzalishaji umeme kwa kutumia Jotoardhi na kusema kuwa nchi inaweza kuzalisha umeme wa megawati 5000 kutokana na chanzo hicho ambacho hakijaanza kutumika tofauti na nchi ya Kenya ambayo inazalisha takriban megawati 200.

Kwa ujumla, Waziri wa Nishati amewaeleza Washirika hao wa maendeleo kuhusu maeneo yote yanayohitaji ushirikiano ambayo ni miradi ya uzalishaji, usafirishaji, usambazaji umeme na kuongeza ujuzi kwa wataalam nchini.

Akizungumza kwa niaba ya washirika hao wa maendeleo, Mwakilishi kutoka Umoja wa Ulaya, Jenny Correia Nunes, amemshukuru Waziri wa Nishati kwa kuitisha kikao hicho ambacho kimejenga uelewa wa pamoja kati ya pande hizo mbili na kushauri kuwa utaratibu wa vikao vya pamoja uwe ni endelevu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na washirika mbalimbali wa Maendeleo pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma

MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI

$
0
0
Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo  kikuu cha Dodoma ( UDOM)kitivo cha elimu amekwama nauli ya kufika chuoni  baada ya wazazi  wake kutamka bayana kuwa hawana uwezo hata  ya kupata nauli ya kumsafirisha  binti yao kufika chuoni .
Bahati  Njete (21) mkazi wa Minazini wilayani Namtumbo amechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma  huku  wazazi wake hawana  uwezo  hata wa kumpatia  nauli ya kufika  chuoni  ili  akaendelee  na masoma yake.
Akiongea  na Ofisa ustawi wa jamii wilaya ya Namtumbo Irene Kitula ofisini kwake  Bahati alisema  wazazi wake wanahali ngumu za kimaisha na mafanikio aliyoyapata ni kutokana na misaada ya wasamaria wema  ambao walijitolea kwa hali na mali kumsaidia toka kidato cha kwanza  hadi cha sita.
Aidha  Bahati alidai kumaliza elimu ya sekondari katika sekondari ya kata Narwi  iliyopo wilayani Namtumbo na kisha kuchaguliwa kuendelea na masomo kidato cha sita katika shule ya sekondari ya  Igowole  iliyopo mkoa wa Njombe.
Ofisa  ustawi wa jamii alimfikisha mwanafunzi huyo mpaka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Namtumbo ili apatiwe kibali cha kuomba kuchangiwa fedha  kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufika chuoni  na zimsaidie akiwa chuoni pia.
Kwa  mujibu wa  mwanafunzi mwenyewe Bahati  alidai kusoma katika mazingira magumu kulingana na hali ngumu za wazazi wake lakini anawashukuru  wasamaria wema walioweza kumchangia kwa hali na mali mpaka kufikia hapo alipofikia .
Hata hivyo anaendelea kuwaomba wasamaria wema hao wasichoke  kumsaidia  bali waendelee kumsaidia kupitia namba yake ya simu 0718792037 ili aweze  kutimiza ndoto zake  za maisha baada ya kumaliza chuo.

WANANCHI WANASHUHUDIA MAAJABU MAKUBWA NDANI YA MIAKA MITATU YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI-WAZIRI JAFO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Dodoma

WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Rais Dk.John Magufuli ikiwa imetimiza miaka mitatu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo amesema kuna mambo makubwa ya kujivunia ambayo yamefanyika ndani ya muda huo.

Pia ameeleza hatua kwa hatua namna ambavyo Wizara yake imeshiriki kikamilifu katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora katika sekta mbalimbali nchini huku akieleza namna anavyomsukuru Rais Dk.Magufuli kwa namna ambavyo amemuamini na kumteua kuhudumu nafasi hiyo.

Waziri Jafo ambaye ni miongoni mwa mawaziri vijana waliopata nafasi ya kuaminiwa na Rais Magufuli amesema hayo katika mahojiano maalumu na timu ya waandishi wa habari wa Michuzi Blog na Michuzi TV walipofika ofisini kwake katika Jiji la Dodoma.

Ambapo pamoja na mambo mengine mahojiano yalijikita katika kuzungumzia miaka mitatu ya Rais Magufuli na mchango wa Tamisemi katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa Watanzania wote.

Waziri Jafo kabla ya kuelezea maendeleo makubwa ambayo yamefanyika kwenye sekta mbalimbali ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imebeba ajenda ya wananchi na hilo amekuwa akilizungumza mara kwa mara.

Amefafanua ajenda hiyo imetokana na kiu ya

wananchi ya kutaka mabadiliko na kwamba hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 karibu Watanzania wote walisema wanataka mabadiliko.

“Watanzania wote walisema wanataka mabadiliko na hivyo kuundwa kwa Serikali ya Awamu ya Tano kumetokana na ajenda ya wananchi ya kutaka mabadiliko. Rais Magufuli baada ya kuingia madarakani akawa anajua jukumu lake ni kuhakikisha anakwenda na kiu cha wananchi ya kuleta mabadiliko,”amesema Jafo.

Hivyo amesema wakati Rais Magufuli anatimiza miaka mitatu, kwanza kabisa anamshukuru kwa uamuzi wake wa kumchagua na kumkabidhi ahudumu kwenye wizara hiyo ya Tamisemi na kufafanua unapozungumzia Tamisemi maana yake unazungumzia maisha ya watu ya kila siku.

Jafo amesema ukiangalia bajeti ya nchi asilimia 21 iko chini ya wizara yake na asilimia 72 ya watumishi wote iko kwake.Pia miradi mingi ya maendeleo ya wananchi iko chini ya Tamisemi na hivyo Wizara hiyo ikishinda kutekeleza majukumu yake maana yake hata mabadiliko ya kimaendeleo nayo yatakwama.

“Wizara ya Tamisemi ndio inayohangaika na maisha ya wananchi ya kila siku na hivyo kwa ujumla wake lazima iwe na mikakati ya kuchagiza ukuaji wa maendeleo ya wananchi ili kufikia uchumi wa kati.Mwananchi akikosa huduma atalalamika na malalamiko yake yatakuwa yanafikisha ujumbe yale mabadiliko ambayo ameyategemea hayapo,”amesema.

Waziri Jafo amesema wakati Rais Magufuli akiwa ametimiza miaka mitatu , utabaini mtazamo wake umejikita kuleta mabadiliko kwa Watanzania wa kada zote kwa kuhakikisha nchi yetu inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

“Mtazamo wa Rais ni kwamba nchi yetu lazima ifikie uchumi wa kati na ili kufika safari hiyo lazima tuchague njia ya kupita ambayo ni ujenzi wa viwanda na ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano inahimiza ujenzi wa viwanda.

“Katika kwenda na mtazamo wa Rais wangu mchapakazi ndio maana katika wizara yangu agizo langu la kwanza ilikuwa ni kufanikisha ujenzi wa viwanda.Nikatoa maagizo kwa wakuu wa mikoa wote nchini watenge maeneo ya ujenzi wa viwanda.Pia nikafanya tathimini iliyokwenda sambamba na kutoa maagizo ya kila mkoa kujenga viwanda 100 ndani ya miezi 12.Katika hilo tumefanikiwa,”amesema.

Waziri Jafo amesema wakati anatoa agizo la ujenzi wa hivyo viwanda wapo waliosema amekurupka lakini ukweli alikuwa anajua anachokifanya na hivyo kampeni hiyo imesaidia kwani kuna viwanda vidogo 2600 vimejngwa ndani ya miezi 12 na Desemba mwaka huu atapata taarifa rasmi.

"UCHOVU NI SABABU INAYOPELEKEA AJALI ZA BARABARANI" -- DKT. MPOKI

$
0
0
Na WAMJW, Dar es Salaam.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa moja ya sababu za ajali barabarani, ni uchovu wa madereva.

Dkt. Mpoki ameyasema Novemba 13, 2018 wakati wa kufungua mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya Hospitali nchini.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Dkt. Mpoki amelitaka jeshi la Polisi nchini kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa madereva kubadilishana kwani suala la uchovu linachangia kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani.

Aidha, akitolea mfano suala la uchovu, dereva kutoka Mwanza au Bukoba kwenda Dar es Salaam, basi ashuke Singida ili aingie dereva mwingine kumalizia safari na hiyo itasaidia kuepusha ajali.

“Tumemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi atusaidie kama mchango wa Polisi katika kupunguza ajali kwa kuhakikisha kwamba wanaweka utaratibu wa madereva wanaendesha kwa muda maalum. Kuliko ilivyo sasa madereva wanaweza kuendesha siku nzima, Hivyo wanakuwa wachovu na kuchangia kwa kiasi kikubwa sana ajali mbalimbali barabarani” amesema Dkt. Mpoki.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya  akizungumzawakati wa  kufungua mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya Hospitali nchini  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizindua kitabu cha mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi  wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje  ya hospitali nchini Tanzania
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (MUHAS), Profesa Appolenary Kamuhabwa akizungumza machache  wakati wa ukufungua wa mafunzo ya watoa huduma za tiba  jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi  wa idara ya dharura hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt .Juma Mfinanga akipokea  kitabu hicho  cha mafunzo  kutoka kwa Katibu Mkuu  Dkt. Mpoki  Mara baada ya kukizindua

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UGENI KUTOKA BENKI YA NMB OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya NMB ulioongozwa na Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki hiyo, Ndg. Tom Borghlos (wa pili kushoto) walipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Ndg. Jos Lange, Afisa wa Benki ya NMB, Ndg. Juliana muwanga (wa tatu kulia), Mkuu wa Biashara Benki ya NMB, Ndg. Donatus Richard (wa pili kulia) na Meneja kanda ya kati, Ndg. Nsolo Mlozi

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB, Ndg. Tom Borghlos (wa pili kushoto) pale ugeni kutoka Benki hiyo ulipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mjumbe wa Bodi NMB, Ndg. Jos Lange na Afisa wa Benki ya NMB, Ndg. Juliana muwanga
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Benki ya NMB ulioongozwa na Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki hiyo, Ndg. Tom Borghlos (watatu kulia) walipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Mjumbe wa Bodi wa Benki ya NMB, Ndg. Jos Lange pale ugeni kutoka Benki ya NMB ulipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Biashara Benki ya NMB, Ndg. Donatus Richard. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TUMEAMUA KOROSHO YOTE IBANGULIWE NCHINI-MHE HASUNGA

$
0
0
Na Mathias Canal-Wizara ya kilimo, Mtwara

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa wizara yake itatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa korosho yote inabanguliwa hapa nchini.

Ameyasema hayo jana tarehe 13 Novemba 2018 wakati akieleza malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho.

Hasunga alisema kuwa kuruhusu wafanyabiashara kubangulia nje ya nchi korosho za wakulima wa Tanzania ajira nyingi zilikuwa zikipotea huku watanzania wakisalia kuhangaika kutafuta ajira kwani ajira nyingi zilipelekwa nje ya nchi.

“Baada ya kujiridhisha tumeamua sasa hahutasafirisha korosho ghafi tunataka korosho yote iwe inachakatwa nchini kwenye viwanda vyetu, kwa hiyo korosho zote zilizokuwa zinachukuliwa na wafanyabiashara kwenda kubanguliwa sijui wapi huko tumezuia” Alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema kuwa viwanda vya kubangua korosho nchini vingi vimekufa kwa sababu ya ubadhilifu wa wananchi wachache na baadhi ya hujuma za watu lakini serikali imedhamiria kuanza kubangua kwenye viwanda vilivyopo kabla ya hatua za kuanzisha viwanda vingi vya ubanguaji.

“Tunamuwezesha mkulima kwa bei ya shilingi 3300 ili imsaidie kufanya kazi zake zingine ili aweze kuongeza uzalishaji katika msimu ujao wa mwaka 2018/2019 na kuepuka kushuka kwa uzalishaji” Alisisitiza Mhe Hasunga.Alisema baada ya kukamilika uhakiki wa maghala yote ya kuhifadhia korosho serikali itaanza kulipa malipo yote stahiki kwa wakulima yatakayotolewa na Benki ya kilimo Tanzania (TADB).

“Na tumeshaandaa fedha zao tunataka wakulima walipwe haraka iwezekanavyo lakini tumeanza kumjali mkulima kwanza halafu taasisi zingine zinazofaidika na korosho zitafuata” Alisisitiza

Mhe Hasunga amewapongeza wakulima kwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito wakati serikali ilipokuwa ikitafuta ufumbuzi wa zao la korosho.
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akieleza malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho jana tarehe 13 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari kuelezea malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho jana tarehe 13 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

GEREZA LUDEWA KUPATIWA TREKTA ILI KUONGEZA UZALISHAJI WA CHAKULA CHA WAFUNGWA

$
0
0
Na Lucas Mboje, Ludewa
KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameahidi kulipatia trekta moja Gereza la Kilimo Ludewa ili kuongeza uzalishaji wa chakula cha wafungwa.
Kamishna Jenerali Kasike ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na uongozi wa Gereza hilo baada ya kuwasili Wilayani Ludewa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Jeshi hilo.
Amesema kuwa Gereza Ludewa ni miongoni mwa magereza 13 ambayo tayari yameainishwa katika mpango mkakati wa Jeshi la Magereza katika kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa waliopo magerezani hivyo lazima liwezeshwe zana za kilimo.
 “Nafahamu kuwa trekta lililopo hapa Gereza Ludewa ni la muda mrefu na ni chakavu, hivyo nitawapatieni trekta jipya ili muweze kuongeza uzalishaji wa chakula cha wafungwa”. Alisema Jenerali Kasike.
Pia, Kamishna Jenerali Kasike amehimiza uongozi wa Gereza hilo kuzingatia suala zima la uadilifu na amewataka kujiepushe na vitendo vyote vya ubadhilifu wa mali za umma.
Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza hilo, SSP. Akley Mkude amesema kuwa  katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2017/2018 gereza hilo lililima ekari 200 za mahindi na kufanikiwa kuvuna gunia zaidi ya 1700 ambazo zitatumika kulisha magereza yote ya Mkoa wa Njombe na Iringa. 
Aidha, ameongeza kuwa  malengo ya msimu huu wa mwaka 2018/2019 ni kulima ekari 700 za mahindi, ekari 40 za maharage, ekari 30 za alizaeti pamoja na bustani ekari 5 za mbogamboga. 
Gereza Ludewa lina eneo lenye ukubwa wa ekari 3500, Gereza hilo linajishughulisha na kilimo cha mahindi, maharage, alizeti pamoja na bustani za mbogamboga. Pia, linajishughulisha na miradi ya ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kuku wa kienyeji pamoja na uhifadhi wa mazingira.

 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na Maofisa na askari wa Gereza Ludewa alipowasili kuendelea na ziara yake ya kikazi ya kutembelea magereza mbalimbali Mkoani Njombe, Novemba 13, 2018.
 Mkuu wa Gereza Ludewa, SSP. Akley Mkude(kushoto) akimweleza jambo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo  Novemba 13, 2018. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike akipanda mti wa mparachichi katika Kambi ya Jeshi la Magereza ya Kidewa iliyopo Mkoani Njombe kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Ludewa Novemba 13, 2018.
 Ghala la kuhifadhia mahindi yanayozalishwa katika Gereza Ludewa. 
 Baadhi ya Askari wa Gereza la Wilaya Ludewa  wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani).
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Andrea Tsere(wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Ludewa( Picha na Jeshi la Magereza).

MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2019/20 KUZINGATIA MAONI YA WABUNGE

$
0
0
Na Saidina Msangi na Farida Ramadhani-WFM.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema kuwa Serikali itazingatia maoni na ushauri wa wabunge wote katika Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

Waziri Mpango alitoa kauli hiyo Bungeni wakati akiahirisha mjadala wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2019/2020.

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maoni ya wabunge kuhusu kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kuongeza bajeti ya kilimo, Dkt. Mpango alisema kuwa uongezaji wa bajeti ya kilimo ni muhimu lakini lazima ufanyike kwa ulinganifu wa mahitaji ya kibajeti ya sekta nyingine muhimu.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa sekta ya kilimo ina mwingiliano mkubwa na sekta nyingine. Mwenendo bora wa kilimo unategemea sana uwekezaji wa sekta saidizi hasa miundombinu ya umwagiliaji, barabara vijijini, umeme kwa ajili ya kuendesha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, uzalishaji wa zana za kilimo, dawa, elimu na afya kwa wakulima” alisema Waziri Mpango.

Aidha, waziri Mpango aliongeza kuwa ni muhimu kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika sekta za kilimo na uvuvi, kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na kutafuta masoko ya kikanda na kimataifa.Akizungumzia miradi mikubwa inayotajwa kukwama Waziri Mpango alifafafanua kuwa miradi iliyokwama imetokana na masharti hasi ya wawekezaji ambayo hayana maslahi kwa Taifa.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
 Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA- Bw. Charles Kichere (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili kushoto) na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu.

Kuelekea katika kipindi cha maandalizi ya  bajeti ya mwaka 2019/2020 wito umetolewa kwa  Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu na maeneo mengine kote nchini kuyapa kipaumbele masuala ya Lishe katika mipango na bajeti za Halmashauri zao, ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele wakati mafunzo maalum yaliyotolewa kwa baadhi ya viongozi na maafisa Lishe, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.

Kihwele amesema takribani asilimia 34 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima wana udumavu, hivyo ipo haja ya kutilia mkazo suala la lishe ili kutoathiri maendeleo ya ukuaji wa watoto, uwezo wao wa kufikiri na maendeleo yao kitaaluma(shuleni).

“Asilimia 34 ya watoto wa  nchi nzima wenye umri chini ya miaka mitano wana utapiamlo, suala hili linaathiri sana watoto, mfano matokeo yao shuleni na uwezo wa kufikiri, ndio maana serikali imeweka lishe kama kipaumbele na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama wasimamizi tunapita kwenye Halmashauri nchi nzima kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya lishe katika bajeti ya mwaka 2019/2020” alisema.
 Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele  akizungumza na baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
 Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa   akiwasilisha mada kuhusu mipango na bajeti ya masuala ya lishe Mkoani Simiyu kwa baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Kai.B. Mbaruk akizungumza na baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Vijana, wanawake na walemavu wala neema Manispaa ya Sumbawanga

$
0
0
Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imetoa shilingi milioni 70.5 kwa vikundi 21 vya vijana, wanawake na walemavu ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 yenye adhima ya kuwainua wananchi kiuchumi ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Manispaa ya Sumbawanga imedhamiria kutekeleza maelekezo ya serikali kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani na kuwezesha vikundi hivyo ambapo tangu mwaka wa fedha 2018/2019 uanze mwezi Julai hadi mwezi Novemba Halmashauri tayari imeshakusanya Shilingi bilioni 1.1 ambayo ni nusu ya makusanyo ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka huu.

Fedha hizo zilitolewa katika hafla fupi ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyekabidhi hundi kwa vikundi hivyo na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule, Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na vikundi husika.

Akisoma taarifa ya kukabidhi fedha hizo kwa vikundi Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya alisisitiza kuwa Ili dhamira ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati na Tanzania yenye Viwanda itimie shughuli utoaji wa mikopo lazima iwe endelevu na kuwa halmashauri imejiimarisha katika kukusanya mapato yake ya ndani ili kuleta matunda kwa kutoa mikopo.

“Vikundi hivi  vinajishughulisha na Usindikaji mafuta, chakula,vinywaji, Useremala, Utengenezaji wa Chaki na ushonaji, ufumaji na utengenezaji wa Mabatiki na Ufugaji wa kuku na ngombe wa maziwa. Pia Halmashauri inatarajia kutoka kiasi cha mkopo kilichobakia kwa mwezi Januari, 2019 kitakachokuwa kimekusanywa kutokana na makusanyo ya ndani.” Alisema.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanakikundi cha Wanawake cha Tupendane kinachojishughulisha na utengenezaji wa mabatiki kilichopokea hundi ya Shilingi Milioni 3.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (aliyeshika kipaza sauti) akitoa maelezo mafupi kwa kikundi cha sanaa za maigizo cha Great Mind Association (GMA) (wawakilishi wawili wamesimama kushoto) muda mfupi baada ya kikundi hicho kupokea hundi ya shilingi Milioni 3 ili kukuza shughuli zao za sanaa na miradi mingine ya kikundi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

BARABARA ZA KISASA KUONGEZEKA NCHINI

$
0
0
Imeelezwa kuwa ujenzi na usimamizi bora wa barabara za kisasa katika miji mikuu utachochea kukua kwa haraka kwa uchumi na kuvutia biashara za bidhaa na utalii hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amesema hayo jijini Arusha leo, wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa  uliondaliwa na Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), na Wizara yake unaohusu mapinduzi ya sekta ya usafirishaji na mabadiliko ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea na kusisitiza kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kutenga bajeti inayokidhi ili kutekeleza miradi ya ujenzi na usafirishaji hapa nchini.
Aidha, amewataka watalaam wa Wizara na Taasisi zake kushiriki kikamilifu, kujifunza ili kupata utaalam na uzoefu kutoka nchi zilizoendelea katika sekta ya miundombinu ya barabara na usafirishaji.
"Tumejipanga kuhakikisha tunakuwa na barabara bora zinazoweza kupitika wakati wote na zinazounganisha nchi yetu na nchi jirani ili kuvutia huduma za biashara, masoko, kilimo na viwanda ifikapo 2025", amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.
Mkutano huo wa kimataifa unaoongozwa na kauli mbiu isemayo "Mapinduzi ya Nne ya Sekta ya Usafirishaji" unahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi 25 duniani unawaweka pamoja wadau wa barabara kubadilishana uzoefu na teknolojia mbalimbali katika kuboresha miundombinu ya barabara na usafirishaji miongoni mwa nchi wanachama.
Nchi zinazohudhuria mkutano huo ni Bangladesh, Botswana, Canada, Jamhuri ya Czech, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Ufaransa, Ujerumani, Ghana na Japan.
Nyingine ni Kenya, Liberia, Madagaska, Msumbiji, Nepal, New Zealand, Nigeria, Rwanda, Seirra Leone, Afrika Kusini, Korea kusini, Sudan Kusini, Sri Lanka, Uturuki, Uganda, Uingereza na mwenyeji Tanzania.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo utaangalia matokeo ya uwekezaji katika miundomibinu ya usafirishaji na kujadili kwa undani changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea ikiwemo  ufinyu wa rasilimali za kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na uboreshaji wa huduma nyingine za kijamii kama maji, afya, elimu na nishati kwa wakati mmoja.
Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), lenye nchi wanachama 121 lilianzishwa mwaka 1909 na Tanzania ilijiunga mwaka 1992 ambapo mwaka huu Chama cha Barabara (TARA), kimeteuliwa kuwa mwakilishi wa Kamati ya Kitaifa ya PIARC hatua itakayoongeza fursa za uzoefu na teknolojia kwa Tanzania.
Mkutano huo uliofunguliwa rasmi leo unawakutanisha wataalam wa masuala ya barabara na teknolojia utafungwa kesho ambapo zaidi ya washiriki 200 wanahudhuria.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
 Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akihutubia wadau wa sekta ya ujenzi na usafirishaji (hawapo pichani), katika Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), jijini Arusha.
 Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), akipongezwa na  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), Bw. Patrick Mallejacq, mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), jijini Arusha. kushoto ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga.
 Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe,  akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), jijini Arusha. Kushoto ni Katibu Mkuu wa PIARC, Bw. Patrick Mallejacq na kulia ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), uliofanyika jijini Arusha.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Kilimanjaro kufanya kazi kwa kushirikiana, kuheshimiana na kupendana.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani humo.

“Mheshimiane, muwajibike wote tunajenga Tanzania mmoja tutangulize maslahi ya Taifa na si maslahi binafsi” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais aliwasili mkoani Kilimanjaro tarehe 8 Novemba 2018 ambapo alifanya ziara katika Wilaya ya Rombo, Wilaya ya Moshi, Same, Mwanga, Siha na Hai.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais alikagua miradi mbali mbali na kuweka mawe ya msingi katika ujenzi na mengine ufunguzi.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais aliwataka Viongozi wa Halmashauri kukusanya mapato na kubuni njia zingine za kupata mapato, pia alizihimiza kufanya mambo yao ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria.

Makamu wa Rais amezitaka halmashauri kutochukua ushuru wa mazao shambani na badala yake waanzishe soko maalum la mazao ambalo mkulima atapeleka mazao yake hapo.

Aidha Makamu wa Rais alitoa maagizo kwa mkoa kuhakikisha wafanyakazi wa viwandani na msahambani wanapewa msaada wa kutambua na kupata haki zao za msingi.

Kwa upande mwingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa mkoa wa Kilimanjaro una migogoro mingi ya ardhi ambayo hatua zitachukuliwa karibuni haswa kwa waliojimilikisha mashamba ya Ushirika na pia upo nyuma katika kulipa kodi za ardhi.

Waziri wa Ardhi amesisitiza watu wote waliouziwa viwanja kwenye eneo la kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools wasiendeleze kwani hati zote 39 zimefutwa na eneo litakabidhiwa kwa Kituo cha Wawekezaji.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Watendaji wa mkoa Kilimanjaro wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani humo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISIEMI Mhe. Selemeni Jafo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Kilimanjaro kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TANGAZO LA MAONESHO YA TATU YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA

WAHAMIAJI HARAMU 110 WAKAMATWA SHINYANGA...43 WARUDISHWA KWAO

$
0
0
Idara ya Uhamiaji mkoani Shinyanga imekamata wahamiaji haramu 110 wakiwemo raia wa kigeni 103 na Watanzania saba kwa kuishi nchini Tanzania kinyume cha sheria.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Novemba 14, 2018 Msemaji wa idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Godson Mwanawima, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya Idara ya Uhamiaji mkoa wa Shinyanga kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka 2018. 

Alisema wahamiaji hao haramu wengi ni kutoka katika nchi za jirani ambapo Burudi wamekamata 46, Rwanda wakiwa 13, pamoja na wengine kutoka nchi za Ethiopia, Kenya,India na China.

"Katika kipindi cha miezi mitatu,tumekamata na kuhoji watu 110 kati yao raia wa kigeni wakiwa 103 na Watanzania saba,kati ya wageni hao 103, wahamiaji 43 wamerudishwa kwenye nchi zao na 60 walibainika kuwa na vibali halali hivyo kuwaruhusu kuendelea kuishi hapa nchini",alieleza Mwanawina. Aliyataja maeneo ambayo wamekamata wa hamiaji haramu wengi kuwa ni wilaya ya Kahama kwenye mashamba ya Tumbaku, Mpunga na migodi na kwenye mgodi wa Mwakitolyo uliopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Naye Mrakibu msaidizi mkuu wa upelelezi na Operesheni Idara ya Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Filemon Meena, aliwataka watanzania kuachana na tabia ya kuhifadhi wahamiaji haramu, ambao wamekuwa wakivuruga amani ya nchi. Katika hatua nyingine aliwahimiza watanzania kila mmoja ajitahidi kuwa na kitambulisho cha taifa (NIDA), ambapo itafikia kipindi bila ya kuwa na kitambulisho hicho watakosa huduma za kijamii ikiwemo matibabu, lengo likiwa ni kukomesha kuwepo kwa hawamiaji haramu hapa nchini. 
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Godson Mwanawima, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga leo ofisini kwake.
Mrakibu msaidizi mkuu wa upelelezi na Operesheni Idara ya uhamiaji mkoa wa Shinyanga Filemon Meena akielezea kuhusu Operation wanazoendelea nazo kushughulika na wahamiaji haramu.Picha na Marco Maduhu Malunde1 Blog

MNADA WA HADHARA MALI ZA EUROPEAN UNION, UNICEF, FAMILY HEALTH INTERNATIONAL, WORLD BANK GROUP & BAM INTERNATIONAL BV TANZANIA DAR ES SALAAM

$
0
0
UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na EUROPEAN UNION, UNICEF, FHI360, WORLD BANK NA BAM INTERNATIONAL watauza kwa mnada wa hadhara Fanicha za ofisini, vifaa vya maofisini, magari, genereta na makontena matupu tarehe 17 November, 2018 Jumamosi kuanzia saa 3:30 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza, Mtaa wa Lion, 
Dar es salaam

Mali Zitakazouzwa: Meza za Ofisi 70, Viti vya Ofisi, Chest drawer,  Vitanda, Magodoro, Book case, Steel Cabnet, Fridge, Mashine kubwa za kufua, Canon Photo copy mashine10 model C2220i,2225i & 2230i colour, Power bank 3KVA(UPS) Viyoyozi vingi (A/c Split unit) Fertilizer Spreader m/c, 8 units assorted GYM machines,Trailer 2 Tons na vingine vingi. 

Magari, Trela,Genereta na Samani  zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza,Lion Street kuanzia tarehe 14 mpaka 16 November, 2018, saa 4:00asubuhi mpaka saa 11:00 jioni.

Makontena yanaweza kukaguliwa BAM International eneo la mradi JK Nyerere International Air port Terminal 3 November 14 – 16,2018 Saa 3:00asubuhi mpaka Saa 5:00asubuhi na Saa  7:00mchana mpaka Saa 10:00jioni.
MASHARTI YA MNADA.
Mnunuzi  wa Fanicha atatakiwa kulipa malipo yote kwa keshia (cashier). Na mnunuzi wa    Gari, Kontena na genereta atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 5 za kazi  mwisho wa kulipa tarehe 23,November 2018 saa 10:00 jioni, ukishindwa kulipa kwa muda huo Gari, Kontena au Genereta litauzwa  kwa mshindi mwingine aliyefata  na dhamana haitarudishwa.
Malipo kwa njia ya VISA na Master cards za bank ya CRDB yanakubalika.
Mali zote zitauzwa kama zilivyo bila dhamana.
Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru na kodi zingine zote.
Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa baada ya kulipa malipo yote pamoja na kodi
Kila mtu atatakiwa lazima kuwa na bid namba itakayopatikana getini.

Kwa maelezo zaidi waone:
UNIVERSAL AUCTION CENTRE 
PLOT NO: 5 “E” LION STREET SINZA             DAR ES SALAAM
CELL NO:  0754 284 926,  0757 284 926           E-mail: universalauction@hotmail.com


SAKATA LA KOROSHO: WAKAZI WA LINDI WAONGEA

MEYA IRINGA AWASHANGAZA MADIWANI AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32

$
0
0
KATIKA  hali  isiyoya kawaida   kikao  cha  baraza la madiwani  wa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa ambacho  kwa wiki  iliyopita  madiwani  wa chama  cha mapinduzi (CCM)  walisusia  kikao   hicho  mstahiki  meya   Alex  Kimbe amewashangaza  wengi  baada ya  kuendesha  kikao  kwa  dakika 32  na  kugoma kusikiliza  hoja binafsi .

Kikao   hicho  kilianza  saa 2.00  hadi saa 2.32  huku  madiwani  takribani 10 wa  chama  cha  demokrasia na maendeleo (Chadema)  wakiwa na ukumbini na CCM   akiwemo  diwani  mmoja pekee  na   naibu  meya  Joseph  Lyata    kiliweza  kuendeshwa  kwa aina  yake  baada ya  mstahiki  meya   kufungua  kikao  hicho  kwa   sala  baada ya hapo kuwaita  bila  kutokea wajumbe  watatu wawili wa CCM na mmoja wa  Chadema  kuuliza maswali ya  papo kwa  papo kwa  meya   .

Kutokana na  wajumbe hao  wa  kikao  kutokuwepo  alifunga  zoezi hilo  na  kuendelea  na agenda  nyingine za  kikao  ikiwa  ni pamoja na  kusoma  taarifa  za  kamati  mbali mbali  na  kuruhusu  wenye  maswali  juu ya kamati hizo  kuuliza maswali  baada ya  hapo  alitangaza  kuzikataa  hoja  binafsi  ambazo   takribani  tatu ambazo  zilikuwepo  kwa madai ya  kutozingatia  kanuni  za  baraza  hilo kwa  hoja  hizo  kufikishwa kwa maandishi kabla ya   kuletwa katika  baraza .

"  Ndugu  wajumbe  kwa  kuwa hakuna  hoja binasi  zilizopo  ni za mdomo  tuu  naomba  kumkaribisha katibu  wa  kikao kwa  maneno  machache na  baada ya  hapo  nifunge  kikao  chetu "  alisema  meya  Kimbe  .

Kuwa  anawashukuru  wajumbe  waliofika kwa  wakati katika  kikao  hicho  ambacho  kimsingi  kilitangazwa  kuanza saa 2 .00 asubuhi   hivyo  wajumbe  waliochelewa  wamechelewa  kikao   hicho  alisema  na  kutangaza  kufunga  kikao  huku  baadhi ya  madiwani  wakiendelea  kuwasili  ukumbini .

Wakizungumza mara  baada ya  kikao  hicho aliyekuwa  meya wa Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi (CCM)  alisema anashangazwa na hatua ya  kikao  kumalizika kwa  muda  mufupi  wakati  kulikuwa na hoja za  msingi  hasa  kwenye kamati ya mazingira  juu ya  eneo la Kihesa  Kilolo  eneo la  uwekezaji  ambalo waziri  wa  ardhi nyumba na maendeleo ya makazi na  waziri wa TAMISEMI  walishauri  eneo hilo  kutojengwa  viwanja  vya   michezo na badala  yake  kujenga vitega uchumi kama  ukumbi wa  mikutano wa AICC .

lla alisema anashangazwa  kuona anapingwa na meya  na  kuwa   hoja   hiyo  haina nafasi katika  kikao  hicho  na  badala yake  kuzuia  kujadiliwa na  kukimbilia  kufunga  kikao .
Baadhi ya madiwani  Halmashauri ya  Iringa  wakiwa katika  baraza leo

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

MADIWANI TABORA WATAKA OCD KWENDA KUJIBU TUHUMA ZA MGAMBO KUPIA WANANCHI

$
0
0
Na Tiganya Vincent, Tabora
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora limetaka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora aitwe kwa ajili ya kujibu tuhuma zinawakabili baadhi ya askari wake na migambo za kuwapiga na kuwaibia wananchi mali zao wakati wa Doria zao.

Madiwani hao wametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha robo ya kwanza ya Baraza hilo kufutia hoja iliyowasilishwa na Diwani wa Kata ya Itojanda Alphonce Shushi ya uwepo wa vitendo vya unyanyasaji wananchi vinavyofanywa na Mgambo.

Alisema Migambo hao kwa kushirikiana na baadhi ya Askari wanapokuwa katika Doria wamekuwa wakiwapiga na kuwanyanyasa na kuwahumiza baadhi ya watu.

Aliongeza kuwa baadhi yao wamekuwa wakidiriki hata kuchukua mali za watu wanapowakata kwa kisingizio cha kufanya Doria.

Naye Diwani wa Kata ya Isevya Ramadhani Shabani alisema migambo hao badala ya kusaidia kupambana na uhalifu wao ndio wako mstari wa mbele kuiba na kuwanyanyasa wananchi mitaani.

Alisema kuwa kazi yao kubwa ni kupiga watu na kufukizana na madreva wa pikipiki na wakati mwingine kuwabambikizia makosa.

Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Ifucha Rose Kilimba alihoji sababu zilizomfanya OCD kushindwa kuhudhuria kikao  Baraza la Madiwani wakati siku zote amekuwa akihudhuria au akituma mwalilishi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti siku zote OCD anahudhuria vikao leo kwanini ameshinwa kuhudhuria na hata kumtuma mwalilishi labda amejua kuwa tutamuuliza juu ya unyanyasaji unaofanywa na hao migambo anawatumia” alisema.

Alisema kitendo hicho kinasikitisha kwa walitaka wamweleze kero ambazo Migambo hao kwa kushirikiana na baadhi ya askari wanasababisha.

elezea kusikitishwa kwake na kitendo cha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora kushindwa kuhudhuria kikao chao licha ya kumpatia taarifa kwa ajili ya kujibu tuhuma zinawakabili baadhi ya askari wake na migambo.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Ng’ambo George Mpepo alimuomba Mstahiki Meya kusogeza mbele hoja hiyo ili OCD apewe taarifa ya kuhudhuria kwa ajili maoani na maswali ya Madiwani kuhusu  kero ambazo wanazipata wananchi kutoka na askari na migambo wanapokuwa katika Doria.

Alisema baadhi ya Migambo hao wanahistoria ya wizi na hivyo wanatumia fursa hiyo na Doria kuchukua mali za wananchi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora. Leopold Ulaya amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wake kuhakikisha anamweleza Mkuu huyo wa Polisi aweze kuhudhuria kikao kijacho(kesho) kwa ajili ya kupokea maoni na kujibu maswali ya Madiwani kuhusu unyanyasi unaofanywa na Migambo kwa wananchi na boda boda.
 Diwani wa Kata ya Itojanda Manispaa ya Tabora Alphonce Shushi  akitoa hoja  jana wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani ya kujadili jinsi Mgambo wanavyopiga na kunyanyasa wananchi wakati wa Doria.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora. Leopold Ulaya akifungua kikao cha Baraza Madiwani jana kilichokuwa kikipitia taarifa za Kata mbalimbali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Nduguru.

Benki ya TPB yasaidia vifaa Taswa SC

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Benki ya TPB imeendelea kuisadia  klabu ya  Waandishi wa habari za michezo  nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo ambavyo vitatumiwa na timu hiyo katika michezo yake mbalimbali.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja  Mawasiliano wa  Benki ya TPB Chichi Banda alisema kuwa wamesaidia msaada huo ni sehemu ya shughuli za Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini na muendelezo wao katika shughuli za kijamii ambapo mbali ya michezo, pia usaidia afya na elimu.

Chichi alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaTaswa SC ambayo mara kadhaa imekuwa ikitwaa ubingwa katika mashindano maalum ya vyombo vya habari yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha.

Alisema kuwa benki ya TPB ni wadau wakubwa wa michezo na mbali ya Taswa SC, pia usaidia timu nyingine.

“Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa faraja kubwa sana kwetu, ”alisema Chichi.

Mwenyekiti waTaswa SC, Majuto Omary aliishukuru benki ya TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na kuahidi kutumia vifaa hivyo  kwa umakini mkubwa na kushinda katika mechi zao mbalimbali.

“Tunajivunia uwepo wa Benki ya  TPB kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao katika benki hii na vile vilekuomba wadau wengine kufuata  mfano  kwa kuisaidiaTaswa SC ili iweze kufanikisha shughuli zake,” alisema Majuto.
 Meneja Mawasiliano wa TPB Bank, Chichi Banda (Kulia) akikabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (Taswa SC), Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika jana. TPB Bank imetoa msaada ikiwa sehemu ya shughuli zao za kijamii.
Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (Taswa SC), Majuto Omary (kulia) akitoa neon la shukrani mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Meneja Mawasiliano wa TPB Bank, Chichi Banda katika hafla fupi iliyofanyika jana. TPB Bank imetoa msaada ikiwa sehemu ya shughuli zao za kijamii. 

KAMANDA MUSLIM SASA KUWANYAKUA MADEREVA WA SERIKALI WASIOFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

$
0
0
*Asema inasikitisha watumishi wa umma kupoteza maisha kwa ajali
*Awataka waache kukimbia mwendo kasi, kupita magari bila uangalifu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunas Muslimu ametoa onyo kali kwa madereva wa Serikali ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali zinazokatiza maisha watumishi wa umma ambao Serikali imetumia fedha nyingi kuwaandaa huku akisisitiza atakayevunja sheria atamnyakua tu na sheria kuchukua mkondo wake.

Amesisitiza umuhimu kwa madereva wote nchini wakiwamo hao wa Serikali kuhakikisha wanatii sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo zinaepuka iwapo sheria zitazingatiwa. Kamanda Muslim ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na Michuzi Blog iliyotaka kupata kauli yake kutokana na kuibuka kwa ajali za barabarani ambazo nyingi zinahusisha magari ya Serikali ambapo amesema jambo la msingi ni kuhakikisha madereva wanatii sheria zilizopo.

"Tumedhamiria kuchukua hatua kwa madereva wote wa Serikali wanaoshindwa kuheshimu sheria za usalama barabarani na matokeo yake kusababisha ajali ambazo kimsingi zinaepukika.Madereva wote wa Serikali wote wamekwenda chuo na wanajua vema sheria za usalama barabarani.Hivyo hizi ajali ambazo zinatokea kwangu naona ni maksudi na wala hakuna sababu nyingine zozote zenye mashiko.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images